Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 715.
Tulipoishia:
Roma amefanikiwa kurudi upya kwenye ulimwengu wa majini watu na kufika katika makao makuu ya miliki ya Xia kwa ajili ya kumuokoa Rufi , katika harakati za kuingia bila kujulikana anamuua Jinni ambaye ni Mlinzi afahamikae kwa jina la Cheli na kisha anachukua uhusika wake , mara baada ya kuingia ndani hatimae akijifanyisha kufanya Doria lakini anashitukiwa na anaambiwa asimame hapo hapo alipo.
Roma alikuwa ashahisi akisogelewa kwa muda mrefu lakini hakutegemea kama jini huyo angemuamrisha kusimama tena kwa sauti kubwa , mara baada ya kugeuka aliweza kuona jini mzee ambaye amevalia joho la rangi nyeusi akiwa na nywele ndefu za rangi nyeupe.
Uso wake ulikuwa ni ule wa kujiamini na alikuwa akimwangalia kwa namna ya ajabu , ni kama vile mwewe anavyoangalia vifaranga na kumfanya Roma kuwa na wasiwasi.
Alikuwa ni jini ambaye yupo katika levo ya maji ya barafu na Roma aljiambia huyo sio mwepesi wa kudili nae mara moja.
Roma palepale akijiepusha kujulikana aliinamisha kichwa chake chini kama ishara ya heshima.
Huyo jini mzee alifahamika kwa jina la Lao , ndio ambaye alifika ulimwengu wa kawaida na kumkamata Rufi akiwa na Lahani, kazi yake ndani ya makao makuu hayo alikuwa ni Mtumishi Kiongozi.
Mara baada ya kumuona Roma anaelekea upande ambao haukuruhsiwa kufanyiwa doria pamoja na kuongea na walinzi kila mara ilimfanya kumshuku.
Walinzi wote ndani ya eneo hilo walikuwa wakisimamiwa na yeye mwenyewe na alijua huyu mtu anaefahamika kwa jina la Cheli , alikuwa ni jini wa kawaida ambaye anafanya kazi chini ya familia ya kiongozi mkuu wa miliki.
Master Lao alikuwa akimjua Cheli ni moja wapo ya majjini waliopo mwishoni mwa levo ya nafsi ambao ni waaminifu na hawawezi kuonekana wakitembea tembea sehemu ambazo hawaruhusiwi.
“Cheli kwanini umekuja huku eneo ambalo sio lako?”Aliuliza mara baada ya kumona hamsalimii , Roma hakutaka kusalimia kwani hakutaka kugundulika.
“Nastahili adhabu kwa kukiuka majukumu yangu?”Aliongea Roma huku akijifanyisha kuwa muoga.
“Nyanyua kichwa chako na ongea na mimi ukiwa unaniangalia”Aliongea huku akipiga hatua kumsogelea Roma karibu huku akitoa nguvu ya kijini ya kuogofya.
Upande wa Roma alionyesha kuathirika na muonekano wa Mtumishi Lao lakini kwa wakati huo alikuwa akiongea na moyo wake , alijiambia hilo eneo ni katikati ya makao makuu ya miliki hii anaweza kumuua ndio lakini lazima ataamsha walinzi wakuu ndani ya eneo hilo na mpango wake wa kumuokoa Rufi ungefeli au kuingia hatarini.
“Kwanini hunipigii saluti?”Aliongea na palepale Roma kwa haraka aliinua mkono wake na kumpa saluti yake.
“Umesahau mimi ni nani?”Aliongea Mtumishi Lao huku akizidi kuhisi kuna kitu hakipo sawa kuhusu Cheli , mlinzi huyo mara nyingi alikuwa akipiga sautli lazima ataje jina lake , lakini kitendo cha kutotaja jina ilimaanisha kwamba hakumfahamu , sasa alijiuliza inawezakaje.
Lao alishakuwa Mtumishi ndani ya familia ya viongozi wa miliki kwa muda mrefu sana , ni zaidi ya miaka mia moja na yeye mwenyewe umri wake ilikuwa ni miaka mia mbili , hivyo asilimia tisini ya majini wote wanaoshi ndani ya miliki hio walikuwa wakimfahamu.
Roma alijikuta akipatwa na jasho la ubaridi , hali ilikuwa ikiendelea kuwa mbaya na kama ataendelea kubakia hapo angeweza kumtambua.
“Wewe sio Cheli , niambie wewe ni nani?”Aliongea na palepale alinyanyua mkono wake na kufanya nguvu za kijini kuendelea kumtoka kwa wingi na alikuwa tayari kumkamata Roma.
Lakini muda ule Roma akili yake ilikwisha kucheza tayari na alishapata mpango wa kumaliza hio hali.
“Guru Master!!!”
Aliongea Roma na palapele alinyoosha kidole nyuma yake akijifanya kama vile yupo kwenye mshangao kwa kuona mtu nyuma.
Ijapokuwa ameishi miaka mingi lakini hakuwa akijua hila za kibinadamu za kutoroka na ndio alichomfanya kwa kujifanyisha kushangaa mtu aliekuwa nyuma yake na aligeuka kweli kwani alikuwa akitegemea kumuona Laofi.
Baada ya kugeuza kichwa chake aliishia kulaani katika kichwa chake na kujiona ni mjinga kwani kama kweli Laofi amekaribia basi angeweza kuhisi uwepo wake , akiwa na hasira aling’ata meno yake na kumgeukia Roma lakini Roma alishaondoka mbele yake na kukimbia.
“Unathubutu vipi kukimbia?”Aliongea kwa hasira na palepale aligeuka kama kivuli na kumpandia Roma hewani na kuanza kumfukuzia.
Roma wakati huo alikuwa akitumia nguvu ya kijini katika levo ya nafsi hivyo spidi yake ilikuwa ndogo na ingemuwezesha kukamatwa na jini ambaye yupo katika levo ya maji ya barafu hususani kwa mtaalamu kama Lao.
Baadhi ya majini wa levo za juu pia waliweza kumshuhudia Mtumishi Lao kumfukuzia jini ambaye yupo katika levo ya nafsi lakini hawakujisumbua kumsaidia wakiamini kwamba kwa uwezo wake ataweza kummudu , shukrani kwao Roma aliona kabisa hio ndio nafasi ya kujitoa katika hali hio ya mtego.
Upande wa majini walinzi waliokuwa katika levo ya nafsi na baadhi waliopo katika levo ya moto wa njano walitaka kujichukulia sifa kwa kwenda kumsaidia Mtumishi lao hivyo waliunga nyuma katika kumfukuza Roma.
Upande wa Roma hakuwa na wasiwasi , ilimradi hakukuwa na jini ambalo lipo levo ya maji ya upako ingekuwa rahisi kudili na majini hao wa levo ya chini , hivyo alijiambia anapaswa kukimbia kwenda mbali kadri awezavyo.
Kufumba na kufumbua Roma alikuwa zaidi ya kilomita ishirini mbali na makao makuu ya miliki ya Xia na upande wa Master Lao alikuwa akimfukuzia kwa kasi na kumsogelea karibu.
Palepale Lao alitoa tabasamu la kifehdnuli na kisha alitoa mjeledi wa mkanda rangi ya silver ambao una urefu kama futi saba hivi kwenye hifadhi pete yake , ulikuwa na mafundo fundo yalifungwa kwa namna ya kiajabu.
Wale walinzi waliokuwa wakifatilia nyuma mara baada ya kuona Dhana hio ya mjeledi wote walijikuta wakitoa kicheko cha furaha.
“Huyu mwizi hana bahati , Mtumishi kashatoa tayari
Dhana yake ya Mjeledi wa ngurumo ya radi , ile ni
Dhana ya daraja la kati na ina nguvu ya kueleweka”
“Nishawahi kusikia mjeledi wa ngurumo unaweza kushambulia na kuzuia , nguvu yake ni sawa na Dhoruba ya radi lakini kwa bahati mbaya sijawahi kuona ikitumika”
“Tokea siku nyingi nilikuwa nikitamani kuonyesha uwezo wangu , lakni wezi ni adimu sana kuja makao makuu ya familia ya viongozi , nadhani hata leo nimekosa nafasi”
Walinzi walikuwa wakiongea huku wakiamni Roma anakwenda kupoteza pambano , wote kwa pamoja walipunguza spidi wakiona haina maana ya kukimbia kwa spidi.
“Ewe mwizi onja radha ya mjeledi wangu wa ngurumo ya radi!!!”
Muda huo mara baada ya Master Lao kuona umbali kati ya Roma umekuwa mfupi aliunganisha mjeledi wake ule na nguvu za kijini na palepale ulianza kuwaka moto na kutoa shoti kama za radi huku ukiambatana na ngurumo.
Shoti zile za radi zilikuwa na spidi mno kwani zilimsogelea Roma kwa spidi , ilikuwa ni kama vile ule mkanda unaongezeka urefu wake lakini haikuwa hivyo ilikuwa ni kutokana na nguvu ya kijini ambayo imetumika hivyo zile Radi ndio zilionekana kama vile mkanda umeongezeka.
Upande wa Roma muda huo alijikuta akishangazwa na Dhana ile ambayo inatoa moto kama radi vile.
Ili dunia kubalansi asili yake ilitengenezwa na nguvu za aina mbili zinazopingana lakini kuvutana kwa wakati mmoja , Ying and Yang , Chanya na Hasi , maji na moto, mbingu na ardhi n.k.
Elementi nyingine za dunia kama vile Dhahabu miti , ardhi na upepo vyote vimewezekana kutokana na nguvu mbili ambazo hazifananani lakini kuvutana.
Hivyo likija swala la Dhana na Nishati za mbingu na Ardhi asilimia kubwa elementi ambazo hutumiwa na majini ni maji na moto.
Asilimia kubwa ya majini wa kawaida hawawezi kutumia radi ambao wenyewe huita moto wa mbingu(Heavenly fire) lakini wanao uwezo wa kutumia nguvu zao za kijini katika kubadilisha nishati ya kiroho ili kucheza na maji na moto hata zaidi ya hapo.
Kuna baadhi ya mbinu za kucheza na moto na maji na kuzalisha kitu kingine kabisa na kuwa na nguvu kukaribiana na radi, kwa mfano mbinu ya majini wa kikaskazini ifahamikayo Dark ice soul ambayo hutumiwa zaidi na Hongmeng , hio ni mbinu ambayo imetokana kati ya kufungamanishwa roho na barafu.
Lakini sasa ukizungumzia elementi za radi ni za kipekee sana , radi hutokana na elementi zote mbili za moto na msunguano wa maji ya barafu katika mawingu.
Kwahio mchanganyiko wa hasi na chanya siku zote unakuwa ni hatari sana na ndio asili ya Adhabu ya mapigo tisa ya radi ambayo nguvu yake inakuwa ni zaidi ya nishati za mbingu na ardhi.
Kama sio hivyo pengine Zeus asingeweza kuwapiga majini kwa kutumia siraha yake ya ngurumo miaka elfu ishirini iliopita , ijapokuwa Zeus siraha yake haikuwa na nguvu kama mapigo tisa ya radi ngurumo lakini ilikuwa ni kitu ambacho kina athari kubwa kwa majini.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba majini wanaoogpa sana Radi kuliko kitu chochote kile na ndio Dhiki yao kubwa wanayoihofia sana.
Roma alijua radi ambayo inatoka katika mjeledi wa Lao ni radi ya kawaida kabisa ambayo imetengenezwa kwa kunyumbulisha elementi za dunia hivyo haiwezi kulingana na ile inayotoka juu mawinguni lakini hata hivyo hakutaka kuidharau nguvu hio.
Sasa Roma mara baada ya kuona sasa yupo mbali na miliki ya Xia hakutaka tena kuficha uwezo wake wa kijini , nishati ya mbinu na ardhi ya andiko la urejesho wa azimio ili uzingira mwili wake na kutengeneza kinga na mara baada ya shoti zile za radi kugusana na mwili wake ulitokea mlipuko ambao ulisambartisha nguvu ile ya radi.
“Ina,, inawezakanaje..!?”
Mzee huyo jini alijikuta akikosa muda kabisa wa kuchukua hatua , alikuwa amechelewa kuepuka na alijikuta akianza kuhema , alijaribu kuzungusha mkanda wake ule wa kimjeledi ili kumrushia Roma boriti za shoti ya radi.
Roma aliangalia shoti hizo ambazo zinamsogelea zikiwa katika rangi ya bluu na alitoa tabasamu la kejeli na palepale alijiambia sio mbaya angalau alikuwa akitafuta sura yenye cheo ili kuweza kumtafuta Rufi ndani ya makao makuu hayo bila kushitukiwa na amejileta mwenyewe.
Dakika ileile alikiita chungu cha maafa na kikatokea na kuanza kumeza zile shoti zote za radi na palepale nguvu ya mnyama ilitengeneza nguvu ya kani mvutano na kuushikilia mwili wa jini Lao.
Jini Lao alijikuta akiogopa mno , alijitahidi kujiokoa akimbie lakini alishindwa kabisa , ilikuwa ni kama vile
mtu anavyotumbukia kwenye shimo na hakuna pa kushikilia , alitumia nguvu zake zote za kijini kujishikilia lakini nguvu ya roho ya mnyama ilikuwa kibwa mno.
“Wewe … wewe ni nani?! , hebu niachiliee”Aliongea kwa kutetemeka huku akiwa na hasira mno kiasi cha kufanya uso wake kuwa mwekundu , katika maisha yake hakuwahi kutoa kilio cha kuomba kuachiliwa kama hivyo kwa miaka yote mia moja.
Roma hakutaka kujisumbua sana na aliangalia walinzi
ambao ameambatana nao kumfukuzia na walionyesha dalili za kutaka kukimbia na Roma hakutaka kuwapa nafasi na palepale aliachilia moto wa rangi ya Zambarau uliogeuka kama vinyoka na kushambulia majini wote hao ambao walikuwa katika levo ya nafsi na moto , waligeuzwa majivu palepale.
Master Lao mara baada ya kuona tukio hilo palepale alijikuta akikosa ujasiri tena wa kujiokoa , mtu anaepambana nae uwezo wake ulikuwa ni hatari mno na ilimkumbusha paleplae uwezo wa mkuu wao wa miliki jini Anjiu.
Roma mara baada ya kuhakikisha majini wale amewaua na hakuna ijini mwingine karibu hakutaka kumeza jini Lao na chungu chake hivyo alimsogelea karibu zaidi.
“Nadhani nimesikia wakikuita Mtumishi mkuu , nadhani wewe ndio unaefahamika kwa jina la Lao?”Aliongea Roma.
“Kwahio vipi kama ndio mimi , umetoa wapi ujasiri wa kutaka kuingia katika ngome ya miliki ya Xia, kama una akili ni bora ukaniacha niende zangu ,
haijalishi uko vizuri kiasi gani lakini huwezi kumshinda Master wa miliki ya Xia”Aliongea kwa sauti.
“Haha.. unachekesha , yaani ulitaka kuniua halafu unaniambia nikuachie , hivi akili yako imeota kutu kutokana na kuzeeka?, kama unataka kuendelea kuishi , fanya kama ninavyosema , jibu maswali yangu yote kwa uaminifu na nikimaliza nitakuondolea nguvu zako za kijini na kukugeuza paka na kukuacha uende zao , ukikaidi nitakuminya mpaka unabakia hewa”
Alijikuta aking’ata meno yake kwa hasira huku akijaribu kujiondoa katika mvutano wa chungu lakini kila alivyojaribu hakuona namna kabisa ya kujiokoa.
Ijapokuwa alikuwa katika levo ya maji ya barafu lakni Roma alikuwa katika levo ya juu kabisa ya mzunguko kamili wa mapigo tisini na tisa ya radi zambarau na Dhana yake ilikuwa ni ya daraja la juu kabisa ya kihistoria , hakuna jini lolote hata ambalo lipo katika levo ya maji ya upako kuweza kuepuka kama tu halina Dhana ya daraja la juu, hivyo kwa lugha nyepesi kwa Mtumishi Lao hakuwa na uwezo wowote wa kujiokoa.
“Acha kujaribu bahati yako , ninaweza kukua kwa kukunja kidole tu”Aliongea Roma akiwa siriasi.
Master Leo alijiambia hata kama uwezo wake wa kijini ukiondolewa ataweza kuendelea kuishi na anaweza kuwa chini ya uangalizi wa familia ya mkuu wa majini kama kiinua mgongo cha kuwahudumia kwa zaidi ya miaka mia moja , alijiambia hata kama akigeuka paka au kiumbe chochote anayo nafasi ya kujifunza na kurudisha mwili wake na kuendelea na maisha,
“Okey , uliza maswali yako?” Hatimae alikubali.
“Je wakuu wa miliki ya Xia wamemkata Rufi wa miliki ya Kekexil?”
“Huh!?”
Master Lao hakutegemea swali hilo kutoka kwa Roma , alitegemea angekwenda kumuuliza mbinu za mafunzo ya kijini au siri za miliki hio.
“Hilo ndio swali lako , kwanini unamuulizia , umetokea miliki ya Kekexil?”
“Acha kuongea ujinga na jibu maswali yangu , Rufi yupo wapi , na anaendeleaje?”Aliongea Roma kwa mara ya pili na palepale jini Lao aliingiwa na wazo na kutoa tabasamu la kifedhuli.
“Ndio unajaribu kumuokoa Rufi , hehe.. kama unataka kumuokoa usije kunigusa maana atakufa kwa uhakika”
Lao alijiambia angekuwa juu zaidi kama angemtumia Rufi kumtishia Roma lakini asichokijua Roma alikuwa mjanja tena zaidi ya neno lenyewe na alikasirika sana baada ya kuona jini huyo anamtishia maisha kwa kutumia mtu mwingine.
Palepale aliondoa kile chungu na kisha akamkaba shingo jini Lao kwa nguvu na kuachia nguvu ya kijini ya daraja la juu zaidi .
“Pumbavu zako , unathubutu vipi kunitishia , unafikiri mimi ni mtoto wa miaka mitatu kwamba ni rahisi kunidanganya?”
Msisimko wa kimauaji ambao ulikuwa ukimtoka
Roma ulibadilisha hali ya hewa na kumpelekea jini Lao kuhisi ubaridi , kidogo tu ajikojolee , kwenye maisha yake hakuwahi kukutana na adui amezingirwa na nguvu ya vifo kama Roma , nguvu hio mara nyingi hutokana na mtu ambaye ameua sana zaidi ya maelfu ya watu.
Kabla hajaomba hata msamaha kwa kumchokoza Roma alijishutikia mkono wake ukichomolewa begani na kufanya damu nyingi zimtoke.
Roma hakuishia kwenye kunyofoa mkono wake tu kwani palepale aliruhusu na nguvu ya moto kumtoka na kuanza kumuunguza jini Lao.
“Arhggggg…!!!”
Baada ya kuona mkono wake umenyofolewa macho yake yalijawa na ukali huku akiendelea kupiga yowe la maumivu.
“Nitakuuliza kwa mara nyingine , Rufi yupo wapi?”Aliongea Roma huku awamu hio sauti yake ikibadilika na kuwa nzito mno.
“Yupo … yupo katika chumba cha stoo kwenye jengo la kutengenezea vidonge.. bado yupo hai?”
“Jengo la kutengenezea vidonge ndio lipi?”
“Lipo kusini kutoka Jumba la Jade , ni jengo lenye ghorofa tatu kwenda juu , kuna alama za kimaandishi katika jengo hilo hivyo itakuwa rahisi kugundua , yupo chumba floor ya tatu”
“Wewe unaweza kwenda bila shida , je kuna vizuizi vyovyote kuinga katika jumba hilo la utengenezaji wa vidonge , kuna walinzi wangapi?”
“Mimi kama Mtumishi mkuu wa Jumba la mkuu wa miliki ninaweza kuingia na kutoka nitakavyo , walinzi wataondoa safu ya ulinzi na unachotakiwa kufanya ni kuwaambia wakufungulie mlango , ndani kuna mzee mmoja tu ambaye anahusika kutengeneza vidonge na hakuna mwingine zaidi”
Lao alionekana kushika adabu na kujibu kila maswali , alijua kabisa uwezo wake ungeondolewa lakini hakutaka kupoteza kiungo kingine cha mwili wake.
“Umejibu vyema , swali lingine la mwisho ni majini wangapi ambao wapo levo ya maji ya upako au zaidi ndani ya miliki ya Xia?”
Roma alikuwa na wasiwasi na jambo hilo , kama kutakuwa na zaidi ya watano basi atapaswa kuwa makini zaidi na zaidi na pia ingekuwa ngumu zaidi katika kumuokoa Rufi.
Kwani hata kama atamtoa kwenye chumba hicho basi atapaswa kumlinda huku wakati huo akitafuta njia ya kuondoka , Chungu cha kijini bado hakikuwa katika uwezo wake wote hivyo asingeweza kuwashambulia wote kwa pamoja halafu wakati huo akimpa ulinzi Rufi.
“Kuna wazee watatu , Mkuu wetu namba moja Mzee
Anjiu , Mkuu wetu namba mbili Master Zianji na Guru Mzee Laofi”
Roma alifurahi na kuona hakutakuwa na hatari kubwa
.
“Nimejibu maswali yako yote naomba uyarehemu maisha yangu tafadhali”Aliongea kwa kubembeleza na Roma hakuuliza maswali mengi zaidi.
“Yaani nikuachie , nadhani umekua kipofi kwa kuishi muda mrefu , hivi unafikiri muwindaji anaweza kuachia kitoweo kichague kufa au kuishi?” “Muongo mkubwa wewe’Aliongea kwa hasira .
“Crack!!!”
Roma kwa kutumia nguvu ya kijini palepale aliivunja shingo yake na Lao kupoteza maisha palepale na hakupata hata nafasi ya kumjua Roma ni nani haswa.
Roma baada ya kufanya muaji alitoa pete yake ya hifadhi na kisha akavaa mavazi yake na kuchukua Dhana yake ya Ngurumo , baada ya kuangalia hifadhi yake aliweza kuona baadhi ya vitu ambavo ni kama zawadi kutoka kwa miliki hio na hakujua matumizi yake hivyo aliachana navyo.
Kulikuwa na kifaa kimoja tu ambacho aliweza kukishangaa , ni chupa ndogo ambayo ndani yake ilikuwa na kimiminika cha rangi ya damu ya mzee na hakikuwa na harufu , Roma alitumia nguvu ya kijini ya utambuzi na aliweza kugundua kina nguvu kubwa ya giza.
Aliona pengine sio kitu kiziuri hivyo alifunika mfuniko wake na kisha akatupia kwenye hifadhi yake bila maswali mengi.
Baada ya kuunguza maiti yake na kuwa majivu alibadilisha muonekano wake na kisha uwezo wake wa kijini kwenda levo ya maji na kisha alianza safari ya kurudi makao makuu kama Mtumishi Lao.
Safari yake ya kurudi haikuwa na shida kubwa kwani alikuwa akitumia sura ya Master Lao ambaye anacheo kikubwa tu ndani ya makazi hayo makuu ya miliki.
Walinzi mara baada ya kumuona hawakuonyesha tofauti yoyote zaidi ya heshima na walimwita mtumishi kiongozi.
Upana wa makao makuu hayo ulikuwa ni mkubwa mno kiasi kwamba ni ngumu kujua wale walinzi waliondoka hawajarudi.
Roma mara baada ya kuzunguka zunguka ndani ya makazi hayo ya majiini hatimae aliweza kufika mbele ya jengo ambalo lina alama juu ya jengo la kutengenezea vidonge.
Alitumia uwezo wake kuchunguza eneo hilo na hatimae aliweza kupata uwepo wa Rufi ndani ya jengo hilo lakini hata hivyo alijua hatakiwi kuzembea hususani katika wakati huo muhimu , alijifanyisha kuwa na utulivu na kwa kujiamni alianza kutembea kuusogelea mlango.
Majini walinzi ambao walikuwa na muonekano wa kizee walikuwa wamesimama mlangoni , wote wakiwa katika levo ya maji yya upako , nywele zao wote zilikuwa nyeupe , ijapokuwa walipewa vyeo vya wazee wa miliki lakini walimpa heshima Mtumishi Lao. “Jambo gani limekuleta katika jengo la utengenezaji wa vidonge Mtumishi usiku usiku , je Mkuu wetu kuna chochote anachotaka?”Aliuliza mmoja huku akiwa na uso uliojaa bashasha.
Roma hakuwa na uvumilivu hata kidogo na kujiambia kwanini wasifungue tu mlango , maswali mengi ya nini, lakini hata hivyo aliamua kujibu.
“Ndio”

SEHEMU YA 716.
“Kuwa mtumishi hakika ni kazi yenye ubize sana , sio tu kwamba unapaswa kuongoza wafanyakazi ndani ya makao makuu lakini vilevile unapaswa kumhudumia mkuu wetu”Aliongea yule mwingine.
Roma aliona ni kama vile wanamchawia na aliishia kutoa pumzi ya ahueni na kisha akatoa tabasamu.
“Nina timiza wajibu wangu tu kama Mtumishi, kwenu nyie marafiki zangu naombeni mnifungulie mlango”
“Oh bila shaka tusamehe kwa kukuchelewesha Mtumishi”Waliomba radhi na kisha waliondoa kizuizi katika mlango kwa kutumia nguvu zao za kijini na palepale mlango wenyewe bila kuguswa ulifunguka.
Roma mara baada ya kuingia katika chumba kikubwa cha kwanza alikuwa akihisi nguvu kubwa ya kiroho katika hewa.
Sakafu yake yoto na kuta mpaka madirisha madini ya Jade ndio yametumika katika ujenzi ili kuzuia nguvu za kiroho kutoka nje, katika floo ya kwanza tu kulikuwa na rundo la mimea na viungo vingi ambavyo vilipangiliwa katika mtiririko wa kueleweka.
Lakini kwa kulinganisha Jumba jeupe la miliki ya Kekexil na miliki hio haikuwa na hazina kubwa ya madawa.
Kwa mfano tu katika lile Jumba Jeupe kulikuwa na floor tano zote ambazo zimetumika katika kuhifadhia mimea ya kimadawa, likija swala la aina , kiasi , ubora na uadimu wa mimea na vidonge Xia hawapandi hata kidogo kwa Kekexil.
Ilionekana kila miliki ilikuwa na aina yake ya utajiri kwa ajili ya kuishi , miliki ya Kekexil ilisifika kwa kuwa na madawa lakini miliki hio ilisifika kwa kuwa na utajiri wa madini ya jade .
Ukweli ni kwamba Roma alijua hata kama aliwaibia Kekexil ingewachukua tu angalau mwaka kurudisha kila kitu sawa.
Muda huo ndani ya floo hio wazee wawili walikuwa wapo makini wakitengeneza vidonge kwa kutumia moto wa rangi ya njano na nyekundu , lakini pia kulikuwa na vijakazi ambao walikuwa wakipangilia mimea na viungo.
Mara baada ya kumuona Roma majini hao waliinamisha vichwa vyao kuonyesha heshima , ilionekana Master Lao sio tu kuwa maaruf lakini alikuwa na cheo kikubwa ndani ya makao makuu ya miliki hio zaidi ya utumishi.
Kwasababu Roma hamu yake ni kumuona Rufi hakutaka kabisa kuongea nao sana na alifuatisha ngazi kuanza kuelekea juu , lakini dakika hio hio aliweza kushuhudia mwanamke wa kijini akitokea juu kuja chini akiwa ameambatana na mzee mwingine ambaye alikuwa amevalia mavazi kama vile ni Monk.
“Niwie radhi sana sana , sio kama nakuwa mkatili lakini kuna awamu ya kwanza tu ambayo imekamilika ya vidonge vya daraja la juu na tayari nishavitawanya kwa watu muhimu ndani ya familia kulingana na maagizo ya Lodi mkuu mwenyewe , kama awamu nyingine ikikamilika ninakuahidi wewe utakuwa ni wa kwanza , mimi ni mwanaume wa vitendo”
“Oh ,.., haina haja ya kuwa siraisi hivyo Cheluni , ninataka vidonge hivyo kwa ajili ya kijana wangu Lahani , sina uelewa mume wangu anafikiria nini kwa kutompatia mtoto wake vidonge vya daraja la juu
wakati anajua anatarajia kufikia levo ya maji meupe”Aliongea yule mwanamke akionyesha huzuni.
“Hakika unampenda sana kijana wako , nimevutiwa lakini nadhani mkuu wetu anatamani kuona Lahani anapita levo hio kwa nguvu zake mwenyewe kwasababu mwanzoni amemeza vidonge vingi , kama ataendelea kutegemea vidonge kupanda levo itamletea madhara huko mbeleni na atapata tabu kwenye kupanda levo za juu zaidi kutokakna na msingi wake ktuokuwa imara”Waliendelea kuongea na dakika hio hio waliweza kufika katika floor ya chini.
“Oh … Mtumishi nakuoa upo hapa , kuna maagizo yoyote kutoka kwa Mkuu wetu?”Aliuliza jini aliefahamika kwa jina la Cheluni.
Roma alikuwa na wasiwasi na kwa bahati nzuri alikuwa ashasikia majina yao vinginevyo asingewafahamu ni wakina nani.
Mwanaume huyo alifahamika kwa jina la Cheluni na alikuwa ndio anaesimamia jengo hilo na alikuwa kwenye levo ya maji ya barafu na inawezekana akawa ndio mwenye nguvu zaidi ukiachana na wale ambao wapo tayari katika maji ya upako.
Kuhusu huyo mwanamke mrembo alikuwa ni mke wa Mkuu wa miliki hio Lodi Anjiu na kwa maelezo ya Sui ilikuwa sahihi kabisa alikuwa mwishoni mwa levo ya maji meupe.
“Mzee Chuleni nimekuja kuchukua vidonge kwa ajili ya mkuu wangu”
“Kumbe , basi mimi ndio namsindikiza mke wa mkuu wetu na nitakufuata kuchukua vdonge , subiri kidogo Mtumishi”
Roma alitingisha kichwa chake huku akitamani waondoke tu , lakini kwasababu ameambiwa asubiri hakuona haja ya kwenda juu peke yake kwani angehatarisha misheni yake.
Muda uleule mara baada ya mke wa Anjiu , bibie Anjiu Leiana kumpita, Roma aliweza kunusa harufu yake ya marashi na yalikuwa yakifurahisha pua mno.
Kilichomshangaza zaidi Roma ni kwamba mrembo huyo mara baada ya kukutananisha nae macho alimkonyeza na ilikuwa ni wazi kabisa alikuwa akijilengesha.
Ijapokuwa ilitokea ndani ya sekunde tu wakati wengine hawajaona lakini Roma hakuamni kile kilichotokea , alikuwa katika sura ya Mtumishi wa makazi hayo na alijiuliza inawezekana vipi mke wa bosi mkuu wa miliki hio kumtega mtumishi au wana mambo yao ya siri yaliokuwa yakiendelea.
Roma aliishia kukunja sura na hakutaka kujisumbua sana alichokuwa akipaswa kufanya hapo ni kumtamfuta Rufi na sio vinginevyo na kisha kuondoka.
Jini Cheluni mara baada ya kumtoa nje Jini Leiana alirudi ndani kwa haraka na kisha alichukuana na Roma mpaka floor ya pili .
Roma mara baada ya kufika katika floor hio aliweza kuona vidonge vingi ambavyo vilikuwa vimepikwa na kuhifadhiwa katika shelfu , kulikuwa pia na majini wa levo ya maji barafu waliokuwa wakilinda katika kila kona , ki ufupi ni eneo ambalo lilikuwa na ulinzi mkali sana.
Roma palepale alijua mtumishi Lao alimdaganya , maana alidhania ni kweli hakuna walinzi lakini eneo hilo ulinzi wake sio wa kawaida na alijua kama atamtoa Rufi lazima agesababisha vurugu kubwa mno , kutokana na wingi wao alijua angepoteza muda kupambana nao mpaka muda ambao majini wa levo ya maji ya upako watakapo fika.
“Mtumishi naweza kujua ni vidonge gani unahitaji kwa ajili ya mkuu wetu?”
“Oh .. Master anahitaji vidonge Washa kumi”
“Vidonge washa kumi!! , hivi si kwa ajili ya mapambano ya ana kwa ana , au anawapatia wanajeshi wetu wanaondoka?”
“Master hakuniambia ni kwa ajili ya nini lakini ninadhani ni kwa ajili hio”
Cheluni alikuwa akiuliza tu kwa ajili ya shauku na sio kwamba hakuwa akimwamini Mtumishi , muda ule alimchukua Roma mpaka katikati ya chumba na kulikuwa na jiwe kubwa ambalo limekaa kama meza na mara baada ya kuorodhesha vidonge ambavyo Roma alihitaji alimwambia asaini.
Roma hakutegemea utaratibu huo , ilionekana walifanya hivyo ili kuzuia majini wasichukue vidonge bila utaratibu maalumu.
Ilikuwa bahati kwa Roma aliweza kuona sahihi ya Lao pembenni yake na aliigizia vilevile ilivyo kwa kutumia nguvu za kijini hivyo hakushitukiwa
Baada ya utaratibu ule alitoa kichupa cha rangi ya kijani ambacho ndani yake kuna vidonge nane vya Washa na kisha kumpatia Roma.
“Tushamalizana Mtumishi , tuondoke sasa”Aliongea huku akimpa ishara lakini Roma palepale alisimama akuonyesha hajamaliza..
“Mzee Cheluni kuna jambo lingine kuhusiana na msichana ambae yupo floor ya tatu?”
“Msichana ambae yupo floor ya tatu … unamzungumzia Rufi mfungwa wetu?” “Ndio , Mkuu kaniambia nimpeleke pia ana maswali anataka kumuuliza”Aliongea Roma na kumfanya Cheluni kuonyesha mshangao.
“Rufi tayari amekwisha kukabidhiwa kwa baraza la wazee na yalikuwa ni maamuzi yake , ashaanza kutumika tayari katika majaribio ya vidonge kwanini anamuhitaji tena , si tulimuuliza maswali yetu yote?”
Roma alijikuta akipandwa na jazba na kauli hio , ilionekana walimtesa Rufi katika kumuuliza maswali na hali hio ilimtia mashaka atakuwa katika hali gani.
“Imekuwa ngumu kujua sababu ya maagizo ambayo nimepewa na mkuu wetu , mmi natii tu maagizo yake kwa kumpeleka”
Cheluni palepale alionyesha ishara za wasiwasi juu ya Roma kwani hakuwa mjinga , alijua namna ambavyo Lao mtumishi anavyoongea ni tofauti kabisa siku hio lakini hakuweza kuona nini tatizo kwani alikuwa ni yeye
“Unaweza kumtoa hapa kwa kupata kibali kutoka kwa wazee wenyewe au upate ruhusa kutoka kwa Guru Laofi , mimi Cheluni sijawahi kufanya makosa katika kulinda hili eneo , sitaki kuingia katika historia kwa kuwa wa kwanza kukiuka sheria , Rufi ana thamani kubwa kwa miliki yetu na nina vidonge bado vya kufanyia majaribio nione ukali wa sumu yake , siwezi kumruhusu kirahisi kuondoka ndani ya jengo hili nitapata wakati mgumu kutoa maelezo mbele ya baraza la wazee”
Roma alikuwa na hasira alijua vyema asingeweza kuharakisha kwenda juu bila ya kujua hali yake Rufi , pengine anaweza kumuingiza katika hatari zaidi kama atakurupuka.
“Unaonaje tukifanya hivi , sitoondoka nae lakini
utanipeleka na nimuulize maswali machache tu na kumuacha?”
Dakika hio hio ambayo Roma alitamka kauli hio alijutia palepale kwani ilimfanya Cheluni kuzidi kuwa na wasiwasi.
“Mtumishi , Rufi ni mfungwa na yupo chini ya baraza la wazee ,Mkuu wetu na wewe pia mnaelewa hili , unaonekana kutaka sana kuonana nae , ni maagizo ya mkuu kweli?”
“Mzee Cheluni unamaanisha nini? , ninachofanya ni kumpunguzia mkuu wangu mzigo , ila kwasababu unanikataza kwenda basi nitaenda kuchukua kibali kutoka kwa mkuu mwenyewe”
Cheluni alimwangalia Roma machoni kama vile kuna kitu ambacho anatafuta lakini Roma hakuonyesha hali ya hofu na wote waliangaliana usoni.
Mwishowe Cheluni hakuona tofauti yoyote kutoka kwa Roma , mwanzoni alijua labda mtu aliekuwa mbele yake sio Mtumishi kutokana na makosa ya wazi anayoyafanya lakini alionyesha kuridhika.
“Kama ni hivyo Mtumishi nenda kalete kwanza kibali cha maandishi na nitakupatia huyo mwanamke , sio tu wewe hata mtoto wa Mkuu na mke wake hawawezi kumtoa humu bila ruhusa”
Bwana huyo alionekana kuwa imara kwenye msimamo wake na yote hayo ni kwasababu Lao Mtumishi alikuwa akichukuliwa ni kijakazi licha ya cheo chake.
Lao hakuwa mrithi wa moja kwa moja katika familia ya wakuu wa miliki na hakukuwa na uwezekano wa kulazimisha kufanya kitu.
Roma mara baada ya kukataliwa alijikuta akizidi kuwa na wasiwasi na alitamani kuharibu jengo zima lakini alijua akikurupuka kimaamuzi itamuweka Rufi katika hali mbaya, ilikuwa ni bahati kwake tu kwamba Rufi alikuwa hai mpaka wakati huo.
“Rufi naahidi nitakutoa ndani ya hili eneo mapema tu , naomba uvumilie kwa muda mfupi”Aliwaza Roma akikodolea macho jengo hilo na kisha akaondoka.
Roma hakutaka kuendelea kujifanyisha ni Lao Mtumishi tena kwani angegundulika muda si mrefu , katika akili yake alikuwa akikumbuka maneno ya Cheluni kwamba Guru Laofi ndio ambaye ana uwezo wa kumchukua Rufi bila hata ya ruhusa , hivyo wazo lake mara moja lilimwingia akilini , aliona kitu pekee cha kufanya ni kumuua huyo Laofi na kisha kuchukua uhusika wake , ijapokuwa ingekuwa ngumu kutokana na kwamba yupo katikati mwa levo ya maji ya upako lakini alijiambia atajitahidi kwani ndio njia pekee ya rahisi.
Baada ya mpango huo Roma alianza kuulizia wapi alipo Master Laofi ili tu kumdanganya na kumpeleka eneo la mbali na kisha kumuua.
Wazo hilo lilikuwa kichaa kutokana na uwezo wa Laofi lakini kwa Roma ni wazo la kawaida , kwake yeye mtu ambaye anawazia sana matokeo hawezi kufanikiwa kwenye maisha yake.
Dakika chache mara baada ya Roma kukata kona aligundua kuna anaemfatilia kwa nyuma na hio ni mara baada ya kunusa harufu ya marashi.
Majini wanakuwa na marashi ambayo sio ya kawaida kabisa hasa majini wakike na Roma pua zake ziliweza kunasa harufu hio na dakika hio hio aliweza kusikia sauti nyororo ikimwita.
“Unaenda wapi Mtumishi Lao?”
Mrembo jini Leiana alitokezea mbele ya Roma , alikuwa ni mweupe sana na midomo myekundu kama vile inavuja damu huku macho yake yakiwa ni yale ya kuita.
Mwanaume wa kawaida hawezi kuhimili mvuto wa mwanamke huyo , isitoshe hata hivyo sio wa kawaida lakini kwa Roma kutokana na kuwa na nguvu za kijini alikuwa vizuri kwenye kuhimili mvuto wake.
Licha ya kwamba Roma hakujua uhusiano uliokuwepo kati ya Mtumishi Lao na Leiana kutokana na uzoefu wake alijua tu lazima kuna mahusiano ya siri yanaendelea.
“Madam , siendi popote , je kuna maagizo yoyote unataka kunipatia?”Aliongea Roma kwa heshima na kauli yake ile iliamsha kicheko cha nguvu kutoka kwa Leiana na kisha alimsogelea karibu Roma na kuanza kugusa kifua chake na vidole vyake kama vile anatafuta uvimbe.
“Acha woga basi , hakuna mtu anaetuona hapa , nadhani ulinielewa nilivyokukonyeza nilimaanisha nakusubiria nje au mpango wako ni kunipotezea siku hizi?”
“Ni kwamba…”Roma alijikuta akishikwa na mshangao na alijiambia kinachokwenda kutokea ni usumbufu , ilionekana huyo mzee aliechukua sura yake licha ya kuonekana mtiifu lakini alikuwa ni muhuni.
Kwa Leiana alionekana yupo tayari kwa ajili ya kufanya ngono na mpenzi wake wa siri lakini upande wa Roma hakuwa na mudi ya kufanya mapenzi na jini kwa mara ya pili..
“Bibie ,,, ninapaswa kupeleka kwanza vidonge kwa mkuu wangu”Aliongea Roma akitafuta namna ya kumkimbia lakini kauli yake ilimfanya Leiana kukasirika kiasi cha kusambaza nguvu za kijini.
“Pumbavu zako unaweza kumdanganya Cheluni lakini sio mimi , Anjiu amejifungia kwa siku nyingi akiendelea na mafunzo na hajawahi kutoka nje anakuagiza vipi vidonge , hii sio mara yako ya kwanza kutumia janja ya aina moja kuiba vidonge , hebu acha maigizo tayari upo kwenye kundi moja na sisi na huwezi kukimbia , usiniambie unataka kunipotezea sasa hivi na kuendelea kuwa mbwa wa familia, kama kweli wewe ni mtiifu na mwaminifu kwanini ukakubali kufanya mapenzi na mimi nilivyokutega ile siku , unataka nimwambie Laofi uongo wako akakusemee , naamini utakufa kabla hata hujajielezea”Aliongea maneno mengi akionekana kukasirika.
Roma alijiuta akishangaa na palepale akili yake ilicheza , ashajua Laofi , marehemu Lao Mtumishi , Leiana na pengine Zianji wote ni kundi moja.
Anjiu ndio sehemu ya master kumi mwenye nguvu katika miliki yote ya kijini lakini nani angeamini kama familia yake yote inamsaliti.
Kutokana na meneno ya Leiana Roma aliona ni ngumu kumkataa kwa nguvu kwani hakuwa na sababu na juhudi zake zote hizo alizofanya zingekuwa bure.
“Bibie acha zako , najua nini cha kufanya”Aliongea Roma
“Mhmh … bora unajua “Aliongea huku akiweka uso wake kama vile anatia huruma , uwezo wake wa kubadilika kihisia ulikuwa mkubwa mno kuliko hata spidi ya kufunua kurasa ya kitabu , alikua na kila sifa mara awe kama vile ni mtoto wa darasa la saba , mara awe mtu mzima , muda mwingine awe mama.
“Nilijua unataka kuniacha mara baada ya kuona uchi wangu , hivi unajua ni kwa kiasi gani ningeumia , tafadhari usinifanyie hivyo tena”Aliongea huku akishika sura ya Mtumishi feki kwa kuiparaza kistaarabu kabisa huku akirembua macho yake.
Roma aliishia kumeza mate hakuwa akimtamani licha ya kwamba alikuwa mzuri na hakutegemea tokea mwanzo wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi licha ya kwamba Leiana ni mke wa mkuu wake, Roma alijiambia huku sio ujinini bali ni mitaa ya madanguro.
Hata hivyo Roma aliamini uwezo wake wa kuigiza uhusika wa mtu mwingine na mara baada ya kuthibitisha hakuna anaewaangalia palepale alimshika mrembo Leiana kiuno na kutokana na gauni lake kuwa jepesi alikuwa akihisi ulaini wa ngozi yake.
“Hehe … hatimae mtumishi amegeuka mtundu”Aliongea huku akipiga kibao mkono wa Roma kimahaba.
“Wewe mkorofi hapa sio mahali salama , hebu twende kwenye Banda la Wingumbingu, nina kazi siriasi na wewe usiku huu”
Roma alijiuliza Banda la Wingumbingu ndio wapi , hakuwa na uelewa maana ni mgeni na alijifanyisha tu kwamba anaelewa eneo hilo.
“Hakuna tatizo mrembo wangu , wewe tangulia na
nitakufuatisha”Aliongea
“Unajifanya upo makini , unajua tunapaswa kwenda kila mtu kivyake lakini kwa leo haina haja maana Anjiu amejifungia kuendelea kuvuna nishati , hana muda wa kutusumbua”Aliongea na palepale alipaa kuelekea upande wa mashariki.
Roma alifuata nyuma nyuma kwa spidi ya kawaida na ilikuwa ngumu kuonekana kwani kulikuwa na giza.
Haikupita hata nusu dakika waliweza kufika eneo ambalo ndio kuna banda linaloitwa Wingumbingu.
Ni kama Gazebo mtindo wa nyumba iliojengwa kwa kutumia mianzi katikati ya bwawa , usanifu wake ulikuwa ni ule wa kawaida na kuzunguka eneo hilo kulikuwa na maua mengi sana ya kupendeza ilionyesha dhahiri ni eneo la mapumziko..
Ilikuwa ni sawa kuwepo kwa maneno kama hayo , isitoshe ulimwengu wa kijini una eneo kubwa kuliko wakazi wake.
Mara baada ya kuingia ndani , Leiana alimrukia Roma na kuanza kubusu lipsi zake kwa pupa bila ya kujali ndevu za Lao mtumishi.
Baada ya kuanza shambulizi kwa kuweka ulimi wake ndani ya midomo ya Roma alianza kutoa miguno ya kimahaba na kumfanya Roma kuona majini wana hisia kali kuliko hata binadamu kwani mara ya mwisho wakati akiwa na jini Manyani hata yeye ndio alienzisha mashamblizi.
Roma alijiambia leo tena ameletwa eneo hilo kwa nguvu kwa ajili ya kufanyishwa ngono na jini lenye umri zaidi ya miaka mia , alijiambia au ni kwamba Mungu anaelewa hobi yake sana ndio maana anajitahidi kumbariki.
Lakini Roma akili yake ilikuwa ikimuwaza Rufi tu kwa wakati huo , ijapokuwa Leiana alikuwa mrembo lakini hakuwa tayari kufanya nae chochote.
Muda huo Roma aligundua eneo hilo ni mbali kutoka makazi na kama angeamua kumuua huyo mwanamke katika eneo hilo basi ingekuwa ni rahisi bila hata ya kushitukiwa na kisha kwenda kumtafuta Laofi.
Dakika hio hio wakati akiwaza hatua ya pili ya kuchukua , Leiana aliacha kile alichokifanya na kuanza kulamba lipsi za Roma.
“Wewe mtukutu tutatulia kwanza kwasasa , watafika muda si mrefu , nitakuhudumia baada ya biashara yetu kuisha”
Maneno hayo yalimfanya Roma kushangaa ndani kwa ndani , na kujiambia inamaana kuna wengine wanaokuja ndani ya eneo hilo na ndio maana akasema kuna biashara ya siriasi , lakini alijisikia vizuri na alitamani Laofi ndio awe anafika bila kukosa ili mpango wake uwe mwepesi.

SEHEMU YA 717.
Hazikupita dakika hata mbili tayari Roma alihisi ongezeko la nguvu za kijini katika eneo hilo na mkandamizo wao ulimfanya kujua mmoja wapo alikuwa katika levo ya maji ya upako katikati na mwingine alikuwa mwanzoni pia mwa levo ya maji ya upako.
Ilikuwa ni kama alivyotamani iwe , kwani jini mwenye maringo Laofi alievalia joho staili ya wachina wanapofunga ndoa maarfu kwa jina la Chanqsan , alikuwa ametangulizana na Zianji ambaye yeye alivalia joho staili ya kanzu nyeupe iliofungwa na mshipi kiunoni kama Shemasi.
Roma alianza kusitasita , na kujiambia majini wa levo ya maji ya upako kwa wakati mmoja ndio wamefika , umbali kati ya eneo hilo na ngome ya familia ya mkuu wa majini ni karibu sana.
“Kama nitapigana nao hapa sidhani kama nitawaua mara moja , vipi kama mmoja akipigana na mimi na mwingine kukimbia kuomba msaada nitakuwa nimekwisha , nadhani sina jinsi zaidi ya kusubiri na kutafuta nafasi ya kumtoa jini Laofi ndani ya hili eneo kwenda mbali na kisha kumuua”Aliwaza Roma.
“Hahaha… nadhani tumekuja muda mbaya na kuharibu mnachokifanya na Mtumishi wetu”Aliongea Laofi huku akiingia kwenye kijumba hicho.
Leiana alitoa tabasamu murua na palepale alijirusha na kwenda kutua kwenye kifua cha Mzee Guru Laofi na kujikunja kama vile hana mfupa.
“Ndio kwamba Mzee Guru umeshikwa na wivu?”
“Vipi kama nikisema ndio , utakuwa na furaha?”Aliongea huku akitoa tabasamu la kifedhuli huku utukutu ukijioneysha kupitia macho yake na palepale alipeleka mkono wake na kuanza kuminya maembe dodo ya Leiana.
Upande wa Zianji mara baada ya kuingia ndani ya eneo hilo hakuonyesha mshangao ni kama vile hakuwa akijali kinachoendelea.
Yaani alivyomwangalia shemeni yake ni kama vile anaangalia mwanamke kahaba.
Roma kila kilichokuwa kikiendelea hapo ndani hakujua acheke au alie , ilionekana Zianji sio tu kwamba Laofi alikuwa chini yake lakini pia Mtumishi marehemu alikuwa chini yake kutokana na kuwatunzia siri.
Sasa Roma alijiuliza imekuwaje Anjiu jini mkuu wa miliki ya Xia kushindwa kuelewa kinacheondelea au ni kwamba wapo vizuri katika kuigiza au alikuwa bize sana na maswala ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi.
“Vizuri hebu tuingieni kwenye maswala ya siriasi ya biashara zetu kwanza na baada ya hapo nitamla huyu horny b**tch”aliongea Laofi na kisha akamwachia Leiana na kumgeukia Roma.
“Mtumishi maendeleo yanakwendaje kuhusiana na kazi tuliokupatia?”
Roma alijikuta akichanganyikiwa , kazi!, Kazi gani hio hakujua ni kazi gani na aliishia kuonyesha utulivu tu.
“Imekamilika”Aliongea.
Ukweli ni kwamba kuigiza katika mazingira hatarishi kama hayo ilikuwa ni ujasiri usiokuwa wa kawaida.
Jini Laofi na jini Zianji wote walionyesha mshangao na kisha kuangaliana mara baada ya kusikia jibu la Roma huku wasiwasi ukionekana kwenye nyuso zao.
“Umemaliza!!? , usituambie umemaliza kutumia damu yote ya mnyama wa kishetani , si nilikueleza mapema kwamba licha ya kwamba ina nguvu kubwa itahitajika siku au mwezi katika kujikusanya mwilini, bila ya kuitumia kidogo kidogo kwa miaka miwili mfululizo haiwezi kuleta athari kwa jini mwenye nguvu kama Anjiu, nilikuelekeza unatakiwa kutumia tone tu la damu ili kuzuia harufu yake , kiasi cha damu tulichokupatia ni kwa matumizi ya miezi mwili mitatu hivi kwanini umeharakisha kuimaliza yote , vipi kama Anjiu akigundua tunamuwekea , juhudi zote zitakwenda na maji”
“Damu ya mnyama wa kishetani!!!?”Swali lilijitokeza katika kichwa cha Roma na palepale alikumbuka maongezi yao kule msituni, alikumbuka pia kimiminika cha damu ya mzee alichokiona katika hifadhi ya Mtumishi Lao.
“Kwahio hio damu ya mnyama wa kishetani kapewa mtumishi Lao kwa ajili ya kumuwekea Anjiu kutokana na ukaribu wao , ni kwamba tu sijui athari zake zikoje”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake.
Roma palepale alibadilisha muonekano wake ili kuonyesha kama alikuwa akitania.
“Msiwe na wasiwasi , nilichokuwa nikimaanisha ni kwamba kazi inaenda vizuri”
Mara baada ya kuongea kauli ile wote watatu walionyesha kuwa na ahueni na Laofi alimsogelea Roma na kumpiga piga begani.
“Endelea kufanya kazi nzuri Mtumishi , tunajua ni ngumu kufanya hila mbele ya Anjiu lakini ndio nafasi yetu ya pekee kummaliza , tunakiasi kidogo tu cha hio damu kutoka Kekexil , ilisemekana ni ya miaka mingi iliopita hivyo inawezekana hiko ndio kiasi kidogo cha mwisho kilichobakia , unatakiwa kuitumia vizuri na mara baada ya Anjiu kutawaliwa na hio damu tutapambana nae na wakati huo tutaweza kumuondoa madarakani , Wewe mtumishi hatimae utaachana na kazi yako ya ukijakazi na kuwa moja ya wazee wanaoheshimika , kizazi chako kijacho hakitakuwa cha vijakazi bali kizazi tukufu”
Kwa haraka haraka masharti hayo yalionekana kweli kuleta tamaa lakini hata hivyo Roma alijua kilichomfanya Mtumishi Lao kumsaliti bosi wake ni kwasababu ya mtego aliowekewa na Leiana , mtego
wa kimapenzi la sivyo asingeweza kumsaliti , mwanamke huyo alikuwa mrembo sana wa kumpagawisha kila mwanaume wa kijini.
“Asantte kwa uungwana wako Guru Mzee , ni heshima kwangu”Aliongea Roma na kumfanya Leiana kubetua mdomo.
“Mtumishi hebu fikiria ulimuona Lahani akikuwa hatua kwa hatua tokea alivyotoka Palao na anakuchukulia kama babu yake na mara baada ya Anjiu kufariki Lahani atachukua madaraka , je si na wewe cheo chako moja kwa moja kitapanda?”
Roma alitabasamu na kumwangalia jini huyo , hakushangaa matendo yake kumbe yote hayo anafanya kwa ajili ya kumfanya mtoto wake kuwa na cheo kikubwa , lakini hata kama Lahani atakuwa na cheo moja kwa moja atakuwa kama kiongozi kivuli tu na nyuma ya pazia watakao ongoza miliki hio ni Laofi na Zianjji.
“Ukweli ni kwamba Mtumishi nimekuitia hapa kwa sababu nyingine , ninatamani unisaidie kupata taarifa kwa ajili yangu”Aliongea Laofi.
“Nipe maagizo yako Guru”Aliongea Roma.
“Siku chache zilizopita mara baada ya wewe kwenda kumkamata Rufi pamoja na Lahani huko duniani , Anjiu alimwita kiongozi wa koo ya Wang , jini
Wang Mian hapa makao makuu baada ya hapo Wang Mian alimchukua binti yake na kwenda nae ulimwengu wa kawaida lakini sijui kuna kipi kinaendelea , wala sababu ya kwenda ulimwengu wa kawaida ni ipi”Aliongea Laofi.
Roma alijifanyisha kushangaa pia lakini palepale sasa alikuja kugundua nini kilichotokea.
Kwahio kitendo kile cha kumfanya yeye kwenda kutoa andiko lake la urejesho ulikuwa ni mpango wa Jini Anjiu na mtu aliekutana nae ndio jini aliefahamika kwa jina la Wang Mian.
Roma aliijiuliza kama ni hivyo kwahio kupotea kwa mtoto wa Master wake Magdalena ilimaanisha amerudi huku ujinini , lakini kama walidanganya kwanini alikuwa na kitu ambacho kilimtambbulisha kwa Tang Luyi , yaani kile kidani, lakini pia kwanini amepotea bila ya kuaga, kuna mpango gani unaendelea ndani ya hio miliki mpaka kufanya janja hio ili tu kupata andiko lake.
“Wasiwasi wetu ni kwamba tukio lile linahusiana na binti yake XiaoXiao mtoto wa binadamu mwanamke kutoka ulimwengu wa kawaida , kitu pekee ambacho kinamuunganisha Anjiu na ulimwengu wa kawaida ni binti yake na mwanamke binadamu aliemzalia mtoto , ijapokuwa hadhi yake ni ya chini lakini bado ni mtoto wa Anjiu , likija swala la kurithi kiti cha mfalme na yeye pia anayo nafasi ili mradi tu Anjiu
awe na uthibitisho mama yake alikuwa ni bikra na hana makando makando mengine”
“Kuongezea , baada ya Xiao kurudi kutoka duniani uwezo wake wa kijini uliongezeka kwa kasi mno , nadhani kuna mambo mengi ameweza kjifunza alivyokuwa ulimwengu wa kawaida na kipaji chake ni kizuri na hahitaji kidonge kuweza kuingia levo ya nafsi , tukio hili limewafanya baraza la wazee kumwangalia Xiaoxiao kwa ukaribu zaidi , kama atafanikiwa kupata ufunuo wasiwawasi wetu Gurusi Mkuu lazima atamwangalia kwa jicho lingine na kama Anjiu akifa bado kutakuwa na usumbufu wa nani arithi kutokana na uwepo wake…”Aliongea Leiana kwa kirefu.
Roma alishangaa kidogo alikuwa akikumbuka siku ya kwanza mara baada ya kufanya maongezi na Xiaoxiao chini Tanzania katika fukwe ya Kawe alimwambia alikuwa Tanzania kwa ajili ya kumtafuta mama yake ambaye ni binadamu kutoka Afrika, ukiachana na hayo pia alikuwa na hasira na Xiaoxiao kwa kuamini pengine ndie alivujisha taarifa ya uwepo wa Rufi nchini Tanzania
Kwa haraka haraka aliona pengine XiaoXiao ana kipaji kikubwa cha akili ndio maana uwezo wake unapanda kwa haraka lakini alimshusha vyeo kutokana na tukio la Rufi kutekwa.
“Kama ni hivyo Guru na Master Zianji ni kipi ambacho mnataka nifanye?”
“Ni rahisi sana , tunachotaka kujua ni kitu gani Anjiu amemwambia Wang na binti yake kufanya , wewe ndio mtu wake wa karibu nina uhakika atakuambia kitu , kama utafeli unaweza kutumia cheo chako cha utumishi na kwenda kuongea na kiongozi wa familia ya wang , tunachotaka kujua ni ubini wa mama yake XiaoXiao katika ulimwengu wa kawaida na baada ya hapo ndio tutajua namna ya kudili nae , kama ni mwanamke kicheche tutaachana nae lakini kama ni mwanamke ambaye anacheo huko duniani tutahitajika kufanya kitu”
Roma palepale mawazo yake yalikuwa wazi sasa , kwahio ilimaanisha XiaoXiao mama yake mzazi sio Mwafrika kama alivyoambiwa bali alikuwa ni Master yake Magdalena, Tang Luyi kutoka ngome ya Tang, lakini swali kama ni hivyo vipi kuhusu Wang mian ambaye Tang Luyi alisema ndio mwanaume aliekuwa nae katika mahusiano.
Roma hakuelewa lakini hata hivyo aliona akubaliane na maagizo hayo kwa muda , isitoshe sio kama anaenda kuyafanyia kazi kwani yeye siio mtumishi. “Nimekuelewa nitalifanyia hili kazi nikisharudi”
“Wewe mtukutu haina haja ya kuwa na haraka , nataka kwanza uniahidi utalifanyia hili kazi kwa juhudi zako zote , huyo Chotara ni wa kawaida kuliko dume langu Lahani”Aliongea Leiana huku akiwa mbele ya Roma na kuongea kwa sauti ya kimapozi akitumia mbinu ya ziada kumshawishi Roma mtumishi feki.
Laiti wangelijua mtu wanaeongea nae ni feki , sijui wangelichukuliaje swala hilo, mpaka hapo ilimaanisha Roma alikuwa akijua uchafu wote unaoendelea katika miliki hio.
“Hehe … kwa hali hii nadhani shemeji yangu hawezi kuendelea kuvumilia zaidi”Aliongea Zianji huku akimwangalia Leiana kwa kejeli na kisha alimshikilia na kumrushia kitandani.
“Hey taratibu basi tabia yako kila siku unanifanyia fujo”Aliongea lakini sura yake ilionyesha kuhitaji fujo zenyewe.
Yaani ilionekana wanaume wote watatu walikuwa chini ya himayya yake , anawahonga penzi huku akihakikisha mpango wa kumfanya kijana wake kuwa mrithi unakamilika.
Dakika chache mbele Leiana hakuwa na nguo hata moja mwilini na alipandiwa juu juu na Zianji na kuanza kupelekewa moto , alikuwa na ngozi nyororo mno na kitendo kilichokuwa kikifanyika kilimfanya Roma kuwa na njaa kali.
Lakini hata hivyo alishindwa kuchukua hatua na Laofi ambaye alikuwa pembeni alikuwa akimwangalai kwa wasiwasi.
“Kwanini Mtumishi wetu leo anaonekana kama vile hana mudi”Aliongea Laofi huku akimshika Roma bega.
“Ni kwasababu Master Zianji anaendeleza kazi hivyo sitaki kumwingilia?”Aliongea Roma akijitetea.
“Una matatizo gani wewe leo? , sijawahi kukuona ukiwa na huo upole kwa miaka mitatu yote …. Kwani huyu mwanamke si tunamfanyaga wote watatu kwa pamoja , hebu anza kazi Mtumishi acha mambo yako bwana , unastahili kupata huo utamu , halafu si hobi yako ni kupitia njia ya uwani wewe… sehemu hio ni ya kwako peke yako leo hii haiguswi na mtu”Aliongea Jini Laofi huku akitoa kicheko.
Roma alijikuta akipagwa na kujiuliza kwa mshangao ‘ Njia ya uwani’ , aliona kabisa majini hao walikuwa wanafanana kabisa na binadamu mambo yao.
“Pumbavu inamaana mtumishi Lao yeye alikuwa
akipendelea kumchezea huyo mke wa bosi wake kupitia njia ya uani!!?”
Laofi ambaye alikuwa akitoa kicheko cha furaha alikuwa tayari akisaula na dakika chache mbele alijiunga, staili aliowekwa Leiana ilishangaza pengine bado haijagunduliwa na watenda Dhambi wa dunia kwani licha ya kuingiliwa na watu wawili kwa mpigo lakini njia ya Uwani ilikuwa haijaguswa na kumpa uhuru mtumishi kundelea.s
Leiana mara baada ya kuona upande mwingine hakuna mtu alionyesha kukasirika mno na kumwangalia Roma.
“Wewe mshezi unashangaa shangaa nini , hebu njoo
, inaumiza kusubiri ujue”
Roma alijiambia mwanamke kahaba kama huyo imekuwaje akawa mke wa mkuu wa miliki , Roma licha ya kushangazwa na kitendo hicho lakini hata yeye mwenyewe hakuwahi kuwa mtakatifu na alitoa tabasamu la kifedhuli na kusaula haraka haraka.
“Arghhh… ndugu Mtumishiii… leo yamekuwaje mbona kila kitu chako ni tafauti”Alilalama Leiana mara baada ya ujazo usiokuwa wa kawaida kumwingia.
“Hehe … mambo ya vidonge vya Tinya hayo”Aliongea Roma akijitetea na mwanamke yule aliishia kutingisha kichwa chake tu akionyesha kuridhika.
“Pumbavu zako wewe mshezi, yaani umejipatia vitu vizuri lakini umetuweka gizani”Aliongea Zianji.
Mpambano ambao ulimfanya Roma kujihisi yupo ndotoni ulimalizika ndani ya nusu saa , ukweli ni kwamba Roma alitumia nguvu za kijini kumaliza haraka lakini kwa namna moja ama nyingine hakuchukulia zoezi hilo kama Adhabu , alijipa kisingizio cha kufanya yote hayo kwa ajili ya misheni hivyo ki ufupi ni kwamba aliinjoi.
Mara baada ya kazi kukamilika Leiana alijirusha ziwani na kujishafisha na baada ya hapo kila mtu alirudi katika usiriasi wake kama kawaida na kila mmoja alichukua njia ya kurejea makao makuu .
Roma alifuata nyuma nyuma ya Laofi mpaka ngomeni na mara baada ya Laofi kuachana na Zianji , Roma alizunguka na kwenda kutokea kwa mbele.
Laofi mara baada ya kumuona Roma akija upande wake akiwa na tabasamu alionyesha hali ya kushangaa.
“Kwanini umenifuata mpaka huku , si nilikuambia hatupaswi kukutana mara kwa mara tukiwa wenyewe tu ili kuepuka kushitukiwa kabla ya damu haijaisha , Anjiu mpaka sasa bado ni tishio kwetu”
“Guru nimeona nitumie fursa hii kukualika kwenda kukuonyesha kitu”Aliongea Roma na kumfanya Laofi kushangaa.
“Ni kitu gani kwanini hukuongea kabla hatujarudi?”
“Nakuamini wewe tu ndio maana sikutaka kuongea mbele ya wenzetu”
Laofi hakuwa na tatizo na uongo wake kwasababu
Zianji na Leiana walikuwa na ukaribu wa kindugu na Anjiiu ni rahisi kumuua lakini Laofi yeye alikuwa tofauti alikuwa akimchukia sana Anjiu kwa viwango vya juu.
Hio ni kwasababu Anjiu na baba yake waliiba cheo chake na baba yake kwa hila zao na wao ndio walipaswa kuwa warithi wa kiti cha ukuu wa miliki.
“Niambie ni kitu gani hicho?”Aliongea Laofi huku akikunja sura.
Roma palepale alitoa kidonge cha daraja la juu kabisa kutoka kwenye hifadhi yake , kidonge hicho mara baada ya kutoa kilisambaza nguvu ya kijini isiokuwa ya kawaida na kiling’aa kama vile ni dhahabu iliomulikwa na tochi , ni kidonge ambacho alitengeneza siku ya jana yake kwa kutumia mimea alioba Kekexil na kilikuwa cha ajabu kwani alitumia kanuni ya andiko la Malkia wa Tushani , zawadi ambayo alipatiwa na Aoiline.
“Hicho nii….”Jini Laofi alishindwa hata kuongea vizurf kutokana na hali ya mshangao na mshituko na palepale alisogea na kumpokonya Roma
“Kidonge Poyana!!!, umetoa wapi hiki kidongea , kanuni ya kutengeneza aina ya hivi vidonge imekwisha kupotea miaka mingi iliopita , hakuna kabisa kidonge cha namna hii katika ulimwengu wa kijini , isitoshe ‘pureness’ ya hiki kidonge inaaminika kuwa ni kamilifu, ni kitu cha thamni kubwa ambacho miliki yetu haiwezi kutengeneza”
Ilikuwa ni haki yake kuonyesha mshangao na msisimko huo kwasababu kidonge hicho ndio hutumiwa na majini ambao wanataka kuvuka levo ya nafsi kwenda levo ya Dhiki na sio tu kwamba kinakuvusha lakini pia kinasaidia katika kuhimili maumivu ya Dhiki.
“Siku mbili zilizopita nilienda kukamilisha kazi moja hivi na ndio nilivyokuja kusimama katika ardhi moja ya theruji upande wa kaskazini , kilichonifanya kusimama ni kwamba kipande cha ardhi katika eneo hilo kilikuwa ni cha tofauti kabisa kutokana na ishara ya nguvu za kijini zilizokuwa zikitoka , nguvu yake ya kiroho katika eneo hilo ilikuwa ni ya kutisha na ndio ilinifanya kuanza kutafuta sababau ni nini maana sio kawaida na nilipoangalia ndipo nilipokutana na maboksi ya vidonge , ilionekana ni kama uzio wa ulinzi wa vidonge hivyo ulifungunka na kufanya eneo hilo la hifadhi ya vidonge kuwa wazi , nina uhakika ni hazina ambayo iliachwa na majini wa enzi , sikutaka kuficha hivi vidonge na niliamua tu kuficha katika maeneo ya karibu na ndio nilivyorudi huku kwa haraka kwa ajili ya kukuambia”
“Kweli!!!?”
Jini Laofi alikuwa katika kiwango cha juu cha mshangao , alipatwa na msisimko mno kiasi cha meno yake kucheza , aliona ni kitu ambacho hakiwezekani lakini hakuwa na tatizo la kutokuamni ilihali alikuwa ameshikilia kidonge hicho adimu mikononi mwake .
“Sasa kama ni hivyo kwanini umeamua kuniambia , ungeamua kuficha au kuweka kwenye hifadhi yako na hakuna jini ambae angegundua?”
“Guru Mzee ukweli ni kwamba vidonge hivi sidhani kama vingenisaidia , kipaji changu kipo ukingoni na tayari mimi ni mzee , ninachotamani ni kuona uwezo wako unapanda ili kuwa na nafasi ya kumshinda Mkuu wetu Anjiu , nitaridhika kama nikichukua kiasi kidogoo tu na kuhusu kuviweka katika pete yangu sikuweza kupata huo ujasiri”
Laofi liishia kufumba macho yake kana kwamba anaingia kwenye tafakari na mara baada ya kuwaza hatimae macho yake yalionyesha hali ya tamaa.
Alijiambia kwasababu Lao uwezo wake ni wa chini basi hana mpango wa hila anaomwandalia na hata kama ikiwa hivyo ni rahisi kudili nae.
“Vizuri kama nitaviona kwa macho yangu ninaahidi kukupatia zawadi kubwa…. hehe Mtumishi ongoza njia nikajionee mwenyewe”
Laofi alikuwa ashajua Mtumishi aliekuwa mbele yake ana kasoro, mara nyingi alipenda kujiita Kijakazi mwanajeshi au mfuasi lakini siku hio hakutaja kabisa maneno hayo kama ilivyotabia yake.
Lakini bado nguvu ya Jani la upofu ilikuwa kubwa mnno na hakujua utofauti wowote wa kimaumbile kutoka kwa Roma.
Roma yupo ndani ya mtego wa jini mkuu Anjiu , Laofi na yeye kaingia mtegoni unadhani atachomoka??
.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 718.
Roma alishamsoma jini Laofi alikuwa ni mwenye tahadhari kwa kila kitu lakini bado tu hakutaka kujali kwani mpango wake ni kupata upenyo wa kumuua , haikujalisha alikuwa makini au vipi.
Mara baada ya Roma kuoona wameenda mbali kabisa na makazi ya ngome za majini , Roma alianza kushuka chini kuelekea kwenye kilele cha mlima wenye barafu.
“Guru angalia”Aliongea Roma .
“Wapi?”
Laofi ambaye alikuwa akifuatilia aliangalia kijimlima kilichokuwa mbele yake lakini hakuweza kuhisi kitu cha ajabu kuhusu huo mlima , lakini ni dakika hio hio Laofi alianza kuhisi ongezeko la nguvu za kijini ambazo zinamsogelea kutoka pande zote.
“Lao Lizeli!!!”Aliita kwa nguvu kwa kutaja majina yake yote mawili huku sura yake ikifubaa.
“Sanyua!!!!”
Aliongea kwa nguvu na palepale ndani ya sekunde tu kiwiko cha madini ya silver kilionekana na kutengeneza upanga ukatao kuwili unaofanana na kioo na aliupiga moja kwa moja kuelekea kwenye Chaos Cauldron.
“Boom!!!”
Mlipuko mkubwa ulitokea na kutengeneza mng’ao mkali uliotoka katika ile siraha , cheche zilisambaa kama vile ni vimulimuli na kupotelea angani.
Mtikisiko uliotokea kutokana na mlipuko huo ulisababisha maporomoko ya mawe na kutengeneza eneo hilo kama vile halina hewa.
Wakati huo nguvu ya ajabu ilimshikilia Laofi kumuweka mbali na mvutano wa nguvu ya Chaos.
Kwa kutumia nguvu zake zote za kijini katika levo ya maji ya upako alifanikiwa kujiokoa katika shambulio la kushitukiza kutoka kwa Roma
Roma alishangaa pia inaonekana huyo mzee uwezo wake wa kijini sio wa kinyonge na ni ngumu kudili nae , lakini Roma alijua amefanikiwa kukwepa shambulizi lake kwa kutumia Dhana ilioitwa Sanyua.
Sanyua ilionekana ni Dhana ambayo ina uwezo wa kukusanya nguvu ya kiroho na kuigeuza kuwa nguvu ya upanga yenye uwezo wa kutengeneza mlipuko.
Upande wa Lao tayari ashaanza kukimbia akiwa na uso uliopauka , siraha yake ya Sanyua ilikuwa nyuma ikiwa imetengeneza upanga unaotoa mwanga na ilikuwa ikielea angani bila kushikiliwa.
Roma alijikuta akipatwa na msisimko , alijua akifanikiwa kumuua Laofi basi moja kwa moja Dhana hio ingekuwa ni ya kwake , ilionekana ni Dhana ambayo ipo daraja la kati mwishoni na kama ingetumiwa na mtu ambaye ana uwezo mkubwa wa kijini basi ingefanana tu na Dhana ya daraja la juu.
Kubwa zaidi ni kwamba siraha hio ilikuwa na muonekano mzuri mno , kiwiko chake kilikuwa cha madini ya Silver huku upanga wake ukiwa ni wa kung’aa , moja kwa moja aliona itafaa kuwa zawadi kwa mmoja wa warembo wake , alijiambia inaweza kumfaa Rose.
Wakati huo jini Laofi alikuwa katika kiwewe kutokana na nguvu kubwa ambayo imeonyeshwa na Roma , ilikuwa ni kubwa mno kwake kukadiria na palepale aliamini sio Mtumishi Lao.
Lakini hakuwa pia mjinga kubakia hapo na kumuuliza Roma ni nani hivyo wazo pekee ambalo lilikuwa katika kichwa chake ilikuwa ni kukimbia kadri awezavyo.
Alijua kama atabakia na kupambana atakufa kwani nguvu zake za kijini pamoja na Dhana yake ilikuwa na nguvu kubwa kuliko yeye , palepale wazo lilimwingia inamaana alimleta hapo kwasababu ya kumuua, aliishia kung’ata meno kwa hasira kwa kuingia mtegoni.
Upande wa Roma hakuwa na wazo la kumuacha amtoroke kwani hio ndio nafasi yake ya pekee na palepale alitoa tabasamu ovu..
“Unakimbia kwenda wapi , unafikiri nitaweza kukuruhusu?”
Baada ya kauli hio Chungu kile kikiwa kimegeuza mdomo wake kuelekea upande wa Jini Laofi kilianza kumfukuzia kama vile ni kimondo kutokana na spidi yake na mwanga uliokuwa ukitolewa , huku nguvu kubwa ya kani mvutano ikiwa ni kubwa mno na kumshikilia jini Lao ili asiendelee kukimbia.
Ijapokuwa Roma alikuwa mbali lakini alikuwa na uwezo wa kukielekeza chungu chake namna ya kufanya kazi hata kwa mbali , ijapokuwa hakikuweza kummeza moja kwa moja Jinii Laofi lakini spidi yake ilikuwa imepungua mno na kufumba na kufumbua Roma alikuwa ashamfikia.
Donge la maji ya kiroho ambalo lilikuwa na rangi nyeupe na bluu iliopauka lilionekana katika kiganja cha mkono wake na palepale alilirusha kuelekea upande wa Laofi.
Laof mara baada ya kurushiwa donge lile kwa ustadi wa hali ya juu alilipasua kwa kutumia Dhan yake ya Sanyua ili kukinga maji yale yasimfikie, ni siraha ambayo ilionekana kuwa na nguvu kubwa hivyo iliweza kuyazuia yale maji kutokumfikia kutokana na kudhalisha presha kubwa ya nguvu kama ile ya mlipuko wa bomu.
“Wewe ni nani, kwanini unataka kuniua?”
Katika moyo wake alikuwa na woga mkubwa mno , adui yake alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kutumia maji ya kiroho kama siraha na hakuwahi kusikia kuna jini ambaye yupo ndani ya ulimwengu huo mwenye uwezo huo.
Unachopaswa kuelewa katika nguvu za kijini ni majini wachache sana ambao wanao uwezo wa kugeuza nguvu za mbingu na ardhi na kuwa maji ya upako ,unaweza ukawa katika levo hio lakini bado ukakosa namna ya kuyatumia maji ya kiroho kama siraha , kitu pekee ambacho majini hufaidika wanapokuwa katika levo ya maji ya upako ni kwamba nguvu zao za kijini zinaimarika mno na ufahamu wao wa kuzuia mashambulizi na kujilinda pia unakuwa mpana.
Asilimia kubwa ya majini ambao wanao uwezo wa kutumia maji ya kiroho kama siraha ni wale ambao wanauelewa na siri iliokuwepo katika mapigo tisini na tisa ya radi ya anga.
Sasa Laofi alikuwa na uelewa huo na palepale aliamini kama adui yake amekwisha ‘master’ siri ya mapigo ya radi tisini na tisa si atakuwa ni mzee , kwanini anamshambulia yeye?.
Roma hakutaka kupoteza muda wake kuongea nae na aliita tanuru lake la maafa juu mara baada ya kuona maji ya kiroho hayana athari kwake hivyo aliamua kumwelekezea nguvu yote ya Chaos Cauldron.
Chungu kile kilitokea juu yake , huku awamu hio kivuli cha mnyama kilichokuwa ndani yake kilionekana kikitokeza kichwa kutoka kwenye chungu kile ambacho kilikuwa na giza ndani yake na kuachia kani mvutano ya hali ya juu sana huku mdomo wake ukiwa wazi kana kwamba ni mamba mwenye njaa kali.
“Hio ni roho ya mnyama wa maafa!!!?”
Alijikuta akipatwa na mshituko mara baada ya kuona kivuli cha yule mnyama , alikiuwa ashamsoma roho huyo katika historia, kabla hata hajajua nini kinaendelea nguvu ya kijini iliokuwa imezingira ile Dhana yake ya Sanyua ililipuka palepale na kusambaratishwa ndani ya sekunde na sasa nguvu ya mvutano ilianza kumshikilia kwa kasi kubwa, ulikuwa ni mvuto ambao ulikuwa mkubwa mno kwa jini Laofi kuhimili.
Cheche zilionekana na kupotea kama vile ni nyota , kwa mtu wa mbali angevutiwa na anachokiangalia lakini kwa Laofi alikuwa akishindana na nguvu ya kifo.
Laofi mara baada ya kuona anakosa mhimili palepale aliamua kushuka chini ardhini na ilikuwa bahati kwake alikuwa amefanikiwa kujichomoa katika nguvu mvutano ya Chungu.
Lakini hata hivyo alijua asingeweza kuhimili shambulizi lingine la Roma kwasababu alikuwa tayari amejeruhiwa kwa ndani.
Roma mara baad aya kuona yupo ardhini palepale alitengeneza kitenesi cha moto mweupe(Soul fire or Pure fire) akinuia kuunguza roho ya jini huyo.
Laofi mara baada ya kuona sasa kifo kinamkaribia aliona njia pekee ya kupona ni kuomba kuhurumiwa.
“Ewe mungu mkuu ulietukuka naomba unirehemu,
sijui ni kwa namna gani matendo yangu yamekuchukiza lakini naomba unirehemu mimi mja wako , nipo tayari kufanya chochote , nipo tayari kukupa siraha zangu na vidonge , tafadhari yasamehe maisha yangu”
Katika wakati huo Jini Laofi alikuwa ashajikatia tamaa katika kupambana na sio hivyo tu hata ule mpango wake wa kisasi katika kuongoza miliki ya Xia haukuwa na muhimu tena baada ya kusimama mbele ya mshindani ambaye alikuwa na uwezo mkubwa , ndoto zake kwa wakati huo aliona ni ujinga.
“Ninaweza kupata kila kitu chako baada ya kukuua”
Aliongea Roma na bila ya huruma palepale alirusha ule moto wa kiroho na mara baada ya kugusana na mwili wake alianza kutoa kilio cha kusaga meno.
Moto wa kiroho haukuwa moto wa kawaida kama moto ambao nnaonekana duniani ni moto ambao unatengenezwa kwa nguvu zza mbingu na ardhi na uwezo wake sio kuunguza mwili bali huunguza roho , ni moto wa mateso kwani unaweza kukuunguza muda mrefu na ushindwe kufa , majini wanawiita moto wa jehanamu.
“Arghhh..!!!”
Kilio kikali cha Jini Laofi kiliweza kusikika kwa juu na sauti yake kupotelea mbali kadri ilivyokuwa ikisafiri na kufifia kabisa na palepale roho yake na nafsi vikawa vimeungua na kuacha mwili ukiwa mzima.
Jini mkuu ambaye yupo katika levo ya maji ya upako hakuwa na uwezo wa kuhimili nguvu ya moto wa nafsi na kuisha palepale.
Dhana ya Sanyua ilibakia kuelea angani huku mwanga wake ukififia mara baada ya Master wake kufa na Roma alikusanya nguvu za kijini katika mkono wake na kisha alinyoosha na kushikilia kiwiko chake na dakika ileile mwanga mkali ulitoka katika ile Dhana kana kwamba ni ishara ya kwenda katika miliki ya mtu mwingine.
Roma alichomoa pete katika kidole cha Maiti ya jini Laofi na kisha aliangalia hifadhi yake ilikuwa na nini na baada ya kuangalia alikuta baadhi ya vitu abavyo havikuwa na maana sana pamoja na chupa kadhaa za vidonge na viungo , vitu ambavyo Roma hakuvitamani.
Kulikuwa pia na Dhana za daraja la chini na Roma alizichukua na kisha akatupia kwenye hifadhi yake ya pete.
Roma palepale alichukua mavazi ya Laofi na kuyavaa kisha akabadilisha muonekano wake na kufanana nae na akarekebisha uwezo wake mpaka katikati mwa levo ya maji ya upako na hatimae sasa aliona mpango wake wa kuingia katika maabara ya kutengenezea vidongeuingekuwa rahisi.
Roma mara baada ya kuona namna ambavyo Laofi ameshindana nae na kumchakaza na mapigo mawili tu alikuwa na hali ya kujiamini na kujiambia mkuu wa miliki hio Jini Anjiu hawezi kuwa na ushindani mkubwa sana.
Baada ya kuunguza maiti ya jini Laofi haraka sana alirudi makao maku ya miliki ya Xia , awamu hio alikuwa na maringo na hali ya kujiamini kuliko mwanzo na wale walinzi mara baada ya kumuona Guru Laofi waliinamisha vichwa vyao kama ishara ya kumsalimia na kisha mlango ulifunguliwa bila hata ya swali.
Roma mara baada ya kuingia hakutaka kabisa hata kupoteza muda katika floor ya kwanza kwani alienda moja kwa moja mpaka floor ya pili.
“Je kuna maagizo yoyote kutoka kwa Guru mpaka kuja usiku huu?”
Cheluni aliulizia katika sauti ya upole , muonekano wake ulikuwa umebadilika mno kuliko Roma alivyomuona mwanzo na ilionyesha alikuwa akimpa heshima kubwa jini Laofi.
“Ninataka kumuuliza Rufi baadhi ya maswali na sitegemei usumbufu wowote kutoka kwa yoyote”Aliongea Roma kwa sauti ya kibabe.
Cheluni alijikuta akishangaa na kujiuliza kwanini ni Rufi tena , lakini hata hivyo hakuthubutu kuuliza swali.
“Tafadhari nisamehe Guru , binti wa mkuu amelekea huko muda si mrefu na hajatoka bado”
“Binti wa mkuu!?”
Roma palepale alielewa nini anachomaanisha , aliamini lazima atakuwa ni Xiaoxiao lakini alijiuliza kwanini ameenda kumuona Rufi , Roma alikuwa na wasiwasi pengine msichana huyo kuna kitu kibaya anamfanyia Rufi.
“Vizuri , nitamwambia ashuke”Aliongea Roma na kisha kwa mbwembwe zote alifyatua mkono wa vazi lake la joho kuonyesha ukuu wake na kisha alianza kupiga hatua kuelekea juu bila mlinzi yoyote kumzuia.
Jini Cheluni msimamizi wa jengo hilo aliishia kuvuta pumzi ya ahueni , alikuwa na wasiwasi anakwenda kuadhibiwa kwa kutompatia huduma nzuri mfungwa.
Roma mara baada ya kufika floor ya tatu palepale aliweza kuhisi uelekeo wa sehemu ambayo Rufi yupo na kufumba na kufumbua alikuwa mbele ya mlango wa chumba cha stoo ambacho mlango wake ulikuwa wazi.
Kitu cha kwanza kuona palepale kilimfanya akili yake kuwa tupu na hasira nyingi zilimvaa palepale , ilikuwa ni kama vile anaungua kutokana na nguvu za kijini ambazo zinauzunguka mwili wake.
Mrembo XiaoXiao ambaye amevalia gauni rangi ya pink huku nywele zake akiwa amezifunga kwa nyuma alionekana kuchuchumaa pembeni ya msichana ambaye alionekana kuwa dhaifu mno., Alikuwa ameshikilia mdomo wake kwa nguvu huku akionekana kumlazimisha msichana huyo kula kitu kwa nguvu kutokana na ukinzani wake.
Msichana aliekuwa katika hali mbayao alikuwa ni Rufi , msichana mrembo ambaye alikuwa na ngozi ambayo sio ya kawaida lakini muda huo hakuwa na ngozi ile tena kutokana na kuharibiwa.
“Unafanya nini!!?”
Roma palepale kwa spidi kubwa alimsogelea XiaoXiao na kumpiga teke la mbavu ambalo lilimrusha na kwenda kujigonga ukutani.

SEHEMU YA 719.
Ijapokuwa XiaoXiao alikuwa ashaingia katika levo ya Nafsi tayari lakini utimamu wake wa mwili haukutofautiana na wa mwanajeshi wa kawaida na pia alikuwa na mwili wa kibinadamu hivyo ilikuwa ngumu kuhimili teke la Roma kiumbe ambaye nguvu zake hazikuwa kwenye matumizi ya nguvu za kijini tu bali pia alikuwa ni mtu alietengenezwa maabara.
Baada ya kujigonga ukutani palepale alidongoka chini na kutema damu nyingi chini.
Ilikuwa ni kama vile mifupa yake ilikuwa imempasuka na aliishia kusikilizia makali ya maumivu huku chozi likimtoka , alijitahidi kupiga magoti huku akitetemeka na kumwangalia Roma kwa macho ya woga.
“Guru Mkuu , Master ,… XiaoXiao nimekosea naomba msamaha wako”
“Umemlisha nini?”Aliuliza Roma huku sauti yake ikionyesha makasiriko.
“Nime… nime “Alikuwa aking’ata lips zake kwa wasiwasi huku akishindwa kuongea na kabla hata hajamaliza kuongea palepale kikohozi kilimpata na kutema damu nyingine chini na kuchafua nguo yake kifuani.
Rufi ambaye alikuwa amempa mgongo Roma palepale aligeuka na kumwangalia kwa tabasamu lenye uchungu ndani yake.
“Kuna haja gani ya kwenda mbali namna hio , hata kama amenimezesha vidonge vya kusaidia vidonda vyangu kupona haimaaniishi kwamba nitaishi muda mrefu , hata kama wewe ni mzee wa kuheshimika huogopi hasira ya baba yake kwa kumuumiza hivyo?”Aliongea Rufi asijue anaeongea nae ni mwanaume ambaye alikuwa akimuwazia kwa muda mrefu.
Sasa Roma palepale alijikuta akishangaa kidogo mara baada ya kusikia vidonge vya kusaidia kuponya vidonda.
Aligeuza macho yake na kuangalia vidonge ambavyo vimedondoka chini na kuvichunguza na kweli ilionekana ni vidonge vya daraja la chini ambavyo kazi yake kubwa ni kuponyesha majeraha.
Kwahio inamaanisha huyu Xiao sio kwamba alikuwa akimlisha Sumu Rufi bali alikuwa akimlazimisha kumeza hivi vidonge kwa faida yake?
Roma alijiuliza huku akiwa amebung’aa bila ya kusogea , huku hisia mchanganyiko zikimvaa na alimwangalia Xiaoxiao ambaye alikuwa akizuia machozi kutoka , alikuwa akitetemeka kwasababau woga ulikuwa umemvaa.
Kwa wakati huo Xiao hakuonyesha yule msichana mchangamfu ambaye alikutana nae nchini Tanzania na alionekana ni msichana ambaye hana ile hali yake ya kujiamini na zaidi ya kuonyesha machozi pekee.
Roma hajazoea muonekano wa Xiaoxiao aliokuwa nao na kuna hali ya huruma na kuumia ilimvaa palepale na kujiuliza au alimdhania vibaya , kama sio kumdhania vibaya kwanini yupo hapo akionekana kumsaidia Rufi, inamaana sio yeye ambaye alitoa taarifa za uwepo wa Rufi nchini Tanzania.
Maswali mengi yalijaza kichwa chake na hali ya hatia ilimshika kwani kama kweli alimdhania vibaya basi ni mara ya pili jambo hilo linatokea lakini kwa muda huo kama ni kweli hakuwa katika nafasi ya kumuomba msamaha na alijiambia labda siku nyingine.
“Ondoka ndani ya hiki chumba na nisikuone tena hapa”Aliongea Roma kwa amri kwa sauti nzito.
Ijapokuwa alikuwa katika mshangao kwa jini huyo mzee wa miliki kutokumuadhibu lakini hakutaka kubakia hapo na aliishia kutingisha kichwa chake, kabla ya kupotea kabisa nje alisimama na kugeuka nyuma.
“Guru … najua maneno yangu kwako ni bure … lakini ,, lakini kuna ulazima wa kumfanyia hivi Sister Rufi? … inatia sana huruma”
“Ondoka!!”
Roma alifoka huku macho yake yakiwa mekundu kwasababu ya hatia iliokuwa ikimtafuna , alikosa ule ujasiri wa kumwangalia tena usoni kwa kile alichomfanyia.
Katika hali ya huzuni XiaoXiao aliondoka katika floor hio kichwa kikiwa chini na kutoka kabisa nje.
Roma mara baada ya kuhakikisha sasa floor hio haina jini yoyote na kulikuwa na usalama alivuta pumzi nyingi za ahueni na kuzishusha na sasa kurudi kaitika hali yake ya Roma Ramoni.
“Umekuja usiku wote huu , unataka kunilisha vidonge tena kufanya majaribuo , kwanini kuwa na haraka huoni naweza kufa mpaka ikifikia asubuhi?” Aliongea Rufi huku uso wake ukiwa na ile hali ya kejeli mbele ya jini Laofi , katika chumba hicho ambacho hakikuwa na mwanga pamoja na kupitia mateso makali hakuwa tena ni mwenye kujisumbua kuhusu uhai na kifo kwani muda huo ni kama nafsi imemtoka.
Ukweli ni kwamba alijua maisha yake yangekuwa yashaisha kama asingekuja kukutana na Roma Ramoni kwenye maisha yake , alijua licha ya kwamba alikuwa katika ulimwengu wa kawaida muda wowote angekamatwa au vinginevyo hata sumu ambayo ilikuwa ikimtafuna kwenye mwili wake ingemuua na kufia katika ardhi ambayo hakuwa na ndugu.
Mungu si Athumani hatimae akamuonyesha mwanga wa tumaini , tumaini ambalo hakuwahi kuwaza kwenye maisha yake angeweza kuwa nalo na ilimfanya kuridhika kwa wakati huo na kujiambia hata akifa hana majuto kwani mama yake amemjua na amefahamu nini maana ya kupendwa.
Kitendo cha kumuona mwanamke huyo akiwa kama
vile amejikatia tamaa ya maisha, lakini vilevile baada ya kalui yake ya kulishwa vidonge ilimfanya kuumia mno na kila hatua aliokuwa akipiga kumsogelea ni kama vile miguu yake imefungwa minyororo.
“Rufii..!!!”
Roma machozi yalimtoka na aliishia kuita jina la mwanamke huyo na uso uliojikunja huku akionyesha hali ya kutetemeka na kabla hata hajamfikia alijikuta akikosa mhimili na kupiga magoti chini kama vile mtu ambae yupo mbele yake amekwisha kuacha roho yake na sasa anaangaliana na mwili, lakini Rufi hakuwa amekufa bali alikuwa amempa mgongo na hali hio ilimfanya kuwa na hali ya hatia kwa kufeli kumlinda.
Majuto na maumivu havikuwa vikitosha kuelezea hisia zake alizokuwa akisikia moyoni , ni mateso ya namna gani aliokutana nayo kama mwanamke mpaka kutamka neno kifo kwa wepesi namna hio.
Rufi alijikuta akipagawa mara baada ya kusikia sauti yake , sekunde tu mara baada ya fahamu zake kufanya kazi machozi mengi yalianza kumtoka kama vile ni maporomoko ya maji.
Alidhania machozi yalikuwa yamekauka muda mrefu kutokana na kuliasana lakini muda huo ni kama mto uliofunguliwa mara baada ya kufungwa kwa muda maji yajikusanye.
Mateso , majonzi , maumivu , hasira na upweke …., kila aina ya hisia zilimvaa kiasi cha kutaka kumgeuza kuwa kichaa lakini kwa wakati mmoja alikuwa katika hali ya furaha kiasi cha kutaka kuzimia.
Ghafla tu akili ya Rufi ilikuja kugundua jambo na palepale aliziba uso wake na viganja vya mikono yake huku akitingisha mwili wake kama vile ni nguo inayotolewa maji kwa kutingishwa ikionyesha dhahiri alikuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa mno.
Roma aliishia kumsogelea kwa magoti na kisha kumkumbatia kwa nyuma , uchafu na nguo zake zilizochanika vilikuwa vikitoa harufu lakini kwa Roma hakujali kabisa.
“Sorry… I’m sorrry .. it’s my fault .. I know its useless for whatever I said but I can guarantee you that you’ll not face anything like this again ….Rufi, if you wish to blame me or hate me just go ahead ,,, it’s all my fault..”
Aliongea Roma akimaanisha kwamba anaomba radhi na anaamini chochote alichoongea ni bure na hawezi kumfanya apitie madhira hayo tena , anamwambia kama ni kumlaumu amlaumu kwa vyovyote vile kwani ni makosa yake.
Rufi bila ya kugeuka alitingisha kichwa chake kwa ishara ya kumkataa Roma huku machozi mengi akishindwa kuyazuia kumtoka.
“Hubby … ondoka .. ondoka na usiniguse”
“Siwezi kukuachia tena , unaweza kunifokea au kunipiga lakini sitaki kukuacha tena”Aliongea Roma huku akimkumbatia kwa nguvu.
“Niachie bwana nenda zako”Aliongea Rufi kwa sauti yenye kitetemeshi.
Roma palepale aliona kuna kitu hakipo sawa kuhusu Rufi ilikuwa ni kama vile kuna kitu anajaribu kumficha kwani hakumwangalia hata mara moja usoni na alikuja ndita na kutaka kumgeuza Rufi lakini alionekana kukataa kuangaliana na Roma na hata alivyomlazimisha kugeuka aliinamisha kichwa chini kama Mbuni.
“Rufi nini tatizo?, hutaki kuniangalia?”
Roma alionekana kutofurahia hali ile na kwa nguvu aliinua kichwa chake na kisha aliondoa nywele ambazo zimefunika uso wake.
Licha ya kujitahidi kuficha uso wake lakini makovu pamoja na majeraha yaliokuwa usoni hayakuwa yakifichika kabisa kwani yalikuwa makubwa.
“Hii nii…!!”
Roma alijikuta akivuta pumzi nyingi na kisha alimlaza Rufi chali kwenye sakafu na kisha kushika uso wake na kuangalia kwa umakini.
Kulikuwa na makovu makubwa ya alama ya X kwenye uso wake na yalikuwa yakiogofya kwa kuangalia.
“Noo… naomba usniangalie … hapana usiniangalie tafadhai..!!”
Alianza kulia sasa kilio cha kwikwi kwa huzuni na kuondoka katika mikono ya Roma na kujikunyata akificha uso wake, ilikuwa ni dhahiri kwamba utu wake ulikuwa umeshushwa na kuwa sifuri na hakujiona ni wa thamani tena hata mbele ya mwanaume anaempenda.
Roma alikuwa na hasira mno kiasi kwamba kiini cha macho yake kilibadilika rangi kutoka kijani na kwenda njano na kisha kwenda rangi nyekundu huku mishipa ya damu ikianza kutanuka katika sura yake ikiwa ni kama vile muda wote angebadilika na kuwa jitu, palepale ngurumo isiokuwa ya kawaida ilimtoka na kufanya nguvu ya kijini kuanza kumzingira kama vile ni kimbunga.
Roho ya mnyama wa maafa palepale ilianza kuchukulia faida hali hio na kujaribu kumtawala Roma, ule ugonjwa wake ambao alishauponya kupitia nguvu za kijini ni kama sasa unataka kujidhihirisha , ugonjwa wakubadilika na kuwa jitu,. Ugonjwa wa sayansi ya kirusi iliowekwa katika mwili wake inayomfanya seli za mwili kutanuka na kubadilika ki umbo.
Kwa jinsi ambavyo macho yake yalikuwa yakibadilika ilikuwa ni kama vile muda wowote angeshikwa na ukichaa na ilikuwa ni hatari mno,
“Nani … nani kakufanyia hivi Rufi?”
Roma alikuwa akijitahidi sana kushindana na ukichaa ambao unataka kuteka ufahamu wake , alijua kabisa kama hasira ikiendelea kumwendesha basi atapoteza uwezo wa kujitawala na alipaswa kumuokoa Rufi.
Katika hali kama hilo chaguo pekee ilikuwa ni kumkumbatia Rufi ili kuongeza nguvu hisia zake za kiakili ili kudhibiti hali yake.
Rufi alikuwa akitetemeka mno kiasi cha kutawanyisha machozi yake kama mvua.
Mwanamke siku zote utu wake upo kwenye muonekano wake , ukitaka kmfanya ajisikie si mtu tena basi wewe haribu muonekano wake kwanzia sura , hivyo hivyo kwa mwanaume ukitaka kumuharibu kisaikolojia njia ni moja tu kuharibu uanaume wake, ni tabia ya kiakili ya kibinadamu na ndio ambacho alifanyiwa mpaka kujihisi si wa thamani tena.
Hatimae Roma hali yake iliweza kurudi na palepale aliparaza mkono wake katka uso wa Rufi na kutoa tabasamu hafifu lilojaa hisia za uchungu.
“Acha ujinga kujiona sio mrembo tena , kwani si nilishawahi kukuambia hata kama wenzako wakichelewa kuzeeka na wewe kugeuka mzee nitaendelea kukupenda , kwanini nikudanganye” Roma mara baada ya kumaliza kauli ile palepale alimwinamia Rufi na kuanza kubusu majeraha na makovu yake yote inchi kwa inchi , ilikuwa ni kama vile anakwenda kubusu kila jeraha ambalo lipo katika mwili wake.
Rufi alijihisi kukosa pumzi na ilikuwa ni kama vile mwili wake unakwenda kuyeyuka muda wowote.
Ni dakika hio hio ambayo sasa alikuja kuelewa maana ya hisia za kifo na alijihisi kutokuwa na majuto hata Mungu akimchukua muda huo.
Hakuelewa hata tabasamu limetokea wapi , ile hali ya utulivu na kujiamini ilimrejea sasa na kurudi katika hali yake kutokana na Roma alichokuwa akimfanyia.
“Hubby … wewe ni mjinga .. kwanini unatoa machozi ilihali uwezo wa kuniponyesha unao?”Aliongea Rufi.
Dakika ileile ni kama sasa Roma alikumbuka , kumbe ninao uwezo wa kumponyesha bwana ,pumbavu nalia nini sasa.
“Rufi hebu nipe dakika chache tu nitakuponya na kukurudisha katika muonekano wako wa kirembo” Wanasema pale mmoja anapopitia Kiwewe cha mshituko inatokea hali ya kusahau kitu ambacho sio rahisi kusahaulika na mtu huyo atakuwa kipofu kutokana na hisia zake.
Baada ya Roma kuona uso wa Rufi ukiwa katika hali mbaya alikuwa katika maumivu na kujilaumu kilichotokea na kujikuta akisahahu kama alikuwa na uwezo wa kumponya mtu kwa kutumia nguvu za andiko la urejesho.
Haijalishi uimara wa ufahamu wako ukoje ila kutakuwa na wakati tu lazima utakutana na hali ambayo utajihisi uoga na hio yote itategemea na ukubwa wa hali yenyewe kama inatosha kumuogopesha mtu.
Ijapokuwa Rufi alikuwa amezaliwa na kiwango kikubwa cha nishati ya Yin lakini likija nguvu ya andiko la urejesho wa Azimio liliponya kila kitu.
Kipindi kile kule Australia Roma hakuweza kumponya Rufi kutokana na kwamba majeraha yake yalikuwa ni ya ndani ya mwili katika sehemu tata,sehemu ambayo nguvu yake kubwa ya mkataano ndio ilipo.
Hivyo Roma mara baada ya kukumnbuka uwezo wake palepale alitoa kidonge cha mchanganyiko wa mifupa ya majini Joka , vidonge ambvyo alitengeneza katika ulimwengu wa majini pepo ili kumlisha Rufi.
“Hubby acha kupoteza hiko kidonge kwa ajili yangu , ni cha thamani mo na kimetokana na mfupa wa joka, unaweza kuniponyesha majeraha yangu hata kwa kidonge cha daraja la chini tu”
“Acha kuongea sana , fanya kama ninavyokuambia , kwanini niruhusu mpenzi wangu kumeza kidonge cha daraja la chini?”Aliongea Roma kwa sauti iliojaa kiburi.
Rufi alikuwa na furaha baada ya kusikia maneno ya mpenzi wake na aliishia kutingisha kichwa kwa utii.
“Ninapaswa kuondoa ngozi yako ambayo imekwisha athirika katika uso wako , inaweza kukuletea maumivu hivyo haina haja ya kuharakisha tunaweza kufanya taratibu”
“Hakuna shida , ninaweza kuvumilia hata maumivu yaweje”Aliongea Rufi akitabasamu na alikuwa sahihi maumivu makali aliopitia katika mwili wake yalikuwa makubwa mno kuliko hata maumivu ambayo angeweza kupata kwa kuponyeshwa.
Kwa Rufi kupigwa mateke na kutema damu maumivu yake yalikuwa ya kawaida sana , maumivu makali ni yale ya sumu ambayo yapo ndani ya mwili wake.
Roma mara baada ya kumsikia akiongea kwa namna ya kutokuwa na wasiwasi alimuonea huruma.
“Rufi najiuliza kama tusingekutana kule Marekani pengine sasa hivi ungekuwa ukiishi maisha yako ya furaha sehemu au angalau wasingerweza kukupata kirahisi na kuteseka namna hii”
“Huwezi kuhisi mateso bila hisia za upendo, Hubby usifikiirre sana , nitalia kama hutoniponyesha uso wangu mapema”Aliongea na kumfanya Roma kuvuta pumzi.
“Fumba macho yako na lala chini kisha jilegeze”
Roma alifikiria kidogo na kisha palepale alitengeneza maji ya baridi na kumwagia usoni.
Maji ya barafu hayakuwa na athari ya kuyeyusha sura kama maji ya kiroho lakini yalikuwa na uwezo wa kugandisha kitu chochote sekunde tu , lakini Roma aliyapunguza ukali wa baridi , alifanya vile kwa nia ya kumtengeneza ganzi.
Kwa utaalamu wa hali ya juu ile ngozi ya juu ilianza kukauka na kutengeneza ngozi nyingine kwa chini ambayo ni kama imegandishwa na barafu na Roma alianza kuiondoa huku akitumia nguvu ya Andiko la urejesho kurahisisha kuongezeka kwa kasi seli za ngozi kwa haraka sana ili kuziba zile ambazo zimekufa.

SEHEMU YA 720.
Roma alitumia umakini mkubwa kwani kazi hio haikuwa ikitaka kasoro hata kidogo maana matokeo yasingekuwa mazuri , katika mchakato wote Rufi aliishia kutoa tabasamu tu bila kufumbua macho yake ,ilikuwa ni kama vile alikuwa akifurahia kinachoendelea.
Dakika kama kumi na tano hivi mbele Roma alikuwa ashamaliza na aliishia kutoa pumzi ya ahueni.
“Vizuri , unaweza kufumbua macho yako sasa”Aliongea Roma na tataribu Rufi alifumbbua macho yake na kukaa kitako huku akianza kugusa uso wake kwa kutetemeka mikono na Roma aliishia kutoa tabasamu tu.
Ngozi yake ya uso ilikuwa imerudi katika ubora wake , ilikuwa ni nyororo, ya kuteleza na ya mvutano na palepale machozi yalimtoka.
Hata hivyo hakuna mwanamke ndani ya dunia hii ambaye hana mashaka na muonekano wake ndio maana biashara kubwa ambazo zinafanya vizuri ni za vipodozi .
Roma aliishia kucheka tu na palepale kwa kutumia uwezo wake wa kijini alitengeneza kioo cha maji ya barafu mbele yake ili kujiangalia.
“Angalia sura yako sasa kipenzi changu Rufi , sijakudanganya nimeweza kukuponya , sasa hivi umekuwa mrembo kuliko hata mwanzo”Aliongea Roma kwa furaha.
Baada ya kujiangalia na kuona kila kitu kipo katika ukamilifu aliishia kumkumbatia Roma kwa furaha na kumbusu mara kibao.
Dakika hio kabla hata Roma hajaongea chochote mrembo huyo alianza kutoa kilio cha kwiki akianza kutoa machungu yake yote moyoni ambayo amepitia.
Wakati hayo yakiendelea upande mwingine mita kdhaa nyuma ya jengo hilo njia ya kuelekea jumba la mkuu wa miliki.
Chini ya nyota alionekana Xiao ambaye alikuwa akitembea haraka haraka kurudi nyumbani kwao.
Alikuwa ashapona majeraha yake lakini damu ilikuwa bado ikionekana katika kifua chake.
“My dear sister , umetoka wapi usiku wote huu?”
Sauti kali ilisikika kutoka mbele yake na Xiao aliishia kuangalia kivivu na kuona sura ya mwanaume mtanashati aliekuwa amevaa mavazi yaliomkaa vizuri na kumpendezesha .
“Kaka…!!”Aliishia kumung’unya maneno akishindwa kujibu swali lake.
“Unafikiri sijui ni wapi umetokea , kuna mtu alikuwa bize sana kwenda na kurudi katika jumba la kutengenezea vidonge”Aliongea kinafiki na kumfanya Xiao kushikilia gauni lake eneo la kifuani na kuinamisha kichwa chini.
“Nilikuwa nikijiuliza kwanini kila nikimpiga sana nikienda namkuta amepona , nilifikiri ni baraza la wazee ndio waliokuwa wakimpnnyesha kumbe ni wewe hayawani”
“Kaka .. Rufi anatia sana huruma”
“Eti Rufi , kumbe huyo malaya siku hizi nae ana jina?”Lahani alikuwa katika kiwango cha juu cha hasira.
“Ashawahi kuwa mchumba wako , isitoshe familia yetu imemfanyia mambo engi mabaya kwanini bado tunaendelea kumtesa , imetosha sasa”
“Kimya!!”
“Hebu jiangalie na ukarimu wako feki…wewe ni msaliti na sitaki tu kukupiga kwani sitaki kufokewa na baba maana unapenda kujitia sana huruma mbele yake , lakini Xiao nataka ujue hili , usijione siwezi kukufanya chochote kwasababu una undugu na mimi na baba anakulinda , ijapokuwa umeitwa kurudi nyumbani lakini haibadilishi ukweli wewe ni binadamu dhaifu , uliezaliwa na binadamu wa hadhi ya chini , huna haki ya kuwa mrithi wa miliki , unamuonea huruma Rufi kwasababu ni mpuuzi mwenzako unaefanana nae , wewe ni binadamu na siku zote utabakia kuwa kiumbe dhaifu “
“Kaka kwanini unaongea hivyo , ijapokuwa kuna utofauti kati yetu lakini siku zote nakuchukulia kama kaka yangu , baba ameniambia nikutii kila unachoongea na nimeishi kwa kufanya hivyo, kwanini unanibagua namna hio?”
“Acha unafiki , kama kwelu ulikuwa ukinisikiliza kwanini uwezo wako umeongezeka kwa haraka ndani ya muda mfupi kiasi cha kuwafanya wazee kukuangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida, , ulisema mwenyewe mimi kaka yako ndio ninakwenda kukalia kiti cha madaraka lakini ninachoona sasa ulikuwa ni unafiki na unajifanyisha tu ukisubiria muda sahihi wa kuchukua hatua baada ya kuridhisha wazee”
Xiao alimwangalai kaka yake kwa namna ambavyo alikuwa amefura kwa hasira.
Sauti yake ilikuwa kali kama kengele kwenye akili yake na alishindwa kuongea neno lolote kwa wakati huo.
Hali ya kukosa tumaini pekee ndio ambayo ilikuwa ikionekana kwenye macho yake , ulimwengu ulikuwa ni tofauti na ambavyo alikuwa akifikira.
Alijiambia kwanini kila mtu anamshuku , kaka yake aliekuwa mbele yake alikuwa akitisha kiasi cha kutaka kukimbia lakini hapo ndio nyumbani kwao na hata kama akienda ulimwengu wa kawaida hakuwa na ndugu .
Ukweli ni kwamba mwanzoni aliamini pengine dunia ya kawaida ni ya tofauti lakini siku ambayo alitaka kunyongwa katika fukwe ya bahari mtazamo wake ulibadilika kabisa , mtu ambaye alitaka kumnyonga ni mtu ambaye alimpenda kwa muda mfupi sana licha ya kwamba hakuwa akimjua vizuri lakini akataka kumnyonga , ndio siku ambayo alijua hakupaswa kuwa wa ulimwengu wa kawaida na mahali pake ni ulimwengu huo wa majini.
Lakini kuja katika ulimwengu wa kijini nako alijitahidi sana kupatana na kaka yake kwa kuonyesha utii lakini hakuna ambaye alionyesha kujali juhudi zake , sio kaka yake tu lakini pia hata mama yake wa kambo.
“Mnafanya nini hapa?”
Sauti ilisikika kutoka kusikojulikana na kumfanya Lahani kutetemeka kwa hofu na kwa tahadhari aliinua uso wake kuangalia angani na alionekana mwanaume wa makamo ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kijani mtindo wa Hanfu , huku nywele zake ndefu zikipeperushwa na upepo na kumfanya aonekane ni kama malaika.
“Baba..!!”
Lahani alikuwa katika hali ya mshituko mno kwasababu hakuweza kudhania kama baba yake alikuwa ashamaliza mafunzo yake ya kijini katika eneo la kujitenga na sasa ametoka.
“Nyie mnachojua tu ni kugombana na kunidhalilisha badala ya kujifunza au kupumzika katika vyumba vyenu , mnataka wazee wa baraza kuja hapa na kuona mkibishana?”
“Baba nilikuwa nikiongea nae kistaarabu tu , hakuna jambo kubwa”
“Nadhani unajiona umekuwa si ndio ,si tu kwamba unaniona kama mjiga lakini pia wewe kama mwanaumeunaoogopa kushindwa na msichana”
“Baba sithubutu kukudanganya”Aliongea huku akikamaa mwili.
“Tokea ulivyokuwa mdogo wewe ndio uliekuwa ukipokea matunzo na ufahari wote wa familia na sasa kwasababu dada yako kaingia levo ya nafsi ndio unaanza visa , hakika unajua kunifurahisha mimi baba yako”Aliongea huku sauti yake ikionekana haina furaha hata kidogo.
“Baba naomba uniwie radhi , sitokuangusha”Aliongea akikiri amekosea.
“Kwasababu umekiri haya ondoka na rudi wenye chumba chako , ngoja tu nikuambe kuna majini ambao wapo rika lako kutoka Panas na Kekexil ambao tayari wapo levo ya maji ya barafu , kama hutoweza kuingia levo ya maji ya barafu kabla ya mashindano ya jicho la anga kati ya miliki tatu utaonja dawa yangu”
Lahani aliishia kuitikia kwa sauti kubwa na bila ya kupenda alimpiga jicho la pembeni Xiao na kisha aliondoka.
Baada ya Lahani kuondoka alimwangalia binti yake kwa macho makali na kisha alivuta pumzi na kuzishusha kama mtu anaejituliza.
“Unapaswa kurudi ndani acha tabia ya kujibishana na kaka yako”
Xiao aliishia kuinua uso wake na kumwangalia baba yake ambaye alikuwa akielea.
“Baba sikupenda kujibishana na kaka”
“Haijalishi na sijali pia , sisi ni familia kubwa kushindana sisi kwa sisi ni kawaida , kama utaweza kuvumilia na kumshinda kaka yako inamaanisha kwamba uwezo unao lakini kama utashindwa kuvumilia inamaanisha huna thamani ya kuwa binti yangu wala sehemu ya familia yetu tukufu na hakuna ambae atakuonea huruma”Aliongea katika sauti ya kawaida.
“Baba kwanini kila mtu hanipendi hata kama najitahidi kutoingilia maisha yao , kaka ni mrithi halali tayari na sijawahi kuomba urithi wake, tokea nilivyokuwa mdogo uliniambia mama yangu ni binadamu wa kiafrika na amekwisha kufa hivyo mimi ni mtoto bila ya mama hivyo napaswa kuwa mtiifu ili nisichukiwe… nilichotamani katika maisha yangu ni kuwa sehemu ya familia na kupokea upendo , nilipokuwa katika ulimwengu wa kawaida nilishikwa na wivu mno kuona watoto wengi wa kibinadamu wanaishi kifamilia , ijapokuwa wamezungukwa na vifo na magonjwa , majozi na maumivu lakini bado niliwaonea wivu , kwasababu tu wanajua nini maana ya familia , baba unaweza kuniambia je nachukiza sana ndio maana kila mtu hanipendi au familia yetu haipaswi kuwa ya kawaida kama familia nyingine , kuna ulazima wa sisi kushindana ndugu kwa ndugu?”
Aliongea katika hali ya huzuni lakini mkuu wa miliki hio Jinin Anjiu muonekano wake haukuwa umebadilika hata kidogo licha ya kwamba nyusi zake zilicheza kwa sekunde , alionekana hakuathirika kabisa kihisia licha ya binti yake kutia huruma , hakika alikitendea haki cheo chake cha ukuu wa miliki.
“Kama unataka kupata majibu ya maswali yako , njia ipo?”
“Ni njia gani baba?”Aliuliza huku akiwa na tumaini kutoka kwa baba yake.
“Become stronger untill when you posess the stregth to face anyone without fear ,then you‘ll understand why you would have such confusion”
(“Kuwa na nguvu zaidi mpaka uweze kumkabili mtu yoyote bila woga , ndipo utaelewa kwanini ulikuwa katika huo mkanganyiko”)
Mrembo Xiao alishangazwa na jibu la baba yake lakini pia kuonyesha ishara za kuchangyikiwa na hakujua ni kwa namna gani swali lake linahusiana na maswala ya nguvu..
“Hatima yako ipo mkononi mwako mwenyewe , ingawa mimi ni baba yako mzazi ,siwezi kukulinda milele na sitokuambia ni kesho ipi uchague , ndugu yako pia ni mtoto wangu , ni yupi kati yenu atakaeweza kuishi hadi mwisho mimi sijui na itategemeana na mioyo yenu kama itachagua mwelekeo sahihi”
Muda ambao amemaliza kauli hio hakuwa tena mbele ya macho ya Xiao Xiao .
Xiao aliishia kusimama alipokuwa bila kusogea akiwa anafuta machozi yake , ilikuwa ni kama vile ameelewa baba yake alichokuwa akimaanisha.
*******
Baada ya Rufi kumaliza kilio chake Roma aliamua kumuondolea nguvu hasi katika meridiani zote tisa , nguvu ya kijini ambayo ilikuwa ikielekea kulipuka katika mwili wake na kuachilia kiasi cha sumu kuathiri mwili wake.
Baada ya kumaliza, kwa kutumia uwezo wake alitengeneza maji ya mvuke katika mwili wa Rufi kama ‘hotspring’ vile na kumfanya kutakata mwili mzima, Rufi hakuwa na aibu tena kuwa uchi mbele ya Roma kwani washalala pamoja mara kibao.
Baada ya kutakata Roma alitoa nguo za Edna katika hifadhi ya anga na kisha kumpatia avae na akaja kurudi katika muonekano wake wa kupendeza tena akiwa hana alama yoyote kama alikuwa katika mateso , hakika nguvu za kmbingu na ardhi zilikuwa na matokeo ya ajabu.
Baada ya Rufi kuwa sawa sasa ndio alikumbuka Roma alikuja hapo akiwa na sura ya Laofi na alitaka kujua Roma amefanikiwa vipi kuiga sura yake.
Roma alimwelezea kila kitu kwa ufupi na alishangaa mara baada ya kusikia uwezo wa jani la pofi , baada ya kusikia pia mlezi wake Sui amemuokoa machozi ya furaha yalimtoka maana katika kipindi chote alijua alishauliwa..
“Mama mlezi wangu bado yupo hai na umemuokoa , babe asante sana”
Kitendo cha Roma kumsaidia mlezi wake kilionyesha kumgusa mno na kuona pengine mateso yake ya muda mfupi yalikuwa ni kwa ajili ya kumpeleka Roma Kekexil kumsaidia mlezi wake.
Alichokifanya Roma hakuna mwanaume wa kawaida ambaye anaweza kukifanya.
Mahaba yake mbele ya Roma yalizidi kuchanua , pengine ndio maana wanawake hao walikuwa wakimpenda sana bila ya kujali alikuwa ameoa.
Baada ya kumaliza kuongea na kuuliza maswali yake na kujibiwa sasa Roma hatimae uso wake ulirudi katika usiriasi .
“Rufi sasa ni muda wako kujibu maswali yangu , nilisikia kwa Bi Wema ni XiaoXiao , Lahani na mzee mmoja ambao walikuja kukuteka , si ndio?”
“Ndio ni Lahani na Mtumishi wa familia anaefahamika kwa jina la Lao Lize, kuhusu Xiaoxiao…, Ijapokuwa bado siamini nani alivujisha taarifa za uwepo wangu Tanzania lakini XiaoXiao anaonekana hapendi mateso ninayopitia, sidhani kama alihusika”
“Nini kinakufanya uongee hivyo?”
“Wakati wamefika nyumbani XiaoXiao alionyesha kutaka kunikingia kifua lakini kaka yake alimfokea , muda wote nilipokuwa hapa ndio yeye pekee ambaye atakuja na kunilisha vidonge vya kuniponyesha kwa kunilazimisha , kuna siku Laofi alimkamata na alimfokea kweli lakini hakuacha kuja .... kwasasa nikikumbuka vizuri nadhani ni mimi ambaye sikuwa nikizuia hasira zangu , namuonea huruma lakini nashindwa kuziuia hasira zangu kutokana na familia yake inachonifanyia… nina uhakika hata kurudi kwake huku alilazimishwa” Roma alifikiria na kuona pengine alimdhania vibaya , mara baada ya Roma kuwaza kwa dakika palepale wazo liliibuka katika kichwa chake, ni kama sasa anakumbuka kuna majini kutokea pande za Afrika ambao wana uhusiano na Raisi Jeremy majini kutoka miliki ya Panas.
Roma palepale alijikuta akijikasirikia mara baada ya kusahau kitu muhimu kama hicho , ijapokuwa hakujua uhusiano uliopo kati ya familia hizo na Panas lakini kuna uwezekano ndio ambao walivujisha taarifa.
Roma alijiambia kama kweli wao ndio ambao wamehusika ili kumtengenezea uadui na miliki hizo za kijini ataivamia Panas na kuua kila jini bila ya huruma.
Kuhusu Edna baba yake juwa Jeremy asingejizuia kumuua kama na yeye anahusika.
“Rufi kabla hatujaondoka kuna kitu nataka kwanza kuhakiki”Aliongea Roma akiwa siriasi na palepale sura yake ilianza kuingiwa na ule msisimko wa kimauaji.
“Nani ambaye alikuharibu sura?”
“Hubby kwanini tusipotezee hili na kuondoka kimya kimya?”
“Hapana!!, najua una wasiwasi juu yangu lakini najua mwisho wangu , siwezi kuona anaendelea kuishi ili hali kakutesa namna hii , nitamuua na kumrarua na kuhakikisha roho yake naingamiza”Aliongea Roma lakini Rufi aliishia kukaa kimya akionekana kusita kutaja jina lake,
“Hata usiniambie nishajua ni nani lazima atakuwa ni Lahani”Aliongea na Rufi hakujibu lakini macho yake yalimsaliti,
“Hehe.. huyo mwanaharamu si ndio mtoto wa mkuu wa miliki na nasikia jini Anjiu anae mtoto mmoja tu wa kiume , nitakizimisha kizazi chake kijacho leo hii”Aliongea Roma akiwa na nia ovu inayoonekana dhahiri kwenye macho yake na ilimfanya Rufi kuogopa na kumshika mkono kwa namna ya kumsihi aachane na mpango wake wa kisasi.
“Hubby Jini Anjiu uwezo wake sio wa kawaida , ijapokuwa ni sehemu ya Master kumi wa ulimwengu wa kijini lakini kwake ni tofauti , ndio jini mwenye nguvu kati ya master wote kumi na ameweza kuimiliki kikamilifu mbinu yote ya Roshinisutra katika viwango vya juu kabisa na hapo bado hatujazungumzia uwezo wake wa ku’manipulate’ elementi zote tano … nimesikia pia amefanikiwa kuiweza mbinu ya nguvu ya mafunzo ya siri ifahamikayo kwa jina la Three legged Golden Crow , hakuna jini katika miliki ambaye ameweza hio mbinu zaidi yake , pengine labda miaka elfu moja ijayo , ni mbinu ambayo inamsaidia kutengeneza Mystic flame kati ya nishati za mbingu na ardhi , nguvu yake ni ya kutisha sana katika mashambulizi unapaswa kuwa makini”
“Mystic flame!!!?”
Roma aliongea kwa hali ya mshangao na palepale alikumbuka andiko la kikanuni ambalo lilikuwa katika lile jumba jeupe kule Kekexil , andiko lile lilianisha kwamba katika ulimwengu ukiachana na moto wa kawaida pamoja na radi , kuna kitu kingine ambacho kinaitwa moto wa kimaajabu(Mystic flame) na maji ya kimaajabu(Mystic water).
Maajabu hayo ya maji na moto yameitwa hivyo kwasababu yanatokea katika hali tatanishi kutokana na sanaa ya kipekee au nguvu maalumu kutoka katika Dhana.
Three legged golden Crow kiswahili chake ni Kunguru wa dhahabu wa miguu mitatu(Google kuelewa zaidi).
Ukizungumzia maji ya kimaajabu ni kama ilivyo kwa mbinu ya siri ya Dark Ice Soul , inasemekana mfungamanisho wa nguvu ya kiroho ya giza na maji hudhalisha maji ambayo ni sawa na maji ya kimaajabu.
Ijapokuwa maji hayo katika elimu ya kimajini hayana nguvu kama ilivyo kwa maji ya kiroho na ya barafu lakini kwa asilimia kubwa maji hayo nguvu yake ililingana na maji meupe katika mbinu za kawaida za mafunzo ya kijini.
Mfano mwingine ni ndege wa kihadithi anaefahamika kwa jina la finiksi(Phoenix), inasemekana moto wake ulikuwa ni mkali sana kuliko moto wa aina yoyote ile , hata moto wa bluu ambao unaunguza sana haufikii moto unaozalishwa na ndege huyo.
Sasa tukija katika ndege mnyama wa kimaajabu anaefahamika kwa jina la Three-legged golden Crow katika elimu ya majini inasemekana ni Ndege wa Kimungu ambaye huhusishwa na jua.
“Ndio , inasemekana ni jini mmoja tu ambaye aliweza ku’master’ mbinu ya Three Legged golden Crow , ijapokuwa nguvu ya moto wake inaweza isiwe kama hio ya mnyama halisi lakini inachukuliwa ukali wa moto wake ni ule wa uhakika, kama sio hivyo majini wengi wangeweza kufanikisha kujifunza hio mbinu , kadri mbingu inavyokuwa ngumu kujifunza ndio ukali wake unayvokuwa mkubwa , ni hasara tu kwamba Jini Anjiu ni mara chache sana anapambana na kwa miaka mingu hajawahi kupata mshindani wa levo zake hivyo sijui nguvu yake halisi ikoje”
Namna ambavyo Rufi alikuwa akielezea ni kama vile alikuwa akimuogopesha Roma ili tu waondoke hapo bila ya vurugu , lakini muda huo Roma alikuwa akijihisi msisimko mno kwa kupambana na mtu mwenye uwezo mkubwa kama huyo,
“Hakika inafurahisha , kadri adui anavyokuwa na nguvu ndio nitakavyojihisi kufanikiwa baada ya kumuua , ina faida pia katika mafunzo yangu kwani inaniongezea uzoefu , Rufi ni muda sasa wa kukutoa hapa, nikishakufikisha kisiwani salama salimini nitarudi tena kumuua Lahani,jini yoyote akituzuia nitamuua”
Rufi aliishia kushangaa tu , ashasahau mwanaume huyo hakuwahi kujua tafsiri halisi ya hofu , kitu pekee ambacho aliona anaweza kufanya ni kukubaiana nae licha ya kwamba alikuwa na wasiwasi.
Roma hakujali tena kuchukua uhusika wa jini Laofi na alijiambia kila jini ambaye atakutana nae kwenye jengo hilo anapaswa kukutana na kifo kwa kumtesa Rufi wake.
Baada ya kumshikilia mrembo wake mkono safari ya kutoka kwenye jengo hilo hatimae ilianza.
Cheluni na majini wengine ambao walikuwa katika floor ya tatu walishangazwa kuona mtu ambaye hawamjui tena mweusi ambaye amevalia mavazi ya jini Laofi akiwa ametangulizana na Rufi.
“Wewe ni nani!?”Aliongea kwa jazba na palepale nguvu za kijini zilianza kujidhihirisha na Roma aliishia kutoa tabasamu la kifedhuli na alijiambia kutokana na eneo hilo kuwa dogo basi hao majini wasingeweza hata nafasi ya kukimbia.
Dakika ileile aliiita Dhana yake ya Chungu , na nguvu ya giza ya mnyama wa maafa ndani ya sekunde ilimeza kila kidonge kilichokuwa hapo ndani pamoja na mimea yake na kugeuza nguvu yake kama kionjo tu kwa Roma.
Roho hio ya mnayama ilionyesha ishara ya njaa na kiu kali na kivuli chake kilichoambatana na macho ya rangi ya kaa la moto yalizunguka kila pande kwa namna ya kutisha.
Muonekano wa chungu kile haukuwa ukitisha hata kidogo , kilichokuwa kikitisha na kuogofya ni ile roho ya mnyama hasa pale mnyama mwenye muonekano kama wa Mamba anapojitokeza, ilikuwa ikitisha mno lakini kwa Roma hakuwa na hofu hata kidogo kwani kwake mnyama huyo ni kama mbwa wake katika kumsaidia kumshinda adui.
“Ni mnyama gani huyo!?”
Walijikuta wakipiga makelele na Roma hakutaka hata watumie Dhana zao kumshambulia kwani palepale aligeuza maji ya kiroho na kuwa vinyoka nyoka na kwenda kuwapasukia kama mabomu na kuanza kuwasambaratisha.
Hakuna majini ambao wapo levo ya chini ambao walikuwa na uwezo wa kuhimili nguvu ya maji ya upako na waliyeyushwa mara moja huku wakitoa vilio mpaka nafsi zake zilivyobakia si kitu , walikufa vifo vibaya bila hata ya kufanya shambulizi.
Baada ya mnyama yule kuwatafuna kwa mbwembwe kama zote , alizidi kucheza cheza macho yake akitoa msisimko wa mauaji , ngurumo ya besi ilisikika kama vile ni simba ambaye yupo kwenye banda na anataka kuchoropoka mara baada ya kuona kitoeo.
Nguvu za kijinni za Roma hazikufanana na nguvu za giza za mnyama huyo , ukweli ni kwamba Roma alikuwa akimtumia huyo mnyama kutimiza haja zake tu.
Mara baada ya kumaliza kuua kila jinni aliekuwa katika floor hio na kumlisha mnyama vidonge vyote,alikitanguliza chungu mpaka floor ya kwanza huku yeye akishuka.
Majini wawili ambao walikutwa wakiwa bize kutengeneza vidonge hawakupewa hata nafasi ya kushituka kwani walivutwa kama vumbi mmoja baada ya mwingine na wote wakatafunwa,
Wengine ambao walibakia Roma aliwaua kwa kutumia moto wa ragi ya zambarau na kisha aliunguza mimea yote na viungo vyote kama kawaida yake katika harakati za kutia hasara majini.
Nguvu kubwa ya kutoisha ambayo ilikuwa ikizalishwa na chungu hicho pamoja na nguvu ya Roma iliwatisha wazee majini ambao walikuwa wakilinda katika eneo la nje na wote bila kujiuliza wanakifuata kifo waliingia ndani kuangalia kuna nini.
Mara baada ya kufika tu waliweza kiumuona Roma na Rufi wakisogelea upande wao wakitaka kutoka.
Kilichowapagawisha na kuogopesha zaidi ni moto ambao ulikuwa ukicheza cheza katika kiganja cha Roma , moto ambao licha ya umri wao mkubwa hawajawahi kuona jini yoyote akiutawala kirahisi namna hio.
Kilichowapagabishwa zaidi ni mara tu baada ya lichungu la kijani ambalo lilikuwa kama shimo jeusi lilivyotokea mbele yako likisafisha njia na mnyama wa maafa hakuambiwa cha kufanya kwani aliwavuta kama karatasi wale majini na wote akawatafuna huku nguvu zake akizisharabu na kuzipeleka kwa bosi wake.
“Kimbia kumtaarifu mkuu wa miliki”
Mlinzi mmoja wa mwisho aliesalia alipigiwa kelele na mwingine ambaye alikuwa akitumbukia kwenye mdomo wa chungu.
“Haha.. unafikiri ataweza kukimbia kirahisi hivyo”Roma alitoa tabasamu la kifedhuli na palepale alikiamrisha chungu chake kumfukuzia yule jini na ni ndani ya sekunde tu na yeye alivutwa kama karatasi na kuanza kutafunwa na mifupa yake.
Rufi ambaye alikuwa akifuata kwa nyuma aliishia kushangaa na kupagawa kwa wakati mmoja, hakuwahi kutegemea Chungu hicho kuwa na uwezo mkubwa wa namna hio mpaka kuweza kushambulia majini wa levo ya maji kwa urahisi sana .
Roma mara baada ya kuua walinzi wote wa jumba la kutengenezea vidonge alimchukua Rufi na kutoka nae nje ya jengo hilo , lakini sasa sekunde ambayo anafikiria kuficha chungu chake na kuanza safari ya kukimbia aliweza kuhisi nguvu kubwa ya mkandamizo inasogelea eneo hilo.
Alamu iligonga katika masikio yake na kukunja ndita na palepale alijua nguvu hio inatokea nyuma yake na alikigeuza chungu kile kumkinga kupitia nyuma
Mtikisiko mkubwa ulisikika palepale kama vile ni tetemeko la ardhi , majengo yote yalianza kutikisika kiasi kwamba ni kama makao yote makuu majengo yake yanakwenda kuporomoka.
Kufumba na kufumbua tu Roma alipata kuona boriti ya mwanga wa zambarau na nyekundu kutoka angani kama mwanga wa Laser ukiwasogelea kwa ajili ya kuwashambulia

Lakini mwanga ule kama vile ni radi ulienda kutua katika kile chungu na palepale eneo lote lilitawaliwa na mwanga kama vile radi inashambulia mnara.
Roma alishangaa mno na kama asingechukua hatua mapema Rufi angekuwa ashajeruhiwa kwa kiwango kikubwa , kwa haraka haraka Roma aliamini hata kama anaweza kuzuia mashambulizi lakini nguvu ya kijini inayongezeka kila sekunde ilikuwa ni kubwa mno na ya kutisha.
Roma aliinua uso wake na kuangalia angani na hapo ndipo alipoweza kumuona mwanaume wa makamo ambae amevalia joho la rangi ya kijani huku mikono yake akiwa ameinganisha kwa nyuma na kidevu chake akiwa amekinyanyua kwa juu kwa namna ya pekee.
“Jini Anjiu”
Ijapokuwa Roma hakuwahi kumuona ana kwa ana mkuu huyo wa miliki ya Xia lakini aliweza kusema jini huyo kweli anaendana na cheo chake.
Alishindwa kabisa kuona levo ambayo Anjiu alikuwa amefikia katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi , ijapokuwa aliweza kuotea yupo levo ya maji ya upako lakini nguvu zzake za kijini zilikuwa kubwa mno.
Unafikiri Roma atamuweza Jini Anjiu,m ngoja tuone.
END OF SEASON 24.
ITAENDELEA.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA.

Mono no aware

SEASON 25

SEHEMU YA 721.
Kama Roma angeweza kufananisha uwezo wa Jini Anjiu na Bi Tigola basi uwezo wa Tigola ungekuwa ni kama maji yaliojazwa nusu kipimo kwenye glass huku Jini Anjiu uwezo wake ni glass iliojaa maji mpaka pomoni na kuanza kumwagika, ni uwezo ambao ulikuwa nje ya matarajio yake.
Kwa haraka haraka Roma alijua pengine Anjiu ni jini pekee ambaye anaweza kuingia katika mzunguko tisa ya awamu ya mapigo tisa ya radi.
Anjiu dakika ileile aliangalia mavazi ya Roma na kumfanya amwangalie kwa macho yaliojaa kejeli.
“Ni ujasiri wa namna gani uliokuwa nao , nadhani tayari umemuua Laofi”Aliongea.
Kauli yake ile ilimshangaza Roma ambaye alianza kuhisi hisia zisizokuwa za kawaida.
“Ulijua tokea muda mrefu?”Aliuliza Roma.
“Unanichukulia mwepesi , unadhani nitaacha kuwa makini baada ya kile ulichokifanya katika miliki ya Kekexil , unadhani naweza kufeli kulinda miliki yangu?”Aliongea
Dakika ileile ma elfu ya majini yalitokeza kila pande katika makao makuu hayo ya miliki na Roma aliweza kuhisi uwepo wao kutokana na msuguano wa nguvu za kijini .
Kufumba na kufumbua majini wenye vyeo vya juu katika miliki hio walikusanyika nyuma ya mkuu wa majini Anjiu. Huku walinzi kutoka katika kila familia wakimzingira Roma na Rufi.
Zianji , Leiana , XiaoXiao na Lahani na wengine wote walikuwepo , dakika ambayo Lahani alimuona Rufi na Roma hasira zilijidhihirisha kwenye macho yake.
Upande wa XiaoXiao aliishia kuziba mdomo wake kwa mshangao akiwa haamini kile anachokiona.
Kwa kutumia mkono tu Jini Anjiu alianza kusambaza sauti yake katika makazi yote ya majini katika eneo hilo la makao makuu.
“Kila mmoja na anisikilize , huyu ni mwizi ambae amemuua Guru mkuu Tigola wa Kekexil, jina lake ni Roma Ramoni kutoka dunia ya binadamu na Rufi ni mpenzi wake , alitumia hila na kumuua mtumishi Lao na mzee wetu mkuu Laofi mapema ya leo , hajaishia hapo tu bali pia ameiba hazina zetu ndani ya jengo la kutengenezea vidonge na kuuwa majini wenzetu zaidi ya kumi na mbili na sasa anajaribu kumtorosha mfungwa wetu Rufi kutoka hapa”
Maneno ya mkuu huyo wa majini yalifanya kila jini alieweza kusikia katika ngome hio kushikwa na mshituko.
Hakuna ambaye aliamini Laofi alikuwa ameuliwa na Roma , mzee ambaye alikuwa akiheshimika kwa uwezo wake wa levo ya maji ya kiroho.
Mara baada ya Zianji kusikia kauli hio alijikuta akipauka mwili , na alijikuta akiangalia mavazi ya Roma.
“Huyu binadamu anao uwezo mkubwa wa nguvu za mbingu na ardhi na anamiliki Dhana ya hatari ya Chungu cha maafa , haina haja ya kujitoa kafara bila maana yoyote na mimi kama mkuu wa miliki hii nitamuadhibu”
Maneno ya jini mkuu Zianji yalifamfanya kila jini aliemsikia kuwa na heshima juu yake.
Malezo yake ya kuchukua hatua zidi ya mwizi yalikuwa yamemjengea heshima kati ya majini hao kwa kuwazuia kutotoa kafara maisha yao , kwani kama mtu huyo alikuwa na uwezo wa kumuua Laofi ilimaanisha kwamba wao hawakuwa na uwezo wa kudili nae hata kwa kuunganisha nguvu.
Upande wa Roma alikuwa na hasira kwa kuona kila alichokuwa akifanya alikuwa akijiingiza ndani ya mtego aliowekewa na Anjiu.
Laofi alikuwa ni gugu katika utawala wa jini Anjiu na kutokana na kukosa sababu ya kuweza kudili nae basi aliacha Roma amsaidie kufanya kazi hio na mara baada ya hapo alijitokeza baada ya Roma kuiba ndani ya jengo la kutengenezea vidonge ili amkamate akiwa na ushahidi na baada ya hapo amshughulikie ili ajichukulie umaarufu na heshima.
Roma aliishia kutoa kicheko kutokana na maneno yale licha ya kwamba alikuwa na hasira kwa kuingia mtegoni.
“Hakika uvumilivu wako sio wa kawaida , kwasababu ulishajua tokea muda mrefu nilichomfanyia mtumishi Lao lakini pia ukajua lazima nitamshambulia Laofi basi lazima utakuwa pia unajua uhusiano wa kimapenzi uliopo kati ya mke wako na Lao ,Zianji na Laofi , umesalitiwa kwa zaidi ya miaka na sasa unajaribu kunichokoza waziwazi hahaha…huna aibu”
“Whoaa…!!!”
Kila jini ambaye amesikia maneno hayo alijikuta akitoa mshangao kutokana na kile Roma alichosema.
“Acha kutafuta namna ya kujiokoa kwa kuongea upumbavu , umemuua Lao na Laofi na sasa hivi unamsingizia mke wangu na Zianji , unafikiri unaweza kuondoka hapa kwa kuongea huo ujinga?”
Baada ya kuongea maneno wale wazee na raia wa miliki hio waliona lazima Roma anadanganya hivyo walimuamini mkuu wao na kumwangalia Roma kwa macho ya kimauaji.
Zianji alikuwa akitoa kindoo cha jasho na kutokana na mambo kufikia hatua kama hio alijua lazima kaka yake alikuwa akijifanyisha hajui kinachoendelea na kumtetea kwasababu Roma hakuwa na ushahidi kwa wakati huo.
Lahani na Xiao walikuwa na muonekano tata katika nyuso zao mara baada ya mama yao kuhusishwa kufanya Dhambi na mmoja ya wanafamilia.
Roma alishangaa kwa namna ambavyo Anjiu alipotezea swala hilo bila ya kuonyesha hali ya kukasirika na alijikuta akikosa usemu na alijuliza ulikuwa ni uungwana au ndio kwamba anafurahia kusalitiwa.
Ghafla tu muda uleule Anjiu alitumia uwezo wake wa kijini kuongea na Roma bila ya wengine kusikia.
“Wewe mtukutu umenidharau sana , hivi unafikiria Leiana ataniathiri kwa matendo yake , ngoja nikuambie ana cheo cha kuwa mke wangu tu lakini sijawahi kumchukulia kama mwanamke wangu hivyo kwanini nijali kama ananisaliti , kama unataka nikupunguzie adhabu rudisha mbinu ya Andiko la Urejesho wa azimio maana hapa huwezi toka kwani upo kwenye miliki yangu”
Hakuna jini ambalo lilikuwa likisikia kutokana na kwamba wote uwezo wao ulikuwa wa chini sana.
Roma alishangazwa na kauli yake mara baada ya kuona sasa hajamuathiri kwa namna yoyote Anjiu, alikuwa akiongea ukweli kabisa hakuwa akimchukulia Leiana kama mke wake hivyo hakujali kupigwa mtungo na mdogo wake na majini wengine katika miliki , ndoa yao ilikuwa ni ya maneno tu , Roma alijiona ni mjinga na alipaswa kujua jini mwenye nguvu kama huyo asingeshindwa kuona kile kinachoendelea.
“Si nilishakupatia andiko , au ndio umeshindwa kujua kama ni halisi au ni feki?”Aliongea Roma akimjibu.
“Tunazo mbinu nyingi za mafunzo ya kijini katika miliki yetu kuliko hata miliki zote katika ulimwengu huu , ulichonipatia licha ya kutokukamilika ni mbinu tunayoita hatua tisa za Andiko la Ahadi, unaniona mimi ni mjinga”
Roma alishangazwa na kauli yake , Hatua tisa ya Andiko la Ahadi ni kitu gani au ni kama vilevile ilivyo kwa miliki ya Kekexil kuwa na andiko lake lakini hawajui maana yake.
Roma alishangaa na kujiuliza kwanini mbinu yake ya Andiko la urejesho kila mahali inaitwa majina tofauti tofauti au ni kwamba kuna maana ambayo hajawahi kuijua iliopo nyuma ya andiko hilo , je kama ni hivyo Andiko lilitokea wapi?.
Roma mara baada ya kuona Anjiu hakuwa akiamini maneno yake hakuona haja ya kumuaminisha kwani kama ni andiko ni kweli alimpatia lakini ilionekana lilifanana na hatua tisa za mbinu ya ahadi kama alivyosema.
Muda uleule Roma macho yake yalikwenda kutua kwa jini Lahani aliekuwa nyuma ya baba yake.
Ijapokuwa hajawahi kumuona ana kwa naa lakini aliweza kumfahamu kutokana na chuki iliokuwa imepamba uso wake.
Muda huo Roma alimuona Lahani kama mfu kwa kile alichomfanyia mpenzi wake Rufi.
Kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa utambuzi palepale jini Anjiu alijua nini ambacho Roma anaangalia.
“Lahani ondoka hapa”
Aliamuamrisha mtoto wake na kumfanya kushangaa huku akijiuliza baba yake anamaanisha nini kumpa agizo hilo.
“Haha… una uhakika anaweza kunitoroka?”
Sekunde ambayo Roma anatamka kauli hio alikuwa ashachomoka alipokuwa amesimama na kumsogelea Lahani kwa spidi.
Ndio muda ambao Lahani alipatwa na kiwewe na mshangao kwa kujiuliza inakuwaje anataka kumuua mbele ya baba yake na majini wote hao, haogopi kifo.
Lakini ukiachana na mawazo yake aliweza kugundua mkandamizo wa nguvu za kijini kutoka kwa Roma ulikuwa ni mkubwa mno na kumuogofya na kujiuliza ilikuwaje Rufi akaja kukutana na huyo kichaa , alijiambia amewezaje kufikia hatua hio ya nguvu za kijini kwani anaonekana kuwa katika umri sawa na yeye.
Lahani alikuwa katika hali ya woga mkubwa mno na akili yake ilikuwa ni kama imeshikiliwa na Roma kwani alishindwa kuchuukua maamuzi ya kukimbia kama alivyoamrishwa na baba yake.
Lakini Anjiu alikuwa ashaliona hilo hivyo alimzingira Lahani na ngao ya kijini na kufanya majini waliokuwa wakiangalia tukio hilo kupatwa na ahueni.
“Unathubutu vipi kwenda kinyume na maneno yangu , unadhani utaweza kushindana na mimi kwasabbau ya hicho chungu chako cha maafa?”Aliongea Anjiu na palepale aliinua mkono wake juu kama vile anapokea kitu hewani na kitenesi cha mwanga kama wa moto wa Zambarau kilitokea na sekunde ileile kitenesi kile kibadilika umbo na kumsogelea Roma kama vile ni boriti ya mwanga wa Laser.
“Pumbavu nani kasema nitatumia Cauldron?”
Roma na yeye alijibu kijeuri wakati akishuhudia nguvu ya shoti ile iliokuwa kama vile ni radi na Roma hakutaka kujaribu bahati yake kuacha imguse katika mwili wake kwani hakujua nguvu yake ikoje na palepale na yeye alitoa moto wa mchanganyiko wa rangi nyeupe na elementi za radi ya zambarau na kurushia lile shambulizi na sekunde ambayo shambulio la Anjiu linakutana na siraha ya Roma ya kijini palepale boriti yake ya moto ilipanguliwa na kusambaratishwa bila hata ya kumfikia.
Mng’ao wa rangi nyekundu na zambarau ulimulika eneo lote huku nguvu yake ya kijini ikiwaogofta majini waliokuwa karibu na kuwafanya wakimbie kwenda mbali.
Roma mpango wake ni kupigana na Anjiu kwa kutumia chungu lakini alikipa maagizo ya kumlinda Rufi kwani hakutaka majini wengine kumshambulia wakati akiwa bize katika kupambana na Anjiu.
Sasa mara baada ya Roma kuona Lahani alikuwa mbele yake , hakutaka kupoteza fursa hio kumshikisha adabu kwa kile alichomfanyia Rufi kwani anaweza asimpate tena kama akimuacha.
Kwa mzunguko mmoja tu wa mashambulizi sasa Roma aliweza kujua uwezo halisi wa Jini Anjjiu, kimahesabbu Roma alikuwa katika levo ya mapigo tisini na tisa ya radi ya Zambarau na Anjiu yeye alikuwa mwishoni mwa levo ya maji ya upako hivyo kwa haraka haraka ni kwamba hamuwezi Roma, lakini licha ya hivyo nguvu zake za kijini zilikuwa kubwa mno kuliko jini yoyote ambaye yupo katika levo ya majji ya upako.
Moto wa rangi ya zambarau wa Roma licha ya kwamba ulikuwa na nguvu kuliko moto wa radi ya Zambarau wa jini Anjiu, haukumpa nafasi ya juu katika kushinda.
“Usije kujaribu”Aliongea Roma kwa nguvu mara baada ya kuona Lahani anataka kukimbia.
Na Roma alizunguka kama vile ni mwanariadha na kurusha moto wa rangi ya bluu uliiokuwa katika maumbo ya nyoka kumfukuzia Lahani.
Lahani hakuwa na uwezo wa kumshinda Roma katika spidi ya mashambulizi yake na ni sekunde tu aliweza kuhisi nguvu ya ajabu ukimsogelea kwa nyuma na alijikuta akipagawa lakini baba yake alikuwa na spidi sana kwani palepale alitupia boriti za moto wa kimaajabu na kwenda kuzuia mashambulizi ya Roma
Kilichosikika hapo ni ngurumo tu kama vile anga linataka kudondoka huku nguvu ya moto ule wa vinyoka ulififia.
Jambo lile lilimtia hasira Roma , ijapokuwa moto wa Anjiu haukuwa na nguvu lakini ulikuwa na masafa ya maajabu ambayo yalikuwa yakiingiliana na moto wake wa rangi ya bluu.
“Mshindani wako ni mimi”
Aliongea Anjiu mara baada ya kutokea mbele ya Roma huku akimrushia mashambulizi ya nguvu za kijini yalioambaana na moto wa radi ya zambarau akimlenga Roma kichwani.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Roma kukutana na mshindani mwenye spidi namna hio na kama sio wepesi wake wa kuzuia na kukwepa pengine mashambulizi yale yangemfikia , lakini tofauti na kuwa na wasiwasi Roma alifurahi.
“Nice , wewe ndio umejileta mbele yangu”
Aliongea Roma na palepale madonge ya maji ya upako yaliokuwa kama vile ni mapovu yalianza kumtoka Roma na kwenda kumshambulia Anjiu na Lahani kwa wakati mmoja.
“Maji ya upako!!”
Kutokana na umbali wao kuwa karibu sana ilikuwa ngumu kwa Anjiu kukwepa maji hayo ya kiroho kutokana na athari zake lakini alikuwa mepesi sana kwani aliruka na kwenda kutua upande mwingine.
Miondoko yake ilikuwa rahisi mno kama vile ni spidi ya shoti za umeme na aliruka na wakati uleule kuachia moto wa radi ya zambarau kwenda kwa Roma na kumpiga kwa pembeni.
Roma mara baada ya kupigwa na ule moto wa radi palepale alisogea mita hamsini hivi kurudi nyuma huku maji yake ya upako yakisambaratishwa.
Upande wa Lahani mara baada kwa shida sana kukwepa mashambulizi ya Roma alijikuta akishikwa na woga usiokuwa na kifani , kama angeguswa hata na tone moja tu la maji hayo basi angepotezwa mazima.
“Pumbavu!”
Roma alitingishika kwa hasira kwani hakutegemea mashambulizi ya Anjiu ya radi ya zambarau kuwa na aina flani hivi ya masafa(freuency) ya ajabu lakini pia spidi yake kuwa kubwa mno na kujiongeza yenyewe , yaani shambbulizi lake lilikuwa na spidi ndogo kuliko moto huo na kumfanya shambulizi lake kumkosa Lahani na wakati huo kupokea shambulizi kutoka kwa Anjiu.
Ngozi yake iliwasha kila mahali na sehemu ya shati lake lilikuwa limechanika lakini kwa bahati nzuri utimamu wa mwili wake ulikuwa sio wa kibinadamu hivyo hakuumia.
Roma mara baada ya kugeuka aligundua Lahani amefanikiwa kukimbia na ilikuwa ngumu kumfikia tena.
“Pumbavu nimremruhusu yule msheni kuniponyoka”Aliongea Roma huku aking’ata meno yake kwa hasira na msisimko wa nguvu ya kimauaji ulianza kumvaa palepale.
Majini wa miliki hio walikuwa wakiangalia kwa hofu kutoka kwa mbali na mara baada ya kuona shambulizi la mkuu wao limempiga Roma wote kwa pamoja walishangilia.
Kuhusu XiaoXiao aliishia kutoa pumzi ya ahueni mara baada ya kaka yake kukimbia na sekunde iliofuata wasiwasi wake aliuelekezea kwa Roma na kisha akageuza uso wake kwa baba yake na katika hali hio hakuwa na chakufanya , ilionyesha dhahiri hakutaka baba yake kushindwa na pia hakutaka Roma kushindwa na kufa mbele yake,mwenye alishangazwa na hisia hizo.
“Nini tena , hicho ndio kitu pekee unachoweza kufanya lakini bado unajaribub kumua mwanangu huku huwezi hata kutoroka hapa”Aliongea Jini Anjiu kwa kejeli.
“Hakuna shida , nitakuua wewe kwanza na baada ya hapo nitamuua yule mshenzi”Aliongea Roma na sekunde hio hio alimsogelea Jini Anjiu kwa spidi huku mkono wa kulia akiwa na shambulizi la moto wa bluu na upande mwingine akiwa na shambulizi la moto wa zambarau.
Anjiu hakutaka kuzembea na kutokana na kumiliki radi ya rangi nyekundu iliokuwa imemzingira kama ngao aliamua kukumbana na mashambulizi ya Roma ya moto huku akitaka kutumia fursa hio kumpiga Roma na shambulizi la kushitukiza.
Mapema tu muunganiko wa moto na radi ulionekana angani na wimbi la nguvu za kijinni ulipasuka kwa wakati mmoja na kusababisha majini ambao walikuwa na uwezo mdogo kukimbilia mbali zaidi.
Wote waliishia kujiondolea ule woga kwa kile kinachoendelea kwani kila mmoja alikuwa na hamu ya kuona mapigano kati ya washindani wawili ambao wote wapo katika levo zinazokaribiana.
Ijapokuwa Roma moto wake wa bluu na Zambarau ulikuwa na nguvu lakini ulikingwa na mashambulizi ya shoti za mwanga wa zambarau na kuzimshwa na kwa kuangalia tu aliona hana uwezo wa kushinda kwa mbinu hio.
Rufi ambaye alikuwa akiangalia kila kitu alijihisi moyo wake kuuma na dakika ileile alikuja kupata uelewa wa jambo.
“Hubby kuwa makini hio ni mbinu ya juu ya kijini ya Xia ifahamikao kwa jina la Radi mshale wa zambarau uvukao anga , ni muunganniko wa atomu za madini na moto na uwezo wake ni kusambaratisha kila aina ya shambulizi , mbinu pekee yenye safu ya juu ndio inayoweza kupita”
Roma mara baada ya kusikia maelezo hayo palepale sasa alishaelewa na kujua kumbe huo ndio mtego wa huyu jini mzee ngoja sasa amuonyeshe.
SEHEMU YA 722.
Roma mpango wake ilikuwa ni kutumia uwezo wake wa kijini ili kumshinda Anjiu lakini hakuweza kuelewa, ijapokuwa mashambulizi yake ya radi yalikuwa na ukubwa kiwango flani basi kama atamshambulia kwa pande zote Anjiu hatokuwa na uwezo wa kuzimisha mapigo yake yote.
Kwa wakati mmoja hakuamini kama Anjiu alikuwa na uwezo wa kuhimili maji yake ya upako kama yatamgusa.
“Haha.. unaonekana kujua vitu vingi”Aliongea Anjiu huku akimwangalia Rufi.
“Zianji hebu leta hao majini wote waliopo levo ya maji ya barafu wavunje ulinzi wa nguvu ya Chungu”
Zianji ambaye alikuwa amesimama kwa mbali palepale alielewa uhalisia ulivyo , mwanzoni alitaka kushikirikiana na Laofi katika kumshambulia Anjiu kaka yake lakini wakati huo Laofi alikuwa amekwisha kufa hivyo alipaswa kusikiliza maagizo ya Anjiu kama anataka kuendelea kuishi kwa amani.
Baada ya macho yake kutua katika sura ya Rufi ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa nguvu ya chungu cha maafa , alitoa taasamu la kejeli na aliongoza dazeni ya majini ambao wapo katika levo ya maji ya barafu kwa ajili ya kukishambulia.
Miliki hio ilionekana kuwa na mbinu nyingi za mafunzo ya kijini na mashambulizi mbalimbali yalirushwa kuelewa eneo ambalo Rufi alikuwa amesimama akipewa ulinzi na Caudron.
Chnngu kile kiliweza kumeza kila aina ya mashambulizi lakini sio yote na kilianza kupata athari na nguvu yake ilianza kufifia.
Roma alikunja ndita na alikumbuka kama chungu hicho kikiendelea kuwa katika hali ya ki ulinzi kitakuwa na uwezo wa kuhimili kwa muda mrefu kidogo hivyo hana haja ya kuwa na wasiwasi.
Baada ya kupatwa na wazo hilo palepale alikusanya nguvu kubwa ya andiko la urejesho na kuunganisha na nishati ya mbingu na ardhi na kuanza kumzingira kwa ukubwa.
Na palepale aliamua kupambana na moto wa radi ambao unamshambulia bila ya kukoma , muda huo huo Roma alitengeneza donge kuubwa la maji ya kiroho ambalo lilikuwa likipanuka kwa spidi kubwa mno kiasi cha kufikia saizi ya futi kumi.
Lilikuwa kama puto kubwa ambalo linanesa nesa hewani na halikuweza kupasuka kila baada ya kukutana na mashambulizi ya radi.
Dakika ileile majini wote walianza kupatwa na hofu na ilikuwa ni kama vile kitu cha ajabu kina wavamia kutoka juu mbinguni.
Jini Anjiu palepale alijikuta akisawajika uso kwa kushindwa kuamini Roma alikuwa na uwezo wa kukusanya kiasi kikubwa hivyo cha maji ya kiroho kwani ilihitaji nguvu kubwa mno za kijini.
Chini yake kile chungu cha chuma kilikuwa kikitoa mng’ao kila mara baada ya kumeza mashambuizi na kuendelea kumlinda Rufi na mfululizo wa milipuko ya Dhana haikuonekana kuwa na mwisho na kumfanya Rufi kujihisi anakwenda kua majivu muda wowote , lakini kwa wakati huo hakuwa na jinsi zaidi ya kusimama chini ya chungu hicho huku akiwa amafumba midomo yake asipige yowe.
Kwa bahati nzuri ni kwamba kadri walivyokuwa wakikishambulia ndio kilivyokuwa kikiongezeka nguvu kwani kilikuwa kikinyonya nishati yao na sasa kilianza kunesa nesa hewanni na nguvu yake kupanuka zaidi na kuwafanya wale majini kushindwa kuvunja fensi yake ya ulinzi.
Anjiu alikuwa makini mno huku akiendelea kushambulia lile donge la maji ambalo Roma ametengeneza na moto wake wa shoti za radi ya Zambarau huku akijiuliza ni kitu gani ambacho Roma anapanga kufanya muda huo na maji yote hayo.
Lakini dakika hio hio Roma sasa alijua hatimae muda umewadia na palepale alilirusha lile donge la maji kwenda juu zaidi ya angani huku akipiga kelelele ya ‘Nendaa’
Baada ya kufika angani palepale alilipiga na mshale wa nguvu y a kijini na likapasuka kama vile ni puto ambalo lina maji ndani yake na mvua ya maji ya kiroho ilianza kunyesha katika mzingo wa kilomita mia moja.
Mpasuko ule ulisababisha matone mengi kudondoka na kusafiri kwa kutumia nguvu ya kijini na hakukuwa na uwezekano kwa majini wa levo za maji ya barafu kuweza kukwepa matone yale kwani ilikuwa ni sawa na kukwepa mvua bila ya mwamvuli.
“Arghhhh…!!!”
Vilio viliweza kusikika mara baada ya matone yale kugusana na miili ya majini waliopo katika levo ya maji ya barafu na kuanza kuwayeyusha.
Dakika ileile Chungu chenyewe hakikukaa kizembe kwani kilitumia kama fursa na kuanza kunyonya nguvu zao za kijini kwa spidi kubwa mno huku kikizungukwa hewani kama pia.
Muda huo huo Roma na yeye aliweza kupokea shambulizi la radi ya zambarau kutoka kwa Anjiu lakini shambulizi hilo halikumuua kama ambavyo shambulzi lake limewamaliza majini wale wa levo ya maji ya barafu.
Zianji ndio peke yake ambaye aliweza kuepuka kwani uwezo wake ulikuwa wa juu hivyo alijitengenezea ngao kama mwamvuli na kisha kukimbia na muda huo Anjiu na yeye aliweza kupokea matone mengi ya maji ya kiroho lakini hakuathirika kwani nguvu zake za kijini zilikuwa zimenzingira kwa kumtengenezea ngao.
Lakini muda huo mashambulizi yake yalikoma kwani utimamu wake wa mwili haukufnana na wa Roma hivyo alianza kupambana na maji yale yasimdhuru.
Roma pia hakuwa na mpango wa maji yake ya kiroho kumuua na alichokuwa amepanga ni kuondoa hao majini wasumbufu wa Xia ili kuwaelimisha kwamba hayo sio mapigano ya levo zao.
Mara baada ya kuona Anjiu ameacha kushambulia alichukulia fursha hio na kuanza kumshambbulia kwa kasi na maji ya upako Anjiu.
Jini Anjiu aliona kukaa sehemu moja na kuangalia namna ambavyo ngao yake inayeyushwa taratibu taratibu na maji ya upako aliona ingekuwa ni chaguzi mbaya sana.
Hasira ilimshika palepale katika macho yake sio kwasababu ya hila za Roma lakini vilevile kutokana na kuua majini wengi kwa wakati mmoja.
“Unathubutu vipi , unakitafuta kifo”
Kwa wakati huo alikuwa na hasira mno kiasi cha kutokujali mbinu ya Andiko la Urejesho tena na alichotaka nikumuua Roma tu.
“Pata kionjo cha moto wangu wa ndege wa miguu mitatu , Moto wa ukweli, Ndege wa Dhahabu”
Palepale moto ambao ulikuwa ukifanana na mwanga wa jua ulionekana mbele yake na kutengeneza umbo la ndege wa miguu mitatu(Three Legged Golden Crow) , miguu yake ilikuwa mirefu saizi ya futi tatu huku mabawa yake yakiwa pia katika umbo kubwa la kimaajabu.
Na mwanga kama wa jua ulianza kuwaka kwa kuongezeka katika eneo hilo na kumeza giza lote na ndani ya sekunde tu yale maji yake ya upako yalikaushwa palepale.
Muda huo Jinni Ajiu alikuwa amebadilika kabisa na kuonekana kama vile ametengenezwa kwa moto wa jua.
Roma alikuwa ashasikia hio mbinu kutoka kwa Rufi hivyo alishaielewa kwa kiasi lakini kwa wakait huo hakuweza kuamini ilikuwa ikiogopesha kiasi hicho.
Aina ya moto huo wa kimaajabu ulikuwa ukikaribiana na nguvu halisi ya moto wa jua.
Sasa Roma hatimae alijua ni kwanini Rufi alisema ni Jini huyo pekee ambaye aliweza kumaster mbinu hio.
Lakini kitu kingine ambacho Roma aliweza kujua ni kwamba licha ya kwamba ni mbinu yenye nguvu lakini ukali wake unategemeana na nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi na kwa jini kama Anjiu ambaye ndio kwanza yupo mwishoni mwa levo ya maji ya upako hakuwa na uwezo wa kutoa nguvu yake yote.
Ndege yule ambaye alikuwa katika umbo la moto alianza kupiga piga mabawa yake , ijapokuwa ni ndege ambaye yupo katika umbo la moto lakini msuguano wa moto ule na elementi za hewa ulifanya eneo lote kusikika vilio ambavyo havikueleweka.
Roma alijaribu kumkwepa yule ndege kwa spidi lakini licha ya hivyo alijikuta akiunguzwa na yale mabawa yake na palepale alijikuta akitoa mguno wa maumivu na kuhisi ni kama vile mwili wake unachemshwa katika pipa la mafuta.
Lakini hata hivyo mafuta ya kawaida hayawezi kumpa madhara makubwa lakini maumivu alioweza kuyapata kusikia hapo yalikuwa sio ya kawaida kabisa.
Ilikuwa ni bahati kwamba uwezo wake wa Andiko la urejesho ulifanya kazi na kumponyesha ndani ya sekunde na kuondoa seli ambazo zimeunguzwa.
“Sidhani kama nitaendelea kuhimili kama nitaendelea kupokea mashambbulizi ya aina hii”Aliwaza Roma.
Kwa mara nyingine anakutana na jini ambaye yupo vizuri kuliko yeye kutokana na kutokuogopa moto wa anga wala moto wa rangi nyeupe na wa bluu, ukweli ni kwamba Roma hakuwa na uelewa wa kutosha na moto huo wa kimaajabu na hivyo aliona anaweza kuzidiwa.
Hali ya mshangao iliweza kumkumba jini Anjiu mara baada ya kuojna Roma alivyoweza kupona kwa spidi kubwa lakini haikumrudisha nyuma katika kufanya shambulizi lingine.
“Ndege wa Dhahabu wa miguu mitatu,Yang’wi katika umbo halisi , kusanyiko la ndege elfu moja!!!”
Aliongea jini Anjiu kwa sauti kama vile anaita viumbe hao na ndani ya sekunde tu kundi la ndege wengi sana ambao wapo katika maumbo ya moto walionekana wakija katika eneo hilo kwa spidi kubwa na walionekana kwa dhahiri ya macho kutokana na giza.
Majini wote wa miliki hio walijikuta wakipatwa na woga usio na kifani akiwemo Zianji mwenyewe kasoro Xiao tu ambaye aikuwa na hali ya wasiwasi mkubwa mno.
Kutokana na miliki yao kutokumbwa na adui mwenye uwezo mkubwa kwa kipindi kirefu hawakuwahi kuona uwezo halisi wa mbinu hio ya ndege wa miguu mitatu.
Roma hakuweza kupata hata muda wa kufikiria ni hatua gani afanye kukabiliana na hao ndege na palepale alijitengenezea ngao ya maji ya barafu kuzingira mwili wake kwa kujua kabisa asingeweza kuwamaliza hao ndege kwa shambulizi moja.
Lakini sasa mara baada ya wale ndege wa moto kugusana na ngao yake ya barafu iliyeyushwa palepale , licha ya kwamba baadhi yao waliweza kuzimishwa lakini ilikuwa ngumu kuzuia shambulizi hilo.
Roma alishikwa na mshangao na hakuwa na namna zaidi ya kukimbia ili kuepuka moto wao usigusane na mwili wake lakini hata hivyo spidi yao ilikuwa kubwa mno na alijua asingeweza kuwahimili kuwakwepa wote na wangemuweka kati.
Chini ardhini Chungu kilipo, Rufi alikuwa kwenye woga mkubwa mno na uso wake ulipuaka.
“Hubby chukua chungu , huna haja ya kunilinda”Aliongea kwa nguvu huku akitamani kulia.
Alijua kama Roma angekuwa akitumia chungu hicho cha maafa basi uwezo wa Jini Anjjiu ungepungua mpaka nusu yake kwasababu kilikuwa na uwezo wa kuhimili mashambulizi mengi kwa wakait mmoja.
Lakini Roma hakuwa na mpango wa kutumia chungu hicho kwani hakutaka kumuweka katika hatari licha ya kwamba alijua angekuwa na nafasi kubwa ya kushinda kama angekitumia.
Sababu nyingine ya kutotumia chungu hicho ni kwamba Anjiu bado hakuwa ametumia Dhana yoyote katika mashambulizi na alijua kama angeshindana nae kwa kutegemea chungu hicho basi anaweza kushindwa kirahisi.
Ki ufupi ni kwamba Roma hakutaka kushindana na Anjiu kwa kutumia chungu kwasababu hata yeye hatumii Dhana bali uwezo wake tu wa kijini , hivyo alitaka kama ni kumshinda basi amshinde kwa uwezo wake na sio kwa Dhana.
Sababu pia ya kutotaka kutumia chungu ni kutokana na kwamba mpango wake ni kuja kupitia mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi hapo baadae ili kuweza kuimarika zaidi na zaidi na hilo ili litokee basi anahitaji kupambana na jini mwenye uwezo mkubwa zaidi na utalaamu wa hali ya juu ili aaweze kujifunza.
Wale ndege wa miguu mitatu ambao majini huwaita kwa jina la Yang’wi baadhi yao walikuwa wakigongana wao kwa wao na kusababisha mlipiko na wengine kumpiga na kumfanya Roma kutetemeka kutokana na ukali wa moto ambao unamtengenezea majeraha.
Lakini Roma hakutaka kukata tamaa zaidi ya kutumia moto wa bluu na wa zambarau kuendelea kushambulia kwa spidi kubwa.
Roma alijua kwasababu Anjiu hakuwa na uwezo wa kumuua basi nafasi ya kupambaana nae ipo tu isitoshe hao ndege wasingeweza kuhimili nguvu yake ya mapigo tisini na tisa ya radi ya Zambarau
Lakini alipatwa na kiwewe kwasababu hakuwa na uwezo wa kujitoa katika mtego wa hao ndege kwani alikuwa akijilinda zaidi ya kufanya mashambulizi.
Walikuwa ni wengi sana na akishambulia huyu alikuwa akishambuliwa na huyu zaidi sana ni kwamba nguvu ya kiijini ya moto huo kutoka kwa Anjjiu ilionekana haina kikomo.
“Huyu mtukutu anajifanya mwamba kutotaka kutumia Dhana yake, Mkuu wetu lazima atafanikisha kumdhibiti”
“Kama tulivyoratarjia kwa jini wa kwanza kuweza kubobea katika mbinu ya Yang’wi kwa zaidi ya miaka elfu moja , kumbe hii ndio nguvu yake halisi tunayoiona, ni hivyo tu hautotoweza kufanikisha kuijua”
“Haha….huyo binadamu ni mshenzi sana ameua majini wetu wengi , anapasswa kuwa kaa la moto”
Majini hao wa miliki ya Xia walikuwa washamuona Roma kama mfu tayari , walijua kila ukinzani ambao angeweka ungekuwa ni bure tu na hakutofautiana na mnyama ambaye yupo kwenye zizi.
XiaoXiao aliishia kuweka mkono wake mdomoni bila ya kujielewa akiendelea kung’ata kucha zake kwa wasiwasi na alijiuliza huyu mwanaume mbaya ashamuumiza mara kibao kwanini bado anaonyesha kumjali.
Muda huo katika hali hio hatarishi Roma bado alikuwa na utulivu huku akifikria namna ya kudili na hao ndege wa moto.
“Sina namna nyingine lakini kwasasa napaswa kutumia ile mbinu, ijapokuwa bado haijaimarika lakini nadhani inaweza kufanya kazi”Aliwaza Roma bila ya kuelewrka ni mbinu ipi , lakini ilionyesha ni dhahiri ile siku ambayo alikuwa akifanya mazoezi aligundua mbinu hio
SEHEMU YA 723
Roma mara baada ya kuamua kutumia mbinu ya ufunuo ambayo aliweza kugundua hakuwa na haja tena ya kujizuia na palepale mkono wa kulia alitengeneza moto wa kiroho wa rangi nyeupe na kishoto kwake alitengeneza maji ya kiroho na baada ya palepale kama vile anapiga makofi aliunganisha moto ule wa kiroho na maji yale ya kiroho.
Fission(mgawanyiko) wa nguvu ya maji ya kiroho na moto wa kiroho ulikuwa ni wa hatari mno kwani ni kama vile ni rutubisho la atomu na atomu na kutengeneza nguvu ya kinyuklia lakini sasa nguvu hio kuwa kubwa zaidi ya mara kumi ya nyuklia na kutengenza mionzi ya hatari ya uyeyushaji.
Roma alipokuwa katika mafunzo alijaribu kuunganisha moto wa rangi ya bluu na maji ya upako na jaribio lake lilikubali lakini alikuja kugundua maji ya upako na moto wa upako vilikataa kuunganishika na kutengeneza kitu kama bomu.
Upotofu wa kimwili aliokuwa nao Roma haukuwa wa kawaida kwani kitendo kile cha kuunganisha nguvu mbili ambazo zinakataana zilimsababisha athari kubwa katika roho yake na kumtengenezea maumivu.
Ukweli ni kwamba licha ya kwamba mwanzoni aliona mbinu hio ilikuwa ikikataana haikumaanisha kwamba haikuwa ikifanya kazi , kilichokuwa kikimchanganya ni kwamba kuna kitu ambacho alikuwa akishindwa kuelewa kuhusu nguvu hio.
Katika spidi ya kupepesa macho , ngurumo kubwa ilisikika mara pamoja na wimbi kubwa la nguvu za kijini, palepale alifanikisha kuunganisha elementi za maji ya kiroho na moto wa kiroho na kutokea ktiu cha ajabu mbele yake.
Ilikuwa ni kama donge la moto wa rangi ya samawati na moto ule ulikuwa ni kama vile unaunguza anga na kutengeneza nguzo ya moto ambayo ilienda moja kwa moja mpaka mawinguni.
Tukio lile lilimfanya Jini Anjiu ambaye amesimama karibu kuanza kuhishi hisia za kifo kwani roho yake ilikuwa ikifurukuta na mshituko ulimshika palepale.
Wale ndege wake mfano wa kungnru waliendelea kumshambulia Roma bila kukoma na kuacha majeraha ya vidonda katika mwili wake, maumivu yale makali ya ule moto ndio ambayo yalimpatia ufunuo wa ajabu Roma , ilikuwa ni kama vile mtu anavyoamua kujinyonga na kabla ya kukata Roho anaona Jehanamu ilivyo na kutaka kughairi kufa.
Palepale alijikuta msisimko wa mwili ukiongezeka na kupitia mawazo yake tu ule moto wa rangi ya samawati uligawanyika na kuwa kama vile ni vinyoka nyoka vingi sana vyenye mabawa na kuanza kupambana na wale ndege kwa spidi kubwa mno na wale ndege walianza kukosa nguvu na kupotea mmoja mmoja.
Upande wa mita kadhaa mbali na Roma jini Anjiu alionyesha hali ya maumivu kwani yeye ndio ambaye alikuwa akiwadhibiti ndege hao kutumia nguvu zake za kijini hivyo mashambulizi ambayo ndege wake walikuwa wakipokea maumivu aliyasikia yeye.
“Inawezekana vipi!!”
Alijikuta akipatwa na mshituko usiokuwa na kifani na kukunja ngumi yake huku uso wake ukipatwa na kiwewe.
Anjiu macho yalimtoka na kuwa mekundu mara baada ya kuelewa sasa moto ambao Roma ametengeneza ulikuwa ukiharibu ndege wake na kumtengenezea kupatwa na athari kubwa katika nafsi yake.
Aliona kabisa kama mashambulizi hayo ya moto wa Roma wa ajabu ukiendelea kumshambulia basi anaweza kupoteza roho yake kabla hajamuua.
Roma ambaye alikuwa akishambiliwa na ndege wale sasa alijua walikuwa wakiathirika na wengine walikuwa wakikwepa ule moto hivyo alijikuta akiachia kicheko cha furaha.
Hakuamini angeweza kutengeneza siraha ya ajabu katikati ya maumivu ambayo ilikuwa na uwezo wa kuzima mashambulizi ya moto wa majabu uliokuwa ukizaliwashwa na dnege hao wa miiguu mitatu.
Ndege wale sio kwamba walikuwa wakijitegemea uwezo wao ulikuwa umeunganishwa na uwezo wa Anjiu , hivyo alijua fika kila kinachowapata wale ndege kina mpata na Anjiu na sio kwa namna ya kimwili bali kiroho zaidi.
Kwahio kama angeendelea kuwatumia katika mashambulizi basi atashindwa kuwadhibiti na ataishia kutumia mashambulizi ya radi wa Zambarau.
Dakika chache baadae wale ndege walianza kupoteza nguvu na kuanza kupoteza maumbo yao na kuanza kusambaa kama majivu angani na kuacha cheche pekee.
Roma alijikuta sasa akivuta pumzi ya ahueni na mara baada ya kumuangalia Anjiu sasa ule muonekano wake kama wa jua ulikuwa umepungua kabisa.
Maelfu ya majini wa miliki hio walijikuta wakishangazwa na jambo lile na kuogopa kwa wakati mmoja , hawakuamini ule moto wa ajabu uliotokea umeweza kudhibiti nguvu ya moto wa Yang’wi.
Mara sasa baada ya kuona Roma kapindua meza hakuna jini hata mmoja ambaye alikuwa na ujasiri kwenda kumsaidia mkuu wao , kwani waliona kabisa pambano hilo sio levo zao hivyo waliishia kuangalia tu bila ya kutoa msaada.
Muda uleule Roma alitumia nguvu ya andiko kuponyesha majeraha yake ya moto na mudi yake ilikuwa imeimarika huku akiwa ameshikilia moto wake wa rangi ya samawati ambao haukuwa na mng’ao wowote , yaani ilikuwa ni kama vile ni donge la moshi na hakuamini kama ameweza kupata ufunuo huo katika hali hatarishi kama hio na alijiambia mambo kama hayo hayatokei kwa bahati mbaya.
Mara baada ya kuona Rufi alikuwa salama nguvu yake ya kimauaji iliongezeka kwa kasi na sasa dhamiri yake ilikuwa ni kumuua Anjiu kwa kutumia ule moto ambao bado hakuwa akijua hata aupe jina gani na baada ya hapo amuue na Lahani.
Lakini sasa wakati akitaka kufanya hivyo alikuja kuona Anjiu hali yake ilikuwa ya ajabu kidogo , alikuwa ameshika kichwa chake huku mwili wake ukiwa umejikunja na meridiani zake za mwili zilikuwa zikipanuka kama vile ni vidonda vyenye usaha na alikuwa akitoa kilio cha ajanbu kama vile ameshikwa na ukichaa , ilionekana wazi alikuwa katika hali ya maumivu makali.
Dakika ileile michirizi ya rangi nyeusi ilianza kujitokeza katika sura yake huku nguvu ya giza ya ajabu ikianza kumtoka na kucha zake zilikuwa zikirefuka na kurudi katika hali ya kawaida.
“Baba..!!!”
Xiao ambaye alikuwa mbali alijikuta akipiga ukulele mara baada ya kumuona baba yake kuwa katika hali ile.
Wazee wengine wa miliki hio walikuwa katika hali ya mshangao pia kutokana na kile kinachoendelea na waliishia kuongea wenyewe kwa kumung’unya maneno.
Hata Roma mwenyewe alikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa , bado hakuwa amedili nae lakini amebadilika na kuwa hivyo na palepale msisimko wa nguvu za giza uliokuwa ukimtoka ulimfanya kuhisi ni kama vile kuna mahali aliweza kuhisia nguvu hio.
“Devil beast blood!!”
Roma aliongea mara baada ya akili yake kufanya kazi na kukumbuka damu iliofahamika kwa jina la Damu ya mnyama wa kishetani.
Alikumbuka kutokana na msisimko wake wa giza mara baada ya kuona ile chupa ambayo alikuwa ameipata katika hifadhi ya pete ya mtumishi Lao, lakini pia aliweza pia kusikia kuhusu hio damu ilivyokuwa ikitumika kama sumu kwa Anjiu.
Ilionekana sasa damu hio ya kishetani ya mnyama ndio ilikuwa imeanza kufanya kazi , lakini Roma alijiuliza si Laofi na wenzake walisema ingechukua miezi kadhaa mpaka kuonyesha athari zake.
Roma aliishia kumwangalia Jini Anjiu kwa mbali ambavyo alikuwa na muonekano wa ajabu, ulikuwa ni muonekano wa mshangao na sio wa wasiwasi lakini uliojaa utata ndani yake na mchanganyiko wa furaha na ufumbuzi.
Roma alijiuliza kwanini yupo vile , au na yeye pia hajui kwanini sumu hio imefanya kazi mapema.
Ukweli hapo enzi za kale katika hadithi za majini aliwahi kuwepo jini hatari sana ambaye alikuwa katika umbo la mnyama ambaye alibatizwa jina laTaowu.
Inasemekana mnyama huyu mara baada ya kuzidiwa na mashambulizi kutoka ulimwengu wa kijini alikimbilia katika ulimwengu wa kawaida katika bara la Asia
Kabla ya jiniTouwu kutorokea katika ulimwengu wa kawaida alikuwa amejeruhiwa sana na inasemekana ndio wakati ambao majini waliweza kukinga damu yake kutoka katika majeraha.
Sasa haikueleweka Taowu alikufa vipi lakini mababu wa kijini katika miliki ya Kekexil ndio ambao walikuwa na damu hio ya Taowu na ilikuwa ikirithishwa katika kila kizazi.
Ni damu ambayo ina elementi za ajabu na sumu kali sana baada ya kuingunanisha na baadhi ya elementi nyingine za sumu.
Kwa majini wenye nguvu kama Anjiu ilikuwa ngumu sana kumuwekea sumu kwani anao uwezo wa kuhisi kila aina ya nguvu ya ziada inayoongezeka katika mwili wak.
Lakini sasa likija swala la hio damu ya kishetani ya mnyama ilikuwa imetengenezwa kwa namna ambayo ni ngumu sana kwa jini yoyote kuweza kuigundua pale inapoingia mwilini.
Hivyo mara baada ya Laofi kuingia dili na jini Mohi kutoka Kekexili walimpatia mtumishi wa karibu wa Anjiu ambaye ni Lao kwa ajili ya kumuwekea katika kifaa maalumu cha kuchomea ubani.
Kwahio moja kwa moja wakati Anjiu alipokuwa akivuna nishati alikuwa akivuta hio sumu taratibu bila ya kujua kwa miaka miwili mfululizo.
Sumu hio mara nyingi inafanya kazi taratibu na kadri ambavyo alikuwa akiinusa ilikuwa ikimuathiri nafsi yake na kumfanya kuwa na hali ya ukichaa na mwishowe kwenda kinyume na masharti ya nguvu za kijini za kawaida na moja kwa moja angekosa uhalali wa kuendelea kubakia katika ulimwengu huo , kwani watu ambao wana nguvu ya giza ya ukichaa moja kwa moja walistahiri kwenda kuishi katika ulimwengu wa majini pepo au majini wakuu wa ulimwengu huo kumuua kutokana na kumuepusha kuua watu kutokana na ukichaa.
Jini Mohi alikuwa tayari kufanya dili kutoa damu hio kutoka Kekexil licha ya uadimu wake kwasababu alijua masharti yake ya matumzii yalikuwa magumu sana kwani inahitajika muda mrefu mpaka athari zake kuonekana , pili Kekexil siku zote walitaka kuona kifo cha Anjiu ili kupunaguza nguvu ya miliki hio.
Laofi na Zianji licha ya kiujua hilo hawakujali sana kwani matamanio yao ni kuwa na madaraka tu maswala ya kuwa na nguvu wangefikiria baada ya kufika katika nafasi ya juu.
Lakini ndio hivyo katika hali ya kutokutegemewa Laofi na Lao wameshakufa , hivyo ilimaanisha wasingeendelea kumuwekea Anjiu damu hio.
Lakini kwa bahati mbaya sasa Roma aliweza kuiamsha athari ya sumu hio kwa kutumia moto wake mpya wa rangi ya samawati kabla ya muda muafaka.
Roma hakutaka kuonyesha huruma kutokana na muonekano wa jini Anjiu , kwani miliki hio ilikuwa imemtesa sana Rufi na kumchukulia kama mnyama.
Katika ulingo wa kupambania uhai na kifo huruma ni sawasawa na kujishambulia mwenyewe.
Hivyo Roma hakutaka kujizuia na palepale alitengeneza moto mwingine akiwa tayari kumshambulia jini Anjiu.
“Usije kumuumiza baba yangu!!”
Ghafla tu mwanamke alievalia mavazi ya pinki aliweza kuja kutoka mbali na kusimama mbele ya jini Anjiu huku akimkodolea macho Roma.
Hakuwa mwingine bali ni Xiao ambaye alikuwa akijaribu kumzuia Roma kutokumshambulia Anjiu.
Kulikuwa na maelfu ya majini hapo ndani akiwemo Zianji lakini hakuna hata mmoja ambaye alipata ujasiri na kumzuia Roma na kumsaidia Anjiu , ni Xiao peke yake ambaye yupo katika levo ya nafsi aliepata ujasiri wa kusimama mbele ya Roma na kumzuia.
Roma alijikuta akisimama palepale na kumwangalia msichana huyo ambaye machozi yashaanza kujitengeneza katika macho yake.
Kulingana na sheria zake mtu yoyote ambaye atamzuia kumuua adui yake basi anapaswa kufa wa kwanza lakini Xiao alikuwa tofauti kwasababu alikuwa amemkosea.
Tokea mwanzo alikuwa amemdhania vibaya na kumuumiza lakini pia Rufi alikuwa na deni kwa Xiao.
Roma muda ule baada ya kugeuza macho yake na kumwangalia Rufi aliona alikuwa akitingisha kichwa akimwashiria asifanye chochote kumuumiza Xiao.
“Toka mbele yangu sitaki kukuumiza”Aliongea Roma huku akiwa amekunja ndita.
“Kuniumiza? Kuniumiza mara ngapi wakati ushafanya hivyo mara kibao, lakini bado unataka kumuua baba yangu , wewe ni mtu mbaya sana kama unataka kumuua baba yangu nitapigana na wewe kwani sikuogopi”Aliongea Xiao.
Roma aliishia kupanua mdomo wake akitaka kuongea lakini maneno yalishhindwa kumtoka , kama asingekuwa na kiburi cha kuzaliwa basi angemuomba msamaha lakini hali aliokuwa nayo wakati huo ilikuwa ni ya kifo na uhai.
Ghafla tu Anjiu ambaye alikuwa ameinama hatimae aliweza kusimama wima kwa kujikaza sana , uovu ulikuwa ukioneakana kwenye macho yake ambayo ni kama yamegeuka na kuwa ya mnyama.
Ilionekana bado alikuwa akipambana na nguvu ya ushetani wa mnyama Taowu kwa kutumia utayari wa ufahamu wake,kilichokuwa kikimtokea ni kama Roma alivyokuwa akipambana na uchizi wake.
Dakika hio hio Anjiu aliweza kuzuia ule ukichaa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kijini na aliinua uso wake na kumwangalia binti yake ambaye hakuwa na woga kusimama mbele ya Roma.
Ijapokuwa Anjiu alisifika kwa na ukiburi lakini matendo ya Xiao ni kama yalimgusa na kujiuliza huyu ni binti yake kweli ambaye anafanya vitu vya kijinga kwa kutaka kushindana na mtu ambaye yupo juu ki uwezo.
Licha ya kujiuliza maswali hayo hakuweza kujizuia kujisikia vizuri kwa kile mtoto wake ambacho alikuwa akitakakufanya.
Hakuwa na uelewa ni wapi anaelekea tokea muda ambao aliamini ufunuo mkubwa aliokuwa nao ulikuwa sio juu ya huruma na aliamini mtu mwenye nguvu ndio anaeweza kuongoza dunia.
Kwake kinachojulikana kama ujamaa, urafiki na upendo si chochote bali mawazo potofu yasioendeshwa na akili na ndio chanzo cha udhaifu.
Kidonge kimoja tu cha daraja la juu kinaweza kumgeuza rafiki kuwa adui, uongozi unaweza kugeuza ndugu kuuana lakini mara baada ya kupanda juu zaidi kilevo kila kitu kilionekana kuwa si kitu mbele yake.
Alitafuta ufunuo bila kujali chochote anachokiona kama kizuizi na akapambana wazi na kwa siri kwa njia yoyote ile inayohitajika ili kuvunja vifungo vyote vya mafanikio.
Na ni katika wakati huo hatimae kile alichokuwa akikitafuta kilikuwa wazi.
Ghafla alihisi hali ya akili ya ajabu ambayo haijawahi kumtokea hapo awali ,maumivu yalioigusa roho yake yalioletwa na nguvu ya damu ya mnyama wa kishetani yalikuwa makali mno kiasi cha kushindwa kuvumilia
Miridi za mwili wake zilikuwa zikiuma kama vile alikuwa akichemshwa katika sufuria.
Katika hali hio ya maumivu hatimae mawazo mbalimbali yalianza kupita moja baada ya jingine ndani ya sekunde moja tu.
“Xiao ondoka nenda mbali…”Aliongea Anjiu katika sauti hafifu.
“Baba!?”
Xiao aligeuka na kumwangalia baba yake katika hali ya tahamaki na akajaribu kumpa baba yake mkono lakini aliishia kusukumiwa mbali.
“Nimesema ondoka”
Kutokana na kusukumwa na nguvu iliokuwa kubwa kiasi ilimfanya kwenda mbali lakini kutokana na hofu Xiao hakutaka kusogea mbele tena.
Hatimae Anjiu alisimama katika urefu wake tena na kumwangalia Roma kwa hali ya tabasamu la ajabu.
Roma palepale alihisi kuna kitu hakipo sawa ,Jini ambalo lipo mbele yake halikuonekana kama limepatwa na ukichaa kutokana na damu bali uwezo wake umeongezeka zaidi na zaidi ndani ya sekunde tu.
“Kumbe ndio ilivyo … hatimae nime elimika”
Tabasamu hafifu lilimtoka akionyesha hali ya kuridhika , tofauti na kumshambulia Roma alinyanyua kichwa chake juu na kunyooosha mikono yake yote angani kama vile mtu anaepokea baraka kutoka kwa Mungu au mtu aneonyesha ishara ya shukrani.
Mkondo wa nishati giza palepale ulianza kujikusanya katika mwili wake lakini haikumsababishia madhara kama ilivyokuwa ikitegemewa bali muda huo ilikuwa ni kama nguvu ya kijini.
Isitoshe damu ya mnyama wa kishetani ilitoka kwa jini wa kishetani afahamikae kwa jina la Taowu , ijapokuwa ni kiasi kidogo tu lakini ni cha thamani kutokana na uhalisi wake.
Muda huo ni kama sasa ile damu ambayo ilikuwa ndani ya mwili wake imeungana na mwili wake na kuwa sehemu moja ya kimwili.,
Unachopaswa kuelewa ni kwamba katika ulimwengu wa kiroho damu ina nguvu sana kuliko kitu chochote na ndio uhai wenyewe , hivyo ni sawa na kusema damu ina unganiko la nafsi ndio maana damu hio malengo yake ilikuwa ni kumfanya Anjiu kuchanganyikiwa kwa kuvamiwa na pepo kichaa.
Lakini sasa tofauti na mategemeo ni kwamba ile roho chafu ambayo ilikusudiwa kumuumiza hatimae imepatana na roho yake.
Roma sasa aliweza kuona nguvu ambayo ilikuwa ikimtoka Anjiu katika mwili wake ilikuwa ni kubwa sana kuliko mwanzo
Roma hakutaka kumpa nafasi kuendelea kupona na kutoboa na palepale alimshambulia Anjiu na ule moto mweusi
Lakini sasa Anjiu hakuonyesha kukwepa kabisa shambulizi lake na palepale alianza kumung’unya maneno kama anasali.
“Askari wa kiroho pepo wa ndani!”
Mara baada ya kuongea ile kauli Roma aliweza kuona Anjiu ni kama vile kivuli cheusi kinamtoka , Roma mara baada ya kuangalia kwa umakini aliona ni kivuli cha Jini Anjiu mwenyewe.
Ilikuwa ni kama vile amejigawa kati na kubadilika na kuwa jini katika umbo la roho.
“Boom!!!”
Dakika ileile ule moto wake ulivyokwenda kukutana na askari pepo ,shambulizi la Roma lilipotea palepale bila ya kuleta madhara.
“What the hell!!”
Roma alijikuta akitamka kauli hio mara baada ya kushangazwa na jambo lile lakini jini Anjiu hakuonyesha kabisa kushangaa.
“Miaka nane iliopita uwezo wangu uliweza kufika katika mwishonni mwa levo ya maji ya kiroho lakini nilishindwa kuingia katika Dhiki tisa za mapigo ya radi , sikuweza kwasababu mwili wangu haukuwa na uwezo wa kuhimili mapigo, ili kuzuia athari katika mwili wangu nilihamisha uwezo wangu wa ziada na kulipa nguvu pepo la ndani ili kuendelea kutafuta njia , baadae wakati nikiendelea kutengeneza Dhana nilikuja kutengeneza nafsi yangu ya pili inayofanana na mimi na kuipa jina la Askari wa ndani wa kipepo ambaye umemuona , hio ni Dhana yangu ya kijini , ijapokuwa ni ya daraja la juu ila kadri uwezo wangu unavyoongezeka itaweza kubadilika kutoka kuwa nguvu ya kipepo na kuwa nguvu ya nishati ya mbingu na ardhi”
Maneno yake hayakumshangaza Roma tu bali yalishangaza majini wote ambao walikuwa katika eneo hilo mara baada ya kuona mkuu wao alikuwa amefikia kiwango hicho cha uelewa .
Alichokifanya Anjiu ni kulipa nguvu pepo la ndani ya mwili wake na kisha akaligeuza kuwa Dhana na hapo ndipo alipotoa uwezo wake wa kijini kwenda katika hilo pepo.
Alifanya hivyo kutokana na kwamba mwili wake ulikuwa Dhaifu kuhimili mapigo tisa ya radi , hivyo ili kuepuka adhabu ya mbingu ndio akaamua kutumia njia hio ili kuendelea kutafuta suluhisho la kuimarisha mwili wake.
Sasa uelewa huo wa kugeuza pepo la ndani kama Dhana ni uwezo wa hali ya juu sana katika ulimwengu wa watu na majini ambao wanavuna nishati za mbingu na ardhi na ili kufikia hapo inamaana kwamba uwezo wako haupo tena katika levo ya maji ya kirho bali ni zaidi ya hapo.
Boom .. Boom.. Boom !!!”
Wakati kila mmoja akiwa katika hali ya mshangao anga lilifunikwa na wingu kubwa ambalo lilikuwa likizungukwa kwa kasi kubwa mno na kusababisha ngurumo za radi , ilikuwa ni kama vile ni ngurumo za wanyama wengi wakitoa sauti kwa pamoja.

SEHEMIU YA 724.
Radi ya mbingu hatimae inapiga tena , Roma ambaye ashawahi kupitia steji hio alikuwa na uelewa na tukio hilo.
“Haiwezekani kwanini ndio anaingia katika levo ya mapigo tisa ya radi wakati huo wakati yeye tayari ashapitia mapigo tisini na tisa lakini akawa na uwezo wa kumpa ushindani mkubwa?”
Ki ufupi ni kwamba Anjiu hakuwa amepitia mapigo ya radi bado licha ya kwamba uwezo wake ni wa juu , alikuwa katika levo ya kuiepuka Dhiki katika levo ya maji ya kiroho hivyo uwezo wake ulikuwa ni kama unalingana na Roma.
Hakuweza kupitia Dhiki kwasababu hakuwa na njia ya kuweza kuhimili mapigo ya radi hivyo kutengeneza kwake Dhana inayofanana na yeye ni kwamba angeruhusu yule askari wake wa kipepo kupokea mapigo kwa niaba yake na nguvu ya radi ile ingemuingia yeye.
Sasa Roma wazo ambalo alikuwa nalo ni kwamba kama alikuwa hajapitia mapigo ya radi na alikuwa na uwezo huo , inamaanisha kwamba kama atafanikiwa kupita inamaana atakuwa na uwezo mkubwa kuliko wa kwake.
Pengine kuna mambo mengi ambayo hakuwa akiyaelewa kuhusu nguvu za kijini na levo ya Dhiki ndio maana Anjiu alikuwa na nguvu kubwa kuliko yeye licha ya kwamba alikuwa amepitia mapigo ya radi tisini na tisa.
Ndani ya dakika moja tu wingu ambalo lilikuwa likizunguka lilitengeneza kitu kama vortex hivi na radi na mawaingu yalianza kupiga shoti za radi huku kasi ya mawingu kuzunguka ikiongezeka maradufu.
Majjini wote ambao walikwua katika eneo hilo walikuwa katika hali ya mshangao kwani ndio wanaanza kuona kwa mara ya kwanza Dhiki ya radi tisa.
Anjiu ambaye ndio alichokoza anga na kutengeneza radi hio hakutaka kujifcha tena na alisimama katika eneo lileile huku juu yake mawingu yakiendelea kutengeneza msuguano.
Majengo hayo ya madini ya Jade kama radi itapiga hapo ilimaanisha kwamba yangegeuzwa na kuwa majivu lakini hakutaka kujali tena kuhusu majengo ambayo yapo chini yake.
“Baada ya mapigo ya radi kunishukia ndio nafasi pekee ya kuweza kunishinda , chukulia kama hutofanya shambulzi wakati huo na kuendelea kuangalia na nikafanikiwa kupita hutokuwa na uwezo tena wa kunishinda”Aliongea huku akiwa amefumba macho yake katika utulivu kabisa akisubiria mapigo ya radi.
Roma alijihisi ni kama vile anadhalilishwa na kauli yake na kujiambia ana uhakika gani atashindwa hata kama akipitia hio dhiki au ni kwamba haogopi kuuliwa na nguvu hio ya radi.
Ijapokuwa alikuwa na Dhana yake ya askari wa kipepo ilikuwa ngumu kuhimili mapigo hayo na ilimfanya Roma kuwa katika maswali.
Dakika hio Roma alihisi kuongezeka kwa mchecheto wa chungu chake chini.
Ndio muda ambao Roma alianza kukumbuka wakati anapita katika mnara akitokea ulimwengu wa majini pepo ni chungu hicho hicho ambacho kilipitia mapigo tisini na tisa ya radi na kuigeuza ile radi kuwa nishati yake sasa alijiuliza vipi kama atakipatia nafasi ya kupitia mapigo tisa ya radi si inamaana kitakuwa na uwezo wa kusharabu nguvu hio ya radi na kumuongezea nguvu maradufu.
Roma wazo palepale lilimwingia na kujiambia au azuiemapigo hayo ya radi yasimfikie kwa kutumia chungu chake , alijiambia pia inaweza kumuwezesha kupata uzoefu utakaomsaidia akija kupitia mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi.
“Nitamziuia”Aliongea
Roma mara baada ya kujua hio ni nafasi adhimu sana kutumia , hakutaka kuchelewa na alikiita chungu kutoka chini pamoja na Rufi.
Baada ya kumshikilia Rufi vizuri katika kiuno chake ili kumlinda kwa ukaribu hatimae alikisukumiza chungu chake kwenda juu zaidi angani ili kikapitie mapigo ya radi.
Anjiu na majini wengine walishangazwa na jambo hilo na kujuliza Roma anajaribbu kufanya nini.
“Unataka kuharibu mpango wangu sio?”Anjiu aliongea kama vile hakuwa ametegemea Roma kuchukua maamuzi hayo hivyo alikuwa akitegemea labda Roma alikuwa akipanga kumshambulia lakini alionekana kutaka kuzuia mapigo yale ya radi yasimfikie.
Anjiu alionekana kuwa na hasira mara baada ya kuona chungu kile kipo juu yake.
“Huwezi kufanikiwa, Askari wa kipepo nenda!!”Aliongea na palepale askari wake wa kipepo alimsogelea Roma kwa ajili ya kumshambulai.
“Yang’wi na moto wa Dhahabu!”
Sauti ilitoka katika lile pepo na palepale liligeuka na kuwa moto na kuanza kumfukuza Roma.
“Shit… hili pepo lake lina mbinu kama zake tu”Aliongea Roma huku aking’ata meno yake kwa hasira
“Kuwa makini mpenzi, kwasababu akili yake imegawanyika na nafsi yake,Anjiu anao uwezo wa kuliendesha na akili yake tu , hivyo kama utatumia moto wa samawati kulipiga hakutakuwa na mafanikio,utafanikiwa kuliweza kwa kutumia moto wa kiroho”Aliongea Rufi ambae alikuwa akijitahidi kutokuona hofu.
Ijapokuwa haikuwa vizuri kupambana akiwa na mwanamke pembeni yake lakini alishukuru kwmaba pepo hilo halikuwa na nguvu kama alivyokuwa jini Anjiu mwenyewe .
Ndio hivyo tu kanuni za anga hazikufanya kazi vizuri katika ulimwengu huo na kama angezitumia ingekuwa rahisi kulishinda.
Roma mara baada ya kuona Rufi alikuwa na pointi hakutaka kuzembea tena na palepale alitengeneza moto wa rangi nyeupe na wa zambarau na kwenda kulishambulia.
Muda uleule hatimae anga lilianza kuangaa mara baada ya awamu ya kwanza ya radi kupiga.
“Boom!!”
Radi ambayo ilikuwa kama mti wenye matawi iliweza kushuka chini katika ulimwengu huo wa kijini na kupiga kwa sauti ya kuumiza masikio.
Ijapokuwa pigo hilo halikuwa kali kama lile ambalo alishawahi kupokea lakini ilimpelekea Roma kuhisi kiwewe kutokana na maumivu.
Alijua kabisa licha ya kwamba alikuwa akielewa nguvu huo ya radi tisa lakini bado haikumaanisha kwamba anaweza kupokea mapigo yake kila anapotaka.
Dakika ambayo chungu kile kilifikiwa na ile radi ile roho ya mnyama ilikuwa ndani yake ilitoa ngurumo kubwa mno ambayo iliweza kusikika katika akili ya Roma.
Nusu ya radi hio ilimezwa na chungu cha maafa na palepale ilibadilishwa na kuwa nishati ya mbingu na ardhi na kusababisha kile chungu kutoa mng’ao kama vile kimetengenezwa kwa madini ya almasi.
Nguvu za Roma palepale zilianza kuongezeka kwa kasi kubwa mno mara baada ya nguvu ya nishati ile ya radi kumuingia.
Upande wa Jini Anjjiu alipokea kiasi kidogo tu cha ile radi na kama utajumlisha na uwezo wake basi alichopokea ni kidogo sana na hakina faida.
Akiwa katika hali ya kuchukia lile pepo lake lilianza kumshambulia Roma na moto wa randi ya zambarau lakini mashambulizi hayo kwa Roma hayakuwa kitu kabisa na aliweza kuyazuia.
Muda huo Roma hakutaka kumshambulia Anjiu kwani alijua kama atamuua basi na Adhabu hio ya Dhiki ingeacha mara moja na asingeweza kufaidika nayo.
Yaani kwasababu radi alieisababisha ni Anjiu basi kama angekufa na radi hio ingeacha na Roma asingeweza kunufaika , kwani alikuwa akitaka kutumia radi hio kujiongezea nguvu yaani tofauti na Anjiu kupokea mashambulizi ya radi yeye ndio alikuwa akiyapokea.
Dakika ileile mara baada ya wingu kuzunguka kwa kasi radi nyingine iliokuwa katika rangi ya Zambarau na bluu ilishuka, awamu hio ilikuwa pana mno na yenye nguvu kuliko ya mwanzo.
Kama awali mara baada ya kufikia chungu iliweza kumezwa kiasi na nyingi ilimshukia Anjiu.
Roho ya mnayama ilifurahia kwa mara ya pili na kujikusanyia nguvu kubwa zaidi na kuisafirisha kwenda kwa Roma na nusu kujinufaisa yeye , Roho yake ambayo ilikuwa imepunguzwa nguvu na Roma mwanzoni sasa ilionekana kuamka tena baada ya kurutubishwa na radi..
Roma aliweza kuhisi uwezo wake kuongezeka kwa asilimia tisa hivi , mwanzoni uwezo wake ulikuwa mdogo kiasi kufikia radi ya mapigo mengi lakini kwa nguvu yake iliovyongezeka aliona anakaribia.
Uelewa huo ulimfanya kuwa na furaha kwakuwa tu na Dhana ya chungu pamoja na mapigo ya radi hio hakuwa na haja ya kuwa na wasiwasi tena kwa uwezo wake kuongezeka taratibu taratibu.,
Ambacho majini walikuwa wakitumia miongo kufikia yeye alikuwa anakikamilisha ndani ya siku chache tu.
Lakini muda uleule jini Anjiu alianza kutoa kicheko cha juu ambacho kilikuwa kikiumiza masikio na kisha kumwangalia Roma kwa kejeli.
“Hahah.. Chaos!!, Roma Ramoni napaswa kukushukuru kwa kunisaidia kuizuia radi hii vinginevyo ningekuwa nusu mfu hata kama ningekuwakama wewe ambaye mwili wako umeimarishwa na mwanga wa kiuungu , kwangu kiasi hichi kidogo cha radi nilichokipata kinanitosha kabisa”
Roma palepale alishikwa na mshangao na hasira kwa wakati mmoja na kujua kumbe alikuwa akijifanyisha kukasirika ili tu yeye atumia chungu chake kumsaidia kupita dhiki ya mapigo ya radi hio.
Ni ngumu sana kwa majini kupita levo ya mapigo ya radi bila ya kuwa na Dhana, kitendo cha Roma kuwa na Dhana ambayo ina uwezo wa kuhimili mapigo ya radi kama hio ilikuwa ni fursa kwa Anjiu kuweza kuitumia.
Aliamua kumtega Roma kwa kujifanyisha amekasirika ili tu Roma atumie chungu chake kukinga radi ili yeye asiathirike kimwili.
Majini walichokuwa wakikitafuta katika mapigo ya radi sio kupigwa na radi yote bali ni kutumia radi kuweza kupanua uwezo wa wa kufikiria na hatimae kuufikia ufunuo katika mbingu za juu.
Unapaswa kuelewa nguvu za kijini hazipo katika mkusanyiko wa nguvu za kijini bali ni ile uwezo wa akili ya ufumbuzi inavyopanda viwango kwenda mbingu za juu zaidi na kadri ambavyo unapata ufumbuzi ndio namna ambavyo uwezo wako moja kwa moja unapanda na hicho ndio ambacho alikwua akilenga Anjiu , yaani wakati Roma akilenga kufyonza nishati ya radi upande wa Anjiu yeye alikuwa akilenga kufumbua fumbo.
Lakini swali lingine likaibuka katika kichwa cha Roma na kujiuliza yalikuwa ni mapigo mawili tu ya radi ambayo yameshuka kwanini afichue mpango wake mapema kabla ya awamu zote?.
Roma alijikuta akiwa kwenye tafakari kutaka kujua Anjiu alikuwa akifikiria nini lakini alikuwa akipoteza muda na bado alishindwa kujua ni kipi ambacho anafikiria.
“Hubby fuata moyo wako usifuate maneno yake ya upotofu”Aliongea Rufi mara baada ya kuona Roma anashindwa kuchukua maamuzi.
Lakini sasa Roma alishindwa hata kumsikiliza kabisa Rufi na kuendelea kuwa katika tafakari nzito na ni sekunde ileile awamu nyingine ya mapigo ya radi ilishuka na awamu hio chungu hakikuweza kuimeza yote kutokana na ukubwa wake na kiwango kikubwa kilimshukia Anjiu.
“Haha…nimefanikiwa!!”
Aliongea Anjiu mara baada ya kupona maumivu ya radi na katika hali ya kushangaza wimbi kubwa la nguvu za kijini lilimtoka na akawa ni kama vile amebadilika kabisa na kuwa mwingine.
Nguvu ya kijini ambayo ilikuwa imenzingira iliongezeka maradufu na kusababisha upepo mkali ndani ya hilo eneo na mchanga kuamka kutoka ardhini.
Majini ambao walikuwa wamesimama mbali kuangalia kile kinachoendelea waliishia kushikwa na mshangao mara baada ya kuhisi mkandamizio usiokuwa wa kawaida ukimtoka mkuu wao.
Zianji alijikuta aking’ata meno kwa hasira huku akimuonea wivu kaka yake kwa wivu na kujiambia ni kwa mara nyingine kaka yake anapanda levo mbele ya macho yake.
Roma aliemshikilia Rufi aliinua sura yake juu na kumwangalia Anjiu ambaye alikuwa amebadilika kabisa katika uwezo wake wa nguvu za kijini, kutokana na kusita sita hatimae ameweza kumfanya Anjiu kufaidika na uwepo wa Dhana yake na kupanda levo maradufu.
Licha ya kwamba Anjiu alikuwa amepitia mapigo machache tu ya radi uwezo wake uliongezeka na kuwa mkubwa mno na kulingana kikamilifu na uwezo wa Roma.
Yaani kwa lugha nyepesi ni kwamba Anjiu hakuwa na haja ya kupitia mapigo tisini na tisa ya radi ili kufikia levo za Roma bali alihitaji ufumbuzi wa nguvu ya radi ili kuweza kupanda levo.
Yaliwezekana yote hayo kutokana na maarifa mengi aliokuwa nayo juu ya nguvu za mbingu na ardhi kuliko Roma ambaye ndio ana miaka michache tu tokea anze kujifunza.
“Umenishindwa , Roma Ramoni wewe ni mtoto na hujui mambo mengi kuhusu nishati za mbingu na ardhi , wazo moja tu linaweza kuamua nani ni mshindi na nani amepoteza pambano kati ya watu wawili wenye nguvu sawa , uliweza kudanganyika na maneno yangu na imekupelekea kushindwa , mwanzoni ulikuwa na uwezo mkubwa kuliko mimi katika vitu vingi lakini sasa hivi uwezo wako hauna utofauti mkubwa na wangu na nguvu zangu za kijini ni kubwa kuliko zako hivyo huniwezi tena na nitakumaliza hapa hapa”
ITAENDELEA.
0687151346 WATSAPP ONLY
 
Shukran sana
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware

SEHEMU YA 701.
Ni dakika chache tu mara baada ya mlinzi aliefahamika kwa jina la Quif kutoka ndani ya eneo hilo aliweza kurudi akiwa ametangulizana na mwanaume ambaye alionekana amechanganya rangi , alikuwa na rangi ya kiafrika kwa mbali na ya kiarabu na jambo hilo lilimshangaza Roma kidogo.
Upande wa Zomu na Zato walikuwa na shukrani sana juu ya Roma kwa kile ambacho ameamua kukifanya, maana hawakumsaidia kwa chochote lakini kaamua kupambana na jini ambaye yupo mwishoni mwa levo ya nafsi.
Katika maisha yao kwenye ulimwengu huo Roma alikuwa mtu adimu sana ambaye ameamua kuwasaidia bila mawaa.
Kwa jini ambalo lipo kwenye levo mwishoni mwa levo ya nafsi na jini ambalo lipo mwanzo mwa levo ya nafsi utofauti wao ni ile presha wanayotoa pamoja na ukali wa mapigo.
Mwanaume ambaye alifahamika kwa jina la Feilo alikuwa kweli katika levo ya nafsi na alionekana muda wowote anaweza kuvunja kwenda levo ya dhiki.
“Feilo tofauti na kutotumia siraha zako za kimaajabu usijizuie kwenye matumizi ya nguvu, tumia asilimia mia moja ya nguvu zako za kijini kumshambulia Xiao Cheni”Aliongea Mohi.
Yuile bwana alimwangalia Roma kwa macho ya mshangao kama vile ilikuwa jambo la ajabu sana kutumia nguvu zake zote kwa mtu ambaye yupo na uwezo wa chini.
Lakini kwasababu alikuwa ni jini mwenye uwezo ambaye yupo chini ya miliki ya Kekexil hakuwa na namna ya kukataa maagizo ya mkuu wake
“Kwasababu Mkubwa namba tatu amenipa ruhusa sitokuwa na huruma , kama ukiona umeshindwa usijilazimishe kuvumilia”Aliongea Feilo akimwangalia Roma usoni.
Muda uleule wote walisongea kwenye uwanja wa mapambano Roma akiwa upande wa kulia na Feilo akiwa upande wa mashariki na upande kushoto kwao ndio jukwaa lilipo Mohi na ndugu zake wakiwa wanaangalia kinachokwenda kutokea.
Feilo paleplae hakujizuia na mwili wake ulizingirwa na nguvu za kijini na alimsogelea Roma kwa nguvu na kumpiga ngumi.
Mapambano ya aina hio mara nyingi ni adimu sana kuyaona , kwani mapambano ya majini yanakuwa ni yale ya kutumia kila Dhana walizokuwa nazo , lakini Feilo hapo hakuwa akituia siraha zake za maajabu zaidi ya kutumia mwili wake kupambana..
Kwa jinsi ambavyo Feilo alikuwa akishambulia kwa haraka haraka Roma alijua lazima atakuwa na mafunzo ya Kishaolini , kwani alikuwa akitumia mbinu maarufu ya kimapambano ya Shaolini Luohan na jambo hili lilimshangza na kujiuliza au Feilo sio jini.
Ngumi za Feilo zilikuwa ni kama nyundo na kama sio kwa Roma kuwa na mbinu za kuzuia mgongano usiwe mkubwa basi pengine kwa mtu wa kawaida ingekuwa kifo palepale maana aliunganisha nguvu zake za kijini na ngumi yake.
Roma hakutaka kutumia mfumo rasmi wa kimapambano kama Kung Fu hivyo alichanganya changanya na yote hio ni kumzuia Feilo asijue ni mbinu gani atatumia kumshambulia.
Feilo alirusha teke kupangua ngumi ya Roma na palepale alijizungusha kama ufito na kumpiga Roma kifuani na teke kwa nguvu sana na kumpelekea Roma kurushwa hewani kama mpira.
Ilikuwa ni kama vile amepatwa na presha ya bomu kutokana na namna alivyorushwa na teke la Feilo.
“Teke moja tu la kushitukiza tayari amefyatuka namna ile , huyu ni takataka”Aliongea jini Manyani lakini dakika ileile alijikuta akipatwa na mshangao huku akimwangalia Roma.
“Inawezekana vipi hii?”Aliongea akiwa na mshangao mkubwa
Kitendo cha Roma kupigwa teke na kupaishwa hewani kwa kuchora Parabola kabla hata hajatua chini Roma alijizungusha kistadi kabisa na kutua chini na miguu yake yote na sehemu ambayo amepigwa na Feilo hapakuwa na ishara yoyote ya kuumia.
Mohi na Lilsi wote walionyesha hali ya mshangao , wote walitegemea pigo lile lingemharibu kabisa Roma lakini ajabu alionekana hajaumia kabisa na walijikuta wakishangaa , walikuwa ni majini ambao wameishi muda mrefu lakini hawajawahi kuona mtu ambaye ana mwili mgumu kama Roma.
“Inaonekana angalau atakuwa na faida”Aliongea jini Mohi huku akiangalia kwa umakini kiachokwenda kutokea.
Muda huo Feilo na yeye alishaona hali ambayo sio ya kawaida kutoka kwa Roma lakini kwa wakati huo hakutaka kujali , alichokuwa akiwaza ni kushinda kwani hakutaka kuabika kwa kupoteza pambano kwa binadamu ambaye ndio kwanza ameingia katika levo ya Nafsi hivyo palepale alimsogelea Roma na uanza kumshambulia kwa kasi.
Upande wa Roma bado hakuona njia nzuri ya kumdhibiti Feilo bila ya kushitukiwa , hivyo aliishia kukubali kupokea mapigo kutoka kwake , mbinu ya kishaolini ya Luohan huwa faida yake ni kwamba pigo lake moja linalenga kulegeza mwili hivyo Roma alipokea mapigo mengi makubwa ya tumbo na kifuani,
Lakini hata hivyo Roma licha ya kupigika hakutema damu wala kutapika wala hakuna mfupa au viungio vya mifupa ambavyo vilipatwa na shida.
Mpaka mwishoni Feilo alikuwa ametumia mapigo ishirini na tatu kjaribu kumshambulia Roma lakini hakukuwa na dalili ya kumshinda na mapigo saba pekee ndio ambayo yalikuwa yamebaki..
Kwa dili ambalo Roma aliingia na mkuu namba tatu wa majini ni kuhimili kupigwa mapigo therathini lakini mpaka hapo alikuwa amepokea mapigo ishirini na tatu tayari hivyo yalikuwa yamebakia mapigo saba tu.
Roma nguo zake zilikuwa zishaharibika kabisa lakini hakuonekana kuwa na jeraha la aina yoyote na alisimama kwenye uwanja akiwa na tabasamu akisubiria kupigwa mapigo ya mwisho.
“Mbinu zako za kuvumilia mapigo ni nzuri mno lakini unapaswa kuwa makini kwani awamu hii mapigo ninayokwenda kukushambulia nayo hayatakuwa butu”Aliongea Feilo
Na palepale Roma aliweza kumuona Feilo uso wake kubadilika na kuwa na sura ya Simba huku akiongea maneno ya ajabu kama vile mtu anaenena kwa lugha.
“Om!woll!oh!bahi bahi!mi Hum!!!”
Roma palepale alijua nini ambacho anafanya Feilo , alikuwa akimtupia laana , Roma alijua ni laana kwani alishawahi kupambana na Monk na kuongea kauli hio hio.
“Sijategemea Feilo kuwa na huo ujuzi , kwa ninavyojua huo ni uchawi wa kishaolini wa ngurumo ya Simba”Aliongea Jini Mohi akimwambia Lilsi.
“Inawezekana , hii nguvu ya uchawi inaonekana kuwa na nguvu,ongezeko la nguvu ya kijini ni kama wimbi la bahari ambalo halina mwisho , kama Feilo ataingia levo ya kuipita dhiki , itakuwa ni laana yenye nguvu mno kuwahi kuwepo katika ulimwengu wetu”Aliongea Lilsi.
Upande wa Roma hakujali maoni yao kabisa , kwake hapo anaigiza na kama akitaka kumuua Feilo ni kwa kuchezesha kidole tu lakini kwa muda huo alikuwa akijifanyisha mdhaifu mbele ya Feilo ili malengo yake kutimia.
Upande wa Feilo alikuwa siriasi mno na mara baada ya kubwabwaja kwa muda mrefu nguvu yake ya kijini iliongezeka maradufu na palepale aliachama kwa nguvu na kuanza kunguruma na sauti iliomtoka hapo ni kama vile ni Simba wa Nyika.
Lakini ukubwa wa sauti hio ulikuwa ni mkubwa mno na ilimfanya kuona hio kweli ni nguvu ya kichawi kwani ni kama sauti inatokea angani na sio kwenye mdomo wa Feilo.
Haikuwa sauti tu bali iliambatana na wimbi la upepo mkali mno na ilifanya hata waliokuwa wakiangalia kutumia nguvu za kijini kuhimili wimbi la upepo.
Upande wa Roma alijifanyisha hata yeye alikuwa akifurukuta kutokana na nguvu ya upepo ule na alijikuta akielea bila kupenda na alihisi maumivu makali kutokana na kwamba hakutumia nguvu ya kijini kujilinda kwa kuogopa kugundulika.
Feilo aliendelea kunguruma kama simba kwa zaidi ya dakika tatu huku akimpa tabu Roma kutokana na mwili wake kunyongwa nyongwa na wimbi la nguvu za kijini , mpaka anakuja kumaliza Roma alidondoka chini akiwa hoi na damu zilimtoka kwenye mdomo wake huku akijitahidi kusimama akitetemeka.
Mchezo huo ulipaswa kumalizka kwa namna hio , Roma alijiambia isingekuwa uhalisia kama angeshinda bila hata ya kutoka damu.
Licha ya Roma kutoka damu kitendo cha kuweza kuhimili nguvu ya kichawi ya ngurumo ya Simba iliwashangaza kila mmoja na kukubali utimamu wake wa kimwili.
“Hii inawezekana vipi…”Feilo alijikuta akishangaa mno na alijikuta akikosa ile hali ya kujiamini aliokuwa nayo na alionekana kabisa amekata tamaa ya kuendelea kumshambulia Roma.
Jini mkuu namba tatu na wengine wote walikuwa kwenye mshangao na furaha kwa wakati mmoja , ilikuwa ni kama wameokota Hazina na wote waliona Roma angekuwa na msaada mkubwa mbeleni kama wangemfua vizuri kimapambano.
Zato na Zomu wote walikuwa na furaha , ilionekana Roma kweli ni kama alivyosema anaweza kuhimili mapigo therathini na mpaka hapo waliamini wanaweza sasa kupata vidonge kama walivyoahidiwa.
“Mkuu namba tatu , siwezi kuendelea zaidi , hata kama naweza kumalizia mapigo yangu matatu yaliobakia lakini siwezi kumshinda Xiao Cheni”Aliongea Feilo.
Upande wa Roma alimwangalia Feilo na kujiambia huyu bwana inaonekana ni mtu mwenye busara mno , mwanzoni alijiambia anapaswa kuwa makini lakini bwana huyo aliamua kuishia katikati pasipo kumalizia mapigo , kama angeendelea Roma alikuwa na hofu angetumia uwezo wake wa kijini wa zaidi ya levo ya nafsi kujilinda na ingemfanya kugundulika.
“Feilo wewe ni bindamu wa kwanza wa kizazi cha ujana uliefanikisha kuingia katika levo ya nafsi mapema , hakika upo vizuri nje na nilivyofkiria , umefanya kazi nzuri na nitatuma mtu kukuletea kidonge kingine kwa ajili ya kukusaidia”Aliongea Mohi na palepale Roma sasa alielewa hisia zake zilikuwa sawa Feloi hakuwa jamii ya kijini bali alikuwa ni binadamu aliengia ujinini , Roma alijulza Feilo ana stori gani, ila kwa muda huo hakuweza kupata majibu.
Upande wa Feloi mara baada ya kuambiwa angepatiwa kidonge cha kijini alijikuta akiwa na furaha , vidonge ni kitu cha thamni kubwa na watu waliokuwa wakipewa mara nyingi ni wanafamilia.
“Asante sana Master , nitajitahidi kwa uwezo wangu wote na kungia kwenye levo ya Dhiki ndani ya muda mfupi”Aliongea na Mohi alimpa ishara ya kuridhika na jibu lake.
“Xiao Cheni umefanya vizuri pia , miliki yetu ya Kekexil inajali vipaji bila ya kujali wewe ni binadamu au Jini , ninamuagiza sasa hivi mkuu wa Chemba, Mkuu Ganyo kukuandalia nafasi ya kuishi na kuendelea kujifunza na utapewa vidonge vitatu vya Poya kwa ajili ya kukusaidia”
“Asante sana Mkuu namba tatu , lakini vipi kuhusu Zomu na Zato kupata vidonge?”
“Vidonge vya daraja la wingu bado vipo katika utengenezaji na itachukua kama mwezi mpaka kukamilika”Aliongea na kuwafanya Zato na Zomu kunyongea, pengine waliona Mohi anaenda kinyume na ahadi yake.
“Mnadhani baba anawadanganya?, ijapokuwa ni kweli vidonge vya wingu vina thamani kubwa lakini hatuwezi kuwa na uchoyo navyo”Aliuliza yule jini ambaye alikuwa amevalia suti na buti
“Zilha yupo sahihi , mimi Mohi mkuu namba tatu wa ukoo siwezi kwenda kinyume na ahadi yangu”
“Mkuu namba tatu usituelewe vibaya , tupo tayari kusubiri”Aliongea Zomu na kumfanya Zilha macho yake kuonyesha furaha.
“Zomu na Zato mnaonaje mkifanya hivi , kwasababu itachukua mwezi mpaka vidonge kukamilika , mtapatiwa sehemu ya kuishi hapa makao makuu pamoja na familia yetu”
“Huo utakuwa ni usumbuvu kwa familia”
“Nimeongea hivyo ili kuwapa fursa , ili kuweza kuvuna nishati ya mbingu na ardhi kwa haraka mnapaswa pia kuwa vizuri katika mapambano ya kutumia siraha , Master Shagoni muda si mrefu atafika hapa kwa ajili ya kufundisha namna ya kutumia siraha kwa majini ambao watatuwailisha , je nyie hamtaki pia kujifunza kutoka kwa Master Shagoni?”
Zomu na Zato walijikuta wakijawa na furaha mara baada ya kusikia kauli hio kutoka kwa Zilha , kama wangepata mafunzo kutoka kwa Master Shagoni ingekuwa ni fursa kwao kwani ndani ya miliki hio Master Shagoni aliaminika kwa kuwa na mafunzo ya juu sana ambayo husaidia majini wengi katika kupanda levo.
Upande wa Lilsi na Manyani walimwangalia Zilha kwa macho yasiokuwa ya kawaida , lakini hata hivyo hawakumzuia kwa kile ambacho ameongea na anapanga.
Baada ya kila kitu kumalizika hatimae Roma alipokelewa rasmi na kwenda kutafutiwa eneo la kuishi na sehemu ambayo pia angetumia kwa ajili ya kujifunzia mafunzo ya kijini.
Hakuna aliekuwa akijua yupo hapo kwa misheni maalumu ya kumtafuta mpenzi wake Rufi na hakuna aliemjua kutokana na kwamba alikuwa akitumia sura ambayo ni feki.
Eneo hilo lilikuwa ni kubwa mno na kulikuwa na familia kadhaa za majini lakini Roma mazingira haya aliyaona kidogo yalikuwa na utofauti sana na ulimwengu wa majini pepo.
Majini hao wote walionekana kama binadamu lakini katika kila jini ambalo ameona hakubahatika kuona jini mdogo yaani mtoto wala jini ambalo lina umri kuanzia miaka mitano kushuka chini , asilimia kubwa ya majini ambao ameona wanajifunza mbinu za anga wengi wao wapo na umri wa miaka kumi hivi kuendelea alijikuta akiwa na maswali mengi watoto wako wapi au ndio kwamba majini hawazai.
Sehemu ambayo Roma alionyeshwa pa kuishi ilikuwa ni karibu na sehemu ambayo Zato na Zomu wamepatiwa pia kukaa kwa muda hivyo ilikuwa rahisi kwa Roma kuongea neo.
Muda huo Roma aliamua kuwapa vidonge vya daraja la kati ambavyo vimetengenezwa kwa moto wa njano ambavyo amepewa na Mohi kama zawadi , Zato na Zomu walikataa vidonge vile lakini Roma aliwalazimisha na kuwaambia wasipopokea itamaanisha sio marafiki na hapo ndio walipokea.
Majini hawakupenda kuishi na deni ndio maana walisita kupokea lakini kwasabau Roma aliwapa kama ishara ya urafiiki wao walipokea.
Kitendo kile cha kuwapatia vidonge kilimfanya Zato kumwangalia Roma kwa macho ya kimahaba mno na kumfanya hata Roma mwenyewe kushangaa.
Asilimia kubwa ya majini wa kike katika ulimwengu huo wanaguswa sana na vitendo vya upendo , ukiwaonyesha ukarimu kidogo tu basi ndio tiketi ya kukupenda tena haswa ambaye anaonyesha huo ukarimu awe ni binadamu mwenye uwezo wa kijini.
Ukweli ni kwamba wanapenda pia kuzaa na binadamu kuliko na majini wenzao kwasababu wanapata nafasi ya kuwapakata watoto wao, lakini kisheria majini wa kike hawakuruhusiwa kutembea na binadamu labda kwa misheni maalumu ya kikoo.
Roma aliwapa vidonge hivyo kwa ajili ya kutaka kuwauliza maswali na sio vinginevyo na baada ya kukaa nao na kuongea alikuja kugundua vitu vingi sana lakini katika maelezo yao hakuweza kupata taarifa yoyote inayohusiana na Rufi.
Roma alijiambia ni muda sasa wa kuanza kumtafuta ndani ya makazi hayo lakini alijiuliza ni kwa namna gani ambayo anaweza kutembea bila kushitukiwa
Kingine ambacho kilimpa maswali ni kwamba hakuweza kukutana na majini ambao Rufi alisema wanacheo cha Super Master katika ulimwengu huo na kutokuwaona kwao kulimfanya kupatwa na wasiwasi.
Wakati Roma akiwa amekaa peke yake akiwaza cha kufanya hatimae Feilo bwana aliepigana nae alikuja alipo.

SEHEMU YA 702.
“Bro vipi mazingira , umeridhika na hapa unapoishi?”Aliuliza Feilo akiwa na tabasamu usoni
Roma kwa kumwangalia tu huyo bwana alijiua tayari alishapotezea yale ambayo yametokea na kutoa tabasamu la kirafiki.
“Bwana Feilo , kuna kitu unataka nikusaidie?”
“Hapana, ni kwamba nimekuja kukupa taarifa kwamba kila jini au biadamu anaekaribishwa katika miliki ya Kekexil anapata fursa ya kuingia kwenye Jumba jeupe la fahari ya milki kwa mwaka mara moja na kuchagua mbinu mbalimbali za kijini ambazo unataka kujifunza , huu mwaka ni mara yangu ya tatu kuingia na ndio najiandaa kwenda kuchangua mbinu nyingine ya kujifunza, naamini Bro Cheni na wewe utapenda kwenda ndio maana nimekuja”
Roma mara baada ya kuskia kauli hio palepale alipatwa na wazo , alikuwa na wazo la kuingia kwenye hili Jumba Jeupe mara baada ya kuambiwa na Zomu kwamba jengo hilo ukiachana na kuhifadhia vitabu na vidonge lakini pia kuna gereza la wafungwa, Sasa Roma alijiuliza kama Rufi ameletwa kwenye ukoo huo si inamaanisha atakuwa ndani ya hilo jengo.
“Asante sana Bro Feilo, hata mimi pia napenda kwenda”Aliongea Roma na kisha akasimama na kuongozana nae kuelekea huko.
“Bro mbinu yako ya mafunzo inashangaza sana , je unaweza kunishirikisha na mimi nijifunze?”Aliuliza.
“Unaonekana kuvutiwa na mbinu yangu sio?”
“Kuna jambo ambalo hulijui kuhuu mimi bro , ukweli ni kwamba kabla ya kuja huku nilikuwa mwanajeshi Komandoo kutoka jeshi la Vietnam , baada ya kukutana na Master na kunileta huku aliniambia kwamba sitokuwa na uwezo wa kutosha kupanda levo kwasababu mwili wangu ni mchafu, lakini sikutaka kukatishwa tamaa na maneno yake na kwanzia hapo nilijifua kwenye mafunzo na kila kilichokuwa mbele yangu nilijifunza na hatimae nimefikia hatua hii ya leo lakini bado nina shauku na mbinu nyingi”
“Ukweli ni kwamba nina uwezo ambao sio wa kwaida bila hata ya kuwa na nguvu za kijini , na sijui hata huu mwili imekuwaje nikawa nao”Aliongea Roma.
Alikuwa akidanganya hakuwa tayari kumwambia kwamba alikuwa amemulikwa na mwanga wa kiuungu.
Walitembea wakiongea na kupita kwenye uwanja mkubwa ambao kuna watu wengi waliokuwa wakijifunza mbinu za kijini na shauku ya Roma kutaka kujua kwanini haoni watoto ilimvaa palepale.
“Feilo kwanini kwenye huu ulimwengu sioni majini watoto wadogo?”Aliuliza Roma.
“Bro inaonekana bado hujajua mambo mengi , hata mimi nilishangaa hivyo hivyo wakati naanza kuja , majini wao uzao wao ni tofauti na binadamu , wao wanazaa roho kwanza kabla ya mwili”
“Unamaanisha nini wanazaa roho kwanza kabla ya mwili?”
“Ipo hivi bro majini wanabeba ujauzito kama kawaida lakini kinachotokea ni kwamba mtoto anaezaliwa anakuwa hana nguvu zozote za kijjini hivyo moja kwa moja anakuwa kama roho , yaani kama unavyoona pepo lilivyo ndio wanavyozaliwa , kwa maneno marahisi wanakuwa ni majini bila miili ya kibinadamu”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa na kumwambia aendelee kumwelezea.
Kwa maelezo yake ni kwamba majini wakishajifungua watoto wao wanakuwa ni majini kamili , yaani majini ambao hawana miili ya kibinadamu na wanakuwa kama roho , sasa ikishatokea mama wa kijini amejifungua mtoto huchukuliwa na kupelekwa sehemu iliopewa jina kama Palaoni, hio ni sehemu ambayo ni kama hospitali ya majini vichanga na kazi yake kubwa huko Palaoni ni hutunza majini wachanga ambao hawana miili mpaka pale watakapopata miili yao ndio hutolewa na kwenda kuungana na familia.
Feilo anasema inaweza kuchukua mwaka mmoja mpaka miaka kumi jini kutoka Palao baada ya kupata miili na hili hutokea kutokana na kufundishwa namna ya kuvuna nishati za mbinu na ardhi na kadri jini linavyokuwa na uwezo wa kunyonya nishati kwa haraka ndio ambavyo linapanda levo kwa haraka na kufanikiwa kupata mwili na mara nyingi miili yao wanaipata ikiwa ni mikubwa kabisa kama binadamu wa miaka kumi na tano na kuendelea.
“Kwahio ikitokea kama jini halijapata mwili inakuwaje?”
“Mara nyingi hatua ya kwanza jini kupata mwili ni kupitia hatua ya kuishinda laana ya kipepo ndani yake na ndio hufanikiwa kupanda levo na kupata miili yao , lakini kama ikitokea jini halijaweza kufanikiwa kupata miili ya kibinadamu kwa kutokushinda Laana hugeuzwa nyoka au kiumbe chochote na kisha hupelekwa kwenye mnara na kusafirishwa kwenye ulimwengu mwingine”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli ile
“Unamaanisha ulimwengu wa majini pepo?”
“Bro ushawahi kusikia huo ulimwengu?”
“Ndio nishawahi kusiia sikia kuhusu habari zake”
“Mimi sina habari za kutosha lakini inasemekeana huko pia baada ya majini kujifunza namna ya kulipa pepo nguvu wanaweza kufanikiwa kupata miili ya kibinadamu”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa sasa inavyokuwa.
Ilionekana na ulimwengu huo ulikuwa na mnara vilevile wa kuelekea ulimwengu wa majini pepo , lakini aliona inaleta maana maana Roma alikumbuka Zimo alimwambia kabisa kuna watu mbalimbali wanaofka katika uliwmengu huo kwa njia mbalimbali.
“Ikitokea roho ikigoma kupatiwa mwili wowote hata wa mnayama nini kinatokea?”
‘”Bro hapo sijajua lakini nilichoweza kusikia ni kwamba kuna majini ambao wanabakia bila miili maisha yao yote , wanakuwa kama roho na hawana uwezo wa kujionyesha kwa binadamu bali wanao uwezo wa kumwingia binadamu na kumtawala, lakni mara nyingi inatokea mara baada ya jini huyo kutoroka Palao”Aliongea na hapo Roma alikuwa sasa ameelewa kitu muhimu sana.
Pengine wale wanaomiliki majini ndio hawa ambao walikosa miili na kutoroka na kwenda kumiliki nafsi za binadamu au kumilikiwa na binadamu.
“Inaonekana binadamu tumependelewa muonekano ambao unapendwa na kila kiumbe”Aliongea Roma.
“Upo sahihi lakini licha ya hivyo majini wanaamini binadamu bila nguvu za kijini atakuwa ni dhaifu tu, lakini wanapenda sana kuonekana kama binadamu , kwani kuwa na mwili wa kibinadamu inamaanisha kuishinda laana waliopewa na Mungu”
“Unataka kusema majini nao wanaamini uwepo wa Mungu…?.”Aliuliza lakini palepale Feilo alishindwa kumjibu kwani ndio walikuwa wapo nje ya geti.
Ukweli kuna mambo mengi sana Roma alijifunza na maneno ya Feilo yalikuwa sahihi , katika majini wote ambao amepishana nao wote wapo levo ya nafsi , aidha mwanzoni mwa levo ya nafsi au mwishoni mwa levo ya nafsi hakuona jini ambalo lipo kwenye levo ya mzunguko kamili wala nusu mzunguko , pengine aliamini labda hao ambao wapo katika nusu mzunguko na mzunguko kamili ndio ambao wapo huko Palao wanalelewa mpaka watakapopata miili na kurudi kwenye familia zao.
Roma pia aliweza kuona majini wengi ambao wamepita Dhiki na ambao pia wameiepuka dhiki na kuweza kufanya maajabu ya juu kabisa.
Ilionekana Dhana ndio ambazo ziliwafanya kuwa na uwezo wa kuipita dhiki lakini kitu ambacho pia Roma aliona ni kwamba asilimia kubwa ya wengi ambao wameipita dhiki nguvu yao ilikuwa ndogo mno na alijua pengine wamepitia mapigo machache ya radi maana alishawahi kusikia majini wana Dhana ambazo huwasaidia kuepuka radi awamu zote.
Lakini hata hao ambao wamepitia pigo moja moja la radi au mawili walikuwa na uwezo ambao sio wa kawaida na Roma alijiambia kwa nguvu yao kama watakusanyika kama mia hivi na kumshambulia kwa wakati mmoja atakachokifanya ni kukimbia tu maana hakuna namna.
Au vinginevyo apitie tena mapigo mia tisa tisini na tisa ya radi nyeupe ndio ambapo angekuwa na uwezo wa kupambana na makundi makubwa ya majini waliovuka Dhiki.
Kilichomfanya Roma na Fileo kutoendelea kuongea ni mara baada ya kufika getini , kulikuwa na geti ambalo lilijengwa kwa muonekano ambao sio wa kawaida , chuma chake cha rangi nyeusi kilionekana kuwa kizito mno kwa kuangalia tu kwa nje , halikuwa geti kama ya binadamu wanayojenga.
Sasa katika geti hilo la kuingilia kulikuwa na Ajuza alievalia gauni la hariri rangi ya gray, alikuwa ni mzee sana kutokana na mikunjo mingi katika uso wake na alikuwa amefumba macho.
Ilionekana alikuwa akilinda hilo geti kwa muda mrefu sana hila kusogea hata hatua kwani mavazi yake yalikuwa na vumbi jingi mno, yaani alionekana kama vile ni Ajuza lakini pia kwa namna abavyo Roma alimuona ni kama vile ni sanamu alikuwa amekaa bila kusogea na ilionekana alikaa hapo bila kuondoka kwa muda mrefu sana pengine mwaka.
“Mimi Feilo na Xiao Cheni tunaomba kwako Bibi kufungua mlango wa geti”Aliongea Feilo kwa sauti.
Roma ambaye alikuwa pembeni yake mwanzoni hakutaka sana kujali muonekano wa huyo jini Ajuza lakini baada ya kumchunguza kwa umakini aliwez kuona kitu ambacho hakipo sawa.
Roma hakuweza kuona yule bibi yupo katika levo gani ya nguvu za kijini, kumbuka alikuwa na mwili wa kibinadamu hivyo alipaswa kuwa na nguvu ya kijini lakini Roma alishindwa kuona alikuwa levo ipi.
Jawabu pekee ambalo Roma alifikiria ni kwamba pengine alishindwa kuona uwezo wake kutokana na levo yake kuwa kubwa mno , kwani kadri jini linavyopanda levo ndio uwezo wake unavyozidi kujificha ndani kabisa.
Roma palepale akili yake ilicheza , alijiuliza au hawa ndio Masters waliojificha ambao Rufi alizungumzia kwamba walikuwa levo za juu kabisa katika kuipita dhiki.
Roma hakutaka kujaribu hata kuonyesha mshangao na kushitukiwa maana hakujua hata muda huo kama tayari ashagundulika ameficha uwezo wake na sura yake au Lah, ukweli huyo ajuza alimtia Roma wasiwasi.
Kwa maelezo ya Fileo eneo hilo la ghorofa ndio sehemu ya thamani zaidi katika ulimwengu hio , hivyo ilileta maana jini mwenye nguvu kubwa kuwa mlinzi.
Yule bibi hakujihangaisha hata kufumbua macho yake na kuwaangalia na palepale nguvu ya kijini ilimtoka na kwenda kuvamia lile geti la chuma kiguumu sana na palepale kama vile ni maporomoko ya mawe geti lile lilifunguka taratibu na kuacha uwazi.
“Asante sana bibi”
Aliongea Feilo kwa shauku kubwa na kumpa ishara Roma waingie ndani.
Dakika hio hio mara baada ya kuingia waliweza kukutana na korido ndefu mbele yao ambayo pembeni yake kulikuwa kumesimikwa mawe makubwa mno ya rangi nyeupe.
Jumba hilo tofauti na geti pekee kila kitu kilionekana kuwa rangi nyeupe tupu.
“Bro yule bibi ndio nani?”Aliuliza Roma na Feilo hakuelewa kwanini Roma kauliza swali hilo na aliishia kujikuna kichwa.
“Sijui sana kuhusu yeye lakini jina lake halisi ni Tigola ambaye ni sehemu ya familia ya Kekexil ambaye anahusika na ulinzi wa hili jengo ,kila mtu anamwita Bibi tu , sio mimi tu ambaye simjui lakini pia wakubwa wote ambao wapo hapa kwa miongo mingi hawajui chochote kuhusu yeye na haijulikani kama ashawahi kutoka ile sehemu aliokaa au lah lakini uje usiku au mchana utamkuta pale nje ya geti akilinda, inasemekeana kwamba nguvu zake za kijini ni kubwa mno lakini ni makisio tu kwani haijawahi tokea akapigana na mtu au jini yoyote yule”aliongea
Roma alijiambia huenda ni kama alivohisia , inaonekana huyo bibi yupo levo ya kudhibiti maji ndio maana hakuna ambaye ameweza kujua ni levo ipi amefikia.
Kwa alichosema Rufi ni kwamba wapo Master wakubwa katika ulimwegu huo wa kijini ambao kazi yao kubwa ni kuhakikisha usalama wa ulimwengu huo lakini hakna ambaye alishawahi kuwaona hao Master kwa macho zaidi ya kusikia habari zao tu.
Kwa kifupi hata majini wenyewe wa kizazi cha kati hawajui kama wapo au hawapo.
“Xiao Cheni unaweza usijue hili , ila hili jengo lilijengwa zamani sana na falme ya kijini iliofahamika kama Falme ya majini wa kijani , asili ya Kekexil ni miti na mimea ndio maana unaona hata nyumba zao nyingi zimejengwa kwa kutumia miti, kila mwanafamilia katika jumba la kifalme hupata nafasi ya kujifunza mbinu ya kijini ambayo hufahamika kwa jina la Aoki , hii mbinu ni siri yao na wanajifunza wao tu na ndio namna ambavyo wanalinda nguvu yao na ukuu wao ndani ya miliki , hili jengo lote lina floor mia moja na nane kwenda juu na kila floor ina kazi yake,mbiu ya Aoki pekee ndio haihifadhiwi ndani ya hili jengo , juu kabisa katika floor za mwisho mwisho ni sehem ya kutengenezea vidonge na huko dio Master wenye nguvu ndio wanapoishi na floor ya mwisho kabisa ndio sehemu ambapo kuna gereza la kuwafungia majini”Aliongea na kumfanya Roma kushanga.
“Unafahamu kila mfungwa ambaye yupo katika hilo gereza”
“Sijui na sijawahi kufika pia , ninachojua ni kwamba wafungwa wao ni wale ambao wanaenda kinyume na miliki ya Kekexil , wengine ni wasaliti na wengine wamefanya makosa kulingana na sheria , mara nyingi kama wana nguvu za kijini hawawekwi gerezani zaidi ya kuuliwa kabisa au kutupiwa mnarani lakini baadhi yao makosa yao ni madogo hivyo wanawekwa kizuizini kutumikia adhabu, mara ya mwisho kuona mfungwa anaingizwa ni kipindi cha vita ya kijini kati ya miliki tatu, sisi wa levo za chini tunaishia maktaba tu, upande wa juu kabisa huko wanaoruhusiwa kuingia ni familia ya Wakuu wa milki na kuna ulinzi mkali mno”
Roma alijiuliza atawezaje kwenda huko juu , hisia zake zilimwambia pengine Rufi atakuwa amefungiwa huko lakini kulikuwa na walinzi ambao wanalinda vidonge hivyo ilikuwa ngumu kufika.
Roma na Feilo waliendelea kupanda ngazi kwenda juu , jengo hilo halikuwa pana sana na hata ngazi zake zilikuwa sio pana lakini kwa namna moja kwa namna ambavyo limejengwa ungejiuliza ni teknolojia gani imetunika kukamilisha ujenzi wake kwani angle zake zilikuwa zimekaa kimaajabu ajab na ni refu mno na hakuna uhakika wa matumizi ya Cranes za kujengea.
Roma aligundua jengo hili pia lilikuwa na ulinzi wa nguvu za kijini na kila ukifika katika floor unatakiwa kuvunja kizuizi na kupita na kama nguvu zako ni ndogo basi uwezekano wa kupita unakuwa mdogo kwani uzio hautokuruhusu kupita.
Jengo hilo pia lilikuwa kama la majaribio , kwa mfano jini ambalo lipo katika levo ya nafsi ambalo linataka kwenda katika floor za juu zaidi kuona mbinu mpya za mafunzo itashindikana kwani nguvu zake ni ndogo, kila ngazi ilikuwa ikipitwa na jinni kulingana na uwezo wake.
Kwa maelezo ya Feilo ni kwamba kuna baadhi ya majini wanalazimisha kwenda floor za juu lakini waangalizi wa jengo hiloo wanawakataa pale wanapolazimisha kuvunja uzio na hio ilifanyika katika hio miliki ili kuwapa majini motisha ya kujifunza zaidi na zaidi.
Lakini kwa wakuu wa familia wao ni tofauti, kwa mfano msichana aliefahamika kwa jina la Manyani na Zilha hawa wanaingia ndani ya jengo hilo bila kuzuiwa kwani ndio wamiliki wa ukoo mzima na ndio viongozi.
Baada ya Roma na Feilo kupaa na kwenda kutua katika floor ya tano waliona ingekuwa ngumu kwenda zaidi floor za juu kabisa , sio kwamba Roma hakuwa na uwezo wa kwenda lakini kila alichokifanya alihakikisha kinakuwa ndani ya levo ya nafsi ili asingundulike mapema kabla ya misheni yake.
“Xiao Cheni hii ni floor ya tano , yenyewe sio mbaya sana mara ya mwisho nilivyofika niliingia floor ya tatu , ngoja tuone kilichomo ndani ya floor ya tano”Aliongea Feilo na wote kwa pamoja waliingia katika floor hio ya tano.
Roma alitamani kwenda juu zaidi lakini kwasababu Feilo alimchukulia kama rafiki aliona akae nae kwenye hio floor ya tano.
Feilo alionekana kuwa binadamu ambaye ana shauku ya kupanda levo mno kiasi cha kumfanya Roma kumuonea huruma na kujiambia kama isingekuwa misheni yake ndani ya ulimwengu huo wa kijini basi angempatia vidonge v ya kumuwezesha kupanda levo kwa haraka..
Baada ya kuingia kwenye Floor hio kulikuwa na mikusayansiko ya vitabu vingi pamoja na ‘scrolls’ na maandishi yaliokuwa kwenye miti , vitabu vingi vilionekana kuchakaa chakaa , ilikuwa ni maktaba ya kale sana lakini ilikuwa safi.
Roma alianza kukagua huku Feilo yeye akiwa bize kuchngua mbinu za kichawi kwa ajili ya kujifunza.
Mbinu za kichawi zipo kabisa katika maandishi , nguvu za kijini zenyewe sio uchawi kwasababu ukishaingia katika levo ya nafsi moja kwa moja unapata ufunuo wa namna ya kutumia elementi za dunia kutengeneza maajabu , lakini sasa majini wengine ili kujiongezea nguvu wanajifunza na mbinu za kichawi.
Kwa mfano Feilo mbinu yake ya kichwi ya ngurumo ya simba alijfunza hapo hapo kutumia vitabu ambavo vinapatikana katika jumba hilo jeupe .
Upande wa Roma alitemebea upande ambao aliona vitabu ambavyo kwa kiasi flani viliandikwa kwa mfumo mzuri wa karatasi na baada ya kukagua Roma macho yake yalichaua mara baada ya kuona vitabu vya dini vingi ndani ya eneo hilo.
Moja wapo ya vitabu vya kidini alivyoona ni Biblia na Quran tena zile ambazo zimeandikwa katika lugha ya kiarabu cha kidini na kiebrania kabisa.
Roma palepale alikumbuka swali ambalo alimuuliza Feilo juu ya majini kuamini katika Mungu na baada ya kuona vitabu hivyo aliona pengine swali lake limejibiwa nusu , kama hawaamini uwepo wa Mungu kwanini wamehifadhi vitabu vya kidini ndani ya hilo eneo.
“Nilikuuliza kuhusu majini kuamini Mungu kama binadamu , naona hapa kuna kitabu cha Enock kilichoandikwa kwa Kieabrania na Quran”Aliongea Roma.
“Broo majini hawachukulii biblia au Quran kama imani bali wanachukulia hivyo vitabu kama mbinu ya kuwasiadia kupanda levo”
“Unamaanisha nini kusema hivyo?”
“Binadamu ambao wanaamini katika uwepo wa Mungu wanatumia Biblia na Quran kama msingi wa sala na mafundisho , upande wa majini wao wanatumia maneno ndani ya vitabu vya dini kama msaada wa kuzitoa akili zao katika mazingira ya kawaida, kwa mfano kuna majini wanatumia mistari ya biblia na Quran katika kuvuna nishati na wanafanikiwa , ni maswala ya kimbinu tu hapo tofauti na kiimani , kama mimi nimejikita katika kutumia maandishi ya vitabu vya Budha katika kujifunza ipo hivyo kwa kila jini , kuhusu majini kuamini uwepo wa Mungu au kutokuwepo kwa Mungu ni swali gumu kulijibu moja kwa moja kwani imani kwao inaendana na matokeo”
“Unamaanisha kile ambacho kinawasaidia ndio huweka imani yao hapo”
“Umenielewa vizuri hapo, Bro chagua na wewe mbinu yako hapo , kama unachagua mbinu ya mistari ya kibiblia au Quran kuna muongozo wake upo chini hapo”
“Muongozo gani?”
“Sio biblia au Quran yote hutumika katika mafunzo ni baadhi ya maandiko tu ndio wanatumia”Aliongea na kumfanya Roma kuelewa lakini kwake hakuwa akitafuta mbinu ya kujifunza bali alikuwa akishangaa vitu ambavyo vinapatikana hapo ndani.
Ukweli kulikuwa na vitabu vingi sana ambavyo vilikuwa katika lugha mbalimbali, vingine vilikuwa katika ‘Code’ maalumu na vingine viliandikwa kwa michoro ya nyota nyota na viumbe wasioelezeka.
Roma alishangaa na kujiambia kama hii floor tu ina vitabu vngi hivi na kuna zaidi ya floor mia moja je vitabu hivyo vingine vinashikiria siri gani.
Roma alikuja kupata kitabu kingine kikubwa mno na juu kilikuwa na maandishi ya Great Ancient practice Codes, Roma mwanzoni hakujua kinahusiana na nini lakini mara baada ya kukifungua ndani na kuanza kusoma alijikuta akishangaa kwani ni kitabu ambacho kilikuwa kikielezea mafunzo yote ya kuvuna nishati na utofauti wa kila levo na maajabu yake , ilikuwa ni kama Enclopedia.
Roma alikaa chini na kuanza kujifunza kuhusu kile kitabu maandishi yake , kilikuwa kizito mno kama vile ni ndoo ya maji hivyo alifanya kukibwaga chini na kufundua karatasi moja moja.
“Bro hicho ndio kitabu cha muongozo nilichokuambia , ukiendelea kusoma kwenda mbele ndio utaona ni maandiko yapi katika biblia na Quran hutumiwa na majini kama mbinu za kujifunzia mafunzo ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi , kila floor kuna hicho kitabu” Aliongea Feilo na kumfanya Roma kutingisha kichwa na kuendelea kupitia, shauku yake ilikuwa ni kutaka kujua nini kitatokea mara baada ya kuipita dhiki
Jambo moja ambalo Roma alipata kuelewa ni kwamba kuna Dhiki nyingi sana ambazo zinahusiana na mafunzo ya kijini lakini ambazo zilimshangaza ni Dhiki ya awamu sita ya barafu na Dhiki ya mapigo ya radi , Dhiki humjengea mtu msingi tu wa kuelewa nini kipo mbele yake na kama ukishafanikiwa kudhibiti elementi za anga na kutengeneza aina zote tano za moto basi moja kwa moja unakuwa umefaulu kuingia katika levo ya Tuzo , hii ni levo ambayo Roma hakuelewa sana inazungumzia nini lakini alichoweza kufahamu ni kwamba kuna zaidi ya levo ya kupigwa na mapigo ya radi na kilichomfurahisha zaidi sio lazima kupitia mapigo yote ya radi ndio upande levo au kuwa na nguvu kubwa bali ni namna ambavyo unapitia changamoto na kuzitatua.
Roma alipitia haraka haraka kitabu hicho na akaacha na kisha akaanza kutafuta kitu kingine cha kusoma , vitabu vipo vingi hivyo alichagua kutokana na hisia zake zinavyomtuma.
Roma alivutiwa na Scroll moja iliofunikwa na ngozi ya Simba , Scroll ni karatasi ambalo limekunjwa kunjwa na katika hio shelf Scroll hio ilikuwapeke yake kabisa tofauti na eneo lingine.
“ Bro hio karatasi hata mimi nimekwisha isoma , haieleweki kabisa na imetengwa kutokana na ugumu wake , inasemekeana majini ambao wametumia mbinu inayopatikana katika hio karatasi waliweza kufikia levo ya tano tu na hawakufanikiwa hata kupata miili ya kibinadamu”Aliongea Feilo.
Roma alijiuliza kwanini imewekewa ngozi tofauti na karatasi nyingine , ilionekana ni kitu chenye thamani ndio maana namna kilivyotunzwa ni tofauti na karatasi nyingine.
Yaani karatasi lake limebandikwa kwenye ngozi na ndio ikakunjwa kunjwa, ilimaanisha kwamba imeongezea ulinzi wa kutokuharibika.
Dakika ile ambayo Roma anafungua alijikuta akishagnaaa mno , huku akiwa haamini macho yake.
“Maandiko ya urejesho wa Azimio usiokoma”
Roma alisoma kwa mashaka kidogo huku akificha mshangao wake licha ya kwamba alikuwa ameshangaa kuona kitu hicho ndani ya eneo hilo.

SEHEMU YA 703.
Dakika ileile Roma alijiambia au kitendo cha kutoa andiko lile kule China kwa mtu mwenye Mask ndio ameleta andiko hilo ndani ya hili eneo, lakini kwa haraka sana aliona haiwezekani , kama kweli mtu angechukua mbinu yake lazima angeficha na asingeweka eneo la wazi hivyo kwa kila jini kuona.
Andiko hilo lilikuwa likifanana na mbnu yake kabisa ya mafunzo aliofundishwa na Master Tang chi , utofauti ni kwamba mwishoni kuna maandishi yameandikwa kwamba ni andiko ambalo halijatimia.
Roma alikagua na aligundua kuna utofauti wa kimatamshi tu lakini kila kitu kipo vilevile.
Roma alijiuliza kwanini miliki ya Kekexil ina mbinu yake , au ni mbinu ambayo pia ilimilikiwa na majini na wakashindwa kujifunza.
Kwa haraka haraka alianza kusoma maandiko yale na kutumia mbinu yake kuyakagua na palepale ni kama akili yake inampotea hivi na alishindwa kuona nguvu yake kabisa na aliamua kuacha.
Wakati wakiendelea kuwa bize ndani ya floor hio hatimae aliongezeka mtu mwingine na Roma palepale alimjua alikuwa ni binamu yake Rufi , bwana aliefahamika kwa jina la Zilha , alikuwa ni bwana ambaye mavazi yake ni kama vile sio jini kabisa hakuwa akivalia kitamaduni kama maijini wengine.
“Feilo wewe unaweza kwenda lakini Xio Cheni yeye atabaki nina mauzngumzo nae”Aliongea Zilha na kumfanya Feilo kushangaa Zilha anataka kuongea nini na Roma.
Baada ya Feilo kutoka na kubakia Roma jini Zilha alitoa tabasamu la kihuni mbele ya Roma.
“Xiao Cheni , nipo hapa na vidonge vya daraja la kwanza , je utapenda kutumia?”Aliongea na kumfanya Roma ashindwe kusoma mawazo yake kwani hakujua hata anafikiria nini, ila kitu kimoja tokea mwanzo alishajua huyo bwana ni muhuni.
“Nitashukuru sana kama utanipatia kaka mkubwa”aliongea Roma kwa upole na kumfanya Zilha kutabasamu.
“Nitakupatia vyote lakini unapaswa na mimi kunisaidia jambo moja”
“Chochote utakachotaka nitakusaidia Master”Aliongea Roma.
“Ni rahisi sana , wewe si una ukaribu na Zomu na Zato , saa nne ya leo usiku tafuta namna yoyote ya kuhakikisha unamtenganisha Zomu na dada yake , mbali kabisa itakuwa vizuri zaidi , kwa mfano unaweza kumpeleka Zomu kwenye uwanja wa mazoezi kule , yaani hakikisha tu hakai karibu na Zato…”
Roma palepale alijua nia ya Zilha kutokana na namna ambavyo alionekana kuwa na tamaa.
Ijapokuwa majini wengi walikuwa wakipambana kupanda levo lakini kuna wengine ambao wanajua kabisa hata kama wajitahidi vipi hawawezi kupanda levo hivyo wanachokifanya ni maisha ya starehe tu na moja wapo ni Zilha yeye hakujali maswala ya mafunzo bali alijali starehe ya kujivinjali na warembo wa kijini.
“Mimi Xiao Chen lazima nihakikishe natimiza agizo lako”Aliongea Roma
“Vizuri kama mpango ukienda vizuri nitahakikisha familia ya Zaola haikuletei shida”Aliongea na Roma aliishia kutabasamu na kujiambia huyu kajileta mwenyewe, baada ya usiku itajulikana.
Roma mara baada ya kushuka ghorofani alikutana na Feilo nje na kuanza safari , Feiloi alimuuliza Roma Zilha alikuwa na habari gani na Roma aliwambia tu kwamba alikuwa akiulizia kuhusu mbinu yake ya mafunzo kiasi cha kuwa na uwezo wa kuhimili mapigo mengi.
Kabla ya Roma kuachana na Feiloi alipendekeza usiku ajifunze mafunzo ya kuvuna nishati na mtu ambaye yupo levo ya juu zaidi yake na Roma alimwambia itakuwa vizuri kama wataungana na Zomu usiku kujifunza na Feiloi alifurahi na kumwambia yupo tayari kujifunza na jini ambalo lipo levo ya juu kuliko ya kwake na hapo ndio Roma alimwambia muda mzuri itakuwa ni saa nne usiku.
Roma hakuelekea moja kwa moja sehemu anapoishi maana hakuwa bize kama majini wengine ambao mara zote wanajifunza kuvuna nishati za mbingu.
Roma aliweza kumkuta Zomu akiwa bize anafanya tahajudi kama kawaida.
“Xiao Cheni unadhurula sana na sio vizuri kwa mafunzo yako”Aliongea mara baada ya kumuona.
“Ndio tuseme kwamba hutaki nikikaribia”Aliongea Roma hku akimwangalia jini huyo alivyokuwa ametokwa na jasho kwa kujifunza , walionekana walikuwa wakitumia juhudi kubwa sana katika mafunzo kuliko hata wanawake wake wanavyojifunza na alijiambia nadiko wanalo lakini hawajifunzi.
“Muda wowote na sehemu yoyote tunakukaribisha , umekuwa msaada kwa familia yetu na tutakumbuka wema wako milele, hata hivyo naamini ndani ya mwaka mmoja utaweza kuingia katika levo ya kuipita dhiki wakati huo utasimama kwa kujiamini kati ya majini wote wa koo hii na kupewa majukumu, pengine utashiriki katika mashindano”
Roma wakati alipokuwa akipiga stori na Zomu aliweza kumwambia kuhusu mashindano ambayo yanafanyikka ndani ya ulimwengu huo wa kijini kila baada ya miaka mia moja.
Mashindanno hayo yalikuwa yakihusisha majini ambayo yapo katika umri chini ya miaka hamsini kujumuisha koo zote kubwa za kijini zenye nguvu , ni mashindao ambayo yanafanyika kila baada ya miaka mia moja na ndio maana kaka yake Lilsi afahamikae kwa jina la Master Shagoni aliitwa kwa ajili ya kutoa mafunzo.
Sababu ya mashindano hayo ilikuwa ni kam ulimwengu wa majini pepo , ila hapo kuna utofauti ni kwamba wao wanashindana kwa ajili ya kuingia kwenye jicho la Anga.
Katika ulimwengu huo wa kijini kuna kaburi kubwa ambalo limejengwa katika upande wa kusini mwa miliki hizo , inasemekana kabuli hilo lipo kama fremu ya mlango mkubwa sana ambao upo ishara ya alama ni kama mfano wa ile fremu pale Dubai ya mlango.
Sasa inasemekana mahali hapo ndio kuna jicho la Anga , yaani kwao jicho la anga inamaanisha ni kama mlango wa kuingia ulimwengu mwingine kabisa wa kijini pepo.
Wanasema kwamba ukishangia kwenye hilo jicho la Anga ni kama umeingia kwenye ulimwengu mwingine wa majini pepo ambao ni wakali sana ambao hawapatani kabisa na majini wa kawaida na binadamu.
Yaani ni kama ulimwengu wa majini pepo lakini upande huo ni tofauti kidogo na ulimwengu wa majini pepo.
Sasa jicho hilo hufunguka kila baada ya miaka mia moja katika hesabu za ulimwengu wa kijini na huruhusu majini wa kawaida kungia katika jicho hilo ili kufika katika ulimwengu mwingine na kujikusanyia hazina.
Inasemekeana ulimwengu huo una vitu vingi vya thamani kwa ajili ya majini kama vile siraha za maajabu na vidonge.
Sasa unaambiwa tabia kubwa ya ulimwengu huo walioupwa jina la jicho la Anga ni kunyonya nguvu za majini wanaotembelea kila baada ya kufunguka kwake , hivyo mashindano yalikuwa yakifanyika ili kuruhusu majini wachache kuingia kwani kama wakiruhusu majini wengi kuingia jicho hilo hujifunga lenyewe kutokana na kunyonya nguvu nyingi ya kijini na likishajifunga inamaana kwamba ni zaidi ya miaka mia moja mingine katika kusubiria mpaka kufunguka tena.
Viumbe ambao wanaishi huko inasemekana ni roho za majini mara baada ya kufariki kwao.
“Kwahio hilo jicho likifunguka roho ambao wapo ndani ya ulimwengu huo hawarudi kwenye ulimwengu huu?”
“Huko pepo hao hawana miili , asilimia kubwa wote wapo katika mfumo wa pepo na sheria za jicho la Anga linaruhusu pepo kuingia na sio kutoka , hivyo mara nyingi majini wanapoingia katika ulimwengu huo pepo hao wanawashambulia sana ili kuiba miili yao na kurudi katika huu ulimwengu”
Roma alisikiliza Stori hizo za kustaajabisha , ijapokuwa maelezo ya Zomu hayakumwingia akilini vizuri lakini alitamani kwenda kujionea mwenyewe kama angepatta hio nafasi.
Alitaka kujua nini kinapatikana katika huo ulimwengu ambao mlango wake ni kama jicho.

TO BE CONTINUED.
Naaaaam
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom