Simulizi ya Kijasusi: Mlango wa 77 "DOOR 77"

Kumekucha,
Ila kutoa taarifa Napo sawa.
Waeleze wasomaji kuwa."Naweka hadithi ila haitoisha,ukitaka uimalize malipo yapo Kama ifuatavyo.

Ila ukikaa kimya sio,kwani wanaozimaliza wanna nn.

Kingine unapoanza kupositi unakuwa umejishauri mwrnyewe.
Kama hutaki karaha,peleka kwenye group lako,happy ni uwanja was wote.

So,punguza manunguniko na kejeli,kwa maana hakuna aliyekulazimisha,Bali watu wameingia wakakutana nayo.Lazima waifatilie,inapokatushwa na hayo yoote yanajitokeza.

Wasikuchoshe,nawe usiwachoshe.
 
MLANGO WA 77 "DOOR77" Sehemu 03
Mtunzi; Robert Heriel
Whatsapp 0693322300

Sehemu 03

ILIPOISHIA

“ Imaculata?” Peter Mirambo akajikuta anang’aka. Lakini kabla Tarikh hajaongea chochote Mlango ukafunguliwa wakaingia wanaume wawili waliovalia suti zilizowakaa vyema, Peter Mirambo akasalimiana nao, kisha mwanaume mmoja akamwambia Peter Mirambo amfuate ofisini. Wakati Peter bado akiwa hajaelewa vizuri nini kinaendelea akashangaa moja ya watu wale waliokuja akitoa bastola na kumpiga yule kijana risasi ya kichwa, Tarikh akadondoka chini wakati Peter akiwa anajaribu kumzuia yule mwanaume asimpige Risasi lakini alikuwa amechelewa.

ENDELEA
Peter akawa anajaribu kumnyanyua Tarikh kuona kama atakuwa hai lakini alikuwa keshapoteza maisha. Kwa hasira akamfuata yule mwanaume aliyempiga Tarikh risasi kisha akampiga ngumi ya uso, yule mwanaume akadondoka chini, akamfuata pale chini kisha akamkunja shati kwenye kifua na kumnyanyua juu kwa nguvu.

“ Kwa nini umemuua? Nakuuliza why did you kill him?” Peter akafoka huku akiutazama uso uliokuwa unavuja damu puani wa yule mwanaume. Yule mwanaume wa pili akamshika Peter na kuwaamulia. Kisha akamruhusu yule mwanaume aliyemuua Tarikh kuondoka. Ingawaje Peter alikuwa anahangaika kutaka kumzuia yule mwanaume asiondoke lakini haikuwezekana.

“ Noo! Kwa nini umemruhusu huyo muuaji aondoke, ni nani?” Peter Mirambo akamgeukia Bekha ambaye ndiye alikuwa ameingia na yule mwanaume.

“ Tulia! Punguza hasira Peter.” Bekha akasema,

“ Yule mwanaume ni nani nimekuuliza? Mimi ndiye nimekabidhiwa hii operesheni, watu wote waliochini yangu katika hii kazi ninawajua na wote waliuawa jana tulipokuwa kwenye misheni isipokuwa Mimi na wewe, huyu jamaa uliyekuja naye sio miongoni mwa ambao nilikabidhiwa. Tafadhali Bekha” Peter Akasema.

“ Alikuja. Baada ya kunisalimu akatoa simu yake mfukoni kisha akapiga namba Fulani, haikuita sana ikapokelewa, hapohapo akanikabidhi pasipo kusema chochote, nikaiweka sikioni, kisha nikasikia sauti ya upande wa pili ambayo bila ya kunisalimia ikaniambia kuwa nimpeleke huyo mwanaume kwenye chumba cha mahojiano. Kisha simu ikakata” Bekha akasema,

“ Hivyo tuu! Alikuwa ni nani aliyekuwa akiongea?”

“ Alikuwa ni CDF Haidari Mwera” Bekha akajibu.

“ Lakini hii inawezekanaje? Na kwa nini huyu mwanaume amuue huyu shahidi haramia?” Peter akauliza kwa sauti ya chini huku akimtazama Bekha.

“ Hata mimi nimeshangaa kitendo kilichotokea”

Peter akatembea mpaka alipoufikia mlango, akaufungua kisha akatoka akimuacha Bekha akiwa anazungumza. Moja kwa moja akaenda kwenye vyumba ambavyo wale Maharamia waliwekwa kwani kila haramia aliwekwa kwenye chumba chake. Peter alipigwa butwaa mara alipoona maiti ya haramia mwingine ikiwa imelala sakafuni ikiwa inajeraha la risasi kichwani. Hakutaka kupoteza muda akasonga kwenye chumba kilichokuwa kinafuata, nako akakutana na hali ileile. Hapo akazidi kuchanganyikiwa, akasonga kwenye chumba cha mwisho cha tatu, huko akakutana na hali tofauti kidogo. Haramia huyu alipigwa risasi ya tumbo na kifua. Naye alikuwa amekufa.

“ Hii inamaanisha jambo gani? Inawezekana vipi?” Peter alikuwa akijiuliza huku akiwa anakagua maiti ya haramia wa tatu. Hakuna cha ziada, akatoka na moja kwa moja akaelekea mapokezi ambapo alimkuta yule Mwanamke aliyevalia kijeshi aliyewaletea kifungua kinywa. Yule mwanamke aliona uso wa Peter ukiwa umebadilika na hiyo ilimaanisha kuna tatizo. Akauliza:

“ Vipi Peter kuna tatizo?” Kabla Peter hajajibu, wote wakatazama lilipodirisha ambalo lilionyesha kwa nje, hapo waliona geti linafunguliwa na punde wakaona Gari la CDF Haidari Mwera likiingia. Baada ya gari kuegeshwa akashuka CDF akiwa yupo ndani ya gwanda la kijeshi kama ilivyodesturi yake. Baada ya walinzi wa nje kumpa heshima, akasonga kuingia ndani. Peter hakujua ni kwa nini mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio. Alikuwa na wasiwasi. “ Kuna jambo haliendi sawa hapa. Sasa kama CDF ndio kamuamuru yule mwanaume awaue, kilichomleta yeye sasa hivi ni kitu gani?” Peter akawaza huku akitazama mlango wa mapokezi ukifunguliwa na punde CDF akatokea akiwa anamkabili. Peter Mirambo akatoa heshima ya kijeshi, na yule mwanamke wa kijeshi naye akatoa.

“ vipi kazi inaendeleaje?” CDF akauliza huku akimtazama Peter Mirambo, hapo Peter akawa haelewi ajibu nini. Kabla hajajibu, mawazo yake yakakatishwa na sauti ya cdf;

“ Wako wapi hao vijana mliowakamata?” Kufikia hapo Peter nguvu zikawa zimemuisha, mapigo ya moyo yalifufuka na mwili ulianza kupata moto. “ kwa mara ya kwanza ninaenda kushindwa vibaya, nimezidiwa mbinu” Peter akawaza,

“ Wako wapi?” Akauliza tena, mara hii akiwa anamtazama Peter kwa udadisi, aligundua kuna jambo halipo sawa kwa jinsi uso wa Peter ulivyokuwa.

“ Mkuu..!”

“ Sitaki kusikia excuse yoyote, maneno kinyume na nilichokutuma hapa hayaitajiki” Cdf akamkatisha Peter. Punde Bekha akatokea, akatoa heshima ya kijeshi kisha akawa anawatazama kwa zamu Cdf pamoja na Peter.

“ Mkuu uliongea na Bekha” Peter akasema, hapo CDF akamgeukia Bekha, akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akamgeukia Peter, akasema;

“ Kuhusu nini?”

“ Mkuu si uliongea na mimi Kupitia yule mwanaume uliyekuwa umemtuma, tukazungumza kwenye simu, ukaniambia nimpeleke yule mwanaume kwenye chumba cha mahojiano” Bekha akasema,

“ Mimi!”

Hapo ukimya ukatokea, wote tulikuwa tukimtazama Bekha tusijue kama tunapaswa kumuamini au laa. CDF kakataa kuwa hakuongea na Bekha. Sasa nani mkweli na nani muongo. Kama tukimuamini Bekha basi tungemfanya Cdf kuwa muongo, na kama tukimuamini cdf basi Bekha angekuwa muongo.

“Bekha! Uliongea na mimi leo? Embu onyesha simu yako najua kwa level yako huwezi kuzungumza na simu pasipo kuweka rekodi” cdf akasema.

“ Mkuu! Nilitumia simu ya yule mwanaume ambaye alijitambulisha kuwa ulimtuma”

“ Alisema anaitwa nani”

“ Hakujitambulisha jina lake. Yeye baada ya kunisalimu akatoa simu kutoka mfukoni mwake akabonyeza na kupiga simu, ilipoita akanikabidhi, kisha nikaongea na wewe” Bekha akasema,

“ Kwa hiyo ulishindwa hata kutazama kwenye kioo cha simu aliyokupa kuona namba au jina la mtu utakayeenda kuongea naye?”

“ Mkuu hapo ndipo nilikosea, yaani simu ilipopokelewa moja kwa moja niliposikia sauti yako sikuwa na haja ya kuangalia namba na jina Mkuu” Bekha akasema akiwa anawasiwasi mwingi.

“ Kwa hiyo wako wapi? Au ndio wamechukuliwa na huyo mtu?” Cdf akauliza, hapo tukawa tunatazamana na Bekha. Wakati huo yule Mwanamke mwanajeshi aliyevaa kijeshi akiwa ameshika kitabu cha wageni. CDF akaondoka na kuelekea moja kwa moja kwenye chumba cha mahojiano pamoja na vile vyumba walivyokuwa wamewekwa wale maharamia. Baada ya kitambo kidogo akarudi akiwa amefura kwa hasira.

“ Mmekuwaje wajinga kiasi hicho? Mpaka mnaruhusu uzembe kama huu watu kama ninyi ambao tunawategemea. Kwa hiyo hakuna hata mmoja aliyebakia. Yaani hii imewezekanaje wezekanaje?”

“ Hamkufanikiwa kumhoji yeyote kati yao?” Cdf akauliza huku akitutazama kwa macho ya hasira.

“ Ndio nilikuwa nimeanza kumhoji Tarikh”

“Tarikh ni nani?”

“Ni moja wa wale maharamia Mkuu”

“ Ennhee! Angalau umenipa moyo, nakujua Peter ulivyohodari na mahiri kwa kazi ya kuhoji. Naamini utanipa furaha” CDF akasema, wakati huu zile hasira zilikuwa zimepungua, uso wake ulikuwa angalau unatazamika.

“ Sikufanikiwa Mkuu, wakati ndio naanza kumhoji ndipo Bekha alipoingia na yule mwanaume, na alimuua palepale kabla hajafanya chochote”

“ Bekha! Unaona uzembe ulioufanya? Embu mkamateni Bekha mkamuweke sehemu maalumu kwa watu wa aina yake. Watu wazembe kama ninyi ndio mnaweza kuliuza taifa lenu kirahisi kama hivi” Cdf akasema na papohapo Bekha akakamatwa, Peter alitaka kuzuia lakini nafsi yake ikamuonya.

“ Siamini kama Bekha anaweza kuwa alinidanganya, lakini kama hakunidanganya ni nani aliyekuwa ameongea naye kwenye simu?” Peter akawa anawaza.

“Mkuu yule mwanaume aliandika jina lake hapa” Yule mwanamke mjeshi akasema akiwa amefungua kile kitabu cha wageni, akamkabidhi, Cdf akawa anasoma jina la yule mwanaume ambalo lilisomeka Dismas Sabuni Kazarage, mbele kulikuwa na namba ya simu na sahihi yake. “Embu ipigie hiyo namba” Cdf akasema, yule mwanamke mjeshi akachukua simu kisha akaipigia ile namba, akaweka sauti kwenye simu “Loud speaker” Ikaanza kuita, “Krii krii! Krii Krii! Krii krii! Kisha ikapokelewa. Sauti ya upande wa pili ilikuwa ya mwanamke.

“ Hello” Hapo Cdf, Peter na Yule mwanamke mjeshi wakatazamana, Cdf akamuashiria Mwanamke mjeshi aendelee kuongea, bado kwenye simu sauti ya mwanamke ilikuwa ikisema; Hellow!

“Hello! Habari?” Mwanamke mjeshi akaitikia,

“ Salama, naongea na nani?” Mwanamke wa kwenye simu akauliza,

“ Samahani nitakuwa nimekosea namba, lakini tunaweza kufahamiana?”

“ Sidhani, kwa kheri” mwanamke wa kwenye simu akasema na akawa kama anataka kukata simu lakini punde ikatokea sauti ya kiume ikisema “ mchezo ndio kwanza umeanza” alafu simu ikakatika. Jambo moja ambalo la kushangaza ni kuwa sauti ile ilimshtua sana Cdf ni kama alikuwa akiijua. Uso wa Cdf ulipoteza utulivu. Akaomba tena kile kitabu ili aingalie ile namba, akawa anaisoma kwa macho namba moja mpaka nyingine. Jambo hilo Peter aliligundua Kupitia kuisoma saikolojia ya Cdf akajikuta anamuuliza;

“ Unaifahamu hiyo namba Mkuu?”

“ Eeeh! Mmmh ndio, hapana ninamaanisha siifahamu” Cdf akawa anababaika wakati anajibu swali hilo jambo ambalo liliwatia wasiwasi Peter pamoja na Yule Mwanamke Mjeshi.

“ Inaonekana Cdf anaijua vizuri hiyo namba au anaijua sauti ya mzungumzaji wa kwenye simu au ile sauti ya kiume. Hapa kuna jambo” Peter akawaza.

“Ulichukua vitambulisho vyake wakati alipoingia?”

“ Hapana Mkuu, vitambulisho wanaachaga kule nje getini kwa Walinzi” Mwanamke Mjeshi akasema,

“ Sawasawa” Akatoka akiwaacha pale ndani, kisha wakawa wanamtazama akiwa nje Kupitia dirisha. Wakamuona akipanda kwenye gari lake kisha geti likafunguliwa akaondoka.





SURA YA PILI

“ Hamjambo watoto wazuri”

“ Hatujambo! Shikamoo! Tunaomba pesa ya kula Mjomba.” Watoto Chokoraa waliitikia na kumsalimia Tobias Marengo.

“ Msijali pesa nitawapa. Mnaziona hizi” akawaonyesha akiwa ndani ya gari, wale watoto chokoraa walipoona zile pesa wakapigana vikumbo wakigombea kuingia kwenye dirisha la gari. Tobias akazikwepesha na kuzificha.

“ Tulieni, nitawapa. Lakini kabla ya kuwapa niambieni yupo wapi Imaculata?” Tobias akasema. Wale watoto wakawa wanatazamana kila mmoja akiwa anajiuliza huyo Imaculata ni nani. Tobias aliweza kuzisoma vizuri nyuso za wale watoto na kugundua hawalifahamu jina hilo, “ Kale katoto kalinidanganya jina” Akawaza. “ pengine hapa sio Maskani moja” akawaza na kabla hajamaliza mtoto mmoja akasema,

“ Mjomba! Huyo unayemuuliza hana jina jingine?” Tobias akamtazama yule mtoto, kisha akatingisha kichwa kuashiria hana. “ Mjomba hapa kama unavyotuona wengine hatujuani majina, kuna makundi manne ambayo kila kundi lina watoto wa maskani moja, hivyo ni ngumu kujuana majina hapa. Labda utuambie huyo msichana anafananaje?”

“ Oooh! Mmesema hapa yapo makundi manne? Kuna kundi lolote ambalo leo halipo? ” Tobias akauliza,

“ Makundi mawili leo hayapo hapa, nafikiri yatakuwa maeneo ya Mwenge, au Maeneo ya Kariakoo kule” Yule mtoto Chokoraa akasema, maelezo yake yalimfanya Tobias atabasamu na kumsifu mtoto yule kimoyomoyo. Akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpatia yule mtoto kisha akatoa nyingine na kumpa kiongozi wa kundi jingine la watoto chokoraa. Kisha akaondoka akichukua uelekeo wa barabara ya Bagamoyo kuikabili Mwenge. Kutokea Daraja la Salenda mpaka Mwenge sio mbali sana, ni mwendo wa dakika kumi na tano kwa mwendo wa kawaida kama hakuna foleni. Macho yake aliyaelekeza nje kutazama huku na huku kuona kama angemuona Imaculata, lakini hakuweza kumuona. Akafika Mwenge Mataa, akakatisha upande wa kushoto barabara ya Sam Nujoma akikabiliwa na Mlimani City. Akiwa amekata tamaa kabisa ghafla kwa mbali kwenye Mzunguko wa barabara ya Mlimani City alishtuka kumuona Imaculata akiwa na kundi la watoto chokoraa wenzake wakiwa wanatembea pembezoni mwa barabara jua kali likiwa linawachoma.

Tobias moyo wake ukiwa umelipuka kwa furaha akapunguza gari mwendo kabisa, akawa anaendesha polepole huku akiwamtathmini Imaculata na wenzake, tayari alikuwa ameshamaliza ile Roundabout akasonga nao mpaka kilipokuwa kituo cha daladala cha Mlimani City kwa mbele. Hapo akasimamisha Gari lake pembeni ya barabara mbele yao. Kisha akashusha kioo cha dirisha la gari. Imaculata bila ya kuwa na hili wala lile walipolifikia lile gari, Imaculata alishtuliwa na sauti kutoka katika dirishani kwenye lile gari., Alipomtazama aliyeita alimkumbuka ni yuleyule Mjomba aliyempa pesa jana kule Salenda Darajani.

“ Shikamoo Mjomba”

“ Marhaba Imaculata, unanikumbuka?” Tobias alizungumza kwa sauti yenye upendeleo na ukarimu huku akiachia tabasamu .

“ Nakukumbuka Mjomba”

“ Kumbe mnafika mpaka huku, poleni sana wadogo zangu” Hapo kimya kidogo kikatokea, ni kama Imaculata na wenzake walikuwa wakijadili maneno “wadogo zangu” wakati wakimtazama umri wake unalingana na babu yao hivi.

“ Mnaelekea wapi sasa hivi?”

“ Sisi! Aanha! Tunaelekea nyumbani”

“ Nyumbani ni wapi? Ninaweza kuwapa Lifti mpaka nyumbani” Tobias akasema,

“ Hapana Mjomba, tunashukuru”

“ Dada acha tupande tuu mimi nimechoka kutembea” Mtoto mmoja chokoraa akamkatisha Imaculata.

“ Tupande tuu Dada” Mtoto mwingine akadakia. Hapo Imaculata hakuwa na chaguo zaidi ya kuwasikiliza wadogo zake. Wakapanda kwenye gari la Tobias na safari ikaanza.

“ Hamkuniambia nyumbani kwenu ni wapi?” Tobias akasema,

“ Ni pale kimara mwisho, Darajani.” Imaculata akasema,

“ Kwa nini wazazi wenu wamewaruhusu mje huku kuhangaika?” Tobias akasema huku akiwachungulia wale watoto chokoraa Kupitia kioo kilichokuwa juu ya gari.

“ Sisi hatuna waza..zi” Mtoto mmoja akaropoka lakini Imaculata akamkatisha “ Tunaishi na wazazi” Tobias akaelewa kuwa Imaculata anadanganya, na hata jina alilomtajia halikuwa jina la kweli. Lakini hakutaka kumbughuzi wala hakuwa na haraka ya kujua jina lake. Wakafika Kimara Korogwe, Tobias akasimamisha gari Mbele kidogo ya kituo cha Daladala kwenye barabara ya pembeni. Imaculata akashangaa ni kwa nini gari imesimama.

“ Chukueni hii pesa mkalete Dozeni ya chupa za maji na juisi. Shika na hii” Tobias akawapa elfu hamsini, alipotaka kushuka Imaculata Tobias akamzuia, akamwambia “ Wewe kaa tuu acha wadogo zako wakalete, wala sio nzito, mje na Biscut zenye chocolate” Imaculata hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matakawa ya Mzee Tobias Marengo.

“ Rudishia mlango vumbi linaingia” Tobias akasema, hapohapo Imaculata akafunga mlango, alipofunga tuu mlango, Tobias akawasha gari na kuondoka. Imaculata alikuwa akipiga kelele lakini hakukuwa na namna yoyote ya kupata msaada. Akageuka nyuma kuangalia Kupitia kwenye dirisha la nyuma la gari akawaona wadogo zake wakiwa wapo dukani wasijue kuwa dada yao ametekwa.

Itaendelea

1. Jipatie softcopy ya Kitabu cha Mlio Wa Risasi harusini Tsh 8,000/=
Hardcopy. Tsh 15,000/=

2. Kitabu cha Wakala wa Siri Tsh 15,000/=
3. Kitabu cha Kaburi la Mwanamuziki Tsh 15,000/=

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
MLANGO WA 77 "DOOR77" Sehemu 04
Mtunzi; Robert Heriel
Whatsapp 0693322300

Sehemu 04
ILIPOISHIA

“ Rudishia mlango vumbi linaingia” Tobias akasema, hapohapo Imaculata akafunga mlango, alipofunga tuu mlango, Tobias akawasha gari na kuondoka. Imaculata alikuwa akipiga kelele lakini hakukuwa na namna yoyote ya kupata msaada. Akageuka nyuma kuangalia Kupitia kwenye dirisha la nyuma la gari akawaona wadogo zake wakiwa wapo dukani wasijue kuwa dada yao ametekwa.

**********************

ENDELEA
Gari aina ya Alphard Yenye Rangi nyeupe ilikuwa imesimama mbele ya geti kubwa jeusi huku ikipiga honi. Punde lile Geti likawa linafunguka kwa kuteleza na kuachia uwazi ambao ulifanya eneo la ndani lenye mandhari nzuri kuonekana. Pembeni ya Geti alikuwepo mlinzi aliyevalia Sare za rangi nyeusi na kofia, chini akiwa amevalia viatu vyeusi vya kijeshi. Baada ya gari kuingia lile Geti likateleza tena na kujifunga. Mlinzi akawa analifuata lile gari mpaka liliposimama eneo la mbele la jumba kubwa la ghorofa mbili ambalo muundo wake mbali na gharama nyingi za fedha zilizotumika lakini pia ustadi wa injinia aliyelijenga ulionekana. Lilikuwa jumba kubwa sana ambalo nje lilizungukwa na bustani na miti yenye maua yenye kuvutia, uwepo wa Bwawa la kuogelea pia kuliongeza uzuri na ufahari wa jumba lile.

Mlango wa mbele ukafunguka kisha akatoka Tobias aliyekuwa kama mtu mwenye uharaka, bila kupoteza muda wala kuipokea salamu ya mlinzi akaufuata mlango wa nyuma wa gari lake na kuufungua, alafu akamtoa Imaculata aliyekuwa analia. Jambo hilo lilimfanya yule mlinzi aingiwe na hofu iliyochangamana na mshangao. Pasipokusema chochote, Tobias akawa anamkokota Imaculata aliyekuwa analia huku akijaribu kufurukuta, nyuma yake akimuacha mlinzi akiwa anashangaa tukio hilo. Mlinzi akapanda ndani ya lile gari ndilo Alphard Nyeupe na kuiendesha mpaka eneo la maegesho ambapo yalikuwepo magari mengine mawili ya gharama.

“ Nataka kurudi nyumbani, nirudishe kwa ndugu zangu” Imaculata akasema,

“ kuanzia leo hapa ndio nyumbani kwenu, sahau kuhusu ndugu zako. Unastahili kuishi maisha mazuri Imaculata. Wewe ni malaika mdogo” Mzee Tobias akasema huku akiwa amemuachia Imaculata kwenye sebule kubwa yenye kila aina ya samani zinazoyapa macho na moyo furaha.

“ Hapa sio kwetu. Nakuomba Mjomba, nirudishe kwa wadogo zangu, sina maisha mazuri nikiwa mbali nao. Mimi ni mama kwao, mjomba!”

“ Sikiliza Malaika mdogo, kama unataka nikurudishe kwa wadogo zako ni lazima unifanyie jambo” Tobias akasema, hapo Imaculata akawa anamtazama kwa uso wa maswali. “Jambo gani” Uso wake ulionyesha swali hilo. Tobias pasipo kusema chochote akaita “ Madame! Madame!” Kisha mlango wa upande mwingine ukasikika ukifunguliwa na kujifunga kisha sauti ya mwanamke ikasikika ikiitikia “ Abee” kisha mwanamke wa makamu akajitokeza “Abee Boss, shikamoo” Yule mwanamke akasalimia.

“ Muogeshe huyu, hakikisha anatakata, kisha muandalie chakula kizuri ale, chochote atakachokihitaji mpatie. Usimsumbue, huyu ni Malaika mdogo, anaitwa Imaculata” Tobias akasema lakini akakatishwa na Imaculata.

“ Nirudishe kwetu, sitaki kukaa hapa wala sitaki kuogeshwa. Tafadhali Mjomba naomba unirudishe kwa wadogo zangu, wananitegemea” Kimya kidogo kikatokea wakati Imaculata akiwa anaomba kwa ishara za unyenyekevu, mara apige magoti mara aweke mikono kifuani basi ilimradi kumsihi Tobias amuachie lakini Tobias alikuwa na roho ngumu sana. Tobias akawa anaondoka, Imaculata akataka kumfuata nyuma lakini Madame akamkamata Mkono,

“ Tafadhali Aunty naomba unisaidie” Imaculata akasema lakini Madame hakumzingatia sana, akamvuta na kumburuza kwa nguvu bila kumuonea huruma. Kisha akamkokota mpaka walipotokea upande wa ndani kabisa ambapo kulikuwa na nuru hafifu na taa zinazotoa mwanga uliodhibitiwa mbele kidogo kulikuwa na ukumbi wenye bwawa la kuogea kama jakuzi hivi lakini hili lilikuwa kubwa kidogo kuliko jakuzi la kawaida. Ndani ya Bwawa lile kulikuwa na taa zenye rangi ya zambarau zilizofanya maji ya bwawa kuakisi rangi hiyo. Jambo ambalo lilimfanya Imaculata asisimkwe kwa hofu.

Hakuwa akilia tena isipokuwa alikuwa akishangazwa na mandhari ya eneo lile, alikuwa akitazama huku na huku, macho yake yakikabiliana na nuru hafifu ya eneo lile. Mbele kidogo akaona bustani yenye maua mazuri na sehemu yenye viti na meza za mzunguko. Kwa mbali kidogo kama hatua ishirini na tano hivi kwenye ile bustani alishtuka kuona mwanamke lakini hakuwa anaonekana vizuri kutokana na nuru hafifu. Yule mwanamke alikuwa anakunywa kinywaji chake polepole huku wakitazamana na Imaculata.

“ vua nguo Malaika Mdogo”

“ Niite Imaculata inatosha” Imaculata akajibu huku polepole akianza kutoa nguo ya juu bado alikuwa akitazamana na yule mwanamke wa kwenye bustani. Alipomaliza kuvua nguo zote na yule madame naye akavua nguo zake zote. Sasa wote walikuwa uchi wa mnyama, Imaculata alistaajabu mno kwa kitendo alichokifanya yule Madame. Yule Madame alikuwa mwanamke wa Makamu, umri wake ulikuwa sawa na Mama yake au zaidi ya mama yake. Imaculata aliona aibu kutazamana na Madame. Akafumba macho yake. Kisha yule Madame akamsogelea akiwa anatembea akimzunguka huku akiongea kwa sauti ndogo.

“ Hatujisafishi tukiwa tumevaa nguo, miili yetu ya thamani ndio tunayoisafisha” Hapo Madame alikuwa amefika nyuma ya mgongo wa Imaculata, kisha akamkaribia mpaka walipogusana, alafu akainama mpaka karibu na sikio lake. Akaanza kumchua kwenye mabega yake huku akimwambia” namna hii! Namna hii! Hivi na hivi! Mwili kuwa safi, mwili kuusafisha” Hapo Imaculata akawa anakunja uso wake kama mtu anayesikia raha lakini kuna wakati ni kama alikuwa akipata maumivu. Haikueleweka moja kwa moja alikuwa anahisi vipi.

Madame akaacha kumchua kisha akaondoa mdomo wake kwenye sikio la Imaculata, akatembea akiwa nyuma ya mgongo wake, “Nini kinaendelea” Imaculata akawaza akiwa bado amefumba macho yake. Akayafumbua polepole akapokelewa na hali ileile na mbele yake bado alikuwa anamuona yule mwanamke aliyekuwa anakunywa bustanini. Mara hii yule mwanamke hakuwa anamtazama Imaculata ila alikuwa anapangusa simu yake.

“ Keti hapa Malaika Mdogo” Madame akasema, jambo ambalo lilimfanya Imaculata ashtuke baada ya kuisikia sauti yake. Akaketi. Madame alipokuwa akienda mbele ya Imaculata, kwa upesi sana Imaculata akafumba macho yake. Kitendo hicho kilimfanya Madame atabasamu. Kisha akasema “ Nakumbuka nilipokuwa na umri mdogo kama wako. Nilikuwa binti mwenye aibu nyingi kama wewe. Ni kawaida kwa mtoto mdogo kuwa na aibu kwa mambo mageni na mazito atakayoyaona. Lakini usijali utazoea”

Imaculata hakusema chochote, alibaki kimya kama kondoo aliyembele ya mchinjaji. Madame akafungua mfuko ambao ulitoa harufu nzuri, ilikuwa sabuni. Kisha akachukua Kifaa Maalumu chenye mpira ambao ulikuwa umeunganishwa na lile Bwawa la kuogea mfano wa Jakuzi. Akawasha kile kifaa, kikawaka kisha akaseti sehemu yenye maji ya uvuguuvugu, kisha akamkaribia Imaculata na kukishika kichwa chake. Akamwomba Imaculata amsaidie kumshikia kile kifaa. Imaculata akakibeba kile kifaa bado akiwa amekaa kwenye kile kiti maalumu cha kuogea ambacho kumbe kwenye kile kiti kilikuwa na Earphone maalumu za kuogea. Madame akachukua zile Earphone na kumuwekea masikioni mwake. Imaculata bado alikuwa kimya huku mapigo ya moyo yakipiga kwa nguvu nyingi. Alitamani kumuuliza swali Madame kuhusu kile kifaa alichovalishwa masikioni lakini alijizuia.

“ Naomba hii” Madame akachukua kile kifaa maalumu chenye mpira uliounganishwa na Bwawa kisha akabonyeza kitufe kwenye kile kifaa na hapohapo maji ya vuguvugu yenye utamu yakawa yanammwagikia Imaculata, wakati hilo likiendelea Madame akabonyeza kitufe kingine kwenye kile kiti na papohapo Imaculata akaanza kusikia muziki kwenye zile earphone alizokuwa amewekewa masikioni. Zilikuwa earphone maalumu kwaajili ya kuogea, ambazo zinazuia maji kuingia maskioni na kutoa muziki.

Madame akawa anammwagia maji na lile bomba huku Imaculata akisikiliza muziki uliokuwa ukiimba, mwimbaji wa wimbo ule alikuwa mwanamke ambaye alikuwa akiimba kwa hisia kali sana, sauti yake nzuri lakini yenye kuhuzunisha iliyapeleka mawazo ya Imaculata mbali mno;

“ Furaha uko wapi, wapi umeenda

Umeniacha Mkiwa, Furaha wapi umeenda

Furaha wapi upo popote nitakufuata,

Dunia hii bila wewe, maisha yangu yanawaka moto.

Furaha njoo hata mara moja, nami nitabasamu.

Tazama kila siku kwangu ni kilio,

Haijatokea hata siku nikacheka,

Jana ilikuwa tufani, leo tetemeko

Mbele za watu mimi kioja, moyoni kuna miiba,

Furaha uko wapi, angalau nami nicheke”

Imaculata alijikuta akiingia katika shimo lenye huzuni, ujumbe wa wimbo huo ulihusu maisha yake moja kwa moja. Ingawaje hakujua mwimbaji wa wimbo huo lakini alijikuta akiguswa na kile kilichokuwa kinaimbwa. Mawazo yake yakasonga mpaka kichwani akawa anaona filamu “ Watoto wadogo wenye umri chini ya miaka kumi walikuwa wamevalishwa mavazi meupe mfano wa majoho. Watoto wale walikuwa wanatembea wakiwa kwenye mistari miwili iliyokuwa imenyooka, kila mstari ulikuwa na watoto kumi na mbili hivi. Walikuwepo wakike na wakiume wakiwa wanatembea miguu yao ikienda sambamba kwa mfanano. Mbele yao kulikuwa na Mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa joho lenye rangi ya damu ya mzee kwa upande wa juu na nyeupe kwa upande wa chini. Kichwani yule mwanamke alikuwa amevaa Kofia hivi la mfano wake, walikuwa wakitembea katika njia ambayo upande huu na upande huu kulikuwa na nyasi ambazo zilikuwa zinaelekea kukauka, nyasi zile zilikuwa zikipepeswa na upepo. Imaculata naye alikuwa mmojawapo katika wale watoto yeye akiwa yupo nyuma kabisa ya mstari wa kushoto. Kila mara Imaculata alikuwa akigeuka nyuma ambapo aliona tambarare ndefu yenye nyika na vichaka vifupi ambapo vilikabiliwa na milima yenye misitu mizito iliyofunikwa na ukungu. Akiwa anatazama nyuma ghafla kwa mbali akaona Mwanamke hivi aliyekuwa akitembea akiwafuata huku akiita lakini Imaculata hakuwa akiisikia ile sauti. Imaculata alikuwa amesimama huku watoto wenzake wakimuacha kwenye ule msafara, muda wote alikuwa akimtazama yule mwanamke ambaye alikuwa akimfuata huku akiita, Imaculata akaanza kupiga hatua kumfuata yule Mwanamke aliyekuwa akimuita na sasa sauti yake ilikuwa inasikika kwa mbali ikiita “ Julieta! July! Julieta” kadiri sauti ile ilivyokuwa ikiongezeka ndivyo Imaculata alivyokuwa akikaza mwendo kumfuata yule mwanamke. Punde akakamatwa mkono kutokea nyuma, akageuka, uso kwa uso akakutana na yule mwanamke mwenye vazi lenye rangi ya damu ya Mzee na rangi nyeupe, yule mwanamke aliyekuwa akiongoza msafara wa wale watoto wadogo, “ Unaenda wapi?” Yule mwanamke akauliza, Imaculata akanyoosha mkono upande wa nyuma bila kugeuka, “ Kuna nini?” Yule mwanamke akasema, hapo Imaculata akageuka, alishtuka kutokumuona yule mwanamke aliyekuwa akimuita”

Hapohapo ile filamu iliyokuwa inapita kichwani mwake ikakatika, na hiyo ni baada ya Madame kumnyanyua na kumtupa kwenye Bwawa la kuogea. Kisha Madame naye akajirusha Bwawani, akimfuata Imaculata aliyekuwa akihangaika kujitetea maji yasimdhibiti. Madame aliona kuwa Imaculata hakuwa na ujuzi wa kuogelea, na hiyo ilimaanisha anahitaji msaada. Madame akamfikia Imaculata kisha akamkamata akamuweka kwenye mhimili wake.

“Nitakufundisha namna ya kuudhibiti uhai. Kuyadhibiti maisha kwa namna ya ajabu kabisa” Madame akasema huku akimtazama Imaculata aliyekuwa akiyachuja maneno aliyoyasikia katika ubongo wake.

“ Maisha na uhai. Subiri nikuonyeshe kimoja baada ya kingine, polepole utajionea siri iliyojificha katikakati ya macho ya watu wengi” Madame akasema huku akimvuta Imaculata kwenye kingo ya lile bwawa, alipomfikisha akamuachia. Kisha akasema,


“ Haya ni Maji. Maji yanasiri ya udhibiti wa maisha” Hapo akawa anayachezea kwa kuyarusha rusha na kuuogelesha mkono wake upande huu na upande huu jambo ambalo liliyafanya maji yakatike na kuupisha mkono wake. Imaculata akawa anasikiliza huku akiutazama ule mkono wa Madame.

“Maji ni uhai”

“ Maji ni uhai” Imaculata akawaza akiyafuatisha maneno ya Madame.

“ Ikiwa maji ni uhai ni kwa nini ukiingia ndani yake ukiwa na uhai unazama na unaweza ukafa ikiwa hautachukua hatua mapema ya kujiokoa au kuokolewa? Uliwahi kujiuliza Jambo hilo Malaika mdogo?” Madame akasema,

“ Maisha hayakunipa bahati ya kujiuliza maswali ya namna hiyo. Wenye bahati ndio wananafasi ya kujiuliza maswali ya udadisi na kiugunduzi. Mchana kwangu ni hekaheka na songombingo, Usiku ni mapambano ya kujilinda na wadudu na wanadamu wabaya” Imaculata akasema,

“ Hiyo ndio sababu uko hapa. Hii kwako ungeihesabu kama bahati njema ambayo ni nadra sana kwa watu wengi kuipata. Maji huzamisha watu waliohai wasio na ujuzi wa kuogelea, pengine wasio na watu wa kuwaokoa na dhoruba itokeapo. Ukiweza kuogelea na kufuata kanuni za kuyadhibiti maji wakati unapoogelea basi kanuni hizohizo zitumie katika kukabiliana na maisha yako. Unavyoyaona maisha ni kama bahari kubwa yenye maji mengi, bahari hutaka kuyazamisha na kuangamiza maisha ya watu wasiokuwa na maarifa na ujuzi wa kukabiliana na mawimbi”

Madame alikuwa akiongea kama mhadhiri anayehutubia wanafunzi wa chuo. Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Imaculata kujiona kama mwanafunzi aliyedarasani. Maneno ya Madame yalianza kumvutia, na sasa ile aibu ya kuyakwepesha macho yake mbele ya Madame ikawa inaanza kupungua. Mvuto wa maneno yenye ujuzi ni sumaku kwa ubongo wenye kutafuta ufahamu na elimu. Imaculata akamtazama Madame,

“ Subiri, ngoja nikuoneshe jambo” Madame akaanza kuogelea akienda upande mwingine wa lile Bwawa, Alikuwa akiyakata maji kwa kasi kisha akazamia ndani ya maji na kumfanya mwili wake uonekane kama mwale wa moto unaoyumbayumba ndani ya maji, Imaculata alivutiwa na jambo lile. Shauku mpya ya kutaka kujifunza ikamvaa. Madame alikaa ndani ya maji kwa kitambo kidogo kisichozidi dakika mbili kisha akatokea upande wa pembe ya mwisho kabisa wa lile bwawa, hapo akainuka vuuupu! Kisha akaachia mdomo wake “haaaa!” alafu akaupangusa uso wake na kiganja cha mkono wake kuondoa maji yaliyokuwa usoni. Jambo hilo lilimsisimua sana Imaculata, alijikuta akitabasamu kwa mara ya kwanza tokea aingie katika jumba hilo. Tabasamu lake liliashiria mwanzo mpya katika maisha yake. Kila siku ni mpya kwa sababu kila siku inamambo ya kujifunza, siku isiyo na jambo la kujifunza ni sawa na siku iliyopotea, labda pengine niseme siku isiyokuwa na maana yoyote. Kujifunza kila siku ndio maisha yenyewe. Ladha ya maisha ni mambo mapya yanayotokea katika maisha yetu.

Kisha Madame naye akatabasamu, alafu akamnyooshea mkono Imaculata na kumuashiria amfuate. Imaculata akapigwa na butwaa akiwa anamtazama kwa jicho la kumwambia “Mimi nije, nitawezaje wakati sijui kuogelea” Madame akatabasamu akasema;

“ Njoo Malaika Mdogo” Imaculata akaachia ukingo wa lile bwawa na kuanza kutembea polepole ndani ya bwawa akimfuata Madame, wakati huo Madame naye alikuwa akimpa moyo kwa tabasamu huku akimnyooshea mikono yote miwili iliyokuwa inaashiria kumuita Imaculata. Kadiri alivyokuwa akisonga ndivyo kima cha maji kilivyokuwa kinazidi. Sasa maji yalikuwa marefu usawa wa mabega na yalianza kumzidi nguvu na pumzi ilianza kuwa nzito hapo akafumba macho yake, “ Njoo! Polepole! Njoo! Polepole! Njoo! Njoo! Njoo!” Madame alikuwa akiongea kwa sauti ya kunong’ona ambayo Imaculata alikuwa akiisikia kwa namna yenye kuogopesha, hapo maji yalikuwa yamemfikia shingoni na muda wowote yangemshinda nguvu kwani alikuwa akipepesuka, maji yakijaribu kumbeba. sauti ile ikayapeleka mawazo ya Imaculata mbali angali akiendelea kupepesuka.

“ Katika kambi ya Kulelea watoto Yatima, Imaculata akiwa na umri wa miaka sita hivi akiwa bwenini amelala kitandani ambapo kulikuwa na msururu wa vitanda vya double-decker ambavyo vilikuwa katika ukumbi mrefu wa bweni vikiwa vimepangana upande huu kwa upande huu kama jozi za viatu. Imaculata anaamka, ilikuwa asubuhi, kitanda chake kilikuwa cha juu upande wa dirishani. Mwanga wa jua la asubuhi ulikuwa ukimulika katika dirisha lake lililokuwa na Pazia jambo ambalo lilifanya mwanga ule usiingie ndani kutokana na kuzuiliwa na pazia. Ghafla Imaculata akasikia kwa nje kelele za sauti za watu wanaogombana na kurushiana maneno. Imaculata kwa upesi akafungua pazia kidogo kisha akachungulia kwa nje, kwa mbali upande wa geti la kuingilia kwenye ile kambi akaona walinzi wawili, na mwanamke mmoja ambaye alimtambua kama Matron wao wa kile kituo, pamoja na Mwanamke mmoja ambaye alikuwa akivutwa kwa nguvu ili atolewe nje, jambo hilo likamfanya Imaculata akae vizuri kitandani na kuvuta umakini akiwa anachungulia, mwanamke yule aliyekuwa anatolewa getini alikuwa akilia kwa sauti kali yenye uchungu. Ndiye yuleyule mwanamke ambaye alimtokea wakiwa kwenye msafara na wenzake aliyekuwa akimuita kwa jina la Julieta. Imaculata akawa anajiuliza “ Huyu mwanamke atakuwa ni nani? Kwa nini wanamzuia asiingie?” Wakati anawaza hayo punde alishtuka kuona Matron akiwa amegeuka na kuangalia upande wa dirisha lake, kwa upesi Imaculata akajificha na kufunga Pazia. Pumzi ilikuwa ikimtoka kwa kasi, mapigo ya moyo yalishindana kwa nguvu kusukuma damu. Imaculata alikuwa akitweta kwa nguvu, kisha baada ya sekunde kadhaa akasogea polepole kulifuata dirisha na kulifungua pazia kidogokidogo, Mara Paap! Uso kwa macho akatazamana na Matron” filamu hiyo ikakata “Haaapu” akameza maji, Imaculata alikuwa hatarini kuzama majini. “Mamaaa!” Akapiga kelele “Haap!” Akameza maji tena kidogo. Madame akafanya upesi kwenda kumuokoa. Alipomfikia akamkamata na kumbeba. Imaculata akapoteza Fahamu.

Itaendelea

1. Jipatie softcopy ya Kitabu cha Mlio Wa Risasi harusini Tsh 8,000/=
Hardcopy. Tsh 15,000/=

2. Kitabu cha Wakala wa Siri Tsh 15,000/=
3. Kitabu cha Kaburi la Mwanamuziki Tsh 15,000/=

0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
images (32).jpeg


Vitabu ambavyo Vipo tayari

1. Wakala wa Siri. Tsh 15,000/=
2. Kaburi la Mwanamuziki. Tsh 15,000/=
3. Mlio Wa Risasi harusini. Tsh 15,000/= na Softcopy yake Tsh 8,000/=

Namba ya ya miamala.
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
MLANGO WA 77 "DOOR77" Sehemu 05
Mtunzi; Robert Heriel
Whatsapp 0693322300

Sehemu 05

Ilipoishia


, Mara Paap! Uso kwa macho akatazamana na Matron” filamu hiyo ikakata “Haaapu” akameza maji, Imaculata alikuwa hatarini kuzama majini. “Mamaaa!” Akapiga kelele “Haap!” Akameza maji tena kidogo. Madame akafanya upesi kwenda kumuokoa. Alipomfikia akamkamata na kumbeba. Imaculata akapoteza Fahamu.

************************
ENDELEA

Bango kubwa lenye maandishi Makubwa yaliyonakshiwa kwa namna ya kuvutia lilikuwa likitambulisha jengo lile la ghorofa nne kwa jina “ Fahari Bank” CDF alionekana akizipanda kwa kasi ngazi za ile bank akiukabili mlango wa kuingilia. Uwepo wake ulivuta macho ya watu waliokuwa eneo lile. Walikuwa wakimuona kwenye Luninga lakini leo hii alikuwa anapita mbele yao, ndiye Mkuu wa Majeshi. Akafungua mlango na kuzama ndani, mlinzi alipomuona akapiga saluti na kumpisha, CDF hakujali, haraka yake ilikuwa na maana Fulani ya muhimu ambayo aliijua yeye mwenyewe. Mapokezi pamoja na wafanyakazi wa Fahari Bank walipomuona kila mmoja alisimama kwa heshima, huku wateja waliokuwa kwenye misururu ya foleni na wale walioketi kwenye viti wakishikwa na taharuki. CDF bila kumsalimia yeyote akasonga na kupotelea kwenye mlango uliokuwa mbele kabisa. Huko akakutana na korido yenye ofisi zenye milango na madirisha ya vioo na kingo za alluminium. Kila alikopita macho ya taharuki yaliyojawa na umbeya ya wafanyakazi yalikuwa yakimtazama akitembea. Moja kwa moja akasimama kwenye mlango ambao juu yake kulikuwa na kibao kilichoandikwa “HR Manager” akakishika kitasa na kukitekenya lakini mlango haukufunguka.

“ Shikamoo Mheshimiwa” Sauti ya kike kutokea nyuma yake akaisikia. Akageuka hapo akakutana na uso wa mwanamke mmoja ambaye alikuwa anamfahamu kama rafiki yake Dorice Katiti, Mkewe. CDF akamtazama Yule mwanamke kwa macho yenye uchu na wivu.

“ Aliondoka mapema tuu mara alipofika, alisema hajisikii vizuri, hivyo ameenda hospitali”

“ Hospitali gani?” CDF akauliza,

“ sina hakika, ila niliongea naye dakika kumi zilizopita akaniambia ameshatoka hospitali amerudi nyumbani” Yule mwanamke akasema, CDF baada ya kusikia hivyo akatembea kwa kumkabili yule mwanamke, hapohapo yule mwanamke akasogea pembeni akampisha. Cdf akatoka nje na kupanda kwenye gari lake na kuondoka. Haikumchukua muda kufika nyumbani kwake kutokana na mwendokasi aliokuwa akiendesha gari. Akashuka ndani ya gari kisha akasonga na kulikabili geti la nyumba yake huku akiliacha gari nje ya geti la nyumba yake. Akaingia ndani ya geti kisha akasonga mpaka alipoufikia mlango wa nyumba yake, wakati hayo yakiendelea walinzi na mtunza bustani walikuwa wakishangaa na kubaki na maswali ya nini kimetokea au nini kinaendelea. Moja kwa moja akasonga akiipita sebule na kupanda kwenye ngazi kuelekea ghorofa ya pili. Kisha akasimama mbele ya mlango wa chumba, akasikiliza kidogo lakini kulikuwa kimya, akafungua mlango akapokelewa na kitanda ambacho juu yake alikuwa amelala mkewe, Dorice.

Akasonga mpaka alipokaribia kitanda, akawa anamtazama Mkewe, akainama mpaka kitandani kisha akamuamsha, Dorice alipoamka akapiga mwayo mrefu kisha akawa anamtazama Mumewe ndiye Cdf Haidary, macho yake yalikuwa mekundu kama mtu aliyekuwa amelala kwa muda mrefu. “ Hii inawezekanaje” CDF akawaza huku akiwa anamtazama Mkewe.

“ Kuna nini Mume wangu” Dorice akasema,

“ Mbona uko hivyo, kuna nini Mume wangu”

“ aaah! Hamna kitu”

“ Hamna kitu? Mbona umeniamsha” Dorice akasema,

“ Nimeambiwa unaumwa sana”

“ Naumwa sana! Nani huyo kakuambia?”

“ Wewe unafahamu mimi ninafahamiana na watu wengi, pale hospitali ulipoenda kuna mtu ameniambia”

“ Kwa hiyo umeniwekea walinzi wa kunifuatilia” Dorice akasema, akinyanyuka kutoka pale kitandani.

“ Hapana Mke wangu. Umenielewa vibaya. Wewe ni mtu mzima, unaweza kujichunga mwenyewe kwa nini nikuwekee walinzi wa kukufuatilia”

“ Unajua bado najiuliza, sijaelewa. Inaonekana ndio tabia yako. Kama ningekuwa naumwa sana ningeshindwa kukutafuta mwenyewe? Nilikuwa sijihisi vizuri, nikaona nisikusumbue. Sasa nashangaa imekuwaje umejisumbua kwaajili yangu. Huyo aliyekuambia ndiye anaumwa sana. Haidary sijapenda kabisa”

“ Wala usingenisumbua Mke wangu..”

“ Sitaki kufuatiliwa, mimi sio mtoto mdogo. Unanifuatilia kwani hauniamini?”

“ Hapana Dorry, nakuamini sana. Kama nisipokuamini wewe mke wangu nitamuamini nani? Yaishe tusimkaribishe shetani. Pumzika! Usiseme sana usijepandisha homa” CDF akasema akiwa anampetipeti mkewe.

*************************

“ Afande, naomba kitabu cha wageni” Peter Mirambo akasema, akapewa kitabu cha wageni akawa anakipitia, akaona jina la Dismas Sabuni Kazarage pamoja na namba ya simu, ilikuwa namba ileile ambayo ilikuwa kwenye kile kitabu cha wageni cha kule ndani. Akawa anaiandika ile namba kwenye simu yake kisha akaipigia, ile namba ikawa haipatikani. Akakata kisha akapiga tena lakini ujumbe ulikuwa ni uleule yakuwa namba ile haipatikani. Akawa anatafakari.

“ Kuna tatizo?” Yule Afande Mlinzi akauliza,

“ Uliweza kukikagua kitambulisho cha yule mwanaume aliyeingia asubuhi aliyevalia Suti ya rangi nyeusi?” Peter Mirambo akasema,

“ Ndio nilikikagua, nikaona majina yake na picha vyote vilikuwa sahihi”

“ Ulihakiki Jina aliloandika kwenye kitabu cha wageni linaendana na jina lililopo kwenye kitambulisho chake?”

“ aaah! Amm! Nafikiri nilifanya hivyo”

“ Unafikiri au ulifanya hivyo, nahitaji jibu la kueleweka Afande” Peter Mirambo akafoka, jambo ambalo lilimfanya mlinzi aingiwe na hofu.

“ Jina la kitambulisho chake alikuwa anaitwa…! Anaitwa..! Linakuja na kutoka Mkuu…” Afande Mlinzi akawa anajaribu kukumbuka, jambo hilo lilimfanya Peter Mirambo apandwe na hasira zaidi.

“Ndio.. Sadiki,yes nimekumbuka jina lake ni Sadiki”

“ Hapa aliandika jina gani?” Peter akasema huku akimkabidhi Afande Mlinzi kile kitabu cha wageni, akawa anasoma. Baada ya Afande Mlinzi kuona jina lililoandikwa kwenye kitabu na lile alilolisema linatofauti uso wake ukazidi kusongwa na hofu, uzembe kama ule eneo lile alijua usingevumiliwa na ungemletea matatizo makubwa.

“ Nisamehe Mkuu, nimepitiwa” Afande Mlinzi akasema, Peter akaondoka moja kwa moja lilipokuwa gari lake akapanda, Afande Mlinzi akaenda kufungua geti, kisha Peter Mirambo akatoka, “ Sijui ni kitu gani kimetokea, na sijui nini matokeo yake. Nilifundishwa kujua yaliyonyuma ya kisogo changu ambayo siyaoni machoni, ili niweze kujua yatakayotokea baadaye. Sasa kama hili linataka kunipita, hii itamaanisha matokeo yake nitashindwa kuyadhibiti” Peter Mirambo akawaza, akiwa amesimamisha gari nje ya Geti ya ile Sero maalumu akisubiri magari ya kwenye barabara kuu yapite ndipo naye aingize gari lake barabarani. Akiwa ndani ya gari akakumbuka jambo, akashuka kutoka ndani ya gari na moja kwa moja akaenda kwenye maduka yaliyokuwa jirani na ile Sero maalumu. Kulikuwa na Msururu wa Fremu za maduka zilizopangana ambazo ziliuza bidhaa na huduma mbalimbali. Peter akaingia kwenye duka moja ambapo alipokelewa na kijana. Akaagiza apewe Pakti ya sigara, akapewa, kisha akaifungua ile pakti na kutoa sigara moja alafu akaiweka mdomoni, hapo akamuomba yule kijana kiberiti. Akaiwasha sigara mdomoni kisha akavuta pafu moja kuichochea ile sigara ikolee moto. Alipoona imekolea akamrudishia yule kijana kibiriti. Akatoka, wakati anaondoka yule kijana akamuita “Uncle! Uncle!” Peter akageuka nyuma, akamuona yule kijana ameshika kitu mfano wa kitambulisho. Peter Mirambo akarudi mpaka dukani, pasipo kuongea kitu akakipokea kile kitambulisho, alipokisoma alishtuka, “ Sadick Maa” ndilo lilikuwa jina lililopo kwenye kile kitambulisho. Hapo akakumbuka jina hilo alilitaja Afande Mlinzi.

Peter Mirambo akamtazama yule Kijana wa Dukani, na kabla hajasema kitu yule kijana akasema;

“ Nimeona umetokea kwenye geti hilo. Mwenye hicho kitambulisho alikiangusha alipokuwa anapanda ndani ya gari. Nimeona nawe umetokea humo ndani nikajua ni mwenzenu”

“ Gari yake aliipandia wapi?”

“ Alipokuja alisimamisha gari yake hapa, akaniomba aegeshe kwa dakika chache tuu, sikuwa na sababu ya kumkatalia” Yule kijana muuza duka akasema, maneno hayo yalimvutia sana Peter Mirambo. “ Kumbe gari yake aliisimamisha huku nje” Peter alikuwa akiwaza huku akimtazama yule kijana kwa umakini.

“Ulifanya vizuri, ni mfanyakazi mwenzetu, ila nashangaa iweje aje kusimamisha gari huku ilhali humo ndani kuna eneo kubwa la maegesho, alafu kingine mbona gari yake jana ilikuwa mbovu, hiyo aliyokuja nayo ni aina gani ya gari?” Peter Mirambo akasema,

“ Ilikuwa gari nyeusi hivi, Nissan Dualis” Yule kijana akasema huku mara hii akiwa kama mtu mwenye mashaka kutokana na maelezo ya Peter Mirambo. Jambo hilo Peter aliliona akaona isiwe kesi, akamuaga na kurudi kwenye gari lake. Akiwa ndani ya gari mawazo mengi yenye maswali yasiyo na majibu yalipita kwenye akili yake. “Mwanaume huyu atakuwa ni nani” akasema huku akikitazama kile kitambulisho. “ Cdf anasema hakuongea na Bekha, na wala hakumtuma mtu yeyote. Sasa huyu mwanaume katumwa na nani?” Peter Mirambo bado alikuwa akiwaza. Akakumbuka jambo,

Akatoa Laptop yake kisha akaiwasha, sio ile Laptop iliyoharibiwa siku ile ya Operesheni ya kukomboa Meli ya Mandarin iliyotekwa. Hii ilikuwa Laptop nyingine ambayo nayo ilikuwa na program na mifumo kama ileile ya Laptop iliyokwisha haribiwa Baharini. Hii ni kutokana na kuwa nyakati hizi teknolojia imekua sana, kupoteza kifaa cha kieletroniki cha mawasiliano sio tatizo kwani unauwezo wa kurejesha program, data na mifumo ya kifaa kilichopotea Kupitia Recovery and Restore Processes.

Peter Mirambo akabonyeza bonyeza simu yake, kisha akatoa kifaa Fulani cha kiteknolojia, akakiweka ndani ya kifungashio, alafu akatoka na kurudi kwenye lile duka.

“ Kijana, naomba unihifadhie huu mfuko, kuna mtu nitamuagiza aje aupitie. Pia nimeongea na Sadick nimemjulisha kuwa umenipa kitambulisho chake, ameniambia yupo njiani anakuja. Hivyo atakikuta kwako.” Peter Mirambo akasema, akiwa anamkabidhi yule kijana wa dukani ule mfuko na kile kitambulisho. Baada ya kuhakikisha yule kijana kauweka ule mfuko vizuri akaondoka na kurudi ndani ya gari. Akabonyeza bonyeza Laptop yake kisha akawasha gari na kuondoka.

“ Itajulikana tuu!” Peter akasema, huku akiendesha gari kwa umakini, mkono mmoja ukiwa kwenye usukani, na mwingine akiwa ameshikilia sigara ambayo kuna wakati alikuwa anaipachika mdomoni kisha anavuta pafu kadhaa alafu anaitoa na kuishika mkononi. Tayari ilikuwa imehitimu saa sita za mchana, miale ya jua ikiwa inachoma vilivyo.

“ Itawezekana vipi lakini yule mwanaume afanye uzembe wa makusudi wa kuangusha kitambulisho chake?” akawaza, kisha akasindikiza wazo hilo na kupiga pafu ndefu ya sigara, kisha akasimamisha gari kutokana na taa za kuongoza magari kuwaka rangi nyekundu kwa magari ya barabara aliyokuwepo.

“ Uzembe wa mtu kama yule mwanaume ni mtego kwa watu wasio na ujuzi, lakini sio kwangu mimi Peter Mirambo. Alifikiri kila mtu anaingia kirahisi kwenye mitego. Nakuhakikishia nitakukamata, na wewe ndio utakayeniambia nani yupo nyuma ya haya yote. Unaua watu ili kuficha nini, hutaki ijulikane watekaji wa Meli ya Mandarin Pacific? Kila kaburi litafukuliwa, mizoga na mifupa yote nitaitoa” Peter Mirambo alikuwa akiwaza, tayari taa za kuongozea magari zilimruhusu, akatia gia na kusonga. Tayari alikuwa amefika Makao makuu ya jeshi, baada ya gari lake kukaguliwa, naye akatoa kitambulisho, akaingiza gari, akashuka ndani ya gari. Kisha akasonga moja kwa moja kwenye ofisi ya CDF lakini hakumkuta. Akaitoa simu yake mfukoni kisha akampigia simu, lakini simu ya CDF ikawa haipokelewi. “ Hii inamaana gani?” Peter akawaza, akaamua arudi kwenye gari lake. “ Kuna jambo haliko sawa hapa” Akawaza akiwa anarudisha gari lake nyuma huku akikatisha kwa nguvu kidogo.

“ Noo! Peter usifikirie lolote kwa sasa. Sio wakati wake” Akawaza tena, hapo alikuwa akitoka getini na kuwapungia mkono wale walinzi wa lile geti.

“ Nitaanza na Beatrice alafu nitaenda Goba” Peter akawaza, akachukua simu na kubonyeza bonyeza, kisha akaweka sehemu ya sauti. Simu ikawa inaita, Krii! Krii! Haikuita sana ikapokelewa,

“ Handsome! Leo umenikumbuka sio” Sauti ya Kike kwenye simu iliongea,

“ Handsome wapi Betty. Mimi kila siku nakukumbuka”

“ Labda kwenye matatizo. Hivihivi hujawahi kunikumbuka Peter”

“ Mmmh!”

“ Kwani nasema uongo Peter?”

“ Uongo! Tuachane na hayo upo wapi Betty”

“ Saa sita hii nitakuwa wapi zaidi ya kazini? Yaani nimechoka hapa, unajua nimefanya kazi miaka miwili mfululizo pasipo likizo. Nataka niandike barua niombe likizo ya angalau siku thelasini” Beatrice akasema.

“ Miaka miwili tuu unachoka. Sisi kazi zetu hazina likizo Betty. Muda wote upo kazini kwaajili ya nchi. Sema nini najua jinsi ulivyomchapakazi, unapiga kazi binti sio pouwa”

“ Bora umesema mwenyewe. Peter kwa kweli nahitaji nipumzike ili nika- refresh nguvu ya mwili na akili irejee. Ninachojiuliza likizo nikipewa nitaitumia na nani kama sio wewe”

“ Beatrice unauhakika upo kazini? Unaongea hivyo wenzako hapo hawakusikii?”

“ Wenzangu kina nani? Mimi ofisi yangu huijui? Au unamuogopa Leilah?”

“ Ushaanza mambo yako, Leilah anaingiaje kwenye mazungumzo yetu. Naomba leo tuonane bhana”

“ Makubwa! Tuonane wapi na saa ngapi?” Beatrice akasema.

“ Popote tuu lakini kuna ishu nataka unisaidie”

“ Nilikuambia huwezi nitafuta kama hauna shida, umeniamini?”

“ Betty ni muhimu sana. Natamani nieleze lakini unajua kabisa mimi sio mzuri wa kueleza kama yule jamaa yako”

“ Hapo ndipo ninapogombana na wewe. Nilishakuambia sipendi umtaje yule mpuuzi. Kumbukumbu zake nilishazifuta, lakini wewe ndiye kila siku unakuwa kama karani uliyetunza kumbukumbu zake.”

“ Basi tuachane na hayo, tunaonana wapi kwa kazi”

“ Sijui nitaangalia kwa maana leo ratiba yangu imebana sana. Sidhani kama kwa leo itawezekana” Betrice akasema huku sauti ya mlango wa ofisi yake ukisikika kwenye simu kama umefunguliwa.

“ Betty ni muhimu. Tafadhali”

“ Peter nimekuambia nitaangalia. Kama nitapata muda nitakujulisha lakini kama ukiona kimya ujue ndio hivyo imeshindikana. Uhakika ni kesho. Si unajua kesho ni Jumamosi?” Beatrice akasema, maneno yake yakamfanya Peter akae kimya huku mngurumo wa gari ukisikika.

“ Peter! Peter!” Beatrice akaita,

“Naam”

“ Baadaye ngoja nifanye kazi, kuna mwenzangu kanisimamia hapa” Beatrice akasema, kisha wakaagana. “ Betty naye anataka kunicheleweshea mambo yangu. Kesho ni mbali! Mambo kama haya kuchelewa kidogo inaweza kuharibu kila kitu” Wakati Peter akiwaza hayo Punde simu yake ikaita tena, alifikiri ni Beatrice anapiga lakini alipotazama kioo cha simu akaona jina la Mchumba wake, ndiye Leilah.

“ Bebe beibe!” Peter akasema mara baada ya kupokea simu yake.

“ Sitaki mimi”

“ Why Mpenzi” “ Coz hunikumbuki, hunipendi wala kunijali. Nisipokupigia haunitafuti”

“ No! Leilah! Ubize wa kazi tuu! Mbona jioni ni lazima nikutafute?” Peter akasema, bado alikuwa anaendesha gari yake akielekea Goba, na mara hii alikuwa maeneo ya Makumbusho.

“Yaani Mpaka jioni, huko ndio kunipenda. Tangu asubuhi, mchana wote kimya, alafu jioni ndio unitafute. Huko ndio kunipenda. Alafu unajitetea”

“ Sio kwamba najitetea, anyway nisamehe mpenzi wangu. Nilikuwa najaribu kukueleza jinsi kazi zinavyonibana..” Peter akasema kwa sauti ya huruma, jambo ambalo lilimfanya Leilah amuonee imani.

“ Usijali Mpenzi wangu, My husband to be. Naelewa. Ila sasa mimi nakumisi sana bebe”

“ Jua ninakupenda…”

“ Najua Peter, unajua leo ni ijumaa, nataka jioni tuonane, nimekumiss sana. Hapa ndio nimetoka kununua chakula ili nipike, hakika utafurahi.”

“ Chakula gani Honey?”

“ Utakipenda! Mimi ndiye Leilah. Ukija jioni utakiona. Yaani utakifurahia sana” Leilah akasema.

“ Lakini Mpenzi, nilifikiri nije kesho”

“ No! Sitaki! Sitaki mimi! Baby why unapenda kuniona nakasirika”

“ Okay! Nitajitahidi..”

“ Kujitahidi hiyo vipi? Sema utakuja. Au nakulazimisha?”

“ Kuna jambo, ila anyways nitakuja mpenzi. Nione mapishi ya Leilah mtoto wa,,”

“ Kipemba” wakaitikia wote kisha wakacheka. Baadaye wakaagana.

“Hapa Ratiba inaweza kuingiliana, Betty anaweza kupiga simu nikaonane naye muda ambao Leilah naye anataka niwe nyumbani kwake” Peter akawaza akiwa amechukua njia ya Bamaga akitafuta Sinza barabara ya Shekilango.

“ Ingekuwa pouwa kama Betty angenitafuta kabla ya muda wa jioni, najua kabisa jioni na usiku wa leo Leilah anahitaji niwe naye. Embu acha tuone jinsi itakavyokuwa” Peter akawaza, wakati huo akiwa ubungo mawasiliano. Hapo akaingia chuo kikuu cha Dar es salaam na kutokea upande wa pili akielekea Nyumbani kwake Goba.
iTAENDELEA
KESHO MCHANA.

Vitabu vilivyotayari
1. Mlio wa risasi harusini Tsh 15,000/= Hardcopy. Softcopy 8000
2. Wakala wa siri Tsh 15,000

namba za miamala
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 
MLANGO WA 77 "DOOR77" Sehemu 06
Mtunzi; Robert Heriel
Whatsapp 0693322300

Sehemu 06
ENDELEA

Jumba lake la Goba ndilo alilokuwa anapendelea kufanya shughuli zake za kipelelezi. Vifaa vyake vya kazi alikuwa akivihifadhi katika jumba hili. Mafundi walioijenga nyumba hiyo ndio watu pekee ambao waliwahi kujua mmiliki wa nyumba hiyo kwa kumuona kwa sura, lakini wengine wote hawakujua. Hata mmiliki wa hicho kiwanja wakati anauza alikiuza kiwanja hicho kwa kampuni iliyojitambulisha kama BUMBLEBEE ambayo ipo mahususi kwaajili ya kuvuna asali na malighafi zake ikiwa ni pamoja na kutengeneza mizinga. Mmiliki wa siri wa hiyo kampuni ni Peter Mirambo lakini kwa umbo la nje yupo mmiliki bandia ambaye ndiye aliyewahi kukutana na muuzaji wa kiwanja hicho.

Kulikuwa kuna nyumba mbili, jumba la ghorofa moja ambalo lilikuwa Upande wa juu ambapo ndipo mbele kulikokuwa na geti, na nyumba kubwa ya kawaida iliyokuwa upande wa chini ambapo ni nyuma kulikokuwa na bustani za mbogamboga na miti ya matunda.

Peter Mirambo akiwa kabeba ile Laptop akaingia ndani ya jumba la ghorofa, kisha moja kwa moja akaenda kwenye chumba chake cha kazi ambacho kilikuwa chumba cha siri kilichokuwa chini kabisa ya ardhi. Akaweka mambo sawa katika mpangilio aliokuwaa anautaka. Chumba chake kilikuwa hakina nuru sana, zilikuwepo taa za kipekee ambazo zilitoa nuru hafifu iliyokadiriwa. Jambo lililofanya chumba kile kiwe na giza upande wa juu na nuru hafifu upande wa chini alipokuwa amekaa kwenye kiti, mbele yake kukiwa na luninga iliyopachikwa ukutani. Chini ya luninga ilikuwepo meza ndefu ambayo juu yake akaiweka Ile Laptop ambayo iliongeza ziada ya vifaa vingine vya kisasa vya kitekonolojia vilivyokuwa juu ya ile meza.

Peter akaiwasha ile Laptop, kisha akabonyeza bonyeza, kwenye kioo kukatokea namba zenye asilimia zilizokuwa zikiongezeka, “asilimia arobaini! Sitini na tano, sabini, themanini, kisha Mia moja. Please wait!” Ndivyo kioo cha Laptop kilivyokuwa kinaonyesha. Punde Kioo cha laptop kikaonyesha picha ya laptop na mshale ulioelekea kwenye picha ya camera ya cctv. Chini ya picha hizo kulikuwa na maelezo yaliyosomeka “ Completely Paired Devices” Kisha chini yake kulikuwa na neno “ Connect” Peter Mirambo akabonyeza kwenye neno hilo. Hapo ikazunguka kwa kitambo kisha moja kwa moja kioo cha Laptop kikaanza kuonyesha video ya kile kilichokuwa kinaendelea kule kwenye lile duka la yule kijana. Peter Mirambo alikuwa amedukua mfumo wa uchukuaji wa picha na video katika cctv camera ya duka la yule kijana.

Kwenye upande wa juu kushoto kwenye Laptop wakati Camera inaendelea kuonyesha na kurekodi matukio yanayoendelea dukani, kulikuwa na vialama vinne ambavyo Peter akavibonyeza, kulikuwa na menu ambayo kulikuwa na video zingine zilizokuwa zimerekodiwa” Video zilizohifadhiwa” Zilikuwa zimehifadhiwa kwa kila lisaa. Peter akabonyeza video iliyorekodiwa muda ambao yule mwanaume alifika. Hapohapo Peter akawa anaipeleka mbele mpaka alipoona gari aina ya Nissani Dualis ikiwa inasimama mbele ya lile Duka la yule kijana.

Akamuona yule mwanaume akishuka na kuzungumza jambo Fulani na yule kijana kisha akaondoka akiliacha gari lake mbele ya lile duka. Alipofika mbali Kamera haikuweza kumchukua hivyo hakuonekana. Peter Mirambo akapeleka mbele tena kidogo, akamuona yule mwanaume akirudi, raundi hii alikuwa na wasiwasi, akiwa anatazama huku na huku na mara kwa mara nyuma. Akamfuata yule kijana akatoa noti ya shilingi elfu kumi kisha akampa yule kijana ile pesa, alafu akaondoka akilifuata gari lake, wakati anapanda akawa anaingiza mkono mfukoni kama anaiweka simu lakini ghafla alipokuwa anautoa mkono ukatoka na kitambulisho, kikaanguka. Peter akarudisha hicho kipande na kurudia kukitazama kwa makini jinsi alivyokuwa anaingiza mkono mfukoni na kuutoa mkono mfukoni. Peter Mirambo akatabasamu. “ Nilikuambia uzembe wa mtu kama wewe ni mtego kwa watu wasio na ujuzi. Sio kwa Peter Mirambo”

Peter akili yake ilimwambia kuwa Yule mwanaume atakuwa amefanya makusudi kudondosha ile kadi. “ Plate number” Akasema, kisha akairudia ile video lakini kwa bahati mbaya lile gari lilichukuliwa ubavu wake na juu, Upande wa mbele na nyuma ambapo kuna Plate number hakukuweza kuchukuliwa na cctv camera. “ Hapana! Huyu mtu anajifanya anaakili sana. Peter bado hawezi kukushinda. Wewe ni zaidi yake” Peter akawaza, mapigo yake ya moyo yakiwa yamefufuka. Wasiwasi wa kukutana na kisiki katika kazi yake ikamkumba. Hapo akanyanyuka na moja kwa moja akalifuata jokofu, kisha akachukua chupa kubwa yenye pombe, akamimina kwenye bilauri ya kioo, kisha akabwia fumba mbili. Alafu akarejea kwenye kiti. Akaweka ile bilauri juu ya meza. Kisha akawa anaitazama ile video kwa umakini. Hapo akashtuka, akarudisha nyuma tena, akaachama mdomo, kisha akatabasamu. Akachukua ile bilauri ya kioo na kubwia tena fumba la pombe mdomoni. “Nilikuambia wewe ni bora” Akajiambia. Kwenye ile video ilionyesha jirani la lile duka la yule kijana kulikuwa na Saluni ya kike yenye milango ya vioo iliyofunguliwa, hivyo wakati gari la yule mwanaume linakuja na kuondoka vile vioo vilionyesha upande wa mbele na nyuma wa ile gari ambapo zilikuwepo Plate number. Peter akachukua kalamu yake na kuiandika ile Plate number.

Masuala ya uchunguzi yanahitaji umakini katika kuzikusanya taarifa, kuzitafsiri, kuzichanganua na kuzihifadhi. Kila jambo na kila kitu katika mazingira wakati matukio yanaendelea hutoa na kuhifadhi taarifa muhimu kwaajili ya kutunza kumbukumbu ya kile kilichotokea. Wapelelezi na majasusi mahiri wanajifunza zaidi kwenye namna ya kuwasiliana na mazingira. Kusikia sauti ya vitu visivyosema, kuona yale yaliyojificha.

Peter Mirambo akaenda bafuni kuoga. Alipomaliza tayari muda ulikuwa umesonga yapata saa tisa adhuhuri. Njaa ilikuwa imeshagonga hodi katika tumbo lake. Asingeweza kujipikia, chaguo alilokuwa amebakiwa nalo ni kwenda kununua chakula. Akatoka na kupanda kwenye gari huku mara kwa mara akitazama simu yake kuona kama Beatrice amemtafuta lakini hakuambulia kitu. Akafika Mbezi Beach akaingia moja ya migahawa maarufu, akaagiza chakula na akala.

“ Who is Imaculata?” Peter akawaza, akiwa anajifuta midomo yake na kitambaa baada ya kumaliza kula. Maelezo ya Tarikh aliyeuawa ambaye aliyatoa hayakuwa yanajitosheleza yalimfanya afikirie sana. “Imaculata ndio nani? Ndio nini? Wapi yupo? Imaculataaa.. “ akawaza. Tayari ilikuwa saa kumi na nusu, muda ulikuwa unakimbia kama siku ya kiama. Punde ujumbe kwenye simu yake ukaingia, “ Nimekumiss sana Mpenzi. Usichelewe kuja. Mwaaaa” Alikuwa ni Leilah mpenzi wake. “ Usijali! Mapema tuu nitakuwa hapo. Nakupenda Mpenzi” Akajibu.

Kisha simu yake ikaita, alikuwa ni CDF Haidary Mwera.

“ Nini kinaendelea huko. Umefikia wapi?” CDF akasema,

“ Aaaah! Bado naendelea kufuatilia kilichotokea”

“ Haujapata chochote mpaka sasa, bado huyo aliyekuja kuua wale vijana hujampata wala kumjua?”

“ Niko mbioni Mkuu. Nipe muda..”

“ Muda nimeshakupa tayari lakini umefanya uzembe mapema kabisa, unafikiri kwa hali hiyo tutafika. Vipi uliweza kwenda kumhoji Bekha?”

“ Hapana mkuu” “ Unasubiri nini? Uzembe wa aina ile sio wa kupuuzwa Peter. Haujafundishwa hivyo?” CDF akasema,

“ Inawezekanaje Bekha afanye uzembe wa namna ile?” Peter akawaza akiwa anaitafakari sauti ya CDF, bado CDF alikuwa akizungumza;

“ Kwa sasa unaenda wapi?”

“ Naenda kufuatilia ile namba iliyokuwa kwenye kitabu cha wageni ambayo uliipigia simu akaongea mwanamke”

“ Achana nayo” CDF akasema, Peter akakaa kimya akijiuliza kwa nini, hata kukutana na Beatrice ni kwaajili ya mawasiliano ya hizo namba.

“ Achana nayo. Nimetoka kufuatilia, Wametumia teknolojia ya Voice changer kubadilisha sauti, hivyo hapo muhimu ni kufuatilia mwanaume yule ni nani aliyeongea na Bekha”

“mmh! Anhaa! Sawa Mkuu haina shida”

“ Vizuri! Au ulikuwa tayari unataarifa Fulani muhimu uliyoipata ambayo inaweza kutupa muelekeo mzuri” CDF akasema,

“aa ndio! Hapa..ana. Nilikuwa namaanisha hapana” Peter akajibu,

“ Okay! Anyway, fuatilia jambo hilo kwa haraka. Usisahau kumhoji Bekha” CDF akasema, kisha wakaagana. Peter akaingia ndani ya gari lakini maswali mengi yalikuwa yakigonga kwenye kichwa. “ Teknolojia ya Voice Changer, sawa inawezekana. Lakini mbona nimhoji Bekha sasa wakati tayari ameshagundua kuwa huenda yule mwanaume aliyempa simu Bekha alitumia teknolojia ya kubadili sauti ya kwenye simu na kuchukua sauti ya CDF ili kumrubuni Bekha. Kwa nini CDF anasisitiza nimhoji Bekha?”

“Achana nayo. Nimetoka kufuatilia” Maneno ya CDF yakajirudia kichwani mwake. Hapo tayari ilikuwa imehitimu saa kumi na moja na nusu jioni. Alikuwa akielekea Nyumbani kwake Makongo. Kwa vile aliambiwa asifuatilie ile namba hakuona umuhimu wa kupigiwa na Beatrice. Sasa alikuwa amefika nyumbani kwaajili ya kuoga na kujiweka sawa akakutane na mpenzi wake Leilah. Alimkuta Housemaid kama kawaida akiendelea na majukumu yake. Baada ya kujiandaa alikuwa tayari kutoka tena. Hiyo ilikuwa inakaribia saa moja jioni, usiku ukiwa umeingia. Simu yake ikaita, alikuwa ni Leilah! “ Yeas Beibe! Niko njiani. Sio muda nitakuwa hapo. I love you too” Peter alikuwa anaongea, kisha akakata. Akafika Kimara Mwisho lilipokuwa Daraja, hapo akamkumbuka Julieta. “ Aliniambia yeye na wenzake wanaishi kwenye daraja hili” Akawaza akiwa anapita chini ya Daraja hilo huku akichungulia Kupitia dirisha akilitazama lile daraja. Mbele kidogo kulikuwa na U – turn ambayo aliitumia kwenda upande wa pili ambapo kulikuwa na Hospitali pamoja na Kanisa Katoliki. Akasonga mbele kidogo, akaipita hospitali mbele kidogo akakutana na watoto wadogo chokoraa. Akasimamisha gari, akawatazama walivyokuwa wanaokota okota uchafu, na vyakula vilivyokuwa vinatupwa na wapita njia. Hapo akashuka ndani ya gari kisha akawafuata. “Msile uchafu. Chukueni hii” akasema akiwa anawakabidhi mkate aliokuwa ameununua muda mfupi tuu. Wale watoto wakaangaliana kisha wakaukimbilia ule mkate na kumpora Peter. Tukio hilo lilifanya watu wakawa wanamshangaa Peter na wale watoto. Akawapa elfu tano kisha akarudi kwenye gari lake. Hiyo ilikuwa yakaribia saa mbili za usiku.

Akiwa ndani ya gari punde simu ya ikaita, alikuwa ni Beatrice. Hapo akajikuta moyo unadunda. Hakujua apokee au asipokee. Lakini kama asipopokea haitakuwa ni uungwana. Akapokea,

“ Handsome! Njoo tayari nimesharudi nyumbani na nimetulia” Beatrice akasema, “ Sawa nakuja, nashukuru” Peter akasema, hapohapo Beatrice akakata simu.

Peter akashusha pumzi kwa kuchoka.” Niende kwa Leilah mpenzi wangu au niende kwa Beatrice? Huku mapenzi kule kazi” Akawaza. “ Lakini CDF kaniambia nisifuatilie” Akawaza, huku mbele yake Kupitia kioo cha gari lake akiwaona wale watoto wakigawana vipande vya mkate aliokuwa amewapatia. Taa za maduka na giza zikafanya tukio hilo kuwa la namna yake. “ Beatrice ananisaidia kwa kazi nyeti kama hizi. Kama nisipoenda hatanifurahia. Na vipi upande wa Leilah” Akawaza,

Akili nyingine ikamjibia, “ Leilah ni mpenzi wako, atakusubiri. Wewe nenda kwa Beatrice ukafanye kazi, kisha urudi kwa mpenzi wako. Utakuwa umeua ndege wawili wa jiwe moja”

“Yes” Peter akasema, akili yake hiyo alikubaliana nayo. Lakini mara ghafla akili yake ya upande mwingine ikamwambia “ Beatrice anakaa Kigamboni. Mpaka uende, ufanye kazi, kisha urudi utakuwa umechelewa. Unauhakika Beatrice ukifika atakuruhusu uondoke?” Hapo Peter akajikuta akijiegemeza polepole kwenye kiti cha gari kwa kuchoka.

Vipi wewe ungechagua uende wapi?

Peter akawasha gari, huyo akasonga mbele kuelekea kwa Leilah lakini kabla hajamaliza umbali wa mita miamoja akakatisha gari na kurudi. Alikuwa akiendesha sasa mbiombio kwa fujo na kutimua vumbi jambo ambalo liliwafanya wapita njia kumpisha, wakimshangaa na wasio na uvumilivu kumtukana. Lakini waliyekuwa wanamtukana wala hakuwa anawasikia hivyo ilikuwa kazi bure. Akatokea Morogoro Road, akatisha kushoto kuelekea upande wa Mjini. Hapo akaongeza mwendo huku akijisemesha “ Naenda mara moja, nitarudi kwaajili yako. Mara moja tuu” Alikuwa anaongea mwenyewe “ Narudi sasa hivi, umesikia mrembo” hapo alikuwa akisema huku akiingalia simu iliyokuwa inaita, aliyekuwa akipiga ni Leilah, huku kioo cha simu hiyo kikionyesha picha ya Leilah aliyekuwa anatabasamu. “ Sasa hivi narudi mpenzi” akasema tena na kila alipokuwa anasema ndivyo alivyokuwa anaongeza mwendo, muda huu alikuwa anapandisha kwenye Flyover ya ubungo. Leilah bado alikuwa anapiga simu huku akituma ujumbe.

“ Niko njiani Mpenzi, muda mfupi nitakuwa hapo” Peter akasema, Leilah akakata simu.

Hapo alikuwa ameshafika Kivukoni. Baada ya kuvuka kwenye kivuko. Dakika tano zilikuwa nyingi. Alikuwa amesimama kwenye geti la kijivu. Akapiga honi. Kisha Mwanamke mrefu mwenye wembamba wa kati akatoka akiwa kavaa kipenzi kifupi kilichoishia robo ya juu ya mapaja yake, na kiblausi chepesi kilichokuwa hakina kifunguo kilichotawanyika huku na huku kama koti, katikati akiwa kavaa kitopu kilichoyastiri maziwa yake madogo yanayofanana na mwili wake, na kuacha kitovu nje. Baada ya kufungua geti, Peter akaingiza gari, geti likafungwa.

“ Ukiwa na shida ndio unanisumbua, ni lini utanitafuta ukiwa na shida na mimi?” Beatrice alikuwa akiongea huku akitembea mbele ya Peter kizembezembe na kwa kudeka akimuongoza njia Peter kuelekea ndani.

“ Nafikiri kabla hatujafanya chochote, tungeanza kazi Betty” Peter akazungumza alipomuona Beatrice anaenda kwenye jokofu kuchukua kinywaji. Beatrice akamkata jicho ambalo Peter alijikuta akisema “ Kama utakavyo My Lady” Hapo Beatrice akachukua chupa kubwa la Wine. Kisha akafika alipokuwa ameketi Peter naye akaketi kwenye lilelile Sofa. Akamimina Wine kwenye vikombe maalumu vya kunywea Wine. Kisha akaifunga ile chupa yenye Wine iliyobakia.

“ Unahitaji nikufanyie kazi gani?” Mazungumzo yakaanza mara baada ya kila mmoja kubwia fumba moja la wine.

“ Kuna kazi Betty. Hii inaweza kuwa kazi yangu ya kwanza kuwa ngumu.” “ Kivipi”

“Ingefaa ungeleta vifaa kabisa, tuwe tunazungumza huku kazi ikiendelea”

“ mmmh! Mbona kama unaharaka! Leo haulali?” Wakati Beatrice anaongea hayo, punde simu ya Peter ikaanza kuita,

“ Nilijua tuu!” Beatrice akasema alipoona jina la Leilah kwenye simu ya Peter, simu ikiwa inaita.

“ Pokea! Mpokelee simu Mke wako. Unaogopa?” “ Sio kwa sasa!” Peter akasema. Akiwa anabonyeza ile simu na kuondoa sauti ili hata Leilah akipiga simu isije ikapiga kelele. Baada ya kufanya hivyo akamtazama Beatrice kisha akasema “ Beatrice naomba unifanyie kazi iliyonileta hapa. Usiku huu kabla ya saa nne nina kikao na mtu muhimu…”

“ Leilah.. sio!” “ Inatosha Betty, kama haupo tayari kunifanyia kazi niambie, nisipoteze muda wangu. Kazi iliyombele yangu ni ngumu, inategemea kile kilichonileta hapa. Boss wangu amenipa muda mchache, alafu na wewe unataka kuupoteza muda huo…” Peter akafoka huku akimtazama Beatrice.

“ I’m sorry! Ni hasira tuu. Sijakusudia kusema neno la kukuumiza, kazi utakayonifanyia ninatakiwa kuipeleka kama ripoti kwenye hicho kikao cha saa nne. Na ndio maana ilikuwa muhimu ya mimi kuonana na wewe leo” Peter akasema, Beatrice akaamka kisha akaondoka akielekea chumbani. Jambo lililomfanya Peter abaki kumsindikiza na macho asijue nini alichoamua Beatrice. Kitambo kidogo Beatrice akarejea akiwa amebeba Laptop yake pamoja na vifaa Fulani vya kiteknolojia. Akaweka ile Laptop na vile vifaa juu ya meza kisha naye akaketi bila kusema chochote. Akachukua chaji ya Laptop na kuichomeka kwenye Laptop na kuiunganisha kwenye Switch Socket alafu akaiwasha laptop. Wakati Laptop inawaka akachukua kifaa Fulani cha kiteknolojia akakichomeka kwenye Laptop. Ilikuwa Usb Security Key ambayo ni kifaa cha kielektroniki ambacho moja ya kazi yake ni kulinda na kutunza neno la siri la mtumiaji wa simu au vifaa vya kikompyuta na programa au Apps zilizo kwenye simu au Kompyuta ikiwemo Laptop. Baada ya Laptop kuwaka Moja kwa moja Beatice aliingia kwenye programu maalumu ambayo aliboibonyeza ilihitaji neno la siri “Password” hapohapo akaingia kwenye faili jingine la Usb Security Key akabonyeza bonyeza kisha likaja neno la siri, akachukua hilo neno la siri na kuingiza kwenye ile Programu maalumu papohapo ile Programu ikafunguka, na kuonyesha alama za kitekonolojia ambazo Beatrice pekee ndiye aliyekuwa anazijua.

Peter Mirambo alikuwa anatazama tuu. “ Nafikiri tunaweza kuanza” Beatrice akasema kwa sauti isiyo na mzaha. Ni kama alikuwa amechukizwa. Hata hivyo Peter Mirambo hakujali.

“ Leo asubuhi kuna simu ilipigwa pale ofisini kwetu, nataka kujua simu hiyo ilitokea wapi?” Peter akasema,

“ Ilikuwa asubuhi ya saa ngapi, anyway! Naomba unitajie IEE 802 ya ofisi yenu” Beatrice akasema, Peter akawa anaitaja huku Beatrice akiingiza kwenye Laptop. Baada ya kuiingiza akabonyeza sehemu iliyoandikwa link. Kisha kioo cha Laptop kikawa kinaonyesha kiduara kinachozunguka kama kinatafuta mtandao.

IEE 802 ni mkusanyiko wa viwango vya mtandao ambavyo vinashughulikia vipimo halisi vya safu ya kiungo cha data kwa teknolojia kama vile Ethernet na Wireless. Na hapa Beatrice alikuwa akitaka WI-FI “wireless Fidelity” ya Sero Maalumu. Alichokuwa anataka kukifanya ni kudukua mfumo wa WI-FI ya Kule Sero Maalumu.

“ Mtandao leo haupo vizuri” Beatrice akasema, dakika kumi zilikuwa zimeisha tangu Laptop ianze kutafuta mawimbi ya mtandao na kiungo cha data kutoka kwenye wi-fi aliyokuwa ameitoa Peter. Kwenye mfuko wa Suruali wa Peter simu bado ilikuwa inaita, alikuwa akiisikia ikitetemeka kwenye paja lake lakini hakutaka kuitoa. Akaangalia saa yake ya mkononi ambayo ilikuwa inaonyesha ni saa tatu na robo.

“ Hicho kikao chake sidhani kama utawahi. Naona mtandao leo uko chini” Beatrice akasema.

‘ Hakuna njia nyingine ya kuongeza kasi ya mtandao?” Peter akasema, Hapo Beatrice akamtazama, akabinua mdomo wake, alafu akayafinya macho yake kidogo.

“ Njia zipo”

“ Sasa kwa nini tunasubiri. Tutumie njia hizo. Huoni muda umeenda” Peter akasema,

“ njia zingine tukizitumia zitatoa ujumbe wa hatari kwenye mfumo wa ulinzi wa mtandao wa nchi. Hiyo inaweza ikasababisha wakaona kile tunachokifanya na kukiwekea kizuizi cha kimtandao. Kama hiyo haitoshi hata hapa tulipo watapaona Kupitia mifumo ya kimtandao. Unafikiri nini kitatokea kama tukikamatwa?”

“ Kwa hiyo tutatusubiri mpaka muda gani?”

“ Peter! Mimi nitajuaje? Muhimu ni tuwe na subira” Beatrice akajibu, ukimya kidogo ukatokea kisha Beatrice akaongeza “ Kama ningejua unaharaka kwa kiwango hiki wala nisingekubali uje nyumbani kwangu”

Peter wala hakuzungumza kitu, hata kile kinywaji kwake hakikuwa na maana yoyote. Kilichokuwa kimemleta ilikuwa kazi, lakini ndio hivyo tena mambo hayaendi kama alivyokuwa amefikiria. “ Maskini Leilah atakuwa amenisubiria mpaka amechoka. Lazima atakuwa amechukia. Hiki nilichomfanyia hakipendezi” Peter akawaza, muda huo Beatrice alikuwa anapangusa simu yake akiperuzi mtandaoni. Kuna wakati alikuwa akicheka, kuna wakati alikuwa anabonyeza vitufe kwa kupendezwa kwenye machapisho yaliyomfurahisha. Kuna wakati alikuwa anafungulia video ambazo zilikuwa zinapiga kelele na kumshtua Peter ambaye alikuwa akimuwaza Leilah.

Peter aliangalia tena saa, ilikuwa saa nne kasoro robo. Hapo akanyanyuka, jambo ambalo likamfanya Beatrice aache kuchezea simu yake na kumtazama. Peter akatembea mpaka kwenye Showcase ya Luninga, akachukua Remote ya Luninga na kuiwasha. Kisha akarudi kuketi.

“ Hapo umefanya la maana, huu mtandao leo unaweza kukufanya leo ukalala hapa” Beatrice akasema, Peter akamtazama kwa macho ya hasira zilizodhibitiwa alafu akampuuza, akawa anaangalia muziki uliokuwa unaendelea kwenye luninga. Punde wakati Peter amehamisha umakini wake kwenye Luninga akasikia Beatrice akisonya, Peter akamtazama Beatrice kisha kwenye Laptop. “ Yes! Yes! Wozaaa!” Peter akaruka huku akishangilia baada ya kuona Laptop ikiwa imefunguka.

“ Muone umefurahi eeh! Yaani hii Laptop imejua kunikera” Beatrice akasema,

“ Kazi nzuri sana Betty, wewe ni mwanamke bora katika taaluma hii. Kila siku nakuambia taifa hili linajivunia wewe. Unaona! Huyu hapa! Ilikuwa muda huu! Embu itazame hii namba” Peter akasema akiwa ameinama kwenye Laptop. Macho yao wote yalikuwa kwenye Kioo cha Laptop.

“ Kaa Basi!” Beatrice akamuambia Peter kwa sauti ya mtu ambaye amechukizwa.

“ Hii namba imesajiliwa kwa jina Sadick Maa Suleiman, tarehe ya usajili ni jana. Imewasiliana na namba mbili. Namba ya kwanza ni hii” Beatrice akasema, Peter akawa anaiangalia ile namba, akaikumbuka ndio ileile namba iliyokuwa imeandikwa kwenye vitabu vya wageni.

“ Namba ya pili ni hii” Beatrice akasema, raundi hii Peter akasonda kidole kwenye Laptop, hapo akawa anatoa macho “ Zimefanana mbona hizi namba” Peter akasema,

“ Hazijafanana!” Wakajikuta wakisema wote kwa pamoja. Baada ya Peter kuona tofauti ya namba moja ya katikati.

“ Hii ya kwanza inatisa wakati hii ya pili inasita. Zote zipokatikati” Bearice akasema, Peter macho yake bado yalikuwa kwenye kioo cha Laptop. Zile namba zilikuwa zimefanana sana kiasi kwamba kama mtu asipokuwa makini katika kuzitazama anaweza kujua ni namba moja. “Angalia usajili wa namba ya pili”

“aaam! Ooh! Hii imesajiliwa kwa jina la Dismas Sabuni Kazarage. Nayo Imesajiliwa jana muda uleule iliposajiliwa namba ya kwanza, eneo lilelile na wakala wa usajili ni yuleyule. Hii imepiga kwa namba ya kwanza, kisha kuna namba ilijaribu kuipigia lakini haikuwa inapatikana” Beatrice akasema, maelezo hayo yakamkumbusha Peter alivyokuwa akiipigia namba ile asubuhi.

“ Namba hii ya kwanza ilipigiwa na namba hii asubuhi, walizungumza dakika moja na sekunde tano. Mpigaji alipiga akiwa Ofisini kwenu, mpiwaji alikuwa maeneo ya Mjini” Beatrice akasema huku akibonyeza kwenye alama ya nyekundu kama ishara ya mahali ilipokuwa simu ya aliyepigiwa, punde kwenye kioo ikatokea ramani, kwenye ile ramani kulikuwa na kitufe kiduara chekundu, wakaikuza mpaka walipoona jina la Hoteli ambapo muongeaji wa ile simu alikuwako.

“ Alikuwa kwenye hii Hoteli” Beatrice akasema, Peter akawa anasoma jina la ile Hotel.

“ Vipi kuhusu Voice Changer Teknolojia, haikutumika?” Peter akasema,

“ Mmmh! Embu ngoja tuone. Sidhani lakini…!” Beatrice akarejea nyuma kwenye mfumo wa awali, akawa anazihakiki zile namba, kisha akasimama na kwenda chumbani. Baada ya dakika mbili alikuja na CD mbili zenye picha na alama za kiteknolojia. Akaingiza moja ya zile CD kwenye Laptop. Kisha Laptop ikaanza kunguruma alafu ikanyamaza. Ikaja video yenye maandishi Fulani ambayo Beatrice aliyabonyeza. Kisha ikatokea picha ya mdoli uliovaa Earphone masikioni, akaubonyeza, ikatokea sehemu inayohitaji kuijaza maneno au namba. Beatrice akarudi kwenye ile Programu maalumu akanakili Code Fulani na kujakuipachika kwenye ile sehemu inayohitaji kujazwa kwa maneno au herufi. Kisha akabofya. Ikazunguka kwa kitambo kisha ujumbe ukatokea “ No voice changer detected”

“ Hapa walikuwa wanazungumza sauti zao zikiwa halisi, hakuna aliyeghushi au kughushiwa. Embu tuweke hii” Beatrice akasema, ujumbe huo ulimchanganya sana Peter. “ Mbona CDF alisema sauti zilichezewa” Peter akawaza, akakatishwa na sauti ya Beatrice “ Hii ya sauti simu iliyopigiwa imechezewa”

Peter mirambo akausogeza uso wake karibu na Laptop kisha akayafinya macho yake kutazama kwa umakini. “ Nafikiri muda huu ndio yule mwanaume alipoingia akampa Bekha simu. Kwa hiyo Bekha hapa alisema kweli” Peter akawaza,

“ Simu zote hazikuwahi kutumia laini isipokuwa siku ya kuanzia jana ziliposajiliwa laini za simu”

“ Hiyo inamaanisha zilinunuliwa jana mahususi kwaajili ya kazi hiyo?” Peter mirambo akadakia kwa swali.

“ Unaweza ukasema hivyo” Beatrice akasema huku akimtazama Peter aliyekuwa anawaza “ Nini kilichomfanya CDF awe na hofu baada ya kusikia wale wazungumzaji wa simu waliokuwa wanaongea na Mwanamke mjeshi?” Peter akawaza.

“ Vipi Peter, nafikiri kazi yako imeshakamilika, sasa hivi ni saa nne na dakika ishirini, wahi kwenye kikao chako”

“ Bado kazi ya mwisho”

“ Kazi gani tena Handsome mwenye maringo?”

“ Nataka nijue Mmiliki wa gari lenye Plate number hii. Pia angalia kama linamfumo wa kimtandao, maana magari mengi ya siku hizi yameundwa kwa mfumo unaoweza kudhibitiwa katika mifumo ya mtandao wa intanet”

“ Sikiliza Peter, wewe wahi kwenye kikao, mimi nitafuatilia na nitakujulisha kabla haujafika kwenye hicho kikao, kwa sasa unachoweza kufanya ni kuondoka usijesema nimeshindwa kukusaidia Handsome wangu” Beatrice akasema, uso wake ulionyesha kujali, macho yake yalitoa nuru ya iliyoakisi upendo uliomo moyoni mwake. Peter akamtazama Beatrice kisha akaachia tabasamu.

“ Huyu ndiye Betty ninayemjua. Toka siku ya kwanza nilikufahamu kwa moyo wenye kujali, na akili yenye maarifa…”

“Shiiii!” Beatrice akaweka kidole mdomoni na kumzuia Peter asiendelee kuongea. Kisha akasema,

“ Muda umeenda. Fanya uende Mpenzi”

Peter akasimama kisha akajiweka sawa tayari kwa kuondoka, “ Kwa heri Beatrice, nakutakia usiku mwema” Akasema,

“ Huwezi kuondoka kama hivyo Peter” Beatrice akasema, Peter akamfuata Beatrice kisha wakakumbatiana, hapo Beatrice akiwa kwenye kifua cha Peter akanong’ona “ Nilifanya makosa makubwa nyakati zile. Najutia maamuzi yangu. Nimepoteza kitu cha thamani katika maisha yangu. Sitaki kuyaharibu maisha yako Peter. Tayari nilikuumiza, kila siku nikikumbuka najiona sistahili kuishi katika ulimwengu wenye kupendwa. Nisamehe Peter” Machozi yakawa yanamtoka huku akisikia mapigo ya Peter yakiongezeka kupiga.

Damu na machozi vinapokutana hisia za huzuni na uchungu huzaliwa. Beatrice alikuwa akiusikia moyo wa Peter ukigonga kama kengele ya kanisa inayowaita wenye dhambi wenye kutubu. Sasa alikuwa amejisalimisha kwa Kuhani ili aungame makosa yake. Thamani ya msamaha aliokuwa anauhitaji ulikuwa zaidi machozi yake.

“ Nahitaji kuwa huru Peter. Nimekuwa mfungwa wa miaka mingi wa hatia hii. Hatia imechafua uzuri wa moyo wangu. Nikipita bararani au hata ofisini watu hasa wanaume wakware hunisifia kwa uzuri huu wa nje wasijue uzuri wa nje ni kama tamthilia ya kuigiza iliyobuniwa. Ninajiona nikizunguka mbele ya nzi, kila nikijaribu kuwafukuza nashindwa. Mimi ni mchafu”

“ Inatosha Beatrice. Nilikusamehe. Wewe ni rafiki mzuri” Peter akasema, akiwa amemnasua Beatrice kwenye kifua chake, sasa alikuwa anamtazama Beatrice ambye uso wake ulikuwa umetepeta kwa machozi.
iTAENDELEA
KESHO MCHANA.

Vitabu vilivyotayari
1. Mlio wa risasi harusini Tsh 15,000/= Hardcopy. Softcopy 8000
2. Wakala wa siri Tsh 15,000

namba za miamala
0693322300
Airtelmoney
Robert Heriel
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom