Simulizi ya kweli: Niliishi kuzimu siku saba

Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
SEVEN DAYS IN HELL (SIKU SABA KUZIMU)- 70
ILIPOISHIA:
Wakati wote wakiendelea kulia, nilisikia mlango ukifunguliwa tena, nikamuona Junaitha akiingia lakini tofauti na wengine, yeye uso wake ulikuwa mkavu kabisa, akatembea harakaharaka mpaka pale nilipokuwa nimelala, akanitazama usoni, na mimi nikamtazama, tukawa tunatazamana huku nikiwa na shauku kubwa ya kutaka kusikia ataniambia nini.
SASA ENDELEA...
“Najua unataka kujua kuhusu Firyaal!” alisema na kabla sijamjibu chochote, akaniambia kwamba kulikuwa na habari mbaya kwa sababu inaonekana maisha yake yanashikiliwa na uzi mwembamba sana unaotenganisha kati ya uhai na kifo. Kwa maelezo yale, nilielewa kwamba anamaanisha kwamba tayari Firyaal alishatoka kwenye ulimwengu wa kawaida, hakuwa na uhai tena.
“Tunaweza kumuokoa kutoka kwenye mdomo wa mauti lakini itatugharimu kukaa siku saba kuzimu,” alisema Junaitha, kauli ambayo ilitufanya wote ndani ya wodi ile tubaki tukimshangaa.
“Inabidi kwanza tuhakikishe wewe umerejewa na nguvu zako kwa sababu unahitajika sana kwenye kazi ya kukata minyororo ya kuzimu ambayo tayari Firyaal ameshafungwa. Nilishusha pumzi ndefu na kutulia pale kitandani.
Akaanza kutupa maelekezo kwamba, nikisharejewa na nguvu zangu, tutaomba ruhusa ya kutoka hospitalini hapo kwa sababu za kiusalama, kisha tutaomba kuondoka na Firyaal kwa ajili ya taratibu nyingine.
“Kuna kitu sijaelewa.”
“Hujaelewa nini?”
“Umesema itatulazimu kukaa siku saba kuzimu?”
“Utaelewa tu,” alijibu Junaitha huku akigeuka na kutoka, akatutaka wote tutulie pale wodini na kama akina Shamila wakitolewa, basi wasiende mbali na mlango wa kuingilia kwenye ile wodi niliyokuwa nimelazwa kwa sababu za kiusalama.
Sikukaa muda mrefu sana, Junaitha alirudi na kunisogelea pale kwenje jeraha langu, akalishika kwa kulikandamiza huku akiongea maneno ambayo hakuna aliyeyaelewa, kisha akato kichupa kilichokuwa na ungaunga fulani, akafungua bandeji upande mmoja na kunyunyizia ule unga kwenye jeraha lango.
Hapohapo nikaanza kuhisi kama moto mkali unawaka kifuani na kadiri ulivyokuwa unaongezeka, maumivu nayo yalikuwa yakipungua na mwili wangu ukaanza kurejewa na nguvu zake.
“Nashughulikia usafiri, kaeni tayari,” alisema kisha akatoka tena, wote wakawa wananitazama kwa makini usoni kuona hali yangu inaendeleaje, kwa mbali nikaanza kutoa tabasamu hafifu lililoamsha matumaini mapya kwenye moyo wa kila mmoja.
Baadaye, Junaitha alirudi tena, safari hii akiwa ameongozana na manesi ambao waliniandaa vizuri, tayari kwa kuondoka. Wakanisaidia kuninyanyua pale kitandani, na kunitoa mpaka kwenye maegesho ya magari, wote tukaingia ndani ya gari na kushtuka kugundua kwamba mwili wa Firyaal pia ulikuwa ndani ya lile gari, akionesha kutokuwa na uhai kabisa.
Akawasha gari na kutusisitiza kwamba hatutakiwi kumgusa Firyaal wala kuzungumza chochote kumhusu mpaka atakapotuambia, akabadili gia na kukanyaga mafuta, gari likawa linaondoka, tukaenda mpaka kwenye geti la kutokea ambapo alizungumza na wale walinzi, wakamfungulia geti.
Tukatoka ambapo alizidi kukanyaga mafuta, gari likawa linakimbia kwa kasi kubwa.
Tuliendelea na safari huku wote tukiwa kimya kabisa ndani ya gari, kila mtu akiwaza lake lakini kubwa tukifikiria hatma ya Firyaal. Safari iliendelea na hatimaye tulifika nyumbani kwa Junaitha, akaingiza gari mpaka ndani ya geti, wote tukashuka huku tukionesha dhahiri kuchoka.
Mimi ndiyo nilionekana kuchoka zaidi kwa sababu bado mwili wangu haukuwa na nguvu kutokana na kupoteza damu nyingi kwenye lile tukio la kupigwa risasi, sambamba na maumivu ambayo yalikuwa yakizidi kupungua kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Shamila na Raya walisaidiana kunishika huku na kule kama ilivyokuwa kule mwanzo, tukaingia ndani na kwenda moja kwa moja kukaa sebuleni. Shenaiza na Junaitha wao walisaidiana kumbeba Firyaal na kumpitisha moja kwa moja mpaka kwenye kile chumba ambacho ndiyo huwa tunafanyia shughuli mbalimbali pale ndani.
Muda mfupi baadaye, Shenaiza alirudi na kujumuika na sisi pale sebuleni, akaenda kuwasha runinga na kwenda kutoa chupa ya maji ya kunywa kwenye friji, akanimiminia kwenye glasi na kuniletea, wote watatu wakakaa pembeni yangu.
Junaitha yeye aliendelea kubaki kwenye kila chumba akiwa na Firyaal, hatukujua anafanya nini kwa sababu yeye ndiye aliyetoa maagizo kwamba sote tubaki sebuleni. Bado ukimya ulikuwa umetawala nyumba nzima, sauti pekee iliyokuwa inasikika ilikuwa ni ya TV tu ambayo hata hivyo hakuna aliyekuwa akiitazama.
Kila mmoja alikuwa akiwaza lake lakini ghafla tulishtushwa na kiashirio cha ‘breaking news’ kwenye runinga, wote tukainua vichwa vyetu na kuanza kuitazama runinga hiyo kubwa na ya kisasa, iliyokuwa imebandikwa ukutani.
“Mungu wangu,” nilisema baada ya kushuhudia picha zetu tukiwa pale hospitalini zikioneshwa, zikifuatiwa na maelezo kwamba sisi ndiyo tulikuwa mashujaa wa lile sakata ambalo sasa lilikuwa limebatizwa jina jipya la Kurasini Scandal, likiwa na maana ya skendo ya Kurasini.
Mtangazaji aliwaambia watazamani kwamba hatimaye walikuwa wamefanikiwa kupata picha za watu ambao ndiyo waliokuwa mstari wa mbele katika kufichua uovu mikubwa uliokuwa ukifanywa na mfanyabiashara mkubwa mwenye asili ya Uturuki, Loris kwa kivuli cha Shirika la Black Heart.
Alitumwagia sifa kedekede kisha baada ya hapo, alisema kwamba mheshimiwa rais alikuwa na maneno ya kuzungumza na wananchi wake ana kwa ana muda huo, ukapigwa wimbo wa taifa kisha mheshimiwa rais akaonekana, akiwa amesimama kwenye viunga vya hospitali alianza kuzungumza na wananchi moja kwa moja kupitia runinga.
Alianza kwa kueleza kuhusu mtikisiko mkubwa uliolikumba taifa baada ya kugundulika kwa kile mwenyewe alichokiita machinjio ya binadamu eneo la Kurasini, akafafanua kwamba mtu aitwaye Loris, ambaye serikali ilimuamini na kumpa kibali cha kuendesha Shirika la Black Heart, ambalo alilisajili kama shirika la kusaidia jamii, alivyogundulika kwamba anafanya biashara nyingine haramu na hatari mno kwa maisha ya wananchi.
Alieleza kila kitu, akasema wamegundua kwamba kumbe Black Heart, kazi yake ilikuwa ni kuwasafirisha watu kwenda nje ya nchi ambako wengi wao walikuwa wakienda kuuawa kisha kutolewa viungo muhimu kwenye miili yao, huku wengine wakiuawa hapahapa nchini na viungo vyao kwenda kuuzwa nje ya nchi.
Alionesha kusikitishwa mno na kugundulika kwa sakata hilo ikiwa ni muda mrefu umepita tangu kuundwa kwa shirika hilo, jambo ambalo lilimaanisha kwamba wananchi wengi tayari walishatolewa sadaka kwa sababu ya dhiki zao.
“Najua ni watu wengi ambao walienda kuonana na Loris kwa lengo la kuomba misaada, iwe ni kwenda kusomeshwa nje ya nchi, kufadhiliwa matibabu nje ya nchi au kutafutiwa kazi lakini wakaishia kutolewa kafara,” alisema mheshimiwa rais na alipofika eneo hilo, alishindwa kuzuia machozi yasimtoke, akavua miwani yake na kutoa kitambaa, akajifuta machozi na kuendelea kuzungumza.
Mwisho alitutaja majina, akianza na Junaitha, akaja mimi, Raya na Shamila huku akiwataja Shenaiza na Firyaal kwa utambulisho wa juujuu, nadhani alifanya hivyo kwa sababu za kiusalama, akasema anahitaji kuonana na sisi ikulu na kutoa maagizo tutafutwe mahali popote tulipo ili akatupongeze kwa kazi nzuri tuliyoifanya.
Alieleza kwa kirefu jinsi tulivyofanikisha suala hilo na vikwazo ambavyo tulikumbana navyo, akasema kwamba anajua tulipingwa sana lakini kwa sababu ya ushujaa wetu, tumefanikisha kufichuka kwa sakata hilo kubwa. Akatupa pole kwa yote na kutupongeza sana.
Alipofikia hapo, picha zetu zilirushwa tena runingani tukiwa tunatoka hospitalini kisha wimbo wa taifa ukapigwa tena na huo ukawa mwisho wa habari hiyo. Kwa muda wote huo tulikuwa kimya kabisa, tukiwa ni kama hatuamini tulichokuwa tunakiona.
Kwangu mimi kila kitu kilikuwa zaidi ya muujiza, yaani sisi ndiyo tulikuwa tukitangazwa na mheshimiwa rais mwenyewe kwamba ni mashujaa wa nchi? Hakika ilikuwa ni zaidi ya muujiza. Nilijikita nikishindwa kuyazuia machozi ya furaha yasiulowanishe uso wangu, hali ilikuwa hivyohivyo kwa wenzangu wote, hakuna ambaye hakutoa machozi ya furaha.
“Tunastahili, uwezo wetu wa kutumia nguvu za ndani ndiyo uliotufikisha hapa,” alisema Junaitha, wote tukageuka na kumtazama, hatukuwa na habari kwamba kumbe na yeye alikuwa akiitazama taarifa hiyo ya habari, akaja pale tulipokuwa tumekaa, tukakumbatiana huku wakiwa makini wasinitoneshe kidonda changu.
“Nimeshamaliza kumuandaa Firyaal twendeni tukamalizie kazi iliyosalia,” alisema Junaitha, tukainuka na kuanza kutembea taratibu kuelekea chumbani, kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana ndani ya moyo wake.
“Niliwaambia lakini, bila shaka sasa mnaamini,” alisema Junaitha, wote tukamuunga mkono kwa sababu ni kweli alituambia kwamba tukifanikisha suala lile, nchi nzima itatujua sisi ni akina nani na kutupa heshima tuliyokuwa tukistahili.
Tulienda mpaka chumbani ambako Firyaal alikuwa amelazwa chini huku mishumaa saba ikiwa imewashwa na kuzungushiwa pande zote, kuanzia kichwani mpaka miguuni. Alikuwa amemfunga kwa sanda nyeupe ambayo hata sikujua ameipata wapi lakini eneo la usoni lilikuwa wazi.
“Mpendwa wetu Firyaal amelala usingizi wa kifo, kuna uwezekano wa asilimia 50 kwa 50 wa kumrudisha duniani lakini hata ikitokea tumeshindwa, bado kwetu hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa kwa sababu kwa kipindi kifupi alichoishi duniani, Firyaal alikuwa ameishi kikamilifu.
Alituelekeza nini cha kufanya, wote tukakaa chini kwa mtindo wa tahajudi, mimi nilikaa upande wa kichwa cha Firyaal, Junaitha yeye alikaa upande wa kushoto wa kifua chake, jirani kabisa na moyo wake, Shamila alikaa upande wa miguuni kwa namna ambayo mimi na yeye tulikuwa tukitazamana, Raya na Shenaiza wao wakakaa upande wake wa kulia.
“Inatakiwa wote tuanze kwa kufanya tahajudi ya pumzi huku tukiunganisha nguvu, kila mmoja akitulia kwa kadiri ya uwezo wake na kuweka uzingativu, tunaweza kuiamsha upya pumzi ya Firyaal, akaanza upya kupumua na kurejea duniani,” alisema, akaanza kutuelekeza nini cha kufanya lakini mwisho alitoa angalizo:
“Kazi haitakuwa nyepesi kwa sababu tayari pumzi zake zimeshahama upande na kuelekea upande wa pili ambao ni kuzimu, kwa hiyo suala la kuzirudisha lilikuwa ni lazima lihusishe safari ya kuelekea kuzimu, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu.
Je, nini kitafuatia?
History nzurii sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom