Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,983
- 10,804
Simulizi : C.O.D.EX. 1
Mwandishi : TARIQ HAJI
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES
C.O.D.EX. 1 ................... SEHEMU YA 1
Allen James ni jina langu, ni dereva wa taxi katika jiji moja maarufu sana duniani Los Angels maarufu kama LA. Kama kawaida mapema vijana tunaingia kazini kutafuta mapeni. Nikiwa nasubiria abiria ghafla aliingia mtu na kunambia niondoe gari. Nami nikifanya hivyo lakini nlipoangalia nyuma niligundua jamaa alikuwa akitoka damu na nlipojaribu kumwambia nimpeleke hospital alikataa na kunambia nimpeleke sehemu ambayo atakua salama. Nilijaribu kufikiria ni sehemu gani hiyo jibu lililokuja kichwani mwangu ilikuwa ni nyumbani kwangu.
Bila kuchelewa niliekea nnapo ishi, nilijaribu kumpatia huduma ya kwanza lakini alikuwa tayari kashapoteza damu nyingi sana hivyo uwezekano wa kuishi ulikuwa mdogo sana. Mwisho kabisa aliniita na kuninong'oneza CODE X, kisha akanipa kitu kama kitambulisho na picha, akanambia nisimtajie mtu yeyote neno lile hadi nitakapomuona mtu alienipa kwenye picha kisha hapo nae akaaga dunia. Nilibakia mdomo wazi nisijue nini cha kufanya kabisa.
Wakati nikiendelea kuwaza hivyo ghafla nikaskia gari zikifunga breki nje ya nyumba yangu. Nilipoangalia kupitia dirisha sikuamini macho yangu baada kuona watu waliovalia suti nyeusi huku wakiwa na silaha nzito. Mshale wa hatari uligonga kichwani mwangu na bila kufikiria nikajikuta nimenyanyuka na kuelekea ulipo mwili wa yule mtu. Nilichomoa bastola yake kwa ajili ya kujihami na haraka haraka nikapitia mlango wa nyuma..
Hata sijui ni kitu gani kilinipata lakini akili yangu iliniambia nielekee moja kwa moja New York City. Na bila kuchelewa niliingia kwenye gari yangu na safari ikaanza. Kwa bahati mbaya sana mmoja wao aliiona gari yangu na kuwashtua wenzake. Kivumbi kakaanza hapo, nilijitahidi kuwakimbia lakini wapi gari zao aina AUDI zilikuwa na uwezo mkubwa sana, hivyo walinifikia na kuanza kunigonga. Nlipoona mambo yanazidi kuwa magumu niliamua kuwapatisha ajali tu, nilifanikiw kwa gari kadhaa lakini bila mategemeo nilipgwa mzinga na gari yangu ikapinduka.
Niliwahi kutoka kabla hawajanifikia na nikaanza kujibizana nao kwa risasi. Mwenyewe nilikuwa najishangaa maana sijawahi kuenda hata polisi lakini kwa jinsi nilivyokuwa nashambuliana nao ni kama nilikuwa nimebobea kwenye utumiaji wa silaha. Nilipohakikisha nimewamaliza nilichukua gari yao moja na safari ya kuekea New York ikaanza.
Safari ya kuelekea New York ikaanza, huku njia nzima nlikuwa nawaza uwezo ule wa kupigana nimetoa wapi maana tokea nipate fahamu zangu sikuwahi kujifunza ngumi. Lakini niliona bora niachane na mawazo hayo. Usiku ulinikuta njiani hivyo nikaona bora nitafute Motel nilale. Siku ya pili mapema niliendelea na safari yangu yenye sintofahamu nyingi, niliwasili New York mnamo saa nne na kidogo.
Niliacha gari sehemu ya maegesho na kuanza kutembea kwa miguu lakini kwa umakini sana. Nilitembea mpaka kwenye hotel moja hivi na kuingia, maajabu nilioyakuta mapokezi yalizidi kunichanganya maana yule mschana aliekuwepo pale alinichamgamkia utasema labda tunajuana kwa muda mrefu sana. Bila hata kuongea kitu alinipa funguo ya chumba. Nilimshukuru na kuondoka huku moyoni nikijaimbia lazima nitafute muda niongee nae kwani anaonekana kujua mengi kuhusu mimi.