FaizaFoxy anavyokomaa kupinga mapenzi nje ya ndoa wengi humuona nuksi humu, sasa tazameni hata Shy tuliekuwa nae JF miaka na miaka na yeye yuko kweny kundi la huyo dada na katajwa jina.
Jamani, wacheni huu upuzi, Jamii inawahitaji. Tena bora uumwe ufe, lakini ile sasa ya kukaaa kuhangaisha ndugu, jamaa na marafiki kukushughulikia kwa maradhi ya kujitakia? bora uumwe magonjwa ambayo hukujitakia na hayako kwenye uwezo wako kuyazuwia, lakini haya ya ngono yanazuilika jamani na njia ni moja tu "abstinence".
Nakumbuka jamaa yetu mmoja alikuwa akiumwa sana kwa muda mrefu, "complications" za UKIMWI na neno lake kila tukienda kumuona ni "nisameheni jamani", nna uhakika alikuwa anaona vibaya anavyotutesa kwa raha zake.
Sote tukapime afya zetu mara tatu au nne. Tukishajijua, tujipangie maisha salama zaidi yasiyo na maambukizi ya ukumwi. Inawezekana. Tusiambukize wengine kwa makusudi.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.