Simulizi ya kusisimua- (penzi la mfungwa)

PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi:Sharobaro la Jf
CONTACT:0765168293

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU-23

"Haya manyanyaso siwezi kuyavumilia,mimi ni mwanaume na yeye pia ni mwanaume. Sasa kwanini niogope? Iweje niitwe mzuri na mwanaume mwenzangu,ama kwanini ajione yeye ni mwamba humu ndani eti kisa amepewa cheo cha kutuongoza? Hapana. Mimi ni Zabroni, hivyo kile nilicho kisimulia itabidi nikiweke hadharani ili heshima itawale",alisema Zabroni ndani ya nafsi yake,muda huo akiwa amelala na wafungwa wenzake. Baada kusema hayo alijishika kwenye msuri wa mkono akakumbuka hana hirizi ambayo ingempa walau nguvu. Hapo sasa ndipo kumbukumbu ilipomjia zaidi,akakumbuka namna gani Veronica alivyomteka kimapenzi mpaka kupelekea kupoteza dawa yake ambayo ingemfanya asikamatike kirahisi. Zabroni hakuishia hapo,alikumbuka pia kifo cha Bukulu ambaye alikuwa ni rafiki yake kipenzi. Neno la mwisho ambalo Bukulu alimwambia Zabroni kabla hajakata roho ni kwamba Bruno ndio aliyemfanyia hicho kitendo,kwa maana hiyo Zabroni alijua fika kuwa Bruno karudi uraiani kwani alidhani kwamba baada kumsababishia msala basi atakuwa anehukumiwa jela kitu ambacho kilienda kinyume na jinsi alivyodhania. Bruno yupo,na ndio huyo aliyeamua kujibadisha jina na kujiita Mr Rasi.
Pumzi alishusha Zabroni mara baada kutoka kwenye dimbwi la mawazo,kisha akaanza safari ya kulitafuta lebe la usingizi ambalo kiukweli lilimuwea ngumu kumjia ingawa mwishowe alifanikiwa japo alichelewa sana.
Kesho yake aljajiri kama ilivyo ada,kengere ya kuwamsha wafungwa iligongwa. Wafungwa wote walikurupuka haraka sana kukimbilia mstarini kasoro Zabroni ambaye yeye alikuwa bado amelala kwa sababu usiku wa jana alichelewa kulala kwahiyo alikuwa akimalizia usingizi aliokuwa nao,asijue tayari kumekucha. Wafungwa walihebu namba,na hapo ndipo namba ya Zabroni ilipo kosekana. Amri ikatoka kwa mkuu wa gereza,amri ambayo ilimtaka nyampala Bluyner akakague kila chumba wanacholala wafungwa. Bluyner kwa madaha huku akitunisha mbavu zake,alizipiga hatua kwenda kukagua chumba kimoja baada ya kingine ili kujihakikishia kama kuna mfungwa kasilia ama katoroka. Hatimaye akiwa nje alimuona mfungwa mmoja akiwa amelala,aliingia ndani akamkuta ni Zabroni.
Alichuchumaa kisha akamtingisha kitendo ambacho kilimkurupusha Zabro kutoka usingizi akakutana na uso wa adui yake ambaye ni Bluyner. Bluyner akacheka kidogo kisha akasema "Naona unalala tu kama upo kwa mama yako" alisema Bluyner, maneno ambayo yalimfanya Zabroni kumkumbuka marehemu mama yake. Alijitahidi kufanya juu chini ili akamtibie mama yake ugonjwa aliokuwa akiumwa ugonjwa wa kupooza,lakini bahati mbaya juhudi hizo zikawa zimeota mbawa baada mama yake kufia ndani kwa kuteketezwa nyumba yao. Hivyo nikama Bluyner aliweza kumkumbusha Zabroni machungu aliyokuwa ameanza kuyasahau kichwani mwake,hasira za ghafla zilimjia ambapo alikunja ngumi nzito kisha akamtupia Bluyner. Bluyner aliiona,akaikwepa kisha akasimama ili amuadabishe vizuri. Zabroni naye akawa si haba, alisimama kidete ili akabiliane naye.
Wakati hayo yanaendelea kati ya Zabroni na Bluyner,upande wa pili alionekana Tina akiwa sebuleni na shangazi yake wakipiga zogo. Tina alisema "Yani Ant nikwambie kitu?.."
"Niambie wala usijali "
"Kweli nimeamini siku zote usimdhanie mtu kutoka na matendo yake"
"Ni kweli ulicho kisema Tina,haya nieleze unamaana gani kusema hivyo?.."
"Maana yangu ni kwamba. Kuna siku fulani nilikuwa kwenye kituo cha daladala nasubiri gari ili nirudi nyumbani,sasa bwana akatokea kibaka akanipokonya mkoba wangu akakimbia nao. Nilipiga kelele kuomba msaada lakini hakuna mtu hata mmoja aliyenisaidia ila mkaka mmoja hivi ambaye yani kimuonekano alionekana yupo yupo tu..alimkimbiza yule kibaka akamkamta akanirudishia mkoba wangu. Kiukweli nlishukuru sana sijui hata nisemeje dah"
"Daah hapo sasa nimekuelewa "
"Ndio hivyo we unadhani yule kibaka angekimbia na hela zote zile ingekuaje?.."
"Mmh ndio siku ile nilipokutuma ukanitolee pesa Bank?.."
"Ndio siku hiyo hiyo"
"Laah! Mungu wangu, enhe huyo mtu aliyekusaidia ulimpa hata ya maji?."
"Hapana sijampa lakini usijali ant. Siku zote milima haikutani ila binadam hukutana. Nina uhakika ipo siku nitakutana naye nitampa japo kidogo ili akafanyie mambo yake.."
"Huo ndio uugwana mwanangu sawa?.."
"Sawa ant"
"Ulimuuliza jina lake?.."
"Ndio kaniambia anaitwa Mr Rasi"
"Anhaa sawa hapo nadhani itakuwa rahisi sana kumfahamu pindi mtako kutana. Haya chai tayari sijui utakunywa ama utawangojea Wenzako"
"Ngoja niwasubiri tu,kwani wameenda wapi? "
"Angel kaenda kwa rafiki yake mara moja, Gift naye sijui kaenda wapi. Maana anatembea sana siku hizi"
"Doh basi ngoja ninywe, sijui watarudi muda gani"
Baada ya maongezi hayo,shangazi yake Tina alifurahi sana kumuona Tina akiwa katika hali ya furaha. Kwani Tina alipofikishiwa taarifa ya kuhusu kifo cha wazazi wake alijikuta muda wote akiwa mnyonge hana furaha,kiasi kwamba hatakama umchekeshe namna gani abadani hacheki zaidi ya kuachia tabasamu kidogo na kisha kurudi katika hali yake ya ukiwa. Lakini siku hiyo Tina alionekana kuwa katika hali tofauti kabisa kitu ambacho kilimfanya shangazi yake kufurahi akiamini kwamba tayari binti huyo anaanza kusahau yaliyopita.
Kwingineko ule ugomvi wa Zabroni na Bluyner uliingiliwa kati na askari ambao waliwaamulia,haikuwa kazi nyepesi ila walifanikiwa. Bluyner alionekana kumkunjia uso Zabroni ilihari Zabro naye akionekana kumkunjia uso Bluyner ingawa tayari muda huo Zabrini alikuwa akivuja damu puani na mdomoni,alizidiwa nguvu na ujanja katika hilo pambano. Na endapo kama askari wasinge ingiliaa kati basi Zabroni angekiona cha mtema kuni.
Siku hiyo Zabroni hata uji hakunywa,moyo wake ulikuwa umefura hasira. Mawazo mfurulizo yalilindima kichwani mwake huku damu kama maji ikimtoka puani,hivyo punde si punde alizidiwa akaanguka chini akapoteza fahamu. Alizinduka akiwa Hospital akiwa ametundikiwa dripu ya damu na maji,mkononi akiwa amevishwa pingu huku kando kando yake amesimamiwa na askari mkononi akiwa na bunduki. Askari huyo alikuwa mzee wa makamo. Zabroni akastuka kujikuta katika mazingira hayo kwa sauti ya chini akamuuliza Askari huyo aliyepewa jukumu la kumlinda"Nimefikaje mahali hapa?.."
Askari huyo aiimtazama Zabroni,hakika alitia huruma. Akajibu "Baada ya ule ugomvi ulitokwa damu nyingi iliyokupelea kupoteza fahamu ndio maana upo mahali hapa unapatiwa huduma",Mara baada kujibiwa hivyo alinyamanza kidogo kisha akarudia kusema "Sawa asante kwa jibu lako lakini naomba kufahamu kwanini huyu mtu anafanya matendo kama haya halafu mnachukulia kawaida? Je, ikowapi haki ya mfungwa kama kunamanyanyaso kama haya",Hapo huyo Askari hakumjibu Zabroni bali alikumbuka siku kadhaa zilizopita jinsi Bluyner alivyomtishia kumpiga. Ukweli Bluyner alionekana kuwa tishio kwa wafungwa wenzake hata na Askari baadhi pia.
"Loh huyu binadam sijui anaroho gani, kiukweli hata mimi tabia yake nimeichoka. Nafikiri siku nikihamishwa hapa nitafurahi sana ",alijibiwa Zabroni na askari baada kukumbuka jinsi alivyonusurika kupigwa na Bluyner.
"Upo tayari kuona mtu huyu anaibishwa?..",alihoji Zabroni.
"Unamaana gani?.
"Maana yangu ni kwamba huyu mtu nimuadabishe"
"Acha utani,umenusirika kifo halafu leo hii umuadabishe?..", alijibu Askari huyo huku akimtazama kwa jicho la huba mtukutu Zabroni. Zabroni akakaa kimya kidogo kisha akasema.
"Ndio kila kitu kinawezakana ila kama utanisaidia jambo moja"
"Jambo gani?..", aliuliza Askari huku akimkodolea macho Zabroni. Zabroni akajibu "Wakati rasmi nakabidhiwa jezi za gerezani nilivuliwa hirizi yangu,ambayo ndio kila kitu kwangu kujihami na maadau. Sidhani kama itakuwa imetupwa,naimani itakuwa imehifadhiwa tu"
"Enhe kwahiyo? .."
"Naomba ufanye juu chini ukanichukulie kisha unikabidhi tafadhali sana",alijibu Zabroni safari hiyo akiongea huku machozi yakimtoka. Askari huyo aliyemsimama kiukweli alimuonea huruma. Akamwambia "Je, unauhakika utaweza? Nipotayari kukuletea hicho kitu chako"
"Nitaweza asilimia mia moja"
"Sawa ",alijibu Askari huyo aliyepewa jukumu la kumrinda mfungwa Zabroni wakati huo anafanyiwa matibabu.
Baada ya siku nne Zabloni tayari alionekana kuwa sawa kiafya kimwili na akili pia,siku hiyo anarudi jela ilikuwa shagwe na vifijo kutoka kwa wafungwa wenzake. Pole kwa wingi zilimfikia Zabroni kwa yaliyomkumba huku wengine wakimsifu kwa kuamua kujitosa kupigana na nyampala Bluyner kijana ambaye ni tishio kwa kila mfungwa. Kitendo alichokifanya Zabroni kilikuwa cha kishujaa sababu tangu jamaa huyo ahukumiwe jela hakuna mfungwa hata mmoja aliyejaribu kukabiliana naye lakini Zabro alithubutu japo alichezea kichapo. "Zabro...Zabro..Zablo..Zabrooooni",Ni shangwe zilizokuwa zikitoka kwa wafungwa ambao walionyesha kufurahishwa na ujio wa Zabroni. Zabroni alibaki kusimama huku akiachia tabasamu pana,alipogusa upande bega lake alipofunga hirizi yake mkono wa kulia akagundua hirizi ipo. Haraka sana akatazama upande wa kushoto umbao walionekana Askari magereza wanne akiwemo na yule aliyemsaidia kumpatia hirizi,Askari huyo akamnyooshea Zabroni dole gumba akimanisha ishara kuwa mambo ni safi. Naye Zabroni akajibu kwa kuitikia kwa kichwa kisha akajiunga na wafungwa wenzake,wakati huo moyoni akijisemea "Veronica Veronica Zabroni nakuja kuifanyia upasuaji sehemu hiyo iliyopoteza nguvu zangu sababu hicho ndio chanzo cha haya yote "

----USIKOSE SEHEMU IJAYO----
 
PENZI LA MFUNGWA
Mtunzi :Sharobaro la Jf
CONTACT : 0765168293

SEHEMU YA SIBA-07

Lakini kabla kijana Zabroni hajawafikia wazee hao,machale yalimcheza. Bila kuchelewa alijibadilisha akawa katika sura yake ya kawaida kisha akapotea maeneo hayo ambapo mzee Ngurumo na mwenyekiti walipo fika eneo lile alilopotelea Zabroni kamwe hawakuweza kumuona,zaidi walijikuta wakihisi joto ambalo nalo hawakuweza kulitilia maanani kwani walikuwa na haraka za kwenda kutazama nyumba ya nani inaungua. Mwenyekiti alipo kuta nyumba yake ipo salama alifurahi sana lakini pia hakusita kutoa pole kwa jirani yake aliyechomewa nyumba,wakati huo huo mzee Baluguza naye alionekana kuinamisha uso wake chini akitafakari jambo fulani. Lakini punde si punde mzee huyo alitoka kwenye dimbwi la tafakari baada kuguswa bega na mwenyekiti,Baluguza aligeuka akakutana na uso wa Mwenyekiti. "Kulikoni mwenzetu naona umetukimbia kimaajabu" Alisema Mwenyekiti akimwambia mzee Baluguza, kwa sauti ya unyonge huku akiutazama ule moto unaolanda kwenye nyumba alisema "Hii ni kawaida yangu mzee mwenzangu,naona hakuna muda wa kupoteza. Kesho naomba uitishe mkutano wa kijiji ili nimuumbue mbaya wenu " alisema mzee Baluguza.
Kesho yake palipo pambazuka mbiyu ya kijiji ililia, taarifa zikagonga masikioni mwa wanakijiji kwamba kutakuwa na mkutano wa wakijiji siku hiyo. Hivyo haitakiwa mwanakijiji yeyote akose kuhudhulia. Mbiyu hiyo aliisikia na kijana Zabroni ,akiwa kitandani kwake. Akajiuliza "Wanamikakati gani mbweha hawa?..ni lazima na mimi nihudhulie ili nijue wanamikakati gani ",alisema Zabroni huku akisimama kutoka kwenye kitanda chake,alichukuwa bukta yake iliyokuwa imekatwa miguu kwa kuzidiana kisha akaelekea mahili yalipo makaburi ya wazazi wake. Hapo Zabroni alienda kwa niaba ya kuyasafisha kabla muda wa mkutano haujawadia, na pindi kijana huyo akifanya hicho kitendo upande wa pili kijiji kilionekana kuzizima majonzi. Wanakijiji walikuwa wakisikitika kuwapoteza wanakijiji wenzao waliokufa usiku wa jana kwa ajari ya moto,hali hiyo ikawafanya kuwa na shauku kila mmoja kufika mkutano ni. Hali hiyo ilimpelekea mazishi kufanyika mapema sana ili watu wawahi,haikuwepo haja tena ya kukaa msibani mpaka jioni kwani hali iliyokuwepo sasa ilitisha kila familia haikuwa na amani nyumbani kwake,wazee kwa vijana wote walianza kuogopa. Hivyo siku hiyo waliposikia mbiyu wakaamini kuwa huwenda mbiyu hiyo ikawa na jambo la heri katika kijiji chao.
Na hatimae Muda uliwadia sasa,watu walianza kukusanyika mkutanoni. Kwa muda wa nusu saa wanakijiji wote walikuwa wamefika ingawa si wote kwani kuna baadhi walikuwa bado wanajiandaa kuanza safari,ilihari wengine tayari walikuwa wameanza. Vile vile Upande mwingine Zabron naye alianza safari ya kujongea kwenye mkutano huo,nia na madhumuni kutaka kusikiliza mikakati gani inayo endelea kijiji hapo. Na wakati Zabroni alipokuwa akitembea njiani,Ghafla mbele yake akaona kamba. Alipoiona kamba hiyo akajipapasa kwenye mfuko wa bukta yake akakuta kibiriti. Aliachia tabasamu baada kujihakikishia kwamba kibiriti anacho upesi akaichukuwa kamba hiyo akaenda nayo mpaka kwenye nyumba moja ambayo ya mzee Ngurumo. Alipo fika hapo alitazana kulia na kushoto kuangalia usalama wake akagundua hakuna mtu yoyote mahali hapo. Pasipo kupoteza muda aliifunga kamba kwenye fito ya nyumba kisha akailaza hatua mbili za mtu mzima kutoka mahali ilipo nyumba. Kwa mara nyingine tena akarudia kutazama kila pande, alitazama kulia na kushoto pia nyuma yake hakuona mtu,haraka sana akachukuwa nyasi kavu akizisambaza kidogo juu ya kamba ile kisha akafyatua njiti, nayo ikaripua moto akaishusha kwenye zile nyasi nazo zikanasa moto ambao pole pole ulitembea kwenye ile kamba ya kitambaa. Kamba ambayo pia ilikuwa pana na ndefu kwa kiasi chake. "Mchezo umekwisha", alijisemea ndani ya nafsi kisha akaondoka kuelekea kwenye mkutano wakati huo huo huo mzee Baluguza alionekana kutoka ndani ya nyumba ya Mwenyekiti huku mkononi akiwa na jungu ambalo lilikuwa na makorokoro mengi ndani yake, wanakijiji walitulia kimya mpaka mzee huyo anafika kwenye umati wa wanakijiji. Alipo fika alisimama akitaka kusema jambo,lakini kabla hajasema akamuona Zabroni naye akijisogeza kwenye mkutano. Mzee Baluguza alimkazia macho ila mwishowe akajifanya kupotezea ili mtukutu Zabroni asijishuku. Zabroni alifika mkutanoni akaungana na wenzake alitulia chini akisubiri kujua kipi kinacho taraji kutokea. Muda huo huo Baluguza akamnong'oneza Mwenyekiti, akamwambia "Nenda kanichukulie nyayo za yule kijana"
"Kijana yupi? .."alihoji Mwenyekiti huku akiwa makini kumsikiliza mtalamu Baluguza.
"Kijana yule tuliyepisha naye juzi jioni wakati ulipokuja kunipokea", mwemyekiti alivuta kumbukumbu kwa muda wa sekunde kadhaa mwishowe akakumbuka kuwa mtu mwenyewe ni Zabroni mtoto wa mzee Ndalo. "Sawa nitazijuaje hizo nyayo?..", kwa mara nyingine tena aliuliza Mwenyekiti. Mzee Baluguza alikaa kimya kidogo huku akichukuwa kipande cha kitambaa ambacho kilionekana cheusi kisha akamkabidhi Mwenyekiti halafu akamwambia "Kavaa saganyoka,hivyo ni rahisi sana kuzigundua. Nenda haraka chukua mchanga kudogo hapo alipo kanyaga kisha niletee hapa nimalize kazi", alijibu mzee Baluguza. Mwenyekiti akiwa na wasiwasi kwa kijana Zabroni alifanya kama alivyo ambiwa kisha haraka sana akarudi wakati huo mzee Fungafunga akiwa kama mmoja ya baraza la wazee kwenye mkutano huo yeye alikuwa akiwaongelesha huku mzee Baluguza akifanya yake. Mara baada kumaliza ndipo huyo mzee alipo simama na kisha kusema "Habari zenu wanakijiji, jina langu naitwa Baluguza nadhani wapo wanaonifahamu na wasio nifahamu. Nimekuja hapa kutokomeza hili janga linalo endelea hapa katika kijiji chenu. Haya mauwaji yakinyama, yanatisha lakini leo ndio siku kuu ambayo mtu huyu mshenzi na mjinga atagundurika. ", aliongea kwa kujiamini kabisa Baluguza punde akaendelea kusema." Rafiki yako ndio huyo huyo adui yako, kwa maana hiyo basi kikulacho kinguoni mwako. Mtu anayefanya vitendo hivi wala hatoki nje ya kijiji hiki ila mpo naye humu humu" alisema Baluguza, akameza mate halafu akaendelea kusema. "Kwa maana hiyo basi leo lazima agundulike huyu mtu anaye uwa watu wasiokuwa na hatia, na akishagundulika ndipo kijiji kitaamua mtu huyu afanywe kitu gani. Je, mpo tayari?.." Sauti za wanakijiji zilipasa zikisema "Tupo tayariiiiii!" Lakini wakati wanakijiji hao wanapasa sauti zao kutaka kumfahamu kirusi wa kijiji mara ghafla ule moto uliokuwa ukitambaa kwenye kamba hatimae ilifika kwenye nyumba,nyumba ya mzee Ngurumo ikaanza kuteketea ikiwa mchomaji yupo hapo hapo kwenye mkutano wakati huo mzee Baluguza akitaraji kumuumbua mchomaji huyo mbele ya wanakijiji.

ITAKUAJE HAPO tukutane sehemu ijayo!

Sent using Jamii Forums mobile app
Htr
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom