Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

  • Thread starter Kanungila Karim
  • Start date
SPYMATE

SPYMATE

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2013
Messages
994
Points
1,000
SPYMATE

SPYMATE

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2013
994 1,000
Jamaa wamemtimua kwenye group lao baada ya kumbaini ndiye anayevujishia humu.
 
demigod

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Messages
5,123
Points
2,000
demigod

demigod

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2015
5,123 2,000
SEHEMU YA 09.

Sikupata hata muda wa kujibu chochote, Raya akanikumbatia kwa nguvu mwilini na kuanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, japokuwa sikuwa tayari kwa alichokuwa anakitaka, nilijikuta kwenye wakati mgumu mno, kwani ukichanganya joto la mwili wake na uzuri aliokuwa nao, ukizingatia kwamba tulikuwa wawili tu, nilijikuta nikishindwa cha kuamua, ‘Jamal’ wangu naye akaanza usumbufu.
SASA ENDELEA…
Nilishindwa kujizuia, na mimi nikamkumbatia Raya, kitendo ambacho kilimfurahisha mno, akausogeza mdomo wake kwangu, nami nikafanya hovyohivyo, ndimi zetu zikagusana, nikamsikia akitoa migumo ambayo ilizidi kuipagawisha akili yangu.
Japokuwa sikuwa mtaalamu sana kwenye mambo ya kikubwa, nilijitahidi kadiri ya uwezo wangu kumuonesha Raya kwamba na mimi sikuwa mshamba, ‘amsha-amsha’ ziliendelea na hatimaye kipyenga kikalia kuashiria kuanza kwa mpambano wa kukata na shoka, usio na refa wala jezi, huku nikishindwa kuzidhibiti papara zangu.
Wakati nikijiandaa kusakata kabumbu, ghafla mawazo juu ya Shenaiza na kilichokuwa kinaendelea kule nyumbani kwangu yalipita kwa kasi kubwa ndani ya kichwa changu, nikashangaa ‘Jamal’ wangu ambaye muda mfupi uliopita alikuwa ngangari ile kinoma, akianza kunywea na kupoteza kabisa ukakamavu wake.
Raya ambaye tayari alishajiweka tayari kupokea ‘mashuti’ ya nguvu kutoka kwangu, alishtushwa na kilichotokea, akaacha kila alichokuwa anakifanya.
“Vipi tena jaman mpenzi wangu, na..ta…ka…,” alisema Raya kwa sauti iliyokuwa ikikatakata, ikitokea kwenye matundu ya pua zake.
“Subiri kidogo,” nilisema kwa aibu kubwa, sikuwahi kutokewa na hali kama hiyo hata mara moja, nikashangaa imekuwaje? Sikupata jibu. Ili kuzuga, ilibidi niamke na kujifanya nataka kwenda maliwatoni, nikamuacha Raya amelala palepale huku akiwa kimya kabisa, akionesha kuugulia maumivu ya ndani kwa ndani.
Harakaharaka nilitoka na kuelekea choo cha ndani, nikajifungia mlango na kuanza kutafakari kuhusu kilichotokea. Nilijisikia aibu sana kwani sikujua Raya atanichukuliaje kama amenitafunia kila kitu na kuniwekea kabisa mdomoni lakini nimeshindwa kumeza. Japokuwa ulikuwa ni usiku sana na kulikuwa na baridi, nilifungulia maji ya bomba la mvua na kuanza kujimwagia. Nilisimama huku maji yakiendelea kunimwagikia kwa zaidi ya dakika tatu mpaka nikaanza kutetemeka kwa baridi.
Nikafunga bomba na kurudi chumbani ambako nilimkuta Raya amelala vilevile kama nilivyomuacha. Nikawa najisemeshasemesha ili ‘kuua soo’, nikajifuta maji na kupanda kitandani, nikamvutia Raya kifuani kwangu ambapo alikuja mzimamzima, ni hapo ndipo nilipogundua kwamba kumbe alikuwa akilia.
Lawama zake kubwa kwangu ni kwamba sikuwa nikimpenda na ndiyo maana nilimfanyia hivyo lakini kiukweli, wala sikuwa nimepanga hayo yatokee bali nilijikuta tu nikiishiwa ukakamavu.
Nikawa nambembeleza kwa maneno matamu na kwa mara ya kwanza nikamtamkia kwamba nampenda sana japokuwa nilisema vile ili kumtuliza. Alifurahi sana aliposikia maneno hayo kutoka kwangu, nikamuona akitabasamu na kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, na mimi nikawa naonesha ushirikiano.
Niliamini safari hii nitaweza kukata kiu yake kwani ‘Jamal’ wangu naye alishaanza kuonesha ushirikiano, akawa anafura kwa hasira na kunipa matumaini makubwa kwamba nitaifuta aibu kubwa iliyokuwa inataka kunikabili.
Tuliendelea kufanya ‘warm-up’ kwa dakika kadhaa lakini safari hii Raya alionesha kutotaka kuchelewesha tena mambo, kabla hata kipyenga cha kuashiria kuanza kwa mpambano hakijalia, yeye alitaka kujianzishia mpira mwenyewe.
Katika hali ambayo sikuitegemea, mawazo juu ya Shenaiza yalijirudia tena akili mwangu, nikawa sijui nini kilichoendelea baada ya mimi kuondoka, kama ilivyokuwa mwanzo, ‘Jamal’ wangu akanywea, jambo lililomkasirisha sana Raya, safari hii akawa analia kwa sauti kama mtu aliyepokea taarifa za msiba.
“Kwa nini unanitesa hivi Jamal? Kwani mimi nina kasoro gani mpaka unifanyie hivi?” alisema huku akilia, nikaanza upya kazi ya kumbembeleza huku nikijisikia aibu kubwa ndani ya moyo wangu. Haikuwa kazi nyepesi kumtuliza Raya mpaka atulie, nikawa najaribu kujikakamua na kumfosi ‘Jamal’ wangu arudi tena mchezoni lakini ilikuwa sawa na kazi bure.
Mpaka kunapambazuka, hakuna kilichofanyika zaidi ya kubembelezana, saa kumi na moja alfajiri, wote tulipitiwa na usingizi mzito na tulipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni saa moja za asubuhi. Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuzinduka, nikajaribu kujikakamua tena kuona kama angalau naweza kufanya chochote lakini ilikuwa sawa na kazi bure, Jamal wangu alikuwa amelala doro, jambo lililonifadhaisha sana.
Muda mfupi baadaye Raya naye aliamka, macho yake yakiwa yamevimba na kuwa mekundu kutokana na kulia sana, akaenda chumbani kwake na kuniacha nikijiandaa. Baada ya kumaliza kujiandaa, nilitoka hadi sebuleni ambako nilimkuta Raya akiandaa kifungua kinywa.
Ule uchangamfu aliokuwa nao kwangu uliyeyuka kama theluji iyeyukavyo juani. Nilitamani sana ajue kwamba sikuwa nimemfanyia makusudi bali lilikuwa ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wangu lakini haikuwezekana, alichoamini Raya ni kwamba sikuwa nampenda na nilifanya vile kumkomoa.
Tulipata kifungua kinywa kimyakimya, kwa kuwa sikuwa najua kilichotokea nyumbani kwangu usiku ule, sikuwa na muda wa kuendelea kukaa pale, nilimuaga Raya na kumwambia tutakutana kazini baadaye lakini cha ajabu, alikataa katakata kuniacha niondoke peke yangu, akaniambia atanisindikiza na kama ni kuomba ruhusa kazini, niombe ya watu wawili, mimi na yeye.
Ulikuwa ni mtihani mkubwa sana kwangu kwa sababu kwa kilichotokea kati yangu na yeye, nilihitaji kupata muda wa kukaa peke yangu na kutafakari kwa kina kilichosababisha hali ile iliyonitokea usiku.
Lakini kubwa zaidi, sikutaka kumuingiza kwenye matatizo yangu na Shenaiza, kwa kuwa nilikuwa nimeyaanza mwenyewe, nilitaka nikayamalize mwenyewe. Hata hivyo, sikutaka pia kuendelea kumuudhi, ikabidi nimkubalie ambapo tulitoka na safari ya kuelekea nyumbani kwangu ikaanza.
Tukiwa njiani nilimpigia simu bosi kazini na kumueleza kwamba nilikuwa nimepatwa na matatizo makubwa na kwamba nitachelewa kufika kazini. Sikutaka kumfafanulia kilichotokea, kwa bahati nzuri alinielewa. Nilimpigia pia simu Justice na kumtaka asizungumze chochote kazini kuhusu nilichomwambia jana yake.
“Sasa mbona umeomba ruhusa peke yako? Kwa nini usiniombee na mimi kama tulivyokubaliana?” Raya aliniuliza kwa sauti ya chini, iliyoonesha dhahiri kwamba hakuwa na furaha, Nilishindwa cha kumjibu zaidi ya kumtaka apige mwenyewe simu na kuomba ruhusa kivyake ili tusije kuonekana kwamba tumepanga kutega kazi kwa makusudi.
Kwa bahati nzuri naye alikubaliwa, tukaendelea na safari ya kuelekea kwangu kwa kutumia Bajaj ambayo Raya ndiye aliyelipa, kadiri tulivyokuwa tunazidi kukaribia kwangu ndivyo mapigo ya moyo wangu yalivyokuwa yanazidi kuongezeka, sikujua nitakutana na nini.
Nilimuelekeza dereva njia ya kupita kwani sikutaka kutokezea upande wa mbele wa mtaa niliokuwa naishi, nilitaka tutokezee uchochoroni kwa sababu za kiusalama, kweli dereva yule alinielewa na safari iliendelea. Hatimaye tukafika kwangu, tukashuka kwenye Bajaj na kumwambia yeye aondoke zake, tukaanza kupita kwenye uchochoro unaotokezea kwangu.
Tulipokaribia kufika, huku mapigo ya moyo wangu yakizidi kupiga kiasi cha kunifanya nitokwe na kijasho chembamba japokuwa bado ilikuwa ni asubuhi na kulikuwa na kibaridi, nilishtuka zaidi baada ya kuona umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika mbele ya nyumba niliyokuwa naishi.
“Mungu wangu,” nilisema huku nikifikicha macho na kutazama vizuri, kuna muda nilikuwa nahisi kwamba huenda nipo ndotoni lakini haikuwa hivyo, sikuelewa pale kwangu kuna kilichosababisha watu wajae kiasi kile.
Je, nini kitafuatia? Usikose next
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
114,664
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
114,664 2,000

Mkuu huko kote zilishapita ipo episode ya hamsini na kitu usiturudishe nyuma
 
kichaa msafi

kichaa msafi

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Messages
849
Points
1,000
kichaa msafi

kichaa msafi

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2017
849 1,000
oya vipi tena nikajua ni oya oya kumbe step 41 nyuma
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
114,664
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
114,664 2,000
ILIPOISHIA:
Muda mfupi baadaye, wote tulikuwa ‘saresare maua’, akanisukuma kwa nguvu kwenye uwanja wa fundi seremala, nikaangukia mgongo, akaja juu yangu kwa kasi, maandalizi ya mechi ya kirafiki isiyo na jezi wala refa yakaendelea huku akionesha kunikamia kama Simba na Yanga zinavyokamiana zinapokutana uwanjani.

63-SASA ENDELEA...
Kipyenga kilipolia tu, Shamila ndiye aliyekuwa wa kwanza kugusa mpira, akawa anabutua mashuti ya nguvu na kunifanya nihisi kama atanielemea na kunishinda ndani ya muda mfupi tu, jambo ambalo kwangu lingekuwa aibu kubwa.

Nikajipanga na kuanza kwenda naye sawa, akawa akipiga mashuti kwa kubutua, mimi naukontroo mpira na kumpiga chenga za mwili, wakati mwingine nikawa natambaa na chaki kama Christiano Ronaldo, jambo lililofanya kibao kigeuke, badala ya yeye kuwa ananishambulia kwa kasi, ikawa mimi ndiyo namshambulia.

Ilibidi nitumie ujuzi wa hali ya juu kuwahi kummaliza nguvu ili nimalize mchezo kwani Junaitha naye alikuwa akinisubiri na sikujua alikuwa na lengo gani.

Kutokana na jinsi nilivyokuwa namshambulia Shamila kwa akili, haikuchukua muda mrefu, akatangaza kusalimu amri, akanikumbatia kwa nguvu!
“Nakupenda sana Jamal, nataka unioe, nataka niwe mkeo wa ndoa,” alisema Shamila kwa sauti kama mtoto mchanga, nikamnong’oneza sikioni kwamba asiwe na wasiwasi, nitamuoa, nikamuona akitabasamu na kuangukia upande wa pili kama mzigo. Haikuchukua muda, akawa anakoroma kuonesha kwamba tayari alishapitiwa na usingizi mzito, hakujua kama nilikuwa nacheza na akili yake.

Kwangu mimi ilikuwa ni zaidi ya ushindi kwani nilijua sasa hatanisumbua tena. Harakaharaka nikainuka na kuchukua gwanda zangu na kuzitia mwilini, ikabidi nirudi kwanza kwenye chumba changu. Harakaharaka nikaenda kujimwagia maji huku nikitafakari kilichotokea muda mfupi uliopita.

Kiufupi nilikuwa nimebadilika sana, sikuwa Jamal yule ambaye hata mimi mwenyewe najijua. Awali nilikuwa muoga sana wa wanawake, hata Raya, msichana aliyetokea kunipenda kwa moyo wake wote, ilinichukua muda mrefu sana mpaka kuja kukutana naye kimwili lakini sasa, nilikuwa kama jogoo, kila tetea anayepita mbele yangu sikuwa naona hatari kumpitia. Hata sielewi ujasiri huo niliupata wapi.

Wakati nikiwa naendelea kujimwagia maji, ni kama Junaitha alichoka kunisubiri kule chumbani kwake, nikashtukia akiingia chumbani kwangu. Nilimtambua kuwa ni yeye hata kabla sijamuona kutokana na jinsi alivyoniita.
“Mbona huji jamani, mi nakusubiri mpaka nachoka bwana!” alisema huku akikaa kitandani. Nikamwambia kuwa nilikuwa nasikia sana joto kwa hiyo niliamua kujimwagia maji kabisa.

“Sasa si ungekuja kulekule kwangu uoge?” alisema. Kwa kuwa tayari nilishamaliza, nilijifunga taulo na kutoka.
“Utasababisha hawa watoto wajue siri yetu bure! Nataka nikiingia chumbani na wewe uwe umeshafika,” alisema kwa sauti yenye mamlaka, nikacheka huku nikijifuta maji. Alisimama na kusogea mlangoni, akachungulia huku na kule, alipoona hakuna mtu, alitoka na kuusindika mlango.

Harakaharaka nilivaa nguo zangu, nikatoka na kufunga mlango, nikatembea kwa umakini mpaka kwenye mlango wa chumba cha Junaitha, nikausukuma, ulikuwa wazi, nikaingia mpaka ndani.
Wewe ni mwanaume wa kipekee sana Jamal, samahani usione kama nakufosi kuwa na mimi kwa sababu nimekuzidi kila kitu na hapa upo kwangu, hapana! Ni kwa sababu sijawahi kukutana na mwanaume kama wewe maishani mwangu.

Mtu anaweza kukuona mdogo kwa nje lakini una mambo makubwa sana,” alisema Junaitha na kunisogelea, akanikumbatia kwa nguvu, nikalihisi joto la mwili wake kwenye mwili wangu.
Japokuwa nilikuwa nimetoka kwenye mchezo muda mfupi uliopita, kwa jinsi Junaitha alivyokuwa akihamasisha, nilijikuta nikiwa tayari kwa mpambano mwingine, japokuwa hata sheria za mchezo hazikuwa zikiruhusu kilichokuwa kinataka kufanyika.

Haukupita muda mrefu, tuliingia uwanjani tena lakini tofauti na Shamila, Junaitha alikuwa na utaalamu wa hali ya juu. Naye hakuwa na papara kama mimi, maandalizi ya kupasha viungo moto yalienda taratibu, kipyenga kilipopulizwa, kila mmoja akawa anacheza kwa staili ya kumvizia mwenzake, ladha ya mchezo ikawa tofauti kabisa na Shamila.
Mtanange wa kukata na shoka uliendelea, hata sijui nguvu za kuhimili mikikimikiki nilizipata wapi kwa sababu kwa jinsi nilivyomudu kucheza na mpira, hata Junaitha mwenyewe hakugundua kwamba nimetoka kulisakata tena kabumbu muda mfupi tu uliopita.

Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa mpambano huo, Junaitha alikuwa hajitambui, nikajikokota na mpira wangu kwapani kwa sababu kama sheria zinavyosema, mchezaji akipiga hat trick anaondoka na mpira wake, nikavaa gwanda zangu na kurudi chumbani kwangu, nikimuacha Junaitha naye anakoroma.

Nilipofika na kujitupa kitandani, kutokana na jinsi nilivyokuwa nimechoka, sikuelewa tena kilichoendelea mpaka nilipokuja kuzinduka alfajiri ya siku ya pili. Junaitha ndiye aliyekuja kuniamsha, cha ajabu eti akawa ananilaumu kwamba kwa nini sikulala kule kwake, akawa ananiuliza niliondoka muda gani? Nikajua kwamba kwa vyovyote na yeye ndiyo alikuwa amezinduka alfajiri hiyo.

Kwa kuwa siku hiyo tulikuwa na ratiba ngumu sana, tulianza kujiandaa, tukawaamsha watu wengine wote ambapo Shamila alikuwa mgumu sana kuamka kwa madai kwamba bado mwili wake ulikuwa umechoka, ikabidi Junaitha atumie nguvu.
Saa kumi na mbili juu ya alama, wote tayari tulikuwa tumeshajiandaa, tukakaa mezani na kunywa chai iliyoandaliwa na Junaitha kisha baada ya hapo, tukatoka.

Ilibidi tutumie gari la Junaitha ambalo kabla ya hapo, sikuwa najua kama anamiliki gari. Lilikuwa ni Toyota Alphard la kisasa, akasema tukitumia ile Noah ya akina Firyaal itakuwa rahisi kutambulika.
Gari tulilopanda lilikuwa na vioo tinted, jambo lililofanya iwe vigumu kwa mtu wa nje kuona kilichokuwa kinaendelea ndani, Junaitha mwenyewe ndiyo akakaa nyuma ya usukani na mimi nikakaa pembeni yake. Kwa jinsi tulivyokuwa tumejikausha, isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuhisi kwamba kuna mchezo ulikuwa ukiendelea kati yetu.

Hata Shamila mwenyewe, japokuwa mara kwa mara alikuwa akinitazama kwa macho ya kuibia, hakuweza kuhisi chochote, achilia mbali mpenzi wangu Raya ambaye muda wote alikuwa ametulia. Tulitoka na breki ya kwanza ilikuwa ni kwenye kituo kikuu cha polisi, Junaitha akatutaka wote tubaki ndani ya gari, akashuka na kuingia kituoni.

Baada ya kama dakika ishirini, alitoka akiwa ameongozana na askari mmoja aliyekuwa na nyota nyingi mabegani, ambaye alionesha ishara tu, askari zaidi ya sita wenye silaha wakaingia ndani ya difenda, Junaitha akarudi kwenye gari letu na yule askari akaungana na vijana wake.

“Kuna watu itabidi tuwapitie, mwanasheria wetu pamoja na yule mwandishi wa habari, nadhani wote tayari watakuwa wanatusubiri sehemu tuliyokubaliana,” alisema Junaitha. Nikamuuliza swali:

“Kwa hiyo hapa tunaelekea wapi?”
“Tulia jamal, mbona una haraka, nimesema leo ndiyo leo na watu wote watatujua sisi ni akina nani.

Shenaiza na Firyaal, naomba mkaze mioyo yenu maana kinachoenda kutokea kwa baba yenu siyo kizuri lakini lazima tufanye hivi,” alisema Junaitha, akawasha gari, tukaondoka huku ile difenda ikitufuata kwa nyuma.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
K

kifimbodo

Senior Member
Joined
Apr 23, 2015
Messages
154
Points
225
K

kifimbodo

Senior Member
Joined Apr 23, 2015
154 225
Sasa bro c umalizie tu.!! Maana karoho kwangu kameanza kwenda mbiooo kujua nn kinatokea.!
Asante kwa kutukumbuka.!!
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
6,136
Points
2,000
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
6,136 2,000
Nawahi seat nitakuja kusoma baadae
 
maliyamtu

maliyamtu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2017
Messages
1,706
Points
2,000
maliyamtu

maliyamtu

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2017
1,706 2,000
Shunie umetuonjesha alafu umetutelekeza
 
Nguvu moja

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Messages
3,408
Points
2,000
Nguvu moja

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2017
3,408 2,000
Hii vitu unaweza ota usiku
Ukapiga kelele
 
Forum statistics

Threads 1,325,761
Members 509,278
Posts 32,202,083
Top