Sina Imani na serikali ya nchi yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Sina imani na Jakaya Kikwete, Mizengo Pinda, Shein na watendaji wote wakuu wa serikali.
Sina imani kwa sababu siiamini, na siwaamini na hawaaminiki.
Siwezi kuiamini kwa sababu imeshindwa kusimamia mambo ya msingi.
Imejenga matabaka kwa makusudi, huku ikijua madhara yake,
Viongozi wa Kikristo wanauawa na waliobaki wanatishiwa maisha.
Viongozi wasio makini wamefumba macho, kwa kuwa wanashindwa kuzuia walichokipanda.Wasio na akili wanalifurahia jambo hili.
Wanatuadaa kijinga kuwa eti ni wahuni.
Mhuni anawezaje kuvumiliwa akitenda kosa "linalofanana" akiwalenga watu wale wale kila siku.
Mnawezaje kunisadikisha kuwa hamjamtuma huyo muhuni kufanya anayoyafanya kila siku huku mkimlinda.
Kwanza mmejuaje kuwa ni wahuni kama hamuwafahamu?
Hofu yangu isije ikawa anayetegemewa kumdhibiti muhuni akawa ndiye muhuni wa kwanza, akiyasimamia yote yatendwayo na hao "wahuni".
Tatizo viongozi wamelala, wanataka kutulaza na sisi, historia itawahukumu.
Hakuna apendaye machafuko nchini kwake, lakini ULEGELEGE ambao viongozi wanao japo hawapendi kuambiwa, utatughalimu.
Dini haijawai kuwa chanzo cha tofauti zetu, lakini sasa hivi hadi tunaoneana aibu kutazaman usoni,
Ujinga mtupu, kiongozi hajali hatma ya Taifa, anachotaka yeye kuendelea kupata "KULA" tu, anachochea watu kutengana kwa maslahi yake binafsi.
Unashindwa kusimama mwenyewe kwa miguu yako unategemea MIGUU YA DINI!!!
Tujiulize hizi dini zimeanza jana??????
Mbona wazee wetu tangu enzi za wakoloni waliishi vizuri, hawakutenganishwa na huu upuuzi wa dini?
Kwa nini leo ndiyo iwe hoja kuu ya kututenganisha?
Tutegemee AKILI ZETU, tujiepushe na kujiburuza kwa wenye TAMAA YA MADARAKA wakati uwezo wa kuongoza hawana, maana watataka kutumia njia zisizo halali kutaka uongozi au kuendelea kuongoza.
Viongozi mkubali matokeo, kuna vipindi tofauti, someni alama za nyakati, ukiona watu hawakupendi tena, tambua kuwa ni wakati wa kuwapisha wengine kuendelea kuongoza, ili utakapotoka walau wakukumbuke kwa uliyoyafanya hata kama ni machache