Sina imani na Division 1.7 wanazopata wanafunzi siku hizi kidato cha nne

nami nina wasiwasi kama wewe. sisi tuliopiga single digit kwanza tulikuwa na uelewa mkubwa sana. sasa unakuta dogo ana 1.9 lakini ukimtikisa vizuri kichwa unamkuta mweupe tu
 
Usishangae sana mkuu mpaka ma professor wetu wanaingia Agrey ili wawekewe whatsapp na kufunguliwa google account
 
Miaka hiyo na sasa ni tofauti wakuu, tusikae kuwaza tu kua serikali inajitekenya na kucheka yenyewe.

Hebu fikiria upatikanaji wa vitabu na vifaa vya shule ilivyo rahisi kwa sasa. Pia wingi wa shule na wanafunzi kunafanya hata urahisi wa kupata maarifa mapya toka shule mbalimbali.

Siku hizi kuandaa mitihani ya kujipima shuleni ama shule na shule ni rahisi na inafanyika mara kwa mara, kitu ambacho kinasaidia sana ufaulu.

Maswali kwenye mtihani wa mwisho hayatoki mbinguni, ni walimu hao hao ndio hutunga na mengi ni hayo hayo ambayo wanafunzi wanayafanya kwenye mitihani ya kujipima kila leo, na maswali mengi yanajirudia rudia.

Sasa hiyo miaka ya zamani shule zilikua ngapi?? Vifaa vya kiada na ziada vilitosha ama vilikua vinapatikana kama sasa?? Vipi elimu kupitia mitandaoni mliweza kuipata.
Mwisho hizo one kali kabisa inawezekana kabisa ukizingatia saivi elimu ni biashara, so wamiliki wanafanya kila njia mwanafunzi apige freshi shule ipae.
 
Wewe jua tu zimepatikana kihalali, mengine waachie wenyewe yasikuumize kichwa...
 
Zile one simple sana kizipiga mkuu. Ungesoma english medium ungepiga tu. Alafu inaonekana hata watoto wako home work ufuatilii home work. Mtoto wa darasa la nne anasoma science ya form three kwann usipige one?
Mkuu umetia chumvi nyingi. Kama topic gani ya science ambayo mtoto wa darasa la1V anaisoma au anaweza kujibu maswali yake ambayo form 3 anaisoma. (Kumbuka masomo ya science ni Maths, Physics, Biology, na Chemistry). Hata ukiweka Geography. Shule za msingi masomo niliyotaja isipokuwa maths ni somo moja linaitwa science.
 
Chukua mtihani wako was 99 au 98 kwenye "review" halaf MPE mtt yeyote kama akiushindwa then conclude kwamba wanabebwa
 
Div. Kipindi cha maggu ziliwekwa kumfurahisha tu ila ukweli vijana ni watupu mno wengi ni wafuasi wa nyau fc (mbumbumbu)

Shule niliyosoma haijawahi kuwa na dv 1 zaidi ya 20 kwa mwaka mmoja ila chini ya maggu ilipiga 1 zaidi ya 40 tena wakiwa wamekaa likizo ya korona zaidi ya miezi 2 nikajua n katika kumfurahisha mwamba
Hilo bichwa lako ni kabati la meno tu
 
Mkuu umetia chumvi nyingi. Kama topic gani ya science ambayo mtoto wa darasa la1V anaisoma au anaweza kujibu maswali yake ambayo form 3 anaisoma. (Kumbuka masomo ya science ni Maths, Physics, Biology, na Chemistry). Hata ukiweka Geography. Shule za msingi masomo niliyotaja isipokuwa maths ni somo moja linaitwa science.
Chumvi gan wewe somesha watoto utaelewa one izo possible
IMG_20210926_190955_994.jpg
IMG_20210926_191005_570.jpg
 
Kama sikosei, enzi zetu A ilikuwa inaanzia 81%, B 61%, na C 41%. Kwa sasa kuna uwezekano A inaanzia 70%.
 
Hapana. Msiwaonee wivu watoto wenu. Div. one siku hizi haiwezi kuwa ngumu kama zamani hata kama mitihati ni kiwango kama cha zamani. Zamani zetu unaenda shule hata kiingereza hatujui. Miaka yote ya miwili ya kwanza tunakimbizana kujua lugha, ndo uanze kukazana na shule.

Siku hizi watoto wengi hasa waosoma hizo shule za akina St. Fransis, Feza Boyz, Minian n.k wamepitia shule za English Medium. Hawa kwao lugha siyo tatizo. Ukiangalia syllabus za hawa vijana kuanzia darasa la V wanasoma ile sayansi ambayo mimi na wewe tumeikuta form II na III.
 
Back
Top Bottom