Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,869
- Thread starter
- #21
Sehemu ya 19
Maggie aliishi kwa hofu tele, kila siku kichwa chake kiliendelea kumfikiria Andrea na kuamini kuna siku mwanaume huyo angekuja kumuharibia na hivyo kukosa mabilioni aliyokuwa akiyafikiria.
Moyo wake uliwaza kabisa kummaliza, hakutaka kuona akiishia kupata aibu na wakati alikuwa na uwezo mkubwa wa kubadilisha mambo, yaani kama yalikuwa hivi, sasa aliyapeleka na kuwa vile.
Siku ziliendelea kukatika, akili yake ilifikiria zaidi harusi ambayo aliambiwa angefunga na Gosling, alimuonyesha mapenzi ya dhati huku kila siku akimwambia katika maisha yake hakukuwa na mwanaume aliyekuwa na nguvu moyoni kama alivyokuwa yeye.
Hilo likamfanya Gosling kumwamini kwani kile alichokizungumza ndicho alichokuwa akifanyiwa na msichana huyo aliyejua kupenda, msichana ambaye aliweza kuubadilisha moyo wake na kuingia kwenye mapenzi mazito na wakati hakuwa akitamani hata siku moja.
“Yaani harusi ambayo tutafunga, nitataka ibaki vichwani mwa watu, yaani izungumziwe kila kona,” alisema Gosling huku akimwangalia Maggie.
“Kweli?”
“Niamini!”
Hilo ndilo alilolifikiria Gosling, alikuwa kijana mdogo ambaye alipambana sana mpaka kupata utajiri mkubwa, aliamini ili kumuonyeshea mwanamke unampenda sana ilikuwa ni lazima kumfanyia mambo makubwa ambayo yangekaa kichwani mwake maisha yake yote.
Baada ya kukaa wiki kadhaa akamwambia mchumba wake huyo achague sehemu ambayo angependa sana waende kutembea, iwe kwenye mbuga ya wanyama au sehemu yoyote ambayo angependa waende pamoja.
Msichana huyo hakuwa na pupa ya kuchagua, alihitaji muda na hivyo kuchukua simu yake na kuanza kuangalia mbuga za wanyama.
Macho yake yakatua katika mbuga kubwa ya wanyama ya Serengeti na Ngorongoro ambazo zilimfanya kusisimka na kumwambia Gosling alihitaji kwenda huko kwani moyo wake ungejisikia furaha kama angekwenda kuwaona wanyama.
“Hakuna tatizo,” alisema Gosling.
Alichojali ni kumuona Maggie akiwa na furaha tu, akajipanga na kuwaambia walinzi wake walitakiwa kujiandaa na safari ya kuelekea nchini Tanzania kutalii hivyo walitakiwa kufuatilia vibali vyote vya safari.