hayo yote hayahusiani na misimamo yangu ya kutotaka kuwa mtumwa kwa mwanaume, ila kwa taarifa tu ndoa yangu ni ya kanisani
Nauliza hivyo ili nikuweke sawa, hayo mawazo ya hao unaosema wana support na kusema "mimi naachana nae" wengi hawana ndoa wala hawajui kwenye ndoa kuna nini tena wala ilo swala halijawahi kuwatokea, ivyo wao uzani ndoa ni kama u boyfrnd na u girlfnd kikitokea hiki ama kile namuacha. Watu wana ndoa wanafamilia (watoto), walifunga ndoa halali na wameshajijenga na mtu kaomba msamaha usifikiri hata siku moja kwamba kuna urahisi wa kuachana, labda useme utaikimbia nyumba yako ila si simple kama mnavyodhani, achana na fikra za hao wenye mawazo ya u boyfrnd na u galfnd ama watu walioingia ndoani jana ambao hawajajijenga na hawana familia mbele wala nyuma. Ndoa ni zaidi ya lile linaloitwa tendo la ndoa pale kitandani, Jaribuni pia kuwaza zaidi ya pale kitandani
Kama umeoa mkeo ana tabu sana ila kama bado namuhurumia huyo mtarajiwa
We nijibu tu hayo maswali ya msingi ili nikuweke sawa,, wala usiwe na hasira za kutaka kushambuliana kwa maneno, humu hatujuani so we should respect each other, na kama hakuna lililo sahihi ktk maelezo yangu likosoe kwa hoja tatizo mabinti wengi huingia kwenye ndoa pasipo kujua ndoa ni nini ila usukumwa na pressure za kuona mtu kaolewa ama rafiki na wakati mwingine kiu yao ya kutaka kuonekana wana share kitanda ki halali na mwanaume
Nafikiri wanaume wengi ndo hawajui maana ya ndoa wanaoa tu alimradi umri umefika na anahitaji mwanamke ndani wa kumzalia watoto, usitake kuniambia maana ya ndoa kwa mwanamke ni kuvumilia mumeo anapozini nje
Don't get me wrong, soma thread ya mtoa uzi. Alimfunia mwenzie ofisini tena mara moja wakaombana msamaha ila yeye tu amepoteza hamu, mimi si support uzinzi hapa, ila naongea hali halisi ya tukio, jinsi wengi wasivyojua ndoa ni nn?? Sasa ebu nijibu hayo maswali yangu ya msingi hapo juu ili Tuwekane sawa.
Sinimeshakujibu kwamba nimeolewa ndoa ya kanisan
Ndoa yako ni ya muda gani??Je mmejijenga kimaisha na mna watoto atleast wawili?
Tuna miez 6 tu
Sina mpango wa kuolewa mara ya pili kama hii itanishinda
Sasa uoni kua unajidanganya kama uliweza kujawa wivu na maumivu kwa kuona mumeo kafanya mapenzi na mwanamke mwenzio, huo unaonekana ulikua ni wivu wa kimapenzi yaani ulikua unaumia kwanini unachopewa wewe apewe mtu mwingine..Je unaposema hutaolewa tena utaweza kukaa na kuishi bila mwanaume???na Ule wivu ulitokea wap???Na kwanini ulishindwa kuishi bila mwanaume hapo kabla na ukaolewa na uyo wa kwanza??Mi nadhani sasa utaamini nilivyosema kua haya ni mambo ambayo watu humu uongea sababu hayajawakuta
Yani tunaweza kukesha hapa bila muafaka manake sielewi unachokiongea sana sana nabaki kukushanga na kuhis pengine hata ww hunielewi hivyo basi naomba hii topic tuifunge kila mmoja abaki na msimamo wake
Yani tunaweza kukesha hapa bila muafaka manake sielewi unachokiongea sana sana nabaki kukushanga na kuhis pengine hata ww hunielewi hivyo basi naomba hii topic tuifunge kila mmoja abaki na msimamo wake