Siku hizi vijana wanafaulu sana, nini kinachangia?

The ice breaker

JF-Expert Member
Apr 20, 2023
543
1,163
Bonjour

Siku hizi imekuaje naoana madogo wanapiga sana mabanda ya kutosha, Yani division one za single digit zimekuwa nyingi sana.

Yani tofauti na miaka yetu, ukipiga one utajulikana mpka ofisi ya wilaya, ila now days daaa madogo wanafahuru sana.

Kuna mdogo wangu kanipigia Banda za kutosha ana A zote za PCM, duuu.

Miaka yetu kwanza ukipiga tu division ni respect sana, yani ilikuwa sio kawaida, tofauti na miaka hii ya Hawa watoto wa Kizimkazi.

Sasa najiuliza Hawa madogo wanasoma sana au ubora wa Elimu upo juu tofauti na zamani.

Nakumbuka mwaka wangu, mm nilipiga two ya mwanzo, matokeo yakarudiwa tena, nikabahatika kula one ya mwisho, nikala chuma changu Cha PGM daaa.
 
Miundombinu ya elimu imeboreshwa kwa kiasi chake. Hizo enzi zenu shule za advance zilikua chache sana. Kwa mkoa mzima, zilikuwepo moja au mbili. Sasa mkifaulu wengi mtapelekwa wapi?

Chuo kikuu ilikua ni hapo mlimani. Admission capacity haizidi watu elf 20, mngewezaje kufaulu wengi?

Sasa hivi kila kata ina shule ya sekondari, na ndani ya wilaya moja kuna shule kibao za advance. Lazima NECTA walegeze. UDOM pekee inaweza kubeba wanachuo zaidi ya elf 50, vijana wasipofaulu madarasa yatabaki kufugia popo!

Siku hizi mtoto anaweza kwenda shule, akarudi nyumbani kula chakula cha mchana na akarudi tena shule kwa masomo ya jioni. Enzi zenu safari ya kwenda shule tu asubuhi ni masaa matatu, lazima mshangae watoto wakifaulu sana sasa hivi!
 
Watoto wana akili na pia wanasoma vitu vinaeleweka sisi tulikua tunasoma vitabu vya Juma na Roza sijui Kibanga ampiga Mkoloni wakigeuka sijui fikiri kabebwa na Jogoo huku Sadiki akili za kufauru utazipata wapi kesho asubuhi mwalimu anaamka na msizwa kageuka jiwe ndio hao wapo wizarani huko Wachina na Mabepari ya Magharibi yanawaletea mikataba ya hovyo hovyo na wanakubali na kusaini bila hata kusoma baadae Wananchi wakipiga kelele wanastuka haa huu mkataba haupo sawa mambo ya sadiki mimi masikini hayo..
 
Lishe Bora ya kujenga ubongo

Walimu wazuri

Miundombinu mizuri

Umri wa kuanzia shule mdogo zamani jitu Lina miaka 15 ndio linaanza darasa la kwanza

Watoto kusoma muda mwingi badala ya kufanya mikazi kama kilimo nk

Shule kuwa karibu mtoto hachoki kutembea umbali mrefu anafika Darasani akiwa Hana uchovu

Wazazi kuwa na mwamko wa elimu na kuhamasisha Watoto kusoma tofauti na zamani

Uwepo wa vitabu vya kutosha vya masomo yote
 
Not education performance but any form of performance in life is well improve as time go. Education, music, sports, technology list to the Moon....talking education itself their infrastructure improved as well as human resources there which trigger a big result.

Believing that education High performance is a sign of declining our education you have a problems in your mind.
 
Back
Top Bottom