Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,662
- Thread starter
- #41
SEHEMU YA 20:
Wakati ule namuaga Amina nikamuona Mustafa ameinuka.
“Unaondoka?” Amina akamuuliza.
“Ndiyo, nataka kwenda nyumbani nioge nibadili nguo. Nilikuwa Kibaha tangu asubuhi.”
“Basi utampa lifti shoga yangu, umuache nyumbani kwake.”
“Hakuna tatizo. Twende Mishi,” Mustafa akaniambia kwa furaha.SASA ENDELEA
Nikanyanyuka kwenye kiti na kumuaga Shabir.
“Shabir kwaheri, tutaonana siku nyingine,” nilimwambia.
“Usijali, tutaonana,” Shabir akaniambia.
Nikaondoka na Mustafa. Tukiwa nje ya hoteli Mustafa alinipakia kwenye gari lake. Alikuwa na gari jipya aina ya Range Rover la rangi nyekundu.
Akaliwasha gari tukaondoka.
“Unaishi wapi?” akaniuliza mara tu alipoliondoa gari.
“Naishi Kimara Baruti.”
“Unafanya kazi wapi Mishi.”
Hapo nilisita kumjibu ukweli kwa vile sikuwa na kazi na nilikuwa nimeolewa. Nikaishia kumuuliza:
“Mimi…?”
“Si ndiyo.”
“Niko nyumbani tu.”
“Uko na wazazi wako?”
Ilibidi nimkubalie.
“Ndiyo, bado naishi na wazazi.”
“Unaonaje tukiwa marafiki?”
Moyo wangu ulishituka ingawa nilitarajia kuwa angeniambia hivyo.
Uso wangu ukawa umepatwa na tabasamu la fadhaa.
“Si tumeshajuana?” nikajidai kumuuliza.
“Kujuana tu haitoshi, nataka tuwe marafiki kabisa.”
Mustafa aliponiona nimesita nikifikiria kumkubalia au kumkatalia alianza kunimwagia sera.
“Unajua nilipokuona pale hotelini moyo wangu ulishituka sana ndiyo maana nilipoona unamuaga shoga yako na mimi nikainuka haraka. Nilikuwa nataka nipate nafasi ya kuzungumza na wewe.”
“Nilikuona na nilijua ulikuwa na jambo.”
Mustafa akacheka.
“Kumbe ulishanisoma?”
“Sasa kitu gani kilichokuvutia?” nikamuuliza kwa kuzuga.
“Ni wewe mwenyewe jinsi ulivyo,” Mustafa alinijibu haraka kama vile jibu hilo lilikuwa mdomoni mwake.
“Nikoje?”
“Mishi unauliza jibu? Au una bwana anakupa pesa nyingi?”
Kabla sijajibu, Mustafa akaongeza:
“Pesa si tatizo kwangu. Juzijuzi tu nilikuwa India. Nimekuja na pikipiki mia mbili.”
“Shabir alituambia wakati ulipompigia simu.”
“Huwa nashirikiana naye.”
Wakati Mustafa akiniambia hivyo mawazo yangu yalikuwa mbali. Nilikuwa kwenye mjadala mkali ndani ya moyo wangu. Upande mmoja wa akili yangu ulitaka nimkubalie kwa sababu ya tamaa ya kupata pesa. Nilijua nikiwa naye pesa ya kuweka akiba haitanisumbua, nitakuwa kama Amina.
Lakini upande mwingine wa akili yangu ulisita kumkubalia kwa sababu nilikuwa mke wa mtu, kuwa na mwanaume mwingine wa pembeni ni jambo ambalo sikulizoea.
Jambo la ajabu ni kuwa wakati nikijadiliana na akili yangu kuhusu suala hilo nilikuwa nikipata ujasiri wa ajabu wa kumkubalia. “We mkubalie tu..unaogopa nini..kwanza mume wako yuko safarini…akija akikaa siku tatu anaondoka tena, akienda huko anakaa mwezi mzima…Mustafa ana gari nzuri anakwenda nchi za nje mara kwa mara… huyo ndiye mwanaume wa kuwa naye…” niliisikia sauti ikinishawishi ndani ya moyo wangu.
Nilijaribu kuipuuza kwa hofu ya kuisaliti ndoa yangu lakini sikuweza. Nikajikuta nikimuuliza Mustafa:
“Kwani wewe huna mke.”
“Mke wangu unaweza kuja kuwa ni wewe,” akaniambia na kunizidisha tamaa.
“Yaani huna mke?” nikamuuliza tena ili nipate uhakika.
“Sijaoa bado.”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu sijampata anayenifaa.”
“Lakini mimi nisingependa kuolewa kwa sasa.”
Nilipotoa jibu hilo nilikuwa nimeshalegea. Nilikuwa kama ngamia niliyesalimu amri nikisubiri kuchinjwa tu.”
“Hata mimi sina nia ya kuoa kwa sasa. Nahitaji tu nipate mwenzangu wa kuniliwaza.”
“Basi usijali, mimi nipo.”
“Utanionesha mtaa unaoishi.”
“Nishushe tu hapahapa.”
Sikutaka Mustafa anifikishe nyumbani kwangu na pia sikutaka aijue nyumba ninayoishi. Akasimamisha gari.
“Umeshafika nyumbani kwenu?” akaniuliza.
“Tumekaribia lakini nataka nishuke hapa, kuna rafiki yangu nataka nimuone.”
“Sasa tutakutana lini tena?” Mustafa akaniuliza.
“Niambie wewe.”
Mustafa alifikiri kidogo kisha akaniambia:
“Nipe namba yako ya simu.”
Nikampa namba yangu na yeye akanipa yake.
“Kabla ya kunipigia kwanza nitumie sms,” nikamwambia.
“Usijali.”Mustafa akanionesha kuwa alikuwa amekusudia hasa kuwa na mimi, alitia mkono mfukoni akatoa pochi yake na kunipa shilingi laki moja.
Je, nini kiliendelea?