Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,870
- Thread starter
- #121
SEHEMU YA 40
Alipofika, alifurahi kuwaona, walifanana naye kupita kawaida, moyo wake ukawa na furaha mno, kila alipokuwa na Catherine moyo wake uliridhika, alijiona kupata kila kitu tofauti na kuwa na Maggie ambaye hakuwa na mapenzi makubwa kama aliyokuwanayo kwa Catherine.
Alikaa huko na kupanga mambo mengi, aliendelea kumpa pesa za kufungulia biashara kubwa, alimfanya kuwa mtu mwenye thamani ambaye hakutakiwa kuhofia kuhusu maisha yake hata kidogo kwa kuwa pembeni alikuwepo yeye.
Hakutaka kumficha Catherine juu ya kile kilichotokea nchini Marekani, alimwambia hakuwa na uwezo wa kuzalisha tena kwa kuwa mbegu zake hazikuwa na nguvu hata kidogo.
“Kwa hiyo?” aliuliza Catherine.
“Sitokuwa na mtoto mwingine zaidi ya hawa hapa,” alisema Gosling.
“Pole sana mpenzi!”
“Nashukuru! Ila ninafikiria jambo moja,” alisema.
“Lipi hilo?”
“Kuwagawia watoto wangu utajiri wangu wote. Yule Maggie ninaishi naye ilimradi tu, ni mke wangu lakini hakuna anachonipa katika maisha yangu, ni kama rafiki yangu, hizi mali zote ni lazima niwape watoto wangu,” alisema Gosling.
Alikaa na mpenzi wake huyo, japokuwa alizaa lakini Catherine hakuchoka, kila siku alionekana kama mwanamke mpya kabisa. Ujuzi wake kitandani ulikuwa ni zaidi ya ule aliokuwanao kipindi cha nyuma.
Walifanya sana mapenzi na baada ya wiki moja akarudi nchini Marekani. Maisha yaliendelea, biashara alizokuwanazo ziliendelea kuingiza pesa nyingi, alikuwa bilionea ambaye kila siku alikuwa akiongeza kiasi kikubwa cha pesa kiasi kwamba alionekana kuwa bilionea mkubwa sana hapo baadaye.
Baada ya wiki mbili, Catherine akawasiliana na Gosling na kumpa habari zilizomshtua mno, habari ambayo ilimfanya kuhisi kama kulikuwa na kitu kilichotokea nyuma ya pazia.
“Ulisema huna uwezo wa kumpa mimba mwanamke?” aliuliza Catherine kwenye simu.
“Ndiyo!”
“Hapana! Si kweli!”
“Kwa nini?”
“Nina mimba yako! Umenipa mimba, katika kipindi ulichokuja nilikuwa kwenye siku zangu za hatari Gosling, tumefanya mapenzi na umenipa mimba,” alisema Catherine kwenye simu huku akionekana kuwa na furaha tele.