Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,870
- Thread starter
- #101
Sehemu ya 33
Leo, mwanaume yuleyule aliyemsababishia matatizo alimwambia ni lazima atoe siri. Ndani ya gari alihuzunika sana na kitu kimoja kilichokuja kichwani mwake ilikuwa ni lazima amuue, hata kama angetumia kiasi kikubwa, ilikuwa ni lazima amnyamazishe milele.
“Kama nikimlipa dola milioni hamsini, inamaana siku nyingine akihitaji pesa atakuja kwa gia hiihii, kuyaepuka yote ni lazima nimuue,” alisema Maggie huku akiendesha gari lake.
Hakutaka kurudi nyumbani, alichohitaji ni kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mwanaume huyo anauawa haraka sana. Akaingia Google na kuanza kutafuta makundi ya watekaji yaliyokuwa yakipatikana katika Jiji la Washington DC.
Akafanikiwa kuona makundi mengi lakini kundi pekee lililokuwa hatari lilikuwa Brothers ambalo liliundwa na wanaume wengi weusi.
Hilo ndilo alilotaka kuonana nalo. Hakujua lilipokuwa likipatikana lakini kwa kupitia mwandishi wa habari wa Gazeti la Talk, akafanikiwa kupewa maelekezo mahali ambapo kundi hilo lilipokuwa.
Mwandishi huyo hakujua kilichotakiwa kufanyika, alichukulia poa na kutoa maelekezo ya kina. Maggie akaelekea katika mtaa alipoelekezwa ambapo kundi hilo lilipopatikana.
Baada ya dakika kadhaa akasimama mbele ya ghorofa kubwa, lilionekana kama limetelekezwa, ndani yake kulikuwa na vijana waliyojitolea kuishi maisha ya ajabu, kuvuta bangi, madawa ya kulevya na wasichana waliokuwa wakijiuza kwa kiasi kidogo cha pesa.
Hakutaka kuteremka, kwa jinsi mahali pale kulipoonekana, ilikuwa ni lazima kufuatwa kwa kuhisiwa alikuwa mtu mbaya. Kile alichokifikiria ndicho kilichotokea, mwanaume mmoja aliyekuwa na bunduki akaanza kumsogelea, aliliona gari hilo likiwa limesimama kwa dakika mbili, halikuwa limeondolewa mahali hapo hali iliyomfanya kuhisi inawezekana alikuwa polisi au adui aliyekuja kushambulia.
“Hey bitch! What the *** are you doing here?” (Hey wewe malaya! Unafanya nini hapa?) aliuliza mwanaume huyo huku akimwangalia Maggie ambaye aliteremsha kioo na kumwangalia mwanaume huyo.
“I want to see Joker,” (Ninataka kumuona Joker)
“Who the *** is he?” (Ndiye nani?) aliuliza mwanaume huyo huku akimwangalia Maggie.