Simulizi ya maisha na upelelezi: Ishini badala yangu wanangu

Simulizi ya maisha na upelelezi: Ishini badala yangu wanangu

Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715

Sehemu ya 13

"Nimegundua Njia ya kufanya ili kumbukumbu zako zirejee haraka. Inaonekana kumbukumbu zako hazipo mbali". Alisema Inspekta Jasmine akitabasamu zaidi. Njia iliyomjia akilini ilimfanya afurahi.

"Njia gani hiyo Afande?". Kinje akauliza huku akiweka umakini kuisikia njia hiyo

"Ngoja nitaisema Abuu akiwa pamoja nasi. Si unaweza kutembea?" Kinje akajibu kwa kutikisa kichwa kuashiria anaweza.
"Twende katika wodi alipopumzishwa Abuu sasa hivi"

Kinje akanyanyuka haraka akaambatana na Inspekta Jasmine kuelekea Abuu alipo. Wakazipita wodi kadhaa kisha wakaingia kwenye wodi moja.
Abuu akiwa juu ya kitanda alipomwona Kinje alitabasamu. Katika mkono wake wa Kushoto alifungwa kitambaa cheupe pamoja na mguuni pia.

"Ah Kinje. Nilikuwa na hofu sana juu yako mdogo wangu". Alizungumza Abuu kwa upendo. Macho yake yalionyesha wazi kumjali mdogo wake.

"Nipo sawa Kaka' vipi kuhusu wewe?"

"Ni mkono na mguu tu umeshtuka, ndani ya siku mbili tatu hizi nitarudi kwenye hali yangu kabisa. Vipi Inspekta taarifa mpya ipo?" Alisema Abuu huku akimtazama Inspekta Jasmine

"Kuna wazo limenijia ndiyo maana nimekuja na Kinje hapa. Kuna kitu kakumbuka leo. Ni kuhusu ile siku anatoka Zanzibar. Wale watu waliowasababishia ajali asubuhi ya leo amesema alipanda nao boti moja siku ile anakuja Dar es Salaam. Nimegundua kwamba kumbukumbu zake zipo njiani kurejea. Na akiyaona mazingira ambayo aliyaishi hapo kabla au watu ambao hawakumbuki inamsaidia kukumbuka vya nyuma kwa wepesi zaidi. Mfano alipowaona wale vijana wawili waliokuwa wanawafwatilia kumbukumbu ya wapi aliwaona ilimrejea"
Alieleza Inspekta Jasmine

"Sasa ni njia gani hiyo umegundua Afande?" Aliuliza Abuu.

"Nakumbuka uliniambia Kinje anaye mke. Naona ni vyema nikaambatana naye kuelekea Zanzibar" Inspekta Jasmine akaweka tuo kwanza, akawatazama Abuu na Kinje kwa zamu kisha akaendelea...
"Nadhani akimwona mke wake anaweza kukumbuka mengi zaidi. Hivi sasa si bado hakumbuki kama ana mke?" akauliza huku akimtazama Abuu. Abuu akajibu kwa kutingisha kichwa juu na chini.
"Ngoja tujaribu hii plani" Alisema Inspekta Jasmine.

"Mpango mzuri sana huu Afande. Wewe ni Genious sana yaani. Tena mngeenda leoleo Afande au unaonaje?" Alishauri Abuu. Kama Abuu na Inspekta Jasmine walikubaliana kwa pamoja basi Kinje hakuwa na budi kukubaliana nao pia

"Sasa tutaendaje huko wakati hata sipakumbuki?'' Kinje akahoji. Wote wakatazamana

"Hapo ndio changamoto ilipo. Hivi Abuu si ulisema huwa unawasiliana na Mke wa Kinje? Hebu tupe namba yake itatusaidia" Inspekta Jasmine alisema.

"Afande ujue kinachonishangaza ni tokea siku ile Kinje alipopatwa na haya kila nikijaribu kumpigia mkewe hadi leo namba yake haijawahi kuwa hewani. Nilitaka nimfahamishe pia hali halisi ya huku lakini ndo hivyo huwa simpati. Sijui alibadili namba? Hata kwenye simu ya Mme wake hakuwahi kumpigia zaidi tu ya usiku wa ile siku Kinje alipowasili Dar" alieleza Abuu

"Looh. Hili nalo tatizo. Halafu uliniambia Kinje alimwacha kule akiwa ni mjamzito?" aliuliza Jasmine huku akiongeza umakini kidogo. Alishaanza kuhisi jambo la tofauti kidogo kuhusu mke wa Kinje.

"Naam. Kinje aliniambia mkewe ni mjamzito, lakini nyumbani kwao napakumbuka vizuri. Ngoja nikuelekeze namna ya kufika kwao"
Abuu alianza kumwelekeza Inspekta Jasmine namna ya kufika ilipo nyumba ya Kinje. Baada ya maelekezo Kinje na Inspekta Jasmine wakamuacha Abuu pamoja na Askari mmoja wa kumwekea ulinzi
Maandalizi yalifanyika mchana huohuo kwa ajili ya safari ya kuelekea Zanzibar ilipo nyumba ya Kinje..
Nyumba ambayo mwenye nyumba hakuwa anaikumbuka nyumba yake. .

Majira ya Saa kumi Jioni Kinje pamoja na Inspekta Jasmine wakaianza safari ya kuelekea Zanzibar kwa kutumia usafiri wa Ndege kutoka shirika la ndege la Air Tanzania. Safari ile iliwachukua takribani nusu saa tu ndipo wakawasili Zanzibar. Kwa kufuata maelekezo waliyopewa na Abuu walielekea mtaa wa Jang'ombe. Baada ya lisaa limoja wakawasili mtaani hapo na kutua katika nyumba moja iliyozungushiwa ukuta mrefu. Nyumba hiyo ndiyo nyumba ambayo Kinje alimwacha mkewe kabla hajaelekea Dar es Salaam.
Kinje alipoitazama nyumba ile ni kama vile ilikuwa ikimkumbusha baadhi ya matukio, kila akiyapa umakini matukio hayo ndipo kumbukumbu hiyo inampotea. Kichwa kikaanza kumuuma kwa sekunde zipatazo kumi kisha hali yake ikakaa sawa.
Chozi likamdondoka baada tu ya kugusa geti jeusi la nyumba ile. Alimkumbuka Mkewe. Kumbukumbu ya mkewe kipenzi ilimjia

"Clara!"
Jina hilo lilimjia kichwani mwake.
"Ni Jina la nani hili?" Alijiuliza mwenyewe

Wakati huo Inspekta Jasmine alikuwa pembeni akitabasamu baada ya kugundua Kinje amemkumbuka mkewe. Akaamini kama ameweza kumkumbuka mkewe basi hata kumbukumbu nyingine zipo au zinakaribia kuja.

Kinje akajaribu kusukuma mlango mdogo wa geti aone kama umefungwa lakini lilionekana kuwa wazi. Alikumbuka haikuwa kawaida ya mkewe kuacha geti wazi. Iweje leo liwe wazi?
Wakaingia ndani huku akitangulia Kinje kisha Inspekta Jasmine akafuata nyuma. Nyumba ilionekana kupoa sana, Ni kama haikuwa na mtu wa kuishi ndani. Mbali na hivyo pia mazingira aliyaona ni tofauti sana na yale ya mwanzo kabla hajaelekea Dar es Salaam. Mazingira yalikuwa ni machafu sana.

"Mh mke wangu atakuwa wapi? Hii nyumba haionyeshi kama kuna mkaaji kabisa.... Clara mke wangu! darling''. Maneno yalimtoka Kinje mfululizo. Aliweza kuita kila jina alilowahi kumwita mkewe Clara lakini ukimya ulitawala..

"Hebu tujaribu kuingia ndani. Kwani hapa si kwako kabisa au ulipanga?" Inspekta Jasmine akahoji

"Hii nyumba niliijenga kwa pesa yangu mwenyewe. Sijaipanga wala kupangisha kwa kiumbe yeyote". Akajibu Kinje.
Walifika hadi mbele ya mlango wa chuma, mlango ambao ni wa kuingia ndani ya nyumba ya Kinje. Wakiwa tayari kwa kuingia ndani ghafla wakasikia mchakacho getini. Wote kwa pamoja wakageuka nyuma kutazama kuna nini.

"Mikono Juu wotee" Aliamrisha mmoja wa Polisi walioingia ndani ya geti. Walikuwa ni polisi wapatao watatu mikononi mwao walishikilia bastola zilizowaelekea Kinje na Inspekta Jasmine. Mbali na polisi hao pia alikuwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Jang'ombe.
Polisi mmoja akasogea kwa mwendo wa tahadhari, akamsogelea kwa ukaribu zaidi Inspekta Jasmine. Inspekta Jasmine taratibu akaushusha mkono wake kuupeleka katika mfuko wa koti alilovalia ili aweze kutoa kitambulisho chake awaonyeshe yeye ni nani. Hakufanikiwa kukitoa.

"Wewe we mwanamke. Usithubutu kufanya ujanja wowote nitamwaga ubongo wako" Alifoka Polisi aliyekuwa akimsogelea Inspekta Jasmine.
"Wote bonyea chini, mikono kichwani" polisi yule alizidi kuamrisha. Kinje alipiga magoti na kuiweka mikono yake kichwani haraka. Lakini Jasmine hakufanya hivyo.
Polisi yule akasogea zaidi nyuma ya Inspekta Jasmine aliyempa mgongo. Akajaribu kumpiga Inspekta Jasmine sehemu ya gotini ili aweze kupiga goti chini. Alienda yeye chini huku Inspekta Jasmine akibaki amesimama vilevile

"Yaani unaniangusha? Hahahahaha utanijua leo Mjinga wewe". Akafoka Polisi yule huku akizunguka kuelekea mbele ya Inspekta Jasmine. Sasa aliweza kumwona Inspekta Jasmine usoni. Akaangusha bastola yake chini huku akitetemeka

Inspekta Jasmine! Tafadhali nisamehe mkuu sikujua kama niwewe". Alisema polisi yule huku akielekea chini.
Awamu hii alipiga magoti yeye. Kinje akajitahidi kuzuia kicheko lakini ikashindikana. Akacheka kwa sauti ya juu baada ya kumshuhudia polisi yule akitetemeka mbele ya Inspekta Jasmine

Je nini kitatokea? Tukutane sehemu ijayo.

Ofa ya leo Jioni, Lipia Tshs 700 kwenda namba ya M pesa 0765824715 ili uweze kutumiwa yote. Ukishalipia nitext whatsapp kwa namba 0621249611
 
Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715

Sehemu ya 14

"Yaani unaniangusha? Hahahahaha utanijua leo Mjinga wewe". Akafoka Polisi yule huku akizunguka kuelekea mbele ya Inspekta Jasmine. Sasa aliweza kumwona Inspekta Jasmine usoni. Akaangusha bastola yake chini huku akitetemeka

"Inspekta Jasmine!" Alihamaki Polisi yule .
"Tafadhali nisamehe mkuu sikujua kama niwewe". Alisema polisi yule huku akielekea chini.
Awamu hii alipiga magoti yeye. Kinje akajitahidi kuzuia kicheko lakini ikashindikana. Alicheka kwa sauti ya juu baada ya kumshuhudia polisi yule akitetemeka mbele ya Inspekta Jasmine
"Usijali Andrea, ni mambo ya kawaida haya pindi uwapo kazini. Vipi Kuna usalama kweli? Maana naona mmekuja na mabunduki kwa kasi katika nyumba ya watu" Aliuliza Inspekta Jasmine huku akijitahidi kumtoa hofu polisi yule.

"Usalama upo Mkuu. Tulipokea taarifa kutoka kwa wananchi wa hapa kwetu kwa kushirikiana mwenyekiti wa mtaa kuhusu utoroshwaji wa mali za humu ndani, tukajaribu kupeleleza kama ulivyotutaka Mkuu, ndipo tukagundua kumbe yule mwanamke alikuwa anavitorosha na isitoshe alitaka kumwibia mumewe ili akimbie." Alizungumza polisi yule aliyejulikana kwa jina la Andrea. Kinje aliposikia maelezo haya aligwaya.

"Alitaka kuniibia? Kivipi aniibie wakati ni mke wangu?" Kinje aliingilia kati.

"Aliulizwa na majirani mbona anafungasha vitu vya humu ndani kama anahama? Akadai mmehamia Tanzania Bara hivyo hamtaishi tena hapa Jang'ombe, alidai kapokea simu kutoka kwa mumewe. Mwenyekiti wa mtaa alipojaribu kukutafuta kwenye simu hukupatikana, ikabidi azuiliwe kuondoka hadi wewe uthibitishe hilo. Majirani pamoja na mwenyekiti walipomzuia walitokea vijana wawili kuja kumsaidia wakatoroka kuelekea kusikojulikana. Tumejaribu kupelelez na kufwatilia ni wapi alielekea lakini hatujafanikiwa" Andrea alieleza
"Huyu mwanamke alitaka kuniibia mshenzi huyu, sikumpa hizo taarifa mimi, kwanza Dar nilienda kumwona mgonjwa na si kuhamia. Ina maana kabeba kila kitu changu?" Alilalama Kinje huku akijaribu kuusukuma mlango ule wa chuma. Ulifunguka, akaingia ndani hadi sebuleni
Huko akakutana na ukaribisho mwanana wa sebule iliyonuna. Kila kitu kilibebwa na kubakia tu makochi na baadhi ya mapambo ya ndani. Vitanda, kabati, Tv na hata nguo zake pia hazikuwemo.
Nyumba ilisafishwa ikasafishika haswa

"Tutaanza na huyo mkeo. Bila shaka kuna jambo limejificha nyuma ya pazia". Alisema Inspekta Jasmine aliyekuwa nyuma ya Kinje. Kinje akageuka kumtazama

"Jambo lipi hilo Inspekta?"

"Kuna vitu kila nikivitafakari haviniingii kabisa akilini. Mkeo simu ya mwisho kukupigia ni usiku wa siku ile ulipofanyiwa upasuaji na kuibiwa figo. Baada ya hapo hakuwahi kukupigia tena. Umesema yule ni mkeo?..." aliuliza Inspekta Jasmine huku akimkazia macho Kinje. Kabla hajampa nafasi ya Kujibu Kinje alianza kuelekea mlangoni atoke nje. Mara akasita kidogo kisha akamgeukia Kinje.
"Kama ni mkeo basi angepaswa kukutafuta ajue ni kwanini umekuwa kimya ghafla tangu uelekee Dar es Salaam,. Mbali na kukupigia basi hata simu yake ingekuwa hewani asubiri labda wewe umpigie. Lakini hakuwa hewani, simu alizima. Kwa maelezo ya Abuu ni kwamba kila siku alijaribu kumpigia ampe habari kukuhusu lakini hakumpata. Inaonyesha alipoona umeondoka naye akaondoka. Swali la kujiuliza ni kwanini aliondoka baada ya wewe kuelekea Dar na hadi kuibiwa figo? Huu mpango wa kuibiwa figo alishiriki kuupanga na isitoshe siamini kama yule alikuwa na mapenzi ya dhati nawe. Hebu niambie ulikutana nae katika mazingira yapi hadi mkaoana?" Aliuliza Inspekta Jasmine

Kinje alivuta pumzi ndefu, akaitoa taratibu kisha akampa mgongo Inspekta Jasmine. Akaanza kueleza ilikuwaje...

Mimi na Clara tulionana mwaka mmoja uliopita. Nakumbuka ilikuwa ni jioni moja nikiwa katika kufunga biashara yangu sokoni niweze kurejea nyumbani ndipo Clara aliponijia. Nilidhani alikuwa ni mteja pindi nilipomuona, lakini haikuwa hivyo. Alidai yeye ni mgeni hapa Zanzibar na hana mwenyeji. Alihitaji tu nimsaidie kumpata dalali wa nyumba za kupanga ili aweze kupangisha chumba. Ni hilo tu, alimtaka dalali. Nikaona mbona hii fursa sasa? Tangu asubuhi biashara haikuwa nzuri siku hiyo hivyo nikaona ni vyema mimi ndio niwe dalali ili nipate angalau ile pesa ya udalali.

'Hapa umefika Dada. muhimu hesabu chumba ushakipata'. Nilimwambia
Nikamtaka anisubiri hadi nifunge biashara yangu, na baada ya hapo tukaongozana hadi katika nyumba moja kubwa maarufu hapa Jang'ombe iliyosheheni wapangaji wengi. Nyumba hiyo haipo mbali sana na kwangu, ni mwendo wa kama nusu kilometa tu kutoka hapa nyumbani.
Pale nilimpeleka nikazungumza na mwenye nyumba, baada ya chumba kupatikana nikafanikiwa kupata hela yangu ya udalali.
Baada ya Clara kupata chumba pale haikuishia hapo tu. Ukaribu kati yangu na yeye ukazidi kuwa mkubwa na mara nyingi hatukusita kutembeleana. Pia mara kwa mara alifika katika biashara yangu na alikuwa mteja mkubwa sana kwangu.
Baada ya mwenzi kupita siku moja aliniomba kama itawezekana aungane nami katika biashara yangu. Alinionyesha mtaji wake ambao ilikuwa ni shilingi laki Tatu. Sikusita kumkubalia maana biashara yenyewe haikuwa na mtaji mkubwa kwa upande wangu.
Kwa kuwa sikuwa na mke wala mfanyakazi basi tulifanya biashara ile ya viazi pamoja na Clara kwa uaminifu mkubwa sana. Kuna wakati mimi nilikwenda mashambani kwa wakulima kutafuta viazi nikamwacha yeye aendelee na biashara sokoni. Hivyo tulizidi kuwa karibu zaidi na zaidi. Na tulizoeana kama marafiki tu.

Nakumbuka siku moja majira ya saa tatu usiku alifika nyumbani kwangu. Siku hiyo nilikuwa mgonjwa hivyo sikuweza kwenda sokoni pamoja naye.
Usiku huo alifika kunijulia hali na pia kuleta mahesabu ya mauzo ya siku hiyo.
Siku hiyo baada ya kukamilisha mahesabu kabla hajaondoka nakumbuka aliniambia hivi..

"Sasa Kinje tumeshazoeana na kujuana tabia zetu kadha wa kadha kwanini tusiishi pamoja kuliko mimi kuendelea kuishi kule nalipa kodi kubwa na isitoshe hiyo pesa nayoilipa tunaweza kufanyia mambo ya maana? Pia kama hivi unaumwa nadhani nikiwepo wala hutahangaika sana, utapata muda wa kutosha kupumzika."

Haya mawazo niliyapa uzito na kwa kiasi fulani, nikaona kama ni wazo zuri hili, tena tukiishi pamoja tutaweza kubana matumizi na kufanya mambo ya maana. Isitoshe pia nilishaanza kumtamani kwani Clara alikuwa ni msichana mzuri akichangizwa na weupe wake wa asili hivyo nilikubaliana naye.
Baada ya siku mbili hivi hali yangu ikawa sawa ndipo tukasaidiana kuvileta vyombo pamoja na nguo kutoka nyumba ile aliyopanga na kuleta hapa kwangu. Tukaanza kuishi pamoja lakini kila mtu chumba chake. Alikuwa ni mwanamke mwenye mitego sana kila mara tukiwa nyumbani. Alikuwa mkarimu, mpole, mstaarabu na mwenye sauti ya kudeka pia pindi tuwapo pamoja. Lakini pindi tuwapo sokoni alikuwa ni mpambanaji haswa na pia alikuwa makini na kazi yake.
Hii ikanifanya kuvutiwa naye. Na baada ya majuma kadhaa uzalendo ukanishinda, tukaanza kuishi ndani ya chumba kimoja, kitanda kimoja na shuka moja pia.
Japokuwa historia yake ya nyuma sikuwa naifahamu alipotokea lakini upendo na uaminifu vilitawala kati yetu na hivyo tukawa kama mke na mume japo bila ndoa. Tulianza harakati za kufunga ndoa ya kiserikali lakini kwa bahati mbaya likatokea tatizo.
Julieth ambaye ni mtoto wa Abuu Kaka yangu alipatwa na maradhi ya figo.
Tulipaswa kumsaidia ndipo mimi nikaonekana kuendana vinasaba kati yangu na Jenifer.
Kinje alieleza
"kwanini julieth na Kinje damu zao ziendane wakati Kinje si baba yake? Bila shaka kuna jambo limejificha hapa" aliwaza Inspekta Jasmine.

"Mlipokuwa mkiishi pamoja vipi kuhusu mawasiliano yake ya simu yalikuwaje?" Aliuliza Inspekta Jasmine. Muda wote Kinje akieleza, yeye alikuwa akiyarekodi maelezo yake kupitia simu yake

"Hilo ni jambo ambalo mara nyingi tulikuwa tukigombana sana. Tuliishi kwa upendo mkubwa sana lakini ugomvi wetu ulikuwa ni pale ninapoigusa simu yake" Kinje alisema.

Je! Ni kipi kimejificha nyuma ya pazia? Inspekta Jasmine amehisi jambo gani kutoka kwa Clara?
Tuwe wote katika sehemu ijayo. Pia vipande vyote vilivyosalia vinapatikana kwa ofa ya Tshs 700 tu. Lipa kwenda kwenda M-PESA namba 0765824715 kisha njoo inbox kwa namba 0621249611 nikutumie
 
Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715

Sehemu ya 15
"Hilo ni jambo ambalo mara nyingi tulikuwa tukigombana sana. Tuliishi kwa upendo mkubwa sana lakini ugomvi wetu ulikuwa ni pale ninapoigusa simu yake" Kinje alisema.
"Clara hakutaka kabisa niishike simu yake japokuwa simu yangu aliishika. Hii ikanipa wasiwasi wenda anachepuka, lakini haikuwa hivyo. Clara hakuwahi kwenda mahali bila ya mimi na pia sikuwahi kusikia hata skendo kumhusu yeye kwa kipindi ambacho nilienda kutafuta bidhaa. Sijui ni kwanini alikuwa akificha simu yake, lakini hilo ni jambo ambalo mara nyingi tulikuwa tukigombana sana"
Kinje alizidi kueleza

"Sasa ngoja nikufahamishe jambo fulani kama ulikuwa haufahamu. Huyo Clara nilianza kumchunguza tangu siku ile umepoteza kumbukumbu zako baada ya kudungwa sindano kule Royal Hotel.katika kumfwatilia nimegundua huyo Clara kabla ya kukutana nawe alishaingia katika mahusiano na wanaume zaidi ya kumi na mbili, ukijumlisha na wewe ni wa kumi na tatu."

"Eti unasemaje! Clara huyuhuyu nimjuaye mimi au mwingine? Mbona alikuwa ni mwanamke mstaarabu sana yule?" Kinje aligwaya. Hakuamini kama anayoongea Inspekta Jasmine yana ukweli ndani yake.

"Ndio unisikilize sasa nikuambie ili upate kufahamu huyo mkeo alikuwa ni nani haswa. Ile siku kaka yako aliponiambia kuwa kila alipojaribu kumpigia Clara hakupatikana ndipo nilipoanza kumtilia shaka. Nilianza kumchunguza, nikawasiliana na wale askari wawili uliowaona mda si mrefu wanisaidie kufwatilia huku wakishirikiana na mwenyekiti wenu wa hapa Jang'ombe. Walipoanza kumfwatilia walikuta ameshahamisha kila kitu ndani kwako na kuondoka. Kiufupi nimeweza kugundua Clara alikuwa kikazi zaidi kwako na si kimapenzi na kibiashara kama unavyofahamu.
Clara alienda kwa mwanaume wa kwanza kwa ajili ya kutafuta kitu fulani hivi, lakini hakufanikiwa kukipata, akaenda na kwa mwanaume wa pili kukitafuta lakini kama ilivyokuwa kwa mwanaume wa kwanza hakukipata kitu hicho, akaenda kwa mwanaume wa tatu hadi wa kumi na mbili, wote hawakuwa na kitu hicho. Ila alipokuja kwako, ukamruhusu aingie katika maisha yako alifanikiwa kukipata kitu hicho"
Alieleza Inspekta Jasmine.

"Unaposema kwangu alikuja kufwata kitu nakuwa sikuelewi kabisa. Yaani unaniacha njia panda kwakweli. Ni Kitu gani hicho afande?" Kinje akauliza huku wasiwasi ukizidi kumtawala.

"Clara alikuwa ni miongoni mwa wanawake wengi waliopewa kazi ya kumtafuta mtu ambaye vina saba vyake vinashabihiana na vina saba vya mtu fulani. Hivo ili iwe rahisi kufahamu ni nani mwenye vinasaba hivyo basi yeye na wenzake walipaswa kuingia katika mahusiano kwanza na wanaume. Katika mahusiano kuna hatua ya kupima afya kwanza ili kila mtu amjue mwenzake yupo katika hali gani. Hivyo wanawake wengi baada ya kupima afya na wanaume zao hawakufanikiwa kupata walichohitaji, wakaendelea kuwatafuta wanaume wengine hadi apatikane wanayemhitaji.
Kwa upande wa Clara Wanaume wengi alidumu nao kwa mwenzi mmoja kutokana na kutokupata chochote baada ya vipimo. Alipokuja kwako aliona kama wewe ni kijana ambaye hadi akuteke kimwili ni kazi kidogo kutokana na biashara uliyokuwa ukiifanya. Ilimchukua mienzi kama miwili ndipo akakuteka kihisia ndipo mkaweza kuishi pamoja.
Japo hujaniambia kama mliwahi kwenda kupima afya yenu lakini najua mlifanya hivyo. Katika kupima kwenu majibu yaliyokuja yalimfurahisha maana vinasaba vyako vilifanana na vya mtu ambaye alikuwa akitafutiwa figo. Sasa baada ya hapo aliwasiliana na waliompa kazi akawataarifu kuwa amefanikiwa na hapo harakati za kukupata wakutoe figo zilianza. Mkiwa mnaishi pamoja si kuna kipindi ulikuwa ukimwona anafanya vitu kama anataka kuhama? Kama vile kupanga vitu kwenye begi badala ya sandukuni, kufua kwa ghafla manguo mengi na kadhalika" alisema Inspekta Jasmine.

"Halafu kweli aisee. Kuna siku nilipoamka nilikuwa nimechoka hadi nikashindwa kwenda kazini kwa sababu mwili ulikuwa dhaifu sana. Nahisi aliniwekea madawa ya usingizi kwenye chakula ili atimize adhma yake. Kumbe Clara alikuwa shetani!" Alisema Kinje kinyonge. Nguvu zile za kusimama zilimwisha, taratibu akajiegemeza.

"Ndio hivyo. Siku hiyo ilikuwa ni dalili ya kwamba ulitakiwa utolewe figo lakini ikashindikana. Alipokuja kusikia unatakiwa ukamchangie mtoto wa kaka yako figo basi hapo mpango wao walihisi kama utaharibika na ndipo wakafanya mpango wewe ukifika dar es salaam ulale hotelini ndipo wamtume mwanamke wa kukulaghai maana walishakufahamu ya kuwa wewe ni mwepesi sana kwa wanawake. Mpango wa kukupata ulifanikiwa na ndipo walipokutoa figo yako ikapelekwa kwa mtu huyo ambaye alikuwa na shida nayo" Inspekta Jasmine alizidi kueleza.
Kinje alibaki kinywa wazi akiwa haamini anachokisikia japo kilikuwa na ukweli ndani yake. Ilibidi akubaliane na hali ilivyo maana hawezi kubadilisha chochote kilichotokea. Wakati wakifikiri namna ya kufanya kwa wakati ule aliingia Andrea
"Mkuu, tunafanyaje sasa maana imekuwa ni ngumu kumpata yule mwanamke. Hatujajua bado atakuwa wapi maana tumepeleleza kila kona hapa Zanzibar." alisema Andrea baada ya kuingia ndani.

"Huyu mwanamke tutampata tu. Kwasasa inatupasa kwenda Tanzania bara katika hotel aliyoifikia Kinje siku ile. Kuna jambo nimelihisi". Alisema Inspekta Jasmine huku akimtazama Kinje.

"Hivi huyu mwanaume uliwahi kumwona mahali kati ya hapa Zanzibar au Bara?" Inspekta Jasmine aliuliza huku akisogeza picha Kinje alipo aweze kuitazama.
Macho ya Kinje yakagutuka kama vile yalikuwa usingizini. Ile taswira iliyo katika pichani ilimtia kiwewe.

"Huyu huyu si... Huyu nilimwona hotelini ile siku. Ile siku kabla sijaonana na Devotha nilimwona huyu mwanaume. Hiyo siku nilipokwenda kutafuta chakula nilisikia kelele za mwanamke akilalamika kubakwa. Alikuwa ni Devotha akilia. Niliposogea eneo lile nilimwona huyu mwanaume akimvutavuta Devotha. Na aliponiona siku ile alimwacha Devotha na kukimbia. Ni nani huyu mwanaume na picha yake umeitoa wapi?" Aliuliza Kinje huku akitetemeka kwa jaziba. Kiganja chake cha mkono kilichoikamata picha ile kililowa kwa jasho.

"Kwa hiyo uliamini kwamba huyu mwanaume ni kweli alitaka kumbaka Devotha ile siku?. Walikutegea ili wakupate baada ya kukuona ukitoka nje ya chumba chako." Alisema Inspekta Jasmine huku akirudisha picha ile katika mfuko wa koti alilovalia.

"Andrea utaendelea na uchunguzi hapahapa zanzibar, naamini huyu mwanamke bado yupo hapa zanzibar asakwe unguja na pemba yote hadi apatikane. Akipatikana bila shaka tutafahamu mengi ambayo bado hatujayafahamu." alisema Inspekta Jasmine huku akitoka nje. Nje alikutana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Jang'ombe akiwa pamoja na polisi wengine wawili.
" Mwenyekiti tunakushukuru kwa ushirikiano wako kwetu. Japo hatujampata huyu kwanamke lakini sapoti yako pia imetusogeza hatua kadhaa mbele." Alisema Jasmine huku akipeana mikono na mwenyekiti wa mtaa wa Jang'ombe. Waliagana na Mwenyekiti pamoja na Afande Andrea.
Usiku wa siku hiyo Kinje pamoja na Inspekta Jasmine walilala katika nyumba ya wageni hadi palipokucha alfajiri ndipo walipoianza safari ya kurejea Jijini Dar es salaam huku wakiacha msako mkali Zanzibar wa kumsaka Clara popote alipo. Hawakufahamu ya kwamba Clara jina lake halisi ni Delila.

"Clara na Devotha lazima wapatikane, lazima niwapate. Nikimpata mmojawapo nitapiga hatua kubwa sana. Nitawapata tu"
Inspekta Jasmine alijisemea mwenyewe akiwa ndani ya Ndege ya kukodi akirejea Dar es salaam.
Walipofika Dar es salaam walielekea kwanza moja kwa moja hadi Muhimbili hospital kuangalia maendeleo ya Abuu.
Abuu akaelezewa yote yaliyotokea huko zanzibar, akaachwa pale hospitalini na Askari wawili kwa ajili ya kumwekea ulinzi kwa wakati wote akiwa hospitali.
Sasa Inspekta Jasmine, Adrian Kaanan au ukipenda mwite Askari Kijana pamoja na Kinje waliongozana kwenda hoteli ya Royal kwa lengo moja tu. Kumtafuta Devotha. Uzuri ni kwamba Kinje amerejewa na kumbukumbu zake hivyo ni rahisi kumfahamu Devotha kama atamwona. .
Baada ya dakika chache kupita waliwasili Royal hotel na gari ndogo aina ya Land cruiser. Inspekta Jasmine moja kwa moja alielekea katika ofisi ya meneja akiwaacha Kinje na Adrian ndani ya gari.
Alikaribishwa hadi ofisini na meneja wa hoteli, wakaketi

"Nam meneja, kama nilivyojitambulisha hapo awali, Naitwa Inspekta Jasmine Wahab, Ni Inspekta wa Jeshi la polisi kutoka kituo cha polisi cha Kati. Nipo hapa kwa swala moja tu". .. alisema huku akimtazama mwanaume yule aliyevalia suti nyeusi ya gharama sana
"Bila shaka unalikumbuka tukio la tarehe 28 December, Ndilo lililonileta hapa Meneja" alisema Inspekta Jasmine. Aliuona mshtuko kutoka kwa meneja baada ya kumtajia tarehe ya tukio.

"Nalikumbuka vizuri Inspekta, kama nilivyosema siku ile huyo mwanamke aliyelala na Kinje si mfanyakazi wa hapa kabisa. Baada ya tukio lile tuliwaacha mpitishe uchunguzi wenu kwanza ili nasi tuweze kuwabaini wafanyakazi wa hapa walioshiriki kupanga jambo hili baya lililoichafua hoteli yetu kwa kiasi kikubwa sana". alisema meneja huku akijaribu kupepesa macho kushoto na kulia

"Meneja anaonekana kufahamu kitu. Bila shaka nikimchunguza vizuri nitapata chochote kutoka kwake" aliwaza Inspekta Jasmine.

Nini kitajiri? Sehemu ijayo si ya kukosa.

Ofa, ofa,
Jipatie vipande vyote vilivyosalia kwa Tshs 600 tu. Lipia kwenda M pesa namba 0765824715 kisha njoo whatsapp kwa namba 0621249611 nikutumie
 
Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715

Sehemu ya 16

"Meneja anaonekana kufahamu kitu. Bila shaka nikimchunguza vizuri nitapata chochote kutoka kwake" aliwaza Inspekta Jasmine.

"Sawa meneja. Sisi tunamhitaji mfanyakazi wako mmoja tuweze kuhojiana nae zaidi maana siku ya tukio aliagizwa kinywaji na huyo mwanamke aitwaye Devotha na pia walionekana kufahamiana." alisema Inspekta Jasmine huku akinyanyuka kutoka kitini.

"Haina shida afande, mnaweza kumchukua awasaidie. Si unamfahamu?" alihoji Meneja.

"Nikimwona nitamkumbuka. Nipe msaada wako wa kuwaita wafanyakazi wote wa kike wa hapa. Ni jambo la dakika moja tu" alisema Inspekta Jasmine.
Baada ya sekunde chache wahudumu wote wa hoteli waliokuwa zamu siku hiyo walikusanyika pamoja kuitikia wito wa meneja. Kila mtu alitaka kufahamu kuna nini maana haikuwa kawaida kuitwa kwa pamoja.
Wafanyakazi walianza kusailiwa na macho ya Kinje. Alimtazama mmoja mmoja ili aweze kumwona mwanamke yule aliyewaletea kinywaji siku ile akiwa na Devotha chumbani.
Alimwona. Alimwona. Kitendo cha kumtazama tu usoni mwake yule mwanamke aliyakwepesha macho yake kwa haraka.

"Yule pale". Kwa haraka Kinje alimfahamisha Inspekta Jasmine. Yule mwanamke alikosa utulivu kabisa. Mara kwa mara alimtazama meneja, Ni kama alisubiri meneja aweze kutia neno lolote.

"Tutaondoka naye huyu, atarejea leoleo meneja usiwe na shaka" alisema Inspekta Jasmine huku akimpa ishara Adrian. Adrian akamsogelea mwanamke yule na kumsihi aongozane nae kwenye gari. ,

"Usijali Merina. Tupo pamoja nawe katika hili"... Meneja alimtoa hofu mwanamke yule. Adrian akatangulia naye garini huku Kinje na Inspekta Jasmine wakifuata nyuma.

Baada ya tukio lile Meneja alirejea ofisini akiwa na wasiwasi. Alipofika ofisini aliketi kitini kisha akachomoa simu yake katika mfuko wa Suruali. Akatafuta jina lililohifadhiwa kama JJ na kupiga.

Upande wa pili Inspekta Jasmine akiwa ndani ya gari, upande wake wa kushoto alikaa Merina, binti waliyemchukua kutoka Royal Hotel. Siti za mbele alikaa Kinje, pembeni yake alikaa dereva. Adrian Kaanan alikuwa akiliendesha gari lile kuelekea Kituo cha polisi cha kati.
Wakiwa ndani ya gari, Inspekta Jasmine alikamata simu yake baada ya kutoa mlio mkali. Akaibofya kwa takribani sekunde sita, Akaiweka sikioni huku akijipongeza kwa jambo alilolifanya katika Ofisi ya meneja. Wakati ule alipoingia katika ofisi ya meneja wa royal hotel hakutoka hivihivi. Chini ya meza ya meneja alipachika kifaa kidogo mithili ya punje ya harage, kifaa hicho kilikuwa ni mahususi katika kurekodi mazungumzo yote yatakayoendelea ndani ya ofisi ile endapo ikitokea kutakuwa na mazungumzo ya simu. Kama meneja atazungumza na simu basi Inspekta Jasmine angefwatilia maongezi hayo kwa msaada wa Kifaa kile.
Kifaa hicho alipewa kama zawadi na mpelelezi mahiri nchini aitwaye Daniel Mwaseba baada tu ya kukamilisha kazi ya kurejesha nyaraka za siri zilizokuwa zimeibiwa kutoka serekalini. Mkasa huo ulipewa jina la Elizabeth Neville na mwandishi mmoja.
Na sasa alikuwa akiisikia sauti ya meneja kutoka katika simu yake kwa msaada wa kifaa kile alichopewa na Daniel Mwaseba. .

"Mambo yameanza kuharibika Bosi"
"Wametoka muda si mrefu hapa..... Ndiyo..... Ila wameondoka na Merina.
"Sawa nimekuelewa Bosi"

Inspekta Jasmine alisikia sauti ya Meneja ikizungumza. Hakubahatika kuisikia sauti ya upande wa pili. Inspekta Jasmine akatabasamu huku akijipongeza tena kwa kuacha kifaa kile ndani ya ofisi ya meneja. Walikuwa bado ndani ya gari, Waliiacha barabara ya Temeke na kuifuata barabara inayoelekea kilipo kituo cha Kati.
Adrian kupitia kioo cha pembeni aliweza kushuhudia gari ndogo aina ya Noah ikiwafuatilia. Akamtaarifu na Inspekta Jasmine. Wakati huohuo simu ya Inspekta Jasmine ilipiga kelele tena kwa mara ya pili, lakini hakugundua. Alikuwa makini kuitazama gari ile inayowafwatilia
Merina aligeuka nyuma kutazama baada ya kuona Adrian ameongeza kasi. Akakumbuka maneno ya bosi wake siku moja baada ya tukio la Kinje kutolewa figo.
"Siku utakayoufungua mdomo wako basi ndiyo siku utakayoaga dunia. Utakufa siku hiyo Merina" aliyakumbuka maneno haya Merina. Alianza kutetemeka kwa hofu

"Wataniua hao jamani nitakufa mimi" alisema Merina huku akizidi kutetemeka kwa woga, hakuwahi kuona mfukuzano wa magari kama alivyokuwa anaona leo.

"Usijali Merina hawawezi kukuua ukiwa katika mikono yangu. Unahisi kwanini wanataka kukuua?" aliuliza Inspekta Jasmine huku akimkazia macho Mwanamke yule anayefahamika kama Merina. Wakati huo Adrian alikuwa akizidi kukanyaga mafuta kwa ajili ya kuwapoteza watu wale wanaowafuatilia.

"Waliniambia siku nikisema nitakuf.."
Ghafla risasi ikapita pembeni kidogo ya sikio la Merina. Kioo chote cha nyuma ya gari kilipasuliwa vibaya sana na sasa sehemu ile ilikuwa wazi kabisa. Sasa waliweza kuonekana na wafuatiliaji vizuri.
Adrian alikuwa ni mtaalamu wa kucheza na barabara, ni mienzi michache tu ilipita tangu afundishwe na Daniel Mwaseba namna ya kulifanyia gari utundu pindi akimbizwapo na maadui. Alikumbuka sana siku hiyo akiwa na Daniel katika Misheni ngumu iliyopewa jina Mtoto wa Rais na Mwandishi mmoja. Siku hiyo walikuwa wakimfwatilia mtu mmoja, katika fuatilia yao wakajikuta wanawekwa mtu kati baada ya gari nyingine kutokea nyuma yao. Siku hiyo yeye ndiye alikuwa akiliendesha gari huku Daniel Mwaseba akiwa pembeni yake.
Leo hii yupo na Inspekta Jasmine pamoja na raia wengine wawili. Alipaswa kuruka mtego huu. Sasa alikusudia kuwapoteza maadui. Wakati huo Inspekta Jasmine hakuwa na hofu yoyote, alifahamu vyema uwezo wa Adrian katika wasaa kama ule. Ni Kinje na Merina tu ndio walikuwa na hofu. .

Adrian aliendesha gari ile mithili ya nyoka aliyepigwa rungu akijaribu kujiokoa. Gari nalo lilimtii na kuenda kwa staili ile ile ya nyoka. Barabara yote ilikuwa ni kama yake kwa jinsi alivyokuwa akiendesha. Alipeleka gari kulia na kushoto ili kuzikwepa risasi zinazopigwa kuja walipo.
Baada ya dakika mbili hivi palikuwa kimya, na muda huohuo kikasikika king'ora cha polisi kikilia. Zikafika gari za askari wa usalama barabarani na kuwazuia. Inspekta Jasmine akachomoa kitambulisho chake na kuwaonyesha askari wale.

"wabaya tumewaacha nyuma kule" Alisema Inspekta Jasmine huku akirejesha kitambulisho chake mfukoni. Askari wale wakaelekea kule walipoelekezwa na Inspekta Jasmine.
Simu ya Jasmine ilitoa tena mlio kwa mara nyingine. lakini kama ilivyokuwa kwa mara ya pili, hakuusikia mlio ule. Baada ya dakika sita waliwasili katika kituo cha Kati wakiwa na Merina pamoja na Kinje.
Bila kuchelewa Merina aliingizwa kwenye chumba kidogo tayari kwa kuhojiwa. Inspekta Jasmine akaingia akiwa na faili ndogo pamoja na kalamu

"Jina nani?"
"Naitwa Merina"
"Miaka yako?"
"23"
"Mnamo Tar 28 mwenzi wa kumi na mbili, majira ya saa 5 usiku ulipeleka kileo katika chumba alichokuwa mteja wenu ambaye nadhani umekwishamwona na unamkumbuka. Ndani ya chumba kile alikuwa na mwanamke mmoja na mwanamke huyo ndiye aliyekuagiza kileo kile. Unakumbuka siku hiyo?" aliuliza Inspekta Jasmine

"Ndi.. yo. . . na. . . nakumbuka" alijibu Merina akiwa na kigugumizi cha ghafla.

"Vizuri sana Merina kama unakumbuka. Ukweli wako ndio utakaokusaidia kukuweka huru, na pia sipendi watu watukutu. Yule mwanamke aliyekuagiza kinywaji siku hiyo unafahamiana nae vipi?" aliuliza Inspekta Jasmine

"Mmmh"

"Sipendi ujing Merina. Mmmh maana yake nini? Unamgunia nani hapa? Hapa tupo kitandani unaguna? Wewe ni bubu?" Inspekta Jasmine alifoka huku akiinuka kitini

"Wataniuaa" alisema Merina huku akitetemeka. Alianza kutokwa na machozi.

Inspekta Jasmine akamsogelea kwa karibu zaidi, akamtazama machoni.
"Hawatakuua, niamini. Upo katika mikono salama Merina. Naitwa Inspekta Jasmine. Jasmine Wahab."

Merina alishtuka sana kusikia jina lile. Ni wiki chache zimepita toka asome jarida lenye kisa kimoja kilichopewa jina 'Biashara ya Watoto' kilichoandikwa na mwandishi nguli wa riwaya za kijasusi nchini, katika kisa hicho aliweza kuisoma shughuli ya Inspekta Jasmine dhidi ya Jambazi mmoja aitwaye Malolo.
.
"Ah kumbe wewe ndio Inspekta Jasmine! Sikuwahi kuwaza kama nitakuja kuonana na mtu mkubwa kama wewe dada yangu. Ninakuahidi nitakueleza kila kitu bila kukuficha" Alisema Merina, uso wake ulijawa na furaha ya ghafla kukutana na Mtu mkubwa kama Inspekta Jasmine, na pia kuhojiwa nae.

"Ni mimi. Twende kwenye point ya msingi sasa. Unamfahamu vipi huyo mwanamke?" aliuliza Inspekta Jasmine huku akirejea kitini

Naam. Nini kitajiri? Tuwe wote sehemu ijayo.
Ofa,... Malizia simulizi hii kwa Kulipia Tshs 600 utumiwe yote. Lipa kwenda M pesa namba 0765824715 kisha njoo inbox kwa namba 0621249611 nikutumie chapu.
 
Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715

Sehemu ya 17
"Ni mimi. Twende kwenye point ya msingi sasa. Unamfahamu vipi huyo mwanamke?" aliuliza Inspekta Jasmine huku akirejea kitini

"Siku hiyo nilikuwa katika majukumu ya usafi ndipo nilipoitwa na meneja ofisini kwake, akanipa pombe kali na kunitaka nikaifungue halafu nitie kidonge alichonipatia, akaniambia ikifika majira ya saa 5 nielekee chumba namba 99 nimpatie Devotha pombe ile. Meneja aliniahidi kunipa laki mbili kama ningefanikisha tu zoezi lile. Mwanzoni sikuwa naelewa lakini majira ya saa nane usiku Devotha alinifuata na kunipatia ile laki mbili aliyoniahidi meneja. Halo ndipo Devotha akanielezea tukio zima lilivyokuwa" Alianza kueleza Merina.

"Huyo Devotha tutampataje?"

"Devotha ni Kahaba, huwa anajiuza kwenye madanguro mara nyingi. Ukielekea Hongera bar utamkuta huko maana mara nyingi ndiyo makazi yake huko"

"Unayo Simu na namba za Devotha?" aliuliza Inspekta Jasmine.

"Ndiyo. Ila yule polisi wa kiume uliyeambatana nae kuja kunichukua anayo simu yangu". Alieleza Merina.
Inspekta Jasmine akatoka nje ya chumba kile na kuelekea moja kwa moja upande wa pili alipo Adrian na Kinje
"Adrian ile simu ya huyu mwanamke umeiweka wapi? Nina shida nayo kidogo" Inspekta Jasmine aliuliza baada tu ya kumwona Adrian akitazama kioo kinachoonyesha upande wa pili wa chumba alipo Merina

"Ipo ndani ya Droo ya Kwanza pale". Adrian alijibu. Inspekta Jasmine akaelekea ilipo kabati kubwa iliyojaa mafaili. Akafungua droo ya chini kabisa, akaichukua simu ile na kurudi chumba kile cha mahojiano. Akaiwasha simu ile na kumpatia Merina.
"Nipatie namba ya Devotha" alisema huku akimkabidhi Merina simu ile. Merina akaipokea, akaitafuta namba ya Devotha, alipoipata alimrudishia Inspekta Jasmine simu.

"Sawa. Utakaa hapa hadi pale tutakaporudi. Kazini hutaweza kurejea tena kwa sababu hata ukirejea watakuua tu. Tukishamkamata meneja na wenzake ndipo utakapokuwa huru." Inspekta Jasmine alisema kwa msisitizo.

"Sawa Afande" Merina alijibu, hakuwa na hofu tena. Ni kutokana na kuwa karibu na Inspekta Jasmine

Inspekta Jasmine akatoka nje, akaungana na Adrian pamoja na Kinje kuelekea huko Hongera Bar.
Askari kadhaa pale kituoni walibaki wakiendelea na majukumu mengine, huku Simon na Patrick wakiachiwa jukumu la kumwekea ulinzi wa kutosha Merina ambaye alishaitoa siri ambayo meneja wake alimhakikishia kuwa angemtoa roho yake pindi tu atakapoufungua mdomo wake.

Kutoka kituo cha polisi cha kati hadi Hongera Bar, safari haikuchukua dakika nyingi, ni dakika 20 tu ziliwawezesha kufika. Ulikuwa ni ukumbi maarufu wenye kila aina ya starehe ya uchafu kushinda bar yoyote ndani ya jiji la Dar es Salaam.

"Tumeambatana na wewe Kinje kusudi tuhakiki kama huyo mwanamke ndiye, japo kuambatana nawe ni hatari maana nasi tunafuatiliwa pia kila tuendapo" Alisema Inspekta Jasmine baada ya gari kusimama eneo la kupaki magari Hongera Bar.
Wakaongozana wote watatu kwa pamoja kuingia ndani ya ukumbi ule.
Ghafla Simu ya Inspekta Jasmine ikaanza kutoa ukelele wa ajabu, na hapo ndipo akakumbuka kile kifaa alichokitega katika ofisi ya meneja wa Royal hotel. Akabofya simu yake kwa haraka na kuweka sikioni

"Kama upo hapo ondoka sasa hivi maana Polisi watafika hapo kukuchukua,'....
"Merina ameshakamatwa na lazima awe ameshakutaja hivyo jitahidi uje Six Park village Bar nitakupatia kiasi cha fedha uelekee zanzibar kujificha hadi kupoe kwanza"

Alisikia sauti ya meneja ikisema. Akatabasamu kwa mbali, akakumbuka kuna wakati simu yake ilitoa ukelele akitoka Royal hotel. Akatazama kwenye orodha ya kumbukumbu na kuicheza audio moja ambayo haikusikilizwa. Akarudisha simu yake sikio la kushoto aweze kusikiliza..

"Wafuatilieni na hakikisheni huyo Mwanamke anakufa asije akaitoa siri"

Alisikia sauti ya meneja ikitoa amri.

"Kumbe wakati tunashambuliwa ni meneja alituma watu, amejileta mwenyewe kwenye kumi na nane zangu huyu" Alijisemea peke yake.
Akizidi kusogea mbele lilipo lango la kuingia ukumbini yeye na Adrian pamoja na Kinje, Inspekta Jasmine alimwona mwanamke akitoka kwa kasi. Haraka akaichukua simu yake na kupiga ile namba aliyopatiwa na Merina, wakati akipiga simu, macho yake yalikuwa yakimtazama mwanamke yule.

"Simameni". Aliwaamrisha wenzake baada ya kumwona mwanamke yule akipokea simu, wakati huo simu yake ilipokelewa. Akajua bila shaka Devotha ni yule mwanamke

"Vipi Inspekta, umeona nini?" Adrian aliuliza

"Kinje." Inspekta Jasmine aliita. Kinje akamgeukia ili kumsikiliza.

"Mwangalie yule mwanamke kule anayekimbia" Inspekta Jasmine alimwambia Kinje
Kinje akayapeleka macho yake hadi upande wa pili, akamshuhudia Devotha akikimbia kufwata uelekeo wa zinapopaki pikipiki za matairi matatu.

"Ni yeye. Namkumbuka vizuri mwanaharamu yule" Kinje alisema baada tu ya kumwona. Alipata hasira ya ghafla baada tu ya kumwona Devotha. Akakumbuka siku ile alipokwenda kumsaidia Devotha alipotakwa kubakwa. Kumbe hakuwa anabakwa wala nini, alitegewa tu mtego.

"Hey Simamaa". Inspekta Jasmine aliamuru kwa sauti ya juu. .

"Adrian muwahi fasta asitukimbie huyu mwanamke" Inspekta Jasmine alisema
Adrian akachomoka kwa kasi kumkimbilia mwanamke yule anayeonekana kuwa na haraka. Ghafla ulisikika mlio wa risasi. Taratibu Adrian akaelekea chini huku akinyoosha mkono mbele kama anaita. Yule mwanamke aliyekuwa akikimbia alisimama na kugeuka baada ya kusikia mlio wa risasi.
Kinje akataka kuwahi pale Adrian alipodondoka lakini kwa haraka Inspekta Jasmine alimzuia kwa kumshika mkono

"Ni hatari, usiende" Alisema huku akiangaza kila kona. Juu ya ghorofa iliyo jirani na ukumbi walipo aliweza kumwona mtu mwenye bunduki ya masafa marefu. Kwa utulivu wa hali ya juu alichomoa bastola yake kwa haraka na kufyatua risasi iliyokwenda moja kwa moja hadi katika kichwa cha mtu yule. Mtu yule akaanguka kutoka juu ya ghorofa hadi chini akiwa tayari ameiaga dunia.
Kila mtu ndani ya ukumbi alianza kutoka nje na kukimbia hovyo baada ya kusikia mlio wa risasi.
Pale alipodondokea Adrian alinyanyuka. Risasi ile haikuweza kupenya ndani ya mwili wake kutokana na kuvalia kizuia risasi katika kifua chake.

"Inspekta fuatilia kule ngoja mimi nimuwahi yule mwanamke naona amepanda pikipiki" Adrian aliropoka kwa nguvu baada ya kunyanyuka. Inspekta Jasmine akatoa pumzi ndefu huku akishukuru baada ya kuona Adrian amesimama na ni mzima kabisa.

"Kinje, chukua huu ufunguo wewe nenda ndani ya gari katusubiri maana hapa si salama tena"
alisema Inspekta Jasmine. Kinje akauchukua funguo wa gari na kuelekea gari lilipo.
Wakati huo Adrian alifanikiwa kukamata bodaboda moja katika kituo cha bodaboda. Akaanza kuifukuzia pikipiki ile ya matairi matatu aliyoipanda Devotha. Alipoisogelea kwa karibu aliamuru dereva yule asimame,
"Polisi hapa, simamaa.." alisema Adrian huku akionyesha kitambulisho kwa mkono mmoja, mkono mwingine ukishikilia vizuri usukani wa pikipiki.
Pikipiki ile ilisimama, kitendo cha kusimama tu Devotha aliteremka haraka na kuanza kukimbia. Adrian naye akaiacha pikipiki na kuanza kumkimbilia Devotha.

"Simamaaa,... Nitakushoot simamaa" Adrian alipiga kelele lakini Devotha hakugeuka wala kusimama. alizidi kukimbia. Adrian akachomoa bastola yake kiunoni na kufyatua risasi kuelekea angani. Mlio ule ulimfanya Devotha asimame kwa Ghafla huku akitetemeka, aliposimamia majimaji yalianza kuchuruzika mapajani hadi chini. Alijikojolea palepale. alijikojolea kutokana na hofu aliyokuwa nayo.
Sasa Adrian alimkamata kiulaini kabisa na kurejea naye hadi pale Hongera bar alipowaacha Inspekta Jasmine na Kinje. Alikuta umati mkubwa wa watu pale pamoja na magari mawili ya polisi.

"Kazi nzuri Adrian. Sasa hapa itabidi tujigawe, wewe na Kinje mtaelekea kituoni kumpeleka huyu mwanamke, Nitakuja kumhoji mwenyewe. Mimi nawahi Six park Village bar kumkamata yule Meneja wa Royal hotel. Nilisikia maongezi yake akimsihi huyu mwanamke waonane pale ili aweze kumtorosha" Alisema Inspekta Jasmine
"Duh! Kumbe meneja naye anahusika" alisema Adrian

Je Inspekta Jasmine atafanikiwa kumkamata Meneja? Majibu tunayo katika sehemu ijayo hapahapa.
Facebook Page tunapatikana kama Simulizi za Gilbert.
 
Itaisha au tutaanza kuvutana chemba?
 
Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715

Sehemu ya 18

"Kazi nzuri Adrian. Sasa hapa itabidi tujigawe, wewe na Kinje mtaelekea kituoni kumpeleka huyu mwanamke, Nitakuja kumhoji mwenyewe. Mimi nawahi Six park Village bar kumkamata Meneja wa Royal hotel. Nilisikia maongezi yake akimsihi huyu mwanamke waonane pale ili aweze kumtorosha" Alisema Inspekta Jasmine

"Duh! Kumbe meneja naye anahusika" alisema Adrian

Adrian Kinje pamoja na Devotha aliyekuwa na pingu katika mikono yake walielekea kituo cha Polisi cha kati. Mwili wa yule mdunguaji aliyeuwawa kwa risasi iliyotoka kwenye bastola ya Inspekta Jasmine ukapakiwa na wale polisi wengine waliofika pale. Simu yake ilipokaguliwa ilionyesha mtu wa mwisho kuwasiliana nae alikuwa ni Meneja wa Royal Hotel. Pia simu ya Devotha ilionyesha hivyo hivyo, wote waliwasiliana na meneja dakika chache zilizopita.

Inspekta Jasmine alifika Six Park village bar, akaandika ujumbe mfupi kwenda kwa Meneja kwa kutumia ile simu ya Devotha.

"Nimefika hapa Boss, nimefanikiwa kumtoroka, muda uleule naongea nawe waliwasili pale. Upo wapi nije?".
Akautuma ujumbe ule akiwa bado ndani ya gari. Alijihadhari meneja asije kumwona kabla ya yeye kumwona ili amkamate kwa wepesi. Mara akaona gari aina ya Suzuki ikiingia na kupaki karibu yake. Punde akateremka Meneja huku akibonyeza simu yake na kuiweka sikioni.
Simu ya Devotha aliyokuwa nayo Inspekta Jasmine iliita. Mpigaji alikuwa ni meneja. Inspekta Jasmine akachomoa bastola yake haraka na kuufungua mlango wa gari. Wakatazamana na meneja uso kwa uso. Mikono yake iliyokamata bastola ilielekea kwa Meneja. Meneja akabaki mdomo wazi asijue nini cha kufanya.
Hakuamini kama amekamatika kiulaini

"Upo chini ya ulinzi kuanzia sasa," Inspekta Jasmine alisema, akaikamata bastola kwa mkono mmoja huku mwingine ukielekea mfukoni na punde mkono ule ulitoka na kitu kisichopendwa na wahalifu. Mkono ulitoka na pingu.

"Kosa gani nimefanya jamani? Aliuliza meneja kwa sauti ya upole.

"Utalifahamu hilo kosa ukifika kituoni" alisema Jasmine huku akimfunga meneja pingu.
____________

Inspekta Jasmine alifika kituoni pamoja na mhalifu wake, moja kwa moja akaelekea chumba cha mahojiano bila kupoteza muda. Alianza na Devotha.
"Jina Lako nani?". Alimuuliza Devotha

"Devotha Thobius". Alijibu kwa kutetemeka

"Miaka yako?"

"Ishi.. ishini na Tano" alijibu Devotha kwa sauti yenye kigugumizi.

"Mh, Ishini na tano ni namba mpya hii au? Hebu taja miaka yako kwa usahihi Devotha" alisema Inspekta Jasmine huku akimtazama Devotha machoni. Devotha alirudia tena kuitaja miaka yake. Alikuwa na miaka ishirini na Tano.

"Kwanini ulikuwa ukitukimbia tulipokuita pale Hongera bar? Ulikuwa ukitii simu ya Meneja wako eti?". Inspekta Jasmine aliuliza,
Devotha alishtuka sana kusikia jina la meneja. Akajua hakuna siri tena iliyojificha. Inspekta Jasmine aliuona mshtuko kutoka kwa Devotha

"Ni..ni tamaa ya pesa iliniponza Afande nisamehe mi sijui kitu.." alijitetea huku akitokwa na machozi.

"ohoo kumbe unakumbuka tarehe 28 mwenzi Desemba, vizuri kama una kumbukumbu., ni nani alikutuma? kwa usalama wako niambie tu". Aliuliza Inspekta Jasmine huku akimkazia macho Devotha

"Kuna mkaka alinifuata ile siku akanipa Laki nne, mimi nikamuuliza ni za nini akaniambia anataka tufanye kazi na kama nipo tayari atanipatia laki nne zingine". Alisema Devotha huku akipepesa macho huku na kule

"Halafu ikawaje? Ulizikataa?," Inspekta Jasmine aliuliza maswali mawili mfululizo

"Nilikubali ndipo akaniambia muda ukifika yeye atanipigia. Baadae alinipigia na kuniambia nije sehemu aliyonielekeza." alivuta pumzi ndefu kisha akaifunga mikono yake kama anasali.
"Afande niahidi maisha yangu yatakuwa salama, wataniua mimi afande" alisema Devotha akiwa bado ameifunga mikono yake mfano wa mtu anayefanya ibada.

"Naitwa Inspekta Jasmine. Ukiwa mkweli hakuna kitakachoshindikana. Utalindwa hata usinziapo, utalindwa uendapo msalani, popote pale utalindwa Devotha. Hawatakuona hadi nitakapohakikisha wanaenda jela. Haya hebu niambie, halafu ikawaje?" alisema Inspekta Jasmine

"Aliniambia tuxheze mchezo. Alidai kuna mtu wanamuhitaji na mimi nilipaswa kumtega ili wampate huyo mtu. Kwenye huo mchezo yeye atajifanya anataka kunibaka nami niigize napiga kelele za kuomba msaada. Akaniambia kuna mtu nikimwona anapita ndio tutaanza huo mchezo, na kama asipopita huyo mtu basi tutabadili mchezo. Kweli baada ya muda yule mkaka uliyekuwa nae kule Hongera Bar alipita. Ndipo aliyenipa kazi alianza kunishikashika maungoni, mimi nikajifanya napiga kelele za kuomba msaada. Kweli alikuja yule mkaka, Akanisaidia, baadae nilienda nae chumbani kwake kulala, alipolala nikaondoka akaja yule mkaka aliyenipa kazi hiyo mimi nikaondoka zangu." alisema Devotha

"Hebu nyoosha maelezo Devotha. Alilalaje lalaje halafu wewe ukaondoka? Haukumwekea vidonge vya usingizi ili alale?" Aliuliza Inspekta Jasmine akimtazama Devotha machoni. Devotha akaanza kutokwa na machozi.
"Nilishawishiwa afande, mimi niliambiwa kuna muhudumu ataleta kinywaji kule chumbani nikipokee, niliambiwa kile kinywaji nisitie mdomoni , nihakikishe kwanza yule mkaka amekunywa, akisinzia ndio nipige simu ili aje. Alipokuja mimi nililipwa nikaondoka zangu afande mimi sikujua kilichotokea.

"Wewe na Meneja mna uhusiano gani? Mbona alikushawishi uondoke pale Hongera Bar uelekee Six park village Bar?" Aliuliza Inspekta Jasmine

"Meneja, meneja yeye..." Devotha hakumaliza alichotaka kusema, alikatishwa na ukelele wa ghafla wa mlango ukifunguliwa kwa fujo. Aliyeingia alikuwa ni Adrian huku akihema haraka haraka.

"Inspekta, inspekta kuna shida. Meneja kauwawa" alisema Adrian baada ya kuingia ndani.

"Unasemaje! Kauwawaje wakati kuna ulinzi hapa kituoni? Nini kimemuua?" Jasmine aliuliza huku akinyanyuka, akatoka nje pamoja na Adrian, akamwacha Devotha pale kitini katika chumba kile cha mahojiano

"Nashindwa kuelewa afande sijui imekuwaje, Nakumbuka afande Edwin alikuja na glasi mbili za juisi ya embe, akanikaribisha moja. Nilipokunywa nilijihisi kwenda msalani maana nilibanwa ghafla na haja kubwa. nilipokwenda msalani wakati narejea nilimwona afande Patrick akija mbio akiniita, ndipo akanielezea mtuhumiwa aliyeletwa ameuwawa" Adrian alisema huku wakiongozana na Inspekta Jasmine wakielekea sero mojawapo ya kuhifadhia hawalifu. Sero hiyo ndani yake ndipo alipowekwa Meneja wa Royal hotel.
Inspekta Jasmine alifika na kushuhudia mwili wa Meneja ukiwa sakafuni umetulia, damu nyingi zilimzunguka eneo la kichwani

"Mleteni Afande Edwin haraka sanaa hapa anieleze ilikuwaje, huu ni uzembe mkubwa sana askari wapo wengi tu hapa halafu yanafanyika mauaji". Alifoka Inspekta Jasmine kwa hasira huku akimtazama Adrian mithili ya Simba aliyejeruhiwa.

"Sawa Afande". Adrian alijibu kiukakamavu, akapiga saluti na kurudi nyuma hatua tatu kinyumenyume.
Mara akaingia polisi mmoja akiwa anahema kwa kasi, akapiga saluti mbele ya Inspekta Jasmine

"Mkuu amekimbia Edwin, Edwin amechukua pikipiki ya Afande Adrian na kukimbia nayo Afande.... Jambo Afande" alisema polisi yule.
Inspekta Jasmine hakusikia salamu wala kuiona saluti aliyopigiwa. Taarifa ya kukimbia kwa Edwin ndiyo aliyoisikia, na ilimshtua sana.

"Yeye ndiye aliyefanya hivi, lazima tumpate mshenzi mkubwa huyu anathubutu kusaliti jeshi la polisi, anastahili kifo. Ametoka mda gani?" alisema Inspekta Jasmine huku akimsogelea polisi yule ambaye hana cheo chochote.

"Sekunde chache tu zilizopita wakati naingia afande, ni sasa hivi tu afande. Ameondoka na Pikipiki ya Adrian" alisema polisi yule

"Adrian twende, wewe ita mwenzako mmoja muuondoe huu mwili hapa mpeleke kufanyiwa uchunguzi, pia msafishe hapa pakae sawa. Chumba cha mahojiano si ruhusa mtu kuingia, umenielewa?"

"Ndiyo Afande" alijibu polisi yule kwa ukakamavu mkubwa.

Adrian pamoja na Inspekta Jasmine wakamuacha Kinje pale kituoni, wakaelekea garini na safari ya kwenda alipoelekea Edwin ikaanza.

Wakiwa ndani ya gari Simu ya Inspekta Jasmine iliita. Akatazama mpigaji ni nani, ni moja ya polisi wa palepale kituoni. Hakuitilia sana maanani simu ile, iliita hadi ikakata.
Ilipokata tu simu ya Adrian nayo ikaanza kuita.

"Huyu anataka nini? Tumetoka sasa hivi tu hapo kituoni anapiga, au kuna shida nini!" alijiuliza Adrian huku akiwa makini kuendesha gari. Inspekta Jasmine alimsikia

"Hebu nione ni nani huyo anapiga!" aliuliza Inspekta Jasmine. Adrian akamsogezea Jasmine simu ile. Kuiona tu alihisi kuna kitu hakipo sawa.

"Aah ni huyu ametoka kunipigia mda si mrefu kwenye simu yangu. Hebu ipokee tusikie anasemaje, wenda kuna tatizo"
Adrian akabofya sehemu ya kupokea na kuweka sauti ya juu ili wote wasikie

"Afande rudinii.. Kuna tatizo huku rudini Edwin ame.." ilisikika sauti simuni lakini sauti ile ilikatishwa ghafla, haikuendelea tena. Simu ikakatwa.
Kunani tena huko kituoni?, Edwin amefanyaje? Usikose sehemu ijayo hapahapa Gilbert akusimulie. Inaitwa Ishini Badala yangu Wanangu.

Tukikaribia kuimaliza hii, tunajiandaa na mpyaaa[emoji91][emoji91][emoji2960]
 
Back
Top Bottom