Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 345.

“Inamaana haukufahamu kama Dr Elvice Daniel ni Afisa usalama mpaka siku ya kifo chake?”Aliuliza Roma hio ni mara baada ya Suzzane kumueleza kwamba Elvice alikuwa ni afisa usalama.
SEHEMU YA 342 - 344 Siioni msaada tafadhali
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 625.
Roma mara baada ya kumuona Edna ameacha kuuliza maswali na kushangaa jiwe la madini aliompatia alijikuta akivuta pumzi ya ahueni maana alijua kama Edna angeendelea kuongea mwisho wa siku angeshia kumwambia ukweli wote.
“Nitamuambia Ron kutafuta mhunzi wa kuaminika , hilo jiwe ni kubwa sana na linaweza kukatwa katikati nakutegnenezwa vito vya vingi na unaweza kuchagua kinachokufaa”Aliongea Roma.
“Hapana , sioni inaweza kuwa salama kumpa mtu mwingine , isitoshe nitatafuta huyo mhunzi mimi mwenyewe , kama utalitoa wewe wanawake wengine wataliona na wanaweza wakataka uwapatie na wao”Aliongea na kumfanya Roma misuli yake ya uso kucheza.
“Babe kwahio unasema utalifiicha ndani milele bila watu kuliona?”Aliuliza na Edna alitingisha kichwa lakini hata hivyo akionekana kuwa na furaha kupatiwa jiwe hilo na hakujali kama litakaa ndani ili mradi tu awe na uwezo wa kuliangalia pale anapohitaji pasipo ya kuwafanya wanawake wa Roma kuliona.
Roma hakuongea neno lolote lakini wakati huo aliona kwamba alikuwa na majiwe kama hayo mengi tu ambayo ameyachukua kwa ajili ya hao wanawake, haraka sana hakutaka kumuonyesha Edna kwani angeweza kuyachukua yote hivyo aliona huko mbeleni angetafuta namna ya kuwakabidhi kwa siri.
“Nadhani umeniletea mimi tu , lakini nataka nikuonye , isije ikatokea nikagundua umewapa na wanawake wengine”Aliongea Edna akiwa siriasi.
“Ah.. kwanini nifanye hivyo sasa!?”Roma alijikuta akikosa ujasiri , ijapokuwa aliongea hivyo lakini kijasho cha baridi kilianza kumtoka , alijiambia huyo mwanamke ni kama anayajua mawazo yake , alikuwa akipanga kuwapatia wanawake wengine mawe hayo kwa siri lakini Edna alishaona tayari mpango wake.
Kumuona Edna akiwa ameshikilia jiwe hilo kwa mkono mmoja uzuri wake ulizidi kuongezeka na alikuwa ni kama ua huku tabasamu lake likizidi kuyafanya mapigo yake ya moyo kudunda kwa kasi zaidi , Roma mwishowe alishindwa kabisa kuvumilia njaa yake na kiu aliokuwa nayo kwa muda mrefu na palepale alimsogelea na kumrushia katikati ya kitanda huku jiwe lake likidondokea kwenye mto.
“Ah…nini wewe,, kwanini unaharaka hivyo , hebu kaoge kwanza..”Aliongea kujitetea lakini Roma hakujali maneno yake na tayari alikuwa ashajichimbbia katikati ya kifua chake.
“Siwezi kusubiri zaidi ,,, nimevumilia kwa muda mrefu..”
“Lakini ni siku nyingi zimepita kwanini ushindwe dakika chache za kuoga..”
“Basi tukaoge wote”
“Mh.. usinifanye mjijnga , najua mpango wako ni kufanyia bafuni”
“Kama ni hivyo tulia basi wewe mwanamke … halafu hii sketi ni ya namna gani , vishikizo vyake viko wapi?”
Roma alipeleka mkono kila mahali bila ya kujua kama kweli alikuwa akitafuta vishikio au ndio alikuwa akitaka kuminya makalio , dakika hio hio mkono wake ulikuwa ushatumbukia sehemu nyingine kabis akitafuta vishikizo.
Edna hakuwa hata na nguvu ya kumzuia anachotaka kufanya katikati ya mapaja yake na alijiambia kuziba na mkono ni kujisumbua tu , hivyo aliacha afanye anavyotaka isitoshe kwa wakati huo na yeye moto ulikuwa ushawaka kwenye mwili wake.
Ikiwa ni jioni Blandina alimwagiza kijakazi kwenda kuwaamsha kwani Lanlan alikuwa akiwahitaji lakini kijakazi huyo alirudi akiwa na sura iliokuwa imepata moto kutokana na kile alichokisikia na Blandina kwa uzoefu wake aliweza kujua nini kinaendelea na aliishia kutabasamu.
Alijiambia ni vizuri hivyo kwasababu wanaweza kupata mtoto mapema , hivyo alimsaidia Lanlan kukamilisha homework yake kazi ambayo ilikuwa ni ya Edna.
Katika kitanda cha sita kwa sita Edna Edna alionekana akiwa amejilaza kichomvu huku nusu ya mwili wake ukiwa juu ya Roma , katika hali kama hio kichwa chake kilikuwa kikiwaza vitu vingi.
Baadhi ya wanawake pengine hawawezi kupata uzoefu wa hali ya juu wa utamu ambao anaupata kwenye maisha yao yote lakini kwake yeye mume wake alikuwa akimfikisha kunako bila shida yoyote, hio ndio faida kubwa ambayo alikuwa akiipata kwa mwanaume huyo ambaye amekaa kihuni huni.
Upande wa Roma alikuwa amejiachia m mkono mmoja alikuwa ameupitishia begani kwa Edna akimfanya amlalie kifuani huku yeye akiwa na sigara yake kubwa aliotoka nacho China akiivuta huku akipuliza moshi wake kwa raha zote , hakujali kabisa kuhusu mwili wake uliokuwa uchi na muda huo kiungo chake kilikuwa kimesimama kama mlingoti wa bendera ya raisi.
Edna alijikalia kivivu kwa nusu saa na nguvu zake angalau ziliweza kumrudia , mafunzo ya kijini yalikuwa yamemsaidia sana kuendana na spidi ya Roma la sivyo kwa mikiki yake angepoteza fahamu, aliishia kutabasamu na kisha akampiga Roma busu la shavuni na kusimama kisha akalisogelea kabati na kutoa kipande cha khanga na kujifunga.
“Honey , nina wazo kuhusu Sophia….”Aliongea Edna na kumfanya Roma ambaye alikuwa katika hali ya utulivu kumwangalia.
“Wazo gani?”
“Wiki moja zilizopita kampuni ya Vexto upande wa habari na burudani tulipitisha zaidi ya bilioni nne za kitanzania zinazowenda kuwekezwa kwenye udhalishaji wa filamu mjongeo ya hadithi ya ‘Shetani Rudisha akili zetu” kutoka kwa mwandishi Singanojr , huu ni uwekezaji mkubwa wa kwanza kufanyika nchini Tanzania na kampuni ya Vexto Media and Entertainment ndio wasimamizi wakuu , mpango wetu ni muvi hii kufanya vizuri na sio kufeli au kwenda kinyume chake..:”
“Hebu subiri , kama ni hivyo Sophia anahusiake na hio bajeti?”Aliongea Roma huku akikunja sura.
“Sophia anakwenda kuwa Sterling wa kike kwenye hii filamu, muvi yake iliopita iliweza kufanya vizuri sana kwenye mtandao wa Netflix na kuibua hisia za watu wengi kutoka mataifa mbali mbali hususani Ulaya na Amerika , nadhani pengine ni kutokana na kuwa ‘endorsed’ na Christen ndio maana, viongozi wa Vexto wamekuja hapa na kunishawishi uhusika wa Sophia na kweli nimekuja kugundua ukiwa Star huwezi kukwepa Skendo , hivyo tofauti na kukimbia ni kuzichukulia Skendo hizo kuzidi kujipandisha ki umaarufu, hivyo wengi wameshauri kwamba Sophia ashiriki katika filamu hii kwani ni ‘Action Movie’ na ile iliotoka chini ya Director Lassay Sophia alifanya vizuri sana hususani upande wa mapigano”Aliongea huku Edna akikaa pembeni ya kitanda akijarbu kumwelezea.
“Edna usinifanye mimi mumeo ni mjinga , Sophia alishatangaza kuachana na maswala ya usanii inawezekanaje filamu ikafanya vizuri , labda unionyeshe ushahidi au unataka tu Sophia kurudi katika maswala ya usaniii?”
“Ndio nataka arudi , huu ni uwekezaji mkubwa na kama Sophia atahusika na filamu ikafanya vizuri kampuni yangu itaimarika na kuwa kubwa zaidi , sio Tanzania tu bali mpaka nje ya mipaka ya Tanzania na hayo ndio yalikuwa malengo yangu tokea mwanzo katika kuianzisha”Aliongea .
Roma alivuta moshi wa sigara mwingi na kabla Edna hajashituka moshi wote ulipulizwa usoni mwake na kuishia kukohoa kwa nguvu.
“Kwanini unannifanyia hivi..?”aliongea huku akimfinya.
“Nimefanya hivi ili kuirudisha akili yako katika mstari , Edna kwanini unapenda hela namna hio , ile kampuni ni tawi tu na hata ikifirishika huwezi kupata hasara kubwa , kwanini unataka kumrudisha Sophia ili kuikuza kampuni yako ili ujipatie pesa , halafu sio kwamba hela zenyewe huna , kwanini unataka kumsumbua kama yeye mwenyewe alitangaza hataki maswala ya usanii?”
“Nini ? Kwahio wewe ndio unajifanyisha sasa hivi ndio unamjali sana , Bibi yangu alinifunza jinsi ya kuwa mfanyabiashara tokea nikiwa mdogo , kama nisipojali hela kama mfanyabiashara kuna kipi kingine napaswa kujali , je napaswa kujali wanawake kama wewe , mimi sina njaa ya hela lakini vipi kuhusu wafanyakazi wangu , vipi kuhusu timu ya udhalishaji wa hio filamu , na wenyewe wanafamilia na ndoto za kukamilisha na walifanya kazi kubwa kumpaisha Sophia kimuziki lakini akaamua tu kuachana na usanii na kukimbia kwenda kujificha , kampuni sasa hivi haifanyi vizuri je unadhani ni sawa , sio kama nataka kumlazimisha kufanya kazi , ninachoatka ni yeye kurudi na kufanya kitu anachokipenda mbele ya kila mtu”
Roma aliona ni kweli watu wengi walifanya kazi kubwa kuhakikisha Sophia anaupata umaarufu na kupitia yeye wengine waliweza kupata ujira wao lakini akaacha na kufanya kampuni kuzorota na kuwapa watu mzigo wa kuirudisha katika uimara wake.
“Una uhakika na unachotaka kufanya , sitaki akawe topiki ya kila mmoja kama ilivyotokea , yule baba yake sio mtu mzuri sana jambo baya linapomkuta binti yake” Aliongea lakni Edna alimwangalia Roma kwa jicho la pembeni.
“Kuna kitu kinachoendelea kati yenu sio ndio na unanificha , kwanini hutaki akirudi?”
“Hamna kinachoendelea , naongea kama shemeji yake”
“Naamini hujawehuka na kumgusa na Sophia , itakufanya uonekane mnyama”
Maneno hayo yalimfanya Roma kuingiwa na majuto , alikuwa tayari ni zaidi ya mnyama , alijikatia tamaa yeye mwenyewe na tabia yake lakini hakuwa na la kufanya, Sophia alikuwa amekufa na kuoza juu yake , anaweza kuwa mpole lakini alikuwa siriasi kuhusu hisia zake.
Roma hakuwa akitaka Sophia arudi kwenye usanii kwani ingepelekea mwisho wa siku kugundulika alikuwa aki’dat’e nae , sasa alijiuliza atawezaje kuzuia swala hilo bila ya kuibua mashaka.
“Vipi simu ya Sophia inafanya kazi?”
“Nadhani itakuwa imezimwa”
“Kama ni hivyo basi nitamtafuta mama yake , nina namba yake , nitamweleza mpango wangu na nadhani lazima anikubalie”Aliongea Edna huku akisimama na kuisogelea simu yake.
“Sio lazima kuwa na haraka hivyo , isitoshe wewe sio CEO tena hio kazi anaweza kufanya mtu mwingine”
“Najua lakini Ernest hawezi kulifanyia kazi hili vizuri , hivyo napaswa kuhusika, kuna siku mbili tu ambazo zimewekwa kwa ajili ya kuchagua wahusika hivyo lazima nimshawishi Sophia ndani ya siku hizo”Aliongea na kumfanya Roma kufikiria kitu kingine cha kukwamisha mpango huo na palepale macho yake yalichanua.
“Ah .. Edna mke wangu hatuwezi kufanya hivyo kuna tatizo?”
“Tatizo gani tena?”
“Kumbuka nilikuambia Sophia yupo kwenye levo ya Nafsi kwa msaada wa Aoiline , lazima atapaswa kwenda ulimwengu wa kijini kama sheria inavyomtaka, atawezaje kuwa msainii?”Aliuliza na kumfanya Edna kufikiria kidogo na kisha alitoa tabasamu la kupata njia.
“Kwanini tusifanye hivi , nimesikia kikosi cha wachawi ndani ya Tanzania kimeunda ushirikiano wa maswala ya kijeshi na kikosi cha wachawi kutoka China ambacho ndio kina muunganiko mkubwa na Hongmeng , kwanini usiongee na Afande Tobwe akajaribu kufanya mawasiliano , isitoshe Sophia ni msanii mkubwa tu na kama mara ya mwisho uliweza kumhonga yule mjumbe wao na akakubali basi nadhani na la Sophia linawezekana ,isitoshe yupo hata Omari Tozo ambaye yupo levo ya nafsi na yupo uraiani”
“Unadhani njia hio itafanya kazi?”
“Naamini itafanya kazi, tunaweza kuwapa rushwa hata ya vidonge wakati watakapotaka kumchukua Sophia”Aliongea na kumfanya Roma ashindwe kuongea chochote , mpango wake aliona unaweza kufanya kazi vizuri na aliona kama ataendelea kukwamisha mpango wa Sophia kurudi basi inweza kuibua mashaka kwa mke wake.
Roma baada ya kuona hakuwa na chaguo lingine ilibidi awasiliane na Afande Tobwe na kumuelezea mpango wake kama anaweza kuwaungaisha na wajumbe wa Hongmeng wanaoishi duniani ili Sophia sheria isimguse na Afande Tobwe licha ya kutokuwa na uhakika lakini alisema atajitahidi.
Roma hakuacha kuuliza kuhusu habari za Edna kuua wanajeshi pamoja na wachina waliokuwa katika levo ya nusu mzunguko lakini upande wa Afande Tobwe mwenyewe hakuuwa na maelezo ya kutosha juu ya tukio hilo na hata uchunguzi ambao wamefanya haukuleta mwanga wa aina yoyote.
Baada ya Edna kutoka akimuacha Roma mwenyewe chumbani , Roma mawazo yake hayakuacha kumuwazia Aoiline juu ya kilichotokea baada ya yeye kuondoka.
Baada ya kuona hatoweza kuwa na majibu hata kama akiwaza aliachana na mawazo hayo na kuanza kuwazia juu ya uwezo wake wa kijini ambao hakuwa na uwezo wa kuutumia.
Alifikira namna ya kufanya na katika kuwaza kwake aliona mtu pekee ambaye anaweza kumshirikisha katika swla hilo ni Profesa Clark.
Hakutaka kupoteza muda palepale alitafuta simu yake na kisha akaitafuta namba ya Clark na kuipiga na ndani ya dakika chache tu iliweza kupoktelewa.
“My Dear Roma ramoni , is it reallly you? Are you really back ?”Aliuliza Clarka na kumfanya Roma kushangaa kwani alijua jambo la yeye kupotea lilikuwa siri kama alivyoelezewa na Afande Kweka.

SEHEMU YA 626.
“Clark ulikuwa unajua nilipotea?”Aliuliza Roma akiwa amekunja ndita kidogo akionyesha mshangao wake.
“Bila shaka , nilikuwa nikikufikiria sana lakini nipo huku mbali na sikujua ni wapi ulipo”Aliogea na kumfanya Roma kutabasamu , alijiambia siku zote ilileta raha pale unapojua kuna mtu anakujali.
“Clark vipi lakini kuhusu maendeleo ya mafunzo yako?”
“Naendelea taratibu sana , bado tu nipo kwenye levo ya mwanzo mwa nusu mzunguko, nimejiingiza katika mafunzo ya Kung Fu ili kupanda kwa haraka na kufanya viungo vyangu kufanya kazi vizuri, lakini niseme tokea nimeanza kujifunza kuna vitu nashindwa kuvielewa kisayansi”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.
“Hebu kwanza tuachane na hayo , nina tatizo kwasasa na nahitaji unisaidie kunifanyia uchunguzi wa kiafya”
“Una tatizo!! , unapitia tena mavumivu ya kichwa?”Aliuliza Clark akiwa na sauti ya wasiwasi .
“Sio maumivu ya kichwa ni kitu kingine tofauti na hicho , kwasasa siwezi kutumia uwezo wangu wa kijini..”aliongea Roma huku akimwelezea kile ambacho kimetokea mwanzo hadi mwisho na Clark upande wa pili alionekana kusikiliza kwa umakini.
“Kama ni hivyo basi nadhani haina haja ya kusafiri mpaka huku Uingereza , nitakuja huko huko kujaribu kuangalia tatizo lako nikichukulia kama nafasi ya mapumziko , pia inaweza kupunguza macho ya wengi “Aliongea na Roma alijikuta akiguswa na maneno yake , kwa namna ambavyo alikuwa akiongea ni kama tatizo lake lilikuwa dogo lakini upande wake yeye aliliona ni kubwa lakini hata hivyo alimkubalia na kupanga wakutane Tanzania.
Upande mwigine Roma alikuwa na wasiwasi kwani yeye na Clark walikuwa ni wapenzi rasmi tokea siku ambayo alimuokoa , hivyo aliomba Edna asije akagundua hilo.
Ukweli ni kwamba Roma alikuwa na wasiwasi kwani mbele yake ana mizigo mitatu ya kumwambia Edna ambayo hakuwa na uhakika kama angeweza kuchukuliaje.
Edna alipaswa kujua kuhusu Lanlan , wakati huo huo Roma alikuwa ashafanya kosa na Magdalena mpaka kulala nae , bado yupo Sophia na Clark , wote alishaanzisha mahusiano nao na Edna hakuwa na uelewa wa maswala hayo , hivyo moja kwa moja ni kwamba uendelevu wa mambo hayo ni kama bomu ambalo linahesabu dakika kurudi nyuma na siku yoyote lingeweza kulipuka huku mwenyewe aishindwa kujua ni madhara ya aina gani ambayo yanaweza kutokea.
Wakati Roma akifikiria makosa yake ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake kuyaeupuka palepale aliwakumbuka Rose na Magdalena ambao walikuwa katika visiwa vya bahari ya Mediterranian na ilikuwa ni muda mrefu hajawatafuta kujua maendeleo yao.
Roma palepale na wazo lingine liliibuka katika kichwa chake na kujiuliza kama Sophia anaweza kusamehewa na kuendelea kubakia uraini licha ya kuwa katika levo ya Nafsi , je na Magdalena anaweza kusamehewa, isitoshe Magdalena alikuwa katika mfumo wa kijeshi.
Roma baada ya kuwaza kwa muda mfupi kidogo aliamua kutafuta namba ya Magdalena na kumpigia na ilipokelewa kwa shangwe zote upande wa pili , kwani ilikuwa ni taarifa nzuri kwao kama Roma ameweza kurudi salama.
Roma alimpamba pamba na maneno ya hapa na pale na baada ya hapo alimwelezea swala la yeye pia kuruhusiwa kuishi kawaida licha ya kuwa katika levo ya Nafsi.
“Roma umeshashau kama Mzee Tobwe ni baba yangu? , alishaniuliza pia hilo kabla yako na kuniambia anaweza kutumia koneksheni zake niendelee kubakishwa uraiani”
“Sasa kwanini hukuniambia kuhusu hilo au ilikuwaje?”
“Sikutaka kumpa baba mzigo mkubwa , ulishasema ni sheria ambazo zimeweka kwa ajili ya kuimarisha usalama wa dunia hivyo sikutaka baba avunje sheria kwa ajili yangu , isitoshe sio kwamba ni kuhusu mimi tu kuna Rose na yeye, kwasasa nina furaha mazingira ya huku ni mazuri sana na ya amani pamoja na watu wake kuwa wakarimu , sina haja ya kuomba na mimi kuruhusiwa”
“Inaonekana hamna mpango tena wa kutaka kuishi karibu na mimi , wewe na Rose?”Aliuliza Roma.
“Sisi hatuna shida , tunaweza kuishi popote , tunaweza kurudi pia kama Edna hana shida”Aliongea Magdalena akijaribu kutania na kumfanya roma kucheka kivivu.
“Okey basi hakuna shida , nilidhani hamna furaha kuishi huko mbali na familia ila kama mko sawa basi hakuna shida , mpe simu na Rose niongee nae, nijue ana mishe gani siku hizi?”
“Rose hayupo hapa , anavua samaki anataka mchana wa leo kula chakula cha baharini tu , Mr Ron alituletea wapishi lakini Rose kawakataa na kusema atapika mwenyewe”Aliongea na maneno yake yalimfanya Roma kuona kweli warembo hao walikuwa wakifurahia maisha maana walionekana kuzoea mazingira tayari.
Upande huo mwingine wakati Roma akiongea na Magdalena , Rose alikuwa ameakaa juu ya jiwe kubwa lililotokezea majini huku akiwa amevalia miwani ya jua.
Alikuwa amevalia mavazi ya fukwe , mtindo unaofahamika kwa jina la Hawaian styled Bikini , mtindo ambao ulifanya umbo lake lote kuonekana na kuzidi kuvutia.
Dakika hio hio akiwa bize kusubiria ndoano yake kunasa samaki , alitokea Magdalena nyuma yake akiwa ameshikilia simu.
“Roma anataka kuongea na wewe”Aliongea Magdalena lakini Rose hakuonyesha mshangao zaidi ya kuweka umakini wake kwenye ndoano.
“Amerudi , amekuambia yupo salama?”
“Ndio yupo salama , vipi hutaki kuongea nae mwenyewe”
“Vizuri kama yupo salama .. subiri ,, Ah Magdalena angalia ndoano imekamata , Samaki mkubwa jamani”Aliongea huku akianza kuvuta kwa kuzungusha.
Rose hakuwa mtu ambaye alikuwa akifanya matembezi ya kusafiri , pengine ndio maana kila kitu kilichokuwa kwenye kisiwa hicho kilimshawishi kukifanya , alikuwa na ratiba zake maalumu kuna siku alikuwa akizama chini ya maji kuangalia viumbe hai , siku nyingine alizama msituni kuwinda , siku nyingine ndio kama hivyo alikuwa akivua samaki.
Alikuwa na mambo mengi ya kufanya lakini kwa bahati mbaya ni kwamba uwepo wao kisiwani hapo sio kwa ajili tu ya kustarehe .
Roma hakutaka kuwasumbua sana baada ya kuona wanafurahia maisha hivyo alikata simu na kuwaambia atakuja muda si mrefu kuwatembelea.
Siku iliofuata Roma mpango wake ni kurudi Dar es salaam akiwaacha Edna na Lanlan, alikuwa akitaka kurudi kwa ajili ya kumhoji Qiang Xi kwanini alimuweka gizani licha ya kupewa maagizo na Master Chi.
Roma mara baada ya kuaga wakati wa chakula cha usiku wengine wote hawakuwa na tatizo lakini kwa Edna alijua tu lazima atakuwa amewakumbuka wanawake wake waliopo Dar es salaam lakini hata hivyo hakuwa na muda wa kujali kile anachokwenda kufanya.
******
Wakati mengi na mengi yakiendelea katika maisha ya Roma ya kila siku , upande mwingine nchini Rwanda katika makazi ya Raisi Jeremy alionekana Master 4 akiwa ameketi kwenye Sofa huku akiwa ameshikilia kishikwambi cha kampuni ya Sumsung akipangusa kutoka kulia kwenda kushoto.
Inawezekana kabisa alikuwa ni jini kutoka miliki ya Panasi lakini haikumaanisha kwamba maisha yake yalikuwa tofauti sana na ya binadamu wa kawaida , kwa jinsi tu alivyokuwa akionekana kwa mtu wa kawaida hawezi kugundua kama sio mtu wa kawaida.
“Jeremy hizi ndio taarifa pekee ulizopata kuhusu Roma Ramoni au kuna zingine?”Aliliza .
Raisi Jeremy wakati huo alikuwa ameketi pembenii akimwangalia Master 4 aliekuwa akipekua taarifa alizompatia , ambazo zilikuwa katika mfumo wa kidigitali.
“Ndio Master 4 , ukiachana na taarifa nyingine za international underground organisation”aliongea na kumfanya Master 4 kuishia kuguna.
“Huyu Roma Ramoni ni mtu hatari sana , ndio kwanza yupo kwenye miaka yake ya ishirini kwenda therathini lakini ana mafanikio makubwa namna hii katika mataifa ya Ulaya na Amerika”
“Hakika , ni ngumu sana kushindana nae akiwa katika mataifa yaliondelea tofauti na akiwa huku Afrika ya mashariki , kila serikali kubwa duniani ina wasiwasi nae kutokana na koneksheni zake kuanzia kwenye jeshi na makampuni ya kutengeneza siraha , ni rahisi kusema kwamba kwasasa ndio mfalme wa underwold , bila kusahau pia anamiliki eneo kubwa ambalo amepatiwa hati ya umiliki na serikali ya Uingereza katika bahari ya Mediterranian , ni muunganiko wa visiwa ambavyo vinaitwa Visiwa vya wafu na ndio makao yake makuu na shughuli zake zote zinafanyikia hapo , wahalifu wakubwa walioamua kuachana na maisha yao ya nyuma hutafuta makazi ndani ya visiwa hivyo , ni kwa bahati mbaya kwamba hatuna uwezo wa kupata taarifa uelekeo wa eneo hilo kwani limetolewa katika mfumo wa ramani ya dunia na hata satilaiti zinashindwa kupokea taarifa katika hilo eneo”
“Mh.. hakika ni mtu hatari , ndio maana ni mtu wa majigambo sana , ni kwa bahati mbaya mtu kama huyu hawezi kufanya kazi na sisi ..”Aliongea huku akiendelea kukagua taarifa hizo kupitia Kishikwambi.
“Uwezo wake wa kijini ni mkubwa kiasi cha kufikirika , uongozi wa miliki umeniagiza kuipata mbinu yake ya mafunzo na kumfanya kuwa mmoja wetu lakini naona kabisa misheni hii haiwezi kuwa nyepesi , labda tuweze kupata udhaifu wake”Aliongea.
Wakati huo raisi Jeremy alionekana kuna kitu ambacho alikuwa akitaka kuongea lakini alikuwa akisita sita.
“Master 4 ile siku ya tatu yake baada ya mapambano hapa Rwanda Namba moja alinitafuta kwa ajili ya kikao”
“Namba moja alikutafuta yeye mwenyewe kwa ajili ya kikao?”Aliuliza kwa mshangao
“Ndio , ni muda mrefu sana tokea alivyofanya hivyo”
“Aliongea nini?”aliuliza Master 4 huku akikunja sura.
“Alisema tunavuka mpaka wa kisheria uliowekwa , watu wengi mnatoka katika ulimwengu wa kijini na kusumbua raia”
“Tokea kuundwa kwa umoja wa koo zote za kijini na Namba moja kuwa kiongozi wetu haijawahi kutokea akaingilia katika maswala yetu , sikutegemea awamu hii angezungumzia kuhusu hili”Aliongea Master 4 huku akionyesha wasiwas.
“Master 4 kwani anatisha sana mbona anaonekana wa kawaida?”
“Nakutahadharisha Jeremy , kama kweli Namba moja amesema tumevuka mipaka basi lazima atakuwa anatuchunguza kwa kila tunachofanya , mtu kama yule hawezi kukuita kutaka kuongea na wewe hivi hivi , jaribu kutumia akili yako kufikiria kuhusu hili , je kwanini haijawahi kutokea akabadilishwa na kuendelea kuishi maisha ya kawaida licha ya mambo mengi kutokea kwa zaidi ya miongo ?”Aliuliza na palepale alimfaya Raisi Jeremy kujikuta katika hali ya wasiwasi.
“Ila usiwe na wasiwasi , nadhani anajaribu kuwa makini tu na sheria , wewe bado ni kiongozi wa ukoo wetu katika ulimwengu wa kawaida, kama ungekuwa hufai basi ungeshaondolewa muda mrefu”Aliongea akijaribu kumtoa Jeremy wasiwasi na kisha akaendelea kupitia faili la Roma ambalo limesheheni kila mtu ambaye alikuwa na mahusiano nae.
Master 4 mara baada ya kuendelea kupitia kurasa za maisha ya Roma nchini Tanzania hususani wanawake aliokuwa nao katika mahusiano alijikuta akisimama kwenye picha ya msichana mdogo mweupe.
“Huyu msichana na yeye ni sehemu ya wanawake zake?”Aliuliza huku akimsogezea Jeremy kile kishikwambi.
“Ndio , jina lake anaitwa Rufi, kwa taarifa ambazo tunazo mama yake ni Wema Sufiani kijakazi wa muda mrefu katika familia ya Adebayo na ndio amemzaa huyu binti na mchina mmoja ambaye alikuwa ni machinga anaefahamika kwa jina la Kunlun na baada ya kuzaliwa kwa Rufi alipotea nae.
“Huyo msichana inasemekana alikutana na Roma nchini Marekani na kuanzia hapo ndio uhusiano wao ulipoanzia mpaka ilipoweza kufahamika ni mtoto wa Wema ,kwasasa anaishi na mama yake jijini Dar es ssalaam”Aliongea.
“Mozheng my friend .. hahaha… Rufi!! ni yeye namkumbika ,, hahaha.. inavutia , inavutia , Roma katoa wapi huu ujasiri kuwa na mahusiano na huyu msichana”Aliongea Master 4 alionekana kumfahamu Rufi na baba yake.
“Master 4 kuna kitu kingine kinachohusiana na huyo msichana?”
“Mh ,, hakuna kitu kikubwa zaidi kuhusu yeye lakini naweza kusema ni hazina kwa watengenezaji wa vidonge ,huwezi kuelewa kuhusu hili hata nikikuelezea , tunapaswa kutoa taarifa ya swala hili kwa wahusika wanaomtafuta ,… Roma unaweza ukawa mjanja na kujitosheleza lakini itafikia wakati utahitaji msaada wetu”Aliongea huku akitoa cheko kubwa la ushindi mara baada ya kupata taarifa muhimu ya aina hio.
******
Saa moja moja ndio muda ambao Roma aliweza kufika Dar , alikuwa amechelewa kufika kwasababu alikuwa amechelewa kutoka.
Roma alilaani kitendo chake cha kutoweza kutumia nguvu za kijini kwani pengine kwa muda aliotoka Iringa angeweza kufika Dar ndani ya dakika tu lakini kwa bahati mbaya uwezo huo hakuwa nao na kumbidi kuendesha gari umbali mrefu.
Saa moja na nusu ndio muda ambao aliweza kufika nje ya geti la nyumba ya Dorisi , mazingira yalikuwa yametulia na alitegemea iwe hivyo kwani Dorisi alikuwa akiishi peke yake tokea kuondoka kwa Rose na njia nzima alikuwa akimfikiria , ilikuwa kheri kwa Nasra ambaye Najma alikuwa ni rafiki yake hivyo hakuwa mpweke lakini Dorisi hakuwa na ndugu.
Roma mara baada ya kujifikiria aliona haina haja ya kugonga mlango zaidi ya kuruka ukuta na kwenda kutua ndani kwa ustadi wa hali ya juu.
Baada ya kukagua mazingira, taa za ndani zilikuwa zimewashwa na ilimwambia Dorisi alikuwa yupo hivyo palepale alitembea kitahadhari na kuingia ndani.
Baada ya kufungua mlango wa Sebuleni hakukuwa na ishara ya uwepo wa mtu na moja kwa moja alipandisha ngazi mpaka juu kwenye chumba chake na mara baada ya kufika nje ya mlango aliweza kusikia bomba la maji ya bafuni likitiririsha maji na kujiambia Dorisi muda huu atakuwa ndio anaoga.
Alitoa tabasamu na kisha akashika kitasa na kusukuma mlango taratibu na kuufungua na kitu cha kwanza alichoweza kuona ni nguo za ndani ambazo zilionekana kutoka kuvaliwa zikiwa zimetupwa ovyo juu ya kitanda na hapo hapo aliweza kujiambia hisia zake zipo sawa , Dorisi alikuwa akioga.
Roma macho yake yalivutiwa na nguo hizo na kutoa tabasamu la kifedhuli na kusogea kuelekea ndani ili mradi kuziangalia , lakini ile anapiga hatua ya kwanza na ya pili alijikuta akiguswa na kitu cha baridi kwenye kisogo chake, lakini haikuwa hivyo tu palepale mkono wa kulia wa mtu ambaye amemuwekea siraha kichwani alileta kisu usawa wa shingo na Roma kwa ustadi wa hali ya juu aliruka na kukwepa na kugeuka kwa wakati mmoja na kumshika adui yake mikono.
“Dorisi…!!!”
Roma alijikuta akishangaa mara baada ya kugundua aliekuwa akimshambulia ni Dorisi.
“Hubby ni wewe …!!”
Mapigo ya Dorisi yalikuwa juu juu na alijikuta akiwa na afadhali mara baada ya kugundua ni Roma.
Roma alishangaa kwani Dorisi muda huo alikuwa amevalia suti yake na ilikuwa ni dhahiri ndio kwanza anarudi tokea kazini.
“Babe Dorisi nashindwa kuamini nimeweza kuingia katika mtego ulioniwekea .. haha , umejifunzia wapi haya?”
“Kwaninni hukupiga simu na umekuja kimya kimya , nilijua ni jambazi ndio maana , hebu niachie mikono yangu unaniumiza”Aliongea Dorisi na Roma palepale alijua ni kweli alikuwa ameshikilia kwa nguvu mikono yake yenye siraha.
“Hii mbinu yako ni ya hatari , kama kweli angekuwa ni jambazi basi ungekuwa umemmaliza”
“Hehe.. sikuwa na jinsi , ukiishi mwenyewe unajikuta unatafuta namna ya kujilinda , nimeweza kujifunza hivi kupitia filamu”Aliongea huku akisogea na kwenda kukaa kitandani na kumfanya Roma kumwagalia kwa tabasamu.
Hakuwa amemuona mrembo huyo kwa muda mrefu na aliridhishwa na maendeleo yake kwani alionekana muda wowote angeweza kufika mwishoni mwa levo ya mzunguko kamili.
“Hii mbinu yako imenifurahisha sana Babe Dorisi nadhani tuendelee nayo hivi hivi , mimi nitakuwa kaka jambazi na wewe ni mwanamke unaetoka kazini na kuvamiwa na mimi kaka jambazi na sasa anataka kukubaka”Aliongea Roma na kumfanya Dorisi kuachia cheko huku akivuta mdomo na kumwangalia kwa jicho la pembeni.
“Sitaki kusikia huo ushenzi wako mimi…”
“Hehe leo tutaona , mimi jambazi ndio naanza mambo yangu hivyo”Aliongea Roma huku akimvamia Rose alieanza kujifanyisha analeta vurugu.
Ijapokuwa maneno yake hayakuendana na umri wake lakini ukweli yalimfurahisha Dorisi , inasemekana mtu akiwa mbele ya mpenzi wake anakuwa mtoto na ndio alichokiona Dorisi na alijikuta akikubali kuendelea na filamu yao huku akibakwa na kaka Jambazi.
“Eti wewe mwanamke mbona unaonekana kumpenda kaka Jambazi”
“Wewe kaka Jambazi utakuwa na kimzizi sio bure ..argghh ..Uwiiiii…”
*******
Siku iliofuata Roma alimpigia simu Nasra na kumwambia yupo kwa Dorisi na Nasra mara baada ya kusikia taarifa hio alisema anakuja kupatia kifungua kinywa huko kwani mama yake kasafiri.
Roma hakuwa na kipingamizi , isitoshe Dorosi na Nasra walikuwa ni marafiki wanaofanya kazi ndani ya kampuni moja.
Baada ya wote kukusanyika Roma alipata nao kifungua na warembo wake hao huku akijisikia raha kuwaona kwa mara nyingine na muda wa kwenda kazini ulipo wadia Dorisi na Nasra waliondoka na Roma ndipo sasa alipoanza safari ya kuelekea nyumbani kwa Bi Wema.
Qiang Xi alikuwa akiishi na Bi Wema tokea kuondoka kwa Edna kuelekea Iringa , hivyo Roma alitumia nafasi hio kwenda kumsalimia na Rufi pamoja na Bi Wema lakini pia kupata muda wa kumhoji Qiang Xi kwa kitendo chake cha kumficha juu ya Lanlan kuwa binti yake ilihali alipewa maagizo na Master Chi kumuelezea kila kitu.
Roma hakuwa na gari hivyo alitembea lakini wakati akiwa anakaribia kupita nje ya nyumba yake kuunganisha moja kwa moja kwenda kwa Bi Wema aliitwa nyuma yake upande wa kulia na sauti ya mtu aliemuita aliweza kuitambua ni ya Bi Wema.
“Mr Roma mmerudi!!?”Aliuliza Bi wema akiwa kwenye bashasha.
Bi Wema alionekana kunenepa na mwoneknao wake ulikuwa umebadilika na kurudi kwenye ujana zaidi , pengine ni kutokana kipindi hicho hakuwa akiishi kwa mawazo tena ndio maana uzee ulikuwa ukipotea.
“Nimerudi, Edna yeye bado nimemuacha Iringa na Lanlan”Aliongea Roma na Bi Wema alimuelewa na kumuuliza habari za Iringa.
Bi Wema hakuwa na taarifa za kupotea kwa Roma na kurudi kwake na alijua katika kipindi chote hicho Roma alikuwa Iringa na hakuuliza sana maswali hata alipokuwa akiongea na Edna alijua wapo wote nyumbani.
“Bi Wema ndio nilikuwa nikija kwako”
“Oh!.. ndio nakuja nyumbani , Qiang Xi amenitangulia , tulipanga kusafisha mazingira ya nje leo kwenye bustani”Aliongea na sasa Roma kuelewa na aliona hana haja ya kuendelea na safari bali aligeuza na kufungua gati na kuingia ndani akitangulizana na Bi Wema.
Nyumba ilikuwa imepooza mno , lakini licha ya hivyo ni kama kuna watu waliokuwa wakiishi , mazigira yake hayakuwa ya kipweke sana , hata hivyo hawakuwa wameondoka kwa muda mrefu , ilikuwa ni kama mwezi na siku kadhaa tokea waondoke kuelekea Iringa.
Roma mara baada ya kuona hakukuwa na mabadiliko makubwa zaidi ya nyasi ambazo hazikukaa vizuri aliiingia hadi ndani na ile anafika sebuleni aliweza kumuona Qiang Xi akielekea jikoni akiwa ameshikilia beseni.
“Mr Roma karibu nyumbani”Aliongea Qiang kwa lugha ya kiswahili ilioathiriwa na lugha ya kichina , Roma hakushngazwa na Qiang Xi kuongea lugha ya kisawahili hata hivyo alikuwa ameishi Tanzania kwa muda mrefu hivyo inaleta maana kuanza kuelewa kuongea.

SEHEMU YA 627.
Roma alijikuta akiishia kumwangalia Qiang Xi kwa macho ya kiuchnguzi , ukweli ni kwamba kutokana na upole aliokuwa nao ilikuwa ngumu kusema Qiang alikuwa mtu mbaya.
Baada ya Roma kuongea kidogo na Bi Wema alimwambia Qiang Xi amfuate kuelekea juu ana maongezi na yeye.
Bi Wema kidogo alishangazwa na jambo hilo kwani Roma alionekana kuwa siriasi lakini hakutaka kuuliza wala kujua nini kinachoendelea zaidi ya kujiweka bize kwa kile kilichomleta asubuhi ndani ya nyumba hio.
Upande wa Qiang alimkabidhi Bi Wema Beseni alilokuwa ameshikilia na kisha alipandisha juu kumfuata Roma pasipo ya kuwa na wasiwasi.
“Qiang , babu yake Lanlan kuna chochote ambacho alikuagiza baada ya kukuambia umlete Lanlan kwetu ?”Aliuliza Roma mara baada ya Qiang Xi kuingia katika chumba cha kujisomea cha Edna.
Swali la Roma lilimfanya Qiang Xi kushituka kidogo lakini alijituliza na kumwangalia Roma.
“Mr Roma sijajua ni nini unataka kumaanisha”
“Ni kweli huelewi ni nini namaanisha?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikiwa juu kidogo.
“Sijui ndio..”
Aliongea na Roma palepale alitoa ule ushanga kama Rozari aliopewa na Master Chi akipewa maagizo kumpatia Lanlan kwani angeikumbuka na kumuonyesha Qiang Xi.
“Ushanga wa Master!!!, Mr Roma umezipatia wapi , umekutana na Master?”Aliuliza kwa mshangao huku macho yake yakichanua.
“Hio sio pointi , ninachotaka kusikia kutoka kwako ni barua ulioachiwa na Master Chi iko wapi pamoja na kithibitisho cha Lanlan kuwa binti yangu?”Aliuliza Roma na swali lake lilikuwa bomu kwaQiang Xi na palepale alijikuta mwili wake ukipauka kwa hofu na kuanza kutetemeka.
“Mr Roma , naomba unisikilize…”
“Viko wapi?”Aliongea Roma huku hasira zikianza kumpanda na palepale Qiang Xi akiwa anatetemeka na machozi yakianza kumvaa alijikuta akipiga magoti mbele ya Roma.
“Mr Roma , tafadhari naomba usikilize maelezo yangu , nilikuwa na sababu”
Roma alijikuta akimwangalia , licha ya kwamba alikuwa akitia huruma lakini bado hakuweza kupungza hasira zake mara baada ya kushikwa na hatia ya kuishi na Lanlan muda mrefu pasipo ya kufahamu ni binti yake.
Kwa wenza wa kawaida pengine kuambiana wanapendana ni jambo la kawaida lakini upande wa Roma na Seventeen ambao maisha yao yalikuwa ni ya kupambania maisha yao hawakupata muda hata wa kuelezana ni kwa namna gani wanapendana lakini licha ya yote hayo hisia zao ziliongea mpaka kufanikisha kupata mtoto , hisia zao za pamoja zilikuwa zimetengeneza mizizi ambayo ilikuwa ngumu kung’olewa.
Roma alijiambia pengine Qiang Xi ana bahati , kama jambo hilo lingetokea miaka kadhaa nyuma akiwa na ukichaa wake basi asingeweza kumpa hata nafasi ya kujielezea na muda huo angekuwa ashamuua.
Alijitahidi kuzuia hasira zake na kumwangalia Qiang Xi aliekuwa akitia hruma na kisha akavuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Niambie sababu zako”Aliongea Roma na palepale Qiang Xi alijikuta akishukuru na kufuta machozi yake na mkono
“Mr Roma ninaweza kusema kwamba wewe sio binadamu wa kawaida na hata sasa kwa wakati wote ambao nimeweza kuishi ndani ya hii nyumba naweza kusema wewe ni mungu mtu , kama ilivyokuwa kwa Master, na siwezi kuthubutu kufanya kinyume na maagizo yenu”
“Huwezi kuthubutu , ulinifanya niwe gizani kwa muda mrefu na pengine usingeniambia kama tu nisingekutana na Master”
“Hapana Mr Roma , najua nilifanya makosa lakini nilifanya hivi kwa ajili ya familia yako , kwa ajili yako , Madam na Lanlan”
“Usije kujaribu kunifanyia hila , unadhani mimi ni mwepesi kudanganyika”
“Siwezi kuthubutu , sina uelewa mkubwa na mimi sio msomi na niliacha masomo nikiwa primary tu, hakukuwa na faida yoyote kwa upande wangu miimi kukaa kimya”
“Kama ni hivyo kwanini hukuniambia”
“Nitakuambia kila kitu na sitothubutu kukuficha tena , niliangalia barua aliondika Master mara baada ya kuhisi hatari ya anachotaka kufanya .. nilifanya yote hayo kujua ni wapi anaenda , Master ni mtu ambaye aliniokoa nikiwa hatarini hivyo aligeuka kuwa wa thamani kwangu , hivyo yote nilifanya kuweza kupata kujua ni nini anapanga kufanya ,,, sikujua barua hio ilikuwa ikihusiana na wazazi wa Lanlan”
“Barua iko wapi pamoja na kisu ulichopewa?”Aliuliza Roma akiwa katika mwonekano ambao ni ngumu kujua anafikiria nini.
Qiang Xi mara baada ya kuulizwa swali lile aliwaza kidogo na kisha akasimama na kukimbilia nje na dakika kadhaa aliweza kurudi akiwa ameshikilia kipande cha kisu lakini mkono wa kulia alikuwa ameshikilia simu.
“Mr Roma naomba msamaha wako , barua sikuweza kuitunza lakini nilifanikiwa kui’scan’ kwa kutumia simu …”Aliongea huku akitetemeka.
Roma alimwangalia kwa hasira na kisha akapokea kile kisu na kisha akachukua simu ya Qiang Xi .
Roma alikuwa amezindiwa na hisia za huzuni wakati akiangalia kisu ambacho kipo mikononi mwake , kilikuwa ni kisu ambacho kimefungwa fungwa katika kitambaa cha rangi ya bluu cha hariri.
Hakikuwa kisu cha thamani kubwa lakini historia yake ndio ilimfanya Roma kuona kisu hicho kama cha thamani kubwa kwani mara baada tu ya kukiona mawazo yake yalisafiri miaka mingi iliopita.
Haikueleweka Qiang Xi alitoa wapi akili ya kuiscan barua alioachiwa na Master Chi na kuihifadhi kwa mfumo wa PDF , katika hali kama hio alishukuru kufanya hivyo.
Roma licha ya kukasirishwa na jambo hilo lakini aliishia kusoma barua hio mwanzo hadi mwisho na kila kitu kilikuwa sawa na alivyoelezwa na Master Chi namna ambavyo amekutana na Seventeen na kumuacha Lanlan , Master Chi mwishonni kabisa alikuwa ameandika maneno ya Codes ambayo Roma mara baada ya kuyasoma aliwweza kuyaelewa , yalikuwa ni maneno ambayo ni sawa na ‘signature’ ya barua hio kutbitisha kama yeye ndio ambae aliandika , hakuacha pia kumuusia kuhusu uwepo wa maadui wanaowinda mbinu ya kimaandiko ya urejesho.
“Mr Roma naomba unisamehe , sikuweza kukupatia barua hio na kufanya kama nilivyoagizwa kwani nilijua ukweli wote”
“Kwanini?”
“Mr Roma nimeishi kwa kumlea Lanlan kwa muda mrefu sana mpaka siku ambayo tuliweza kukutana na ninyi , tokea nimeanza kumlea Lanlan nilimchukulia kama binti yangu wa kumzaa lakini kwa upande wake hakuacha kumuulizia mama yake na baba yake , tuliweza kusafiri pamoja huku na kule tukiwa na Master , licha ya kwamba Master alikuwa akimpenda sana Lanlan na kumjali lakini bado Lanlan hakuacha kuulizia kuhusu wazazi wake kila mara alipoweza kuona watoto wakiongozana na wazazi wao , iliniumiza sana kipindi hicho kumuona Lanlan akiwa ni mwenye huzuni ya kukosa wazazi kama watoto wengine , alikuwa ni mtoto wa kipekee na watoto wa aina yake ambao wana akili na nguvu mara nyingi maisha yao huishia kuwa ya upweke , pengine angalau angezaliwa katika familia ya kawaida lakini kipindi hicho hakuwa hata na wazazi , hakuweza kupata kujua nini maana ya mapenzi ya wazazi , hakujua kama wazazi wake walikuwa wanaishi na aliishia kuwaonea watoto wengine wivu..”
“Mr Roma tokea siku ya kwanza Lanlan kumuona Miss Edna , kila siku alikuwa akienda kukaa pale nje ya geti akisubiria kumuona tena , kwa mara ya kwanza tokea nimlee niliweza kuona furaha yake , aliniambia ameweza kumpata mama yake lakini anaogopa ataondoka tena kwasababu hakuwa akimpenda , alikuwa akitia huruma sana na iliniumiza kumuona vile , bahati nzuri Miss Edna akatokea kumpenda Lanlan na kuanza kufikiria kumuasili , Lanlan alikuwa na furaha sana na kwa mara ya kwanza nilimuona akiwa katika hali ya kuridhika .. najua Miss Edna anaweza akafanana na mama yake mzazi lakini mimi kama mwanamke niliweza kuhisi Edna alikuwa akimjali sana Lanlan , alikuwa akimpenda kwa moyo wake wote kama mzazi na swala hilo lilinifanya niridhike na kutotaka kitu kingine zaidi , Lanlan hakuwa akipenda kulala kabisa nilipokuwa naishi nae lakini mara baada ya Madam kuja kwenye maisha yake alianza kulala vizuri na hashituki shituki usiku”Qiang Xi alijitahidi kujielezea , alionekana hakuwa akidanganya , alionekana alikuwa akijali furaha ya Lanlan.
Roma alijikuta akikumbuka namna Lanlan anavyolala na kujikuta moyo wake ukiwa wa moto.
“Mr Roma sijaishi kwenye familia yenu kwa muda mrefu lakini ninawashukuru sasa wewe na Miss Edna , Madam Blandina na Bi Wema na wengine wote ambao ni wazuri kwangu , mimi ni mgeni ndani ya taifa hili lakini niliamua kubakia hapa kwa ajili ya kuendelea kumuona Lanlan.. nashukuru hakuna ambaye amenibagua licha ya kwamba mimi sio wa taifa hili … Sikutaka kukuambia ukweli kwasababu niliogopa familia yako inaweza kuingia kwenye migogoro ambayo inaweza kuwa mikubwa kiasi cha kutengana na athari zikampata Lanlan , najua Miss Edna bado hayupo tayari kuwakubari wanawake wengine lakini hisia zao kwako ni za kweli na wewe ulikuwa ukijaribu kuimarisha familia yako kwa kujitahidi kumbembeleza mkeo ..
“Mimi si kitu , sijasoma lakini nilichotaka ni kumuona Lanlan akiwa na maisha mazuri , nilikuwa nikitaka kumuona akikua kwenye familia yenye furaha na upendo , nilikuwa mbinafsi ndio maana sikutaka kuondoka kwenye hii familia lakini …”Alijikuta akitoa kilio cha kwikwi.
Qiang Xi alijitahidi kujitetea na maneno yake kwa uzoefu wa Roma aliona hayakuwa na walakini , alionekana dhamira yake ilikuwa wazi , alichokuwa akitaka ni kumuona Lanlan akipata malezi stahiki.
Upande wa Roma aliona pengine ingekuwa sawa kama Lanlan angezaliwa na mwanamke mwingine , lakini Lanlan mama yake alikuwa ni Seventeen ambaye Edna anamchukulia kama mshindani wake.
Seveenteen alikuwa ameondoka moja kwa moja lakini kubaki kwa Lanlan kungemfanya kumkumbuka mara kwa mara.
Roma alijua Edna ni mtu ambae ana hasira za haraka ni ni mwepesi kubadilika na asingeweza kupotezea swala hilo kirahisi , pengine angeweza kumvumilia kwa kuwa na wanawake wengine nje lakini sio swala la Roma kuwa na mtu mwingine anaempenda zaidi yake.
Edna alikuwa akimvumilia Roma na kuendela kuishi nae kwa kujua kwamba ni yeye pekee ndio ambaye alikuwa akipendwa zaidi ya wengine wote.
Upande wa Roma aliona pengine Qiang Xi yupo sahihi , kama angejua mapema Lanlan ni binti yake kabla hata mahusiano yake na Edna kuimarika pengine maisha yake yangekuwa tofauti na sasa;.
Licha ya Roma kufikiria mengi lakini ni kwamba kwa wakati huo alikuwa akijua ukweli wote na asingeweza kwenda kinyume na hitajio la Seventeen la kumtambua Lanlan.
Roma mara baada ya kufikiria kwa muda aliishia kumwambia Qiang kwamba asimame na swala hilo alifanye siri mpaka atakapo mpa ruhusa ya kuongea na asiwe na hofu tena na aendelee kuishi nao na iang Xi alishukuru sana huku furaha yake ikionekana.
Mchina huyu alionekana kupenda mazingira ya Tanzania na katika kujitetea kwake alisema alikuwa Yatima huko kwao China na mara baada ya kukutana na Master Chi pamoja na Lanlan wakawa ni kama ndugu zake , sasa Master Chi ameondoka na Lanlan ameweza kumpata baba yake hivyo kama angerudi China ilikuwa ni kwenda kuanza moja, hivyo familia pekee alioona inamfaa ni ya Roma.
Alipenda wanafamilia hao walivyokuwa wakimjali mpaka kufikia hatua ya kumfundisha tamaduni za kitanzania na alikuwa ameridhika.
Roma akili yake ilikuwa imemjaa , alishindwa hata kujua ni kipi ambacho anapaswa kufanya kwa muda huo kwani kila kitu ni kama kipo hatarini kama ukweli utawekwa wazi alihofia familia yake kuvunjika , alihofia mapenzi yake kufikia tamati, dhamiri yake ilikuwa ikimsuta kwa wakati mmoja.
Roma mara baada ya kushuka chini aliweza kukutana na Bi Wema na kumpa maelezo kwamba yeye na Edna wangerudi januari baada ya mwaka mpya hivyo kama kuna tatizo lolote asisite kumpigia simu na Bi Wema hakuona tatizo na alikubali.
Roma siku hio hio alipanga kurudi Iringa , hakutaka kukutana na warembo wake kwani akili yake haikua sawa lakini hata hivyo alisita kuanza safari moja kwa moja kwani wakati akiwa njiani aliweka miadi ya kuonana na Najma nyumbani kwao kwani Juma alikuwa na sherehe ndogo ya kumtoa mtoto wake mara baada ya kutimiza siku arobaini.
Roma mara baada ya kukumbuka ahadi yake palepale alizama kwenye gereji yao ya magari na ksiha akatoka na Lexus na kuianza safari ya kuelekea Mbagala.
Hakuona haja ya kuwasiliana na Najma kwani walipanga kuonana huko huko yeye akishatoka kazini hivyo aliunganisha.
Ilikuwa mchana hivyo msongamano wa magari ulikuwa mdogo na aliweza kutumia dakika chache tu kufika Rangi tatu mbagala na kuchukua njia iliokuwa ikielekea Bias.
Alikuwa ameikumbuka hio mitaa , alikuwa na muda mrefu kidogo hajawahi kufika tokea mara ya mwisho kuja kujitambulisha mbele ya wanafamilia kama mchumba wa Najma na ilimshangaza kuona njia hio ilikuwa imewekwa rami yote na kupendeza tofauti na mwanzo.
Roma mara baada ya kukaribia karibu na nyumba ya Juma aliweza kuona gari zuri ya bei ghali aina ya Lamborgin ikisimama nje ya geti la nyumba ya Juma , mwanzoni wakati gari hio ilivyokuwa mbele aliishia kutoa tabasamu la uchungu kwa kujiambia magari hayo kuwepo Tanzania ni kama uharibifu wa hela kutokana na aina ya barabara kutoruhusu lakini mara baadda ya gari hio kusimama nje ya geti la nyumba ya Juma alijikuta akishikwa na shauku kubwa zaidi ya kumuona mmiliki.
Ni ndani ya dakika moja tu badala ya gari hio kusimama , ikiwa imekodolewa macho na watu wengi wa mtaa hio , hatimae aliweza kushuka mwanaume mtanashati aliekuwa amevalia suti nyeusi na kufungua mlango wa mbele kushoto na kisha alionekana mwanamke mrembo alievalia hijabu akishuka.
Roma aliishia kuguna mara baada ya kugundua mwanamke alieshuka kwenye gari hio alikuwa ni Najma.

SEHEMU YA 628.
Tokea kurudi kwa Najma ncini Tanzania na kuanza kufanya kazi wizarani alikuwa na mabadiliko makubwa , alikuwa ametoka katika usichana na kuwa mwanamke sasa ambaye alikuwa tamanio la wanaume wengi.
Najma alionekana kutotaka kumkaribisha mgeni aliemleta kwani alionyesha ishara ya kuaga ili kuingia ndani , lakini yule mwanaume alimzuia akionyesha kama vile kuna kitu anataka kuongea nae.
Hali hio ilimfanya Roma kuona pengine mwanaume huyo alikuwa katika harakati za kumpata Najma.
Alifikiria hivyo kwani hakuamini Najma ni mwanamke mwepesi ambaye anaweza kumsaliti , lakini licha ya hivyo hali ile haikumfanya kuwa katika hali ya utulivu na alizima gari yake na kisha akatoka nje na kisha akailoki na kuanza kupiga hatua kuwasogelea.
Roma mara baada ya kusogea karibu zaidi ndio sasa aliweza kumuona mwaname mwenyewe ambaye alionekana kuwa na pesa mpaka kumiliki gari kali la namna hio.
Alikuwa ni kijana mrefu wa saizi ya kati ambaye alikuwa na sura ya kihandsome kumzidi yeye na kwa haraka haraka alimkadira umri wa miaka yake inaweza kuwa ishirini na tano kuendelea..
Alikuwa akivutia kwani alionekana ni mtu wa mazoezi na kubwa zaidi alionekana kujiamini , pengine ni haki yake kuweza kumtongoza mwanamke mrembo kama Najma kwani kimuonekano ni sawa na kusema wanaendana.
Roma macho yake ya haraka haraka yaliweza kumkagua kwanzia suti yake ya Versace , viatu vya kung’aa vilivyoendana na mavazi yake pamoja na muonekano.
Upande wa Roma wakati huo alikuwa amevalia kikawaida sana, shati la mikono mirefu la drafti ya rangi ya kijani na nyeusi, jeans nyeusi pamoja na Moka na saa ya bei ghali alionunuliwa kama zawadi na Edna.
“Mheshimiwa nadhanni leo sio muda mzuri , unaonaje tukaweka miadi siku nyingine , naomba unisamehe..”Aliongea Najma huku akiwa kama mwanamke anaemkataa mtu kistaarabu.
“Najma nishakuambia uniite kwa jina langu tu inatosha , ila kwanini leo isiwe muda mzuri,isitoshe sio kama ni mara ya kwanza kukutana na kaka yako pamoja na ndugu zako , nina shauku pia ya kumuona mwanaume ambaye unatoka nae , hujawahi kuwa hivi leo umebadilika sana”
“Si..”
Najma alitaka kuongea lakini palepale alijikuta akiishia njiani mara baada ya kumuona Roma akiwasogelea na macho yake yalichanua huku furaha yake ikiupamba uso wake.
“Roma!!”
Roma alitembea na kumsogelea Najma huku akimpotezea mwanaume alieitwa mheshimiwa na kisha akamkumbatia na kumpiga Najma busu la Shavuni.
Kwa wakati huo Roma alitaka kwenda mbali zaidi na kumbusu mdomoni lakini alimheshimu Najma kutokana na watu wengi walikuwa wakiwaangalia.
Kitendo cha Najma kukumbatiwa kwa haraka hivyo mbele ya watu kidogo tu adondoshe pochi yake lakini aliishia kufurahi mara baada ya kuona Roma alikuwa na wivu na yeye.
Upande wa mwanaume alieitwa Mheshimiwa na yeye hakujali kitendo cha Roma cha ghafla bali alikuwa akimwangalia Najma na kwa uzoefu wake aliweza kuona Najma alionekana alikuwa amependa kweli na hata matumani yake kushuka zaidi na zaidi.
Jambo hilo lilimkasirisha mno kwani ni zaidi ya mwezi tokea aanze kumchombeza mrembo Najma amkubalie hata kumuahidi ndoa moja kwa moja .
Bahati tu ni kwamba alikuwa mzoefu kwani palepale alipotezea hasira zake za kupokonywa tonge mdomoni na mwanaume ambaye alikuwa na mwonekano wa kawaida kabisa.
“Babe huyu mwanaume ndio nani?”Aliuliza Roma huku akimwachia Najma na kujifanyisha ndio eti anamuona huyo mwanaume .
“Huyu ni naibu waziri wa elimu , Mr Salihi Ibuyawanga nilikuwa nikisubiria Uber ili kuanza safari ya kuja huku na aliniona na kunipa lift”Aliongea Najma kwa sauti ya chini.
Roma alishangazwa na maneno ya Najma kidogo , mwanaume aliekuwa mbele yake alikuwa ni mdogo mno kimuonekano lakini alikuwa ni Naibu waziri, alijiuliza ni kipi amefanya mpaka kuaminiwa kwa umri wake huo.
Roma pia aliona mwanaume huyo hakuwa wa kawaida maana kama kweli kazi yake pekee ni ya Unaibu waziri asingeweza kuendesha gari ya gharama kiasi hicho.
“Mr Roma , wewe ndio boyfriend wa Najma?”Aliuliza yule mwanaume , alionekana alikuwa akilijua jina la Roma pengine ni mara baada ya Najma kulitamka.
“Hapana sio sahihi kusema boyfriend , mimi ndio mwanaume wake”Alijibu.
“Oh ! kwahio unamaanisha umemuoa?”Aliuliza bwana Salihi.
Ukweli ni kwamba alishafanya uchunguzi kuhusu Najma na alishangazwa kwa kuona kwamba Najma hakuwa na skendo nyingi hata kipindi alichokuwa anasoma na jambo hilo ndio lilipa motisha ya kutaka kuwa nae karibu zaidi.
“Bado hatujafunga ndoa lakini nnitaendelea kumpenda mpaka siku ambayo yeye mwenyewe ataacha kunipenda”Alijiibu Roma kwa kujiamini.
Upande wa Najma alijikuta akiguswa na jibu la Roma lakini kwa wakati mmoja akiona aibu na alijiambia anawezaje kumuacha ilihali alimpigania kumpata kwa muda mrefu kiasi hicho.
“Hahaha.. wewe ni noma , kila mwanaume anahaki ya kutoka kimapenzi na mwanamke mrembo kama Najma, ila kwasababu hujamuoa natumaini huwezi kutuingilia sana kwani sitaki tuwe na wakati mgumu ilihali ndio mara yetu ya kwanza kukutana , kwasasa kuna maswala napaswa kuyashughulikia hivyo nitaondoka , natumaini tutaonana tena”Aliongea huku akimwangalia Roma kwa tabasamu ambalo limejaa kebehi na kisha akamgeukia Najma.
“Najma msalimie Shangazi na kaka yako Juma , nitawatembelea muda wowote m tafadhari naomba usinikatalie utaumiza nia utu wangu”
Mheshimiwa Salih hakusubiri jibu kutoka kwa Najma kwani palepale aliingia kwenye gari yake na kuigeuza kwa tambo na kuondoka.
Upande wa Roma alijikuta akiguswa na maneno ya kiuchokozi ya Salihi na alitamani kuipiga teke gari yake na kuiharibu palepale , lakini alijitahidi kujizuia.
“Najma ni kwa muda gani amekuwa akikusumbua?”Aliuliza Roma huku akijitahidi kujituliza na Najma alitoa kicheko cha utani kutokana na namna Roma alivyyobadilika.
“Sikuweza kufanya chochote , yeye ndio mkuu wangu wa kazi na nisingeweza kumkataa bila ustaarabu kwani ningefanya mazingira ya kazini kuwa magumu , naogopa pia kupoteza kazi yangu kwani mama ndio kanisaidia”
“Hilo sio tatizo , ninaweza kukuhamishia wizara nyingine kama anakuchukiza”Aliongea Roma kama vile yeye ndio raisi wa nchi.
“Hapana napenda nafasi yangu ya kazi kwa sasa kwani inaendana na nilichosomea na isitoshe unaweza kunihamishia sehemu nyingine na nikakutana na wanaume wengine ambao wananitaka , ni bora nilipo kwasasa kwani waziri Salihi kuonyesha kunitaka kumewafanya wengine wote kutothubutu kunisogelea”
Roma alijikuta akihema ndani kwa ndani na kujiambia Najma asingeacha kutongozwa kwani hakuwa amemuoa , ni swala ambalo halikuwa likiepukika labda tu aachane na maswala ya kazi.
Roma aliishia kukosa chaguo lingine na kuona ni kheri atulie tu licha ya kwamba hakupenda mwanamke wake kusumbuliwa kama hivyo.
“Babe naomba usiwe na wasiwasi , niamini mimi hakuna kitu ambacho kinaweza kutokea kati yetu , natembelea tu upepo kwa sasa , mwanaume wa aina yake ni wale ambao sio wavumilivu na muda wowote atajikatia tamaa , isitoshe kuna samaki wengi ziwani wa kuvua , pengine amevutiwa na mimi kwa muda tu na muda si mrefu anaweza kuona samaki mwingine, isitoshe tetesi ninazosikia anaweza kupandishwa cheo muda si mrefu”Aliongea Najma na kumfanya Roma kuguna.
“Familia yake ikoje , bado anaonekana mdogo na nafasi yake ni kubwa na unasema atapandishwa cheo?”
“Sijafatilia sana ila kwa ninavyosikia ni kwamba baba yake ni mfanyabiashara na kipindi ambacho raisi Senga yupo kwenye harakati za kampeni alisaidia kwa kiasi kikubwa kwenye kumfadhili , licha ya hivyo nasikia ametoka na GPA ya kwanza kutoka chuo cha Yale Marekani , hivyo ni sawa na kusema nafasi yake inalingana na elimu yake , ni mtu mwenye malengo na elimu ya Tanzania , mheshimiwa amemuweka kama naibu waziri mara baada ya kumpatia ubunge kutokana na mawazo yake ya kutaka kubadilisha mtaala wa elimu wa Tanzania ambao hauendani na kasi ya teknolojia hivyo inaaminika ili malengo yake kutimia atapandishwa cheo na kuwa waziri kamili au katibu mkuu wa Wizara , hizo ni fununu tu”Aliongea Najma kwa kirefu.
Ilikuwa ni kama Roma alivyotegemea , lakini hata hivyo alijiambia Najma hawezi kumuacha yeye na kwenda kwa ndugu naibu waziri Salihi.
Baada ya kuongea kwa dakika chache wakiwa pembeni ya geti Najma aliweza kuitwa na mwanamke ambaye Roma alimtambua ni shangazi yake na wote kwa pamoja waliona wasitishe mazungumzo na kuingia ndani.
Roma mara baada ya kuingia ndani aliweza kupokelewa na Juma ambaye alikuwa amevalia kanzu.
Mazingira ya nyumba ya Juma yalikuwa yamebadilika mno na kwa haraka haraka Roma aliamini nyumba haikuwa ikipangishwa tena kwani ilifanyiwa usafi kuanzia nje mpaka ndani na hata chumba chake cha kihistoria kilikuwa kimebadilishwa muonekano.
Sherehe ilionekana haijaanza bado na kuna wanawake wengi waliokuwa ndani ya geti wakionekana kuwa bize na mapishi , hata hivyo ilileta maana kwani muda ulikuwa ni saa nne za asubuhi kwenda saa tano.
“Bro..!!”Juma aliita huku akiweka tabasamu bashasha huku wakipeana kumbatio ambalo waswahili wa mtaani wanasema ni la kisela.
“Mazingira yamebadilika sana , naona hata room yangu imebadilika kimuonekano”
“Hahaha.. upo sahihi shem , kudra za mwenyezi Mungu zimefanya haya yote kuwezekana, karibu sana bro nyumbani , nilikuwa nikiona kila kinachoendelea hapo nje ila nilitulia kwanza muyamalize hahaha..”
“Hahaha.. kumbe ulikuwa ukituona?”
“Ndio nakuambia hivyo ndugu yangu , unapaswa kuchukua hatua mapema Najma anazidi kuwa maarufu na hadhi yake imepanda”
“Kwa maneno yako , inaonyesha sio mara ya kwanza kuletwa na gari?”Aliuiza Roma mara baada ya kukaa kwenye kiti cha plastiki chini ya turubai.
“Siwezi kusema ni mara nyingi kwani muda mwingine analala huko kwenye apartment yake , ila naweza kusema kila wakati anaokuja anaongozana na Naibu waziri , nadhani pia shida ya usafiri unachangia”Aliongea na kumfanya Roma aone tatizo lipo wapi na alitamani kujipiga kibao.
Aliweza kumsaidia Najma kupanga kwenye Apartment lakini akasahau kitu muhimu sana kumpatia,
Hakukumbuka kumnunulia gari , isitoshe Najma hadhi yake ilikuwa ya juu hivyo asingeweza kupanda daladala ,pengine pia Najma alihitaji usafiri lakini alishindwa kumwambia.
Roma palepale aliona hili haliwezi kuendelea hivi , ngoja atumie upluto wake kuhakikisha gari inasafirishwa hata kwa ndege kuja Tanzania.
Palepale alimwita Najma huku akiingia mtandaoni na kutafuta picha za magari tofauti tofauti ili kumuonyesha ni aina gani anapenda amuagizie.
ITAENDELEA KUHUSU SIKU NO PROMISE'S
Ndioooo
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR
Mono no aware.

SEHEMU YA 629.
Ijapokuwa Najma alikuwa amepata kazi ya hadhi yake lakini bado mshahara wake haukumtosha kununua gari pamoja na kuweza kulihudumia, hivyo kitendo cha kutumia Taxi pamoja na Uber kwenda na kurudi kazini ni kama ilimpa nafasi Naibu waziri Salihi kujenga nae ukaribu kwa kumpatia Lift.
Roma sasa baada ya kupata wazo hilo ndio aliona umuhimu wa kumnunulia gari Najma.
Najma alitaka kuchagua IST gari ya kawaida lakini Roma aligoma kwa kuona gari hio haikuwa na usalama mzuri lakini pia haikuwa ikiendana nae kimuonekano kama mwanamke wake ,hivyo aliamua kumchagulia Mercedenz benz E class Amg 53 ya rangi ya pollar white mettallic ambayo iligharimu zaidi ya Dollar elfu tisini.
Najma alihofia kwa kuogopa gari hio inauzwa hela nyingi lakini Roma alimtoa hofu na kumwambia anao uwezo wa kumnunulia ya thamani zaidi ya hio ili mradi tu iwe na vipengele vya kiusalama wakati wa kuitumia.
Roma hakujali sana kuhusu bei alichojali ni usalama wa gari wakati wa kuendesha ndio maana aliichagua , alifurahi pia kuona Najma alikuwa akijua kuendesha gari hivyo alimwambia aanze kufuatilia leseni.
Roma alikuwa na hela ambazo alizipata Korea kusini baada ya kumuuzia babu yake Yezi vidonge hivyo haikuwa shida kwake kufanya malipo ya haraka haraka na ilikuwa kama bahati kwani Fredi alimwambia gari hio ipo Showroom na ni mpya kabisa Zero kilometer na waende wakaikague, upande wa Roma aliona ni bora wachukue hio kuliko kuagiza nje ya nchi jambo ambalo lingeifanya kufika kwa kuchelewa.
Fredi alikwua ni ndugu yake Roma aliekuwa akijihusisha na uuzaji wa magari kutoka Ulaya , ndio yule ambaye aliwaalika Edna na Roma kwenye sherehe yake ya kuzaliwa na kumfanya Desmond kutaka kumbaka Edna akisaidiwa na Kizwe ndani ya Maple Speed resort.
Upande wa Najma hakuwa na shida na alikuwa tayari kupokea chochote ambacho anapewa na mpenzi wake Roma.
Juma yeye alifurahi kuona dada yake kapata gari ambalo linaendana na muonekano wake lakini kwa wakati mmoja alishangazwa na wepesi wa Roma kutoa zaidi ya milioni miambili za kitanzania kwa ajili tu ya kununua gari.
Roma hakukaa sana nyumbani kwa Juma na baada ya sherehe kukaribia mwisho mwisho alimchukua Najma na kuondoka nae kuelekea posta waterfront sehemu ambayo alielekeza Fredi ndio Showroom yake ya magari inapopatikana.
Roma alikuwa na mpango wa kurudi Iringa siku hio hio kwa gari hivyo hakutaka kupoteza muda mrefu kubakia Dar , isitoshe kile kilichomleta alikuwa ameshakifanyia kazi.
Wakiwa ndani ya gari Roma alimuuliza Najma juu yamaendelo yake ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na Ardhi na alisema anaendelea vizuri japo hakuwa akijua yupo levo ya ngapi lakini ashaanza kuelewa vitu vichache na Roma alimtia moyo kwa kumwambia ajipe muda wa kufikiria ndio ingekuwa rahisi kwake kuweza kujifunza kwa haraka na ubongo wake kupanuka na kuweza kuelewa siri juu ya uhusiano wa mbingu na ardhi.
Upande mwingine mara baada ya Naibu waziri Salihi kuachana na Roma moja kwa moja alielekea ofisini kwani ilikuwa ni muda wa kazi bado, ijapokuwa hata kama asingerudi hakuna ambaye angemuuliza lakini kutokana na kutaka kuweka mfano mzuri kwa wafanyakzi walio chini yake basi alijitahidi kuonekana kazini muda mwingi.
Hata hivyo hakuwa na muda mrefu tokea ateuliwe kuwa naibu waziri , alikuwa na miezi mitatu tu ofisini , yaani yeye na Najma walipishana mwezi mmoja tu yeye akiwa amemtangulia.
Bwana huyo mara baada ya kuwasha tarakishi yake na kufanya kazi kwa muda mfupi aliishia kuegamia kwenye kiti chake huku akionekana kukosa utulivu wa kimawazo.
Picha ya Najma kukumbatiana kimahaba na Roma
ilikuwa ikimsumbua katika akili yake na kumpelekea kukosa utulivu wa kimawazo.
Ukweli ni kwamba mwanzoni aliona pengine Sophia alikuwa akimdanganya juu ya kuwa na mpenzi , aliona huenda ni mbinu tu za Najma kutaka kumkataa pamoja na aibu za kike na hilo lilimpa hamasa zaidi kwani kwa muonekano wake pamoja na hela alizokuwa nazo ni wanawake wachache sana ambao walikuwa na uwezo wa kumkataa hivyo kitendo cha Najma kumkataa kilimpa hamasa ya kuweka juhudi ya kumpata zaidi na zaidi.
Lakini siku hio aliweza kuthibitisha maneno ya Najma mara baada ya kumuona akikumbatiana na mwanaume mbele yake kimahaba , kwake ni kama amepigwa kofi la uso jambo ambalo kwenye maisha yake halijawahi kumtokea.
Lakini licha ya hayo bado hakuwa amekata tamaa , ukweli ni kwamba sura ya Roma ilikuwa ikija na kupotea katika akili yake na hakuwa akimjua vizuri na hio yote pengine ni kutokana na kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu akifanya kazi ubalozini pamoja na Umoja wa mataifa kabla ya kurudi Tanzania.
Alikuwa amekariri namba ya gari ya Roma pamoja na jina lake fupi na wakati akiwa njiani aliweza kuwasiliana na mtu aliemfahamu yeye ili kumsaidia
kumchimba Roma ni nani kwa kuamini kama angepata kujua jina la usajili wa gari yake basi
angepata jina lake kamili na kuweza kufatilia taarifa zake, hakutaka kumpotezea kutokana na kwamba alionekana ni wa kawaida katika macho yake.
Wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo kuwaza namna ya kuushinda moyo wa mrembo Najma simu yake ilianza kuita na haraka haraka aliichukua na kuangalia jina la mpigaji na aliishia kutoa tabasamu.
“Umefanikiwa?”Aliuliza mara tu baada ya kupokea simu.
“Ndio mheshimiwa, Gari hio ilisajiliwa kwa jina la Shedrack Kengeu kabla ya kuhamishiwa usajili wake kwenda kwa Roma Ramoni mmiliki wa sasa , kwa taarifa nilizoweza kupata ni kwamba ni mume wa Edna Adebayo mwenyekiti na mmiliki wa kampuni ya Vexto international , hakuna taarifa kubwa zaidi kuhusu yeye ila alishawahi kuwa mgurugenzi wa kampuni ya Vexto Media”
“Vipi kuhusu familia yake?”
“Taarufa ambazo zipo kwenye Database ya serikali zinaonyesha alikuwa ni Yatima kabla ya kulelewa nchini Marekani , amemaliza pia ndani ya chuo cha Harvard shahada yake ya kwanza ya masoko, tofauti na hivyo hakuna kitu cha maana sana kuhusu CV yake”Aliongea na kumfanya Naibu waziri Salihi kushangaa kidogo
Ukweli ni kwamba taarifa aliopatiwa haikuwa kamili kutokana na cheo chake hivyo asingeweza kupewa kila taarifa inayohusiana na Roma, ijapokuwa Roma alishatambulika kwa baadhi ya watu kama mtoto wa Raisi Senga lakini bado ni taarifa ambayo haikuwa ikijulikana kwa watu wengi na watu baadhi waliishia kukisia tu Raisi Senga alikuwa na mtoto mwingine wa kiume lakini haikufahamika moja kwa moja kama alikuwa ni Roma Ramoni, pengine ni kutokana na kwamba jina hilo halikuwa na uhusiano wowote na familia ya Afande Kweka.
Ukiachana na kwamba hakuwa ameishi Tanzania kwa muda mrefu lakini alikuwa akifahamu kampuni ya Vexto, kwani ndio kampuni kubwa ndani ya Afrika ambayo imeweza kufikia Ulaya katika maswala ya ki uwekezaji, lakini pia alikuwa akimsikia Edna kutokana na kuwa katika orodha ya watu matajiri kutooka Afrika akiwa ndani ya kumi bora
Taarifa ya Roma kuwa mume wa Edna ilionekana kumshangaza na kumgusa bwana huyo , kwani ni jambo ambalo hakuwa ametegemea , ijapokuwa hakuwa akimfahamu Edna vizuri lakini alijua ni mwanamke wa hadhi ya juu sana ndani ya Tanzania.
Ijapokuwa hakuelewa kwanini Edna amekubali kuolewa na mwanaume kama Roma ambaye
alionekana hajatulia lakini kwake aliona ni taarifa nzuri sana kama ingevuja mitandaoni kama Roma alikuwa akichepuka na Najma.
Baada ya kupata wazo mujalabu alitoa tabasamu la kifedhuli na kisha aliinua simu yake na akaingia mtandaoni na kutafuta mawasiliano ya kampuni ya Vexto katika website yao na kisha akaipiga na iliita ndani ya dakika kama mbili hivi bila kupokelewa na alipojaribu mara ya pili ndio iliweza kupokelewa na sauti nyororo ya mwanamke.
“Hello , naongea kutoka makao makuu ya kampuni ya Vexto international , kuna lolote nikusaidie tafadhari”Sauti ilisikika hivyo katika masikio ya naibu waziri Salihi.
“I am Salihi Ibuyawanga , The Vice minister of education , I would like speak to one of chairman , Miss Edna Adebayo, this is urgent matter , please contact her on my behalf”
“Mimi ni Salihi , naibu waziri wa elimu , ningependa kuongea na mwenyekiti wa bodi , miss Edna Adebayo , hili ni jambo la muhimu tafadhari wasiliana nae kwa niaba yangu”
Mtu wa mapokezi hakuwa mjinga , watu wengi walikuwa wakipiga simu wakitaka kuongea na Edna kwa sababu mbalimbali , kuna ambao walikuwa wakipiga huku wakijinadi na kusema wanauza gunduzi za kiteknolojia za hali ya juu, kuna ambao pia walikuwa wakisema wanatokea katika kampuni kubwa za kifedha na wanataka ubia wa kibiashara , kuna wengine ambao wanasema ni ndugu wa vigogo flani serikalini , kuna wengine walijitambulisha ni maraisi wa mataifa ya madogo ya Afrika.
Hivyo kwake haikuleta mantiki kwa naibu waziri wa Elimu kupiga simu mapokezi, hivyo mrembo huyo wa mapokezi aliongeza umakini katika kusikiliza maelezo yake.
“Waziri Salihi , naomba taarifa zako zaidi ili kutambua uhusika wako tafadhari”
“Jambo langu ni kuhusiana na mume wake Roma
Ramoni , gari yake ina namba za usajili kutoka wilaya
ya Bagamoyo 0067BN Lexus Rx 450, unaweza kuthibitisha na nitakupatia dakika moja tu , utawajibika kama kuna jambo baya litatokea kwa kushindwa kuunganisha simu yangu”Aliongea Waziri Salihi kikauzu , alionekana kuchafukwa na roho pengine wivu ndio ambao ulikuwa ukimsukuma kufanya yote hayo.
Upande wa dada wa mapokezi alishangazwa na jambo hilo kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mtu kupiga simu na kuzungumzia kuhusu mume wa boss Edna.
Roma alikuwa maarufu kwa wafanyakazi hao kwani alikuwa mume wa mwanamke mrembo na tajiri Edna hivyo hakuna ambaye hakuwa akifahamu jina lake.
Dakika ileile aliwasiliana na idara ya usalama ya kampuni na kuthibitisha taarifa za Roma na ndani ya sekunde chache tu taarifa ilimrudia ikiwa imethibitishwa na palepale aliwasiliana na Recho.
Ijapokuwa Recho hakuwa teka sekretari wa Edna lakini alikuwa bado akihusika na ku’manage’ simu zote ambazo zinamuhusu Edna.
Baada ya Recho kuongea na Waziri Salihi ambaye taarifa yake ilikuwa ikihusiana na Roma, alijikuta akipatwa na shauku lakini aliamua kujituliza na kutouliza maswali mengi na aliuliza maswali ili kumtambua Salihi kama kweli ni Naibu waziri na baada ya kuthibisha ni yeye kweli palepale alihamisha simu ile kwenda kwa Edna.
Upande wa Edna alikuwa Iringa na muda huo alikuwa akiongea na simu na Daudi mkurugezi wa kampuni ya Vexto Media juu ya maandalizi ya show ambayo imepangwa kufanyikia Iringa , Show ambayo ilikuwa inakwenda kuutanganzia uma kwamba Sophia amerejea katika kiwanda cha muziki, sasa wakati akiwa bize katika kutoa maelekezo ndio namba mpya ilionekana ikipiga kupitia namba yake maalumu ambayo hupokea simu zinazohusiana na maswala ya ofisi.
Aliipotezea namba ile na kuendelea na maongezi yake na Mkurugenzi lakini mtu aliekuwa akipiga alionyesha hali ya kutokata tamaa hata mara baada ya kumaliza mazungumzo yake.
Baada ya simu kupigwa kama mara tano mfululizo bila kukoma palepale alisita kidogo kuipokea lakini baada ya kujishauri kwa dakika kadhaa aliamua kuipokea na kuweka sikioni.
“Is this chairman Edna from Vexto
international?”Sauti ya mwanaume ilisikika na Edna aliitikia kivivu kwa namna ya kuguna.
“Mimi naitwa Salihi , naibu waziri wa elimu , nina jambo nataka kukuelezea kuhusiana na mume wako Roma Ramoni , nimeona ni busara kama utajua kuhusu hili”Aliongea na kumfanya Edna kukunja ndita huku akionyesha mshangao, hakutarajia kama simu hio ilikuwa ikihusiana na Roma.
Alijiuliza imekuwaje Roma akajiingiza kwenye migogoro na Naibu waziri wa Elimu.
“Unaweza kuendelea”
“Tuna mtumishi wa kiserikali afahamikae kwa jina la Najma Waziri ambaye ana mahusiano ya kimapenzi na Mr Roma Ramoni , jambo ambalo linaweza kupelekea uchafuzi wa taswira ya wizara, nadhani kama taarifa hii itasambaa kwenye vyombo vya habari itakuletea pia aibu wewe pamoja na kampuni yako”
Edna mara baada ya kusikia maelezo hayo moyo wake uliuma na alijihisi shoti za umeme za baridi zikisambaa kuanzia kwenye magoti, taarifa hio ni kama ya onyo kwake lakini kwa wakati mwingine ilikuwa kama ya kikandamizi, lakini kwa wakati mmoja alishindwa kuikataa kwani ni jambo ambalo ana uelewa nalo , ilikuwa kidogo tu akae kwenye sakafu.
Baada ya kuvuta pumzi ndefu na kuishusha alijitahidi kujituliza kadri awezavyo lakini alipotaka kuongea ni kama kuna kitu kimemkaba kooni na macho yake yalimuwasha ikionyesha muda wowote machozi yanaweza kumtoka.
Ijapokuwa alikuwa akielewa uhusiano huo lakini kusikia habari hizo kutoka kwa mtu mwingine ilikuwa ikiuma sana kwani ni kama dhihaka kwake.
“Ndugu Mwenyekiti, je unanisikiliza?”Salihi aliuliza mara baada ya kuhisi kimya kirefu kutoka kwa mwenyekiti.
“Nimekusikia…”
Edna alijitahidi na kutoa kauli hio na kisha akakata simu palepale , hakujua sauti yake ingesikika vipi kama tu angeendelea kuongea ndio maana aliikata.
Edna alishindwa hata kujielewa ni kipi anajisikia moyoni mwake na alijiuliza tangu lini akawa hivyo , ni lini kaanza kupoteza utulivu wake ambao ni sifa kubwa ya jina lake.
Alijikuta akikimbilia chooni kwenye sinki na kufungua maji na kisha akatumbukiza sura yake ndani ya maji akijaribu kujituliza na kisha akainua uso wake ulioloana na maji kujiangalia kwenye kioo.
Macho yake mazuri yaliangalia kioo akijaribu kujiangalia lakini kwa wakati huo ni kama hakuwa akijiona vizuri.
Palepale alijikuta kichwa kikianza kumuuma na kama vile kuna kengere zinazosikika katika kichwa chake na alijikuta akifumba macho akisikilizia maumivu lakini wakati huo ilikuwa ni kama vile yupo ndotoni , kwani ile ndoto ambayo ilikuwa ikijirudia rudia kila anapolala usiku ilianza kujitokeza tena katika akili yake.
Dakika hio hio mlango wa chumba chake uliweza kufunguliwa kwa nguvu huku sauti ya Lanlan ikisikika kumuita akiwa ameshikilia
Lambalamba(Icecream) mbili mkononi za kampuni ya Azam.
Edna mara baada ya kusikia sauti ya Lanlan alijikuta akitoka katika mawazo ambayo yalikuwa kama ndoto kwake na kujiweka sawa na kufungua mlango na kutoka.
“Bibi kamnunulia Lanlan icecream nikamuomba amnunulie na mama yake”Aliongea Lanlan huku akimwangalia mama yake ambaye aliekuwa na maji usoni.
Edna muonekano wake ulionyesha kutotaka kupokea Lambalamba hizo lakini Lanlan aliendelea kumnyooshea mama yake kama ishara ya kupokea.
Edna hali yake ya kimawazo palepale ilipungua na aliweza kulazimisha tabasamu akimwangalia Lanlan na uso wake wa kitoto uliojaa ukarimu ndani yake , alijikuta akichuchumaa na kisha kushika nywele zake ndefu.
“Lanlan nitang’ata hii ya kwako kidogo na unaweza kula zote , ina sukari na meno ya mama yatauma”Aliongea Edna na kushika ile ya Lanlan aliokuwa akilamba na kuing’ata kipande.
Lanlan mara baada ha kuridhika na maneno ya mama yake palepale alikimbilia nje kwenda kutafuta mtu mwingine wa kushirikiana nae kula hizo lambalamba , alikuwa tayari ashazoea mazingira na alichukulia hapo ni kama nyumbani kwako na alikuwa ashazoeana na kila mu.
Edna alijikuta akifumba macho yake mara baada ya
Lanlan kuondoka na palepale michirizi ya machozi iliweza kuonekana katika mashavu yake lakini hakuna ambaye alikuwa akijua kama alikuwa akilia kutokana na ubaridi wa lambalamba aliopewa na Lanlan au ni ubaridi uliopo kwenye moyo wake.
Wakati mrembo huyo akionekana katika hisia za uchungu palepale simu yake iliweza kuiita na aliichukua na mara baada ya kuangalia na kuona anaepiga ni Wendy alipokea na kuweka sikioni.
“Boss tayari maandalizi ya show yashakamilika na Meneja Ummy atakuwa Airport Iringa na Sophia usiku wa leo na baada ya hapo ratiba ya tukio lenyewe itaanza kujadiliwa”
“Ni muda gani ambao Sophia atafika Airport?”
“Itakuwa ni saa mbili kamili usiku , tayari tushatuma mtu wa kumpokea kumpeleka hotelini”
“Haina haja , nitaenda kumpokea mdogo wangu mimi mwenyewe , sijaonana nae kwa muda mrefu , hivyo uliowaagiza wanaweza kufanya kazi nyingine”Aliongea Edna.

SEHEMU YA 630.
Baada ya Edna kufanikiwa kumshawishi Sophia kurudi kuendelea na maswala ya usanii alipanga show yake ya kwanza aifanyie jijini Iringa , ijapokuwa ni show iliopangwa kwa haraka kufanyika lakini kutokana na hela pamoja na koneksheni ya vyombo
vingi vya habari jijini Dar es salaam iliweza kutangazwa kwa haraka sana na ikawa habari kubwa na show hio ikawa inategemewa na kila mmoja.
Sophia alikuwa ashaanza safari ya kurejea Tanzania tokea siku ya jana , hivyo moja kwa moja alipaswa kutua Mwanza akitokea Dubai na kuanza safari ya moja kwa moja kwenda Iringa kwa ndege kwani Show ilipaswa kufanyika siku iliofuatia hivyo maandalizi ya mapema kabla ya show hio yalipaswa kufanyika wakati Sophia mwenyewe akiwepo.
Wendy mara baada ya Edna kusema yeye ndio ataenda kumpokea mdogo wake , basi hakutaka kupinga na aliishia kukata simu na kutoa maagizo kwa wale ambao wameagizwa kwenda kumpokea Sophia kutoenda.
Edna alijiambia asingemwambia chochote Roma kuhusu Naibu waziri Salihi alichoongea , alijua kama akisema basi Roma ni lazima angelipiza kisasi pengine cha kumuua kabisa.
Edna hakuona maneno ya Waziri yalikuwa na uongo
, ni kweli kabisa Roma alikuwa akijihusisha kimapenzi na Najma ,hivyo anawezaje kuwa na kinyongo kwa kauli yake, hivyo aliamua kupotezea licha ya kwamba bwana huyo alionekana kama vile alikuwa akimtishia na kumfikishia ujumbe kwamba amkanye mume wake kuachana na Najma la sivyo angevujisha taarifa.
Edna aliamua kujituliza na alijiambia pengine Roma akirudi anapaswa kuongea nae kuhusu hilo na hakupaswa kumfanya mama mkwe wake kujua hilo , pengine ingeonekana labda anawatumia ili kumpa presha Roma.
Edna alikuwa ukingoni, maswala ya kifamilia kwake yalikuwa ni magumu sana kuliko hata maswala ya kibiashara na alijiona muda wowote anaweza kupata uchizi.
Ijapokuwa hakuwa akijivunia na maisha yake ya miaka michache iliopita , maisha ya kutokuwa katika mahusiano lakini kwa wakati huo alikuwa akipitia furaha na huzuni kwa wakati mmoja, alikuwa na furaha alikuwa na familia , lakini alikuwa na huzuni kutokana na michepuko ya mume wake.
Edna mara baada ya kujikalisha chini na kuwaza kwa muda aliishia kung’ata meno yake kwa hasira huku akijituliza na baada ya hapo alichukua simu yake na kuanza kupiga kudili na maswala mengine.
Saa moja kamili Edna alikuwa ashamaliza kula chakula cha usiku na aliweza kuaga anaelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea Sophia.
Familia hio haikumzuia kwani walijua Edna na Sophia ukaribu wao ni wa kindugu zaidi.
Lanlan mara baada ya kusikia habari za mama yake kwenda kumpokea Sophia alianza na yeyekulilia kuongozana na mama yake kumpokea Aunt Sophia na ilimfanya Edna kukosa chaguo lingine na kuondoka nae.
******
Ili kurahisisha ukuaji wa maendeleo ndani ya Tanzania Raisi Senga aliweza kuingia madarakani na sera yake ya kujenga miundo mbinu ili kurahisisha usafiri kati ya mikoa na mikoa.
Miongoni mwa mikoa ambayo ilipewa kipaumbele katika miundo mbinu ni pamoja na Iringa ambayo ilipendelewa kwa kujengwa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa.
Mwanzoni mwa ujenzi huo Raisi Senga alipingwa na wengi kwa kusema anapendelea ukanda wa anakotokea kwani kulikuwa na uwanja wa Songwe tayari ambao upo karibu na Iringa lakini mara baada ya kiwanja hicho kufunguliwa yale maoni hasi yalizima kwani kiliweza kuwa kiwanja maarufu ndani ya muda mfupi na kiliweza kupokea wasafiri wengi kwa siku na kuongoza kwa kuwa kiwanja chenye ubize mkubwa namba tatu nchini.
Ni kiwanja kikubwa ambacho kilikuwa na uwezo wa kuruhusu ndege mbili za abiri za ukubwa wa wastani kutua kwa wakati mmoja huku zile kubwa zikipeana nafasi ya kutua baada ya nyingine kwa zaidi ya dakika kumi tu.
Hviyo ni rahisi kusema kilikuwa na uwezo wa kuhudumia ndege tatu mpaka nne kwa wakati mmoja.
Ijapokuwa hakikuwa kikihudumia ndege za usafiri wa moja kwa moja kutoka mataifa makubwa lakini wasafiri wa kutoka nchi za Afrika jirani na Tanzania zilikuwa zikitua mara kwa mara katika kiwanja hicho.
Kulikuwa na Terminal mbili ya kwanza ilikuwa karibu kabisa na maegesho ya magari ambayo ilihudumia wasafiri wa kimataifa na nyingine ya kuzunguka upande wa pili yake ilikuwa ni terminal ya kuhudumia wasafiri wa ndani.
Hivyo ukiingia ndani ya kiwanja hicho unaanza kukutana na Terminal ya kimataifa ndio unaelekea Terminal ya wasafriri wa ndani.
Edna mara baada ya kufika kiwanjani hapo aliingia mpaka ndani ya jengo la kusubiria wageni wa ndani wanaowasili akiwa amevalia miwani yake ili kuzuia watu wengi wasimfahamu.
Hata hivyo licha ya eneo hilo kuwa na watu wengi wanaotoka na kuingia haikuwa kama uwanja wa ndege wa Dar es salaam.
Baada ya kusubiria ndani ya dakika kumi hatimae makundi ya wasafiri yaliweza kutoka kwa awamu , huku wengi wao wakiwa ni wazungu na watu wa kiasia , waafrika walikuwa wachache sana katika makundi hayo.
Kati ya kundi hilo la waliokuwa wakiwasili alikuwepo Sophia ambaye alikuwa amejichanganya katikati ya watu akiwa amevalia miwani ya jua pamoja na barakoa usoni na sweta la kofia, ilikuwa ngumu kumjua lakini Edna aliweza kumuona kwa haraka na hata kwa Sophia aliweza kumtambua Edna kwa haraka, pengine ni kutokana na mafunzo yake ya kijini aliokuwa nayo.
“Aunt…!!”
Lanlan aliekuwa amesimama alitoka kwenye mikono ya mama yake na kukimbia upande wake.
Sophia hakuonyesha kushangazwa na uwepo wa Lanlan na aliishia kuongeza spidi kumsogelea akitoka katika kundi la watu na alishukuru mara baada ya kuona hakuna mtu ambaye alikuwa akiwaangalia wala hakukua na mapaparazi.
Ijapokuwa alikuwa na aibu kutokana na hatia yake ya kuwa na mahusiano na Roma lakini alikuwa na furaha kumuona Edna kwa mara nyingine.
“Sis , wewe ndio umekuja , ungetuma mtu kuja kunipokea haikuwa na haja ya kuja mwenyewe kwani naenda hotelini moja kwa moja”
“Haina shida , sijakuona muda mrefu hivyo niliona nije mwenyewe , isitoshe ulikuwa katika hali ya hatari ndio maana , Lanlan amekumis pia”Aliongea Edna akitoa tabasamu.
Sophia alijua Edna alichokua akimaanisha mara baada ya kusema mazingira ya hatari , alijua alikuwa akizungumzia juu ya ulimwengu wa majini pepo.
Sophia hisia zake zidi ya Lanlan sasa zilikuwa za tofauti kwani alikuwa akifahamu ni mtoto wa Roma.
Kutokana na kuona Edna hakuwa na uelewa wowote alijiuliza sijui ni lini Roma angemuweka wazi Edna juu ya Lanlan kuwa mtoto wake na Seventeen.
Kwa wakati huo Sophia hakutaka kufikiria sana na alimbeba Lanlan kwenye mikono yake huku akimpiga busu la shavuni.
“Lanlan unakula nini, mbona umekuwa mzito hivi jamani?”Aliuliza Sophia mara baada ya kumpakata , lakini Lanlan alitingisha kichwa chake kukataa kama hajaongezeka uzito.
“Hapana , Lanlan ni mtoto mzuri, mama anakataa nikila mpaka nikishiba”
Kwa kauli yake pengine watu wangesema Edna anamnyanyasa Lanlan lakini kwa Sophia aliekuwa akijua ulaji wa Lanlan alijua maana ya maneno hayo.
Sophia hakuwa peke yake , alikuwa ametangulizana na meneja wake Ummy na alishangazwa na maneno ya Lanlan na kujiambia Edna ni mtu makini kujaribu kuzingatia ulaji wa chakula cha binti yake ili asinenepe vibaya.
Edna hakutaka sana watu wa nje ya familia yake kusikiliza maongezi yao na alimwambia Ummy kwa kauli kavu achukue Taksi kumpeleka moja kwa moja hotelini yeye ataondoka na Sophia.
“Boss , nashukuru sana umekuja kutupokea lakini sidhani kama ni sawa kukusumbua”
“Nimesema nitaondoka nae mwenyewe ,, kuna haja ya mimi kurudia rudia?”Aliongea kikauzu kwa kuona meneja huyo anashindwa kujiongeza.
Meneja Ummy alijikuta akiogopa macho ya kikauzu ya Edna na aliishia kutingisha kichwa kwa kuitikia na alichukua begi lake akiondoka, hakutaka kusubiri tena kwani aliogopa kupoteza kazi yake.
Sophia alimuonea huruma Meneja wake lakini kwa wakati mmoja akionea wivu namna Edna alivyoongea kibabe kwani ni kitu ambacho yeye hakuwa akiweza , ukali wa Edna uliwafanya wafanyakazi wengi kumtii kila anapotoa agizo bila ya kuuliza mara mbili mbili.
“Tuondoke nitakupeleka moja kwa moja hotelini na tutakuwa na kikao cha muda mfupi na nitakuacha , najua kwanzia kesho utakuwa bize ndio maana nimeandaa kikao usiku huu huu”Aliongea Edna huku wakitembea kurudi upande wa magari yanakoegeshwa.
“Sis , unafikiri ninaweza kufanya vizuri kama mwanzo , naona kama watu wanachuki na mim?”Aliongea Sophia akiwa na wasiwasi kutokana na skendo yake ya mwanzo.
“Utafanya vizuri ndio , ilimradi tu nyimbo zako na uigizaji wako utakuwa mzuri basi naamini utarudi katika ubora wako na kupanda juu zaidi , kupitia hela itakuwa rahisi pia kusafisha jina lako na kila mtu atakukubali tu , wasanii mnapaswa kuushawishi umma na kazi zenu na si vinginevyo , nina imani na wewe..”
“Kumbuka pia nimetumia zaidi ya mabilioni ya hela kuanzisha kampuni yote ya burudani na habari , unataka kweli kampuni yangu kufirisika , ninaweza
kuwa tajiri lakini pia sipendi hasara , ninataka kuendelea kukutegemea kama mgongo wa kamapuni upande wa burudani”
Sophia alijua Edna alikuwa sahihi na maneno yake ni kwa ajili ya kumpa motisha lakini hakuacha kujisikia vihaya , alitamani ni kheri Edna kumlaani ili mradi tu ajisikie vizuri .
Lakini licha ya yote Sophia alipanga kufanya kazi vizuri ili tu kutokumuangusha Edna ambaye ameweka tumaini kwake.
Wakati wakielekea upande wa maegesho ya magari waliweza kupita nje ya mlango wa wasafiri wa nje ya nchi wanaowasili na Edna alijikuta akisimama baada ya kuona kitu na Sophia hivyo hivyo alisimama na kuangalia upande ambao Edna alikuwa akiangalia.
Alikuwa ni Roma ambaye alionekana mbele yao akitembea kuingia jengo hilo la wageni wanaowasili, ijapokuwa hakuwa na muonekano wa kuvutia kama wengine kutokana na staili yake ya uvaaji lakini Edna na Sophia waliweza kumuona kwa haraka kutokana na kwamba alikuwa mtu muhimu kwenye maisha yao.
“Isn’t that daddy?”AliulizaLanlan mara baada ya kumuona Roma pia.
Edna na Sophia waliangaliana huku wakiwa kama na mshangao kwenye macho yao .
“Mbona inashangaza, ni yeye ndio lakini kwanini ameshindwa kugundua uwepo wetu?’Aliongea Edna akionyesha kuchanganyikiwa, alijua kutokana na Edna na Sophia kuwa na mafunzo ya kijini na Roma kuwa na uwezo wa juu wa kimafunzo basi lazima angehisia uwepo wao , hususani kwa Sophia ambaye alikuwa katika levo ya Nafsi.
“Inaonekana kuna mtu kaja kumpokea”Aliongea Sophia mara baada ya kumuona Roma kazama
ndani ya jengo la wasafiri wa kimataifa wanaowasili.
Edna licha ya kwamba alikuwa na hasira na Roma lakini mara baada ya kumuona akielekea jengo la wasafiri wa kimataifa wanao wasili alijikuta akijawa na shauku ya kutaka kujua Roma anampokea nani na kwanini ashindwe kuwaoana.
Roma hakuwa na habari kama kuna watu waliokuwa wakimfatilia nyuma yake na yote hio ni kutokana na kwamba hakuwa akitumia kabisa uwezo wake wa kijini kutokana na hatari ya kupatwa na uchizi kwasababu ya Cauldron.
Mpango wa Roma ni kumpokea Clark na kumpeleka Hotelini kabla ya kwenda nyumbani na muda ambao alifika hapo ndio alikuwa akitokea Dar.
Ni ndani ya dakika tano tu kupita hatimawe kundi la wazungu ambao walionekana kuwa ni watalii liliweza kuonekana likitoka na haikumchukua muda mrefu kwani Roma aliweza kumuona Clark aliekuwa nyuma peke yake na alimpungia mkono.
“Clark!!!”
Clark aliweza kumuona pia Roma mara baada ya kusikia sauti yake , hakuwa amebeba begi kubwa kama wasafiri wengine.
“Roma..!!”
Aliita Clark huku akiweka tabasamu usoni na kufanya watu kuzidi kumwangalia kwa macho ya matamanio kutokana na urembo wake huku wakiangalia ni mtu gani ambaye amekuja kumpokea huyo mrenbo , lakini dakika chache walijikuta wote wakishikwa na hasira na kutoa matusi mara baada ya kumuona Clark akimkimbilia mwanaume ambaye alikuwa ni wa kawaida mbele ya macho yao tena mweusi.
Clark hakuwa na aibu pengine ni kutokana na uzungu wake kwani mara baada ya kumfikia Roma palepale alijirusha kwenye mikono yake huku akimpa mabusu moto moto.
Roma alishangazwa na mabusu ya kushitukiza ya Clark lakini hakuweza kukwepa kwani Clark mwenyewe hakuwa na wasiwasi na macho ya watu yaliokuwa yakiwaangalia.
Roma alimshika kiuno mrembo Clark na kisha akampiga kibao cha makalioni kwa namna ya uchokozi na muda huo huo walijikuta wakipeana french kiss.
End of season 21

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

SEASON 22

SEHEMU YA 631.
Pengine ingekuwa tukio la kuvutia kwa wenza kubusiana ndani ya airport kama tu Edna , Sophia na Lanlan wasingekuwa wakiwafahamu watu hao.
Lakini kwa bahati mbaya , wenza hao walikuwa wakifanya mambo yao pasipo ya kujua kama kuna watu muhimu wanawaangalia.
Sophia na Edna sasa waliweza kujua uwepo wa Roma ndani ya eneo hilo ni kwa ajili ya kumpokea Clark.
Kama Clark angekuwa makini basi angeweza kumuona Edna na Sophia lakini kutokana na umakini wake kuelekezea kwa Roma basi alishindwa kuwaona lakini kwa wakati mmoja kama usingemjua Clark ungesema anafanya makusudi kwani alienda mbali na kupitisha mikono na kuiloki nyuma ya shingo ya Roma akibembea huku akifurahia busu nyevu.
Ijapokuwa kwa tamaduni za kiafrika kupeana denda hadharani ni jambo la mshangao kidogo lakini katika mazingira kama hayo ambayo wageni wengi walikuwa ni wazungu na wasomi basi halikuwa jambo kubwa sana zaidi ya kuonekana kivutio hususani kwa mrembo kama huyo kubusiana na mwanaume wa kawaida kama Roma, wengi waliwaelewa kwa kuona kwamba siku zote hisia hazivumiliki hususani pale unapommisi umpendae.
Edna palepale alimrudhisha Lanlan nyuma yake ili tu asione kile baba yake anachokifanya.
Uso wake mwanzoni ulikuwa umepauka lakini ulianza kujikunja kwa hasira kiasi cha kumfanya Sophia kuanza kupatwa na hofu.
Wakati huo Sophia alianza kumchukia Roma na kujiuliza kwanini ameshindwa kujua uwepo wao ndani ya hilo eneo , au anafanya yote hayo makusdi kumkomoa Edna na yeye?.
Kwa kile alichokuwa akikikumbika ni kwamba Roma hakupaswa kuwa na mahusiano na Clark hivyo alijiuliza kam yameanza yalianza lini.
Sophia alikuwa na wivu pia wakati huo lakini ulifunikwa na wasiwasi wake aliokuwa nao juu ya Edna , ijapokuwa Sophia hakuwa na ukaribu mkubwa na Clark lakini alijua mrembo huyo alikuwa na sehemu yake pekee katika moyo wa Roma.
Clark alikuwa ni rafiki wa muda mrefu wa Roma kwa zaidi ya muongo mmoja na uzuri wake pamoja na umuhimu katika maisha ya Roma haukupishana sana na Edna.
Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba katika uzuri Edna na Clark wameachana kidogo sana , ukija kwenye mafanikio pia Clark alikuwa amepishana na Edna kidogo hivyo ni sawa na kusema kama Edna ungemchagulia mshindani basi Clark ndio mshindani wake mkubwa , isitoshe pia ni Princess wa Wales cheo ambacho ni cha ziada lakini kinachompa ‘status’ ya hali ya juu.
Mwanamke wa aina hio Edna alimuogopesha mno kuliko hata wale wanawake wengine wa kule Dar es salaam , kwa mfano Neema Luwazo licha ya mafanikio makubwa lakini alikuwa sio mzuri kumshinda Edna na pia alikuwa akikaribia kuuaga ujana.
Wanasema baadhi ya watu wamezaliwa katika kimo cha juu ambacho watu wa kawaida hawawezi kufikia hata wapambane vipi basi ndio kwa Clark.
Kama vile ndio sasa ameridhika kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea palepale alimwambia Sophia waondoke haraka.
Upande wa Edna ni kama alikuwa ndotoni na huku akitamani baada ya kufumbua macho ajue kile alichoona hakina ukweli wowote .
Upepo wa ubaridi wa hali ya juu ulitawanyisha machozi yake kiasi cha kumfanya akili yake kurudi katika uhalisia.
Ilikuwa ni ukatili mkubwa kwa yeye kama mke kuangalia tukio hilo laivu na ilizidi kuuma kwa kuona kwamba haikuwa ndoto.
“Mommy ..”Aliita Lanlan mara baada ya kuhisi kuna kitu hakipo sawa na Edna alimwangalia.
“Who is that aunt daddy ‘s kissing? Is she onother aunty..?”Aliuliza Lanlan akimaanisha kwamba yule shangazi ni ambaye baba yake anamkiss ni nani , je ni shangazi mwingine.
Lanlan alikuwa akiwatia wanawake wa Roma mashanganzi zake , hivyo mara baada ya kuona tukio la baba yake kufanya vile alijua lazima atakuwa ni shangazi mwingine kama Rose , Nasra na wengineo.
“That is not your dad..”(Yule sio baba yako)
“But he …”(Lakini ni..)
“I said he isn’t, Can’t you listen to me”Aliongea Edna akipandisha sauti akimkatisha Lanlan kwa kumfokea.
Lanlan aliishia kunyamaza lakini bado alionekana kushangazwa na maneno ya mama yake kwani asingeweza kutokumfahamu baba yake.
Baada ya kuingia kwenye gari Edna aliendesha kuelekea hoteli ya Iringa Highland bila ya kuongea neno lolote.
Sophia alikuwa na wasiwasi sana akiwa kwenye gari , alijiambia Edna alikua amemuona Roma na Clark na yupo kwenye hali hio vipi akigundua kuhusu yeye.
Alijiambia atamwambia Roma wawe makini kuyafanya mahusiano yao kuwa siri kwa kugopa kumuumiza Edna.
“Sis , pengine Princes Clark alikuwa na shauku kubwa ya kumuona Roma ndio maana, hata hivyo hawezi kukaa kwa muda mrefu hapa
Tanzania”Aliongea Sophia akijairbu kumtuliza
“Huna haja ya kumtetea , nimeona vya kutosha na namjua alivyo , mimi sio kipofu”Aliongea Edna kwa kikauzu.
Sophia aliishia kujikunyata huku akijua kabisa hana kingine cha kuongea kutuliza hali ya Edna.
“Sikia Sophia huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi , cha msingi zingatia kazi yako na ukifanya vizuri itanifurahisha”Aliongea Edna mara baada ya kuona hali ya wasiwasi isiokuwa ya kawaida kwenye uso wa Sophia.
Ukweli ni kwamba hakuwa na wasiwasi juu ya tukio ambalo limetokea , kilichokuwa kikimpa wasiwasi ni kwamba na yeye alikuwa kwenye mahusiano ya kutatanisha pia.
Dakika chache tu waliweza kufika na kuingia ndani ya hoteli na waliweza kumkuta Ummy akiwasubiria na alimpokea Sophia begi lake na kutangulia mbele.
Upande mwingine Roma mara baada ya kusabahiana na Clark alimchukua na kuelekea moja kwa moja mpaka Kigombola Medical Research University, moja wapo ya chuo kilichozinduliwa miaka mitatu iliopita ndani ya jiji la Iringa chini ya uongozi wa Raisi Senga lakini kikapewa jina la raisi msataafu Kigombola kutokana na yeye ndio mwasisi wa ujenzi wake, kilikuwa chuo kikubwa mno ambacho kimejengwa kwa ajili ya mafunzo ya kitafiti katika maswala ya magonjwa yasioambukiza kama vile Saratani , moyo na mengineyo.
Ijapokuwa Clark alikuwa na furaha kumuona Roma lakini bado alijali sana kuhusu afya yake .
Ndani ya gari Roma aliweza kuelezea kuhusu hali yake na maswala ya Chaos Cauldron na Clark aliweza kuelewa vizuri kutokana na kuanza kujifunza mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
Hakuwa na mpango wa kumponyesha Roma bado hivyo alichokuwa akidhamiria ni kumfanyia vipimo vya awali na ndio aanze kufikiria namna ya kumsaidia.
Upande wa Roma matumaini yake yalikuwa chini kutokana na kwamba alijua mafanikio ya teknolojia kuweza kufubaisha nguvu ya Roho ya mnyama huyo ilikuwa ni ngumu kufanikiwa, lakini alitaka kuona kama Clark anaweza kutibu dalili za uvimbe(Benign) kichawni basi angeweza kuwa na uwezo wa kuitawala akili yake kwani uvimbe huo ndio kichocheo cha yeye kupatwa na uchizi.
Baada ya kufika nje ya geti kuingia chuoni hicho walielekezwa na mfanyakazi na kwenda kusimamisha gari chini ya jengo refu kwenda juu ambalo chini yake lilikuwa na kibao cha utawala.
Kilikuwa chuo lakini pia kulikuwa na hospitali ndani yake hivyo eneo lilikuwa limechangamka.
“Clark unapanga kukaa hapa?”Aliuliza Roma.
“Ndio , mkuu wa chuo amenikubalia kutumia vifaa vya maabara nipendavyo , nimezoea kukaa ndani ya maabara kuliko hotelini”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kidogo lakini pia hakuacha kuangalia mandhari ya kuvutia ya chuo hicho na kujiambia Tanzania imepiga hatua kwa kuwa na taasisi hio.
“Na yeye ni mwanafunzi wako?”
“Sio mwanafunzi wangu , ana miaka tisini tayari niliweza kumfahamu kupitia Profesa Shelukindo na alinikubalia moja kwa moja mara baada ya kumwambia nitampatia kanuni ya matibabu ya saratani ya ini bure , nina kanuni nyingi za kimatibabu hivyo sikiuona shida”
“Kwahio kwa kurahisisha ni kwamba kukualika kwangu kumesaidia taifa katika maswala ya kitafiti?”Aliongea Roma akijaribu kumtania.
“Ninaweza kufanya chochote kwa ajili yako kwasabab nishakuwa wako tayari”Aliongea na kumfanya Roma aone siku hizi Clark amezidi kuwa muwazi katika kuongea kimitego.
Baada ya kuingia ndani na kutembea umbali mfupi kukaribia mlango wa kuingia waliweza kupokelewa na daktari mwenye muonekano wa kizee ,Alikuwa ni Profesa maarufu Tanzania aliefahamika kwa jina la
Justice Damiani Mandu , wanafunzi wengi hupendeleea kumwita Profesa Mandu au Dokta Mandu.
Hakuwa peke yake alikuwa na madaktari wengine pamoja na baadhi ya watu wa utawala na mara baada ya kusalimiana nao Clark aliwapa ruhusa wengine kuondoka na kisha aliongozana na Profesa Mandu na walihamia kwenye jengo lingine lililojengwa kwa vioo upande mmoja na ndani ya dakika chache walifika kwenye floor ya nne na Profesa Mandu alitoa maelezo kwa ufupi juu ya eneo hilo la maabara na kisha Profesa Clark mara baada ya kuridhika alitoa karatasi iliokunjwa na kumpatia na kisha wakaagana huku Profesa huyo akionyesha furaha ya waziwazi huku akijiambia anakwenda kustaafu kwa heshima.
Roma aliishia kupumua kwa ahueni na kukumbuka msemo wa kingereza unaokwenda kwa jina la ‘knowledge is power’.
Clark hakutaka kufikiria sana kuhusu vitu vilivyokuwa hapo ndani na palepale aliingia kazini bila ya kuchelewa licha ya kwamba ilikuwa ni usiku sana.
Alionekana kuwa siriasi wakati akianza kukadiria vifaa kwa ajili ya kuanza vipimo.
Roma alisubiria kwa uvumilivu kutokana na kwamba aisngeweza kusaidia chochote na mara baada ya lisaa limoja kupita , Clark alianza vipimo pamoja na kufanya uchambuzi.
Mpaka anakuja kumaliza ilikuwa ishatimu saa tano na inaelekea saa sita za usiku na Clark alimharakisha Roma kuondoka kwenda nyumbani kwasababu alihitaji muda wa kufanyia kazi vipimo vyake.
Roma alimuaga baada ya kumkiss kwenye paji la uso akionyesha kuwa ni mwenye shukrani kubwa kwa kile anachomfanyia na kisha akaondoka .
Wakati Roma anakaribia kufika nyumbani gari la Edna na lenyewe lilikuwa nyuma yake na baada ya kuingia ndani na kusimamisha Edna alishuka na kisha akafungua mlango wa nyuma na kumtoa Lanlan ambaye alionekana kuwa usingizini.
Roma kwa haraka haraka alijua Edna alikuwa ametoka kufanyia kazi maswala ya Sophia kurudi katika usanii lakini alishangaa kuona alikuwa ameenda na Lanlan.
Roma alitoka na yeye haraka haraka kwenye gari yake na kumsogelea Edna huku akionekana kuna kitu alikutwa kiutaka kumwambia.
“Babe wife.. je tunaweza ..”Kabla hata hajamaliza sentesi yake Edna alimpita kama vile hamjui.
Haikuwa mara ya kwanza Edna kufanyiwa hivyo lakini siku zote alikuwa akijua sababu ni nini lakini wakati huo hakujua ni kipi kinaendelea maana walikuwa vizuri tu juzi yake.
“Wife nini tatizo , nimefanya kosa gani awamu hii?”Aliuliza Roma mara baada ya kukimbilia mbele akijaribu kumzuia Edna.
Walinzi waliokuwa zamu waliweza kuhisi kuna kinachoendelea lakini walijifanya hawaoni chochote na kujiweka bize na wanachofanya.
Edna hakujisumbua hata kumwangalia usoni zaidi ya kumpita kwa mara nyingine.
Roma aliishia kukuna kichwa chake akionekana kuchanganyikiwa huku akimfuata nyuma nyuma, baada ya kuona namna ambavyo Edna alikuwa na ukauzu hakujua namna ya kuanza nae mazngumzo. “Edna usiwe hivyo , niambie chochote nitabadilika kama nimefanya kosa , kama huna furaha juu ya jambo niambie na nitajirahidi kukufurahisha , nilikuwa nikiwaza kuwatoa out wewe na Lanlan siku ya kesho”Roma alijitahidi kumbembeleza lakini Edna hakuonyesha nia yoyote ya kutaka kumjibu , baada ya kuingia ndani ya chumba chake palepale alifunga mlango na Roma aliishia kusikia ufunguo ukizungushwa kwa ndani na kumfanya Roma kuishia kushika ukuta huku akikosa cha kufanya.
Ilikuwa tayari ni usiku sana hivyo wanafamilia wote walikuwa wamekwisha kulala muda mrefu na hakuna ambaye alikuwa akijua kinachoendelea.
Roma alijikuta akipigwa na bumbuwazi , huku akijiuliza kwanini ana mikosi , alikuwa tayari amechanganyikiwa kutokana na uwezo wake wa kijini na sasa na mke wake alikuwa akimpa kisogo, lakini licha ya hivyo hakuwa akijua kosa lake ni nini.
Dakika hio hio kabla ya kujua agonge mlango Edna afungue au achukue uamuzi gani simu yake ilitoa ‘notification’ ya ujumbe wa meseji na alivyoangalia ni Sophia aliemtumia.
“Roma , upo huru kuongea sasa hivi?”Roma aliishia kutabasamu kutokana na umakini wa Sophia na palepale alitoka mbele ya mlango wa chumbani kwake na kutafuta eneo tulivu na kumpigia,
“Upo Iringa tayari?”Aliuliza Roma na Sophia aliitikia kwa kuguna.
“Ndio unajiandaa kwa kurudi kwenye mziki ndio maana mpaka sasa hivi hujalala tu?”Aliuliza Roma lakini Sophia hakujibu.
“Roma Sister asharudi tayari?”Aliuliza na Roma macho yake yalichanua na kuamini pengine Sophia alikuwa anajua nini kimetokea.
“Kidogo tu nisahau kukuuliza , nini kimempata , alikuwa na ukauzu kiasi cha kuogopesha , nimefanya kosa gani awamu hii?”
“Ndio nilichokuwa nataka tuongee , alikuja kunipokea Airport na tuliweza kukuona wewe na Clark ..”Aliongea Sophia kwa kusita sita na Roma macho yalimtoka.
“Mliniona mimi na Clark .. unamaanisha anajua mimi na Clark?”Aliuliza Roma huku akikunja ngumi kwa hasira.
“Ndio , alionekana ametulia lakini inaonyesha amekasirika mno , Roma Seriously, kwanini umeshindwa kujua kama tupo nyuma yako?”Aliuliza Sophia huku akionyesha na yeye kukasirika.
Roma alijiambia mwenyewe hata mimi sikutaka mnione , ni kwamba sikuwa na uwezo wa kutumia uwezo wangu, lakini licha ya hivyo hakuwa na ujasiri wa kumuweka wazi Sophia juu ya hilo.
“Sijui nilikuwa nikiwaza nini kiasi cha kushindwa kuwaona ,,, asante lakini kwa kuniambia la sivyo ningepata uchizi wa kutafuta makosa yangu”Aliongea na kumfanya Sophia kupumua kwa nguvu.
“Mimi kwa upande wetu nadhani ni vizuri tukiendelea kufanya siri naogopa anaweza akashindwa kuvumilia , isitoshe yupo Lanlan pia , unapaswa kusubiri kwa muda pia kabla hujamwambia chochote kuhusu Lanlan”
Roma alikuwa na mawazo sawa na ya Sophia lakini bado aliona ni swala la muda tu kwani hisia mara nyingi hazijifichi kwani itafikia mahali Sophia asingeweza kujificha mbele ya Edna.
Roma alijaribu kufikiri njia ya kuweza kumbembeleza Edna lakini hata hivyo aliona ni kheri kusubiri apate nafasi kwani Edna hakutaka hata kumwangalia usoni.
Roma baada ya kuona hana pakulala alitafuta chumba chochote cha wageni ambacho kilikuwa wazi na kisha akajitupia kitandani huku akikosa hata hamu ya kuoga na alijitahidi kuutafuta usingizi lakini alishindwa kabisa.
Ni masaa machache kabla ya kupambazuka , Edna alionekana akitingishika akiwa usingizini huku akiongea.
“Hapana,,, sio mimi,, siwezi ,,, Hubby …ah!!!”
Edna palepale alishituka kwa nguvu na kukaa kitandani huku jasho likimtoka akiwa katika mavazi ya kulalia.
Baada ya kuona yupo ndani ya chumba chake alijikuta akipatwa na ahueni .
Lanlan aliekuwa amelala pembeni yake aliishia kutingishika kidogo huku akiwa kama amesikia Edna akiongea akiwa ndotoni.
Blanketi lilikuwa limefunika tumbo tu huku miguu yote ikiwa wazi , kwasababu ilikuwa ngumu kwake kuugua Edna hakumlazimisha kumfunika.
Lanlan alionekana na yeye kuongea kwa dakika chache maneno yasioelewweka na kisha aliendelea kuuchapa usingizi
Edna aliishia kumshika shika Lanlan nywele zake za Ki’half-cast huku akionekana kuogopa kulala tena kwa kuogopa kuota tena.
Edna alikuwa ameshapoteza hesabu ya mara ngapi aliweza kuota ndoto hio ya aina moja , kwani alikuwa akiota mchana na usiku , mwanzoni alijua pengine alikuwa akiota kwasababu ya kuwa na wasiwasi na Roma mara baada ya kupotea , lakini hata baada ya kurudi alikuwa akiota kitu cha aina moja.
Edna alivuta pumzi nyingi kabla hajaangalia saa na kuona ilikuwa ni saa kumi na moja alfajiri , muda ambao kwa Iringa ilikuwa mapema sana lakini alijiambia muda huo anaweza kuamka na kuendelea na kazi.

SEHEMU YA 632.
Asubuhi wanafamilia wote walikusanyika eneo la nje katika kiambaza kwani kulikuwa na padri aliefika kwa ajili ya kuongoza sala maalumu.
“Edna huyu mtukutu yupo wapi?”Aliuliza Afande Kweka alikuwa akijua kurudi kwa Roma kwani jana yake alimpigia simu.
Edna mara baada ya kuulizwa swali hilo alishindwa hata ajibu nini kwani hakujua hata alilala wapi na asingeweza pia kusema jana alimfukuza kwenye chumba chake.
“Babu si..”Edna alikosa jibu na Blandina palepale aliona kuna tatizo na aliamua kuingilia.
“Ngoja nikamwite”Aliongea Blandina huku akijiandaa kutoka lakini alisimama mara baada ya kusikia sauti kutoka upande wa kulia.
“Nipo hapa”Aliongea Roma huku akiwa na mavazi ya jana lakini lakini utofauti ni kwamba alikuwa amevaa Apron ya upishi akionekana alikuwa jikoni.
“Roma kwanini..”
“Hahaha… niliamka mapema niliamua leo kuhusika na maandalizi ya kifungua kinywa”Aliongea Roma na kumfanya Afande Kweka misuli yake ya uso kukaza kidogo.
“Huyu ni father Selestin kutoka parokiani na leo amefika hapa kwa ajili ya maombezi maalumu na sisi wanafamilia wote”Aliongea Afande Kweka.
“Ah…unamaannisha yupo kwa ajili ya kutuombea kwa Bodhidhativa?”
“Acha upuuzi na maswala yako ya Bozitavazi ni kwa ajili ya kutuombea kwa Mungu”Aliongea Afande Kweka , hakumlaumu Roma kutoongea maneno yake ya kipuuzi maana alijua pengine hata kanisa halijui.
Aliishia kumtambulisha Roma kwa Father Selestin na kisha maombezi yalianza kwa muda mfupi na kisha aliaga huku akikataa kubakia kwa ajili ya kifungua kinywa na kusema yupo kwenye maombi.
Asubuhi hio wanafamilia wakiwa mezani Roma alijitahidi kuongea na Edna kwa kumpatia chakula maalumu alichomwandalia lakini majibu yalikuwa yale ya kimikato mikato na hakugusa chakula alichopewa na kufanya wanafamilia hao kuona kuna kitu hakipo sawa kati yao.
“Edna mmegombana , kwanini hamuongeleshani?”Blandina alijikuta akikosa uvumilivu mara baada ya kuona vituko vinavyoendelea kati ya Roma na Edna
“Hatujagombana..”Aliongea Edna huku akiwa ni mwenye kulazimisha tabasamu.
“Vijana wa siku hizi mna’complicate’ mambo sana , hamjui namna ya kuvumiliana , mkikoseana wekeni wazi na ongeeni myamalize na ndio namna pekee ya kujirekebisha na kusonga mbele , nyie mna bahati sana mpo pamoja katika umri mdogo , mkishazeeka mnaweza msiweze kuonana tena na kujutia nafasi ambazo mlipaswa kumaliza sintofahamu zenu na kuishi kwa furaha”Aliongea Afande Kweka ambaye licha ya uzee wake alijua kuna vita ya baridi iliokuwa ikiendelea kati ya Roma na Edna.
Kila mmoja alikuwa kimya juu ya maongezi yake , ilikuwa ni kama vile anamkumbuka mke wake marehemu.
“Edna mimi siwezi kusimama upande wowote kati yenu , Roma anaweza kuwa kichwa kigumu lakini sio mjinga , anajitahidi kukubembeleza ili uweze kumsikiliza na kumsamehe , hivyo leo wote kwa pamoja ondokoni na binti yenu mkatembee , Roma mchukue mkeo na mpeleke duka lolote na mnunulie anachotaka ,Edna usisahau kununua na nguo pia kwa ajili ya kesho kwenda kutembelea ndugu, mpe nafasi mumeo ya kurekebisha makosa yake , na wewe Roma jitahidi kumfanya mkeo kuwa ni mwenye furaha ili kuyaziba madhaifu yako , Edna nataka ukirudi leo nikuone unatabasamu sawa?”Aliongea Afande Kweka na Edna alijisikia vizuri na kuitikia kwa kichwa.
Upande wa Roma alimshukuru mzee huyo kumpigia pasi maana ni kweli kama asingekuwa akijutia makosa yake asingeamka asubuhi asubuhi na kuwaambia wafanyakazi wamuachie yeye jiko kwani anataka kumpikia mke wake.
Upande wa Blandina alimwangalia mzee huyo na kuona huenda anafanya yote hayo kutokana na kumuonea huruma Roma kutokana na juhudi alizoweka.
Lakini hakuacha kuwaza na kusema pengine Edna ndio mwenye makosa na Edna anambebesha Roma mzigo wote , aliwaza hivyo maana aliona ni kama Edna anamtawala mtoto wake.
Upande mwingine kwenye mitandao habari za Sophia kurudi kwenye kazi zake za kisanii zilikuwa zikienea kwa kasi sana huku show yake ilioandaliwa kufanyika Iringa ikivuma huku kubwa zaidi ni uhusikaji wa wasanii wengine wakubwa ambao wangemsindikiza .
Zote hizo zilikuwa ni juhudi za Edna kutaka kumfanya Sophia kufanya kitu anachokipenda lakini kwa wakati huo akiifanya kampuni yake ya habari na burudani kufanya vizuri
Mpango ulikuwa ni kumtambulisha amerudi na hapo ndipo angeweza kupewa ofa ya kuigiza katika muvi ambayo kampuni ya Vexto Production walikuwa wakipanga kuidhalisha.
*****
Ilikuwa ni asubuhi ya siku ya jumamosi katiak jengo la wizara ya elimu iliingia gari kali aina ya Mercedenz Benz E Class Amg 53 , siku hio ndani ya jengo hilo hakukuwa na watu wengi pengine ni kutokana na kwamba ilikuwa ni wikiendi.
Baada ya gari ile kuegeshwa katika eneo husika aliweza kutoka Najma ambaye asubuhi hio ni kama vile uzuri wake umeongezeka mara mbili zaidi ya jana yake , pengine ni kutokana na kutembelea gari nzuri ndio maana ilimfanya kupendeza.
Siku hio hakuwa amevalia Shungi na kufanya kuzidi kupendeza na mtindo wake wa nywele wa twende kilioni, ni aina ya msuko wa kawaida lakini uliendana sana na muonekano wake.
Roma alikuwa ni mwepesi sana , jana mara baada ya kwenda kukagua gari na kuridhika nayo palepale alitoa zaidi ya milioni miambili kwenye akaunti yake na kuziingiza kwenye akaunti ya Fredi na kukamilisha malipo na baada ya hapo alimwambia Fredi kuagiza mtu kulipeleka nyumbani kwa Najma baada ya usajili kukamilika huku yeye akiondoka nae.
Upande wa Najma hakuwa na tabia za majigambo na wala hakuona ni jambo kubwa sana kuendesha gari ya bei ghali lakini hakuweza kujizuia kutaka kuonyesha kwa watu ni gari gani ambayo mpenzi wake amemnunulia.
Dakika ileile wakati akifungua mlango wa kushoto wa abiria akitoa begi la laptop yake ya mapakato ili afunge mlango kuelekea juu , gari aina ya Lamborgin iliingia eneo la maegesho na kwenda kusimama kando yake.
Baada ya gari ile kusimama kioo cha mbele kilishushwa na Naibu waziri Salihi alionekana na alishangaa mara baada ya kuona gari hio mpya ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Najma na aliishia kulazimisha tabasamu.
“Najma hii ni gari yao?”Aliuliza.
“Ndio Mheshimiwa Naibu waziri , asante kwa kunipa
lift kwa kipindi chote nadhani kwanzia sasa sitokusumbua tena”Aliongea Najma huku akiweka tabasamu ambalo lilizidi kumnyong’onyesha waziri. “Roma ndio kakununulia?”
“Ndio”
“Je unajua kwamba ameoa na mke wake ni mmiliki wa kampuni ya Vexto?”Aliuliza na kumfanya Najma kushangazwa na hilo.
“Nadhani hilo ni swala ambalo halikuhusu mheshimiwa , ni ukorofi kwa wewe kuanza kufatilia maisha ya wengine , ninaondoka kama huna kingine cha kuongea”
“Simama hapo hapo”Aliongea kwa namna ya kufoka huku akitoka nje ya gari.
“Ni kipi kizuri umekiona kwake , nimekuwa nikikubembeleza kwa muda mrefu kwa moyo wangu mkunjufu lakini umeshindwa hata kunipatia nafasi , yule ameoa tayari lakini bado tu unamng’ang’nia , ni upande upi ni mzuri sana kuliko mimi?”Aliongea kwa sauti na kumfanya Najma kuwa na wasiwasi kwani alikuwa akiona hasira yake.
“Sitaki kumlinganisha mpenzi wangu na mwanaume mwingine , mapenzi sio sawa na kununua kitu kwamba utachagua kwa muonekano wa vipimo maalumu, Mheshimiwa mimi nakuheshimu sana lakini naomba pia uyaheshimu maisha yangu binafsi hususani ukiwa hujui chochote kuhusu mimi”Aliongea kijeuri na wakati huo huo wakati Naibu waziri akijiandaa kuanza kuongea tena gari nyeusi aina ya Bentley iliweza kuingia na kwenda kusimama kando ya gari ya Salihi.
Wakati Salihi akikunja sura kutokana na ujio wa gari hio upande wa Najma alishangazwa kwani ilikuwa ni gari ya muonekano wa kifahari.
Dakika hio hio mwanamke mtu mzima mwenye muonekano wa kujipenda aliweza kutoka nje ya gari.
Alikuwa amevalia mavazi ya kuvutia mno , ijapokuwa sura yake ilionekana kuwa haijajikunja lakini kwa haraka haraka kwa mtu mwenye uzoefu angeweza kugundua mwanamke huyo ametumia ‘Botox injection’ kwa ajili ya kuzuia makunyanzi.
“My dear son , thank goodness you’re still here , the traffic was pretty bad and I thought I’ ll miss you”Aliongea yule mwanamke na kumfanya Najma kushangaa na kujiuliza inawezekanaje mwanamke huyo akawa mama kwa mheshimiwa ilihali muonekano wake ni kama vile ana miaka arobaini. “Unafanya nini hapa?”Aliuliza Salihi kwa kingereza.
“Nilitaka kuwa na muda mzuri na wewe , hatujaonana muda mrefu na nimekuja nchini lakini umekuwa ni wa kuniepuka”
“Hapana , nenda nyumbani nitakuja huko huko nina maswala ya kushughulikia sasa hivi”Aliongea na kumfanya yule mwanamke kumwangalia Najma kwa macho ya dharau.
“Oh , you found yourself a b*tch, what is wrong ? It sees like you two were quarrelling , she doesn’t like you”
“Oh nakuona umejipatia Ma**ya , tatizo ni nini , mlionekana mlikuwa mkigombana , hakupendi?”
“Asha jaribu kukaa kimya , ingia kwenye gari yako uondoke na uache kuongea ujinga”
“Mimi ni mama yako , kwanini nipotezee matatizo yako? Najua jina lake anaitwa Najma Waziri, najua hata mahali anapoishi”Aliongea kwa majigambo.
Najma alijisikia vibaya kwani macho ya huyo mwanamke yalikuwa ni ya kijeuri mno. “Ulikuwa ukimfuatilia , wewe Asha umechoka kuishi maisha mazuri?”
“Unapenda kunifokea kwasababu tu nashindwa kukupotezea, wewe ni mkatili sana , hakupendi lakini bado tu unanikatli , fanya utakavyo lakini jua mimi ni mama mzuri kwako , babu yako na wajomba watafika kwa ajili ya chakula cha usiku leo hii hakikisha unakuwepo , ole wako uache huyu Ma..ya akucheleweshe”
Baada ya kumsonya Najma alirudi kwenye gari yake na kisha liligeuzwa kijeuri na kutolewa ndani ya hilo eneo.
Upande wa Salihi alionyesha kuna kitu hakipo sawa na alimwangalia Najma kwa macho makali kwa muda mfupi na kisha na yeye aligeuza gari yake na kuondoka.
“Edna nimekuonya kuhusu mumeo lakini ukanipotezea na ukaaenda mbali na kumruhusu amnunulie gari mpenzi wake …,, , Roma kwahio unajaribu kunidhalilisha kwa kumnunulia mpenzi wako gari kwa kutumia hela za mke wako , ni ujinga wa namna gani huu , hebu ngoja tutaona ni karata gani nyingine unaweza kucheza , unathubutu vipi kuniibia mwanamke wangu?”Aliongea kwa hasira huku aking’ata meno
Roma na harakati zake nini kitajili? Vipi kuhusu ndoto za Edna ,Usikose.
ITAENDELEA.

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI : SINGANOJR
WATSAPP : 0687151346.

Mono no aware.

SEHEMU YA 634.
Salihi wakati akiwa kwenye gari lake akiendesha kwa pupa kusonga mbele alijikuta akipata wazo na kutoa simu yake haraka haraka na kutafuta namba flani alioisave kwa jina la Uncle na kuipiga.
“Hahaha ...Mheshimiwa Naibu kwanini unapiga tena kuna tatizo, nimealikwa leo kwa ajili ya kufika nyumbani kwenu kwa ajili ya chakula cha usiku” Sauti upande wa pili ilisikika .
“Mjomba haina haja ya kuongea kwa matani na kujishusha, wewe ni mkubwa kwangu na sijakupatia heshima yako inavyostahili tokea nirudi nchini” “Kwanini unaongea kwa upole hivyo?, Au kuna kitu unataka kuniomba, pengine kama ni swala la kukupigia debe kwa baba yako hilo niachie mimi”Aliongea na kumfanya bwana Salihi kutoa tabasabu la uovu.
“Mjomba najua wewe ni Mkurugenzi msaidizi , kwanini nikuhangaishe na maswala yangu madogo kwa kwenda kumtaarifu baba”
“Kama ni hivyo basi niambie tatizo lako nikusaidie mwenyewe”
“Mjomba shida yangu ni kwamba nimejikuta nakuwa na kinyongo na Edna Adebayo bosi wa kamouni ya Vexto , najua moja ya kampuni yake tanzu inajihusisha na maswala ya udhalishaji wa kemikali, unaonaje ukinisaidia kwa kumtengenezea tatizo katika kiwanda chake ili tu kuharibu maswala ya kiudhalishaji”Aliongea na kufanya upande wa pili kusikia mguno na ukimya wa sekunde kadhaa.
“Hapana Bwana mdogo , sio kama sitaki kukusaidia lakini mtu unaemzungumzia hapo ni Edna , ingekuwa kampuni nyingine tofauti na ya Kanani, Vexto na Maple ningekusaidia, Edna sio mfanyabiashara wa kawaida , Nguvu ambayo ipo nyuma yake sio ya kawaida kabisa hivyo ni ngumu sana kugusa kampuni yake , kwanini una kimyongo nae., mbona haupo makini mjomba??”Aliongea mwanaume alieitwa Mjomba akiwa siriasi.
Salihi alijikuta akishikwa na mshangao kwani mjomba wake huyo hakuwahi kuogopa mtu na siku zote ni mtu wa kutii kila analomwambia kwa kuogopa anaweza kumuongelea vibaya mbele ya baba yake.
“Kwanini Mjomba , Si Edna ni mfanyabiashara mwenye akili tu ambaye amezoea kuonea kampuni za chini yake , sidhani kama kuna haja ya kuogopa kwani ninachokijua hata ndugu zake karibia wote wamefariki”
“Upo sahihi Edna anaweza kuwa mfanyabiashara wa kawaida mwenye akili na familia yake kufariki lakini hebu jiulize mwenyewe ni kwa muda.mrefu kampuni yake imekuwa ikifanya vizuri bila hata ya kupatwa na changamoto ambazo kampuni nyimgine hapa nchini zinapitia , Kampuni yakr haigusiki sio kwasababu yake tu bali ukweli ni kwamba mume wake Roma Ramoni ni mwanafamilia wa ukoo wa Kweka ambae inasemekana anatarajia kufanywa mrithi,huwezi kujua haya maana umekaa sana nje ya nchi na network yako ya taarifa ni ndogo , umefanya vizuri kuanza kuawasiliana na mimi”
“Nini!!, unasema mwanafamilia wa ukoo wa Kweka,
Kwahio unamaana ya kwamba Roma ndio mtoto wa Raisi Senga kama inavyosemwa??”
“Upo sahihi nadhani licha ya kuishi kwako nje ya nchi una fununu ya nguvu ya familia hio kwa sasa”
Salihi alijikuta akipigwa na mshangao wa aina yake na alilaani kukaa kwake nje ya nchi kumemfanya kutojua mambo mengi yanayoendelea nchini , pengine ni kutokana na tabia yake ya kutopendelea kufatilia maswala ya siasa.
Hata kurudi kwake nchini alilazimishwa na familia yake kuingia katika ulingo wa siasa, lakini ukweli ni kwamba sio aina ya maisha alioyataka .
Alikuwa na uelewa mchache juu ya familia ambazo zinanguvu kubwa nchini , familia ya Mzee Atanasi ambayo ndio imemtoa Tajiri Azizi , familia ya Kweka ambayo ndio.imeshikilia jeshi na familia ya kigombolana ndio inakuja familia yao ambayo imelishikilia taifa kiroho(Hapa utaelewa baade kidogo)..
Sasa Salihi alikuwa amekwisha kuzisikia habari za wanajeshi kushambuliwa mkoani Iringa , ijapokuwa taarifa hio ilikuwa ni ya siri lakini kwa nafasi yake ya kiungozi aliweza kuzipata lakini sasa hakujua kama mtu ambaye amehusika ndio Roma Ramoni.
“Bwana mdogo , nadhani tufanye kama hujazungumzia kabisa hili swala , hatuwezi kunufaika nalo , sio kwangu tu pengine hata ukoo wetu wote hauwezi kushindana na yule shetani”
“Mjomba huu ni ujinga ,kwanini tumuogope Roma na ukoo wake , hawamiliki hii nchi na hata kama watataka kutushambulia chama hakiwezi kuruhusu kwani ni swala ambalo linaweza kuibua mpasuko wa kitaifa , usisahau baba pia ndio alifanya juhudi kubwa ya kutoa ufadhili kwa ajili ya kumfadhili raisi Senga”
“Hehe ,, upo sahihi kabisa haiwezi ikatokea familia yetu kushambuliwa kirahisi , isitoshe na sisi pia tuna mizizi ndani ya taifa hili ambayo haionekani kwa macho”Aliongea mjomba wake Salihi.
“Sema mjomba ni bora nimejua hili mapema, la sivyo ningejiingiza kwenye matatizo, naomba usimwambie chochote baba maana hakawii kukasirika”
Waziri Salihi mara baada ya kujua kwa udani kuhusu ukoo wa Roma alona haikuwa na haja kwenda mbali
zaidi kwa ajili tu ya kujiridhisha na hasira yake ili hali athari zinaweza kuwa kubwa.
Aliwaza pengine atafute nafasi ya kuweza kumbembeleza Najma ili apotezee ugomvi wao uliotokea, Waziri Salihi alijiambia ni kheri aendelee kuwa rafiki wa kawaida wa Najma kuliko kuwa na adui aliejificha.
“It is better to be a cautious crow than fearless one, for the cautious crow lives a long life” Aliwaza akijiambiani kherikuwa kunguru muoga kwani anaishi miaka mingi.
******
Kama Edna na Roma walivyoambiwa na Afande Kweka kutoka pamoja na Lanlan kwenda kutembea ndio kilichotokea.
Ijapokuwa Edna alikuwa na hasira na Roma lakini hakutaka kabisa kupotezea uwepo wake , akiwa kanuna hivyo hivyo aliamua kuondoka nae , hakutaka pia kuonekana kama mwanamke kiburi asietii wakubwa na mume wake, isitoshe alikuwa kwenye mazingira ya ukweni hivyo ilimaanisha asingeweza kufanya kila anachotaka.
Ikiwa ni muda wa jioni ya saa kumi na mbili na nusu wakati Edna na Roma bado hawajarudi nyumban, alifika mgeni ambaye alimshangaza kidogo Afande Kweka kwani ni kwa kipindi kirefu sana hajawahi kuonana nae.
Babu yake Sophia, yaani Jenerali mstaafu wa jeshi aliepokea kijiti kutoka kwa Afande Kweka , mara baada ya kumtelekeza Mariaum bibi yake Edna akiwa mjamzito alioana na mwanamke aliefahamika kwa jina la Sumaiya ambaye alikuwa ni mwanajeshi mwenzake katika kitengo cha wachawi.
Ni sahihi kusema Afande Athumani kipindi hicho akiwa chini ya uongozi wa Afande Cammilius Kweka kama mkuu wa jeshi ndio aliekuwa Kanali akisimamia kitengo kipya kilichoundwa jeshini maalumu kwa ajili ya kupambana na nguvu za giza, yaani kikosi cha wachawi.
Kipindi hicho wakati kikosi hiko kinaanzishwa hakukuwa na mwanajeshi yoyote ambaye alikuwa na mafunzo ya kichawi , hivyo ni kama lilikuwa ni wazo ambalo lilianza kutekelezwa na jeshi na msimamizi mkuu alikuwa ni Kanali Afande Athumani.
Wakati kitengo hichi kinaanizishwa tayari Kanali
Athumani ashafunga ndoa na mwanajeshi mwenzake aliefahamika kwa jina la Kapteni Sumaiya Mbale, au Kapteni Mbale kama alivyofahamika sana , mwanajeshi machachali sana jeshini ambaye pia alikuwa mtoto wa kigogo wa kiserikali wakati huo.
Kati ya wanajeshi waliochaguliwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya mafunzo ni Kapteni Mbale mke wa Afande Athumani ambaye alijitolea mwenyewe
,ilikuwa ni wakati ambao tayari ashamzaa
Ramadhani ambaye alikuwa ndio mtoto wa pili kwa Afande Athumani ukiachana na Adebayo ambaye alikuwa ni mtoto wa nje ya ndoa aliezaliwa na Marium.
Inasemekana mara baada ya Kapteni Mbale kurudi mafunzoni alimkuta Afande Athumani alishaoa mke wa pili afahamikae kwa jina la Fatuma ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari na habari hio mara baada ya kumfikia, Kapteni Mbale ambaye alipandishwa cheo na kuwa Meja mara baada ya kurudi nchini alikasirika sana na kuitaka talaka mara moja na mgogoro ulikuwa mkubwa mno kiasi cha kupelekea Afande Athumani kumpa talaka yake licha ya kwamba alichokifanya sio kosa kwani ilikuwa ni sheria ya dini yake ya kiislamu kumruhusu kuoa wake zaidi ya wawili lakini kwa Afande Sumaiya Mbale hakusikia la mwadhini.
Miaka kadhaa baada ya Afande Athumani kupandishwa cheo na kuwa mkuu wa majeshi upande wa Sumaiya alikuwa ashajiunga na kikosi cha usalama wa taifa na kupewa misheni maalumu akiwa undercover katika kivuli cha ubalozi nchini China.
Na kwanzia hapo maisha ya Sumaiya mara nyingi yalikuwa nje ya nchi , alikuwa jasusi mbobezi ambaye alihamishwa kwenda nchi mbalimbali kijasusi mara baada ya kukaa China kwa muda mrefu na ilisemekana rafiki yake mkubwa alikuwa ni Abbess Yumiao Master wa dhehebu la Shushan ambaye alikutana nae wakati wa mafunzo ya kichawi katika dhehebu hilo.
Sifa kubwa ya Sumaiya ni hasira za haraka na kutojali , inasemekana ni aina ya tabia alioweza kuipata mara baada ya mume wake kuoa mke wa pili, wazungu wanaweza kuita tabia ya Sumaiya kama ‘Bad temper’.
Lakini licha ya hivyo alikuwa akimpenda mtoto wake Athumani sana na pia vilevile alikuwa akimpenda mjukuu wake Sophia kwa viwango na ndio aliempa presha AbessYumiao kukaa macho katika Dehebu la Shushani ili tu kumpata Sophia mara baada ya kupotea kwake.
Sasa jambo moja unalotaka kuelewa ni kwamba kitendo cha Ramadhani baba yake Sophia kulazimisha Sophia kuolewa na Roma nyuma yake alikuwepo huyo Sumaiya bibi yake Sophia, jasusi mbobezi ambaye ana historia yake kwa mchango alioweza kufanya katika upande wa usalama wa taifa.
Maisha ya Sumaiya kwa miaka yake yote ni nchini Marekani na mara baada ya kustaafu kwa hiari yake alihusishwa kuwa jasusi chini ya kikosi cha Dhoruba nyekundu japo habari hizo hazikuwahi kuthibitishwa na yeye mwenyewe alipinga vikali kuhusishwa na shutuma hizo miaka ya nyuma , lakini kutokana na sintofahamu serikali ya Tanzania iliacha kabisa kumuhusisha na maswala ya kiserikali na kwanzia hapo alionekana mara chache sana nchini Tanzania.
Afande Kweka alikuwa akimuheshimu sana Sumaiya kutokana na ujasusi wake, mwenyewe alikuwa akijiita jasusi lakini kwa Sumaiya alikuwa pia ni Konkodi lakini hata hivyo bado hakuwa akimzidi hata kidogo.
“Bi Sumaiya ni siku nyingi hatujaonana, je upo hapa Iringa kwa ajili ya Sophia?”Aliuliza Afande Kweka mara baada ya kusalimiana na mgeni.
“Unaweza sema hivyo Mr Cammillius , lakini nipo pia hapa kwako kwa ajili ya Sophia”Aliongea na kumfanya Blandina kushindwa kuelewa anataka kumaanisha nini.
“Madam kuna shida yoyote kuhusu Sophia?”Aliuliza Blandina alikuwa akimjua vizuri.
“Mjukuu wangu Sophia na Roma ni wapenzi na hiki ndio ambacho kimenileta”Aliongea na kumfanya Blandina kushika mdomo huku Afande Kweka misuli yake ya uso ilicheza.
Wote walijua hio sio taarifa nzuri kwani kama Edna ataijua basi matatizo makubwa yanaweza yakajitokeza , isitoshe muda huo walikuwa wameenda kutembea kwa ajili ya kumaliza hali ya kimigogoto ambayo ilikuwa ikiendelea kati yao.
“Inaonekana hamna taarifa juu ya hilo , lakini Sophia mara aada ya kurudi kutoka huko alikopotea aliweza kusema kila kitu , mimi licha ya kwamba sijaishi muda mrefu na Sophia lakini namjua vizuri na hata mwanangu Ramadhani anamjua Sophia vizuri , ni msichana mwenye aibu sana na sio jambo rahisi kuziweka hisia zake wazi , labda niwaeleze tu Sophia kuacha kwake usanii ilikuwa ni kutokana na hisia zake za kimapenzi juu ya Roma, ninachomaanisha ni kwamba Sophia yupo siriasi kuhusu uhusiano wake na kwasababu tunajua tabia ya Sophia ni ya upole basi nimeamua kuingilia hili kati”Aliongea kwa kujiamini tena kwa sauti kubwa, alionekana ni wale wanawake ambao hawana upole ndani yao.
“Nadhani ukiachana na hilo kuna lingine pia unataka kutoka kwetu si ndio, maana sidhani kama kuna haja ya kuingilia mahusiano yao kama ndio wameamua?”Aliongea Afande Kweka.
“Upo sahihi ukiachana na mahusiano yao pia nina sababu nyingi”
“Unaweza kutuelezea tukusikie”Aliongea Afande Kweka huku akinywa kidogo kahawa yake, ijapokuwa taarifa hio ni mbaya lakini alionyesha utulivu.
“Mwanzoni nilitaka Sophia kuwa mke wa pili kwa Roma , lakini hilo kwa sasa nadhani haliwezekani hivyo nimekuja na ombi lingine”Alipozi na kisha akaendelea.
“Kwa ninavyojua ni kwamba Roma hana uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito mpaka afikie mwishoni mwa levo ya nafsi kwenye mafunzo ya kijini, sidhani kama mnalijua hilo?”
“Upo sahihi”Alijibu Blandina.
“Basi nadhani pia mnapaswa kuelewa kwamba
Sophia mpaka sasa amekwisha kufikia katika levo ya
Nafsi hivyo uwezekano wa yeye kupata ujauzito wa Roma ni mkubwa na kama itatokea, tunataka mtoto wa Sophia kuwa chini ya ukoo wetu”Aliongea na kumfanya Blandina kushangaa lakini upande wa Afande Kweka hakuonyesha mshangao ni kama alitarajia hilo.
Afande Kweka alikuwa akijua uzao wa Roma sio wa kawaida, pengine ni sawa na kusema ni mwanzo wa kizazi kipya katika uso wa dunia.
Mwanzoni alipoambiwa maneno hayo na Paster Cohen hakuwa akiamini lakini mara baada ya kurudi kwa Lanlan ndio aliweza kujua maana ya maneno yake.
“Uzao wa Roma ni mwanzo wa kizazi kipya chenye uwezekano wa kuwa na thamani kubwa au cha hatari kwa dunia”Kauli hio ilitoka kwa Paster Cohen siku moja mara baada ya kumuona Lanlan.
Ukweli ni kwamba siku ambayo Paster Cohen alifika nyumbani kwa Afande Kweka malengo yake makuu ni kuweza kumuona Lanlan na kuthibitisha matarajio yake na mara baada ya kumuona ndio sasa aliweza kuyaelewa maelezo ya Hades wa Zamani ambaye alimwambia kauli sawa na aliomwambia Afande Kweka ya kizazi cha Roma kinaweza kuwa cha hatari au chenye uthamani mkubwa kwa dunia.
Pastor Cohen ndio watu waliokuwa wakijua kama mpango LADO ungeweza kufanikiwa basi moja kwa moja ndio mwanzo wa kizazi kipya na katika maisha yake alitamani kuona kizazi chenyewe kabla ya siku zake hapa duniani kufika mwisho na mara baada ya kumuona Lanlan ndio sasa aliweza kuridhika.
Upande wa Afande Kweka tokea mwanzo alijua haikuwa bahati mbaya kwa familia ya Athumani kumtaka Sophia kuwa na mahusiano na Roma alijua tu Sumaiya alikuwa akivuta kamba kwa siri akimtangulizia mtoto wake mbele.
Roma anaweza kuja kuwa na watoto wengi zaidi ya ilivyotarajiwa lakini kumfanya mtoto mmoja kutokuwa sehemu ya ukoo ilikuwa ni stori nyingine kabisa.
Afande Kweka alionekana kuwaza kwa muda na kisha akafumba macho yake na kuyafumbua.
“Ninaweza kuelewa nia yako na pia ninaweza kuruhusu hili ila lazima kuwe na masharti” “Nipo tayari kuyasikiliza”
“Kama mtoto huyo atakuwa nje ya ukoo wetu inamaanisha kwamba jina lake la ukoo haliwezi kuwa la Kweka hivyo moja kwa moja atakuwa na jina la ukoo kutoka familia yenu na pia hawezi kupata urithi wowote kutoka kwetu , familia yenu itahusika na elimu yake pia jamboa ambalo linamaanisha hata mbinu ya kipekee ya Roma ya mafunzo ya kijini hawezi kupata”Aliongea Afande Kweka na alimfanya Bi Sumaiya kuonyesha kutoridhishwa na jambo hilo.
“Afande nakuelewa unachomaanisha lakini ninachojua ni kwamba mbinu hio asili yake ni kutoka taifa la China katika dhehebu la Tang hivyo moja kwa moja ni kwamba haiwezi kuwa ya familia yako kama urithi”
“Upo sahihi lakini ni raia kutoka taifa la Tanzania ambaye ameweza kujifunza hii mbinu na ikaonyesha mafanikio , hivyo ni sawa na kusema ni Roma pekee ambaye anaijua , hivyo moja kwa moja itaendelea kubakia chini ya ukoo wetu”
“Lakini huyu mtoto atakaezaliwa atakuwa ni mtoto wa Roma pia?”
“Upo sahihi atakuwa ni damu ya Roma na hio ni faida kubwa kwenu kwani atakuwa ni mtoto wa tofauti , nadhani hicho ndio unacholenga hivyo kuhusu mbinu ya kijini hatoweza kuipata”Aliongea Afande Kweka akiwa siriasi na kumfanya Bi Sumaiya sura yake kujikunja.
“Hilo haliwezekani”Aliongea.
“Madam huwezi kulazimisha huo ndio msimamo wa kifamilia”Aliongea Blandina na kumfanya Afande Kweka kupata ahueni maana hakutaka kujibishana na mwanamke huyo ilihali msimamo wake upo wazi.
Dakika hio hio akiwa hajui aendeleze vipi maongezi hayo akipandwa na hasira kama kawaida yake aliweza kupata ahueni mara baada ya kuweza kuhisi ujio wa Roma, alikuwa na nguvu za kijini pia katika levo ya Nafsi pengine ndio maana hakuonekana kuzeeka sana.
“Vizuri Roma amerudi mwenyewe nitaongea nae yeye nione kama anakubaliana na hili au lah, hakuna mtu mwingine anaepaswa kuingilia kama akikubali”Aliongea na ilikuwa ni kama alivyoongea kwani Roma palepale aliweza kutokea akiwa ameshikilia mifuko mkononi.
Alikuwa ametangulizana na Edna ambaye alionekana amechangamka kwani walikuwa wakiongea na Roma muda huo wakati wakiingia ndani ya nyumba hio huku akiwa amemshikilia Lanlan mkono na uso wake ulipambwa na tabasamu na lilipotea mara baada ya kumuona bibi yake Sophia.
Wataalamu wa mahusiano wannasema mbinu pekee ya kuweza kumpa mwanamke furaha pale unapomkosea ni kumpeleka Shopping anunue kila kitu kinachomfurahisha na mwanamme kulipia na hilo lilionekana kufanya kazi kwa Edna.
Edna alikuwa akimjua bibi yake Sophia nje ndani na alishawahi kukutana nae na sifa zake pia alishawahi kuzisikia kutoka kwa bibi yake na karibia zote hazikuwahi kuwa taarifa nzuri ,pengine bibi yake alikuwa ‘biased’ kutokana na kwamba ndio mwanamke aliemchukulia mwanaume anaempenda huku yeye akitelekezwa.
Ukweli ni kwamba Edna alikuwa akijua fika kwamba bibi yake Sophia hakuwa akimpenda.
Kila mtu aliekuwa hapo ndani alionekana kupatwa na ahueni mara baada ya kuona Roma na Edna wamepatana lakini uwepo wa bibi yake Sophia walijua kabisa utageuza hali ya hewa muda wowote.
Roma mara baada ya kumuona huyo mwanamke mapigo yake ya moyo yalidunda , alikuwa akimjua ni bibi yake Sophia licha ya kwamba hajawahi kuonana nae na habari zake alikuwa akizisikia juu juu.
Sophia alishawahi kumuonyesha picha yake na hata
Edna pia alikuwa akimjua na alishawahi kumdokezea , ukiachana na wasiwasi wake juu ya uwepo wake hapo nyumbani lakini alishangazwa na namna ambavyo alionekana kuwa kijana licha ya kuwa na umri wa miaka mingi na alijua pengine alikuwa na mafunzo ya kijini.
“Mr Roma nadhani sina haja ya kujitambulisha kwani Sophia amesema unanifahamu , mimi ndio bibi yake na nitaenda moja kwa moja katika swala ambalo limenileta hapa kuhusu Sophia”
“Bibi nakujua ndio lakini hatujawahi kuonana , nadhani tunapaswa kusalimiana vizuri kabla hatujafanya maongezi”Aliongea Roma huku akiweka ile mifuko ya nguo chini sakafuni akitaka kusalimiana nae.
“Tutafahamina rasmi kama utajibu maswali yangu kwanza ,Je utawajibika moja kwa moja kwa watoto wako na Sophia?”Aliuliza mwanamke huyo huku akimpotezea Edna kama hajamuona vile.
Swali hilo lilikuwa kama bomu na halikumpiga yeye tu lakini pia lilimgusa Edna aliekuwa nyuma ya Roma.
Roma alimwangalia mwanamke huyo katika muonekano usiokuwa wa kawaida wa huzuni lakini pia muoneknao wenye maswali na kujiuliza imekuwaje huyo mwanamke akajua uhusiano wake na Sophia.
Roma hakuwa akijua kwamba Abbess na Bibi yake Sophia walikuwa marafiki na ndio maana Sophia alienda kuchukulia mafunzo katika Dhehebu la Shushani , pengine ni uzembe wake kutouliza au ni kosa la Sophia kutokumweleza.
Moyo wake ulitetemeka mara baada ya kumpiga macho Edna aliekuwa nyuma yake na kujiambia ni balaa gani hii inakwenda kumtokea tena.
“Nini tatizo? Ulikuwa ukifanya siri, kwanini unaonekana kuwa katika hali ya mshituko, Au ulikuwa ukimdanganya Sophia kwa kumridhisha kuwa nae katika mahusiano kwasababu anakupenda , Roma nadhani hunijui vizuri nitakuua kama ukimuumiza mjukuu wangu kihisia, mimi ndio Afande Mbale muulize babu yako ananijua vizuri nilivyo mapepe”

SEHEMU YA 635.
Edna mara baada ya kusikia maneno ya bibi yake na Sophia uso wake ulibadilika palepale huku akikumbuka siku ambayo Sophia alikuwa akijaribu kumfariji mara baada ya kumuona Roma akibusiana na Clark.
Edna siku ile alijaribu hata kumwambia maneno ya kumtia moyo ili tu apunguze wasiwasi juu yake.
Edna mpaka hapo alijua kabisa siku ile yeye ndio mjinga , alianza kuchukia, kumbe alikuwa akifanywa mjinga hata na Sophia , alijaribu hata kuji ‘assert’ kwa kujiambia kila kitu kipo sawa na anaelewa kila kitu.
Mbele yake kulikuwa ni kiza na mwanaume aliekuwa pembeni yake ni kama vile hakuwa akimjua , kwake ilikuwa ni kama vile ndio mwisho wa dunia.
“Edna!! Edna… naomba unisikilize”Roma aliweza kyaona mabadiliko ya Edna, mabadiliko ambayo hayakuashiria uhai badala yake yamejazwa na chuki ya kifo.
Bi Sumaiya aliweza kujua amefanya kosa kubwa, maneno yake yameonekana kuwa bomu kwa Edna kuliko hata alivyotegemea.
Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kunyanyuika alipokuwa amekaa na kumkimbilia Edna na kumshikilia mkono .
“Edna usiwe kama hivi , ndio tumejua sasa hivi kama Rima amekusaliti , tutamuadhibu kwa ajlili ya hiloo … Edna kwanini mikono yako ni ya baridi hivyo , unaumwa?”Aliongea Blandina huku akihisi mshangao kutokana na ubaridi wa Edna ni kama vile ameshika maiti.
Edna hakuongea chochote alikuwa amesimama kama sanamu , hakuwa akitoa machozi,hakuwa akionekana kama alikuwa akiumia ila alikuwa amesimama kama vile ni msukule uliokosa nafsi na kufanya kila mtu aliekuwa akimwangalia kujawa na wasiwasi.
“Unafanya nini , umebadilika hivyo kwasababu tu ya Sophia, hata hivyo Sophia sio mwanamke wa kwanza
Roma kukusaliti nae , kwa maoni yangu ulipaswa kujiandaa kwa hili”Aliongea Bibi yake Sophia huku akikunja sura.
“Inatosha”
Roma aliongea kwa nguvu , pengine kama Mwanamke huyo hakuwa na uhusiano na Sophia basi angekuwa ashamuua hapo hapo au penginge kumchapa kibao.
“Sijafanya kosa lolote , Edna hana undugu wowote na mjukuu wangu , hivyo haileti maana kuwa kama hivyo”
“Madam unaenda mbali , unafikiri hatujui kwamba ulifanya hila na kumpokonya bibi yake Edna mume wake , lakini uliishia wapi wakati alipooa mwanamke mwigine ukamkimbia , yaani wewe ya kwako yamekushinda unataka na Edna kuwa sawa”Aliongea Blandina baada ya kukosa uvumilivu.
“Kimya”Aliongea kwa nguvu bibi yake Sophia huku akionyesha hasira waziwazi .
“Hivi unajua wewe ni kama mtoto kwangu , usitake niende mbali na kuweka wazi ujjinga wako uliofanya miaka na miaka”.
“Una mdhalilisha Edna tena akiwa nyumbani, unadhani naogopa ukiyasema mabaya yangu , unaweza kuongea chochote lakini siwezi kukuruhusu kumdhalilisha Edna”
Blandina na Bi Sumaiya walianza kuwakiana, upande wa Roma alishindwa kujua namna ya kumbembeleza Edna kwa muda huo kwani asingeweza pia kusema kama hakuna kinachoendelea kati yake na Sophia.
Alijua kusema hana mahusiano na Sophia isingekuwa kudanganya wengine bali angejidanganya mwenyewe na pia angemuumiza Edna na Sophia kwa wakati mmoja.
Dakika hio hio ni kama Edna alijua nini cha kufanya kwani alimpiga Roma jicho kali na kisha akageuka akitupa kila alichoshikilia chini.
“Edna unaenda wapi?”Aliongea Roma akitaka kumsogelea na kumzuia kwa kumshika mkono lakini alionekana kuchelewa kwani Edna alikuwa fasta na ndani ya dakika chache tu alikuwa nje ya nyumba.
Lanlan alitaka kumfuata mama yake lakini Roma palepale alimpakata na kumuweka kwenye mikono ya mama yake.
“Lanlan kuwa mtoto mtiifu ,baki hapa usubirie chakula cha usiku ule ulale”Aliongea Roma na palepale alikimbilia nje kumfuata Edna.
Blandina alitaka kumuita Roma lakini aliishia njiani kwani alishindwa hata kutoa sauti.
Lalan anaweza kua mtoto lakini alikuwa ashajua wazazi wake wapo katika migogoro , akiwa na mwonekano wake ambao muda wote ni kama mtoto mwenye furaha aliishia kuangalia upande wa nje baba na mama yake wakipotea bila ya yeye kutoka kwenye mikono ya bibi yake.
Roma ile anafika nje aliweza kumfikia Edna ambaye tayari ashaingia kwenye gari ya Audi nyekundu na Roma alitaka kumzuia kwa mbele lakini alipigwa jicho hilo ambalo licha ya kwamba aliona kupitia kwenye kioo cha gari lakini ilitosha kumuogopesha.
Edna hakujali kusimama kwake mbele na aliendesha gari kwa kasi kama anataka kumgonga na Roma alikuwa mwepesi kwani alisogea pembeni na gari ikapita.
Roma hakutaka kusubiri na palepale alikimbia upande wa nyuma magari yanapo egeshwa na palepale alichukua gari ya BMW ya Afande Kweka na kisha aliliwasha na kulitoa nje ya geti.
Roma mara baada ya kutoka nje ya geti gari ya Edna ilioekana ikikata kona kwa ustadi wa hali ya juu kuingia barabara kuu ya kuelekea mjini.
Roma alishangazwa na uwezo wa hali ya juu wa Edna kuendesha gari lakini hata hivyo alijua kwa uwezo wake wa kuendesha gari basi angeweza kumfikia , alijiambia kama aliweza kumshinda Tusiman mwendesha magari maarufu wa dunia anashindwaje kumshinda Edna.
Lakini sasa Roma mara baada ya kuingia kwenye barabara kuu alikuwa ameachwa umbali mrefu sana huku akisikia mngurumo wa gari ya Edna ukiwa sio wa kawaida kabisa namna ambavyo gari ilikuwa ikibadilisha gia zake na kusonga mbele.
Roma jasho lilimtoka na kujiuliza au uwezo wa Edna kuendesha gari unahusiana na kile kilichotokea wakati akiwa hayupo mpaka kuua wanajeshi.
Ilichukua dakika kama tatu tu walikuwa wapo mjini kuingia kwenye ‘Raundi about’ na ile Edna anapita tu taa za kuongoza magari ziliwaka na kumzuia Roma na Semi Traller iliokuwa ikitokea upande wa kushoto kwake ilimzibia njia na kujikuta aking’ata meno yake kwani mpaka hapo alijua kabisa Edna kamchezea mchezo wa hila.
Mpaka ile gari yenye makontena mawili juu kupita Roma hakuweza kuiona gari ya Edna mbele yake na ilimfanya Roma kukosa chaguzi nyingine na kuanza kuifukuzia kwa mara nyingine.
Kwa wakati huo Roma hakuwa na wasiwasi kwa Edna kupata ajali kwani kwa uwezo wake ule aliamini haukuwa wa kawaida kabisa kuweza kupata ajali.
Roma aljikuta akilaani kutokuweza kwake kutumia uwezo wa kijini , pengine muda huo angeamua kusafiri kwa kuteleport na ingemuokoa kwenye taabu zote za kukimbizana na mke wake.
Roma hakuwaza ingekuja siku kukimbizana na Edna kwenye barabara kama hivyo , ilikuwa ni kituko na ilionekana ni kama Roma na Edna wamegeuka na kuwa maadui.
Dakika kama kumi tu gari ya Edna iliweza kufika katika hoteli ya Iringa Highland , sehemu ambayo ndio ambapo show ya Sophia inayoonyeshwa laivu kupitia V-TV ilikuwa ikipaswa kufanyika masaa machache yajayo.
Roma mara baada ya kufika nje ya hoteli hio alijua pengine Edna amekuja kwa ajili ya Sophia na alishindwa kuelewa nini anakwenda kufanya na palepale aliona aharakishe kuingia.
Lakini sasa Roma ile anataka kuingia alizuiwa na walinzi na kutakiwa kuonyesha kadi ya mwaliko , tiketi au kitambulisho lakini Roma hakuwa na chochote mfukoni.
Ilikuwa rahisi kwa Edna kupita kwani alikuwa ndio mmiliki wa wa kampuni ya Vexto Media lakini kuhusu yeye hakuwa akifahamika sana.
Roma aliamua kuegesha gari pembeni ya barabara na alitumia njia nyingine kuingia ndani , ijapokuwa sehemu ambayo alikuwa ameegesha palikuwa na kibao cha kuonyesha hapuruhusiwi kuegesha lakini hakuona haja ya kutafuta sehemu nyingne , aliamini hakuna shida ili mradi gari yake ilikuwa na Plate namba za jeshi.
Roma mara baada ya kuingia ndani ya hoteli hio alianza kukimbia kuelekea upande wa ukumbi ulipo kwani ni eneo ambalo lilikuwa limetanganishwa na hotel.
Alikuwa akikimbia huku akipiga simu kwa Sophia na bahati nzuri iliweza kupokelewa.
“Sophia .. ulimwambia bibi yako kuhusu sisi?”Aliuliza Roma.
“Sijamwambia mimi , MasterYumiao na bibi ni marafiki, hivyo aliniuliza kuthibitisha tu na sikuwa na jinsi”aliongea Sophia.
Roma alijikuta akijutia mara baada ya kusikia maelezo ya Sophia , alijua pengine Sophia alielezea kuhusu ulimwengu wa majini tu kumbe alielezea kila kitu mpaka mahusiano yao, lakini hakumlaumu na aliona yeye ndio mwenye makosa , alipaswa kumuuliza Sophia kuhusu bibi yake au angempa tahadhari tokea walipokuwa kwenye ulimwengu wa majini pepo.
“Dada yako Edna yupo eneo la ukumbini anajua kila kitu na amekasirika mno, sijui anapanga kufanya nini lakini nisaidie niweze kumdhibiti , usiruhusu afanye jambo lolote la kijinga”Aliongea Roma.
Alijua kabisa Sophia angeweza kumdhibiti Edna kwani tayari alikuwa levo ya Nafsi.
Upande wa Sophia alijuta , alijua bibi yake alikuja Iringa kwa ajili ya show yake kumbe kilichomleta ni jambo lingine.
Upande wa Edna ambaye alifika mapema aliweza kufika ndani ya hoteli hio na kutoka kwenye gari na kuanza kupiga hatua kuelekea upande wa ofisi za ukumbi huo jengo maalumu ambalo maandalizi hufanyikia.
Edna alikuwa kauzu mno, muonekano wake ni kama wa gaidi ambaye muda wowote angejitoa muhanga kwa kujilipua na bomu.
Edna mara baada ya kuingia katika chumba maalumu cha kubadilishia na maandalizi kilichojumuisha wanawake alianza kuangalia watu waliokuwemo ndani humo huku akiitafuta sura ya Sophia na haikumchukua dakika nyingi mpaka kuiona.
“Chukua watu wako ondoka nao”Aliongea Edna kikauzu akimpa maagizo Ummy Meneja wa Sophia.
Ummy hakuthubutu kuongea chochote na aliwapa ishara wafanyakazi waliokuwa wakimlemba Sophia na wote kwa pamoja walikimbilia nje na sasa waliobaki alikuwa ni Edna na Sophia peke yao.
“Sis…. Najua .,. najua unanichukia , nimekusaliti lakini siwezi kuzuia hisia zangu ,,,, nime..”Sophia alianza kutetemeka huku akiogopa macho ya Edna.
Edna alisogea bila kuongea nae lolote na palepale alimchapa kofi Sophia la uhakika kiasi cha kumyumbisha na kurudi nyuma mpaka kushikilia kioo ukutani.
Kofi hilo halikuwa la kawaida kabisa kwani lilimpeleka Sophia kuhisi kengele kwenye masikio yake.
Sophia alikua na uwezo wa kulikwepa lakini hakufanya hivyo , alitaka kumruhusu Edna kutuliza hasira zake hata kama ni kwa kumpiga lakini hakutegemea kofi lake lingekuwa na maumivu makali kiasi hicho kiasi cha kumfanya kuwa katika hali ya kizunguzungu licha ya kwamba alikuwa tayari kwenye levo ya Nafsi.
Kwa Edna ambaye alikuwa mwanzoni mwa levo ya mzunguko kamili asingeweza kuwa na nguvu za aina hio , lakini kwa Sophia aliona pengine ni kwasababu hakujizuia ni kama aliamua kumzimisha kabisa.
Sophia mara baada ya kuona amepigwa kibao cha aina hicho alishikwa na huzuni na kuona Edna hakuwa tena na zile hisia za undugu wa udada kati yao na hio ilimaanisha ni kwa kiasi gani amekasirika.
“Sister najua umekasirika ,, nipige kama ndio njia pekee ya kukufanya ujisikie vizuri”
“M*laya mkubwa wewe”Aliongea Edna kwasauti ya kusikika kabisa na Sophia hakutegemea Edna anaweza kuongea hivyo na moyo wake uliuma na alishindwa kuzuia machozi .
“Nadhani unaniona kama mjinga si ndio , nimetengeneza mpango wote wa wewe kurudi katika tasnia ya sanaa na kukutia moyo kufanya kazi kwa juhudi nikifikiria upo upande wangu lakini kumbe ulikuwa ukinionea hurma, Sophia maigizo yako ni ya hali ya juu sana , ulikuwa ujinga wangu kufikiria kwamba wewe huwezi kunisaliti , nilishawahi kuwaza na kujisemea wewe ni mwanamke mwaminifu na mpole kuliko wote ambao nishawahi kuwaona ,,, nilikuamini sana na nikafanya mambo makubwa kwa ajili yako kwa hiari yangu kabisa lakini mwisho wa siku ukaamua kumtega mume wangu kimapenzi kama wale wanawake wengine , hivi huna aibu hata kidogo , Dhamiri yako ipo wapi , hebu jiulize unautoa wapi ujasiri wa kuongea hayo maneno yasio na aibu mbele yangu , unaitafuta huruma yangu si ndio?”Aliongea Edna na Sophia alikuwa akilia kwa kwiki.
“Dada ,, sijawahi kuitaka huruma yako , najua nimekukosea na sina chaguo lingine zaidi ya kukuruhusu kunipiga na kunifokea ,,, nitakuacha unifanye chochote ili mtadi tu kukufanya ujijisikie vizuri”
“Unanijaribu ukidhania sitokufanya chochote”Baada ya kuongea hivyo palepale Edna alimchapa vibao vingine viwili kulia na kushoto tena kwa nguvu kiasi cha kumfanya Sophia kurudi nyuma kwa maumivu na aliishia kushika ukuta ili kujizuia asidondoke chini.
Ilikuwa bahati kwake alikuwa na mafunzo ya kijini kwani uvimbe na vidole mashavuni kwake viliweza kuponyeshwa kwa haraka, lakini Edna alionekana hakuwa na mpango wa kuishia hapo.
“Unajitia huruma ukidhani nitakuacha , kwahio hutaki kupigana na mimi , unafikiri nitaacha eh , sio kwamba nina mpango tu wa kukupiga na kuliacha lipite, Lazima nikuue leo mshenzi wewe”Aliongea na sauti yake ile ilimfanya Sophia kujua kuna kitu cha hatari kina kwenda kumtokea
Macho ya Edna yalikuwa ya mejaa ukatili wa hali ya juu mno , ni kama vile sio yeye na hali hio ilimuogofya.
Ilikuwa ni kama Edna ametawaliwa na pepo la giza na alimwangalia Sophia ka macho ambayo hayakuwa yale ya Edna anapokuwa na hasira bali macho hayo yalikuwa ni yale ya kimauji.
Sophia aijiuliza ilikuwa kweli mpango wa Edna kuja hapo kwa ajili ya kumuua.
Sophia hakuwa na muda wa kujiuliza maswali mara mbili mbili na alijiuliza imekuwaje Dada yake akabadilika ndani ya muda mfupi na kuwa hivyo.
Edna alikuwa ni kama wale wacheza Karate kwani palepale alimshambulia Sophia akilenga shingo yake eneo ambalo mtu yoyote akipigwa hawezi kupona na Sophia palepale alikwepa kwa ustadi.
Sophia mara baada ya kukwepa alipulizwa na upepo wa sauti namna ambavyo mkono huo uliweza kuikata hewa na alijua kabisa Edna ametumia nguvu zake zote kufanya shambulio la aina hio.
Lakini haikua mwisho, Edna alionekana kuwa mwepesi sana kwani baada ya shambulizi lake kukata hewa palepale alifyatuka na mguu wa kulia na kumpiga Sophia kifuani.
Teke lile lilikuwa na nguvu isiokuwa ya ajabu kwani Sophia alirushwa na kwenda kujipigiza kwenye ukuta huku akiishia kuugulia maumivu.
Halikuwa pigo la kuweza kumuumiza kivile kutokana na uwezo wake , lakini wakati akiugulia maumivu alisogelewa tena huku Edna akiwa ametanguliza ufunguo wa gari mbele akinuia kumtomboa macho Sophia.
Sophia alitumai uwezo wa kijini kukwepa mashambulizi ya Edna lakini pigo la kifuani ni kwamba alishindwa kulikwepa na alishangaa kuona kwamba ilikuwa ni kama alitegemea namna anavyokwepa. Alijiambia haikuwa kawaida hii.
Sophia palepale alijua asingeweza kupambana na Edna kwa njia za kawaida na palepale aliita nguvu ya kijini ili kujilinda.
Edna mara baada ya kumkaribia Sophia alikumbana na wimbi la nguvu ya kijini ambalo lilimrudisha nyuma na alionekana kukosa balansi na kwenda kujibwaga kwenye sakafu.
“Sister..!!”
Sophia alijua alishamuumiza Edna na pigo lile na kuanza kumkimbilia lakini ni kama alikuwa akitegwa kwani ile anakaribia Edna alifyatua mguu wake wa kushoto na kumfyeka Sophia kuanzia katika eneo la kwenye magoti akinuia kumpiga mtama na pigo lake lilionekana kufanya kazi kwani Sophia alishindwa kukwepa ndani ya muda na alijikuta akidondoka chini na kupigiza makalio chini.
“Umesema utaniacha nikupinge nitakavyo , ili nitulize hasira zangu , mbona sasa hivi unanizuia”Aliongea Edna huku akitoa tabasamu la uovu na muda huo alishamrukia Sophia ili kutompa nafasi nyingine ya kutumia nguvu zake za kijini na kumkaba shingoni huku kigoti cha miguu yake akiwa amekibana tumboni kwake kwa kulenga Meridian za mwili sehemu ambayo ndio senta ya kutawala nguvu za kijini mwilini.
Sophia aliishia kufurukuta tu huku machozi yakimtoka, Edna hakuwa na utani kabisa palepale aliinua ufunguo wa gari yake na kupelekea uswa wa Koromeo la Sophia akinuia kummaliza kabisa.

SEHEMU YA 636.
Kama sio Roma kuwahi kuingia ndani ya eneo hilo na kumsukumia Edna mbali basi pengine angemuua Sophia.
Roma mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi mno huku akijawa na hatia kumuona namna Sophia alivyokuwa katika hli ya mshituko.
Edna mara baada ya kusukumwa kwa nguvu alisimama palepale na kumpiga macho Roma na wote walijikuta wakiangaliana kama mabeberu.
Upande wa Roma alimwangalia Edna kwa macho yaliojaa utofauti wa kihisia , lakini upande wa Edna alikuwa na macho ya chuki, pengine macho ambayo hajawahi kumwangalia nayo Roma.
Ilikuwa ni bahati kwa Roma aliweza kukutana na Ummy mpaka kuja kutafuta na kufika hilo eneo ndani ya muda na kama sio hivyo pengine angemkuta Sophia akiwa mfu.
Roma alishindwa kabisa kumjua Edna kihisia, alikuwa ni kama mwanamke tofuati kabisa na anavyomjua , uhatari wake ,sumu yake iliomjaa , ukali wake na sura yake alikuwa akifanana kwa asilimia mia moja na mwanamke ambae kwenye maisha yake pengine asingeweza kumsahau.
“Edna umekuwa kichaa , ni kweli ulikuwa ukitaka kumuua Sophia?” Aliuliza Roma lakini ajabu Edna alianza kucheka huku akionyesha dharau za waziwazi.
“Kwani hukujionea mwenyewe , vipi kwani wewe mnyama? , ndio tuseme upo kwenye maumivu sasa hivi kumuona mpenzi wako mpya akitaka kufa mbele yako,, bado hajafa haina haja ya kuumia”
Roma mara baada ya kusikia maneno ya mnyama aliweza kukumbuka onyo la Edna kwamba akimgusa na Sophia basi atakuwa ni mnyama ,ilionekana mwanamke huyo hakuwa akisahau anachoongea.
Alijikuta palepale hasira zake zidi ya Edna zikishuka zenyewe na kugeuka kuwa hatia , alikuwa ni yeye ambaye amepelekea hayo yote kutokea.
Roma aliachana na Edna na kisha aliinama na kumsaidia Sophia kusimama na alijikuta akiumia kumuona namna ambavyo alikuwa kama amechanganyikiwa.
“Sophia na wewe umekuwa mwehu , ulipaswa kujilinda na nguvu za kijini hata kama hukuwa na mpango wa kushindanna nae”
“Si…”Alijikuta machozi mengi yakimtoka kiasi cha kutia huruma mbele ya Roma.
“Niliogopa nitamuumiza”Aliongea.
“Wewe unafiikiri huyu ni mwepesi kuumia ilihali katumia mbinu zangu za mafunzo , anaweza kuwa katika levo ya mwanzo mwa mzunguko kamili,
hivyo ngao yako ya kijini haiwezi hata kumsababishia mchubuko”
Sophia aliishia kuinamisha kichwa chake chini , uwezo wa kupigana alikuwa nao lakini alishindwa kushindana nae kwani alimuona ni dada yake.
Pengine katika hali kama hio ni mawazo ya kinafiki kufikiria kama Edna ni dada yake ilihali amemua kutoka kimapenzi na mume wake , lakini ile heshima ya udada aliokuwa nayo zidi ya Edna ndio iliomzuia kutoshindana na kumtaka ampige atakavyo huku akishindwa kuelewa Edna alikuwa siriasi akitaka kumuua.
“Edna usifanye hivi tena , haijalishi ni hasira kiasi gani unazo unapaswa kuzitolea kwangu , ni kweli Sophia anakuita dada lakini sio dada yako ,huoni sio halali kutolea hasira zako kwake?”
“Kwahio unamaanisha kwamba utafanya ngono na kila mwanamke ambaye hana undugu na mimi?” “Unajua kabisa sijamaanisha hivyo , najua nimekukosea na kukusaliti lakini si ndio wewe ambaye ulimsukumia Sophia kwangu?”
“Kwahio unanilaumu si ndio?”
“Nakuelezea ukweli , tokea siku ambayo ulijua Sophia sikuwa na mahusiano nae kama nilivyokuambia na ana hisia na mimiza kimapenzi ulichukua uamuzi gani , wewe ndio uliemruhusu mwenyewe kuishi na sisi na ukaenda mbali na kufungua kampuni kwa ajili yake na kunifanya mkurugenzi , ulijua ana hisia za kimapenzi na mimi lakini hukuwahi kumchukulia siriasi. Mimi naona wewe ndio umetufunga tuwe pamoja , au ndio ulikuwa ukinijaribu ,ulikuwa ukipima uwezo wa Sophia kujizuia , nilimkataa mara kibao kwa ajili yako na nikamuumiza lakini yeye yupo siriasi na hisia zake na siwezi kumuacha aendelee kuteseka , huna haja ya kumuamulia nani wa kumpenda kwasababu sio mdogo wako , ukiachana na kunipenda hakuna kitu kingine ambacho amekufanyia ni kibaya , lakini wewe unataka kumuua , mbona hujafanya hivyo kwa wengine , amekuruhusu umpige utakavyo haikumaanisha kwamba hakuwa na uwezo wa kujilinda ,ana mafunzo ya Kung Fu huyu na ana uwezo wa nguvu za kijini mkubwa kulikowa kwako , kwanini unakuwa mkatili kwake?”
“Kwahio unamaanisha napaswa kumshukuru kwa kuvumilia kwa ajili yangu , hebu nyooka ueleweke sitaki maneno mengi”
“Namaanisha hupaswi kumshukuru lakini vilevile hupaswi kumchukia , kama unataka nichome kisu moyoni nife mimi lakini yeye usimuumize”
“Haha.. nikuchome na kisu wewe , unaniona mimi mjinga , nikishakuchoma na hicho kisu si utakichomoa na kupona hapo hapo , naamini naweza hata kuutoa moyo wako na kuutupa na ukautufauta na kuuweka na ukaendelea kufanya kazi”Aliongea kwa macho ya kejeli na kisha alichukua funguo zake na kumpita Roma kuelekea mlangoni.
“Unaenda wapi?”
“Haikuhusu”
“Nifuatae twende nyumbani”Aliongea Roma akijaribu kumzuia asipite. Mlangoni lakini macho ya Edna yalibadilika palepale na alikunja ngumi yake na kumrushia Roma akinuia kumpiga tumboni lakini Roma alikuwa mwepesi kukwepa.
Roma alikuwa mwepesi kwani licha ya kukosa uwezo wake alikuwa na mafunzo ya hali ya juu ya zaidi ya miaka sita hivyo ilikuwa ngumu kumgusa kwa shambulizi kama hilo , lakini sasa Roma baada ya kukwepa alitaka kumshika mkono ili kumzuia lakini Edna alimpiga Roma teke la mzunguko na kumsukumia mbali na mlango na Edna hakuishia hapo tu.
Roma mara baada ya kuinama kuugulia maumivu ya teke lile Edna alileta lingine usawa wa kiuno lakini Roma alikuwa ameliona na alijikuta akipigwa na mshituko na kuishia kulikwepa huku akitaka kumshika Edna mabega lakini ni kama alitarajiwa angefanya hivyo kwani Edna alimkwepa na kurudi nyuma.
“Mashambulizi yako ni makali mno na ya haraka , kama ungekuwa kwenye uwanja wa vita ungekuwa na uwezo wa kuua kila mtu na shambulizi moja kutokana na maeneo unayolenga , sio mashambulizi yaliozidi bali ni ya kimahesabu ambayo yameunganika katika mtindo kamilifu, huwezi kufikia levo ya aina hii kwa mazoezi yako ya muda mfupi ulioyafanya , ndio maana haishangazi ulifanikiwa kumzidi Sophia”Aliongea Roma akitafsiri mashambulizi ya Edna.
Roma sasa aliweza kuelewa hali ilivyokuwa lakini hali ya wasiwasi iliweza kukijaza kichwa chake huku akikunja ndita.
“Edna nani kakufundisha mapigano?”
“Nimesema hayakuhusu”Aliongea na palepale Sophia alikuwa amesogea karibu yake na kabla hata hajaelewa nini kinachotokea alipokea shambulizi lingine la kiwiko cha mkono ambacho kilimrudisha nyuma kwa kasi ya ajabu
Kwasababu hakuwa ametegemea hilo alijikuta akikosa balansi na kudondoka kama furushi na kujjigonga kwenye meza na kudondokea kwenye kapeti.
Kitafsiri ni kwamba pigo hilo lilikuwa ni la kihisia zaidi , Sophia alikuwa nyuma ya Edna akitaka kumuomba msamaha wakati huo Edna alikuwa ameangaliana na Roma lakini Edna alijua Sophia yupo umbali gani kutoka kwake na kuachia pigo la ajabu namna hio.
“Edna umekuwa kichaa?”
Roma alijikuta akitetemeka na alitaka kumpiga Edna kibao lakini mkono uliishia hewani huku akianza kutetemeka , alishindwa kabisa kumpiga.
Angewezaje kumpiga mwanamke anaempenda kwa kiasi kikubwa , Edna alimwangalia kwa jicho la dharau na kisha alisogelea mlango na kutoka.
Awamu hii Roma hakuwa na uwezo wa kumzuia tena na alimuacha aondoke huku akijaribu kutuliza akili yake na hasira zake kabla ya kumsogelea Sophia.
Sophia upande wake alijitahidi kusimama huku akishika kiuno chake kilichokuwa na maumivu akikwepa Roma kumshika.
“Niko sawa”
“Sophia ni…”Roma hakujua hata ni kipi aongee katika hali kama hio na aliishia katikati.
“Nipo sawa ninachopaswa ni kujipaka makeup tu kwa ajili ya kufanya show, Roma nenda sasa kabla mtu hajaingia hapa”
“Show tena … Sophia wewe ni mpole au ni mjinga?”
“Mimi sio mjinga ,najua ana hasira sana lakini pia nina uhakika hakuwa akitaka kuniua .. nitafanya kazi kwa bidii ili uwekezaji wake usiende bure ,, huwezi jua pengine akipata hela za kutosha kupitia mimi anaweza kuwa na furaha , siwezi kumuomba msamaha wowote , hivyo ndio kitu pekee ambacho naweza kufanya kwa ajli yake”
Roma alijikuta akishika kiuno huku akivuta pumzi nyingi na kuzishusha, akili yake wakati huo ilikuwa imejaa maswali kibao pamoja na wasiwasi.
Katika mapambano bila ya kutumia mbinu zozote za kijini Roma alikuwa akijiamini mno na kujiita Master wa mbinu, lakini kitendo cha kupigana kwa muda mfupi na Edna mashambulizi yake ni ya kiwango cha juu mno na mbaya zaidi hakuwa akipambana kujilinda alikuwa akipambana kuua ,ilikuwa ni afadhali ru kwamba alikuwa hana siraha ya aina yoyote la sivyo ingekuwa ni habari nyingne.
Edna kufikia uwezo huo haikumhitaji mazoezi tu ya kimwili bali kulihitajika kipaji na uzoefu wa kimafunzo , katika dunia ya leo Roma alikuwa akijua watu wa mapigano ya mbinu hio walikuwa ni wachache sana akiwemo Noriko Okawa Master wa kundi laYamata Sect aliemuua na yeye mwenyewe.
Roma alijiuliza kuna mangapi Edna alikuwa akimficha au kuna kitu kingine kisicho cha kawaida ambacho hakijui.
Bila ya kujali ukweli Roma sasa anaamini kwamba Edna ndio muhusika ambaye ameua wale wanajeshi mara baada ya yeye na Lanlan kutekwa , kwa uwezo ambao ameonyesha aliona kabisa isingekuwa tatizo kwa Edna kupambana na watu kumi wenye siraha.
Baada ya Roma kumwambia Sophia ajilinde mwenyewe , aliamua kuondoka kumtafuta Edna akihofia anaweza kufanya jambo lingine la kijinga.

SEHEMU YA 637.
Roma wakati akitoka nje kabisa ya geti la hoteli hio Edna ndio kwanza alikuwa akitokomea barabarani akichukua uelekeo wa kurudi nyumbani.
Roma hakujiuliza mara mbilimbili na aliingia kwenye gari yake na kuanza kumfatilia kwa nyuma , awamu hio umbali kati yao ulikuwa mkubwa sana na hakuwa na uhakika kama anaweza kumpita.
Dakika chache mara baada ya kutoka eneo la mjini Roma aliweza kuwa na uhakika Edna alikuwa akielekea nyumbani , lakini kwa wakati mmoja hakujua kama alikuwa na mpango gani maana kwa alvyokuwa na hasira hakuwa na uhakika kama swala hilo linaweza kuisha kwa kumbembeleza.
Baada ya gari kusimama nje ya geti , Edna hakujisumbua hata kuliingiza ndani na alishuka na kisha akachoma moja kwa moja mpaka ndani akiwa na uso uliojaa usiriasi.
Walinzi waliishia kumpisha kwa tahadhari kwani alionekana kutokuwa wa kawaida ,ijapokuwa alikuwa mrembo wa sura lakini ule msisimko aliokuwa akisambaza haukua wa kawaida kabisa.
Ilikuwa ni usiku na familia yote ilikuwa mezani kwa ajili ya chakula cha usiku wakiongozwa na Afande Kweka mwenyewe na hawakuwa na haja ya kuwasubiri tena kwani hawakuwa na uhakika kama maswala yao yanaweza kutulia.
Bibi yake na Sophia hakuwepo tena ilionekana alikwisha kuondoka katika hilo eneo , lakini hata kama alitaka kubaki uwezekano wa kukaribishwa ungekuwa mdogo kutokana na hali ya hewa alioichafua.
Edna mara baada ya kuingia eneo la sebuleni kila mmoja alishituka na walishikwa na wasiwasi kutokana na ukauzu wake kama vile ni Jemadari anaejiandaa kumwangamiza adui.
Edna macho yake yalikuwa kwa Lanlan tu ambaye alikuwa amekalishwa juu ya kiti miguu ikining’inia akijiandaa kuanza kula .
Alikuwa na furaha ya kuona chakula licha ya kwamba wazazi wake hawakuowepo , hamu yake ya kula haikuathirika hata kidogo lakini mara baada ya kumuona mama yake alitoa tabasamu.
“Mama amerudi , Mama njoo ule chakula”
Edna mara baada ya kusikia sauti ya Lanlan muonekano wake ulibadilika kutoka katika hali ya ukauzu na kuwa katika hali ya kimaamuzi.
Na bila kujali wanafamilia waliokuwa wakimwangalia alimsogelea Lanlan na kumbeba juu juu.
“Eh! Edna unafanya nini?”
“Nini kinaendelea , Roma yupo wapi?”
Waliuliza wanafamilia wote waliokuwa wakijiandaa kupata chakula cha usiku lakini Edna hakujali mshangao na kuchanganyikiwa kwao.
Lanlan aliekuwa amebebwa juu juu aliangalia chakula kilichokuwa kwenye meza kwa macho ya huruma.
“Simama hapo hapo”
Roma aliekuwa anakuja kwa kukimbia mara baada ya kuingia tu alimzuia Edna kwa sauti ya kufoka na alijua kumbe kuja nyumbani mpango wake ni kucmchukua Lanlan.
“Wapi unampeleka?”Aliuliza Roma kwa sauti ya chini.
“Tunakuacha”Aliongea Edna kwa sauti kavu.
“Huna haki hio”Aliongea Roma huku akikunja ngumi yake.
“Hustahili kuwa mume wangu wala kuwa baba wa binti yangu , nina mchukua kwa ajili ya kumuweka mbali na wewe”
Roma aliona huu ni ujinga , anasemaje hana haki ya kuwa baba wa Lanlan ilihali yeye ndio amemzaa na Seventeen.
Roma hakuwa na mpango wa kutangazia familia kama Lanlan ni mtoto wake , lakini pia hakuwa tayari kumuona Lanlan akiiishi mbali na yeye tena, hivyo alibakiwa na chaguo moja tu kumwambbia Edna ukweli.
Alijiambia anaweza kukubali hasira zake na laana zake pamoja na kudharauliwa lakini sio kuruhusu mtu yoyote kumchukua mtoto wake hata kama ni Edna.
“Nyie wawili mnafanya nini ?Kwahio mnapanga kupena talaka na giza lote hili mbele yangu?”Aliuliza Afande Kweka kwa sauti ya juu ya mikwaruzo akishindwa kuvumilia.
“Roma, nini kimetokea ,kwanini hali imefikia hivi?”Aliuliza Blandina kwa wasiwasi akiogpa hasira za Afande Kweka.
“Alitaka kumuua Sophia na nikamzuia”Aliongea Roma mara baada ya kuvuta pumzi na kuzito.
“Nini!!!?’
Kila mtu alishangazwa na kuali ya Roma kwani ni kama vile hawajamsikia vizuri na kuishia kutoa midomo.
“Nipishe huko , ninaondoka na Lanlan”
“Nimesema huwezi , Lanlan ni binti yangu , hata kama unataka kuondoka ondoka peke yako na huwezi kuondoka nae”
“Mimi ndio niliefanya maamuzi ya kumuasili na nitakuwa mimi ninaeondoka nae , huna haki ya kumchukua kutoka kwangu”Baada ya kuongea hivyo alimpita.
Lanlan masikini aliishia kutoa kilio cha kwikwi akishindwa kuelewa ugomvi huo wa wazazi wake , kwani mpaka hapo alishajua wanaachana.
“Lanlan ni binti yangu wa kumzaa!!”Roma alishindwa kujizuia kabisa mara baada ya kuona Edna anakaribia mlango kutoka.
Ilikuwa ni kama kumetokea tetemeko la Ardhi huku kauli yake ikizuia muda kutokuendelea.
Edna ambaye alikuwa ndio anataka kutoka alijikuta akiganda huku akiwa amempatia Roma mgongo.
Afande Kweka ndio wa kwanza kutoka kwenye mshangao , ukweli ni kwamba mzee huyo hakuwa kwenye mshangao bali alikuwa kwenye maigizo ya mshangao maana alikuwa akijua kila kitu lakini hakutegemea jambo hilo lingekuja kujulikana katika mazingira ya ugomvi.
“Wewe mtukutu umesema nini… Lanlan ni mtoto wako wa kumzaa?”Aliuliza na Roma aliishia kutingisha kichwa huku ni kama mzigo uliokuwa umemlemea kifuani kwake ukishuka na kumpa ahueni ya kupumua.
“Ndio Lanlan amezaliwa na mwanamke ambaye nilikutana nae nje ya nchi , jina lake anaitwa Seventeen , alipoteza maisha mara baada tu ya kumzaa Lanlan na babu yake Lanlan ambaye alikuwa ni mwalimu wangu ,Master Tang Chi ndio ambaye alimlea.. kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wake hakuweza kumleta Lanlan kwangu mapema kama alivyoagizwa na Seventeen, nilivyopotea niliweza kukutana nae kwa bahati mbaya na akaniambia ukwel..”
Yalikuwa maneno machache lakini ujumbe wake ulikuwa mwingi sana kuusharabu wote kwa dakika moja , mwili wa Edna kwa wakati huo ulikuwa ukitetemeka.
“Unaongea upuuzi, una ushahidi gani?”Aliongea Edna huku machozi yakianza kuloanisha macho yake
Roma kwa wakati huo hakuwa na huruma tena kwani alishaamua kuweka ukweli wote wazi , alijiambia kwasasa anapaswa kujifikiria yeye na mtoto wake kwanza.
Baada ya kujitahidi kudhibiti maumivu yaliokuwa kwenye moyo wake , Roma aliingia upande wa Email katika simu yake na kisha kutafuta picha za barua alizozichukua kwa Qiang Xi , barua ambayo iliandikwa na Master Chi na baada ya hapo alitoa Ushanga wa kibudha na kumuonyesha Lanlan.
“Grandpa’s Beads”Aliongea Lanlan kwa sauti ya mshangao huku macho yake yakichanua akimaanisha kwamba ushanga huo ni wa babu yake.
Edna tumaini lake la mwisho ambalo alikuwa nalo ni kama limebomoka, alikuwa kama mtu ambaye amejenga ukuta wa bwawa la maji kwa kutumia saruji ambayo haina ubora na sasa maji yamebomoa na kuanza kukauka.
“Hii barua imepigwa picha na Qiang Xi baada ya kupoteza ya karatasi na ina majibu yote kwani ni Master Chi ambaye ameaindika na kumkabidhi
Qiang kwaajili ya kunipatia baada ya siku ishirini na tisa kupita, lakini hakufanya hivyo kwani aliogopa ukweli unaweza kuharibu familia yangu, kwasasa siwezi kujizuia zaidi kwasababu unajaribu kunipokonya binti yangu , nisamehe kwa kukuumiza kwa mara hii nyingine lakini siwezi kuuficha huu ukweli , ninapaswa kufanya hivi kwa ajili ya Lanlan”
Roma aliweka simu iliokuwa na picha katika mikono ya Edna,iliokuwa na picha ya barua na kisha akamchukua Lanlan.
Edna hakusita kusoma kilichokuwa kikionekana , ilikuwa ni barua ilioandikwa kwa kingereza lakini alielewa na kadri alivyokuwa akisoma machozi yalizidi kumtoka na kugonga kwenye kioo cha simu na alishindwa kumaliza na palepale simu aliomnunulia Roma kama zawadi ilidondoka kwenye tailizi na kutengeneza ufa.
Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kukurupuka kutoka kwenye kiti na kwenda kuichukua ile simu na kuangalia yaliyomo na kadiri na yeye alivyokuwa akisoma ndio wasiwasi na hatia ilivyoanza kumjaa.
“Roma unasema kweli Lanlan … , Namaanisha
Lanlan kumbe wewe ni mjukuu wangu kabisa, Roma nataka kusikia kwako mwenyewe kwa mara nyingine hebu rudia”Aliongea Blandina huku mikono ikimtoka jasho na aliishia kumshika Roma mkono na Lanlan kwa wakati mmoja.
Upande wa Afande Kweka aliishia kuegamia kiti chake kivivu akiangalia kinacheondelea kwa hamu zote lakini kwa wakati mmoja akimuonea huruma Edna.
“Mmeona wenyewe , Lanlan ameweza kuujua ushanga huu lakini pia Qiang Xi anaujua ukweli wote , Seventeen pia alituma Lanlan kuja kwangu kwa kuweka uthibitisho wa kisu kilichovunjika na zaidi ya yote Lanlan kazaliwa tofauti na watoto wa kawaida kama mwili wangu ulivyo, mnadhani hii inatokea kwa bahati mbaya , siku zote nilikuwa nikihisi muunganiko na Lanlan nadhani yote haya ni kufanana kwetu kwa damu”Aliongea Roma kwa kirefu.
“Lanlan babu yako amesema huu ushanga wa kibudha ni kwa ajili yako , ameenda sehemu ya mbali kucheza na rafiki yake na itachukua muda mrefu mpaka kurudi , lakini usijali kwa sababu mimi baba yako nipo hapa, utakula kila chakula kitamu utakacho kipenda na hakuna mtu wa kumchokoza binti yangu tena”
Lanlan alikuwa ni jiniasi na alishaaelewa maneno ya Roma na aliishia kugeuza kichwa chake na kumangalia mama yake kwa huruma.
“But daddy isn’t mommy Lanlan’s too?”Aliuliza akisema lakini baba si hata mama ni mama wa Lanlan.
“No , I’ m not your monny , your mother’s name is Seventeen and she is dead , From now on . I won’t have anything to do with you two anymore”
“Hapana mimi sio mama yako , mama yako anaitwa Seventeen na ameshafariki, na kuanzia leo sitohusika na chochote kwenu nyie wawili tena”
Edna aliongea manenno yake kwa sauti ya kusikika kwa kila mmoja na kisha aligeuza na kutoka nje kimya kimya.
Afande Kweka anahadithia na kusema kivuli cha
Edna kilikuwa ni kile cha mtu ambaye ametelekezwa na aliekosa tumaini lakini kwa wakati mmoja kilikuwa ni kivuli kilichojaa ujeuri ndani yake.
Unadhani huo ndio mwisho wa Edna na Roma , usikose yajayo.

papaaa singano

singano mutu ya pesa mingi

singano mutu ya watu

singano ukifa huozi mutu roho safi

mungu akupe nn tena tajiri?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom