Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,742
- 870,514
Mavi ya kale hayanuki.
Hii ni simulizi nyingine ya kweli way back 2007 Mwananyamala.. Bado nilikuwa single hivyo naomba nisipigwe mawe na wale wanaharakati wa baki na mmoja
Wanaopafahamu Royal bar usiku wanajua pana nini.. Kwa wale wasiojua palikuwa ni kiwanja kizuri kwa mawindo ya take away.
Nilifika pale usiku wa saa mbili pamejaa ila kwa bahati meza moja ya katikati ilikuwa na binti wa kiarabu na mhudumu mmoja tu... Nikawahi siti... Nikatoa na ofa za vinywaji mambo yakawa level kabisa... Lakini nikimwangalia yule binti.
Alikunywa reds mbili... Umri wake na mwonekano wake hakuwa kwenye list ya take away au walau kufanania nao.... Kwenye mazungumzo nikaja kugundua ndio kafika dar toka Tanga na dadaake ndio kamdamp pale... Dadaake anafahamiana na yule mhudumu na dadaake by then alikuwa mbongo muvi
Nilikomaa na kukaza mpaka tukaondoka wote... Nilikuwa naishi mitaa ya Tiger nikiwa nimepanga nyumba nzima na kwa wiki ile nilikuwa pekeyangu pale nyumbani... Nyumba ya geti ma ma grill... Niliingiza gari.. Nikafunga geti vizuri. Nikamkaribisha ndani na kufunga milango na magrille yote vizuri... Sikutaka kumuamini kwa asilimia mia... Nikamkaribisha chumba cha wageni alale hapo
Kulipopambazuka nikampitisha royal lakini akiwa na wasiwasi sana kuhusu dadaake kuwa angemuwakia... Nilijitambulisha kwake na kujieleza.. Alikuwa bado ana mavune na uso wa pombe nadhani alikesha club..... Nikaondoka job lakini ndio kama hivyo nikawa nimeshapata mchumba
Siku moja nikiwa Meeda bar Sinza nikampigia simu aje.. Kwanza akachelewa lakini kuna kipindi akawa hapokei simu na mwisho ikawa haipatikani... Story yake ni kwamba walikuwa Royal na dadaake na wanaume 3... Kumbe mmoja anamtaka.. Kwahiyo walipotoka pale yeye aligoma kwenda wanakotaka akafanya fujo mpaka wakamshusha lakini tayari akiwa kachaniwa blauzi yake.. Ni kweli ilikuwa imechanika na ilibidi tununue nguo kwenye boutique moja jirani
Jamani chondechonde nawaambia KITI HAPIGWI... mimi nikaanza gubu la kutomwamini anachoongea... Pombe yake ni redds... Mimi nilikuwa nameza grants bapa... Lakini ghafla akaanza kuibugia... Nikatoa mimacho.... Akaimaliza yote tukalipa tukaondoka... Tulipofika kwenye gari akasema tusiende nyumbani.. Hajisikii kwenda huko bali tutafute gesti... Tukapata Blue gesti haiko mbali na Meeda karibu na kanisa Katoliki kuja kutokea playtime au Igongwe
Baada ya kulipia chumba, tukaacha gari na kutoka nje kulikuwa na kipub, pale tukagonga tena bapa ya grants.. Nikasema leo...!!! Sijui...!!!
Tukarudi ndani.. Tukatinga chumbani mlango ukafungwa akatupia funguo mezani.. Ile gesti ilikuwa na vyumba vikubwa na vidogo sisi tulichukua kikubwa chenye masofa kabisa na tv chogo kubwa tu.. Kitanda 6x6 madirisha la aluminum makubwa yenye mapazia marefu, sabuni spesho sio kipande na ndala za rangi moja bila V
Tukiwa chumbani nikalianzisha tena... Ila akatoa msonyo huo sijapata kuusikia popote tangu kuzaliwa.. Pombe zikaniambia usikubali kusonywa na mwanamke... Loh nikaachia kelebu ya ukweli... Dunia simama nishuke... Akapepesuka kidogo.. Kisha akapata balance.. Akanijia kwa force kweli.
Kabla sijamuwahi nikatandikwa kofi la ukweli sana mpaka nikaona nyota nyota... Sijakaa sawa lingine na lingine na lingine.. Nikawa natafuta uvungu wa kitanda ulipo.. Natambaaa... Muda wote huo anasema.... Kiti HAPIGWI.. Kiti kakukosea NINI.. Kakunyima nini... Kwanini humuamini KITI... Kiti HAPIGWI.. Uwaa kofi.. Kiti HAPIGWI uwaa lingine.. Nikajaribu kusimama nikarushwa mpaka kwenye sofa..
Hapa sasa nikajua huyu ninayepambana naye sio yeye.. Kwa mwili wake ule na wangu asingeweza kunisulubu kiasi kile.. Nilikuwa natamani kupiga kelele za msaada lakini nikaona nitachekwa sana... Akili ziliponirudi nikajua kiti ni nani... Nikakimbilia funguo nitimke akaniwahi nikarushwa mpaka kitandani
Nikasema sasa hapa akija kwa juu akanikalia nimekwisha.. Alivyokaribia nikamkwepa na kumuwahi akawa chini niko juu... Nilifanya hivyo huku naomba samahani nyingi sana nafikiri zilifika 30 kwa dakika....
Samahani zile huku nikiwa nimemkandamiza kitandani zikaanza kumlainisha na taratibu akaanza kushusha pumzi huku sura yake halisi ikirudi. Mpaka akatulia kabisa na kulala usingizi mzito... Mimi sikulala mwili ulikuwa unauma wote.. Pombe zimekata kabisa.... Alikuwa akijigeuza kidogo tu nashtuka....
Nilikaa macho mpaka alfajiri nilipopitiwa na usingizi
Niliamshwa na mhudumu aliyeleta breakfast... Kuniona tu akawa ananipa pole huku anatabasau kumbe ule mziki wa usiku waliusikia wote.. Kuna baadhi ya madirisha yalikuwa wazi lakini yakawa yamefunikwa na mapazia
Alipokuja amka alikuwa hoi sana na kwa mtazamo tu hakujua kabisa kilichotokea jana yake.... Ilinichukua zaidi ya miezi karibia 5 kuja kumsimulia kilichotokea siku ile