Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 38,858
- 90,344
- Thread starter
- #121
Tayari vipande vitaanza kudondoka
Chuma kinaendelea Leo.
Nitashusha vipande kama vyote
usitutenge tena Robert Heriel Mtibeli huu utunzi ni mahiri sana [emoji1474][emoji1474][emoji1474] .Chuma kinaendelea Leo.
Nitashusha vipande kama vyote
Chuma kinaendelea Leo.
Nitashusha vipande kama vyote
Unazingua broChuma kinaendelea Leo.
Nitashusha vipande kama vyote
Unazingua bro
Mkuu Kimyaaaaaa
Hata sjui,kuleteana alosto tu..Mwisho wa kusoma hadithi za huyu jamaa🙌Hivi hii story iliishiaga wap?
Kaz nzur mkuuKABURI LA MWANAMUZIKI EP 13
Mtunzi: Robert Heriel
0693322300
ILIPOISHIA
Dora kuwa sehemu ya wale niliopewa kazi ya kuwafuatilia katika Mpango wa Operation Tonardo, uwepo wa jina la Osman Midevu kwenye simu ya Muarabu Ashraf Amur uliniongezea imani ya kuwa Dora ni miongoni mwa wahusika hatari wanaohitajika kukamatwa na kupewa adhabu kali.
ENDELEA
Nikarudi chumbani kwangu, nikafungua ile programu ya udukuzi iliyokuwa kwenye Laptop yangu, nikapekua mpaka nilipoipata namba ya Dora, Nikaidukua kujua yupo maeneo gani, mtandao ulikuwa unasumbua lakini hatimaye mfumo ukaleta ramani ambayo ilikuwa na kitufe chekundu kilichokua kinamwakuamwakua kwa kung’aa na kupunguza mng’ao wake, nikakuza ile ramani ili eneo lile niweze kujua lipo mtaa gani, ramani ile ilikuwa mfano wa Google map, nikashtuka kuona mfumo unaniambia simu ya Dora ipo Mbezi Beach, karibu na Little Star Medium School, “ Hii si ni nyumba ya Osman Midevu?” Nikajikuta nikiropoka kwa sauti huku nikitazama kioo cha Laptop kwa umakini na jinsi kile kitufe chekundu kwenye laptop kinavyomwakuamwakua. Sasa nilijihakikishia kuwa Dora na Osman midevu ni washirika, sikutaka kupoteza muda nikaenda kwenye kabati langu, nikachukua bastola mbili, moja nikaiweka kwenye kiuno, nyingine nikaiweka kwenye viatu. Kisha nikachukua Kamera nne ndogo sana, nikazitia kwenye mifuko ya koti nililokuwa nimelivaa, nikachukua simu maalumu ambayo niliiunganisha na mfumo wa ile laptop, baada ya kuchukua yale yote niliyoona yananifaa, nikaingia ndani ya gari langu, nikaondoka.
Nikiwa njiani nikakumbuka kuwa nina wiki mbili sijaongea wala kuonana na Neema, nikachukua simu kisha nikampigia Neema, simu haikuita sana ikapokelewa na neema akazungumza;
“ Shikamoo Kaka”
“ Marhaba Ney mwanamuziki, hujambo” Nikasema,
“ Hahah! Niko pouwa kabisa! Umeona mdogo wako kimya..”
“Nakuambia we acha tuu! Nikasema huyu Gibson kamteka Mdogo wangu, sijui kampa nini?” Nikasema, hapo pakatokea ukimya kidogo jambo ambalo likanifanya nishangae, nikawa naita;
“ Neema! Neema! Heello! Nee..” Nikasikita sauti kwa mbali kama yamajibishano baina ya Neema na mwanaume mwingine hivi, lakini sikuweza kusikia vizuri, kisha simu ikakatika. “Heeh! Ajabu hii” Nikasema huku nikiwa natazama kioo cha simu, bado naendesha gari nikitokea nyumbani Goba kuelekea Mbezi Beach. Nilikuwa naendesha gari kwa mwendo mdogo, nikaipigia tena namba ya Neema. “ Namba unayoipigia kwa sasa haipatikani tafadhali jaribu tena Baadaye” taarifa hiyo ilikaribisha hofu moyoni mwangu, “Neema yupo wapi? Haikuwa sauti ya Gibson. Naifahamu sauti yake, Neema atakuwa yupo na nani? Kwa nini simu ikatike, alafu aizime. Tangu namchukua Neema Kumlea, haijawahi kutokea jambo kama hili” Nikawa nawaza tayari nikiwa nimefika Mbezi shule. Akili yangu iliniambia kuwa kuna jambo haliko sawa, “Neema na Gibson wamegombana?” Nikawaza, lakini sikutaka kuingilia mambo ya mahusiano ya Mdogo wangu Neema.
Baada ya kufika Bagamoyo Road nikakatisha upande wa Kulia, ulipo muelekeo wa Mjini, hapo nikatembea kwa dakika moja nikaikuta ile njia iendayo Little Star Medium School ambayo ipo mkono wa kushoto, nikakatisha kuifuata. Ilikuwa majira ya saa mojamoja za asubuhi, pilikapilika za watu ndio zilikuwa zinachanganya watu wakikimbia kwenda makazini. Nikaegesha gari langu Mita arobaini kabla ya kuifikia nyumba ya Osman Midevu ambapo Geti la nyumba yake nilikuwa naliona kwa mbele. Nikiwa ndani ya gari, nikaitoa ile simu maalumu niliyoiunganisha na mfumo wa Laptop kule nyumbani, nikaona kwenye ile simu bado kitufe chekundu kilikuwa kinamwekua kwenye nyumba ya Osman Midevu, jambo hili likanipa moyo. Nilikuwa makini kuangalia wapitanjia waliokuwa wanatumia ile barabara ambao wengi walikuwa Wasaidizi wa kazi za ndani wakiwa wanawasindikiza watoto wadogo wenye sare kwenda shuleni, mara chache yalipita magari ya watu binafsi ambao bila shaka walikuwa wakienda katika shughuli zao. Lisaa limoja liliisha, utulivu ukaongezeka eneo lile, hapakuwa tena na watoto waliokuwa wakienda au kupelekwa shule, utulivu ule ulinivutia kufanya jambo, nikataka nishuke ili niende katika ile nyumba ya Osman, nikaiseti Saa yangu ya mkononi, kisha nikaiunganisha na kifaa maalumu kilichokuwa ndani ya gari. Kabla sijashuka, nikashtuka kuona geti la nyumba ya Osman likifunguliwa. Nikaitoa upesiupesi bastola yangu mafichoni na kuiweka juu ya mapaja, nikamuona kijana mmoja hivi mrefu wa kati mwenye, maji ya kunde aliyevaa kapero akitoka mule ndani, akasimama mbele ya lile geti akatazama upande wa ile shule ya Little Star, kisha akageuka upande nilipokuwa nimeegesha gari, hapo nikajirudisha chini polepole kwa kuteleza na mgongo, nikamuona akilitazama gari langu kana kwamba anashangaa uwepo wake eneo lile. Kitambo kidogo akalipuuzia, akageuka na kutembea upande wa ile shule, nikamuona akiingia kwenye kiduka Fulani kilichokuwa eneo la ile shule, “Hii ni nafasi” Nikawaza huku nikichukua upesiupesi Kofia iliyokuwa Viti vya nyuma vya gari, nikavaa alafu nikachukua Gloves nyeusi za mikononi nikazivaa, Kisha nikashuka upesiupesi, bastola yangu nikiwa nimeificha kiuoni, shati nikiwa nimelichomoa likiwa linaning’inia. Macho yangu yalikuwa makini kumtazama yule kijana aliyekuwa anahudumiwa kule dukani, kwa bahati Yule Kijana hakuwa amefunga Geti dogo alipotoka, nikalikagua lile Geti upesiupesi, nikaona Kamera, lakini sikuijali sana, Kofia niliyokuwa nimeivaa ilizuia kwa kiasi kikubwa uso wangu. Nikachungulia ndani, hapakuwa na mtu isipokuwa uwanja mkubwa wenye vigae, upande wa kulia kulikuwa na kijumba cha mlinzi ambacho nacho hakikuwa na mtu ila mlango wake ulikuwa wazi, nje pakiwa na kiti pamoja na Radio iliyokuwa inaongea. Nikajua yule kijana ndiye alikuwa pale.
Mbele kabisa kwenye ule uwanja wenye Vigae yalikuwepo magari mawili, Moja lilikuwa na rangi jeusi, Benzi. Jingine lilikuwa Ni landCrusser V8 yenye rangi kama udongo hivi. Bado nilikuwa nimesimama katikati ya lile Geti nikiwa nusu ndani nusu nje. Lilikuwa jumba kubwa sana la kifahari, lenye ghorofa mbili, ubavu wa kulia kutokea nilipokuwa nimesimama kulikuwa na miti mizuri ya maua, huku chini ya ile miti kukiwa na vibustani vya kupendeza, katika kingo za lile jumba kulikuwa na Mawe yaliyoundwa kiufundi yakiwa yanarusha maji kumwagilia bustani zilizokuwa pembezoni mwa kuta za lile jumba. Ubavu wa kushoto wa ile nyumba ambao uliangaliana na kijumba cha mlinzi, kulikuwa na nafasi kama mfano wa barabara inayoelekea upande wa nyuma wa lile jumba. Nilipotazama mbele kabisa kuifuata nafasi hiyo kama barabara macho yangu yakapokelewa na magari mengine mawili yaliyokuwa ndani ya kichanja maalum cha maegesho ya magari. Nikasonga upande wa Kulia, nikayapita yale magari mawili yaliyokuwa mbele ya lile jumba, kisha nikapita ubavu wa kushoto wa lile jumba wenye mitimiti na bustani za maua, nikapanda juu ya mti mmoja na kuipachika Kamera ya Siri ambayo ilikuwa inaangalia upande wa Getini, nikiwa juu ya mti nikamuona yule kijana akiwa amerudi akiwa kabeba Soda ya kopo “Takeaway” na maandazi, akaviweka kwenye kile kiti, kisha akaingia ndani ya kile kijumba cha mlinzi, baada ya kitambo akatoka akaenda kukaa kwenye kiti. Nikaachana naye.
Nikazunguka upande wa nyuma wa lile jumba, nikiwa natembea kwa tahadhari mkono mmoja ukiwa eneo la kiunoni ilipokuwa Bastola yangu, nikiufuata ukuta wa jumba lile. Upande wa nyuma nikapokelewa na Mandhari ya kuvurtia zaidi, kulikuwa na Bustani nzuri yenye kijani cha ajabu, Bwawa la kuogelea, pembeni ya lile bwawa kulikuwa na ndege wawili wazuri wenye rangi nyeupe. Nilipoona hali ipo shwari nikasonga upande wa kushoto kuufuata ukuta wa lile jumba, hapo nikakutana na Mlango, nikaweka sikio moja kwenye mlango kupima utulivu, kulikuwa kimya, nikakitekenya kitasa, mlango ulikuwa umefungwa, nikatoa funguo Malaya kisha nikafungua ule mlango polepole pasipokutoa sauti, nikapokelewa na korido ambayo kwenye kuta zake upande huu na upande huu kila baada ya hatua tano chini kabisa kulikuwa kumepachikwa taa zenye mvuto wa kipekee ambazo zilitoa nuru isiyong’aa sana na kufanya korido ile iwe na nuru hafifu, hapo nikaichomoa Bastola yangu, mazingira yale hayakuwa rafiki sana, na lolote linaweza kutokea. Bado kulikuwa kimya mno hali hiyo ilinifanya niingiwe na wasiwasi. Nikawa napiga hatua polepole kwa tahadhari, sasa pumzi yangu ilianza kuleta kiherehere na mapigo ya moyo yakawa yananisaliti, hata hivyo nilifundishwa kudhibiti pumzi na mapigo ya moyo niwapo katika mazingira kama yale.
“ Ukimya huu sio bure” Nikawaza, nikakumbuka jinsi yule kijana Mlinzi alivyokuwa ametoka nje ya Geti, nikahisi huenda ule ulikuwa ni mtego, Kabla akili yangu haijaenda mbali zaidi. Saa yangu ya mkononi ikawa inatetema, hii ilimaanisha kunamtu ameligusa gari langu kule nje. Akili yangu ikakosa utulivu, nikabonyeza ile Saa yangu, hapo nikaona Kupitia kioo cha Saa, mwanaume mmoja akiwa anajaribu kulifungua gari langu, nikiwa bado namtazama Mwanaume yule ambaye sikuweza kumuona uso wake kutokana na teknolojia ya saa yangu ya kijasusi, ambayo ilitumia zaidi Body Sensor, na wala sio kuwa ilikuwa imeunganishwa na Kamera za ndni ya gari. Natazama Mbele yangu akatokea mwanaume mmoja akiwa kanishikia Bunduki, nami nikawa nimemshikia bastola yangu tukiwa tunatazamana huku nuru ikiwa ni hafifu kutokana na taa za ile korido, nikiwa natafakari chakufanya, nikshtushwa na mwanaume mwingine akitokea nyuma ya yule mwanaume wa kwanza akiwa naye anabastola, akifuatana na Osman Midevu, Osman hakuwa na Silaha, aliponiona akatabasamu, na kabla tabasamu lake halijaisha nyuma yake akatokea mwanamke, ndiye Dora akiwa anakikombe cha kahawa, nikawa napiga hatua polepole kurudi nyuma nikiwa nimewanyooshea bastola, nikiwatazama kwa umakini kuchunga mienendo yao. Kabla sijapiga hatua ya nne nyuma nikashtuka kusikia sauti kutokea nyuma yangu ikaniambia “ Tulia hivyohivyo, ukijitingisha nitamwaga ubongo wako chini” Sauti ile ikanifanya ninyoshe mikono juu kujisalimisha.
“ Weka silaha yako chini, ujanja wowote utakuwa tiketi yako ya kuzimu” Sauti ileile isiyo na mzaha kutokea nyuma ikaniamrisha, nikatazamana na Dora, kisha Osman alafu nikaliona tabasamu la Kifedhuli likichanua katika uso wake. Nikaitupa silaha chini, hapohapo nikahisi kichwa kizito, nikaanguka chini, giza likafunika macho yangu, sikujua nini kiliendelea baada ya hapo.
*****************************************
ITAENDELEA
Lipia Tsh 15,000/= kupata kitabu cha Kaburi la mwanamuziki Namba ya muamala 0693322300 Airtelmoney