Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 13,464
- 19,808
Kisa cha kweli kilichompata rafiki yangu.
SEHEMU YA KWANZA
Umasikini ulikua chanzo cha mimi kugundua mapema kabisa tofauti iliyokuepo kati ya baba na mama yangu, Nililala na baba na mama yangu chumba kimoja hadi nilipoanza darasa la kwanza hapo ndipo uhalisia ukauzidi nguvu ukimya wa kuzuga kila kitu kipo sawa na hapo tukalazimika kuamia nyumba iliyokua na chumba na sebule. Usiku baada ya kupata chakula natoa meza na kutandika godoro langu na kulala. Awali lilikua jambo la kawaida lakini hadi nafikia kumaliza darasa la saba akili ilikua imefunguka na kinagaubaga nilitambua haikua jambo la afya hata kidogo kulala pale sebuleni huku chumba kile kikiwa wazi sehemu ya juu kikiyaruhusu masikio yangu kusikia kila kilichoendelea katika chumba cha wazazi wangu.
Nilizaaliwa peke yangu kwa wazazi wale wawili lakini sikua peke yangu kwa baba yangu wala mama yangu, Mama alikua na mtoto wa nje na baba alikua na watoto wawili wa nje niliwahi kuwaona siku moja japokua sikutambulishwa moja kwa moja kua wale ni ndugu zangu hivyo ninilijiongeza tu lakini ukiniuliza mpaka sasa jibu langu ni kua nilizaliwa peke yangu na hata yote yaliyonitokea yalinikuta peke yangu hua inafika kipindi nasema laiti ningelijua ningelilazimisha nitambulishwe kwa ndugu zangu lakini kama mjuavyo neno ''ninge'' huchelewa kuja na nikawaida yake kuchelewa, Niliendelea kuishi sebuleni huku akili yangu ikiendelea kunasa jambo ambalo linanichkiza sana baba yangu mzazi hakua na sauti mbele ya mama yangu na mbaya zaidi kuna kipindi alikua akipigwa mbele yangu.
Hakika nilifedheheka sana lakini sikua na lolote la kufanya nilikua mtoto maisha yakaendelea, Nilifanikiwa kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lakini alikua mama yangu aliyekataa nisiende shule kuna shamba ni heri nilime kwanza iliipatikane pesa ya kutosha na mwaka unaofuata nitaenda shule. Ilikua kama mama alivyosema baba hakua na neno la kubadilisha kilichozungumzwa. Hivyo sikuendelea na shule na haikua kwa mwaka mmoja ilikua moja kwa moja hadi ujana wangu. Sawa nilijua mama yangu alikua akimnyanyasa baba yangu lakini sikujua kwanini mwanaume mzima kunyanyaswa na mwanamke nilijitama mimi jinsi nilivyokua imara shuleni dhidi ya wanafunzi wenzangu sikua nikionewa na aliethubutu kunionea nilimkabili na kumfunza adabu sasa kama mimi niliweza kufanya yale inakuaje nizaliwe na baba mnyonge namna ile? Hii iligoma kabisa kuniingia akilini na laiti kama baba asingeweza kufanana na mimi kwa sura ningeweza kuamini kabisa kua sio baba yangu wa kunizaa. Mawazo yale yalibaki kama yalivyo na nikakubali sitasoma nikaendelea na kulima huku nikilala sebuleni na kuendelea kusikiliza fujo za baba na mama kila siku walikua wakipigana na kutukanana sikujua nini chanzo nilibaki kua msikilizaji tuu.
Miaka ikakatika hadi siku ile ambapo utata ulikuja nilikua na umri wa miaka kumi na saba [17] wakati huo lakini usingeweza kukubali kwa macho maana nilikua na mwili uliokomaaa na pia umbile refu. Hii ni kutokana na kufanya kazi ngumu za kujiingizia kipato kwa sababu kwa kipindi hicho mama aliniambia nimeshakua mkubwa tayari hivyo nianze kujitafutia nilijiuliza sana itakua vipi mama wa kunizaa aweze kunitamkia maneno kama yale sasa najitafutia vipi wakati elimu sina na yeye ndio aliyetoa kauli ili nisiendelee na masomo, Maisha yakaendelea....
Mapenzi bila pesa kufanikisha kumpata unaemuhitaji hua ni kazi ngumu sana tena isiyokua ujira zaidi ya kupata matusi kutoka kwa mlengwa, Mimi pia ni mwanadamu licha ya ugumu wa maisha pale nyumbani bado hisia za mapenzi zilikua palepale. Niliangukia kwa mtoto wa mwenyekiti wa mtaa wetu ambaye enzi hizo nilisoma nae shule ya msingi lakini yeye aliendelea hadi alipofanikiwa kumaliza kidato cha nne na hatimaye kuingia chuo cha afya, Hakika hatukua tukifanana kuanzia namna ya kuzungumza mavazi, kutembea hadi kusalimia watu mwenzetu kila kitu alikifanya katika namna aliyoijua yeye sikuyajali haya yote nikasema kua huyu ndio ninaehitaji kumuoa na hapo nikawa nimejipa adhabu mpya, Karaha za nyumbani na hofu ya kumtamkia Janet [Sio jina halisi] kua nampenda. Ili kuiridhisha nafsi yangu nikawa najitahidi mara kwa mara kwenda katka duka la mwenyekiti wa mtaa ambapo Janet alikua akiuza kwa muda huku akisubiri mahali akapangiwe kazi. Nilikua naridhika sana kusalimiana nae na kupiga soga za hapa na pale japokua hakua akionyesha ushirikiano sana na ikafikia sura na sauti ya Janet ikawa tiba ya maradhi yangu.
Sikujua kama itafika siku nitazungumza na Janet kwa kirefu lakini iyo siku ilifika bila mimi kujua kama ni sikua sahihi ama laa, Niliamini katika kile nilichoamini sikujua kama haikua siku sahihi.
Ilikua ni siku ya ijumaaa ambapo nyumbani hapakua na utaratibu wa baba yangu kwenda msikitini kwa kifupi hakujali zaidi juu ya jambo hili na hivyo kuniambukiza mimi [mtoto umleavyo ndivyo akuavyo]. Lakini Ijumaa hii ilikua ya tofauti sana baba yangu alishinda msikitini na alishiriki swala zote kuanzia alfajiri na siku hii lishinda akiwa amevaa kanzu tu, Nilimsikia mama yangu akicheka sana pale ambapo baba alirudi kutoka swala moja alipocheka baba alikua mkimya sana bila kusema neno lolote. Jioni mida ya saa moja nikiwa dukani kwa mwenyekiti nikipiga soga na Janet nilimuona baba yangu akizungumza na mtu aliyekua akiuza visu hatimae nikamuona akinunua kisu. Badala ya kukibeba kikawaida hakufanya vile alitazama kushoto na kulia kisha upesi akafunua kanzu na kukificha kisu kile. Hapo tayari alikua ameshalipia, Akaondoka kwenda zake bahati nzuri hakuniona. Sikujali sna kuhusu tukio lile alilofanya baba nilijali zaidi kuyatazama macho ya Janet. Baada ya hapo nilienda kwa mama lishe akanihudumia na saa mbili usiku nilikua nyumbani.
Kama kawaida kulala sebuleni nikaanza kupangua vyombo ili nilale, Alaaaaa! sikukiona kisu kipya alichonunua baba na mbaya zaidi sikujua kama alikua ndani ama laa!. Nilitamani kuuliza lakini nilishangazwa na ukimya uliokua katika chumba cha wazazi wangu..........
NGOJA NIPUMZIKE KIDOGO. ITAENDELEA