Sehemu ya 27.
“Unatakiwa kuwa na nyumba yako, tena ambayo hakuna sehemu nyingine inapopatikana! Umenifanya nijione mwanaume mpya, ninaahidi kutokukuacha hata kama nitaona mwanamke mwingine,” alisema Gosling huku akimwangalia Catherine kwa macho yaliyoonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa akimpenda.
Ili kumuonyeshea alimaanisha, akamwachia kiasi cha dola elfu ishirini ambazo zilikuwa ni zaidi ya milioni arobaini na kuchukua business card, akampa kwa ajili ya mawasiliano na kuondoka.
Alipofika ndani, akaenda kulala huku kichwa chake kikimfikiria Catherine tu. Siku hiyo msichana huyo alibadilisha maisha yake kiasi cha kumuona Maggie aliyekuwa pembeni kama gogo fulani alilopelekewa kuwa nalo.
Alichanganyikiwa na Catherine, alimwahidi kumpa gari, kumjengea nyumba lakini hayo yote yalionekana si kitu kwa kile alichofanyiwa usiku huo.
Mule chumbani alipokuwa Catherine, hakuamini kama alipewa kiasi kikubwa ambacho hakufikiria hata siku moja kama angeweza kupewa.
Alimshukuru Mungu, alikumbuka aliahidiwa gari, akaingia Google na kuanza kuyaangalia magari hayo, hakuamini alichokiona, yalikuwa ni magari ya thamani ambayo ilikuwa ni zaidi ya dola laki tano au milioni moja ambazo zilikuwa ni zaidi ya bilioni moja.
“Mungu wangu! Huyu mwanaume ni tajiri ama?” alijiuliza.
Hapohapo akaichukua ile business card, akaliangalia jina lile na kuliandika katika tovuti ya Google, kilichokuja ndicho kilichomshtua zaidi, hakuamini macho yake baada ya kugundua kuwa Gosling alikuwa miongoni mwa mabilionea wakubwa duniani.
Akajuta, aliona kile alichomfanyia mwanaume yule hakikustahili, kwa pesa alizokuwanazo ilikuwa ni lazima kumfanyia zaidi ya vile alivyomfanyia.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa wawili hao kuonana. Hawakuishia kufanya siku hiyo, kila siku usiku walikuwa wakikutana chumbani na kufanya mapenzi kama kawaida yao.
Japokuwa walitakiwa kurudi Serengeti hotelini lakini kwa Gosling ilikuwa vigumu kukubali kwani aliona kama angekwenda huko Catherine angeibiwa na mwanaume mwingine.
Walipanga kukaa Tanzania kwa wiki moja lakini kwa kuwa Catherine alikuwa mtamu, wakakaa mwezi mzima ndipo wakarudi nchini Marekani.