Mabadiliko ni lazima katika jamii yoyote ila ili kuleta mabadiliko mikakati na mbinu kadhaa zinatakiwa kuandaliwa. Matatizo yaliyopo ktk nchi yetu ni ya-kimfumo zaidi,na kwa kuwa mfumo uliopo hauendani na hali ya dunia tuliyopo ni dhahiri hata akiweke m2 mwingine yeyote hatakuwa na tija. Tatizo ninaloliona mimi kwa kupitia vyombo vya habari ni kwamba tumekuwa tukifikiri kwamba m2 au wa2 fulani wanaweza kuleta mabadiliko kwa namna tunavyotaka iwe jambo ambalo ni ndoto.
Mimi c mwanachama wa chama chochote lakini nakerwa na hali iliyopo nchini kwa kuwa inaniumiza, lakini kama utaniambia kwa mtizamo wangu nini kifanywe na vyama vya ushindani(c upinzani) ni kuanza kuandaa mfumo ambao utaleta madadiliko na kuwafanya waaminiwe na jamii kwa ujumla na c kundi la watu katika jamii.Mfumo huo unatakiwa kuanzia ngazi ya chini ambako ndiyo watanzania wengi fukara/maskini wanaishi.
Vyama vya ushindani vimekuwa vikonekana katika baadhi ya maeneo wakati wa kampeni tu baada ya chaguzi wananchi wanabakia na maisha yale yale tabu zil zile na hawaoni matokeo ya wale waliowachagua.
Mi nafikiri pamoja na vyama vya upinzani kuikosoa serikali na watendaji wake, vingekuwa na harakati za kuandaa mfumo wa Tanzania mpya ambayo inawezekana . Hata km serikali iliyopo madarakakani itajiuuzulu yote na kuwapa vyama vingine kuunda serikali bado hakutakuwa na mabadiliko, na mwishowe watabaki kulaumiana na kulumbana.
Hivyo basi ningependa katika mikutano ya vyama vya ushindani wangekuwa wanatoa elimu kuhusu katiba kwa kuelezea vile vipengele ambavyo vinafanya nchi yetu iendelee kuwa shamba la bibi katika rasilimali, namna ya kuweka utawala bora(ikiwamo kuboresha jeshi la polisi, na mfumo wa mahakama) Ni vema wananchi wafahamu kwamba taifa la Tanganyika na baadae Jamhuri ya Tanzania haikuwahi kuwa na Sheria zake(tulirithi katiba ya watawala) ambayo kwa wakati huo kiwango cha sayansi na teknoloji ilikuwa ndogo na hata wananchi walikuwa wachache sana, hivyo hakukuwa na hizi changamoto tulizonazo sasa.
Hivyo kwa wale wapenda maendeleo badala ya kuendelea kulumbana juu ya mambo ambayo hayatusaidii, anzisheni mijadala ya katiba kwa kuelezea mabadiliko yafanyike wapi katika katiba ya sasa.
Kwa viongozi wa vyama vya ushindani imarisheni vyema vyenu wilayani, vyama vingi havina ofisi wala viongozi makini, mnapokuwa na viongozi wanadharauliwa na jamii inayowazunguka ni dhahiri inatoa picha mbaya ya chama husika.
Naomba kuwasilisha.