gilbert35
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 247
- 474
Simulizi Ya Maisha na Upelelezi; ISHINI BADALA YANGU WANANGU
Mwandishi; GILBERT EVARIST MUSHI
PHONE: 0765824715
Sehemu ya Kwanza
Sauti ya maji ndiyo iliyokuwa ikisikika ndani ya masikio yake mawili, akajaribu kukisogeza kichwa chake karibu zaidi na koki ya bomba inayotiririsha maji bafuni mle lakini bado hakuweza kuuweka sawa ubongo wake uliokuwa ukiwaza mengi. Muda wote akiwa bafuni anaoga akili yake haikuwa bafuni, Alikuwa akiiwaza safari yake ya Kuelekea Dar es Salaam. Tena katika Hospitali kubwa ya Taifa ya Muhimbili.
Macho yake akayaelekeza katika sabuni aliyokuwa akiitumia kuogea. Akapeleka kidole gumba hadi juu ya sabuni ile na kuanza kukita kidole kile, hali iliyopelekea kutokea shimo katikati ya sabuni. Hakuishia hapo tu, akaichukua na kuanza kuimega kidogo kidogo kwa kutumia kucha zake. Ikawa si tena sabuni bali ni vipande vya sabuni.
Akiwa bado Bafuni sauti ya mke wake ilisikika ikimwita.
"Honey simu yako inaita, huko bafuni humalizi kuoga tu mume wangu?"
"Nakuja Kipenzi".. Haraka alitoka bafuni na kuiwahi simu ile. Alihisi mpigaji atakuwa ni Kaka yake aitwaye Abuu.
Hisia zake zilikuwa sahihi haswa, mpigaji alikuwa ni yeye, Abuu Abdallah. Ndugu yake wa damu kabisa.
"Vipi Kinje" Sauti ya Kaka yake ikamsabahi.
"Safi Kaka, kwema huko?"
"Kwema kiasi mdogo wangu. Umekata tiketi ya boti ya saa ngapi kuja huku?" aliuliza Kaka yake
"Safari inatarajia kuanza saa 12 Jioni kaka, nimeshauriana na mke wangu hapa nikaona nikate tiketi ya jioni kabisa ili nifike huko kwenye saa mbili hivi usiku." Kinje Akamjibu kaka yake
"Ohoo. Sawa Mdogo wangu. Ufike salama basi maana Kesho ndio siku yenyewe. Si unalijua hilo?"
"Natambua hilo kaka". Kinje alijibu kisha akavuta pumzi ndefu. Alimaliza kuzungumza na simu ile na kuitupia kitandani. Mke wake muda wote alisimama mbele yake akimtazama kwa macho yenye uchungu mkubwa. Ni kama alitaka kulia lakini alijikaza tu.
"Usijali nitakuwa sawa tu Mke wangu". Kinje alijaribu kumtuliza mkewe. Licha ya Clara kuambiwa vile lakini hakuyajali maneno ya mumewe, alishindwa kujizuia, akamsogelia Kinje na kumkombatia. machozi nayo yakashindwa kujizuia, yakaitafuta njia ya kutokea. Alianza kutokwa machozi
"Kila mara wewe ni wa kusema tu utakuwa sawa. Hujali ni kiasi gani sijapendezwa na hili Honey, hujali pia hisia zangu. Kwa hili siwezi kuwa sawa Kinje." Alilalama Clara huku mdomo wake ukiwa karibu kabisa na sikio la Kinje
"Vipi kama usiporudi? Nitaishije? Huyu mtoto aliyeko tumboni mwangu atapata wapi upendo wa baba kama tu baba yake ananiacha peke yangu na sina imani kama aterejea tena? Tafadhali kipenzi usiniache nakuomba. Mwambie kaka yako atafute hata mtu mwingine mume wangu, sitaki ukae mbali nami, sihitaji kukupoteza Kinje."....
Alizungumza Clara kwa Majonzi makubwa huku akimpigapiga Kinje kwa mkono wake laini kifuani pake.
Kinje akavuta pumzi ndefu na kuiachia taratibu huku akitafakari nini afanye. Alipaswa kwenda Dar es salaam, hakuwa na namna ya kuikwepa safari ile. Kaka yake wa tumbo moja anayeishi Dar es salaam alimhitaji kutokana na matatizo yaliyomkumba mwanaye wa pekee wiki chache zilizopita. Binti yake aitwaye Julieth alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya Figo. Figo moja ilifeli na hivyo ilihitajika figo nyingine.
Julieth mbali na kubakiwa na figo moja, nayo ilishapata maambukizi kutoka katika figo ile ya kwanza kutokana na kucheleweshwa kwenda hospitali, hivyo daktari alishauri mtoto Julieth aondolewe figo zote na kupatiwa figo nyingine. Figo iliyoharibika zaidi ikatolewa na ikabaki ile yenye unafuu kidogo.
Zoezi la kutafuta figo haikuwa kazi rahisi, walipaswa kutafuta namna ya kufanikisha mtoto Julieth aweze kupata figo. Iliwalazimu yeye na kaka yake watafute mtu ambaye vinasaba vyake (DNA) vitaendana na vya Julieth. Mtoto Julieth alihitaji mtu mwenyevina saba vya kufanana naye.
Abuu hakuwa na mtoto mwingine zaidi ya Julieth, alitamani mwanaye aweze kuzinduka tena kutoka kitandani kwani muda wote alikuwa ni mtu wa kitandani tu. Mke wake Abuu alipoteza maisha miaka kadhaa iliyopita baada tu ya kumzaa Julieth hivyo Julieth alibakiwa na mzazi mmoja tu ambaye ni Abuu.
Katika kutafuta mtu, kitu cha ajabu ni kwamba Kinje ndiye aliyeonekana vinasaba vyake kufanana na Julieth kwa asilimia 99.9%. Kinje Hakuwa na hiyana, kwenye kumchangia figo mtoto mdogo tena isitoshe ni mtoto wa kaka yake?
Hilo akaliridhia. Na zilibakia siku mbili tu ili Kinje na Julieth waweze kuingizwa katika chumba maalumu cha upasuaji, figo moja itoke kwake na kwenda kwa Julieth.
Hiki ndicho kilimfanya mke wa Kinje akose raha. Alihofia juu ya usalama wa mumewe endapo atatolewa figo moja na kubakiwa na moja.
"Sikia mke wangu, Mwanadamu akibakiwa na figo moja sio mwisho wa maisha mke wangu, na pia nguvu hazipungui, kazi atapiga kama mwanzoni kabisa. Si unamjua balozi wetu wa hapa Jang'ombe? Mbona Yeye ana figo moja lakini bado anadunda na maisha vizuri mke wangu?, kumchangia mtu figo sio mwisho wa uhai mke wangu nielewe ".
Alizidi kumsihi mkewe huku akimfuta machozi,. Baada ya muda kidogo Mkewe akapoa, Kinje akajiandaa kwa Safari ya kuelekea Bara na hatimaye maandalizi yalikamilika.
Kabla ya kuondoka Mke wake alimlisha chakula kama mtoto mdogo, akamnywesha na juisi ya embe. Muda wote akifanya hivyo hakuwa katika uchangamfu. Hofu yake ilikuwa juu ya mumewe tu. Alitamani kuongozana naye kwenda Jijini Dar es Salaam lakini haikuwezekana kutokana na hakukuwa na mtu wa kusimamia miradi yao biashara na ukijumlisha Clara alikuwa ni mjamzito
Majira ya Saa Kumi na nusu jioni Kinje aliagana na mke wake tayari kwa safari ya kuelekea Jijini Dar es salaam kwa usafiri wa Meli. Mkewe akalikita busu zito katikati ya paji la uso la mumewe huku machozi yakimtoka. Kinje naye akajiandaa kujibu kwa Kumpiga busu katika tumbo lake lililotuna kutokana na ujauzito aliokuwa nalo.
"Pandisha gauni lako mpenzi nimbusu mwanangu, nimwambie ninatoka kidogo sitakawia kurudi". Kinje akamsihi huku akididimiza magoti yake chini taratibu.
Mkewe alikataa.
"Nibusu tu hivyohivyo bwana, hadi nijifunue jamani?" Clara alisema kwa sauti ya madeko. Kinje akakumbuka hii si mara ya kwanza kwa mkewe kumkatalia pindi ahitajipo kubusu tumbo lile bila kuwepo na kizuizi cha nguo. Pia kuna wakati akiligusa tumbo la mkewe, huonekana kushtuka ghafla na kumkatalia.
Akaamua kuliacha lile likapita. Alimbusu mkewe kwa namna alivyotaka.
Wakaagana.
Kinje alifika Bandarini majira ya Saa kumi na moja na nusu jioni, akakamilisha baadhi ya taratibu za msingi kabla ya kupanda meli ndogo ya abiria na mizigo kuelekea Tanzania Bara, na taratibu zilipokamilika safari ilianza rasmi majira ya saa kumi na mbili jioni. Kutokana na umbali wa kutoka Zanzibar hadi Bara, safari ilitarajiwa kuchukua takribani masaa mawili na nusu tu.
Kinje akiwa ndani ya meli, kuna jambo lilimshangaza sana. Katika siti za abiria zilizokuwa mbele yake kulikuwa na wanaume wawili waliokuwa wakimtazama mara kwa mara. Walikuwa wakimtazama huku wakizungumza kama vile wanamjadili. Ilikuwa ni kama vile wamemfananisha ama wanamfahamu kwa jinsi walivyokuwa wakimtazama kwa macho ya udadisi. Kwa upande wa Kinje sura hizi zilikuwa ngeni kabisa kwake kwani hakuwahi kuziona hapo kabla.
Kuna muda Kinje alielekea msalani, akiwa msalani alisikia mazungumzo ya watu wawili wakiteta jambo. Akajaribu kusikiliza mazungumzo yale yaliyokuwa yakifanyika msalani.
"Niamini Edgar. Bosi alinitumia picha yake kabisa, ni yeye huyu jamaa." alisikia sauti ikisema
"Kama ni yeye basi itakuwa bingo kwetu. Hatutakuwa na kazi kubwa sana. Zoezi litafanyika leo leo usiku. Cha kufanya ni kuleta kasoro humu ndani ili meli ikawie kufika Dar,".. Sauti ya pili ilijibu.
Kinje hakuyatilia maanani sana maongezi yale, alifanya kilichompeleka msalani kwa wakati ule kisha akarejea katika siti yake. Kitendo cha kukaa tu, mbele yake akawaona vijana wale wawili waliokuwa wakimtazama mara kwa mara wakitokea upande wa msalani. Akagundua yale maongezi aliyoyasikia kule msalani bila shaka walikuwa ni wao.
"Ni kasoro gani hiyo wanataka kuileta huku ili meli ichelewe kufika bara?." Kinje alijiuliza huku akiwatazama vijana wale, hakupata jibu. Akajionya tabia ya kufwatilia yasiyomuhusu.
Akiwa katika lindi la mawazo akayaelekeza macho yake hadi pale walipoketi vijana wale wawili, macho yake yaligongana na macho yao, kwa haraka vijana wale waliangalia pembeni, Kinje akapata kuhisi kuna jambo halipo sawa. Lakini bado hakutilia maanani kivile.
"Sasa mbona kila muda wananitazama mimi tu? Na kwanini macho yetu kila yakigongana wanaonekana kukwepesha?"..... Kinje aliwaza.
"Ah itakuwa ni mawazo yangu tu. Au labda wamenifananisha," Alijisemea, akaamua kuachana na mawazo yale
Je vijana hawa wana lengo gani na Kinje? Kinje atafanikiwa kufika Tanzania Bara salama? Tuwe wote katika sehemu ijayo ya Simulizi hii itakayokufundisha mengi. Njoo Gilbert akusimulie