Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,974
- Thread starter
- #21
Sehemu ya 20.
Nikiwa najizoa zoa kwenda kumsalimia, akili ilikuwa ikiuliza maswali mengi sana.
"Je, ndiye aliyeniita?"
"Kama ni yeye anataka kuniambia nini?"
"Mh! Eliza akijua nilikuwa na mumewe hotelini si patachimbika?"
"Za leo shemeji?" nilimsalimia huku nikikaa kwenye kiti. Alikuwa amekaa peke yake kiasi kwamba nilishangaa kwanini sikumuona nilipoingia.
"Salama tu, karibu sana," aliniambia huku akinisaidia kwa mkono wake mmoja kukiweka kiti vizuri.
"Asante," nilimjibu huku nikimkazia macho ya kumsoma usoni kama ni yeye kweli aliyeniita.
"Vipi kumbe unafikaga mpaka huku?" aliniuliza.
Hata kama ni wewe ungejua si yeye aliyeniita.
"Aah kuna mtu amenipigia simu ameniambia yuko hapa. Sasa nimekuja nashangaa simuoni," nilimjibu.
"Aisee au kaenda chooni, ungemsubiri au umpigie simu umwambie kwamba umeshafika," aliniambia. Kauli yake hiyo ilizidi kunijulisha kuwa si yeye aliyeniita.
Nilichukua simu bila kumwambia kama nimejaribu lakini hapatikani.
"Kha! Mbona sasa hapatikani?" nilisema nikijifanya ndiyo nagundua muda ule.
"Hapatikani sasa itakuwaje? Msubiri lakini. Au akikukuta umekaa na sisi ni soo?" aliuliza.
"Hapana, hakuna tatizo."
"Ni mwanaume au mwanamke?"
"Ni mwanaume," nilimjibu nikiendelea kushikashika simu yangu.
Mara kidogo alikuja mtu mwingine na kukaa kwenye meza aliyokaa mume wa Eliza. Hata mimi nilipofika pale niliona kama kulikuwa na mtu kwani kulikuwa na glasi yenye bia na chupa yenye bia nusu.
Huyo mtu alinisalimia kisha akaendelea kunywa. Mume wa Eliza alinitambulisha kuwa yule mtu ni rafiki yake kipenzi, wamekutana pale kunywa na kwenda kulala.
"Nashukuru kumfahamu," nilisema.
Mhudumu alikuja kunisikiliza, niliagiza bia na kuanza kunywa sambamba na wenyeji wangu.
Kuna wakati nilimuona mume wa Eliza akitoa simu yake mfukoni, nikamuuliza namba yake nikidhani huenda ni yeye aliniita akaizima sasa anaiwasha. Aliponitajia namba zake zilikuwa ni tofauti na zile za aliyeniita, hata mitandao ni tofauti.
Niliisevu namba yake kisha nikai-beep. Ikaita.
"Hiyo yangu," nilimwambia nikiwa nimehakikisha siye mwenyewe.
*
*
Je, nini kitaendelea?