Simulizi: Tugawane Maumivu

Simulizi: Tugawane Maumivu

Sehemu ya 39.

"Mdogo wangu kukaguliwa ndiyo sitaki, lakini kweli nilikuwa na jamaa fulani sehemu," Eliza alininong'oneza sikioni.
"Wapi?"
"Mabibo."
"Jamaa mwenyewe siyo shemeji?"
Nilimuona Eliza akijiumauma huku akishindwa kuniangalia.

"Enhe vipi?" shemeji alitokea.
Eliza na shemeji walipoangaliana macho, kila mmoja alionesha tabasamu laini. Kama dada Light angekuwepo naamini pale pale angeisoma hali fulani na pale pale ndio ingekuwa mwanzo wa uchunguzi wake.

Itaendelea.....
.
 
Sehemu ya 59.

"Lakini ni baada na yeye kuanza kutembea na mke wangu, Eliza," alisema mume wa Eliza na kumtazama mkewe ambaye bado alikuwa ameinamia chini...akaendelea.
"Na nina imani mpaka leo wanaendea."
Mimi nilimkazia macho Eliza kisha nikamkazia macho shemeji. Walijua kwanini nilifanya vile.

Mume wa Eliza akaendelea.
"Tena nina apa kwa jina la Mungu kwamba nina kila ushahidi ila sitaki tu kuutoa, kama mtataka leo nitautoa."

Nilimuona shemeji kama amelowa vile, alihema kwa nguvu kisha akashusha pumzi. Alimwangalia mkewe kisha akamuangalia Eliza.

"Kwa hiyo shemeji ulipogundua mwenzio anatembea na mkeo kwanini usiwashike ukatoa talaka au ukawaita wazee wakawaweka chini?" nilimuuliza mume wa Eliza.

"Aa niliona kote huko ni kujisumbua, maisha yasingekuwa mazuri katu. Ili kuyafanya maisha kuwa mazuri ni bora mara mia na mimi nitembee na mkewe," alisema mume wa Eliza.

"Kwa hiyo kwa kutembea na dada 'angu umeyafanya maisha kuwa mazuri?"
"Sana tu."
"Mmegawana maumivu," nilisema.

Kwa maana hiyo mume wa Eliza alipogundua kwamba shemeji yangu anatembea na mkewe Eliza na yeye aliona ili wagawane maumivu ni kutembea na mke wa mwizi wake huyo ambaye ni dada Light. Yaani wana hatari hawa.

Lakini namshukuru Mungu, kwani baada ya majadiliano marefu kila mmoja alibaini kosa lake ingawa wa kwanza kutenda ndiye alikuwa na kosa kubwa zaidi, wote walishikana mikono wakaombana samahani huku kila mmoja akiahidi kutorudia tena.

Hata hivyo, pale pale shemeji alisema kwamba, amepata nyumba nyingine, Changanyikeni na tungehamia huko siku si nyingi mbele.

"Sawa bwana mzee, sisi tupo, japokuwa tutawamiss sana," alisema mume wa Eliza.

Mimi niliwaasa kwamba, licha ya shemeji kuhama, lakini watakuwa wametenda jambo la busara sana kama wote, kwa ratiba zao watakwenda kupima afya zao ili kufanya maisha yao kuwa bora na salama. Wakakubali.

MWISHO.

Ahsante kwa story cheupe dawa Shunie

Chapter closed...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom