SIMULIZI YA KWELI:Niliolewa na wanaume watatu

SIMULIZI YA KWELI:Niliolewa na wanaume watatu

Sure.. Bahati mbaya sikumbuki lilikuwa ni gazeti lipi ila no miongoni ya yanayo milikiwa na shigongo..

Na nilikuwa msomaji kipindi hicho[emoji28]
Basi usiongee kwa sauti acha aendelee kutumwagia mautamu
 
SEHEMU YA 03:
Kumbe mna kazi!” “Wewe ndiye unaona tuna kazi lakini sisi wenyewe tumeshazoea.” Baada ya kumkatisha yale mazungumzo yake ya kunidadisi maisha yangu, nikawa nimemchanganya kidogo, hakunidadisi tena hadi tuliposimamishwa na polisi wa usalama barabarani. Walikuwa polisi wanne waliokuwa wameegesha gari lao pembeni na kusimama kando ya barabara. Nikaogopa. “Wakikuuliza wewe nani, waambie ni mke wangu. Usiseme ni abiria. Haturuhusiwi kuchukua abiria,” dereva Musa akaniambia. Nikamkubalia kwa kichwa. “Ficha hiyo mirungi.” Nikaificha chini ya siti. Ile iliyokuwa midomoni nikaitema haraka. Dereva naye alifanya hivyohivyo. SASA ENDELEA… olisi mmoja akaja kwenye dirisha la upande wa dereva. “Mambo?” Akatuuliza. “Poa.” Dereva akamjibu na kumuuliza. “Inakuwaje?” “Safi. Niambie?” Kabla ya dereva kumjibu kitu, polisi akauliza. “Mnatoka wapi?” Macho yake yalikuwa yakiangaza-angaza ndani ya gari kama yaliyokuwa yakitafuta kitu. “Tunatoka Kigoma,” dereva akamjibu. “Mmepakia abiria?” Moyo wangu ukashituka. “Umemuona wapi abiria?” Dereva akamuuliza. “Si huyo msichana umekaa naye!” “Hapana. Huyu si abiria, ni mke wangu. Natoka naye Kigoma. Alikuwa amekwenda kwao. Nilivyokwenda Kigoma juzi nimeamua nirudi naye.” “Sasa si ameshakuwa abiria?” “Hapana. Ni sisi wenyewe tu. Abiria ni yule anayelipa nauli. Huyu anasaidia kunizuia na michepuko ya njiani.” Polisi huyo akacheka na kumuita mwenzake. “Angalia huyu dereva eti anasema amemchukua mke wake amzuie na michepuko,” akamwambia. Polisi aliyeitwa naye akatuchungulia. “Lakini ni mke wake kweli?” “Jamani ni mume wangu, tumeamua kuja pamoja,” nikasema. “Mmetoka wapi?” “Tumetoka Kigoma,” nikajibu mimi. “Mmepakia nini?” “Kuna bidhaa tu za Wahindi,” alijibu dereva. “Hebu leta risiti zake tuone kama zimelipiwa kodi.” Dereva akachukua mkoba wake aliokuwa ameuweka pembeni mwa mlango wa gari akatoa stakabadhi mbalimbali na kumpatia polisi huyo. “Hebu shuka utueleze,” polisi aliyepokea stakabadhi hizo alimwambia. Dereva akashuka. Walikwenda nyuma ya gari wakazungumza. Baada ya robo saa hivi dereva akarudi peke yake akiwa na stakabadhi zake mkononi.
Alizitia kwenye mkoba wake kisha akaliwasha gari, tukaondoka. “Umewapa ngapi?” Taniboi wake akamuuliza. “Nimewapa elfu tano tu.” “Umewapa za nini?” Nikauliza mimi. “Kawaida tu. Maswali yote yale walikuwa wanataka hela tu.” “Wameangalia huo mzigo?” Nikamuuliza. “Hawakuangalia chochote.” Nikacheka. Dereva akatoa mirungi yake na kuanza kutafuna. Na mimi nikatoa yangu tukaendelea kusaga. Baada ya muda kidogo nilianza kukihisi kile kitu wanachokiita ‘handas’. Nilijiona nimechangamka na kuwa na maneno mengi. Sasa msemaji nikawa ni mimi. Nilikuwa nikieleza kila kitu mpaka nilivyokuwa mtoro shuleni na kuishia darasa la saba. Wakati tunaingia jijini Dar kulikuwa kumeshaanza kupambazuka. Saa ya ndani ya gari ilionesha kuwa ilikuwa saa kumi na moja na dakika arobaini alfajiri. “Sasa mtanipeleka nyumbani?” Nikamuuliza dereva. “Nitakupa nauli upande daladala. Sisi tutaishia hapahapa Kimara,” dereva akaniambia. Alilisimamisha lori pembeni mwa barabara akafungua mlango na kushuka kisha akaniita. Nikashuka kwenye gari. Kichwa kilikuwa kizito kwa mirungi. Uchovu wote wa usingizi ulikuwa umenitoka. Niliposhuka, dereva aliniita nyuma ya gari akanipa shilingi elfu arobani. “Zinakutosha?” Akaniuliza. “Kwa nauli tu zinatosha kabisa. Nashukuru,” nikamwambia. “Naomba namba yako,” akaniambia. Nikampa. Na yeye akanipa yake. “Umesema unaishi Ilala?” “Ndiyo.” “Basi nitakupigia mchana tuzungumze.” “Sawa.” “Nenda kapande daladala uende au wataka nikuongeze mirungi?” “Imetosha. Siwezi kula mingi, kumeshakucha.” Dereva akacheka kisha tukaagana. Nikaenda kupanda daladala. Nilipofika nyumbani, walikuwa bado wamelala. Nikamuamsha shangazi niliyekuwa ninaishi naye. Nikamuamkia na kumwambia kwamba nimerudi. “Umekuja kwa basi gani asubuhi hii?” Akaniuliza. “Nilipata lifti ya lori, nimekuja bure na pesa ya kupanda daladala pia nimepewa.” “Una bahati mwanangu.” “Basi nililopanda kwanza liliharibika njiani, ningefika tangu jana jioni.” Baada ya kuzungumza kidogo na shangazi niliingia chumbani kwangu. Niliweka mkoba wangu nikavua mavazi niliyokuwa nimevaa na kujifunga khanga na taulo. Nikaenda kuoga.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 04:
Baada ya kuzungumza kidogo na shangazi niliingia chumbani kwangu. Niliweka mkoba wangu nikavua mavazi niliyokuwa nimevaa na kujifunga kanga na taulo. Nikaenda kuoga.
Niliporudi nilitaka nilale lakini usingizi ulikuwa umeniruka. Nikawasha TV na kukaa kwenye kochi. Niliangalia matangazo ya magazeti asubuhi ile huku nikimuwaza yule dereva Musa aliyenipa mirungi iliyorusha usingizi wangu.
Nikajiambia kama si yeye huenda muda ule bado ningekuwa njiani, sijafika Dar.
Licha ya kuoga maji baridi nilikuwa nikiona joto kwani mwili ulinichemka sana. SASA ENDELEA…
Ilipofika saa tatu asubuhi wakati nakunywa chai, dereva Musa alinipigia simu, nikaipokea.
“Hallo Musa, vipi huko?” nikamuuliza.
“Huku poa tu, uko wapi?”
“Niko nyumbani?”
“Sasa vipi?”
“Vipi nini?”
“Na wewe unajifanya kama hujui, nataka tukutane.”
“Tukutane wapi?”
“Popote tu tutakapopanga.”
“Kwa ajili gani?”
Musa alisita kabla ya kunijibu;
“Mazungumzo tu,” sauti yake ilikuwa imenywea.
“Yapi sasa, yasiyoongeleka kwenye simu?” nikamuuliza.
“Mbona una maswali mengi?” Ilikuwa sauti ya kubembeleza.
“Lazima nikuulize niweze kukuelewa.”
Alipoona nimembana akabadili mada.
“Unajua kesho asubuhi naondoka.”
“Unakwenda wapi?” nikamuuliza.
“Naenda Burundi. Kuna mzigo napeleka.”
“Ahaa, kesho unakwenda Burundi?”
“Ndiyo, nitaondoka saa kumi na mbili asubuhi.”
“Niletee zawadi.”
“Zawadi gani?”
“Yoyote tu utakayopenda.”
“Nitakuletea japokuwa hukutaka kukutana na mimi leo.”
“Sijakataa isipokuwa sitakuwa na nafasi kwa leo.”
Pakapita ukimya mfupi kabla ya Musa kuniambia;
“Sawa, basi tutakutana hapo nitakaporudi.”
“Unatarajia kurudi lini?”
“Sijui lakini safari zetu zinachukua wiki tatu mpaka nne.”
“Kumbe mnakaa sana?”
“Tunachelewa zaidi kwenye mipaka. Kunakuwa na foleni ndefu za magari.”
“Nakuombea Mungu uende salama na urejee, tukutane.”
“Nashukuru. Nitakupigia kabla sijaondoka.”
“Sawa.”
Musa akakata simu.
Nilipomaliza kunywa chai ndipo nilipoanza kuhisi usingizi. Nikaingia chumbani. Nilijitupa kitandani nikalala hapohapo.
Nilikuja kuamshwa saa saba mchana. Aliniamsha shangazi akaniambia;
“Amka uje ule, chakula tayari.”
Usingizi ulikuwa umenikolea. Sikutaka kuamka.
“Kula tu shangazi, mimi naendelea kulala.”
“Nikuwekee chakula?”
“Kwani umepika nini?”
“Nimepika pure.”
“Usiniwekee.”
Shangazi akaondoka.
Nikaendelea kulala hadi saa nane na nusu nilipoamka na kwenda kuoga.
Niliporudi chumbani mwangu, shoga yangu Amina akanipigia simu. Alikuwa msichana wa Kirangi mwenyeji wa Kondoa Irangi. Tulijuana nilipokuwa shule. Yeye alianzia darasa la nne akitokea Kondoa.
“Niambie Amina…” nikamwambia mara tu nilipopokea simu yake.
“Poa tu. Mzima?”
“Mimi mzima shoga. Mbona kimya sana?”
“Si ndiyo nimekukumbuka shoga yangu.”
“Halafu unajua ndiyo nimerudi kutoka Kigoma.”
“Kumbe ulikwenda Kigoma?”
“Nilikuwa Kigoma tangu juzi. Mwenzangu basi liliharibika njiani. Nimekuja na lori. Tumefika alfajiri. Nimechoka, sina hamu.”
“Tukutane basi tupige stori.”
“Nitakuja nyumbani. Hivi sasa naenda kula chakula. Nikitoka hapo nakuja.”
“Unakwenda kula wapi?”
“Hapo Afrique Restaurant.”
“Nikufuate.”
“Njoo.”
“Basi nakuja.”
“Poa.”
Amina akakata simu.
Nikavaa kisha nikamuaga shangazi na kutoka. Afrique Restaurant ilikuwa mtaa wa tatu kutoka mtaa niliokuwa nikiishi, hivyo niliweza kwenda kwa miguu kwani hapakuwa mbali sana.
Ilikuwa ni sehemu ambayo nilipenda kwenda kula chakula kila nilipokuwa na pesa. Niliwahi kufika mara kadhaa nikiwa na Amina, hivyo alikuwa akipajua vizuri.
Nilipofika hapo nilikuta watu wachache sana. Nilikuta watu wachache kwa sababu haikuwa sehemu inayojaza watu kwa vile vyakula vyake vilikuwa ghali sana. Mimi mwenyewe nilikuwa nakula hapo pale ninapopata pesa za bure kama zile elfu arobaini alizonipa Musa.
Ni kwa sababu nilikuwa napenda sana starehe na maisha ya kifahari.
Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 05:

Musa akakata simu. Baada ya hapo sikulala tena. Nikawa ninamuwaza Musa, dereva wa malori aliyenipa lifti ya gari kutoka Kigoma.
Baada ya muda kidogo simu yangu ikatoa mlio wa kupokea meseji. Nilipoitazama meseji yenyewe, nikaona Musa amenitumia shilingi elfu hamsini. SASA ENDELEA…
Nilipoona ile meseji ya pesa kutoka kwa Musa nilitabasamu peke yangu.
“Hakuniambia kama angenitumia pesa,” nikajisemea.
Nilirejea kwenye eneo la kutuma meseji nikaandika maneno mawili tu.
“Asante sana.”
Kisha nikamtumia Musa. Baada ya muda kidogo, meseji nyingine kutoka kwa Musa ikaingia.
Nilipoisoma ilisema; “Usijali.”
“Yule kaka ananifurahisha sana,” nikaendelea kujisemea peke yangu.
Nilishuka kitandani nikaenda uani kujisaidia kisha nikarudi chumbani na kulala tena.
Kitendo kile cha Musa cha kukumbuka kuniaga na kunitumia shilingi elfu hamsini kilinipa imani kuwa angeniletea zawadi, tena zawadi ya kuridhisha.
Sikukosea. Zilipita wiki tatu hivi. Siku hiyo nilikuwa nyumbani nimelala. Ilikuwa kama saa nane na nusu, Musa akanipigia simu.
Nilipopokea simu yake akaniambia;
“Niko Mlandizi, tunarudi.”
“Poleni kwa safari,” nikamwambia.
“Tunashukuru, safari ilikuwa nzuri.”
Nikataka kumuuliza kuhusu zawadi aliyoniahidi lakini nilisita. Niliona aibu kumuuliza.
Badala yake nikamuuliza kitu kingine.
“Mtaingia saa ngapi Dar?”
“Kwenye saa kumi na moja hivi.”
“Unadhani tutaonana kwa leo?”
“Ni wewe tu. Kama utakuwa na nafasi, njoo pale tuliposimama siku ile tuonane.”
“Nije saa ngapi?”
“Njoo saa kumi na moja.”
“Sawa, nitakuja.”
Baada ya hapo sikulala tena. Nikaanza kujitayarisha. Ilipofika saa tisa na nusu nikatoka. Nilikwenda kupanda daladala hadi Kariakoo kisha nikapanda nyingine iliyonipeleka Kimara.
Wakati ninashuka kwenye daladala Musa akanipigia tena.
“Umeshafika?” akaniuliza.
“Ndiyo nashuka kwenye daladala.”
“Harakisha uje hapa, tumeingia mapema.”
“Sawa, ninakuja.”
Niliposhuka kwenye daladala nikatembea kwa miguu kuelekea pale mahali tulipoachana na Musa siku ile. Nililiona kwa mbali lori lenye trela limeegeshwa mahali hapo. Nikahisi lilikuwa ndilo lori alilokuwa akiendesha Musa.
Nilipolifikia Musa alifungua mlango wa dereva akashuka. Nilifurahi sana kumuona. Alikuwa amependeza sana japokuwa alikuwa anatoka safari.
“Oh! Muadhamu hujambo?” akaniuliza kwa kunichangamkia.
“Sijambo, za safari?”
“Nzuri. Niambie.”
“Poa tu.”
“Kuna mzigo wako ndani ya gari” akaniambia.
“Ni mzigo mkubwa?” nikamuuliza.
“Ni mkubwa kiasi,” akaniambia kisha akafungua mlango wa gari. Akamwambia taniboi wake;
“Hebu shusha lile boksi.”
Taniboi wake akashusha boksi kubwa. Akaliweka chini kando ya mlango.
“Ni nini?” nikauliza.
“Ni sabufa kubwa,” Musa akaniambia na kuongeza;
“Nimeinunua Bujumbura.”
Kwa kweli nilifurahi sana. Nikamuuliza Musa;
“Ndiyo zawadi yangu uliyoniletea?”
“Ndiyo hiyo.”
“Asante sana kwa zawadi nzuri.”
“Itabidi ukodi bajaj. Hili boksi ni kubwa na zito.”
“Sawa. Nitakodi bajaj.”
Musa akamuagiza taniboi wake alete bajaj. Taniboi akaenda kukodi bajaj. Bajaj ilipofika Musa alimwambia alipakie lile boksi. Boksi lilipopakiwa Musa alitoa pochi yake akanipa shilingi laki moja.
Hapo ndipo nilipoanza kumpenda Musa.
“Nitakupigia,” akaniambia baada ya kunipa pesa hizo.
Alikuwa ameshanilegeza.
“Sawa. Nipigie tuzungumze.”
“Okey, basi wewe nenda. Tutazungumza zaidi kwenye simu.”
“Sawa.”
Nikajipakia kwenye bajaj na kuondoka. Ilipofika saa nne usiku nikiwa nyumbani, Musa akanipigia simu tukazungumza sana. Katika mazungumzo yake alinieleza wazi kuwa alitaka kuwa na mimi kimapenzi. Aliniambia alikuwa amenipenda tangu ile siku ya kwanza aliponipa lifti.
Lakini na mimi nilikuwa nimeshampenda. Kilichonifanya nisite kumpa jibu ni kutojua tabia zake. Nilikuwa ninahitaji kujipa muda wa kumchunguza na kujiridhisha naye kabla ya kumkubalia ombi lake.
“Usijali, ninakufikiria,” nikamwambia.
“Nitakuja kukutembelea huko Ilala kesho.”
“Karibu. Utakuja mida gani?”
“Itakuwa jioni.”
“Kama saa ngapi?”
“Nafikiri itakuwa saa kumi.”
Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA

Musa akakata simu. Baada ya hapo sikulala tena. Nikawa ninamuwaza Musa, dereva wa malori aliyenipa lifti ya gari kutoka Kigoma. Baada ya muda kidogo simu yangu ikatoa mlio wa kupokea meseji. Nilipoitazama meseji yenyewe, nikaona Musa amenitumia shilingi elfu hamsini.

SASA ENDELEA…



Nilipoona ile meseji ya pesa kutoka kwa Musa nilitabasamu peke yangu. “Hakuniambia kama angenitumia pesa,” nikajisemea Nilirejea kwenye eneo la kutuma meseji nikaandika maneno mawili tu. “Asante sana.” Kisha nikamtumia Musa. Baada ya muda kidogo, meseji nyingine kutok kwa Musa ikaingia. Nilipoisoma ilisema; “Usijali.” “Yule kaka ananifurahisha sana,” nikaendelea kujisemea peke yangu. Nilishuka kitandani nikaend uani kujisaidia kisha nikarudi chumbani na kulala tena. Kitendo kile cha Musa cha kukumbuka kuniaga na kunitumia shilingi elfu hamsini kilinipa imani kuw angeniletea zawadi, tena zawadi ya kuridhisha. Sikukosea. Zilipita wiki tatu hivi. Siku hiyo nilikuwa nyumbani nimelala. Ilikuwa kama saa nane na nusu, Musa akanipigia simu. Nilipopokea simu yake akaniambia; “Niko Mlandizi, tunarudi.” “Poleni kwa safari,” nikamwambia. “Tunashukuru, safari ilikuwa nzuri.” Nikataka kumuuliza kuhusu zawadi aliyoniahidi lakini nilisita. Niliona aibu kumuuliza. Badala yake nikamuuliza kitu kingine. “Mtaingia saa ngapi Dar?” “Kwenye saa kumi na moja hivi.” “Unadhani tutaonana kwa leo?” “Ni wewe tu. Kama utakuwa na nafasi, njoo pale tuliposimama siku ile tuonane.” “Nije saa ngapi?” “Njoo saa kumi na moja.” “Sawa, nitakuja.” Baada ya hapo sikulala tena. Nikaanza kujitayarisha. Ilipofika saa tisa na nusu nikatoka. Nilikwenda kupanda daladala hadi Kariakoo kisha nikapanda nyingine iliyonipeleka Kimara. Wakati ninashuka kwenye daladala Musa akanipigia tena. “Umeshafika?” akaniuliza. “Ndiyo nashuka kwenye daladala.” “Harakisha uje hapa, tumeingia mapema.” “Sawa, ninakuja.” Niliposhuka kwenye daladala nikatembea kwa miguu kuelekea pale mahali tulipoachana na Musa siku ile. Nililiona kwa mbali lori lenye trela limeegeshwa mahali hapo. Nikahisi lilikuwa ndilo lori alilokuwa akiendesha Musa
Nilipolifikia Musa alifungua mlango wa dereva akashuka. Nilifurahi sana kumuona. Alikuwa amependeza sana japokuwa alikuwa anatoka safari. “Oh! Muadhamu hujambo?” akaniuliza kwa kunichangamkia. “Sijambo, za safari?” “Nzuri. Niambie.” “Poa tu.” “Kuna mzigo wako ndani ya gari” akaniambia. “Ni mzigo mkubwa?” nikamuuliza. “Ni mkubwa kiasi,” akaniambia kisha akafungua mlango wa gari. Akamwambia taniboi wake; “Hebu shusha lile boksi.” Taniboi wake akashusha boksi kubwa. Akaliweka chini kando ya mlango. “Ni nini?” nikauliza. “Ni sabufa kubwa,” Musa akaniambia na kuongeza; “Nimeinunua Bujumbura.” Kwa kweli nilifurahi sana. Nikamuuliza Musa; “Ndiyo zawadi yangu uliyoniletea?” “Ndiyo hiyo.” “Asante sana kwa zawadi nzuri.” “Itabidi ukodi bajaj. Hili boksi ni kubwa na zito.” “Sawa. Nitakodi bajaj.” Musa akamuagiza taniboi wake alete bajaj. Taniboi akaenda kukodi bajaj. Bajaj ilipofika Musa alimwambia alipakie lile boksi. Boksi lilipopakiwa Musa alitoa pochi yake akanipa shilingi laki moja. Hapo ndipo nilipoanza kumpenda Musa. “Nitakupigia,” akaniambia baada ya kunipa pesa hizo. Alikuwa ameshanilegeza. “Sawa. Nipigie tuzungumze.” “Okey, basi wewe nenda. Tutazungumza zaidi kwenye simu.” “Sawa.” Nikajipakia kwenye bajaj na kuondoka. Ilipofika saa nne usiku nikiwa nyumbani, Musa akanipigia simu tukazungumza sana. Katika mazungumzo yake alinieleza wazi kuwa alitaka kuwa na mimi kimapenzi. Aliniambia alikuwa amenipenda tangu ile siku ya kwanza aliponipa lifti. Lakini na mimi nilikuwa nimeshampenda. Kilichonifanya nisite kumpa jibu ni kutojua tabia zake. Nilikuwa ninahitaji kujipa muda wa kumchunguza na kujiridhisha naye kabla ya kumkubalia ombi lake. “Usijali, ninakufikiria,” nikamwambia. “Nitakuja kukutembelea huko Ilala kesho.” “Karibu. Utakuja mida gani?” “Itakuwa jioni.” “Kama saa ngapi?” “Nafikiri itakuwa saa kumi.”
 
SEHEMU YA 07:

Lakini na mimi nilikuwa nimeshampenda. Kilichonifanya nisite kumpa jibu ni kutojua tabia zake. Nilikuwa ninahitaji kujipa muda wa kumchunguza na kujiridhisha naye kabla ya kumkubalia ombi lake. “Usijali, ninakufikiria,” nikamwambia. “Nitakuja kukutembelea huko Ilala kesho.” “Karibu. Utakuja muda gani?” “Itakuwa jioni.” “Kama saa ngapi?” “Nafikiri itakuwa saa kumi.”


SASA ENDELEA…

Sasa tutakutana wapi?” Nikamuuliza. “Niambie wewe.” “Nitakusubiri kwenye kituo cha daladala zinazotoka Kariakoo.” “Sawa, basi nisubiri hapo saa kumi.” “Usijali.” Musa akakata simu. Nilikuwa nimepanga maswali yangu ya kumuuliza nitakapokutana naye. Majibu yake ndiyo yangekuwa vigezo muhimu kwa upande wangu vya kuamua kuwa naye au kuacha kuwa naye. Siku ya pili ikawadia. Nikaisubiri saa kumi kwa hamu. Mpaka ilipofika saa tisa na nusu nilikuwa nimeshajitayarisha. Nilivaa nguo yangu nzuri na kujitia manukato ya kuvutia, nikatoka. Mwendo wa robo saa tu ukanifikisha kwenye kituo cha daladala. Nilitaka tukutane hapo kwa sababu sikuwa na mahali pengine ambapo ningemtajia na yeye akaweza kupaelewa kwa urahisi. Kabla hata ya kufika saa kumi kamili Musa akashushwa na pikipiki. Nilihisi ilikuwa bodaboda kwani mara tu baada ya kuteremka alimlipa mwenye pikipiki. Alikuwa hajaniona mpaka nilipomfuata na kumgusa bega. Musa akagutuka na kugeuka upande niliokuwa nimesimama. “Oh Mariam. Nilikuwa nataka nikupigie simu,” akaniambia. Mkono wake tayari ulikuwa mfukoni. Alikuwa bado akiniita Mariam baada ya kumdanganya siku ile. “Unipigie simu ya nini?” Nikamuuliza kivivu. “Nikwambie nimeshafika.” “Kwani si tulipatana tukutane hapa saa kumi?” “Kwa hiyo?” “Ni wajibu wangu, mimi nije hapa na wewe uje hapa, si suala la kupigiana simu tena.” “Nilikuwa sijakuona.” “Twende zetu,” nikamwambia. Ilikuwa kidogo nimshike mkono kama vile tayari tulikuwa wapenzi. Tukafuatana kuelekea upande wa Buguruni. “Tunakwenda wapi?” Akaniuliza. “Kwani wewe unataka twende wapi?” Na mimi nikamuuliza. “Sehemu yoyote tu ya kupumzika.” “Ndiyo tunakwenda.” Pakapita kimya kifupi kabla ya Musa kuniuliza.
Inaendekea Vipi sabuufa linatoa vizuri?” “Sana. Tangu asubuhi nilikuwa nasikiliza muziki tu!” Tulikwenda kwenye hoteli moja, tukaingia na kukaa kwenye viti. Musa akaniuliza nilikuwa nahitaji kinywaji gani. Sikutaka kutaja kilevi chochote, nikaagiza soda tu. Na yeye akaagiza soda. Tukaanza mazungumzo. Mazungumzo yetu yalikwenda mpaka yakafika mahali ambapo niliweza kumuuliza Musa kama alikuwa ameshaoa. “Nimeshaoa,” akanijibu. Hicho kingekuwa kigezo cha kutosha cha kumkataa Musa japokuwa nilishaanza kumpenda. Nikajidai natabasamu nilipomuuliza tena. “Una watoto wangapi?” “Mtoto wangu alikuwa mmoja na alishafariki dunia. Kwa sasa sina mtoto.” “Kwani mke wako hana ujauzito tena?” “Tulishaachana muda mrefu.” “Uliponiambia umeshaoa nilijua una mke.” “Ulikosea kuniuliza. Ungeniuliza una mke ningekwambia sina lakini umeniuliza umeshaoa, ndiyo maana nikakujibu nimeshaoa lakini haikuwa na maana kuwa nina mke.” “Hapo nimekuelewa. Mliachana lini na mke wako?’ “Karibu miaka mitatu sasa.” “Kwa nini mliachana.” “Ni kwa sababu binafsi.” “Niambie.” “Riziki inapokwisha watu mnaachana tu.” Nikatikisa kichwa. “Lazima kuna sababu. Inaonekana wewe una matatizo.” “Hapana. Yule mwenzangu ndiye aliyekuwa na matatizo. Wivu aliuzidisha kupita kiasi. Kila siku tulikuwa tunagombana kwa sababu ya wivu wake.” “Kwa hiyo ndiyo ukaona umuache?” “Siyo kwamba niliona nimuache, sote wawili tulifikia uamuzi kuwa tuachane kwa sababu tusingeweza kuishi katika hali ile ya kugombana kila siku.” “Sasa kwa nini hujaoa kipindi chote hicho?” “Bado niponipo kwanza.” Aliposema hivyo tukacheka. “Unajua Musa unaonekana una mabibi wengi, vinginevyo ungekuwa umeshaoa. Huwezi kukaa kipindi chote hicho bila mke.” “Unaweza kunidhania hivyo kwa vile hujui tabia yangu lakini mimi ni mtu ninayejichunga sana. Sina tabia za kipuuzi, ndiyo maana nimechelewa kuoa. Ninataka ninapooa niwe nimeoa mke siyo jike.” “Lakini msichana wa nje huwezi kukosa japokuwa mmoja.” “Nataka uwe wewe. Wewe ndiye chaguo langu.” “Unataka kunioa au…” “Kuoana ni matokeo tu kama tutaoneshana tabia nzuri na mapenzi ya dhati baina yetu.” “Unaishi wapi?” “Mimi nipo Kimara.” “Unaishi katika nyumba yako au ya kupangisha?
 
SEHEMU YA 08;

Sina tabia za kipuuzipuuzi, ndiyo maana nimechelewa kuoa. Ninataka ninapooa niwe nimeoa mke siyo jike.”

“Lakini msichana wa nje huwezi kukosa japokuwa mmoja.”
“Nataka uwe wewe. Wewe ndiyo chaguo langu.”
“Unataka kunioa au…”

“Kuoana ni matokeo tu kama tutaoneshana tabia nzuri na mapenzi ya dhati baina yetu.”
“Unaishi wapi?”
“Mimi niko Kimara.”
“Unaishi katika nyumba yako au ya kupangisha?”
SASA ENDELEA…

“Ni nyumba ya kupangisha.”
“Unaishi peke yako humo ndani?”
“Tuko familia mbili, mimi na mwenzangu lakini hatukutani. Kila mtu yuko upande wake.”
“Kama unaishi hivyo ni vizuri kwa sababu unaepukana na umbeya.”

“Tatizo linakuwa ninaposafiri, inabidi nimlete ndugu aje alale hadi ninaporudi. Kwa sababu ya kulinda nyumba, siku hizi wezi ni wengi” “Ndiyo hivyo. Je wewe mwenzangu unaishi kwenu au…?” Musa naye akaniuliza. “Kwanza mimi wazazi wangu wote wawili walishafariki, ninaishi na shangazi yangu.”
“Uliwahi kuchumbiwa au kuolewa?”

“Masomo yenyewe nimemaliza mwaka jana tu, kidato cha nne.” Hapo nilisema uongo ili aone nimesoma na bado ni mdogo. “Kumaliza masomo mwaka jana si hoja kwamba usipate mume akakuchumbia.”
“Labda nikwambie sijachumbiwa wala sina mume.”

“Sasa unashughulika na nini?”
“Kwa sasa nipo nyumbani tu.”
“Mbona sikuelewi, nakumbuka siku ile tulipokuwa tunatoka Kigoma uliniambia kuwa unaleta mchele kutoka Mbeya?”

Ndiyo maana unaambiwa njia ya muongo fupi na ukiwa muongo usisahau. Nilikuwa nimeshasahau kama nilimdanganya hivyo. Kumbe mwenzangu bado anakumbuka. Nikatunga uongo mwingine.
“Wewe umeniuliza kwa sasa ninashughulika na nini, ndiyo nikakujibu niko nyumbani. Hiyo biashara ya mchele ninayo, sema kwa sasa nimepumzika kidogo.”

Pakapita kimya cha sekunde kadhaa. Musa alikuwa ameukubali uongo wangu. Alikuwa akinywa soda huku akipepesa macho yake akitafuta la kuniambia. Mimi nilikuwa nimeinamia chupa ya soda huku nikiivuta kwa mrija taratibu. Hakuwa akijua kwamba nilikuwa namtazama kwa pembeni mwa macho yangu.

“Sasa Mariam utakuja lini kunitembelea nyumbani?” akaniuliza ghafla baada ya kuuchomoa mrija midomoni. “Wewe unataka nije lini?”
“Mimi nataka hata leo.”
“Kwa leo haitawezekana, tupange siku nyingine.”
“Kama lini?”

“Nitakwambia siku ya nafasi yangu, usijali.”
“Kwa nini usiniambie hii leo.”
“Musa mbona una haraka hivyo?”
Musa akacheka. Nikayaona meno yake. Licha ya kula mirungi na kuvuta sigara, yalikuwa meupe na yenye mwanya wa juu. Niliyapenda.

“Unacheka nini?” nikamuuliza kwa mzaha ingawa nilishajua kilichomchekesha.
“Nimecheka kwa hivyo ulivyoniambia kuwa nina haraka.”
“Harakaharaka haina Baraka,” nikamwambia.
“Ninajua lakini ngojangoja nayo huumiza matumbo!”

Hapo na mimi nikacheka. Musa aliponiona nacheka naye akacheka.
Mpaka tunaondoka hapo hotelini sikuwa nimempa ahadi yoyote ya kwenda kwake zaidi ya kumwambia asubiri.

Nikamsubirisha sana. Zilipita wiki nne. Nilikuwa nikimsumbua tu na yeye hakukata tamaa wala kuonesha kuchukia. Katika kipindi chote hicho tulikuwa tukiwasiliana na alikuwa akinipa pesa pamoja na zawadi mpaka nikawa namtegemea yeye kipesa kwani sikuwa na mwanaume mwingine.

Napenda niseme kuwa kwa mtindo wake huo alinilegeza, nikawa mdogo kama piritoni na nikalegea kama mnyoo. Nilikuwa kama mbuzi niliyekwishatiwa mikononi na kusalimu amri, nilichokuwa nasubiri ni kuchinjwa tu!

Hivyo ndivyo nilivyoanza uhusiano na Musa dereva wa malori. Uhusiano wetu haukukaa sana ukawa uchumba. Siku ile ambayo Musa aliifikisha barua ya uchumba kwa shangazi yangu nilifurahi sana.
Barua yake ilipokelewa na siku ya pili yake akarudishiwa majibu ya kukubaliwa kwani uhusiano wetu ulikuwa ukifahamika.

Mwezi mmoja baadaye Musa alilipa mahari yangu, sasa tukajiandaa kufunga ndoa.
Wakati ule wa maandalizi ya ndoa ndipo nilipomtonya rafiki yangu Amina. Nilimpigia simu nikamuita nyumbani. Alipokuja ndipo nikamueleza kwamba nataka kuolewa.
Amina akashituka.

“Unaolewa na nani?” akaniuliza kwa shauku.
“Naolewa na Musa.”
“Musa huyu mwanaume wako, dereva wa malori?”
“Ndiye huyohuyo dada.”

“Mbona mmeharakisha hivyo?”
“Ah! Mwenyewe ndivyo alivyotaka.”
“Ni hatua nzuri. Sasa ndoa yenyewe itakuwa lini?”

“Ndiyo tuko kwenye maandalizi, hatujapanga siku lakini haitachukua muda mrefu.”
“Hongereni kwa kufikia uamuzi huo lakini nataka uje unitambulishe kwa mchumba wako kabla hamjafunga ndoa. Unajua sijawahi kukutana naye!”
“Basi subiri Jumapili, tutakuwa hoteli fulani nitakuita.”
“Hapahapa Ilala?”

“Ndiyo, itakuwa hapahapa Ilala.”
“Saa ngapi?”
“Itakuwa mida mida ya usiku.”
“Poa. Nataka nimuone tujuane kabla ya ndoa yenu.”
“Usijali.”

Je, nini kiliendelea?
 
SEHEMU YA 09:

“Nawapongeza kwa kufikia uamuzi huo lakini nataka uje unitambulishe kwa mchumba wako kabla hamjafunga ndoa. Unajua sijawahi kukutana naye!”
“Basi subiri Jumapili, tutakuwa hoteli fulani nitakuita.”
“Hapahapa Ilala?”

“Ndiyo, itakuwa hapahapa Ilala.”
“Saa ngapi?”
“Itakuwa midamida ya usiku.”
“Poa. Nataka nimuone tujuane kabla ya ndoa yenu.”
“Usijali.”
SASA ENDELEA…

aada ya mazungumzo yetu na Amina tuliagana, Amina akaondoka.
Kwa kawaida kila siku ya Jumapili, kama Musa hakwenda safari huwa tunakutana katika hoteli moja pale Ilala. Tunakula chakula cha usiku na kuzungumza machache kisha anaondoka zake.
Jumapili ilipowadia Amina alinipigia simu kunikumbusha juu ya ile ahadi yetu. Nikamwambia kuwa ninaikumbuka.

“Tutakapokuwa wote nitakupigia,” nikamwambia nikimaanisha nitakapokuwa na mchumba wangu Musa nitampigia ili aje.

Saa moja usiku Musa akanipigia simu kunijulisha kuwa ameshafika hapo hotelini. Hapakuwa mbali sana na nyumbani kwetu. Na mimi nikampigia Amina.
Nikamwambia nikutane naye hapo hotelini. Baada ya kumweleza hivyo nikaanza mwendo wa miguu kuelekea huko hotelini. Nikiwa njiani nilimpigia tena Musa kumjulisha kuwa nitakuwa na rafiki yangu.
“Nani?” Akaniuliza.

“Humjui, ndiyo nataka nikutambulishe.”
“Anaitwa nani.”
“Amina.”
“Uliwahi kunitajia jina lake lakini sijawahi kukutana naye.”
“Ndiyo nataka leo umuone mjuane.”
“Sawa. Ninawasubiri.”
“Poa.”

Nikakata simu.
Wakati nafika pale hotelini nilikutana na Amina kwenye mlango.
“Eh! Shoga umekuja na bodaboda nini?” Nikamuuliza kwa mshangao.
“Kwa nini?” Akaniuliza.

“Jinsi ulivyowahi ni kama uliyekuja na usafiri.”
“Hapana nimekuja kwa miguu tu,” Amina aliniambia kisha akacheka.
“Au ni hamu ya kumuona shemeji yako?” Nikamuuliza kwa mzaha.
Amina akaendelea kucheka.
“Umejuaje?”

Aliponiambia hivyo tukacheka sote.
“Wala usiumie shoga, shemeji yako utamuona leo tena yeye ameshafika,” nikamwambia.
“Yuko wapi?”
“Yuko ndani.”
“Twen’zetu nikamuone.”

Tukaingia ndani ya hoteli. Tulimkuta Musa akiwa amekaa kwenye meza ya peke yake akitusubiri. Nilimuona akitafunatafuna, nikajua alikuwa anatafuna mirungi kisirisiri. Mezani kwake kulikuwa na chupa ya cocacola na ya maji safi.

Alipotuona alijifuta midomo yake kwa kitambaa kisha akakaa vizuri.
“Vipi unasaga?” Nikamuuliza.
“Umejuaje?”

“Si nimekuona unatafuna halafu umeweka chupa ya maji na cocacola.”
“Nilikuwa namalizia miti yangu ya mchana. Sijui hii tasnima yangu nitaiweka wapi?”
“Tasnima ndiyo nini?”

Nikavuta kiti na kuketi. Amina naye akaketi.
“Hili tonge la mirungi lililoko mdomoni,” Musa akanijibu.
“Ndiyo linaitwa tasnima?”
“Ndiyo.”
“Na ninyi mna maneno ya ajabuajabu, eti tasnima!” Nikamtazama Amina kisha nikacheka.

Nilijua Amina pia alitaka kucheka lakini alijikaza kwa kumuonea aibu shemeji yake.
“Amina shemeji yako huyo, umuone, umjue, umfahamu,” nikamwambia Amina.
“Shemeji habari za siku?” Amina akamsalimia Musa huku akimpa mkono.
“Nzuri shemeji.”

“Musa huyo ni rafiki yangu kipenzi, anaitwa Amina,” nikamwambia Musa.
“Oh! Nimefurahi kumfahamu, karibu shemeji.”
“Sasa hilo tasnima lako si uende ukalitupe nje,” nikamwambia Musa.
“Hili halitupwi, linahifadhiwa tu kisha baadaye ninalirudisha mdomoni.”
“Amina unawasikia watu wa mirungi hao?” Nikamuuliza Amina.
“Lakini si uliniambia hata wewe unakula,” Amina akaniambia.
“Nakula lakini siyo kivile.”

“Sasa ni nyote.”
“Hebu nisaidie shemeji yangu, asinisakame mimi kumbe na yeye pia yumo,” Musa akasema.
Kikafuatia kicheko.
“Hebu kalitupe bwana…” nikamwambia Musa baada ya kucheka.
Musa akainuka na kutoka.

“Naona mnapendana sana,” Amina akaniambia.
“Umeona eeeh!”
Mhudumu akatufuata na kukatiza mazungumzo yetu. Alitupa menyu. Nikaangalia orodha ya vyakula kisha nikamwambia.

“Ngoja bwana mkubwa aje.”
Mhudumu huyo akaondoka.
Musa aliporudi nikamuuliza.
“Tutakula nini?”

“Kila mtu atakula anachopenda.”
“Mimi nataka chipsi kuku,” nikasema kisha nikamtazama Amina.
“Utakula nini Amina?” Nikamuuliza.
“Nitakula hizohizo chipsi kuku.”

Je, nini kiliendelea? Usikose kufuatilia
 
Back
Top Bottom