SIMULIZI YA KWELI:Niliolewa na wanaume watatu

SIMULIZI YA KWELI:Niliolewa na wanaume watatu

SEHEMU YA 36:

Aliondoka asubuhi akiwa hana habari ya safari. Baadaye mchana alirudi akaniambia kuwa atakuwa na safari.
“Utaondoka saa ngapi? Nikamuuliza haraka.
“Nitaondoka usiku. Hivi sasa gari iko bandarini inapakia mzigo.”
“Hapa nyumbani utaondoka saa ngapi?”
“Nimekuja kuchukua begi langu, nikiondoka ndiyo nimeondoka. Sitarudi tena.” SASA ENDELEA…
“Poa,” nikajisemea.
Hivyo ndivyo nilivyokuwa nataka.
“Hutawahi kula chakula?” nikajidai kumuuliza.
“Kwani umeshapika?”
“Ndiyo ninapika.”
“Sitakisubiri, acha niende. Nitakula hukohuko.”
“Hao matajiri zenu wanapenda kuwapa taarifa za ghafla sana. Ilitakiwa wakwambie mapema kuwa utakuwa na safari.”
“Ndiyo kazi zetu zilivyo. Tumeshazoea.”
“Poa. Safari njema.”
Musa alichukua begi lake akatia vitu alivyovitaka kisha akaniaga. Wakati anatoka nikamuuliza:
“Kondomu zako huzihitaji tena?”
Musa aligeuka mara moja akanitazama kisha akasema:
“We’ acha mzaha wako.”
Nilisimama kunako mlango nikamtazama alivyokuwa akitembea kuelekea kwenye kituo cha daladala. Wakati namtazama mawazo ya Mustafa yakaanza kunijia.
Nikarudi ndani na kufunga mlango. Niliketi kwenye sebule nikajiambia kuwa sitapika tena. Nitakwenda kupika kwa Mustafa.
Nilisubiri yapite masaa mawili nikatia baadhi ya vitu vyangu kwenye mkoba wangu kisha nikatoka. Sikuchukua nguo. Nilikwishahamishia kwa Mustafa baadhi ya nguo zangu na viatu. Nilichukua vitu vidogovidogo tu ambavyo Mustafa asingeweza kuvizingatia.
Kabla ya kwenda Mbezi nilipitia sokoni nikanunua vitu ambavyo nilihitaji kupika. Nilipofika Mbezi Mustafa alikuwa hayupo. Kwa vile nilikuwa na funguo zangu nikafungua mlango na kuingia ndani.
Niliingia chumbani nikabadili nguo kisha nikazima simu yangu na kuiweka kwenye chaji ili Mustafa akija aone simu iko kwenye chaji. Sikutaka anipigie wala sikutaka Musa anipigie.
Baadaye nikatoka chumbani na kuelekea jikoni na kuanza kupika.
Yalikuwa majira ya saa kumi na moja Mustafa aliporudi nyumbani na kunikuta nimeketi sebuleni nikiangalia CD ya filamu ya Kihindi.
“Mbona hukunifahamisha kama umeshakuja?” akaniuliza.
“Kwani ulitaka kuleta msichana wako?”
“Mishi acha mzaha wako, una ‘surprise’ za ajabu sana. Halafu nilikupigia ukawa hupatikani.”
“Simu ilikuwa kwenye chaji. Mimi mwenyewe nilikuwa jikoni napika.”
“Kwani ulikuja saa ngapi.”
“Tangu saa sita niko hapa.”
Nilimdanganya. Muda niliofika, saa sita ilikuwa imeshapita.
“Umepika nini?”
“Nimepika wali na nyama.”
Nilipomwambia hivyo Mustafa aliinuka na kuelekea chumbani. Baadaye alirudi tena sebuleni. Alionekana alikuwa anatoka kuoga.
Tukaendelea na mazungumzo.
Kabla ya mwezi mmoja kukamilika Mustafa akaenda India. Alipoondoka tu nikarudi kwa Musa. Musa aliporudi kutoka Burundi alinikuta nipo nyumbani.
Kwa vile safari zake nyingi zilikuwa za Burundi, alipoondoka tena kwenda Burundi nikahamia Mbezi kwa Mustafa. Mustafa alikaa India kwa wiki nzima. Aliporudi alinikuta nipo nyumbani kwake.
Baada ya mwezi mmoja nikajikuta nina mimba. Sikujua ile mimba ilikuwa ni ya nani lakini nilikisia kuwa ilikuwa ya Mustafa. Nikaitambulisha mimba yangu kwa waume wote wawili. Kila mmoja akajua nina mimba na mimba ni yake.
Kwa vile waume wangu wote wawili walikuwa wakisafiri nje ya nchi na wakiwa huko hukaa kwa zaidi ya wiki. Niliendelea kutumia mtindo uleule wa kuhamia kwa mwanaume mmoja pindi mwenzake anaposafiri.
Kwa bahati njema walikuwa wakisafiri kwa nyakati tofauti hivyo kuniwezesha mimi kuweza kuwa kwa mwanaume mmoja pale mwenzake anapokuwa hayupo. Ile mimba iliendelea hadi ikatimiza miezi tisa. Hakukuwa na mwanaume wangu yeyote aliyegundua kuwa mimba hiyo ilikuwa ya watu wawili.
Kuna siku Mustafa alikuwa amekwenda China kununua bidhaa. Lakini Musa alikuwepo na nilikuwa nyumbani kwake. Musa akaniambia kwamba anataka asafiri lakini anasita kwa sababu naweza kuumwa na uchungu wakati wowote na nitakuwa peke yangu.
Wakati akiniambia hivyo Mustafa alishanipigia simu kunijulisha kuwa anarudi kesho yake.
Nikamwambia Musa kuwa anaweza kwenda safari.
“Mimi nitakwenda kwa shangazi.”
“Shangazi ataweza kukuhudumia?” akaniuliza.
“Kwa nini asiweze. Yeye mwenyewe ameniambia niende.”
“Kama ameshakwambia basi unaweza kwenda, acha mimi niende safari.”
Siku ile Musa akaondoka. Sikwenda kwa shangazi. Musa alipoondoka nikaenda Mbezi kwa Mustafa.
Mustafa alirudi siku iliyofuata na siku hiyohiyo nikaumwa na uchungu. Mustafa alinikimbiza na gari hospitali. Nikajifungua usiku mtoto wa kiume. Alikuwa amefanana sana na Mustafa.
Mustafa alikuja hospitali asubuhi akamkuta mtoto ameshazaliwa. Akampa jina hapohapo.
“Mwanangu ataitwa Amani,” akaniambia.
Nikatabasamu na kumuuliza:
“Umempa jina la nani wako?”
“Ni jina la babu yangu mzaa mama yangu,” akaniambia.
Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 37:

Mustafa alinikimbiza na gari hospitali. Nikajifungua usiku mtoto wa kiume. Alikuwa amefanana sana na Mustafa.
Mustafa alikuja hospitali asubuhi, akamkuta mtoto ameshazaliwa. Akampa jina hapohapo. Alimuita Amani.
Nikatabasamu na kumuuliza.
“Umempa jina la nani wako?”
“Ni jina la babu yangu mzaa mama yangu,” akaniambia.
SASA ENDELEA…
Kwa vile nilikuwa na afya njema na mwanangu alikuwa na afya njema, nikaruhusiwa kutoka hospitali asubuhi ileile. Nikarudi Mbezi.
Shangazi yangu alikuwa hajui kama nilikuwa nimejifungua na sikutaka ajue haraka. Pia sikumfahamisha lolote Musa ingawa namba aliyokuwa anaitumia Burundi nilikuwa nayo.
Mustafa aliniletea mfanyakazi wa kunisaidia kazi ili mimi niweze kumlea yule mtoto. Nikajiambia ili niweze kutekeleza mambo yangu vizuri nijenge uhusiano wa kirafiki na yule msichana ili anapogundua siri zangu asimueleze Mustafa.
Nilimpa baadhi ya nguo zangu za thamani. Pia nikawa nampa siri zangu ndogondogo na kumsisitiza kwamba asiwe anamueleza Mustafa maneno yetu.
Yule dada wa kazi ingawa hakutambua dhamira yangu kiundani alinielewa. Tukawa marafiki sana.
Mustafa alipohakikisha kuwa nilikuwa na mtumishi wa kunisaidia, akaanzisha tena safari zake za nje ya nchi ambazo alikuwa amezisimamisha kwa muda.
Siku ile alipoondoka na mimi niliondoka kwenda kwa shangazi lakini mtumishi nilimuacha nyumbani kwa Mustafa. Nilimdanganya kwamba mama yangu aliyekuwa akiishi Ilala alikuwa mgonjwa hivyo nilikuwa nakwenda kumjulia hali na kwamba nitakuwa huko kwa wiki nzima.
“Wewe utabaki hapahapa, utakuwa unajipikia chakula unachotaka mwenyewe, mchele upo, unga upo, maharage yapo, dengu lipo. Ni wewe tu,” nikamwambia.
“Sawa dada, kwa hiyo wewe utarudi baada ya wiki moja?”
“Nimepanga hivyo lakini tutakuwa tunawasiliana kwa simu. Kama kutakuwa na tatizo lolote utaniambia.”
“Sawa.”
“Nikija nikute nyumba ipo safi, yaani angalia mazingira kama vile uko kwako.”
“Sawa dada.”
Nikafungua pochi yangu na kumpa shilingi elfu thelathini.
“Hizi zitakusaidia kununua vitafunio au kitu chochote unachotaka.”
“Asante dada.”
Nikaondoka. Nilikwenda kwa shangazi. Shangazi alishangaa alipoona naingia na mtoto. Alikuwa akijua kuwa nilikuwa mjamzito lakini habari ya kujifungua hakuwa nayo.
“Ni mwanao huyo?” akaniuliza.
“Ni mwanangu.”
“Umejifungua lini?”
“Kama wiki mbili hivi.”
Nilimdanganya. Ukweli ni kuwa tangu nilipojifungua zilikuwa zimepita karibu wiki nne.
“Mbona hamkuniambia?”
“Mume wngu alikuwa hayupo na mimi mwenyewe baada ya kujifungua nikawa na tatizo la presha ya kushuka, nikalazwa. Nimetoka hospitali jana.”
“Sasa ni nani aliyekuwa anakusaidia.” “Wauguzi wa hospitali walikuwa wakinisaidia na pia majirani zangu walikuwa wanakuja hospitali.”
“Kwa nini hukutuma mtu kuja kuniambia?”
“Niliona nitakutia wasiwasi shangazi, wewe mwenyewe umeshakuwa mtu mzima. Sitaki usumbuke shangazi yangu.”
“Mh! Wewe mtoto una moyo mgumu sana!”
“Yameshapita shangazi, usijali.”
Shangazi akamchukua mwanangu na kumbeba.
“Mmempa jina gani?”
“Siku ile naumwa na uchungu baba’ke ndiyo anaondoka kwenda Burundi, si unajua safari zao…”
“Una maana hajarudi hadi sasa?”
“Hajarudi bado na mimi siwezi kumpa jina mtoto bila yeye.”
“Kwani alikwambia atarudi lini?”
“Huwa haniambii siku ya kurudi, anarudi siku yoyote tu. Inaweza kuchukua hata wiki sita.”
“Kumbe anachelewa sana.”
“Anachelewa.”
“Na hana taarifa kuwa umejifungua?”
“Hana.”
Baada ya kumdanganya shangazi nilikaa kwake kwa siku mbili. Siku ya tatu yake Musa akanipigia simu kunijulisha kuwa anakuja. Siku hiyohiyo nikaondoka kurudi nyumbani kwangu Kimara.
Musa aliporudi usiku alinikuta nyumbani. Akashangaa kunikuta nimeshajifungua.
“Umejifungua lini?”
“Hii ni wiki ya tatu tangu nijifungue.”
“Hongera mke wangu, umenizalia mtoto wa kiume?”
“Wewe ulipenda mtoto wa kike?”
“Wa kwanza akiwa wa kiume ni vizuri.”
“Mpe jina basi?
“Huyu ni baba yangu mzee Ramadhani. Kama angekuwa hai angefurahi kumpata mjina wake.”
“Mbona huniulizi matatizo yaliyonipata?”
“Umepata matatizo gani?”
“Nililazwa hospitali siku tatu, presha ilikuwa imenishuka baada ya kujifungua.”
Eh! Pole sana. Sasa nani alikuwa anakusaidia?”
“Shangazi, nilipotoka hospitali nikaenda kukaa kwa shangazi anisaidie.”
“Inabidi nikutafutie dada wa kazi.”
“Ndiyo nilikuwa nataka kukwambia.”
“Ningejua ningekuja naye, huko vijijini tunakopita kuna wasichana wengi wanaotaka kazi za ndani.”
“Sasa itabidi umtafute hapahapa.”
“Nitajitahidi.”
Siku ile Musa alilala kwa furaha ya kupata mtoto. Asubuhi kulipokucha aliondoka mapema kuliko kawaida yake. Ilipofika saa nne akarudi akiwa na taniboi wake. Alikuwa ameshika mfuko uliokuwa na vitu vya mtoto, nguo, nepi, chandarua na kijigodoro kilichokunjwa, akaviweka juu ya kochi.
Vitu hivyo tayari nilikwishanunuliwa na Mustafa lakini Musa hakuwa na habari.
Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 38

Siku ile Musa alilala kwa furaha ya kupata mtoto. Asubuhi kulipokucha aliondoka mapema kuliko kawaida yake. Ilipofika saa nne akarudi akiwa na taniboi wake. Alikuwa ameshika mfuko uliokuwa na vitu vya mtoto akauweka juu ya kochi.Vitu hivyo tayari nilishanunuliwa na Mustafa lakini Musa hakuwa na habari.
SASA ENDELEA…
Musa akamzungumzia taniboi wake kuhusu suala la dada wa kazi. Taniboi huyo akatuambia kwamba kama tutampa nauli anaweza kumuagiza kutoka kijijini kwao Chalinze.
“Utamuagiza lini?” Musa akamuuliza.
“Nyinyi mnamtaka kwa lini?”
“Ikiwezekana hata kesho.”
“Naweza kumuagiza hii leo kama mtanipatia pesa ya nauli, kesho anaweza kuja.”
“Nauli ya nani sasa, ya wewe kumfuata huko au ya yeye kuja huku?”
“Nauli yake yeye, mimi nitamtumia mama yake kwenye simu.”
“Kwa hiyo atakuja yeye mwenyewe?”
“Ndiyo, atakuja yeye mwenyewe, akifika hapa atanipigia simu nimfuate alikoshukia.”
“Sawa. Nikupatie kiasi gani?”
“Nipe elfu ishirini tu.”
“Tukitoka hapa nitakupa.
Walipoondoka Musa alirudi tena usiku, akaniambia taniboi wake ameshamuagiza dada wa kazi ambaye atanisaidia kazi za ndani. Tulitarajia kuwa angekuja siku iliyofuata lakini hatukuona mtu, siku ya tatu yake ndiyo taniboi wa Musa alipowasili naye nyumbani.
“Anaitwa Mage,” akaniambia kisha akamwambia Mage:
“Aliyekuagiza ndiye huyo na nyumba ambayo utafanya kazi ndiyo hii. Huyo ni mke wa dereva wangu. Naomba uoneshe uaminifu, nidhamu na bidii ya kazi.”
“Sawa. Nitakuwa muaminifu na nitafanya kazi kwa bidii,” Mage akatuambia na siku ile ndipo alipoanza kazi.
Ikapita wiki kabla ya Musa kupata tena safari ya kwenda Burundi. Mara kwa mara nilikuwa nawasiliana na mtumishi wangu wa Mbezi. Nilikuwa nikimuuliza hali ya pale nyumbani na kama Mustafa ametokea.
Majibu yake yalikuwa ya kuniridhisha. Alikuwa akiniambia anaendelea vizuri na hakukuwa na matatizo. Kuhusu Mustafa aliniambia bado hajatokea.
“Utarudi lini dada?” Kila mara alikuwa akiniuliza.
“Siku ya kurudi nitakwambia, usijali.”
Siku ile aliyoondoka Musa kwenda Burundi ndipo nilipompigia simu dada wa kazi wa Mbezi nikamwambia nitakwenda kesho yake. “Angalia kama atatokea Mustafa mwambie nimempeleka mtoto hospitali, usimwambie kuwa niko huku umesikia?”
“Ndiyo dada.”
“Anaweza kugomba kwa sababu sikumuaga.”
“Sasa nimwambie umekwenda hospitali gani na umeondoka muda gani?”
“Muda wowote atakaofika mwambie dada ameondoka sasa hivi kwenda hospitali, halafu nipigie simu uniambie.”
“Akiniuliza mtoto ana nini nimwambieje?”
“Mwambie alikuwa analia sana, mama yake anadhani tumbo linamuuma.”
“Sawa. Umesema utarudi kesho?”
“Natarajia kurudi kesho.”
Niliongea na dada wa kazi huyo asubuhi, nikashinda pale nyumbani hadi jioni. Ilipofika saa moja usiku akanipigia simu:
“Dada kaka amekuja,” akaniambia. Moyo wangu ulishituka kidogo.
“Una maana mume wangu?” nikamuuliza.
“Ndiyo.”
“Umemwamabiaje?”
“Vile ulivyoniambia.”
“Akasemaje?”
“Ameniuliza mtoto alikuwa analia sana, nikamwambia ndiyo alikuwa analia sana.”
“Enhe…”
“Ameniuliza mmekwenda hospitali gani nikamwambia sijui.”
“Alikuwa anataka kutufuata.”
“Labda.”
Sikutarajia kuwa Mustafa angerudi siku ile ambayo nilikuwa nimepangia kulala Kimara. Ile habari ikawa imenishitua.
“Sasa itabidi uje. Usipokuja atajua nimemdanganya,” dada wa kazi akaniambia.
“Nitakuja,” nikamwambia kisha nikakata simu na kuizima kabisa.
Niliogopa kuwa Mustafa angeweza kunipigia na kuniuliza niko hospitali gani, nikakosa jibu. Nikajiandaa kuondoka.
“Mage nimepigiwa simu, shangazi yangu anaumwa naenda huko na nitalala huko huko, ninakuachia nyumba. Mlinzi yupo nje hakuna tatizo,” nikamdanganya Mage.
“Huyo shangazi yuko wapi?” Mage akaniuliza. Maneno yangu yalikuwa yamemuingia.
 
Pre-Std 7 na uandishi huo? Siyo kweli ni uongo wa kufungulia siku.
Hata hivyo hadithi unayoileta hii, ilikwishasimuliwa kitambo humu jf.
Ililetwa kwa mafungu kama unavyofanya wewe.
 
Hii story kwangu ni marudio tu. Kama vile nishawahi kuisoma kwenye gazeti la Shigongo maana miaka iliyopita kidogo sikuwahi kupitwa na gazeti lolote la udaku karibia miaka 4 mfururizo.

Angalia usishtakiwe
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi @Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad @Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO @multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden
bwii ONTARIO Kobe The Vein @Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya SITAKI ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo @shedede kamtu33 SteveMollel Ngushi DONALD stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 Ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush
 
SEHEMU YA 40

Mustafa alinikimbiza na gari hospitali. Nikajifungua usiku mtoto wa kiume. Alikuwa amefanana sana na Mustafa.

Mustafa alikuja hospitali asubuhi, akamkuta mtoto ameshazaliwa. Akampa jina hapohapo. Alimuita Amani.

Nikatabasamu na kumuuliza.

“Umempa jina la nani wako?”

“Ni jina la babu yangu mzaa mama yangu,” akaniambia.

SASA ENDELEA…

Kwa vile nilikuwa na afya njema na mwanangu alikuwa na afya njema, nikaruhusiwa kutoka hospitali asubuhi ileile. Nikarudi Mbezi.

Shangazi yangu alikuwa hajui kama nilikuwa nimejifungua na sikutaka ajue haraka. Pia sikumfahamisha lolote Musa ingawa namba aliyokuwa anaitumia Burundi nilikuwa nayo.

Mustafa aliniletea mfanyakazi wa kunisaidia kazi ili mimi niweze kumlea yule mtoto. Nikajiambia ili niweze kutekeleza mambo yangu vizuri nijenge uhusiano wa kirafiki na yule msichana ili anapogundua siri zangu asimueleze Mustafa.

Nilimpa baadhi ya nguo zangu za thamani. Pia nikawa nampa siri zangu ndogondogo na kumsisitiza kwamba asiwe anamueleza Mustafa maneno yetu.

Yule dada wa kazi ingawa hakutambua dhamira yangu kiundani alinielewa. Tukawa marafiki sana.

Mustafa alipohakikisha kuwa nilikuwa na mtumishi wa kunisaidia, akaanzisha tena safari zake za nje ya nchi ambazo alikuwa amezisimamisha kwa muda.

Siku ile alipoondoka na mimi niliondoka kwenda kwa shangazi lakini mtumishi nilimuacha nyumbani kwa Mustafa. Nilimdanganya kwamba mama yangu aliyekuwa akiishi Ilala alikuwa mgonjwa hivyo nilikuwa nakwenda kumjulia hali na kwamba nitakuwa huko kwa wiki nzima.

“Wewe utabaki hapahapa, utakuwa unajipikia chakula unachotaka mwenyewe, mchele upo, unga upo, maharage yapo, dengu lipo. Ni wewe tu,” nikamwambia.

“Sawa dada, kwa hiyo wewe utarudi baada ya wiki moja?”

“Nimepanga hivyo lakini tutakuwa tunawasiliana kwa simu. Kama kutakuwa na tatizo lolote utaniambia.”

“Sawa.”

“Nikija nikute nyumba ipo safi, yaani angalia mazingira kama vile uko kwako.”

“Sawa dada.”

Nikafungua pochi yangu na kumpa shilingi elfu thelathini.

“Hizi zitakusaidia kununua vitafunio au kitu chochote unachotaka.”

“Asante dada.”

Nikaondoka. Nilikwenda kwa shangazi. Shangazi alishangaa alipoona naingia na mtoto. Alikuwa akijua kuwa nilikuwa mjamzito lakini habari ya kujifungua hakuwa nayo.

“Ni mwanao huyo?” akaniuliza.

“Ni mwanangu.”

“Umejifungua lini?”

“Kama wiki mbili hivi.”

Nilimdanganya. Ukweli ni kuwa tangu nilipojifungua zilikuwa zimepita karibu wiki nne.

“Mbona hamkuniambia?”

“Mume wngu alikuwa hayupo na mimi mwenyewe baada ya kujifungua nikawa na tatizo la presha ya kushuka, nikalazwa. Nimetoka hospitali jana.”

“Sasa ni nani aliyekuwa anakusaidia.” “Wauguzi wa hospitali walikuwa wakinisaidia na pia majirani zangu walikuwa wanakuja hospitali.”

“Kwa nini hukutuma mtu kuja kuniambia?”

“Niliona nitakutia wasiwasi shangazi, wewe mwenyewe umeshakuwa mtu mzima. Sitaki usumbuke shangazi yangu.”

“Mh! Wewe mtoto una moyo mgumu sana!”

“Yameshapita shangazi, usijali.”

Shangazi akamchukua mwanangu na kumbeba.

“Mmempa jina gani?”

“Siku ile naumwa na uchungu baba’ke ndiyo anaondoka kwenda Burundi, si unajua safari zao…”

“Una maana hajarudi hadi sasa?”

“Hajarudi bado na mimi siwezi kumpa jina mtoto bila yeye.”

“Kwani alikwambia atarudi lini?”

“Huwa haniambii siku ya kurudi, anarudi siku yoyote tu. Inaweza kuchukua hata wiki sita.”

“Kumbe anachelewa sana.”

“Anachelewa.”

“Na hana taarifa kuwa umejifungua?”

“Hana.”

Baada ya kumdanganya shangazi nilikaa kwake kwa siku mbili. Siku ya tatu yake Musa akanipigia simu kunijulisha kuwa anakuja. Siku hiyohiyo nikaondoka kurudi nyumbani kwangu Kimara.

Musa aliporudi usiku alinikuta nyumbani. Akashangaa kunikuta nimeshajifungua.

“Umejifungua lini?”

“Hii ni wiki ya tatu tangu nijifungue.”

“Hongera mke wangu, umenizalia mtoto wa kiume?”

“Wewe ulipenda mtoto wa kike?”

“Wa kwanza akiwa wa kiume ni vizuri.”

“Mpe jina basi?

“Huyu ni baba yangu mzee Ramadhani. Kama angekuwa hai angefurahi kumpata mjina wake.”

“Mbona huniulizi matatizo yaliyonipata?”

“Umepata matatizo gani?”

“Nililazwa hospitali siku tatu, presha ilikuwa imenishuka baada ya kujifungua.”

Eh! Pole sana. Sasa nani alikuwa anakusaidia?”

“Shangazi, nilipotoka hospitali nikaenda kukaa kwa shangazi anisaidie.”

“Inabidi nikutafutie dada wa kazi.”

“Ndiyo nilikuwa nataka kukwambia.”

“Ningejua ningekuja naye, huko vijijini tunakopita kuna wasichana wengi wanaotaka kazi za ndani.”

“Sasa itabidi umtafute hapahapa.”

“Nitajitahidi.”

Siku ile Musa alilala kwa furaha ya kupata mtoto. Asubuhi kulipokucha aliondoka mapema kuliko kawaida yake. Ilipofika saa nne akarudi akiwa na taniboi wake. Alikuwa ameshika mfuko uliokuwa na vitu vya mtoto, nguo, nepi, chandarua na kijigodoro kilichokunjwa, akaviweka juu ya kochi.

Vitu hivyo tayari nilikwishanunuliwa na Mustafa lakini Musa hakuwa na habari.

Je, nini kiliendelea? Usikose kufuatilia
 
SEHEMU YA 41

ILIPOISHIA

Back
Top Bottom