Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI SINGANOJR


Mono no aware.

SEHEMU YA 641.
Muda wa jioni Roma alikuwa tayari ashafannikiwa kumtoa Najma Gerezani ambako alikuwa amezuiliwa, ijapokuwa swala hilo alikuwa amelimaliza kwa upande wake hakutaka liishe hivyo hivyo kwani ulikuwa ni uchokozi wa waziwazi.
Roma hakutaka kujali kuhusu mwanamke aliemfungia Najma alikuwa akitoka katika ukoo gani
na ana nguvu kiasi gani lakini alichokuwa akitaka ni aidha Najma kuombwa msamaha na mwanamke huyo afahamikae kwa jina la Asha pamoja na mtoto wake Naibu waziri Salihi kwa kupiga magoti mbele yake na kusujudu mara tatu au alipize kisasi kwa kuunguza makazi yao kama hatatotii sharti lake.
Roma alichagua kuunguza makazi hayo kutokana na taarifa za siri alizosikia kuhusiana na familia hio.
Kazi ya kupeleka maagizo hayo kwenda kwa mwanamama huyo pamoja na mtoto wake alimpatia Jamali ambaye alifika nae katika Gereza la Ukonga na kumtoa Najma.
Upande wa Jamali hakupinga kupeleka maagizo hayo kwani mpaka wakati huo alikuwa alishamjua Roma ni nani na nguvu yake ndani ya taifa la Tanzania.
Kuhusu Najma aliamua kumnunulia gari nyingine aina ya Mercedenz Benz AMG C 43 coupe , Roma aliamua kuchukua gari hio kwani ndio pekee yenye muonekano mzuri iliokuwa imebakia katika ShowRoom ya magari ya Fredi na alimpa maagizo kumpelekea Najma siku itakayofuata akishamaliza kuisajili, ilikuwa ni gari ambayo haikuwa na gharama kubwa kuliko ile ya mwanzo.
Najma ijapokuwa gari ilioharibika aliipenda kuliko hio lakini alifurahi kwamba Roma alikuwa amemnunulia nyingine ambayo pia muonekano wake ulikuwa mzuri japo hakupenda rangi yake kwani ilikuwa ni nyeusi na yeye alipendelea nyeupe.
Kutokana na wasiwasi wa familia ya Najma Roma aliamua kumpeleka mpaka nyumbani kwao na kuwatoa wasiwasi kwamba swala kama hilo haliwezi kujirudia tena na kisha aliaga na kuondoka kurudi nyumbani kwani muda ulikuwa umeenda.
Roma mara baada ya kufika Ununio hakutaka kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Nasra bali alitaka kuonana na Edna kwanza.
Roma alishajua mpaka hatua ambayo wamefikia kwa wakati huo ingekuwa ngumu kumpigia simu na akapokea hivyo aliamini njia pekee ni kwenda moja kwa moja nyumbani na kugonga mlango kuonana nae ana kwa ana..
Upande wa Bi Wema alikuwa na mawazo mno kwa kile kilichotokea , lakini kwa wakati mmoja aliona pengine jambo hilo lina faida kwa Rufi ambaye ni binti yake kwani alikuwa tayari sehemu ya wanawake wa Roma hivyo aliona kama Edna angepewa talaka basi pengine Rufi angechukua nafasi yake , lakini kwa wakati mmoja aliona hata kama jambo hilo likitokea yeye angejigawa vipi.
Alikuwa amemlea Edna tokea mtoto na alikuwa akimchukulia kama binti yake pia na hakutaka kukubali ukweli wa Roma na Edna kuachana.
Bi Wema ambaye alikuwa bize na usafi wa nyumba aliweza kumuona Roma ambaye alikuwa akiingia na alijikuta akishikwa na simanzi na kwenda kumpokea.
“Mr Roma imekuwaje wewe na Edna jamanii , nimesikia kutoka kwake Lanlan amezaliwa na mwanamke wako hapo zamani , ni kweli?”Aliuliza Bi Wema na kumfanya Roma kushangaa kwani hakutegemea kama Edna angemhadithia Bi Wema kila kitu.
“Ndio BiWema , samahani kwa kukufanya uwe na wasiwasi , Edna yupo nyumbani?”
“Ameondoka leo asubuhi asubuhi kuelekea Mwanza na ameambatana na wanahisa baadhi kwa ajili ya kukagua Ardhi ambayo anapanga kuwekeza, sina uhakika kama atarudi siku gani”Aliongea Bi
Wema.
Roma alijikuta akivuta pumzi , hakuamini Edna angefanya hivyo na kutompa nafasi nyingine ya kumuona maana kusafiri kwa haraka hivyo ni kama alikuwa akimkwepa.
Ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kumtafuta sehemu alipo kama akitaka , lakini hakutaka kulaziimisha.
Aliona isingekuwa sawa kumuomba msamaha mbele za watu , labda tu kama atakuwa ni kichaa.
Hakutaka kuonekana kama alikuwa akimuogopa sana au alikuwa akimtegemea hivyo hakutaka kujishusha , alijua ana makosa lakini kama mwanaume alikuwa na mpaka ambao hakutaka kuuvuka kwa ajili ya mwanamke tu.
“Mr Roma unaonaje ukienda kumtafuta na mkaongea na kuyamaliza , ninavyojua anampenda sana Lanlan na hili ni swala ambalo haliwezi kuwa sababu ya
kuachana kwenu , ndoa haivunjiki kirahisi namna hii”
“Bi Wema hili ni swala ambalo halijasababishwa na sababu moja au mbili , ni swala la kimtazamo na kikanuni , na kama halikubaliki basi kila kitu hakina maana”Aliongea Roma na kumfanya Bi Wema kukosa cha kuongea.
******
Ni ndani ya mkoa wa Kilimanjaro , pembezoni mwa mto uliozungukwa na msitu mkubwa katika eneo la tambarare ambalo limezungukwa na mlima upande wa kusini , sasa ndani ya eneo linapatikana jumba kubwa ambalo limezungukwa na ukuta mrefu kwenda juu.
Ni ukuta ambao ni ngumu sana kuona
kinachoendelea ndani kwa raia ambaye yupo nje ya ukuta huo.
Eneo hili lilikuwa la kifahari mno na mahadhi yake yalikuwa yamejengwa kwa mtindo wa tamaduni za kiarabu.
Ni eneo lenye ukubwa wa zaidi ya Ekari thelathini ambalo linamilikiwa na familia moja.
Kutoka mjini kuja katika eneo hilo kulikuwa na barabara nzuri ya lami ambayo imejengwa kwa viwango vya juu mno pengine kuliko barabara zote ndani ya mkoa wote wa Kilimanjaro.
Kwa wenyeweji wa mkoa huo wanasema kwamba
ujenzi wake ulianza miaka mingi iliopita baada ya serikali kuuza eneo hilo kwa mwarabu mmoja ambae alikuwa akijitukuza ni mtanzania kwa kujipatia jina la Kitanzania lakini ukweli hakuwa mtanzania.
Kwa mtu ambaye hana uelewa akifika ndani ya hili eneo pengine angesema ni hoteli , lakini ukweli sio hoteli bali ni eneo maalumu ambalo limejengwa kama makazi ya kimila ya Familia moja.
Kulikuwa na majengo matatu ya Ghorofa nne kwenda juu ambao ubunifu wa vyumba vyake kwa ndani vilikuwa vimejaa ufahari wa aina yake.
Mazingira yalikuwa yakivutia sana ndani ya eneo hili na ulinzi wake ulikuwa ni wa masaa ishirini na nne , kulikuwa na ulinzi mkali uliombatana na teknolojjia.
Inasemekana kwamba wamiliki wa eneo hilo hukusanyika kwa mwaka mara mbili , yaani katikati ya mwaka na mwisho wa mwaka lakini hata hivyo taarifa hizo hazikuwa na uthibitisho wowote kwani kilichokuwa kikiendelea ndani ya jengo hilo ilikuwa siri kwa wanafamilia na wahusika.
Sasa hili eneo ndio ambalo linamilikiwa na familia ya Naibu waziri Salihi.
Ni wakati wa usiku wa saa mbili ndani ya jengo hili katika eneo la ukumbi wa chakula walionekana watu wengi wanaume kwa wanawake waliokuwa wameketi kwenye meza ndefu ambayo ilikuwa imejaa aina mbalimbali ya vyakula na vinywaji ambavyo havina pombe ndani yake..
Kati ya watu waliokuwepo ndani ya hilo eneo alikuwa ni mke wa waziri wa mazingira Bi Asha aliekuwa amevalia mavazi ya heshima ya tamaduni za kiarabu.
Pembeni yake Asha ameketi mume wake aliefahamika kwa jina la Nguzo Ibuyawanga au unaweza kumuita Nguzo Salim Sharif.
Familia hio mwasisi wake alikuwa akiitwa Sharifu lakini mara baada ya kukaa sana nchini Tanzania alibadilisha uraia wake na kuitwa jina la tamaduni za kitanzania ambalo ni Ibuyawanga.
Asilimia kubwa za watu waliokuwa ndani ya eneo hilo walikuwa ni waarabu kamili na machotara yaani waliochanganya rangi nyeusi na nyeupe.
Kwa jinsi ambavyo walikuwa wengi ungedhania kulikuwa na tafrija ambayo ilikuwa ikifanyika lakini ukweli ni kwamba haikuwa sherehe bali ibada za kimila ambazo zilikuwa zikihusisha wana ukoo wote.
Stori nyingi ambazo zilikuwa zikiongelewa hapo ni maswala ya kibiashara tu na mali ambazo kila mmoja alikuwa akimiliki na kuongoza lakini pia koneksheni mpya za kibiashara amazo wameweza kupata.
Ukiachana maswala ya kibiashara lakini pia maswala ya siasa yalikuwa yakiongelewa pia .
Wakati zogo lililojazwa na vicheko vya pesa likiendelea ndani ya eneo hilo simu ya Asha mke wa waziri wa mazingira ilianza kuita kwenye mkoba wake uliokuwa pembeni kiasi cha kumfanya mume wake amwangalie na Asha palepale aliingiza mkono ndani ya mkoba wake na kisha akaiweka Silence lakini mara baada ya kuita na kukata iliita tena kwa mara nyingine na mume wake alimpa ishara ya kutoka nje kuipokea na Bi Asha alitingisha kichwa na kisha alichukua simu na kutoka nje.
“Madam Asha , kwa jina naitwa Jamali Kidula mkuu msaidizi wa kituo cha polisi kutoka Oysterbay Dar es salaam , nataka kukupatia taarifa zinazohusiana na Najma”
“Mkuu msaidizi ?, Afande Mkanye kwanini hajanitafuta yeye mwenyewe na umenitafuta wewe , vipi kuhusu huyo m*laya hawajamvunja hata mguu huko gerezani kama nilivyoagiza?”
“Afande Mkanye anaumwa na amenikabidhi mimi hili swala… Madam nadhani unapaswa kujiandaa kiakili juu ya hili swala kwani lishakuwa kubwa , pengine unapaswa kumwambia mume wako , Waziri Nguzo au yoyote ndani ya familia yako”Aliongea Jamali ambaye alikuwa anaogopa kuongea kwenye simu kutokana na sauti yake kujaa kitetemeshi.
“”Unaongea kichekesho gani , kuna haja gani ya mimi kutoa taarifa ndani ya familia yangu , unataka niwaambie namna ambavyo nimeamua kudili na huyo m*laya, Afande Jamali unataka kukosa nafasi yako hapo polisi?”
“Hapana Madam , ninachokuambia ni kwamba
Najma amechukuliwa na boyfriend wake Mr Roma
Ramoni..”Aliongea Afande Jamali akimwelezea Asha namna ambavyo Roma alikuja kumtoa kwa nguvu Najma Gerezani.
“Nini! Kumbe huyo m*laya ni mpenzi wa huyo mwendawazimu kutoka familia ya Kweka pia”Aliongea huku sura yake ya maringo na kiburi ikimpotea palepale.
Hakuamini kama Najma mwanamke mpole na wa kawaida ambaye kwa utafiti wake alikuwa masikini tu alikuwa mpenzi wa Roma Ramoni.
Ukubwa wa familia yake ulimfanya kumjua Roma tokea muda mrefu kama mtoto wa Raisi Senga lakini sio hivyo tu alikuwa akimjua Roma kwa ukatili wake kwa kile alichokifanya Iringa, taarifa zake alikuwa nazo licha ya kwamba jeshi lililifanya kuwa za siri.
“Kama huyo Roma ashamchukua inamaanisha kwamba hakuna kibaya kilichomkuta huyo m*laya wake , hivyo hili swala limeisha”Aliongea awamu hii akijitahidi kuwa mpole.
Kwa sauti yake ilivyosikika pengine Afande Jamali upande wa pili alikuwa akitabasamu kwa siri maana ilikuwa imejaa uoga ndani yake.
“Madam , Mr Roma hana mpango wa kuacha hili swala lipite hivi hivi ,, isipokuwa tu, kama wewe na Naibu waziri mtafika nyumbani kwa Nasra na kupiga magoti na kumsujudia mara tatu kisha kuomba msamaha au vinginevyo..”Aliongea na kumfanya Mwanamke huyo macho kuwaka.
“Anapanga kutufanya nini?”
“Anasema atageuza makazi ya familia yenu kuwa majivu..”
“Huo ujasiri anautoa wapi ,, umemuambia ukubwa wa familia yetu ndani ya Tanzania?”
“Nimemuambia lakini anaonekana sio mwenye kujali kuhusu hilo, Madam nadhani amekasirika sana , kwanini hili swala usilimalize kwa nia njema , mimi nitakuwa mtu kati kuhakikisha linaisha kwa amani na pande zote mbili kuridhika , nadhani itakuwa vyema kama utafika Dar na kukaa chini na kuongea na mr Roa ili liishe kwa amani”
“Unafikiri inawezekana kirahisi hivyo mimi Farhat kufuata hayo masharti yake ya kipuuzi ,mimi simuogopi na asinitishe, wewe subiri mpaka wazee ndani ya familia yake wamwambie ukubwa wetu tuone kama atathubutu…Afande Jamali hebu aongea na huyo Roma kama ni hela ya fidia mimi nitampatia ili swala liishe lakini swala la kumpigia magoti m*laya wake na kumsujudia asahau”Aliongea na kisha palepale akakata simu na kuvuta mdomo kwa jeuri.
Ijapokuwa Asha hakuwa na uwezo wa kushindana na Roma ana kwa ana lakini alijua watu waliokuwa ndani ya familia yake walikuwa na uwezo huo hivyo hakuogopa, Aliamini kama Roma angemfanya chochote kibaya familia yake lazima ingemsaidia.
Ukweli ni kwamba alichokijua ni Roma kuwa mtoto wa raisi wa Tanzania tu wa nje ya ndoa lakini hakumjua Roma upande wake mwigine.
Afande Jamali mara baada ya kumaliza kuongea na Asha simu yake ilianza kuita tena na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Omari na alipokea haraka haraka na kuweka simu sikioni
“Kaimu kuna maagizo mengine unataka kunipatia?”
“Wakuu wa usalama wamesema swala hili lisiingiliwe na polisi kwa kupendelea upande wowote, kama chochote kitatokea wasiliana na jeshi la polisi mkoani Kilimajaro kulinda raia wasiathirike , hakikisha swala hili halihatarishi usalama wa raia na mali zao lakini pia lisiibue taharuki”
“Kaimu unamaanisha kwamba familia hii kuna ambacho kitawatokea?,Kama ni hivyo si itakuwa hatari?”
“Acha kuongea upuuzi , kinachofanyika ni kuangalia kinachoendelea na jeshi la polisi hakikisha halihusiki”Aliongea Omari na kisha kakata simu.
Jasho lilianza kumtoka kwenye paji la uso wake na palepale alitafuta namba ya Roma na kumpigia kumpa maelekezo.
Wakati Roma anamtoa Najma kituo cha polisi alikuwa ameambatana na Afande Jamaali na ndio aliempa maagizo ya kutoa tarifa kwenda kwa Mke wa familia ya Nguzo kuhakikisha mwanamke anaeitwa Farha mama mzazi wa naibu waziri Salihi anafika nyumbani kwa Najma na kuomba msamaha kwa magoti pamoja na kumsujudia Najma.
Upande wa nyumbani kwa Roma usiku aliweza kumuita Dorisi , Rufi na Bi Wema kujumuika sehemu moja kwa ajili ya chakula katika nyumba ya Nasra.
Baada ya chakula Rufi alianza kucheza gemu na
Lanlan huku Bi Wema na Qiang walitaka kumsaidia Nasra kuosha vyombo lakini alikataa na kusema ataviosha mwenyewe.
Bi Wema alishangazwa na uchakalikaji wa Nasra katika kufanya kazi za nyumbani , kwani alikuwa ni yeye aliepika chakula kitamu na baada ya chakula alitaka kuosha vyombo mwenyewe ilimfanya Bi Wema kumkubali Nasra na kujiambia alikuwa mwepesi mno , pengine ndio mwanamke ambaye amefuzu katika ufanyaji wa kazi za nyumbani kuliko wenzake wote.
Ilikuwa kweli Nasra pangine ni kutokana na aina ya maisha aliokulia ndio maana alikuwa mwepesi kwani ukiachana na maswala ya upishi alikuwa vizuri sana likija swala la kazi za nyumbani alikuwa ni ‘Wife material’ na nyumba yake ilikuwa safi mno na vitu vimejipanga licha ya kwamba hakuwa na mfanyakazi wa ndani wa kumsaidia.
Bi Wema aliona pengine ndio maana Edna na yeye alikuwa akihimiza kujua kupika kutokana na ubora wa Nasra.
Upande wa Roma wakati akiwa bize kuongea na Dorisi simu yake ilianza kuita na alipoangalia jina la mpigaji alikuwa ni Afade Jamali na palepale alipokea.
“Mr Roma , Bi Asha kasema yupo tayari kukulipa kiasi chochote cha pesa kama fidia ya usumbufu wewe na Najma lakini kuhusu swala la kuwapigia magoti haliwezekani””
“Nadhani ananiona natania nilivyosema nitaigeuza makazi yao kuwa majivu?”Aliongea Roma huku akikunja sura.
“Sijajua Mr Roma , lakini mimi kama mwanausalama wa taifa hili nataka jambo hili liishe kwa amani pia , ijapokuwa najua sina uwezo wa kukuzuia Mr Roma kwenda mbali juu ya hili lakini naomba lisije kuibua taharuki na kujeruhi watu wasio na hatia”
“Okey umeeleweka , ninakata simu sasa kwani naona hakuna kingine cha kunielezea”Aliongea Roma na kisha palepale alikata simu na muda huo Nasra na yeye alikuwa ashafika na kukaa kwenye Sofa akiwa na simu yake.
“Babe kuna kilichotokea leo?”Aliuliza Dorisi na
Roma alitingisha kichwa kukubali huku akianza kuelezea kile kilichomtokea Najma na Nasra alijikuta akishangazwa na jambo hilo na kumhuzunikia rafiki yake Najma.
“Honey , kwahio unapanga kwenda kuunguza makazi yao , unataka nikusaidie?”Aliuliza Rufi.
“Rufi acha utani , huwezi kuvuna nishati za mbingu na ardhi na hataka useme ukachome moto halitowezekana kirahisi?”
“Sijamaanisha kukusaidia kuchoma moto , namaanisha hujui eneo lenyewe lilipo na ramani yake iko vipi, ninaweza kulitafuta kwa njia ki udukuzi na kuona namna lilivyokaa”Aliongea Rufi.
Roma alifurahi na kuona wazo la Rufi ni zuri kwani licha ya Roma kuambiwa kuhusu familia hio kujenga makazi ya kifahari ndani ya Tanzania mkoani Kilimanjaro hakujua uelekeo wake.







SEHEMU YA 642.
Haikueleweka nini kimetokea usiku lakini Roma alilala na wanawake watatu kitanda kimoja usiku kucha tena bila ya wasiwasi wala hatia.
Ilikuwa ngumu kuamini kama Nasra na Dorisi wanawake wanaoheshimika kazini wangeweza kuunganishwa wote kwa pamoja juu ya kitanda kimoja.
Roma mara baada ya kupata kifungua kinywa alimchukua Rufi na kisha wakaelekea Uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea Clark.
Roma alikuwa ashamweleza Rufi juu ya shida yake na mpango wa Clark kuja Dar kwa ajili ya kumuuliza maswali ambayo yangemsaidia kutibu tatizo lake.
Roma alipanga kumruhusu Clark kuishi nyumbani kwa Rufi kwa siku kadhaa , haikuwa kwa malengo mabaya , isitoshe hakutaka kumfanya chochote Clark kwa wakati huo ili aweze kupanda levo haraka katika mafunzo ya mbingu na Ardhi.
Rufi ndio aliekuwa akiendesha baada ya kumkatalia Roma kuendesha gari yake.
Bi Wema alikuwa na hela sio mchezo kwani alifanikisha kumuagizia Rufi gari kutoka Dubai aina ya BMW X6 xDrive 40i ya mwaka 2022 ya rangi ya bluu.
Ni gari ambazo zilikuwa na watu wachache sana ndani ya Tanzania na ni ngumu sana kuzikutaShowroom kutokana na ughali wake na mara nyingi ziliagizwa kwa oda maalumu.
Ilikuwa ngumu kwa mtu wa nje kutokuamini kama Rufi mama yake ni Kijakazi wa familia ya Edna maana hata hao watoto wa matajiri wakubwa nchini ni wachache waliokuwa wakitembelea ghali za bei hio.
Kabla Roma hajaanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege hakuacha kwenda nyumbani kwake kumwangalia Edna kama karudi lakini aliishia kujikatia tamaa mara baada ya kukuta nyumba ipo kimya.
Hata Bi Wema mwenyewe hakujua ni siku ngapi ambazo angekaa nje ya mkoa wa Dar es salaam.
Baada ya Roma kuona hana cha kufanya zaidi ya kusubiri alirudi na kisha akaingia garini na kuianza safari.
Roma akiwa safarini alikuwa akifikiria namna ya kutimiza kisasi chake zidi ya familia ya mwanamke afahamikae kwa jina la Asha mama wa naibu waziri , baada ya kuwaza sana alifanikiwa kupata wazo ambalo lilimfanya kutoa tabasamu la kifedhuli na kisha palepale alipekua majina yaliokuwa kwenye simu yake na akapiga namba alioisevu kwa jina la Samweli Nguluma.
*******
Upande mwingine katika makao makuu ya nchi mkoani Dodoma alionekana Raisi Senga kama kawaida akiendelea na majukumu yake ya kuwatumikia watanzania.
Mara nyingi Raisi Senga aliipenda Ikulu ya Dar es salaam na kuna muda alikuwa hata akimlaani aliemaliza ujenzi wa Ikulu ya Chamwino kwani kwake ilikuwa ikipa usumbufu wa kufanya safari za mara kwa mara kwa kuhama Dar na kwenda.
Lakini kutokana na kuheshimu juhudi za serikali kujenga ikulu kubwa mkoani Dodoma alikuwa akihakikisha matukio yote makubwa ya kitaifa kama kuapisha wateule alikuwa akiyafanyia Dodoma.
Siku hii akiwa ofisini kwake kama kawaida aliingia Kabwe msaidizi wake wa karibu ambaye mara nyingi alikuwa akimwamini sana.
“Kabwe ukiwekaga huo muoneknao lazima kuna taarifa nzuri unayotaka kuniambia , hebu weka wazi”Aliongea Raisi Senga huku akiweka tabasamu la ukarimu.
Ukweli ni kwamba tokea kifo cha raisi Kigombola lakini pia kupunguzwa kwa nguvu ya familia ya Mzee Longoli na wafuasi wake alikuwa na amani sana , alikuwa akihisi kama nchi yote sasa ipo mikononi mwake , lakini licha ya hivyo kuna jambo moja tu ambalo bado halikumpa ile raha ya madaraka aliokuwa akiitaka na kuishia kuwa na hatia.
Kabwe mara baada ya mheshimiwa kuongea na yeye alijikuta akitoa tabasamu licha ya kujitahidi kujizuia.
“Mheshimiwa siamini kama mpango ungeenda kama ulivyosema?”
“Unamaanisha mpango gani , nina mipango mingi Kabwe”Aliongea.
“Nazungumzia swala la kilimanjaro mheshimiwa linaenda kama ulivyopanga”
Kabwe mara baada ya kuongea kauli hio macho ya mheshimiwa Senga yalichanua na kuonyesha shauku yake waziwazi.
“Hii ni ripoti mheshimiwa iliotoka kwa Afande Jamali”Aliongea Kabwe na kumpatia mheshimiwa Tablet(Kishikwambi) ya kampuni ya Apple.
Raisi Senga alianza kusoma kwa umakini sana taarifa ile na kadri alivyokuwa akiendelea alijikuta uso wake ukipambwa na tabasamu.
“Haha.. hahaha..”
Mheshimiwa Senga alijikuta akitoa kicheko kikubwa sana huku akionekana kufurahi kiasi cha kumpelekea kusimama.
“Mheshimiwa hongera sana , kama ikiendelea hivi ni hakika kila kitu kitaendelea kama ulivyopanga” “Kabwe nadhani ni mapema sana kunipa hongera , kwasasa itabidi tuone kinachoendelea”Aliongea Raisi Jeremy huku akionekana kuwaza jambo.
Taarifa ambayo alikuwa akisoma ilikuwa ikihusiana na Najma kuwekwa Gerezani na Mke wa waziri wa Mazingira lakini haikuishia hapo ilienda mpaka namna ambavyo Roma alienda kumtoa Najma kituo cha polisi na kisha kutoa masharti kwa Bi Asha kwenda kumuomba msamaha Najma na majibu ambayo Asha alirudisha.
“Mheshimiwa mpaka sasa sijaelewa sehemu moja , najua familia ya Mzee Sharifu ina nguvu sana ambayo haionekani , lakini pia kwa miaka mingi wamekuwa wakifanya mambo yao bila ya kuingilia serikali, je kuna sababu zozote kuwatengenezea ugomvi na Mr Roma ukizingatia walikuwa na msaada mkubwa kwako wakati wa kampeni?”Aliuliza Kabwe na kumfanya Raisi Senga kumwangalia Kabwe kwa macho yenye wasiwasi na kisha palepale akakaa chini.
“Kabwe ni kweli familia ya Mzee Ibuyawanga ina nguvu sana ndani ya taifa lakini ushawahi kujiuliza kwanini yule mzee alikimbilia nchini Tanzania na kuanzisha makazi yake hapa mpaka kuutaka uraia kwa nguvu zote , lakini sio hivyo tu akataka serikali kumpatia ulinzi?”Aliongea na kumfanya Kabwe kidogo kuonyesha mshangao , ukweli ni kwamba hakuwa na taarifa hizo pengine ndio mara ya kwanza anajiuliza swali hilo.
“Usingeweza kuyajua haya Kabwe kwasababu umeingia katika mfumo wa serikali juzi juzi , kuna usiri mkubwa juu ya familia ya Mzee Ibuyawanga ambayo siwezi kukuambia kwani ni siri ya kiserikali ambayo faili lake lilitekelezwa katika awamu ya pili , ila unachopaswa kujua kwasasa ni kwamba yule mzee ni msaliti wa ndugu zake na imani yake kwa kutumiwa na mataifa ya Magharibi”Aliongea Raisi Senga na taarifa hio ilionekana kumshangaza Sana Kabwe kwani ilikuwa ni mpya kwake .
“Mheshimiwa sijawahi kusikia hili , ijapokuwa ni kweli nishawahi kusikia kuna sababu kubwa ya Mzee Sharifu kuhamishia makazi yake Tanzania”
“Kwa usalama wako kwasasa hupaswi kujua mengi , ila mpango huu ukifanikiwa faida haitokuwa kwangu tu lakini pia itakuwa kwa Taifa lote la Tanzania”Aliongea huku akiongeza usiriasi kwenye maneno yake na Kabwe alitingisha kichwa kumwelewa.
“Kwasasa hakikisha unaanza mchakato wa kumuamsha shushu wetu ndani ya familia ya Mzee Ibuyawanga ili tupate kujua kinachoendelea , kwa ninamvyomjua Roma lazima atafanya kila kitu kama ninavyomtegemea”Aliongea na Kabwe alitingisha kichwa kukubali maagizo.
“Afande Jamali pia katoa taarifa ya wakuu wa usalama wapo neutral kwenye swala hili mheshimiwa na anaomba maoni yako”
“Kama wakuu wametoa msimamo wao sina haja ya kuwaingilia, Jenerali Tozo ana mawazo sawa na yangu hivyo sidhani kama litakuwa tatizo”Aliongea na kumfanya Kabwe kutingisha kichwa.
“Vipi kuhusu taarifa nyingine inayoendelea kuhusu Roma?”
“Taarifa ya leo alionekana uwanja wa ndege akimpokea Princes Clark kutoka Uingereza akitokea Iringa , hakuna taarifa nyingine kubwa”Aliongea na Raisi Senga alitngisha kichwa kuonekana kumwelewa.
“Endelea kuongeza umakini ili tujue kila anachokifanya , ninachotaka ni mpango wangu huu
kufanikiwa, ongeza umakini wako na nakukumbusha kwamba chochote kitakachotokea swala hili halihusiani kwa vyovyote vile na serikali yangu , hakikisha unashirikiana na Jamali kwa ukaribu”
“Sawa mheshimiwa”Aliongea Kabwe na Raisi Senga alimwashiria kutoka.
Baada ya Kabwe kutoka Raisi Senga aliegamia kwenye kiti chake huku akionyesha kuwaza jambo.
Ukweli ni kwamba Raisi Senga alikuwa akipata habari za Roma za kila siku , alikuwa akijua hata swala la Roma na Edna kugombana,alikuwa akijua pia Lanlan ni mjukuu wake kabisa.
Mpango wa Raisi Senga ilikuwa ni kumtumia Roma ili kuweza kushinda vipingamizi vyake vyote ambavyo vinajitokeza katika uongozi wake , alipanga kama atakuja kuwa huru na hatia ambayo ilikuwa ikimtafuna basi moja kwa moja angeweza kuwa huru na kuanzia hapo angeweza kujitokeza mbele ya Roma na kumuita mtoto wake.
Kwenye watu waliokuwa wakisubiria kurudi kwa Roma pia kwa hamu kubwa alikuwa ni Raisi Senga yote hayo ni kutokana na mipango yake aliokuwa amepanga kwa ajili ya kumtumia Roma.
Kitendo cha Roma kupotea aliamini kabisa ingevuruga kila kitu ambacho alikuwa amekiweka kwenye mjongeo.
“Huu ulikuwa ni mpango thabiti , nilikuwa kama Kabwe mara baada ya mpango huu kuelezewa kwangu , Suzzane ujio wako kwangu umenisaidia sehemu kubwa , nipo tayari kurekebisha kosa nililolifanya kwa msukumo wa chuki zangu”Aliongea mwenyewe Raisi Senga akionekana kuwaza.
Lakini katika mawazo yake anaonekana kumtaja Suzzane.







SEHEMU YA 643.
MIEZI KADHAA ILIOPITA.
Ni miezi kadhaa iliopita , ikiwa ni siku ya jumanne katika makazi ya mrembo Suzzane Kibaha eneo maarufu lililokuwa likifahika kwa jina la Mji wa kisasa.
Suzzane kama kawaida siku ya jumanne yote aliendelea na kazi zake kama kawaida kwa niaba ya Edna katika usimamizi wa kitengo cha Athena.
Siku hii Suzaane alikosa utulivu kuliko siku zote ambazo amezoeleka pale ambapo anakuwa kazini,
Alionekana kama mtu ambaye alikuwa akitarajia mtu kumpigia simu kwani muda wote alikuwa akiangalia simu yake kama kuna meseji imeingia.
Aliendelea kutokukosa utulivu karibia siku nzima mpaka wakati ambao anarudi kwenye Apartment yake baada ya muda wa kazi kukamilika.
Athena kilikiwa kama kitengo cha ujasusi ndani ya kampuni ya Vexto , kikundi hiki licha ya kwamba kazi yake ilikuwa ni kununua hisa na kuziuza lakini pia kilikuwa kikikusanya taarifa nyingi sana ambazo moja kwa moja zilikuwa zikihusiana na kampuni ya Vexto.
Katika kipindi chote cha miezi sita kazi yao kubwa ilikuwa ni kuifanya kampuni ya Nebula Inc kuwa chini ya umiliki wa Edna swala ambalo waliweza kulifanikisha ndani ya siku chache sana kabla hata ya Edna hajarudi nchini Tanzania akitokea Korea kusini.
Mtu aliekuwa akiongoza kitengo hicho alikuwa ni mwanadada Suzzane na Amiri na hawa ndio ambao walikuwa wakiripoti moja kwa moja kwa Edna.
Yaani kwa maneno marahisi ni kwamba matawi yote ya Vexto yaliokuwa ndani ya nchi na nje ya nchi taarifa zake za siku nzima zilikuwa zikichambuliwa na kampuni na kitengo hicho na kisha kama kutaonekana utata taarifa zote moja kwa moja zingeenda kwa Edna ili kutolewa maamuzi.
Ukiachana na kuongoza kitengo cha Athena ,
Suzzane pia alikuwa mtendaji mkuu wa Edna Foundation , shirika ambalo lilikuwa likisaidai watu wenye uhitaji.
Ni sawa na kusema ukiachana na Suzzane kuwa msaidizi wa siri wa Edna lakini upande mwingine alikuwa na cheo kikubwa sana na ndio mtu ambae alikuwa akijua siri nyingi sana zinazohusiana na Edna.
Ukubwa na ufanisi wa kitengo cha Athena ulidhihirika kwa namna ambavyo waliweza kuinunua kampuni ya Nebula Inc nyuma ya mgongo wa wa benki ya biashara ya JR ambayo ilikuwa ikimilikiwa na familia ya Rothchild ikimtanguliza Edna kama muwakilishi wao.
Kukamilisha mpango wa kampuni ya Nebula ndio ilikuwa ni sehemu ya mafanikio ya kuifanya kampuni ya Vexto international kuwa Vexto Group.
Sasa kutokana na ubize ambao walikuwa nao Athena ilimfanya hata Suzzane kuwa bize kama kiongozi lakini siku ya jumanne aliwashangaza wafanyakazi wenzie kwa namna ambavyo alikuwa ‘distracted’ kazini.
Wasichokijua ni kwamba licha ya Suzzane kuwa kama kiongozi lakini alikuwa na maisha binafsi ambayo siku zote yaliwafanya kujiuliza kwanini Suzzane hakuwa na mpenzi licha ya uzuri wake.
Sasa siku hio Suzzane akiwa sio mwenye kujali maswali waliokuwa nayo wafanyakazi wenzake alirudi kwenye nyumba yake kwa ajili ya mapumziko huku akionyesha kidogo kunyongea , alionekana kama mtu ambaye alikuwa akitegemea jambo lakini jambo lenyewe halijafanikiwa ndio maana alionekana kidogo kukosa raha.
Suzzane mara baada ya kujilaza kwenye Sofa akiangalia runinga alijikuta akipotelea usingizini.
Ukweli ni kwamba ilikuwa haki kwa wafanyakazi wa Athena kumshangaa Suzzane kwani katika wanawake ambao walionekana ni wapweke Suzzane alikuwa akiongoza , hajawahi kuonekana kuwa na mwanaume tokea kifo cha mpenzi wake Elvice.
Suzzane akiwa amepotelea usingizini alijikuta akishituka mara baada kengele ya nyumba yake kugonga, kabla ya kwenda kujua nani alikuwa akimgongea aliangalia saa ya ukutani na alikuja kuona kwamba alikuwa amelala muda mrefu zaidi ya masaa manne kwani muda huo ilikuwa ni usiku wa saa moja ikienda na nusu.
Suzzane akiwa katika hali ya uvivu alijikuta akisimama na kuelekea mlangoni na kabla ya kufungua mlango alibonyeza kitufe cha Telekom ili kuangalia sura ya mtu aliekuwa akigonga na mara baada ya kuona sura ya mgeni wake alijikuta macho yake yakichanua na palepale alifungua mlango.
“Suzzane..!!!”
Sauti nzuri na nyororo iliweza kuita jina la Suzzane mara baada ya kufungua mlango na kukumbatiana.
“Nadia karibu sana”Aliongea Suzzane akimkaribisha Nadia
Ndio alikuwa ni mrembo Nadia Alfonso mwanasheria wa kimataifa ambaye aliweza kujizolea umaarufu kwa kusimamia kesi za wanasiasa wakubwa duniani lakini pia akiwa kama mwanasheria wa makampuni makuwa duniani ikiwemo kampuni ya Vexto ambayo ipo chini ya mrembo Edna Adebayo.
Haikuwa mara ya kwanza kwa Suzzane kukutana na Suzzane , ukweli ni kwamba waliweza kukutana mara nyingi sana katika mazingira ya kikazi na mara chache nje ya mazingira ya kikazi.
Nadia Alfonso alikuwa ni mwanasheria wa kampuni ya Vexto hivyo Suzzane kukutana nae katika mazingira ya kikazi halikuwa swala la kushangaza sana , lakini pia Suzzane alikuwa ni msadizi wa karibu wa Edna hivyo pia aliweza kukutana Nadia pia katika mazingira ambayo yalikuwa nje ya kikazi , mazingira ambayo yamemfanya kuwa na maswali mengi mpaka siku hio.
“Nilijua usingefika , nilishajikatia tamaa, Karibu sana”Aliongea Suzzane akionyesha uchangamfu.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kufika katika huu mji , hakika kweli ni mji wa kisasa unavutia sana, unaendana na sifa ambazo nimezisikia , lakini pia hata hapa ndani kwako ni pazuri mno , nadhani napaswa na mimi kuamia huku”Aliongea Nadia aliekuwa akiangaza angaza kulia na kushoto kwa namna ya kukagua mazingira.
Nadia alikuwa amevaa amependeza , ilikuwa kama kawaida yake kwa kujipenda ukiachana siku hio kuvalia kama vile anaenda mazoezini lakini ukweli ni kwamba amependeza pengine umbo lake ndio ambalo linamfanya kila mavazi anayovaa kumfanya awe ni mwenye kupendeza.
“Mgeni unatumia kinywaji gani
nikuandalie?”Aliongea Suzzane mara baada ya Nadia kuketi.
“Una mvinyo wowote?”Aliuliza na Suzzane alitoa tabasamu.
“Ninao mvinyo karibia aina zote maarufu maarufu kwa ajili ya watu ambao hawako kwenye mahusiano”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kucheka.
“Suzzane siamini kwa urembo wako huo unaweza kuwa Single”
“Wewe sio wa kwanza kuniambia hivyo?”
“Mh..!!, Why?”Aliuliza huku akionyesha macho ya mshangao.
“Ni stori ndefu Nadia pengine ndio ambayo imetufanya tuonane leo hii”Aliongea
“Inaonekana tunaendana kwa kiasi kikubwa , basi nitaomba uchague yoyote nadhani nitaipenda , ili itusaidie kwenye maongezi yetu”Aliongea Nadia.
Suzzane alitabasamu na kisha alisogelea jokofu na kutoa chupa ya mvinyo na kisha alienda kuchukua glass mbili na kuziweka juu ya meza ya kioo.
“Huu ni mvinyo nimetokea kuupenda sana , unaitwa Sauvignon Blanc una mchanganyiko wa radha ya chungwa , Zabibu na miti shamba nadhani utaipenda”Aliongea Suzzane huku akimimina na Nadia alitoa tabasamu na baada ya kuwekewa kidogo kwenye Glass alichukua na kuonja
“Wow!!, ijapokuwa ndio nimeanza kuiona kwa mara ya kwanza naamini nikiizoea ni tamu”Aliongea Nadia.
“Unaonekana una uzoefu mkubwa wa kunywa mvinyo?”
“Sana , mimi ni mlevi wa mvinyo na nimefurahi kuonja radha mpya”Aliongea huku akishika ile chupa na kujaribu kusoma maandishi yake na alishangaa kuona inatengenezwa hapa ncini Tanzania.
“Ulisema ulitegemea sitokuja , nadhani ulikuwa na shauku kweli ya kuniona?”
“Acha tu , nimechoka kuishi kwa maswali mengi”
“Sikutaka kukuambia nakuja muda gani kutokana na kwamba ratiba zinabadilika lakini pia kuna vitu vingi ambavyo nimeviandaa kabla ya kuja hapa , nadhani leo nitalala hapa hapa kama hutojali”Aliongea
“Usijali wewe jisikie huru kabisa na unakaribishwa kuja kulala muda wowote”Aliongea.
“Haha.. asante , Suzzane unaonekana kuwa mchangamfu tofauti na muonekano wako , hata hivyo nadhani nitapata rafiki wa kwanza kutokea hapa nchini”
“Nadhani tutaendana vizuri , isitoshe ujio wako wa leo naamini una majibu mengi ambayo yanaweza kutuweka karibu zaidi au Laha , shauku yangu nikutaka kujua majibu ya ombi langu”Aliongea Suzzane akionyesha ni mwenye shauku na Nadia alikunywa mvinyo kidogo na kisha akweka Glass chini.
“Kwanza Nasra licha ya kwamba naamini kuna sabababu nyingi ambazo zimekusukuma mpaka kuomba kuwa mwanachama lakini nikupongeze pia kwa ujasiri wako”
“Upo sahihi ,, Asante Nadia”.
“Labda naweza kujua sababu ambayo imekusukuma mpaka kufanya maamuzi yako japo kwa ufupi tu
kabla sijaanza kukupatia taarifa niliofika nayo”Aliongea Nadia huku akionyesha umakini kwa kumkazia macho Suzzane.
“Sijui nianze wapi lakini kubwa zaidi nataka kujua kwa undani kwanini Elvice alikuwa akihusishwa na umoja wa Ant Illuminat mpaka kifo chake kikamkuta , nataka kujua maana ya maneno ya Chriss kwannini alisema napaswa kuendeleza pale alipoishia Elvice katika kutibu dalili za ugonjwa unaoanza kujionyesha”Aliongea huku akianza kumwelezea kwa ufupi historia yake ya kimapenzi na Dr Elvice Danieli pamoja na maneno ambayo aliongea na Chriss mara ya mwisho kabla hajamkutanisha na Edna.
Nadia alimsikiliza mwanzo mwisho , ijapokuwa ni kweli alikuwa akiijua hitoria ya Elvice Daniel lakini kuisikia kutoka kwa Suzzane mwenyewe ilimfanya kupatwa na huzuni.
“Unaonekana ulimpenda sana Elvice, ndio kitu ambacho kinakufanya mpaka sasa kuendelea kuwa Single??”
“Nadia ninayaogopa mahusiano , ukweli ni kwamba sijiamini mimi mwenyewe najaribu kumsahau Elvice lakini nimeshindwa . nakosa amani ni kama sauti ya Elvice kila siku inaniita , nigeweza kujiingiza kwenye mahusiano na kusahau haya yote lakini siamini kama ninaweza kumudu mahusiano”Aliongea kwa kutia huruma.
“Naelewa unachopitia Suzzane lakini amini kabisa kifo cha Elvice hakijaenda bure, hivyo mzigo uliokuwa nao unapaswa kuutua sasa”
“Natamani kufanya hivyo lakini bado nahitaji kuendelea pale alipoishia Elvice , najua alichokuwa akifanya ni kitu kikubwa ambacho kina manufaa kwa dunia na hio ndio saabu yangu kubwa ya kutaka kuendelea alipoishia”
“Nimekuelewa , lakini Suzzane kuwa mwanachama ni swala la kujitoa , ni swala ambalo lina hatari kubwa na pengine unaweza kupatwa na kitu kilichompata Danieli , kama una mashaka unapaswa kufikiria mara mbili”
“Nadia tokea siku ambayo nilifanya maamuzi na kufikisha ombi langu kwako nimekaa kwa muda mrefu nikafikiria na kufanya maamuzi, nahisi hili ni swala ambalo napaswa kufanya sio kwa ajili ya Elvice tu lakini pia kwa ajili ya Edna”
“Edna..!!”
“Ndio Nadia, ntaka pia kumlinda Edna kadri niwezavyo hili ni juu ya ahadi yangu niliowekeana na mama yake”Aliongea na Nadia alionekana kufikiria.
“Lakini Edna tayari yupo chini ya ulinzi wa Roma mume wake , kama ni mtu ambaye anatakiwa kumlinda Edna basi ni Roma , kwanini unaamini wewe unaweza kumlinda?”.
“Kuna mambo mengi ambayo kwasasa yanaendelea katika maisha ya Edna na mimi ndio mtu wa pekee ambaye namjua nje ndani , ni kweli Edna anapaswa kulindwa na mume wake , lakini upande wangu sijawahi kumwamini mume wake Roma , ni mtu wa wanawake wengi , ijapokuwa Edna anaonekana kumpenda lakini nina wasiwsi na kudumu kwa mahusiano yao”Aliongea na Nadia alionekeana kufikiria.
“Suzzane naweza kusema kwamba kutokana na taratibu na sheria za uoja kwasasa hujakidhi vigezo vya kujiunga ..”Aliongea na kumfanya Suzzane kuonyesha hali ya kutofurahishwa na maneno ya Nadia.
“Kwanini Nadia kuna vigezo gani ambavyo napaswa kuwa navyo?”
“Ili kujiunga kigezo kikubwa kinachoangaliwa ni ushawishi wako katika jamii , yaani hapa namaanisha ukiachana na wewe binafsi unapaswa kuwa na kitu cha kipekee cha faida katika umoja, hapa kwa maneno marahisi unapaswa kuwa angalau Public Figure , lakini vielelezo vyako vinaonyesha wewe ni mwanasheria na mfanyakazi wa kawaida wa kampuni ya Vexto”Aliongea na suzzane alionekana kumwelewa.
Ijapokuwa hata kwa Elvice mpenzi wake hakuwa na kigezo cha wazi mpaka kukubalika kuandaliwa kuwa mwanachama lakini kifo chake kilionyesha kwamba alikuwa na kitu kikubwa cha faida kwa umoja.
Hizo zilikuwa kanuni za kawaida sio kwa umoja wa siri wa Ant illuminat lakini mpaka upande wa Illuminat yenyewe ama Freemason .
Kigezo kikubwa kinachoangaliwa ni ushawishi wako katika jamii uko vipi na kama utajiunga katika umoja utakuwa na faida gani na ikitokea unapewa ajenda flani ambayo unapaswa kuisukuma kwa jamii je utafanikisha vipi , hivyo ni baadhi ya vigezo.
Suzzane alikuwa ni msomi hivyo alikuwa na uelewa na meneno ya Nadia.
“Kwahio kwa maneno yako ni kwamba sina nafasi ya kujiunga?”
“Nafasi unayo Suzzane, unaweza ukakosa vigezo wewe lakini ukafanikiwa kuingia kupitia mtu ambaye amekidhi vigezo lakini sio mwanachama”
“Unamaanisha nini?”Aliongea Suzzane huku akionyesha mshangao na Najma alitoa tabasamu na palepale alifungua mkoba wake na kutoa kishikwambi na alipangusa kwa dakika chache na kisha akampatia Suzzane.
Suzzane mara baada ya kuangaliwa kitu kilchokuweno kwenye kioo cha kishikwambi kile alionyesha muonekano wa kutolewa.
“Unamjua?”
“Ndio huyu si mheshimiwa Raisi Senga , hakuna raia anaejielewa akashindwa kumjua raisi wa nchi”
“Huyo ndio atakufanya ukidhi Vigezo Suzzane nduo maana nimekuuliza mara mbilimbili unamjua , unaweza ikawa kweli unamjua kama raisi wa nchi lakini humjui yeye kama yeye ni nani”
“Sijakuelewa Nadia , mheshimiwa Raisi ananifanya vipi kukidhi vigezo”
“Kama utamshawishi kujiunga na umoja wetu basi utakuwa umepiga hatua ya kwanza kabla ya kuthibitishwa rasmi kama mwanachama”Aliongea
Nadia huku akionyesha usiriasi na kumfanya
Suzzane kushikwa na mshangao mkubwa
“Nadia nitaweza vipi kumshawishi raisi wa nchi kujiunga na umoja ambao mimi mwenyewe si ujui vizuri?”
“Swali Zuri Suzzane , Umoja utakupatia taarifa zote kuhusiana na mheshimiwa Raisi Senga pamoja na mpango wa awali , hili ni swala nyeti sana na linaweza kuwa hatari kwako kwani taarifa ambayo utakwenda kuijua ni ‘Top Secret’ kosa kidogo tu inaweza kuwa mwisho wako Suzzane , hivyo kwanzia leo nipo Tanzania na nitakuwa na kupa maelekezo hatua kwa hatua”
“Ofcourse kama haupo tayari kazi hii anaweza kupewa mtu mwingine Suzzane”Aliongea Nadia mara baada ya kumuona anafikiria.
“Sijajua namshawishi vipi lakini nitajaribu”Aliongea Suzzane.
“Suuzzane hili sio swala la majaribio , ukishaanza hakuna kurudi nyuma tena na lazima ufanikiwe vinginevyo unaweza kupatwa na tatizo kubwa sana au ukashindwa kuendelea kuishi hapa Tanzania ,Suzzanie kama utakubaliana na swala hili jua umeyaweka maisha yako Rehani hivyo fikiria mara mbili mbili , je upo tayari?”
Kwa jinsi ambavyo Nadia alikuwa siriasi ilionyesha ni kwa namna gani ambavyo swala lenyewe lilikuwa nyeti.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUME BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR

Mono no ware.

SEHEMU YA 644.
Ni siku kadhaa baada ya mazungumzo kati ya Suzzane na Nadia kumalizika , huku Suzzane akiamua kufanya kazi ambayo itamuwezesha kukidhi vigezo ili kupata nafasi ya kupata uwanachama wa Ant-Illuminat.
Ikiwa ni siku ya jumamosi Suzzane aliweza kupokea ujumbe wa meseji kutoka kwa Nadia uliokuwa ukimtaarifu kwamba maombi ya miadi yake na Raisi Senga imeweza kufanikiwa na anapaswa kusafiri mpaka mkoani Dodoma makao makuu ya nchi kwa ajili ya kuonana nae.
Suzzane mara baada ya kupata taarifa hii mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio sana , ijapokuwa alikuwaakijiamini katika mambo mengi , lakini swala ambalo ameamua kulifanyia kazi halikuwa swala dogo ambalo ni la kuongea na mheshimiwa Raisi tu na likaisha hapo bali ni mwanzo wa kitu kingine, dakika na sekunde ambayo atatamka kile ambacho kimemfanya kutaka kuongea na raisi huyo basi ni mwanzo wa maisha mapya.
Suzzane alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha na alijitahidi kujiambia kwamba kila kitu kitafanikiwa kama alivyopanga.
Kilichokuwa kikimpa wasiwasi Suzzane ni kwamba Nadia alimwambia kwamba licha ya kwamba hatua yake ya kwanza katika misheni ya kumfanya Raisi Senga kuwa mwanachama wa Ant -Illuminat ni kuonana nae na kuongea nae kile alichomwambia lakini hatua ya pili hakuwa akiijua.
“Suzzane hatua ya kwanza unayotakiwa kufanya ni kuhakikisha Mheshimiwa Senga anakuamini , jambo hili sio jepesi kwasababu ‘trust is earned over time’ na ili uweze kufanikiwa lazima kwanza uwe na sababu binafsi ya yeye kukuamini”
“Sababu binafsi ya kuniamini? , hapo sijakuelewa” “Hakuna jaribio ambalo anapewa binadamu ambalo lipo nje ya uwezo wake , wewe kupewa hii kazi ili kukidhi vigezo ni kwasababu mahesabu yanaonyesha
ni swala ambalo unaweza kulifanyai kazi na likafanikiwa”
“Kwanini unahisi hili ni jaribio ambalo lipo ndani ya uwezo wangu?”
“Kwasababu ya historia yako na Dr Elvice , kitendo cha kuwa Single mpaka sasa ukiendelea kumuweka Elvice moyoni mwako licha ya kwamba amefariki muda mrefu ndio sababu, unajua Suzzane kwanini nilikuambia uniambie kuhusu historia yako na DrElvice wewe mwenyewe licha ya kwamba uliandika katika maombi yako?”
“Sijajua?”
“Nilitaka nikusome hisia zako wakati wa kumzungumzia Elvice , umeongea kwa hisia sana kiasi cha kuweza kunifanya ni kuamini , hiki ndio ambacho nilichokuwa nikitaka kuona kutoka kwako , mimi kama ‘Handler’ wako kwanzia sasa, Suzzane ili jaribio kama litafanikiwa pengine ni swala ambalo linaweza kukuweka huru na ili uelewe namaanisha nini lazima pia nikuambie ukweli namna ambavyo Elvice alifariki na nani alihusika”Aliongea Nadia na kumfanya Suzzane kumwangalia Nadia kwa macho yaliojaa umakini kuliko mwanzo.
“Unamjua aliemuua Elvice?”
“Najua alieagizwa kumuua Elvice lakini swala ambalo lipo nyuma ya kifo cha Dr Elvice ni swala ambalo Umoja ndio unajua”Aliongea Nadia na kumfanya Suzzane kupatwa na shauku ya kutaka kujua.
“Nataka kujua Nadia nani alimuua Elvice? , iwe ni
kwa kuagizwa au ni kwa kufanya maamuzi yeye mwenyewe”
Nadia alifikiria kidogo na kisha akaingiza mkono wake kwenye mkoba ambao amefika nao na kisha alitoa picha na kumpatia Suzzane.
“Huyo ndio ambaye amehusika na kifo cha mpenzi wako Elvice , kwa jina anaitwa Salim Shariff ni jasusi mstaafu wa kikosi cha Dhoruba nyekundu na kwasasa anafahamika kwa jina la Salimu Ibuyawanga ni baba yake Waziri wa Mazingira bwana Nguzo Ibuyawanga”Aliongea Nadia na kumfanya Suzzane mikono kumtetemeka huku machozi yakianza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake.
“Una ushahidi gani wa kuniaminisha huyu ndio kahusika?”
“Suzzane hilo ni swali ambalo utaweza kulipata siku ambayo utakuwa mwanachama kamili wa umoja wa Ant – illuminat, Chriss umesema amekuambia Elvice alikuwa akipambana na ugonjwa ambao dalili zake zimeanza kujionyesha basi kama ni uonjwa maambukizi ya huo ugonjwa yameanzia kwa huyu mtu”Aliongea na Suzzane ambaye machozi yalikwa yameupamba uso wake aliyafuta na kisha akamwangalia Nadia.
“Unataka nifanye nini?”
“Ili uweze kufanikiwa kumfanya Raisi Senga kukuamini ni kumpatia mpango ambao utaweza kumuondoa huyu mtu hapa nchini, familia ya Ibuyawanga ni familia ambayo nguvu yake haionekani ambayo Serikali inaiogopa”
“Unamaanisha nini nguvu ambayo
haionekani?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Nadia amwambie asogeze sikio amnong’neze na Suzzane alifanya hivyo na mara baada ya Nadia kuonekana kuongea jambo alijikuta akishangaa kwa kutoa macho.
“Hili swala ni la kweli?”
“Ni swala la kweli, Serikali ya Tanzania haina nguvu ya kumuondoa huyu mtu kwasababu ya hio nguvu yake lakini kama nguvu nyngine itajitokeza kutaka kuisaidia serikali kupambana na huyu mtu basi ni hakika atachukua hatua ni maswala ya kidiplomasia zaidi , wewe sasa itakuwa ni fursa kwako kumwelezea Raisi Senga juu ya nguvu hii ambayo ipo tayari kumsaidia huku ukitumia sababu yako binafsi ya kisasi zidi ya familia hio kumfanya Raisi Senga akuamini”
Suzzane alikuwa kwenye mfululizo wa kuwazia maongezi yake na Nadia mara ya mwisho kabla ya siku inayofuatia kuanza safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya kuongea na mheshimiwa.
Kwanza kabisa Suzzane alipaswa kumwelezea
Mheshimiwa juu ya kisasi chake zidi ya familia ya
Ibuyawanga na baada ya hapo alipaswa kutumia
‘Codes’ katika kuelezea nguvu ambayo ingeweza kumsaidia Raisi Senga kupambana na nguvu ya ziada ambayo inaendesha nchi kwa mgongo wake.
“Suzzane hakikisha unapangilia maneno yako vizuri kama nilivyokuelekeza na baada ya hapo mpatie mheshimiwa mpango wako kwa kutumia tatizo analopitia, inawezekana asikubaliane na wewe hapo kwa hapo lakini lazima atakaa chini na kufikiria ulichomuambia na atafanya maamuzi”Alimalizia kuongea Nadia kauli ambayo na Suzzane pia alikuwa akiikumbuka vyema.
Suzzane kabla ya kuanza safari yake alianza kuandaa mpangilio wa maneno yake , ijapokuwa alikuwa akisifika kwa kujiamini tokea akiwa mdogo lakini mazingira mapya ambayo anaenda kukutana nayo siku ya kesho hakuwahi kuyapatia uzoefu hivyo presha ilikuwa juu na aliamini kitu pekee cha kupunguza wasiwasi wake ni kujiandaa vizuri.
Juu ya meza ambayo Suzzane alikuwa akifanyia kazi katika kujiandaa kulikuwa na picha kadha wa kadha ambazo zilikuwa zimepangiliwa , wakati huo huo alikuwa ameshikilia karatasi ambayo ina maandishi ya kurasa takribani nne ambayo ndani yake pia ina picha hizo hizo zilizokuwa zipo juu ya meza lakini ambazo zimetengenezewa kopi na kuambatanishwa, moja wapo ya picha hio ilikuwa ni ya Naibu Waziri Salihi mtoto wa Waziri wa mazingira.
******
Ni siku moja baada ya Raisi Senga kuweza kukutana na Suzzane na kufanya mazungumzo.
Katika saa zote ishirini na nne tokea mazungumzo hayo yamalizike Raisi Senga alipatwa na hisia tofauti tofauti sana , kwanza kabisa alipatwa na mshangao , alipatwa na hofu na pia akapatwa na wasiwasi.
Siku chache nyuma kupitia chaneli yake ya siri sana ya taarifa ya watu anaowaamini ndani ya Ikulu iliweza kumletea taarifa ambazo zilikuwa zikihusiana na mtu ambaye alikuwa akihitaji miadi ya kuonana nae akiwa ndani ya ikulu ya Dar es salaam , haikuwa taarifa tu ya mtu huyo kuomba miadi bali ni kwamba alietuma ujumbe huo aliambatanisha na sababu(bait) ya yeye kukubali kukutana nae.
“Need an appointment , I can help you avoid signing an unfair contract that is against Tanzanian Culture”
Ujumbe huo ulikuwa na tafsiri ya mtu kuhitaji miadi
, na mtu huyo anasema anao uwezo wa kumsaidia kuepusha kusaini mkataba ambao unaenda kinyume na Tamaduni za watanzania.
Siku ambayo mheshimiwa Senga aliweza kupokea huu ujumbe kwanza alipatwa na kiwewe , ni kweli kwamba kulikuwa na mkataba ambao alikuwa akilazimishwa na wakuu wake katika umoja wa siri aliojiunga kuusaini ili utekelezwe Tanzania lakini alishindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu akiwa katika Dilema kwani kitendo cha kutia saini mkataba huo ilikuwa ni kwenda kinyume kabisa na kile alichokuwa akikiamini hata kabla ya kuwa raisi.
Ni kweli kwamba alikuwa ashafanya makosa makubwa ya kujinga katika umoja huo na kufanya au pengine kuendelea kufanya mambo ambayo yanaenda kinyume na kile alichokiamini lakini mkataba uliokuwa mbele yake ulikuwa ukivuka mpaka ambao kama angeuvuka basi ingekuwa ngumu kurudi tena.
Sasa wakati akiendelea kuwa katika Dilema anapokea ujumbe wa aina hio k wa kutumia chaneli ya siri ya mawasiliano ndani yake ambayo ni tofauti kabisa na mfumo wa kawaida wa mawasiliano ikulu.
“Kabwe ipo namna ya kurudisha jibu?”Aliuliza Raisi Senga siku mbili baada ya ujumbe huo kutumwa.
“Ndio mheshimiwa”
“Okey, nimekaa na nimefikiria juu ya hili swala kwa undani , mtu ambaye ametuma taarifa hii anaonekana sio wa kawaida sana kwani chaneli ya maswalisiano alioitumia tunaijua wachache sana , hivyo nitahitaji kwanza kuonana nae kabla ya kufatilia kosa limetokea wapi mpaka kutokea kwa chaneli yetu kuingiliwa”AliongeaMheshimiwa Senga.
“Lakini mheshimiwa…”
“Kabwe najua wasiwasi wako , lakini nishafanya maamuzi tayari, wasiliana nae na mpatie hizi taarifa”Aliongea Raisi Senga na kisha alimpatia Kabwe faili lililokuwa mbele yake.
Ijapokuwa Kabwe alionyesha wasiwasi lakini hakutaka kupinga maagizo ya mkuu wake wa kazi.
Sasa kilichomshangaza Raisi Senga ni kwamba alikuwa na shauku kwanza ya kutaka kujua ni nani aliekuwa amemtumia ujumbe na kutaka kuonana nae , mategemeo yake yalikuwa ni kuona mtu ambaye hajawahi kumuona katika macho yake , lakini alijikuta akishangaa mara baada ya kuoa mtu huyo alikuwa ni Suzzane.
Raisi Senga alikuwa akimjua Suzzane kwa muda mrefu tokea akiwa ni Sekretari na mwanasheria binafsi wa mama yake Edna.
Licha ya mshangao wake lakini hakutaka kudharau , alitaka kujua imekuwaje kuwaje pia akawa ni Suzzane mtu ambaye alikuwa akitegemea kwa hamu kuonana nae ndani ya Ikulu ya Chamwino tena kwa siri sana.
Raisi Senga baada ya kufanya mazungumzo na Suzzane mpaka kumaliza alijikuta akishangaa sana kile ambacho Suzzane alikuwa amemuambia , hakuwa akimwamini kabisa Suzzane kwa kile alichomwambia kwani kwa nafasi aliokuwa nayo Suzzane na kwa uzoefu wake asingekuwa na taarifa nyeti aliomwambia lakini pia asingeweza kujua kuna mkataba ambao anataka kusaini ambao unaenda kinyume na tamaduni za watanzania.
Ijapokuwa Suzzane hakumwambia ni watu gani wapo nyuma yake , lakini alipatwa na shauku zaidi na zaidi ya kuonana nao lakini hakuishia hapo tu saa na muda ambao Suzzane anaondoka ikulu tayari mheshimiwa ashaagiza watu kuanza kumfatilia na kumpatia taarifa ya kila mtu anaekutana nae.
Ikiwa ni siku moja sasa mara baada ya kuwaza kwa kina ,siku hio akiwa ndani ya ofisi yake aliamua kufanyia kazi mpango wa Suzzane huku akiwa na nia ya kutaka kujua nani yupo nyuma ya Suzzane mpaka kutaka kumsaidia.
Sasa ikiwa ni siku kadhaa tokea Suzzane kufanya mazungumzo na Raisi Senga, Raisi alifanya uteuzi kwa kumteua Salihi Nguzo kuwa mbunge na naibu waziri wa elimu.
Ulikuwa ni uteuzi ambao ni wa kushsangaza kwani Salihi alikuwa na umri mdogo sana kuaminiwa nafasi kubwa ndani ya serikali , tena mbaya zaidi ni kwamba Salihi alikosa udhoefu wa siasa za Tanzania kwani alikaa nje ya Tanzania kwa muda mrefu.
“Nadia hongera kwa kutimiza hatua ya kwanza ya misheni yako”Sauti ya mwanadada Nadia iliweza kusikika katika simu upande wa pili.
“Asante sana Nadia , yote haya yamefanikiwa kwa maelekezo yako mimi mchango wangu ni mdogo”
“Sio kweli Suzzane , ulichokifanya ni jambo ambalo linahitaji mtu jasiri na wewe umeweza kuonyesha ujasiri wako , hongera sana kwa hilo hii ni hatua nzuri ambayo inakuingiza katika kitu kingine”
“Asante sana , nini kinafuata baada ya hapa?, Mlengwa wetu wa kwanza ambaye ni Dorisi amebadilika , kwasasa kutakuwa na changes”
“Mlengwa mwingine ni nani?”
“Nitakutumia taarifa Suzzane kila kitu kikiwa
‘Confirmed’ kwasasa kaa ukiwa ‘Alert’ na usinitafute kwa muda mpaka nitakapokutafuta mimi”Aliongea Nadia na kisha simu ilikatwa palepale.
Wote walikuwa wakitumia simu za batani tena namba tofauti kabisa ya mtandao wa Safaricom na wakati Suzzane anawasiliana na Nadia alikuwa yupo bafuni.
Suzzane alikuwa akijua anafatiliwa na maafisa kipenyo hivyo alijitahidi kuchukua tahadhari.






SEHEMU YA 645.
Ilikuwa ni muda wa mchana Roma alionekana akitoka katika hoteli ya kimataifa ya Maple iliokuwa ikipatikana pembezoni mwa fukwe ya upepo Beach.
Roma wakati akitoka ndani ya hoteli hio alijikuta kumbukumbu zake zikimrudisha nyuma namna ambavyo alimlera Edna mahali hapo na kukisi nae kwa mara ya kwanza.
Moyo wake ulijikuta ukianza kuwa mzito mara baada ya kufikiria hali yake ya kimahusiano na mke wake, Roma alijiambia kuna mlima mkubwa mbele yake ambao anapaswa kuvuka ili tu kumrudisha Edna katika himaya yake na kumuondolea mawazo ya kutaka kuachana nae.
Roma wakati akishangaa shangaa mazingira , alitamani hata kumpigia simu Neema Luwazo ili waburudike muda huo wakiwa pamoja lakini hakuwa hata na hamu ya kufanya hivyo, isitoshe alijua pengine atakuwa kazini muda huo.
Ukweli mara nyingi anapokuwa na mgogoro na Edna ile hali ya kutaka kutembea na wanawake wengine ilikuwa ikipungua kwa kiasi kikubwa sana, ilikuwa ni kama vile anapokuwa na amani na Edna hisia zake zinakuwa wazi na anapata hamasa ya kutoka na wanawake wengine , lakini inapotokea ugomvi ndio utulivu wa akili yake hutoweka na kujikuta akikosa hamu ya kustarehe na warembo wake.
Pengine sio yeye tu ambaye alikuwa akijua kuhusu hilo , hata wanawake wake alikuwa wakiliona hilo na ndio maana walikuwa wakiomba Edna kuendelea na Roma ili tu Roma aweze kuwa na utulivu wa akili na wao kufurahia penzi.
Roma alikuwa hotelini hapo kwa ajili ya kuonana na Samweli Nguluma ambaye alikuwa na dili amempatia kwa ajili ya kumsaidia siraha za kimagendo ambazo alihitaji zisafirishwe mpaka mkoani Kilimanjaro.
Samweli Nguluma ambaye ni baba yake Benadetha na mkuu wa kundi la Zoa Zoa lenye makazi yake katika mkoa ya Mwanza na Shinyanga alionekana kuwa mzito kukubaliana na ombi la Roma.
Lakini faida ambayo Roma aliipendekeza kwake kama kile anachokwenda kufanya kitafanikiwa , ilimfanya kufikiria mara mbilimbili na baada ya maongezi ya muda mfupi ya kukubaliana katika masharti Samweli Nguluma alikubali kumsaidia Roma mahitaji yake huku akimpa onyo la kumtahadharisha kama isitokee akawa na uhusika wowote kama mambo yataenda kinyume na mipango yake na Roma alimtoa hofu na kumwambia hakuna wa kumtaja.
Upande wa Nguluma alishangazwa na kitendo cha Roma kuhitaji siraha ilihali alisifika kwa kuwa na nguvu kubwa zaidi ya bomu lakini hakutaka kuuliza maswali na alijitahidi kujenga nae urafiki bila ya kusahau kuchomekea topiki inayohusiana na binti yake Benadetha.
Licha ya bwana huyo kuingizia topiki hio Roma alibakia na msimamo wake uleule na kumwambia ni kama mara ya mwisho alivyomwambia walipokutana kwenye msiba wa babu yake Mzee Atanasi.
Mara ya mwisho Roma mara baada ya kukutana kwa mara ya kwanza na baba yake Benadetha aliweza kuambiwa na mzee huyo kwamba anataka kuwa mkwe wake , jambo ambalo Roma alikataa kata kata akisema hataki kuhusika na Benadetha kimapenzi.
Sasa siku hio ni kama Samweli nguluma aliendeleza pale alipoishia lakini Roma alionekana kumkatalia.
Roma alikuwa na haki ya kukataa isitoshe wakati huo alikuwa katika migogoro na mke wake Edna , hivyo hakutaka kuongeza tatizo lingine mbele ya safari ya jitihada za kumrudisha mke wake.
Roma alimuonea huruma Benadetha kwa kusikiliza maelezo ya baba yake , kulingana na maelezo ya Mzee Nguluma ni kwamba Benaetha amekataa kuwa na wanaume wote ambao baba yake amependekeza kuolewa nao na akaenda mbali kusema kwamba wanaume hao hawana vigezo anavyovitaka.
Baba yake Samweli Nguluma alijua tatizo pekee ni Roma , pengine Benadetha kwa kumuona Roma alishamchukulia kama ‘reference’ ya mwanamme anaemtaka jambo ambalo ni gumu kutekelezeka kwani Roma alikuwa ni tofauti na binadamu wa kawaida na kama Benadetha ataendelea kusimamia vigezo vya mwanaume anaemtaka kufanana na vya Roma basi atazeeka akiwa hajaolewa.
Wazazi wa benadetha waliishia kuangushia lawama kwa Roma ambaye amemchanganya mtoto wao.
Saa saba na nusu ndio muda ambao Roma aliweza kufika nyumbani na alishangaa mara baada ya kuingia eneo la sebuleni kumkuta Amina akiwa anacheza gemu na Lanlan.
Roma alikuwa amemkumbuka sana mrembo huyo kwani tokea atoke ulimwengu wa Majini pepo hakuwahi kumuona na alijikuta hata akishikwa na hatia kwa kutokumtafuta.
Nyumbani kwa Nasra ni kama yalikuwa ndio makazi mapya ya Roma , Nasra alikuwa akichakalika kweli kwani aliweza kubadilisha ratiba zake na kuhakikisha anaenda kazini na kurudi mapema na kupika chakula cha Roma na Lanlan kwa wakati na kisha kurejea kazini.
Amina alikuwa amependeza mno , alikuwa amevalia suti ya rangi ya Bluu na scarf nyeupe ya mua maua shingoni , alionekana kama vile ni wale wahudumu wa ndgea au wafanyakazi wa benki.
Amina mara baada ya kumuona Roma alisimama akitaka kumkimbilia amkubatie na Roma alichanua mikono vilevile kumpokea lakini kabla hata ya Amina hajamfikia Lanlan alishamuwahi na kujirusha kwenye mikono ya Roma na kuloki mikono yake kwenye shingo yake.
“Daddy needs to hug Lanlan first before hugging others”Aliongea Lanlan akimaanisha baba yake anapawa kumkumbatia yeye kwanza kabla ya wengine.
Roma alijikuta akitoa kicheko kwani ni kama Lanlan anamuonea wivu baba yake na kumwangalia Amina kwa kumchokoza.
“Babe wangu Amina sidhani kama kwa staili hii utakuwa na maelewano mazuri na watoto , hebu angalia namna ambavyo Lanlan ananipenda”Aliongea Roma na Amina alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira na kujiambia atawezaje kujilinganisha na Lanlan mtoto wake wa damu.
“Lanlan unaonaje ukimuachia baba yako , nitahakikisha nakupeleka kucheza siku ya wikiend sawa”Aliongea Amina na Lanlan mara baada ya kusikia ofa hio palepale alimuachia Roma na kumkumbatia Amina.
“Aunt Amina wewe ni mzuri sana”Aliongea Lanlan kwa kingereza
Roma alikuwa anajua kabisa binti yake hakuwa mtu mwaminifu kabisa kutokana na matendo yake mengi ya kisaliti aliokuwa akiyafanya kutokana na ahadi za chakula pamoja na kutolewa our matembezini kucheza na licha ya yote hayo Edna alikuwa akiyavumilia.
Lakini upande wa Roma bado aliona hio sio sawa kwa Lanlan na anatakiwa kumfunza kwani ilikuwa na wajibu wake , aliona kama ataendelea kutokuwa na msimamo kutokana na kupewa zawadi ingekuwa tatizo huko mbeleni.
Baada ya chakula cha mchana kuweka mezani Lanlan alichukua fursa hio kuanza kumpamba Nasra kwamba chakula chake ni kizuri na maneno meingine ya kumtia moyo kiasi cha kumfanya Nasra kutamani kumpiga busu, lakini zote hizo ni mbinu za Lanlan kumtaka Nasra kuongeza ubunifu zaidi kwenye mapishi.
Roma hakutaka hata kujishugulisha na tabia ya Lanlan kwa wakati huo maana ilimfanya kutamani kumpiga atulie.
Baada ya chakula Roma alitumia nafasi hio kuongea na Amina na aliweza kugundua kuna mengi ambayo yalikuwa yakiendelea , ilionekana baadhi ya ndugu wa Amina upande wa baba yake walianza kutaka kujumuishwa katika maswala ya urithi kutokana na hali yake ya kiafya.
Lakini ukiachana na hilo pia Amina alionekana alikuwa na majukumu mengi kiasi cha kumfana kukosa muda wa kuendelea kujifunza mafunzo ya kunyonya nishati za mbingu na ardhi.
“Natamni Nasra uje kunisaidia , najiona kabisa sijazaliwa kwa ajili ya kufanya biashara maana nashndwa kabisa kuongea na wafanyabiashara na kukutana na baadhi ya wawekezaji , kama Nasra utakuwa tayari kuja katika kampuni yangu nitakupa asilimia tatu ya Equity ya kampuni yote ya Kanani Group”
“Asilimia tatu!? , kulingana na thamani ya kampuni yenu hapo asilimia tatu ni zaidi ya mabilioni ya hela”AliongeaNasra kwa mshangao kwani ni kiasi kikubwa cha pesa cha kumfanya bilionea.
“Wewe ni kama ndugu yangu kwasasa na maamuzi yangu sidhani kama yatapingwa na bodi ya wakurugenzi maana asilimia ninazokupa ni za kwangu … Nasra kusema ukweli Sister Edna ana nguvu kubwa sana hata pasipo ya uwepo wako wewe , uwepo wa Dorisi na Benadetha unamtosha kabisa , kwanini usifanye kazi kwenye kampuni yangu na ukawa CEO Msaidizi , nitakulipa mara mbili zaidi ya unachopokea ndani ya Vexto?”
“Kuna watu wengi sana wanataka kunitoa ndani ya kampuni ya Vextoila nilikataa , ijapokuwa nina asilimia chache za umiliki wa kampuni ya Vexto nataka kutimiza ahadi yangu niliowekeana na CEO aliepita kipindi cha nyuma, Kama Edna hatonichukia basi maisha yangu yote naweza nikafanyia kazi ndani ya Vexto”Aliongea Nasra akikataa ombi la Amina.
“Lakini Sister Edna na kipenzi chetu wanataka kuachana , hautojisikia vibaya kuwa mbele yake ukienda kazini ?”Aliongea kwa sauti ya chini huku akimwangalia Roma.
“Kwanini unaongea hivyo Amina , hatujaachana rasmi kwa maandishi lakini tayari ushaanza kutamani nafasi ya Edna?”Aliongea Roma na Amina alikataa haraka haraka kwa kutingisha kichwa.
“Huo ujasiri natoa wapi , hio nafasi yenyewe kwangu ni ndogo sana isitoshe ninachoona Sister Edna ana hasira tu kwasasa na zikiisha atarudi kama zamani , halafu kwanza hakuna ambaye alikuambia umguse Sophia yalikuuwa makosa yako hebu muone , ijapokuwa kwa sasa ni star wa kimataifa na unaweza kujihisi umefanikiwa kumuweka chini yako kama mwanaume wake lakini umefanya maamuzi ya kukurupuka”
Roma kusikia maneno hayo ni kama aliona hayajakaa sawa , kwani sio kama yeye ndio alimfosi Sophia kumpenda , alichofanya ni kutotaka kumuona akiendelea kuteseka kwa ajili yake.
“Anyway , Sophia siku hizi anaendeleaje , maana sijafatilia taarifa zake tokea nirudi?”Aliuliza Roma.
“Kurudi kwa Sophia kumeiinua kampuni ya Vexto Media sana , ukijumlisha na ufanyaji mzuri wa filamu yake ya mwisho alioigiza chini ya Penguin Production amekuwa maarufu kimataifa na kwasasa anapokea Dili nyingi za kibalozi na pia kuombwa kuhudhuria katika matamasha mbalimbali, kulingana na tafiti iliofanywa na kituo cha utafiti cha Yugen Africa kimakadirio inaonyesha filamu aliogiza Sophia imetazwamwa na watu bilioni moja , ‘Endorsement’ ya Christen imefanya kazi kubwa katika mafanikio haya na mashabiki zake wanatarajia kumuona katika filamu nyingine tofauti”Aliongea Nasra.
“Kupitia hio filamu ameingiza kiasi gani kwa kampuni na yeye binafsi?”Aliuliza Amina
“Kulingana na makato ya kimkataba na kampuni Sophia ameweza kupata kiasi cha bilioni tano za kitanzania na kampuni inapata bilioni saba za kitanzania , japo hizi ni namba ambazo hazipo Fixed kwani mauzo yanaendelea”
“Kwa maneno yako ni kwamba Sophia siku hizi amekuwa maarufu kuliko mwanzo”Aliongea Roma huku akiona hio ni hatari zaidi kwani kadri Sophia anavyozidi kuwa maarufu ndio ugumu wa mahusiano yao.
“Honey kwanini usimpigie simu , ukamjulia hali?”Aliuliza Amina.
“Kwasasa hapana, Sophia yupo makini na ni mueelewa na isitoshe kwasasa atakuwa bize , haina haja ya kumsumbua”
Baada ya kuongea na warembo hao kwa muda mfupi Amina na Nasra ndio waliokuwa wa kwanza kuondoka, huku kila mmoja akiwa na miadi ya kibiashara.
Roma yeye baada ya kucheza cheza gemu na Lanlan hatimae alianza kusinzia na Qiang alimchukua na kwenda kumlaza.
Roma mara baada ya kuona hana cha kufanya aliamua kutoka na kuelekea mjini kwa mara nyingine kumtafuta Rufi.
Ijapokuwa Rufi alikuwa akiishi na mama yake , lakini pia alikuwa akiishi katika Apartment aliokuwa akiishi mwanzo lakini alikuwa ameigeuza kama ‘Computer lab’ sehemu ya kufanyia maswala yake yanayohusiana na tehama.
Ilikuwa ni kama maabara kutokana na wingi wa tarakishi ambazo zliokuwa zimefungwa na Rufi mwenyewe.
Roma tokea mara ya mwisho kufika hapo hakuwahi kwenda tena na mara baada ya kufika awamu hio alishangaa kukuta vitu hivyo na alishindwa kuelewa ni kitu gani ambacho Rufi alikuwa akifanya kupitia hizo tarakishi lakini hata hivyo hakutaka kuhoji sana.
Lakini kwa wakati mmoja alishangazwa na uwezo wa Rufi , kwani Rufi maisha yake yote alikulia katika ulimwengu wa majini lakini muda mchache ambao aliishi katika ulimwengu wa kawaida alikuwa amekusanya maarifa mengi sana kuhusu tarakishi , lilikuwa jambo la kushangaza kwake kwa wakati mmoja.
“Umefanikiwa?”Aliuliza Roma mara baada ya kumsogelea Rufi aliekuwa amekondolea Code za Programng akionekana kuunda Software.
Upande wa Rufi alikuwa ashajua ujio wa Roma tokea muda mrefu kwani yeye ndio alifungua mlango kwa njia anazozijua yeye bila ya kuamka kwenye kiti chake cya mzunguko.
“Nimefanikiwa kwa urahisi , shukrani kwa kinipatia access terminal za satilaiti yako ya Crogo, kwasasa nilichoweza kuona hapa ni kwamba karibia wanafamilia wote wa ukoo wa Ibuyawanga wamekusanyika mkoani kilimanjaro na hakuna ambaye ametoka”
“Vipi kuhusu eneo alipo Asha?”Aliuliza Roma na palepale Rufi alibonyeza tarakishi haraka haraka na ndani ya sekunde tu ramani ya mkoa wa kilimanjaro na mkoa wa Arusha kwa pamoja iliweza kujitandaza kwenye skrini.
“Yupo pia ndani ya eneo moja , kwenye hiko kidoti chekundu”Aliongea Rufi , ilikuwa rahisi kupata uelekeo wa Asha mke wa Waziri wa
Mazingira kwa kutumia namba ya simu yake.
“Kazi nzuri Rufi , ninachotaka sasa ufanye ni kumtumia meseji kwa namba isiokuwa na jina ukimweleza kujileta yeye na mtoto wake mbele ya Najma na kuomba msamaha kwa kusujudu au vinginevyo makazi yao yatageuka majivu”Aliongea Roma.
“Vipi kama angefika na kuyamaliza , si ungemfanya Najma kutoa hasira zake kwa kumpiga?”Aliuliza Rufi.
Ukweli ni kwamba siku ambayo Roma alienda kumtoa Najma alimkuta akifanyishwa kazi na polisi mmoja aliefahamika kwa jina la Catheryn , kitendo kile ambacho Roma aliweza kushuhudia Najma akifanyiwa na Afande huyo kilimuuzi kabisa na alimlazimisha Najma kulipiza kisasi kwa kumvunja mkono huyo Afande , Najma mwanzonni alikataa lakini Roma alimlazimisha kwa kumfokea na mwisho wa siku Najma alitoka gerezani akiwa amevunja mkono wa Afande Catherine Bonge.
Ijapokuwa hayakuwa makosa ya Afande Catherine Bonge kumnyanyasa Najma lakini Roma aliona kitendo cha kukubali uovu kwa ajili ya hongo malipo yake ni maumivu.
Najma alikuwa mpole sana na hilo Roma halikumpendeza na aliona kama Najma ataendelea kuwa mpole basi haitokuwa na maana kabisa hata ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
“Usiwe na shaka , najua hata kama tumtumie hizo meseji hawezi kuja , kwanza hata msamaha wenyewe hakujisumbua kuomba zaidi ya kutaka kunilipa hela , mtu kama huyu anajiona matawi ya juu na lazima ashushwe kwa lazima, mpango wangu ni kwenda kutia moto makazi yao leo usiku”Aliongea Roma.
“You are indeed Nasty”Aliongea Rufi ..





SEHEMU YA 647.
Upande mwingine mkoani Kilimanjaro katika makazi ya kifahari ya famiia ya Ibuyawanga alionekana Bi Asha au Farha kwa jina lake lingine akiwa amevalia mavazi ya kulalia huku mkononi akiwa ameshikilia mvinyo.
Alikuwa amesimama kwenye dirisha ambalo limetengenezwa kwa usanifu wa mtindo wa kifaransa(French Window) , mtindo ambao ulifanya dirisha kuwa kubwa kiasi cha kulingana na urefu wake na kumfanya kuweza kuangalia mandhari ya msitu akiwa ndani ya jumba hilo katika horofa ya tatu.
Baada ya kugeuza kichwa chake nyuma yake alikuwa ni mume wake waziri wa Mazingira aliekuwa amekaa juu ya kitanda kikubwa cha sita kwa sita huku pembeni yake kukiwa na tarakishi ya kampuni ya Apple na mbele yake kulikuwa na Runinga kubwa ya nchi 83 ya teknolojia ya Oled iliokuwa ikionyesha habari za kimataifa kupitia chaneli ya Aljazeera.
“Mpenzi , je hizo taarifa za kimpropaganda zinakuvutia zaidi kuliko mwanamke mrembo kama mim?”Aliongea kwa mapozi ya kimitego lakini Waziri hakuonyesha kumwangalia kwani alikuwa bize akiangalia habari ya kimapigano huko Urusi na Bi Asha ambaye alikuwa amevaa vazi la kimitego alisimama mbele ya mume wake.
“Huh.. uliniambia meneno matamu ya kuvutia kipindi ambacho ulikuwa ukinitongoza mpaka nikakubali kuolewa na wewe baada ya kifo cha mkeo , sasa ushanioa unaonyesha kutonitamani tena , hauogopi naweza kukuacha muda wowote , isitoshe sio kama nilikubali kuolewa na hela zako , kama ni hela baba anazo na ananipenda mno na kunidekeza”Aliongea.
Waziri mara baada ya kusikia neno ‘baba yangu’ palepale alishituka , hakutaka kukosa sapoti kutoka kwa familia ya mke wake kwani alikuwa na mpango wa kugombea uraisi mara baada ya Raisi Senga kumaliza uongozi wake.
Ukweli ni kwamba hakumuoa mwanamke huyo kutokana na kwamba alikuwa akimpenda bali alimuoa kwa ajili ya kutimiza mipango yake ya kuwa raisi wa nchi hii, hivyo hisia zake zidi ya mwanamke huyo zilikuwa ni za kufosi sana.
Ili kutomkasirisha mrembo huyo aliefanya upasuaji wa sura na umbo palepale alinyayua uso wake na kumwangalia na kisha akatoa tabasamu na kutoka kitandani na kisha alimshika kiuno chake na kumkalisha kwenye kitanda na kuanza kumfanyia Masaji.
Upande wa Asha alijiona mshindi na alitoa tabasamu la kejeli baada ya kuona kwamba alikuwa na uwezo wa kumfanya Waziri wa Mazingira kumfanyia masaji.
“Kutokana na ubize wangu najikuta nakosa muda wa kukaa kama hivi na kuangalia habari , lakini hebu muone unapenda kujifanyisha mtoto kila tunapokuwa pamoja , tumeona muda mrefu mno bado tu unataka kuwa kama msichana mdogo”Alijitahidi kubadilisha kutoridhika kwake kwa kuchomekea maneno ya kumpumbaza lakini pia na ya kijembe.
Asha alitaka kuchukua glasi ya mvinyo wake ili kunywa kidogo huku akichanua miguu yake kwa mtindo wa helufi V ili kumfanya mwanaume huyo kufanya kazi ya kumfurahisha lakini zoezi lake liliingiliwa na ujumbe wa meseji kwenye simu yake.
Baada ya kuchukua ile simu na kuangalia ujumbe wenyewe furaha yake ilipotea.
“Nini tatizo mke wangu?”Aliuliza mheshimwia baada ya kuona mabadiliko ya Asha.
“Ni ujumbe mwingine wa kunidhalilisha , hebu achana nayo tu”Aliongea lakini licha ya hivyo ilikuwa ngumu kwa Waziri Nguzo kupotezea swala hilo na alishikilia paja la mwanamke huyo kwa nguvu.
“Kuna kitu unanificha, kama ni swala kubwa unapaswa kunishirikisha”
“Kama huna mambo ya kufanya ni bora ukaweka
ubize kudili na watoto wako wawili wa kiume”Aliongea.
“Huh .. nini Tatizo la Ayubu na Salihi?”Aliuliza mheshimiwa huku akikunja sura.
“Tabia zao sio nzuri , hivi unajua kwamba Salihi jana alifanywa kubewa kurudishwa nyumbani baada ya kulewa yeye na kaka yake, kaka yako alikuwa akicheka sana matendo ya watoto wako kwasababu wa kwake wamekua katika maadili , ikiendelea hivi hakuna yeyote ambaye anaweza kupata urithi , leo ni siku ya ibada ya kimila na jini Husna bado hajachagua mrithi, lakini bado tu analewa , ataongozaje ibada ili hali ananuka pombe , unajua mwenyewe hawezi kuingia madhabahuni akiwa amejinajisi”Aliongea kwa kulalamika.
“Lakini hio ni kazi yako ya kuwaangalia , unajua mimi nipo bize na maswala yangu ya kisiasa na wewe ndio mama yao kwanini usiwazuie?”
“Unajua mwenywe wananiona kama kituko kwasababu tu mimi ni mama yao wa kambo , isitoshe mtoto wako mkubwa hata wewe mwenyewe sidhani kama anaweza kukusikiliza , au nasema uongo?”:
“Huyo mpuuzi anathubutu vipi , hebu leo toa maagizo Salihi atakaa na mimi karibu na Ayubu mwambie achukue nafasi ya Salihi kwani na yeye pia anaweza kuongoza ibada”Aliongea.
Asha aliishia kutoa tabasamu ambalo kwa nje lilionekana kama la roho nzuri lakini ndani yake limejaa unafiki , alijiambia huyu mwanaume anaonekana kujiamini lakini ni mdhaifu , nani angeweza kutegemea mwanaume ambaye anaheshimika kama waziri na pia mtoto wa pili wa mzee Sharifu kuwa dhaifu hivyo na sio tu mbele ya watoto wake lakini mpaka kitandani.
Hakupenda tu tabia ya kulewa kwa Salihi kwani mara nyingi huishia kulala na changudoa na kama sio hivyo asingejisumbua kumfatilia.
Baada ya Waziri kutoa maagizo hayo hakuongea zaidi na alijikuta akianza kumridhisha mke wake kwa kutumia mdomo na ulimi.
*****
Upande mwingine Roma mara baada ya kuachana na
Rufi aliweza kupokea ujumbe kutoka kwa Samweli
Nguluma ikimpa taarifa mzigo unakaribia kufika Kilimanjaro na ili kusitokee polisi kuunasa basi anapaswa kuwepo mwenyewe.
Roma mara baada ya taarifa hio alitoa tabasamu na kisha alianza safari ya kuelekea mkoa wa Kilimanjaro.
Alitaka kutumia usafiri wa gari lakini aliona ingemchukua muda mpaka kufika hivyo alichagua ndege kuelekea huko.
Ratiba za ndege kuelekea mkoani kilimanjaro zilikuwa ni nyingi sana kutokana na upande huo kuwa sehemu ya kitalii zaidi na wasafiri wengi wanaofika Dar es salaam walikuwa wakielekea Kilimanjaro hivyo saa kumi na moja na nusu Roma aliweza kupanda ndege ya shirika la Taifa.
Ilimchukua dakika kama sabini tu kuwa angani mpaka kufika Kilimanaro na kutoka nje ya uwanja wa ndege.
Roma ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika mkoani Kilimanjaro hivyo baada ya kushuka tu kwenye ndege alipiga namba ambayo alitumiwa na baba yake Benadetha na kutoa maagizo na ndani ya dakika hio hio alimpatia mwendesha Taksi simu na baada ya bwana yule kuongea kwa dakika akionekana kupokea maelekezo Roma aliingia ndani ya gari.
Giza lilikwua lishaingia tayari na baada ya Roma kutoka nje kidogo ya Wilaya ya Hai gari ile ilisimamishwa nje ya duka moja la vifaa vya spare za magari , sehemu iliokuwa na gereji pembeni na Roma alilipa na mwendesha Taksi aliondoka.
Roma mara baada ya kusogelea duka hilo aliweza kukutana na kijana alievalia Shati kubwa la mtumba oversize la draft na buti zake kubwa na Jeans akivuta sigara.
Roma hakushangazwa sana na mavazi hayo kutokaa na uzoefu wake wa maeneo mengi na alimsogelea na kisha akampatia tano.
“Wewe ndio Mr Roma!, Boss amenionyesha picha yako , unaweza kuniita Paskali au Mr P”Aliongea kwa rafudhi yake ya kichuga chuga huku akimpatia Roma sigara, Roma alikataa na kisha aliingiza mkono kwenye koti lake la suti na kisha akampa pakini nyingine ya sigara na bwana yule mara baada ya kuiangalia alionyesha kuona jina geni lakini alishukuru na kuiweka mfukoni.
“Asante kwa kunisubiria Mr P , vipi nimechelewa sana na kuharibu ratiba zako nyingine?”Aliongea Roma kwa upole na uongeaji wake ulimfanya bwana yule kuonyesha tabasamu na hali ya kujisikia vizuri.
Ijapokuwa alikuwa akiaminiwa sana na Bosi wake Samweli Nguluma na kupewa kazi zinazohitaji ufanisi wa hali ya juu lakini hata bosi wake hakuwa akimpa heshima kulingana na msaada wake , lakini Roma ambaye alikuwa akimjua kama mtu mzito alionyesha kuwa Humble , ilimfanya kujisikia vizuri.
Mwanzoni alijua Roma asingemjali sana kuhusu yeye na angekuwa ni kama mabosi wengine ambao anakutana nao lakini baada ya kumuona kama mtu asiejikweza ilimpa motisha ya kumsaidia.
“Hapana kabisa bosi wangu , hii ndio kazi yangu hivyo hata ungekfika usiku usingeniharibia ratiba”Aliongea akijitetea na Roma alitingisha kichwa kumuwelewwa.
“Vipi una mzigo wangu?”Aliuliza Roma huku akikagua mazingira ya watu waliopo , kulikuwa na mafundi makenikia waliokuwa wakihangaika na magari makubwa ya mizigo ndani ya hilo eneo.
“Ndio mzigo umefika mapema tu nusu saa iliopita, na jambo la bahati hakuna sehemu polisi walipotusimamisha na kutukagua”Aliongea Paskali huku akisimama na kutembea na Roma upande wa pili kwenye geti ambalo lilikuwa lina ukuta mkubwa ulioenda hewani na baada ya kuingia ndani waliweza kukutana na gari kubwa yenye bodi la Kontena nyeupe lenye nembo shirika la Bohari ya dawa MSD.
Paskali alifungua haraka haraka na kisha akamuonyesha Roma kilichopo ndani yake na kumfanya atoe tabasamu huku akimpongeza ndani kwa ndani Samweli nguruma kwa kuongoza kuwa mhalifu Tanzania maana kwa amani ya nchi hii hakuamini jambo lake lingekuwa rahisi namna hio.
“Asante bro , lakini vipi kuhusu hili gari , kuna uwezekano halitoweza kurudi tena hapa, kutakuwa na tatizo”
“Bila shaka bro , Bosi kaagiza kwamba kila kitu ni cha kwako , lakini unapaswa kuwa makini kwani mzigo huu ni hatari na unaweza kuigeuza hata hili gari kuwa majivu”
“Usiwaze , hivi vitu vinawafaa wao ila sio mimi”Aliongea Roma huku akijua kwamba uwezo wake hata kama gari hilo limlipukie hakuna uwezo wa kupata madhara.
Mwili wake ulikuwa sio wa kawaida na kulingana na data za Zeros organisation inaaminika kwamba kutokana na kumulikwa na miale ya teknoloijia ya jiwe la Kimungu anaweza kuwa hai hata akipigwa na bomu , hapo ni kabla haijajumuishwa uwezo wake wa kijini.
Paskali hakujua kuhusu hilo , pengine alikuwa akijua ni nani anakwenda kushindana nae , lakini bosi wake alimwambia kutokuuliza maswali mengi, lakini bado alikuwa akijiuliza inawezekanaje mtu mmoja kwenda kukamilisha kazi ya hatari namna hio.
Roma mara baada ya kukabidhiwa mzigo wake hakutaka kundelea kubakia hapo aliingia ndani ya gari hilo na kisha aliliwasha na kulitoa nje kwa mbwembwe na baada tu ya kuingia barabarani alimpigia simu Rufi.
“Rufi nipe uelekeo?” Aliongea Roma.
“Subiri kidogo?”
“Kuna tatizo”
“Uelekeao wa Asha naona umebadilika , tofauti na kwenda moja kwa moja geti la mbele yake , unapaswa kuzunguka nyuma , kilomita mbili kutoka ulipo kuna barabara inayoeleka kulia kwako chukua hio na utakuta geti mwisho kabisa wa barabara upande wa kusini karibu na msitu”
“Nini kimebadilika?”
“Nimejaribu kudukua mawasiliano ya mmoja ya wanafamilia , inaonekana kuna ibada ya kimizimu ambayo inafanyika kwenye Madhabahu yao iliopo maili moja kutoka yalipo makazi , inaangaliana na geti la upande wa kusini”Aliongea Rufi na palepale Roma alitoa tabasamu lililojaa uovu ndani yake.
“That is perfect , itaniokolea muda wangu kuzunguka zunguka sehemu moja kwenda nyingine , naona hata Mungu mwenyewe ananisaidia katika hili”Aliongea Roma.
“Babe hio familia inamiliki eneo kubwa mno , ninawasiwasi itakuwa ngumu kuharibu makazi yao yote, isitoshe wana watu wengi sana ambao pia ni wafuasi wao ,, kama mpango ni kuchoma moto basi uwezekano wa kuzimwa kabla haujakithiri ni mkubwa”Aliongea.
“Tutaona kitakachotokea , lakini hakikisha unanipatia taarifa kwa kila kinachotokea”Aliongea Roma na kisha alikata simu na kuseti ramani yake vizuri na kuendeleza safari.
Inasemekana kwamba ukiachana na Mzee Sharif wakati huo akijulikana kama muislamu alieshika dini lakini ilionekana ilikuwa ni kujionyesha tukwani alikuwa ikisalia kitu kingine kabisa.
Jambo hilo liliwakasirisha sana watu wa dini enzi hizo na kumpa onyo mara kwa mara kuachana na
Ukafiri wa kuasi dhidi ya dini ya kiislamu lakini
Mzee huyo hakutaka kuacha huku akiamini kwamba anachokifanya ni kuendeleza urithi ulioachwa na mababu zake.
Ilishangaza sana kwa mzee kama huyo kuwa na msimamo wa aina hio na hata baadhi ya watu walihoji kwanini alikuwa na msimamo wa aina hio , je kuna kipi cha siri juu ya mungu anaemsalia lakini hakukuwa na majibu kwani ilikuwa ni siri yake.
Mzee Sharif alikuwa ni raia wa nchi ya Kuwait na inasemekana alikuwa na utajiri wa kutisha sana unaotokana na madini pamoja na kumiliki visima vingi vya mafuta na hili lilimfanya kuogopwa na watu hata pale ambapo alikuwa akisalia miungu anayoijua yeye.
Upande wa serikali ya Marekani kupitia kitengo chao cha CIA walimtumia Tajiri Sharif kutaka kuipa kampuni yao ya Gulf Oil Corporation nguvu ya Ihtikar(Ukiritimba) wa kusafirisha mafuta yote kuingia nchini kwao lakini pia kuwa wasambazaji pande nyingine za dunia.
Serikali ya Marekani ilimtumia tajiri Sharif kutokana na kumuona kama ‘Weak point’ kutokana na msimamo wake wa kidini na waliweza kufanikiwa kwani waliweza kutumia tabia yake kwa manufaa , kwa mfano Mzee Sharif ukiachana na dini yake alipenda sana pesa na ni kupitia pesa iliomfanya kusaliti nchi yake na baada ya kushitukiwa ndio ikawa mwisho wa nguvu yake ndani ya taifa hilo kwani ilikiwa ni kama ule uvumilivu waliokuwa nao Raia juu ya Mzee huyo ulifika ukingoni..
Katika hatua za kujiokoa Mzee huyu aliweza kutolewa na serikali ya Marekani pamoja na mali zake na kukimbilia hapa nchini Tanzania na huo ndio ukawa mwisho wa kampuni ya Gulf Oil nchini Kuwait , kwani ilitaifishwa na serikali rasmi, hio ni historia iliomtokea Mzee Sharif miaka hio ya sabini.
Kabla ya kuja nchini Tanzania aliishi Marekani kwa miaka miwili mfululizo na katika miaka hio alitumiwa na Serikali ya Marekani kama Asset ya kutoa taarifa za uchimbaji wa mafuta nchini Kuwait , taarifa ambazo ziliifanya serikali hio kuweza kutengeneza mirija yao nchini humo.
Inasemekana baada ya kuishi miaka miwili nchini
Marekani ndipo alipofanya maamuzi kuhamia nchini Tanznia huku sababu kubwa alisema kwamba mungu anaemsalia kalichagua taifa hilo.
Serikali ya Marekani ikatumia ubabe wake na kuhakikisha Mzee huyo anapata eneo nchini Tanzania na permanent guaramtee protection , ni kweli raisi wa kipindi hicho aliweza kuidhinisha
Mzee Sharif kuuziwa eneo kubwa sana huko mkoani Kilimajaro na makazi yake yakaanzia hapo , ijapokuwa swala hilo mwanzoni liliibua sintofahamu kwa raia lakini ilikuwa ni kama upepo ambao huvuma ukiwa unasafiri mpaka kutoweka..
Baada ya kukaa nchini Tanzania mzee huyo alijenga eneo hilo makazi ya kifahari sana na mwanamke wa kwanza kumuoa alikuwa ni Mzanzibar na ilisemekana baada ya kujifungua tu alipoteza maisha hapo hapo , akaoa mwanamke mwingine ambaye alimzaa Waziri Nguzo na baada ya kujifungua na yeye alikufa hapo hapo.
Kitendo cha kufairki kila mwanamke ilianza kuibua maswali kwa ndugu wa familia ya mke lakini Mzee huyo aliweza kuzima kila skendo na maisha yakaendelea.
Lakini ajabu ni kwamba utaratibu huo haukuishia kwa yeye tu hata kwa watoto wake baaada ya kuoa kila mwanamke anaejifungua anakufa siku hio hio , lakini utofauti kidogo ulionekana kwa Waziri Nguzo kwani mke wake alijifungua mara mbili mtoto wake wa Kwanza ambaye alimwita jina la Ayubu na kisha baada ya kuzaliwa kwa Salihi ndio akafariki na ndipo alipokuja kumuoa Asha.
Asha mpaka wakati huo hakuwa amejifungua mtoto yoyote na Waziri na hakuwa na mpango huo wa kuzaa ili atolewe kafara.
Ukiachana na maswala ya ndani ya familia Mzee Sharifu alijitambulisha kama Mtanzania halisi na tokea kuishi kwake Tanzania alijijengea koneksheni za kisiasa kwa namna ya kipekee sana , kwanza hakuwa akichagua upande wowote wa kuungana nao bali alitumia pande zote ndani ya Tanzania kujinufaisha , ukichana na maswala ya kisiasa pia alikuwa ni tajiri mkubwa sana ambaye alikuwa na biashara nyingi za mabasi pamoja na vituo vya mafuta nchini, ukiachana na biashara zake za kihalali lakini pia alikuwa akijihusiha na biashara nyingi za kimagendo ikiwemo uuzaji wa madawa pamoja na pembe za Tembo.
Hivyo kuingia kwa Mzee Sharif nchini ilikuwa ni kwa msaada wa serikali ya Kimarekani.
Lakini ukiachana na hayo kuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea ambayo ilifanya serikali ya Tanzania kutoweza kumgusa kwa kipindi kirefu sana.
Ndani ya eneo hilo familia nzima ilikuwa imekusanyika kama ilivyom desturi yao kukusanyika kila ifikapo mwisho wa mwaka na kufanya ibada za kimila kumsalia mungu wao.
Katika kipindi hicho familia inapokusanyika ulinzi unakuwa mkali sana kuliko siku zote na ikiwa ni saa mbili za usiku walinzi waliokuwa na siraha nzito walikuwa wakiimarisha ulinzi kiasi kwaba hata paka akitaka kuingia ndani ya eneo hilo angeweza kuonekana.
Sasa ikiwa ni mwisho mwisho wa ibada wakati wakipata chakula cha usiku ghafla tu walinzi walishituka mara baada ya kuona gari linalowasha taa kuja upande wa geti la kusini huku likiwa na kasi kubwa.
Eneo hilo licha ya kujengwa barabara nzuri ya viwango vya lami haikuwa ikitumika mara kwa mara hususani nyakati za usiku hivyo kusogea kwa gari hio kuliwapa mashaka walinzi.
Kilichoshangaza zaidi ni kwamba gari hio haikuonekana mwanzoni kabisa na ilikuja kuonekana
ikikaribia geti , pengne hata kama haikuwa ikinguruma vipi kuhusu taa zake.
Ukweli ni kwamba Roma alitumia mlima wa eneo hilo kuendesha gari pasipo ya kuiwasha na licha ya pia kuwa na giza hakuathirika kuendesha gari , alifanya hivyo ili kuwapa surprise na wakati anakaribia geti ndio aliwasha taa sasa na kupiga honi mfululizo.
Muda uleule walinzi kadhaa waliokuwa ndani walitoka nje ya geti na kisha wakasimama katikati ya barabara kuingia getini huku wakiipa ishara ya kusimamisha lakini kutokana na mwendo wa gari hio waliona kabisa hakuna dalili ya kutosimamishwa
Walinzi walijikuta wakipigwa na mshangao na walihofia pengine gari hio imekosa breki ndio maana ilikuwa kwenye mwendo mkali namna hio .
Hali ya makelele pamoja na msuguano wa tari za gari na barabara ilikuwa ni kama vile ni mnyama ambaye anakaribia kuwararua
Dakika ileile ambayo wanakumbuka siraha zao na kutaka kushambulia gari ilikuwa tayari ipo mbele yake na kabla hata hawajajipanga.
“Bang!!”
Gari ile iilingia na geti na kupita huku likiharibika na walijikuta wakitoa yowe huku baadhi ya walinzi wakipata majeruhi na Roma hakujali anaekufa.







SEHEMU YA 648.
Upande wa familia ya Mzee Sharif baada ya ibada walikusanyika katika eneo moja kwa ajili ya chakula cha usiku.
Ilikuwa ni familia kubwa kweli ikiunganishwa mpaka na pande za wajomba.
Mzee Sharif pengine ndio mtu ambaye ameishi miaka miaka mingi sana ndani ya taifa la Tanzania , inasemekana ana miaka mia moja na ishirini lakini bado alikuwa na nguvu zake licha ya kuonekana mzee sana.
Na swala hilo lilishangaza hata watu wa nje ya familia hio , lakini ukweli ni kwamba kuna siri nyingi sana juu ya Mzee Sharif mwenyewe ambazo pengine hata watoto wake hawakuwa wakizijua.
Wakati wakiongea kwa furaha na kucheka palepale alikuja kiongozi wa Walinzi bwana mweusi ambaye kwa kumwangalia tu ni Mmasai ambaye ameachana na tamaduni zao.
Kabla hata yule bwana hajaongea neno lolotea ghafla tu king’ora kilianza kutoa mlio na kufanya watu wote kukurupuka.
“Uvamizi!!”Mzee Sharif ndio aliekwua kwa kwanza kuongea hayo maneno huku watoto wake na wajukuu wake wake wakifatia kushangaa
Mfumo wa alarm ya nyumba hio tokea uwekwe ni zaidi ya miaka kumi iliopita na haijawahi kutokea hata siku moja ikatumika , hivyo swala hilo halikuwa la kawaida kabisa.
“Kimyaa..!!”
Mzee aliongea kwa sauti kubwa akitumia lugha ya kiswahili na sauti yake iliiibua hofu ambayo sio ya kawaida kwa wanafamilia hao , kwani aliogopesha , ijapokuwa alikuwa mzee lakini mkandamizo aliokuwa akisambaza haukuwa wa kawaida hata kidogo.
“Kuna nini?”Aliuliza akimwangalia yule mlinzi. “Kuna mtu amevamia geti na fuso na sasa inaonekana anaeleka upande huu bosi”Aliongea kwa hali ya kutetemeka.
“Unasema kuna mtu katuvamia na Fuso , tena ndani ya eneo langu haha… pamoja na uzee wangu huu wa kuishi miaka mingi sijawahi kutegemea mchezo
wa aina hii kutokea , pengine nakaribia kufa”Aliongea na palepale alimgeukia mtoto wake mkubwa ambaye ni mfanyabiashara.
“Wewe mtukutu , hebu chukua walinzi wote waliomo humu ndani tuelekea upande wa getini”Aliongea.
“Baba , ngoja nitafute mtu wa kumuua , wewe huna haja nya kujisumbua kuamka hapa unapaswa kuendelea kula chakula”Aliongea Waziri.
“F**ck you , acha kujifanyisha mjuaji mbele yangu?”Aliongea na palepale alimpiga teke Waziri na alijikuta akidondoka na kiti chake chini kama furushi.
Kila mmoja alishangazwa na jambo hilo , hakuna ambaye alitegemea mzee huyo angekuwa na nguvu ya kumpiga Waziri mwenye mwili mkubwa na kudondoka namna hio .
Naibu waziri Salihi , Asha na wengine wote walijikuta wakiwa katika mshituko kwani mzee ambaye siku zote walimzoea kumuona akitembea na mkongojo leo hii alionekana kuwa na nguvu kiasi cha kunyanyua mguu wake bila msaada wowote na kutoa kichapo.
Baadhi ya walinzi walioshuhudia tukio hilo hawakushangazwa ni kama walishamshuhudia mzee huyo kufanya kitu kama hicho na uzee wake.
Wanafamilia hao walikuwa wakijua kwamba utajiri wao na nguvu yao ndani ya Tanzania haikutegemea koneksheni , na utajiri waliokuwa nao bali kile walichokuwa wakimiliki, kitu cha siri sana ambacho pengine hakuna mtanzania wa aina yoyote angeweza kutegemea kama kinamilikiwa na Mzee huyo.
Ndio kitu ambacho kilimfanya Mzee huyo kufurumushwa kwenye nchi yake na kukimbilia nchini Tanzania na kuendelea kukiabudia.
Dakika ileile ni kama jeshi limekusanyika kwani kila ndani ya eneo hilo walinzi waliweza kukusanyika sehemu moja na Mzee huyo akiwa ametangulia alianza kutembea kueleka uelekao wa geti ambalo limevunjwa.
Jengo hilo la ibada ambalo hutumika kwa ibada ililikuwa lipo katikati ya eneo hilo , lakini likiwa karibu zaidi na geti kubwa ambalo ipo upande wa kusini , upande ambao una msitu mkubwa.
Geti la upande wa Kaskazini ndio ambalo lilikuwa karibu na makazi ya watu na la upande wa Kusini ndio ambalo lilikuwa likiunganisha na barabara inayoingia msituni.
Dakika ileile ambayo Mzee Sharif anafika akiongozana na familia yake , kila mmoja alijikuta akipagawa baada ya kuona tukio hio kwani kilichoharibiwa sio geti tu bali hata jengo lao la ibada eneo la mlangoni lilikuwa limevamiwa na gari hilo na ni vumbi tu lilikuwa limetanda.
Baada ya kufika karibu mzee alijikuta akipatwa na ahuenni mara baada a kungundua kilichoharibika ni uzio na mlango tu na eneo la ndani hakuna kilichoharibipka , pengine ni kutokana na uwepo wa ngazi nyingi kwenda juu kuingia madhabahuni.
Roma alikuwa akisbiria wote wakijikusanye eneo moja , mwanzoni alifurahi kwamba angewakuta wakifanya ibada lakini alichukia mara baada ya kugundua amechelewa na washasambaa, lakini hakujali baada ya kutoka nje ya gari alisimama juu ya ngazi na kutoa sigara yake na kuiwasha huku akisubiria wote wajitokeze.
Baada ya Asha na Salihi kumuona Roma walijikuta wakipigwa na mshituko wa aina yake na kujiuliza mtu huyo alikuwa kaifanya nini hapo.
Mzee Sharif akiwa na hali yake ya uzee alimwangalia Roma kwa macho ya mshangao kwani hakutegemea mtu aliefanya uharibifu nyumbani kwake kwa kuvamia alikuwa wa kawaida sana.
Eneo hilo licha ya kwamba lilikuwa ni usiku lakini taa za Spotlight zilikuwa zikimulika na kufanya liwe kama mchana.
“Hahaika una uasiri wa aina yake , wewe ni nani?”Aliuliza Mzee huyo kwa kiswahili fasaha.
“Baba haina haja ya kuongea nae , muue”Aliongea Waziri , hakumchukia baba yake licha ya kupokea kipondo cha teke.
“Kimya , hujaruhusiwa kuongea”
Roma alijikuta akishangaa mara baada ya kumkagua huyo mzee, ijapokuwa uwezo wake wa kijini ulikuwa dhaifu kuliko mwanzo lakini mara baada ya kumchunguza Mzee Sharif aliweza kugundua alikuwa na nguvu za kijini ndani yake.
Roma kama alivotarajia , hakuwa mtu wa kawaida kabisa mara baada ya kupewa historia ya mzee huyo pamoja na nguvu zake , ni kama kile alichoshuku kimepata majibu yake, lakini ilimshangaza kwa kuona mtu wa aina hio kujichimbia hapa Tanzania na kuitawala nchi nyuma ya pazia.
Kilichomleta Roma ukiachana na kutaka kulipiza kisasi chake , ni shauku yake aliokuwa nayo kulingana na maelezo ambayo ameyapata kutoka kwa Omari.
“Oii..Asha hapo , nimekutumia meseji mara kibao lakini ukaamua kunidharau , unafikiri nilichokuwa nikikuambia nilikuwa natania , vipi sasa hivi , je upo tayari kunisujudia?”Aliongea Roma akimnyooshea kidole mwanamke Asha aliekuwa amevalia Abaya ya rangi nyeusi.
Na muda huo huo Roma aliwasha sigara nyingine na kupiga pafu la moshi na kuutoa kwa pua kama vile ni gari moshi.
Asha miguu yake ilikuwa ikimtetemeka mno na watu wote walijikuta wakimwangalia kwa macho ya kiulizo.
“Asha nini kinaendelea?”Aliuliza Waziri wa Mazingira baada ya kukumbuka muda ambao alimuuliza mwanamke huyo na akapotezea swali lake.
Asha hakupata tena ujasiri wa kuongea uongo na palepale alisogea mbele ya Mzee Sharif.
“Baba nimekosea sana , nimekosea familia yote ya Sharif lakini nilikuwa na sababu zangu”Aliongea kimaigizo.
“Niambie nini kilichotokea?”Aliongea Mzee Sharif na palepale Asha alianza kuelezea tukio la Najma huku akibadilisha ukweli.
Alisema kwamba Najma alikuwa akimtega Salihi kwa ajili ya kupata nafasi kubwa zaidi ndani ya wizara na kusema kwamba alijaribu kumpa hadi onyo lakini kaishia kutukanwa hivyo akaagiza watu wake kumpa onyo kwa kuharibu gari yake na baada ya hapo polisi wakafika na kumpeleka kituoni kwa ajili ya mahojiano lakini Roma akafika na kumtoa huku akiongezea kwa kusema kumbe alikuwa akicheza kotekote.
“Baba walitaka niende nikawasujudie lakini mimi nikakataa na kuwaambia kwamba nitawafidia kwa kitu kingine lakini hakukubaliana na hilo , sikutegemea kama ataenda mbali hivi , ni makosa yangu baba naomba uniadhibu”Aliongea huku akicheza mchezo wa akili.
Kwa wanafamilia hao ambao walikuwa wakimjua tabia yake waliona pengine stori aliotoa ni ya kutengeneza lakini licha ya hivyo alikuwa akichukuliwa kama mwanafamilia
Licha ya kwamba familia ya Roma ilikuwa na nguvu haikumaanisha kwamba Familia ya Sharif ilikuwa ikimuogopa na hata kama ni mzee mwenyewe Sharif asingekubali mwanafamilia kujishusha na kumsujudia Roma.
Kwao taswira yao ndio ilikuwa kitu kikubwa sana , na mzee huyo alijiona yupo juu kuliko watanzania wote na inasemekana alikuwa ameua sana watanzania ambao wamefanyakazi kwake na kuonyesha utomvu wa nidhamu.
Isitoshe pia waliona Roma hakuwa na sabababu ya kuwavamia kwani mtu ambaye ameguswa sio kwamba ni mke wake bali ni mchepuko tu.
Muonekano wa Mzee Sharif ulikuwa ni ule usio wa kusomeka kwa wakati huo.
Wanafamilia wote walikuwa wakimjua Roma na wameweza kusikia pia alikuwa na nguvu za kijini na wengi walikuwa wakimjua kama mtu mkatili sana.
Tokea Mzee Sharif kujua nguvu ya Roma na ukichaa wake alitahadharisha watoto wake kuwa neutral na kuhakikisha kwamba hawachokozani nae kwa namna yoyote ile lakini kitu ambacho pengine amekosea mzee huyo ni kutokumuonya Asha , pengine ni kutokana na kutegemea mume wake angefanya kazi hio.
“Wewe mtoto , najua uwezo wako , lakini umevuka mipaka awamu hii”Aliongea Mzee Sharif.
Roma hakujisumbua na palepale alisogelea nyuma ya gari lake na kisha akafungua mlango kwa nyuma kuonyesha mzigo ambao amebeba na wale waliokuwa wakijua wanachokiona ni nini walijikuta wakishikwa na mshangao.
Ilikuwa ni gari zima ambalo limejaa aina flani ya mabomu ambayo yakikutana na moto hutengeneza mlipuko.
Roma mara baada ya kuongea na Mzee Samweli
Nguluma alikuwa akihitaji mabmu aina ya C4 au RDX mzee huyo alimwambia kwamba hana uwezo wa kupata aina hayo ya mabomu lakini anaweza kumsaidia kitu kingine cha kusababisha milipuko, mwenyewe akiyaita mawe ya kutengenezea fataki au mabomu ya kienyeji.
“Mnaonaje , mwenye macho haambiwi tazama , ijapokuwa haya hayana nguvu kubwa kama bomu la kisasa lakini kwa wingi huu wa gari zima yatakuwa na uwezo wa kuunguza hilo jengo lote la ibada zenu za kipuuzi, yaani leo itakuwa ni show ya kuwangalia milipuko ya fataki angani hehe..”Aliongea Roma na kufanya watu wote kushikwa na baridi.
“Asha,, wewe mjinga , kwanini umeyasababisha haya”Aliongea waziri akimfokea mke wake , alikuwa akiigiza ili kuepuka lawama kutoka kwa baba yake. “Nguzo usitake kumbebesha mwanangu kila kitu , kama ungekuwa makini haya yote
yasingetokea”Aliongea baba yake Asha Mzee flani mwenye muonekano wa kihindi , alikuwa akifahamika kwa jina la Mzee Hamisi Maya , alikuwa ni mtoto wa Tajiri Maya kutoka india.
Baada ya mzee yule kuongea vile palepale alimgeukia Roma na kumwangalia kwa kejeli huku akikumbuka tukio moja ambalo aliliratibu yeye mwenyewe linalohusiana na Raheli mke wa Adebayo , yaani mama yake Edna.
“Wewe mtoto , unafikiri nchi hii ni ya kwako kwasababu tu raisi ni baba yako na unatokea katika familia ya Kweka , nakuambia awamu hii umegusa sehemu mbaya sana , jaribu kulipua hili eneo uone , nitahakikisha natoa koromeo lako nje”
“Unaongea sana , wewe nitakufanya uwe mfano kabla ya show yenyewe kuanza”Aliongea Roma na kisha aligeukia gari lake na kuchukua bomu moja na kulishika mkononi na kisha akamsogelea lakini palepale walinzi waliinua siraha zao wakimkinga kwa mbele.
“Simama hapo hapo , nitakuchukulia hatua na kukupoteza kama utaendelea na ujeuri wako , hakuna anekuogopa hapa?”Aliongea Mzee Sharifu akionya lakini Roma hakutishika na maneno yake na baada ya kuona analeta ujeuri alitoa ruhusa ya kushambulia.
“Traa.. tata,, tatata,, ta..”
Milindimo ya milipuko ya risasi ilianza kusikika mfululizo kiasi cha kutengeneza kiwingu lakini mpaka wanakuja kumaliza wakijua wamemaliza kazi Roma alikuwa mzima na ni sigara yake tu ilioharibika.
“Wewe ni nani … usiniambie ni yule mtu”Aliongea Mzee Sharif kwa woga akishindwa kuamini macho yake.
Edna yuko wapi , atarudiana na Roma kama Amina anavyosema atatulia , usikose.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA
MTUNZI: SINGANOJR



Mono no aware.

SEHEMU YA 648.
Alichokuwa akitaka kufanya Mzee Hamisi ni kujichukulia pointi mbele ya Mzee Sharif kwa kujaribu kumfokea Roma ili aonekane siku zote atasimama upande wao.
Pengine alijua labda Roma asingeweza kumfanya chochote kutokana na kwamba alikuwa peke yake na hana uwezo wa kushindana nao , labda hivyo ndio
alivyofikiria lakini ukweli ni kwamba ilikuwa kosa lake kubwa sana kunyanyua mdomo wake mbele ya Roma ambaye kwenye maisha yake hakupenda sana kutishiwa.
“Nyie watu hata shabaha hamna , angalau mlipaswa kulenga kichwa lakini ona sasa mmeniharibia sigara yangu”aliongea Roma huku akipotezea maneno ya Mzee Sharif na palepale kwa spidi kubwa aliruka na teke na kumpiga Mzee Hamisi kiasi cha kumfanya kudondoka chini na hakuishia hapo tu alimkandamiza na kiatu chake na kumfanya Mzee huyo kutema damu.
“Wewe mwanaharamu hebu muachie haraka”
“Baba..!!”
Asha hakuamini baba yake alikuwa amepigwa na pigo la namna hio na alikuwa akitema damu.
Walinzi wale licha ya kwamba mwanzo walijaribu kumshambulia Roma na kutoona mafanikio lakini walijaribu tena na kuanza kushambulia kwa awamu nyingine lakini kilichotokea ni nguo za Roma tu ambazo zilichanika.
“Nishaelewa nini nakwenda kufanya , nitakulisha hili bomu ndani ya mdomo wako”Aliongea Roma huku akitoa taasamu la kifedhuli.
Mzee Hamisi alitamani kupoteza fahamu lakini ilishindakana kabisa na kuzidi kuogopa kile ambacho kinakwenda kumtokea.
Wengine wote walikuwa wakiangalia tu kinachotokea na hakuna ambaye alikuwa na ujasiri wa kusogea kumsaidia Mzee Hamisi.
“Wewe mtukutu , unajua unachokifanya , hivi unafikiria tutakuacha ufanye unachotaka kwasababu tu una kiji uwezo?”Aliongea Mzee Sharif mara baada ya kumuona Roma akitoa kijipini ili kumlisha Mzee Hamisi bomu.
Mzee Hamisi anaweza kuwa sio mwana ukoo wao lakini alikuwa akitoka kwenye ukoo wa Mzee Maya hivyo kama angefariki mbele yao ingeathiri sana taswira yao.
Mzee yule aliona kama atachelewa kuchukua hatua basi atachelewa kumukoa mzee Hamisi.
“Acha”
Alifoka na kufumba na kufumbua tu aliikuwa ashapotea aliposimama na ile anakuja kuibukia alikuwa sehemu nyingine kabisa tena akiwa tofauti kabisa, yaani lile umbo lake la kizee lilipotea palepale.
Nguvu za kijini zilimtoka kwa wingi na ajabu ni kwamba kucha zake zilirefuka mithili ya Jini huku mikono yake ikiota manyoya.
Roma alishangazwa na jambo lile , ijapokuwa hakuwa na uwezo wa kutumia nguvu zake za kijini , alimuona hakuwa wa kawaida pia hivyo hisia zake ziliweza kumsoma Mzee Sharif kwa spidi yake ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Ile mzee Sharif anamkaribia kwa ajili ya kumshambulia, Roma alishamuona na ile anataka kuushika mkono wake na kucha zake ndefu Roma aliinama kuelekea chini na palepale akaachia ngumi ambayo ilimpiga Mzee Sharif kifuani karibu na bega lake la kulia.
Mzee Sharif alijikuta akitema damu , ngumi ile haikuwa ya kawaida na ni kama vile alikuwa amepigwa na jwe.
“Baba..!!”
“Boss!!”
Kila mmoja aliita, huku wale waliokuwa wakijua uwezo wake wakishangaa kuona Roma ameweza kumjeruhhi huyo mzee , sekunde moja iliopita walijikuta wakishangazwa na uwezo wake lakini baada ya sekunde moja nyingine alikuwa amepigwa pigo la kumfanya kutema damu.
Haikuwa kwao tu ambao walikuwa katika mshangao , hata Mzee Sharif mwenyewe alikuwa katika hali ya mshangao na taharuki , hakuweza kutarajia katika maisha yake anaweza kukutana na adui ambaye anaweza kumpiga pigo moja tu na kumjeruhi.
Aliweza kuona Roma hakutumia nguvu za kijini katika kumshambulia lakini ngumi yake ilikuwa na nguvu isiokuwa ya kawaida.
Mtoto wake mkubwa palepale alimrukia baba yake na kumdaka asije akadondoka chini.
“Wewe mzee , naona umeingia kwenye levo ya Nafsi muda si mrefu, msingi wako wako wa mafunzo ni mzuri lakini unapaswa kwanza kutibu afya yako kwanza , ninaweza kukuharibu viungo vyako kama nitakupiga pigo lingine”Aliongea Roma.
Mzee Sharif alikuwa akitaka kuongea neno lingine lakini palepale alijikuta akitapika damu nyingi huku akianza kuhema kwa tabu kama vile mbwa ambaye amekimbia maili nyingi.
“Haiwezekani , wewe ni shetani , hujatumia nguvu zozote za mbingu na ardhi , wewe ni nani haswa , au unatokea kule kwenye ule ulimwengu?”Aliongea Roma alishajua mzee huyo alichokuwa akijaribbu kumaanisha , pengine alikuwa akimaanisha Hongmeng au koo nyingine za kijini .
Lakini licha ya hivyo Roma hakutaka kujali sana mzee huyo ametokea wapi kwanini ana uwezo kidogo wa kijini , alichokuwa akitaka ni kumaliza kazi hapo ili kuondoka kwani hakutaka kupoteza muda mwingi.
Roma palepale alimsogelea Mzee Hamisi na alitoa pini ya bomu ambalo alikuwa ameshikilia na mkono wa kushoto na kisha alilitumbukiza kwenye mdomo wakekwa nguvu kiasi cha kumn’goa baadhi ya meno.
Sasa kilichowashangazwa ni kwamba licha ya Roma kulitoa pini pamoja na kulitumbukiza ndani ya mdomo wa baba yake Asha hakuonyesha nia ya kukimbia na alisimama hapo hapo.
Ilikuwa ni kufumba na kufumba tu mlipuko mkubwa ulitokea na kuwafunika wote Roma na Mzee Hamisi.
Baada ya moshi ule wote kuisha Roma alikuwa amesimama vilevile akiwa hajapatwa na jeraha la aina yoyote ile.
Kila mmoja ikiwemo Mzee Sharif waliishia kumwangalia Roma kwa mshituko wa aina yake , huku wakijiuliza maswali je Roma ametengenezwa na chuma , kwanini hajapatwa na madhara ya mlipuko wa bomu.
“Babaaaa…!!!!”
Asha alijikuta akitoa ukulele mkubwa wa majonzi huku akishindwa hata kusimama tena na kuishia kupiga magoti akiangalia upande aliokuwepo baba yake kwa majonzi makubwa akiwa ameharibika uso.
Roma hakujali kabisa kilio chake na palepale aliupiga teke mwili wa Mzee Hamisi na ulienda kudondoka mbele ya Asha lakini tofauti na kumwangalia baba yake aliamka na kukimbia na kwenda kujificha nyuma ya wenzake akiogopa.
Kila mmoja alikuwa na uso uliosawijika kutokana na hofu kubwa , ukatili wake ambao haukuw awa kibinadamu ulianza kuwafanywa kuwa vichaa na kujihisi ni kama vile wapo ndotoni.
“Nimemaliza na kionjo sasa , huu ni muda sasa wa show ya mlipuko wa mafataki”Aliongea Roma.
Wakati kila mmoja akiwa ameshikwa na bumbuwazi Roma alikuwa akitoa maboksi yaliokuwa na mabomu nje ya gari akiyapangilia kwa ajili ya kuharibu jengo lao la ibada.
Awamu hio hakuna ambaye alikuwa na ujasiri hata wa kumsogelea kwani walimchulia kama vile ni mnyama kama Simba.
“Baba usimchokoze tena “Aliongea mtoto mkubwa wa Mzee Sharif akionya.
“Baba usikurupuke , anajua hatuwezi kumfanya chochote ndio maana amekuja hapa akiwa peke yake”Aliongea Waziri.
“Boss , Roma anafahamika kwa kuwa na roho ya kishetani , kwasasa hatuwezi kushindana nae na tunapaswa kukimbia kwa ajili ya kujipanga upya”Aliongea bwana mmoja aliehamika kwa jina la Bahe.
“Mkurugenzi wa kampuni ya Maya Pharmaceutical amekwisha kufariki , nyie wengine wote mliobakia hapa mnapaswa kuondoka kabla hamjapatwa na kitu kibaya zaidi”Aliongea akiwapa ishara ndugu wa Mzee Hamisi pamoja na watu wengine ambao walikuwa wakisalia hapo.
“Bosi unapaswa kuondoka kwanza?”Aliongea Bahe.
“Ondokeni , la sivyo nitawapiga risasi”Alifoka Mzee Sharif.
Mzee Sharif alionekana hakutaka mtu yoyote ndani ya familia yake kuuliwa na Roma hivyo aliwafukuza kuondoka katika hilo eneo huku akibakia yeye peke yake.
Muda huo Wazir Salihi alikuwa kwenye mshituko mno , ijapokuwa alikuwa amezisikia habari za Roma na ukatili wake lakini hakutegmeea alikuwa zaidi ya vile alivyosikia.
Hakutaka hata kubakia kwa sekunde moja ndani ya eneo hilo na aliondoka na wengine wote.
Asha aliekuwa akimuomboleza baba yake hakujali tena zaidi ya kuondoka kimya kimya huku akitangulia mbele kabisa.
“Baba wewe huondoki?”Aliuliza mtoto wake mkubwa
“Wewe na Nguzo mnaweza kuondoka , nitakuwa sawa”Aliongea huku akisimama vizuri kwani tayari alishapona majeraha yake kutokana na kuwa katika levo ya Nafsi.
Wakati watoto wake wakikimbia kuondoka hilo eneo Mzee huyo aliwaangalia kwa nyuma na kuishia kutoa tabasamu la Dharau.
“Ngoja tuone anaweza kufanya nini?”Aliongea mwenyewe huku akimwangalia Roma ambaye alishamaliza kutoa maboksi yote ya mabomu.
Roma hakujali kama watu wote wamekimbia kwani mpango wake ilikuwa ni kulipua hayo makazi yote na kuyageuza majivu wala sio kuua mtu , Mzee Hamisi alimuua kutokana na kiherehere chake.
Roma hakupenda kudharaulika na kuonekana kama mbwa mnyonge anaejua kubweka lakini meno ya kung’ata hana ndio maana alienda mbali mpaka kufika katika hilo eneo.
Roma mpango wake kwanza aliokuwa nao ni kupunguza nguvu ya familia hio kutokana na taarifa alizosikia kuhusu familia hio kufanya biashara za Magendo na kumiliki kundi la kihalifu.
Ilionekana hata Mzee Samweli Nguluma alikuwa akijua nguvu ya Mzee Sharif na ndio maana hata baada ya Roma kumweleza mpango wake aliogopa.
Sasa Roma alimwahidi baba yake Benadetha kwamba baada ya kukamilisha kazi hio atampa nguvu ya kundi lake la zoa zoa kuweza kuchukua biashara zote za Mzee Sharif za magendo na faida ambayo atakuwa akipata kupitia biashara hio angempatia yeye.
Roma alitenganisha maboksi yaliokuwa na mabomu katika makundi nane , na kwa mahesabu yake aliamini kama yangelipuka yote kwa wakati mmoja basi ingekuwa rahisi kuharibu jengo hilo la madhabahu.
Roma mara baada ya kuridhika na kazi yake alimgeukia Mzee Sharifu na kumwagalia kwa tabasamu la kikarimu kama vile amekuwa mtu mzuri.
“Ni kwa bahati mbaya hii show utaingalia wewe mwenyewe maana ndio umebakia wenzako wamekimbia”Aliongea Roma na kisha alichukua uzi
flani hivi kama wa barui ambao alikuwa aueunganisha na maboksi yote uliokuwa na uwezo wa kusababisha cheche ambazo zingeweza kulipua mabomu hayo.
Mzee Sharifu alikuwa na hasira kali mno , alitamani kumdhibiti Roma lakini kwa nguvu zake asingeweza.
Dakika hio hio wakati Roma akijiandaa kuendelea na kazi yake palepale mlango wa dhehebu lao la ibada ulifunguliwa kwa kusukumwa kwani ulikuwa umeharibika.
Palepale alionekana mtu aliekuwa kama kivuli cha rangi ya majivu , huku akisababisha upepo mkali sana kiasi cha kukusanya vumbi lililokuwa limetulia.
Ilikuwa ni kufumba na kufumba yale maboksi yote yalitawanyika kutoka katika mstali ambao umetengwa na Roma kwa ajili ya kuweza kulipuka na baada ya kusambaratika palepale yalianza kuripuka kwa spidi kubwa bila ya kusababisha madhara.
Roma kama angekuwa na uwezo wake wote wa kijini basi pengine angeweza kuhisi uwepo wa mtu huyo ndani ya hilo Dehehebu kwani ni dhahiri alikuwa akitumia nguvu za kijini.
Mtu yule alikuwa na muonekano wa kiarabu na alikuwa amevalia vazi la kanzu nyeupe kama vile ni mzimu na baada ya kutoka alienda kusimama juu angani.
Roma aliinua macho yake na kumwangalia na macho yasiokuwa ya kawaida , na aliweza kugundua kwamba alikuwa ni mzee kidogo na alijiuliza au yeye ndio anaabudiwa.
Roma ijapokuwa hakuweza kuangalia levo yake ya nguvu za kijini lakini aliweza kumkadiria kuwa katika levo ya nafsi huku akiwa na uhakika ni jini lenye mwili wa kibinadamu.
Jambo hilo lilimshangaza sana Roma na kujiambia hakika familia ya huyo Mzee Shariif ilikuwa ni ya aina yake.
Roma alijiambia kama kweli mtu huyo alikuwa akiishi katika jengo hilo kwanini yule mjumbe wa Hongmeng hajamchukua na kumpeleka katika ulimwengu wa kijini kama iliyokuwa kazi yake.
Mzee Sharif alianza kuongea na yule mtu kwa lugha ya kiarabu ambayo Roma kwa haraka haraka alijua alikuwa akimuomba msamaha kwa usumbufu uliojitokeza.
Roma palepale alijua ndio maana Mzee huyo aliwaambia wengine kuondoka kumbe hakutaka kuifanya siri ambayo ipo ndani ya Sinagogi lake hilo kufichuka.
“Wewe binadamu mtoto ni mpumbavu , nitakuacha uondoke sasa hivi kwasababu unatokea katika familia ya raisi wa taifa hili”Aliongea yule mtu kwa lugha ya kiswahili lakini Roma alimpotezea.
“Ongea kama ulikuwa ukiogopa kupigwa bomu mpaka kufa ndio maana umejitokeza , haya sasa umeharibu mabomu yangu , nitaharibu vipi hili jengo?”
“Unathubutu vipi kuongea kijeuri hivyo , hivi unajua unaeongea nae ukuu wake ukoje , huyu ndio jini Imrah Sharif mlinzi wa roho za miungu wetu, hata babu yako na baba yako hawana uwezo wa kutugusa, wewe huo ujeuri unatoa wapi?”Aliongea Mzee Shairf.
“Mimi ni mimi , sio babu wala baba , kuna haja gani ya kutaja majina yao hapa , wewe pia ni mzee kwaninin unajifanya kama mtoto, nitahakikisha siondoki hapa bila ya kuharibi hili eneo”
Wote kwa pamoja waliangaliana wakionyesha mshangao wa kuona Roma bado hakuwa na hofu kabisa na jini Imrah











SEHEMU YA 649.
Jini Imrah ndio lilikua mlinzi mkuu toka kujengwa kwa jengo hilo , lakini licha ya hivyo haikuwahi kutokea kukutana na binadamu ambaye anaweza kumwangalia bila hofu kama Roma.
“Hakika wewe ni binadamu kichaa kwa kutaka kuthubutu kuharibu jengo la ibada ya miungu wetu, lakini siwezi kukuruhusu”Aliongea
Roma alijikuta akipandwa na hasira kwa kuona mabomu yake yameharibiwa hivyo kazi yake ya kutaka kulipua hilo eneo kuwa ngumu kidogo , lakini alijiambia si wameyataka wenyewe basi atamuonyesha yeye ni mtu wa mbinu nyingi.
“Wewe Jini Mzee, nakushauri usiende mbali maana nitakuua, umeharibu mabomu yangu niliokuwa na mpango wa kuyatumia kuunguza hili eneo , lakini naona sina jinsi na kulibomoa kabisa”Aliongea Roma.
Hakutaka kukata tamaa kizembe lakini kwa wakati mmoja pia hakutaka kupigana na huyo Imrah , kwani aliaminni bila nguvu zake za kijini ingekuwa ngumu kumshinda.
Roma palepale alifanya maamuzi ya kukimbilia kuingia ndani ya Sinagogi lile lakini kabla hajaingia ndani yule mtu alishafika mbele yake huku akiwa na hasira kali kwani hata kucha zake zishachomoza.
Mtu huyo alionyesha kukasirika kwani alitegemea Roma angepambana nae , lakini alionyesha kuwa na nia nyingine tofauti na yeye kama mlinzi wa
Madhabahu hio mtu kama Roma hakuruhusiwa kuingia.
Akiwa na hasira iliopanda kwa kiasi kikubwa palepale alitengeneza kitenesi cha nguvu ya kijini kwenye mkono wake na kisha alimsogelea Roma na kumpiga kwa nguvu eneo la kifuani.
Roma mara baada ya kupokea shambulio lile aliishia kutoa tabasamu la kifedhuli, alijua kabisa licha ya kwamba mtu huyo alikuwa na nguvu ya kijini katika levo ya nafsi lakini bado hakuwa tishio kwake.
Upande wa Imrah alidhani Roma angerushwa na shambulizo ile lakini kilichoweza kusikika ni kishindo tu lakini Roma hakusogea hata inchi.
Roma hakujali mshangao wake na palepale alipiga teke ule mlango ambao ulikuwa unakaribia kuharibika na palepale ulidondoka na kwenda kuhaaribu samani zilizokuwa karibu na mlango.
Mzee Sharif na Imrah wote walijikuta wakiwa katika mshangao kwa tukio lile , kwani kila kitu kilikuwa nje ya mategemeo yao.
“Sharif , nenda mbali na hapa kadri uwezavyo , ngoja nimchukulie siriasi”Aliiongea Imrah.
“Yes”
Mzee Sharif hakuthubutu kuongea chochote na palepale aliondoka katika hilo eneo.
Roma mara baada ya kuingia ndani ya eneo hilo alijikuta akishangazwa na mishumaa iliokuwa imechomwa kwanzia mwanzoni mwa mlango mpaka mwishoni tena ikiwa imepangwa kwa ustadi wa aina yake.
Ijapokuwa hakutumia uwezo wake wa kijini lakini alihisi kuna nguvu ya kiroho ambayo haikuwa ya kawaida , Roma alijiambia hii madhabahau inahusiana na nini , lakini hata hivyo hakuwa na majibu na hata angeuliza asingeweza kupata majibu anayotaka kwani mida huo alikuwa akichukuliwa kama adui.
Mlinzi wa Madhabahu hio , jini Imrah hakutaka kuchelewesha tena kumshughulikia Roma baada ya kumuona akielekea ndani kabisa ya madhabahu yao ya kidini.
Roma kabla hajashika kiango cha mshumaa uliokuwa karibu palepale jini Imrah alishamfikia na kumzuia huku akikusanya nguvu nyingi za kijini ili kumshambulia Roma.
Roma kitendo cha kuzuiwa kwa mbele kilimfanya kukasirika mno na palepale macho yake yalibadilika rangi na kuwa ya rangi nyekundu tii,
Imrah wakati anamshambulia Roma na pigo la kijini aligundua kuna kitu hakipo sawa kwani shambulizi lake ni kama kuna kitu kama ngao ambacho kimezuia na palepale alijikuta akinusa hatari na aliruka na kurudi nyuma huku akishangazwa na kubadilika kwa macho ya Roma.
Roma mara baada ya kuona amerudi nyuma alimfuata huko huko akighairisha kwanza kuelekea mbele kabisa ya Madhabahu kujionea kinachoabudiwa hapo ndani ni nini mpaka kuwa na mlinzi mwenye nguvu za kijini.
“Ni aina gani ya mbinu za kijini ulizokuwa nazo , umewezaje kuhimili shambulizi langu?”Aliuliza Imra. “Sikutegemea pia kama una aina ya kipekee ya mashambulizi , inaonekana ufunuo wake sio wa kawaida , lakini naamini nikiishika shingo yango na kuivunja nitakuwa nimekumaliza”Aliongea Roma.
“Unakiburi sana , unategemea tu nguvu zako za kimwili na sio nguvu za kijini, halafu unaona unaweza kunishinda”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi.
“Kulingana na The gods treaty , nitakuwa sivunji sheria kudili na jini kama wewe ambaye upo kwenye levo ya Nafsi ukiwa kwenye ulimwengu wa kawaida eneo ambalo hustahili kuwepo”Aliongea Roma.
Imrah alionekana kushangazwa na kauli ya Roma lakini hakuwa na muda wa kufikiria na palepale aliweza kumuona midomo yake ikicheza cheza.
“Unseal!!!”
Aliongea Roma kwa nguvu na palepale kulitokea mkandamizio wa hewa mkali sana na ilikuwa ni kama eneo lote anga lake lilikuwa limesimama na hakuna upepo.
Kitendo kile kilimpagawisha Imrah na palepale aliita nguvu za kijini kujilinda na ule mkandamizo huku wakati mmoja akiwa katika kiwewe.
“The Space Laws ? You are a god?”Aliongea kwa mshangao mara baada ya kumuona Roma akitumia kanuni za anga na alijua watu waliokuwa na uwezo hao ni miungu pekee.
“Lazima nikamilishe kilichonileta , kutumia kwangu
kanuni za anga itakuwa njia rahisi ya
kukumaliza”Aliongea Roma huku macho yake yakiwa sio ya kawaida na palepale aligeukia jengo ambalo lilikuwa limeenda hwani lililokuwa mita kadhaa kutoka aliposimama.
Palepale alianza kuongea maneno aliokuwa akiyajua yeye huku akichezesha mikono yake kwa nguvu na palepale ni kama kuna kitu kinachotingisha anga kwani lile jengo lilikatika katikati kuanzia ghorofa ya pili na kubomoka kwenda chini.
Ilikuwa ni kama vile kumetokea tetemeko la Ardhi kwa namna jengo hilo lilivyoharibika na kuacha kiwingu cha vumbi , lilianza kucheza cheza lile jengo kama vile ni taswira ya sura kwenye maji yanayocheza cheza .
Ijapokuwa Roma uwezo wake wa kutumia kanunu za anga haukua mkubwa kama wa Poseidon , Athena na Apollo lakini kudili na Imrah kwake ilikuwa rahisi sana.
Pengine jini Imrah lilikuwa kwenye levo ya nafsi na kwa kutumia kaunni za anga anaweza kushidwa kumjeruhi lakini ilkikuwa ni rahisi kwake kuharibu majengo.
“Space Crumble!!!”
Aliongea Roma na palepale jengo lingine ambao lilikuwa na usanifu wa kipekee lilibomoka na kuporomoka kwenda chini kama vile limejengwa na mchanga bila nondo.
Imrah alijikuta macho yake yakibadilika na yenyewe na kuwa kama mwezi huku michirizi ya damu ikijitengeneza kwenye macho yake , hakutaka kumuacha Roma kuendeleza na anachokifanya kwani angeharibu eneo lote.
“Mshenzi mkubwa wewe nakuua”Aliongea na palepale alimsogelea Roma kwa spidi na kisha akampiga ngumi iliounganishwa na nguvu za kijini.
Roma alijaribu tena kutengeneza ngome anga lakini iliweza kuharibiwa kirahisi na nguvu za kijini za Imrah
“Kanuni zako hazina nguvu na sio tisho lolote kwangu”Aliongea kwa majjigambo.
“Na mapigo yako yote ni kama mtekenyo , fanya unachotaka lakini ndio unaniongezea spidi ya kuharibu hili eneo”
Imrah palepale alimsogelea Roma kwa kasi akirusha ngumi ambayo kwa spidi yake ilionekana ni kama vile imerefushwa na mara baada ya kumpiga Roma haikumletea madhara kabisa na alielewa nini maana ya neno Mtekenyo.
Roma wala hakujali aliendelea kuharibu majengo kwa spidi kubwa kwa kutmia kanuni za anga.
“Unaonaje niendelee kufanya uharibifu au niharibu jengo lenu la ibada pekee?”Aliuliza Roma lakini hakuna chaguzi ambayo ilikuwa nzuri kwa Imrah Roma alikuwa na uwezo wa kuharibu majengo yote kwa pamoja kwa kutumia kanuni ya anga ya mtikisiko lakini aliamua kuharibu jengo moja moja ili mradi tu kumtesa Imrah.
“Wewe ni kichaa”Aliongea Imrah kwa nguvu na kisha palepale alionekana kufanya maamuzi na alipotea kuingia katika jengo lao la ibada.
Roma mara baada ya kuona amekimbilia kwenye jego hilo na yeye alijawa na shauku ya kutaka kujua nini ambacho kinaendelea na alifuata huko huko.
Mara baada ya kufika ndani ya jengo hilo eneo la madhabahuni aliweza kumuona akiwa amepiga magoti chini kwa namna ya kusujudu.
“Mimi , Imrah Sharif nimekutana na adui mkengeufu ambaye simuwezi hivyo naomba ruhusa kuhamisha Roho zenu pamoja na Hazina sehemu nyingine”Aliongea kwa kiarabu akiwa amesujudu.
Roma mara baada ya kusikia neno Hazina alijikuta mapigo yake ya moyo yakiongezeka kwa shauku na palepale kwa kutumia macho yake yasiokuwa ya kawaida alianza kuchunguza eneo lote na aliweza kuona juu ya kiango katika meza iliotengenezwa kwa jiwe jeupe kuna boksi lenye muonekano tofauti na maboksi yote yaliokuwa hapo ndani, lenyewe lilikuwa na kitako kilichotengenewa kwa dhahabu.
Roma mara baada ya kumuona Imrah anasogelea lileboksi palepale alitumia kanuni za anga na kunyoosha mkono wake na palepale ilikuwa ni kama vile unyooshe mkono kwenye vioo vya saluni ndio kilichoonekana , kwani mkono wa Roma uliongezeka urefu ghafla tu na aliweza kulifikia lile boksi na kisha alilitupia katika Sumeru.
“Wewe mwanaharamu rudisha hazina yetu”Aliongea jini Imrah kwa hasira.
Kazi ya jini Imrah ukiachana na kulinda roho ambazo hazikujulikana ni za nini , lakini pia alikuwa akipaswa kulinda hio hazina kwa namna yoyote ile.
Na hata wakati akiwa amepiga magoti akisujudu alikuwa akiongea na roho pamoja na hadhina hio ili kuweza kupata kibali cha kutoa vitu hivyo nje ya eneo hilo , lakini hakutegemea kama Roma angetumia hila na kumuwahi.
“Hehe.. wewe jini umekuwa mjinga eti , ushasema mwenyewe ni hazina tena kwa sauti kubwa , unafikiri ni nani ambaye anaweza hapendi hazina, nishaharibu majengo yenu yote nadhani angalau pia ni vizuri kufaidika na hazina, mimi sio mjinga napenda sana kuiba vitu vya wengine hususani vitu vyenye majina ya kusisimua kama Hazina”
“Wewe sio binadamu , kwanini unadhalilisha familia yako?”Aliongea kwa kufoka.
“Huwa sijali nikisikia mpenzi wangu akiniambia mimi sio binadamu , lakini wewe unatoa wapi ujasiri wa kusema mimi sio binadamu ili hali wewe mwenyewe sio binadamu..?”
“Rudisha hio Hazina haraka kabla matatizo hayajakupata”
“Unaongea kuhusu hazina gani , mimi sijui chochote kuhusu maswala ya Hazina”Aliongea Roma akijifanyisha hajui anachozungumza nini.
“Hebu nisikilize kwa umakini ukoo wetu wa kijini wa Sharif lazima utalipiza kisasi kwa kila kitu ambacho umefanya siku ya leo , hakuna mtu ambaye ataweza kukusaidia wakati mabaya yatakapokujia”
Baada ya kuongea hivyo alianza kukusanya vibao flani hivi vilivyokuwa viking’aa kwa madini yasio ya kawaida na baada ya kumaliza aliviniigiza vyote kwenye boksi la mbao.
Hakuwa tayari kupigana ndani ya madhabahu kwa kutii sheria ya kimadhabahu , hata kama ikitokea yupo kwenye hali ya namna gani sheria ilikuwa ikimzuia kupigana eneo la madhabahuni, lakini hata hivyo alijua hata kama akivunja sheria na kushindana na Roma asingemuweza.
Roma mara baada ya kuona mshindani wake ashaoondoka alitoka nje na kutafuta mafuta kwenye kibanda cha jenereta na kisha aliyamwaga kuanzia mangoni mpaka eneo la madhabahu na kisha alidondosha ile mishumaa yote chini na kisha akatoka na mlipuko mkubwa wa moto uliweza kuonekana ukisindikizwa na cheche za umeme na huo ndio ukawa mwisho wa madhabahu ya kijini ya mzee Sharif.
Upande wa juu kwenye kijimlima familia yote ilikuwa imesimama njiani ikiangalia chini kwenye makazi yao yaliosifika kuwa ya kifahari zaidi pengine ndani ya Afrika nzima lakini ndani ya dakika chache tu sifa yake yote imeharibika.
Kutokana na giza waliweza kuona kiwingu cha moto kikitekekeza jengo lao la ibada.
“Baba jini Imrah na yeye ameshindwa kumdhibiti?”Aliuliza mtoto mkubwa wa Mzee Sharif.
“Lazima alikuwa na uwezo ambao ameficha , ni ngumu sana jinni Imrah kushindwa na binadamu kulingana na uwezo wake na uzoefu”Aliongea Mzee Sharif huku akiwa na uso ambao haukuweza kusomeka anafikiria nini.
Dakika hio hio Jini Imrah aliweza kujitokeza mbele yao akiwa amebeba boksi kubwa na kulitua mbele yao.
Wale walinzi waliokuwa wamesimama walishituka kwa hofu huku wakishindwa kumjua mtu huyo ni nani , ni kama waliona mzimu wa kiarabu.
“Ewe Ilia Salim Sharif , napaswa kwenda kutoa taarifa makao makuu a ndani kuhusu hili , hatuwezi kuusamehe ukoo wa Kweka kwa hiki alichokifanya mtoto wao , ondoka na hizi Roho za mababu omba washirika wetu freemason kuzihifadhi katika madhabahu yao kwa muda”Aliongea Imrah huku akiweka boksi lile kistaarabu sana ardhini.
Baada ya kusikia maneno hayo Mzee Sharif alijiuliza nini kimetokea , inamaana mkuu wake katika imani , jini la cheo cha ulinzi wa Imrah amemshindwa Roma.
Jini Imrah liliangalia nyuma likianglia moto unaowaka kwa masikitiko na palepale kufumba na kufumbua aliyeyuka na kupotea na kufanya wale walinzi kurudi nyuma huku wakianza kufikicha macho yao, wengine wakijipiga vibao ili kuamka ndotoni.
“Babu Jini Imrah amemaanisha nini kusema kwenda kutoa taarifa makao makuu?”Aliuliza Maimuna ambaye ni mtoto wa mtoto mkubwa wa Mzee Sharif, alikuwa mrembo sio mchezo na rangi yake ya mchanganyo
“Baba tunapaswa kufanya nini sasa , atatufuata na hapa ujue tukiendelea kusimama”Aliongea Waziri Nguzo.
“Unaogopa?”
“Baba najaribu kuwa na wasiwasi na usalama wa kila mmoja”
“Mtoto wako pamoja na mkeo wamefanya kazi nzuri ya kumchokoza Roma, mnapanga kufanya nini baada ya hapa?”Aliuliza Mzee huyo huku akimwangalia kwa hasira.
“Baba sijui kilichotokea , Salihi pamoja na Asha wamefanya haya bila ya kuniambia”Aliongea na palepale yeye na mke wake walipiga magoti mbele ya mzee Sharif.
Salihi mara baada ya kuona wazazi wake wakiomba huruma ya babu yake na yeye aliungana kuomba kusamehewa.
“Kupiga magoti ndio kitu pekee mnachoweza kufanya , yaani mmemfanya yule shetani kaja ndani ya makazi yetu na kuharibbu kila kitu nilichokilinda zaidi ya miaka mia moja lakini nyie mnachojua ni kupiga magoti , Asha pamoja na Salihi nawatahadharisha sitojizuia kuwaua kama mtafanya kosa la namna hii kwa mara nyingine”Aliwafokea na hakuna hata mmoja ambaye alinyanyua mdomo wake kupimga maneno yake
Ayubu alijikuta akiona aibu kuona baba yake pamoja na mama yake wa kambo na mdogo wake wakipiga magoti.
“Babu sisikii sauti yoyote kutoka ndani , atakuwa ashaondoka”Aliongea Maimuna.
“Kipi kingine ambacho anaweza kufanya , ni mkorofi sana , kashachoma moto madhabahu yetu na sasa ameondoka anavyojisikia , nyie subirieni nitahakikisha anajutia hiki alichokifanya leo”Aliongea.
Mzee huyo hakujua kama Roma alikuwa ameiba na hadhina yao , kitu ambacho alikilinda kwa miaka mingi tokea kukabidhiwa urithi na baba yake. Huenda angejua hilo kichwa kingemuwaka moto kwani ilikuwa ni kama uhai wake.
Hazina hio ndio kitu pekee ambacho kilimfanya kufurumushwa kwenye nchi yake na kukimbilia hapa Tanzania.
Pengine jini Imrah liliona aibu kumwambia mzee huyo kama hadhina ambayo alikuwa akiilinda imeibiwa.
Upande mwingine Roma mara baada ya kuangalia jengo la madhabahu kutekea ghafla tu aliweza kuona kivuli cha mtu kikitua ndani ya eneo hilo na alipoangalia kwa umakini aliweza kugundua ni Mjumbe kutoka Hongmeng ambaye kazi yake ni kukusanya watu wenye nguvu a kijini na kuwarudisha katika ulimwengu wa kijini






SEHEMU YA 650.
Ijapokuwa Roma hakujua Mjumbe huyo amesafiri vipi kwa haraka na kuja katika hilo eneo ,l akini alijua pengine ni kitendo cha Jini Imrah kutumia nguvu za kijini au yeye kutumia kanuni za anga.
“Kwanini umefanya hivi?”Aliuliza mara baada ya kuangalia jengo ambalo linateketea. “Walinichokoza wenyewe na sikuwa na namna zaidi ya ku’unseel kanuni za anga ili kudili na mlinzi wao ambaye yupo kwenye levo ya Nafsi, sijavunja kanuni yoyote”
“Umejitafutia matatizo makubwa, hii familia inaweza ikaonekana ya kawaida kwenye ulimwengu wa kawaida lakini sapoti yake sio ya kawaida kama unavyofikiria”
“Mbona unaongea kwa namna ya kuniogopesha , mimi nilijua watu na majini wote waliopo kwenye levo ya Nafsi lazima wapelekwe katika ulimwengu wa kijini, kwanini uone nilichokifanya ni cha kugopesha wakati wewe ni mjumbe”
“Ukweli ni kwamba sijui sana haya maswala kwani ni mara yangu ya kwanza kuwa mjumbe na sijawahi pia kuishi katika ulimwengu wa kawaida hapo kabla , wakati nakuja hapa umoja wa majini ulinipa tahadhari ya kutogusa baadhi ya familia ambazo zinawaabudu”
“Umoja wa majini?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“Ndio kuna umoja wa majini na kiongozi wake anafahamika kwa jina maarufu la Master namba moja , inasemekana ana uhusiano mzuri sana na
serikali ya Marekani na baadhi ya jumuia za siri kama Freemason”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa kidogo.
“Nishachoma hili eneo tayari na nimempiga yule jini , kilichofanyika kimekwisha kufanyika ,siwezi kukimbia tena, unaonaje tukiongea kuhusu hili siku nyingine”Aliongea Roma hakutaka kumuuliza ametokea wapi lakini hata hivyo ashajua tayari amejipalia makaa na muda si mrefu anapaswa kudili na matokeo.
Tokea siku ambayo Roma alimhonga vidonge huyo mjumbe kwa ajili ya kumuacha Rose aisiende ulimwenguwa kijini alikuwa mpole sana mbele ya Roma ni kama vile alitarajia angepewa rushwa nyingine.
Mjumbe alimwangalia Roma kwa macho ya ki udadisi na alijikuta akishangaa mara baada ya kutokuona dalili yoyote ya nguvu za kijini kwenye mwili wake.
Hali ile ilimuongezea shauku na palepale aliruhusu nguvu za kijini kuingia katika mwili wa Roma ili kujaribu kumchunguza lakini ile nguvu yake ya kiudadisi ilipogusana na nguvu za Roma alijihisi akili yake inataka kupatwa na uchizi na alijiondoa haraka huku hofu ikimvaa.
“Wewe… umemua kuficha nguvu zako makusudi ili kunitega?”Aliuliza kwa mshangao.
“Unao uwezo wa kujua nguvu zangu , kwanini niufiche ili kukudhuru?”Aliongea Roma.
Mjumbe alijikuta akiona Roma kaongea pointi lakini alikuwa katika hali ya taharuki na kujiuliza
imekuwaje Roma uwezo wake ukawa mkubwa huo kuliko mara ya mwisho alivyomuona.
Ukweli ni kwamba kama uwezo wake ungekuwa unalingana na wa Roma angemvamia na kuchukua mbinu yake ya kimafunzo.
Roma kwasababu gari yake aliokuja nayo imeharibika aliamua kutumia kauni za anga kusaifiri kuelekea mjini..
******
Upande mwingine jijini Mwanza ikiwa ni usiku , mwanaumke mrembo alieonekana kukaa katika kiti cha kiofisi ndani ya chumba cha Presidential Suite katika hoteli ya Hilton iliokuwa kandokando ya Ziwa Victoria.
Sehemu aliokuwa amekaa ilikuwa ikimruhusu kuona upande wa pili wa Ziwa , kulikuwa na giza hivyo alichoweza kuona kwa mbali ni miale ya mwanga wa taa rangi ya njano upande wa mbali sana katikati ya Ziwa.
Kwa mtu mwenye uelewa na shughuli za Ziwani angejua kabisa miale hio ilisababishwa na watu waliokuwa wakivua kwa kutega samaki na mwanga wa karabai.
Mwanamke huyu mrembo alikuwa amevalia koti la Beige brand ya Chanel ambalo lilikuwa na mkanda uliofungwa kiunoni.
Mkono wa kushoto alikuwa ameshikilia shavu akilitomasa huku mwingine ulikuwa umeshikilia nyaraka zilizokuwa kwenye meza akiziangalia kwa umakini kwa kuzisoma.
Ilikuwa ni saa saba za usiku lakini mwanamke huyo hakuonyesha ishara yoyote kama muda wowote angepunzika , aliendelea kupitia kurasa hadi kurasa na kisha akimaliza nyaraka hii anahamia kwenye nyaraka nyigine.
Muda huo huo mwanamke mrembo mwingine
alievalia gauni aliingia kwenye chumba hicho akiwa ameshikilia kikombe cha kahawa na kukiweka juu ya meza yake huku akiwa na macho yaliojaa usingizi.
“Boss , muda umeenda sana, unaonaje ukipumzika sasa?”Aliongea yule mwanamke kwa upole ishara ya kumbembeleza bosi wake, alikuwa ni Recho na bosi alikuwa ni Edna.
Recho alikuwa akijiandaa kwa ajili ya likizo yake ya mwisho wa mwaka na kusafiri kuelekea nje ya nchi na mpenzi wake lakini ghafla tu bosi anampigia simu na kumwambia ajiendae kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza kwa ajili ya ukaguzi wa maeneo ya ki uwekezaji.
Ijapokuwa alikuwa na haki ya kukataa lakini bado aliona sio jambo zuri kufanya hivyo kutokana na msaada mkuwba ambao Edna alikuwa amefanya kwenye maisha yake.
Edna hakuwa na msaidizi , ijapokuwa alikuwepo
Suzzane lakini hakutaka kumsumbua kwani alikuwa amempa kazi nyigine kabisa hivyo mtu pekee ambaye aliona angeweza kumsaidia ni Recho ndio maana alimpigia simu.
Bila shaka safari hio ilikuwa na posho kubwa sana kwa Recho kwnai alikuwa akifanya kazi mbili kwa wakati mmoja lakini alikuwa na wasiwasi juu ya mpenzi wake.
Chumba hicho cha Presidential Suite kilikuwa ni kikubwa mno na kilikuwa na vitanda vinne , na ilikuwa ni bahati kwani kukaa na Edna kwenye chumba kimoja ilimrahisishia kupokea maagizo kutoka kwa bosi wake na kuyafanyia kazi.
Ilikuwa ni siku ya pili tokea wafike jijini hapo lakini kila siku ilikuwa ni ya maswali sana kwa upande wa Recho juu ya bosi wake.
Recho alishindwa kuelewa kwanini Edna akarudi ghafla tu kutoka Iringa na kuonekana kama mtu mwenye mawazo , je amegombana na Roma.
Edna aliinua uso wake na kumwangalia Recho na kisha alitoa tabasamu hafifu.
“Usijali Recho , huna haja ya kunisubiria mimi , unapaswa kupumzika sasa”
“Naweza vipi mimi msaidizi wako kulala wakati wewe bosi wangu unafanya kazi?”
“Usijali kuhusu hilo , nimekuambia ufanye hivyo”Aliongea Edna na kisha alichukua kikombe cha kahawa na kisha akanywa kidogo lakini Recho alikuwa amesimama vilevile akionekana kama mwenye kushangaa
“Bosi , huwezi kukaa macho kama hivi , ni siku ya tatu leo hujalala hata mara moja , hatuna haraka na tunachokifanya kwanini hutaki kupumzika?”
Edna aliishia kulamba midomo yake , ukweli hata kama asingelala asingepatwa na shida yoyote kutokana na uwezo wake wa kijini lakini bado haikuwa vizuri kwa mtu kama Recho ambaye kutolala kwake kulimtia wasiwasi.
Edna palepale aliweka kikombe kile cha kahawa na kisha alisimama na kusogelea dirisha na kuangalia mandhari ya nje..
“Recho vipi kama nitakuambia kwamba nashindwa kulala kwasababu naogopa kuota , utaweza kuniamini?”Aliuliza Edna bila ya kugeuka huku akitoa kicheko kama anajicheka yeye mwenyewe. “Unaogopa kuota , Bosi ni kwasababu haupo vizuri kimawazo?”
“Hata mimi sijui chochote lakini najua kwamba siwezi kulala na nikapata usingizi”Aliongea na kumfanya Recho kuonekana kuwaza.
“Bosi samahani kama nitavuka mpaka , je haya yanakutokea kwasabau ya ugomvi wako na mume wako ., kama ni hivyo utakuwa unajiumiza bure , haijalishi tatizo ni kubwa kiasi gani unapaswa kukaa
chini na kuongea nae tofauti ya kukimbia na kumuepuka”
Recho aliweza kusikia mapigo ya moyo wake yalivyokuwa yakidunda wakati akisubiria jibu la Edna.
Mwanaume wa bosi wake ni aina ya watu ambao asingeweza kuwapata na aliekuwa mbele yake ni bosi yake aliekuwa akimheshimu sana.
Edna aligeuka na kumwangalia Recho ambaye alikuwa na wasiwasi na kisha alitoa tabasamu hafifu.
“Wewe pia ulifanya nae?”Aliuliza swali ambalo lilimshangaza Recho na palepale ile hali ya usingizi ambayo alikuwa nayo ilipomtea mara moja.
Edna kwa kumuangalia Recho aliekosa jibu aliweza kupata majibu yake palepale.
“Nitakuwa nimeuliza swali la kijinga , ulionekana kumpenda wakati mnafanya wote kazi idara moja ,
namjua sana sio mtu mzuri na hawezi kukuacha mwanamke mrembo kama wewe”
“Hapana .. hapana …Bosi”Recho chozi lilianza kumtoka kwa hofu aliokuwa nayo.
“Boss naomba unisikilize maelezo yangu , mimi ndio nilikuwa mkosaji . ile siku nilikuwa kwenye maumivu makali sana ya moyo na alikosa ujasiri wa kuniacha katika hali yangu niliokuwa nayo … nimekusaliti mara moja lakini sikuwahi kuwaza kurudia tena ,,, najua kabisa yule sio levo yangu , isitoshe mimi ni mwanamke nilieachika ,..”Recho alitamani kupiga magoti.
“Hakuwa na ujasiri ,, hahaha..”Edna alionekana kucheka kauli ya Recho kusema Roma hakuwa na ujasiri wa kumuacha.
“Recho huna haja ya kupaniki , sikulaumu kwa yaliotokea , ana wanawake wengi sana na nishazoea , ni kwamba tu kauli yako imenikumbusha kitu … nakumbuka siku ambayo nnilimuomba anioe alikubali kutokana na kukosa ujasiri wa kunikatalia kama ilivyokuwa kwako …”Aliongea huku akimhadithia Recho kile kilichotokea mpaka Roma kukubali kumuoa.
Recho alishindwa kumwelewa Edna , hakuamini kama alijaribu kumtishia Roma kwa kuigiza kujiua ili mradi tu akubaliane nae.
Edna kuhadithia kile kilichotokea alijikuta akiona kwamba Roma wakati ule hakujali yeye ni nani na chochote kuhusu maisha yake , Edna aliamini Roma aliweza kufanya nae mapenzi na kuutoa usichana wake kwasababu tu hakuwa mwanamke kahaba bali alikuwa ni mwanamke anaefanana na Seventeen hivyo hata kukubali kwa Roma ilikuwa ni kwasbabau hio hio yeye anafanana na Seventeen.
Edna alifumba macho yake kwa muda na kisha akayafuumbua na alionekana kama mwanamke ambaye ameamua jambo.
“Recho unaniamini?”Aliuliza Edna na Recho alitingisha kichwa kukubali
“Kwanini?”
“Sijui tu lakini ningependa pia kuamini maamuzi yako unayotaka kufanya siku zote ni sahihi”Aliongea Recho na Edna alitabasamu na kisha alipiga hatua mpaka kwenye meza aliokuwa akifanyia kazi na kisha alichukua nyaraka na kuishika mkononi.
“Chukua hii na uisome uielewe , wewe ndio utahusika kufanyia kazi kila kitu kilichomo humo”Aliongea na Recho alishika ile nyaraka na kuanza kuisoma na kadri alivyokuwa akiendelea kusoma alijikuta uso wake ukikunjamana kwa mshangao.
“Bosi hii ,,, kwanini?”
“Umesema mwenyewe unaniamini , hivyo fanya kama ninavyokuambia”Aliongea Edna huku akionekana kabisa hakuwa na mpango wa kuelezea kile ambacho Recho alikuwa akikisoma.
Unafikiri ni nyaraka gani?
*****
Siku iliofuata Roma aliweza kufika Dar es salaam saa kumi na moja kamili za asubuhi na mara baada ya kuoga maji ya moto alijisikia vizuri mno na mudi yake imerudi baada ya kuona amelipa kisasi chake kwa kuharibu makazi ya familia ya Mzee Sharif.
Kutokana na mudi yake kuwa nzuri palepale alimuamsha Nasra aliekuwa usingizini na kupiga kimoja na kisha akalala.
Saa tatu kamili asubuhi Roma aliamshwa na simu ambayo ilikuwa ikiita mfululizo na alipoichukua na kuangalia mpigaji ni babu yake na alipokea na kuweka sikioni kivivu.
“Wewe mtukutu , ushajua namna ya kumaliza hili ulilolianzisha?”Sauti bila salamu ilisikika.
“Mzee usiniambie unaogopa?”
“Nimepigiwa simu na Balozi wa Marekani kwa mara ya kwanza kwenda ofisini kwake , sijawahi kuitwa tokea nistaafu jeshi , yaani umeniingiza kwenye matatizo wewe”
“Balozi wa Marekani anahusikaje na yaliotokea hapa nchini?”
“Unaonekana hujui hata ukubwa wa hili swala ambalo umesababisha , hili ni swala la kidiplomasia na sidhani kama litaisha kirahisi, unapaswa kujiandaa wewe na wanawake wako , lakini pia usihusishe
familia yetu katika hili na taifa kwa ujumla unapaswa kuwajibika mwenyewe”
“Babu acha hizo basi ndio nini kuninikatili , ushasema mimi ni mrithi wako , kwanini unataka kuniachia nidili nalo mwenyewe”
“Shenzi nani kakumbia uende kuharibu makazi ya watu?, je ulinnishirikisha?”Afande Kweka alionekana kukasirika mno.
“Basi punguza presha Mzee , Unaweza kuuambia uma ukoo wa Kweka hauhusiki na mimi nimefanya haya kutokana na bifu langu mwenyewe na familia hio”
“Huna haja ya kuniambia cha kufanya , nishatoa ripoti yangu kabisa hatuhusiki katika hili na umemua wewe mwenyewe , lakini napaswa kukushauri pia kama mtu niliekula chumvi nyingi , achana na maswala ya kuua watu kila unapojisikia , muda mwingine haijalishi nani anakosa au nani yupo sahihi , unachopaswa ni kuangalia tatizo lenyewe chanzo chake kiko vipi…”
“Unamaanisha nini Mzee?”Aliuliza Roma lakini palepale simu ilikatwa.




SEHEMU YA 651.
Roma alimlaani Mzee Kweka kwa kupenda kumuweka hewani na palepale alirusha simu yake pembeni.
Roma mara baada ya kupiga mswaki na kujiweka sawa , alikumbuka Hazina ambayo aliiba huko Kilimanjaro na palepale alichukua lile boksi na kuangalia kilichopo ndani.
Roma alishangaa , kilikuwa ni kitu cheusi kilichokuwa kimewekwa ndani kinacholingana na kokoto lakini yenye muonekano wa kuvutia kidogo.
“Hiki ni kitu gani?”Roma alijiuliza huku akijiambia pengine ni Dhana ya kijini na hakuweza kuhisi nguvu yake kwasababu hakuwa na uwezo wa kutumia nguvu za kijini.
Lakini bado ilimfanya Roma kutodhania ni kitu cha kawaida mpaka kuitwa Hazina kutokana na muonekano wake, maana kitu hicho kilikuwa kama vile ni ishara ya kitu flani lakini hakuweza kujua ni kitu gani.
Roma hakutaka kufikiria sana , alirudisha kama ilivyokuwa hazina hio ambayo hakujua maana yake na kisha akapotezea swala hilo kwa muda.
Baada ya kushuka chini aliweza kumuona Lanlan akiwa tayari ashaanza kunywa chai kwa kushikilia chapati za maji huku Qiang akiwa anamsaidia kumnywesha maziwa.
Kwa jinsi mashavu yake yalivyotuna ilikuwa ngumu kuamini kama alikuwa akimeza vizuri kile ambacho anakula.
Roma pia alishagazwa na uwepo wa Amina na Rufi waliokuwa wamekaa eneo la sebuleni wakiangalia runinga.
“Nyie mnafanya nini hapa asubuhi yote hii?”Aliuliza Roma huku akifinya mashavu yao.
“Ushasahau nimemuahidi Lanlan kumpeleka kucheza , napaswa kutimiza hadi yangu kwani leo ndio nipo free”Roma alimwangalia Lanlan na kuona alikuwa akimwangalia kwa namna ya kumwambia asikatae.
“Hubby , unaonaje tukienda pamoja , tukiwa wengi ndio itakuwa vizuri zaidi”Aliongea Rufi.
“Lazima niende pia , vipenzi vyangu nyie mnaenda pamoja na binti yangu lazima niwasindikize kama bodigadi , wote nyie ni warembo hivyo nina wasiwasi mtaibiwa”
“Unapaswa kuwa na wasiwasi labda na sisi tu lakini sio Lanlan , itakuwa vizuri kama wavulana wa huko hawatamuogopa Lanlan”Aliongea Nasra.
“Nasra wewe hujui tu , lakini Lanlan akishakuwa mkubwa atakuwa mrembo haswa , naamini majitu isiokuwa na adabu itamsumbua sana ili kumharibu mapema iwezekanvyo”Aliongea na kumfanya wote wamwangalie namna ambavyo amekosa aibu.
Baada ya Roma kupata kifungua kinywa aliingia kwenye gari ya Amina na kuendesha kuelekea Kawe eneo maalumu ambalo limekuwa maarufu kwa ajili ya michezo ya watoto.
Baada ya kufika watoto walikuwa wengi mno maana ilikuwa ni kipindi cha likizo ya mwisho wa mwaka.
Lilikuwa ni eneo lenye hali ya hewa nzuri kutokana na kuwa ufukweni na Roma alipata muda mzuri wa Kurelax maana tokea arudi ni mwendo wa hekaheka.
Baada ya Lanlan kucheza kwa muda mrefu ilikuwa ishatimia saa saba mchana na alirudi na kumwambia baba yake njaa inamuuma na Roma aliwachukua na kisha wakasogea upande mwingine eneo hilohilo sehemu yenye mgahawa wa kisasa na kisha walikaa na kuagiza chakula.
Wakati wakiendelea kula Lanlan aliacha kula na kuangalia upande wa nje huku akionekana kama kuna kitu amekiona na kukitamani, ilimfanya na Roma kuangalia upande wa nje na kugundua pembeni yao kuna mtu aliekuwa akichoma mishikaki.
Rufi aliweza kugundua alichokuwa akihitaji Lanlan na palepale alisimama na kuchukua pochi lake.
“Mnaweza kuendelea kula nitaenda kununua kwa ajili ya Lanlan”
Lanlan mara baada ya kusikia kauli ya Rufi aliinua kijiko chake kwa furaha zote na Roma aliishia kutabasamu na kufuta punje za pilau zilizokuwa zimemgandia pembeni.
Ni mara baada ya Rufi kumaliza kupewa mzigo wake wa mishikaki sasa wakati akijiandaa kulipia palepale alisikia sauti pembeni yake.
“I want those two”
Sauti ya kike pembeni yake iliweza kusikika , ijapokuwa mtu alieongea hio kauli alitumia kingereza lakini kidogo tu Rufi adondoshe mishikaki kwenye mchanga lakini alijizuia, hata hiyo alikuwa amechelwa kwani pochi lake lilimponyoka na kudondoka chini kutokana na kutetemeka.
Haraka haraka aliinama na kuchukua pochi lake na kumpatia muuza mishikajji hela yake na kutaka kuondoka bila ya kugeuza sura yake.
“Subiri”
Sauti ya kike ambayo iliagiza mshikaki ilimzuia kuondoka na yule mwanamke palepale alikimbia na kwenda kusimama mbele ya Rufi ambaye hakugeuka. “Hey! Ni wewe kweli.. Aaa..Shemeji!!!”Aliongea yule msichana huku akionyesha hali ya kuwa furaha na mshangao kwa wakati mmoja.
“Miss utakuwa umenifananisha”Aliongea Rufi huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Shemeji kwanini unajifanya hunijui , ni mimi Xiao Xiao , tulikutana wakati ulipochumbiwa na kaka yangu”Aliongea huku akiinamisha kichwa chake kutaka kumwangalia Rufi ambaye alikuwa na mabadiliko.
“Hapana sio mimi umennifananisha” Rufi alionekana kutetemeka mno.
Ukweli alilaani sana katika hali kama hio , hakujua imekuwaje akakutana na Xiao Xiao msichana ambaye alikuwa akimjua fika kwani alikutana nae katika ulimwengu wa kijini kabla ya kutoroka.
*******
Nje ya hoteli ya Serena alionekana Suzzane akishuka kwenye gari aina ya Audi ya rangi nyekundu na kisha kumpatia Valet ufunguo baada ya kutoa pochi yake.
Baada ya kuweka mkoba wake kwenye kwapa palepale alianza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hilo la hoteli huku akigeuka nyuma akiangalia kama kuna mtu anamwangalia.
Suzzane alikuwa amebadilisha mtindo wa nywele , siku hio alikuwa amevalia Wigi na kumfanya kuonekana mtu mwingine kabisa.
Baada ya kuingia eneo la mapokezi na kupokelewa na mwanadada aliepamba uso wake kwa tabasamu palepale aliongea kidogo na mwanadada yule alichukua simu yake na alionekana alikuwa akiongea na ndani ya dakika chache alitabasamu na kisha akampa ishara Suzzane ya kuendelea kutembea.
Suzzane mara baada ya kuingia kwenye Lift alivuta pumzi kwa kutuliza presha yake na kisha alibonyeza kitufe kuruhusu Lift hio kumpeleka katika Floor husika.
Alijiangalia mavazi yake kwa kujichunguza na kuona yupo vizuri na na amependeza , kwa jinsi ambavyo alikuwa na wasiwasi ni kama mwanamke ambaye anaenda kukutana na mpenzi wake kwa mara ya kwanza.
Baada ya Lift kupandisha na kufika floor ya tatu , ilisimama na kufunguka na alionekana mwanaume alievalia suti na miwani nyeusi.
Suzzane alimpiga mwanaume huyo jicho la pembeni kumchunguza lakini hakuonyesha hofu na yule mwanaume hakuonyesha kumjali Suzzane kwani aliingia kwenye lift na kisha kutulia bila ya kubonyeza kitufe chochote.
Suzzane hakuwa mshamba , alijua pengine mwanaume huyo alikuwa akielekea Floor sawa ndio maana hakugusa vitufe lakini hakuacha kuwa na wasiwasi.
Baada ya Lfit kufunguka katika Floor namba sita wote kwa pamoja walitoka na mwanaume yule alichukua upande wa kushoto na Suzzane alichukua upande wa kulia.
Suzzane alijikuta akipatwa na ahueni na kisha alitembea kwenye Korido yenye msururu wa vyumba na ndani ya dakika chache tu aliweza kufika katika mlango wenye namba 123 na aligonga mara moja na dakika hio hio mlango ulifunguliwa na kisha akaingia.
“Shosti unaonekana kuwa na presha juu juu”Sauti nyororo ilisikika ikiongea na kumfanya Suzzane kuhema kwa nguvu kwa hali ya ahueni.
“Sijui nakua paranoid au nini lakini niseme hata nikienda chooni tu nakuwa na wasiwasi”Aliongea Suzzane huku akilazimisha tabasamu na kujaribu kuangalia mazingira.
Nadia alitoa tabasamu na kisha alimsogelea Suzzane na kumpa ishara ya kutaka kumkumbatia na Suzzane hakuwa na hiyana ya kukataa kumbatio.
“Unafanya vizuri Suzzane , ukishazoea kila kitu utaona ni kawaida”Aliongea na Suzzane lile kumbatiao kidogo lilionekana kuwa dawa kwake kwani aliweza kutulia.
“Unaonekana kuwa mzoefu Nadia , ulishawahi kufanya kazi ya hatari kama hii?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Nadia kutoa tabasamu.
“Nishawahi kufanya kazi ya hatari mara tatu ya hii, mwanzo wakati napewa misheni ya kufanya nilikuwa kama wewe tu ndio maana nimesema unafanya vizuri”Aliongea na kisha Suzzane alimimina maji kwenye glasi na kisha akampatia Suzzane huku akimwambia akae.
Suzzane baada ya kunywa maji yale alijihisi angalau ameweza kupoa.
“Presha ilipanda zaidi mara baada ya kukutana na mtu kwenye Lift , alikuwa amekaa kama mwanausalama, aliniogopesha mno , nikajua ni watu wa Raisi Senga”
“Oh .,.. huyo atakuwa ni mwanasalama kweli , hakika unafanya kazi nzuri Suzzane , lakini hupaswi kuwa na wasiwasi , kuna raisi kachukua makzi ndani ya hii hoteli”
“Raisi!!!”
“Ndio , ni taarifa za siri sana za kiusalama , nimejua hayo kutokana na kwamba nimekutana nae kwa ajili ya mazungumzo, kwasasa sitokuambia ni raisi wa taifa gani”Aliongea Nadia huku akitoa tabasamu.
Na kisha alisimama na kwenda kutoa mvinyo kwenye jokofu na ksha akafika nao na kuuweka mezani na kuanza kujimiminia.
“Hongera Suzzane kwa mara nyingine, kila kitu kimeenda kama tulivyopanga”Aliongea Nadia na huku akimpatia Suzzane glasi ya mvinyo na mara baada ya Suzzane kupokea alimpa ishara ya kugongesheana Cheers.
Baada ya Suzzane kunywa ile Wine kidogo alijikuta akitoa macho kutokana na utamu wake.
“Vipi umeipenda?”
“Ina radha tamu kweli?”
“Yeah hii ni Chateu Margaux, nilipanga kushare hii zawadi na wewe siku ya leo”Aliongea na kumfanya Suzzane kutabasamu na kuangalia chupa ya Wine hio.
Hakuwa mshamba alijua huo ni mvinyo wa bei ghali sana , pengine kama angetaka kuununua basi angefilisika.
Waliongea kwa dakika kadhaa huku wakionyesha kucheka na kufurahi kwa pamoja kama marafiki na kumfanya Suzzane kupotezea hofu yake.
“Kila kitu kimeenda kama tulivyopanga Suzzane, unajisiije mara baada ya kufikia hatua hii?” “Wakati naanza kufanyia kazi huu mpango sikuwahi kudhania kama ungefanya kazi, yaani hapa hisia zangu siwezi kuzielezea”
“Suzzane kila kitu ndani ya dunia hii kinawezekana ukiwa una taarifa sahihi”Aliongea.
“Ilikuwaje mkaweza kuja na huu mpango?”
“Ni maswala ya kisaikolojia Suzzane , kama ungekuwa na mafunzo ya kijasusi basi ungejua mambo mengi yanawezekana sana kwa kusoma saikolojia ya mtu na tabia zake, tulichofanya ni kufaitlia maisha ya Salihi ya kila siku ili kujua tabia zake, we did it randomly at first without any plan lakini mara baada ya Asha kuingia kwenye Equation tuliweza kufinilize kila kitu na here we are”Aliongea .
“Unajua mpaka sasa kuna baadhi ya vitu nashindwa kuelewa , Salihi kutoka kimapenzi na mama yake wa kambo ni swala ambalo nashindwa kuliprocess kabisa”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kutoa kicheko.
“Hii dunia Suzzane ina mambo mengi na huwezi kuyajua yote , laiti ungejua hata nusu robo tu basi maisha yako yangebadilika kabisa, anyway tunapaswa kuachana na hayo , leo nataka kukuambia kwamba kesho ndio siku yako ya mwisho ya misheni yako”
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha kesho ndio siku ya kumshawishi Raisi Senga kujiunga na Umoja wa Ant- Illuminat , lazima iwe kesho Suzzane kabla hajalazimishwa kusaini mkataba wa kishenzi”
“Sijakuelewa swala hili linahusiana nini na Mkataba wa kishenzi?”
“Suzzane we are Ant – lluminat, ikimaanisha kwamba tunaenda kinyume na namna dunia inavyoendeshwa , hiki ndio tunachopambana nacho, kuna kitu kikubwa sana kimepangwa kukamilishwa hapa Tanzania na mimi misheni yangu ni kukizuia kwa namna yoyote lakini kabla hilo halijatokea wewe unapaswa pia kukamilisha misheni yako, kumbuka ulichoambiwa kule Qatar”Aliongea na kumfanya
Suzzane kumwangalia Nadia kwa macho ya kuuliza.s

ITAENDELEA.
 
Thank you Singano .Jr.....tupo tunakufuatilia kwa ukaribu sana. Mambo ni moto mambo ni fire. Hakika Simulizi imejaa ikajazika, imepangwa ikapangika...Hongera kwa weredi wa hari ya juu Ndugu yetu Singano Pluto Jr.

Tunasubiri mwendelezo.
 
SEHEMU YA 589.

Wanajeshi wote hakuna ambaye aliamini kama Kamanda wao ndio amekufa hivyo ,ilikuwa ni kama vile wapo ndotoni na muda wowote wangeamka na kuona sio kweli.

Kamanda mwenye cheo cha ubrigedia jenerali alikuwa amekufa kiwepesi kwa namna hio .

Matendo ya Roma yaliwaambia kabisa hawakuwa wakiota bali walichokuwa wakiona ni uhalisia mara baada ya kurushiwa mwili wa Kamanda wao uliolegea shingo.

“Baba kamuua Brigedia Makwera haitaleta shida zaidi?”Aliuliza Damasi ambaye alikuwa kwenye taharuki kwa kila ambacho ameshuhudia.

Ni moja wapo ya watu waliokuwa na woga zaidi ya wengine wote na alimuogopa Roma maradufu , ijapokuwa mwanzoni alikua akijua ana uwezo mkubwa na ni mkatili wa hali ya juu lakini kwa matendo ambayo ameyaona kwa macho yake alijihisi kabisa huenda Roma sio mtoto wa Raisi Senga na alisingiziwa mahali.

“Kuna kipi cha kufanya wakati tayari unaona ashakufa”Aliongea Kamanda Mstaafu ,Mzee Kweka huku akionyesa hana wasiwasi wowote , ilikuwa ni kama vile hata yeye angechukua maamuzi yaleyale.

Lakini huo ndio ukweli inawezekana Roma alitengenezwa kisayansi na akawa na ukatili wa hali ya juu na kuua kwake ikawa ni kitu kidogo lakini ukweli ni kwamba Afande Kweka ni moja wapo ya watu wakatili sana sana ambao washawahi kuwepo ndani ya Taifa la Tanzania , watu wengi ambao walimpinga ndani na nje ya jeshi aliwaua kwa siri sana kwa mbinu tofauti tofauti , hivyo anachokifanya Roma ni kama karithi tu na utofauti wake na Roma ni staili zao tu za kuua , yeye alikuwa akiagiza watu wake kutekeleza vifo lakini upande wa Roma alikuwa akiwa hadharani bila hofu yoyote.

Damasi aliekuwa akitaka kutokwa na machozi alitaka kuongea lakini Afande Kweka alonyesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumsikiliza na palepale aliwapa ishara walinzi wake wamsogelee na kisha akatoa maagizo ambayo waliyafanyia kazi kwa haraka haraka.

Upande wa Denisi lisha ya kuonyesha mwonekano usiokuwa wa kawaida kama wa kukata tamaa lakini yeye hakuona shida kwa watu waliokufa.

“Kamanda wenu ndio huyo amekufa , je bado mnataka kuendelea kumuonyeshea utii muungane nae au utii wenu mtauojesha kwa taifa?”Aliuliza Roma huku akitoa tabasamu lake lilelile la kuogopesha na kuwafanya wale wanajeshi kushikwa na baridi ya woga

“Master Roma , tulilazimishwa kufanya hivi tu , kwanzia leo tupo tayari kukutambua kama Kamanda wetu mpya”Aliongea mmoja ya mwanajeshi mwenye jino la mbele lililokatika.

“Upo sahihi Kamanda Makwera alitumia madaraka yake vibaya kwa faida zake mwenywe , alistahili kufa , nipo tayari kufanya chochote ambacho Master Roma ataniambia”Mwingine aliunga hoja juu kwa juu lakini kauli zao hazikumfurahisha Roma hata kidogo na palepale alichukua bunduki kutoka kwa mwanajeshi aliekuwa karibu yake na ilikua kwa spidi sana wale wanajeshi wote wawili waliokuwa wakimpamba walipasuliwa kichwani palepale na kudondoka chini.

Kila mmoja alimwangalia kwa mshituko mara baada ya tukio hilo na walishindwa kujua anataka kufanya nini.

Roma hakujali mshangao wao kwani alitupa siraha pembeni huku akiwa na uso wa kutokuathirika na kile alichokifanya.

“Bado hamjaelewa tu , nimesema onyesheni utii wenu kwa Taifa sio mimi , au mnanniona mimi ni Makwera wenu kudhania mimi ni mhaini ambaye muda wowote naweza kuanzisha vita?”Aliongea Roma na wale wanajeshi wote waliangaliana huku sura zao zikipauka kwa wasiwasi

Mpaka hapo walijua Roma ni mtu ambaye hatabiriki ndio maana moja kwa moja walikosa ujasiri wa kuongea tena kwa kugopa kusema kimakosa.

“Master Roma tafadhari punguza jazba , tupo tayari kupigana kwa ajili ya taifa letu tutapigana zidi ya wahaini wote wa nchi mpaka mwisho wa maisha yetu “Aliongea mmoja wapo alieonekana kumuelewa Roma na wengine wote walionekana kuelewa na waliongea kwa sauti kwamba wanakwenda kupigana na kuonyesha utii kwa manufaa ya taifa na sio kwa ajili ya mtu mmoja mmoja.na hata wale waliojificha waliweza sasa kutokea misituni na kuungana na wengine.

Ni kama vile dakika hio ilikuwa ikisubiriwa kwani muda uleule waliingia wanajeshi makomandoo kwa spidi zote na kuimarisha ulinzi huku wale waliokuja na Marehemu Afande Makwela wakiponywa siraha zote na kukalishwa chini ya ulinzi.

Dakika hio hio Brigedia Jenerali wa jeshi mkoa waSongea , Afande Murasa aliiweza kufika akiwa na kombati za jeshi.

Na mara baada ya kutoka tu kwenye gari alimsogelea Afande Kweka na kumpigia saluti ya heshima na kugeukia wanajeshi aliokuja nao na kuwapa maelekezo huku yeye akiongozana na Afande Kweka mpaka kwenye ofisi yake ndogo kuanza mazungumzo.

Kila kitu kilitokea kwa kasi sana , ni swala la dakika kama ishirini tokea kuanza kwake na kumalizika .

Afande Tobwe alimwangalia Roma bila kuongea chochote , ijapokuwa walikuwa ni Wakwe lakini alimuogopa.

Kila mwanajeshi aliekuwa njiani alimpishaRoma kwa woga sana na yeye hakujali na muda huo alikuwa amechafuka mwili mzima kwa damu na alitembea kuelekea upande wa nyuma alikomuona Denisi.

“Kaka niseme ujasiri wako umetuokoa , kwa staili hii nadhani kwanzia leo hii kila mtu ndani ya jeshi atatuogopa”Aliongea Denisi mara baada ya kusogelewa na Roma.

“Ndio unavyoona?”Aliongea Roma kwa sauti kali na ghafla tu huyu hapa ashaishika shingo ya Denisi na kuining’iniza hewani.

Kitendo kile kilishangazaza watu sana akiwemo Damasi mwenyewe na hata afande Kweka ambaye alishatoka nje akiambatana na Afande Murasa.

“Master Roma tafadhari punguza hasira?”Walinzi waliongea kwa hofu.

“Ndio, Denisi ni mdogo wako”Wasaidizi na walinzi walijaribu kubembeleza

“Roma tafadhari naomba usimuumize mdogo wako”Sauti ya Damasi iliweza kusikikika kwa nyuma huku akisukuma watu kupita kusogea mbele.

Damasi hakujali tena kule kumuogopa Roma bali alimsogelea na kumshika mkono wake wa kushoto akimbembeleza.

“Roma mwanangu nakuomba , mdogo wako najua amefanya makosa mengi nyuma lakini sasa hivi amebadilika , unatakiwa kumpa na yeye nafasi ya kijirekebisha , huwezi kumshambulia tu bila sababu”Aliongea huku akianza kutoa machozi ya kiutu uzima.

“Roma umesema unaamini Denisi ndio anakufanyia njama lakini huwezi kumshambulia bila ushahidi”Aliingilia Afande Kweka.

Ijapokuwa alikuwa akisita kumuachia Denisi lakini kutokana na mbinu nzuri aliokuwa nayo Denisi kujificha hakuwa na uwezo wa kumuua bila kuwa na ushahidi wa kueleka.

Roma alimwangalia Denisi kwa macho ya kumpa tahadhari na kisha akamsukumia mbali.

Damasi alijikuta akihema kwa ahueni huku akimwangalia Roma kwa macho ya shukrani.

“Brigedia Murasa amenipa taarifa hapa ya kinachoendelea na Afande Tozo yupo Dar es salaam na uchunguzi unakaribia kumalizika na wote waliohusika watakamatwa na kupelekwa mbele ya sheria na hali ya hewa ikitulia watatuutaarifu”Aliongea Afande Kweka.

“Nadhani wanajua kabisa kilichoendelea hapa na wanaangalia tu namna ya kulimaliza hili swala”

“Haijalishi makusudio yao ni nini , walionekana wapo tayari kutumia hela zao kutaka kutuyumbisha lakini sasa yameisha na hili watalimaliza kwa njia zao za kisiasa”

“Vyovyote vile ni sawa tu , hata hivyo sitaki kuuwa viumbe dhaifu tena”Aliongea Roma na kisha aliondoka.

Wakati tukio lote hilo linatokea Edna alikuwa yupo upande wa nyuma.

Muda ambao Roma alifika upande wa nyuma kuingia kwenye Korido ya chumba chao aliweza kumuona Edna ambaye alikua akitembea kurudi nyuma na mbele akionekana kama mtu mwenye kuchanganyikiwa.

Lakini alijikuta akisimama mara baada ya kumuona Roma akiwa kama mwenye hali ya furaha lakini alijikuta akishituka mara baada ya kuona damu katika mwili wake.

Roma aliweza kujua mshangao wa Edna ulikuwa ukihusiana na nini na alijikuta akinusa shati lake lwenye damu na kutoa tabasamu la kifedhuli.

“Mh .. damu zinanuka vibaya hizi , Edna mke wangu usiwe na wasiwasi nitaenda kuoga kwenye chumba kingine”Aliongea Roma huku akitaka kugeuka kuelekea upande mwingine wa vyumba lakini Edna alimkimbilia na kumshika mkono.

“Unaongea kuhusu nini wewe , kwanini ukaoge kwenye chumba kingine , unataka watu wanifikirie vibaya, tumekuwa pamoja kwa muda mrefu hivyo nishazoea , ni damu tu na vinyama nyama kwanini unataka kuyakuza, hebu nifuate huko”Aliongea huku akitangulia kuingia ndani.

Roma moyo wake uliridhika mara baada ya kusikia meneno hayo kutoka kwa mke wake na alishukuru kumuona Lanlan hayupo.

Edna alimwingiza Roma mpaka kwenye bafu lao na baada ya kufika alifungua vifungo vya shati lake pamoja na suruali na kutupia pembeni na baada ya hapo alifungulia bomba la maji ya mvua na kuacha yamwagikie Roma huku yeye akitoka tena na kuchukua sabuni maalumu ya kuogea ya marashi na kurudi nayo akiwa ameshikilia taulo.

Roma alishangazwa na namna Edna ambavyo hakuzingatia mwili wake uliokuwa hauna nguo .

“Mke wangu ni lini umebadilika , nakumbuka mara ya mwisho ulikuwa na aibu hata ya kuingia kwenye chumba changu”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushituka kwani akili yake haikuwa ikizingatia mwili wa Roma bali damu zilizokuwa kwenye mwili wake.

“Nini?”

“Ndio maana wahenga wanasema ndoa ni kaburi la mapenzi , nadhani kuanzia sasa inabidi nikuite Mama Lanlan”Aliongea Roma kwa kumtania.

You Suck , nilikuwa nikijaribu kukusaidia kukusafisha na sasa unaanza kunichokoza , nitaenda kulala na Lanlan mimi wewe endelea”

“Edna my Darling , nilikuwa nikitania , usichukulie siriasi , ukiachana na hayo Lanlan yuko wapi?”

“Karudi kulala tena kwenye chumba cha babu yake , inanifanya niwe na wasiwasi maana kila akishiba tu anakimbilia kulala”

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi , bado ni mdogo na kuvuna nishati za mbingu ni kuumiza ubongo hivyo ni kawaida, kipindi hicho mimi sikuweza hata kuuruhusu usingizi unichukue ili kuweza kuishi , nilihitajika kuvuna nishati kadri niwezavyo ndani ya muda mfupi kabla ya maadui zangu hawajanipata .. lakini kwa yeye kila kitu anacho na hana haja ya kuhofia usalama wa maisha yake , hivyo naweza kusema amebarikiwa kuliko nilivyokuwa mimi , tena hili jambo linanijia akilini sasa hivi , tokea nije Tanzania nilikuwa nikijiwazia mimi mwenyewe lakini siku hizi kila ninachofanya ni kwa ajili yako na yeye.”Aliongea Roma huku akiendelea kuwa bize na kujisafisha.

Na kukabidhiwa Taulo na mke wake kujifuta maji tayari nguo Edna ashaziandaa na kumsaidia kuvaa naRoma mara baada ya kukaa chini picha ya Denisi ilimjia akilini mwake na kumfanya kuanza kuwa na wasiwasi usioelezeka.

Roma alisita sita kumfanya Denisi chochote kutokana na kujali uwepo wa Damasi tu.

Nitatafuta namna ya kumuua kwa siri”Alijiwazia Roma.

“Unafikiria nini tena?”

“Sio jambo kubwa , nawaza ni kwa namna gani huyu mzee ataweza kulimazliza hili swala”

“Najua sikupaswa kuuliza kilichotokea , lakini nataka kusikia ukweli wote kutoka kwako”

“Nini unataka kujua?”

“Kama bado tupo hatarini?”Aliongea Edna akiwa na wasiwasi.

“Bado nipo na hivyo usiwe na wasiwasi”

“Kama ni hivyo basi niahidi kitu kimoja , kama kitu chochote kitatokea niambie , unanijua mwenyewe mimi sio mwanamke ambaye ni mjinga , nina uwezo wa kuchanganua mambo pia”Aliongea kwa upole na kumanya Roma kumuona mke wake amegeuka na kuwa mke mtiiifu mbele yake na kuonekana kama mtoto.

Roma palepale alinyanyua mkono wake kutaka kushika shavu lake lakini mara baada ya kufikiria kitendo alichokifanya dakika kadhaa zilizopita alijikuta akiishia njiani na kuurudisha , ni kama akili yake ilikuwa ikihofia kumchafua mke wake.

Edna aliona kitendo kile na palepale alichuhukua mkono wake na kuuweka kwenye shavu lake.

“Kwanini hujafanya ulichodhamiria wakati sijakuambia uache , au unaniona mimi mchafu?”

“Hapana mikono yangu ndio nahisi bado inanuka damu na hata kucha zangu sijazisafisha vizuri”

“Nimeongea lolote kuhusu hilo ?”Aliuliza Edna huku macho yakianza kuwa mekundu.

“Mhmh..”Roma alishindwa kuendelea kuongea zaidi ya kuguna na Edna alimsogelea karibu zaidi.

“Hivi unajua kwamba hata mikono yako ichafuke vipi na damu au ni maiti ngapi umweza kushika kwangu ni mikono hii hii ambayo ilinisaidia kipindi nilichokuwa kwenye matatizo , ni mikono hii ambayo ilinikumbaita na kunifanya nilale na ni hiii ambayo ilimshikilia binti yangu .. haitotokea nikaiona ni mikono michafu kwasababu hii ni mikono ya mume wangu , mikono ya mtu ninaempenda”

Roma aliguswa na maneno yake na hakuamini kama ni Edna ambaye anaongea.

“Edna mke wangu nani kakuandikia Script au ni zile roboti za mtandaoni”Alitania Roma.

“Mimi nipo siriasi”Aliongea na kumfanya Roma kumeza utani wake na palepale alisimama na kumbeba juu juu na kumrushia katikati ya kitanda na Edna ashajua nini kinakwenda kutokea.

“Tiusifanye sasa hivi bado ni mapema na sijaoga bado”Alilalamika .

“Mke wangu wewe hujali kama mikono yangu ni michafu kwanini nikuache uoge , isitoshe My darling wife unanukia vizuri muda wote”Aliongea na baada ya pale alijichimbia kwenye kifua cha mkewe na kuanza kazi na ndani ya madakika kadhaatu Edna hakuweza kumpinga tena na kumuacha afanye atakavyo lakini ghafla tu Roma aliacha anachokifanya na kusimama huku akiangalia mlangoni.

Edna alishangaa mara baada ya Roma kuacha lakini alielewa mara baada ya kuona mlango ukifunguliwa.

“Mommy, mommy! Is dady back”(Mama , mama , je baba amerudi)

Lanlan mara baada ya mwili wake wote kuingia ndani alianza kukagua mazingira , mashavu yake yalitingishika mara baada ya kuwaona wazazi wake na alianza kuonyesha hali ya kutoelewa hali inayoendelea.

“Dady ,mommy what kind of game are you playing?”Aliuliza Lanlan akisema ni mchezo gani wanacheza.

Edna alijikuta akibadilika rangi na kuwa mwekundu , alitamani aingie uvunguni , ilikuwa ni afadhari nguo zake bado hazikutolewa mwilini.

“Baba na mama yako tunachukua mazoezi sawa chubby”Aliongea Roma

“Mazoezi!! , Lanlan anataka pia kuchukua mazoez na nyie”

“Lanlan utachukua mazozi kama haya ukishakuwa mkubwa… sasa hivi nenda kacheze na babu yako , usije huku ndani mpaka tutakapotoka”Aliongea Roma lakini Lanlan alionyesha hakufurahishwa na kauli ya baba yake na aliendelea kumwangalia Roma kwa kutia huruma kwani aliona ni kama vile baba yake anamfukuza.

Roma suruali yake ilikuwa ikishituka shituka kama ina uhai na akili yake ni kama anaelekea kuupata uchizi.











SEHEMU YA 590.

Hali aliokuwa nayo Roma ilimfanya Edna kutamani kucheka huku akisahau aibu yake.

“Lanlan kuwa mtoto mzuri na utoke , Lanlan ushawahi kuonja nyama ya Kondoo wa kukaanga?”

“Kondoo ndio wanyama gani baba?”

“Ni wanyama wenye tabia ya kulia, ‘Baa .. baaa’ , ni nyama nzuri sana ikikaangwa, nitahakikisha unaonja kitu kipya kama utaenda kuendelea kucheza na babu yako”

“Daddy you have to keep your promise , I’ll go to play wirh great grandfather”Aliongea akimaanisha kwamba Roma anapaswa kutii ahadi yake na yeye anaenda kucheza na babu yake mkubwa na akakimbilia nje huku akisahau kufunga mlango tena na kumfanya Roma kung’ata meno yake kwa hasira lakini hata hivyo alimuona Lanlan ni mwepesi kudanganyika kila nyama inapotajwa na alishuka kwa hasira na kuubamiza mlango.

“Huyu litoto tundu napaswa kulifundisha , anaachaje mlango wazi kwa mfano” Aliongea na kama chui alimrukia Edna kitandani na namna suruali yake ilivyomtoka kiunoni huenda ni rekodi mpya ya dunia.

Dakika chache mbele chumba chote kilijaa sauti za mguno wa kimahaba kutoka kwa Edna.

*******

Upande mwingine jijini Dar es salaam wakati Roma yeye akijipongeza baada ya kuua ilikuwa ni zamu ya Raisi Senga kukamilisha kile alichopanga.

Hakuamini kila kitu kilienda kama alivyopanga , ijapokuwa namna ambayo Roma ametatua tatzio ilikuwa ndio kama alivyotarajia lakini ukweli ni kwamba aligundua alikuwa na mtoto ni katili mno na kuzidi kumugoopa mara mbilimbili.

Katika jengo la ikulu chumba cha mikutano kulikuwa na kikao kizito ambacho kilikuwa kimeitishwa tokea jana yake na hakikuhusisha wale watu tu ambao walikuwa wamehusika katika mpango wa kumtengenezea Roma matukio.

Raisi wa Visiwani pia alikuwepo katika kikao hicho na baadhi ya wanasiasa wakubwa ambao Raisi Senga alikuwa akijua kabisa utulivu uliokosekana nchini ulianzishwa na wao.

Muda huo mara baada ya kuingia katika chumba hicho na kunagalia sura za kila mtu alietii wito alijikuta akitabasamu ndani kwa ndani na kujiambia yes huo ndio muda wa kukamilisha ndoto yake ya siku nyingi.

Wakati kikao hicho kikiwa kinaendelea ndani ya ikulu, upande wa mitandaonni wananchi walikuwa wamecharuka mara baada ya sauti zinazosemekena kuwa za Waziri wa nishati , Waziri wa ulinzi, Afande Makwera na Mke wa raisi Kigombola kusambaa kwa kasi.

Maudhui yaliokuwa kwenye sauti hio ndio kitu kilichowafanya wananchi kuweza kusikia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwani mipango yote ya Afande Makwera kushawishiwa kumshambulia Afande Kweka na mjukuu wake ziliweza kusikika , ijapokuwa hakukuwa na uthibitisho wa moja kwa moja wa kusema sauti hizo zilikuwa za watu hao lakini zilifanya kila mtu kuwa katika Dilema na kubwa zaidi ni kwamba mtu alieanza kuzisambaza alisifika kuwa kinara kwa kumkosoa Raisi Senga mtandaoni.

Ni dakika chache tu mara baada ya Sauti hizo kusambaa ndipo taarifa ya kifo cha Afande Makwera kilipoweza kutangazwa kwa kuthibitishwa na mkuu wa majeshi wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijinni Dar es salaam , huku sababu halisi kuwekwa wazi , uthibtishwaji wa kifo hicho na namna kilivyotokea haikuhitaji elimu ya kuthibitisha yale maongezi ya sauti yaliokuwa yakisambaa mtandaoni kuwa kweli.

Lakini swali moja tu liliibuka nani ambaye aliwarekodi wenzake kwani vikao hivyo ni vya siri,lakini ilibakia kuwa habari ilioibua mjadala na kumshuku huyu na huyu .

Wakati hayo yanaendelea upande wa Mheshimiwa raisi wa visiwani alikuwa amenywea sana kiasi cha kushindwa hata kumwangalia Raisi Senga usoni , ile hali yake ya kujiamini aliokuwa nayo siku kadhaa zilizopita ilikuwa imemshuka sana na hakuwa yeye tu bali pia kwa baadhi ya wanasiasa wengine.

Hali ya woga ilianza kuwatawala kila mmoja huku wakiwa kama watu ambao wanasubiri hukumu yao kutolewa na Senga, lakini kwa wakati mmoja na wao walikuwa na maswali lukuki imekuwaje mipango yao ikawa inajulikana kwa uwazi namna hio na walianza kuangaliana kwa hasira.

Wakati ambao walikuwa wakijiuliza maswali hayo , upande wa Raisi Senga na yeye alikuwa akijiuliza swali ni nani ambaye yupo nyuma yao , kwani hata kabla ya kufanya kikao hicho alikuwa na mazungumzo ya siri na Raisi wa Visiwani na kujaribu kumhoji lakini mwisho wa siku na yeye hakuwa na jina la mtu ambaye yupo nyuma yao zaidi ya kumjua akiitwa The Don.

Raisi Senga ijapokuwa kila kitu kilienda upande wake , lakini kile ambacho siku zote alikuwa na wasiwasi nacho ni kama kimefufuka upya.

“The Doni amerudi tena?”Ndio kauli aliojiambia.

Raisi Senga ni kwa muda mrefu sana ambao alikuwa akihitaji kumjua The Doni , mtu ambaye alikuwa nyuma ya hayati Raisi mstaafu Kigombola lakini mpaka siku hio hakuwahi kumjua wala kumuotea ni nani , mwanzoni hisia zake zilimwambia ni Roma lakini hakuweza kuthibtisha hilo na kwa yalitokea ni kama yamemthibtishia kabisa kwamba Roma hakuwa The Doni.

Hivyo licha ya kushinda mpango wake lakini bado moyo wake ulikuwa mzito juu ya huyu mtu aliejiita The Doni na kuna hisia pia zilimwambia huenda Denisi ana ukaribu na The Doni kwasababu Yan Buwen alikuwa na ukaribu na The Doni kwa maelezo ya hayati Kigombola, lakini licha ya kuwaza sana hakutaka kusumbua kichwa chake kwanza na kuanza kufikiria namna ya kumaliza swala lililokuwa mbele yake.

Kikao hicho kilijumuisha na Katibu mkuu wa Chana cha Maendeleo na waliweza kujadiliana kwa zaidi ya masaa manne huku mwishoni wakikubaliana vitu vingi.

Lakini matokeo ya kikao hicho yalijumuisha kwa kukamatwa kwa baadhi ya watu ambao sauti zao zilisikika na jeshi la polisi kwa ajili ya uchunguzi huku mheshimiwa Raisi wa Visiwani akipewa nafasi ya mwisho ya kwenda kutuliza wananchi wake ndani ya masaa mawili tu.

Wakati kila kitu kikienda kila alivyopanga hatimae Raisi Wa Visiwani mheshimiwa Huseni Husani alitoa hutuba fupi akiwa ikulu na mbele ya jopo la waandishi wa habari na viongozi wenzake kuwaasa wananchi kuwa na utulivu huku akienda mbali kukanusha Roma kuhusika katika mauaji ya Kamanda Razaq na kusema yote hio ilikuwa ni mipango ya adui kutaka kuigawanya nchi na uchunguzi yakinifu unaendelea kumbaini.

Baada ya hotuba ya Raisi wa Zanzibar , Muongeaji mkuu wa Serikali alitoa Tangazo kwamba siku inayofuata Mheshmiwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atalihutubia taifa kupitia ikulu ya makao makuu ya nchi mkoani Dodoma.

Kutarajiwa kwa hotuba yake hio iliwafanya wananchi wa Tanzania kuwa na shauku ya kutaka kujua kile ambacho Raisi anakwenda kuhutubia.

*********

Kabla hayo yote hayajatokea upande mwingine mwanadada Suzzane ni moja ya watu ambao walikuwa kwenye tafakari nzito sana kuhusu bosi wake Edna kwa kauli yake ya mara mwisho ambayo alimpatia siku moja kabla ya kustaafu kuwa CEO wa kampuni.

“Suzzane kwanzia sasa nataka uachane na uchunguzi wote wa maswala yanayohusiana na mama yangu , najua kila kitu kwa sasa na nawaza namna ya kukabiliana na kilichopo mbele yangu , sitokuambia ni lakini taarifa hii ni siri kwako na asitokee mtu yoyote ukamwambia”

Kauli hio ya Edna ilimchanganya sana mwanadada Suzzane , sababu kubwa ya kumchanganya ni kutokana na namna ambavyo aliitamka , lakini pia kukosa maelezo sahihi ya kile kilichotokea siku kadhaa zilizopita katika hoteli ya Peacock.

Suzzane alikuwa ni tofauti na Edna katika siku ile , alikua kwenye mshangao na maswali mengi kwa kile kitu kilichotokuwa kimetokea , alijiuliza Edna alitoa wapi ile pete na swali hili hakujiuliza yeye mwenyewe bali aliulizwa na wanachama ambao walikuwa ni wa taasisi ambayo ni kama mara ya pili anaisikia jina, jumuia ya siri ya kitaasisi iliojiia Ant- illuminat.

Kitu pekee ambacho kilimfanya Suuzzane kutaka sana kujua kuhusu mama yake Edna ni kutokana na kifo cha mpenzi wake Dr Elvice Daniel , siku zote alitamani kulipa kisasi ka wale waliomuua mpenzi ake kabla hata hawajafunga ndoa lakini mpaka wakati huo hakuwa amepata mwanga namna ya kulipiza kisasi.

Sasa ni masiku tokea mrembo Suzzane akiwa katika mawazo , siku ambayo nchini Tanznia kukiwa na mambo makubwa yanayoendelea , Suzzane yeye alikuwa ndani ya jiji la Doha nchini Qatar.

“Karibu sana Suzzane kwenye umoja wetu wa siri , umefanya maamuzi sahihi sana”Sauti ya mrembo Nadia Alfonso iliweza kusikika ndani ya gari la kifahari refu aina ya Limuosine , gari yenye ufahari wa kila aina ndani yake na kumfanya Suzzane kuwa mara yake ya kwanza kupanda gari aina hio.

“Asante Nadia lakini bado ni mwenye wasiwasi?”Aliongea Suzzane na kumfanya Nadia kutabasamu kidogo.

“Wasiwasi wako ni wa muda , ukishajua nini maaana halisi ya umoja wetu basi hofu yako yote itaisha , kwasasa uvae ujasiri unapokwenda kutamblishwa kwa mara ya kwanza na kupewa nafasi ya awali ya uanachama na kupokea misheni yako ya kwanza ya kujithibitisha”

“Misheni ya kwanza ya kujithibitisha!!!?”Aliuliza Suzzane na kumfanya Malkia wa sheria , mrembo Nadia kutoa abasamu na kuangalia nje.

“Tushafika Suzzane”Aliongea Nadia na kumfanya Suzzane kuangalia mazingira ya nje na kuweza sasa kuelewa kwamba akili yake ilikuwa mbali sana kwnai hakujua hata ni namna gani waliweza kuingia ndani ya ukuta mrefu huku mbele yao kukiwa na jengo kubwa kama hoteli.

*******

Muda wa mchana Roma aliweza kutoka chumbani bila wasiwasi , lakini upande wa Edna alikuwa na aibu kwani ni kama vile kila mtu ndani ya nyumba hio alikuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea na aliishia kuangalia chini huku akitembea kwa mwendo wa kujilaizmisha kwani miguu yake ilikuwa haipo vizuri.

Roma mara baada ya kutokezea kwenye bustani mahali ambapo Afande Kweka hukaa na kuota moto, aliweza kumuona mzee wake akiwa na Lanlan wakiwa katika umakini mkubwa wa kimaongezi.

“Nyie watu mnaongea nini mpaka kuwa na umakini hivyo?”Aliuliza Roma kwa kiswahili

“Daddy , babu alikuwa ananihadithia stori namna alivyoweza kuwashinda watu wabaya”Aliongea .

“Babu yako huyo anajua kujisifia tu kama utaendelea kumsikiliza”

“Ukorofi huo”Aliongea huku akimpotezea na kujivuta mwili na muda uleule kijakazi aliweza kuwasogelea.

“Master mtu wa hoteli ametupigia simu na kuuliza kama kuna kingine zaidi tunatakakuagiza”

“Waambie waandae tulichowaagiza kama kuna cha kuongezea wanaona inafaa basi wafanye hivyo”Aliongea na yule mfanyakazi wa kiume aliitikia na kuondoka.

“Mnazungumzia nini mambo ya hoteli hoteli?”

“”Unapata wapi ujasiri wa kuniuliza wakati ni wewe mwenyewe ulioemwambia binti yako utampa nyama ya mnyama anaelia ‘Baa.. baa ‘wa kukaanga, mimi hao kondoo nawatolewa wapi muda huu , nimeamua kupitia hoteli maarufu hapa Iringa wanaopika nyama ya Kondoo watuandalie”

“Asiee wewe mzee upo makini , wakati naongea hata sikuwa siriasi , angalau umefanya mambo kua mepesi hehe..”Aliongea Roma na kumfanya Afande Kweka kutoa tabasamu la kifedhuli ambalo linafanana kabisa na la Roma licha ya uzee wake.

“Lanlan leo usiku ukalale na wazazi wako na umwambie baba yako akuhadithie stori , anazo stori za kimapigano nzuri zaidi kuliko za kwangu”Aliongea na kumfanya Lanlan kumgeukia baba yake kwa shauku aone anasema nini.

Roma alijikuta midomo yake ikicheza alijua tu huyo babu yake anamfanyia makusudi, alikuwa akimzuia kutofanya mazoezi na mke wake.

Edna hakuwa mbali na aliweza kusikia kila kitu lakini hata hivyo alikuwa na shauku na yeye ya kusikia stori ambayo Roma atamwambia Lanlan.

“Kijana najua una Stamina nzuri lakini ni kheri kujizuia muda mwingine..”Aliongea huku akipotezea muonekano wake

*****

Upande mwingine nje ya chumba cha Damasi alionekan Denisi ambaye ni kama vile alikuwa akijishauri lakini dakika ileile aligonga mlango na ukafunguliwa na mama yake ambaye alishangaa kumuona Denisi.

“Vipi Denisi uliesema unaenda kumsaidia baba yako baadih ya majukumu kwanini upo hapa?”

“Kila kitu kinaonekana kumalizika hivyo hakuna kingine ambacho ninaweza kufanya”

“Kama ni hivyo , mbona unaonekana kama una kitu unataka kuongea na mimi?”

“Ndio mama , lakini sio kitu kikubwa sana, nilitaka kuona unaendeleaje , lazima utakuwa kwenye mshituko mkubwa kwa kilichomtokea Binamu Aloni na tukio la leo pia”Aliongea na kumfanya Damasi kutabasamu kwa mbali na kisha akamshika mtoto wake mkono.

“Denisi najua unanijali sana kama mama yako ila nipo sawa , ninajisikia vizuri kwa kupumzika kwa muda mrefu kidogo , kaka yako ndio ambaye anannigopesha , ni mtu mwepesi sana na hasira zake”Aliongea na kumfanya Denisi kumwangalia Damasi kwa macho ya huruma.

“Mama , kwanzia sasa jitahidi kujali afya yako , usiwe na wasiwasi sana na siku zote kumbuka afya yako ni muhimu”Aliongea na kumfanya Madam Damasi kuwa na mshangao kidogo na kumwangalia Denisi kwa wasiwasi.

“Kwanini unaongea maneno hayo ghafla tu , ni kama vile hayapo sawa”

“Mama ni kwasababu binadamu tunabadilika muda mwingine hata kama hatutaki kubadilika , siku zote tunalazimika kufanya maamuzi na kubadili maisha yetu kwa sababu ya watu na matukio “

“Unazidi kunitia wasiwasi na maneno yako Densi kuna kitu chochote kinakusumbua , niambie mimi mama yako na kama sitoweza kukusadia nitakuombea kwa baba yako akusaidie yeye”

“Hapana sina tatizo , nimefurahi kwamba upo sawa , ninatoka sasa kwenda kambini kwani kuna mambo nataka kudili nayo na naweza nisirudi kwa muda”

“Sawa nenda mwanangu huna haja ya kuwa na wasiwasi na mimi”Aliongea Damasi bila ya kufikiria mara mbili mbili na baada ya Denisi kutembea mita kadhaa aligeuka na kumwangalia mama yake aliekuwa akimwangalia.

“Kwaheri ya kuonana mama”Aliongea ndani ya nafsi yake na Damasi ambaye hakujua nini kipo kichwani mwa Denisi aliinua mkono wake kwa tabasamu na kumpiugnia mkono wa kwaheri bila kujua hio ndio kwaheri ya moja kwa moja kuiona sura ya mwanae wa kiume katika uhalisia.

Na mara baada ya kuingia kwenye gari lake palepale macho yake yalibadilika rangi na kiini cha macho kupotea na kuwa kama vile ni sananmu la rangi ya Silver.

ITAENDELEA.
Noma
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANO JR



SEASON 21

SEHEMU YA 601.

Moli alijitahidi kupotezea hofu ya kumuogopa Roma na kisha akaanza kuwaelezea kuhusu eneo hilo lilivyo.

Kwa maelezo yake ni kwamba eneo hilo lilikuwa likiiitwa ulimwengu wa mapepo kutokana na kwamba viumbe ambao walikuwa wakipatikana hapo ni wale majini ambao walikuwa wakijifunza mbinu za kuvuna nishati ya mbingu na ardhi ili kulipa nguvu pepo la ndani(inner demon) kutawala mwili.

Inaaminika kwamba kila binadamu au kila kiumbe ana pepo lililo ndani yake na ndio pepo hio ambalo huibua hisia hasi katika roho ya kiumbe , kwa mfano wa hisia hasi ni kama chuki husda na wivu na mengineyo ya mfano huo.

Sasa kuna aina mbili za kuvuna nishati za mbingu na ardhi aina ya kwanza ni ile ya kulishinda pepo la ndani na hatimae kuweza kupata ufunuo wa siri za ulimwengu na aina ya pili ni kwenda kinyume chake yaani kulipa nguvu pepo la ndani ili kukutawala na kukufunulia siriza ulimwengu.

Aina hizi mbili za uvunaji wa nishati ndio ambazo zinatofautisha majini, kuna majini ambao wanawachukia binadamu na kuwaona ni viumbe dhaifu na kuna wale ambao wanaheshimu binadamu , asilimia kubwa ya majini wabaya wanaochukia binadamu ndio ambao wanajifunza mbinu za nishiti za kuamsha pepo la ndani(inner demon).

Sasa hapo zama za kale baada ya majini wanaojifunza mbinu za kuamsha pepo kuonekana ni hatari kwa binadamu walitokea kutenganishwa kwa kutolewa katika ulimwengu wa majini wa kawaida na kutengwa katika ulimwengu mwingine ambao haukuwa wa kawaida , ulimwengu ambao ilikuwa ni ngumu kuweza kuwasiliana na binadamu tofauti na majini ambayo yanavuna nishati kwa ajili ya kushinda pepo la ndani.

Yaani kwa maneno marahisi wale majini wazuri kama wa Hongmeng , Panas na Kekexil hawa wanavuna nishati kwa staili ambayo ni kwa ajili ya kushinda hisia zao hasi na hatimae kufunuliwa wasio yajua, ni kama mtu anavyosali au kuswali na Mungu wake ndio kinachotokea.

Ulimwengu huo sasa wa majini yanayoenda kinyumena njia za kawaida ndio ukapewa jina la Demonic Realm, yaani ulimwengu wa majini mapepo.

Njia pekee ambayo iliwekwa kwa ajili ya kusafiri kuingia katika ulimwengu huo ni kupitia minara au majengo maalumu ambayo kazi yake ni kuvuta kila aina ya nguvu kubwa ya kipepo katika dunia ambayo binadamu hawezi kuhimili.

Moli anasema katika watu ambao waliweza kuingia katika ulimwengu huo kila mtu aliingia kwa staili yake , kuna ambao waliingia kupitia minara iliokaa kimajengo na kuna wengine ambao waliingia kwa njia ambazo hazikuwa zikieleweka na kushindwa kupata majibu.

Mnara inayozungumziwa hapa ni mfano wa ile ya kuongozea meli au ndege sio minara ya simu, mara nyingi inajengwa kama nyumba flani hivi kwenda juu na hata ule wa Shushani ulikuwa hivyo hivyo ila tu ni kwamba ulitofautiana na minara mingine ya kichina ya kitamaduni.

Kwa duniani kuna uwezekano wa kuwa na njia nyingi za kuingia katika ulimwengu huo lakini ukiwa ndani ya ulimwengu huo wa Kidemonic njia ya kutoka nje ni moja tu ambayo ni Mnara wa Mbingu.

Hivyo ilikuwa ni rahisi kusema ulimwengu huo ni wa viumbe hatari visivyokuwa na huruma kutokana na namna yao ya kujifunza mbinu ya kuvuna nishati ilikuwa ikiendana kinyume na ile ya kawaida na kuwapelekea kupandwa na mashetani .

Sasa Moli anamwambia Roma kwamba ili aweze kutoka hapo ndani lazima autafute huo mnara wa mbingu ambao upo katikati ya ziwa na aweze kupitia mapigo tisini na tisa ya radi rangi ya zambarau na bluu ndio aweze kutoka.

Inaaminika kwamba mapigo hayo ya Radi tisini na tisa hayakufanana na yale mapigo tisa ya duniani , mapigo hayo katika ulimwengu huo huwa yana athari za kipekee sana ya nguvu za giza kama vile nishati za giza na nguvu ya kiroho ya giza.

Anasema imepita zaidi ya miaka elfu kumi na haijawahi kutokea jini lolote ambalo liliweza kufaulu kupigwa na mapigo tisini na tisa ya radi na kuweza kutoka katika ulimwengu huo au kupona.

Hivyo kutokana na hilo kila kiumbe kilichoingia katika ulimwengu huo pamoja na majini yenyewe ya pepo yaliokuwepo yalikubali kwamba hakuna namna ya kuweza kutoka katika ulimwengu huo kupitia huo mnara labda kwa njia nyingine ambayo bado haijagunduliwa.

“Hii sehemu ambayo tupo sasa ni Msitu Giza aneo ambalo linamilikiwa na Mbweha wa Jade, ukienda kaskazini mbali huko kuna koo nne za kimajini katika msitu wa Mianzi Zambarau , ukienda mbali mashariki huko unakutana na ukoo wa Mazimwi hatari, eneo ambalo linafahamika kama Bonde Joka ambao ukoo wenyewe unafahamika kwa jina la koo ya Joka kuu.

“Bro mimi nina miaka mia tatu hivyo inanifanya kuwa mkubwa kwako, hivyo mimi kama kaka yako ninakushauri kwamba ijapokuwa una nguvu kubwa za kimaajabu kuliko mimi haziwezi kuwa kubwa kuliko wakuu wa koo husika”Aliongea Moli akimpa Roma tahadhari.

Sophia alionekana kuogopa sana kutokana na maelezo hayo na mbaya zaidi aliposikia kuhusu uwepo wa majini wenye nguvu zaidi ya Roma.

“Je unajua miliki za kijini nje ya hapa kama vile Hongmeng , Kekexil na Panas?”Aliuliza Roma ambaye hakuwa katika hali ya woga hata kidogo.

“Nishawahi kusikia kuhusu Hongmeng na inasemekeana ni miliki ya majini wadhaifu tu wa kawaida kuhusu sehemu zingine sijapata maarifa huenda ni kutokana na nguvu yao kuwa ndogo”

“Kwahio unasema kwamba ulimwengu huu ndio wenye nguvu zaidi kuliko wa majini ya maeneo mengine”

“Inaweza kuwa kweli au isiwe kweli , lakini unapaswa kuelewa kwamba hii sehemu ilikuwepo miaka zaidi ya elfu hamsini iliopita kabla hata kwa ujio wa wale viumbe kutoka sayari nyingine waliojiita miugnu miaka elfu ishirini iliopita, kuna sehemu nyingine ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuwafanya binadamu kuwa salama, sisi tunaamini kwamba roho ya kiumbe chochote haipotei hivyo kama kweli miaka iliopita kabla ya ujio wa binadamu kulikuwa na wanyama wakubwa na wakali kama inavyohadithiwa basi roho zao zitakuwa zimeshikiliwa katika upenyo maalumu kama hili eneo?”

Roma alielewa baadhi ya maneno ya Moli , ilikuwa ni kweli kabisa miugu walikuja miaka elfu ishirini iliopita na katika kipindi hicho binadamu walikuwa wakiishi kawaida na hakukuwa na majini katika uso wa dunia hivyo moja kwa moja ni kwamba ulimwengu wa majini kama huo ulikuwepo kabla yao.

Kuhusu roho za wanyama wakubwa wakali waliokuwepo alijikuta akianza kuhishi huenda ni kweli kutokana na kumiliki Cauldron ambayo ndani yake ilikuwa na roho ya mnyama mwenye nguvu.

Roma alimuonea huruma Sophia kwa kuja nae katika eneo hilo la hatari , kuhusu Lekcha alijiambia ni haki yake kukamatwa katika ulimwengu huu kwasababu nguvu ya nishati ya ant-matter ilikuwa ni tishio sana lakini huku akiomba isitokee Lekcha kuweza kupata namna ya kujiongezea nguvu akiwa katika eneo hili kwani anaweza kumpa changamoto kutokana na kwamba hakuwa na uwezo wake kamili.

Baada ya maongezi ya muda, Moli aliangalia anga na kuona tayari lishakuwa jeusi na hakutaka kuulizwa maswali mengine .

“Bro Roma nimekuja katika huu msitu kwa ajili ya kutafuta mmea adimu , hapa ni eneo la mpakani na sikutegemea kukutana na yale majitu , ila kwa kunisaidia kwako lazima kutakuwa kumewaamsha wamiliki wa hili eneo , hivyo angalau unapaswa kuwa makini katika eneo hilo lote la Mbweha wa Jade, najua mpango wako ni kutaka kwenda kuona mnara lakini nakushauri kama mnataka kuwa salama tafuteni uelekeo wa Ziwa la mbingu”

“Kwa maelezo ambayo umenipatia haiwezi kunisumbua kwenye kutafuta uelekeo na safari ikawa ndefu?”

“Ni kheri safari yenu iwe ndefu kuliko kukamatwa na walinzi wa jumba la Mbweha wa Jade , mkuu wao anafahamika kwa jina la Mbweha wa anga wa mikia tisa na ndio ambaye ana uwezo mkubwa sana katika hili eneo kimapambano , yupo juu katika daraja la tisa huku akilindwa na mapepo wa anga therathini na sita na majitu kama mlioyaona hapa 72 hivyo fikirieni mara mbilimbili”

Roma aliweza kuelewa uvunaji wa nishati katika huo ulimwengu ulikuwa umegawanyika katika madaraja tisa na kila baada ya kupita madaraja matatu ilimaanisha nguvu na zenyewe zinaongezeka.

Kwasababu wote walikuwa na muonekano mbaya basi wanapofikia katika levo ya tatu tu ndio huweza kupata maumbo ya kibinadamu.

Unapaswa kuelewa katika ulimwengu binadamu ndio kiumbe ambaye ana muonekano mzuri kuliko aina yoyote ile ya kiumbe na asilimia kubwa ya hawa viumbe wasioonekana wenye miili mibaya ndoto yao ni kuwa na miili ya kibinadamu na hata hapo mwanzo ilisemekana majini yalikuwa yakiwaonea wivu binadamu kwa kuwa na maumbo mazuri ya kuvutia ndio maana majini mabaya wakawa wanawaingia binadamu na kuwatawala kiroho.

Katika mafunzo ya kawaida ya kijini ili kuweza kuwa na uwezo wa kujitengenezea mwili wa kibinadamu sharti ni kuingia katika levo ya Nafsi.

Kwa maelezo ya Moli alielewa kwamba katika hilo eneo hakukuwa na levo ya kuipita dhiki kutokana na kukosekana kwa radi za mapigo tisa.

Kundi la kwanza la majini ambalo uwezo wao ni wa kawaida ni kuanzia daraja la kwanza mpaka la tatu , kundi la kati ni kwanzia daraja la nne mpaka la sita , kundi hili lilikuwa la watu wachache zaidi, kundi la mwisho ni kuanzia saba ndio waliitwa majini pepo ya anga au mashetani pepo wa anga”

Roma hakutaka sana kujali kuhusu uwepo wa Mbweha wa anga wa mikia tisa na isitoshe kwa maelezo ya Moli hakuna ambaye alikuwa akimfahamu vizuri na kingine inasemekana alikuwa tofauti sana na majini na hakuwa ni mwenye kujali sana , wasiwasi wa Roma muda huo ni namna ya kutoka katika ulimwengu huo tu kwa namna yoyote ile.

Roma aliagana na Moli kisha yeye na Sophia walianza kutembea kuelekea upande wa Kaskazini , kulingana na maelezo ya Moli mji wa kwanza watakao kutana nao ni Mji wa Wingu Jeupe , ambao ndio mji mkubwa zaidi ndani ya miliki ya Mbweha wa Jade na itawachukua siku tatu katika kutembea.

Walipewa taarifa nyingine ya kutafuta mawe maalumu ndani ya mji huo ambayo yanaitwa kama mawe ya kiroho ambayo hutumika kama hela au njia ya kibiashara.

Roma hakutaka kutumia njia ya pemeni kama ambavyo ameelekeza Moli maana kutokana na maelekezo yake njia rahisi kufikia ziwa la mbingu ambapo kuna mnara ni kupitia ndani ya jiji la Wingu jeupe.

*******

Siku tatu ziliweza kupita na taratibu za maombolezo ya kifo cha Denisi ziliweza kufanyika ndani ya Iringa, haikuwa na maana ya kwenda Songea kwa ajili ya kuomboleza msiba kutokana na kwamba hakukuwa na mwili wa kuzika , hivyo kilichofanyika ni ibada ya kawaida tu kupitia kanisa la kikatoliki na kuruhusu jamaa na marafiki kutoa salamu za pole.

Licha ya maombolezo hayo, wanafamilia hao walikuwa katika hali ya wasiwasi kuhusu Roma , katika siku hizo tatu waliweza kupewa taarifa zote kutokea China kuhusu kupotea kwa Roma na Sophia kupitia mnara.

Ilikuwa ngumu kuamini kwa tukio hilo lakini kutokana na maajabu aliokuwa akifanya Roma iliwafanya kuamini kwamba ni kweli wameweza kupotea.

Asilimua kubwa ya wana ukoo waliogopa zaidi kupotea kwa Roma kwani alikuwa ni kama ashakuwa mhimili kwa ukoo wao kwa yale ambayo yametokea hivi karibuni , waliogopa maadui zao kuwachukulia hatua na kujaribu kuwayumbisha kwani kupotea kwa Roma ilimaanisha uwiano wa kinguvu kubadilika , hatua za awali walizochukua ni kufanya jambo hilo kuwa siri ya familia.

Afande Kweka alionekana kuchoka kweli kutokana na kutopata usingizi kwa zaidi ya siku tatu mfululizo , katika eneo la sebuleni alikuwa amekaa pembeni ya raisi Senga pamoja na Damasi ambaye macho yake yalikuwa yamevimba na mbele kabisa alikuwa amekaa Blandina mama yake Roma pamoja na Edna aliempakata Lanlan.

Kushoto kwao kulikuwa na mgeni ambaye ni mchina alievalia mavazi ya kitamaduni , alifahamika kwa jina la Abbess Yumiao na ndio aliekuwa ni mkuu wa Dhehebu la Shushani na ndio aliefika hapo kutoa taarifa.

Wageni wengine walikuwa ni wazazi wa Sophia , Balozi Athumani pamoja na mke wake.

“Tuliweza kutafuta kuzunguka eneo lote la Shushani lakini hatukuweza kupata chochote , tunaomba radhi kwa hilo “Aliongea yule Master.

“Na amini mmefanya kazi kwa jitihada kubwa , hata hivyo unaonekana ulikuwa ukimpenda Sophia hivyo haiwezekani ukakubali apotee kirahisi”Aliongea Afande Kweka kwa kingereza.

“Jamani Sophia wangu mimi,……”

Mama yake Sophia alikuwa akitoa machozi na kuwafanya watu wote waliokuwa hapo ndani kumuonea huruma.

“Sophia atakuwa sawa naamini yupo na Roma na mimi namwamini atamrudisha akiwa salama, huna haja ya kuendelea kulia, Roma ni mwanangu na imani yangu inaniambia atarudi salama”Aliongea Blandina akijaribu kumpoza Mama Sophia lakini wakati huo huo na yeye akitoa machozi , ilikuwa ni kama alikuwa akijifariji.

“Blandina haina haja ya kuendelea kulia , hatujapokea taarifa mbaya, naamini ataweza kurudi muda si mrefu”Aliongea Raisi Senga huku akimwangalia Damasi ambaye muda wote alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.

“Upo sahihi mwanangu Roma atakuwa sawa ,naamini hilo..”Aliongea huku akifuta machozi.

“Okey kwasasa tutaliacha hili kwa jeshi letu kitengo cha wachawi , Master Yumiao na kitengo cha jeshi la Wachawi kutoka china cha Yellow Flame iron Brigade na wao ndio watatupa taarifa ya kile kinachoendelea, Senga umefanya vizuri kwa kuongea na uongozi wa serikali ya china kwa kuruhusu wanajeshi wetu kuweka kambi katika dhehebu la Shushani naamini muda wowote wataweza kupata fununu”Aliongea Afande Kweka na Raisi Senga alitingisha kichwa.

















SEHEMU YA 602.

Siku tatu ziliweza kuwawezesha kutoka katika Msitu wa Giza , ijapokuwa ulimwengu huo ulikuwa ni ardhi ambayo haijagawanyika lakini eneo lilikuwa kubwa mno.

Roma kadri ambavo alikuwa akitembea ndio uvumilivu wake ulizidi kupungua na ili kurahisisha safari aliweza kutumia nguvu yake ya kijini kujaribu kupaa kwa kuruka ruka ruka kama chumba ili kufupisha safari.

Inasemekena mwishoni mwa eneo hilo kulikuwepo na bahari isio na mwisho ambayo mito yote katika eneo hilo humwaga maji yake na kwa maelezo ya Moli ni kwamba wasafiri washawahi kusafiri lakini hawakuwahi kufika mwisho na kuona ardhi ndio maana wakaipa jina la Bahari sio na mwisho.

Mto ambao ulikuwa ukipita katika jiji la Wingu jeupe ulikuwa na upana wa kilomita moja au zaidi na kwasababu ya mvuke uliokuwa ukitoka pamoja na Ukungu ilifanya jiji hilo kuitwa Jiji la wingu Jeupe kutokana na kwa mbali liliweza kuonekana nyumba zilizofunikwa na wingu.

Kilichomshangaza Roma na Sophia ni kwamba licha ya eneo hili kuwa la majini lakini miundo mbinu yao ilikuwa ni ya kawaida kabisa kama ya binadamu, kulikuwa na kila aina ya staili ya usanifu wa nyumba karibia tamaduni zote na mpangilio wake ulikuwa ni wa kueleweka kwani kulia na kushoto kulikuwa na nyumba huku katikati kukiwa na barabara,

Halikuwa aneo kama ulimwengu wa kawaida kutokana na kukosa ule ukisasa, lakini hata hivyo haikushangaza sana kwani kuna watu wengi ambao walikuwa wakiingia katika ulimwengu huo kutoka dunia ya kawaida na kuleta ustaarabu wa aina tofauto tofauti.

Kwa muonekano wa eneo hilo ni kama vile majini hao hawakuwa na tamaa ya kuujenga mji kuwa wa kisasa zaidi na sababu ya moja kwa moja haikueleweka na isitoshe Roma hakuwa na taarifa za kutosha.

Tokea kuumbwa kwa binadamu aliweza kupewa mamlaka ya kutawala viumbe vyote hata wale wasiokuwa wakionekana huenda ndio maana kila kitu majini yalichofanya kilikuwa kikiendana na binadamu wa kawaida.

“Bro tunaingia hivi hivi tu bila tahadhari , vipi kama wakitushambulia?”Aliuliza Sophia aliekuwa akiangalia jiji hilo kwa wasiwasi kupitia mlimani.

“Tunapaswa kuingia ndio hata kama watakuwa ni wakali zidi yetu , kwanza kabisa bado siamini maneno yote alioongea Moli hivyo lazima nifike katika mnara huo na kujionea mwenyewe kwani ndio njia pekee ya sisi kutoka huku, pili kama alivyotuambia lazima tutafute mawe ya kiroho ili kuweza kununua wanyama wa kijini ili tuweze kusafiri kwa urahisi na kutoka katika hilo eneo”

Kwa maelezo ya Moli ili kuishi katika eneo hilo hakuhitajika pesa bali mawe ya kiroho ndio hutumika kama njia ya biashara.

“Bora uwezo wangu ungekuwa mkubwa , kwa staili hii ninakwenda kuwa mzigo tu kwako”

“Hivi unajua siku zote sisi wanaume hatupendi wanawake wenye nguvu , tunapenda mwanamke ambae ni tegemezi, hakuna mwanaume ambaye atakupenda kaa una nguvu kumzidi na huna unachomtegemea”

“Sidhani ni kweli, kama ni hivyo kwanini mpaka leo hii hujaweza kuzikubali hisia zangu”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta hewa kwa nguvu.

“Hilo limetokea wapi katika muda kama huu? , aisee naona unazidi kuwa mwanamke jasiri”

“Unataka niwe muoga , nishakaa chini na kufikiria tayari , kama kweli hatuwezi kutoka huku , hakuna wa kujali maswala ya kimaadili, hivyo matatizo yetu yote yatatatulika kirahisi”Aliongea akimaanisha kwamba kama hawawezi kutoka inamaana yeye na Roma wanaweza kuwa wapenzi.

Roma hakuteka kuendelea kusikiliza maneno ya Sophia na aliishia kumwambia waanze safari ya kuingia ndani ya jiji hilo na Sophia hakutaka kuendelea kuongea kwani aliogopa kumkasirisha.

Haikuwachukua dakika nyingi hatimae waliweza kuingia katika mji huo huku wakiangaliwa na majini hao kwa macho yasiokuwa ya kawaida .

Katika ulimwengu huo elimu haikupewa kipaumbele , kinachopewa kipaumbele ni mafunzo ya uvunaji wa nisahti pekee na kufika katike levo ya kuweza kuwa na mwili wa kibinadamu.

Jini ambalo halina mwili wa binadamu mara nyingi huonekana dhaifu sana na hufanya kazi za kitumwa.

Cha kuwashangaza zaidi ni kwamba ndani ya eneo hilo kulikuwa na wanyama wa ajabu sana ambao walikuwa wakitumika kama vile ni farasi , hakukuonekana magari na vifaa vingine , maisha yao yalikuwa ni yale ya kikale zaidi.

Kila kitu kilionekana kuwa kipya kwa Sophia , lakini kwa namna moja ni kama anafanya utalii.

Ni muda huo huo wakati wakipita katika jengo ambalo lilikuwa limefunikwa na ngozi nyingi kwa nje alionekana mwanamke jini aliekuwa katika mwili wa kibinadamu akiwaangalia , alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa na mwonekano wa kiarabu.

Alikuwa amevaa gauni refu ambalo lilikuwa na mkato wa kuacha shingo wazi huku akiwa amevaa cheni kubwa za madini ya dhahabu tupu ambazo zilikuwa ni za kuwaka waka.

“Wewe mwanaume wa kibinadamu nadhani wewe ni mgeni”Aliongea yule mwanamke kwa lugha ya kingereza lakini rafudhi yake haikuwa ni ya kunyooka , Roma aliamini huenda alikuwa akizungumza lugha nyingine tofauti na kingereza.

“Nimekuja huku bila ya kujielewa , nadhani unaweza kuniona mgeni”

“Unaonekana sio wa kawaida , karibia ya wote walioweza kukamatwa na mnara ni kwasababu ya aina moja”

“Inaonekana watu wengi wamekuja huku kabla yangu , tumeingia hapa lakini hakuna ambaye ametuongelesha zaidi ya kuangaliwa tu, ni kama jambbo ambalo limezoeleka”

“Upo sahihi , siwezi kusema kuna binadamu wengi lakini binadamu wanakuja mara kwa mara , nyie mnaweza kuwa binadamu lakini hapa hamchukuliwi kama alien , jina langu naitwa Mei , je tunakuitaje”

“Niite Roma Ramoni”

“Oh.. Braza Romaa,,!!!”

Aliongea huku akimsogelea Roma karibu kabisa huku akisuguanisha manyonyo yake na kifua cha Roma kwa staili ya kumtega.

“Braza Roma kwasababu ushakuja huku unapaswa kuyachukulia maisha kawaida , unaonaje ukiingia ndani na kuungana na wengine kula raha”Aliongea na kumfanya Roma kuangalia jengo hilo na kuweza kugundua nini kinafanyika huko ndani.

“Kwahio hata huku mna madanguro?”Aliuliza wakati huo Sophia alionekana kuwa na aibu kwa namna ambavyo Mei alikuwa akijigusanisha manyonyo yake na Roma.

“Kuna tatizo gani juu ya hilo , majini pia yana hisia , unadhani ni binadamu tu ambao wanapaswa kuuza miili yao na sisi majini hatuwezi?”Aliuliza lakiini Roma alipotezea.

“Nimeambiwa kwamba hela katika ulimwengu huu ni mawe ya kiroho kutoka bahari isio na mwisho , sina hayo mawe hivyo siwezi kutoa malipo hata kama nikiingia”

“Roma..!!”Aliita Sophia kwa hasira na kumfanya Roma amwangalie.

“Huwezi kuingia nae huyo , kwanini unataka kufanya hivyo wakati una mke anakusubiria?”Aliongea na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasamu kwa uchungu , hakuelewa ni kwanini sasa hivi ndio anaanza kuwaza kuondoka katika hilo eneo.

“Lakini si ndio maana nimesema sina mawe ya kiroho”

“Wewe…:!!”

“Hakuna shida , unaweza kupata hayo mawe hata baadae , unachotakiwa unaweza kujiandikisha na kupata huduma na kisha utalipia baadae”

“Ah.. kwahio hamuogopi kwamba naweza kukimbia bila kuwalipa”Aliuliza Roma.

“Haishangazi ndio maana nasema wewe ni mgeni hapa , hili ni jiji la Wingu Jeupe na Bwana Mkuu Baiju ni sehemu ya majini pepo 36 ambaye anapendelewa sana na jenerali mkuu wa Jade, hivyo yoyote ambaye atashindwa kulipia deni lake atakutana na kifo cha maumivu”Aliongea Mei na kumfanya Roma kuelewa na sasa kusita sita.

“Basi nitapita, sijui namna ya kutengeneza hela hapa , sitaki kufa kifo cha maumivu kwa kushindwa kulipa deni , unaonaje ukiniambia sehemu ambayo naweza kupata hayo mawe pamoja na majini wanyama wa kusafiria?”Aliongea na kumfanya jini pepo Mei kufikiria kidogo.

“Braza Roma kama unahitaji hayo mawe unaonaje tukifanya biashara?”

“Niambie hio biashara”

“Huyu mwanamke hawezi kuishi kwa muda mrefu ndani ya ulimwengu huu na jini pepo lolote lenye mwili wa kibinadamu linaweza kumuua , huwezi kumlinda hivyo unaonaje tukibadilishana, mimi nitakupa mawe na yeye atabakia hapa katika Danguro langu na kutoa huduma kwa wateja , anaweza pia kuweza kulipwa bonasi ya Mawe na kuendelea kuishi”

Roma mara baada ya kusikia biashara hio alielewa ndio maana mwanamke huyo aliwasogelea , kumbe alikuwa na lake jambo la kutaka kumchukua Sophia kwa ajili ya biashara, alijiambia hauzwi mwtu hapa.

Sophia mara baada ya kusikia anataka kuuzwa alimsogelea Roma na kujibana kwake kwa hofu.

Roma alijaribu kumtuliza Sophia na kumwambia hakuna kibaya ambacho kinaweza kumpata.

Roma hakuwa tayari kumuuza Sophia kwa ajili ya kujipatia mawe, hivyo alimwambia Mei kwamba wanaondokana watajua mbele kwa mbele.

Upande wa yule jini pepo wa kike baada ya kuagana nao aliwaangalia na kutoa tabasabasamu lisilokuwa la kawaida na palepale baada ya kuwaona wametokomea upande wa mbele alibadilika na kuwa mwewe na kisha akapaa na kuondoka.

Roma baada ya kuelewa baadhi ya mitaa hio walipita pamoja na kuja kutokezea katika soko na hapo ndipo aliposhangaa kuona watu mbalimbali wakiongea lugha wanazozijua , ilikuwa rahisi kwake kuwasiliana kutokana na kujua lugha nyingii.

Roma aliulizia bei ya wanyama wa kusafiria na alipotajiwa ndio alipogundua wale wanaosafiri kwa kasi tena kwa kupaa walikuwa ghali sana na wale wa chini wanaofananana na nguruwe au Kenge walikuwa ndio wa bei rahisi.,

Hivyo ilikuweza kuwapata hao wanyama alipaswa kukusanya mawe mengi ya kiroho.

Inasemekana mawe hayo hupatikana katika bahari isio na mwisho na wale ambao wanaoenda kuyatafuta huwa ni kama wanaenda vitani kwani kuna viumbe wakali sana chini bahari ambao wanapaswa kupigana nao na kisha kuweza kuchukua mawe hayo.

Hivyo upatikanaji wake ulikuwani mdogo sana ndani ya hilo eneo na ndio maana yalikuwa ni adimu na thamani kubwa.

Roma alitamani kuwa kibaka na kuibia baadhi ya majini ndani ya hilo eneo lakini alijizuia kwa kuamini huenda angeweza kukasirisha mamlaka na kujiingiza katika matatizo.

Jiji la Wingu jeupe halikuwa na vurugu kama alivyodhania , ilikuwa ni sehemu iliokuwa na utulivu na kila mtu alikuwa na mambo yake , ijapokuwa walikuwa wakikodolewa macho lakini hawakujali na kuendelea na safari.

Baada ya kutoka nje ya jiji hilo waliweza kufikia kijimlima ambacho kilikuwa kikiwapa uwezo wa kuona upande wa chini wa bonde , ilikuwa ni eneo ambalo lilikuwa na mwonekano mzuri mno.

Roma paepale alitaka kumshika Sophia ili apae nae mpaka upande wa chini wa bonde hilo lakini aliweza kuhisi kundi la watu wakija upande wao.

Dakika chache tu ilikuwa ni kama hisia zilivyomwambia kwani waliweza kusogelewa na watu ambao walikuwa wamepanda juu ya wanyama kama Kenge(Thunder Lizard) na kuwazuia kwa mbele.

Wanyama hao walikuwa ni warefu mno na wanene waliokuwa wamepakwa rangi ya dhahabu kwa juu huku wakiwa na mapembe makubwa , walikuwa wakitisha lakini walikuwa ni wapole mno kutokna na uwezo wao mdogo wa akili , walikuwa wakishambulia na mapembo yao tu hivyo ndio maana mara nyingi yalipendelewa kutumiwa kama nyenzo ya usafiri.

“Mnaonekana wageni ,Je nyie ni wapya katika hili eneo?”Aliuliza mmoja wapo , walikuwa wakiwaangalia kwa ujeuri wa hali ya juu.

Aliekuwa akiwaongoza alikuwa amevalia Vest ya ngozi ya chui na uso wake ulikuwa mpana na umekaa kama chapati huku mdono ukiwa kama kijishimo, licha ya kubahatka kuwa na mwili wa kibinadamu lakini alikuwa mbaya wa sura mno na Roma alijiambia huenda hio ndio sura mbaya ya kibinadamu alioweza kuona katika maisha yake.

“Sisi ni wageni ndio , je kuna kitu chochote mnataka kutoka kwetu?”Alijibu Roma akiwa mpole maana alishagundua walikuwa na uwezo mkubwa kama Moli.

“Mnaweza kupita katika hili eneo lakini kabla ya hapo mnapaswa kulipia ushuru”Aliongea huku akitoa tabasamu.

Roma alijikuta akiwaza , hakuamini mpango wake wa mwanzo wa kutaka kuiba sasa umegeuka na yeye ndio anataka kuibiwa , alitamani kupaa na Sophia katika hilo eneo na kuwakwepa lakini aliona hilo sio chaguo bora.

“Jamani kama kweli mnatuona sisi ni wapya na tumewajibu hivyo mnawezaje kutaka ushuru ilihali hatuna mawe ya kiroho , kwanini msitusamehe kwa leo”

“Binadamu siku zote hamkosagi maneno nyie , kama tusipokusanya ushuru tunawezaje kupata hela , kama huna unaweza kulipia kwa kumtoa huyo mwanamke na wewe kuondoka , isitoshe hana nguvu zozote za ziada na atakuwa mzigo kwako”

“Nilijua ni Madanguro pekee ndio ambayo yanaweza kufanya biashara waziwazi , nadhani mambo ni ya kimkanganyiko sana ndani ya hili eneo”

“Madanguro gani, mimi ndio mkuu wa hili eneo kwenda kule chini na kila mtu ananijua jina langu mimi Baba Huja , unatakiwa kujifikiria mara mbilimbili la sivyo nitaruhusu hawa Kenge wetu kuwala nyama”Roma alijikuta akikunja sura lakini hata hivyo hakutaka kuogopeshwa na maneno yake maana aliona kama ni kupambana nao angeweza kuwaua wote.

“Hamtaki kutupisha ilihali tunaomba kwa upole , basi sawa hata hivyo nilikuwa nikitafuta mtu wakumuibia ,Shukeni kutoka kwenye hao wanyama wenu na mtoe mawe yenu yote ya kiroho na nitawatunuku kifo cha kistaarabu”

“Hahahaa… mmemsikia ? Binadamu mgeni anapanga kutuibia sisi , hivi hata unajua nani mkuu wa hili eneo lote”

Roma hakutaka kupoteza muda palepale alisogelea jini lililokuwa karibu yake kwa kasi kubwa na kulipiga ngumi na kusababisha liteme damu kutokana na baadhi ya viungo vyake kuharibika.

Baada ya kulishambulia na ngumi ile palepale liligeuka na kuwa kama kifaru huku ikionekana ameacha shimo katika ngozi yake.

Wale hawakutajarajia kama Roma anaweza kupigana , kwanza alikuwa na spidi kubwa kiasi cha kuwashangaza , yule jini aliegeuka kifaru alidondoka chini palepale na kufariki.

“Muueni”Aliongea kwa nguvu yule bwana Huji akiwaamrisha aliokuja nao na wote kwa pamoja walimwangalia Roma kwa macho makali.
Burudan
 
SEHEMU YA 603.

Wale majini walionyesha hasira za hali ya juu kutokana na kushuhudia mwenzao akipoteza maisha na palepale waliruka kutoka kwenye wale wanyama na kumsogelea Roma kwa spidi na kuanza kumshambulia.

Uwezo wao wa kimapigano mara nyingi ulitegemea zaidi kipaji na ulijumuisha upepo , mawe ,moto na barafu, mbinu zao hazikuwa chini na zile za majini ya kawaida pamoja na binadamu wanaojifunza mbinu za mbingu na ardhi

Roma hakuweza kukwepa mapigo yao kwani alijua akijiwekea ngao ndio ambavyo atazidi kupoteza nguvu zake kwa kiwango kikubwa hivyo alichokifanya ni kuita moto wa rangi nyeipe kujaribu kuwaunguza lakini ni kama walionekana walikuwa na mbinu za kuhimili moto huo sababu walianza kuongezeka ukubwa na kubadilika miili yao

Roma mara baada ya kuona mbinu hio haiwezi kufanya kazi palepale alifungua anga ya Sumeru na kuvuta Dagger ya damu ya Dragoni alioiiba kwa majini ya Hongmeng na kushambulia nayo.

Yale majini mara baada ya kuona kile kisu waliweza kukifahamu na walionyesha hofu lakini Roma hakujali kwani ndani ya dakika chache alikuwa ameshawafyeka, kisu hicho kilikuwa na tabia kwamba jeraha lake ilikuwa ni ngumu kupona lenyewe kwa haraka hivyo iliwapelekea kupoteza damu kwa haraka sana na kupoteza nguvu.

Jini pepo pekee ambalo lilikuwa limebakia ni yule kiongizi wao na baada ya kuona wenzake wote wamekufa alijikuta akipandwa na hasira maradufu.

“Nitakuuua !”Aliongea na palepale mkononni kwake kiliokana kisu cha kumeta meta na kumsogelea nacho Roma kwa kasi kwa ajili ya kumchoma , lakini Roma alionekana kuwa mwepesi kwani alimkwepa na akachukulia faida wepesi wake na kupeleka kisu chake nyuma lakini Huja alionekana kuwa na hisia kali kwani kwa wepesi aliosogea pembeni na kikapita.

Baada ya kuona hakuwa na uwezo wa kumshinda Roma alimwangalia kwa wasiwasi.

“Una bahati sana..”Aliongea akitaka kukimbia lakini Roma hakutaka kumruhusu aondoke na akaite wengine, palepale alimsogelea kwa kasi na kumchoma na kisu eneo la bega na muda huo huo akaita moto wa rangi nyeupe na kuanza kumuunguza lakini alionekana kuwa mjanja kwani palepale alipotea mbele ya Roma kwa kukimbia kwa spidi kubwa na kumfanya Roma ashindwe kumfukuzia kwa kuhofia kumuacha Sophia.

Baada ya kuwadhibiti wote kulibakia wale wanyama ambao walikuwa wamebeba mizigo aina ya viroba na Roma alimwambia Sophia aache woga na aanze kukagua kutafuta vitu ambavyo vinaweza kwuasaidia mbele ya safari.

Baada ya kukagua kwa dakika kadhaa Roma aliweza kukuta mawe ya kiroho yaliokuwa yakizungumziwa , yalikuwa ni mawe ya aina yake yalikuwa meupe sana huku ndani yake kukiwa na kitu cha rangi nyekundu kilichokuwa kikionekana, ni kama vile madini ya Almasi kwa nje na kwa ndani wekundu wake ni kama wa madini ya Rubi laini kitu pekee cha tofauti kuhusu mawe hayo yalikuwa yakipiga shoti ukishika mkononi.

Roma alijaribu kuyachunguza na kugundua kile kiini cha ndani kilikuwa ndio nguvu ya kiroho yenyewe kwani alijaribu kutumia uwezo wake kunyonya nguvu yake na kweli ndani ya dakika alihisi msisimko wa aina yake ukimwingia mwilini kama vile alikuwa akivuna nishati za mbinu na ardhi na ndani ya dakika chache tu kile kiini kilipotea.

Sasa wakati akiwa anaendelea kusachi Kenge wa mwisho aliekuwa na mzigo mkubwa ndipo alipoweza kugundua ndani yake kulikuwa na msichana mdogo aliekuwa amebebwa na alikurupuka palepale mara baada ya kiroba kile kufunguliwa.

“Naombeni msiniue waliniteka”Aliongea kwa kupiga kelele na kumfanya Sophia amsogelee kwa haraka.

“Hatuwezi kukuua usigope”Aliongea Sophia akijaribu kumtuliza , alikuwa na mwonekano wa kirembo mno na kwa haraka haraka sura yake ni kama vile ni mhindu.

“Nadhani ndio kwa mara ya kwanza ameweza kuupata huu mwili wake , nguvu zake ni za chini mno kuliko wengine”Aliongea Roma mara baada ya kumchunguza.

“Ndio nimeingia daraja la tatu la kupata mwili”Aliongea lakini upande wa Roma kuna kitu ambacho sio cha kawaida ambacho alikuwa akikiona kwa msichana huyo lakini hakutaka kujifanya mjuaji sana kwani hata hivyo mbinu hizo zilikuwa zikifanyika kinyume tofauti na yeye.

Majini ili kuweza kuishi walihitajika sana kuwa na nguvu kuliko hata wanavyokula chakula ili tu kuendeleza kudumisha miili yao.

Inasemekana wale ambao wanakaribia kuingia katika levo ya Nafsi hutengwa mahali palipotulia sehemu maalumu na hupewa jiwe la ndoto linalofanana na yai na kisha hulikalia na kulipa joto huku wakiendelea kutahajudi kwa muda mrefu na wakati wakianza kupokea miili yao huwa sio kwa chaguzi zao , kinachoanza kuonekana kwao ni kama ndoto wanaona sura ya mtu mbele yao na huyo mtu ndio mwili wao na kinachofanyika ni kuhakikisha wanapandisha nguvu zao mpaka kuweza kuumiliki .

“Unaitwa nani?”Aliuliza Sophia , alionekana kupata furaha mara baada ya kupata msichana mpole ambaye anaweza kumuuliza maswali.

“Naitwa Aoli, nilikuwa nikielekea katika mji wa Mto Wa Anga karibu na ziwa la mbingu ninakoishi lakini nikaja kukutana na hawa majini pepo wa gredi ya juu na kunikamata”

Maelezo yake yaliwafahamisha kabisa ni dhahiri walikuwa wamemteka kwa ajili ya kwenda kumuuza kwenye Danguro

“Unaonda karibu na Ziwa la Mbingu ?!!”Aliuliza Sophia huku akiwa na furaha kwani hata wao ndio walikuwa wanaelekea.

“Nina uhakika utakuwa unaijua njia ya mkato ,unaonaje tukiongozana pamoja kuelekea huko?”

“Sophia itakuwa hatari kama tukimruhusu akaungana na sisi , nitapaswa kulinda watu wawili kwa wakati mmoja”Aliongea Roma , alimuona msichana huyo wa kijini kuwa mrembo lakini uwezo wake wa kijini ulikuwa wa chini sana na hata yeye mwanzoni alishangaa kwani hakutegemea jini kuwa na mwili na nguvu zake kuwa za chini.

“Sio kweli, huyu yupo kwenye daraja la tatu ambalo ni sawa na levo ya Nafsi hivyo uwezo wake ni mkubwa kuliko wa kwangu na anaweza kujilinda , isitoshe kama tukimuacha hapa si wale watu watarudi na kumchukua tena na kuingia hatarini”Aliongea na kumfanya Roma kukosa neno alikuwa sahihi anaweza kuwa katika hatari lakini alihofia kuongozana na mtu asiemjua.

“Master mimi ni jini wa kawaida tu nisie na uwezo mkubwa , kama tutakuwa katika hatari unapaswa kumlinda mwenzako , sitokuwa na makasiriko zidi yako kwa kutokunilinda , ninajua njia ya karibu kuelekea Ziwa la Mbingu na itawachukua muda mchache kufika mkiwa chini ya uongozi wangu , nyie si wageni nitaendelea pia kuwaelezea baadhi ya mambo msio ya jua”

Roma alijiambia alikuwa na akili , kwani maneno yake yalikuwa yakivutia, ni kweli hawakuwa wakijua njia na mambo mengi pia kuhusu huo ulimwengu hawakuwa wakifahamu.

Sophia mara baada ya kuona Roma anawaza sana alimsogelea na kumwambia kwa taratibu kwamba hakuna ambaye ataweza kumshinda huko njiani hivyo waondoke nae kwani anatia huruma na Roma alitingisha kichwa kukubal.

******

Katika ulimwengu huo huo upande mwingine kando ya ziwa ambalo limezungukwa na msitu wa Mianzi Zambarau alionekana mwanaume ambaye alikuwa na nywele za rangi nyeupe kama mvi hivi , alikuwa amevaa kanzu ya Rangi ya Zambarau huku akiwa na ushanga mkubwa kwenye shingo yake kama Rozari iliotengenezwa na madini ya Jade, alikuwa ni bwana ambaye alikuwa na mwonekano wa kichina na muda huo alikuwa ameegamia kwenye jiwe huku akiwa ameshikilia ufito wa muanzi uliokuwa na kamba ambayo iimeingia majini , alionekana alikuwa akivua samaki.

Nyuma yake kulikuwa na nyumba ambayo ilikuwa imejengwa na Mianzi tupu iliokuwa ikifuka moshi.

Mtu huyo alionekana kuwa katika hali ya raha akifurahia kile alichokuwa akifanya, huku mkono wake wa kulia akiwa ameshikilia kifaa kama kikombe kilichotengenezwa kwa mianzi , ilionekana ni kifaa ambacho kilikuwa na kinywaji ndani yake kwani alikuwa akipeleka mdomoni na kunywa kwa kila baada ya dakika tatu huku akipiga mluzi akionekana kama anaimba.

Dakika hio hio pua yake ilicheza akiwa kama mtu ambaye alikuwa amenusaharufu nzuri na palepale alttupia pembeni ile fimbo na kukimbia kuelekea upande wa kwenye kile kijumba lakini kabla hata hajafika mwanaume mwingine alionekana akitoka katika hicho kijumba akiwa mkononi ameshikilia kibuyu cha mvinyo kama chungu vile , mwanaume huyo pia alikuwa ni mchina ila yeye akiwani mwenye nywele nyeusi.

“Inanukia vizuri “Aliongea yule bwana mwenye nywele nyeupe huku akipeleka pua yake kwenye kile chungu na kunusa huku akionyesha hali ya kufurahi.

“Braza Chi kama nilivyotegemea , inaonekana uwezo wako wa kutengeneza mvinyo ni wa hali ya juu sana , uko vizuri sana katika utengenezaji wa pombe , hii ndio uliniambia unatengeneza kabla ya mvinyo eh?”Yule bwana mwenye nywele nyeusi alishika udevu wake kama vile anautelezesha na mkono na kisha akamwangalia yule mwanaume mwenye udevu wa mvi kwa tabasamu.

“Wang Han Manasaba wa enzi ya Tang hapo zama za kale kama alivyoimba katika ushairi wa Liangzhou, ndipo vikombe vya Jade vilipojaa Divai, sauti ya mtirriko wa pipa ikawaambia na ondokeni…. nimekuandalia huu mvinyo kwa ajili yako, je Braza Zao umeandaa vikombe vya Jade?”Aliongea na kumfanya yule bwana kuanza kuwaza kuhusu Shairi hilo , walionekana ni kama vile walikuwa wakiongea kimafumbo kukumbushiana mambo ya kale hata hivyo alikumbushia ushairi wa Wang Han kuoka enzi ya Tang.

“Braza Chi nimejaribu kuvitafuta vikombe hivyo ila sijavipata , niliwaagiza ndugu zangu Mao Tai na Du Kang kwenda kutafuta katika milima ya Qillian lakini hawakuweza kupata , walivyoleta ni kutoka mlima ya Kunlun , je tunaweza kutumia hata hivyo?”

Mwanaume alieitwa kwa jina la Braza Chi alivuta pumzi na kuzishusha huku akimwangalia Braza Zao..

“Inasikitisha sana lakini sio mbaya tutatumia hivyo hivyo”

Yule mzee Zao mwenye nywele nyeupe alitoa tabasamu pana la furaha huku macho yake yote yakiangalia chungu kilichojaa mvinyo.

Na dakika ileile alionekana ameshikilia vikombe viwili vya Jade ambavyo haikueleweka amevitolea wapi na kuviweka katika meza ya jiwe lililochongwa.

Dakika hio hio wakati akitaka kuchota mvinyo kwa ajili ya kujaza kikombe kingine aliweza kutokeza mbele yao mtu mwingine aliekuwa amevalia kanzu na mwenye nywele za Zambarau, alikuwa ni Moli.

“Kaka Zao je umemuomba Master Chi kukutengenezea kilevi , nimeweza kunusa harufu yake hata nilipokuwa mbali”Moli aliangalia kwa macho ya tamaa chungu kilichokuwa kimejaa mvinyo.

“Bro umekuja muda muafaka , Master Chi ndio amenitengenezea huu mvinyo na sasa upo tayari , njoo ukae na wewe uionje radha yake lakini Du Kang yule mtukutu ameniletea vikombe viwili tu vya Jade kutoka milima ya Kunlun hivyo itakubidi utumie kikombe cha Muanzi.

Walikuwa wakifuata tamaduni za kichina , wenyewe wanaamini utamu wa mvinyo hutofautiana na kikombe ambacho huandaliwa , kikombe cha Jade ndio kinachofanya Mvinyo kuwa mtamu zaidi.

Upande wa Moli alionekana kuwaelewa vizuri kwani hata yeye alikuwa akizungumza lugha ya kichina tena kile cha kale.

Baada ya kuwekewa mvinyo kwenye kikombe chake cha mti na kuonja alijikuta macho yake yakichanua kwa utamu.

“Master Chi wewe ni kaka yangu wa ukweli kuanzia sasa , licha ya kuwa mgeni kwenye huu ulimwengu lakini umeweza kumfanya kaka yangu Zao kulia mara kibao kupitia mvinyo wako”Aliongea na Master Chi alijikuta akicheka.

“Braza Moli ni mara chache sana kukutana na marafiki wazuri kwenye maisha yetu , sikuweza kudhania ninaweza kukutana na mtu ambaye tunafanana kwenye vitu vingi , mwanzoni nilikuwa nishaachana kabisa na mambo ya pombe lakini baada ya kukutana na nyie mabraza nimekosa uvumilivu”

“Eh..!!”

“Braza Chi kabla yako nilikuwa na Moli tu kama ndugu yangu lakini hajui chochote kuhusu maswala ya kutengeneza pombe na anajali sana kukusanya mimea , waliochini yangu wengine wanachojua ni kuvuna nishaiti za mbingu na ardhi , nilikuwa nimeboreka sana kabla haujaja”

“Bwana wetu mkuu wa majini ya kishetani na mmiliki wa Msitu wa Mianzi Zambarau , wewe ndio kiongozi wa majini ya kishetani na unasifika kwa uwezo wako mkuu ndani ya ulimwengu huu lakini ajabu ukaagiza majini ya Gredi ya chini kukutafutia vikombe vya Jade , naamini ni kwasabbau tu wanakuheshimu ndio maana hawakuwa na jinsi , wenzetu wakisikia ulichokifanya wataishia kucheka”

“Hata sijali , yule Mbweha kutoka Jumba la Jade mwenyewe ana mambo ya kipuuzi tu kama mimi , ni mkubwa kuliko mimi na pia ni mzuri zaidi ya wale minyoo katoka Korongo la Joka ,lakini akili yao muda wote ni kuwaza namna ya kutoka ndani ya huu ulimwengu na wasivyojua wanapoteza nguvu na hela zao kwa ajili ya mambo ya kipuuzi”Aliongea huku akitingisha mabega.

“Tuachane nao na tufurahie maisha yetu kwa kunywa mvinyo , Braza Zao unaonaje?”Aliongea Master Chi huku akiinua kikombe chake cha Jade.

“Vizuri sana , sijawahi kukutana na mtu kama wewe unaefurahia sana pombe”Aliongea na palepale alijaza na cha kwake na wakagongesheana na kuendelea kunywa kwa furaha.

“Braza Zao nimetoka Msitu wa Giza na kidogo tu niingie matatizoni lakini kwa bahati nzuri kuna mgeni ambaye ni binadamu alienisaidia”

“Eh… kuna mtu mwingine amefika tena? , haukutumia kadi yangu? , ila sidhani kama wale watu wa miliki ya Mbweha wa Jade wanaweza kukudhuru ilihali wanakujua upo chini yangu “

“Nilitaka kupambana nao lakini wakati nataka kuitoa ndio walitokea hao binadamu na kunisaidia”Aliongea na kisha akamgeukia Master Chi.

“Master Chi sidhani kama ushawahi kusikia binadamu anaevuna nishati za mbingu na ardhi katika ulimwengu wa nje … jina lake anaitwa Roma Ramoni”Aliongea na palepale macho ya Master Chi yalibadilika na kuwa makali






SEHEMU YA 604.

Moli mara baada ya kuona mshangao wa Master Chi palepale alikumbuka namna ambavyo Roma aliweza kutengeneza vinyoka nyoka vya moto.

“Nilijua tu , alikuwa akitumia mbinu za moto katika kushambulia lakini sijawahi kusikia mtu yoyte ambaye ashawahi kufanya hibyo , Roma alikuwa a uwezo wa kuwasha Dragoni za moto bila tabu yoyote na palepale nilikumbuka mbinu zako Master unazotumia zinafanana”

Bwana Zao alijikuta akishangazwa na jambo hilo baada ya kusikia maelezo yote ya Moli.

“Master Chi je huyo ni mwanafunzi wako?”Aliuliza na kumfanya Master Chi kutoa pumzi nyingi huku uso wake ukiwa ni ngumu kuusoma na kisha akapeleka kikombe chake cha mvinyo mdomoni na kunywa pafu moja.

“Huyu mtu siwezi kusema alikuwa ni mwanafunzi wangu bali tulishawahi kukutana na kufahamiana, naamini hili limepangwa kutokea .. nililazmishwa kuja huku kwasababu nilikuwa nikitaka kuuliwa , je na yeye ndio kilichomtokea kama mimi?”Aliuliz lakini swali lake lilimlenga yeye mwenyewe.

“Moli kama wewe ulikuwa ushaona ana tumia mbinu sawa na za Braza Chi kwanini usingekuja nae hapa?”Aliuliza Bwana Zao huku akionyesha kutopenda.

“Sikuwa nikijua kama anafahamiana na Master Chi , isitoshe mpaka sasa una mtegemea zaidi Master Chi kwa ajili ya Mashindano ya Mbingu, sikutaka kuvujisha taarifa za uwepo wake ila nilimshawishi kuja na mimi katika msitu wa Mianzi Zambarau kwa zaidi ya mara mbili lakini alikataa na kusema yeye safari yake ni kuelekea katika Ziwa La Mbingu hivyo nilimuacha kwani sikutaka kuingilia mambo yake”



“Kama hivyo ni kweli basi sasa hivi naweza kukisia atakuwa kwenye miliki ya Mbweha wa Jade , Braza Chi ninaweza kukusindikiza kwenda katika jumba la Mbweha wa anga mikia tisa kama unataka kumfuata”Aliongea Mzee Zao na kumfanya Master Chi kuwaza kwa dakika kadhaa.

“Yupo imara sana na sidhani kama uwezo wake ni wa chini kuliko wa kwangu kulingana na maneno ya Zimo , Majini hata hivyo hayawezi kuonyesha nguvu zao zote , naamini atakuwa sawa . isitoshe hawezi kufika katika mnara wa Mbingu kabla mashindano ya Mbingu kumalizika , tutakuwa na uwezo wa kukutana nae tukielekea katika Ziwa la mbingu”Aliongea Master Chi na kumfanya Zao kutoa kicheko hafifu.

“Unaonekana upo makini kweli , kama ni hivyo kwanini tusipige mkupuo mwingine wa kinywaji chetu , bado ipo ya kutosha , tunaweza kuongezea maana kilevi chake sio kikali sana”

‘Tutakynywa kutosheka leo hakuna namna”Aliongea huku akijiambia atajua mwenyewe huyo mtukutu wa maka mingi iliopita , hakutaka kujishughulisha na kile ambacho kitamtokea na pia hakuwa na nguvu ya kumjali katika mazingira kama hayo , hivyo anapaswa kunywa kujigalagaza.

Moli ambaye hakuwa mnywaji sana aliishia kutingisha kichwa chake huku akiwa ni kama anawaonea huruma kwa ulevi wao.

******

Roma alikuwa na uhukika yule jini Huja angekwenda kuleta wenzake hivyo alichokifanya ni kumbeba Aoli pamoja na Sophia na kisha akapaa nao ili kwenda umbali mrefu kutoka katika eneo hilo.

Roma hakutaka kumuacha nyuma ilihali alikuwa ashakubali kuongozana nae na isitoshe pia uwezo wake ulionekana kuwa mdogo.

Roma licha ya roho yake kujiambia muda wowote watakamatwa lakini hakutaka kujisumbua kuhusu hilo , alijiambia atapambana na kila ambalo litakuwa mbele yake.

Baada ya kuweza kupita kilima hatimae waliweza kufika sasa katika ardhi ya tambarare , katika eneo hilo kitu pekee ambacho aliona atumie kuweza kurahishisha safari ni mbinu nyingine ambayo alijifunzaga iliokuwa ikitofautiana na mbinu za kijini , ilikuwa ni Qinggong .

Roma hakuwa akitembea bali alikuwa akikimbia huku akiruka ruka kwenda mbele kama vile ni chui anaejaribu kufukuzia swala, kuhusu Aoli alikuwa akipambana kuweza kumfukuzia Roma bila kuchoka asiachwe mbali.

Baada ya kupumzika walianza kutembea taratibu taratibu na Sophia alimuuliza Aoli mwonekano wake wa mwazno kabla ya kuwa na mwili wa kibinadamu ulikuwa vipi lakini Aoli alionekna kuona aibu.

Majini ni viumbe ambao wanachukia sana miili yao wanayo zaliwa nayo na ndio maana mara nyingi hata kama wakipambana na adui wakiona ni mkubwa kiliko wao wanaacha na kukimbia.

Mbinu pekee ya kuweza kutumia nguvu zao zote ni lazima wabadilike maumbo yao.

Roma yeye hakufuatilia mazungumzo yao na aliuliza mara chache kuhusu taarifa ambazo alikuwa akihitaji tu kwa ajili ya kumsaidia kufika mwisho wa safari yake.

“Mister Roma je unapanga kutoka kwenye huu ulimwengu kupitia Manara?”Aliuliza Aoli lakini Roma aliona mrembo huyo wa kijini anauliza swali ambalo lipo wazi.

“Nadhani siendi huko kucheza eti, nasikia lakini radi inayotokea katika huo mnara ni ngumu sana kuhimili?”Aliuliza Roma na Aoli alionekana kushangaa kidogo.

“Mr Roma utanisamehe kwa uongeaji wangu wa moja kwa moja , licha ya kwamba uwezo wako unakaribiana na majini pepo ya anga na Majini Shetani ya anga haiwezekani kabisa kuweza kuhimili mapigo tisini na tisa ya mpangilio wa radi”

“Kila mtu ananiambia haiwezekani , ninapaswa kuondoka katika huu ulimwengu , nitafanya lisilowezekana kuwezekana”

“Hakika unaonekana ni jasiri mno , lakini nakuasa kuwa makini usijjilazimishe sana kama utaweza kupata nafasiya kuingia katika huo mnara la sivyo utakufa”

“Unamaanisha nini kupata nafasi , huo mnara sio kila mtu ambaye anaweza kuufikia?”

“Ndio , Mnara wa mbingu haupo wazi kwa kila mtu , mara nyingi unakuwa umezigingwa na radi ya zambarau, ukiwa umefungwa haitokuwa rahisi kuweza kuufikia na kuupanda isitoshe sehemu ya kuingilia kwenye mnara inafunguka mara moja tu kila baada ya miaka sitini”

“Miaka sitini!!?”Roma alitoa mshangao huku akipandisha sauti yake wakati akiuliza.

“Kwahio unamaanisha napaswa nisubiri kwa miaka sitini mpaka niweze kutoka?”Aliuliza na kumfanya Aoli kutoa tabasamu.

“Una bahati kubwa mnara huo mwaka huu unatimiza miaka sitini tokea kufunguka kwake maara ya mwisho , hivyo ndani ya mwezi ujao utafnguka kwa mara nyingine”Aliongea na kumfanya Roma macho yake kuchanua kwa furaha.

“Kama ni hivyo basi naweza kusema nimekuja huku ndani ya muda muafaka”

“Ndio lakini ..”Aoli alionekana kupumua kwanza.

“Lakini nini?”

“Unapaswa kukidhi vigezo kama unataka kuingia ndani ya mnara huo , vigezo ni mpaka ushinde Mashindano ya Vita ya mbingu”

“Mashindano ya Vita ya Mbingu unamaanisha nini?”Aliuliza Sophia akionekana kushangaa.



“Ili kukuelewesha vizuri napaswa kukuelezea stori ilivyo tokea mwanzo , ukiachana na mawe ya kiroho ambayo yanachimbwa chini ya bahari , sehemu nyingine ambayo ina nguvu za kiroho ni ndani ya mnara huo ambao upo juu ya Ziwa , nishati hio inatokana na Radi inayopiga ndani ya hilo eneo , floor ya kwanza ya mnara huo haina radi lakini kwasababu ya uwepo wa kiwango cha juu cha nishati ya kiroho kuna mimea adimu sana inakuwa hapo ndani , ni mimea amayo inatafutwa sana na wakuu wote wa huu ulimwengu , kuna pia hazina za kiroho ambazo hupatikana katika hilo eneo , hizo hazina pamoja na mimea husaidia sana katika kupanda levo kwenye uvunaji wa nishati ya mbingu na ardhi , lakini kutokana na hilo katika Floor hio mara nyingi inageuka kama eneo la machinjio.

Miaka elfu kumi iliopita wakuu wote wa majini waliweza kuona kwamba wanazidi kupungua siku hadi siku kama wataendelea kuchinjana kila baada ya mnara huo kufunguka ili tu kuingia , hawakutaka mbinu zao za kuvuna nishati kupotea hivyo ili kurudisha tumaini kwa ulimwengu huu yakawekwa makubaliano kwa kila upande kutuma wawakilishi kila baada ya miaka sitini kushindania nafasi ya kuingia katika mnara huo na kuweza kupata hio mimea na baadhi ya hazina hizo , kupitia mashindano hayo hakukuwa na haja ya watu kufa kwani anaeshinda ndio anaeingia , ni shindano pia ambalo limeandaliwa kwa ajili ya kuongeza spidi ya watu kujifunza mbinu za kijini ili kila miaka sitini inapokaribia waweze kupata nafasi ya kushindana , kwa mwaka huu lazima shindano hili lifanyike

Huu ulimwengu umegawanyika katika miliki kubwa tatu ambazo zilijigawa miaka mingi iliopita, kuna miliki ya Mbweha wa Jade , Miliki ya msitu wa Mianzi zambarau na Bonde la Joka”

Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo alijiambia kweli hawa majini sio wa kuchezea, wanaonekana kuwaza mbali sana mpaka kuandaa mashindano hayo.

“Kwahio unamaanisha kama nitalazimisha kuingia ndani ya huo mnara nitashambuliwa na hizo nguvu tatu si ndio?”

“Hilo sio tatizo , kuna baadhi ya majini wengine wanajitegemea lakini kutokana na koo tatu kuwa na washindani wenye nguvu sana , basi mara nyingi wale wanaopenda kushindana kwa kujitemgea wanakosa ujasiri”

“Bro Roma kama kweli wapo levo ya daraja la tisa si inamaanisha uwezo wao ni mkubwa kuliko wa kwako?”Aliuliza Sophia.

“Kama hao viongozi watatu wa juu kila koo wapo kwanini wasipigane wao kwa wao mpaka kutuma wawakilishi?”

“Hao watatu waliweza kupata umaarufu wao miaka mingi iliopita na wanajua fika , kama watapambana wenyewe kwa wenyewe inaweza ikachukua hata mwaka na asipatikane mshindi hivyo mnara utafunga ndio maana wanatuma wawakilishi , sheria ya mashindano ni kwa wale tu ambao hawakuwahi kushidana , yaani majini wapya ambao wanataka kupata umaarufu na heshima , mara nyingi wanaonda kupamban ni wale walio katika levo ya Pepo wa anga na shetani wa anga”

Roma mara baada ya kusikiliza maelezo hayo alipata kitu cha kufanya lakini kwa wakati mmoja alikuwa na mgogoro wa nafsi.

Alijiambia anaweza akashinda kama tu ataweza kuwa mwakilishi wa moja wapo ya koo , lakini kama ataingia peke yake nafasi ya kushinda inaweza kua ndogo au isiwezekane kabisa na itambidi kusubiria miaka sitini ijayo kuweza kuingia tena.

Roma tokea aingia katika huo ulimwengu bado hajakutana na jini ambalo lipo levo ya daraja la saba lakini Moli mwenyewe ambaye uwezo wake ulikuwa ni wa chini alionekana kuwa ni hatari, hivyo Roma alikosa kujiamini kama ataweza kushinda hao majini ambao watakuwa katika daraja la saba ,nane na tisa.

“Aoli katika mashindano yaliopita nani alishinda pambano?”

“Ni Majoka mawili kutoka Bonde la Joka na ukiachana na lililopita na la nyuma yake zaidi walishinda hao hao , hao Drago ni majini ambao wapo chini ya mkuu wa majini Majoka na washindi hao wote kwa sasa wana vyeo vikubwa , mmoja ni Joka mjumbe wa shetani , Joka Mjumbe wa upepo na Joka Mjumbe wa ngurumo, ndio watawala ambao hata mkuu wao hawagusi kabisa kutokana na uwezo wao lakini licha ya hivyo bado wanatuogopa sisi majini tuliopo chini ya Bwana wetu mzuri, Mbweha wa mikia tisa”

“Kwa jinsi unavhyoongea ni kama vile umekutana na kiongozi mkuu wa Mbweha wa Jade?”Aliongea Roma huku akicheka.

“Bwana wetu ni jini pekee lenye muonekano mzuri kuliko kitu chochote ndani ya ulimwengu huu , urembo wake hakuna ambaye ashawahi kuufikia wala kuufananisha na kitu”Aliongea akijaribu kumsifia.

Roma hakutaka kupingana nae maana hata hivyo bado hajakutana na huyo mrembo anaeitwa Mbweha wa mikia tisa.

“Hata awe mrembo vipi hawezi kumfikia mke wangu”Aliwaza Roma huku hisia za kumkumbuka mke wake Edna zikimvaa na kuzidi kupatwa na hali ya kutaka kurudi duniani.

Dakika hio hio wakati Roma akimuwazia Edna alijikuta akishituka mara baada ya kuhisi mkandamizo wa hewa wa aina yake unatokea upande wa kusini.

Ilikuwa ni kufumba na kufumbua mwanaume aliweza kuonekana mbele akiwa angani amepanda ndege mkubwa mno wa rangi nyeupe na kwa jinsi ambavyo alikuwa akipepea alifanya upepo kupeperusha majaini.

Ndege huyo alikuwa akifanana sana na Shakwe wa baharini lakini yeye alikuwa mkubwa mno na kwa jinsi ambavyo alikuwa akipaa ilimshangaza sana Roma.

Roma alijiambia kama angekuwa na uwezo wa kupaa ndege mkubwa kama huyo basu ingemrahisishia kuzunguka katika miliki yote ndani ya muda mfupi.

Wakati Roma akimtamani yule ndege upande wa mwanaume huyo alikuwa akimwangalia Roma kwa chuki, na kitendo cha kuona Roma hamwangalii ilimfanya kutoa tabasamu la kifedhuli.

“Nadhani utakuwa ndio wewe binadamu mgeni mwenye uwezo wa kijini?”Aliuliza mwanaume huyo , alikuwa na nywele ndefu mno ambazo zilikuwa zikifika kiunoni za rangi ya kahawia, alikuwa amezifunga na kitambaa chekundu na kufanya mkia wake kupiga piga mgongoni.

Aoli alionyesha hofu na aliweza kujificha nyuma ya Roma kwa Woga ni kama vile mtu anapomuona mtu wa heshima.

“Mister Roma huyo ni Bwana mkuu wa jiji loote la Wingu jeupe , ni moja wapo ya majini therathini na sita ya uwezo wa anga anaitwa Baiju

Ni Roma pekee ambaye alikuwa akiweza kumwangalia moja kwa moja machoni , mkandamizo wake wa hewa ulikuwa mkubwa mno kwa mtu wa kawaida kumwangalia .

“Wewe upo katika daraja la tatu , kwanini umeongozana na hawa binadamu?”Aliuliza akimwangalia Aoli kwa hasira.

Aoli alionekana kutetemeka mno akikosa ujasiri wa kuongea .

“Tushaondoka katika mji wako tayari, je umenifuata mpaka huku ili angalau niongeze muda wangu wa kukaa”Aliongea Roma mara baada ya kumtuliza Aoli.

“Una maneno marahisi mno , umewaua watu wangu na kisha ukamjeruhi generali wangu Huja , nilitaka kupotezea lakini kilichoniuzi ukaamua na kuiba na mawe yao ya kiroho , unanichukuliaje kwa mfano kama unaweza kuondoka kirahisi”Aliongea na Roma kama kawaida alitoa tabasamu la kifedhuli.

“Nilijnua tu, inawezekanaje Huja akateka msichana mdogo na kumbeba kwenye kiroba hivi hivi , kumbe wana sapoti zote kutoka kwako?”

“Kuteka nini , sijui chochote kuhusu hilo , ninachojua ni kwamba nakudai uhai wako”Dakika hio hio alioongea aliruka kutoka kwenye ndege wake na kisha akampiga Roma teka la kifua.

Jini Baiju uwezo wake wa kijini ulikuwa katika daraja la nane ambao ulikuwa ukichukuliwa ni wajuu kati ya majini therathini na sita ya uwezo wa anga , wakati alipokuwa akiita nguvu zake za kijini miti ilianza kuyumba kutokana na upepo mwingi ulikuwa ukijikusanya na haikuwa miti tu hata mawe yalianza kuruka

Roma aliwaambia Sophia na Aoli kukimbia huku akikwepa shambulio la kwamba la wimbi la upepo na palepale aliita moto wa rangi nyeupe na kuungannisha na wa njano kwenye mikono yake.

Baiju uso wake ulibadilika mara baada ya kuona mpira wa moto huo lakini hata hivyo hakuonyesha kuuhofia.

Kwa jini la uwezo wake moto wa rangi nyupe na wa njano haukuwa na uwezo wa kumpa majeraha makubwa , alichopaswa kufanya ni kujikinga tu na nishati ya mbingu na ardhi.

Roma alianza kumrushia mipira ya moto kwa spidi zote lakini Baiju alikuwa mtaalmu mno wa kukwepa na kujikinga kwa wakati mmoja, baada ya kuona amekwepa sana palepale mkono wake uliadilika na kuwa kama mkuki mrefu wenye kumeta meta huku ukiwa na ncha kali isokuwa ya kawaida.

Roma palepale aliweza kukumbuka katika maneno ya Aoli aliomwambia ni kwamba majini yakifikia katika levo flani ya juu yanakuwa na uwezo wa kubadilisha viungo vyao kuwa siraha kutokana na kujiunganisha na vyuma , haijalishi muonekano wao ukoje lakini siraha hizo zilikuwa na urofauti kabisa na viungo vya mwili.

Aoli pia alimwambia kwamba majini ya kipepo hayana uwezo wa kutengeneza Dhana kama majini ya kawaida lakini siraha zao hazikuwa za kupuuzwa hata kidogo na isitoshe hata kama ikiharibika inaweza kurudi katika umbo lake.

“Nguvu yako ya moto haiwezi kuhimili nguvu ya panga zangu za upepo”Aliongea huku akitoa kicheko na alipigisha hewani ile siraha yake na palepale kulidhalishwa visu vya aina nyingi kwa wakati mmoja ambavyo vilikuwa vikiambaa kwa upepo tu kumshambulia Roma.

Roma hakutaka kuleta masikhara kukinga visu hivyo na mwili wake, hivyo palepale aliita nguvu ya kijini na kujaribu kuvizuia huku akivikwepa kwa spidi kubwa kwa sarakasi za kila namna , kuna kingine manusura kimtoboe kichwani lakini aliwahi kukwepesha kichwa na kikaambulia nywele.

Roma wakati huo aliweza kuelewa kitu, kadri visu hivyo vilivyo kuwa vikikata upepo na kutoa ile sauti yake ya Swiii.. vilikuwa vikisababisha mapigo yake ya moyo kwenda mbio mno.

“Pumbavu kabisa , hizi sauti zina matatizo gani”Alilaaani Roma maana ni kama mishipa ya damu inataka kumpasuka.

Roma palepale aliweza kugundua nini tatizo mara baada ya kuona tabasamu la kifedhuli la Baiju.

Tofauti na kuwa na makali hatari kama viwembe , suati zao za mkato wa hewa zilikuwa zikitegneneza mtetemo(vibration) ambazo zilikuwa na madhara kwa nguvu ya kijini iliokuwa ndani ya mtu

Roma kama mwili wake ulikuwa dhaifi angeweza kutema damu palepale.

“Unathubutu vipi kutumia mbinu zako hizo za hila”

Roma alikuwa amekasirika kiwango cha rami , wakati akiwa anasukumia mbali vile visu kwa kutumia nguvu ya mbingu na ardhi , palepale aliiita donge la Maji kubwa kama kitenesi kwenye mkono wake na baada ya kuliachia hewani Donge lile liligeuka barafu na kupasuka pasuka kama cheche na kuanza kumeza sauti ya mawimbi ya visu.

Baiju alionekana kushangazwa na kitendo hicho , hakuamini kama Roma alikuwa na uwezo wa kuita maji ya kiroho na kuyagandisha.

“Huu ni uchawi ,,, hio ni mbinu gani umetumia katika mafunzo yako?”Aliongea kwa kujiwazia na mpaka hapo aliona kabisa hakuna matumaini kwa shambulio lake la visu, hivyo aliamua kutumia mkuki wake kuanza kumsogelea Roma na kumshambulia nao.

Alionekana alikuwa na mpango wa kumuua kabisa Roma na pigo moja lakini upande wa Roma alionekana kutoa tabasamu lakifedhuli.

“Nilikuwa nikisubiri ufanye shambulio la aina hio”Aliongea Roma na palepale alichezesha mikono yake na kulitokea mng’ao kama wa moshi na palepale alimsogelea Baiju kwa spidi kubwa na kushika ncha ya ule mkuki wake na palepale barafu ilianza kusambaa kutoka katika ncha ya mkono wake na kuanza kumsogelea Baiju na kumfunika kwa kasi ya ajuu mno.

Baiju alijikuta akitoa ukulele kutokana na baridi kali aliokuwa akiisikia mwilini na alijitahidi kuvuta ule mkuki kutoka kwa Roma lakini ulikuwa umeshikiliwa vyema.

Sophia aliekuwa akiona mbali alijikuta akiruka ruka kwa kushangilia mara baada ya kuona matumaini ya Roma kushinda.

“Aoli angalia Bro Roma anashinda , Bwana wenu wa mji hana uwezo wa kumshinda , kwa staili hii naamini Bro Roma anaweza kuingia katika mnara , wewe unaonaje?”

Sophia alishindwa kuona mabadiliko ya ghafla ya Aoli huku macho yake yakiangalia namna ambavyo Baiju aligeuka barafu kwa ghafla.

“Huenda anaweza kuwa na kaji uwezo ..”Aliongea huku akitabasamu ki ovu na palepale alisogea kwa spidi kuelekea sehemu ambayo Roma na Baiju wanapambana , Sophia alitaka kumzuia lakini ile anataka kumshika ni hewa tu aliweza kushika kwani Aoli alikuwa na spidi ya hali ya juu na ilimfanya na yeye kuanza kumkimbiza

Baiju alijikuta akianza kutoa matusi kwa kutokuwa makini na kuanza kushindwa pambano kirahisi namna hio , Roma palepale hakutaka kumchelewesha alitaka kuinguza roho yake na moto wa Bluu kwani ulikuwa tayari ushajitengeneza katika mkono.

“Umekuja mwenyewe kwangu na sikuwa na kinyongo chochote na wewe lakini hata hivyo sitaki kusumbuana na mtu kama wewe hivyo nitakupeleka moja kwa moja kuzimu”aliongea Roma

“Huwezi kuniua ,,, Bwana wangu hawezi kukuruhusu uniue na atakuua wewe”Aliongea huku akishindwa kuzungusha chingo yake kutokana na kukabwa na barafu.

Roma hakutaka kusumbuka na maneno yake na ndio alikuwa akianza kutaka kuruhusu mpira ule wa moto wa rangi ya bliuu kuelekea kwake lakini ghafla tu mikono yake iliokuwa imeshikilia ule mpira wa moto ilifungwa fungwa na kamba ndeefu ya nguo ya hariri kwa nguvu kiasi cha kushindwa kudhibiti ule moto na palepale ulizimika.

Alijikuta akishangazwa na kitendo hicho kwani aliamini mtu pekee ambaye anaweza kuuzima moto wake ni mwenye uwezo mkubwa kuliko wa kwake.

Roma alijikuta jasho likimtoka na palepale kwa haraka sana aligeuza shngo yake na kuangalia nani ambaye amemshambulia kwa ghafla sana.

Roma mara baada ya kuangalia alijikuta akishikwa na mshituko mara baada ya kuona aliefanya hivyo ni Aoli na hata kamba ya hariri iliokuwa imemshikilia ilikuwa ikitoka kwake.

“Baiju alijikuta akisogea pembeni haraka sana na kujiifcha mara baada ya mkuki wake kuachiwa., lakini wakati huo huo alijikuta akipauka uso mara baada ya kumuona Aoli.

“Bwana wangu …. Bwana wangu…!!!”

Sophia alijikuta akisimama ghafla mara aada ya kushitukia tukio lile na aliishia kuachama tu.

Upande wa Roma akili yake ni kama ilikosa kufanya kazi kwa muda na hisia zake zilikuwa ni kama mtu ambaye alikuwa akiamini ukweli flani na sasa anaambiwa huo ni uongo.

“Wewe ni nani haswa?”Aliuliza Roma na kumfanya Aoli kumwangalia kwa dharau na palepale kama vile anamulikwa na tochi usoni na haraka sana mwili wa Aoli ulibadilika kabisa na kuwa mwanamke mwingine kabisa aliekuwa ni mrembo wa ajabu.

Mwanamke ambaye alikuwa mbele yake alikuwa amevalia mavazi ya hariri nyeupe huku yakiwa na kamba kamba zilizokuwa zimejiachia kama vile ni Ribon huku zikipepewa na upepo , nywele zake zilikuwa ndefu na nyeusi zikiwa zimefungwa na kitambaa .

Kwa jinsi ambavyo alikuwa akimwangalia Roma ni kama anamtega , ijapokuwa mavazi yae yalikuwa ya kawaida sana lakini uzuri wake haukujificha.

Hakukuwa na maneno sahihi ya kumwelezea kwani alikuwa ni kama uso wake unabadilika badilika na kuzidi kuwa mzuri , mbaya zaidi eneo lote lilijaa marashi ya aina yake ambayo yalitamanisha pua.

“Mister Roma mimi ndio mkuu wa miliki yote ya eneo la Mbweha wa Jade na jumba la kimalkia, naitwa Aoline , Nice to meet you”Aliongea huku akibadilisha muonekano wake na kuweka tabasamu la kiheshima , kwa namna ambavyo alikuwa akimwangalia Roma ni kama vile anamwambia naomba unipende.

ITAENDELEA.
Sawa
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA



MTUNZI :SINGANOJR.

WATSAPP: 0687151346.



SEHEMU YA 605.

Baiju miguu yake katika vigoti ililelegea palepale mara baada ya kujua mwanamke ambaye hakuwa amemtambua ni Aoiline mkuu wake.

“Bwana wangu , sikujua kama upo hapa tafadhari naomba unisamehe”Aliongea kwa kutetemeka huku akiwa amemsujudia chini , hakuwa tena yule mwenye kiburi.

Aoiline aliachana na Roma na kisha alimsogelea Baiju kwa hatua hafifu huku uso wake ukiwa ni ule wa kichokozi , hakuonyesha kabisa kuwa na hasira.

“Baiju nimepewa ripoti kwamba unakusanya kiwango kikubwa cha mawe ya kiroho kupitia Madanguro , ukiichukulia faida kwa mimi kutokuwa makini na maswala hayo , inaonekana umeweza kuteka majini wanawake kwa tamaa zako”

“Bwana wangu wananisingizia tu , waliochini yangu ndio ambao wamefanya kosa hilo kwa kunipatia rushwa , nitahakikisha nina wahukumu vifo nikirudi”Aliongea Baiju huku akionekana kutengeneza kisingizio.

“Hata mimi naona , kwa hio unasema mimi ndio mkosaji hapa kwa kusingizia si ndio?”Aliongea huku kitingishcha kichwa chake kama mtu ambaye anajaribu kumwelewa.

Baiju alitaka kutingisha kichwa kujaribu kujitetea kwamba hakupaswa kumbebesha lawama zote lakini hakuweza kufanya chochote wala kukubali kama ana kosa na uso wake ulibadilika rangi na kuwa mwekundu kutokana na presha ambayo ilikuwa ikijiandaa kumkumba.

“Umekuwa na mimi kwa zaidi ya miaka mia mbili , nimekufanya uwe Bwana wa mji wangu wa Wingu Jeupe na ukapokea tani na tani za mawe ya kiroho kutoka katika maghala ya mji na watu wengi wakakuonea wivu lakini bado ukaamua kukusanya zaidi Mawe ya kiroho kupitiia Danguro , Ingekuwa ni sawa kama tu ungekuwa ukidanganya hao ambao walikuwa wakipenda kufanya kazi chini yako lakini ukathubutu kuteka wale ambao wanajaribu kupita katika mji wetu , hivi unadhani mimi siwezi kuishi bila wewe , unafikiri mimi ni mwepesi kudanganywa?”

Jasho la baridi lilimtoka Baiju na kuloanisha nguo zake na aliishia kutingisha kichwa chake akiwa amekiinamisha chini akishindwa hata kumwangalia Aoiline.

“Bwana wangu, Sikuwa nikifikiri sawa sawa , tafadhari naomba unisamehe kwa dhambi nilizoafanya kwa zaidi ya karne moja”

“Sawa”Aliongea huku akikusanya nguo za mkono wake na kutingisha kichwa.

“Itakuwa ni ukatili kama sitoweza kukupa nafasi , nitakusamehe kwa kuwateka wasichana wa kijini nyuma ya mgongo wangu”Aliongea na kumfanya Baiju kufurahiswa na maneno yake huku akitaka kuanza kusujudu kwa mara nyingine lakini Aoiline alimkatisha.

“Lakini hata hivyo napaswa kukuadhibu kwa jambo moja”

“Ah..!”Alitoa sauti huku sura yake akipeleka chini kwa mara nyingine akiwa kama amechanganyikiwa.

“Watu wako hususani Huji wameniteka siku ya leo na wakaniingiza kwenye kiroba ,… ningekuwa mrembo wa kukuingizia hela ndani ya Danguro leo kama sio Mr Roma kunisaidia”

Hio ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Baiju na sasa aliweza kuelewa kwanini Aoiline alibadilisha mwonekanno wake , kila kitu kilikuwa ni mtego wa kumkamata na ufisadi wake.

Ingekuwa afadhari kama angekamata wanawake wengine lakini sasa alikuwa amemsaliti hata Bwana wake hakukuwa na sababu ya kuachwa hai.

Dakika hio alivyojaribu kuunganisha Dot katika akili yake , Baiju alijiambia hakukuwa na faida yoyote ya yeye kuomba kusamehewa au kujitetea na anapaswa kufanya kitu chochote kile ili kuweza kukimbia na kutoka katika hio miliki, alijiambia kama ataweza kufika katika Korongo la Joka , Mfalme wa Majoka lazima angemlinda kwani alikuwa ni jini mwenye uwezo mkubwa wa kimapambano katika levo ya nane.

Baada ya kupatwa na mawazo hayo hakutaka tena kuchelewa, palepale aliita kwa hisia ndege wake mweupe kwa ajili ya kumshambulia Aioline .

Ndege mweupe na yeye akasikia kuitwa na mkuu wake , na palepale lilitoa kilio kikubwa cha juu huku likipiga piga mabawa yake kumsogelea Aoiline moja kwa moja.

Aoline hakuonakana yule mpole tena kwani alibadilika na alikuwa na uso wa kikauzu usio kuwa wa kawaida na kwa Roma ni kama alikuwa akimuona Edna party two, ilikuwa ni kama vile hewa iliokuwa ikimzunguka imeganda.

“Wewe mjinga , unathubutu vipi kujaribu kunipinga mimi?”Aliongea kwa nguvu na palepale kulitokea mwanga kama nguzo mbili nyuma ya gauni lake na nguo moja ya mwanga ilimshikilia yule ndege kwa kumfunga funga.

Roma aliangalia kwa ukaribu zile nguzo zilizokaa kama kamba kamba na palepale ndipo alipogundua ni mikia na pale ndipo alipojihakikishia kweli huyo ni jini ambaye alikuwa akiitwa Mbweha wa mikia tisa.

Mikia yake ilikuwa ni mirefu mno na haikuwa ya kawaida , ilikuwa ni kama boriti au nguzo.

Yule ndege licha ya Roma kumuona mkubwa lakini mbele ya ile mikia alionekana kuwa mdogo mno kwani alikamatwa na akawa hafurukuti kabisa.

Ndege yule alianza kutapa tapa kama vile kuku ambaye anapoteza uhai na ndani ya dakika tu damu zilionekana kuruka juu , ilionekana alikuwa amekamuliwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha viungo vyake kuharibika na hata manyonya yake yalianza kusambaa angani.

Sophia alishindwa kabisa kuangalia kitendo kile lakini kwa Roma alikuwa akiona kitu kile kama hasara kwani yule ndege alimpenda na kujiambia angalau kabla ya kutoka katika ulimwengu huo amwendeshe hata mara moja.

Wakati Aoiline akidili na ndege Baiju alikuwa ashakimbia kwa kupaa umbali mrefu kidogo , lakini bahati mbaya kwake ni kwamba mkia mwingine wa Aoiline ulikuwa ukimfukuzia na ulikuwa ukiongezeka urefu kadri alivyokuwa akikimbia kwenda mbali..

Roma ni jambo lingine ambalo lilimshangaza kwani hakuamini kama mkia huo ungekuwa na uwezo wa kuongezeka urefu na kusafiri umbali mrefu tena kwa haraka sana.

Ni kufumba na kufumbua tu Baiju alipigwa na mkia ule kwa nguvu mara baada ya kusogelewa na alijikuta akitema damu kutokana na kichapo.

“Rudi”

Ule mkia ulimviringa Baiju kufumba na kufumbua tu na kumvuta nyuma na kisha kumrudisha ardhini mbele ya Aoiline na dakika ileile ulipotea katika macho yao , ilikuwa ni kama vile haukuonekana kwani licha ya urefu wake ulirudi ndani ya mwili wa Aoiline kwa spidi kubwa mno.

Roma alijikuta akitengeneza sauti kupitia ulimi wake , Roma alikuwa akijua mwanamke huyo alikuwa na mikia tisa na ameonyesha mwili tu na kilichotokea sio cha kawaida.

Pengine siraha yake kubwa ni hio mikia na kama atapambana nae basi atakuwa ni moja ya washindani hatari ambao ashawahi kukutana nao kwani angekuwa na uwezo wa kujikinga na wakati huo huo akishambulia.

Kwa spidi yake hio na nguvu zake za kijini aliona kabisa hata yeye hakuwa akimuweza kimapambano kabisa, na hakutaka kujiona yeye ni mkubwa zaidi hivyo alikubali Aoiline alikuwa ni levo ya juu kuliko yeye.

Baiju alijikuta amepauka mno kwa woga , alikuwa tyari amekwisha kujikatia tamaa katika kukimbia na aliishia kusujudu kadri awezavyo na kujaribu kuomba kuhurumiwa , lakini licha ya kujitetea huko kulifanya tabasamu la kikatili la Aoiline kuzidi kutisha.

“Bwana nimetenda dhambi zidi yako , unaweza kuondoa nguvu zangu zote za kijini na kunigeuza kuwa mnyama lakini tafadhari naomba usinie , naomba unisamehe”

“Siku zote nilikuwa mpole sana kwa viongozi kama nyie , kwanini nikuondolee nguvu zako za kijini ?,Baiju je utanisaidia jambo moja?”

“I’m willing to redeem myself!”Aliongea

“Great”

Kufumba na kufumbua Aoline alikuwa nyuma ya Baiju na kuishika shingo yake na palepale mkandamizo wa hali ya juu ulianza kumtoka.

“Sophia kuwa makini”

Aliongea Roma na palepale alimsogelea Sophia na kumzingira na nguvu ya kijini kwani tayari ashajua ni nini kinachokwenda kutokea .

Aoiline alikuwa akipanga kumkandamiza na nguvu yake ili kuweza kutawala uwezo wake hivyo kutokana na mkandamizio mkubwa ambao alikuwa akijaribu kutoa Aoiline ilikuwa ngumu kwa Sophia kuweza kuhimili na angetema damu kwani mara nyingi inakuwa kama vile ni mlipoko wa bomu.

Ilikuwa ni kama vile mwanamke huyo mrembo amegeuka na kuwa mungu wa huo ulimwengu kwani macho yake yalikuwa yamebadilika kabisa na kile kiini cheusi kilikuwa kimempotea kwenye macho na jicho likabakia jeupe kama vile ni barafu.

Dakika ileile Aoiline alifumbua mdomo wake na meno yake yaliongezeka urefu kama Vampire na kuyapelekea katika shingo ya Baiju na kumng’ata.

Baiju sura yake mwanzo ilikuwa imepinda kutokana na mkandamizo mkubwa lakini mara baada ya kung’atwa mwili wake ulibonyea palepale .

Sophia aliekuwa nyuma ya Roma hakuweza kupata ujasiri wa kuangalia kile kinachotokea kwani iliogopesha , upande wa Roma alikuwa katika bumbuwazi kwa kile kinachotokea

Alijiambia swala la kunyonya damu ni la kawaida kwani kilichofanyika ni kujaribu kunyonya nguvu za lile jini lakini hakutegemea mwanamke mrembo kama huyo ndio ambaye anafanya kitendo hicho.

Kile kitendo huenda angekuwa ni binadamu wa kawaida ambaye anaangalia angepoteza fahamu palepale , Sophia kwa kiasi hakuwa wa kawaida kwani alikuwa ashaishi na Roma na kuzoea baadhi ya mambo ya ajabu ya namna hio.

Dakika chache tu mwili wa Baiju ulibadilika na Akawa Kunguru mkubwa ambaye ameoza huku mifupa yake ikianza kuonekana na Aoiline alimsukumia mbali maiti ile ya Kunguru na kuanza kuilamba midomo yake kwa damu zilizokuwa pembeni, alikuwa ni kama vile analamba asali kwa jinsi alivyonekana kufurahia.

Baada ya mkandamizo wa hewa kuondoka ndio aligeuza macho yake kwa Roma huku akiachia mkandamizo wa kawaida kama vile alikuwa akijaribu kumuogopesha Roma.

“Mr Roma huna haja ya kuniangalia hivyo na kuniona kama mchawi mnyonya damu , nimefanya hivi kwa zaidi ya miaka elfu moja , hatima yake ilikuwa ni kifo hata hivyo , kwanini nisimtumie kama kirutubisho , Au naongea uongo?”

Roma alikuwa akianza kuwa na wasiwasi juu yake , hata kama alionekana kuwa mrembo wa kuita lakini matendo yake na uwezo wake wa kijini ulimpa mashaka makubwa na kushindwa kuijua nia yake halisi juu yao.

“Nadhani tunapaswa kuendelea na safari yetu maana ushamaliza maswala yako”Aliongea Roma na kisha akamwangaliaSophia akimwambia waanze safari ya kuondoka hapo haraka iwezekanayvyo.

Sophia hakuwa na shida na alikubali kuondoka , yule Aoiline ambaye alitaka kuwa nae karibu hakumtaka tena maana alikuwa akitisha.

Aoiline palepale alitoa tabasamu la kifedhuli na kufumba na kufumbua alikuwa mbele ya Roma na kuwazuia wasiondoke.

“Mr Roma tupo karibu na jumba langu la kimalkia kwanini msiende kupunzima kwa muda”

“Hakuna shida sana juu ya hilo , safari yetu ni kuelekea kando ya ziwa la Mbingu”Aliongea Roma huku akijaribu kutafuta upenyo wa kumpita.

“Hata kama nimekudanganya kuhusu ubini wangu , lakini sikuwa nikidanganya kuhusu mambo mengine , kuna zaidi ya wiki tatu mpaka kwa mnara kufunguka , kwenda huko ni kupoteza muda wako tu”

“Mimi naweza kutokuwa na akili kama wewe lakini siwezi kuwa kichaa kabisa na kuanza kupigana na mtu kama wewe ambaye umeishi maisha marefu , lazima una nia nyingine hivyo acha kuzunguka zunguka”Aliongea Roma mpaka hapo alijua mwanamke huyo hakuwa na nia ya kuwaruhusu waondoke kirahisi.

“Mr Roma sisi majini tunaweza kufikiria pia na sio wanafiki kama binadamu , mosi nimekuja huku kwasababu nimesikia taarifa kutoka kwa watu wangu ndio maana nimekuja kujionea mwenyewekama ni kweli Baiju alikuwa akitenda mambo ya kifisadi, kitu kingine pia waliniambia kwamba kuna binadamu wageni ambao wameweza kufika katika ulimwengu wetu , Watu watatu ambao ulipigana nao katika msitu wamekuongelea vibaya sana lakini sikuwachukulia siriasi na sina nia ya kuwalipizia kisasi kwa uliowafanyia”

“Lakini bado siamini mtu kama wewe unaweza tu kunialika kwako kwa ajili ya kupumzika”Aliongea Roma huku akitoa tabasamu.

“Nimeongea vya kutosha je tunaongozana au hatuongozani”

“Hatuongozani”Aliongea Roma kwa sauti huku akitingisha kichwa chake kukataa kusisitizia msimamo wake.

Aoiline alitoa pumzi ya kukatishwa tamaa huku akimwangalia Roma kwa masikito.

“Kama hutaki kuongozana na mimi basi sina budi kukulazimisha”Baada ya kuongea hivyo msisimko aliokuwa ukitoa ulibadilika kabisa na macho yake hayakuwa mazuri tena kwani yalibadilika na kuwa ya chuki.

Roma alishindwa kuelewa chuki yake inatokana na nini , aliajiambia kwanini kumbadilikia namna hio ndani ya dakika tu wakati hajamchokoza.

Roma palepale alimsukumia mbali Sophia ili tu asije akapata madhara na baada ya kumuona ameenda mbali zaidi aliita nguvu zake za kijini ili kuweza kuhimiri mkandamizio uliokuwa ukitolewa na Aoiline.

Dakika hio hio Aoiline muonekano wake wa kirembo ulikuwa umebadilika na kuwa kama vile ni jitu kubwa la kutawala , macho yake yalikuwa ni kama yale ya kutaka mtu yoyote anaemuona kumsujudia.

Roma hakutaka kumruuhusu msichana kama huyo kuendelea kumkandamiza , hakutaka tena kulinda nguvu yake ya kijini isipotee na alimsogelea Aoiline kwa nguvu zake zote.

Mpira wa moto wa bluu ulionekana katika mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto ulitegneneza maji ya kiroho ya kuosha uovu.

Aoiline alitoa tabasamu la kejeli kama vile alikuwa akidharau kile anachotaka kufanya.

Awamu hio hakutoa mikia yake bali nguo yake ilianza kutengeneza kamba kama Ribbon kutoka kwenye nguo yake ya hariri akidhamiria kupigana na hio .

Roma hakutaka kujali mbinu yake ambayo anataka kutumia na dhamira yake ilikuwa ni kutaka kumchapa na maji ya kiroho akiamini hata tone lake linaweza kumletea madhara.

Lakini nguo yake ile haikuwa nguo kama nguo kwani ilikuwa ikidhalisha kiwango kikubwa cha nishaiti isiokuwa ya kawaida na kadri ilivyokuwa ikipepea kuelekea upande wa Roma ni kama ilikuwa ikimzuia asimfikie.

Roma alijikuta akishangazwa na uwezo wake , aliweza kujua mtu anaepambana nae ndio yupo katika levo ya juu kabisa ya daraja la tisa la mafunzo ya kijini ya kuita pepo.

Kutokana na mkandamizio wake kuwa mkubwa Roma alijikuta akiamini huenda hata Athena akashindwa kabisa kudili nae.

Kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao mpizani wake Roma alianza kupoteza pambano mapema kabla hata hajaanza kushambulia kwani alishindwa hata kubadilisha nguvu zake kuleta faida katika kushambulia.

Aoiline hakuonyesha kutumia nguvu yoyote alikuwa ni kama vile anacheza na zile kamba za nguo zake za hariri na alianza kuzifanya zipeperuke hewani na zilikuwa zikitoa nguvu kubwa mno .

Roma palepale aliweza kufikiria huenda mbinu yake haikuwa ikitegemea muundo au nguvu bali alikuwa akitegemea akili yake na ufahamu . mpaka hapo alijua kwamba ulimwengu huo wenyewe ulikuwa kikwazo kwake hivyo hakuwa na namna ya kumshinda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom