Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI :SINGANOJR.
WATSAPP: 0687151346.

SEHEMU YA 605.
Baiju miguu yake katika vigoti ililelegea palepale mara baada ya kujua mwanamke ambaye hakuwa amemtambua ni Aoiline mkuu wake.
“Bwana wangu , sikujua kama upo hapa tafadhari naomba unisamehe”Aliongea kwa kutetemeka huku akiwa amemsujudia chini , hakuwa tena yule mwenye kiburi.
Aoiline aliachana na Roma na kisha alimsogelea Baiju kwa hatua hafifu huku uso wake ukiwa ni ule wa kichokozi , hakuonyesha kabisa kuwa na hasira.
“Baiju nimepewa ripoti kwamba unakusanya kiwango kikubwa cha mawe ya kiroho kupitia Madanguro , ukiichukulia faida kwa mimi kutokuwa makini na maswala hayo , inaonekana umeweza kuteka majini wanawake kwa tamaa zako”
“Bwana wangu wananisingizia tu , waliochini yangu ndio ambao wamefanya kosa hilo kwa kunipatia rushwa , nitahakikisha nina wahukumu vifo nikirudi”Aliongea Baiju huku akionekana kutengeneza kisingizio.
“Hata mimi naona , kwa hio unasema mimi ndio mkosaji hapa kwa kusingizia si ndio?”Aliongea huku kitingishcha kichwa chake kama mtu ambaye anajaribu kumwelewa.
Baiju alitaka kutingisha kichwa kujaribu kujitetea kwamba hakupaswa kumbebesha lawama zote lakini hakuweza kufanya chochote wala kukubali kama ana kosa na uso wake ulibadilika rangi na kuwa mwekundu kutokana na presha ambayo ilikuwa ikijiandaa kumkumba.
“Umekuwa na mimi kwa zaidi ya miaka mia mbili , nimekufanya uwe Bwana wa mji wangu wa Wingu Jeupe na ukapokea tani na tani za mawe ya kiroho kutoka katika maghala ya mji na watu wengi wakakuonea wivu lakini bado ukaamua kukusanya zaidi Mawe ya kiroho kupitiia Danguro , Ingekuwa ni sawa kama tu ungekuwa ukidanganya hao ambao walikuwa wakipenda kufanya kazi chini yako lakini ukathubutu kuteka wale ambao wanajaribu kupita katika mji wetu , hivi unadhani mimi siwezi kuishi bila wewe , unafikiri mimi ni mwepesi kudanganywa?”
Jasho la baridi lilimtoka Baiju na kuloanisha nguo zake na aliishia kutingisha kichwa chake akiwa amekiinamisha chini akishindwa hata kumwangalia Aoiline.
“Bwana wangu, Sikuwa nikifikiri sawa sawa , tafadhari naomba unisamehe kwa dhambi nilizoafanya kwa zaidi ya karne moja”
“Sawa”Aliongea huku akikusanya nguo za mkono wake na kutingisha kichwa.
“Itakuwa ni ukatili kama sitoweza kukupa nafasi , nitakusamehe kwa kuwateka wasichana wa kijini nyuma ya mgongo wangu”Aliongea na kumfanya Baiju kufurahiswa na maneno yake huku akitaka kuanza kusujudu kwa mara nyingine lakini Aoiline alimkatisha.
“Lakini hata hivyo napaswa kukuadhibu kwa jambo moja”
“Ah..!”Alitoa sauti huku sura yake akipeleka chini kwa mara nyingine akiwa kama amechanganyikiwa.
“Watu wako hususani Huji wameniteka siku ya leo na wakaniingiza kwenye kiroba ,… ningekuwa mrembo wa kukuingizia hela ndani ya Danguro leo kama sio Mr Roma kunisaidia”
Hio ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Baiju na sasa aliweza kuelewa kwanini Aoiline alibadilisha mwonekanno wake , kila kitu kilikuwa ni mtego wa kumkamata na ufisadi wake.
Ingekuwa afadhari kama angekamata wanawake wengine lakini sasa alikuwa amemsaliti hata Bwana wake hakukuwa na sababu ya kuachwa hai.
Dakika hio alivyojaribu kuunganisha Dot katika akili yake , Baiju alijiambia hakukuwa na faida yoyote ya yeye kuomba kusamehewa au kujitetea na anapaswa kufanya kitu chochote kile ili kuweza kukimbia na kutoka katika hio miliki, alijiambia kama ataweza kufika katika Korongo la Joka , Mfalme wa Majoka lazima angemlinda kwani alikuwa ni jini mwenye uwezo mkubwa wa kimapambano katika levo ya nane.
Baada ya kupatwa na mawazo hayo hakutaka tena kuchelewa, palepale aliita kwa hisia ndege wake mweupe kwa ajili ya kumshambulia Aioline .
Ndege mweupe na yeye akasikia kuitwa na mkuu wake , na palepale lilitoa kilio kikubwa cha juu huku likipiga piga mabawa yake kumsogelea Aoiline moja kwa moja.
Aoline hakuonakana yule mpole tena kwani alibadilika na alikuwa na uso wa kikauzu usio kuwa wa kawaida na kwa Roma ni kama alikuwa akimuona Edna party two, ilikuwa ni kama vile hewa iliokuwa ikimzunguka imeganda.
“Wewe mjinga , unathubutu vipi kujaribu kunipinga mimi?”Aliongea kwa nguvu na palepale kulitokea mwanga kama nguzo mbili nyuma ya gauni lake na nguo moja ya mwanga ilimshikilia yule ndege kwa kumfunga funga.
Roma aliangalia kwa ukaribu zile nguzo zilizokaa kama kamba kamba na palepale ndipo alipogundua ni mikia na pale ndipo alipojihakikishia kweli huyo ni jini ambaye alikuwa akiitwa Mbweha wa mikia tisa.
Mikia yake ilikuwa ni mirefu mno na haikuwa ya kawaida , ilikuwa ni kama boriti au nguzo.
Yule ndege licha ya Roma kumuona mkubwa lakini mbele ya ile mikia alionekana kuwa mdogo mno kwani alikamatwa na akawa hafurukuti kabisa.
Ndege yule alianza kutapa tapa kama vile kuku ambaye anapoteza uhai na ndani ya dakika tu damu zilionekana kuruka juu , ilionekana alikuwa amekamuliwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha viungo vyake kuharibika na hata manyonya yake yalianza kusambaa angani.
Sophia alishindwa kabisa kuangalia kitendo kile lakini kwa Roma alikuwa akiona kitu kile kama hasara kwani yule ndege alimpenda na kujiambia angalau kabla ya kutoka katika ulimwengu huo amwendeshe hata mara moja.
Wakati Aoiline akidili na ndege Baiju alikuwa ashakimbia kwa kupaa umbali mrefu kidogo , lakini bahati mbaya kwake ni kwamba mkia mwingine wa Aoiline ulikuwa ukimfukuzia na ulikuwa ukiongezeka urefu kadri alivyokuwa akikimbia kwenda mbali..
Roma ni jambo lingine ambalo lilimshangaza kwani hakuamini kama mkia huo ungekuwa na uwezo wa kuongezeka urefu na kusafiri umbali mrefu tena kwa haraka sana.
Ni kufumba na kufumbua tu Baiju alipigwa na mkia ule kwa nguvu mara baada ya kusogelewa na alijikuta akitema damu kutokana na kichapo.
“Rudi”
Ule mkia ulimviringa Baiju kufumba na kufumbua tu na kumvuta nyuma na kisha kumrudisha ardhini mbele ya Aoiline na dakika ileile ulipotea katika macho yao , ilikuwa ni kama vile haukuonekana kwani licha ya urefu wake ulirudi ndani ya mwili wa Aoiline kwa spidi kubwa mno.
Roma alijikuta akitengeneza sauti kupitia ulimi wake , Roma alikuwa akijua mwanamke huyo alikuwa na mikia tisa na ameonyesha mwili tu na kilichotokea sio cha kawaida.
Pengine siraha yake kubwa ni hio mikia na kama atapambana nae basi atakuwa ni moja ya washindani hatari ambao ashawahi kukutana nao kwani angekuwa na uwezo wa kujikinga na wakati huo huo akishambulia.
Kwa spidi yake hio na nguvu zake za kijini aliona kabisa hata yeye hakuwa akimuweza kimapambano kabisa, na hakutaka kujiona yeye ni mkubwa zaidi hivyo alikubali Aoiline alikuwa ni levo ya juu kuliko yeye.
Baiju alijikuta amepauka mno kwa woga , alikuwa tyari amekwisha kujikatia tamaa katika kukimbia na aliishia kusujudu kadri awezavyo na kujaribu kuomba kuhurumiwa , lakini licha ya kujitetea huko kulifanya tabasamu la kikatili la Aoiline kuzidi kutisha.
“Bwana nimetenda dhambi zidi yako , unaweza kuondoa nguvu zangu zote za kijini na kunigeuza kuwa mnyama lakini tafadhari naomba usinie , naomba unisamehe”
“Siku zote nilikuwa mpole sana kwa viongozi kama nyie , kwanini nikuondolee nguvu zako za kijini ?,Baiju je utanisaidia jambo moja?”
“I’m willing to redeem myself!”Aliongea
“Great”
Kufumba na kufumbua Aoline alikuwa nyuma ya Baiju na kuishika shingo yake na palepale mkandamizo wa hali ya juu ulianza kumtoka.
“Sophia kuwa makini”
Aliongea Roma na palepale alimsogelea Sophia na kumzingira na nguvu ya kijini kwani tayari ashajua ni nini kinachokwenda kutokea .
Aoiline alikuwa akipanga kumkandamiza na nguvu yake ili kuweza kutawala uwezo wake hivyo kutokana na mkandamizio mkubwa ambao alikuwa akijaribu kutoa Aoiline ilikuwa ngumu kwa Sophia kuweza kuhimili na angetema damu kwani mara nyingi inakuwa kama vile ni mlipoko wa bomu.
Ilikuwa ni kama vile mwanamke huyo mrembo amegeuka na kuwa mungu wa huo ulimwengu kwani macho yake yalikuwa yamebadilika kabisa na kile kiini cheusi kilikuwa kimempotea kwenye macho na jicho likabakia jeupe kama vile ni barafu.
Dakika ileile Aoiline alifumbua mdomo wake na meno yake yaliongezeka urefu kama Vampire na kuyapelekea katika shingo ya Baiju na kumng’ata.
Baiju sura yake mwanzo ilikuwa imepinda kutokana na mkandamizo mkubwa lakini mara baada ya kung’atwa mwili wake ulibonyea palepale .
Sophia aliekuwa nyuma ya Roma hakuweza kupata ujasiri wa kuangalia kile kinachotokea kwani iliogopesha , upande wa Roma alikuwa katika bumbuwazi kwa kile kinachotokea
Alijiambia swala la kunyonya damu ni la kawaida kwani kilichofanyika ni kujaribu kunyonya nguvu za lile jini lakini hakutegemea mwanamke mrembo kama huyo ndio ambaye anafanya kitendo hicho.
Kile kitendo huenda angekuwa ni binadamu wa kawaida ambaye anaangalia angepoteza fahamu palepale , Sophia kwa kiasi hakuwa wa kawaida kwani alikuwa ashaishi na Roma na kuzoea baadhi ya mambo ya ajabu ya namna hio.
Dakika chache tu mwili wa Baiju ulibadilika na Akawa Kunguru mkubwa ambaye ameoza huku mifupa yake ikianza kuonekana na Aoiline alimsukumia mbali maiti ile ya Kunguru na kuanza kuilamba midomo yake kwa damu zilizokuwa pembeni, alikuwa ni kama vile analamba asali kwa jinsi alivyonekana kufurahia.
Baada ya mkandamizo wa hewa kuondoka ndio aligeuza macho yake kwa Roma huku akiachia mkandamizo wa kawaida kama vile alikuwa akijaribu kumuogopesha Roma.
“Mr Roma huna haja ya kuniangalia hivyo na kuniona kama mchawi mnyonya damu , nimefanya hivi kwa zaidi ya miaka elfu moja , hatima yake ilikuwa ni kifo hata hivyo , kwanini nisimtumie kama kirutubisho , Au naongea uongo?”
Roma alikuwa akianza kuwa na wasiwasi juu yake , hata kama alionekana kuwa mrembo wa kuita lakini matendo yake na uwezo wake wa kijini ulimpa mashaka makubwa na kushindwa kuijua nia yake halisi juu yao.
“Nadhani tunapaswa kuendelea na safari yetu maana ushamaliza maswala yako”Aliongea Roma na kisha akamwangaliaSophia akimwambia waanze safari ya kuondoka hapo haraka iwezekanayvyo.
Sophia hakuwa na shida na alikubali kuondoka , yule Aoiline ambaye alitaka kuwa nae karibu hakumtaka tena maana alikuwa akitisha.
Aoiline palepale alitoa tabasamu la kifedhuli na kufumba na kufumbua alikuwa mbele ya Roma na kuwazuia wasiondoke.
“Mr Roma tupo karibu na jumba langu la kimalkia kwanini msiende kupunzima kwa muda”
“Hakuna shida sana juu ya hilo , safari yetu ni kuelekea kando ya ziwa la Mbingu”Aliongea Roma huku akijaribu kutafuta upenyo wa kumpita.
“Hata kama nimekudanganya kuhusu ubini wangu , lakini sikuwa nikidanganya kuhusu mambo mengine , kuna zaidi ya wiki tatu mpaka kwa mnara kufunguka , kwenda huko ni kupoteza muda wako tu”
“Mimi naweza kutokuwa na akili kama wewe lakini siwezi kuwa kichaa kabisa na kuanza kupigana na mtu kama wewe ambaye umeishi maisha marefu , lazima una nia nyingine hivyo acha kuzunguka zunguka”Aliongea Roma mpaka hapo alijua mwanamke huyo hakuwa na nia ya kuwaruhusu waondoke kirahisi.
“Mr Roma sisi majini tunaweza kufikiria pia na sio wanafiki kama binadamu , mosi nimekuja huku kwasababu nimesikia taarifa kutoka kwa watu wangu ndio maana nimekuja kujionea mwenyewekama ni kweli Baiju alikuwa akitenda mambo ya kifisadi, kitu kingine pia waliniambia kwamba kuna binadamu wageni ambao wameweza kufika katika ulimwengu wetu , Watu watatu ambao ulipigana nao katika msitu wamekuongelea vibaya sana lakini sikuwachukulia siriasi na sina nia ya kuwalipizia kisasi kwa uliowafanyia”
“Lakini bado siamini mtu kama wewe unaweza tu kunialika kwako kwa ajili ya kupumzika”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu.
“Nimeongea vya kutosha je tunaongozana au hatuongozani”
“Hatuongozani”Aliongea Roma kwa sauti huku akitingisha kichwa chake kukataa kusisitizia msimamo wake.
Aoiline alitoa pumzi ya kukatishwa tamaa huku akimwangalia Roma kwa masikito.
“Kama hutaki kuongozana na mimi basi sina budi kukulazimisha”Baada ya kuongea hivyo msisimko aliokuwa ukitoa ulibadilika kabisa na macho yake hayakuwa mazuri tena kwani yalibadilika na kuwa ya chuki.
Roma alishindwa kuelewa chuki yake inatokana na nini , aliajiambia kwanini kumbadilikia namna hio ndani ya dakika tu wakati hajamchokoza.
Roma palepale alimsukumia mbali Sophia ili tu asije akapata madhara na baada ya kumuona ameenda mbali zaidi aliita nguvu zake za kijini ili kuweza kuhimiri mkandamizio uliokuwa ukitolewa na Aoiline.
Dakika hio hio Aoiline muonekano wake wa kirembo ulikuwa umebadilika na kuwa kama vile ni jitu kubwa la kutawala , macho yake yalikuwa ni kama yale ya kutaka mtu yoyote anaemuona kumsujudia.
Roma hakutaka kumruuhusu msichana kama huyo kuendelea kumkandamiza , hakutaka tena kulinda nguvu yake ya kijini isipotee na alimsogelea Aoiline kwa nguvu zake zote.
Mpira wa moto wa bluu ulionekana katika mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto ulitegneneza maji ya kiroho ya kuosha uovu.
Aoiline alitoa tabasamu la kejeli kama vile alikuwa akidharau kile anachotaka kufanya.
Awamu hio hakutoa mikia yake bali nguo yake ilianza kutengeneza kamba kama Ribbon kutoka kwenye nguo yake ya hariri akidhamiria kupigana na hio .
Roma hakutaka kujali mbinu yake ambayo anataka kutumia na dhamira yake ilikuwa ni kutaka kumchapa na maji ya kiroho akiamini hata tone lake linaweza kumletea madhara.
Lakini nguo yake ile haikuwa nguo kama nguo kwani ilikuwa ikidhalisha kiwango kikubwa cha nishaiti isiokuwa ya kawaida na kadri ilivyokuwa ikipepea kuelekea upande wa Roma ni kama ilikuwa ikimzuia asimfikie.
Roma alijikuta akishangazwa na uwezo wake , aliweza kujua mtu anaepambana nae ndio yupo katika levo ya juu kabisa ya daraja la tisa la mafunzo ya kijini ya kuita pepo.
Kutokana na mkandamizio wake kuwa mkubwa Roma alijikuta akiamini huenda hata Athena akashindwa kabisa kudili nae.
Kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao mpizani wake Roma alianza kupoteza pambano mapema kabla hata hajaanza kushambulia kwani alishindwa hata kubadilisha nguvu zake kuleta faida katika kushambulia.
Aoiline hakuonyesha kutumia nguvu yoyote alikuwa ni kama vile anacheza na zile kamba za nguo zake za hariri na alianza kuzifanya zipeperuke hewani na zilikuwa zikitoa nguvu kubwa mno .
Roma palepale aliweza kufikiria huenda mbinu yake haikuwa ikitegemea muundo au nguvu bali alikuwa akitegemea akili yake na ufahamu . mpaka hapo alijua kwamba ulimwengu huo wenyewe ulikuwa kikwazo kwake hivyo hakuwa na namna ya kumshinda.

SEHEMU YA 606.
“Mr Roma huu ni ushauri wangu kwako , nifuate mwenyewe kwa hiari yako au endelea kuwa kiburi na nikufunge na kuondoka na wewe”Aliongea Aoiline.
“Sina jinsi tena”Aliongea Roma katika nafsi yake , katika maisha yake hakupenda kushindwa kirahisi.
Palepale Cauldron iliweza kutokeza na kuanza kutoa moshi kiasi cha kusababisha anga kubadilika huku msisimko wa ajabu kuzingira eneo lote la msitu unaowazunguka na kufanya hata baadhi ya ndege kukimbia.
“Pumbavu kabisa , kwanini una tumia Cauldron?”
Aoiline alikuwa ashaishi muda mrefu sana , muda mfupi alikuwa akijaribu kumuita ‘Mr Roma’ kama kumchokoza lakini mara baada ya kuona dhana hio ya hatari hakutaka tena kumchukulia mwepesi.
“Bado tu unataka kupigana licha ya kuonyesha kufahamu hiki ni nini?”Roma alitumia kiasi kikubwa cha nguvu ya kijini akijiandaa kwa ajili ya kukipa nafasi kumshambulia Aoiline , lakini Aoiline alianza kutoa cheko la hali ya juu.
“Najua hilo ni tanuru la maafa na ni sehemu ya Dhana za kijini ambazo zijashawahi kuwepo lakini licha ya nguvu yake kubwa huwezi kukitumia katika nguvu yake yote kutokana na levo yako kuwa chini , ndio kwanza umeipita Dhiki unadhani unaweza kunishambulia kwa uwezo wako huo , fuata ushauri wangu kama mkubwa kwako usikitumie maana roho ya mnyama iliopo ndani yake itaishia kutawala mwili wako , Roho yake iliopo ndani haiwezi kufa na hata wale miungu hawana uwezo wa kuihimili , kwa haraka haraka naamini Roho ya mnyama hio imekuchagua lakini kama utaendeelea kukitumia ukiwa na nguvu ndogo utaishia kuwa shushu, utakuwa sio binadamu tena na wakati huo ukifikia utakuwa umechelewa kwani huwezi kurudi kuwa wewe tena”Roma alikuwa katika mshangao licha ya kwamba hakuonyesha katika uso wake, alijiuliza je ni kweli chungu hicho kinaweza kumtawala , maneno ya Aoiline yalimfanya moja kwa moja kuwa na moyo mzito.
Aoiline palepale zile kamba za hariri yake zilipotea na kisha akamsogelea Roma kwa mapozi.
“Huwezi kunishinda hata kidogo , Sijawahi kukutana na mshindani wa ukweli katika ulimwengu huu , ijapokuwa uwezo wangu sio wote kutokana na mazingira lakini gepu letu ni kubwa sana , nimekuacha mbali na sina haja ya kutumia uwezo wangu wote kukushinda ni kidogo tu”Roma alijikuta akikunja ngumi yake kwa hasira baada ya kusikia maneno yale.
“Ndio unavyoona , sio mbaya najua nafasi yangu ni ndogo kukushinda lakini sijawahi kujisalimisha kirahisi hivyo”Mwisho wa sentensi yake palepale alikielekeza Chungu chake uelekeo wa Aoiline
Aoilinepalepale alijikuta akikunja macho yake lakini kwa jinsi ambavyo alikuwa akionekana ni kama hakuwa na mpango wa kukikwepa.
“Mjinga sana wewe”
Ghalfa tu mikia mitano iliweza kutokea nyuma yake na kwenda kukishikilia kile chungu , nguvu yake ya mvutano ilitaka kuimeza ile mikia lakini nguvu kubwa ya kijinni aliokuwanayo Aoiline iliweza kushinda na kile chungu kilirushwa kwa nguvu kuelekea hewani kama mpira huku yale macho ya mnyama ambayo mara nyingi huonekana ndani ya chungu kile yalipotea.
Kutokana na Roma kutumia nguvu nyingi kukitawala kile chungu na wakati huo huo Aoiline na yeye kutumia uwezo wake kukidhibiti maumivu aliyapokea yeye, ilikuwa ni kama viungo vyake vya ndani vinapasuka na aliishia kutema damu.
Kitendo hicho kilimuonyesha kwamba Aoiline uwezo wake ulikuwa ni mkubwa sana kuliko isivyokuwa kawaida kwani chungu chake ambacho aliamini kilikuwa na nguvu kiliweza kudhibitiwa kwa sekunde tu bila kuonyesha ukinzani wowote.
Sophia aliekuwa akishuhudia kitendo hicho alijikuta akijawa na wasiwasi mno hasa mara baada ya kumuona Roma akitema damu na alishindwa kujizuia na kumsogelea.
“Bro vipi hali yako?”Aliongea Sophia kwa upole na Roma alijikuta akikosa nguvu na kumuegamia Sophia.
Ijapokuwa alitaka kumwambia kwamba atakuwa sawa lakini alikosa nguvu kabisa hata ya kunyanyua mdomo na aliishia kutingisha kichwa chake tu.
Uwezo wake wa kujiponyesha ulikuwa ni wa taratibu mno kutokana kuwa na nguvu kidogo ya kijini na palepale chungu kile kilipotea.
“Nilikuonya mwenyewe , kwa nguvu zako za kijini Cauldron inaweza kuwa na nguvu kwa majini pepo wa kawaida lakini kwangu hapana”
Alimwangalia Sophia ambaye alikuwa na sura iliopauka na kisha palepale hakuonyesha kutaka kupoteza muda na alirusha kamba zake za hariri na kuwafunga funga.
“Nyie wote wawili tunaondoka pamoja kuelekea Palace”
Roma alitaka kumsukuma Sophia asifungwe na zile kamba lakini hakuweza kabisa na waliishia kuburuzwa wote kama mateka.
Roma hakuwahi kukata tamaa mara baada ya kuingia katika ulimwengu huo uliojjtenga lakini alijihisi kukata tamaa mara baada ya kumuona Aoiline akipaa bila tatizo kwa spidi kubwa na umbali mrefu kirahisi kabisa licha ya kwamba alikuwa akipambana na yeye.
Aoiline alisema kwamba mazingira yalikuwa yakizuia kutumia nguvu zake ,sasa alijiuliza kama ni hivyo uwezo wake ulikuwa ikifikia wapi kama tu ataweza kutoka katika ulimwengu wa kawaida.
Roma hakuona shida kupoteza pambano lakini alimuonea huruma Sophia kutokana na ukiburi wake na mbaya zaidi asingeweza kurudisha nguvu zake ambazo zilikuwa zimepotea na hata kama ikitokea asingeweza kuwa na uwezo wa kumshinda Aoiline.
Alijikuta akikumbuka ule usemi kwamba haijalishi una nguvu kiasi gani lakini kumbuka kuna mwenzako ana nguvu kuliko wewe , ni sawa na kusema haijalishi una akili kiasi gani lakini kumbuka kuna mwingine ana akili kuliko wewe , au unaweza kusema haijalishi unajiona bora kiasi gani lakini kumbuka kuna aliebora zaidi yako hivyo kuna mazingira inapaswa kujishusha na kuukubali ukweli lakini yeye alienda kinyume na sheria hio.
Licha ya kwamba kuna misemo mingi ya kihenga lakini siku zote haifanyi kazi katika kila mazingira , anaweza akawa ameonyesha kiburi lakini dhamira yake ilikuwa ni kutaka kujaribu ndio maana hakuona aibu kushindwa ni vile tu nafsi yake ilikuwa ikijutia kumuingiza aliekuwa nae matatizoni.
Baada kupaa kuelekea mashariki kwa muda mfupi majengo yalianza kujionyesha mbele yao kwa chini.
Yalikuwa ya kitamaduni lakini makubwa na ya kuvutia , mchanganyiko huo wa kitamaduni wa makabila mbalimbali ya watu wa nje ya dunia iliwafanya kujihisi kama vile dunia ya kale imeunganiska sehemu moja, yaani waarabu , wachina , wakorea wazungu pamoja na makablila mengineyo ambayo yalikuwa yakiwakilishwa na sanifu zao za kimajengo.
Baada ya kuingia kwenye jengo moja refu ambalo lilikuwa mlimani waliweza kuona madini ya Nephriti yaliokuwa yamening’inizwa katika korido kuingia ndani kabisa ya jengo la kimalkia, ilikuwa ni kama vile ni yale majumba makubwa ya kifalme lakini ambalo limejengwa kwa mahadhi ya kisanifu tofauti tofauti .
Juu kabisa ya mlango wa kuingilia kulikuwa na ubao juu(Lintel) uliokuwa na maandishi makubwa ya kingereza na lugha isiokuwa ikieleweka , ‘Jade Fox Palace’, ni maandishi ya kubandika na hata kwa mjinga ungejua ni madini ya dhahabu yaliotumika.
Baada ya kuingia kwenye Baraza kubwa ambalo sakafu yake hiakueleweka imejengwa na madini gani kutokana na mtelezo wake palepale Aoiline aimtenganisha Sophia na Roma wakiwa wamefungwa katika staili moja lakini tofauti ni kwamba Sophia alikuwa amepoteza fahamu.
Roma akiwa amesimama katika eneo moja akiwa amefungwa na kamba za hariri palepale sehemu ambayo alikuwa amesimama ilianza kutengeneza duara kwa kuonyesha michirizi ya madini ya dhahabu na ilikuwa ni kufumba na kufumbua Roma alitumbukia ndani na kwenda kutua chini ya Gereza la Ardhini.
Roma alitaka kutoka haraka kabla shimo halijajifunga lakini alizuiwa na mwanga mkali wa dhahabu uliokuwa kama kioo.
“Wewe mtukutu hilo gereza limetengenezwa kwa madini yalitoka katika bahari Isio na mwisho , chuma chake kukuzunguka ni kile cha miaka mingi iliopita na kazi yake kubwa ni kunyonya nguvu za kijini na huu mwanga wa njano uliokuwa juu yako hauwezi hata kidogo kuupita , elewa ushauri wangu , kubali kuwa mfungwa wangu ili usipoteze nguvu zako”
Roma alijikuta akijaribu kupiga ngumi kuta za chumba na alijikuta akiona hakuna namna ya kuweza kutoboa .
“Pumbavu zako kabisa wewe Aoiline , kama unataka kulipiza kisasi cha watu wkao kwanini ipigane na mimi mpaka nife kuliko kunifungia”
Roma alikuwa na hasira alikuwa na hamu sana ya kutoka katika ulimwengu huo kuirudia familia yake , angewezaje kufikia mnara kama ndio hivyo ni mfungwa.
“Nini .. haha!, huwezi hata kushindana na mimi lakini bado unafikiria kwenda kwenye Mnara , mimi mwenyewe licha ya uwezo wangu nina asilimia hamsini tu za kupona mapigo tisini na tisa ya radi, nakushauri uache ndoto zako”
Baada ya kusema hivyo alitembea kuelekea kwenye Majilisi (Chamber au chumba) akiwa amemfunga Sophia vilevile akimburuza akiwa katika hali ya kupoteza fahamu.
Majini waliokuwa ni wahudumu na vijakazi wake walikuwa tayari wamekwisha kujipanga muda mrefu tokea anaingia na Roma .
Baada ya kuingia kwenye Majilisi wahudumu wa ngazi ya juu waliiinamisha vichwa vyao chini kwa heshima, hakuna jini ambao halikuwa na mwonekano tofauti na binadamu.
“Mchukueni na muingizeni kwenye Majilisi ya kushoto , mhudumieni vizuri lakini asiruhusiwe kutoka bila rushusa yangu , mnanielewa?”
“Ndio Bwana wetu”
Wahudumu wale hawakutaka kuuliza mtu huyo ni nani na anatokea wapi zaidi ya kutii maagizo.
Baada ya vijakazi wale kuondoka alitembea na kwenda kukaa kwenye kiti chake kilichotengenezwa kwa madini ya Dhahabu tupu huku pembeni yake kulikuwa na aina ya madini ambayo hayakuwa yakielezekza , ni kama vile ni vinundu vya Akmasi huku ndani yake kukiwa na madini mengine ambayo yalikuwa yakipumua kwa kubadilika badilika rangi.
Alifumba macho yake kwa kuvuta pumzi nyingi huku masikio yake yaliokuwa na uwezo wa kusikia mitetmeo yaliweza kunasa sauti za Roma kushindana na kuta za gereza chini ya ardhi lakini alionyesha kutojali ni kama alikuwa na uhakika asingeweza kutoka.
“God why did you send in onother headless man when I’ve almost forgotten about him?”
“Mungu kwanini ukaamua kutuma mwanaume mwingine kichaa ilihali yule nakaribia kumsahau”
Aliongea mrembo huyo akiwa anaangalia eneo la juu ambalo lilikuwa kama na kioo kinachopitisha mwanga kutoka juu angani na macho yake yalionyesha chuki na huzuni.
Kauli yake ilikuwa ikitafsirika kama vile kuna mtu aliempoteza na sasa anakaribia kumsahau lakini anamuuliza Mungu kwanini kamleta mwingine kichaa..
*******
Kulikuwa na baridi sio ya mchezo ndani ya Iringa kwasababu ilikuwa kipindi cha vuli lakini licha ya hivyo Edna hakuonekana kuathirika kwasababu alikuwa ni tofauti tokea aanze kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
Ilikuwa ni muda wa jioni ndani ya jiji la Iringa, Edna alikuwa amesimama nje ya geti katika shule ya watoto maarufu iliokuwepo karibu na chuo akimsubiria mtoto wake kutoka nje ya geti kama wazazi wangine walivyokuwa wakisubiria.
Wiki mbili zilikuwa zimekwisha kupita tokea kupotea kwa Roma na hakukuwa na habari zozote za kumuhusu.
Familia ya Afande Kweka haikutaka kumruhusu Edna kurudi Dar es salaam na kujifungia akiwa mwenyewe, hivyo wakamshauri Lanlan kuandikishwa shule ya muda ndani ya jiji hilo aendelee na masomo.
Lanlan alikuwa na akili hivyo aliweza kuendana kwa haraka na mazingira ya shule mpya na hakuonyesha malalamiko yote na alipenda michezo iliokuwa ikifanyika shuleni kwao.
Ukweli ni kwamba ukoo huo wa Roma ulikuwa na utajiri mkubwa sana kutokana na kuwa na vitega uchumi vingi na haikuwa hivyo tu hata yeye mwenyewe alikuwa na hela na ingekuwa rahisi kwa Lanlan kutafutiwa mwalimu ili kufundishwa akiwa nyumbani lakini Afande Kweka hakutaka Lanlan akikaa ndani tu aliamini kuchanganyika kwa Lanlan na wenzake kutampatia msingi mzuri wa kijamii.
Edna alikuwa akielewa dhamira yao ni nini hivyo hakutaka kukataa na kuruhusu Lanlan kuanza shule lakini ukweli ndani kwa ndani mrembo huyo alikuwa na huzuni, wakati wengine wakiwa na tabasamu na tumaini yeye muda wote alikuwa akiwaza yu wapi mume wake.
Ni wiki mbili sasa hakuwa akilala usingizi mzuri na alikuwa akisumbuliwa na ndoto nyingi na alishindwa kabisa kuvuta taswira ya kila wazo baya linalomjia , maswali haya ndio yalikuwa yakikitawala kichwa cheke , vipi kama Roma asiporudi milele? , Vipi kuhusu yeye atafanya nini?.
Wanawake wa Roma kutoka Dar walikuwa wakimsumbua kwa kumpigia kutokana na kushindwa kufanya mawasiliano na Roma na Edna hakuthubutu kuwaambia ukweli kama amepotea , aliishia kudanganya kwa kuwaambia kwamba Roma yupo katika sehemu ya kujitenga akiwa kwenye mafunzo makali sana ya kimapigano.
Hakuna alieweza kushuku maneno yake , pengine ni kwasababu walikuwa wakimuamini au matamannio yao zidi ya mwanaume huyo yalikuwa makubwa kuliko wasiwasi wao.
“Mommy!!”
Sauti ya kitoto iliweza kumtoa katika hali yake ya kimawazo na Edna alionyesha tabasamu huku akichanua mikono yake kumpoktea Lanlan kwa kumbatio.
Lanlan alikuwa amevalia koti la Track suit la bluu pamoja na suruali yake kwani siku hio ilikuwa ni ya michezo shuleni
Akiwa na Lanlan mikononi mwake alitembea nae kuelekea kwenye gari huku akimuuliza maswali kama siku zote.
“Lanlan what did you learn today?”
“Leo Lanlan amecheza michezo mbalimbali ya kukimbizana na nilimshinda hadi mwalimu”Aliongea na kumfanya Edna kushindwa kuvumilia kauli yake na kutoa kicheko , Binti yake ndio mtu pekee ambaye alikuwa akimchekesha kama hivyo katika kipindi hicho cha mawazo
“Darling , you have to be easy on your teacher nextime or else it would be hard for the teacher to teach other children”Aliongea na kumfanya Lanlan kutingisha kichwa chake kukubali ushauri wa mama.
“Mama tunaenda kula sasa hivi?”
“Jua bado linawaka na tayari unawaza chakula”
“Mama Lanlan ana njaa”Aliongeana kumfanya Edna kumfinya shavu na kisha kumuingiza ndani ya gari lao la kifahari.
Mwanamke ambaye alikuwa akimwendesha Edna alikuwa ni mjeshi tena Komandoo na alipewa kazi hio maalumu kumuendesha Edna lakini kwa wakati mmoja kumpa ulinzi na mara baada tu ya kuingia ndani ya gari aliliendesha.
Wakati gari yao inaingia barabara kuu ikirudi nyuma kutokea mjini kuelekea nyumbani kwa Afande Kweka ambako ni nyuma kabla hujafika Iringa waliweza kusikia ving’ora vya gari ya kipolisi nyuma yao.
Mjeshi yule alionekana kushangaa mara baada ya kuona kuna polisi wanaomuashiria kusimamisha gari.
“Ma’ am nadhani napaswa kusimamisha”Aliongea na Edna alimpa ishara kwa kutingisha kichwa kukubali bila kufikiria mara mbili mbili.
Baada ya gari yao kusimama pembeni ya barabara walitoka polisi waliokuwa wamevalia mavazi ya kitrafiki na kuwasogelea na mmoja wao aligonga kioo na kuashiria kufungua mlango na dereva kushuka.
“Afisa nadhani sijakiuka sheria zozote za barabara”Aliongea Mjeshi mara baada ya kutoka nje ya gari.
Polisi mmoja ambaye alikuwa na chunusi nyingi usoni alimsogelea yule mjeshi na kwa spidi kubwa aliishikilia shingo yake , kilikuwa kitendo cha kushtukiza, pengine mjeda yule hakutagemea angeshambuliwa ndio maana ilikuwa rahisi kwake kupokea pigo lile kabla bata hajaweza kujitetea, ni mlio wa mifupa tu ulioweza kusikika na palepale alilegea na kudondoka chini.
Edna palepale alishituka na kugundua watu hao hawakuwa polisi kama alivyodhani , ilionekana ni majambazi ambao hawakuwa na nia nzuri kwao
“Mommy they’re bad guys!!”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kuguna.
Polisi yule mwingine hakupoteza muda kwani palele kupitia mlango wa mbele alirusha bomu la moshi kuelekea ndani ya gari na Edna alishindwa kuwa mwepesi na alijishtukia tu tayari mapafu yake yakiweza kuvuta ule moshi.
Best sorry of all the time
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANO JR

SEHEMU YA 609..
Hayakuwa mauaji bali ilikuwa ni uchinjaji wa aina yake , Bwana mwenye chunusi nyeupe licha ya kupitia mafunzo katika sehemu nyingi za dunia lakini hakuwahi kuona mtu katili kama Edna, namna ambavyo amewaua watu wake ilimtisha na kumshangaza kwa wakati mmoja lakini hata hivyo mshangao wake haukudumu kwani mbele ya Edna ilimaanisha kifo kama asiingejaribu kujiokoa.
Hawakutaka kuchelewa kwani palepale na wenyewe walitumia wepesi wao kurudi nyuma kukimbia huku wakimrushia Edna risasi lakini ilikuwa kama vile Edna alikuwa akijua risasi ikitoka kwenye bunduki ‘Trajectory’ yake itakuwa wapi kwani alikwepa kwa sarakasi murua kabisa.
Bahati mbaya mtu mwenye chuusi upande aliochagua kukimbilia ulikuwa hauna mlango na kabla hata hajajua nini cha kufanya alishindwa kukwepa upanga uliorushwa kwake na palepale ulimchoma kifuani karibu na shingo na kutoboa.
“How…..”
Neno ‘How’ ndio kauli yake ya mwisho kuongea kwani alidondoka chini na kuanza kuupambania uhai wake.
Jambazi mwingine baada ya kuona Edna kaelekeza umakini wake kuelekea kwa Bwana mwenye chunusi hakutaka kupoteza nafasi kwani palepale alikimbilia upande wa mlangoni.
“Boom!!”
Ulikuwa mlio wa risasi uliopitia katika eneo la kisogo katika kichwa chake na aliishia kutoa macho tu na kudondoka chini na hakuchukua muda mrefu akakata roho.
Edna mara baada ya kuona amemaliza kazi alitupia pembeni ile bunduki na kumkimbilia Lanlan na kumkumbatia.
Lanlan muda huo licha ya kupigika alikuwa bado na nguvu zake na aliweza kushuhudia kila kitu alichokifanya mama yake na alikuwa akitoa macho ya mshangao akiwa na furaha juu.
“Mommy you are so strong , the bad guys are all dead”Aliongea Lanlan kwa furaha akimaanisha kwamba mama yake ana nguvu kubwa na watu wabaya wote wamekufa.
“Nisamehe, Nisamehe .. Lanlan mama hajakulinda vizuri na ni makosa yangu naomba unisamehe”Aliongea Edna muda huo hakuwa na furaha hata kidogo kwenye macho yake na aliishia kulia kilio cha kwikwi.
Lanlan kutokana na uwezo wake licha ya kupata michupuko lakini hakuwa na maumivu makali na aliishia kutoa tabasamu la kitoto na kusogezea mdomo mashavu ya mama yake na kuyabusu.
Edna tabasamu palepale lilimvaa lakini ilikuwa ni kwa sekunde tu kwani palepale alianza kujihisi uchomvu usiiokuwa wa kawaida huku macho yakianza kubadilika na kuwa na ukungu na ndani ya dakika hio hio alidondoka chini na kupoteza fahamu.
******
Nusu saa mbele nchini Rwanda ndani ya makazi ya raisi Jeremy alionekana Master 4 akiwa ameketi eneo la sebuleni akiwa na Raisi Jeremy aliekuwa amekaa mbele yake upande wa kushoto huku juu ya meza kukiwa na glass za mvinyo.
Muonekano wa Raisi Jeremy haukuwa ule uliozoelekea ni kama alikuwa katika hali ya kutokuamini jambo na hata sauti yake wakati wa kuongea ilisikika ikiwa sio ya kuelezeka.
Mbele yao upande wa kuingilia mlangoni alikuwa amesimama bwana moja mrefu mweusi ambaye alikuwa sehemu ya wanausalama wa raisi Jeremy na alionekana alikuwa akitoa ripoti ambayo ndio hio ilimfanya Raisi Jeremy kutokuamini.
“Una uhakika ni Edna ambaye amewaua hao wajinga?”
“Ndio mheshimiwa , Risasi na visu vilivyokutwa vina alama zake za vidole , Lanlan pia amethibitisha kwa kusema Bi Edna ndio aliehusika kuwaua wote mara baada ya kuhojiwa na Brigedia Tobwe wakati wa kuwaokoa”
“Upuuzi !! Edna hajawahi kujifunza mahali popote mapigano anawezaje kuwaua wanajeshi wa kitengo cha Special forces?”Aliongea kwa kufoka na kumfanya yule bwana mtoa taarifa kuonyesha wasiwasi.
“Mheshimiwa Taarifa ni za uhakika , bado sielewi imekuwaje wakafa lakini ushahidi unaonyesha kila kitu Bi Edna ndio kahusika, pengine kama kuna mtu ambaye anajaribu kuficha ukweli na akaamua kumshikisha Bi Edna siraha ili aonekane ni yeye”
“Unaweza kuondoka”Aliongea huku akiinua mkono wake na bwana yule alitingicha kichwa chake kwa heshima na kisha akageuka na kutoka eneo hilo.
“Master 4 nimefeli kukamilisha kazi .. inaonekana nahitaji muda zaidi kuweza kupata mbinu ya Roma ya mafunzo ya kijini”Aliongea Raisi Jeremy huku akiwa na uso uliosawajika.
“Jeremy umerahisisha mambo , wale wanajeshi wa Kamanda Razaq ni wepesi kuwatawala kutokana na chuki yao zidi ya Roma lakini hawana uwezo mkubwa .. mtoto wako wa nje ya ndoa ana siri nyingi ambazo wewe mwenyewe huzijui, bado tu hujafahamu kuhusu hili?”Aliongea Master 4 akiwa katika muonekano wa kawaida.
“Master bado nashindwa kuamini kama ni kweli ndio kahusika kuwaua , kuna uwezekano kuna mtu amebadilisha ukweli”Aliongea na kumfanya Master 4 kutoa tabasamu.
“Lanlan ni mtoto tu kwanini adanganye , fanya uchunguzi wa kina kupitia wanausalama wako uliowapandikiza na umjue binti yako vizuri au uanze kufikiria mara ya pili kumrudisha katika familia la sivyo itakuwa ni sawa na kujipiga risasi mguuni”
“Niamini Master , nitahakikisha nafanya uchunguzi wa kina kumjua vizuri binti yangu”
“Unatakiwa pia kutumia akili Jeremy , kwasasa haifahamiki Roma Ramoini yupo wapi na itakuwa ngumu kukamilisha mipango yetu akirudi , hivyo usije kupoteza hii fursa”Aliongea na kumfanya Jeremy kutingisha kichwa kukubali.
Kwa jinsi ambavyo alikuwa akipewa maelekezo ni kama vile hakuwa yule ambaye alikuwa raisi mwenye kujiamini , lakini nyuma ya pazia kuna watu ambao waliokuwa wakimwendesha kwa siri.
*******
Upande mwingine nchini Tanzania katika mkoa wa Iringa ndani ya jumba la Afande Kweka, Edna aliweza kufumbua macho yake taratibu na mbele yake ilionekana sura ya kitoto iliokuwa ikimwangalia kwa ukaribu.
Edna alijikuta akitoa tabasamu hafifu na kupandisha uso wake kama vile yupo kwenye ndoto na kumgusa Lanlan shavuni lakini mara baada ya kuona kila kitu ni uhalisia palepale alifumbua macho yake yote na wasiwasi ulimwingia kwa mara nyingine.
“Lanlan tupo wapi..?”
“Umeamka?”Sauti nzito ya mikwaruzo kutoka kwa Afande Kweka iliweza kusikika upande wake wa kulia.
Ni muda huo huo Edna aliweza kugundua kwamba walikuwa nyumbani na palepale aliinuka haraka haraka na kukaa kitako huku akimuweka Lanlan pembeni yake na aliweza kuona sura za wanafamilia wote zilikuwa zikimwangalia.
Ukiachana na wanafamilia watu wengine waliokuwepo hapo alikuwa ni Afande Tobwe aliekuwa kwenye gwanda za kijeshi pamoja na wanajeshi wake baadhi na RCO wa mkoa wa Iringa.
Na Edna kwa kuangalia tu aliweza kuona kuna hali ya wasiwasi katika macho yao.
“Mjomba wewe ndio umetuokoa ?”Aliuliza Edna akimlenga Afande Tobwe , alikuwa akimwita mjomba tokea akiwa mdogo na alikuwa amezoea hivyo.
Afande Tobwe alijikuta akiangaliana na wanajeshi wake huku wakionyesha hali ya kuchanganyikiwa na swali la Edna.
“Edna hukumbuki kilichotokea ?”
“Nini..sikumbuki..”Aliongea kwa kutingicha kichwa lakini lanlan palepale Lanlan alisimama na kuingilia maongezi , ilikuwa ni kama alikuwa akielewa mama yake alikuwa akiulizwa nini.
“Mommy you were so strong , you killed all of the bad guys ! Swoosh Swoosh Swoosh , The all died so Quikly”
“Mama ulikuwa na nguvu , uliwaua wale watu wabaya wote , Swoosh Swoosh Swoosh , na wote tayari wamekufaha kwa haraka sana”Edna alikuwa ni mwenye kuchanganyikiwa wakati akisikiliza maelezo ya Lanlan ambaye alikuwa akielezea kwa vitendo kwa kuruka juu na chini akionyesha namna ambavyo mama yake aliwaua wale watu wabaya.
Afande Tobwe na wengine hawakuwa wakikataa kuhusu jambo hilo pia, walikuwa wanaamini kile ambacho Lanlan anaongea na isitoshe uchunguzi uliofanyika ulibaini alama za vidole katika siraha zilizokuwa katika eneo.
Afande Tobwe na Afande Kweka waliangaliana , wote walionekana kuwa na wasiwasi juu ya kile kilichotokea na namna Edna ambavyo hakumbuki chochote.
“Edna mwanangu ni sawa tu kama hukumbuki chochote ili mradi tu upo sawa”Aliongea Blandina ambaye alikuw ana wasiwasi na afya ya Edna muda wote.
Baadaya Damasi kuondoka na kurejea Dar es salaam yeye alibakia hapo Iringa kwa ajili ya kukaa karibu na Edna kwa kipindi ambacho Roma hayupo.
“Edna ni sawa tu kama hukumbuki chochote hili tukio sio la kawaida lakini vilevile ulikuwa ukijifunza mbinu za kuvuna nishati kwa kipindi kirefu kidogo hivyo inaeleweka unaweza ukawa umefanya wewe , lakini kwanzia kesho na kuendelea utakuwa ukitembea na walinzi, sitaki kuona mpo hatarini tena kabla ya Roma kurudi”
Edna aliishia kutngisha kichwa kwasababu hata hivyo hakuwa akikumbuka chochote lakini bado moyo wake haukuwa katika amani kutokana na kutokuwepo kwa taarifa yoyote kuhusu Roma.
Baada ya kuwa na wasiwasi juu yao Blandina aliandaa haraka haraka chakula kwa kusaidiana na wafanyakazi ili waweze kupumzika mapema.
Ijapokuwa alikuwa akijua wamerudi wakiwa salama lakini kwa upande wake alikuwa na mawazo kama Edna tu juu ya kupotea kwa Roma na nyumba yote ilionekana kukosa ile furaha iliozoeleka.
Muda ulikuwa umeenda kwani ilikuwa ni usiku wa saa mbili kuelekea saa tatu lakini Afande Tobwe bado hakuwa ameondoka .
Alikuwa akijali sana maswala ya familia ya Afande Kweka kutokana na watoto wake kuwa na mahusiano na Roma.
Afande Kweka alikuwa ameketi huku akiangalia baadhi ya picha ambazo zimepigwa kutoka eneo la tukio , namna ambavyo watu walivyokutwa wamekufa na kilichoonekana katika uso wake ni ndita pekee kujikunja.
“Marshall nimefatilia kuhusu hawa watu na nimegundua ni wanajeshi waliofanya uasi chini ya Afande Razaq , wote walikuwa ni makomandoo wa wakihudumu katika kitengo cha special forces, kuhusu hawa wengine ni raia wa kichina na tumeshafanya mawasiliano na ubalozi ili kuweza kuwatambua”
“Haya yote yametokea nje ya uelewa wetu nadhani kuna mtu atakuwa amesaidia katika hili na isitoshe taarifa ya kupotea Roma tulihakikisha ni siri , nina uhakika kuna mtu ambaye aliwasaidia mwenye muunganiko wa kishushu ndani ya taifa”Aliongea RCO wa mkoa wa Iringa.
“Sidhani kama haya yote yanafanyika kutokana na visasi vyao juu yetu, kama ni hivyo wangemuua Edna na Lanlan lakini walichokifanya ni kutaka kuiba mbinu ya mafunzo ya Roma”Aliongea ijapokuwa kauli yake ya mafunzo na mambo kama hayo haikuwelekea kwa mkuu wa polisi lakini hakuuliza.
“Hata mimi nimewaza hivyo lakini kama nitakua sahihi mtu ambaye anaweza kwenda mbali hivyo labda upande wa Rwanda maana ujasusi wao ndani ya Tanzania umekuwa kero sana kwa usalama wa taifa letu, lakini kwa wakati mmoja sidhani kama Raisi Jeremy anaweza akafanya kitu kama hiki”Aliongea Afande Tobwe.
“Jeremy hawezi kujali kushukiwa katika hili , sasa hivi atakuwa hana cha kuogopa kwasababu Roma hayupo, hata kama angejulikana kama mhusika bado hatuna cha kumfanya , isitoshe hata kama tukisema ni yeye anazo sababu za mashiko za kukataa”Aliongea na kisha Afande Tobwe alimgeukia bwana mwingine aliekuwa amembatana nae.
“Muelezee Marshal kuhusu uchambuzi wetu wa tukio”Aliongea na bwana aliefahamika kwa jina la Jecha alianza kuelezea.
“Kutokana na viashiria ambavyo tumeweza kupata katika eneo la tukio lakini pia sababu za vifo vyao , tuliweza kugundua kwamba kama itakuwa ni kweli Bi Edna ndio kahusika, uwezo wake ni wa viwango vya juu sana , Daktari wa maswala ya kiuchunguzi ameweza kuthibitisha watu wote wamekufa ndani ya sekunde therathini jambo ambalo linamaanisha kila mtu alikufa katika ‘interval’ ya dakika tatu , hata wale maninja wa hali ya juu hawawezi kuwa na uwezo huo tukizingatia uwezo wa wanajeshi pamoja na siraha walizokuwaa nazo .
Bi Edna atakuwa na ufahamu mkubwa na bastora walizokuwa wameshikilia na siraha zingine kwani aliweza kutarajia mashambulizi yao na kuweza kushambulia bila ya yeye kudhulika , kwa taarifa tulizokuwa nazo watu wa uwezo huu ni maninja wa hali ya juu duniani wanaofahamika kwa jina la ZERO,Mr Roma Ramoni ni mmoja ya maninja hao lakini ni ngumu kuweza kumpata kama yeye”Aliongea na Afande Kweka uso wake haukuwa katika mabadiliko na aliendelea kuangalia damu zilizokuwa katika picha hizo.
“Tujuavyo Edna ni kweli anajifunza mbinu za mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini kwa levo yake haiwezekanni kuua watu zaidi ya kumi tena ambao ni wanajeshi , kama kweli ndio kahusika basi naweza kusema kuna kitu anaficha na sisi hatukijui”Aliongea Afande Tobwe
“Afande samahani kama nitakuwa naongea kimakosa , lakini kama kuna mtu mwenye uwezo wa aina hii lazima awe amepitia mafunzo ya hali ya juu ya kininja tena kwa ajili ya kuua na mara nyingi ni zaidi ya miaka mitano ya mafunzo makali sana pamoja na uzoefu , lakini kuhusu Bi Edna nadhani kila mmoja wetu hapa tunayajua maisha yake tokea akiwa mdogo”Aliongea Kapteni Jecha.
Eneo lote liligeuka kuwa kimya walijua kabisa Kapteni Jecha alikuwa sahihi , kulikuwana taarifa za kujitosheleza kuhusu Edna tokea anazaliwa mpaka akiwa mkubwa.
“Tukiachana na hayo yote kwasasa nadhani Afande Tobwe uhakikishe wanajeshi hao wanafanyiwa utaratibu wa kimaziko na hao wa wachina endelea kuwasiliana na ubalozi ili tujue ni wakina nani , nitaandaa wanajeshi wa kitengo maalumu kutoka kambi ya Lugalo kuendelea kufanya uchunguzi wa chini chini ili tuweze kujua siri ya Edna ni ipi”Aliongea Afande Kweka.
Ukweli alikuwa na wasiwasi sana huenda kuliko watu wote waliokuwa hapo ndani kwani ni yeye pekee ambaye alikuwa akijua siri nyingi sana kuhusu Edna na yale yote ambayo alikwisha kuyafanya yakiihusisha familia yake.
Yupo Lanlan katika maisha ya Edna mtoto ambaye alikuwa akijua kabisa ni wa Seventeen lakini ghafla tu Edna anakuwa na ujuzi wa juu wa kininja unaofanana na wa kundi la Zero, hisia zake hazikuwa zikieleweka kwa muda huo na alipotezea kila mawazo mabaya ambayo yalikuwa yakiingia katika kichwa chake na kuamua kudili na yale ambayo yalikuwa yakielekeweka na kujiambia Roma akirudi atadili na mke wake maana ndio anamjua vizuri.

SEHEMU YA 610.
Ni ndani ya ulimwengu wa majini pepo katika jumba la kimalkia , alionekana Sophia akiwa ameketi katika kiti kwenye kibaraza cha jumba hilo akikodolea macho mandhari ya nje.
Zilipita siku sita tokea aingie kwenye jumba hilo akiwa amefungiwa bila kutoka lakini Aoiline alikuwa akimtendea vizuri kwani aliwapanga hadi vijakazi ambao walikuwa wakimhudumia kwa zamu kwa kila alichotaka..
Licha ya hivyo haikumletea furaha kwasababu tu hakuweza kutoka nje ya chumba , aliweza kupata taarifa kupitia vijakazi na kufahamu Aoiline alikuwa amemfungia Roma katika gereza la ardhini bila sababu yoyote.
“Unafikiria nini?Au unamfikiria mpenzi wako?”Sauti nyororo iliweza kusikia nyuma yake na Sophia aligeuza shingo haraka haraka na aliweza kumuona Aoiline akiwa anamwangalia kwa macho ya kipole.
Licha ya yeye mwenyewe kuwa mwanamke mrembo lakini hakuwa ameuzoea uzuri na urembo wa Aoiline.
“Hatimae umeweza kujitokeza , unapanga kutufanyia nini?”Aliuliza na kumfanya Aoiline kuziweka nywele zake vizuri zilizokuwa zikipeperushwa na upepo..
“Nimeamua kuja kukuona muda huu kwasababu kama ningekuja mapema ungeonyesha hasira zako tu , ni jambo la kawaida kwa mimi kumtembelea mgeni wangu hususani muda ambao ametulia , kuhusu nia yangu ni rahisi nahitaji nyie watu kubakia hapa kama wageni wangu”
“Mimi sio mjinga, kama umetualika hapa kama wageni wako kwanini umemfungia Roma gerezani?”AliongeaSophia huku akianza kuonyesha kukasirika.
“Nadhani wewe mwenyewe ndio humjui ni mwanaume mwenye kiburi na hata kama ningemuambia abakie hapa angalau kwa miaka kadhaa asingekubali hivyo nikaamua kumfungia kwa lazima”
“Unaongea nini , miaka kadhaa!?, unapanga kumfungia kwa miaka kadhaa?”Aliuliza Sophia kwa mshangao lakini wakati huo sauti yake ikiwa juu.
“Kwanini unashangaa , unadhani naweza kuwaruhusu muondoke na kwenda kupigwa na radi kwenye mnara?”
“Sio hivyo lakini..”Sophia alijikuta akishindwa kuendelea kuongea.
“Kwahio unasema ukweli , Bro Roma anaweza kufa kama ataingia kwenye mnara?”Aliuliza na kumfanya Aoiline kumwangalia Sophia na macho ya kiuchokozi.
“Umekuwa ukimuulizia Roma tokea nimeingia kwenye hiki chimba tofauti na kuuliza kama naweza kukuruhusu kutoka au ni kipi naenda kukufanyia.. inaonekana unamjali zaidi unavyojijali mwenyewe , Dada Sophia ndio kwamba unampenda sana?”
Sophia alijikuta akishitushwa na swali lake na alitingicha kichwa haraka haraka kukataa lakini uso wake uliokuwa ushaanza kutawaliwa na homoni za aibu haukufichika.
“Sio kama nampenda , Bro Roma ni shemeji yangu kwanini nimpende?”Aliongea na kumfahya Aoiline kushangaa kidogo.
“Umesema ni shemeji yako , mbona sio kawaida , kwanini mashemeji wote kwa pamoja mkaja ndani ya ulimwengu huu mkiwa pamoja ? au ndio ulikuwa ukimsaliti dada yako?”
“Wew.. unanisingiuzia , tulikuwa tukishambuliwa na gaidi na ndio ilivyotokea tukavutwa kuja kwenye huu ulimwengu kama ajali , hatukujua chochote kuhusu huu ulimwengu na hakuna kilichotokea baina yetu”
Sophia aliongea hivyo kujitetea lakini muda huo masikio yake yalikuwa ya moto, kila akikumbuka tukio la Roma kipindi kile akiwa hana nguo mapigo yake ya moyo yalisonga kwa kasi sana.
“Hivi unajisikia wewe mwenyewe , tokea tukutane ulikuwa ukimwita Kaka badala ya shemeji hii inamaanisha una hisia za kimapenzi na yeye , isitoshe Roma mwenyewe ameweza kuja na wewe licha ya kwamba unaonekana kama mzigo kwake , inaonyesha anakujali sana hivyo hakuna haja ya kukataa”Aliongea na kumfanya Sophia kuishiwa na maneno.
Mawazo yasiokuwa na idadi yalikuwa yakipiga katika kichwa chake huku akijiuliza maswali mengi.
Ni kweli Roma ananijali kwa kiasi kikubwa? , ni kweli ananithamini? , anahisia sawa na za kwangu? , maswali hayo katika mawazo yake yalimfanya kujionea aibu.
“Ameoa lakini bado mna ukaribu , naamini sio mtu mzuri , wewe ni mwanamke mjinga tu ambaye umetokea kufa na kuoza kwa ajili yake”Aliongea Aoiline huku akitoa tabasamu la kejeli.
“Sio kweli , Roma ni mtu mzuri kwa kila mtu sio kwangu tu..”Sophia alichukua nafasi ya kumtetea Roma.
“Kwahio unasema kwamba kuna wanawake wengine anao wajali si ndio , kama ni hivyo mke wake si atakuwa anatia huruma?”Aliongea huku akikunja ndita,
Sophia alitaka kukataa maneno yake lakini aliishia kati kwani yalikuwa ni ya kweli.
“Unaongea kwa staili ya kufanya kama kuna kinachoendelea kati yetu lakini ukweli mahusiano yangu na yeye ni ya kishemeji , isitoshe ni chaguo la Sister kuendelea kuwa nae licha ya kuwa na wanawake wengine”
“Mh ,, hili halimaanishi kwamba hakuna kitu ambacho hakitotokea hapo baadae , pengine anasubiria muda muafaka wa kukula na wewe”Aliongea huku akitoa tabasamu la kiuchokozi na kuanza kumkagua Sophia kuanzia juu mpaka chini kwa macho ya kijini.
“Nimeweza kuona mpaka sasa wewe ni bikta , kama ni hivyo basi jitahidi kukadhana na mafunzo ya kijini kuliko kuruhusu wanaume wakudanganye”
Sophia hakujibu chochote kama vile alikuwa na hasira kwa Aoiline kumsema vibaya Roma.
“Nakuambia haya kwasababu unaonekana kuwa mtu mwenye moyo mwepesi na wa kikarimu na ndio maana sijakufanya chochote kwa siku zote , kama huniamini tunaweza kumuuliza Roma mwenyewe akufafanulie jinsi ulivyo”
“Unamaanisha nini ..?”Aliongea akionekana kuchanganyikiwa kidogo lakini Aoiline hakumjali kabisa na alimsogelea Sophia na kumbeba juu juu na kutoka nae nje ya chumba.
******
Upande wa mashariki wa ulimwengu huo wa majini pepo kulikuwa na milima ya Volkano mingi mno mingine ikiwa inalipuka mingine ikiwa ni ile Tuli.
Ndani ndani upande wa pili wa milima hio ndio kuna ukoo wa kijini wenye nguvu zaidi , ulikuwa ni ukoo wa kijini ambao ulikuwa umejitenga kabisa na majini wengine katika Korongo la Joka .
Yaani hao ndio majini pekee ambao hawakutaka jamii nyingine ziwaingilie, ni kama vile huku duniani uchukulie mfano wa nchi ya Korea Kaskazini ambao wananchi wao wamefungiwa na kuuziliwa kutoka.
Hii ndio miliki ambayo kuna Majoka wale wakubwa na hata ukiianza kuingia katika Korongo hilo kuna mifupa mbalimbali ya Majoka kila mahali.
Kulikuwa na jengo kubwa sana kama ngome lililojengwa kwa mawe makubwa juu ya kilele cha mlima , usanifu wa jengo hilo ulikuwa ni wa tofauti sana na ule wa jumba la kimalkia la jini Aoiline.
Ni usanifu ambao umejengwa kwa ajili ya kuruhusu Dragoni kutoka na kuingia katika jumba hilo bila shida yoyote.
Dakika hio hio lilionekana Joka kubwa lenye mabawa angani likiiamba ambaa kuelekea upande wa jengo hilo na baada ya kuupigisha mkia wake kulia na kushoto palepale kufumba na kufumbua lilikuwa lishaingia ndani ya jumba hilo.
Dakika hio hio Mara baada ya Joka lile kuingia ndani ya jumba hilo ulitokea mwanga wa kijani ukitoka chini na kugonga paaa na palepale lile Joka lilibadilika na kuwa mwanaume ‘Handsome’ sana , alikuwa ni mrefu alievalia mavazi ya kitamaduni ya rangi ya kijani.
Uso wake ulikuwa ni ule wa utulivu na kujiamini akionyesha ishara ya kumsalimia mwanaume mwingine ambaye alikuwa amekaa eneo la juu kabisa katika jiwe kubwa la madini ya rubi lenye kukaliwa na kiti cha Dhababu cha kifalme.
“Ewe Mfalme nimempata Joka mjumbe wa barafu lakini amejeruhiwa , kutembea kwake kunaingiliana na maumivu hivyo atafika muda si mrefu baadae”Aliongea yule mtu ambaye sura yake haikuwa ikielezeka ilikuwa ni kama vile kila sifa ya kabila hapa duniani alikuwa nayo.
Mwanaume alieitwa mfalme ni wa makamo alieketi katika kiti cha kifalme ambacho ni kama kingo zake zilikuwa mifupa ya mnyama au ndege .
Uso wake ulikuwa ni ule wenye usiriasi mkubwa na mtu yoyote anweza kuhisi hofu kutokana na msisimko aliokuwa akitoa.
Huyo mwanaume ndio mtawala wa Majini Joka katika eneo lote la Korongo la Joka, alikuwa akifahamika kwa jina la Mfalme Wuja.
“Joka Mjumbe wa upepo umekuwa nje ya makazi ya kifalme kwa muda , je Joka mjumbe wa barafu aliingia matatizoni?”Aliongea kwa sauti yake nzito huku akiwa na uso ule usiokuwa na hisia za aina yoyote , haikueleweka alikuwa katika furaha , huzuni au majuto.
“Ewe mfalme, Joka mjumbe wa barafu alienda kufanya doria ili kuweza kutafuta malighafi ulizohitaji lakini alipata ukinzani kutoka kwa Bashe na Yawaragi , wanajeshi wa miliki ya Mbweha wa Jade , kulitokea mpambano mkali kati yao “Alijibu Joka mjumbe wa upepo.
“Nadhani huyo Mbweha aliweza kuhisia kitu na ndio akatuma watu kwa ajili ya kumchunguza lakini licha ya uwezo wake hawezi kulinda kila mtu ndani ya miliki yake , lakini Je Joka mjumbe wa barafu ameweza kukamilisha misheni yake?”
Joka mjumbe wa upepo alitaka kuongea lakini aliingiliwa na sauti kutoka nyuma yake
“Ewe Mfalme , Joka Mjumbe wa barafu amefika”Baada ya sauti ile kutoka kwa kijakazi ghafla tu lilionekana Joka kubwa la rangi ya bluu lenye mabawa huku likiwa na kichwa ambacho kilikuwa kama vile kimezingirwa na barafu.
Baada ya kujibadilisha kutoka katika muonekano wa Joka aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida ambaye alikuwa ni mzee kama wa miaka sitini hivi mwenye ndevu nyeupe na alievalia joho la rangi nyeupe ambalo limefungwa na mshipi wa rangi ya bluu kiunoni, kwa muonekano wake alikuwa ni wa kawaida kabisa.
“Ewe mfalme , niwie radhi kwa kuchelewa kwangu nimeweza kukamilisha misheni”Aliongea na palepale alitoa kijiboksi cha mbao kidogo na kukiweka hewani na palepale kilisafiri mpaka kumfikia Mfalme Wuja.
Baada ya mfalme Wuja kupoktea kiboksi kile alikifungua ndani na palepale zilionekana chupa mbili kama vibuyu za madini ya Jade .
Ijapokuwa chupa hizo zilikuwa zimefungwa kwa juu lakini hazikuweza kuzuia harufu ya damu iliokuwa ikitoka ndani yake.
Mfalme wa Majoka bwana Wuja macho yake yalichanua kwa msisimko mkubwa wa furaha na palepale alisimama na kuanza kutoa cheko kubwa ambalo lilisababisha mwangwi na dakika hio hio na ngurumo za Majoka ziliweza kusikika kila kona kwa kupokezana kusindikiza furaha ya mfalme.
Kwa mtu wa kawaida angeweza kutishika kwelikweli lakini kama utazoea na kuelewa huo ni wakati wa mfalme kuwa na furaha basi usingeweza kuogopa.
“Haha.. umenishangaza sana , nilikuwagiza kwenda kupata damu ya majini pepo ya levo ya anga na mashetani wa anga lakini wewe umeweza kuniletea damu ya majini pepo anga saba na mashetani ya anga sita , hebu nielezee kwa haraka umewezaje kufanya haya yote kuzidi matarajio yangu , Joka mjumbe wa upepo amesema pia ulijeruhiwa , je mejeraha yako ni makubwa zaidi ?”Aliuliza Mfalme Wuja huku akimwangalia Joka mjumbe wa barafu.
Joka mjumbe wa upepo mwenyewe alikuwa katika mshangao , alijua mwenzake aliweza kutimiza misheni lakini hakuwa na taarifa kama aliweza kwenda zaidi ya kile alichoagizwa na kuua zaidi ya majini kumi na tatu wa mashetani wa anga kutoka msitu wa Mianzi Zambarau pamoja na Majini pepo wa anga kutoka utawala wa Mbweha.
“Ewe mfalme haya yametimilika kutokana na rehema zako, nilikuwa kwenye hatari kubwa wakati nilipokuwa nikipambana na Bashe na Yawaragi katika mpaka wa mlima wa Theluji wa Joka jekundu na Msitu wa Kiza , nilidhani ninakwenda kushindwa kukamilisha misheni lakini mgeni wa kibindamu mwenye uwezo usio wa kawaida aliweza kunisaidia na kuwashinda”
“Mgeni!!? Binadamu mwenye uwezo usiokuwa wa kawaida?”Aliongea Mfalme Wuja huku akionekana katika mshitoko wa taarifa ile.
“Nimeweza kupewa taarifa kuna binadamu mwenye mafunzo ya kijini katika jiji la Jiwe Jeupe , je ndio unaemzungumzia?”
“Nadhani atakuwa ni huyo , uwezo wake wa kijini ni wakutisha , mkubwa kuliko wa kwangu , aliniona wakati ambao nilikuwa nikizidiwa nguvu hivyo akachukulia hio kama nafasi na kumuua Bashe na Yawaragi na tukaweza kupata damu yao , alikuwa akitafuta Mnara wa kuweza kutoka katika huu ulimwengu na nikamdanganya kwamba nitamuogoza , kupitia safari nzima nilichagua njia ambazyo zinalindwa na majini pepo anga na kwa msaada wake tuliweza kuua majini anga wengi ambao walitaka kutuzuia , tuliweza kuagana mara baada ya kufika katika mpaka wa Msitu wa Kiza na ndipo nilipomuelekeza kuelekea katika jiji la Jiwe Jeupe na ndipo nilipofanya safari ya kwenda katika bonde la Ziwa kupata damu ya kutosha kutoka kwa mashetani wa anga lakini nilifanikiwa kuyashinda sita tu na ndipo nilipoanza kupungukiwa na nguvu zangu , kwasababu ya hilo walianza kunifukuza na kupatwa na jeraha na ndipo Joka Mjumbe wa pepo alipotokeza na kunisaidia”
Wuja alibadilisha uelekeo wa macho yake na kumwangalia Joka mjumbe wa pepo kwa namna ya kiulizo.
“Ewe Mfalme , niliweza kumkuta Joka mjumbe wa barafu katika mpaka wa bonde la Ziwa na Korongo la Joka , Mkuu wa mashetani Anga bwana Zao alikuwa amejificha muda wote katika Msitu wa mianzi Zambarau, baadhi ya Shetani wa anga wamekuwa dhaifu kuliko mwanzo pengne ndio maana Joka mjumbe wa barafu ameweza kuwaua”
“Nyie watu mnafikiria sana , Joka Mjumbe wa barafu ameyahatarisha maisha yake kwa ajili ya kuniletea damu , siwezi kumshuku hata kidogo, Joka Mjumbe wa upepo msindikize Joka Mjumbe wa Barafu kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu na kupona , kwasasa hupaswi kufanya misheni yoyote mpaka siku ya mashindano”
“Mfalme je damu hio inatosha?”Aliuliza Joka mjumbe wa barafu.
“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , Joka Mjumbe wa barafu umefanya kazi nzuri , unaweza kuondoka sasa”
Joka Mjumbe wa barafu alisita kidogo na kisha akamgeukia mfalme Wuja akionekana na swali
“Ewe mfalme je naweza kujua nani ambaye anakwenda kutuwakilisha katika mashindano yanayokwenda kuanza ndani ya wiki mbili?”
“Kwanini unauliza ?”
“Sijawahi kushiriki hata mara moja na natamani nishiriki, nataka nidumishe mfululizo wa ushindi wetu”
“Nitafikiria juu ya hilo , unaweza kuondoka sasa”
Joka Mjumbe wa pepo alionekana kusita sita lakini alikubali na kuondoka na baada ya kutoka nje aliweza kurudi katika hali ya U’Joka na kuondoka katika ngome ya kifalme.
Upande Mfalme Wuja aliangalia Majoka mawili yakipaa hewani kupitia dirisha na kisha akageuza macho yake kwenye vile vibuyu viwili vya damu huku akiwa na uso usiokuwa ukielezeka.

SEHEMU YA 611..
Roma alikuwa amepoteza hata hesabu ya muda kutokana na kufungiwa gerezani kwa muda mrefu.
Mwanzoni alikuwa amehukia sana na alikuwa na hasira kuja katika ulimwengu huo na kujikuta gerezani lakini kadri muda ulivyokuwa ukisogea alijikatia tamaa huku majonzi yakianza kumvaa na aliona ni kama vile karne moja imepita tokea aingizwe hapo ndani.
Kitaalamu Roma hakupaswa kuwa na wasiwasi au kuathirika kwa kufungiiwa sehemu kama hio lakini aliweza kuona hakuwa na chochote cha kufanya ndio kilichomfanya kuingiwa na majonzi.
Mawazo yake hayakutoka mbali na usalama wa mke wake , Binti yake, warembo wake na Sophia ambaye hakuweza kumuona tokea waingizwe hapo ndani.
Alijiambia ni kipi kitatokea kama ataendelea kubakia hapo kwa muda mrefu .
Kila wazo baya likimjia Roma alijikuta akipambana na ukuta akidhamiria kuharibu hilo gereza kwa kupitia nguvu zake ambazo zishamrudia lakini licha ya kujaribu hivi na vile hakukuwa na matokeo chanya na kuishia kujikalia chini kwa huzuni.
Haikujalisha ni marangapi amejaribu lakini nguvu zake zilikuwa zikimwishia tu huku yeye akishindwa kuwasiliana na elementi za mbingu na ardhi.
Alishindwa kuelewa kwanini Aoiline hakumuua mwanzoni wakati alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, pia Roma hakuweza kuwa na uhakika kama akifa hapo uungu wake unaweza kutoka katika ulimwengu huo na akazaliwa katika mwili mwingine
Muda ulisonga bila ya yeye kuelewa na hatimae ufa wa mwanga uliweza kuonekana juu yake, kitendo cha mwanga kuingia ndani Roma hakutaka kuchelewa na kuhitaji kuondoka katika hilo gereza.
Lakini kabla hata hajatoka mtu mwingine alidondoka chini na palepale mlango wa gereza ukajifunga.
Roma kwa kutumia macho yake ya kichawi aliweza kumuona ni Sophia na palepale hakutaka kujiuliza mara mbilimbili na alimsogelea na kumkumbatia.
Sophia alionekana kupoteza fahamu lakini kwa haraka haraka mara baada ya kumkagua alionekana alikuwa hana tatizo lolote na hata uso wake wa kirembo ulionekana wa moto , hivyo moja kwa moja aliona alikuwa akiishi vizuri.
Wakati Roma akipumua kwa ahueni mwenyewe kwa kuwa na wasiwasi mkubwa , Sophia aliweza kuamka.
“Bro Roma …”Aliita Sophia huku akimwangalia Roma katika giza.
“Una macho makali kweli , umeshanijua ni mimi?”Aliuliza Roma.
“Ni kwasababu naijua harufu yako”Aliongea kwa kumnong’oneza huku akiona aibu za kike.
Roma alijikuta akikosa cha kuongea katika hali hio isiokuwa ya kawaida na aliishia kumuweka Sophia chini kwani alikuwa mikononi mwake amempakata.
“Kwanini upo hapa , Aoiline kuna kitu chochote ambacho amekufanyia?”Aliuliza Roma akibadilisha topiki haraka.
Sophia alijisogeza karibu kabisa na Roma kama kujikumbatisha kana kwamba anaogopa kutenganishwa nae tena huku akitingicha kichwa kukataa.
“Alikuwa mzuri kwangu na alisema ni kwasababu mimi ni mpole na mkarimu..”Aliongea na kumfanya Roma kucheka.
“Inaonekana tayari ukarimu wako umekwisha kulipwa , hivi ananichukia kwasababu tu sikutaka kuondoka nae akiwa katika sura tofauti?”Aliuliza lakini Sophia hakujibu swali lake na alinyoosha mkono wake kujaribu kushika uso wa Roma.
Joto la vidole vyake lilimfanya Roma kutulia , kwa jinsi Sophia alivyokuwa akimshika Roma usoni ilikuwa ni kama vile anashika kitu cha thamani kubwa ambacho hataki kiharibike.
“Sophia unafanya nini?”Roma alitaka kutoa uso wake usiguswe lakini alishindwa kufanya hivyo zaidi ya kumwangalia tu.
“Sikuioni vizuri kwasababu ya giza , nilitaka kukugsa nione kama umekonda?”
“Acha ujinga, na uwezo wangu wa kijini sina haja ya kula chochote , kwanini nikonde , ukiachana na hayo kwanini amekungiza humu na wewe pia?”Sophia alijikuta aking’ata lips zake na kisha akapeleka sura yake chini.
“Nilitaka kuwa karibu yako , nitakaa na wewe hapa kwasababu hataki kukutoa”Aliongea na kumfanya Roma kukunja ndita .
“Kwanini unakuwa mjinga, huwezi kunisaidia chochote hapa , kwanini umekuja kwa ajili ya kupitia mateso wakati ulikuwa ukiendelea vizuri huko juu , wewe sio mimi na nguvu zako bado hazijafikia hata levo ya Nafsi , hutoweza kuchukua muda mrefu na aina hii ya chuma”
“Kwanini nisiweze , ni chaguo langu kwenda popote ninapotaka , Roma kama ulikuwa ukipanga kuongazana na mtu mzigo kama mimi kuelekea katika ziwa la Mbingu , kwanini nishindwe kukaa na wewe katika gereza hili la chini ya ardhi?”
“Ni tofauti “Aliongea Roma huku akitoa tabasamu la uchungu.
“Tofauti yake ni nini ,, nimetaka tu kuwa karibu yako, sikuweza kuwa karibu yako katika ulimwengu wa kawaida kwasababu ya dada yangu , je lazima nijizuie hapa na kukaa mbali na wewe licha ya kwamba sina uhakika kama tunaweza kutoka unajua ni kwa kiasi gani nilikuwa na wasiwasi juu yako wakati wote ambao ulikuwa hapa mwenyewe , unajua ni kwa kiasi gani nilikumisi na ni kwa kiwango cha namna gani nimeweza kujichukia kwa kutoweza kukusaidia kwa chochote ?”Aliongea huku akianza kulia kwa kwiki na kumfanya Roma kumwangalia namna anavyotoa machozi , ukiachana na mara ya kwanza ambayo Roma alikutana nae kule Japani, Sophia wa muda huo alionekana mwenye kupendeka.
“Sophia ,, nisamehe ,, hicho sio nilichokuwa nikijaribu kumaanisha”Aliongea Roma huku moyo wake ukifurukuta na Sophia alitingicha kichwa kwa masikitiko.
“Haishangazi ndio maana watu wanasema sehemu ya mbali zaidi katika ulimwengu ni kusimama mbele ya mtu unaempenda lakini haelewi chochote kuhusu hisia zako , licha ya kwamba nakupenda sana lakini siwezi kusema nakupenda , Roma sitaki kuwa mtu mzuri tena wala kuwa dada mzuri kwa Edna , moyo wangu umechoka , mimi bado mdogo na nataka kuwa mbinafsi pia , je unaweza kunikubalia msichana mbaya kama mimi niwe mpenzi wako?”Sophia alifunguka.
Hewa ya humo ndani ni kama ilikuwa haitembei wakati akimwangalia Sophia , ijapokuwa alihisi aibu na wasiwasi lakini moyo wake ulikuwa ukilia kwa ajili yake .
Kwa kipindi chote alikuwa akijitahidi kuubadilisha upendo wake na kumuona kama ndugu yake , ijapokuwa Sophia alionyesha hisia zake waziwazi lakini Roma hakutaka kuvuka mstari.
Alikuwa akihofia ni maamuzi gani ambayo Edna atachukua , ijapokuwa alikuwa amemuumiza kwa mara nyingi kwasababu ya wanawake wengine lakini Sophia alikuwa ni wa kipekee.
Licha ya kwamba Sophia na Edna hawakuwa na undugu wadamu lakini bado alimchukulia kama mdogo wake Edna.
Edna asingeweza kumchukulia Sophia kama wanawake wengine kutokana na kwamba jina lake lilikuwa na muunganiko mkubwa na familia ya Sophia.
Zamani Sophia alikuwa akijizuia kutokuonyesha hisia zake waziwazi kwa kuogopa kugundulika mbele ya dada yake na hata kuamua kwenda kujichimbia katika matemple ya wachina, lakini katika mazingira kama hayo katika ulimwengu mwingine hakutaka kujizuia , ilikuwa ni kama ile minyororo isiokuwa imemfunga ilikuwa imemuachia na sasa alikuwa huru kuwa karibu na mwanaume anaempenda.
“Sophia .. siwe.,.”
Roma alikuwa akijaribu kumkatalia lakini kabla hata hajamaliza sentensi yake lipsi za midomo yake zilivamiwa.
Sophia hakuwa na mchezo alimsogelea Roma nakupitisha mikono yake kwenye shingo yake na kuanza kumbusu kwenye mdomo na haikuwa kugusanisha tu Lips kwani palepale alipanua mdomo wake na kutoa ulimi nje na kuutumbukiza katika mdomo wa Roma.
Roma alikuwa akiweza kabisa kunusa harufu ya ubikra ya Sophia kupitia ulimi wake.
Sophia kwa namna ambavyo alikuwa akimbusu Roma ilikuwa ni kama vile maisha yake yote anayakabidhi kwake kupitia busu hilo , ni busu ambalo liliwakilisha uvumilivu , hamu na kila kitu kuhusu yeye.
Roma alikuwa hahisi chochote mwanzoni kuhusu busu hilo ,pengine ni kwasababu ya mstari ambao alikuwa ameuweka kati yake na Sophia lakini kadri Sophia alivyyokuwa akichezesha ulimi wake katika midomo yake pumzi yake ilianza kubadilika na kuwa nzito huku akili yake ikianza kuyumba
Bila kujielewa Roma alijikuta akianza kumsugua sugua Sophia katika mgongo wake akionekana ashaanza kukolea.
Sophia licha ya kuwa mzuri wa sura lakini hakuwa na shepu kubwa kuliko wengine lakini bado mwili wake ulivutia sana kimapenzi.
Roma pumzi zake zilizidi kuwa nzito na moyo wake ulizidi kuongeza kasi ya kusukuma damu na mwili uliomkumbatia ulikuwa ndio dawa pekee ya ugonjwa unaoanza kuonyesha dalili.
Mwanamke aliekuwa na hisia nae ameweza kumwelezea hisia zake katika ulimwengu mwingine na alijiambia huenda ni stori nzuri ya kimapenzi wanaitengeneza.
Roma alianza kujidharau yeye mwenyewe kwa kuwa muoga, hakuweza hata kuzielezea hisia zake kama Sophia alivyofanya.
Viungo vya mwili wake vilikuwa vikimuumbua na unafiki wake.
Mkono wa Roma ulikuwa ushatoka na kuingia ndani ya nguo yake na kuanza kuminya minya embe dodo zilizokuwa zinamchoma kiufan..
“Nakupenda sana Sophia ..”Aliongea lakini wakati sauti hio ilipomtoka mdomoni Sophia alimsukuma na kurudi nyuma akijitoa kwake.
Roma alimwangalia kwa macho ya mshangao lakini palepale aliweza kumuona Sophia akimwangalia na tabasamu la dharau .
Mikono yake bado ilikuwa hewani na alijikuta akimeza mate mengi mara baada ya kugundua kuna kitu hakipo sawa.
Tabasamu la dharau lilizidi kuonekana waziwazi mbele yake na kufanya moyo wake kuanza kutoa kilio.
“Wewe ni… wewe ni Aoiline na sio Sophia ?”
Jasho lilimtoka mwanaume huku akiongea kwa sauti na kumfanya Sophia kutoa cheko kubwa na ni kama anga linachezeshwa na palepale Sophia alibadilika na kuwa Aoiline.
Roma alitamani kutoa kilio , alichezewa akili kwa kiasi kikubwa sana, alijiambia ndio maana ilishangaza Sophia aliweza kumtongoza vizuri sana licha ya kwamba bado alikuwa bikra , kumbe alikuwa ni jini mzoefu Mbweha wa mikia tisa.
“Wewe mkorofi kwanini unaangalia chini mara baada ya kuchezewa na mimi”Aliongea Aoiline kwa kumtania.
Roma alijikuta akiona aibu kwa kuweza kudanganywa , lakini katika hali kama hio aliweza kulaumu uwezo wake wa kijini , mbinu yake ya kujibadilisha muonekano wake na kuficha uwezo wake ilikuwa ni ya kutisha.
Sasa mara baada ya kujua huyo alikuwa ni Aoiline je Sophia yupo wapi?.
“Sophia yupo wapi na umemfanya nini?”
“Vipi , ndio unaanza sasa kumuwazia si ndio, unahisi naweza kumdhuru?”Aliongea huku akizungusha nywele zake kimapozi.
“Kama utathubutu kumdhuru basi lazima nilipize kisasi hata kama siwezi kukushinda”Aliongea Roma kwa hasira huku sauti yake ikiwa nzito.
“Hebu muone sasa , kama wewe sijakuuwa kwanini nimuue msichana mdogo kama yeye , kumwaga damu yake hakuna thamani kwangu”
Roma alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kusikia maneno hayo lakini bado hakuweza kuacha kujiona mjinga kwa kuweza kudanganywa na kuchezewa na huyo mwanamke kama mdoli, aliumia kwasababu ilikuwa mara yake ya kwanza kufanyiwa hivyo na mwanamke.
“Vipi , bado tu hujatosheka na unataka kufanya kale kamchezo hapa hapa gerezani?”Aliongea akimwangalia kwa macho ya utani.
“Hehe.. kama utakuwa tayari mimi sina tatizo , nishafanya ngono na wanawake wengi lakini bado sijawahi kumuonja Mbweha wa mikia tisa”Aliongea huku akitoa tabasamu la hasira.
Aouline hakuweza kujali maneno yake ya kiuchokozi , alikuwa na uwezo wa kudhibiti hasira zake kwa kuishi miaka mingi .
“Sina muda wa kupoteza hapa, nimefanya haya yote ili kumfumbua macho Sophia namna rangi yako halisi ilivyo , nilitaka kumuonyesha kwamba shemeji yake Roma Ramoni ni Casanova ambaye anawaza kumla”
Roma alijikuta akishangazwa na maeneno yake na hata ile hasira iliokuwa ndani yake ilipotea ghafla .
“Unaongea nini wewe , kwahio unamaanisha Sophia anajua hiki kilichotokea?”
“Haha..unaniona mimi mjinga eti , unadhani siwezi kuweka Kamera za kiunlizi hapa?”Aliongea na palepale alipiga mwanga wa rangi ya bluu kwenye ukuta kama vile ni Projector na ndani ya dakika tu eneo la nje katika makazi ya kifahari ya mrembo Aoiline yaliweza kuonekana
Ilikuwa ni eneo la ukumbi ndani ya jumba hilo la kimalkia na Sophia alikuwa amesimama kwenye kioo huku uso wake ukiwa mwekundu na wa aibu.
“Hizi chuma sio za kawaida ndio maana nilikwambia zimetokea chini ya bahari isio na mwisho, zinaweza kuonyesha kila kinachoendelea hapa kupitia kioo kwa teknolojia nje ya fikra za kibinadamu , hivyo Sophia kaona kila kitu “Aliongea Aoiline kwa kujivunia.
Miguu ya Roma ni kama ilikuwa ikimlegea , hali hio tatanishi ilimletea kwa kiasi kikubwa hali ya hatia , lakini kwa bahati nzuri ni kwamba Roma hakuwa na aibu , sasa kila kitu kipo wazi aliamua kumsalimia Sophia kwa kujifanyisha hakuna kilichotokea.
“Sophia ni makosa yangu kwa kukufanya uwe hivyo , sitokaa mbali na wewe tena hata kama tukiweza kutoka katika huu ulimwengu”Aliongea Roma , hakujua cha kufanya kwani aliweza kuonyesha hisia zake wasiwasi kwa Sophia feki na siri yake kuwa wazi.

SEHEMU YA 512
Sophia alifurahishwa na maneno ya Roma lakini kwa wakati mmoja alishikwa na aibu, ni machozi pekee alioweza kuyatoa akishindwa kuzuia furaha yake, ile hali ya kumngojea kwa muda mrefu hatimae imeondoka na kila kitu kipo katika wakati uliopo , kila kitu cha kuufanya ulimwengu wake uwe na furaha kipo mbele yak.
Aoiline baada ya kuona namna ambavyo mwanaume Roma Ramoni asivyokuwa na aibu palepale alifunga kioo na kumfanya Roma asiendelee kuwasiliana na Sophia.
“Hivi wewe mkorofi kwanini bado unaigiza kuwa kama Casanova ilihali tayari umeoa , ndio kwamba unajjivunia kwasababu Sophia amekufa na kuoza juu yako?”
“Mimi ni mwanaharamu tu lakini bado sijawahi kutotimiza wajibu wangu , nitawajali kama nawapenda na hakuna mtu ambaye anaweza kuzuia hisia , ninchoweza kufanya ni kuwalinda wanawake wangu mbali na hatari , sifanyi kazi kikamilifu lakini nafanya kila linalowezekana kutimiza haja zao”
“Hakika wewe ni jasiri”Aliongea kwa kumtania.
“Kwanini niwe muoga ilihali dhamira yangu ni ya wazi , mwanaume mwingine ana mwanamke mmoja lakini hakidhi haja zake zote , mimi sio mwaminifu kwa mke wangu lakini ninampenda kiasi cha kutoa uhai wangu kwa ajili yake , licha ya yote yanayotokea naamini ataendelea kunielewa”
“Hakika huna aibu kwa kusema hayo ukiwa na uso usio kuwa na hatia hata kidogo”
“Nadhani sifanyi kosa ilimradi uovu wangu siufichi , mimi ndio mimi na tabia zangu zipo wazi”Aliongea na kumfanya Aoiline kumwangalia kwa macho yasiokuwa na hisia kabla ya kuanza kutoa kicheko.
“Kama yule mtu angekuwa kama wewe , mkweli wa hisia zake..”
“Yule mtu , unamzungumzia nani?”Aliuliza Roma kwa mshangao mara baada ya kumuona Aoiline kaishi njiani.
“Ni wapi ulijifunza mbinu ya Andiko la nguvu ya Urejesho isio na kikomo?”Aliuliza na kumfanya Roma kuwa katika mshangao ,alijiambia anajua mbinu yake kama alivyotarajia.
“Nilikutana na Master mwenye asili kutoka milima ya China, ndio alienielekeza “
“Master wa asili ya kichina..?, niseme kwamba hakika unakipaji kikubwa, hio mbinu ndio kubwa sana dunia nzima na ni ngumu mno , unaweza kukutana na yule mtu kama utaweza kufika levo za juu kabisa za kuhimili mapigo ya radi”Aliongea na kumfanya Roma kuzidi kujiuliza huyo mtu mwenye mbinu kama ya kwake ni nani kwanini hataki kumtaja jina.
“Basi sawa , wewe mkorofi nina kazi nataka kukupatia?”
“Kazi gani?”
“Ushasahau tayari kuhusu shindano la kuingia kwenye mnara , siwezi kushiriki mimi”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa.
“Kwahio unasema kwamba mimi ndio napaswa kukuwakilisha katika mashindano hayo?”
“Ni kazi ambayo ni kama nakusaidia , bingwa wa hayo mashindano ataweza kupata madawa mengi na Hazina ambazo zipo ndani ya mnara, isitoshe nimekusaidia kuweka hisia zako wazi na kujipatia mpenzi mwingine , unapaswa kuwa na shukrani”
“Mimi sina shida ya kushiriki isitoshe ndio ulikuwa mpango wangu , lakini je una uhakika ninaweza kshinda?”
“Haiwezi kuwa tatizo kwako mshindani mkubwa ambaye unaweza kukutana nae ni Joka Mjumbe wa barafu kutoka miliki ya Korongo la Joka , sidhani kama anaweza kukushinda kutokana na uwezo wako , watu wangu mashindano yaliopita waliweza kushindwa lakini haimaanishi wana uwezo mkubwa”
“Kwahio ulitaka nibakie hapa ukiwa na nia ya kunifanya mimi ndio nikakuwakilishe , huogopi kwamba ninaweza kupotea moja kwa moja kwenye mnara mara baada ya kupigwa na radi tisini na tisa?”
“Wewe mkorofi hakika una mawazo mengi ya kufikirika, kwanza huwezi kumuacha Sophia nyuma na pili hata kama utaingia kwenye mnara lazima uingie katika floor ya kwanza ukiwa na mimi hivyo siwezi kukuruhusu”
Aliongea na kumfanya Roma kuona ni kweli yupo sahihi , hawezi kuondoka katika huo ulimwengu na kumuacha Sophia nyuma.
Baada ya kukubaliana Roma alitolewa katika gereza hilo na kuingizwa sasa ndani ndani kabisa kwenye jumba hilo la kimalkia ambalo liliwakilisha ufahali wake katika jamii ya majini pepo.
Sophia alijikuta mapigo ya moyo wake yakiongezeka mara baada ya kumuona Roma , ijapokuwa alikuwa na aibu lakini kitendo cha kumsubiria kwa muda mrefu kumfungukia kilimfanya kujawa na hamu ya kumsogelea na kumkumbatia.
“Punguza presha , au na wewe unataka nikufanyie kama nilivyomfanyia Mbweha?”Aliongea Roma mara baada ya kumpa Sophia Kumbatiao lakini alionekana kuwa na wasiwasi sana kiasi cha Roma kusikia mapigo ya moyo wake yakienda kasi kasi.
“Sio hivyo..”Aliongea Sophia huku akijitoa na kumwangalia kwa wasiwasi Aoiliine akiogpa Roma anaweza kumkasirisha tena na kuishia kurudishwa katika gereza la chuma.
Aoiline hakujali sana kuhusu wao na alisogea na kukaa katika kiti chake cha kimalkia na kama kawaida yake aliangalia katika lile tundu linalopitisha mwanga na aliingia katika mawazo kana kwamba kuna kitu ambacho anakisubiria kwa hamu lakini hana uhakika kama kitatokea.
Dakika hio hio mwanga wa kijani uliweza kuingia katika hilo eneo kwa spidi kali na ndani ya sekunde tu alitokezea mwanaume kijana.
Kutokana na spidi aliongia nayo ilimshangaza Roma hususani katika eneo hilo ambalo hakua na spidi kutokana na kikwazo cha anga.
Alikuwa ni mwanaume wa rika la Baiju na alikuwa kwenye levo sawa na yeye ya daraja la nane lakini spidi yake pengine ni kubwa kuliko ya Baiju.
“Bwana wangu nina taarifa kwako ya dharula”Aliongea huku akionyesha kutomjali Roma na Sophia waliokuwa hapo ndani.
“Iluwa je kuna kitu chochote kimetokea katika mpaka wetu tena?”
“Ndio, Bashe na Yarawagi waliokuwa wakilinda mpaka kati ya Msitu wa Giza na mlima wa Joka jekundu kudumisha maagizo yako waliweza kuendelea na kazi zao kama kawaida lakini jana wakati natembelea kufanya dolia niliweza kugundua …”Alishia njiani.
“Umegundua nini , unaweza kusema?”
“Bashe na Yawaragi hawakuweza kuonekana katika nafasi zao , hakuna viashiria vyvoyote vya Aura zao pia , Huji na wenzake waliweza kupatikana lakini katika eneo ambalo kuna kila alama za mapigano , hivyo ninaamni watakuwa wameuliwa”
“Ukiburi…!!!”
Aliongea kwa sauti huku akisimama na palepale aliachia mkandamizo wa hewa wa kijini usiokuwa wa kawaida na kufanya vijakazi na wahudumu wote kuinamisha vichwa vyao chini kusujudu wakiomba huruma , Iluwa na yeye alikuwa amesujudu hivyo hivyo akiwa kama wengine tu.
Roma alikuwa tayari ashamkinga Sophia wakati akijaribu kushindana na hasira za Mbweha wa mikia tisa , alikuwa akiogopa na alijiambia siku ya jana hakuonyesha uwezo wake wote lakini hapo ilikuwa ni zaidi ya jana yake , aliona kabisa nguvu zake ni kubwa mno na zisizo za kutabirika.
Alijiuliza kama alikuwa na nguvu hizo katika mazingira haya yenye vikwazo vipi siku ambayo atatoka nje.
Roma mwenyewe alikuwa katika levo zaidi ya daraja la sita kama atahesabiwa kwa namna yao lakini bado tu alishindwa kuona uwezo halisi wa Aoiline, alijiuliza au ni zaidi ya daraja la tisa.
“Pumbavu zako wewe Mfalme Wuja , mara ya mwisho umetuma watu wako na kuumiza watu wangu lakini nikaamua kupotezea lakini awamu hii ukaamua kuvuka mpaka na kunichokoza ten.”Aliongea kwa hasira.
“Bwana wangu una mpango gani au ni wewe mwenyewe unaenda kuwaadhibu?”
“Niende mimi? Wanayo hata hio thamani ya jitihada zangu?”
“Bila shaka hawana”Aliongea huku jasho likimtoka katika paji la uso.
Aoiline anaweza kuwa mtu mcheshi muda mwingine lakini anapochokozwa anakuwa ni mtu mwingine kabisa .
“Unaweza kuondoka sasa , kuhusu mipaka hupaswi kufanya lolote , agiza majini pepo wa anga kurudi katika mamlaka zao na wape maelekezo walio chini yao kuchukua nafasi zao”Aliongea na Iluwa akikubali agizo lakini bado alionekana kusita kuondoka.
“Bwana wangu bado nimechanganyikiwa kuhusu jambo moja”
“Ongea”
“Waliochini ya Mfalme Wuja , Majoka matano wapo katika levo ya daraja la nane na sisi majini pepo wa anga tunaweza tusifanikiwe kuwashiinda kwa mapigano ya ana kwa ana lakini kama Bashe na Yarawagi walipigana wakiwa pamoja wasingeweza kufa kirahisi,, labda tu kama kuna mtu mwingine ambaye aliingilia”Aliongea akiwa ameikunja ndita na Aoiline alimuona ana hoja lakini mara baada ya kumwangalia Roma alipumua.
“Unaweza kuondoka nina mango wangu kichwani”Aliongea na kumfanya Iluwa kuchangayikiwa lakini alikubali kuondoka kufumba na kufumbua.
“Nadhani umeweza kusikia majini wa Korongo la Majoka wamekuwa ni wenye viburi , nilikuwa ni mwenye uvivu kulipiza kisasi lakini wameenda mbali wakati huu hivyo nataka ukawape fundisho”
“Mim!?, si ni muda mfupi tu ulikuwa ukiniambia nijandae kwa ajili ya mashindano, lakini sasa hivi unataka tena niende kwenye Korongo la Majoka , vipi kama nitakutana na mfalme wao , ninaweza kufa”
“Unaogopa nini? Unadhani Mfalme Wuja yuko huru mpaka mkutane , hawezi kukufanya chochote ilimradi tu huingi ndani ndani katika mamlaka yake , nataka ukaue baadhi ya Majoka ambao wapo katika levo ya Anga na utakuwa sawa”Aliongea na kumfanya Roma kutoa cheko na kufanya hata wale vijakazi kushangaa maana ni yeye pekee ambaye alikuwa akioongea kwa kjisikia mbele ya Aoiline.
“Je hayo yote ni kwasababu ya kulinda hadhi yako tu , unaniambia hawezi kusadia chochote hata kama watu wake watakuwa wanakufa ndio jinsi mnavyoongoza?”
“Ni sheria ya msituni , kuishi ni kwa mwenye nguvu zaidi , kama unasema tunapaswa kusaidia waliodhaifu kwanini nyie binadamu mnawinda wanyam atofauti na kuwasaidia?”
“Binadamu tunasaidia binadamu , isitoshe nyie wote ni majini, si ndio?”
“Wewe ni mjinga , sijawahi kusema sisi wote ni wa ukoo mmoja, isitoshe nguvu ndio kila kitu , walio chini yangu wananitegemea kwa ajili ya kuishi maisha yasio na usumbufu , wana deni kwangu lakini wao hawanidai hivyo sio jukumu langu la kuwalinda , sijali kuhusu vifo vyao najali kuhusu hadhi yangu , ninachomaanisha kama nyama ya mnyama uliemla leo ana nguvu kuliko wewe je kwanini umle?,Hata kama nyie wawili mngekuwa ni viumbe tofauti mnaweza kuishi kwa amani , hivyo ni ujinga wao kufa ila mimi najali kurudisha hadhi yangu ,sifanyi hivi kulipiza nafanya hivi kulinda hadhi yangu”
Roma alijiambia huyu ni ‘Psycho’ kitu kinachoharibu urembo wake lakini kwa asilimia fulani maneno yake kidogo yalileta maana.
“Sitaki kupingana na wewe , lakini nitakusaidia kama utaniambia nini sababu ya hii migongano, Sidhani kama ni jambo linalohusisha hasira zenu pekee”Aliongea na kumfanya Aoiline kushangazwa na swali lake.
“Sijui chochote na pia sitaki kujua ni mpango gani anao mfalme Wuja , hivyo kwangu siwezi kupoteza muda kuwazia , huenda mpango wake ni kutaka kunishinda au kutoka katika huu ulimwengu , sina matamanio ya kujua mipango yake”
“Kama ni hivyo basi angalau unipe zawadi kwa kukusaidia”
“Kutokumuua mpenzi wako ndio zawadi yangu kubwa kwako”Aliongea huku akimwangalia Sophia kikauzu.
Roma alijiambia hana chochote cha kufanya mbele ya mwanamke huyo na kitu pekee cha kufanya ni kutii maagizo yake.
“Unapaswa kuondoka mapema , kwa spidi yako angalau unaweza kutumia siku sita mpaka saba kwenda na kurudi , utarudi ndani ya muda muafaka wa mashindano”Aliongea na kisha palepale alimrushia Roma Karatasi iliokunjwa kunjwa(Scroll).
Roma aliichukua na kisha aliifungua ndani na kusoma kilichoandikwa na alijikuta akipagawa mara baada ya kugundua ni maandiko yaliopo katika Code maalumu , aliweza kusoma kutokana na kujua baadhi ya historia muhimu.
“Kumbukumbu za utengenezaji wa vidonge vya kijini kutoka kwa Malkia Tushani”Ndio Roma alivyoweza kutafsiri andiko hilo.
Inasemekena Roho ya malkia Tushani ilihusishwa na nafsi ya Mbweha wa mikia tisa kama mlinzi mkuu , yaani mlinzi wa nafsi tokea kufa kwake.
Sasa kusemekana huko kulionekana ni kweli mara baada ya Roma kuona Aoiline kuwa na kumbukumbu ya Andiko lake.
“Ukoo wangu ulikuwa na mahusiano mazuri na binadamu wa kawaida tokea ustaarabu wa kibinadamu ulipoanza , tunazo mbinu ambazo hazihesabiki zinazohusiana na utengenezaji wa vidonge lakini bado hatuna ujuzi wa kutengeneza , hata hivyo hatukuhitaji vidonge kwa ajili ya uwezo wetu , nimekuona una dhana ya tanuru la maafa na unaweza kudhalisha moto wa rangi ya njano na nyeupe kwasababu ya nguvu ya andiko , naamini utakuwa ushajifunza namna ya kutengeneza vidonge, ondoka na hilo andiko la kikanuni, unaweza ukajitengenezea vidonge hivyo mbele ya safari kwani malighafi zake zinapatikna katika ulimwengu huu peke”Aliongea na kumfanya Roma kuguswa.
“Kwanini unanisaidia?”
“Unawakilisha miliki yangu katika mashindano , kwa uwezo wako ulionao ni dhiafu mno , hivyo napaswa kukusaidia”
Roma aliweka andiko lile katika anga la pete ya Sumeru na kumshukuru sana kwa kumpatia kanuni hizo.
“Huna haja ya kunishukuru na nenda katafute na ujue ni nani anamsaidia Mfalme wa Majoka kunidhalilisha, najua kuna unachofikiria lakini sitaki kukuuliza hivyo ondoka uende kama huna swali lingine la kuuliza , nitamlinda mpenzi wako mpaka utakaporudi”
Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi , mwanamke huyo alikuwa akimsoma mawazo yake kama vile ni kitabu.
Roma alikuwa akiwaza pengine ni Lekcha ambaye anasababisha hayo yote baada ya kuvutwa na yeye ndani ya ulimwengu huu.
Lekcha uwezo wake ulikuwa ukiimalika kwa kuweza kutumia miili ya wengine , kama atakuwa ameingia ndani ya ulimwengu huo na kuanza kuyatumia Majini hayo kwa faida zake basi angeweza kupata uwezo wa hali juu sana , isitoshe nguvu zake za ant-matter hazikuwa na kikwazo cha kimazingira.
Roma alikuwa na wasiwasi kwani kama atakutana nae inamaanisha siraha yake kubwa ingekuwa ni Cauldron pekee.
Hakutaka kupoteza muda na palepale aliondoka kwa ajili ya kutimiza maagizo ya Aoiline kwenda katika miliki ya Majoka kutoa fundisho.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI : SINGANOJR.

Mono no aware
Ilipoishia
Tuliishia Lekcha akimfukuzia Roma na Sophia mara baada ya kuingia kwenye mnara na baada ya hapo na Aoiline akafuatia huku akiwapa ishara Master Chi na Master Zao kutokuwafuata.

SEHEMU YA 621.
Master Chi na Master Zao walijikuta wakiangaliana kwa mshangao na palepale wakajiuliza swali la aina moja , je ulikuwa ndio mpango wa Roma na Aoiiline kumfanya Lekcha kuingia kwenye mnara.
Wote kwa pamoja walikuwa wakielewa kwamba uwezo wa Aoiline ulikuwa mkubwa sana hata kwa kuunganisha uwezo wao wote wawili hivyo waliishia kutii maagizo yake na kutowafuata.
Upande wa Roma alikuwa akijihisi ni kama yupo kwenye hatari kubwa huku akiwa amemshikilia Sophia , marashi yaliokuwa yakitoka katika mwili wa mlimbwende huyo hayakuacha kuzitesa pua zake lakini hakuwa katika wakati wa kufurahia.
Lekcha spidi yake ilikuwa ni ya juu mno lakini licha ya kwamba alionekana kuwa na spidi na nguvu kubwa haikumaanisha kwamba hawezi kupata madhara.
Katika floor ya kwanza ya mnara huo hakukuwa na kitu cha kushangaza zaidi ya wingu kubwa lililotanda na ubaridi wa aina yake, walichokuwa na uwezo wa kuona ni kuta za mnara huo ambazo zilikuwa zimejengwa na malighafi za ajabu ambazo zilikuwa na weusi wa aina yake huku kukiwa na maandishi ambayo yalikuwa katika lugha ambayo ilikuwa ngumu kwa Roma kuielewa.
Ni kama Aoiline alivyoweza kusema kwani pia katikati ya eneo hilo kulikuwa na mimea ambayo ilikuwa imeota yenye kutoa maua na baadhi ya matunda , ijapokuwa Roma hakuweza kuifahamu lakini kwa haraka haraka alijua tu ilikuwa na nguvu kubwa kama itatumika katika kutengenezea vidonge , ilikuwa ni mingi sana , hivyo Roma aliamini hata kama wanaongia hapo ndani wanataka kuchukua kila kinachopatikana basi ni ngumu kufanya hivyo kwani muda wa kukaa ndani ya mnara huo ulikuwa ni wa muda mfupi sana kabla ya pazia la mnara huo halijajifunga, na kwa inavyosemekana kama likijifunga radi ya zambarau ilikuwa ikipiga mpaka katika floor ya kwanza.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa kabisa na muda wa kuangalia hio mimea kwasababu ya Lekcha aliekuwa akimfukuzia kwa nyuma na ilikuwa ni bahati tu kwamba spidi ya Aoiline ilikuwa ni kubwa na mikia yake tisa iliweza kumzingira Lekcha kwa mbele ili asiendelee kumsogelea Roma.
Lekcha mara baada ya kuzingirwa na mikia ya Aoiline alitoa tabasamu la kejeli na palepale kwenye mikono yake lilionekana panga kubwa kama mkuki na kabla hata Aoiline hajashitukia tayari mkia wake ulikuwa ushakatwa vipande vipande na kufanya damu nyingi kumtoka na kumwagika chini.
Aoiline alisikia maumivu makali mno huku macho yake yakiangalia kwa mshangao siraha aliokuwa ameshikilia Lekcha.
Ilikuwa ni ile siraha ambayo ilimaarishwa uwezo wake kwa kumwagiwa damu ya maelfu ya majini na kisha kukaushwa kwenye moto wa Lava.
Msisimko wa panga hilo ulimfanya kuweza kujua nini kipo ndani yake na alijikuta akishangaa kwani hakuamini kama Mfalme Wuja katika maisha yake alikuwa akitengeneza siraha ya namna hio na sio tu kwa kutumia majini wa koo zingine lakini mpaka majoka ambao walikuwa ni watu wake.
“Akajiona mjanja sana huku akidhani kwamba sijui ataniua , nilifanya makusudi kumpatia maelezo ya kumfanya anishuku ili kunifuata mwenyewe kwa ajili ya kuniadhibu ili niweze kumteka akili yake bila wengine kujua , sasa hivi siraha hii ya damu ni ya kwangu na ninakwenda kukuchinja nayo leo hii na baada ya hapo nitatengeneza tundu kubwa kwenye huu mnara na kuondoka”Aliongea.
Ilionekana Lekcha ndio aliekuwa ni Joka Mjumbe wa Barafu na kwa maneno yake ilikuwa ni mpango wake kumwambia maneno ambayo yatamfanya mfalme Wuja kumshuku , na mwisho wa siku Mfalme Wuja aliingia katika mpango wa Lekcha na kuishia kumezwa nafsi yake pamoja na sura yake.
Upande wa Aoiline alikuwa akitetemeka kwa hasira kubwa mno , mwanamke huyo alikuwa akiulinda muonekano wa mwili wake kuliko hata anavyolinda maisha yake.
Ijapokuwa alikuwa amebadilika na kuwa katika mwili wa kibindamu lakini bado urembo wake wa Mbweha wa mikia Tisa ulikuwa kwenye mifupa yake , mikia yake tisa ya manyonya ya rangi nyeupe ilikuwa ndio hadhi yake na utu wake , kitendo cha Lekcha kutumia mbinu zake za hila na kukata moja wapo ya mkia wake ilimfanya kupatwa na uchizi.
“Wewe mnyama umennichokoza mwenyewe , nninakwenda kukumaliza leo hii”Aliongea Aoiline kwa hasira kubwa mno.
Na palepale alirudisha mikia yake ndani na kumsogelea Lekcha kwa ukaribu na kuanza kupigana nae ana kwa ana.
Vidonge ambavyo alipewa na Roma viliweza kumsaidia sana katika mapambano hayo kwani mwili wake ulikuwa na nguvu ya kuweza kushindana na upanga wa kichawi uliokuwa umeshikiliwa na Lekcha ambao ulikuwa ukitoa nguvu ya kijini ambayo haikuwa ya kawaida kabisa.
Licha ya kurudishiana mapigo mazito mazito kama vile ni mabomu lakini ajabu ni kwamba hakukutokea hata mtikisiko wa aina yoyote kutoka kwa mnara huo.
Lekcha mwenyewe alijikuta akishangazwa na ugumu wa mnara huo , aliona kama ni kitu ambacho hakitowezekanakutumia kisu chake hicho kuharibu mnara huo kama ilivyokuwa mpango wa Mfalme Wuja.
Ukweli ni kwamba hakuwa na haraka kabisa ya kutoka kwenda katika ulimwengu wa kawaida , aliamini kama ataendelea kubakia katika ulimwengu huo wa majini pepo basi anao uwezo wa kuweza kunyonya kila aina ya nguvu na kufikia katika levo ya juu kabisa ya kuweza hata kuuharibu na kutoka.
“Roma unafanya nini?, mnaweza kuondoka niachieni huyu mnyama nitamuua leo hii”Aliongea Aoiline mara baada ya kumuona Roma anamwangalia akipigana na Lekcha.
Roma hakuona maneno ya Aoiline kuwa ya kimakosa , ijapokuwa aliona huruma kumuacha kupambana mwenyewe lakini alijua fika kama ataendelea kubakia hapo na Aoiline kuendelea kupungukiwa na nguvu zake basi inaweza kumpa shida kutoka ndani ya muda katika mnara huo, isitoshe Lekcha kwa wakati huo alikuwa katika mwili ambao ulikuwa ni ngumu kufa.
Roma hakupenda kuishi akiwa na deni hivyo kwa kuondoka hapo aliamini atakuwa na deni kubwa kwa Aoiline ambalo kamwe hawezi kulilipa.
Roma alijiuliza kwanini Aoiline akatumia nguvu kubwa sana ya kuwafikiria kuhusu usalama wao na hata wakati huo kupambana na Lekcha ili mradi tu waweze kufanikiwa kutoka , Roma aliwaza lakini alikosa majibu.
Upande wa Lekcha alionekana kutokuwa na wasiwasi wakati akipambana na Aoiline na aliishia alimwangalia Roma kwa tabasamu la kejeli.
“Roma unajaribu kutaka kuvuka kwenye huu mnara , huwezi hata kushindana na mimi lakini unafikiria huo upuuzi , unakitafuta kifo chako mwenyewe?”Aliongea .
Roma alijikuta akikunja ngumi yake kwa hasira kama vile alikuwa ameghairisha safari na kutaka kupigana nae lakini palepale aliita chungu chake na kisha akachukua kidonge kimoja na kukimeza kubusti uwezo wake na kisha akausogeezea mdomo wa Cauldron upande wa Lekcha.
“Unajuaje , pengine imepagwa wewe kupigwa na radi ili mimi niweze kutoka kwenye hu mnara”Aliongea Roma na palepale alitoa vidonge viwili na kisha akamwekea Sophia mdomoni ili kurudisha nguvu zake lakini kwa wakati mmoja kumfanya awe na mwili imara.
Na kabla hata ya Sophia hajajua nini mpango wa Roma tayari alishamshikilia kwa nguvu na kuruka nae.
Haikuwa kuruka kuelekea juu bali Roma na Sophia wote kwa pamoja walitumbukia katika Cauldron kana kwamba wao ndio wamenezwa.
Ukubwa wa chungu hicho ulikuwa chini ya udhibiti wa Roma mwenyewe ndio maana waliweza kukaa watu wawili ndani yake bila shida
Lekcha alijikuta akishangazwa na jambo hilo na wakati huo akiwa ameshangaa Aoiline alichukua nafasi hio na kupasua kichwa chake lakini hata hivyo ilikuwa bure kwani sekunde ile ile mwili wake ulirudi upya tena huku akishindwa kuelewa kwanini Roma na Sophia wameingia wao ndani ya chungu cha kijini lakini dakika hio hio aliweza kujua mpango wao.
Chungu kile kilianza kuelea hewani kama vile ni ungo wa kichawi na kuanza kuzunguka kwa spidi huku kikielea angani kuelekea juu zaidi ya mnara.
Roma na Sophia walikuwa wamekaa ndani ya chungu hicho katika hali ya utulivu huku wakikitumia kama ngao ya kujikinga na chochote ambacho kinaweza kuwakuta ndani ya mnara huo.
Roma licha ya kufanya maamuzi hayo lakini bado alikosa ule ujasiri wa kukaa ndani yake kwa muda mrefu.
Upande wa Aoiline yeye hakuwa katika hali ya mshangao , ukweli ni kwamba hata yeye huo ulikuwa ni mpango wake , alitaka kumwambia Roma tokea mwanzo kwamba anaweza kutoka nje ya ulimwengu huo kwa kukitumia chungu hicho kama ngao , lakini hakutaka kusema mapema kwani kama ingejulikana basi kila mtu angetaka kumshambulia na kutaka kupata nafasi ya kupata chungu hicho.
Isitoshe majini pepo hao licha ya kukukaa katika ulimwengu huo ambao ulikuwa na kila kitu , lakini ukweli ni kwamba ni kama walikuwa gerezani na hawakuwa na furaha na kila mmoja ndoto yake ni siku moja kuweza kutoka kwenda katika ulimwengu wa kawaida.
Kulingana na wazo ambalo alikuwa nalo Aoiline lakini piua maarifa yake ya kuishi miaka mingi alikuwa akielewa kwamba Cauldron ni dhana ambayo ni immortal(isiokufa) na ndio maana majini wa enzi hizo waliitumia kuwa mtego wa mnyama wa maafa ambaye alishawahi kuwepo na kuwa tishio kwa usalama wao.
Hivyo kwa mantiki hio kama chungu hicho kilikuwa na sifa ya ui ‘immortal’ ndani yake basi kisingepata tatizo kupitia mapigo tisini na tisa ya radi ya rangi ya zambarau kama Roma angekitumia katika usahihi.
Kwa wakati huo Dhana hio ilikuwa chini ya maelekezo ya Roma kwasababu ilimchagua kama Master hivyo roho iliokuwa ndani yake ndio ingekuwa ni kama ngao yake ya kumlinda na kuweza kuhimili mapigo yote tisini na tisa na hatimae kuweza kutoka katika mnara huo akiwa salama.
Zaidi ya yote ni kwamba roho ya mnyama iliokuwa ndani ya chungu hicho isingependa kuishi kwa kukamatwa na mnara huo maisha yake yote hivyo kwa namna yoyote ile lazima ingeweza kutafuta njia ya kutoka , isitoshe ni roho ambayo ilikuwa na ufahamu wake.
Tokea kuumbwa kwa mnara huo watu wote waliokuwa wamevutwa kuingia katika ulimwengu wa majini pepo ni wale ambao walikuwa ni hatari kwa dunia au mnara uliwaona kama ni hatari hivyo ni rahisi kusema ulimwengu wa majini pepo ulitumika kama gereza kwa viumbe vyote hatarishi kwa binadamu ndio maana haikuwahi kutokea anaevutwa akatoka nje na pengine Roma ni mtu wa kwanza kama angefanikiwa.
Lekcha mara baada ya kuona Caulrdon ikiambaa ambaaa kuelekea Floor ya pili ya mnara huo alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira.
“Roma wewe ni muoga , acha kunikimbia”
Lekcha alijiarib kuruka kuelekea upande wa Cauldron lakini Aoiline alikuwa nyuma yake na aliishika shingo yake kwa nguvu na kuanza kuizungusha kwa nguvu.
Lakini dakika hio hio nguvu ya ant-matter iliweza kuuruidsha mwili wake kuwa kama kawaida lakini hakuwa na muda wa kuwafukuzia Roma na Sophia tena zaidi ya kupambana.
“Unapaswa kuendelea kubakia hapa na kupigana na mimi, nitahakikisha leo hii nakuua”Aliongea Aoiline.
“Malaya mkubwa wewe”Aliongea Lekcha huku akichukia na kutoa panga lake la kichawi na kuanza kupambana nalo.
Yalikuwa ni mapigano makali sana kati ya Lekcha na Aoiline tena ndani ya mnara huo wa hatari katika floor ya kwanza
Upande mwingie katika mwanga hafifu ndani ya Caulrdon , Roma alikuwa amemkumbatia Sophia kwa nguvu huku mwii wake akiuelekezea juu huku akjitahidi kumwambia Sophia maneno ya kumuondoa woga.
“Usiwaze Sophia , nipo hapa na nitakulinda”Aliongea Roma.
Sophia kwa wakati huo alishajua mpango wa Roma ulikuwa ni nini na aliishia kutingisha kichwa chake huku akijikumbatisha kwa Roma.
“Siwezi kuogopa , nitakuwa na wewe Roma hata kama nitakufa”Aliongea na kumfanya Roma kutamani kumfinya lakini moyo wake ulikuwa mzito kutokana na kumuacha Aoiline akipambana na Lekcha peke yake.
Roma kabla hata hajafikiria nini cha kufanya aliweza kusikia ngurumo kubwa kwenye masikio yake na ghafla tu:
“BOOM!!!
Ilikuwa ni kama vile amepigwa na kitu kizito kichwani na kuhisi mwili wake unataka kumlipuka , roho yake ilikuwa ikitaka kumtoka huku nguvu zake za kijini zikianza kufurukuta kwa kiasi kikubwa.
Sophia hakuweza pia kuhimili pigo hilo la radi na aliishia kutema damu nyingi ambayo ilimchafua Roma kifuani.
Upande wa nje wa chungu hicho ni kwamba kilikuwa ndio kinapita katika floo ya kwanza kuelekea ya tatu , sasa kumbe kila floor ilikuwa ikilindwa na tabaka la radi ya rangi ya zambarau ambazo zilikuwa zimekishikilia chumba kana kwamba kuna vifaa maalumu ambavyo vilikuwa vikiwezesha jambo hilo.
Ulikuwa ndio mwanzo tu wa pigo la kwanza lakini bado hawakuwa wamepitia mapigo yote tisini na tisa lakini walikuwa kwenye hali kama hio.
Kulingana na maelezo ambayo Roma aliweza kuyapata, mnara huo ulikuwa na Floor mia moja kwenda juu na katika kila floor ilikuwa ikilindwa na tabaka moja la radi na ili tu kuweza kutoka katika ulimwengu huo inamlazimu kupanda mpaka floor ya juu kabisa swala ambalo litaweza kufanikiwa kama tu ataweza kuhimili kila pigo.
Ilikuwa afadhali alimpatia Sophia vidonge vya kijini la sivyo angekuwa katika hali ya madhara makubwa mara baada ya pigo hilo.
Kwa upande wa Roma hakuwa na jinsi licha ya hatari iliokuwepo hakuwa na namna ya kumuacha Sophia katika uliwmengu huo na kuondoka peke yake.
Sasa walikuwa ndio wanakaribia katika tabaka la pili kuelekea floor ya tatu ya mnara huo na Roma mara baada ya kusikia ngurumo ya radi hakuwa na jinsi tena na alikipa maelekezo chungu kupanua mdomo wake na kuwa mkubwa zaidi ili kuweza kumeza kila radi inayopiga na kweli palepale chungu kile kilikuwa ni kama kimefurahishwa na maagizo hayo kwani roho ya mnyama iliokuwa ndani yake ilinguruma na mara baada ya radi ile kupiga ilimezwa.
Roma alishangazwa na jambo lile, hakuamini kama Cauldron ilikuwa na uwezo wa kumeza radi , lakini hata hivyo hakikuweza kumeza yote kwa asilimia mia moja kwani kuna baadhi ya mapigo yalimfikia yeye na Sophia.
Roma furaha yake haikudumu kwa muda mrefu , aliweza kupata tumaini la kuweza kuhimili lakini kitu cha ajabu ni kwamba mara baada ya Chungu hicho kumeza radi nguvu yake iliongezeka maradufu zaidi na mpaka hapo aliona hio ni hatari kabisa.
Ilionekana dhahiri roho ya mnyama iliokuwa ndani ya chungu hicho ilikuwa ikichukulia jambo hilo kwa faida yake , ilikuwa ikitumia changamoto ya Roma kuweza kujijengea nguvu nyingi ya nishati.
Lakini licha ya hivyo sio kwamba asilimia yote ya nguvu za radi zilizokuwa zikimezwa na chungu hicho zilikuwa zikienda kwa roho ya mnyama , kuna asilimia kadhaa na zenyewe zlikuwa zikimrudia Roma lakini licha ya hivyo ilikuwa ni hatari kwani aliamini mbeleni huko angeshindwa kuwa na uhakika kama akili yake itaweza kutekwa na roho hio basi roho yake itazimwa moja kwa moja.
Katika hali kama hio Roma hakuwa na chaguo asingekuwa na uwezo wa kupambana na radi bila Cauldron kwani madhara yangemfikia Sophia.
Roma mara baada ya kungalia macho ya maumivu yaliokuwa yakitoka kwa Sophia alijikuta roho yake ikifurukuta na kujiambia katika moyo wake ataweza kukidhibiti na kukitawala chungu hicho hata mara baada ya kutoka katika mnara huo.
******
Upande wa dunia ya kawaida katika dhehebu la Shushani kulikuwepo na kambi ya muda mfupi ya wanajeshi wa vikosi vya Tanzania vya kichawi pamoja na kikosi cha kupambana na uchawi kutoka jeshi la China maarufu kama Yellow flame iron Brigade.
Maamuzi hayo yalifanyika ili kuweza kupata ishara yoyote ambayo inaweza kuonekana katika mnara huo na kuifanyia kazi.
Master Abbess Yumiao na yeye alikuwa ni moja wapo ya watu walioweka umakini katika kuangalia mnara huo.
Ilifikia hatua baadhi ya wataalamu kutoka China kutaka kuchimba kuelekea chini ardhini ili kupata kujua namna ambavyo mnara huo ulivyotengenezwa kwa miaka mingi lakini Master Abbes alikataa kabisa na kusema dhehebu lake limepewa jukumu la kulinda mnara huo hivyo haruhusu mtu yoyote kuweza kuugusa.
Ukweli ni kwamba hata yeye alikuwa na wazo hilo lakini imani yake ilikuwa ikimwambia wanaweza kweli kuuharibu mnara huo lakini mwisho wa siku wakakosa majibu ya kile wanachokitafuta hivyo wakaishia kukaa kimya na kusubiria mwisho wa matokeo.
Ilikuwa ni wakati wa asubuhi katika dhehebu hilo, Master Abbes kama kawaida alikuwa ni wa kwanza kuamka na kuendelea kujifunza mbinu mbalimbali za kimapigano kwa ajili ya kujiimarisha zaidi lakini kuvumbua zingine ambazo angeendelea kuwafundisha wanafunzi wake.
Abbess alikuwa ni mwanamke mrembo t licha ya kuitwa Master, alikuwa na muonekano wa ujana na ilisemekena Master Tang Chi na Abbess walikuwa wapenzi.
Abbess alikuwa na muonekano wa kutozeeka kutokana na kwamba alikuwa tayari katika levo ya Nafsi katika mafunzo ya kijini hivyo urembo wake ni sawa na kusema sio wa kawaida , ni kwamba tu hakuwa akijali sana kuhusu muonekano maana hata kichwa chake hakikuwa na nywele.
Alichukua mazoezi alfajiri hio ya saa kumi wakati wengine wote wakiwa katika usingizi kwa muda mrefu na mara baada ya kukaa chini kupumzika alijikuta macho yake yote yakikodolea mnara huo ambayo katika miaka yake mingi ya kuishi hakuwahi kudhania itatokea siku ya kuangalia mara kwa mara kwani ni mnara ambao wake alikuwa ameuzea na kuona hauna kitu chochote cha maajabu.
“BOOM!!”
Ghafla tu wakati akiwa anawaza kwamba haiwezekani Roma na Sophia kuonekana tena kwani muda mrefu umepita iligonga radi ya Zambarau na palepale aliweza kuona watu wakifyatuka kutoka juu ya ule mnara na kwenda kutua chini kama vifurushi.
“Sophia , Mr Roma”Ndio sauti pekee ya juu ya mshituko alioweza kuongea katika hali hio.

SEHEMU YA 622.
Master Abbess alijiona ni kama amechanganikiwa na ugonjwa wa ukichaa wa kuona picha za watu kwenye akili yake ambazo hazina uhalisia, lakini mara baada ya kushangaa kwa dakika kadhaa aliona sio kama alikuwa kwenye ndoto au alikuwa akiona watu katika akili yake.
Dakika hio akiwa katika vazi lake la Robes alikimbia kueleka upande wa Sophia ambaye alikuwa amepoteza fahamu huku bila ya kusahau kuita wengine waliokuwa usingizini.
Baada ya kumfanyia uchunguzi Sophia alijikuta akipigwa na mshituko wa aina yake baaada ya kugundua nguvu aliokuwa nayo Sophia ilikuwa kubwa mno pengine kubwa kuzidi hata ya kwake.
Alishangaa kuona Sophia alikuwa kwenye levo ya Nafsi kwa siku hizo chache ambazo alipotea , jambo hilo lilimshangaza na kumuogopesha kwa wakati mmoja na kujiuliza nini kilichomtokea mwanafunzi wake na kuwa na mafanikio ya aina hio ya haraka sana.
Alijiuliza wamewezaje kutoka katika huo mnara baada ya kupotea kwa siku nyingi na kuweza kupata mafanikio ya aina hio.
Aliijiuliza au ni Hades aliemfanyia hivyo Sophia mpaka kuweza kuwa na uwezo wa aina hio.
Master Abbess ni moja wapo ya watu waliokuwa wakimfahamu Roma , katika mafunzo yake asingeshindwa kufahamu jina lake kwani alikuwa ni mwanafunzi wa mwanaume ambaye alikuwa ni mpenzi wake yaani Master Chi.
Master Abbess mara baada ya kuona Sophia hakuwa katika hatari yoyote ya kiafya alijikuta akivuta pumzi ya ahueni na sasa alimkumbuka Roma ambaye amedondokea upande mwingine akiwa hana fahamu na mara baada ya kumsogelea alijikuta akishikwa na bumbuwazi.
Roma hakuwa amepoteza fahamu bali kwa nguvu zake na uzoefu wake Roma alionekana kuna kitu ambacho alikuwa akipambana nacho katika akili yake , kwani kuna muda hata kichwa chake kilikuwa kikitingishika kama mtu aliekuwa ndotoni.
Haikuwa hivyo tu mwili wa Roma ulionekana kutoa nguvu ya kiroho ya giza na kuuzingira mwili wake kwa kiasi kikubwa cha kumuogopesha.
Roma alidumu vile kwa dakika chache na palepale aliweza kuyafumbua macho yake , lakini ajabu ni kwamba hayakuwa macho ya kibinadamu bali macho ya mnyama ndio aliokumbana nayo Master Abbess na kujikuta akirudi nyuma.
Wakati akishindwa kujua cha kufanya akiendelea kumwangalia Roma , palepale Roma alitoa ngurumo kama ya mnyama na kisha macho yake yakajifunga kwa mara nyingine na alionekana kupoteza fahamu.
Dakika hio hio kundi la wanajeshi wa kichina na wa kiafrika waliweza kumsogela Master Abbes huku wakiwa wanapiga kelele ya mshangao na mara baada ya kuona mwanaume na mwanamke wakiwa wamelala kwenye ardhi kila mmoja alitoa macho ya mshituko huku wakigeuza macho kwenye ule mnara uliokuwa mbele yao.
“Msaidieni Mr Roma na Sophia na kuwapeleka katika vyumba vya mapumziko na kisha toeni taarifa nchini Tanzania na kuwaeleza wamerudi”aliongea Master Abbes akipotezea mshangao wao.
Wanajeshi wale hawakuwa na muda wa kushangaa na palepale waliitt maagizo na kisha waliwabeba Sophia na Roma na kuwaingiza ndani kwenye Matemple hayo ya Dhehebu la Shushani.
******
Hakuna ambaye alikuwa akijua kama Roma alikuwa kwenye mapambano ya nafsi yake pamoja na nafsi ya mnyama iliokuwa inaishi katika dhana ya kijini ya Cauldron.
Katika ulimwengu wa mawazo, roho ya mnyama kama kawaida ilikuwa imeiba sura ya Roma na awamu hio roho ilioekana kuwa na nguvu kubwa kuliko mara ya mwisho nafsi ya Roma ilivyomshuhudia.
Ilikuwa ni sahihi kusema Nafsi hio imepanda levo katika kuvuna nishati za mbingu na ardhi mara baada ya kupitia mapigo tisini na tisa ya radi ya zambarau katika mnara wa Demonic Lock..
Roma aliweza kuona mwili wake ulikuwa umetawaliwa kwa kiasi kikubwa na roho hio ya mnyama kwani nafsi yake ilionekana dhaifu kidogo huku ya mnayama ikionekana kuwa na nguvu kubwa.
“Wewe mtoto , nadhani hili hujatarajia kuliona likitokea , ijapokuwa mapigo tisini na tisa ya radi ya zambarau na bluu ni ya tofauti na radi za kawada lakini nguvu yake inaweza kugeuzwa na kuwa nishati ya mbingu na ardhi ile safi , sasa nusu ya nguvu yote ipo ndani yangu , tuone sasa kama awamu hii unaweza kunishinda”Nafsi ya mnyama iliokuwa katika sura ya Roma iliongea huku ikiangalia nafsi ya Roma kwa tabasamu la kejeli.
Upande wa Roma hakuwa na nguvu lakini alichoweza kutegemea kushinda nafsi hio ni kutegemea imani yake tu na ule utayari wa kushinda , ni kama vile ambavyo mchawi anavyopambana na mtu mwenye imani.
Wakati wakikaribia kutoka katika mnara huo wakiwa juu kabisa ya kilele Roma alikuwa amekosa nguvu kabisa ya kuweza kuhimili pigo la mwisho la radi ya awamu ya tisini na tisa hivyo katika hali ya kutaka kuyaokoa maisha yake ilibidi aruhusu chungu kuweza kumeza asilimia zaidi ya sabini ya nguvu yake.
Ukweli ni kwamba katika mazingira yale ya Radi roho ya mnyama haikuchukulia swala lile kama changamoto kwani radi kwake ni kama kirutubisho cha kurudisha nguvu yake.
Sasa katika wakati huo nafsi ya mnyama ilikuwa katika nguvu za juu sana kwa kuweza kupata faisa ya kupitia mapigo tisini na tisa ya radi.
Roma alijua kwamba kama atakipa nafasi moja tu chungu hicho basi ingekuwa ndio mwisho wake na nafsi yake ingemezwa na roho hio na kutawaliwa moja kwa moja.
“Nini kijana … bado tu unataka kujidhibiti .. nipe mwili wako huu wa kibinadamu uweze kuonja utukufu wa milele”Nafsi ya Cauldron iliongea huku ikitoa tabasamu la kishetani.
“Pumbavu zako wewe utabakia kuwa myama uliefungiwa ambaye unajaribu kutaka kumzidi Master wako badala ya kuendelea kuwa mtumwa wangu milele, Ni kichekesho cha aina yake kutaka kujikweza zidi yangu”Nafsi ya Roma iliongea huku ikitoa tabasamu la kejeli lakini maneno yake yalionekana kuamsha hasira ya nafsi ya myama na ikaanza kucheka kwa hasira.
“Sawa.. sasa hivi unajiona mjanja kijana baada ya kurudi katika huu ulimwengu si ndio , ngoja tuone utaendelea kudumu kwa muda gani , nikuambie tu kama utajaribu kutumia nguvu zako za kijini kwa namna yoyote ile nitakufanya uwe kichaa na huo ndio wakati ambao nitautumia mwili wako , kama huamini jaribu kufanya hivyo tuone nini kitakachokutokea . Hehe … najua kuna watu ambao wanakuwinda na kutaka kuinywa damu yako , kama una akili ni kheri uniachie ni utawale mwili wako kwa adabu kabisa na nitahakikisha hamna ambaye anaweza kukugusa”
Roma alijua kabisa anaongea ukweli,roho hio ya mnyama ilikuwa imepata jeraha na tokea aanze kuitawala ilikuwa ikitumia nafasi hio kuponya jeraha lake na muda wowote ambao atatumia nguvu zake za kijini basi roho hio itaweza kutawala uwezo wake na anaweza kugeuka kichaa.
Roma aliekuwa katika nafsi alianza kujutia kukitumia chungu hicho tokea mwanzo kule katika fukwe za Australia vinginevyo asingekuwa katika hali kama hio.
Lakini tena bila chungu hicho pengine muda huo angekuwa mfu tayari kwani kilimsaidia katika mambo mengi.
Mnyama huyo alionekana kuridhika kabisa na nguvu zake na alikuwa akisubiria Roma kwa hiari yake kumpatia mwili ili aweze kuutawala, hivyo hakutaka kushindana nae ilihali tayari kuna mtego amemuwekea Roma kwenye nguvu zake za kijini na palepale iliamua kumwachia Roma utambuzi wake wa kifikra na Roma na yeye akarudisha uwezo wake wa kimawazo na fahamu na pale kwa namna ya taratibu aliweza kufumbua macho yake na kuvuta hewa safi na sura ya kwanza kuweza kuiona ilikuwa ni ya Sophia ambayo ilionekana ilikuwa ikisubiria kuamka kwake kwa hamu zote.
“Sophia…”Roma alijikuta akishindwa kujiuzuia na kutoa kicheko cha furaha mara baada ya kuona Sophia hakuwa katika hali yoyte ya hatari.
Aliamka taratibu na kukaa kitako huku akianza kuangaza mazingira ya chumba hicho lakini si palepale akajaribu kutumia uwezo wa kijinni kujaribu kukagua mazingira ya eneo alipo lakini ilikuwa ni kitendo ambacho kilimfanya akili yake kuanza kufyonzwa na nguvu ya ajabu na kama sio uwezo wake wa nguvu ya andiko la urejesho basi angepoteza tena fahamu kwa mara nyingine na pengine angeamka akiwa mwingine.
Roma mara baada ya kushinda jaribio hilo kijasho cha ubaridi kilimtoka katika paji la uso wake .
“Roma upo sawa? , unaonekana haupo sawa ghafla tu”Sophia aliongea huku akihoji.
Roma hakuthubutu kumwambia Sophia kile ambacho kilikuwa kikiendelea , kwani ni dakika hio hio ambayo nafsi ya mnyama ilitaka kuimeza akili yake.
Sasa hapa ndio ujue kutofautisha utofauti wa majini wazuri na wale wabaya , majini wabaya ni kama hicho ambacho Roma anapitia, kama Roma angefaka kuwa mtu mbaya basi angeruhusu roho ya kipepo ambayo ndio hio nafsi ya mnyama kuutawala mwili wake ili kuweza kuwa na nguvu lakini kwasababu hakuwa akitaka hilo litokee ndio maana alikuwa akishindana nayo.
Sasa majini wazuri wanajifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi ili kuishinda ile laana ya kipepo iliopo ndani yao na wale wabaya wanaipa nguvu ile laana iliokuwa ndani yao ili waweze kuwa na nguvu kubwa zaidi na kutokana na hilo wakaamua kufungiwa katika ulimwengu wa majini pepo.
Upande wa Roma katika hali kama hio aliamini kitu pekee ambacho anaweza kutumia katika kupambana ni kujaribu kujifunza kanuni za anga na kuzielewa , ijapokuwa alikuwa na uelewa mdogo lakini aliamini kama atatumia muda mwingi kuzielewa basi ingeweza kumsaidia kupambana na maadui zake ambao wangejitokeza katika kipindi hicho ambacho asingeweza kutumia nguvu za kijini.
Katika kipindi kama hicho kutumia nguvu za kijini ilikuwa ni zaidi ya hatari kwani kuna mtego wa nafsi ya mnyama iliokuwa ndani yake.
Katika maisha yake Roma aliweza kupitia changamoto nyingi na hata hio ambayo alikuwa akipitia muda huo alijiambia kwamba angeweza kupata njia ya kuishinda na kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida , alikuwa na imani kwama kila tatizo lina njia yake.
Roma mara baada ya kutoka katika dimbwi la mawazo hatimae aliweza kumuuliza Sophia nini kilichotokea na hapo wapo wapi.
Kwa maelezo ya Sophia ni kwamba Roma alikaa katika hali ya kupoteza fahamu kwa siku mbili tokea watoke katika ulimwengu wa kijini pepo.
Ijapokuwa wataalamu wa kijeshi walishauri Roma kupewa matibabu ya nje lakini Master Abbess alikataa na kuwaonya kwamba hakuna namna ambayo wanaweza kumsaidia Roma bali yeye mwenyewe ndio anaehitajika kupambana mpaka kurudi katika hali yake.
Alishaona nguvu ya giza iliokuwa ikitawala mwili wa Roma , nguvu ambayo ilikuwa kubwa zaidi kwa mtu yoyote kuweza kuishinda ndio maana akazuia aendelee kubakia hapo mpaka atakaporejewa na fahamu.
“Roma huu ni mwezi wa kumi tarehe kumi na nne , inaonekana muda wa ulimwengu ule na huu unalandana”Aliongea Sophia na Roma hakushangaa sana.
“Umemuambia Master wako kilichotokea katika ulimwengu wa majini pepo?”
“Ndio ameniuliza na sikuwa na namna ya kumficha, si haina tatizo si ndio?”
Roma alijua maarifa ya Sophia hayakuwa makubwa kuliko ya kwake hivyo aliishia kumpa ishara ya kupunguza hofu na wasiwasi.
Upande wa vikosi vya kichawi kutoka Tanzania na China waliishia kurekodi maelezo ya Sophia na kuyafanya kuwa ya siri kwani maelezo yake yalikuwa ni ya kufikirika sana ambayo hata wao wenyewe walishindwa kuyaamini.
Baada ya Roma kuamka na kuonana na Master Abbess na kufanya maongezi kwa ufupi hatimae Roma alitolewa katika milima ya Shushani kwa kutumia helicopter kuelekea mji mkuu wa taifa hilo wa Beijing akiwa na Sophia kwa ajili ya kuanza safari ya kurudi nchini Tanzania.
Sophia hakuwa na haja tena ya kukaa katika Dhehebu la Shushani kwani alichokifuata alishakipata katika ulimwengu mwingine na sasa alikuwa na furaha kwani alikuwa katika levo ya juu ya mafunzo ya kijini tena akiwa na mbinu tofauti kuliko wengine wote kwa kuweza kurithi uwezo wa Mbweha wa mikia tisa lakini pia alikuwa ni mpenzi wa Roma.
Roma kwa upande wake moyo wake haukuacha kumuwazia Aoiline katika ulimwengu wa majini pepo , licha ya kuwa na wasiwasi alijiambia Aoiline lazima alikuwa na mpango wake kichwani wakati anamruhusu kuondoka hivyo ana uhakika Lekcha atakuwa amedhibitiwa , licha ya kutokuwa na uhakika aliamua kufikiria upande chanya na kuachana upande hasi, lakini kwa wakati mmoja akimshukuru kwa yote ambayo amemfanyia.
Angalau sasa inaonekana Lekcha ambaye alikuwa ni hatari hakuweza kutoka na yeye kurudi katika ulimwengu wa kawaida , hii ilikuwa ni taarifa nzuri kwani hakutakuwa na usumbufu tena.
Taarifa zilikuwa zimekwisha kutolewa nchini Tanzania tokea kurudi kwa Roma na Sophia hivyo mara baada ya kufika Airport ya Beijing aliweza kukutana na Kassimu mpenzi wake Donyi aliefika kwa ajili ya kumrudisha Tanzania kwa ndege binafsi iliotolewa na raisi Senga.
Roma na Sohia sasa waliweza kubadili mavazi mara baada ya kuingia hotelini na kujisafisha , kwani mavazi waliokuwa nayo ni yale waliopewa na Aoiline katika ulimwengu wa majini pepo kiasi cha kufanya watu wa dunia kuwashangaa kwa mtindo wao wa kizamani.
Wakati Roma akipanda ndege upande wa Sophia yeye alipokelewa na wazazi wake na kutaka kurejea nae kwenda Japani kwa muda kabla hajaanza safari ya kwenda Tanzania , hivyo Roma aliondoka peke yake.
******
Upande wa Tanzania taarifa za kurudi kwa Roma zilipokelewa kwa shangwe zote na hazikumfikia Afande Kweka tu bali ndugu wote wa karibu waliweza kupatiwa taarifa hizo na kusafiri mpaka Iringa kumpokea pamoja na kujjionea wenyewe kama kweli karudi.
Raisi Senga ambaye ashapoteza mtoto tayari wa kiume alietarajia kuwa mrithi wake alijikuta hata yeye akijawa na shauku ya kurudi kwa Roma kwani ndio mtoto pekee wa kiume aliebakia ambaye ni kama tumaini la ukoo wake na kila kitu ambacho angeacha hapa duniani kukiendeleza.
Raisi Senga akiongozana na rafiki yake Raisi Jeremy waliweza kufika Iringa kwa ajili ya kumpokea Roma.
Raisi Jeremy kutokana na kukosa nafasi ya kushiriki katika maombolezo ya kifo cha Denisi alitumia nafasi hio kama kisingizio cha kuja Tanzania mkoani Iringa , lakini ukweli ni kwamba yeye pamoja na Master 4 walikuwa na shauku ya kumuona Roma kwani za ndani kabisa zinasema alikuwa kwenye hali ya kupoteza fahamu kwa siku mbili mfululizo.
Hivyo hawakutaka kuambiwa alipotokea bali walitaka kushuhudia wao wenyewe.
Roma akiwa kwenye ndege aliweza kupewa kila kilichokuwa kinaendelea Iringa na Kassimu aliefika China kumsindikiza.
Wakati huo akiwa kwenye ndege kama kawaida alionyesha utulivu wake , ni kama vile amerudi katika ufalme wake maana huko alikotoka mtawala alikuwa ni Aoiline hivyo maisha ya kule na huku yalikuwa ya tofauti sana.
Ijapokuwa katika ulimwengu huu kuna mbabe wake Athena lakini bado hakumhofia na kuamini siku moja tu atampiga mwanamke huyo kipigo cha juu mpaka aombe msamaha na baada ya hapo hakutokuwa na mwingine duniani ambaye ataweza kumzidi kimapambano..
Alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi kama mwana usalama huku akiwa na miwnai ya jua na mkononi akiwa ameshikilia pakiti ya sigara alioweza kupewa kama zawadi na bwana Cai Yuncheng , Kamanda mkuu wa kikosi cha wachawi kutoka China.
Wakati Raisi Senga akiwa na hisia mchanganyiko za kusubiria ujio wa Roma , upande wa Afande Kweka yeye alikuwa sasa ameacha ile hali yake ya wasiwasi na kwa mara ya kwanza kutoa tabasamu la kizee.
Na siku hio katika familia hio ni kama kulikuwa na sherehe ya kumkaribisha mwana mpotevu kwani ng’ombe dume mkubwa alichinjwa na vyakula mbalimbali viliandaliwa.
Upande wa Edna na yeye alikuja kupewa taarifa siku ya pili baada ya Roma kuanza safari ya kurejea nchini, walifanya hivyo ili kutomfanya kuwa na mawazo.
Sasa Edna wakati akipatiwa taarifa ya kurejea kwa Roma alikuwa akimuogesha Lanlan na kidogo tu atumbukie kwenye Bathtub kwa mshituko.
Edna akawa ndio mtu ambaye alikuwa na shauku kubwa sana ya kumsubiria Roma kurudi na kumuona tena , alikuwa amemkumbuka mume wake , ijapokuwa hakuwa mkamilifu katika mambo mengi lakini alifurahi alikuwa kwenye maisha yake na kumpokea alivyo , hivyo kurudi kwake ni taarifa ambazo zilirudisha furaha yake kwa mara nyingine.
Taarifa haikutolewa kwa Edna tu bali kwa Neema Luwazo na Nasra walipewa taarifa hio ili kuwaondolea wasiwasi.

SEHEMU YA 623,
Safari nzima Kassimu alijitahidi kumuuliza Roma juu ya kile kilichotokea na alikuwa wapi lakini Roma hakumueleza kwa kuona kwamba kijana huyo mdogo asingeweza kumuelewa.
Roma mara baada ya kushuka katika uwanja wa ndege wa Songwe moja kwa moja walisafiri kwa chopa mpaka Iringa mjini na kisha wakachukua gari iliowapeleka mpaka nyumbani na mara baada ya kufika nje ya geti aliweza kushuhudia magari ya aina nyingi ya kifahaari ambayo yalikuwa yameegeshwa ikiashiria ugeni uliokuwa huko ndani ulikuwa mkubwa.
“Bro naona watu wengi wanasubiria kwa hamu ujio wako”Aliongea Kassimu na Roma alitingicha kichwa na kisha akajiangalia kwenye kioo kwenye gari la pembeni kama muonekano wake upo vizuri na kisha akatoa sigara moja kwenye pakti aliokuwa nayo na kisha akaiwahsa na kuvuta moshi.
Kwa mwonekano wake ni kama vile ni Gangstar flani hivi ambaye ndio sasa anarudi nyumbani.
Upande wa ndani, Afande Kweka alikuwa ameketi kwenye sofa katika sebule kubwa ndani ya jumba hilo huku akiwa ameshikilia kikombe cha chai.
Edna alikuwa amekaa pembeni ya Blandina upande wa kushoto akiwa ameshikilia Lanlan huku baadhi ya wageni na wana ukoo wakiwa wameketi kila mmoja kwenye siti yake.
Raisi Jeremy kutoka Rwanda pia alikuwepo akiwa chini ya ulinzi wa Master 4 ambaye muonekano wake ulikuwa umebadilika kwa asilimia kubwa , hakuwa tena ni yule wa kuvalia mavazi yasiokuwa ya kawaida , hapo ndani alikuwa amepiga suti huku akiwa na muonekano wa kisomali uliompatia utanashati wa hali ya juu.
Roma licha ya kuoga na kubadilisha mavazi hakuwa amebadilika sana na hata mara baada ya kuingia eneo la sebuleni nywele zake zilikuwa zimejikunja kunja na hakuwa amezichana kabisa.
“Haha.. naona mpo watu wengi mliokuwa mkinisubiri kwa hamu.. nakuona waziri Wambe pale .. Afande Tozo pia upo”Aliongea Roma huku akiweka tabasamu la bashasha akiongea bila aibu na kuvua miwani yake na kuanza kumpa mkono kila aliekuwa karibu yake.
Watu waliokuwa hapo ndani walikuwa hata wakiogopa kupeana nae mkono kwani walimuogopa lakini licha ya hivyo kila aliepewa mkono aliupokea kwa kutetemeka wakikosa ujasiri wa kwenda kinyume na Roma maana walikuwa wakimjua vizuri na nguvu yake pamoja na wepesi wa kutoa adhabu.
Roma mara baada ya kumfikia Raisi Jeremy macho yake kwanza aliyahamisha kwa Master 4 ambaye alikuwa nyuma yake kama bodigadi , ijapokuwa Roma alimuona bwana huyo kuwa na uwezo wa juu wa kimapigano lakini alijiambbia kama ataingia nae katika ugomvi basi itakuwa ngumu kupambana nae maana yeye asingeweza kutumia nguvu za kijini.
Lakini upande wa Roma licha ya kuwa na kitu kinachoendelea lakini alijitahidi kadri awezavyo kuonekana hana wasiwasi wa aina yoyote na ni yule yule wa jana na leo.
Upande wa Master 4 alikuwa hapo kwa ajili tu ya kumuona Roma alivyo na wapi ametokea na je uwezo wake ulikuwa umeongezeka zaidi na zaidi maana alikuwa ni mtu maarufu sana katika ulimwengu wao wa majini.
Ni dakika hio hio Master 4 alijikuta akipatwa na hisia tofauti kutoka ka Roma ,ilionekana nguvu zake zilikuwa zimebadilika kuliko alivyokuwa mwanzo.
Hakuwa na uwezo wa kuona Roma alikuwa kwenye levo ya ngapi, wala hakuweza kuhisi kama Roma alikuwa na mtego kwenye nguvu zake, bali alichoweza kuhisi ni kama kuna kiwingu cheusi ambacho kimezishikilia nguvu zake.
Alishindwa kzuia shauku yake na kisha akatumia ujini wake kujaribu kumchunguza Roma lakini dakika hio ambayo alitaka kujua uwwezo wa Roma alijihisi ukichaa ukitaka kuitawala akili yake , ilikuwa ni kama kuna nguvu ya ajabu ilimwingia na kutaka kumfanyia uharibifu kwenye roho yake na kumezwa.
Shukrani kwa mbinu zake na uzoefu aliweza kujitoa haraka haraka na kujirudisha katika halli ya kawaida huku jasho jembaba likianza kumtoka na alionyesha hofu ya aina yake.
Alijitahidi kuficha hofu yake na kumwangalia Roma kwa tabasamu bandia. Huku akijiuliza kwanini huyu mtoto alikuwa akitisha na kuwa na madhara makubwa kwake?
Ilikuwa wazi kwamba uwezo wake ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa lakini cha ajabu ni kwamba umejificha ndani kabisa kiasi cha kufanya wengine kuwapa shauku ya kutaka kuutafuta lakini mwisho wa siku wale wanaojaribu walijikuta wakipambana na kitu kisichokuwa cha kawaida.
Alijiuliza ni matukio gani ya kushangaza alikutana nayo huko alikoenda , ni ufunuo gani ambao amepata na ni kwa namna gani uwezo wake umeongezeka nguvu kwa namna hio kwa siku chache alizopotea.
Alijiambia kama ataendelea kuwa na nguvu kwa namna hio basi anaweza kuamini wale ‘Super Masters’ kutoka katika ulimwengu wao ambao ni maarufu kwa zaidi ya karne na karne basi wanaweza wakapata shida ya kupambana na Roma.
Alimwangalia Roma huku akiogopa na kujiambia anapaswa kukaa nae mbali maana alikuwa akiogopesha na yeye alikuwa akiyataka maisha yake.
Roma hakutumia nguvu zake kwa wakati huo lakini haikumaanisha kwamba uwezo wake hana , alikuwa na uwezo wa kuutumia lakini alihofia akifanya hivyo nafsi ya mnyama ingeweza kumtawala moja kwa moja na kugeuka kuwa kichaa.
Kuhusu uwezo wake , ukweli ni kwamba ulikuwa umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana tofauti na alivyoondoka , hata yeye mwenyewe hakuelewa kama kupita kwenye ule mnara kumempeleka mbali sana zaidi ya mara mia moja katika kuwa na nguvu za kijini jambo ambalo hakuna jini ambalo linaweza kupata bahati ya namna hio.
Ni sawa na kusema uwezo wa Roma sasa ulikuwa umebakisha mapigo ya radi ya aina moja tu na kufikia levo ambayo Aoiline alikuwa akimwambia kwamba inaweza kumkutanisha na yule mtu.
“President Jeremy , I am so flattered with your presence here”Aliongea Roma kwa kingereza mara baada ya kupeana mkono na Raisi Jeremy.
“Hehe.. Bila shaka , wewe ni mume wa binti yangu Edna hivyo nilipaswa kuwepo”Aliongea huku akigeuzia macho yake kwa Edna huku ikishindwa kujulikana alifanya makusudi kuongea hivyo au ni kutokana na ukweli kwamba alikuwa baba kwa Edna.
Roma alimlaani bwana huyo kimoyo moyo kwa hila zake za maneno mbele ya Edna, lakini hata hivyo aliachana nae na kisha kumalizia kusalimiana na Afande Kweka na baba yake.
“Mzee nilikuwa nimekamatika kwenye matatizo , je kila kitu kinaenda sawa hapa nyumbani?”
“Kila kitu kipo sawa na angalau hujachelewa kurudi, unapaswa kutoa shukrani pia kwa kila mtu aliefika hapa kwani uwepo wao ni kuonyesha ni kwa namna gani wanakujali”Aliongea na kumfanya Roma awaze na kujiambia haikuwa na haja kwa wao kuja kumpokea kwani hana mpango wa kuwajali hata kama wao walionyesha kumjali.
Baada ya kuambiwa hivyo ilibidi kwanza ageuke na kuwakaribisha kwa kuwaambia wabakie kwa ajili ya chakula cha mchana kwa anaetaka.
Ukweli ni kwamba watu hao sio kama walikuwa wakimjali wala nini , ila walifika hapo ili kuangalia kama huyo mwanaharamu ameumia popote mpaka kumpelekea kupoteza fahamu siku mbili lakini matokeo yake ni kwamba yaliwasikitisha sana baada ya kuona alikuwa salama tena yule yule mwenye majigambo na waliishia kusonya kimoyo moyo maana ukweli ni kwamba hawakuwa wakipenda kutokana na hulka zake.
Hilo lilidhihirika kwani kila mmoja alianza kuweka sababu yake binafsi na kusema kwamba ana dharula na hawezi kujumuika chakula cha mchana na kisha wakaaga na kuondoka mmoja mmoja mpaka wakaisha.
Roma mara baada ya kuona watu hao kila mmoja ameondoka ilibidi sasa amsogelee Afande Kweka ambaye na yeye alikuwa nje akiagana na wageni.
“Mzee naomba unisamehe kwa kuchelewa , nilikuwa mahali ambapo nimeshindwa kujisaidia”
“Haina shida , Afande Tobwe alishaniambia kilichotokea na naelewa , unaweza kurudi ndani kwanza hujasalimiana na binti yako Lanlan”Aliongea.
Roma sasa mara baada ya kusikia jina la Lanlan maneno ya Master chi yalijirudia rudia na alijikuta akiingia ndani kwa haraka na alijikuta sasa akimwangalia Lanlan vizuri kwanzia chini mpaka juu.
Ilikuwa ni kama vile Lanlan alikuwa mpya kwake na hisia za ajabu zilianza kuvaa moyo wake.
Baada ya kuvuta pumzi nyingi na kuzitoa alitembea mpaka alipo mke wake na kisha alimuonyesha ishara ya kumpatia Lanlan.
“Mlete nimkumbatie”Aliongea Roma kwa sauti ya kitetemeshi.
Kwa hali isiokuwa ya kawaida Edna alijikuta akihisi hisia za ajabu kama vile ni za wivu , ni hisia ambazo hakuwa akizielewa .
Alijiambia yaani mtu ndio kwanza anarudi lakini mtu anemuwazia muda wote alikuwa ni Lanlan , alitamani kabla ya Lanlan yeye ndio awe wa kwanza.
Aliona kabisa ni dhahiri kwa zaidi ya mwezi ya mwanaume huyo kuondoka mtu aliemmisi sana ni Lanlan, lakini licha ya hivyo hakuongea neno zaidi ya kutingisha kichwa kimya kimya na kumsogeza Lanlan mbele ya Roma.
Roma alijikuta akitoa tabasamu mara baada ya kumpakata Lanlan aliekuwa mzito kwenye mikono yake ,tofauti na alivyoondoka aliona Lanlan ameongezeka mwili kidogo pengine ni kutoakna na nyama zilizokuwa zikipikwa mara kwa mara ndani ya familia hio.
Alishindwa hata kujielewa ni wakati gani imetokea lakini macho yake yalikuwa yashabadilika rangi na kuwa mekundu kama mtu ambaye anataka kulia.
Roma alishikwa na hatia ya aina yake na kujiambia kwanini alishindwa kumjua Lanlan ni binti yake , muonekano wa Lanlan ulikuwa ukifanana na kila kitu na wa Seventeen alivyokuwa mdogo lakini bado tu alishindwa kuliona hilo.
“Daddy are you crying . do you miss Lanlan?”Lanlan aliuliza mara baada ya kumuona Roma akitoa machozi ya kiume.
“Well , yeah , daddy missed Lanlan so much..”Aliongea Roma huku akijibaraguza na kufuta machozi yake.
“I missed daddy too , but I am hungry”Aliongea Lanlan na kumfanya Roma kutoa cheko.
Ilikuwa ikileta maana, ilikua ni mchana tayari wa saa saba kwenda nae wakati Roma anaingia ndani ya familia hio na Lanlan bado hajakula chochote.
Sasa wakati huo kila mtu alikuwa akishangazwa na mabadiliko ya Roma kwa Lanlan lakini kwa wakati mmoja ikimfanya Edna kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi.
Baada ya kufika kwenye ukumbi wa chakula ndio sasa muda ambao Blandina alijikuta akivuta pumzi na kuchukua nafasi hio kumwangalia mtoto wake kwa ukaribu maana muda wote alikuwa akijaribu kuhudumia wageni kwa kadri awezavyo.
Wanafamilia hao baada ya nusu saa mbeleni waliweza kukaa wote mezani , kutokana na kilichomtokea Roma kufanywa siri Afande Kweka hakuuliza chochote huku upande wa Raisi Senga na yeye hakuongea chochote zaidi kuwa na mwonekano ambao hisia zake hazikueleweka.
Roma aliekuwa ameketi kwenye kiti pembenni ya Edna alijikuta sasa akimgeukia na kumwangalia mke wake na kwa haraka haraka aliweza kuona Edna amekasirika.
Roma alikuwa amejisahau kutokana na ile shauku ya kutaka kumona Lanlan mtoto wake alieachiwa na Seventeen hivyo akasahau kumpa ‘attention’ Edna.
Edna alikuwa ni kweli amekasirika , siku hio alikwua amevalia kikawaida sana , pengine ni kutotaka kufanya watu kumwangalia sana , alikua na mwonekano wa kimama zaidi tofauti na wa kisichana lakini alionekana mrembo kwenye mavazi hayo mepesi.
Vazi hilo alilovaa alilichagua kwa muda mrefu na alilivaa maalumu kwa ajili ya kumpokea mume wake lakini ajabu na alivyotegemea mume wake mara baada ya kuja hakumwangalia hata mara moja na macho yake yote yalikuwa kwa Lanlan na kumsahau yeye.
“Babe Edna naona unazidi kupendeza na kuwa mrembo siku hadi hadi siku , kidogo tu nishindwe kukutambai , je ulinimisi katika siku zote ambazo hatujaonana?”Aliongea Roma kama kawaida yake akiwa amepamba uso wake na tabasamu.

SEHEMU YA 624.
Roma licha ya kujishobokesha kwa Edna hakupewa jibu alilotarajia kwani Edna alijiweka bize na kumsogezea Lanlan Mboga za majani.
“Lanlan acha kula tu nyama muda wote , kula na mboga za majani”Aliongea na kumfanya Lanlan aliekuwa na mafuta mafuta mdomoni kumwangalia mama yake na uso usiokuwa na furaha maana hakuwa akipenda mboga za majani lakini aliishia kuchukua mboga zile zote na kuzipeleka mdomoni na kuzila zote kwa awamu moja na kisha alirejea kwenye utukufu wake wa kula nyama.
Edna aliishia kumshika shavu na kumwambia apunguze spidi ya kula na baada ya hapo aligeukia sahani yake na kuwa bize na chakula akimpotezea Roma.
Roma mara baada ya kuona mwanamke huyo hakuonyesha dalili ya kutaka kuongea nae na alikuwa amenuna alijikuta akila kivivu chakula chake huku akiwaza namna ya kuweza kumrudisha katika hali ya kawaida maana alishajua ni kosa gani alifanya.
Ukweli ni kwamba mzigo wa kisaikolojia aliokuwa nao Roma kwa wakati huo ulikuwa mkubwa mno kwani swala la Lanlan asingeendelea kulibakisha siri kwa muda mrefu.
Isitoshe Seventeen hakuwa mwanamke wa kawaida kwa Roma na Edna hakupenda hata kusikia jina lake kwani alijua fika ni mwanamke wa kwanza kupendwa na Roma na hata mwanzo waliweza kuingia katika migogoro mara baada ya Edna kuona ni kama anafanywa mbadala.
Sasa kama Edna atakuja kujua kama Lanlan mtoto aliekuwa akimpenda kwa moyo wake wote na kuamua kumuasili alikuwa ni binti wa Ex wake hakujua Edna angelichukulia vipi swala hilo.
Kuwaza jambo hilo ilimfanya Roma kuwa na moyo mzito na kutaka kadri awezavyo kumfanya Edna awe ni mwenye furaha , isitoshe ni yeye ambaye alihusika katika kumleta Lanlan katika maisha yake na mwisho wa siku anajua ni binti yake.
Baada ya chakula cha mchana , Blandina alimwambia Edna kumsindikiza Roma kwenda chumbani ili aweze kuoga na kupumzika, ijapkuwa Roma alikuwa vilevile lakini kwa Blandina alisema eti Roma amekonda na anapaswa kutendewa vizuri ili kurudisha afya yake jambo ambalo liliwashangaza watu lakini hakuna aliehoji hata hivyo ni mapenzi ya mama kwenda kwa mtoto.
Lanlan alijikuta akisinzia mara tu baada ya kula chakula cha kutosha na Blandina alimchukua na kwenda kupumzika nae.
Ukweli ni kwamba watu wote waijua Edna kakasirika kutokana na matendo ya Roma kujifanya kutokumuona mara baada ya kufika ndio maana walitaka kuwapa muda wa kuyasuruhisha mambo yao wakiwa chumbani.
Edna ndio aliekuwa ametangulia na mara baada ya Roma kuingia katika chumba chake alifunga mlango kwa funguo kabisa na kisha akamkumbatia Edna kwa nyuma huku akishika kiuno chake , Edna hakuleta ukinzani na kumfanya Roma kugeuka na kumwangalia usoni.
Walijikuta wote kwa pamoja wakiangaliana kwa dakika kiasi cha kufanya pumzi zao kuweza kusikika kwa kila mmoja
Roma alijikuta akishindwa kuvumilia na palepale alimeza mate mengi na kumsogezea Edna mdomo kwa ajili ya kutaka busu huku akishika shingo yake .
Upande wa Edna licha ya kwamba alitaka kufanya kitendo hicho kutokana na kukimisi lakini bado hakuonyesha ile hali ya kuridhika na aliishia kumwangalia tu Roma akihangaika lakini kwa wakati mmoja alionekana kushindana na hisia zake kwani alihisi msisimko.
Roma alijiambia kitu pekee cha kurudisha hali ya Edna ni kumfanyia vitendo vya kimapenzi kuliko kukaa chini na kuongea.
Alipitisha mkono wake kwenye blazier aliovaa na kisha akaanza kusugua sungua manyonyo huku mkono mmoja ukiwa umeshikilia kiuno.
Ngozi ya Edna ilikuwa laini mno kama vile ni ya mtoto mchanga na kumfanya Roma kuzidi kupatwa na hisia , isitoshe alikuwa amekaa muda mrefu bila kufanya hicho kitendo ndio maana hisia zake zlikuwa za juu.
Wakati Roma akiwa bize kufanya manjonjo yake ili mradi tu kumlegeza mke wake mara alihisi maji ya moto yakimdondokea na kumfanya ainue uso wake na kumwangala na hapo ndipo alikutana na Edna ambaye alionekana kulia jambo ambalo lilimshangaza.
“Honey .. kwanini unalia , hey niambie kama hutaki kufanyiwa hivi niache na sio kulia”Aliongea Roma huku akitoa mkono wake ulioshikilia mwili wa Edna.
Roma alitaka kumfuta machozi kwa mkono wake lakini Edna aliuondoa kihasira huku akiyafuta mwenyewe.
“Naonekana mwepesi sana kwako si ndio , unafikiri mimi ni mwepesi kuchokoza? , umekuja tu bila kuniuliza chochote na kuanza kunishika shika unadhani ndio namna ya kunilainisha eh? , unajua ni siku ngapi sikuweza kupata usingizi kwa ajili yako? , naota usiku na nikiamka nazidi kuwa na wasiwasi lakini bado tu nilijifanya nipo sawa mbele ya Lanlan , lakini kuna wewe ambaye ulituacha kwa zaidi ya mwezi bila taarifa yoyote , hivi unajua kama sisi tulitekwa?, unajua kama Lanlan alipigwa ?, yote hayo hujui lakini hata hukutaka kujisumbua kuuliza na hukusema kitu chochote hata baada ya kuniona , kwanini unakuwa mkatili hivyo?”Aliongea Edna huku akionyesha hasira zake waziwazi.
Roma wakati huo alijihisi ni kama kuna kitu kizito kimempiga kichwani , huku hasira zikianza kujikusanya.
“Nani kawafanyia hivyo..”
“Walisema ni wanajeshi waliokuwa chini ya Afande Razaq, walijua haukuwepo ndio maana walituteka kwa ajili ya kulipiza kisasi huku wakitaka pia mbinu yako ya mafunzo , baadhi yao walikuwa hata na mafunzo ya kijini levo ya nusu mzunguko , Lanlan alirushwa ukutani mpaka kwenye sakafu na kupigwa mateke mengi lakini akaamua kukaa kimya..”
“Nini kilitokea baaada ya hapo..”Roma alijihisi moyo wake ukijikunja kunja huku akiuliza kwanini hakuna ambaye amemwambia mara baada ya kurudi tu.
Edna alifuta macho yake na kisha alianza kumwambia Roma kila kitu kilichotokea .
“Afande Tobwe alisema niliwaua watu wote lakini mimi sikumbuki chochote nilichofanya kwani nilipoteza fahamu baada ya hapo na Afande Tozo na wengine hawajui kwanini niliweza kufanya vile..”
Roma mara baada ya kusikiliza alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira , hakuamini kuondoka kwake kidogo tu kuna watu wamekosa adabu mpaka kuja kumchokoza , alijiambia hayo yote ni makosa yake ya kukata nyasi pasipo kuondoa mizizi yake.
Roma mara baada ya kumuona Edna akiwa katika hali ya majonzi alijikuta akimuonea sana huruma , ijapokuwa alishangazwa a namna ambavyo Edna amesema amewaua lakini hakujali kuuliza maswali zaidi, alijikuta akipatwa na ahueni kwa Lanlan kutoongea chochote na alijiambia hakika kweli Lanlan alikuwa ni damu yake , alikuwa amerithi kila kitu kutoka kwake , kwani kama ni mtoto mwingine wa kawaida pengine angeishi kwa hofu baada ya tukio hilo lakini Lanlan alionekana kuwa kawaida.
Roma ilibidi amkalishe Edna kwenye kitanda na kisha akaishika mikono yake na kumfuta machozi kwa upole.
“Najua walikukosea sana kwa kukuchokoza na hakuna mtu ambaye ameniambia kuhusu hili licha ya mambo mengi kutokea , lakini pia kwa upande wangu nilikuwa nikihatarisha maisha yangu , nilikuwa katika hofu ya kuogopa siwezi kukuona tena wewe na Lanlan”
Baada ya kusema hivyo Edna alikuwa ashanyamaza , ijapokuwa alikuwa na hasira lakini alikuwa akijali usalama wa Roma na aliishia kumwangalia kwa macho ya kutaka kusikiliza zaidi.
“Sikutaka kuongea sana kwa watu wa nje juu ya kilichonitokea lakini wewe ni mke wangu na lazima nikuambie kila kitu kilichotokea..”Aliongea Roma na kumfanya Edna kuonyesha tabasamu la furaha, isitoshe hata Blandina na wengine hawakuweza kujua alikotokea Roma na hakuwaeleza hivyo Edna alitafsiri Roma alitaka kumwambia yeye ya kwanza kama mke wake juu ya kila kitu kilichtokea.
Inamaanikika kwamba haijalishi mwanamke ana akili kiasi gani lakini siku zote atapenda kufanywa wa pekee katika akili ya mpenzi wake , maneno ya Roma alijua kabisa ni ya kumpamba lakini mwisho wa siku aliyakubali na kumfanya awe na furaha,hakuweza kujiuzuia kwani huyo ndio mwanaume ambaye anampenda kwa moyo wake wote.
Roma alijitahidi kuanza kumweleza kwanzia namna walivyovutwa kwenye ulimwengu wa majini pepo kadri awezavyo lakini kuhusu Sophia kuwa na mahusiano nae ya kimapenzi hakuongea kwani hakutaka kumkasirisha tena Edna.
Roma hakuelezea pia kama hakuwa na uwezo wa kutumia nguvu zake za kijini tena ili tu kutoleta wasiwasi kwa Edna.
Edna mara baada ya kuelezewa yaliojiri katika ulimwengu huo alijikuta akishangaa mno na kuwaonea huruma kwa yale walioweza kupitia lakini hata hivyo kuna baadhi ya sehemu ziliibua mashaka katika kichwa cha Edna.
“Huyo Aoiline naamini atakuwa mzuri sana si ndio , nina uhakika atakuwa anakupenda ndio maana akaamua kukusaidia , vipi kuna ulichomfanyia mpaka kuwa na upendo wa namna hio?”
“Unaongea ujinga gani , unadhani mimi ni mwanaume ambaye ninaweza kugusa kila mwanamke ambaye yupo mbele yangu , isitoshe yule ni jini tu mwenye umbo la kibinadamu”Aliiongea Roma huku maneno ya Edna yakimfanya kuwa na aibu maana alikumbuka namna alivyopigana denga na yule Mbweha.
Edna hata yeye mwenyewe alifikiria licha ya uzuri waliokuwa nao majini mwisho wa siku watabakia kuwa majini tu ambao wamejitengenezea miili ya kibinadamu .
“Lakini vipi kuhusu Sophia ? wewe na yeye mkoje kwa sasa?”Aliuliza Edna mara baada ya kukumbuka Sophia aliwekaga hisia zake wazi kama anampenda Roma kimapenzi ndio maana jambo hilo lilimpa wasiwasi.
“Acha hizo …”Roma aliongea kwa haraka akijaribu kukataa.
“My Dear wife , kwanini huniamini mimi mumeo? Nilifanya kila kitu ili kuweza kurudi na kukuona , ukiendelea kuongea hivyo utanifanya nijisikie vibaya”Aliongea Roma huku akijifanyisha mpole.
“Kadri unavyojiweka hivyo ndio inaniambia kuna kitu hakipo sawa , Roma siamini unaweza kuwa na ukaribu wa kawaida na Sophia kwa yale yaliotokea..”
Roma alijikuta fuvu lake likipatwa na ganzi kwa muda, alikuwa akiogopa ukweli kujulikana kama ameanzisha mahusiano na Sophia, hakujua Edna angelichukuliaje hilo swala , na kutokana na kwamba hakutaka kuendelea kumuona Edna anaongea aliona atoe siraha yake haraka haraka ili tu kumtuliza.
Licha ya kwamba hakuwa akitumia nguvu za kijini lakini kufungua anga ya ya pete ya Sumeru haikuhitaji nguvu zozote hivyo aliweza kufanya hivyo na kutoa zawadi kwa ajili ya Edna.
Edna alijikuta macho yae yakichanua huku akishindwa kujizuia na kuziba midomo yake kwa mikono yote miwli.
Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona dini kubwa la namna hio la kupendeza ambalo halijapitia kwenye mikono ya wahunzi , kwa ukubwa wa jiwe hilo la Rubi aliamini kama litawekwa kwenye mnada basi linaweza likavunja rekodi ya dunia kwa kuuzwa kwa thamani kubwa lakini kwa kuwa jiwe la kwanza kubwa la Rubi kuuzwa duniani..
Roma aliishia kutabasamu kutokana na mshangao wa Edna na alichokifanya ni kushikilia mikono yake na kuweka lile jiwe la madini ya rubi kwenye mikono yake na kumfanya Edna kulishika kama vile ni kitoto kichanga ambacho ndio kimezaliwa.
“Babe niliua jini Joka moja lenye nguvu na nikaweza kupata hio Rubi kwenye kiota chake , baada ya kulipata nilikuwa nikiwaza kutoka tu katika ulimwengu huo ili nije nikupatie kama zawadi, nadhani ni muda sahihi wa mimi kutimiza hitajio langu, hio ni zawadi yangu kwako mke wangu kipenzi”
Baada ya kusikilizia uzito wa jiwe hilo Edna alijishawishi na kujiambia hakuwa akiota , Roma alishawahi kumuahidi kwamba atampa jiwe kubwa la madini kama jicho la Tembo mara baada ya kumpa Nasra pete ya Almasi lakini licha ya ahadi hio hakuwahi kuamini kama itatokea , , lakini mara baada ya kupatiwa jiwe kubwa la madini ya Rubi aliona nafasi yake kama mke wa Roma imeweza kurudi na sasa yeye ndio anamiliki zawadi ya thamani kubwa kuliko wanawake wake wote.
“Umeipenda?”
“Ndio..”Aliongea huku akitingicha kichwa mara nyingi kama vile alihisi Roma anaweza kubadilisha mawazo na kumpokonya.

Unafikiri nini kilimtokea Aoiline na Lekcha? , Miungu ipo kumi na mbili jumla yao na hatujaiona yote mpaka sasa , je unajua ni stori gani ipo nyuma yao? .
Ndio tunaanza anza kuzikaribia nyama baada ya kumaliza hivi vijimtori vya juu juu hivyo tusipoteze hamu
ITAENDELEA.
 
SEHEMU YA 651.
Roma alimlaani Mzee Kweka kwa kupenda kumuweka hewani na palepale alirusha simu yake pembeni.
Roma mara baada ya kupiga mswaki na kujiweka sawa , alikumbuka Hazina ambayo aliiba huko Kilimanjaro na palepale alichukua lile boksi na kuangalia kilichopo ndani.
Roma alishangaa , kilikuwa ni kitu cheusi kilichokuwa kimewekwa ndani kinacholingana na kokoto lakini yenye muonekano wa kuvutia kidogo.
“Hiki ni kitu gani?”Roma alijiuliza huku akijiambia pengine ni Dhana ya kijini na hakuweza kuhisi nguvu yake kwasababu hakuwa na uwezo wa kutumia nguvu za kijini.
Lakini bado ilimfanya Roma kutodhania ni kitu cha kawaida mpaka kuitwa Hazina kutokana na muonekano wake, maana kitu hicho kilikuwa kama vile ni ishara ya kitu flani lakini hakuweza kujua ni kitu gani.
Roma hakutaka kufikiria sana , alirudisha kama ilivyokuwa hazina hio ambayo hakujua maana yake na kisha akapotezea swala hilo kwa muda.
Baada ya kushuka chini aliweza kumuona Lanlan akiwa tayari ashaanza kunywa chai kwa kushikilia chapati za maji huku Qiang akiwa anamsaidia kumnywesha maziwa.
Kwa jinsi mashavu yake yalivyotuna ilikuwa ngumu kuamini kama alikuwa akimeza vizuri kile ambacho anakula.
Roma pia alishagazwa na uwepo wa Amina na Rufi waliokuwa wamekaa eneo la sebuleni wakiangalia runinga.
“Nyie mnafanya nini hapa asubuhi yote hii?”Aliuliza Roma huku akifinya mashavu yao.
“Ushasahau nimemuahidi Lanlan kumpeleka kucheza , napaswa kutimiza hadi yangu kwani leo ndio nipo free”Roma alimwangalia Lanlan na kuona alikuwa akimwangalia kwa namna ya kumwambia asikatae.
“Hubby , unaonaje tukienda pamoja , tukiwa wengi ndio itakuwa vizuri zaidi”Aliongea Rufi.
“Lazima niende pia , vipenzi vyangu nyie mnaenda pamoja na binti yangu lazima niwasindikize kama bodigadi , wote nyie ni warembo hivyo nina wasiwasi mtaibiwa”
“Unapaswa kuwa na wasiwasi labda na sisi tu lakini sio Lanlan , itakuwa vizuri kama wavulana wa huko hawatamuogopa Lanlan”Aliongea Nasra.
“Nasra wewe hujui tu , lakini Lanlan akishakuwa mkubwa atakuwa mrembo haswa , naamini majitu isiokuwa na adabu itamsumbua sana ili kumharibu mapema iwezekanvyo”Aliongea na kumfanya wote wamwangalie namna ambavyo amekosa aibu.
Baada ya Roma kupata kifungua kinywa aliingia kwenye gari ya Amina na kuendesha kuelekea Kawe eneo maalumu ambalo limekuwa maarufu kwa ajili ya michezo ya watoto.
Baada ya kufika watoto walikuwa wengi mno maana ilikuwa ni kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka.
Lilikuwa ni eneo lenye hali ya hewa nzuri kutokana na kuwa ufukweni na Roma alipata muda mzuri wa Kurelax maana tokea arudi ni mwendo wa hekaheka.
Baada ya Lanlan kucheza kwa muda mrefu ilikuwa ishatimia saa saba mchana na alirudi na kumwambia baba yake njaa inamuuma na Roma aliwachukua na kisha wakasogea upande mwingine eneo hilohilo sehemu yenye mgahawa wa kisasa na kisha walikaa na kuagiza chakula.
Wakati wakiendelea kula Lanlan aliacha kula na kuangalia upande wa nje huku akionekana kama kuna kitu amekiona na kukitamani, ilimfanya na Roma kuangalia upande wa nje na kugundua pembeni yao kuna mtu aliekuwa akichoma mishikaki.
Rufi aliweza kugundua alichokuwa akihitaji Lanlan na palepale alisimama na kuchukua pochi lake.
“Mnaweza kuendelea kula nitaenda kununua kwa ajili ya Lanlan”
Lanlan mara baada ya kusikia kauli ya Rufi aliinua kijiko chake kwa furaha zote na Roma aliishia kutabasamu na kufuta punje za pilau zilizokuwa zimemgandia pembeni.
Ni mara baada ya Rufi kumaliza kupewa mzigo wake wa mishikaki sasa wakati akijiandaa kulipia palepale alisikia sauti pembeni yake.
“I want those two”
Sauti ya kike pembeni yake iliweza kusikika , ijapokuwa mtu alieongea hio kauli alitumia kingereza lakini kidogo tu Rufi adondoshe mishikaki kwenye mchanga lakini alijizuia, hata hiyo alikuwa amechelwa kwani pochi lake lilimponyoka na kudondoka chini kutokana na kutetemeka.
Haraka haraka aliinama na kuchukua pochi lake na kumpatia muuza mishikajji hela yake na kutaka kuondoka bila ya kugeuza sura yake.
“Subiri”
Sauti ya kike ambayo iliagiza mshikaki ilimzuia kuondoka na yule mwanamke palepale alikimbia na kwenda kusimama mbele ya Rufi ambaye hakugeuka.
“Hey! Ni wewe kweli.. Aaa..Shemeji!!!”Aliongea yule msichana huku akionyesha hali ya kuwa furaha na mshangao kwa wakati mmoja.
“Miss utakuwa umenifananisha”Aliongea Rufi huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Shemeji kwanini unajifanya hunijui , ni mimi Xiao Xiao , tulikutana wakati ulipochumbiwa na kaka yangu”Aliongea huku akiinamisha kichwa chake kutaka kumwangalia Rufi ambaye alikuwa na mabadiliko.
“Hapana sio mimi umennifananisha” Rufi alionekana kutetemeka mno.
Ukweli alilaani sana katika hali kama hio , hakujua imekuwaje akakutana na Xiao Xiao msichana ambaye alikuwa akimjua fika kwani alikutana nae katika ulimwengu wa kijini kabla ya kutoroka.
*******
Nje ya hoteli ya Serena alionekana Suzzane akishuka kwenye gari aina ya Audi ya rangi nyekundu na kisha kumpatia Valet ufunguo baada ya kutoa pochi yake.
Baada ya kuweka mkoba wake kwenye kwapa palepale alianza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo la hoteli huku akigeuka nyuma akiangalia kama kuna mtu anamwangalia.
Suzzane alikuwa amebadilisha mtindo wa nywele , siku hio alikuwa amevalia Wigi na kumfanya kuonekana mtu mwingine kabisa.
Baada ya kuingia eneo la mapokezi na kupokelewa na mwanadada aliepamba uso wake kwa tabasamu palepale aliongea kidogo na mwanadada yule alichukua simu yake na alionekana alikuwa akiongea na ndani ya dakika chache alitabasamu na kisha akampa ishara Suzzane ya kuendelea kutembea.
Suzzane mara baada ya kuingia kwenye Lift alivuta pumzi kwa kutuliza presha yake na kisha alibonyeza kitufe kuruhusu Lift hio kumpeleka katika Floor husika.
Alijiangalia mavazi yake kwa kujichunguza na kuona yupo vizuri na na amependeza , kwa jinsi ambavyo alikuwa na wasiwasi ni kama mwanamke ambaye anaenda kukutana na mpenzi wake kwa mara ya kwanza.
Baada ya Lift kupandisha na kufika floor ya tatu , ilisimama na kufunguka na alionekana mwanaume alievalia suti na miwani nyeusi.
Suzzane alimpiga mwanaume huyo jicho la pembeni kumchunguza lakini hakuonyesha hofu na yule mwanaume hakuonyesha kumjali Suzzane kwani aliingia kwenye lift na kisha kutulia bila ya kubonyeza kitufe chochote.
Suzzane hakuwa mshamba , alijua pengine mwanaume huyo alikuwa akielekea Floor sawa ndio maana hakugusa vitufe lakini hakuacha kuwa na wasiwasi.
Baada ya Lfit kufunguka katika Floor namba sita wote kwa pamoja walitoka na mwanaume yule alichukua upande wa kushoto na Suzzane alichukua upande wa kulia.
Suzzane alijikuta akipatwa na ahueni na kisha alitembea kwenye Korido yenye msururu wa vyumba na ndani ya dakika chache tu aliweza kufika katika mlango wenye namba 123 na aligonga mara moja na dakika hio hio mlango ulifunguliwa na kisha akaingia.
“Shosti unaonekana kuwa na presha juu juu”Sauti nyororo ilisikika ikiongea na kumfanya Suzzane kuhema kwa nguvu kwa hali ya ahueni.
“Sijui nakua paranoid au nini lakini niseme hata nikienda chooni tu nakuwa na wasiwasi”Aliongea Suzzane huku akilazimisha tabasamu na kujaribu kuangalia mazingira.
Nadia alitoa tabasamu na kisha alimsogelea Suzzane na kumpa ishara ya kutaka kumkumbatia na Suzzane hakuwa na hiyana ya kukataa kumbatio.
“Unafanya vizuri Suzzane , ukishazoea kila kitu utaona ni kawaida”Aliongea na Suzzane lile kumbatiao kidogo lilionekana kuwa dawa kwake kwani aliweza kutulia.
“Unaonekana kuwa mzoefu Nadia , ulishawahi kufanya kazi ya hatari kama hii?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Nadia kutoa tabasamu.
“Nishawahi kufanya kazi ya hatari mara tatu ya hii, mwanzo wakati napewa misheni ya kufanya nilikuwa kama wewe tu ndio maana nimesema unafanya vizuri”Aliongea na kisha Suzzane alimimina maji kwenye glasi na kisha akampatia Suzzane huku akimwambia akae.
Suzzane baada ya kunywa maji yale alijihisi angalau ameweza kupoa.
“Presha ilipanda zaidi mara baada ya kukutana na mtu kwenye Lift , alikuwa amekaa kama mwanausalama, aliniogopesha mno , nikajua ni watu wa Raisi Senga”
“Oh .,.. huyo atakuwa ni mwanasalama kweli , hakika unafanya kazi nzuri Suzzane , lakini hupaswi kuwa na wasiwasi , kuna raisi kachukua makzi ndani ya hii hoteli”
“Raisi!!!”
“Ndio , ni taarifa za siri sana za kiusalama , nimejua hayo kutokana na kwamba nimekutana nae kwa ajili ya mazungumzo, kwasasa sitokuambia ni raisi wa taifa gani”Aliongea Nadia huku akitoa tabasamu.
Na kisha alisimama na kwenda kutoa mvinyo kwenye jokofu na ksha akafika nao na kuuweka mezani na kuanza kujimiminia.
“Hongera Suzzane kwa mara nyingine, kila kitu kimeenda kama tulivyopanga”Aliongea Nadia na huku akimpatia Suzzane glasi ya mvinyo na mara baada ya Suzzane kupokea alimpa ishara ya kugongesheana Cheers.
Baada ya Suzzane kunywa ile Wine kidogo alijikuta akitoa macho kutokana na utamu wake.
“Vipi umeipenda?”
“Ina radha tamu kweli?”
“Yeah hii ni Chateu Margaux, nilipanga kushare hii zawadi na wewe siku ya leo”Aliongea na kumfanya Suzzane kutabasamu na kuangalia chupa ya Wine hio.
Hakuwa mshamba alijua huo ni mvinyo wa bei ghali sana , pengine kama angetaka kuununua basi angefilisika.
Waliongea kwa dakika kadhaa huku wakionyesha kucheka na kufurahi kwa pamoja kama marafiki na kumfanya Suzzane kupotezea hofu yake.
“Kila kitu kimeenda kama tulivyopanga Suzzane, unajisiije mara baada ya kufikia hatua hii?”
“Wakati naanza kufanyia kazi huu mpango sikuwahi kudhania kama ungefanya kazi, yaani hapa hisia zangu siwezi kuzielezea”
“Suzzane kila kitu ndani ya dunia hii kinawezekana ukiwa una taarifa sahihi”Aliongea.
“Ilikuwaje mkaweza kuja na huu mpango?”
“Ni maswala ya kisaikolojia Suzzane , kama ungekuwa na mafunzo ya kijasusi basi ungejua mambo mengi yanawezekana sana kwa kusoma saikolojia ya mtu na tabia zake, tulichofanya ni kufaitlia maisha ya Salihi ya kila siku ili kujua tabia zake, we did it randomly at first without any plan lakini mara baada ya Asha kuingia kwenye Equation tuliweza kufinilize kila kitu na here we are”Aliongea .
“Unajua mpaka sasa kuna baadhi ya vitu nashindwa kuelewa , Salihi kutoka kimapenzi na mama yake wa kambo ni swala ambalo nashindwa kuliprocess kabisa”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kutoa kicheko.
“Hii dunia Suzzane ina mambo mengi na huwezi kuyajua yote , laiti ungejua hata nusu robo tu basi maisha yako yangebadilika kabisa, anyway tunapaswa kuachana na hayo , leo nataka kukuambia kwamba kesho ndio siku yako ya mwisho ya misheni yako”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kesho ndio siku ya kumshawishi Raisi Senga kujiunga na Umoja wa Ant- Illuminat , lazima iwe kesho Suzzane kabla hajalazimishwa kusaini mkataba wa kishenzi”
“Sijakuelewa swala hili linahusiana nini na Mkataba wa kishenzi?”
“Suzzane we are Ant – lluminat, ikimaanisha kwamba tunaenda kinyume na namna dunia inavyoendeshwa , hiki ndio tunachopambana nacho, kuna kitu kikubwa sana kimepangwa kukamilishwa hapa Tanzania na mimi misheni yangu ni kukizuia kwa namna yoyote lakini kabla hilo halijatokea wewe unapaswa pia kukamilisha misheni yako, kumbuka ulichoambiwa kule Qatar”Aliongea na kumfanya Suzzane kumwangalia Nadia kwa macho ya kuuliza.s
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 652.
Rufi licha ya kwamba alijuwa uwepo wa Xiao Xiao ndani ya jiji la Dar lakini bado hakuamini kama angeweza kukutana nae katika eneo kama hilo la Kawe Beach.
Upande wa Xiao Xiao ukweli ni kwamba haikuwa mara ya kwanza kumuona Rufi, mara ya kwanza alivyomuona hakuamini kama anaweza kuwa Rufi lakini siku hio mara baada ya kumuona kwa mara nyingine hakutaka kudharau hisia zake na aliweza kuthibitisha ni yeye kweli.
Ilimshangaza kumuona Rufi nchini Tanzania mara baada ya miaka mingi ya kutoroka kutoka katika ulimwengu wa kijini.
Rufi licha ya kukamatika hakutaka kabisa kuongea na Xiao na palepale alikimbia kurudi ndani ya mgahawa na Xiao Xiao na yeye alimkimbilia kumfuata.
Roma mara baada ya kumuona msichana huyo wa kichina alikumbuka alivyokutaka nae mara ya mwisho mpaka kuja maeneo hayo hayo na kuachana .
Alikumbuka namna mrembo huyo alivyokuwa akimsumbua kwa kumtumia jumbe za meseji za kumtaka kimapenzi ambazo alidharau na kutomjibu mpaka akajikatia tamaa.
“Nini kinaendelea , kwanini Rufi anakimbiiana na yule mdada?”Aliuliza Amina ambaye alikuwa kwenye mshangao kama Roma .
Muda huo huo kabla Roma hajajibu Rufi alishawafikia na Roma alisimama mbele ya Rufi akimkinga na Xiao Xiao.
Mrembo yule wa kichina mara baada ya kumuona Roma alijikuta akijawa na mshangao kwani ni kama hakutegemea kumuona katika maeneo hayo.
“Hata wewe pia upo hapa , aisee kweli kilichopangwa hakikwepeki nadhani imepangwa tuoanane kwa mara nyingine”Aliongea Xiao Xiao akimwangalia Roma kwa furaha.
“Ndio nipo hapa pia , lakini kwanini unamfukuza Rufi?”
“Rufi!!?Oh.. nafahamiana nae ni shemeji yangu kwa kaka yangu”
“Huyo kaka yako ndio anaefahamika kwa jina la Xiao Hang?”Aliuliza Roma na kumfanya Xiao kutoa macho.
“Umejuaje jina la kaka yangu , au Rufi kakuambia kila kitu?”Aliuliza huku akiwa na mshangao , ingekuwa ngumu kwa Roma kujua jina la kaka yake kwani alikuwa akiishi huko katika jamii ya majini.
Roma hakujibu swali lake na palepale alimshika mkono yule mchina na kisha alianza kumvuta kumtoa nje ya mgahawa huo na ndani ya dakika chache tu walionekana wakiingia upande wa kushoto kwenye vyoo na mabafu ya kubadilishia nguo kwa watu wanaoenda kuogelea.
Amina yeye alikuwa kwenye mshangao kuona Roma amempeleka yule mchina kwenye mabafu .
Upande wa Lanlan hakushangaa kile kilichokuwa kikiendelea na alisimama na kwenda kuchukua kifurushi cha mishikaki na kurudi juu ya meza na kuendelea kula.
Upande wa yule mchina Xiao Xiao hakuelewa Roma anataka kumfanya nini na namna ambavyo alimshika mkono hakuwahi kufanyiwa hivyo na mwanaume na alijikuta mapigo yake ya moyo yakienda spidi spidi.
Pengine alijua labda Roma kadhamiria kwenda kufanya nae bafuni ndio maana anamwingiza huko.
Alikuwa mwekundu kama yai la kisasa kutokana na uzungu wake na aliishia kujiuliza ni kipi ambacho anapaswa kufanya ,ijapokuwa alikuwa akitamani kuonana na Roma kwa mara nyingine na kufanya nae mapenzi ili kuweza kumtumia kupanda levo lakini katika hali kama hio ya kushitukiza alijiona ni kama hakuwa tayari.
Upande wa wanaume ambao walikuwa kwenye mgahawa huo waliishia kumwangalia Roma kwa mshangao na wivu , ukweli ni kama walimdhania Roma na mchina huyo ni wapenzi kwani Xiao Xiao hakuleta ukinzani wakati wa kuvutwa na Roma mpaka kuingiziwa ndani ya mabafu.
Roma hakujali sana macho ya wengi yaliokuwa yakimwangalia , kwani mara baada ya kumfikisha Rufi kwenye bafu ambalo hutumiwa na wanaume aliwapa ishara vijana wadogo waliokuwa wakibadilisha mavazi kuondoka na walifanya hivyo haraka haraka na kisha wakakimbilia nje lakini mmoja wapo ambaye alikuwa mkubwa kidogo aligoma.
“Wewe kama nani mpaka kutuamrisha tuondoke?”Aliongea
Roma alikuwa na hasira na palepale alipiga ngumi ukuta kiasi cha kutengeneza ufa na jambo lile lilimuongopesha yule wmanaume na palepale alikimbia kuelekea nje akiwa kwenye mshangao.
Upande wa Xiao Xiao alikuwa akimwangalia Roma na macho ya aibu , huku akishindwa kuzuia kulegea kutokana na macho yake pamoja na uso ambao ulikuwa umetakata na kumfanya kumuona mtanashati.
Yeah Roma alikuwa amebadilika uso sana tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mbeba mizigo , kipindi hicho alionekana kuwa Handsome sana , pengine ni kutokana na kupanda levo, kilichokuwa kikimpunguzia pointi ni aina ya uvaaji wake tu.
Roma alimshika na kumsukumia Xiao kwenye chumba kilichokuwa pembeni kushoto kwake na kisha akafunga mlango na palepale alikwenda kumkandamiza ukutani huku akimwangalia usoni kwa macho yasiokuwa yakielezeka.
Xiao alikwepesha macho kwa aibu huku akiwa na msisimko wa aina yake na alikuwa akisubiria kwa hamu hatua ya pili ambayo Roma anakwenda kufanya.
Ijapokuwa Roma alionekana kuwa siriasi hali ile ya ki uwanaume ilimfanya kuvutiwa zaidi na aliona kitakacho fanyika hapo ni yale mapenzi ya vurugu na hio ndio ilikuwa ‘Fantasy’ yake.
“Kufanyia hapa sio vizuri , kama vipi tufanye haraka haraka tuondoke…”Aliongea huku akionyesha hali ya aibu za kike na kumfanya kuzidi kupendeza..
Wanawake wa rangi nyeupe ni tofauti kidogo na wanawake wa kiafrika hususani katika swala la mahusiano , ni wawazi sana likija swala la mahusiano na anaweza akaruhusu ngono kufanyika hata na mtu ambaye hamjui vizuri.
Upande wa Roma mawazo yake yalikuwa mengine kabisa muda huo alikuwa akijiuliza ni kipi anapaswa kumfanyia , aliogopa kwamba kama ataenda kusema huko kwenye ulimwengu wao kama Rufi yupo Tanzania basi ingekuwa tatizo.
Roma hakutaka matatizo kwa wakati huo kwani nguvu zake za kijini hakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa wakati huo na asingeweza kumlinda Rufi kama atakamatwa.
Mbaya zaidi kama itajulikana alikuwa na mahusiano na Rufi ndio ingekuwa tiketi ya majini hayo kuja kumvamia na kutaka kumuua maana alijua tabia yao namna moja ni kutopenda kudharaulika.
“Unataka nifumbe macho kwanza kabla hujaanza kunikiss… najihisi sipo tayari lakini unaonekana una hamu, hivyo sijali kama unataka tufanye , isitoshe nilikuwa nikikufikiria sana”Aliongea Xiao huku akiona pengine Roma alikuwa akiona aibu ndio maana alikuwa akimwangalia tu bila kuchukua hatua yoyote.
Xiao Xiao alikuwa ni mzuri haswa wa sura ijapokuwa alikuwa na rangi ya kichina lakini macho yake yalikuwa tofauti kidogo na wachina wa kawaida , kitu pekee ambacho hakuwa nacho ni umbo tu.
Roma alijiwazia alikuwa ameua watu wengi ambao pengine kati yao hawakuwa na hatia hivyo kujiongezea dhambi kwa kuua na mwanamke mrembo kama Xiao lisingekuwa tatizo.
Alijiambia kama mwanamke huyo ataendelea kuwepo hai basi siri ya uwepo wa Rufi nchini Tanzani itafichuka na ili kuficha siri hio kwa wakati huo hatua ya kwanza ni kumuua.
Baada ya kuwaza kwa muda palepale akili yake ilifanya maamuzi na shetani mtoa roho alimvaa na sura yake iligeuka na kuwa ile ya kikatili na palepale alipeleka mkono kwenye shingo yake.
Xiao alijua Roma alikuwa akitaka kuinua kidevu chake , hio pia ni moja wapo ya staili ambayo alipenda kufanyiwa na mwanaume , kunyanyuliwa kidevu na kuangaliwa usoni na mwanaume mwenye uchu kabla ya kubusiwa.
“Xiao Xiao kama utakuwa na kinyongo na mimi kwa kukuua leo hii basi naomba ukiwa kuzimu roho yako initafute na ulipize kisasi, hili halina uhusiano wowote na Rufi hivyo usije kumchukia”Aliongea Roma.
“Unamaanisha nini?”Xiao Xioa alijikuta akiwa katika mshangao huku akichanua macho yake lakini palepale aliweza kugndua kwamba Roma hakuwa akipanga kufanya nae mapenzi bafuni.
Roma hakutaka kuchelewesha muda na palepale alimshikilia shingo kwa nguvu kumkaba na Xiao Xiao alijihisi kuanza kukosa pumzi.
“No .. usinifanyie hivi..”Aliongea lakini Roma kabla hajakaza mkono mlango palepale mlango ulisukumwa kwa nguvu na aliingia Rufi ambaye alionekana kuhema kwa nguvu.
“Hubby usifanye hivyo , tafadhari naomba umuache ,, huyo sio tishio kwetu”Aliongea Rufi kwa kubembeleza.
Wakari Rufi na Amina wakimuona Roma akimwingiza Xiao kwenye bafu palepale waliangaliana na kisha wakapeana ishara ya kwenda kuchungulia nini kinafanyika.
Baada ya kusikia Roma alikuwa akipanga kumuua Xiao Xiao palepale alisukuma mlango kumuokoa.
Xiao Xiao mara baada ya kujua Roma alikuwa akitaka kumuua na sio kufanya nae mapenzi machozi yalianza kumtoka palepale.
“Uli.. ulikuwa ukitaka kuniua?”Aliuliza huku akionyesha mshangao na uso wake wa kirembo ulibadilika na kuwa mwekundu , pengine angekuwa na nguvu za kijini katika levo ya nafsi basi moja kwa moja angekuwa ashampiga Roma.
“Rufi huyu anatokea katika ulimwengu wa kijini , ukoo uliolazimishwa kuolewa nao , kama ataenda kutoa taarifa ..”
“Najua ...”Rufi alijikuta akimeza mate huku akionyesha huruma.
“Najua ni hatari lakiki sitaki kukuona ukimuua mtu ambaye hana hatia .. pengine hujui hili lakini wakati nilipochumbiwa kwenye ukoo wao walinidharau sana na kuniona kama kiumbe cha ajabu lakini ni Xiao Xiao pekee ambaye hakuoneysha kunidharau, sio mtu mbaya na hawezi kufanya kitu ambacho kitaniathiri”
Roma alimwangalia Rufi na kuona anapaswa kutii kile anachomwambia kwani asingefanya hivyo angeziumiza hisia zake.
“Okey fine”Aliongea Roma na kisha akamwachia Xiao Xio
Xiao Xiao alijikuta akichuchumaa na kuanza kulia kilio cha kwikwi huku akiwaangalia wote na kuangalia mkono wake ambao ushavimba kutokana na kushikiliwa kwa nguvu.
“Umenikatali sana , mimi sio kama baba yangu wala kaka yangu , kama yeye mwenyewe hataki kurudi kwanini aende , kwanini umeshindwa kuongea na mimi vizuri tu”Aliongea na kisha palepale akasimama.
“Kama hunipendi si ungesema tu kwamba hunipendi , kwanini ya kutaka kuniua , nilipatwa na furaha baada ya kukuona kwa mara nyingine kutokana na kukuwazia muda wote tokea mara ya mwisho tuonane kwanini unapenda kucheza na hisia zangu hiv, nakuchukia sana , sitaki kukuona tena kwenye maisha yangu”Aliongea awamu hio kwa Kichina kabisa na kisha alitoka nje kwa kukimbia huku akitoa machozi .
“Hubby asante kwa kunisikiliza”Aliongea Rufi akivuta pumzi ya ahueni.
“Natumaini maamuzi yako ni sahihi na hakuna kibaya ambacho kitatokea”Aliongea Roma.
“Kama mambo yatabadilika nitaondoka kuelekea Mediyerranian kuishi na Sister Rose , nadhani hawawezi kuvuka mpaka kuja mpaka kule”Aliongea
“Rufi unarahisisha mambo , kama watataka wanaweza kwenda mahali popoate hata kama ni kwa kupigana na miungu hawatojali , mwili wako ni hazina kubwa kwao kukupoteza kirahisi , isitoshe majiini ni viumbe ambavyo havipendi kushindwa kirahisi”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kutoa machozi.
“Jamani tumekuja hapa kwa ajili ya kumsindikiza Lanlan kucheza hebu tuachane na hayo kwasasa , Nasra ,Dorisi na Lanlan wanatusubiria”Aliongea Amina kwa kingereza huku akitangulia.
“Hubby nimefurahi , tulijua ulitaka kufanya nae kwasababu alikuwa mrembo lakini kumbe ulitaka kumuua kwa ajili yangu , namuoea huruma Xiao Xiao lakini nimefurahi kuona unanijali , Thanks a lot love”Aliongea.
“Nyie warembo siku moja mtaniua”Aliongea Roma huku akimfinya mashavu huku akitoa tabasamu.
Baada ya chakula Lanlan alienelea kucheza michezo akiungana na Nasra na Dorisi na walijikuta wakifurahi sana siku hio.
Ilifikia hatua mpaka Nasra akajiuliza imekuwaje Edna akamuacha mtoto mzuri kama Lanlan kwani uwepo wake tu ulikuwa ukileta furaha.
Roma wakati huo hakuacha kumkumbuka Edna na alijiaribu kupiga simu nyumbani kumuulizia Edna kama amerudi lakini Bi Wema alimwambia bado hajarejea.
“Pengine atarudi jumatatu kwani ndio siku ambayo inatarajiwa kuwa na kikao cha kutangaza mabadiliko ya kampuni ya Vexto”Aliongea Nasra mara baada ya kumuona Roma amekuwa mnyonge.
“Mimi sitaki hata kujisumbua na maswala yake mengine , ninachotaka ni kuongea nae na kuweka mambo sawa tu basi , nimefikiria sana katika hizi siku na nimegundua kuna kitu alikuwa akinificha”Aliongea Roma na Nasra alimshika begani kumtuliza huku akimwangalia kwa kumuonea huruma.
Muda wa jioni wote walirudi nyumbani kwao wakimuacha Amina anapoishi na Roma alichukuana na Lanlan kueleka nyumbani kwa Nasra
Wakati wanaingia getini walishangazwa na uwepo wa magari matatu ambayo hawakuwa wakiyajua, mawili yalikuwa ni Aud rangi nyeusi na moja wapo ilikuwa ni gari aina ya Maserati ya rangi nyekundu.
“Ineonekana tuna ugeni hapa”Aliongea Rom.
“Naona hivyo pia”Alijibu Nasra aliemshika Lanlan mkono.
“Nasra wewe ondoka na Lanlan moja kwa moja kwenda juu akapumzike mimi nitaonana nao”Aliongea Roma na Nasra alitingisha kichwa kumwelewa na kisha alitumia mlango wa nyuma wakati Roma akielekea eneo la seubuleni.
Mtu pekee amaye aliachwa nyumbani alikuwa ni Qiang na mara baada ya kuingia ndani Roma aliweza kumuona mwanadada huyo ambavyo amekosa utulivu kwani alikuwa akizunguka zunguka huko na huko , lakini alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kumuona Roma.

SEHEMU YA 653.
Roma mara baada ya kuingia ndani aliweza kuona sura anazozifahamu , mmoja wapo alikuwa ni Afande Jamali na mwingine alikuwa ni mwanamke kutoka familia ya Sharif.
Alikuwa amevalia suti nyeusi na viatu rangi nyekundu aina ya skuna, nywele zake alikuwa amezifunga kurudi nyuma na kumfanya kuwana mwoneknao wa kujiamini pamoja na wa kuvutia kwa wakati mmoja.
Alikuwa ni mwanadada mrembo Maimuna Sharif ambaye alionekana kama vile ni ofisa kutoka benki kwa muonekano wake kiasi ambacho kama wewe ni mwanaume wa kawaida ingekufanya kukosa hali ya kujiamini mbele yake.
Afande Jamali mara baada ya kumuona Roma palepale alisimama kwa heshima.
“Mr Roma naomba unipe ruhusa yako kukutambulisha , huyu ni Miss Maimuna Sharif Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bale Group na mtoto wa kwanza kutoka kwa mzee Hafidh Sharif”Aliongea Jamali.
“Tunakutana tena Mr Roma”Aliongea Maimuma huku akionyesha tabasamu na kunyoosha mkono wake kumpatia Roma.
Roma aijiuliza mwanamke huyu anafanya nini , alikuwa akikumbuka alimuona siku ya jana yake mkoani Kilimanjaro , lakini licha ya kutoelewa nia ya ujio wake hakuwa akimuogopa hivyo alinyoosha mkono wake kumsalimia.
Roma mara baada ya kugusana na mkono wa mrembo huyo alijikuta akijiambia alikuwa na mkono mlaini mno ijapokuwa haikuwa mlaini kama wa Rufi lakini bado ulikuwa mlaini wa kumpagawisha mwanaume yoyote rijali.
Roma kwa kumwangalia ru Maimuna alijua kabisa sio mwanamke wa kawaida , ilionekana kabisa alikuwa na mafunzo ya kimapigano na alijiambia hakika alikuwa akijua kujijali.
Moja ya mbinu ya kupima kama mtu ana mafunzo ya kimapigano ni kupitia pumzi yake, watu ambao wana mafunzo ya kimapigano hususani ya Kung fu mara nyingi upumuaji wao ni wa tofauti na watu kawaida wanapumua kama vile wanahesamu pumzi inayvoingia na kutoka, kitu kingine pia katika utembeaji wao au pale wanapokuwa wamesimama hii huwatofautisha sana.
Kwa mfano wakati wa kutembea ni kama vile kuna mstari anaofuatisha kwani hatua zake hazipindishiki huku mikono yake yote ikiwa usawa wa mwili , mtu wa kawaida tembea yake inateneza mstari wa Zigzag huku vidole vya miguu yake vinatengeneza angle
Sasa sifa hizo zote alikuwa nazo huyu mwanadada Maimuna ambaye alikuwa mbele ya Roma na kujikuta akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na kujiambia alikuwa na urembo wa mwili na ngozi yake ni laini mno , pia ni mkurugezi wa kampuni ya Bale lakini pia wakati huo huo alikuwa na mafunzo ya mapigano.
Ilikuwa ngumu sana kumkutana mwanamke mwenye mafunzo ya mapigano kuwa na ngozi laini hususani ya mikono.
Wakati wakiwa wameshikana mkono Roma alijikuta akihisi mtekenyo kwenye kiganja chake na palepale aligundua Maimuna alikuwa amemtekenya kwa kutumia ukucha wa kidole cha mwisho.
Jambo lile lilimshangaza na kumfanya Roma ajulize mwanamke huyo anafanya nini , au yupo hapo kwa ajili ya kumtega.
Baada ya kuachiana wote watatu waliweza kuketi chini huku Qiang akiandaa juisi.
“Afande Jamali nadhani hujamleta hapa kwa ajili ya kunisalimia tu”Aliongea Roma akitaka maongezi yaende moja kwa moja katika topiki ambayo imewalata.
“Ndio Mr Roma , sitozunguka zunguka , nipo hapa kama mwakilishi wa wizara ya ulinzi?”Aliongea.
“Mzee Hashim Tozo ndio kakuagiza?”Aliogea Roma akimaanisha waziri wa ulinzi ambaye alikuwa ni ndugu yake Afande Tozo, Roma alishawahi kukutana nae mara kadhaa nyumbani kwa Afande Kweka na alikuwa amezoeana nae japo sio sana,
“Ndio Mr Roma , nipo hapa kufikisha ujumbe kutoka serikalini , serikali ya Tanzania inaheshimu familia yako pamoja na familia ya Mzee Sharif kwani mchango wenu kwa taifa ni mkubwa , Mstaafu jenerali ametoa taarifa yake kwamba familia yake haihusiki na swala lolote lililotokea siku ya jana na kusema unapaswa kuwajibika kwa kila kitu binafsi, hivyo ndio maana tupo hapa kwa ajili ya maongezi”Aliongea.
“Nenda moja kwa moja kwenye pointi”
“Ngoja niseme mimi… Mr Roma nipo hapa kwa ajili ya kutafuta haki ya familia yangu”Aliongea Maimuna
“Haki ya familia yako?”
“Ndio , nimekuja hapa kwa ajili ya kukutaka urudishe hazina yetu , kisha ujenge upya jengo la ibada na baada ya hapo usujudie roho za miungu wetu mara nne”Aliongea Maimuna huku akiwa na uso wenye urafiki.
“Kwanza nikueleze kwamba hio hazina sijui nini maana mimi sina , pili mmefikiria nini kudhania kwamba ninaweza kwenda kusujudia miungu yenu ilihali mimi ndio niliochoma moto jengo lenu la ibada”
“Mr Roma watu waliokukosea ni Salihi naibu waziri wa elimu pamoja na Asha na kama ni kisasi ulitakiwa kuwalipiza wao , kwanini ukahusisha familia nzima katika kisasi chako kwa kuchoma jengo letu la ibada pamoja na kuiba hazina yetu huku ukiharibu makazi yetu , mpaka kuja kwangu hapa ni kwamba familia yetu imekaa chini na viongozi wa kiserikali na kukubali jambo hili kuisha kwa amani na kusahaulika kama utatii matakwa yetu , urudishe hazina yetu na kisha usujudie miungu yetu kuiomba msamaha”
“Kama hiki ndio ambacho kimewaleta mnaweza kuondoka”aliongea Roma akisimama na kisha kunyoosha kidole kuelekea mlango wa kutokea nje.
Maimuna wala hakuonyesha kuathirika , yaani alikuwa akiongea kirahisi mno na palepale alisimama na kisha akamsogelea Roma karibu zaidi kimadaha na kufanya marashi yake makali ya bei ghali kuathiri pua za Roma.
“Mr Roma , siku ya jumatatu jioni nimeandaa sherehe ndani ya hoteli ya Wache Kigamboni, wageni wangu ni wabia wa kibiashara ambao wanashirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni yetu ya Bale Group , unaonaje ukishiriki na wewe?”Aliongea huku akiwa na tabasamu la kiuchokozi.
“Kwanini nihudhurie?”
“Kwasababu nitakupa sababu ambayo itakufanya ushindwe kukataa kuhudhuria , nina uhakika utaweza kukubaliana na matakwa yetu baada ya hio hafla”
“Vipi kama nisipo hudhuria?”Aliuliza Roma na kumfanya Maimuna kutingisha mabega.
“Nina uhakika mwanaume jasiri kama wewe hutopenda kuonekana Muoga mbele ya familia ya Sharif .. Besides I’ m just a frail woman .. alright that is settled, nitakuja kukuchukua mwenyewe hio siku”Aliongea huku akimkonyeza na kisha alimpita kimadaha na kuelekea nje huku akitingisha makalio yake ya wastani kwa fujo kama zote.
Roma aliishia kushika kiuno na kujiambia hakika ameweza kuamsha shauku yake.
“Vipi mmeshawazuia kutumia njia ya fujo katika kulipiza kisasi?”Aliuliza Roma akimwangalia afande Jamali.
“Hata mimi mwenyewe sijui na nafuata tu maagizo ninayopewa na wakuu wangu , lakini nakushauri Mr Roma hii familia haiwezi kuliacha hili lipite hivi hivi kuna nguvu kubwa ambayo ipo nyuma yao , lakini inaonekana hawataki kufanya fujo kudai haki yao , unapaswa kufikiria mara mbili ili kulimaliza kimya kimya”Aliongea Afande Jamali
“Babu alisema kwasababu mimi ndio msababishaji nitawajibika mwenyewe na hakuna mtu wangu wa karibu ambaye ataguswa “
“Inaonekana kuwa hivyo , isitoshe wanawake wako wote sio raia wa kawaida , serikali haitaki hili swala kuingiliana usalama wa raia … maagizo yashatoka kama famili ya Sharif itafanya jambo lolote la kutaka kudhuru familia yako basi tutaingilia”Aliongea Jamali.
“Nimefarijika kusikia hivyo , isitoshe adui yao ni mimi hivyo nipo tayari kuona nini wananniandalia, ninashauku ya kutaka kujua mchezo wao utazaa nini”Aliongea Roma na kumfanya Afande Jamali kushindwa kumuelewa Roma kabisa kwani alionyesha kutokuwa na hofu kabisa.
Baada ya wageni kuondoka na walinzi wao, Roma alikaa hapo sebuleni kwa muda mpaka Nasra aliposhuka na kukaa pembeni yake.
“Hii familia ya Sharif ina nguvu sana?”Aliuliza Nasra.
“Inaonekana , ila kwa sasa nahitaji kufanya maandalizi”
“Unahitaji msaada wangu?”
“Ndio”
“Nini nikusaidie?”Aliongea Nasra akionyesha shauku.
“Simu yangu imeisha chaji , nichajie na kisha niletee laptop yako hapa , kuna mtu nahitaji kuwasiliana nae kwa njia ya online”Aliongea Roma.
Nasra alijikuta furaha yake ya kutaka kumsaidia Roma ikipotea, na kujiambia alijawa na shauku ya bure.
Ukweli ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kutohitaji msaada wowote kutoka kwao iliwafanya kuwa na shauku kama atataka msaada.
Licha ya kuchukia alichukua simu ya Roma na kwenda nayo juu kuichomokea chaji na kisha alishuka na Mackbook Pro na kumpatia na Roma aliunganisha na internet palepale na aliingia mtandaoni na kulipia VPN na kisha akapakua kivinjari cha Tor na kisha akaingia mtandaoni.
“Naweza kuangalia unachofanya?”Aliuliza Nasra akiwa makini na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasam.
“Unaweza ndio kuangalia wewe ni mwanamke wangu”Aliongea
Roma hakuona haja ya kumficha Nasra kile ambacho alikuwa akipanga kufanya , mpango wake ni kutaka kuomba msaada kutoka nje ya nchi kufika Tanzania kwa ajili ya kumsaidia jambo lake.
Roma baada ya kuingia kwenye mtandao wa Deep Web palepale aliandika link ambayo alikuwa ameikariri na dakika hio hio yaliweza kuonekana mawasiliano ya watu mbalimbali na ajabu kila mtu ambaye Roma alikuwa akiwasiliana nae ilimhuhiaji kwanza kuingiza Passcode.
Licha ya kukaa na kuangalia lakini Nasra hakuelewa chochote kwani Roma alikuwa akiwasiliana na watu kwa kutumia lugha tofauti tofauti.
Kitu pekee ambacho aliweza kugundua ni kwamba kila mtu ambaye aliwasiliana nae alionekana kumuheshmu sana Roma
Ilimchukua nusu saa Roma mpaka kumaliza .
“Babe you were so cool”Aliongea Nasra huku akijikumbatisha kwenye kifua cha Roma.
“Umeelewa chochote nilichokuwa nikiongea?”
“Sijaelewa lakini , ulivyokuwa ukiongea inapendeza sana”Aliongea akirembua na kumfanya Roma mzuka kumpanda.
“Lanlan ashalala?”Aliuliza Roma.
“Ndio na anakoroma huyo”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu na kuingiza mkono kwenye kifua cha mrembo Nasra na kuchoropoa embe dodo.
“Kama kashalala unaonaje tukifanyia hapa hapa kwenye sofa na kisha tukaoge wote”Aliongea Roma lakini hakusubiri jibu kwani paleplae alimnyanyua na kisha akamlalia kwa juu na kilichoendelea masofa yatahadithia.
Siku ilofuata ilikuwani jumapili na Roma hakuwa na mpango wa kumpeleka Lanlan kucheza tena.
Siku hio aliona kitu pekee ni kuangalia maendelo yake katika kujifunza mbinu ya Andiko la urejesho, maana aliona Lanlan ni mwendo wa kula bata tu tokea arudi ulimwengu wa majini pepo.
Kutokana na Roma kutokuwa na nguvu za kijini hakuweza kumwangalia Lanlan amefikia levo ya ngapi hivyo kitu pekee ambacho alitaka kujua ni kumchukua na kisha wakaenda hadi msituni na wakati huo akiwa na matofali ya zege.
Baada ya kuyapangilia chini kwa mstali maalumu mawili mwili matatu mtatau na manne nne alimwambia Lanlan aanze kuyapasua kutoka mwanzo mpaka mwisho kwa kutumia ngumi.
Lanlan misuri ya mwili wake ilianza kutuna kama vile ni puto na palepale alianza kuyapasua kwa kasi na ndani ya dakika yote alikuwa ameyapiga na pigo moja moja mpaka kupasuka.
Roma alijikuta akiridhika na alijiambia kutokana na nguvu aliotumia pengine atakuwa katika levo ya Uchoyo au wanaita levo ya kujijali mwenyewe na muda wowote angeingia katika levo ya Takdiri au Hatima kwa lugha nyingine.
Hii ni levo muhimu sana katika mafunzo ya kijini lakini ukiachana katika mafunzo ya kijini lakini pia katika maisha ya binadamu ni moja wapo ya hatua ambayo ni muhimu kwa mafannikio ya binadamu yoyote , ni binadamu wachache sana ambao wanajua Takdiri yao nini katika ulimwengu huu na hao ambao wamebahatika kuijua mafanikio yao ni ya juu sana kuliko wale ambao hawaijui Takdiri yao ni nini.
Kila binadamu huzaliwa na kuwepo katika uso wa dunia kwa kusudi maalumu na ndio maana katika hatua za kujitafuta ili kujua wewe ni nani tofauti na jina lako hutakiwi kuuliza maswali mtu wa nje bali unatakiwa kujiuliza wewe mwenyewe maswali na kutafuta majibu na hapa ndipo utaweza kujua nini Takdiri yako.
Maendeleo ya Lanlan yalimshangaza sana Roma , ijapokuwa yeye wakati wa kujifunza hakutumia vidonge vyvoyote kujibust lakini kwa Lanlan spidi yake ilikuwa ya juu na alikuwa na shauku ya kutaka kujua kitamtokea nini mpaka kupita levo ya kifo na uhai halafu kuzaliwa upya.
Roma alijikuta akimsifia Lanlan kwa kazi nzuri huku akimwahidi mambo mengi lakini Lanlan alitaka kupaishwa juu angani lakini Roma uwezo huo hakuwa nao na alijikuta ile hali ya kutaka kurudisha uwezo wake na kumuondoa mdudu aliekuwa akimtawala kumvaa.
Roma aliona kwamba haijalishi Lanlan uwezo wake unaongezeka kwa spidi namna gani lakini bado tu alikuwa akipaswa kumlinda.
Roma mara baada ya kurudi na kumaucha Lanlan mojakwa moja alielekea katika maabara ya Clark eneo la Makongo juu , maabara ambayo ilikuwa urithi kutoka kwa Profesa Shelukindo.
Roma mara baada ya kufika aliweza kugundua pia Rufi yupo na wote walikuwa bize kupitia baadhi ya vitabu.
“Kuna chochote ambacho mmepata?”Aliuliza Roma akiwaangalia warembo hao namna ambavyo wapo bize.
Clark alikuwa amevalia simple huku nywele zake alikuwa amezifunga na lastick kwa nyuma, muda wote mwanamke huyo alionekana kuwa bize.
“Kulingana na maarifa ya Rufi kuhusu roho mnyama wa maafa , hakuna aina yoyote ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana nayo kwasababu ni mnyama aliewahi kuwepo katika kipindi cha dunia kuwa katika hali ya ukiwa na machafuko , inawezekana alikuwa ni mnyama mwenye nguvu kubwa duniani”
“Dear nipo hapa kwa taarifa nzuri lakini kwanini unaongea kuniogopesha?”
“Mimi ni mwanasayansi na sio motivation speaker , ninachokuambia ni fact , mambo hayapo mazuri sana kwa upande wetu”
“Hubby huna haja ya kujali sana kuhusu alichoongea Clark , ijapokuwa sina wazo namna ya kuishinda lakini tunaweza kushinda kutokana na hasira yake”
“Hasira yake?”
“Ndio”
“Hio ni roho ya mnyama mkali sana ambaye sifa yake kubwa ni kukasirika na kutokuwa na huruma , hivyo tunapaswa kutafuta roho nyingine ambayo ni ya mnyama lakini mpole ili tu kuiamsha ndani yako , ijapokua roho hio inaweza kuwa na nguvu kidogo kushindana na Chaos, hivyo kabla ya jaribio hilo tunapaswa kuanza na nguvu zako za kijini , tunapaswa kuibadili nguvu yako ya kijini na kuiweka katika kitu ambacho kitakandamiza roho yake ya ukali”Yalikuwa ni maelezo mengi ambayo Roma alishindwa kuyaelewa.
“Umeongea vitu vingi , je una mpango wowote?”
“Tuna mawazo tofauti , nilikuwa nikiwaza vipi kama utaombewa kanisani au kusomewa swala msikitini , watu wa dini wana upako wa kutosha, ninachojua nguvu iliopo ndani yako ni ya kipepo hivyo inaweza kusafishwa na nguvu ya kiroho ya nuru ya kidini ambayo ni safi”
“Clark tangu lini wewe kama mwanasayansi ukaanza kuamini katika maombezi”Aliongea Roma kwani siku zote Clark kila mama yake alipokuwa akimlazimisha kwenda kanisani alimwambia hakuna Mungu kwasababu hakuna uthibitisho wa kisayansi.
“Mimi najua mambo mengi kuliko unavyodhania , ijapokuwa sijawahi kuamini katika imani yoyote lakini kuna nguvu ya kiroho ambayo sio ya kawaida katika misikiti pamoja na kanisani ndio maana watu wana imani kali, nimeamini baada ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi”Aliongea na Roma alitingisha kichwa kwani hata yeye alikuwa akikubalaina nae.
“Vipi kuhusu wewe Rufi?”
“Mimi nimeona labda ujaribu kusali kibudha au kihindu, kuna Monk ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya ‘Exorcism’ lakini kazi kubwa ni kuwapata na kuwa na utayari kufanya hio kazi, nimeshindwa kujua ni aina gani ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana na nguvu ya Chaos”
“Kwahio mwishowe tuna uelekeo lakini mpango hatuna”
“Sio kabisa , kama tutashindwa kukusaidia kwa njia za maombezi au Exorcisim basi angalau tunapaswa kupata Dhana za kijini za kiwango cha juu kabisa ambazo zina uwezo wa kushindana na roho ya mnyama wa maafa”
Baada ya Rufi kuongea vile mawazo ya Roma yalimkumbusha kitu kimoja ambacho aliiba katika madhabahu ya Mzee Sharif.
“Nimekuja hapa kwa kitu kingine pia , hebu ngoja niwaonyesheni muone..”Aliongea Roma na kisha palepale alitoa ile Kokoto iliokuwa na jina la Hazina na kisha akampatia Rufi.
“Unaijua hii maana yake?”
Write Note:Exorcism ni kama vile wanavyofanya waganga wa kienyejji katika kufukuza mapepo , sasa katika imani ya Kibudha na Kihindu hufanya hicho kitendo pia kwa muumini mwenye mapepo.

SEHEMU YA 654.
Rufi na Clark walikuwa wameshangazwa sana na neno Hazina na palepale walijikuta wakifungua kile kijiboksi kuangalia kilichopo ndani.
Lakini mara baada ya kuona kitu chenyewe walijikuta wakikosa yale matamannio yao, walijiuliza kokoto inaweza vipi kuwa hazina.
“Ndio nini hiki , ndio Hazina uliokuwa ukisemea , mbona inaonekana kama pande la mkaa lakini uzito wake ni mkubwa kuliko wa mkaa , au ni jiwe?”Aliuliza Rufi.
Clark hakuonyesna kukupurukuka na aliishia kuangalia kwa umakini kujaribu kukagua na kulipatia maana yake kwani palepale aliliweka katika Darubini na kuanza kulikagua kisayansi na ndani ya dakika tano tu alionekana kupata majibu kadhaa.
“Linaonekana kama vile ni ‘Carbide’, kuna aina ya madini ndani yake lakini ajabu pia kuna protini , au ni Fossi , asili mara nyingi inakuwaga na vitu ambavyo vinaonekana kama vimekufa lakini bado vipo hai , hata hivyo vitu vya aina hio sio vingi lakini sio adimu pia”(Fossil ni mabaki ya kale)
Roma alijikuta pia na yeye kuchukia na kujiambia hio takataka kwanini iwe ndio Hazina , lakini kwa wakati mmoja alijiambia familia ya Sharif ni matajiri na hata kiboksi kilichotumika kuihifadhia ni cha madini ya Dhahabu, alijiuliza au ni kumbukumbu.
Roma mara baada ya kuona hakuna majibu ya haraka haraka alificha hazina yake alioona kama takataka na kisha akawaambia waondoke pamoja kwa ajili ya chakula cha mchana
Roma wakati akiwa njiani kurejea nyumbani aliweza kupokea simu kutoka kwa Sophia na kumweleza kwamba yupo Afrika ya kusini anashoot matangazo ya Promosheni ya filamu na angerejea Tanzania hivii karibuni kwa ajili ya Show ya siku ya usiku wa Christmas na Roma alimuahidi kwamba atahudhuria show yake.
Roma mara kutoka nje ya gari aliweza kumkuta Lanlan ambaye alikuwa amelalia tumbo kwenye kibaraza huku makaratasi mengi na penseli za kuchotea zikiwa zimezagaa huku pembeni yake akiwa amesimama Qiang Xi.
Muda huo ilikuwa ni jioni na Nasra alikuwa ameenda Supermarket kwa ajili ya kununua vitu vya kupika usiku.
Roma alimsogelea Lanlan na kisha aliinua karatasi ambazo alikuwa amemaliza kuchora na kisha aliona sura ya Superman na chini yake kuna jina la Daddy.
“Lanlan mimi ndio Superman?”Aliuliza Roma huku Lanlan akiwa bize kukoleza rangi ya mti aliochora na alimgeukia Roma na kutingisha kichwa kukubali kwamba ndio yeye.
“Na huyu mwanamke na msichana ni nani ?”
“Huyo msichana mdogo ni Lanlan na msichana mkubwa ni mama yake Lanlan , Mama ana nwele ndefuu mpaka shingoni”
“Umekosea, Lanlan wetu ni kibonge lakini huyu hapa ni mwembamba”
“Lakini Lanlan hapo amekonda kwasababu amemmisi mama yake”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu.
“Umekonda vipi wakati ulikuwa ukila chakula chote ambacho Aunt Nasra anakuandalia , hujakonda bwana”
“Lakini Lanlan atasikia njaa asipokula , ila anammisi mama yake”Aliongea huku akiwa kama vile anaona aibu kuumbuliwa na kumfanya Roma kutoa cheko.
“Aunt yako Nasra atakasirika , yaani amekupikia chakula kitamu lakini hujamchora?”
“Kwasababu mama simuoni na nammiss ndio maana nimemchora”Aliongea na kumfanya Roma kukaa kimya.
Sio kwa Lanlan ambaye tu alikuwa amemmisi Edna bali hata yeye mwenyewe alikuwa amemkubuka sana .
“Daddy ,Je Mama hatutaki tena?”Aliuliza huku akitia huruma na kumfanya Roma kushangaa.
“Lanlan , unapaswa kukumbuka kwamba mama yako anakupenda na kwasasa hana furaha ndio maana , kila kitu kitakuwa sawa muda si mrefu”
“Nina uhakika Mama ananipenda kwasasabu yeye ndio amenizaa”Aliongea Lanlan akiwa na uhakika na Roma hakuelewa ujasiri wake unatokana na nini.
Ilimfanya kuingiwa na majonzi kwa kuona pengine Lanlan ameshindwa kumtofautisha mama yake mzazi na Edna, Roma alishindwa kujizuia na kumkumbatia.
Qiang ambaye alikuwa akisikiliza maongezi hayo alijikuta akitokwa na machozi tu na kuishia kuyafuta kwa siri.
Hakuna ambaye angeweza kuamini kwamba Lanlan alikuwa ameficha kile anachojisikia na kujitahidi kuonekana ni mwenye furaha muda wote.
Usiku wa jumapili uliweza kuisha vizuri na Roma mara baada ya kuamka alijua ndio siku ambayo Edna atakuwa amerudi na ataenda kazini kama alivyosema Nasra.
Kuhusu hafla ambayo Maimuna aliongea hakutaka sana kuwazia maana ingemfanya tu kuwa na wasiwasi.
Roma alitaka kumsubiri Edna atakaporudi ndio aongee nae lakini alijiambia anapaswa kuchukua hatua yeye kwanza kama mwanaume , alijiambia pengine Edna anasubiria yeye aanze.
Hivyo mara baada ya wazo hilo kumuingia alienda moja kwa moja mpaka nyumbani na aliweza kukutana na Bi Wema ambaye alimwambia Edna alirudi lakini ameelekea kazini.
Roma palepale alifanya maamuzi ya kuelekea huko huko kazini kuonana nae.
Roma mara baada ya kufika ndani ya jengo la makao makuu ya kampui ya Vexto moja kwa moja alienda mpaka Floor ambayo ndio rasmi ofisi ya Mwenyekiti wa kampuni inapatikana , ni ofisini ileile ya Edna lakini ilikuwa imebadilsihwa tu hadhi.
Ijapokuwa Ernest ndio alikuwa CEO lakini hakuwa akitumia ofisi ya Edna ya mwanzo.
Roma mara baada ya kutoka kwenye lift moja kwa moja alitembea mpaka kwenye mlango wa kuingilia ofisni huku akipata burudiko la kiyoyozi na harufu ya kuvutia na kisha aligonga mlango lakini hakuweza kupata mrejesho.
Dakika ileile mlango wa ofisi ya Sekretari ulifunguliwa na aliweza kutoka msichana mrembo kiasi alievalia kinadhifu.
“Wewe ni Mr Roma?”Aliuliza.
“Ndio , wewe ni nani?”
“Mimi ni Sekretari mpya , naitwa Yulia , naamini hunifahamu , upo hapa kwa ajili ya kuonana na Mwenyekiti”Aliongea kwa namna ya heshima.
Ilionekana alikuwa na taarifa zote kuhusu Roma ni nani , ni kama kawaida mfanyakazi mpya lazima ajue Hidden rules za mazingira ya kazi ili kuepuka kufanya makosa na kuwa upande mbaya na watu wakubwa.
Roma aliishia kutabasamu kumuondolea woga , alijua atakuwa ni mbadala wa Recho ambaye alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara.
“Ndio yupo wapi?”
“Yupo kwenye kikao na Bodi ya wakurugenzi , wapo chumba namba tatu cha mikutano”
Kama ilivyotarajiwa , mwanamke mchapakazi ambaye hana mpango wa kuacha.
Roma hakuwa mgeni hivyo alijua chumba namba tatu cha mikutano kipo upande upi na mara baada ya kufika aliweza kuona viti vyote vilikuwa vimejaa na wafanyakazi wa juu wa makampuni pamoja na wanahisa , wote wakiwa na sura za kitaaluma.
Edna alikuwa amekaa mbele kabisa kawenye kiti cha kibosi akiwa kauzu kama kawaida yake , hakukuwa na ishara zozote kama alikuwa na mawazo na ilikuwa ni kama ukauzu wake uliongezeka zaidi na zaidi.
Kila mfanyakazi aliekuwa ndani ya hilo eneo alikuwa akimhofia Edna huku wengine wakionyesha heshima zao , ilikuwa ni kama mawaziri wanavyomheshimu mheshimiwa Raisi.
Baada ya Roma kufungua mlango na kuingia macho yote yalimgeukia huku baadhi ya Sura zikimwonyeshea tabasamu , akiwemo Ernest Komwe na Monika.
Upande wa Dorisi na Nasra walishangazwa na ujio wake kwani hawakutegemea kama angeweza kuja hapo mapema hivyo.
Roma aliwaonyeshea tu tabasamu na ksiha akageuza uso wake kwa Edna na kumwangalia kwa namna isiokuwa ikielezeka.
Kama sio jasiri usingeweza kuingia ndani ya chumba kama hicho ambacho kilikuwa na zaidi ya watu therathini.
Edna alionekana kukunja sura tu mara baada ya kumuona Roma lakini hakukuwa na mabadiliko makubwa , yaani alimwangalia kwa sekunde tu na kisha akampotezea kama hamjui.
Baadhi ya watu tayari walishagundua mabadiliko hayo na kuishia kuwaangalia kwa namna siokuwa ya kawaida.
Roma baada ya kuona namna Edna alivyomwangalia alijikuta akikosa furaha na aliishia kushika kidevu chake na kufunga mlago na kisha akaegamia ukuta kama bodigadi.
Ijapokuwa alitamani kuongea na Edna lakini hakuona haja ya kumsumbua akiwa katika kazi kama hivyo.
“Recho , please continue with your presentation”Aliongea Edna akimwashilia kwa kunyanyua karamu.
Kampuni hio ilikuwa ikitumia mara nyingi lugha ya kingereza katika vikao vyote na mara nyingi hata wafanyakazi wakifanyiwa usaili wanapimwa uwezo wao wa kuongea kingereza kwa ufasaha na kukielewa pia. Isitoshe lazima iwe hivyo kwani kulikuwa na wafanyakazi na baadhi ya wanahisa ambao ni wazungu wasiokuwa wakijua lugha ya kiswahili , akiwemo Rich pamoja na Ernest mwenyewe.
Recho alionekana kukosa utulivu mara baada ya kumuona Roma lakini alijakaza na kisha aligeukia Projector.
“Kutokana na kuundwa kwa Vexto group kimataifa , itahitajika kugawa majukumu kwa wafanyakazi wakubwa wa kampuni kwenda kufanya kazi katika matawi Tanzu ambayo yapo nje ya nchi ili kurahisisha mwenendo mzuri wa kampuni pamoja na kugundua fursa nyingine za kibiashara, Mwenyekiti wetu wa bodi anaamini sisi wafanyakazi wa ngazi ya juu tunapaswa kuwa mfano katika kutoa mchango wa maendelo katika kampuni hivyo , Mwenyekiti amependekeza Dorisi kupandishwa cheo kuwa sawa na Nasra na watapaswa kuondoka nchini kwenda kufanya kazi katika matawi yafuatayo , Dorisi ataelekea Cape Town Afrika ya kusini na Nasra ataelekea Buenos Aires Argentina, watakuwa ndio Wakurugenzi wa makampuni haya yote mawili ambayo yameanzishwa rasmi na kazi zao ni kujenga msingi wa kibiasara katika masoko hayo mapya.

SEHEMU YA 655.
Dorisi na Nasra ni kama vile hawakuwa wamesikia vizuri , hata Roma ambaye alikuwa amesimama vilevile ni kama hajasikia vizuri.
Afrika ya Kusini , Argentina?!!
Roma hakushangaa sana uwezo wa Edna kuchanja mbuga kimataifa hususani kutokana na mtaji waliokuwa nao , hivyo sio jambo la kushangaza kampuni ya Edna kuanzisha tawi jipya Argentina na Afrika ya kusini lakini alijiuliza kwanini anataka kuwatuma Dorisi na Nasra.
Bila shaka kama wataenda huko ilimaanisha kwamba madaraka yao pamoja na malipo yangekuwa makubwa zaidi lakini kuwaagiza wanawake hao wawili kwenda nje ya nchi ni sawa na kuwafukuza tu ndani ya Tanzania.
Dorisi na Nasra waliweza kuhisi kitu na waliishia kumwangalia Edna kwa macho yasiokuwa ya kawaida lakini Edna hakuwaangalia hata kidogo.
“Mwenyekiti , sote sisi tunajua michango mikubwa na uwezo wao mkubwa katika maendeleo ya kampuni na ni sahihi kuwa wakurugenzi wa kampuni tanzu lakini nadhani wangeweza kufanya kazi nzuri zaidi kama wangebakia hapa makao makuu kutokana na uzoefu wao”Aliongea Ernest Komwe akitoa mchango wake.
“Wanapaswa kuongoza kampuni kama ishara ya kutoa mfano kwa wengine watakaochukua nafasi zao , sitojisikia vizuri kama nikituma mtu ambaye sio mdhoefu na biashara zetu , isitoshe kwenda huko kutawafanya kupata uzoefu wa kimazingira , CEO Ernest vipi unataka kwenda wewe?”Swali hilo lilimfanya Ernest kufunga bakuli lake.
Monika ambaye alishawahi kufanya kazi kama msaidizi wa Edna alikuwa akijua tabia yake hivyo alimwangalia mume wake na kumpa ishara ya kutulia.
Kila mmoja alijua kama Dorisi na Nasra wataenda huko watafanya kazi nzuri sana lakini isingekuwa rahisi kwao kwani walikuwa wakienda kukutana na mazingira mapya.
Roma aliekuwa amesimama kwenye kona ya mlango alijikuta akikunja ngumi na kujiambia je anafanya hayo yote kwa ajili ya kumlipizia.
Alijiambia sio tu kwamba wakati huo alikuwa akimpotezea lakini ameenda mbali na kuanza kuwaondoa wanawake wake karibu na kuwatuma nchi ya mbali.
Bila shaka , kama kiongozi mkuu wa kampuni Edn alisifika kwa kutopenda kupingwa akiamua jambo lake , kwa jinsi ambavyo alimwagiza Recho kusoma mapendekezo yake ilikuwa ikimaanisha kwamba alishafanya maamuzi tayari.
“If there is no objection from the vice presidents , we can proceed with the voting process , raise your hand if you approve of this proposal”Aliongea akimaanisha kama hakuna pingamizi kutoka kwa watendaji wasaidizi wa kampuni basi anaekubaliana na pendekezo lake anyooshe mkono kupiga kura.
Kati ya wakurugenzi ambao walikuwepo ni Mzee Alex mmiliki wa zamani wa kampuni ya Jr ambaye ipo chini ya Edna kama mwanahisa mkuu na wote kwa pamoja waliangaliana na kisha walionekana hakuna ambaye alikuwa akipinga kwani walinyoosha mikono kupiga kura ya ndio.
Yaani kwa jinsi wanahisa hao walivyonyoosha wote pasipo ya yoyote kutopinga ni kama vile walikuwa washajiandaa,
Recho alisimama kwa ajili ya kuhesabu kura hizo lakini Edna alimzuia.
“Hakuna haja ya kuhesabu , tayari tuna asilimia hamsini ya kura zote wanaokubali kabla sijatoa kura yangu , inaonyesha wengi wenu mmekubaliana na pendekezo langu , Miss Dorisi na Miss Nasra matawi yote mawili hayajamaliza hata miezi sita tokea yafunguliwe hivyo tunategemea kazi kubwa yenye mchango chanya kutoka kwenu”
Dorisi aliishia kuwa kimya huku macho yake yakiwa tayari ni makundu , ni kama vile muda wowote angetoa machozi , upande wa Nasra alionyesha hasira na wasiwasi kwa wakati mmoja.
“Edna kuna haja ya kwenda mbali hivi , inaonyesha hapa kabisa ulishaongea na Shareholders kupiga kura ya ndio ili sisi kwenda nje ya nchi mbali na Tanzania , umefurahi sasa?”Alisimama Nasra na kubwata huku akimwangalia Edna kwa macho makavu.
Watu wote kimya , hakuna ambaye alikuwa tayari kuongea lolote , ni kama walikuwa wakitarajia dhoruba kuamka muda wowote.
Ilionekana kwa watu hao ni kama kweli Edna alikuwa akifanya makusudi kabisa na hakujisumbua hata kuficha dhamira yake na ilionekana ni kama kuwadhalilisha mbele ya kila mtu.
Lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa tayari kupinga maamuzi ya Edna , licha ya kwamba maamuzi yake yalionekana kuwa na ukakasi.
Mtu pekee ambaye hakupiga kura ya ndio au hapana alikuwa ni Mzungu Richie peke yake , alikuwa amefumba macho kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza.
“Sijaelewa unachotaka kumaanisha”Aliongea Edna akimwangalia Nasra.
“Edna acha maigizo , unakasirisha ujue”Aliongea Nasra akiwa amepaniki hatari.
“Kama hukubaliani na maamuzi ya bodi , tunakukaribisha muda wowote kuleta barua yako ya kujiuzulu”
“Unadhani nnitashindwa kufanya hivyo?”
“Sidhanii hivyo , najua zipo kampuni nyingi ambazo zinakuhitaji”Aliongea Edna bila ya kuonyesha hisia zozote ni kama vile hakuwa akimjua Nasra,
“Benadetha utadili na hili swala , kama Mkurugenzi Mtendaji Nasra akitaka kujiuzlru nipo tayari kununua hisa zake zote kwa thamani mara mbili iliopo sokoni”Aliongea na Benadetha ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kutingicha kichwa tu.
“Edna unafikiri nimesema haya kwasababu ninajali sana kuhusu hisa zangu , unafikiri nitakuwa na furaha kama utanipa hela?”
“Furaha yako hainihusu , asante kwa mchango wako uliotoa kwa kampuni , sitokutendea vibaya kama utaamua kujiuzulu”Aliongea na kumfanya Nasra kujibwaga kwenye kiti huku akimuona kama Edna sio yule ambaye alikuwa akimjua.
“Nasra huna haja ya kuwa hivi , Mwenyekiti wa bodi ashafanya maamuzi lakini ni kweli hatuwezi kwenda nchi za mbali hivyo kwa ajili tu ya kazi hivyo chaguo lililobaki ni kujiuzulu”Aliongea Dorisi.,
“Dorisi unamaanisha nini kwamba hatuwezi , tatizo hapa sio kwenda mbali hivyo , shida ni kwamba hajaongea na sisi kabla , anatuchukulia sisi kama takataka kututupa kila mahali anapoona panafaa , nimeamua kufanya kazi hapa sio kwasababu sina sehemu nyingine ya kwenda kufanya kazi , sijali sana kuhusu nafasi yangu wala mshahara ninaopata wala hisa ninazomiliki, lakini mimi pia kama mfanyakazi wa hii kampuni nina kanuni zangu na utu wangu ambao unapaswa kuheshimiwa”
Dorisi aliishia kukunja sura , alikuwa akijua Nasra alikuwa sahihi lakini ilionekana haiwezekani kuweka mstari kati ya maswala ya kazi pamoja na mambo binafsi.
Dorisi mara baada ya kuwaza hivyo alijikuta akimgeukia Roma na kumpiga jicho na aliweza kugundua alikuwa kwenye mawazo pia kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza , kwani alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Edna tokea siku ambayo nilijiunga na kampuni hii , sijawahi kuwaza kama nitapata chochote , , bibi yako na mama yako ndio watu ambao wamenifanya kuwa Nasra wa leo hii kwa kila kitu nilichokuwa nacho na siku zote nitaendelea kuwa mwenye shukrani , kama shukrani zingeweza kupimwa katika kipimio cha hela basi ningesema faida ambayo nimeingiza kwenye hii kampuni imepita deni ambalo mama yako ananidai , kama sio wewe kuongoza hii kampuni nisingejisumbua kufanya kazi ndani ya kampuni moja kwa miaka yote hio , sikuacha kufuata ndoto zangu na kufanya bidii kwa ajili ya mafanikio ya hii kampni kwa ajili ya mtu yoyote bali nimefanya yote hayo kwa ajili yako , Edna najua ni kweli kabisa nimekukosea wewe binafsi lakini kwanini unataka kunidhalilisha kazini , sijui wengine watanionanje lakini mimi kama mwanamke mwenzio nimekudharau”
Roma alijikuta akiinua uso wake na kumwangalia Nasra ambaye hakutaka kuonekana mnyonge mbele ya Edna , hali yake ya kujiamini na ujasiri wake ilimkumbusha na kumuona kama mwanajeshi.
Edna muonekano wake haukuadilika kabisa , ni kama vile hajamsikia kwa chochote kile alichoongea .
“Kama Miss Nasra na Miss Dorisi watachukua maamuzi ya kujiuzuru , majukumu yao ambayo walikuwa wakiyafanyia kazi kwasasa yatakuwa chini ya Recho , Benadetha pamoja na Rich , nitapenda kuona kila mmoja wenu kuanza kufikiria ni nani ambaye anafaa kurithi kazi zao kabla ya kikao kingine au vinginevyo nitafanya hio kazi mwenyewe”Aliongea kwa kujiamini kabisa.
Ukauzu wake na hali ya kujiamini na kutoathirika iliwaanya wafanyazi kumhofia na kujiuliza inakuwaje akawa haathiriki kwa chochote kutokana na kubweka kwa Nasra.
Nasra alijikuta akimpiga jicho la chuki Edna na palepale alikusanya kila kilichokuwa chake na kisha aliondoka akiwa wa kwanza, ilikuwa ni kama vile alikuwa amepoteza muda mwingi wa kufanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto.
Ni Dorisi peke yake ambaye alijitahidi kuzuia hisia zake zisimvae na palepale na yeye alikusanya vitu vyake na kumsogelea Roma na kumpa ishara ya kumfuata.
“Bado tu unataka kubakia hapa?”Aliuliza Dorisi na Roma alijikuta moyo wake ukijinyonga, katika mazingita kama hayo kama angeonyesha kusita sita ingewafanya kujisikia vibaya zaidi hivyo aliuvaa ujasiri na kisha akawashika mkono na kuondoka nao.
“Tutaenda kwenye hoteli yoyote, na nitawaruhusu mywe bia hadi mlewe mpunguze mawazo , mnaonaje?”Aliongea Roma na wote walitingisha kichwa na kuondoka.
Roma alifanya kama alivyowaambia na aliwapeleka katikati ya jiji na kisha akawaagizia chakula pamoja na vilevi na siku hio Dorisi na Nasra walikichafua haswa kiasi kwamba walilewa chakali.
Baada ya kuelwa wote hakuna ambaye alitaka kuondoka na Nasra na Dorisi wote walitaka kulala hotelini na Roma licha ya kwamba ilikuwa mchana bado.
Roma mara baada ya kujifikiria kidogo aliona awape kile walichotaka na palepale alienda kuchukua chumba na kisha aliwabeba wote kwa pamoja na ulevi wao na kuwabwaga kitandani na kupiga Treesome ya nguvu kwa muda mrefu na mpaka anakuja kumaliza wote walionekana kutosheka na bakora za kimkakati na waliishia kukumbatiana na kisha wakapitiwa na usingizi.
Roma alijikuta akitingisha kichwa na palepale aliangalia saa na kuona ni saa kumi na moja kuelekea saa kumi na mbili.
Ijapokuwa Edna alionekana alikuwa amebadilika nje kabisa ya mategemeo yake lakini hakutaka kupitisha hio siku bila ya kuongea nae , hivyo aliingia bafuni na kuoga na kisha akavaa na kuwaacha.
Kwa spidi aliotumia kuendesha ilimchukua dakika chache tu kufika Ununio na ile anaingia katika barabara ya Ununio Road aliweza kuona gari ya Edna kwa mbele akionekana ndio anarudi kazini.
Dakika chache tu gari iliweza kuruhusiwa kuingia ndani ya geti tena kilichomshangaza zaidi Roma ni kwamba ijapokuwa geti lilikuwa likijifungua lenyewe lakini lilifunguliwa ‘Manual’ tena aliefungua ni Lanlan ambaye pembeni yake alikuwa amesimama Bi Wema.
Roma hakujisumbua kuingiza gari ndani kwani alitoka palepale na kukimbilia ndani,.
“Edna subiri”Aliongea Roma mara baada ya Edna kutoka nje ya gari baada ya kuliegesha lakini ni kama hajamsikia Roma.
Lanlan ambaye alikuwa ndio anamalizia kufunga geti alijikuta akitoa tabasamu la furaha na kuanza kumkimbilia mama yake kwa shangwe huku akimwita Mama.. Mamaaa..
Edna mara baada ya kuitwa vile alisimama na ksiha akamgeukia Lanlan na kumwangali kama vile hamjui.
“Umemuita Mama mtu asiesahihi , mimi sio mama yako”Aliongea kwa Kingereza huku akimtoa Lanlan mikono ambayo imemshikilia.
Kitendo cha Edna kumwambia Lanlan vile kilimfanya kumwangalia kwa macho ya kutia huruma na palepale aliishia kuchuchumaa na kuanza kudondosha machozi chini.
Roma alietaka kuongea tena alijikuta mdomo wake ukiishia hewani na hasira zilimpanda mara baada ya kumuona binti yake akilia.
Lanlan alikuwa na furaha ya kumuona mama yake kwa mara nyingine na hata ujio wake hapo ni kutokana na kujua huo ndio muda wa kurudi kazini lakini jibu la Edna lilimnyong’onyesha , alikuwa ni kama vile amemwagiwa ndoo ya maji ya baridi.
Roma alikubali Edna kumchukia yeye lakini alijiuliza kwanini anamfanyia hivyo na Lanlan ambaye anamchukulia kama mama, uvumilivu palepale ulianza kumpotea.
“Edna naona sasa unavuka mpaka”Aliongea Roma kwa namna ya kufoka huku akimpakata Lanlan na kumfanya machozi yake yaloanishe kifua chake
“Mommy doesn’t want Lanlan again …Mommy doesn’t like me anymore..”Aliongea Lanlan akilia akisema kwamba mama hamtaki tena na mama yake hampendi.
Kilio cha Lanlan kiligusa moyo wa Bi Wema na alijikuta akimsogelea Edna na kumwangalia usoni.
“Edna unafanya nini , huwezi kutolea hasira zako kwa mtoto kisa tu mna ugomvi”Aliongea Bi Wema na palepale alimsogelea Lanlan kwa jaili ya kumtuliza lakini ilikuwa ngumu kutulia.
Lanlani alikuwa na kumbbukumbu za kuachwa na mama yake kwa mara ya kwanza hivyo hicho kinachotokea ni kama alikifananisha na kumbukumbu zake mbaya zilizopita ndio maana kilio hakikiwa cha kawaida.
“Bi Wema mimi sitaki kuhusika nao tena , huyo ni mtoto wake na sisi tumeachana, ni kwamba tu hatujasainishiana maswala ya talaka kwani kuna taratibu za kuchukua”Aliongea
Roma alikuwa akitetemeka kwa hasira mno kutokana na kilio cha Lanlan na alijihisi ni kama ule uchizi wake wa siku nyingi unaanza kumvaa.
“Edna ,,, unaweza kunichukia utakavyo na sitolaumu lakini umemuumiza binti yangu kihisia ,, na hii ni sababu ambayo inanifanya nitake kukua sasa hivi..”
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
WATSAPP:0687151346.

Mono no aware.

SEHEMU YA 655
Bi Wema licha ya kwamba alikuwa na hali ya kutoridhishwa na tabia ya Edna kutolea hasira zake kwa Lanlan lakini hakutaka kumuona akidhulika kwa namna yoyote ile mara baada ya kusikia kauli ya Roma kwamba anataka kumuua.
“Hapana Mr , usiwe mwepesi hivyo , Edna anakufanyia makusudi tu”Aliongea Bi Wema kumtuliza Roma, hakujua kama Roma alikua kwenye hali isiokuwa ya kawaida kwani haikuwa swala tu la kuchanganywa na Edna kwa kukosa huruma lakini kilio cha Lanlan kilikuwa ni pigo lingine ambalo liliathiri moyo wake.
Watu wawili muhimu kwenye maisha yake waliweza kumpa pigo katika akili yake, ilikuwa ni kama vile hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kuziba shimo ambalo limejitengeneza katika moyo wake.
Muda huo akili yake ilikuwa katika hali hatarishi ya kuweza kumezwa na nguvu ya roho ya mnyama iliokuwa ndani yake , ni kama ilichukulia wakati huo ambao hakuwa sawa kiakili kutaka kujaribu bahati ya kuutawala mwili wa Roma.
Roma uwezo wake wa kujidhibiti ulikuwa umepungua kutokana na hali aliokuwa nayo ndio maana alisema anataka kumuua Edna licha ya kwamba hakuwa akidhamiria kufanya hivyo.
Nia ya roho ya kipepo ya mnyama ilikuwa wazi kabisa kile ambacho ilikuwa ikitaka kufanya, ilikuwa ikimsukuma Roma kumuua Edna ili baada ya hapo Roma awe kwenye majonzi makubwa na mwisho wa siku kukosa mhimili na kuchukua mwili wake.
Roho ya kipepo ya mnyama huyo mpango wake ilikuwa ni kuiba uwezo wa kijini wa Roma na baada ya hapo kutawala akili yake na kurudi hai tena kwa kuua roho ya kibinadamu ya Roma na ndio ingekuwa mwisho wa kuishi katika gereza la Cauldron.
Roma akili yake ilicheza haraka sana na kuona roho hio inachotaka kukifanya na alijitahidi kukunja ngumi pamoja na kung’ata meno kwa nguvu kujizuia akili yake isimpotee.
Hakuwa akishindana na Edna bali alikuwa akishindana yeye mwenyewe na Edna hakuwa akilijua hilo, pengine angekuwa na uelewa angepunguza jeuri.
“Unadhani naogopa kufa , kama ningekuwa naogopa nisingeomba Talaka”Aliongea Edna kijeuri.
“Wewe…
Roma alikuwa akipambana na akili yake na maneno yake ni kama yalikuwa yakimsaidia zaidi roho iliokuwa ndani yake kushinda , ijapokuwa asingeweza kumuua lakini hakutaka kujizuia kumpiga kibao.
Lakini kabla hajamkaribia tu Lanlan alianza kumpigia makelele kumtaka asimpige mama yake.
“Daddy don’t hit mommy , Don’t hit her”
Sauti ya Lanlan iliokuwa kali kwenye masikio yake ni kama neno la upako katika akili ya Roma kwani palepale aliweza kuidhibiti akili yake na kuiweza nguvu ya mnyama wa maafa.
Uhusiano wa mtoto na baba katika ulimwengu wa kiroho siku zote unakuwa na nguvu mno , nguvu ya kuweza hata kushinda roho za giza na hiki ndio kilichotokea , sauti ya Lanlan ni kama maneno ya kichungaji au kishekhe.
Katika maisha unahitajika kuwa na sababu kubwa ya kuweza kukupa motisha ya kuendelea kuishi hivyo Roma mara baada ya kuisikia sauti ya Lanlan ni kama ukumbusho kwake kwamba ana mtoto wa kumlea.
“Lanlan hakuwa mtoto mzuri….Lanlan hatakuja kumtafuta mama tena”Lanlan aliongea huku akifuta makamasi yaliochaanganyika na machozi huku akimwangalia Edna kwa mara ya mwisho na kisha kukificha kichwa chake asimuone tena.
Kauli ya Lanlan ilimpa Roma uchungu mwingi moyoni lakini hakuwa na la kufanya, angewezaje kumpiga Edna mbele ya mtoto wake.
“Ninaenda kupumzika ndani kama huna kingine cha kuongea , nipo bize”Aliongea Edna huku akibana vizuri mkoba wake kwapani.
“Subiri..”
Roma hakutaka kumruhusu kuondoka kirahisi , alikuwa bize kushindana na mnyama wa maafa hivyo hakuweza kupata muda wa kuuliza maswali.
“Edna , unasababu yoyote … siamini kama unaweza kuwa mkatili hivi , kama unasababbu kwanini usiniambie , tumepitia magumu mengi pamoja , hivi huamini uwezo wangu , kwanini tusikae chini tukaongea hili likaisha kama wanandoa ?”Roma alongea akiwa katika hali ya matarajio ya jibu la Edna.
Bi Wema hata yeye aliona alichoongea Rioma ni sahihi na kutamani Edna kuurudisha moyo nyuma na kuyamaliza.
Kama kawaida Edna alimwangalia Roma kwa sura ya kejeli huku akitoa tabasamu la kuchukiza.
“Acha kuwa kichekesho, mkataba wangu wa ndoa na wewe ushaisha na sasa nafanya ninachotaka”
“Siamini kama umebadilika hivi ghafla tu”
“Kama unataka tuendelee kua pamoja sawa , lakini lazima nikwambie ukweli hapa hapa uelewe , ni aidha unichague mimi au binti yako”Aliongea akiwa siriasi kabisa.
Roma na Bi Wema walijikuta wakibumg’aa , hakuna ambaye aliweza kuamini masikio yake kama yamesikia vizuri , yaani Edna anamwambia Roma kwamba achague kuishi na Lanlan au amuache aishi na yeye.
“Hapana huyu ni mtoto pekee wa Seventeen na pia ni binti yangu , nawezaje kumuacha ?”
“Kama ni hivyo kesi imeisha ..”Aliongea huku akimwangalia kwa tabasamu la kumdhihakki
“Nina weza kukubaliana na michepuko wako kwasababu hawana uwezo wa kushindana na mimi na ninajiamini, lakini siwezi kukubali kushindania penzi na mwanamke aliekufa ukijumlisha na mtoto alieacha .. kila saa ninapomfikiria Lanlan ninajihisi ni kama vile namuona huyo mwanamke pembeni yako , hata kama umesema mimi sio mbadala wake lakini kwangu nakuona kama mnafiki tu , kuendelea kumuona mbele yangu ni kama tusi kwangu na najihisi kama vile ndoa yetu ni kichekesho kiasi cha kunipatia maumivu makali ambayo sijawahi kuyapitia hapo kabla , maadam huyo mtoto atakapoendelea kuwa na wewe huwezi kumsahau Seventeen kwasababu ndio mwanamke ambaye unampenda sana, mwanamke ambaye ameweza kukuzalia mtoto”
Maneno ya Edna yalikuwa makali mno kuyasikia , ni kama yalikuwa yakiurarua moyo wake.
Alishindwa kuamini ni kweli kwake akimuona Lanlan alikuwa akijisikia kama anateswa kwasababu tu ya Seventeen.
Dakika hio Roma alijiuliza je lilikuwa kosa kumtambua Lanlan kama binti yake kwa kumzaa lakini aliona bado alikuwa sahihi asingemfanya Lanlan kutambulika kama mtoto wa kuasili ilihali yeye ni baba yake mzazi, isingekuwa haki.
“Nadhani tamaa yangu imeniponza , upo sahihi , sijui kama nakupenda sana wewe kuliko Seventeen lakini jambo moja ambalo nina uhakika nalo ni kwamba siwezi kumuacha mtoto wangu kwa namna yoyote ile”
“Ni afadhali umelitambua hilo kwaheri”Aliongea na kisha aliingia ndani bila ya kuangalia nyuma.
“Mr hakuna chochote kingine ambacho unaweza kufanya?”Aliuliza Bi Wema ambaye alikuwa kwenye majonzi.
“Bi Wema najua wasiwasi wako na unahitaji hili liishe lakini nakuomba usiwe na huzuni , unapaswa kuwa na furaha kwa ajili ya Rufi”
“Kwanini niwe na furaha kwenye hali kama hii , hata Rufi mwenyewe hawezi kukubali wewe kuachana na Edna”Aliongea
“Bi Wema nadhani ni muda sahihi kumuacha sasa aende , ni makosa kuendelea kubakia hapa na kumsumbua, isitoshe ndoa yetu imeanza na sintofahamu nyingi , ni kama wakati unapofundishwa kuendesha baiskeli kwa mara ya kwanza unaambiwa unapaswa kugeukia upande unaotaka kudondokea na sio upande mwingine , hivyo ninachoweza kufanya kwasasa ni kuendana na hali ilivyo tofauti ya kuwa king’ang’anizi wa kubadilisha mueleko wa hali , Edna anaweza kunidharau kwa kumchagua binti yangu na kumuacha yeye, anaweza kutokuwa sawa japo siwezi kuona lakini ninachojua hana rafiki wa kuongea nae , naomba umsikilize kile ambacho ataongea , kama akilia msaidie kufuta machozi, kama ataniongelea vibaya muunge mkono , kama akikuuliza nimekuambia chochote naomba umwambie …’ I am sorry’ kwa kila kitu”Aliongea Roma na maneno yake pamoja na muonekano wake vilimfanya Bi Wema na utu uzima wake kushindwa kujizuia kutoa machozi kwani Roma alikuwa akitia huruma.
“Edna anachofanya ni utoto , kitu muhimu kuwafanya wenza kudumu ni upendo , ujuaji una athari ya vitu vingi”
“Kila mtu ni tofauti Bi Wema..”Aliongea Roma na muda huo huo macho yake yaligeukia upande wa getini nje mara baada ya kuona gari aina ya Bentley ikisimamishwa na akili ya Roma haraka haraa ilimwambia huyo lazima atakuwa ni Maimuna kwani alikuwa na miadi nae ya kukutana siku hio.
“Bi Wema kuna sehemu napaswa kwenda , naomba unisaidie kumpeleka Lanlan nyumbani kwa Nasra na umwambie Qian Xi kwenda nae mgahawanni kumnunulia chochote anachotaka maana Nasra hatorudi”Aliongea Roma huku akimkabidhi kwa Bi Wema.
Dakika hio hio Maimuna aliweza kusimamisha gari nje ya geti ambalo halikuwa limefungwa vizuri na kutoka nje ya gari na kuingia ndani kabla hata hajakaribishwa.
Alikuwa amevalia gauni refu rangi nyekundu na kikoti cha rangi nyeusi juu yake , nywele zake hakuwa amezifunga zaidi ya kuzichana kuzirudisha nyuma na miondoko yake ilikuwa ile ya kushawishi macho ya watu kumwangalia.
Baada ya kuingia ndani aliweza kumuona Lanlan na Bi Wema ambao wote walikuwa na dalili ya kulia na kuonyesha mshangao kwa sekunde lakini dakika ileile aliupotzea kwa kuupamba uso wake na tabasamu na kisha alimkimbilia Roma na kwenda kujirusha kwenye mikono yake , kwa jinsi ambavyo aliweza kujikumbatisha kwa Roma ni kama vile alishawahi kufanya hivyo mwanzo.
Roma aliweza kunusa harufu kali ya marashi ya kuvutia kutoka kwa mwanamke huyo na ukweli alishindwa kumkwepa ndani ya muda na kuishia kushika ngozi yake laini , ilikuwa ni kwasababu hakumtegemea kama angekuja kumkumbatia.
Roma ile anataka kujitoa kwake palepale alipitisha mikono yake kwenye shingo huku miguu yake akiipitisha kwenye kiuno cha Roma na kuning’inia kama mtoto mdogo, alienda mbali zaidi na kusugua manyonyo yake yaliosimama katika kifua cha Roma.
Mrembo huyu hakujali sehemu hio ni nyumbani na Edna alikuwepo , ilikuwa ni kama vile alikuwa akifanya makusudi.
Roma jambo lile lilimshangaza na kujiuliza huyu mwanamke anafanya nini , kwanini anafanya haya yote ghafla tu.
“Hehe… Roma huyo ndio binti yako ? She is cute”Aliongea huku akimwangalia Lanlan kwa tabasamu.,
Bi Wema alikuwa kwenye mshituko mara baada ya kumuona mwanamke mrembo kama huyo ambaye hakuwa akimjua akimkumbatia Roma kama vile wanafahamiana na aliishia kumwangalia Roma kwa maswali mengi.
Roma alijikuta akijisikia vibaya kutokana na kitendo hicho kwani pia alikosa maelezo ya kutosha ya kujielezea na aliihisa kujitoa katika mwili wa Maimuna.
“Sidhani kama tuna ukaribu wowote” Aliongea Roma akijaribu kuweka usiriasi kwenye uso wake kutokana na kutokuwa kwenye mudi nzuri lakini maneno yake ya moja kwa moja hayakumuathiri Maimuna.
“Najua jina lake anaitwa Lanlan Ramoni Kweka, ana jina zuri mno , linaendana na muonekano wake”Aliongea na kumfanya Roma kukunja ndita.
“Inaonekana umefanya utafiti wa kutosha”
“Sio vibaya kujua maisha ya mwanaume ninaemtamani”Aliongea huku akimkonyeza Lanlan .
“Acha maneno mengi , nipeleke kwenye hio sherehe”
“Tunaenda babu lakini haina haja ya kuharakisha ..”Aliongea na palepale alitoa Bracelet(bangiri ) ya Dhahabu ambayo juu yake ilikuwa imetengenezewa ua la kumeta meta la madini ya rangi ya Samawi, ilikuwa ni Bracelet ya ajabu mno kuangalia na mwanga wa jua linalozama uliifanya kuwaka wake pale mbele.
Baada ya kuishikilia mkononi alimsogelea Lanlan huku akiwa na tabasamu na kumpa ishara ya kupotkea.
“Lanlan hii ni zawadi yangu kwako”
Hata kama alikuwa ni mdogo lazima angejua kitu kilichokuwa mbele yake kilikuwa kizuri na cha thamani na pengine mtoto yoyote asingekataa lakini kwa Maimuna ilionekana ni kosa alilofanya mbele ya Lanlan.
Zawadi yake hio pengine kwa watoto wa kike wa kawaida wangeipokea lakini ilikuwa ni tofauti kwa Lanlan ambaye alishazoea kuona vitu vizuri kama hiyo hususani alikuwa akiona Bracelet ya Almasi ya Nasra ambayo alikuwa akivaa na pia Edna alikuwa akimiliki jiwe kubwa la madini ya Rubi ambalo alipewa na Roma baada ya kutoka ulimwengu wa maijini pepo.
“Its not tasty , I don’t want it”Aliongea huku akigeuzia kichwa chake pembeni akionyesha ishara ya kutotaka kabisa hata kumwangalia.
Tabasamu lote ambalo lilikuwa limeupamba uso wa Maimuma lilipotea palepale na kubakia kuwa katika mshangao.
Alijiambia inakuwaje zawadi yake isiwe tamu , kwani hiko ni chakula.
Alijiambia hakika mtoto wa kichaa ni kichaa vilevile.
Bi Wema alijikuta akifurahishwa na jambo lile na alitatami kucheka na aliishia kukakamaa mwili kujizuia mbele ya mgeni.
Roma pia alitamani kucheka lakini hakutaka kucheka kwani angeharibu taswira yake , lakini hata hivyo ili kumuonyesha kama Lanlan amefanya jambo la maana palepale aliigiza kama anaingiza mkono mfukoni na alipoibuka alitoka na jiwe lingine la Yakuti ambalo alitoka nalo katika ulimwengu wa majini pepo.
“Yaani unatumia hio takataka yako kutaka kumhonga mtoto wangu , inaonekana familia yenu ya Sharif sio matajiri kama nilivyoambiwa”Aloiongea Roma huku akihakikisha Maimuna anaona lile jiwe la kung’aa sana na kupendeza , kwani alilipitisha taratibu taratibu kama vile yupo kwenye slow motion.
“Lanlan binti yangu ninaekupenda hili jiwe zuri ni kwa ajili yako , Daddy anatoka leo hivyo kuwa mtoto mzuri na kaa nyumbani na aunt Qiang sawa, utaenda nae mgahawani kula chakula chakula cha usiku sawa”Aliongea Roma
Lanlan alijikuta akitoa meno yake madogo huku akitoa kicheko wakati wa kupokea jiwe la thamani , lilikuwa dogo kuliko la mama yake lakini alipenda rangi yake.
Maimuna macho yake yalikuwa kodo kwenye jiwe hilo la ajabu ambalo ni kama vile ni mara yake ya kwanza kuliona .
Alijiambia mbona jiwe hilo ni kubwa hivyo …My goodness ,, the purity and size it would’ve cost 50 million dollar on the Market and he just gave it to a kid as a toy!?
Maimuna hakutaka kuamini , ijapokuwa alijua familia ya Roma ilikuwa na uwezo mkubwa ndani ya taifa hili lakini nguvu yake kubwa ilikuwa ni kwenye maswala ya kijeshi tu na sio maswala ya utajiri., kitu pekee ambacho aliona pengine hakuwa akikijua basi ni Roma wenyewe ndio tajiri,
Maimuna alijikuta aking’ata lipsi zake huku kijasho chembamba kikianza kumtoka , alijiambia pengine hakuwa akimjua Roma vizuri .
Alijiambia pengine alichokuwa akikijua ni kidogo sana kuliko kile ambacho alikuwa akimjua nacho na jambo hilo lilimfanya kumpenda na kumchukia kwa wakati mmoja.
Kwa mwanamke kama huyo hakuwa na matamanio na mwanaume wa kawaida anaetokea katika familia yenye utajiri mkubwa lakini asingeweza kujizuia kutoka kimapenzi na mwanaume wa ajabu na kushangaza kama Roma.
Utajiri na madaraka ni vitu vya juu juu na kitu cha kutamanika zaidi ni nguvu halisi pamoja na haiba ya mwanaume ilivyo.
Hata hivyo hakutaka kujilaumu kwani babu yake mwenyewe hakuwa na taarifa zote kumuhusu Roma nje ya nchi.
Inasemekana kwamba licha ya familia ya Mzee Sharif kuabudu majini ambayo ni chanzo cha utajiri wao lakini pia walikuwa na uhusiano wa karibu na jamii za siri kama vile Freemason na walikuwa wakishirikiana kwenye mambo wanayoendana nayo sambamba ki ajenda.
Familia hio haikuwa na ukubwa kwama wa familia ya Rothchild ambayo ilikuwa ipo kila kona ya dunia lakini walikuwa wamejitengenezea sehemu yao ndani ya dunia.
Maimuna alijua pengine ndio maana Afande Kweka alitangaza kilichotokea aadhibiwe Roma mwenyewe , lakini akiwa na uhakika kwamba Roma ana nguvu ya kushinda.
“Huna ubahili wa aina yoyote … vipi tunaweza kuondoka”Aliongea Maimuna huku awamu hii akiwa mpole lakini hakuacha kutaka kujigusisha na Roma.
Roma alijiambia sjui huyo mwanamke ana kiu ya mwanaume ndio maana matendo yake yapo hivyo au ni nini.
Baadaa ya kumuaga Bi Wema na Lanlan Roma alitoka na kuingia ndani ya gari.
Upande wa Maimuna kabla hata hajaingia ndani ya gari aligeuza shingo yake ndefu na kuangalia nyumba hio na kisha akatoa tabasamu la kejeli.
Baada ya kuingia hatimae gari iliweza kutoka eneo hilo kuelekea katika hoteli ya Wache ambayo ilikuwa Kigamboni.
Asichokijua Roma ni kwamba mara baada ya gari yao kuondoka pazia la dirisha katika Floor ya pili lilionekana kufungwa vizuri na Edna ambaye alikuwa akichungulia.

SEHEMU YA 656.
Ni ndani ya jumba moja la kifahari ambalo lilikuwa lipo Kawe , jumba hilo siku hio lilionekana kuwa na ulinzi mkali kuliko siku zote.
Hio ni moja wapo ya nyumba ambayo mmiliki wake ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Senga Cammilius Kweka , ilikuwa ndio nyumba yake ya mapumziko mara nyingi anapokuwa ndan ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maswala ya kikazi,
Siku hii ndani ya nyumba hio kulikuwa na ugeni kwani mheshimiwa alikuwa akitarajiwa kufika hapo muda wa jioni ya saa moja usiku.
Ijapokuwa wengi waliamini Raisi Senga anafika hapo kwa ajili ya mapumziko kama kawaida yake lakini ukweli ni kwamba alikuwa na miadi ya kukutana na mtu kwa ajili ya kufanya kikao cha siri.
Raisi Senga hakuwa akiamini eneo la Ikulu hata mara moja mathalani kwa wale watu ambao wanamlinda ndio maana kila linapotokea swala nyeti sana ambalo linahitaji usiri mkubwa mara nyingi angesafiri kwenda mikoani kwenye ikulu ndogo au angetoa kisingizio cha kwenda kupumzika katika nyumba yake hio , huku akihakikisha watu anao ambatana nao ni wachache tu wale ambao alikuwa akiwaamini.
Saa moja kamili gari kadhaa za rangi nyeusi za brandi tofauti tofauti zilionekana zikiingia ndani ya jengo hilo.
Uzuri wa mazingira ya eneo hilo yalikuwa yametengena sana na maeneo ya makazi ya uswahilini ya watu hivyo ni watu wachache sana ambao walikuwa wameshuhudia gari hizo.
Baada ya saa moja kupita baada ya gari hizo kuingia hatimae ilionekan gari nyingine ikiingia ndani ya hilo eneo , gari hio ilikuwa ni gari aina ya Aud SUV rangi nyeusi.
Baada ya kusimama eneo la getini kwa dakika kama tano hatimae gari ile iliweza kuruhusiwa kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani hatimae aliweza kuonekana mwanadada Suzzane na Nadia Alfonso wakishuka.
Wote kwa pamoja walikuwa wamevalia mavazi ya suti zinazofanana za rangi nyeusi na walionekana kama vile ni wanausalama.
Suzzane ndio ambaye alionekana kidogo kuwa na wasiwasi lakini kwa upande wa Nadia Alfonso hakuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi , pengine ni kutoana na uzoefu wake.
Baada ya kushuka hawakuacha kukaguliwa na walinzi na kisha dakika chache alitokea Kabwe msaidizi wa karibu zaidi wa raisi kaatika kitengo cha ndani cha siri cha raisi na kuwapokea.
Kabwe mara baada ya kusalimiana nao kwa ufupi aliwapa ishsara ya kumfuata huku yeye akitangulia kuelekea mbele.
Mazingira ya eneo hili hakika yalikuwa yakivutia mno , ni sahihi kusema eneo hilo ni maalumu kwa ajili ya mapumziko kwani lilikuwa limejengwa kwa ufanisi mzuri mno , mtu yoyote ambaye angefika hapo lazima angesema ni ufahari wa juu sana kuwa raisi wa nchi.
Lakini upande mwingine kama kauli hio angeisikia Raisi Senga pengine angepingana nayo , kwani kuwa raisi kwake alichukulia ni kama swala la kujitoa, ni kweli kuna faida zitokanazo na uraisi lakini baadhi ya siri ambazo anazibeba kwa ajili ya taifa zilikuwa kubwa mno ambazo zilihitaji akili yenye utimamu mkubwa.
Nadia alimwangalia Suzzane kwa ishara ya kumwambia kwamba anapaswa kujiamini na kisha waliendelea kusonga mbele.
Ukweli ni kwamba mwanzoni Suzzane ndio alipanga kuja kuonana na Raisi Senga peke yake lakini maagizo tofauti yalikuja yakimtaka Nadia kuhusika katika maongezi hayo ili kuweza kumshawishi Raisi Senga kwa namna yoyote ile kuweza kujiunga na umoja wa Ant Illuminat.
“Mheshimiwa Wageni wamekwisha kufika”Aliongea Kabwe mara baada ya kuingia katika eneo la sebule yenye samani za kuvutia.
Mheshimiwa Raisi alionekana kuongea na simu na kadri alivyokuwa akiongea sura yake ilizidi kujikunja na palepale hasira ilimvaa.
******
Wache Grand Hotel ilikuwa imejengwa juu ya kilima , mwanzoni mwanzilishi wa eneo hilo alihitaji kujenga nyumba za makazi kwa ajili ya biashara lakini kutokana na mazingira ya muinuko aliona ni gharama zaidi kuliko eneo la tambarare hivyo hoteli hio ndio ikajengwa.
Hoteli hio ilinufaika kwa kuwa juu ya kilima hivyo kufanya kuweza kutengeneza mandhari mazuri ya bahari huku ikizungukwa na msitu wa miti.
Unaweza kusema hili ndio eneo pekee ambalo ndani ya kigamboni halijaguswa wala kukaliwa na raia wa kawaida, ni eneo ambalo pia limeuzwa kwa Mzee Sharif kwa ajili ya ujenzi hivyo unaweza kusema kwamba hoteli hio ya Wache ni moja ya hoteli ambazo zimejitenga sana katika mji huo wa Kigamboni.
Roma alishawahi kuona kibao cha hoteli hio lakini ukweli ni kwamba hakuwahi kufika ndani ya hoteli hio kabisa na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kujua kumbe eneo hilo lote lilikuwa likimilikiwana familia hio ya Mzee Sharif.
Roma mara baada ya kufika ndani ya eneo la hoteli hio ya nyota tano aliweza kuona sehemu zaidi ya mia moja za kuegeshea magari lakini katika sehemu hizo ni ishirini pekee ambazo zilikuwa zimechukuliwa.
“Kulingana na magari haya naamini kuna watu zaidi ya ishirini huko ndani”Aliongea Roma.
“ Hupaswi kuanza kujutia sasa hivi kuja hapa , vipi umeguswa kwa familia yetu kukuandalia sherehe?”Aliuliza Maimuna na kumfanya Roma kutingisha mabega , alikuwa akitegemea jambo la namna hio , isitoshe familia hio mara nyingi ilikuwa ikilinda siri zao hivyo mambo yao yalikuwa yakiendeshwa kisiri siri hivyo alikuwa amejipanga kuja kukutana na watu wasiokuwa wa kawaida katika eneo hilo.
Yaani kwa kwa haraka haraka ni kwamba hoteli nzima ilionyesha kutokuwa na wageni wengine zaidi ya familia ya Sharif pekee.
Dakika ileile anatoka kwenye gari kabla hata hajapiga hatua kuingia ndani ghafla tu aliweza kushuhudia wanaume wawili waliovalia majoho ya rangi nyeupe wakiibukia kutoka pande mbili tofauti kwa namna ya kupaa, walikuwa katika umri wa miaka arobaini na hamsini kimakadirio huku wakiwa na vipara pamoja na masharupu mengi usoni.
Walikuwa na macho makali ambayo hayakuwa ya kawaida , licha ya Roma kutokuwa na uwezo wa kutumia uwezo wake wa kijini akili yake ilishamwambia hao sio binadamu wa kawaida, walikuwa na muonekano wa kiarabu lakini kwake aliwaona kama sio waarabu.
Roma moja kwa moja aliamini pengine watakuwa katika levo ya kuipita dhiki katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi au mafunzo ya kijini.
“Acha kukodoa macho wewe mjjinga”Aliongea jini Imrah ambaye alitokea ndani na Roma alimkumbuka vyema kwani alipambana nae kule Kilimanjaro.
“Jinni Marid na Jinn Iftir wapo hapa kwa ajili ya kukuangalia na wote wapo katika levo ya kuipita dhiki wakiwa na uwezo wa kudhibiti moto wa rangi tatu , watahakikisha huondoki hapa kwa namna yoyote”Aliongea .
Roma alijikuta akishangazwa na kauli ya Jinn Imrah , hakutegemea angeweza kukutana ndani eneo hilo na watu wa levo ya juu katika mafunzo ya kijini.
Roma alijiuliza inakuwaje hii familia ikawa na uhusiano mkubwa na viumbe hawa wa kijini kiasi cha kuweza kuita watu wenye uwezo wa juu namna hio ndani ya muda mfupi.
“Acheni kusimama hapo , wewe mlete huyo ndani anasubiriwa”Aliongea akimpa amri mtoto wake wa kike kumwingiza Roma ndani ya hoteli.
Maimuna aliishia kumwagalia Roma kwa tabasamu huku akimpa ishara ya kutembea kuingia ndani.
“Ukoo wenu hauendeshwi kulingana na nani mwenye nguvu zaidi si ndio?””
“Kwanini unauliza hivyo?”
“Jinn Iftiri na Marid wana nguvu kubwa za kijini kuliko Imrah lakini bado tu wanaonekana kusikiliza maagizo yake”Aliongea Roma na kumfanya Maimuna kutabasamu.
“Mr Roma tatizo unatuchukulia poa , yule Master Iftir na Maridi wote ni washirika kutoka matawi yaliopo katika nchi kadhaa , ukizungumzia swala la madaraka Imrah ana madaraka makubwa kuliko wao , wapo watu wenye nguvu za kijini wengi sana pamoja na majini wenyewe na ni wengi kiasi kwamba hata babu mwenyewe hajui idadi yao”
“Unajaribbu kuniogopesha?, kama ni hivyo si mngeweza kutawala hii nchi?”
“Hatuna haja ya kukutisha kwani tuna nguvu ya kukushinda na kuhusu unachokisema kuhusu kutawala taifa hio ni nje ya sheria za kijini, nguvu yetu ipo katika maswala ya nguvu isioonekana tu”Aliuongea kwa kujiamini
Roma mara baada ya kuingia kabisa ndani ya Korido ya hoteli hio aliweza kukutana na mabodigadi waliokuwa wakilinda, ilimshangaza Roma kwani eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali kama vile kuna kiongozi mkubwa wa dunia aliekuwa yupo katika eneo hilo.
Kwa haraka haraka tu Roma aliweza kuamini mabodigadi hao wapo katika levo za chini za mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi na mbaya zote wote walikuwa ni Waraanbu tupu.
Ilionekana dhahiri kabisa familia hio ilikuwa imeandaa maandalizi makubwa ya kutaka kumdhibiti.
Ukiachana na ulinzi mkali hoteli hio ilikuwa na mazingira ya kuvutia mno , kuna hisia zilimwambia Roma pengine hii hoteli haipo wazi kwa kila mgeni ambaye anataka kuja kupumzika ndani ya eneo hilo.
Hisia za Roma zilikuwa sahihi , tokea ujenzi wa hoteli hio kukamilika hakuna Mtanzania wa kawaida ambaye alishawahi kwenda kulala ni watu wachache sana ambao walikuwa wakijua hata muoenekano wake kwani eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali sana kuanzia getini mwanzoni kabisa wa kuingia kwenye eneo hilo mpaka upande wa Fukwe.
Inasemekana kwamba katika vipindi flanni vya mwaka waarabu wengi pamoja na wahindi huonekana wakiingia ndani ya hoteli hio na hata mpaka leo hoteli hio iliaminika kama hoteli ya Waraabu kwani ndio ngozi pekee ambazo zilikuwa zikifika hapo.Lilikuwa kama eneo mbadala tofauti na lile la kule Kilimanjaro
Pengine ni sahihi kuiita Hoteli ya Majini kwani viumbe ambavyo vinafika hapo havikuwa vya kawaida, aidha ni binadamu mwenye nguvu za kijini au majini yenyewe.
Sasa jambo ambalo Roma hakuwa akilijua ni kwamba kulikuwa na ulimwengu wa majini lakini alishindwa kuelewa huyu Mzee Sharif yeye anatokea katika koo ipi ya kijini na alichosalia ni hao majini au kuna kingine zaidi ya kile anachokidhania.
Roma mara baada ya kuingizwa katika ukumbi mkubwa hatimae sasa aliweza kuona sura za watu tofauti tofauti wengi ambao walikuwa wameketi kwenye Zuria la kuvutia huku katikati yao kukiwa na kifaa flani ambacho Roma hata hakuelewa maana yake ila kilikuwa kikitoa moshi wa pink wenye harufu flani ambayo hakuweza kuielewa.
Sura zote zilikuwa ni nyeupe tupu huku kila mmoja akiwa na ndevu nyingi na masharubu, kuna ambao Roma alikuwa akiwahafamu kwani alishawaona lakini kuna wengine ambao hakuwa akiwafahamu kwani sura zao zilikuwa mpya, wote walikuwa wamevalia mavazi ya tamaduni za kiarabu.
Mzee Sharif alikuwa amekaa katikati kabisa kama kiongozi huku akiwa na kiremba cha rangi ya bluu kichwani, pembeni yake alikuwa ameketi jini Imrah , kushoto kwake kulikuwa na mhindu ambaye amevalia tofauti na wengine wote , yeye alikuwa amevalia joho la rangi nyeusi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kila mmoja alikuwa amevalia kitamaduni kasoro Maimuna peke yake ambaye amevalia kisasa zaidi lakini vazi lake likiwa la heshima.
Roma alimwangalia Mzee huyo ambaye amevalia Joho la rangi nyeusi kwa kumchunguza , alikuwa mzee zaidi kuliko Imrah mwenyewe na alikuwa amefumba macho, Roma kwa haraka haraka alijua tu huyo ndio mtu hatari zaidi hapo ndani kuliko wengine wote.
“Mrithi wa ukoo wa Kweka , hatimae tunakutana tena”Aliongea Mzee Sharif.
“Naona watu wengi wapo hapa kwa ajili ya kunikaribisha , kwanini mmejikalisha hapa kizembe tofauti na ukumbi wa chakula kuanza sherehe”Aliongea Roma huku akiwa na tabasamu kama kawaida yake.
“Acha kuigiza wakati unakiona kifo chako”Aliongea mdogo wake Maimuna afahamikae kwa jina la Meki huku akimwangalia Roma kwa kejeli.
Roma hakutaka hata kuongea nae kwani palepale alimsogelea na kisha akampiga teke na kumfanya avamie kimeza iilichokuwa na glasi pamoja na vikombe.
Hakua ambaye alitegemea hilo na walijikuta wakishangaa na kujiuliza au amekuja akiwa amelewa , kwanini ameamua kushambulia kwa kuchokozwa kidogo tu.
Yule mzee mwenye Joho jeusi hatimae aliweza kufumbua macho yake mara baada ya kusikia purukushani hio ya mtu kupigwa kiasi cha kuvamia meza.
“Unafanya nini , unadhani tunakugopa?”Aliuliza Mzee Sharif huku akionyesha hasira za wazi.
“Mjukuu wako ana mdomo mchafu sana na kama ningetaka kumuua mpaka muda huu angekuwa ni kifusi cha nyama tu , nadhani unanielewa mwenyewe”Aliongea Roma.
Meki alijikuta akimwangalia Roma kwa uchungu huku akiugulia maumivu makali.
“Meki ondoka hapa ndani”Aliamrishwa kuondoka
Mwanaume huyo mwenye jina la Meki alimwangalia Mzee Sharif kwa kuchanganyikiwa lakini aliishia kusimama na kisha akatoka nje.
“Roma hatukufanyi chochote kwasababu tunahitaji kufanya na wewe mazungumzo ya kina , hivyo jitahidi kujiuzuia”Aliongea akitoa onyo kwa uso uliokuwa na usiriasi.
“Mnataka kuongea na mimi kuhusu nini? , au ni kuhusu hazina yenu?, niwaambie mapema tu kwamba sijachukua hazina yenu na msije hata kufikiria kutaka niwaombe msamaha”Aliongea Roma lakini hata hivyo hakuna ambaye alikuwa akiamini kauli yake , kila mmoja ni kama walikuwa wakimjua anaigiza tu.
Mzee Sharif alimwangalia kwa ishara mtoto wake mkubwa na palepale alitingicha kichwa na kisha akatoka ndani ya eneo hilo na ndani ya dakika tatu waliweza kufikishwa Naibu waziri Salihi pamoja na Asha huku wakiwa na hofu zaidi mara baada ya kumuona Roma.
“Sikumfundisha vizuri mkwe wangu na mjukuu wangu na wakakuchokoza , unaweza kuwa na kinyongo juu yao na mimi nipo tayari kuwafanya wakuombe msamaha na naahidi hawatolipiza kisasi tena”Aliongea mzee huyo na kisha aliinua uso wake na kumwangalia Roma.
“Unaonaje , ninachoongea hapa nina maanisha kabisa”
“Sijali tena kuhusu wao kuomba msamaha, kama ni fidia nishajilipa kwa kuharibu makazi yenu pamoja na kuchoma jengo lenu la ibada”Aliongea Roma.
“Hakuna shida , kama ni hivyo basi ni zamu yetu”Aliongea na palepale alitoa ishara ya Skrini iliokuwa imefungwa mwishoni kabisa ukutani iwashwe.
Dakika ileile ilionekna vidio katika Tv ile na Roma alipoangalia kwa umakini alijikuta akikunja ndita bila ya kupenda.
Samweli Nguruma ambaye ni baba yake na Benadetha pamoja na mke wake ndio ambao walioneana katika hio vidio wakiwa wapo chini ya ulinzi wa wanaume ambao wameshika mitutu ya bunduki.

SEHEMU YA 658.
Katika vidio iliokuwa ikionekana kwenye skrini hio ilikuwa ikimuonyesha Samweli Nguluma akiwa amefungwa na kamba kwenye kiti huku akiwa amezibwa mdomoni, haikuwa hivyo kwake tu hata kwa mke wake pia.
Ilikuwa bahati kwamba Benadetha na kaka yake hawakuwa nyumbani wakati huo pengine na wao wangeunganishwa katika utekwaji huo .
“Kwa taarifa ambayo tumeweza kuipata ni kwama kundi la Zoa Zoa ambalo lipo chini ya Samweli Nguluma ndio waliokupatia yale mabomu ,je nimekosea?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kujibu lile swali na palepale alitoa simu yake na kutafuta namba ya Afande Jamali na kuipiga.
“Mr Roma najua hali ilivyo kwasasa”Aliongea mara tu baada ya simu ile kupokelewa.
“Unajua nini , si wewe ndio ulieniambia kwamba hakuna mtu mwingine ambaye ataweza kuguswa zaidi yangu?”
“Mr Roma sikujua ulikuw ana uhusiano na Mzee Nguluma mmiliki wa kundi la ZoaZoa , Mzee Nguluma amehusika katika maswala ya kihalifu mengi sana na kukamatwa kwake hakuathiri usalama wowote wa jamii”
“Acha kuongea ujinga , hata kama ni mhalifu haina maana kwamba anaweza kukamatwa na watu ambao sio polisi”
“Ni ,.. Hakuna maagizo yoyote ambayo nimepokea kutoka juu , hivyo hatupaswi kuingilia katika hili swala”Roma aliishia kulaani na kisha palepale alikata simu.
Roma alijiambia kutokana na kukosa uwezo wake wa kijini asingeweza kuwaokoa kwa wakati lakini pia hakutaka chochote kiwatokee kwani asingeweza kumwangalia Benadetha usoni kwani ni yeye ndio aliemhusisha baba yake licha ya kwamba mzee huyo alionyesha wasiwasi wake mwanzo.
Mabwana wote waliokuwa hapo ndani walionyesha sura za furaha kumuona namna ambavyo Roma alikuwa akiteseka.
“Unaonaje sasa, wewe ni mtu wa kukurupuka sana lakini unapaswa kuelewa hii dunia sio yako peke yako , kila mtu ana udhaifu wake, kama utatoa ushirikiano, basi tutapotezea swala la Mzee Nguluma kukusaidia mabomu lakini kama utaendelea na ukiburi wako wewe pamoja na Mzee Nguluma mtalipia gharama”
“Unataka nitoe ushirikiano gani?”Aliuliza Roma na kuwafanya wote kutoa tabasamu wakiona Roma hatimae anaenda kujisalimisha.
“Tutakupa machaguo matatu”
“Oh.. hebu yataje tuone“
Chaguo la kwanza , rudisha hazina yetu m jenga upya madhabahu yetu na kisha omba msahama miungu yetu , nadhani ushaambiwa kuhusu hilo, kuhusu chaguo la pili …”Alisita kwanza na kisha akamgeukia Maimuna na kutoa tabasamu hafifu.
“Chaguo la pili unapaswa kumuoa mjukuu wangu Maimuna Sharif na sisi kuwa wakwe zako”
Kidogo tu Roma adondoke chini kutokaa na mshituko , alitaka kujiambia hajasikia vizuri lakini baada ya kumwangalia Maimuna ambaye alikuwa akionyesha viabu vya kike alijua ni kweli kile alichosikia.
Kauli hio ilimfanya Roma kukumbuka matendo ya mrembo huyo , kumbe alikuwa akijua mpango wa mababu zake ndio maana alikuwa akijilengesha.
“Hebu kwanza tuachane na chaguo la kwanza kwani sitofuata na kuhusu chaguzi ya pili na yenyewe niseme kwamba mimi nishaoa tayari hivyo tupotezee”Aliongea Roma akikataa.
“Kwanini isiwezekane , si tayari ndoa yako na Edna imefikia ukingoni, tunajua aliondoka Iringa akiwa ameweka wazi kabisa anataka talaka mbele ya babu yako na habari hii inajulikana ndani ya familia nyingi ndani ya Dar , kama una wasiwasi na maswala ya mgawanyo wa mali sisi tutampatia kitu cha kuridhisha ili talaka yenu iwe rasmi”Aliongea Maimuna.
“Ndoa sio kama mnavyofikiria wewe, kwamba ni mambo ya kusainishana makaratasi na kufikia mwisho , uhusiano wetu hausiani na makaratasi wala ndugu ,sawa?”
“Acha kuniona mjinga , najua ameshindwa kuvumilia wanawake wako , inashangaza kwamba licha ya urembo wake ameshindwa kukulinda kama mke mpaka ukawa na wanawake wengi lakini sasa hivi anaanza kuchafua hali ya hewa , sioni kama ana stahili kuwa mmoja wa familia yenu wala kuendelea kuwa mkeo”
“Kaa kimya wewe hilo halikuhusu , hivyo acha kuongea ujinga”Alifoka Roma
“Unakasirika nini sasa , ninachokuambia ni ukweli , mimi ni mwanamke na nawajua wanawake wenzangu pia kuliko wewe , kwanini unanifokea kwa kuongea ukweli , nenda kamfokee Edna sio mimi”Aliongea na kumfanya Roma kushindwa hata amfanye nini kwani alioneana kujiamini sana.
“Eti dada ndio tuseme kwamba unataka kuolewa na mimi sana au?”
“Mimi sio dada yako unikome… , tunalingana umri ..”Aliongea huku muonekano wake ukibadilika huku kifua chake kikipanda na kushuka , alionekana kama amewezwa kuitwa dada na Roma.
Lakini hata hivyo muonekano wake wa aibu na kukasirika ulimfanya Roma kumshangaa kidogo na alijiambia pengine kama ni miaka kadhaa iliopita asingekataa mwanamke mrembo kama huyo , lakini kwa kipindi kama hicho ambacho alikuwa akitaka kurudiana na Edna kwa namna yoyote ile hakutaka kuongeza matatizo.
Isitoshe ndoa ni tofuati na kulala na kuamka pamoja hivyo Roma aliamini kama angemgusa huyo mwanamke hatua nyingine lazima ingefuata.
Upande wa Roma alijua kabisa familia hio pengine ilikuwa ikitaka kujikita zaidi ndani ya taifa la Tanzania kwa kutaka kuanzisha undugu na familia yake jambo ambalo aliona ni kichekesho.
“Mjukuu wangu sio wa kawaida , ukiachana na muonekano wake , akili pamoja na kutokuwa binadamu wa kawaida , nina wasiwasi huwezi kupata mwanamke wa aina yake maisha yako yote , unapaswa kujiona wa bahati yupo tayari kuolewa na wewe, Edna anaweza kuwa mtoto wa raisi wa Rwanda lakini bado atabakia kuwa mtoto wa nje ya ndoa , tunaweza kukusaidia kwenye mambo mengi tofauti na familia yake itakavyokusaidia , kama utamuoa Maimuna tutahakikisha familia yenu ni ya kuogopwa sio tu hapa Tanzania bali Afrika mashariki kwa ujumla , tuhakikisha tunawapa nguvu ya kuamua kiongozi wa mataifa ya Afrika mashariki awe nani na biashara nyingi zitakuwa chini yenu”AliongeaMzee Huyo.
Roma alijikuta ni kama akili yake haifanyi kazi vizuri , alijiammbia hata kama atakuja kuachana na Edna basi hawezi kuoa mwanamke mwingine.
“Inatosha , haina haja ya kumsifia mjukuu wako kwani simtamani kwa lolote”Aliongea Roma
Ukweli ni kwamba Maimuna ndio mwanamke pekee ambaye miungu ya ukoo imekumkubali kuwa kama kiongozi wa ukoo baada ya Mzee Sharif mwenyewe na walitaka kumjengea nguvu zaidi kwa kumuozesha kwa Roma ambaye alikuw ana uwezo mkubwa wa nguvu za kijini.
Kitu kingine Maimuna hakuwa msichana wa kawiada kama ambavyo amesema Mzee Sharif , inasemekana mrembo huyo mama yake sio binadamu wa kawaida hivyo waliamini kama wataweza kupata mtoto kupitia Maimuna na Roma basi anaweza kuwa sio wa kawaida na kufanya ukoo wao pamoja na dini yao kuzidi kusambaa duniani kote.
Maimuna alijikuta akikasirika na jambo lile na kung’ata lipsi zake nyekundu kwa hasira kwani kitendo cha Roma kumwambia hamtamani kwa lolote kwake ni kama amedhalilishwa, hakuwahi kuwaza kama kuna mwanamme katika dunia hii ambaye anaweza kumkataa kirahisi kama alivyofanya Roma, alianza kujifananisha ana kasoro gani na Edna kwani wote ni warembo huku yeye weupe wa kiarabu ukimbeba.
“Nsihakuambia hivyo huyu Maimuna atakuwa na msaada kwako , ndio anaekwenda kurithi utajiri wote wa familia yetu , acha kuwa mjinga na kumkataa hii ni bahati siojirudia mara mbilimbili”Aliongea na kuwafanya wale wazee ambao hawakuwa wakijua ukweli kuhusu mrithi wa familia kumwangalia kwa mshangao.
Maimuna licha ya kwamba alikuwa mwanamke lakini ndio mmoja wapo ya wanafamilia ambaye alikuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa akili na kumfanya Babu yake kumkubali, isitoshe alikuwa ametii sheria za ibada kwa kuendelea kuwa bikra mpaka wakati huo.
“Vipi kuhusu chaguo la mwisho?”Aliulizia Roma na kuwafanya waamini kabisa kwamba bwana huyo ameamua kukataa chaguzi ya kumuoa Maimuna.
“Hakuna shaka , kama ijulikanavyo viijana wa siku hizi ni wenye kukurupuka , chaguo la tatu ni rahisi sana , hatujawahi kujizuia kudili na adui yetu , familia ya Mzee Nguluma wote watauliwa halafu wewe utakuwa mateka chini ya familia yetu na tutakuvua nguvu zote za kijini ulizokuwa nazo na tutakutesa mpaka utoe hazina yetu na kisha kukulazmisha kusujudia miungu yetu”
Roma alijikuta akichezesha ulimi wake kwa kutoa sauti kutokana na namna walivyokuwa wakijiamini mpaka kuongea kauli hio.
“Usituchukulie poa , familia yako inaweza kuwa na nguvu ndani ya taifa hili lakini haimiliki nchi , isitoshe jeshi haliwezi kuwasikiliza kwa kila kitu , tunaweza kuimaliza familia yako kwa kuagiza wazee wetu hapa wa kijini kwenda kuua familia yako yote lakini hatuna mpango wa kwenda mbali hivyo”
Roma hakutaka sana kumwamini huyo kikongwe , alijiambia kama kweli alikuwa jasiri wa kufanya makubwa kwanini alikimbia nchi yake na kuja kujificha hapa Tanzania.
“Nitakupa dakika tatu tu za kufikiria , hili ni swala ambalo lazima limalizike leo hii hii”Aliongea .
Roma alijikuta akitoa kicheko cha kebehi na kisha aliingiza mkono mfukomi na kuibuka na simu na kisha alionekana kuandika namba flani flani hivi.
Kila mmoja alionekana kumshangaa na kujiuliza anampigia nani katika wakati kama huo.
Upande wa Roma haikuonekana kama alikuwa akipiga simu hali namna alivyokuwa akiandika ilionekana kama alikuwa akituma ujumbe wa maandishi.
“Roma usije ukafanya janja…”
Dakika ambayo alitaka kuongea ulisikika mtetemeko na mlipuko mkubwa kama vile ni wa ngurumo ya radi.
Dakika hio hio ndege walionekana wakiambizana kukimbia katika mazingira hayo yenye miti.
Sauti haikuonekana kutokea na kuisha bali iliendelea kusikika mfululizo na ndani ya dakika chache tu ndani ya eneo hili lilianza kuzingirwa na moshi mzito sana huku mawe yakianza kuingia ndani ya jengo hilo la hoteli kiasi cha kupasua pasua vioo.
Magari yaliokuwa yameegeshewa nje yalianza kuwika kwa kutoa ving’ora vya alamu na mengine yalianza kulipuka mara baada ya matanki ya mafuta kupasuliwa na mawe,
“Pumbavu alikuwa akituma signal , inaonekana alikuwa ametega mabomu?” Mmoja wapo alipiga kelele mara baada ya kugundua mlipuko uliokuwa ukiendelea ndani ya eneo hilo ni wa mabomu.
Dakika ileile wakati mabomu hayo yakipiga wakiwa katika hali ya kushangaa Roma alimshikilia maimuna kwa spidi kiasi cha kumfanya kushindwa kuchukua hatua ya kumkwepa .
Maimuna alikuwa na nguvu za kijini lakini zilikuwa za chini sana kulinganisha na uwezo wake.
Roma palepale hakutaka kumcheleweshwa kwani alipitishia vidole shingoni kwa spidi na palepale aliweza kupoteza fahamu na kisha akamuweka begani.
“Wewe mzee wa kiarabu Kikongwe usie na aibu , nimeshindwa kuamini kama ulikuwa na mpango wa kunichokoza kwa mara ya pili , kabla ya kutia mguu ndani ya hii hoteli ishatembelewa na vjana wangu muda tu na kutegesha mambomu aina ya C4., nenda kuzimu”Aliongea Roma kwa kufoka.
“Mjingaaa sana wewe!!, unataka tufe wote kwa pamoja hapa , umekuwa kichaa?”
“Haha si ndio mlichokuwa mkikitafuta, siogopi bomu la nyuklia sembuze hivi vibomu vya kawaida nitaondoka na mjukuu wako , mwachie Mzee nguluma na mke wake la sivyo nitahakikksha namtupia baharini sehemu yenye papa na kisha nitaua kila mwanafamilia mwenye jina la ukoo la Sharif na kufuta mizizi yako ndani ya hili taifa , Shwain..”Aliongea Roma na palepale alikimbilia nje.
Kabla hajapiga hatua yule mhindu aliekuwa kimya muda wote akiwa na mavazi yake meusi palepale alipotea alipokuwa amesimama na ile anakuja kuibukia ni mbele ya Roma.
Ilikuwa kama alivyotegemea huyo mzee alionekana anaenda kumletea ngumu katika kushindana nae., spidi yake na msisimko ulikuwa umezidi ule wa jini Imrah.
Lakini hata hivyo Roma alishajua hana namna ya kumkimbia zaidi ya kupigana nae uso kwa uso
“Unakimbilia wapi?”Aliuliza kwa sauti kali ya kuumiza masikio kwa mtu wa kawaida.
“MODAO!!!”
Dakika ileile mkono wake ulianza kuzungukwa na mwanga wa njano na ndani ya dakika tu kulionekana kitu kama chungwa lililoiva likitokea mkononi mwake.
Roma alijikuta akishangaa kwani aliweza kugundua hio ilikuwa ni dhana ya kijini ambayo hakuwahi kuiona ambayo inaitwa Modao , Dhana ile ilikuwa ikitoa msisimko wa ajabu mno na kutengeneza kimbunga cha upepo mkali sana.
Ijapokuwa mabomu bado yalikuwa yakiripuka kuzunguka hoteli hio lakini eneo waliliiokuwa ni kama lilikuwa haliathiriki na milipuko hio.
“Kaeni ndani ya ngao , msisogee la sivyo hamtokuwa salama”Aliongea mara baada ya jengo hilo kuanza kutingishika likionekana linataka kudondoka muda wowote.
Familia hio ambayo ilikuwa na watu ambao wana uwezo mdogo wa nguvu za kijini walijikuta wakipatwa na ahueni mara baada ya kuona wana ulinzi wa kuwatoa ndani ya eneo hilo wakiwa salama.
Dakika ileile jini Iftiri , Imrah na Maridi waliingia ndani na kumzingira Roma huku kila mtu amelipukwa na nguvu isiokuwa ya kawaida ya kijini.
“Unajikuta jasiri kujitengenezea njia ya kutoroka si ndio, lakini nikwambie tu pengine umedharau sana uwezo wetu , leo ndio mwisho wako, hebu onja kwanza uzito wa thamani ya paundi elfu sitni”Aliongea yule mzee wa vazi jeusi,
Roma alijikuta akianza kulaani kimoyo moyo kwani aliona hao majjini hawakuwa na nia ya kumuacha salama kabisa na hawakuonyesha kujali usalama wa Maimuna tena , pengine tayari walikuwa washajua kwamba Roma asingeweza kumua kwani kifo chake ingemaanisha kifo cha Mzee Nguluma.
Wakati majini hao wakiwa na nia ya kumua, familia ya Mzee Sharif ilikuwa katika hali ya wasiwasi kwani waliogopa kifo cha Maimuna ingemaanisha kwamba wangepoteza mrithi aliekubaliwa na miungu wao.
Roma mara baada ya kuona nguvu ya ajabu inamsogelea alitaka kujikinga na mwili wa Maimuna lakini alihofia angeweza kufariki wakati bado alikuwa akimhitaji , aliona pengine akwepe pigo hilo lakini bado spidi yake ilikuwa ndogo na alijikuta akikosa chaguo na palepale alinyoosha mkono kupokea lile shambulizi.
“Modao!!!”
Aliongea kwa nguvu yule Mzee mwenye vazi jeusi na palepale ulitokea mlipuko wa aina yake ambao ulitengeneza mtetemeko wa ardhi ya aina yake.
Sehemu ambayo alikuwa amesimama Roma hakuonekana zaidi ya shimo kubwa la mita moja kwenda chini ndio na palepale ukuta wa hoteli hio uliokuwa umebakia ulidondoka.
Upande wa Roma bado alikuwa amesimama vilevile akiwa chini ya shimo na bado mkono wake ulikuwa ukishindana na nguvu ya kijini ilioruhusiwa kutoka katika Dhana ile ya Modao..
Yule mze mwenyewe alijikuta akiwa kwenye mshangao kwani hakuamini Roma hajathiriwa na pigo lale na aliishia kujiuliza inakuwaje akawa hajaathirika , mwili wake umetengnezwa na chuma.
Upande wa Roma alikuwa kwenye maumivu makali mno , ijapokuwa hajawahi kuyaogopa maumivu lakini alichokuwa akipitia hakikuwa cha kawaida , ni damu pekee ambazo zilikuwa zinaonekana kwenye mkono wake.
Shambulizi lote lile la Modao alikuwa amelizuia na mkono mmoja ndio maana aliweza kupitia maumivu makali kama hayo.
Yule Mzee wa kijiini aligundua maumivu yake , ijapokuwa alionekana kuweza kuhimili shambulio lake kwa mkono lakini bado aliona mikono yake ilikuwa ikimtetemeka na hili lilikuwa udhaifu ambayo ulimpa tumaini la usihindi.
“Sijajua umewezaje kuwa na mwili wa aina hio lakini hainizui kukuua na shambulizi langu la thamani ya paundi elfu sitini”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli na palepale aliita moto wa rangi ya njano na kisha aliunganisha na kile kitenesi kama chungwa kwenye mikono yake na kufanya nguvu yake kuzidi kuwa kubwa maradufu.
Roma alijikuta sasa akihisi ile nguvu ya ile Dhana ikiongezeka uwezo wake kwa zaidi ya mara mia moja na alijihisi mifupa yake inataka kumvunija kutokana na presha aliokuwa akiihisia.
“Mlete Maimuna , huwezi kuvumilia shambulizi langu lingine”Aliongea
“Unapambana na Jinn Ghula ambaye uwezo wake ni mkubwa zaidi katika kuipita dhiki na kwenda mpaka levo ya kudhibiti maji kwa kuyabadilisha mara sita kimuundo . atakuua na shambulizi moja tu”Aliongea jini Imrah kwa tahadhari.
Roma alijikuta akishangazwa na kauli ile na kujiambia inakuwaje akawa na uwezo mkubwa namna hio , alijiambia kama angejua familia hio haikuwa ya kawaida basi asingechoma madhabahu yao.
Shauku yake ya kutaka kuijua hio familia chimbuko lake ilizidi kumjaa,
Roma alijiuliza au pengine kna kitu hakijui kuhusu majini ndio maana yupo kwenye hatari kama hio.
“Acha kuwa mbishi wewe binadamu , Master Ghula hio dhana yake ya Modao inao uwezo wa kukusanya nguvu za kiroho za kikosmiki na kuwa na uzito mkubwa ambao huwezi kuhimili”Aliogea kuzidi kumtia hofu Roma.
“Nitakuuliza mara ya mwisho , je upo tayari kurudisha hazina yetu?”Aliuliza Master Ghula.
Roma damu yake ilikuwa ikichemka mno na aliweza kuhisi namna ambavyo ile Dhana ilikuwa ikikusanya nvuvu ya kiroho ya giza kwa kasi mno.
“Niue tu kama unaweza” Aliongea Roma kijeuri kama kawaida yake na kumfanya Master Ghula macho yake kubadilika rangi palepale na kuwa na kutisha.
“Ukiburi ulioje kutoka kwa binadamu kama wewe , ni hasra kukuua lakini sina namna”Aliongea na palepale upepo mkali ulianza kuvuma na uchafu ulianza kujikusanya katika mikono yake kiajabu , kile kitenesi kama chungwa kilianza kutengeneza kimbunga cha ajabu na palepale alianza kuongea lugha ya kiajabu ambayo Roma alichoweza kusikia ni Mlima wa Tai, Viani Dao…
Ilikuwa ni nguvu ambayo haikuwa ya kawaida kwani katika lile eneo ambalo amesimama Roma kulitengeneza shimo kubwa na pengine kulikuwa na eneo la Ardhini ambalo lilikuwa limechimbwa kaitka hoteli hio kwani Roma alisukumwa kwenda chini mara baada ya mpasuko huku akisindikizwa na pigo takatifu la Modao na hakuonekana tena yeye pamoja na Maimuna na palepale yalifuatia maporomoko ya mawe pamoja na vifusi kufunika lile shimo kwa kasi na ndani ya dakika tu majabali na vifusi viliweza kufunika na kufanya eneo lote kujaa vumbi ambalo sio la kawaida.

SEHEMU YA 659.
Hoteli yote ya Wache ilikuwa imeharibika na kwa mtu mwenye uchungu wa mali pengine angekuwa kwenye masikitiko maiubwa kwani ilikuwa na mvuto usio wa kawaida ndani yake.
Wale wazee wa kijini wote watatu walionyesha kukunja ndita zao , ijapokuwa Roma alionekana kufunikwa na kifusi lakini bado waliweza kuhisi kabisa bado alikuwa hai na pia Maimuna alikuwa hai jambo ambalo lilimfanya ajawe na ahueni.
Kwao Maimuna alikuwa na thamani kubwa zaidi ya Mzee Nguluma na mke wake.
“Baba tayari ashafukiwa na kifusi chini ya Ardhi , Maimuna atakuwa sawa kweli?”Aliuliza baba yake Maimuna aliekuwa katika hali ya wasiwasi.
“Punguza presha , hebu waangalie wazee muonekano wao , inaonekana huyo mwanaharamu bado yupo hai na anamtumia Maimuna kama mateka na chochote kikimtokea Maimuna basi anajua fika familia ya Mzee Nguluma itakuwa halali yetu”Aliongea Mzee Sharif.
“Lakini anaweza kuwa hai lakini vipi kuhusu kupatwa na majeraha”
“Kaa kimya , wazee wanajua wanachokifanya”Aliongwa kwa kufoka.,
“Anatumia mbinu gani ya kimafunzo , mwili wake sio wa kibinadamu kabisa”Aliuliza jini Marid kwa mshangao.
Upande wa Mzee Ghula alionekana kushanga pia na kujiuliza kwa nguvu ya kijini aliotumia kwanini huyo mwanaharamu bado tu hajafa.
Mzee Ghula palepale hakutaka kuamini kama hawezi kumuua Roma kwani alianza kuchanel nguvu nyingine ya kijini ili kuweza kuisindilia kwenye lile shimo ambalo Roma alifunikwa lakini kabla hajamaliza anachotaka kufanya ghafla tu alianza kukumbwa na hali ya woga kwenye akili yake na kujikuta akigeuza macho yake na kuangalia angani.
Wale wenzake pia walikuwa washainusa hatari na walijikuta wakigeuza macho yao wote kwa pamoja kuangalia angani na walijikuta wakiwa hawamini wanachokiona angani.
“Nini kile?”Kila mtu alikuwa kwenye mshhitiko kuangalia kitu ambacho kilikuwa kikiwasogelea kwa kasi.
Kabla hata hawajaelewa waliweza kuona kitu kingine kiibuka kutoka baharini na kupaaa angani na kuanza kusafiri kuelekea upande wao.
“Oh ,. Hapana ni Makombora yale”
“Shit .. hili linawezekana vipi?”Baadhi ya mabodigadi waliokuwa nje ya eneo hilo walijikuta wakijawa na kiwewe.
Mzee Sharif mara baada ya kugundua kinacho wasogelea ni makombora ya kivita alijikuta akipagawa na kujiuliza vitu hivyo si vya kijeshi.
Halikuwa kombora moja , ilionekana yalikuwa yakirushwa kutoka chini ya baharii kuja eneo walipo kutokana na trajectori zao na ilikuwa ni swala kufumba na kufumba yote yashakaribia eneo walipo.
Ilikuwa ni maamuzi ya haraka sana walioyafanya kwani palepale walitengeneza ngao ya kijini na kuwafunika watu wote na wao pia kwa kuunganisha nguvu na makombora yale yalitua yote kwenye ngao na kutoa mlipuko wa aina yake na kuanza kugeuza kile kijimlima kuwa tambarare,
Naibu waziri Salihi , Asha na wengine wote walikuwa wakihisi ngoma za masikio yao zinawapasuka kutokana mlipuko huo huku kila mtu akilaani ni balaa gani hilo wamejitengenezea.
Wale wazee licha ya kwamba walifanikiwa kutengeneza ile ngao lakini hawakuacha kutema damu nyingi chini huku nguvu zikiwa zikiwaishia.
Ilikuwa ni kama vile kuna kambi ya kijeshi ambayo ilikuwa ikiangamizwa moja kwa moja na adui katika hilo eneo kwani yalikuwa yakishuka mfululizo tena kwa kasi bila ya kukosa shabaha.
Baada ya yote kutulia hatimae walianza kupumua lakini muda huo hawakupewa kwani kijimlima chote kilianza kuporomoka kutoka juu kwenda chini baharini na wale majini wote hawakuwa na muda wa kupoteza hata wa kujiuliza Roma na Maimuna wapo wapi kwani waliweza kuwachukua wale wasiokuwa na nguvu za kijini na kuwatorosha kwenye eneo hilo kwa haraka sana.
“Pumbavu zako Roma , nitahakikisha nakuua kwa namna yoyote ile”Aliongea Mzee Ghula kwa hasira akiwa haamini kama amezidiwa ujanja na kuishia kukimbia na Mzee Sharif, alitaka kutumia uwezo wake wa kijini kumchunguza Roma alipo lakini hali ilikuwa tete.
“Huyu mwanaharamu yupo wapi , mbona kapotea siwezi kupata msisimko wake”Aliongea Mzee Ghula kwa hasira mara baada ya kutua eneo la mbali.
“Master si atakuwa na yeye amepasuka pasuka vipande na Maimuna?”Aliuliza Marid.
Mzee Sharif mara baada ya kusikia jina la mjukuu wake likitajwa alijikuta akipatwa na huzuni kubwa na kujiambia pengine lilikuwa kosa kumchokoza Roma.
“Hapana , hawezi kufa yule , inaonekana huu ni mpango aliotuandalia hivyo kuna njia ya kujiokoa ameitegneneza tokea mwanzo”Aliognea
Mzee Sharif hakujua namna ya kuongea kwa wakati huo kwani alikuwa amechafuka na vumbi hatamaniki , zile sura za majigambo zote kwisha na kilichokuwa kimebakia ni hasara nyingine ambayo wameipata siku hio,walikuwa wakijiamini wanakwenda kummaliza Roma lakini ni kama vile wamejipalia makaa
Lakini bado mzee huyo alikuwa akijiuliza mabomu hayo nani ambaye ameyarusha , aliamini kabisa serikali ya Tanzania haiwezi kwenda mbali na kufanya kitu cha namna hio kwani ungekuwa ni ukichaa.
Kama sio serikali ya Tanzania je katoa wapi makombora ya kijeshi , vipi amewezaje kufukia mabomu ndani ya jengo lao la hoteli bila wao wenyewe kujua.
Alijiuliza hata kama serikali ya Tanzania haikuhusika jeshi la Tanzania linafanya kazi gani kulinda mipaka ya bahari.
Aliishia kukumbwa na fedheha kubwa na kujiambia habari hio ikifikia watu itakuwa ni dharau kubwa wamefanyiwa.
Wakati wote wa Kigamboni waliweza kusikia milipuko hio na wengine walikuwa washaanza kukimbia na kudhania taifa linavamiwa.
Ilikuwa ni kwa haraka sana baada ya tukio hilo wanajeshi ndio sasa wanaamka huku simu nyingi na maelekezo yakitolewa kutoka mamlaka ya juu ili kujua nini kinatokea.
Ni ndani ya nusu saa tu taarifa ziliweza kufikia jeshi la Tanzania kuhusu Kichaa afahamikae kwa jina la Roma Ramoni alikuwa akiisambaratisha familia ya Sharif kwa mabomu na makombora na taarifa hio ilipelekea kila mtu kupigwa na mshutuko , ijapokuwa ni habari zilizoenea kwa baadhi ya vongozi lakini zilikuwa za kushitusha mno kwani ni mara ya kwanza raifa kupitia milipuko ya aina hio.
Sasa mjuda ambao Suzzane na Nadia alfonso wanafika ndani ya nyumba ya mapumziko ya Raisi Senga ndio wakati ambao anapokea taarifa ya makombora kurushwa ndani ya kigamboni katika eneo linalomilikiwa na Mzee Sharif huku jeshi likishindwa kujua swala hilo limetokea vipi na makombora hayo yametokea wapi.
Kuna wengine walianza kufananisha milipuko hio na mabomu ya mbagara yaliotokea miaka kadhaa iliopita.
*****
Upande mwingine giza likiwa limetanda juu ya maji ya bahari huku upepo ukivuma kwa kasi kiasi cha kusababisha mawimbi makubwa.
Kilomita kumi katikati ya bahari lilionekana dude la chuma kama lisamaki likubwa la baharinni likiambaa ambaa kwa kasi likielekea katikati ya bahari huku likitoa mkonga wake kwa juu.
Ilikuwa ni manuari ya kijeshi yenye urefu zaidi ya mita moja na kadri ilivyokuwa ikijitokeza juu chuma chake kilichopakwa rangi nyeusi kilionekana vizuri tena bila kupiga sauti yoyote ile.
Ndani ya manuari hio katika eneo la Deck kulikuwa na mwanamke mjapani aliekuwa mrembo akiwa amevalia mavazi ya kawaida , huku nywele zake ndefu akiwa amezifunga kuzirudisha nyuma.
Pembeni yake alikuwa ni mwanaume wa kizungu ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kijeshi ya kiwana majji.
Kombati zake za kijeshi hazikuwa na isignia yoyote ile kuashiria ni jeshi la wapi zaidi ya kuwa na chata kubwa la fuvu.
Mwanaume yule alionekana kuwa katika tabasamu pana huku akimwandalia mwanamke wa kijapani aliekuwa mbele yake na aliweza kuona wasiwasi wake.
Nyuma yake pia kulikuwa na wanajeshi waliokuwa na sura za kikauzu wengine wakiwa ni Wafrika , wengine ni Warabu na wengine wakiwa ni Wazungu wakiwa wamesimama wima kikakamavu.
“Madam Tanya huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani misheni imekamilika kwa asilimia mia moja , kwa mahesabu tuliopiga itachukua zaidi ya nusu saa mpaka jeshi la maji la Tanzania kutushitukia na mpaka wakati huo tutakua kwenye maji ya kimataifa”Aliongea kwa kingereza.
“Colonel Brewester, I don’t care about the Navy , all I care is about His Majesty Pluto’s Safety”Aliongea na kumfanya Kanali Brewester kutoa tabasamu ambalo halikuwa na hofu kabisa alikuwa katika hali ya mchecheto kwani misheni iliomfikisha hapo alikuwa ameikamilisha kikamilifu bila hata jeshi la Tanzania kuwashitukia na muda huo wanaenda kujiegesha kusubiri maelekezo mengine zaidi.
Haya njooni watsapp mmalizie 0687151346
 
SEHEMU YA 651.
Roma alimlaani Mzee Kweka kwa kupenda kumuweka hewani na palepale alirusha simu yake pembeni.
Roma mara baada ya kupiga mswaki na kujiweka sawa , alikumbuka Hazina ambayo aliiba huko Kilimanjaro na palepale alichukua lile boksi na kuangalia kilichopo ndani.
Roma alishangaa , kilikuwa ni kitu cheusi kilichokuwa kimewekwa ndani kinacholingana na kokoto lakini yenye muonekano wa kuvutia kidogo.
“Hiki ni kitu gani?”Roma alijiuliza huku akijiambia pengine ni Dhana ya kijini na hakuweza kuhisi nguvu yake kwasababu hakuwa na uwezo wa kutumia nguvu za kijini.
Lakini bado ilimfanya Roma kutodhania ni kitu cha kawaida mpaka kuitwa Hazina kutokana na muonekano wake, maana kitu hicho kilikuwa kama vile ni ishara ya kitu flani lakini hakuweza kujua ni kitu gani.
Roma hakutaka kufikiria sana , alirudisha kama ilivyokuwa hazina hio ambayo hakujua maana yake na kisha akapotezea swala hilo kwa muda.
Baada ya kushuka chini aliweza kumuona Lanlan akiwa tayari ashaanza kunywa chai kwa kushikilia chapati za maji huku Qiang akiwa anamsaidia kumnywesha maziwa.
Kwa jinsi mashavu yake yalivyotuna ilikuwa ngumu kuamini kama alikuwa akimeza vizuri kile ambacho anakula.
Roma pia alishagazwa na uwepo wa Amina na Rufi waliokuwa wamekaa eneo la sebuleni wakiangalia runinga.
“Nyie mnafanya nini hapa asubuhi yote hii?”Aliuliza Roma huku akifinya mashavu yao.
“Ushasahau nimemuahidi Lanlan kumpeleka kucheza , napaswa kutimiza hadi yangu kwani leo ndio nipo free”Roma alimwangalia Lanlan na kuona alikuwa akimwangalia kwa namna ya kumwambia asikatae.
“Hubby , unaonaje tukienda pamoja , tukiwa wengi ndio itakuwa vizuri zaidi”Aliongea Rufi.
“Lazima niende pia , vipenzi vyangu nyie mnaenda pamoja na binti yangu lazima niwasindikize kama bodigadi , wote nyie ni warembo hivyo nina wasiwasi mtaibiwa”
“Unapaswa kuwa na wasiwasi labda na sisi tu lakini sio Lanlan , itakuwa vizuri kama wavulana wa huko hawatamuogopa Lanlan”Aliongea Nasra.
“Nasra wewe hujui tu , lakini Lanlan akishakuwa mkubwa atakuwa mrembo haswa , naamini majitu isiokuwa na adabu itamsumbua sana ili kumharibu mapema iwezekanvyo”Aliongea na kumfanya wote wamwangalie namna ambavyo amekosa aibu.
Baada ya Roma kupata kifungua kinywa aliingia kwenye gari ya Amina na kuendesha kuelekea Kawe eneo maalumu ambalo limekuwa maarufu kwa ajili ya michezo ya watoto.
Baada ya kufika watoto walikuwa wengi mno maana ilikuwa ni kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka.
Lilikuwa ni eneo lenye hali ya hewa nzuri kutokana na kuwa ufukweni na Roma alipata muda mzuri wa Kurelax maana tokea arudi ni mwendo wa hekaheka.
Baada ya Lanlan kucheza kwa muda mrefu ilikuwa ishatimia saa saba mchana na alirudi na kumwambia baba yake njaa inamuuma na Roma aliwachukua na kisha wakasogea upande mwingine eneo hilohilo sehemu yenye mgahawa wa kisasa na kisha walikaa na kuagiza chakula.
Wakati wakiendelea kula Lanlan aliacha kula na kuangalia upande wa nje huku akionekana kama kuna kitu amekiona na kukitamani, ilimfanya na Roma kuangalia upande wa nje na kugundua pembeni yao kuna mtu aliekuwa akichoma mishikaki.
Rufi aliweza kugundua alichokuwa akihitaji Lanlan na palepale alisimama na kuchukua pochi lake.
“Mnaweza kuendelea kula nitaenda kununua kwa ajili ya Lanlan”
Lanlan mara baada ya kusikia kauli ya Rufi aliinua kijiko chake kwa furaha zote na Roma aliishia kutabasamu na kufuta punje za pilau zilizokuwa zimemgandia pembeni.
Ni mara baada ya Rufi kumaliza kupewa mzigo wake wa mishikaki sasa wakati akijiandaa kulipia palepale alisikia sauti pembeni yake.
“I want those two”
Sauti ya kike pembeni yake iliweza kusikika , ijapokuwa mtu alieongea hio kauli alitumia kingereza lakini kidogo tu Rufi adondoshe mishikaki kwenye mchanga lakini alijizuia, hata hiyo alikuwa amechelwa kwani pochi lake lilimponyoka na kudondoka chini kutokana na kutetemeka.
Haraka haraka aliinama na kuchukua pochi lake na kumpatia muuza mishikajji hela yake na kutaka kuondoka bila ya kugeuza sura yake.
“Subiri”
Sauti ya kike ambayo iliagiza mshikaki ilimzuia kuondoka na yule mwanamke palepale alikimbia na kwenda kusimama mbele ya Rufi ambaye hakugeuka.
“Hey! Ni wewe kweli.. Aaa..Shemeji!!!”Aliongea yule msichana huku akionyesha hali ya kuwa furaha na mshangao kwa wakati mmoja.
“Miss utakuwa umenifananisha”Aliongea Rufi huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Shemeji kwanini unajifanya hunijui , ni mimi Xiao Xiao , tulikutana wakati ulipochumbiwa na kaka yangu”Aliongea huku akiinamisha kichwa chake kutaka kumwangalia Rufi ambaye alikuwa na mabadiliko.
“Hapana sio mimi umennifananisha” Rufi alionekana kutetemeka mno.
Ukweli alilaani sana katika hali kama hio , hakujua imekuwaje akakutana na Xiao Xiao msichana ambaye alikuwa akimjua fika kwani alikutana nae katika ulimwengu wa kijini kabla ya kutoroka.
*******
Nje ya hoteli ya Serena alionekana Suzzane akishuka kwenye gari aina ya Audi ya rangi nyekundu na kisha kumpatia Valet ufunguo baada ya kutoa pochi yake.
Baada ya kuweka mkoba wake kwenye kwapa palepale alianza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo la hoteli huku akigeuka nyuma akiangalia kama kuna mtu anamwangalia.
Suzzane alikuwa amebadilisha mtindo wa nywele , siku hio alikuwa amevalia Wigi na kumfanya kuonekana mtu mwingine kabisa.
Baada ya kuingia eneo la mapokezi na kupokelewa na mwanadada aliepamba uso wake kwa tabasamu palepale aliongea kidogo na mwanadada yule alichukua simu yake na alionekana alikuwa akiongea na ndani ya dakika chache alitabasamu na kisha akampa ishara Suzzane ya kuendelea kutembea.
Suzzane mara baada ya kuingia kwenye Lift alivuta pumzi kwa kutuliza presha yake na kisha alibonyeza kitufe kuruhusu Lift hio kumpeleka katika Floor husika.
Alijiangalia mavazi yake kwa kujichunguza na kuona yupo vizuri na na amependeza , kwa jinsi ambavyo alikuwa na wasiwasi ni kama mwanamke ambaye anaenda kukutana na mpenzi wake kwa mara ya kwanza.
Baada ya Lift kupandisha na kufika floor ya tatu , ilisimama na kufunguka na alionekana mwanaume alievalia suti na miwani nyeusi.
Suzzane alimpiga mwanaume huyo jicho la pembeni kumchunguza lakini hakuonyesha hofu na yule mwanaume hakuonyesha kumjali Suzzane kwani aliingia kwenye lift na kisha kutulia bila ya kubonyeza kitufe chochote.
Suzzane hakuwa mshamba , alijua pengine mwanaume huyo alikuwa akielekea Floor sawa ndio maana hakugusa vitufe lakini hakuacha kuwa na wasiwasi.
Baada ya Lfit kufunguka katika Floor namba sita wote kwa pamoja walitoka na mwanaume yule alichukua upande wa kushoto na Suzzane alichukua upande wa kulia.
Suzzane alijikuta akipatwa na ahueni na kisha alitembea kwenye Korido yenye msururu wa vyumba na ndani ya dakika chache tu aliweza kufika katika mlango wenye namba 123 na aligonga mara moja na dakika hio hio mlango ulifunguliwa na kisha akaingia.
“Shosti unaonekana kuwa na presha juu juu”Sauti nyororo ilisikika ikiongea na kumfanya Suzzane kuhema kwa nguvu kwa hali ya ahueni.
“Sijui nakua paranoid au nini lakini niseme hata nikienda chooni tu nakuwa na wasiwasi”Aliongea Suzzane huku akilazimisha tabasamu na kujaribu kuangalia mazingira.
Nadia alitoa tabasamu na kisha alimsogelea Suzzane na kumpa ishara ya kutaka kumkumbatia na Suzzane hakuwa na hiyana ya kukataa kumbatio.
“Unafanya vizuri Suzzane , ukishazoea kila kitu utaona ni kawaida”Aliongea na Suzzane lile kumbatiao kidogo lilionekana kuwa dawa kwake kwani aliweza kutulia.
“Unaonekana kuwa mzoefu Nadia , ulishawahi kufanya kazi ya hatari kama hii?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Nadia kutoa tabasamu.
“Nishawahi kufanya kazi ya hatari mara tatu ya hii, mwanzo wakati napewa misheni ya kufanya nilikuwa kama wewe tu ndio maana nimesema unafanya vizuri”Aliongea na kisha Suzzane alimimina maji kwenye glasi na kisha akampatia Suzzane huku akimwambia akae.
Suzzane baada ya kunywa maji yale alijihisi angalau ameweza kupoa.
“Presha ilipanda zaidi mara baada ya kukutana na mtu kwenye Lift , alikuwa amekaa kama mwanausalama, aliniogopesha mno , nikajua ni watu wa Raisi Senga”
“Oh .,.. huyo atakuwa ni mwanasalama kweli , hakika unafanya kazi nzuri Suzzane , lakini hupaswi kuwa na wasiwasi , kuna raisi kachukua makzi ndani ya hii hoteli”
“Raisi!!!”
“Ndio , ni taarifa za siri sana za kiusalama , nimejua hayo kutokana na kwamba nimekutana nae kwa ajili ya mazungumzo, kwasasa sitokuambia ni raisi wa taifa gani”Aliongea Nadia huku akitoa tabasamu.
Na kisha alisimama na kwenda kutoa mvinyo kwenye jokofu na ksha akafika nao na kuuweka mezani na kuanza kujimiminia.
“Hongera Suzzane kwa mara nyingine, kila kitu kimeenda kama tulivyopanga”Aliongea Nadia na huku akimpatia Suzzane glasi ya mvinyo na mara baada ya Suzzane kupokea alimpa ishara ya kugongesheana Cheers.
Baada ya Suzzane kunywa ile Wine kidogo alijikuta akitoa macho kutokana na utamu wake.
“Vipi umeipenda?”
“Ina radha tamu kweli?”
“Yeah hii ni Chateu Margaux, nilipanga kushare hii zawadi na wewe siku ya leo”Aliongea na kumfanya Suzzane kutabasamu na kuangalia chupa ya Wine hio.
Hakuwa mshamba alijua huo ni mvinyo wa bei ghali sana , pengine kama angetaka kuununua basi angefilisika.
Waliongea kwa dakika kadhaa huku wakionyesha kucheka na kufurahi kwa pamoja kama marafiki na kumfanya Suzzane kupotezea hofu yake.
“Kila kitu kimeenda kama tulivyopanga Suzzane, unajisiije mara baada ya kufikia hatua hii?”
“Wakati naanza kufanyia kazi huu mpango sikuwahi kudhania kama ungefanya kazi, yaani hapa hisia zangu siwezi kuzielezea”
“Suzzane kila kitu ndani ya dunia hii kinawezekana ukiwa una taarifa sahihi”Aliongea.
“Ilikuwaje mkaweza kuja na huu mpango?”
“Ni maswala ya kisaikolojia Suzzane , kama ungekuwa na mafunzo ya kijasusi basi ungejua mambo mengi yanawezekana sana kwa kusoma saikolojia ya mtu na tabia zake, tulichofanya ni kufaitlia maisha ya Salihi ya kila siku ili kujua tabia zake, we did it randomly at first without any plan lakini mara baada ya Asha kuingia kwenye Equation tuliweza kufinilize kila kitu na here we are”Aliongea .
“Unajua mpaka sasa kuna baadhi ya vitu nashindwa kuelewa , Salihi kutoka kimapenzi na mama yake wa kambo ni swala ambalo nashindwa kuliprocess kabisa”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kutoa kicheko.
“Hii dunia Suzzane ina mambo mengi na huwezi kuyajua yote , laiti ungejua hata nusu robo tu basi maisha yako yangebadilika kabisa, anyway tunapaswa kuachana na hayo , leo nataka kukuambia kwamba kesho ndio siku yako ya mwisho ya misheni yako”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kesho ndio siku ya kumshawishi Raisi Senga kujiunga na Umoja wa Ant- Illuminat , lazima iwe kesho Suzzane kabla hajalazimishwa kusaini mkataba wa kishenzi”
“Sijakuelewa swala hili linahusiana nini na Mkataba wa kishenzi?”
“Suzzane we are Ant – lluminat, ikimaanisha kwamba tunaenda kinyume na namna dunia inavyoendeshwa , hiki ndio tunachopambana nacho, kuna kitu kikubwa sana kimepangwa kukamilishwa hapa Tanzania na mimi misheni yangu ni kukizuia kwa namna yoyote lakini kabla hilo halijatokea wewe unapaswa pia kukamilisha misheni yako, kumbuka ulichoambiwa kule Qatar”Aliongea na kumfanya Suzzane kumwangalia Nadia kwa macho ya kuuliza.s
Ulishatuma hii
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR
WATSAPP:0687151346.

Mono no aware.

SEHEMU YA 655
Bi Wema licha ya kwamba alikuwa na hali ya kutoridhishwa na tabia ya Edna kutolea hasira zake kwa Lanlan lakini hakutaka kumuona akidhulika kwa namna yoyote ile mara baada ya kusikia kauli ya Roma kwamba anataka kumuua.
“Hapana Mr , usiwe mwepesi hivyo , Edna anakufanyia makusudi tu”Aliongea Bi Wema kumtuliza Roma, hakujua kama Roma alikua kwenye hali isiokuwa ya kawaida kwani haikuwa swala tu la kuchanganywa na Edna kwa kukosa huruma lakini kilio cha Lanlan kilikuwa ni pigo lingine ambalo liliathiri moyo wake.
Watu wawili muhimu kwenye maisha yake waliweza kumpa pigo katika akili yake, ilikuwa ni kama vile hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kuziba shimo ambalo limejitengeneza katika moyo wake.
Muda huo akili yake ilikuwa katika hali hatarishi ya kuweza kumezwa na nguvu ya roho ya mnyama iliokuwa ndani yake , ni kama ilichukulia wakati huo ambao hakuwa sawa kiakili kutaka kujaribu bahati ya kuutawala mwili wa Roma.
Roma uwezo wake wa kujidhibiti ulikuwa umepungua kutokana na hali aliokuwa nayo ndio maana alisema anataka kumuua Edna licha ya kwamba hakuwa akidhamiria kufanya hivyo.
Nia ya roho ya kipepo ya mnyama ilikuwa wazi kabisa kile ambacho ilikuwa ikitaka kufanya, ilikuwa ikimsukuma Roma kumuua Edna ili baada ya hapo Roma awe kwenye majonzi makubwa na mwisho wa siku kukosa mhimili na kuchukua mwili wake.
Roho ya kipepo ya mnyama huyo mpango wake ilikuwa ni kuiba uwezo wa kijini wa Roma na baada ya hapo kutawala akili yake na kurudi hai tena kwa kuua roho ya kibinadamu ya Roma na ndio ingekuwa mwisho wa kuishi katika gereza la Cauldron.
Roma akili yake ilicheza haraka sana na kuona roho hio inachotaka kukifanya na alijitahidi kukunja ngumi pamoja na kung’ata meno kwa nguvu kujizuia akili yake isimpotee.
Hakuwa akishindana na Edna bali alikuwa akishindana yeye mwenyewe na Edna hakuwa akilijua hilo, pengine angekuwa na uelewa angepunguza jeuri.
“Unadhani naogopa kufa , kama ningekuwa naogopa nisingeomba Talaka”Aliongea Edna kijeuri.
“Wewe…
Roma alikuwa akipambana na akili yake na maneno yake ni kama yalikuwa yakimsaidia zaidi roho iliokuwa ndani yake kushinda , ijapokuwa asingeweza kumuua lakini hakutaka kujizuia kumpiga kibao.
Lakini kabla hajamkaribia tu Lanlan alianza kumpigia makelele kumtaka asimpige mama yake.
“Daddy don’t hit mommy , Don’t hit her”
Sauti ya Lanlan iliokuwa kali kwenye masikio yake ni kama neno la upako katika akili ya Roma kwani palepale aliweza kuidhibiti akili yake na kuiweza nguvu ya mnyama wa maafa.
Uhusiano wa mtoto na baba katika ulimwengu wa kiroho siku zote unakuwa na nguvu mno , nguvu ya kuweza hata kushinda roho za giza na hiki ndio kilichotokea , sauti ya Lanlan ni kama maneno ya kichungaji au kishekhe.
Katika maisha unahitajika kuwa na sababu kubwa ya kuweza kukupa motisha ya kuendelea kuishi hivyo Roma mara baada ya kuisikia sauti ya Lanlan ni kama ukumbusho kwake kwamba ana mtoto wa kumlea.
“Lanlan hakuwa mtoto mzuri….Lanlan hatakuja kumtafuta mama tena”Lanlan aliongea huku akifuta makamasi yaliochaanganyika na machozi huku akimwangalia Edna kwa mara ya mwisho na kisha kukificha kichwa chake asimuone tena.
Kauli ya Lanlan ilimpa Roma uchungu mwingi moyoni lakini hakuwa na la kufanya, angewezaje kumpiga Edna mbele ya mtoto wake.
“Ninaenda kupumzika ndani kama huna kingine cha kuongea , nipo bize”Aliongea Edna huku akibana vizuri mkoba wake kwapani.
“Subiri..”
Roma hakutaka kumruhusu kuondoka kirahisi , alikuwa bize kushindana na mnyama wa maafa hivyo hakuweza kupata muda wa kuuliza maswali.
“Edna , unasababu yoyote … siamini kama unaweza kuwa mkatili hivi , kama unasababbu kwanini usiniambie , tumepitia magumu mengi pamoja , hivi huamini uwezo wangu , kwanini tusikae chini tukaongea hili likaisha kama wanandoa ?”Roma alongea akiwa katika hali ya matarajio ya jibu la Edna.
Bi Wema hata yeye aliona alichoongea Rioma ni sahihi na kutamani Edna kuurudisha moyo nyuma na kuyamaliza.
Kama kawaida Edna alimwangalia Roma kwa sura ya kejeli huku akitoa tabasamu la kuchukiza.
“Acha kuwa kichekesho, mkataba wangu wa ndoa na wewe ushaisha na sasa nafanya ninachotaka”
“Siamini kama umebadilika hivi ghafla tu”
“Kama unataka tuendelee kua pamoja sawa , lakini lazima nikwambie ukweli hapa hapa uelewe , ni aidha unichague mimi au binti yako”Aliongea akiwa siriasi kabisa.
Roma na Bi Wema walijikuta wakibumg’aa , hakuna ambaye aliweza kuamini masikio yake kama yamesikia vizuri , yaani Edna anamwambia Roma kwamba achague kuishi na Lanlan au amuache aishi na yeye.
“Hapana huyu ni mtoto pekee wa Seventeen na pia ni binti yangu , nawezaje kumuacha ?”
“Kama ni hivyo kesi imeisha ..”Aliongea huku akimwangalia kwa tabasamu la kumdhihakki
“Nina weza kukubaliana na michepuko wako kwasababu hawana uwezo wa kushindana na mimi na ninajiamini, lakini siwezi kukubali kushindania penzi na mwanamke aliekufa ukijumlisha na mtoto alieacha .. kila saa ninapomfikiria Lanlan ninajihisi ni kama vile namuona huyo mwanamke pembeni yako , hata kama umesema mimi sio mbadala wake lakini kwangu nakuona kama mnafiki tu , kuendelea kumuona mbele yangu ni kama tusi kwangu na najihisi kama vile ndoa yetu ni kichekesho kiasi cha kunipatia maumivu makali ambayo sijawahi kuyapitia hapo kabla , maadam huyo mtoto atakapoendelea kuwa na wewe huwezi kumsahau Seventeen kwasababu ndio mwanamke ambaye unampenda sana, mwanamke ambaye ameweza kukuzalia mtoto”
Maneno ya Edna yalikuwa makali mno kuyasikia , ni kama yalikuwa yakiurarua moyo wake.
Alishindwa kuamini ni kweli kwake akimuona Lanlan alikuwa akijisikia kama anateswa kwasababu tu ya Seventeen.
Dakika hio Roma alijiuliza je lilikuwa kosa kumtambua Lanlan kama binti yake kwa kumzaa lakini aliona bado alikuwa sahihi asingemfanya Lanlan kutambulika kama mtoto wa kuasili ilihali yeye ni baba yake mzazi, isingekuwa haki.
“Nadhani tamaa yangu imeniponza , upo sahihi , sijui kama nakupenda sana wewe kuliko Seventeen lakini jambo moja ambalo nina uhakika nalo ni kwamba siwezi kumuacha mtoto wangu kwa namna yoyote ile”
“Ni afadhali umelitambua hilo kwaheri”Aliongea na kisha aliingia ndani bila ya kuangalia nyuma.
“Mr hakuna chochote kingine ambacho unaweza kufanya?”Aliuliza Bi Wema ambaye alikuwa kwenye majonzi.
“Bi Wema najua wasiwasi wako na unahitaji hili liishe lakini nakuomba usiwe na huzuni , unapaswa kuwa na furaha kwa ajili ya Rufi”
“Kwanini niwe na furaha kwenye hali kama hii , hata Rufi mwenyewe hawezi kukubali wewe kuachana na Edna”Aliongea
“Bi Wema nadhani ni muda sahihi kumuacha sasa aende , ni makosa kuendelea kubakia hapa na kumsumbua, isitoshe ndoa yetu imeanza na sintofahamu nyingi , ni kama wakati unapofundishwa kuendesha baiskeli kwa mara ya kwanza unaambiwa unapaswa kugeukia upande unaotaka kudondokea na sio upande mwingine , hivyo ninachoweza kufanya kwasasa ni kuendana na hali ilivyo tofauti ya kuwa king’ang’anizi wa kubadilisha mueleko wa hali , Edna anaweza kunidharau kwa kumchagua binti yangu na kumuacha yeye, anaweza kutokuwa sawa japo siwezi kuona lakini ninachojua hana rafiki wa kuongea nae , naomba umsikilize kile ambacho ataongea , kama akilia msaidie kufuta machozi, kama ataniongelea vibaya muunge mkono , kama akikuuliza nimekuambia chochote naomba umwambie …’ I am sorry’ kwa kila kitu”Aliongea Roma na maneno yake pamoja na muonekano wake vilimfanya Bi Wema na utu uzima wake kushindwa kujizuia kutoa machozi kwani Roma alikuwa akitia huruma.
“Edna anachofanya ni utoto , kitu muhimu kuwafanya wenza kudumu ni upendo , ujuaji una athari ya vitu vingi”
“Kila mtu ni tofauti Bi Wema..”Aliongea Roma na muda huo huo macho yake yaligeukia upande wa getini nje mara baada ya kuona gari aina ya Bentley ikisimamishwa na akili ya Roma haraka haraa ilimwambia huyo lazima atakuwa ni Maimuna kwani alikuwa na miadi nae ya kukutana siku hio.
“Bi Wema kuna sehemu napaswa kwenda , naomba unisaidie kumpeleka Lanlan nyumbani kwa Nasra na umwambie Qian Xi kwenda nae mgahawanni kumnunulia chochote anachotaka maana Nasra hatorudi”Aliongea Roma huku akimkabidhi kwa Bi Wema.
Dakika hio hio Maimuna aliweza kusimamisha gari nje ya geti ambalo halikuwa limefungwa vizuri na kutoka nje ya gari na kuingia ndani kabla hata hajakaribishwa.
Alikuwa amevalia gauni refu rangi nyekundu na kikoti cha rangi nyeusi juu yake , nywele zake hakuwa amezifunga zaidi ya kuzichana kuzirudisha nyuma na miondoko yake ilikuwa ile ya kushawishi macho ya watu kumwangalia.
Baada ya kuingia ndani aliweza kumuona Lanlan na Bi Wema ambao wote walikuwa na dalili ya kulia na kuonyesha mshangao kwa sekunde lakini dakika ileile aliupotzea kwa kuupamba uso wake na tabasamu na kisha alimkimbilia Roma na kwenda kujirusha kwenye mikono yake , kwa jinsi ambavyo aliweza kujikumbatisha kwa Roma ni kama vile alishawahi kufanya hivyo mwanzo.
Roma aliweza kunusa harufu kali ya marashi ya kuvutia kutoka kwa mwanamke huyo na ukweli alishindwa kumkwepa ndani ya muda na kuishia kushika ngozi yake laini , ilikuwa ni kwasababu hakumtegemea kama angekuja kumkumbatia.
Roma ile anataka kujitoa kwake palepale alipitisha mikono yake kwenye shingo huku miguu yake akiipitisha kwenye kiuno cha Roma na kuning’inia kama mtoto mdogo, alienda mbali zaidi na kusugua manyonyo yake yaliosimama katika kifua cha Roma.
Mrembo huyu hakujali sehemu hio ni nyumbani na Edna alikuwepo , ilikuwa ni kama vile alikuwa akifanya makusudi.
Roma jambo lile lilimshangaza na kujiuliza huyu mwanamke anafanya nini , kwanini anafanya haya yote ghafla tu.
“Hehe… Roma huyo ndio binti yako ? She is cute”Aliongea huku akimwangalia Lanlan kwa tabasamu.,
Bi Wema alikuwa kwenye mshituko mara baada ya kumuona mwanamke mrembo kama huyo ambaye hakuwa akimjua akimkumbatia Roma kama vile wanafahamiana na aliishia kumwangalia Roma kwa maswali mengi.
Roma alijikuta akijisikia vibaya kutokana na kitendo hicho kwani pia alikosa maelezo ya kutosha ya kujielezea na aliihisa kujitoa katika mwili wa Maimuna.
“Sidhani kama tuna ukaribu wowote” Aliongea Roma akijaribu kuweka usiriasi kwenye uso wake kutokana na kutokuwa kwenye mudi nzuri lakini maneno yake ya moja kwa moja hayakumuathiri Maimuna.
“Najua jina lake anaitwa Lanlan Ramoni Kweka, ana jina zuri mno , linaendana na muonekano wake”Aliongea na kumfanya Roma kukunja ndita.
“Inaonekana umefanya utafiti wa kutosha”
“Sio vibaya kujua maisha ya mwanaume ninaemtamani”Aliongea huku akimkonyeza Lanlan .
“Acha maneno mengi , nipeleke kwenye hio sherehe”
“Tunaenda babu lakini haina haja ya kuharakisha ..”Aliongea na palepale alitoa Bracelet(bangiri ) ya Dhahabu ambayo juu yake ilikuwa imetengenezewa ua la kumeta meta la madini ya rangi ya Samawi, ilikuwa ni Bracelet ya ajabu mno kuangalia na mwanga wa jua linalozama uliifanya kuwaka wake pale mbele.
Baada ya kuishikilia mkononi alimsogelea Lanlan huku akiwa na tabasamu na kumpa ishara ya kupotkea.
“Lanlan hii ni zawadi yangu kwako”
Hata kama alikuwa ni mdogo lazima angejua kitu kilichokuwa mbele yake kilikuwa kizuri na cha thamani na pengine mtoto yoyote asingekataa lakini kwa Maimuna ilionekana ni kosa alilofanya mbele ya Lanlan.
Zawadi yake hio pengine kwa watoto wa kike wa kawaida wangeipokea lakini ilikuwa ni tofauti kwa Lanlan ambaye alishazoea kuona vitu vizuri kama hiyo hususani alikuwa akiona Bracelet ya Almasi ya Nasra ambayo alikuwa akivaa na pia Edna alikuwa akimiliki jiwe kubwa la madini ya Rubi ambalo alipewa na Roma baada ya kutoka ulimwengu wa maijini pepo.
“Its not tasty , I don’t want it”Aliongea huku akigeuzia kichwa chake pembeni akionyesha ishara ya kutotaka kabisa hata kumwangalia.
Tabasamu lote ambalo lilikuwa limeupamba uso wa Maimuma lilipotea palepale na kubakia kuwa katika mshangao.
Alijiambia inakuwaje zawadi yake isiwe tamu , kwani hiko ni chakula.
Alijiambia hakika mtoto wa kichaa ni kichaa vilevile.
Bi Wema alijikuta akifurahishwa na jambo lile na alitatami kucheka na aliishia kukakamaa mwili kujizuia mbele ya mgeni.
Roma pia alitamani kucheka lakini hakutaka kucheka kwani angeharibu taswira yake , lakini hata hivyo ili kumuonyesha kama Lanlan amefanya jambo la maana palepale aliigiza kama anaingiza mkono mfukoni na alipoibuka alitoka na jiwe lingine la Yakuti ambalo alitoka nalo katika ulimwengu wa majini pepo.
“Yaani unatumia hio takataka yako kutaka kumhonga mtoto wangu , inaonekana familia yenu ya Sharif sio matajiri kama nilivyoambiwa”Aloiongea Roma huku akihakikisha Maimuna anaona lile jiwe la kung’aa sana na kupendeza , kwani alilipitisha taratibu taratibu kama vile yupo kwenye slow motion.
“Lanlan binti yangu ninaekupenda hili jiwe zuri ni kwa ajili yako , Daddy anatoka leo hivyo kuwa mtoto mzuri na kaa nyumbani na aunt Qiang sawa, utaenda nae mgahawani kula chakula chakula cha usiku sawa”Aliongea Roma
Lanlan alijikuta akitoa meno yake madogo huku akitoa kicheko wakati wa kupokea jiwe la thamani , lilikuwa dogo kuliko la mama yake lakini alipenda rangi yake.
Maimuna macho yake yalikuwa kodo kwenye jiwe hilo la ajabu ambalo ni kama vile ni mara yake ya kwanza kuliona .
Alijiambia mbona jiwe hilo ni kubwa hivyo …My goodness ,, the purity and size it would’ve cost 50 million dollar on the Market and he just gave it to a kid as a toy!?
Maimuna hakutaka kuamini , ijapokuwa alijua familia ya Roma ilikuwa na uwezo mkubwa ndani ya taifa hili lakini nguvu yake kubwa ilikuwa ni kwenye maswala ya kijeshi tu na sio maswala ya utajiri., kitu pekee ambacho aliona pengine hakuwa akikijua basi ni Roma wenyewe ndio tajiri,
Maimuna alijikuta aking’ata lipsi zake huku kijasho chembamba kikianza kumtoka , alijiambia pengine hakuwa akimjua Roma vizuri .
Alijiambia pengine alichokuwa akikijua ni kidogo sana kuliko kile ambacho alikuwa akimjua nacho na jambo hilo lilimfanya kumpenda na kumchukia kwa wakati mmoja.
Kwa mwanamke kama huyo hakuwa na matamanio na mwanaume wa kawaida anaetokea katika familia yenye utajiri mkubwa lakini asingeweza kujizuia kutoka kimapenzi na mwanaume wa ajabu na kushangaza kama Roma.
Utajiri na madaraka ni vitu vya juu juu na kitu cha kutamanika zaidi ni nguvu halisi pamoja na haiba ya mwanaume ilivyo.
Hata hivyo hakutaka kujilaumu kwani babu yake mwenyewe hakuwa na taarifa zote kumuhusu Roma nje ya nchi.
Inasemekana kwamba licha ya familia ya Mzee Sharif kuabudu majini ambayo ni chanzo cha utajiri wao lakini pia walikuwa na uhusiano wa karibu na jamii za siri kama vile Freemason na walikuwa wakishirikiana kwenye mambo wanayoendana nayo sambamba ki ajenda.
Familia hio haikuwa na ukubwa kwama wa familia ya Rothchild ambayo ilikuwa ipo kila kona ya dunia lakini walikuwa wamejitengenezea sehemu yao ndani ya dunia.
Maimuna alijua pengine ndio maana Afande Kweka alitangaza kilichotokea aadhibiwe Roma mwenyewe , lakini akiwa na uhakika kwamba Roma ana nguvu ya kushinda.
“Huna ubahili wa aina yoyote … vipi tunaweza kuondoka”Aliongea Maimuna huku awamu hii akiwa mpole lakini hakuacha kutaka kujigusisha na Roma.
Roma alijiambia sjui huyo mwanamke ana kiu ya mwanaume ndio maana matendo yake yapo hivyo au ni nini.
Baadaa ya kumuaga Bi Wema na Lanlan Roma alitoka na kuingia ndani ya gari.
Upande wa Maimuna kabla hata hajaingia ndani ya gari aligeuza shingo yake ndefu na kuangalia nyumba hio na kisha akatoa tabasamu la kejeli.
Baada ya kuingia hatimae gari iliweza kutoka eneo hilo kuelekea katika hoteli ya Wache ambayo ilikuwa Kigamboni.
Asichokijua Roma ni kwamba mara baada ya gari yao kuondoka pazia la dirisha katika Floor ya pili lilionekana kufungwa vizuri na Edna ambaye alikuwa akichungulia.

SEHEMU YA 656.
Ni ndani ya jumba moja la kifahari ambalo lilikuwa lipo Kawe , jumba hilo siku hio lilionekana kuwa na ulinzi mkali kuliko siku zote.
Hio ni moja wapo ya nyumba ambayo mmiliki wake ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Senga Cammilius Kweka , ilikuwa ndio nyumba yake ya mapumziko mara nyingi anapokuwa ndan ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maswala ya kikazi,
Siku hii ndani ya nyumba hio kulikuwa na ugeni kwani mheshimiwa alikuwa akitarajiwa kufika hapo muda wa jioni ya saa moja usiku.
Ijapokuwa wengi waliamini Raisi Senga anafika hapo kwa ajili ya mapumziko kama kawaida yake lakini ukweli ni kwamba alikuwa na miadi ya kukutana na mtu kwa ajili ya kufanya kikao cha siri.
Raisi Senga hakuwa akiamini eneo la Ikulu hata mara moja mathalani kwa wale watu ambao wanamlinda ndio maana kila linapotokea swala nyeti sana ambalo linahitaji usiri mkubwa mara nyingi angesafiri kwenda mikoani kwenye ikulu ndogo au angetoa kisingizio cha kwenda kupumzika katika nyumba yake hio , huku akihakikisha watu anao ambatana nao ni wachache tu wale ambao alikuwa akiwaamini.
Saa moja kamili gari kadhaa za rangi nyeusi za brandi tofauti tofauti zilionekana zikiingia ndani ya jengo hilo.
Uzuri wa mazingira ya eneo hilo yalikuwa yametengena sana na maeneo ya makazi ya uswahilini ya watu hivyo ni watu wachache sana ambao walikuwa wameshuhudia gari hizo.
Baada ya saa moja kupita baada ya gari hizo kuingia hatimae ilionekan gari nyingine ikiingia ndani ya hilo eneo , gari hio ilikuwa ni gari aina ya Aud SUV rangi nyeusi.
Baada ya kusimama eneo la getini kwa dakika kama tano hatimae gari ile iliweza kuruhusiwa kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani hatimae aliweza kuonekana mwanadada Suzzane na Nadia Alfonso wakishuka.
Wote kwa pamoja walikuwa wamevalia mavazi ya suti zinazofanana za rangi nyeusi na walionekana kama vile ni wanausalama.
Suzzane ndio ambaye alionekana kidogo kuwa na wasiwasi lakini kwa upande wa Nadia Alfonso hakuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi , pengine ni kutoana na uzoefu wake.
Baada ya kushuka hawakuacha kukaguliwa na walinzi na kisha dakika chache alitokea Kabwe msaidizi wa karibu zaidi wa raisi kaatika kitengo cha ndani cha siri cha raisi na kuwapokea.
Kabwe mara baada ya kusalimiana nao kwa ufupi aliwapa ishsara ya kumfuata huku yeye akitangulia kuelekea mbele.
Mazingira ya eneo hili hakika yalikuwa yakivutia mno , ni sahihi kusema eneo hilo ni maalumu kwa ajili ya mapumziko kwani lilikuwa limejengwa kwa ufanisi mzuri mno , mtu yoyote ambaye angefika hapo lazima angesema ni ufahari wa juu sana kuwa raisi wa nchi.
Lakini upande mwingine kama kauli hio angeisikia Raisi Senga pengine angepingana nayo , kwani kuwa raisi kwake alichukulia ni kama swala la kujitoa, ni kweli kuna faida zitokanazo na uraisi lakini baadhi ya siri ambazo anazibeba kwa ajili ya taifa zilikuwa kubwa mno ambazo zilihitaji akili yenye utimamu mkubwa.
Nadia alimwangalia Suzzane kwa ishara ya kumwambia kwamba anapaswa kujiamini na kisha waliendelea kusonga mbele.
Ukweli ni kwamba mwanzoni Suzzane ndio alipanga kuja kuonana na Raisi Senga peke yake lakini maagizo tofauti yalikuja yakimtaka Nadia kuhusika katika maongezi hayo ili kuweza kumshawishi Raisi Senga kwa namna yoyote ile kuweza kujiunga na umoja wa Ant Illuminat.
“Mheshimiwa Wageni wamekwisha kufika”Aliongea Kabwe mara baada ya kuingia katika eneo la sebule yenye samani za kuvutia.
Mheshimiwa Raisi alionekana kuongea na simu na kadri alivyokuwa akiongea sura yake ilizidi kujikunja na palepale hasira ilimvaa.
******
Wache Grand Hotel ilikuwa imejengwa juu ya kilima , mwanzoni mwanzilishi wa eneo hilo alihitaji kujenga nyumba za makazi kwa ajili ya biashara lakini kutokana na mazingira ya muinuko aliona ni gharama zaidi kuliko eneo la tambarare hivyo hoteli hio ndio ikajengwa.
Hoteli hio ilinufaika kwa kuwa juu ya kilima hivyo kufanya kuweza kutengeneza mandhari mazuri ya bahari huku ikizungukwa na msitu wa miti.
Unaweza kusema hili ndio eneo pekee ambalo ndani ya kigamboni halijaguswa wala kukaliwa na raia wa kawaida, ni eneo ambalo pia limeuzwa kwa Mzee Sharif kwa ajili ya ujenzi hivyo unaweza kusema kwamba hoteli hio ya Wache ni moja ya hoteli ambazo zimejitenga sana katika mji huo wa Kigamboni.
Roma alishawahi kuona kibao cha hoteli hio lakini ukweli ni kwamba hakuwahi kufika ndani ya hoteli hio kabisa na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kujua kumbe eneo hilo lote lilikuwa likimilikiwana familia hio ya Mzee Sharif.
Roma mara baada ya kufika ndani ya eneo la hoteli hio ya nyota tano aliweza kuona sehemu zaidi ya mia moja za kuegeshea magari lakini katika sehemu hizo ni ishirini pekee ambazo zilikuwa zimechukuliwa.
“Kulingana na magari haya naamini kuna watu zaidi ya ishirini huko ndani”Aliongea Roma.
“ Hupaswi kuanza kujutia sasa hivi kuja hapa , vipi umeguswa kwa familia yetu kukuandalia sherehe?”Aliuliza Maimuna na kumfanya Roma kutingisha mabega , alikuwa akitegemea jambo la namna hio , isitoshe familia hio mara nyingi ilikuwa ikilinda siri zao hivyo mambo yao yalikuwa yakiendeshwa kisiri siri hivyo alikuwa amejipanga kuja kukutana na watu wasiokuwa wa kawaida katika eneo hilo.
Yaani kwa kwa haraka haraka ni kwamba hoteli nzima ilionyesha kutokuwa na wageni wengine zaidi ya familia ya Sharif pekee.
Dakika ileile anatoka kwenye gari kabla hata hajapiga hatua kuingia ndani ghafla tu aliweza kushuhudia wanaume wawili waliovalia majoho ya rangi nyeupe wakiibukia kutoka pande mbili tofauti kwa namna ya kupaa, walikuwa katika umri wa miaka arobaini na hamsini kimakadirio huku wakiwa na vipara pamoja na masharupu mengi usoni.
Walikuwa na macho makali ambayo hayakuwa ya kawaida , licha ya Roma kutokuwa na uwezo wa kutumia uwezo wake wa kijini akili yake ilishamwambia hao sio binadamu wa kawaida, walikuwa na muonekano wa kiarabu lakini kwake aliwaona kama sio waarabu.
Roma moja kwa moja aliamini pengine watakuwa katika levo ya kuipita dhiki katika mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi au mafunzo ya kijini.
“Acha kukodoa macho wewe mjjinga”Aliongea jini Imrah ambaye alitokea ndani na Roma alimkumbuka vyema kwani alipambana nae kule Kilimanjaro.
“Jinni Marid na Jinn Iftir wapo hapa kwa ajili ya kukuangalia na wote wapo katika levo ya kuipita dhiki wakiwa na uwezo wa kudhibiti moto wa rangi tatu , watahakikisha huondoki hapa kwa namna yoyote”Aliongea .
Roma alijikuta akishangazwa na kauli ya Jinn Imrah , hakutegemea angeweza kukutana ndani eneo hilo na watu wa levo ya juu katika mafunzo ya kijini.
Roma alijiuliza inakuwaje hii familia ikawa na uhusiano mkubwa na viumbe hawa wa kijini kiasi cha kuweza kuita watu wenye uwezo wa juu namna hio ndani ya muda mfupi.
“Acheni kusimama hapo , wewe mlete huyo ndani anasubiriwa”Aliongea akimpa amri mtoto wake wa kike kumwingiza Roma ndani ya hoteli.
Maimuna aliishia kumwagalia Roma kwa tabasamu huku akimpa ishara ya kutembea kuingia ndani.
“Ukoo wenu hauendeshwi kulingana na nani mwenye nguvu zaidi si ndio?””
“Kwanini unauliza hivyo?”
“Jinn Iftiri na Marid wana nguvu kubwa za kijini kuliko Imrah lakini bado tu wanaonekana kusikiliza maagizo yake”Aliongea Roma na kumfanya Maimuna kutabasamu.
“Mr Roma tatizo unatuchukulia poa , yule Master Iftir na Maridi wote ni washirika kutoka matawi yaliopo katika nchi kadhaa , ukizungumzia swala la madaraka Imrah ana madaraka makubwa kuliko wao , wapo watu wenye nguvu za kijini wengi sana pamoja na majini wenyewe na ni wengi kiasi kwamba hata babu mwenyewe hajui idadi yao”
“Unajaribbu kuniogopesha?, kama ni hivyo si mngeweza kutawala hii nchi?”
“Hatuna haja ya kukutisha kwani tuna nguvu ya kukushinda na kuhusu unachokisema kuhusu kutawala taifa hio ni nje ya sheria za kijini, nguvu yetu ipo katika maswala ya nguvu isioonekana tu”Aliuongea kwa kujiamini
Roma mara baada ya kuingia kabisa ndani ya Korido ya hoteli hio aliweza kukutana na mabodigadi waliokuwa wakilinda, ilimshangaza Roma kwani eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali kama vile kuna kiongozi mkubwa wa dunia aliekuwa yupo katika eneo hilo.
Kwa haraka haraka tu Roma aliweza kuamini mabodigadi hao wapo katika levo za chini za mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi na mbaya zote wote walikuwa ni Waraanbu tupu.
Ilionekana dhahiri kabisa familia hio ilikuwa imeandaa maandalizi makubwa ya kutaka kumdhibiti.
Ukiachana na ulinzi mkali hoteli hio ilikuwa na mazingira ya kuvutia mno , kuna hisia zilimwambia Roma pengine hii hoteli haipo wazi kwa kila mgeni ambaye anataka kuja kupumzika ndani ya eneo hilo.
Hisia za Roma zilikuwa sahihi , tokea ujenzi wa hoteli hio kukamilika hakuna Mtanzania wa kawaida ambaye alishawahi kwenda kulala ni watu wachache sana ambao walikuwa wakijua hata muoenekano wake kwani eneo hilo lilikuwa na ulinzi mkali sana kuanzia getini mwanzoni kabisa wa kuingia kwenye eneo hilo mpaka upande wa Fukwe.
Inasemekana kwamba katika vipindi flanni vya mwaka waarabu wengi pamoja na wahindi huonekana wakiingia ndani ya hoteli hio na hata mpaka leo hoteli hio iliaminika kama hoteli ya Waraabu kwani ndio ngozi pekee ambazo zilikuwa zikifika hapo.Lilikuwa kama eneo mbadala tofauti na lile la kule Kilimanjaro
Pengine ni sahihi kuiita Hoteli ya Majini kwani viumbe ambavyo vinafika hapo havikuwa vya kawaida, aidha ni binadamu mwenye nguvu za kijini au majini yenyewe.
Sasa jambo ambalo Roma hakuwa akilijua ni kwamba kulikuwa na ulimwengu wa majini lakini alishindwa kuelewa huyu Mzee Sharif yeye anatokea katika koo ipi ya kijini na alichosalia ni hao majini au kuna kingine zaidi ya kile anachokidhania.
Roma mara baada ya kuingizwa katika ukumbi mkubwa hatimae sasa aliweza kuona sura za watu tofauti tofauti wengi ambao walikuwa wameketi kwenye Zuria la kuvutia huku katikati yao kukiwa na kifaa flani ambacho Roma hata hakuelewa maana yake ila kilikuwa kikitoa moshi wa pink wenye harufu flani ambayo hakuweza kuielewa.
Sura zote zilikuwa ni nyeupe tupu huku kila mmoja akiwa na ndevu nyingi na masharubu, kuna ambao Roma alikuwa akiwahafamu kwani alishawaona lakini kuna wengine ambao hakuwa akiwafahamu kwani sura zao zilikuwa mpya, wote walikuwa wamevalia mavazi ya tamaduni za kiarabu.
Mzee Sharif alikuwa amekaa katikati kabisa kama kiongozi huku akiwa na kiremba cha rangi ya bluu kichwani, pembeni yake alikuwa ameketi jini Imrah , kushoto kwake kulikuwa na mhindu ambaye amevalia tofauti na wengine wote , yeye alikuwa amevalia joho la rangi nyeusi.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba kila mmoja alikuwa amevalia kitamaduni kasoro Maimuna peke yake ambaye amevalia kisasa zaidi lakini vazi lake likiwa la heshima.
Roma alimwangalia Mzee huyo ambaye amevalia Joho la rangi nyeusi kwa kumchunguza , alikuwa mzee zaidi kuliko Imrah mwenyewe na alikuwa amefumba macho, Roma kwa haraka haraka alijua tu huyo ndio mtu hatari zaidi hapo ndani kuliko wengine wote.
“Mrithi wa ukoo wa Kweka , hatimae tunakutana tena”Aliongea Mzee Sharif.
“Naona watu wengi wapo hapa kwa ajili ya kunikaribisha , kwanini mmejikalisha hapa kizembe tofauti na ukumbi wa chakula kuanza sherehe”Aliongea Roma huku akiwa na tabasamu kama kawaida yake.
“Acha kuigiza wakati unakiona kifo chako”Aliongea mdogo wake Maimuna afahamikae kwa jina la Meki huku akimwangalia Roma kwa kejeli.
Roma hakutaka hata kuongea nae kwani palepale alimsogelea na kisha akampiga teke na kumfanya avamie kimeza iilichokuwa na glasi pamoja na vikombe.
Hakua ambaye alitegemea hilo na walijikuta wakishangaa na kujiuliza au amekuja akiwa amelewa , kwanini ameamua kushambulia kwa kuchokozwa kidogo tu.
Yule mzee mwenye Joho jeusi hatimae aliweza kufumbua macho yake mara baada ya kusikia purukushani hio ya mtu kupigwa kiasi cha kuvamia meza.
“Unafanya nini , unadhani tunakugopa?”Aliuliza Mzee Sharif huku akionyesha hasira za wazi.
“Mjukuu wako ana mdomo mchafu sana na kama ningetaka kumuua mpaka muda huu angekuwa ni kifusi cha nyama tu , nadhani unanielewa mwenyewe”Aliongea Roma.
Meki alijikuta akimwangalia Roma kwa uchungu huku akiugulia maumivu makali.
“Meki ondoka hapa ndani”Aliamrishwa kuondoka
Mwanaume huyo mwenye jina la Meki alimwangalia Mzee Sharif kwa kuchanganyikiwa lakini aliishia kusimama na kisha akatoka nje.
“Roma hatukufanyi chochote kwasababu tunahitaji kufanya na wewe mazungumzo ya kina , hivyo jitahidi kujiuzuia”Aliongea akitoa onyo kwa uso uliokuwa na usiriasi.
“Mnataka kuongea na mimi kuhusu nini? , au ni kuhusu hazina yenu?, niwaambie mapema tu kwamba sijachukua hazina yenu na msije hata kufikiria kutaka niwaombe msamaha”Aliongea Roma lakini hata hivyo hakuna ambaye alikuwa akiamini kauli yake , kila mmoja ni kama walikuwa wakimjua anaigiza tu.
Mzee Sharif alimwangalia kwa ishara mtoto wake mkubwa na palepale alitingicha kichwa na kisha akatoka ndani ya eneo hilo na ndani ya dakika tatu waliweza kufikishwa Naibu waziri Salihi pamoja na Asha huku wakiwa na hofu zaidi mara baada ya kumuona Roma.
“Sikumfundisha vizuri mkwe wangu na mjukuu wangu na wakakuchokoza , unaweza kuwa na kinyongo juu yao na mimi nipo tayari kuwafanya wakuombe msamaha na naahidi hawatolipiza kisasi tena”Aliongea mzee huyo na kisha aliinua uso wake na kumwangalia Roma.
“Unaonaje , ninachoongea hapa nina maanisha kabisa”
“Sijali tena kuhusu wao kuomba msamaha, kama ni fidia nishajilipa kwa kuharibu makazi yenu pamoja na kuchoma jengo lenu la ibada”Aliongea Roma.
“Hakuna shida , kama ni hivyo basi ni zamu yetu”Aliongea na palepale alitoa ishara ya Skrini iliokuwa imefungwa mwishoni kabisa ukutani iwashwe.
Dakika ileile ilionekna vidio katika Tv ile na Roma alipoangalia kwa umakini alijikuta akikunja ndita bila ya kupenda.
Samweli Nguruma ambaye ni baba yake na Benadetha pamoja na mke wake ndio ambao walioneana katika hio vidio wakiwa wapo chini ya ulinzi wa wanaume ambao wameshika mitutu ya bunduki.

SEHEMU YA 658.
Katika vidio iliokuwa ikionekana kwenye skrini hio ilikuwa ikimuonyesha Samweli Nguluma akiwa amefungwa na kamba kwenye kiti huku akiwa amezibwa mdomoni, haikuwa hivyo kwake tu hata kwa mke wake pia.
Ilikuwa bahati kwamba Benadetha na kaka yake hawakuwa nyumbani wakati huo pengine na wao wangeunganishwa katika utekwaji huo .
“Kwa taarifa ambayo tumeweza kuipata ni kwama kundi la Zoa Zoa ambalo lipo chini ya Samweli Nguluma ndio waliokupatia yale mabomu ,je nimekosea?”Aliuliza na kumfanya Roma kushindwa kujibu lile swali na palepale alitoa simu yake na kutafuta namba ya Afande Jamali na kuipiga.
“Mr Roma najua hali ilivyo kwasasa”Aliongea mara tu baada ya simu ile kupokelewa.
“Unajua nini , si wewe ndio ulieniambia kwamba hakuna mtu mwingine ambaye ataweza kuguswa zaidi yangu?”
“Mr Roma sikujua ulikuw ana uhusiano na Mzee Nguluma mmiliki wa kundi la ZoaZoa , Mzee Nguluma amehusika katika maswala ya kihalifu mengi sana na kukamatwa kwake hakuathiri usalama wowote wa jamii”
“Acha kuongea ujinga , hata kama ni mhalifu haina maana kwamba anaweza kukamatwa na watu ambao sio polisi”
“Ni ,.. Hakuna maagizo yoyote ambayo nimepokea kutoka juu , hivyo hatupaswi kuingilia katika hili swala”Roma aliishia kulaani na kisha palepale alikata simu.
Roma alijiambia kutokana na kukosa uwezo wake wa kijini asingeweza kuwaokoa kwa wakati lakini pia hakutaka chochote kiwatokee kwani asingeweza kumwangalia Benadetha usoni kwani ni yeye ndio aliemhusisha baba yake licha ya kwamba mzee huyo alionyesha wasiwasi wake mwanzo.
Mabwana wote waliokuwa hapo ndani walionyesha sura za furaha kumuona namna ambavyo Roma alikuwa akiteseka.
“Unaonaje sasa, wewe ni mtu wa kukurupuka sana lakini unapaswa kuelewa hii dunia sio yako peke yako , kila mtu ana udhaifu wake, kama utatoa ushirikiano, basi tutapotezea swala la Mzee Nguluma kukusaidia mabomu lakini kama utaendelea na ukiburi wako wewe pamoja na Mzee Nguluma mtalipia gharama”
“Unataka nitoe ushirikiano gani?”Aliuliza Roma na kuwafanya wote kutoa tabasamu wakiona Roma hatimae anaenda kujisalimisha.
“Tutakupa machaguo matatu”
“Oh.. hebu yataje tuone“
Chaguo la kwanza , rudisha hazina yetu m jenga upya madhabahu yetu na kisha omba msahama miungu yetu , nadhani ushaambiwa kuhusu hilo, kuhusu chaguo la pili …”Alisita kwanza na kisha akamgeukia Maimuna na kutoa tabasamu hafifu.
“Chaguo la pili unapaswa kumuoa mjukuu wangu Maimuna Sharif na sisi kuwa wakwe zako”
Kidogo tu Roma adondoke chini kutokaa na mshituko , alitaka kujiambia hajasikia vizuri lakini baada ya kumwangalia Maimuna ambaye alikuwa akionyesha viabu vya kike alijua ni kweli kile alichosikia.
Kauli hio ilimfanya Roma kukumbuka matendo ya mrembo huyo , kumbe alikuwa akijua mpango wa mababu zake ndio maana alikuwa akijilengesha.
“Hebu kwanza tuachane na chaguo la kwanza kwani sitofuata na kuhusu chaguzi ya pili na yenyewe niseme kwamba mimi nishaoa tayari hivyo tupotezee”Aliongea Roma akikataa.
“Kwanini isiwezekane , si tayari ndoa yako na Edna imefikia ukingoni, tunajua aliondoka Iringa akiwa ameweka wazi kabisa anataka talaka mbele ya babu yako na habari hii inajulikana ndani ya familia nyingi ndani ya Dar , kama una wasiwasi na maswala ya mgawanyo wa mali sisi tutampatia kitu cha kuridhisha ili talaka yenu iwe rasmi”Aliongea Maimuna.
“Ndoa sio kama mnavyofikiria wewe, kwamba ni mambo ya kusainishana makaratasi na kufikia mwisho , uhusiano wetu hausiani na makaratasi wala ndugu ,sawa?”
“Acha kuniona mjinga , najua ameshindwa kuvumilia wanawake wako , inashangaza kwamba licha ya urembo wake ameshindwa kukulinda kama mke mpaka ukawa na wanawake wengi lakini sasa hivi anaanza kuchafua hali ya hewa , sioni kama ana stahili kuwa mmoja wa familia yenu wala kuendelea kuwa mkeo”
“Kaa kimya wewe hilo halikuhusu , hivyo acha kuongea ujinga”Alifoka Roma
“Unakasirika nini sasa , ninachokuambia ni ukweli , mimi ni mwanamke na nawajua wanawake wenzangu pia kuliko wewe , kwanini unanifokea kwa kuongea ukweli , nenda kamfokee Edna sio mimi”Aliongea na kumfanya Roma kushindwa hata amfanye nini kwani alioneana kujiamini sana.
“Eti dada ndio tuseme kwamba unataka kuolewa na mimi sana au?”
“Mimi sio dada yako unikome… , tunalingana umri ..”Aliongea huku muonekano wake ukibadilika huku kifua chake kikipanda na kushuka , alionekana kama amewezwa kuitwa dada na Roma.
Lakini hata hivyo muonekano wake wa aibu na kukasirika ulimfanya Roma kumshangaa kidogo na alijiambia pengine kama ni miaka kadhaa iliopita asingekataa mwanamke mrembo kama huyo , lakini kwa kipindi kama hicho ambacho alikuwa akitaka kurudiana na Edna kwa namna yoyote ile hakutaka kuongeza matatizo.
Isitoshe ndoa ni tofuati na kulala na kuamka pamoja hivyo Roma aliamini kama angemgusa huyo mwanamke hatua nyingine lazima ingefuata.
Upande wa Roma alijua kabisa familia hio pengine ilikuwa ikitaka kujikita zaidi ndani ya taifa la Tanzania kwa kutaka kuanzisha undugu na familia yake jambo ambalo aliona ni kichekesho.
“Mjukuu wangu sio wa kawaida , ukiachana na muonekano wake , akili pamoja na kutokuwa binadamu wa kawaida , nina wasiwasi huwezi kupata mwanamke wa aina yake maisha yako yote , unapaswa kujiona wa bahati yupo tayari kuolewa na wewe, Edna anaweza kuwa mtoto wa raisi wa Rwanda lakini bado atabakia kuwa mtoto wa nje ya ndoa , tunaweza kukusaidia kwenye mambo mengi tofauti na familia yake itakavyokusaidia , kama utamuoa Maimuna tutahakikisha familia yenu ni ya kuogopwa sio tu hapa Tanzania bali Afrika mashariki kwa ujumla , tuhakikisha tunawapa nguvu ya kuamua kiongozi wa mataifa ya Afrika mashariki awe nani na biashara nyingi zitakuwa chini yenu”AliongeaMzee Huyo.
Roma alijikuta ni kama akili yake haifanyi kazi vizuri , alijiammbia hata kama atakuja kuachana na Edna basi hawezi kuoa mwanamke mwingine.
“Inatosha , haina haja ya kumsifia mjukuu wako kwani simtamani kwa lolote”Aliongea Roma
Ukweli ni kwamba Maimuna ndio mwanamke pekee ambaye miungu ya ukoo imekumkubali kuwa kama kiongozi wa ukoo baada ya Mzee Sharif mwenyewe na walitaka kumjengea nguvu zaidi kwa kumuozesha kwa Roma ambaye alikuw ana uwezo mkubwa wa nguvu za kijini.
Kitu kingine Maimuna hakuwa msichana wa kawiada kama ambavyo amesema Mzee Sharif , inasemekana mrembo huyo mama yake sio binadamu wa kawaida hivyo waliamini kama wataweza kupata mtoto kupitia Maimuna na Roma basi anaweza kuwa sio wa kawaida na kufanya ukoo wao pamoja na dini yao kuzidi kusambaa duniani kote.
Maimuna alijikuta akikasirika na jambo lile na kung’ata lipsi zake nyekundu kwa hasira kwani kitendo cha Roma kumwambia hamtamani kwa lolote kwake ni kama amedhalilishwa, hakuwahi kuwaza kama kuna mwanamme katika dunia hii ambaye anaweza kumkataa kirahisi kama alivyofanya Roma, alianza kujifananisha ana kasoro gani na Edna kwani wote ni warembo huku yeye weupe wa kiarabu ukimbeba.
“Nsihakuambia hivyo huyu Maimuna atakuwa na msaada kwako , ndio anaekwenda kurithi utajiri wote wa familia yetu , acha kuwa mjinga na kumkataa hii ni bahati siojirudia mara mbilimbili”Aliongea na kuwafanya wale wazee ambao hawakuwa wakijua ukweli kuhusu mrithi wa familia kumwangalia kwa mshangao.
Maimuna licha ya kwamba alikuwa mwanamke lakini ndio mmoja wapo ya wanafamilia ambaye alikuwa ameonyesha uwezo mkubwa wa akili na kumfanya Babu yake kumkubali, isitoshe alikuwa ametii sheria za ibada kwa kuendelea kuwa bikra mpaka wakati huo.
“Vipi kuhusu chaguo la mwisho?”Aliulizia Roma na kuwafanya waamini kabisa kwamba bwana huyo ameamua kukataa chaguzi ya kumuoa Maimuna.
“Hakuna shaka , kama ijulikanavyo viijana wa siku hizi ni wenye kukurupuka , chaguo la tatu ni rahisi sana , hatujawahi kujizuia kudili na adui yetu , familia ya Mzee Nguluma wote watauliwa halafu wewe utakuwa mateka chini ya familia yetu na tutakuvua nguvu zote za kijini ulizokuwa nazo na tutakutesa mpaka utoe hazina yetu na kisha kukulazmisha kusujudia miungu yetu”
Roma alijikuta akichezesha ulimi wake kwa kutoa sauti kutokana na namna walivyokuwa wakijiamini mpaka kuongea kauli hio.
“Usituchukulie poa , familia yako inaweza kuwa na nguvu ndani ya taifa hili lakini haimiliki nchi , isitoshe jeshi haliwezi kuwasikiliza kwa kila kitu , tunaweza kuimaliza familia yako kwa kuagiza wazee wetu hapa wa kijini kwenda kuua familia yako yote lakini hatuna mpango wa kwenda mbali hivyo”
Roma hakutaka sana kumwamini huyo kikongwe , alijiambia kama kweli alikuwa jasiri wa kufanya makubwa kwanini alikimbia nchi yake na kuja kujificha hapa Tanzania.
“Nitakupa dakika tatu tu za kufikiria , hili ni swala ambalo lazima limalizike leo hii hii”Aliongea .
Roma alijikuta akitoa kicheko cha kebehi na kisha aliingiza mkono mfukomi na kuibuka na simu na kisha alionekana kuandika namba flani flani hivi.
Kila mmoja alionekana kumshangaa na kujiuliza anampigia nani katika wakati kama huo.
Upande wa Roma haikuonekana kama alikuwa akipiga simu hali namna alivyokuwa akiandika ilionekana kama alikuwa akituma ujumbe wa maandishi.
“Roma usije ukafanya janja…”
Dakika ambayo alitaka kuongea ulisikika mtetemeko na mlipuko mkubwa kama vile ni wa ngurumo ya radi.
Dakika hio hio ndege walionekana wakiambizana kukimbia katika mazingira hayo yenye miti.
Sauti haikuonekana kutokea na kuisha bali iliendelea kusikika mfululizo na ndani ya dakika chache tu ndani ya eneo hili lilianza kuzingirwa na moshi mzito sana huku mawe yakianza kuingia ndani ya jengo hilo la hoteli kiasi cha kupasua pasua vioo.
Magari yaliokuwa yameegeshewa nje yalianza kuwika kwa kutoa ving’ora vya alamu na mengine yalianza kulipuka mara baada ya matanki ya mafuta kupasuliwa na mawe,
“Pumbavu alikuwa akituma signal , inaonekana alikuwa ametega mabomu?” Mmoja wapo alipiga kelele mara baada ya kugundua mlipuko uliokuwa ukiendelea ndani ya eneo hilo ni wa mabomu.
Dakika ileile wakati mabomu hayo yakipiga wakiwa katika hali ya kushangaa Roma alimshikilia maimuna kwa spidi kiasi cha kumfanya kushindwa kuchukua hatua ya kumkwepa .
Maimuna alikuwa na nguvu za kijini lakini zilikuwa za chini sana kulinganisha na uwezo wake.
Roma palepale hakutaka kumcheleweshwa kwani alipitishia vidole shingoni kwa spidi na palepale aliweza kupoteza fahamu na kisha akamuweka begani.
“Wewe mzee wa kiarabu Kikongwe usie na aibu , nimeshindwa kuamini kama ulikuwa na mpango wa kunichokoza kwa mara ya pili , kabla ya kutia mguu ndani ya hii hoteli ishatembelewa na vjana wangu muda tu na kutegesha mambomu aina ya C4., nenda kuzimu”Aliongea Roma kwa kufoka.
“Mjingaaa sana wewe!!, unataka tufe wote kwa pamoja hapa , umekuwa kichaa?”
“Haha si ndio mlichokuwa mkikitafuta, siogopi bomu la nyuklia sembuze hivi vibomu vya kawaida nitaondoka na mjukuu wako , mwachie Mzee nguluma na mke wake la sivyo nitahakikksha namtupia baharini sehemu yenye papa na kisha nitaua kila mwanafamilia mwenye jina la ukoo la Sharif na kufuta mizizi yako ndani ya hili taifa , Shwain..”Aliongea Roma na palepale alikimbilia nje.
Kabla hajapiga hatua yule mhindu aliekuwa kimya muda wote akiwa na mavazi yake meusi palepale alipotea alipokuwa amesimama na ile anakuja kuibukia ni mbele ya Roma.
Ilikuwa kama alivyotegemea huyo mzee alionekana anaenda kumletea ngumu katika kushindana nae., spidi yake na msisimko ulikuwa umezidi ule wa jini Imrah.
Lakini hata hivyo Roma alishajua hana namna ya kumkimbia zaidi ya kupigana nae uso kwa uso
“Unakimbilia wapi?”Aliuliza kwa sauti kali ya kuumiza masikio kwa mtu wa kawaida.
“MODAO!!!”
Dakika ileile mkono wake ulianza kuzungukwa na mwanga wa njano na ndani ya dakika tu kulionekana kitu kama chungwa lililoiva likitokea mkononi mwake.
Roma alijikuta akishangaa kwani aliweza kugundua hio ilikuwa ni dhana ya kijini ambayo hakuwahi kuiona ambayo inaitwa Modao , Dhana ile ilikuwa ikitoa msisimko wa ajabu mno na kutengeneza kimbunga cha upepo mkali sana.
Ijapokuwa mabomu bado yalikuwa yakiripuka kuzunguka hoteli hio lakini eneo waliliiokuwa ni kama lilikuwa haliathiriki na milipuko hio.
“Kaeni ndani ya ngao , msisogee la sivyo hamtokuwa salama”Aliongea mara baada ya jengo hilo kuanza kutingishika likionekana linataka kudondoka muda wowote.
Familia hio ambayo ilikuwa na watu ambao wana uwezo mdogo wa nguvu za kijini walijikuta wakipatwa na ahueni mara baada ya kuona wana ulinzi wa kuwatoa ndani ya eneo hilo wakiwa salama.
Dakika ileile jini Iftiri , Imrah na Maridi waliingia ndani na kumzingira Roma huku kila mtu amelipukwa na nguvu isiokuwa ya kawaida ya kijini.
“Unajikuta jasiri kujitengenezea njia ya kutoroka si ndio, lakini nikwambie tu pengine umedharau sana uwezo wetu , leo ndio mwisho wako, hebu onja kwanza uzito wa thamani ya paundi elfu sitni”Aliongea yule mzee wa vazi jeusi,
Roma alijikuta akianza kulaani kimoyo moyo kwani aliona hao majjini hawakuwa na nia ya kumuacha salama kabisa na hawakuonyesha kujali usalama wa Maimuna tena , pengine tayari walikuwa washajua kwamba Roma asingeweza kumua kwani kifo chake ingemaanisha kifo cha Mzee Nguluma.
Wakati majini hao wakiwa na nia ya kumua, familia ya Mzee Sharif ilikuwa katika hali ya wasiwasi kwani waliogopa kifo cha Maimuna ingemaanisha kwamba wangepoteza mrithi aliekubaliwa na miungu wao.
Roma mara baada ya kuona nguvu ya ajabu inamsogelea alitaka kujikinga na mwili wa Maimuna lakini alihofia angeweza kufariki wakati bado alikuwa akimhitaji , aliona pengine akwepe pigo hilo lakini bado spidi yake ilikuwa ndogo na alijikuta akikosa chaguo na palepale alinyoosha mkono kupokea lile shambulizi.
“Modao!!!”
Aliongea kwa nguvu yule Mzee mwenye vazi jeusi na palepale ulitokea mlipuko wa aina yake ambao ulitengeneza mtetemeko wa ardhi ya aina yake.
Sehemu ambayo alikuwa amesimama Roma hakuonekana zaidi ya shimo kubwa la mita moja kwenda chini ndio na palepale ukuta wa hoteli hio uliokuwa umebakia ulidondoka.
Upande wa Roma bado alikuwa amesimama vilevile akiwa chini ya shimo na bado mkono wake ulikuwa ukishindana na nguvu ya kijini ilioruhusiwa kutoka katika Dhana ile ya Modao..
Yule mze mwenyewe alijikuta akiwa kwenye mshangao kwani hakuamini Roma hajathiriwa na pigo lale na aliishia kujiuliza inakuwaje akawa hajaathirika , mwili wake umetengnezwa na chuma.
Upande wa Roma alikuwa kwenye maumivu makali mno , ijapokuwa hajawahi kuyaogopa maumivu lakini alichokuwa akipitia hakikuwa cha kawaida , ni damu pekee ambazo zilikuwa zinaonekana kwenye mkono wake.
Shambulizi lote lile la Modao alikuwa amelizuia na mkono mmoja ndio maana aliweza kupitia maumivu makali kama hayo.
Yule Mzee wa kijiini aligundua maumivu yake , ijapokuwa alionekana kuweza kuhimili shambulio lake kwa mkono lakini bado aliona mikono yake ilikuwa ikimtetemeka na hili lilikuwa udhaifu ambayo ulimpa tumaini la usihindi.
“Sijajua umewezaje kuwa na mwili wa aina hio lakini hainizui kukuua na shambulizi langu la thamani ya paundi elfu sitini”Aliongea huku akitoa tabasamu la kejeli na palepale aliita moto wa rangi ya njano na kisha aliunganisha na kile kitenesi kama chungwa kwenye mikono yake na kufanya nguvu yake kuzidi kuwa kubwa maradufu.
Roma alijikuta sasa akihisi ile nguvu ya ile Dhana ikiongezeka uwezo wake kwa zaidi ya mara mia moja na alijihisi mifupa yake inataka kumvunija kutokana na presha aliokuwa akiihisia.
“Mlete Maimuna , huwezi kuvumilia shambulizi langu lingine”Aliongea
“Unapambana na Jinn Ghula ambaye uwezo wake ni mkubwa zaidi katika kuipita dhiki na kwenda mpaka levo ya kudhibiti maji kwa kuyabadilisha mara sita kimuundo . atakuua na shambulizi moja tu”Aliongea jini Imrah kwa tahadhari.
Roma alijikuta akishangazwa na kauli ile na kujiambia inakuwaje akawa na uwezo mkubwa namna hio , alijiambia kama angejua familia hio haikuwa ya kawaida basi asingechoma madhabahu yao.
Shauku yake ya kutaka kuijua hio familia chimbuko lake ilizidi kumjaa,
Roma alijiuliza au pengine kna kitu hakijui kuhusu majini ndio maana yupo kwenye hatari kama hio.
“Acha kuwa mbishi wewe binadamu , Master Ghula hio dhana yake ya Modao inao uwezo wa kukusanya nguvu za kiroho za kikosmiki na kuwa na uzito mkubwa ambao huwezi kuhimili”Aliogea kuzidi kumtia hofu Roma.
“Nitakuuliza mara ya mwisho , je upo tayari kurudisha hazina yetu?”Aliuliza Master Ghula.
Roma damu yake ilikuwa ikichemka mno na aliweza kuhisi namna ambavyo ile Dhana ilikuwa ikikusanya nvuvu ya kiroho ya giza kwa kasi mno.
“Niue tu kama unaweza” Aliongea Roma kijeuri kama kawaida yake na kumfanya Master Ghula macho yake kubadilika rangi palepale na kuwa na kutisha.
“Ukiburi ulioje kutoka kwa binadamu kama wewe , ni hasra kukuua lakini sina namna”Aliongea na palepale upepo mkali ulianza kuvuma na uchafu ulianza kujikusanya katika mikono yake kiajabu , kile kitenesi kama chungwa kilianza kutengeneza kimbunga cha ajabu na palepale alianza kuongea lugha ya kiajabu ambayo Roma alichoweza kusikia ni Mlima wa Tai, Viani Dao…
Ilikuwa ni nguvu ambayo haikuwa ya kawaida kwani katika lile eneo ambalo amesimama Roma kulitengeneza shimo kubwa na pengine kulikuwa na eneo la Ardhini ambalo lilikuwa limechimbwa kaitka hoteli hio kwani Roma alisukumwa kwenda chini mara baada ya mpasuko huku akisindikizwa na pigo takatifu la Modao na hakuonekana tena yeye pamoja na Maimuna na palepale yalifuatia maporomoko ya mawe pamoja na vifusi kufunika lile shimo kwa kasi na ndani ya dakika tu majabali na vifusi viliweza kufunika na kufanya eneo lote kujaa vumbi ambalo sio la kawaida.

SEHEMU YA 659.
Hoteli yote ya Wache ilikuwa imeharibika na kwa mtu mwenye uchungu wa mali pengine angekuwa kwenye masikitiko maiubwa kwani ilikuwa na mvuto usio wa kawaida ndani yake.
Wale wazee wa kijini wote watatu walionyesha kukunja ndita zao , ijapokuwa Roma alionekana kufunikwa na kifusi lakini bado waliweza kuhisi kabisa bado alikuwa hai na pia Maimuna alikuwa hai jambo ambalo lilimfanya ajawe na ahueni.
Kwao Maimuna alikuwa na thamani kubwa zaidi ya Mzee Nguluma na mke wake.
“Baba tayari ashafukiwa na kifusi chini ya Ardhi , Maimuna atakuwa sawa kweli?”Aliuliza baba yake Maimuna aliekuwa katika hali ya wasiwasi.
“Punguza presha , hebu waangalie wazee muonekano wao , inaonekana huyo mwanaharamu bado yupo hai na anamtumia Maimuna kama mateka na chochote kikimtokea Maimuna basi anajua fika familia ya Mzee Nguluma itakuwa halali yetu”Aliongea Mzee Sharif.
“Lakini anaweza kuwa hai lakini vipi kuhusu kupatwa na majeraha”
“Kaa kimya , wazee wanajua wanachokifanya”Aliongwa kwa kufoka.,
“Anatumia mbinu gani ya kimafunzo , mwili wake sio wa kibinadamu kabisa”Aliuliza jini Marid kwa mshangao.
Upande wa Mzee Ghula alionekana kushanga pia na kujiuliza kwa nguvu ya kijini aliotumia kwanini huyo mwanaharamu bado tu hajafa.
Mzee Ghula palepale hakutaka kuamini kama hawezi kumuua Roma kwani alianza kuchanel nguvu nyingine ya kijini ili kuweza kuisindilia kwenye lile shimo ambalo Roma alifunikwa lakini kabla hajamaliza anachotaka kufanya ghafla tu alianza kukumbwa na hali ya woga kwenye akili yake na kujikuta akigeuza macho yake na kuangalia angani.
Wale wenzake pia walikuwa washainusa hatari na walijikuta wakigeuza macho yao wote kwa pamoja kuangalia angani na walijikuta wakiwa hawamini wanachokiona angani.
“Nini kile?”Kila mtu alikuwa kwenye mshhitiko kuangalia kitu ambacho kilikuwa kikiwasogelea kwa kasi.
Kabla hata hawajaelewa waliweza kuona kitu kingine kiibuka kutoka baharini na kupaaa angani na kuanza kusafiri kuelekea upande wao.
“Oh ,. Hapana ni Makombora yale”
“Shit .. hili linawezekana vipi?”Baadhi ya mabodigadi waliokuwa nje ya eneo hilo walijikuta wakijawa na kiwewe.
Mzee Sharif mara baada ya kugundua kinacho wasogelea ni makombora ya kivita alijikuta akipagawa na kujiuliza vitu hivyo si vya kijeshi.
Halikuwa kombora moja , ilionekana yalikuwa yakirushwa kutoka chini ya baharii kuja eneo walipo kutokana na trajectori zao na ilikuwa ni swala kufumba na kufumba yote yashakaribia eneo walipo.
Ilikuwa ni maamuzi ya haraka sana walioyafanya kwani palepale walitengeneza ngao ya kijini na kuwafunika watu wote na wao pia kwa kuunganisha nguvu na makombora yale yalitua yote kwenye ngao na kutoa mlipuko wa aina yake na kuanza kugeuza kile kijimlima kuwa tambarare,
Naibu waziri Salihi , Asha na wengine wote walikuwa wakihisi ngoma za masikio yao zinawapasuka kutokana mlipuko huo huku kila mtu akilaani ni balaa gani hilo wamejitengenezea.
Wale wazee licha ya kwamba walifanikiwa kutengeneza ile ngao lakini hawakuacha kutema damu nyingi chini huku nguvu zikiwa zikiwaishia.
Ilikuwa ni kama vile kuna kambi ya kijeshi ambayo ilikuwa ikiangamizwa moja kwa moja na adui katika hilo eneo kwani yalikuwa yakishuka mfululizo tena kwa kasi bila ya kukosa shabaha.
Baada ya yote kutulia hatimae walianza kupumua lakini muda huo hawakupewa kwani kijimlima chote kilianza kuporomoka kutoka juu kwenda chini baharini na wale majini wote hawakuwa na muda wa kupoteza hata wa kujiuliza Roma na Maimuna wapo wapi kwani waliweza kuwachukua wale wasiokuwa na nguvu za kijini na kuwatorosha kwenye eneo hilo kwa haraka sana.
“Pumbavu zako Roma , nitahakikisha nakuua kwa namna yoyote ile”Aliongea Mzee Ghula kwa hasira akiwa haamini kama amezidiwa ujanja na kuishia kukimbia na Mzee Sharif, alitaka kutumia uwezo wake wa kijini kumchunguza Roma alipo lakini hali ilikuwa tete.
“Huyu mwanaharamu yupo wapi , mbona kapotea siwezi kupata msisimko wake”Aliongea Mzee Ghula kwa hasira mara baada ya kutua eneo la mbali.
“Master si atakuwa na yeye amepasuka pasuka vipande na Maimuna?”Aliuliza Marid.
Mzee Sharif mara baada ya kusikia jina la mjukuu wake likitajwa alijikuta akipatwa na huzuni kubwa na kujiambia pengine lilikuwa kosa kumchokoza Roma.
“Hapana , hawezi kufa yule , inaonekana huu ni mpango aliotuandalia hivyo kuna njia ya kujiokoa ameitegneneza tokea mwanzo”Aliognea
Mzee Sharif hakujua namna ya kuongea kwa wakati huo kwani alikuwa amechafuka na vumbi hatamaniki , zile sura za majigambo zote kwisha na kilichokuwa kimebakia ni hasara nyingine ambayo wameipata siku hio,walikuwa wakijiamini wanakwenda kummaliza Roma lakini ni kama vile wamejipalia makaa
Lakini bado mzee huyo alikuwa akijiuliza mabomu hayo nani ambaye ameyarusha , aliamini kabisa serikali ya Tanzania haiwezi kwenda mbali na kufanya kitu cha namna hio kwani ungekuwa ni ukichaa.
Kama sio serikali ya Tanzania je katoa wapi makombora ya kijeshi , vipi amewezaje kufukia mabomu ndani ya jengo lao la hoteli bila wao wenyewe kujua.
Alijiuliza hata kama serikali ya Tanzania haikuhusika jeshi la Tanzania linafanya kazi gani kulinda mipaka ya bahari.
Aliishia kukumbwa na fedheha kubwa na kujiambia habari hio ikifikia watu itakuwa ni dharau kubwa wamefanyiwa.
Wakati wote wa Kigamboni waliweza kusikia milipuko hio na wengine walikuwa washaanza kukimbia na kudhania taifa linavamiwa.
Ilikuwa ni kwa haraka sana baada ya tukio hilo wanajeshi ndio sasa wanaamka huku simu nyingi na maelekezo yakitolewa kutoka mamlaka ya juu ili kujua nini kinatokea.
Ni ndani ya nusu saa tu taarifa ziliweza kufikia jeshi la Tanzania kuhusu Kichaa afahamikae kwa jina la Roma Ramoni alikuwa akiisambaratisha familia ya Sharif kwa mabomu na makombora na taarifa hio ilipelekea kila mtu kupigwa na mshutuko , ijapokuwa ni habari zilizoenea kwa baadhi ya vongozi lakini zilikuwa za kushitusha mno kwani ni mara ya kwanza raifa kupitia milipuko ya aina hio.
Sasa mjuda ambao Suzzane na Nadia alfonso wanafika ndani ya nyumba ya mapumziko ya Raisi Senga ndio wakati ambao anapokea taarifa ya makombora kurushwa ndani ya kigamboni katika eneo linalomilikiwa na Mzee Sharif huku jeshi likishindwa kujua swala hilo limetokea vipi na makombora hayo yametokea wapi.
Kuna wengine walianza kufananisha milipuko hio na mabomu ya mbagara yaliotokea miaka kadhaa iliopita.
*****
Upande mwingine giza likiwa limetanda juu ya maji ya bahari huku upepo ukivuma kwa kasi kiasi cha kusababisha mawimbi makubwa.
Kilomita kumi katikati ya bahari lilionekana dude la chuma kama lisamaki likubwa la baharinni likiambaa ambaa kwa kasi likielekea katikati ya bahari huku likitoa mkonga wake kwa juu.
Ilikuwa ni manuari ya kijeshi yenye urefu zaidi ya mita moja na kadri ilivyokuwa ikijitokeza juu chuma chake kilichopakwa rangi nyeusi kilionekana vizuri tena bila kupiga sauti yoyote ile.
Ndani ya manuari hio katika eneo la Deck kulikuwa na mwanamke mjapani aliekuwa mrembo akiwa amevalia mavazi ya kawaida , huku nywele zake ndefu akiwa amezifunga kuzirudisha nyuma.
Pembeni yake alikuwa ni mwanaume wa kizungu ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kijeshi ya kiwana majji.
Kombati zake za kijeshi hazikuwa na isignia yoyote ile kuashiria ni jeshi la wapi zaidi ya kuwa na chata kubwa la fuvu.
Mwanaume yule alionekana kuwa katika tabasamu pana huku akimwandalia mwanamke wa kijapani aliekuwa mbele yake na aliweza kuona wasiwasi wake.
Nyuma yake pia kulikuwa na wanajeshi waliokuwa na sura za kikauzu wengine wakiwa ni Wafrika , wengine ni Warabu na wengine wakiwa ni Wazungu wakiwa wamesimama wima kikakamavu.
“Madam Tanya huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani misheni imekamilika kwa asilimia mia moja , kwa mahesabu tuliopiga itachukua zaidi ya nusu saa mpaka jeshi la maji la Tanzania kutushitukia na mpaka wakati huo tutakua kwenye maji ya kimataifa”Aliongea kwa kingereza.
“Colonel Brewester, I don’t care about the Navy , all I care is about His Majesty Pluto’s Safety”Aliongea na kumfanya Kanali Brewester kutoa tabasamu ambalo halikuwa na hofu kabisa alikuwa katika hali ya mchecheto kwani misheni iliomfikisha hapo alikuwa ameikamilisha kikamilifu bila hata jeshi la Tanzania kuwashitukia na muda huo wanaenda kujiegesha kusubiri maelekezo mengine zaidi.
Haya njooni watsapp mmalizie 0687151346
Shukhran mkuu mzigo umetufikia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom