Simulizi ya 'GERANIMO' kwenye front page za magazeti..

Mkuu sio peke yako kuna mada humu nilishawahi kupost nikazikuta magazetini copy and paste! Ubaya hawa acknowledge source! Wengine humu tulisomea uandishi pia sasa tukiamua kurudi huko si itakua kasheshe? Waandishi was habari mjifunze Ku acknowledge source! Huo ndio weledi, otherwise ni wizi wa kitaaluma! Pladgerisim!
 
kuna jamaa facebook anaitwa joseph k nyambeya ni bingwa wa kutoa habari za kijasusi zozote zile ukimuambia tu anakuandalia makala kama alikuwepo vile nina wasiwasi hata hii ulicopy kwake maana ana makala kibao sana
 
Hahahahahah!! You wish..

Haya nenda akakupe posho ya kumfanyia tangazo la bure hapa that is if kama huyo mtu mwenyewe sio wewe!!
Alafu umepotea njia, rudi fesibuku that's where you belong.
 
Ipo wiki, ipo YouTube, ipo web ya Newyok times, ipo web ya Jesse Ventura, etc etc etc ipo kwenye thousands of sources!
Huwezi kusema 'wamekopiana' but FACTS ndizo zinafanana coz facts hazibadiliki but kila mtu ameandika stories yake isipokuwa facts lazima zifanane..
Mkuu usitumie nguvu kubwa kubishana na wapuuzi, hiyo stori wengi wetu tutakua tushaisoma toka vyanzo mbalimbali ila haikua katika mtiririko mzuri kama ulivyotuletea wewe, binafsi nakupa pongezi wenye uelewa tumekuelewa, achana na hao mang'aa wanaokuzingua...
 
alichofanya huyu jamaa ni kuedit kwa kongeza fleva ila siyo muandaji wa story bali amekocopy na kuweka nakshi nakshi
 
Tukisema tuandike stori kuhusu mlima Kilimanjaro, vitu kama urefu wa mlima, barafu iliyo juu ya mlima, vilele vya Kibo na Mawenzi, vyote vitakuwa ndani ya hiyo stori. Tofauti inakuja kwenye mtiririko na utumiaji wa misamiati na mpangilio wake. Hicho ndicho mali ya mwandishi na sheria ya hakimiliki inakilinda duniani kote. Tofauti ya mwandishi mzuri na mbaya ni katika mtiririko wa matukio, uwezo wa kulielezea tukio na matumizi ya msamiati. Hivyo kama The Bold hakukopi na kupesti ile stori kutoka stori nyingine ya Kiswahili, basi ana haki hata kama alichofanya ni kutafsiri tu.

Waandishi wa habari wawe weledi. Mwandishi hapungukiwi kitu akisema makala si yake ni ya mtu mwingine.
 
Tukisema tuandike stori kuhusu mlima Kilimanjaro, vitu kama urefu wa mlima, barafu iliyo juu ya mlima, vilele vya Kibo na Mawenzi, vyote vitakuwa ndani ya hiyo stori. Tofauti inakuja kwenye mtiririko na utumiaji wa misamiati na mpangilio wake. Hicho ndicho mali ya mwandishi na sheria ya hakimiliki inakilinda duniani kote. Tofauti ya mwandishi mzuri na mbaya ni katika mtiririko wa matukio, uwezo wa kulielezea tukio na matumizi ya msamiati. Hivyo kama The Bold hakukopi na kupesti ile stori kutoka stori nyingine ya Kiswahili, basi ana haki hata kama alichofanya ni kutafsiri tu.

Waandishi wa habari wawe weledi. Mwandishi hapungukiwi kitu akisema makala ya yake ni ya mtu mwingine.
kama ingekuwa makala yake basi angeiuza hakuna mtu anayekubali hasara hata siku moja ndio maana tunasema amedit tu hii story ipo mitandaoni kitambo sana
 
Leo asubuhi nilipofika kwenye meza ninayo nunua magazeti siku zote jicho langu likanasa kwenye gazeti la KISIWA.

Kwenye ukurasa wa mbele habari iliyopewa uzito wa juu inasomeka; USIYOYAJUA KUHUSU KIFO CHA OSAMA BIN LADEN.
Nikawa curious kidogo, so nikanunua hilo gazeti nione kama 'yaliyomo yamo?'.. Kufungua ndani duuuuuuuuuuuuhhh gazeti la kisiwa sio 'watu wa mchezo mchezo' yani yani 'wamekopi na kupesti' 100% makala yangu ya 'GERANIMO E.K.I.A: Kutoka makao makuu ya CIA, Langley..'

Sio mbaya though binafsi nimefurahi kuwa makala zetu JamiiForum zimeshiba ndio maana JF imekuwa kimbilio la vyombo vya habari kupata news na makala kama hizi ila ninachowaomba gazeti la KISIWA na wengineo wakumbuke kutoa credit kwa JF kuwa ndio source ya makala yao na mwandishi The Bold.. Fanyeni hivyo wakuu nimeona pale mwishoni mmeandika 'itaendelea toleo lijalo' kwahiyo toleo lijayo toeni credit wakuu (najua mpo humu)..... na kingine nasubiria mnirushie 'ya vocha', LOL
Kawashtaki uchukue hela.

Tena unajua niliisoma ile habari nikaona una kitu kimoja umekosea, nikataka kusahihisha nikapotezea nikasema Kiranga tayari ana reputation ya kujifanya anajua kila kitu, kwa hiyo nisiiendeleze hii reputation, nikapotezea.

Jina la Mkurugenzi wa CIA uliliandika kama Pattena, wakati jina lake ni Leon Panetta.

Hawa mburula kwa jinsi ninavyowajua watakuwa hawajabadilisha kitu hata jina watakuwa wamelichukua hivyo hivyo.

Hilo jina kukosewa hivyo inakuwa kama signature yako kwamba story ilitokea hapa JF kwenye ID yako, mpaka ulivyokosea jina wamekosea hivyo hivyo.

Una kesi hapo unaweza kuwafungulia baraza la maadili ya uandishi.

Hawawezi kuokoteza habari bila hata kukuuliza.
 
Hii makala niliisoma sehemu mbali mbali ila ya kwako inautofuti kidogo ina maana ulichukua kutoka sehemu mbali mbali ukachambua Na kuifanya kumvutia msomaji kwa hilo hongera ila uwe unaweka reference mwisho Wa hadhithi zako kote uliko chukua Na kuwataja waandishi Na vitabu Na makala zao kuwasaidia hawa waandishi uchwara
 
Watu wengine wanapost vituko humu eti wamekopi makala yake hii kitu mbona ni ya siku nyingi sana
 
ulichoandika jamaa anakipinga ndio maana hata mie nambishia ila yeye bado anabisha sijajua kwanini au ni Afisa jeshi la marekani mpaka adiriki kusema ndiye aliyetoa chanzo cha mauji ya Osama
 
kama ingekuwa makala yake basi angeiuza hakuna mtu anayekubali hasara hata siku moja ndio maana tunasema amedit tu hii story ipo mitandaoni kitambo sana

Ili kujua kama ana haki au hana, soma sheria ya hakimiliki Tanzania ya mwaka 1999 (Copyright and Neighboring Rights Act No. 7 of 1999)-tembelea website ya COSOTA(cosota-tz.org).

By the way, ina maana kama una kitu lakini hujauza au huuzi basi kinakuwa si chako tena? Nikipaki gari katika eneo la kuegesha magari, ni halali liibiwe? Likiibiwa nisilalamike kwasababu tu nilipaki sehemu?
 
alichofanya huyu jamaa ni kuedit kwa kongeza fleva ila siyo muandaji wa story bali amekocopy na kuweka nakshi nakshi
Hivi nyie mbona hamjamuelewa mleta story au ni wivu unawasumbua wa kushindwa kuandaa mtiririko mzuri kama alivyofanya? uzuri kaweka hadi vyanzo vya mkusanyo wa utafiti wake nashangaa mnatoa povu la nn.
 
Ili kujua kama ana haki au hana, soma sheria ya hakimiliki Tanzania ya mwaka 1999 (Copyright and Neighboring Rights Act No. 7 of 1999)-tembelea website ya COSOTA(cosota-tz.org).

By the way, ina maana kama una kitu lakini hujauza au huuzi basi kinakuwa si chako tena? Nikipaki gari katika eneo la kuegesha magari, ni halali liibiwe? Likiibiwa nisilalamike kwasababu tu nilipaki sehemu?
ni uzembe wa mtu mwenyewe sasa wenzie wanauza nakala hadi laki 8 halafu anakuja kulalama hapa utafikiri hajasoma shule,muulize muda alioutumia kuandika halafu wenzie wanachuka wanaenda kupiga mkwanja
 
Hivi nyie mbona hamjamuelewa mleta story au ni wivu unawasumbua wa kushindwa kuandaa mtiririko mzuri kama alivyofanya? uzuri kaweka hadi vyanzo vya mkusanyo wa utafiti wake nashangaa mnatoa povu la nn.
hata mie haujanielewa nasema hivi alijitolea bure asilalamike siku nyingine asiwe mzembe kuwanufaisha watu
 
Watu wengine wanapost vituko humu eti wamekopi makala yake hii kitu mbona ni ya siku nyingi sana
Hata habari ya Mkwawa alivyokamatwa na Wajerumani ni ya siku nyingi sana. Lak8nibleo nikifanya uchunguzibwangu na kuiandika kivyangu, gazeti likija ku copy neno kwa neno na kuchapisha bula idhini yangu nina haki ya kulishitaji na kupewa fidia.
 
Back
Top Bottom