SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA SABA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA : wakina Higgno wakaendelea kumtazamia Hilda, hata giza lilipoingia na kwenda kulala bila kumuona mschana huyu, mpaka siku ya nne mida ya saa tano za usiku, wasi wasi ukiwa umetanda moyoni kwa Higgno na wazazi wake, wakihofia kupata kesi endapo kuna jambo baya lita kuwa lime mpata Hilda, Higgno akiwa chumbani kwake na mtoto wa hilda, kwenye mabanda ya uwani, na wazazi wake wakiwa chumbani kwao ndani ya nyumba kubwa, mara wakasikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yao, hapo hofu zika zidi kuwa shika, wakidhania kuwa ni gari la polisi limekuja kuleta taarifa ya Hilda, kama sio kuwasomba, wakiwa wanaendelea kujiuliza ndipo wakaanza kusikia milio mikali mfululizo ya honi za gari ikilindima nje ya nyumba yao ………. ENDELEA NAYO

Nakufanya kuwa kero kwa kina Higgno ambao walishindwa kutoka kwa hofu, mara zile honi zika gota, “hebu nikawagongee, watakuwa wanashangaa tu! maana halijawahi kuja gari hapa nyumbani kwao” ilikuwa ni sauti ya kike iliyojaa ulevi wa kupindukia, “Hilda” jina hilo lilitajwa karibia na wote walioisikia, kuanzia baba na mama walioko nyumba kubwa, mpaka Higgno aliekuwepo kwenye chumba chake, sio yeye peke yake tu ambae aliinuka kitandani na kujiandaa kufungua mlango, hata wazazi wake pia, waliinuka kitandani na kuanza kujiandaa, kutoka nje wakashuhudie kinachoendelea huko nje.
Lakini kabla Higgno hajaufikia mlango akasikia mlango ukigongwa kwa fujo, tena ilionyesha kuwa mgongaji alitumia jiwe kugongea mlango, “fungua bwana usijifanye umelala, unawezaje kupata usingizi kwenye kibanda kama hiki?” ilikuwa ni sauti ya kilevi ya Hilda iliyojaa dharau na kebehi, maneno ambayo hata mzee Frank na mke wake waliyasikia, nao wakafungua mlango na kutoka nje, ambako waliweza kumuona Hilda akiwa amesimama Mbele ya mlango wa chumba cha Higgno, ameshika jiwe mkononi, lakini hakuwa peke yake alikuwa wanaume watatu nyuma yake, huku wote pamoja na Hilda mwenyewe wakipepesuka kwa ulevi.
Baba na mama Higno wakamuona Hilda akiugonga tena mlango wa chumba cha Higno, “fungua bwana wenzako tuna chelewa” alisema tena Hilda akiwa ana ugonga lango ule kwa fujo, “hivi huyu binti mbona amekuwa shetani hivi jamani” aliuliza mama Higgno kwa sauti ya chini, huku wakiendelea kuwatazama wakina Hilda pale mlangoni kwa Higgno, na wakaona mlango unafunguliwa, na kabla aHiggno haja toka nje, wakamuona Hilda ana ingia ndani kwa kumsukuma Higgno pale mlangoni, akifuatiwa na wale vijana watatu, “njoo baby umuone mwanao” alisikika Hilda, na hapo wakamuona Higgno anatoka nje ya chumba kile na kusimama mita kadhaa pembeni ya nyumba ile ndogo.
Naam sauti za vicheko na furaha vilivyo ambatana na sifa na hongera vilisikika toka kwenye ile nyumba ya Higno, “mwanangu hii ni chata yako kabisa” alisikika mmoja kati ya wale wanaume kwa sauti ya kilevi pia, ambae Higgno alimtambua kama Vitus, “nimemtolea kitu” alisikika Hilda, “siku moja inabidi nikamuonyeshe shangazi” alisema mmoja wao, ambae mimi na wewe msomaji tuna mfahamu kuwa ni Talib, “yaani mwanangu hili ni bonge la chata” alisifia tena mwingine, ambae japo alikuwa ndani lakini Higgno aliposikia alijua kuwa alikuwa ni yule mwingine ambae alimkumbuka kuwa ni yule aliemuona na Vitus siku ile wakiwa ndani ya gari wanawasubiri wale vijana wawili waliomvamia mzee Mahamud, “poa wana, tumwache dogo alale, twenzetu tukale bata” alisema Talib, na hapo wakatoka zao na kuelekea kwenye gari, “kesho inabidi nimpige shoping ya nguvu sana” alisikika Talib akiongea kwa kujigamba akiwa anaingia ndani ya gari, wote wakionyesha kuwa wamelewa sana na wenye furaha tele.
Higgno na wazazi wake waliwatazama wakina Hilda mpaka walipotoweka na gari lao, ndipo mama Higgno, alipomgeukia mume wake, “baba Higgno, haya mambo mwisho wake lini?” aliuliza mama Higgno kwa sauti iliyojawa na machungu yaliyotokana na dharau ya hilda ambayo sio kwamba ilifika kwa Higgno peke yake ila kwa familia nzima, “mpaka lini wakati leo ndiyo mwisho” alisema baba Higgno kwasauti iliyojaa hasira kali.
Usiku ule wakina Hilda hawakuishia kwa akina Higgno peke yake, ila walipotoka kwa Higno wakaenda nyumbani kwa kina Hilda, ysani kwa mzee Komba, ambako pia waliwakuta wamesha lala, nako wakapiga honi za fujo mpaka mzee Komba na mke wake ambao ni siku ya tatu sasa hawakuwa wameonja ulanzi, kutokana na kutoweka kwa binti yao Hilda ambae ndie mfadhiri wao wa ulanzi.
Huwezi amini japo walikuwa wamesha lala fofo, lakini ile kusikia honi za gari walikurupuka mara moja na kutoka nje, mzee Komba akiwa amejifunga shuka na mke wake akiwa amejifunga kitenge chakavu, hakika walistaajabika mara baada ya kuliona gari dogo likiwa lime simama mbele ya nyumba yao likiwamulika kwa mwanga mkali wa taa, ambapo kwa heshima ya kawaida, ni kwamba dereva anapofika sehemu kama hii hupunguza mwanga wa taa za gari au kuzima kabisa, maana haikuwa heshima kuwamulika wenyeji tena ukizingatia ni wazazi wa rafiki yao, kwao haikuwa kitu, walizidi kulishangaa lile gari maana haikuwahi kutokea gari kusimama nyumbani pao, toka nyumba ile imejengwa, zaidi ya kuyaona yakipita na njia, “nani hawa au wanaleta taarifa mbaya ya Hilda?” aliuliza mama Hilda huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio, “mh! ndio usiku huu, si wangesubiri asubuhi” alisema mzee Komba, huku wakilikodolea macho gari lile, ambalo licha ya kuwa na muungurumo mbaya kutokana na kukosa huduma muhimu, kama kubarishwa oli za engine na gear box, lakini sauti kubwa ya music ilisikika kwafujo, mioyo yao iliongeza kasi ya kudunda mara walipo uona mlango wa mbele wa gari upande wa kushoto ukifunguliwa, “hoooo! kumbe ni Hilda mwanangu” alipiga kelele mama Hilda, huku akimkimbilia Hilda aliekuwa anashuka toka kwenye gari, mkononi ameshka chupa mbili kubwa za pombe kari, ile ambayo ina picha ya mtunisha misuri, huku Hilda mwenyewe anayumba yumba kama nyasi ndefu wakati wa upepo mkali wa masika, “ni mimi mwanao mama, nimeona nikuletee na wewe ujichane” alisema Hilda kwa sauti ya kilevi kweli kweli, hapo mzee Komba akatoka mbio akishikilia shuka lililotaka kumvuka na kuzidaka zile chupa za pombe, “hapo umefanya jambo la mbolea” alisema mzee Komba huku anavuja mate kama mama mjamzito alieona chachandu ya limao au embe bichi, maana kiukweli pombe hizi za kizungu aliwahi kunywa mara nne, mara ya kwanza kwenye harusi ya bwana Frank na mke wake mama Higgno, miaka zaid ya ishirini iliyo
pita, na mara moja ni miaka minne iliyopita yaani mwaka 2000, kipindi cha uchaguzi wakati wa kikao na mbunge wa kipindi hicho ambae kwa sasa ni marehemu, “baba we jiandae kufaidi, mkweo amesema atahakikisha kila siku unapata mizinga miwili” alisema Hilda kwa sauti ile ile ya kilevi, “yupo wapi huyo mkwe mbona ashuki kwenye gari?” aliuliza mama Hilda huku akisogea kwenye gari, “hooo! kumbe wewe baba, umemkumbuka mwenzio” alipaza sauti mama Hilda mara baada ya kumuona Talib, akiwa ametulia kwenye kiti cha dereva,
Kwa akili ya kawaida ungesema mara baaada ya mama huyu kumuona Talib pengine angemtimua na kumrudishia zile chupa za pombe, “ndio mama, mpotevu amerudi nyumbani” alisema Talib huku akicheka cheka kilevi, huwezi amini ndio kwanza mama huyu alipiga magoti na kusema, “asante baba yangu karibu sana, hapa ni kwako, karibu sana” alisema mama Hilda huku akiwa bado amepiga magoti, na wakati huo mzee Komba nae akasogea kumuona mkwe wake, nae kama mke wake, japo hakupiga magoti lakini alipomuona mkwewe na kumkumbuka, akamsalimia kwa furaha zote, “karibu sana baba, maana walikuwa wanatusema vibaya, eti umemkataa mwenzio na kwamba umetelekeza na mtoto” alisemelea mzee Komba, “mzee utawaziba mdomo, maana tarajia mambo makubwa zaidi” alisema Talib, kwa sauti ile ile ya kilevi.
Naam baada ya maongezi na ahadi nyingi, Hilda akaingia kwenye gari kisha wakaondoka zao, kwa ahadi ya kwamba kesho Hilda angekuja kuwaletea fedha na pombe, huku nyuma mzee Komba na mke wake, wakaanza kunywa konyagi zao, wakianza na chupa ya kwanza ambayo mpaka wanaimaliza ilishatimia saa tisa za usiku, wakashauriana ya kwamba ile iliyobakia wainywe kesho.*******
Naam Kitu ambacho ambacho Talib hakuwa amekijua usiku ule ni kwamba wakati yeye anaendelea kutumia fedha zake zinazotokana na biashara ya samaki na dagaa wa ziwa Nyasa, huku kiasi kikubwa cha fedha hizo zikiwa ni mtaji, na sio faida kama wengine wanavyo fanya, Huku mzee Mahamud alikuwa anaingia na msafara wa mabasi mapya kabisa, ambayo alihitaji kuyapangia safari za mikoani, ikiwa na kuajiri wafanya kazi wapya, ambao watachanganyika na wale wa zamani ili kuyatumia magari hayo, ndio alikuwa anaingia mkoani Ruvuma, na sasa ni mjini songea na kwenda kuyaegensha kwenye gereji yake kubwa iliyopo pembezoni mwa ghara kuu la mkoa wa Ruvuma, ambako alipokelewa na mke wake na bint binti yake Soraya, “mwanangu nimekukosa siku tano tu, nakuona umezidi kuwa mkubwa na mng’aavu, bila shaka kuna ujumbe mzito nitaukuta kwa mama yako” alitania mzee Mahamud, wakiwa njiani wanaelekea nyumbani, ambae kiukweli hilo ndilo lilikuwa tarajio lake kwa umri wa Soraya, mschana ambae hajawahi kumletea aibu, Soraya aliekuwa anaendesha gari alicheka kidogo, “mh! ujumbe gani, unadhani soraya anapango wa kuolewa, angekuwa mkristu tungesema anataka kuwa sister, sijui sasa anataka kuwa nani?” alisema mama Soraya, aliekuwa amekaa seat ya nyuma pembeni ya Soraya aliekuwa dereva, “lakini mama si nimesha kuambia kuwa nikimuona mwanaume mwenye sifa nzuri nitakuambia?” alisema Soraya kwa sauti ya kulalamika, kwamba mama yake anashindwa kumuelewa, ni kama jibu la soraya lilimuingia mzee Mahamud, japo alikaa kimya mpaka walipofika nyumbani na kuingia chumbani kwao, “lakini ni kweli mama Soraya, unajua vijana wengi watakuwa wanahitaji kuwa na Soraya kutokana na sababu nyingine na sio upendo wa kweli, wengi watakuwa na tamaa ya kuwa ni mtoto wa tajiri” alisema mzee Mahamud kwa sauti ya upole, wakati akipembua nguo zake tayari kuingia bafuni, “lakini kumbuka kuwa Soraya pia ni mzuri na mrembo, hivyo sio ajabu kupendwa na mvulana yoyote” alisema mama Soraya, aliekuwa anaweka vizuri begi alilokuja nalo mume wake, “umeongea vyema mke wangu, hapo unaweza kuona ugumu alionao Soraya katika kujua yupi anampenda kweli na yupi anamtamani yeye au utajiri wake” alisema mzee Mahmudu kabla hajaonekana kukumbuka jambo, “hivi sijamuona Talib akija kunipokea, au amkumjulisha kama narudi” aliuliza mzee Mahamud ambae kiukweli alitokea kumuamini, sana Talib kuwa amebadilika kwa tabia, “mh! ukweli ni siku ya nne hatuja muona Talib, pengine amesafiri kwenda Nyasa” alisema mama Soraya.********
Ilikuwa hivi usiku ule ule, mara baada ya bwana Mahamud kupita kwenye lango la jumba lake, mlinzi akarudishia gate na kumpigia Talib, ambae hakupokea simu, akaamua kutuma ujumbe ili muda wowote akishika simu yake auone, “Boss amesharudi” hayo ndio yalikuwa makubaliano ya Talib na mlinzi huyo, ambae ndie alikuwa mshirika wake kwa hapa nyumbani, maana hata anapotoka au kurudi usiku sana, akiwa peke yake au na mwanamke yeyote, yeye ndie anae mfungulia lango, na pengine kumsaidia kuwatoa asubuhi sana wakati wa swala ya Alfajiri.
Ujumbe ule ulimfikia Talib saa moja za asubuhi, akiwa ndani ya chumba cha guest moja bubu ya uswahilini kweli kweli, ni mara baada kukurupuka toka kitandani akiwa amesha jikojolea, ni baada ya kushindwa kuamka akipitiwa na usingizi mzito, kutokana na pombe alizo kunywa jana usiku, na alipousoma ule ujumbe toka kwa mlinzi akainuka haraka na kuokota nguo zake zilizokuwa chini sakafuni, akaziokota na kuzipachika mwilini mwake na kujikagua mfukoni kwa kile alichobakia nacho, alikuwa na shilingi elfu tano tu! akairudisha mfukoni akachukuwa simu yake na funguo za gari akatoka mbio mbio kuelekea nje akimuacha Hilda bado amelala anakoroma kwa usingizi wa pombe, Talib alipitia sokoni akanunua dagaa nyasa wa elfu mbili na samaki wa elfu tatu, kisha akaelekea nyumbani, ambako aliwakuta wanafamilia wakiwa wameshaenda kwenye mihangaiko yao, akakabidhi wale dagaa na samaki, ikiwa ni alama ya kuwa ametokea Nyasa, kisha akamueleza mlinzi kuwa akija mwanamke yeyote kumuulizia amwambie kuwa hayupo, kisha kusema hivyo, Talib akaingia ndani kwake na kwenda kujilaza kwa lengo la kufidia usingizi wa siku nne akiwa na Hilda.
lakini ukweli ni kwamba Talib hakupata hata tone moja la usingizi, sio kwamba aliwaza kuhusu Hilda aliemuacha guest bubu, hakuwaza kuhusu mwanae na ahadi aliyoitoa ya kumfanyia shoping leo hii, hakuwaza kuhusu wakwe zake ambao jana usiku walipiga magoti mbele yake na alijua fika kuwa, mpaka sasa watakuwa wanasubiri chupa za pombe ili waendelee kulewa, ukweli Talib aliwaza juu ya kupata fedha ambayo itarudisha mtaji wa biashara yake, ambayo leo asubuhi ndiyo amemalizia elfu tano ya mwisho kwa kununua dagaa na samaki za kuwadanganyia mjomba na shangazi yake, “lazima mpango wangu ufanikiwe, siwezi kuishi kindezi, mjomba mwenyewe haeleweki, yeye anampa ulaji Soraya wakati mimi kidume nipo” aliwaza Talib, akisahau kuwa Soraya ndie mwenye haki zote za kuwa katika nafasi aliyopo, kwasababu ni mtoto wa Mahamud.******
Huku Luhuila seko nako, asubuhi hii tayari taarifa za Hilda kurudiana na Talib zilisha anza kuzagaa, huku bwana Komba ambae ni kama aliamka na pombe kichwani akitambaza taarifa hizo, ambazo baadhi ya watu walishindwa kuzielewa, maana walichojua wao ni kwamba, Hilda anaishi na Higgno kijana wa mzee Frank.
Mzee Komba alienda kwa mzee Nganyanyuka na kukopa lita ishirini za ulanzi kwa ahadi ya kulipa jioni akiamini kuwa mwanae Hilda atamletea shilingi elfu tatu ya kulipia pombe hiyo, ambayo aliipeleka pale kwake na kuwaita rafiki zake wakina Nyoni, Njogopa, Ngonyani, na wengine kibao, hasa wale waliokuwepo siku ile ya ndoa ya mkeka kwa mzee Frank, na kuanza kunywa pombe hiyo wakishushia supu ya mboga za majani ya maboga, wenyewe wanaita pitiku, na kuendelea kunywa ulanzi wakichangia konyagi, huku wakiamini kuwa kuna nyingine zinakuja baadae.*****
Mida hii mschana mrembo Soraya, alikuwa njiani na dereva wake wanatoka SeedFarm ya Lumecha, kilomita kama ishirini toka songea mjini, ambako alienda kuweka oda ya mbegu za miti ya matunda kwaajili ya kupanda shambani kwake sehemu ambayo alikuwa na malengo nayo makubwa sana, sio shamba pekee ila alikuwa na mpango wa kutengeneza hotel kubwa sana sehemu hiyo na kuanza kutangaza utalii wa kusini mwa tanzania hasa upande wa nyuma ya mji wa songea, ambako kulikuwa na vivutio vingi vya utalii, “da Laylah, unamkumbuka yule kijana alienisaidiaga siku ile nilivyo kamatwa na wanafunzi wa songea boys?” aliuliza Soraya wakati safari inaendelea, “na mkumbuka sana da Soraya inaonyesha unampenda sana yule kaka, yani bado unamkumbuka mpaka leo?” aliuliza Laylah huku anacheka cheka, “mh! sijui kama nampenda, lakini…. lakini… nataka tu nimuone nimuabie asante, kwasababu bila yeye ningesha poteza uschana wangu kwa aibu kubwa sana, tena sio kwangu tu! hata kwa wazazi wangu” alisema Soraya huku safari inaendelea, “halafu kwanini hatukuwahi kurudi kule matogoro kumtafuta tena?” aliuliza Laylah, akionyesha kujishangaa, “kweli bwana, hivi kwanini hatukuwahi kumtafuta kwenye ile barabara, hata hivyo mbona tumepita sana ile barabara lakini hatuja muona, kila ijumaa tunaenda shambani na tunapita kule kule?” aliuliza Soraya, “usikute alikuwa ni mwanachuo na alitokea mkoa mwingine” alisema Laylah, “mh! kwa umri wake yule kama alikuwa anasoma basi ni form one au two” alijibu Soraya, “kama ni hivyo basi sasa hivi atakuwa na mke na watoto kabisa” alisema Laylah, na kauli hiyo ilionekana kummaliza nguvu Soraya, ambae hakujibu kitu zaidi ya kukaa kimya mpaka walipoingia mjini.*******
Wakati mzee Komba akiwa ana fanya yake, hakujuwa kuwa mwanae Hilda ndio kwanza alikuwa anagongewa mlango na muhudumu wa Guest bubu hii, ambayo haitambuliki na msajili wa nyumba za wageni na kushtuliwa toka usingizini, akatazama pembeni yake pale alipolala Talib jana usiku hakuona mtu, na alipo tazama vizuri hakuoan dalili ya uwepo wa mtu huyu, kwa maana ya kwamba hakukuwa na nguo wala viatu vya Talib, zaidi ya mkojo alioumwaga kitandani, “we dada si ufungue mlango lisaa limepita toka saa nne” ilisikika sauti ya mhudumu wa kike toka nje ya mlango, “nilikuwa navaa dada yangu” alisema Hilda huku anafungua mlango ambao haukuwa umefungwa na funguo zaidi ya kuegeshwa na kitasa(kubugazwa), “yaani mwenzio ameondoka mapema tu, wewe unalala mpaka saa tano, unadhani usafi nitafanya saangapi, halafu akikukuta boss si atasema nimechukua hela yako ya leo” alisema yule mhudumu huku anaingia mule chumbani na kuanza kupembua mashuka, “nisamehe dada yangu nilipitiwa na usingiz..” kabla hajamaliza kuongea akakatishwa na yule mhudumu, “usinitanie wewe dada ndio maana ulikuwa umejifungia humu chumbani, kumbe umemwaga mkojo” alisema yule mhudumu, huku ameshika yale mashuka………haya sasa mambo yanazidi kuwa pambe, baba Higgno kawaka kwa dharau walizofanyiwa na hilda, mzee komba ndio huyooo na marafiki zake wana matumain makuuuuubwa huku hilda kakimbiwa gesti na talibu, soraya nae anamtaka kijana mpole amshukuru kwa kumuokoa miaka mingi iliyopita nini kitaendeleaaaa.... Usikose sehemu inayofuata.

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA NANE
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA : “yaani mwenzio ameondoka mapema tu wewe una lala mpaka saa tano, unadhani usafi nitafanya saangapi, halafu akikukuta boss si atasema nimechukuwa hela yako ya leo” alisema yule mhudumu huku anaingia mule chumbani na kuanza kupembue mashuka, “nisamehe dada yangu, nilipitiwa na usingiz..” kabla hajamaliza kuongea akakatishwa na yule muhudumu, “usinitanie wewe dada ndio maana ulikuwa umejifungia humu chumbani, kumbe umemwaga mkojo” alisema yule muhudumu, huku ameshika yale mashuka……ENDELEA SASA

“mkojo?, labda Talib ndie alielala upande huo” alijitetea Hilda ambae mpaka hapo hakujuwa ni kwanini Talib aliondoka na kumuacha hapo guest, “usinitanie we dada nenda kafue uchafu sijui wa bwana wako, sasa unataka akufulie nani?” ndivyo ilivyo kuwa kwa Hilda, kabla hajaondoka hapo Guest alikabidhiwa mashuka na kuyafua kwanza, nae alifanya hivyo huku akiwaza kwanini Talib aliondoka kimya kimya, “labda alipigiwa simu anaitwa haraka, maana anaonyesha kuwa bado ananipenda, si unaona ameahidi kunipa hela za kumnunulia mtoto nguo, halafu aliwaambia wakina mama kuwa atawaletea pombe nyingine” alijipa moyo Hilda, ambae mwisho akapanga kuwa akimaliza kufua aende nyumbani kwa akina Talib akachukue fedha za matumizi kisha aende nyumbani, na kama Talib atapata nafasi atamfuata huko huko kwao.*****
Wakati huo pia mzee Frank, aliondoka nyumbani kwake yeye na mwanae Higgno na mke wake, wakiwa wame mbeba mtoto wa Hilda mpaka kwa mwenyekiti, ambae walimueleza kilichotokea jana usiku nyumbani kwao, nae mwenyekiti, akawaita wajumbe wawili wa nyumba kumi na kuelekea nyumbani kwa mzee Komba, ambako walifika pale saa tano za asubuhi na kukuta watu kibao wakiendelea na sherehe ya pombe, huku wakiongea na kucheka kwa furaha, wakionekana wameshaanza kulewa ulanzi, “hooo! mwenyekiti samahani bwana nilisahau kukualika” alisema mzee Komba huku anainuka na kuwasogelea wageni hawa, ambao hata alipowaona akushukuru kwa ujio wao, “usijali bwana Komba tume jialika wenyewe” alisema mwenyekiti, nao wakapewa viti, sehemu za kukalia ambazo zilikuwa ni matofari kutokana na uhaba wa viti, “hapana bwana Komba hatuwezi kunywa pombe mapema hii, labda tukueleze kilicho tuleta hapa kwako” alisema mwenyekiti baada ya kuona wana letewa vikombe vilivyo jazwa ulanzi, “lakini musituharibie sherehe yetu tafadhari” alisema mzee Njogopa kwa sauti ya kilevi, tena imekuwa vyema tume wakuta nyie ambao mulikuwepo usiku ule ambao tulimkuta Hilda kwa huyu kijana na kumkabidhi kuwa mke wake” alisema mwenye kiti akimuonyesha Higno, “mwenyekiti unazunguka sana, nenda kwenye point” alisisitiza Ngonyani.
Hapo mwenyekiti akaanza kueleza kilicho waleta pale nyumbani kwa mzee Komba, “bwana Komba nadhani unakumbuka siku ile ambayo tulimfumania binti yako nyumbani kwa bwana Frank, akiwa na huyu kijana wa bwana Frank yaani Higgno?” aliuliza mwenyekiti huku akimtazama mzee Komba, “hakuna asiekumbuka mwenyekiti hata sisi tulikuwepo, si ndio tukawapiga gundi kwa mkeka?” alisema Njogopa, kwa sauti ya kilevi, “haswaaaa, najua mulikuwepo, lakini itapendeza kama akijibu bwana Komba” alisema mwenyekiti kwa msisitizo, “ndio nakumbuka bwana mwenyekiti” alijibu mzee Komba yaani baba yake Hilda kwa sauti ya kilevi, “sawa sawa bwana Komba, sasa kuhusiana na hilo, kuna jambo limetokea jana usiku” alisema mwenyekiti, “nilijua tu, yaan tayari imesha kuwa nongwa” alisema mama Hilda kwa sauti ya chini chini, huku anatazama pembeni na kubetua midomo ya kubeza.
Mwenyekiti akamtaka mzee Frank, aeleze kilicho tokea mwanzo mpaka mwisho, na nia ya kuja pale kwa mzee Komba.*******
Naam baada ya kumaliza kufua mashuka ya mikojo, akaruhusiwa kutoka, nae akatoka zake akiwa amevalia nguo zile zile alizotoka nazo nyumbani kwa Higgno siku tano zilizopita, huku njaa ikiwa ina mchamanda kweli kweli, moja kwa moja akaelekea upande wa mjini, alitumia nusu saa kufika kwenye lango la nyumba ya mzee Mahamud akagonga na kufunguliwa mlango mdogo, “habari yako binti, nikusaidie nini?” aliuliza mlinzi huku anamtazama kwa umakini sana Hilda, “nashida na Talib” alisema Hilda kwa sauti ya tahadhari, “mh! we binti bado tu unamganda Talib, wewe si ndie yule uliekuja na wale wazee ulikuwa na mimba?” aliuliza mlinzi kwa sauti ya kutia shaka, “ndio lakini siku hizi ni mpenzi wangu” alisema Hilda kwa sauti fulani hivi ya kujiamini, “yeye anajua kama unakuja sasa hivi, maana mademu wake huwa hawaji mchana, na ameniambia kuwa akija mtu kumuulizia nimwambie hayupo” alisema mlinzi ambae alionekana kumtazama hilda kama mschana alie danganyika kabisa, “we mwambie tu Hilda anakuhitaji hapo nje” alisema Hilda kwa sauti ile ile ya kujiamini, ambae muda huo ukimsogelea ungeweza kuisikia harufu kali ya pombe, na ukizubaa unaweza kulewa kwa harufu hiyo iliyo changanyika na kutokupiga mswaki, “sawa lakini utakubaliana na majibu yatakayo toka, maana mi navyomjuwa Talib huwa hapendi kufuatwa na wanawake hapa nyumbani” alisema yule mlinzi huku anaingia ndani na kufunga lile geti dogo.
Hilda alisimama pale getini kwa dakika tano nzima, njaa ikizidi kumuuma, akimsubiri Talib ambae aliamini kuwa angetoka, mara hilda akasikia gate likianza kufunguliwa, akatabasamu kwa furaha, gate likafunguliwa na akatokea Talib akiwa amekunja uso kwa hasira na chuki, “we! mpumbavu umefuata nini hapa, au unataka kuni haribia kwa mjomba?” aliuliza Talib kwa sauti ya chini, lakini yenye ukali na hasira, “lakini Talib, si ulisema utanipa hela ya kumnunulia nguo mtoto” alisema Hilda kwa sauti ya mshangao, “hivi wewe unaniona mimi fala, yaani mtoto wa mtu mwingine halafu mimi nikamnunulie nguo?” aliuliza Talib, na kumshangaza Hilda ambae alimtazama Talib kama vile ndio anamuona leo kwa mara ya kwanza, “Talib jamani si ulimuona alivyofanana na wewe, usifanye hivyo Talib, mtoto ni wa kwako” alisema Hilda kwa sauti ya kuhuzunisha iliyokaribia kuangua kilio, “anafanana na nani, unadhani angekuwa wangu Higgno angekubali kuishi na wewe na mtoto, yaani wewe unakaa huku siku nne, yeye akae na mtoto ambae sio wa kwake, inawezekana vipi, kama unampenda huyo mwanao si ungeacha kunywa pombe halafu hela ungenunua nguo, hebu ondoka tena usiridi hapa” aliongea kwa harisa na sauti iliyojaa ghadhabu, kama uliwaona jana hakika leo ungeshangaa ni kwanini leo hii Talib yupo hivi.
Ukweli ni kwamba Talib sio tu hakuwa na mapenzi na Hilda, zaidi ya kumchezea na kukata kiu yake, pia alimchukia na kumuona kuwa ndie aliemsababishia akamaliza fedha za biashara yake ya samaki, “basi sawa naomba hata mia mbili ya nauuli” alisema Hilda ambae kiukweli hakuwa na hata shilingi moja, maana hata fedha aliyokuja nayo mjini siku ile alishaitumia siku nyingi, “acha useng.. wewe hela itoke wapi, hebu jikatae haraka usije kunijazia nzi hapa” alisema talib na kufunga gate, akibakia ndani huku Hilda akiwa nje, “jamani Talib, nimekukosea nini lakini? umeshaniharibia kwa Higgno na leo unanifanyia hivi” alilalamika Hilda kwa sauti ambayo ilishindwa kuficha kilio chake.******
“kwahiyo unataka kusemaje, unataka Hilda arudi kwa Higgno au?” aliuliza mzee Komba kwa sauti ya dharau na kebehi na kuwafanya wenzake wakina Nyoni wacheke kwa dharau, ilikuwa ni mara baada ya mzee Frank, kumaliza kuelezea jinsi ilivyokuwa toka siku Hilda alipotoweka, mpaka jana usiku alipoletwa na gari, akiwa pamoja na Talib wakija kumtazama mtoto wao, kisha kuondoka pamoja wakiacha maneno ya kashfa, “unadhani hata Hilda mwenyewe atakubali ujinga kama huo” alijibu bwana Ngonyani, huku wakiendelea kucheka, “bwana Komba, nikiwa kama mwenyekiti ambae nilifungisha ile ndoa ya mkeka ya Higgno na Hilda, leo hii naitengua rasmi” alisema mwenyekiti na hapo kikafuata kicheko cha kejeri, toka kwa mzee Komba na rafiki zake, “yaani mwenyekiti kama ungechelewa nilipanga nije kwako kukueleza swala hilo hilo, unajua huyu kijana sio wa hadhi ya mwanangu, ni kama alikuwa anamfuja tu! subiri sasa uone atakavyo nawiri, na kwa taarifa fupi ni kwamba yule kijana amesema tuandae makoo yetu, kila siku itakuwa ni pombe za kizungu tu!” alisema mzee komba kwa sauti ambayo kama ungeisikia kwa jinsi ilivyojawa na dharau, pengine ungerusha ngumi, kwa hasira, Naaam huyo ndio mzee komba hajui lolote linaloendelea kuhusu Hilda, nini kitajiriiiii? ITAENDELEA.
 
Mzee Komba ataanza kutia huruma tena.
Ila wewe jamaa ni mtunzi mzuri sana.
 
🔥🔥🔥🏃🔥🔥
 
“kwahiyo unataka kusemaje, unataka Hilda arudi kwa Higgno au?” aliuliza mzee Komba kwa sauti ya dharau na kebehi na kuwafanya wenzake wakina Nyoni wacheke kwa dharau, ilikuwa ni mara baada ya mzee Frank, kumaliza kuelezea jinsi ilivyokuwa toka siku Hilda alipotoweka, mpaka jana usiku alipoletwa na gari, akiwa pamoja na Talib wakija kumtazama mtoto wao, kisha kuondoka pamoja wakiacha maneno ya kashfa, “unadhani hata Hilda mwenyewe atakubali ujinga kama huo” alijibu bwana Ngonyani, huku wakiendelea kucheka, “bwana Komba, nikiwa kama mwenyekiti ambae nilifungisha ile ndoa ya mkeka ya Higgno na Hilda, leo hii naitengua rasmi” alisema mwenyekiti na hapo kikafuata kicheko cha kejeri, toka kwa mzee Komba na rafiki zake, “yaani mwenyekiti kama ungechelewa nilipanga nije kwako kukueleza swala hilo hilo, unajua huyu kijana sio wa hadhi ya mwanangu, ni kama alikuwa anamfuja tu! subiri sasa uone atakavyo nawiri, na kwa taarifa fupi ni kwamba yule kijana amesema tuandae makoo yetu, kila siku itakuwa ni pombe za kizungu tu!” alisema mzee komba kwa sauti ambayo kama ungeisikia kwa jinsi ilivyojawa na dharau, pengine gerusha ngumi, kwa hasira, Naaam huyo ndio mzee komba hajui lolote linaloendelea kuhusu Hilda, nini kitajiriiiii? ITAENDELEA.
Du! Mkuu hyo Binti kumuita Hilda ni kama vile hujamtendea haki, añastahili kuwa na jina lililochangamka zaidi, mfano "Jesca" maana ndo mambo Yao hayo😂🤣😂🤣😂🤣🤣😂🤣😂😂🤣😂🤣🤣🤣
 
🤣🤣 Ni Ex wako huyo jesca au?
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA TISA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE : “bwana Komba, nikiwa kama mwenyekiti ambae nilifungisha ile ndoa ya mkeka ya Higgno na Hilda, leo hii naitengua rasmi” alisema mwenyekiti na hapo kikafuata kicheko cha kejeri toka kwa mzee Komba na rafiki zake, “yaani mwenyekiti kama ungechelewa nilipanga nije kwako kukueleza swala hilo hilo, unajuwa huyu kijana sio wa hadhi ya mwanangu, ni kama alikuwa anamfuja tu! subiri sasa uone atakavyo nawiri, na kwa taarifa fupi ni kwamba yule kijana amesema tuandae makoo yetu, kila siku itakuwa ni pombe za kizungu tu!” alisema mzee komba kwa sauti ambayo kama ungeisikia kwa jinsi ilivyo jawa na dharau, pengine ungerusha ngumi kwa hasira…. ENDELEA NAYO

Lakini kwa uvumilivu aliokuwa nao Frank na familia yake ulisaidia kuto kuleta majanga, maana bwana Frank aliekuwa amembeba mtoto wa Hilda, alisogea kwa mzee Komba na kumkabidhi mtoto, “na sisi hatuna shaka bwana Komba umeshamfahamu mkweo na baba wa huyu mtoto, hivyo na kukabidhi mjukuu wako mbele ya mwenyekiti” alisema bwana Frank, kisha akamtazama mke wake aliekuwa amebeba mfuko wa shangazi kaja, na mke wake akajuwa afanye nini, akamkabidhi ule mfuko mke wa Komba yaan mama Hilda, “babu, njoo hapa umsubiri baba yako, tena tajiri mkubwa sana, karibu utaenda kukaa kwenye nyumba ya maana” alisema Komba na wenzake wakacheka kwa furaha na kashfa.
Baada ya makubariano hayo mzee Frank na familia yake mwenyekiti na wajumbe wake wakaondoka zao, wakiwaacha mzee Komba na marafiki zake wakiendelea kunywa ulanzi ambao kwa sasa ndio ulikuwa umebakia, maana ile pombe kali ilishaisha, “jamani, pombe ikiisha, tunaenda kuongeza lita ishirini nyingine, hii ndiyo faida ya kuwa na binti mrembo” alijinasib mzee Komba, pasipo kujuwa kinachoendelea huko mjini kati ya mwanae Hilda na mkwe wake Talib.*******

“unajua da Laylah, kuna wakati huwa nakosa amani kabisa, hasa mama anapo nikumbushia swala la kuolewa” alisema Soraya wakati wana livuka soko kuu na kukata kona kushoto kuingia kwenye barabara ya kuelekea kwao, “ukweli hapo da Soraya, hata mimi huwa unanishangaza, ina maana we hujaona hata mmoja ambae anakufaa?” aliuliza Laylah, huku wakilisogelea gate la kuingilia pale kwao, “mh! Laylah, hebu ona, mbona kama yule mschana pale getini kwetu analia” aliuliza Soraya wakimtazama mschana mmoja aliekuwa amekaa pembeni ya geti la kina Soraya, yaani kwa tajiri Mahamud, akijiziba uso na kufikicha macho, “ndio tena kama namkumbuka yule dada alishawahi kuja hapa kwenu miaka iliyopita” alisema Layla, huku anakanyaga break na kusimamisha gari mbele ya geti, kisha akapiga honi mbili, “hebu kwanza muite huyo dada” alisema Soraya na wakati huo geti lilikuwa linafunguliwa, “we dada njoo mara moja” aliita Laylah, kimtazama yule mschana, alie kuwa amesimama pembeni ya geti, huku akionekana wazi analia, “boss achana nae tu, huyu amekuja kuomba omba nimemuambia aje ijumaa yeye ndio anaanza kulia” alidakia mlinzi, na hapo Soraya akamkata jicho mlinzi, kisha akarudisha kwa yule mwanamke akamuona anajivuta kusogelea gari, “dada unashida gani? mbona unalia nje ya geti la watu, huoni kama unaleta picha tofauti kwa wapita njia ambao wanaweza kusema wakazi wa humu wana wanyanyasa watu?” aliuliza Soraya, ambae alishusha kioo cha seat za nyuma alikokuwa amekaa, “dada inaniuma, yaani Talib ameniharibia maisha yangu mara ya kwanza, amenizalisha, akanitelekeza na kunikataa, nime bahatika kuishi na mwanaume ona sasa leo siku ya nne sijalala nyumbani nipo nae, tulienda kumtukuna mume wangu halafu yeye amemaliza haja zake ananifukuza kama hanijuwi” alisema Hilda huku anaangua kilio, “we dada una maanisha Talib yupo humu ndani, mbona alisafiri kwenda mbinga amerudi saa ngapi?” aliuliza Soraya kwa mshangao na mashaka, “hapa hakuwa mbinga, alikuwepo hapa hapa songea” alisema Hilda huku akifuta machozi na kamasi zilizokuwa zina mtoka, “mh! wewe ndie yule uliekuja mwaka juzi na wazazi wako?” aliuliza soraya kwa mshangao huku akimtazama Hilda kwa mshangao, Hilda akaitikia kwa kichwa, “sasa na we dada, mtu alikukataa akakutelekeza na mtoto, ikawaje umfuate mara ya pili?” aliuliza Soraya kwa sauti ya kustaajabu, huku anapekuwa pochi yake na kutoa noti ya elfu moja, “aya we nenda nyumbani, mimi nitaongea na Talib” alisema Soraya huku anampa Hilda ile noti, Hilda akaitazama kwa mshangao wa kutoamini, kisha akaifumbata mkononi, “asante dada yangu” alisema Hilda huku akipiga nusu goti, wakati huo Laylah, alikuwa anakanyaga mafuta na kuingiza gari ndani, kisha mlinzi akafunga geti, “babu kuna kitu unakihitaji, sijui kama kuna mtu atakusaidia kuhudumia familia yako utakapo fukuzwa kazi” alisema Soraya wakati anakatiza pale getini, akiwa ndani ya gari lake, “samahani boss lakini sikuwa na la kufanya maana niliambiwa nisimkaribishe” alisema mlinzi ambae muda mrefu alishaingiwa na uoga mkubwa, “we haya tu” alisema Soraya, huku Laylah akiendesha gari taratibu kusogea kwenye mlango mkubwa.*******

Habari za kutembelewa na Talib nyumbani kwenye familia ya bwana Frank akiwa na Hilda wamelewa chakari na kuletewa kashfa zilitapakaa sana mtaani Luhila, wanafiki walitoa pole huku mioyoni mwao wakimcheka Higgno, wakimuona ni mjinga wakidhania kuwa anampenda sana Hilda, ambae licha ya vitimbi anavyomfanyia miaka yote lakini bado anamng’ang’ani, hawa kujuwa maisha ya wawili hawa yalikuwaje.
Kutokana na kashfa hizo, hakika Higno alikosa amani moyoni mwake, akashinda akijifungia ndani mwake akiwaza kilicho mtokea na kujiona mwenye bahati mbaya sana, kwanza hakuwa na mwanamke ambae angemuita ni mpenzi au demu wake, halafu anatokea mtu anamchzea mchezo wa ajabu ambao unamletea kashfa na zihaka za hali ya juu, “baba naona week hii wakati nasubiri kwenda kwenye maombi ya kazi bora nikakae kule shambani” alisema Higgno akimueleza baba yake wakiwa wanakula chakula cha mchana, “lakini utakaaje kule shamba wakati hakuna kitanda, pia mazingira sio mazuri ni rahisi kuvamiwa na wadudu au wanyama” alisema baba yake Higgno ambae kiukweli, alifadhaika sana kwa hali ya mwanae ya kukosa amani, “lakini baba Higgy, bora ungemuacha aende akakae shamba, akipata kazi tutampangia chumba mjini” alishauri mama Higgno, ambae pia alihuzunishwa na hali ya mwanae ya kosa amani kwasababu ya kusimangwa mtaani.
Hapo kwa pamoja baba na mama Higgno wakakubaliana na kumkubalia Higgno kwenda kukaa shamba, huku wakimfungashia vitu vingi vya kwenda kukaa navyo kikiwepo kitanda cha kamba, godoro dogo, na matandiko makubwa yenye kuzuia baridi, maana ndie adui mkubwa kwa kipindi hiki cha kipupwe, hawakusahau kumfungashia masurufu ya mchele kidogo unga dagaa chumvi sukari na vitu ambavyo vingemsaidia katika maisha ya kila siku ya kule shambani, Higgo mwenyew hakubakia nyuma alibeba vitu ambavyo aliviona vinge mliwaza kule shamba, kama vile redio casset yake ndogo, ambayo aliinunulia mabetri mpya, pia alinunua ndoano mpya na vifaa vya kutegea kwale na wanyama wadogo wadogo kama sungura na na wengine wa aina hiyo, kisha akafunga mlango wa chumba chake na kumkabidhi mama yake kisha akaondoka zake.*******

Soraya aliingia ndani na kupitiliza jikoni, ambako alitoa maagizo ya kuwekewa chai yeye na Laylah, dereva wake ambae kwa sasa alikuwa kama rafiki yake na msiri wake, “mh! kwani mama amerudi, au kuna mmoja kati yenu alienda sokoni?” aliuliza soraya akiwa ana tazama samaki aina ya mbasa waliokuwa wanaandaliwa kwaajili ya mboga ya mchana, “hapana, hawa samaki amekuja nao kaka Talib, amerudi asubuhi toka nyasa” alijibu mfanyakazi mmoja wa ndani, ambae kazi yake ni jikoni peke yake, “mh! ndivyo alivyowaambia kuwa alikuwa Nyasa?” aliuliza Soraya huku akimtazama dada wa jikoni, “hajasema, lakini akijaga na vitu hivi huwa najua ametoka Nyasa” alijibu mfanyakazi yule na hapo Soraya akatoka na kuelekea sebuleni kusubiri chai, chai ailiyo agiza.*****

Yap! tuachane na mambo yaliyotokea mchana, tuje jioni kabisa, mida ya saa moja, giza lilikuwa linaanza kutanda, mida ambayo Hilda alikuwa anaingia nyumbani kama alivyopanga kufanya hivyo, maana alishindwa kuingia mchana akihofia kukosa jibu la kuwapa wana Luhila, kutokana na mambo kwenda tofauti, hivyo akaona kuwa mida hii ndio sahihi kwa yeye kwenda nyumbani kwao kimya kimya pasipo kuonekana na mtu, hakuwa tena na shilingi hata moja, ni baada ya ile elfu moja kuitumia kwa chakula cha mchana, miguu ilikuwa imemchafuka kwa vumbi kutokana nakutembea mwendo mrefu kwa miguu, uchovu wa mlo mmoja na pombe ya siku nne mfululizo, kukosa usingizi kwa kuchelewa kulala kwa kuepeana dudu vilizidi kunyong’onyesha Hilda, ambae mwanzo aliona kuwa asinge weza kwenda kwa Higgno, kwasababu jana usiku alisha vuluga, lakini dakika kumi baadae alipo karibia kwao, kwa mbali aliona watu kibao wakiendelea kunywa pombe, “nikifika napitiliza ndani moja kwa moja sitaki maswali” alijisemea Hilda, huku akijitahidi kuongeza mwendo.
Lakini alipokaribia akajikuta anasimama ghafla, ni baada ya kuanza kusikia maongezi ya pale nyumbani kwao, “nyie msiwe na wasi wasi tiuka lepa mpaka timale ugimbeee” alimsikia baba yeke akiongea kwa sauti yakilevi iliyo pitiliza, akimaanisha “hatuondoki hapa mpaka tumalize pombe” hilo halikumshtua sana, mpaka alipo msikia akisisitiza tena, “jiandae kunywa mi pombe ya kizungu, atakuja nayo Hilda” hapo Hilda akajikuta akigeuka haraka na kurudi alikotokea, “bora niende kwa kina Higgno, hawa shauri zao, wasubiri mpaka wachoke” alijisemea Hilda huku anashika uelekeo wa kwakina Higgno, yaani kwa mzee Frank…….. ENDELEA KUFUATILIA MKASA HUU HAPA HAPA jamii forums

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHILINI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: Lakini alipokaribia akajikuta anasimama ghafla, ni baada ya kuanza kusikia maongezi ya pale nyumbani kwao, “nyie musiwe na wasi wasi tiuka lepa mpaka timale ugimbeee” alimsikia baba yeke akiongea kwa sauti ya kilevi iliyo pitiliza, akimanisha “hatuondoki hapa mpaka tumalize pombe” hilo halikumshtua sana, mpaka alipomsikia akisisitiza tena, “jiandae kunywa mipombe ya kizungu, atakuja nayo Hilda” hapo Hilda akajikuta akigeuka haraka na kurudi alikotokea, “bora niende kwa akina Higgno, hawa shauri zao, wasubiri mpaka wachoke” alijisemea Hilda huku anashika uelekeo wa kwakina Higgno, yaani kwa mzee Frank.... ENDELEA

Ambako litumia muda mfupi sana kufika kwasababu hapakua mbali sana, kutokana na kitendo alicho kifanya jana usiku, Hilda hakutaka kuonana na mtu mwingine yoyote pale nyumbani kwa akina Higgno zaidi ya Higgno mwenyew, maana alijuwa kuwa angeweza kumtuliza kwa kumtishia mwenyekiti, hivyo Hilda moja kwa moja alielekea kwenye mlango wa chumba cha Higgno kule kwenye mabanda ya nje, akanyonga kitasa kwa maana ya kufungua, lakini akagundua kuwa mlango ulikuwa umefungwa kwa funguo, hapo akageuka na kutazama mlango wanyumba kubwa, hakuona mtu, akageukia mlango wa chumba kile na kujaribu kukinyonga tena kitasa ambacho bado alikuwa amekishikilia, tena safari hii alikinyonga kwa fujo ungesema mtoto au mlevi anaekaribia kuharibu kitasa hicho, “mh! mama tungekuwa tuna fanyaga hivyo ungekikuta kweli” Hilda alishtuka na kugeuka nyuma kutazama ilikotokea sauti hii, ambayo hakuhitaji mkalimani au kamusi kuitambua kuwa ni sauti ya mama yake Higgno, akamuona akiwa anatokea ndani kwenye nyumba kubwa, sasa yeye anafunga mlango halafu mimi nitapitia wapi?” aliuliza Hilda, huku anajaribu tena kunyonga kitasa cha mlango ule, “weeee! hebu subiri kwanza” alisema mama Higgno huku anauondoa mkono wa Hilda kwenye Kitasa, “vipi kuna kitu umekisahau humu ndani, yaani kwa yote uliyoyafanya jana usiku leo unarudi hapa?” aliuliza mama Higgno, kwa sauti ya mashangao huku akimtazama Hilda usoni, lakini huwezi amini, kwajinsi alivyokosa adabu na aibu, Hilda akiwa mwenye macho makavu akajibu, “mama mambo yangu na mume wangu hayakuhusu, wewe umeolewa kwenye nyumba hii na mimi nimeolewa, kama ni kesi au nini nitamalizana na mume wangu” alisema Hilda bila kigugumizi, “eti! mimi na wewe wote tumeolewa, sasa subiri hapo hapo” alisema mama Higgy, huku anaondoka na kuingia nyumba kubwa.
Hilda akabaki ana jaribu kunyonga tena kitasa, “huyu mshenzi yupo wapi, nitaenda kumuambia baba twende kwa mwenyekiti” alipiga kelele Hilda kwa hasira, na wakati huo akasikia sauti toka nyumba kubwa, “mke wangu hebu punguza hasira, kwani kuna nini?” ilikuwa ni sauti ya mzee Frank, Hilda akageuka na kutazama kwenye mlango, akamuona mama Higgno anatoka huku amebeba mwichi wa kutwangia, lakini mume wake akamnyang’anya, “niache ni mfundishe adabu huyu mpuuzi, anaongea na mimi kama vile kwao hakuna wakubwa, “alisema mama Higgno, huku akijaribu kuuchukuwa ule mwichi mkononi mwa mume wake, lakini mzee Frank akamzidi mke wake na kuuchukuwa kabisa, hapo mama Higgno akatazama usawa wa mlango wa jiko, na kuona rundo la kuni pembeni ya banda la jiko la nje, akachomoka mbio na kwenda kuchukuwa kuni moja nyembamba ya mti wa msuku, (ni matunda maarufu mkoani ruvuma,mti wake una fanana na mkorosho) kisha akaanza kumfuata Hilda, “nipige wewe si mwanamke kweli, nipige tuone…” unadhani alimalizia maneno yake, unajuwa Hilda alijuwa anatishiwa, na ukichukulia ni kwamba toka amefika pale hakuwahi kupigwa hata kibao cha bahati mbaya, hivyo akajuwa kuwa mama Higgno anamtishia tu!.
Lakini wazo lake lilikuwa tofauti, kwasababu alishtuka akipigwa na kuni ya mgongoni, ile kutahamaki kwamba ni kweli mama Higgno alishamchoka na leo anamtwanga, kuni nyingine ya bega, ilishuka kwa nguvu na kumuangusha chini, hapo zika mshukia kuni kadhaa za sehemu mbambali, makalioni, mgongoni mabegani, mapajani, ilimradi mama Higgno alikuwa anashusha kipigo, kama mtu aliekuwa anapuna mahindi au mbaazi kwenye kiroba, Hilda aliachia kilio kikubwa na kikari cha uchungu, lakini mama Higgy hakumuachia, “basi mke wangu utauwa” ni baba Higgy, ndie aliegeuka kuwa msaada wa Hilda, tena kwa kumshika mke wake asiendelee kutoa kipigo kwa Hilda, ambae hapo ndipo alipopata mpenyo na kukimbia kuelekea kwao, “mbwa koko, nenda kaipeleke kwa washenzi wenzio” alisema mama Higgno aliekuwa ameshikiliwa na mume wake, “mke wangu umeuwasha moto, walevi wote wataamia hapa kwetu” alisema mzee Frank, akiamini kuwa kitendo cha kumtandika Hilda kinge leta majibu mabaya kwao.******

Yap! mida hii ya usiku wa saa moja na nusu, mita mia moja toka barabara ya vumbi ya mahilo, iliyo katiza pembezoni mwamilima ya matogoro, Higgno alikuwa amekaa nje ya kibanda chake, anaota moto huku anachoma mahindi ya mtoni, wenyewe waita madimbeni, na kusikiliza redio yake, ni baada ya kuwa amesha maliza kufanya mazoezi ya karate, ambapo sasa alikuwa amesha jiifadhia stail nyingi sana kichwani mwake, na kumfanya iwe rahisi yeye kufanya mazoezi hata akiwa peke yake, mwangaza wa moto ulijitahidi, kupenya kwenye giza na kuleta mwangaza kiasi, sauti ya kuni zikilalamika kwa kuteketea kwenye moto zilisikika sambamba na sauti ya madege ya ajabu yaliyopo kwenye msitu uliozunguka eneo ili la shamba zilisikika, “nikipata kazi na mimi nitafute mke” aliwaza Higgno, ambae leo alijiona kama vile mfungwa alieachiwa huru kwa msamaha wa raisi, maana kuishi na Hilda tena kwa ndoa ya kusingiziwa yalikuwa ni mateso makubwa kwake, “natafuta mschana mzuri mpaka watu wa Luhila wakimuona washangae na roho zao” nadhani yalikuwa ni mawazo ya hasira na machungu, kutokana na maneno ya Kashfa yaliyo tolewa na baadhi ya watu wa mtaa huo.
Katika mawazo hayo pia Higgno aliwaza juu ya Talib, “sijui ataniharibia kwa mjomba wake, Sijui nime mkosea nini yule jamaa, yaani kila mara yeye ananifanyia mambo ya hovyo” aliwaza Higgno, huku mara kwa mara ana geuza mahindi yake juu ya jiko, “ila nime koma kumsaidia Hilda, mwanamke ana roho ya kishenzi kama nini” aliendelea kuwaza Higgno, ambae hakujuwa kinachoendelea huko nyumbani kwao.*******

Saa mbili na robo, tayari swala ya inshaa ilisha malizika, Familia ya mzee Mahamud ilikuwa mezani, yaani Mahamud mwenyewe, mke wake, yaani mama Soraya, Soraya binti yao, na Talib, mpwa wao wanapata chakula cha jioni, kama ilivyo kawaida yao “bwana Talib, habari za Nyasa?” alisalimia bwana Mahamud ambae hakumtazama, “mzuri tu mjomba” alijibu Talib akiwa ameinamisha kichwa chini, kama vile hakutaka mtu yoyote atazamane nae, “ina maana Talib ulishindwa kuaga au kupiga simu kuwa umeenda Nyasa, maana leo ndio najuwa kuwa ulienda Nyasa” aliuliza shangazi yake Talib, yaani mama Soraya, japo alikuwa ni Mngoni halisi, lakini ungemtazama unge kubaliana na mimi, kuwa mama Soraya ni mke wa tajiri, tena wakiarabu, vaa yake urembo na uzuri wake, hata mapambo ya kiarabu aliyojitundika kwenye masikio na shingo yake hata mikono yake, “au mwenzetu alikupigia simu” aliuliza mama Soraya akimtazama mume wake, ni baada ya kuona Talib haja jibu lolote, “hapana haja nipigia wala kuniambia, ila nimeona hawa samaki nikajuwa ametokea huko” alijibu Mahmud huku wanaendelea kula, lakini Talib akiombea kuwa maongezi yake yaishie pale pale maana yakiendelea pengine yange umbua mambo, “lakini baba, samaki haimaanishi kuwa alienda Nyasa, si anaweza kuwa aliwanunua hapa sokoni na kuleta mboga nyumbani” alisema Soraya na wote wakamtazama mschana huyu, ambae kwa sasa muonekano wake ni wa kimwanamke mkubwa kabisa ukiambiwa bado hajaliwa kitumbua ungebisha na kuomba ukamkague kwa dau lolote, maana dada la dada haswa, maneno ambayo yalimstua sana Talib na kumfanya ainue uso kumtazama Soraya, bahati mbaya jicho hilo lilionwa na mzee Mahamud pekee, maana Soraya na mama yake walikuwa wametazamana, “we Soraya nawe, tokea lini Talib anaenda kununua mboga sokoni, aanze tu!” alisema mama Soraya, kwa sauti yenye kipinga mizi, “kwani unamuonaje kaka Talib, hawezi kununua mboga na kuleta, basi pengine ndio ameanza leo” alisema Soraya, na hapo Talib akamuona Soraya ni mnoko wa hali ya juu, “huyu mshenzi, anataka kuharibu” aliwaza Talib na hapo hapo mama Soraya akaonekana kung’amua jambo, “inawezekana eti, kwanza umetoka saangapi nyasa mpaka uingie saa mbili hapa nyumbani?” aliuliza mama Soraya, hapo Talib akasisimkwa na kujawa na mzizimo kichwani mwake, “pengine alikuja jana usiku, akaamua kulala na wifi kwenye nyumba ya wageni” alidakia Soraya, wote wakacheka, hata Talib pia alicheka kwa kujilazimisha, “ndio maana nilisema huyu nae bora afe ili nibakie mimi nifaidi, maana atanizibia mambo mengi sana huyu” aliwaza Talib, “Soraya, unawajuwa wifi zako?” aliuliza kwa utani mzee Mahamud, “na mjuwa yule aliezaa nae, halafu umkumbuke mwanao kaka Talib” alisema Soraya, hapo Talib akaachia tusi la nguoni kimoyomoyo, “…… Malaya wewe utaona nitakacho kufanyia, maana alishaona kuwa Soraya amesha juwa kilicho tokea siku nne hizi, ambazo yeye hakuwepo nyumbani “unamzunguzia yule ambae alimkataa kipindi kile?” aliuliza mama Soraya huku ana watazama kwa awamu yaani Soraya na Talib, tena kwa macho ya mshangao, “ndiyo huyo huyo, yani mambo anayo yafanya kaka ndio maana mimi sipendi kuolewa” alisema Soraya, kwa sauti ya masikitiko, “mwanangu matendo ya mwanaume mmoja yasikufanye uwachukie wote, mfano mimi nilikuwa naamini wanaume wenye uwezo mkubwa kifedha ni wanyanyasaji wa wanawake, lakini nime mpata baba yako mwanume safi kabisa, tunaishi kwa amani siku zote” alisema mama Soraya, “ila mwanangu unapaswa kuwa muoga, maana siku zote, ujanja na ujuaji mwingi, mwisho wake giza, mimi kuna kijana nime muona, na ninge penda awe mume wako” alisema Mahmud, kwa sauti tulivu sana, hapo kila mmoja akashtuka na kumtazama Mahmud kwa mshangao, ila kwa Soraya sio mshangao peke yake na mshtuko pia, “baba Soraya, ulisema kuwa tusi mchagulie mtoto mume mbona kama…?” mama Soraya hakumaliza swali lake, mzee Mahamud, akamdaka juu kwa juu, “nimesema ningependa awe mume wake, sio awe mume wake, halafu isitoshe yule kijana sijui anapoishi wala jina lake na wazazi wake, naamini atakuwa ni mcha mungu, maana nidhamu na utu wake ni wa hali ya juu sana” alisema mzee Mahamud, “unamzungumzia yule aliekuokoa toka mikononi mwa majambazi?” aliuliza mama Soraya, na hapo Talib akashtuka kama vile amepigwa shot ya umeme, Soraya akatega sikio kusubiri jibu la baba yake, “huyo huyo, ni kijana mpole mtaratibu, asie na tamaa ya fedha, maana siku ile nilikuwa tayari kumpatia fedha nyingi sana lakini alikataa, na angefaa sana kumsaidia Soraya katika usimamizi wa biashara na miradi yake” alisema mzee Mahamud, hapo Talib akaonekana kushtuka na kuchomwa na maneno yale, “lakini anko, ujuwe kuna watu wajanja na matapeli, pengine alipanga na hao wezi, wakuvamie nae ajifanye amekuokoa” alisema Talib, kwa sauti ya kubeza, “mh! kwa jinsi alivyo watandika, mbona mpango wao unge vulugika, halafu angefanya hivyo kwa faida ipi, mbona fedha alikataa” alisema Mahamud, na mkewe akamuunga mkono, “eti kama lengo lake ni fedha si angepokea alizo pewa” alisema mama Soraya, wakati huo Soraya ni kama alikumbushwa kuhusu kijana mpole aliemsaidia asibakwe na wale wanafuzi wakorofi, “inaweza isiwe fedha, si kama hivyo pengine unataka amuoe Soraya” alisema Talib, akionekana wazi kuto kupendezewa na wazo la mjomba wake, “si angekuwa ameshajitokeza na kumuowa, sasa mwaka mzima anasubiri nini?” aliuliza mama Soraya, na baba Soraya akaunga mkono, “ni kweli, kama ni hivyo tayari angesha jitokeza, halafu angewezaje kufanya jambo hilo la hatari, kwa kitu ambacho kinahitaji maamuzi binafsi, maana hata hajui kama mimi nimewaza jambo kama hilo” alisema mzee Mahamud” Soraya nae akawaza la kwake, lakini hakuweza kuongea chochote, “nyie haya tu! lakini kuna watu wajanja, na wana mipango mirefu” alisema Talib, kwa sauti iliyojaa tahadhari, lakini mzee Mahamud na mke wake wakapotezea kwa kuona hoja ya Talib haikuwa na mashiko, ndio kwanza mama Soraya akamgeukia mwanae Soraya, “umemsikia baba yako Soraya, na wewe tuambie kama umesha miona mkwe wetu mtarajiwa” alitania mama Soraya, na mume wake akadakia, “ni kweli mwanangu utakuwa unatudanganya kama utasema haujawahi kumuona hata mmoja ukafikiria kuwa anaweza kuwa mumeo hapo baadae” maneno hayo yaliongelewa kwa namna ya utani, na wote wakacheka kasoro Talib, ambae alikuwa ametulia kimya anaendelea kukandamiza chakula, “jamani mi staki, kwani kumuona ndio kuwa nae” alisema Soraya, huku anacheka cheka, “kwahiyo umemuona sio, lakini bado hajakuwa mchumba wako?” aliuliza mama Soraya, kwa ile sauti ya mama kwa mtoto, “ndiyo niliwahi kumuona, yule alienisaidia nisipigwe na wale wanafunzi wa songea boys kule TTC, mwaka ule nikiwa form two” alisema Soraya kwa saut iliyo jaa aibu, “bado tu hujasahau, miaka mingi imepita mwanangu” alisema mzee Mahamud huku anacheka kidogo, “asingeweza kusahau kwa wema aliomfanyia yule kijana, na nilichomsifu ni kitendo cha kumsaidia na kumuacha aende, maana wengine wangeanza na ukaribu wa kujipendekeza” alisema mama Soraya, na hapo maongezi yakwa ndiyo hayo, “ni kweli mke wangu, huyo kijana anafanana kitabia na yule alienisaidia mimi” alisema Mahamud, maongezi ya baba na mama Soraya yalimfanya Soraya ajisikie kiu ya kutamani kukutana na kijana mpole, pasipo kujuwa kama atakuwa amebadilika kwa sura na umbo au laa, “usikute ni mtu mmoja, maana siku hizi vijana wenye moyo huo utawatoa wapi” alisema mama Soraya na wote wakacheka kwa pamoja, kasoro Talib, “itapendeza kama akiwa ni mmoja hakika nitamuozesha mwanangu kwa mahali ndogo sana, na kugharamia ndoa yao pasipo mashart yoyote” alisema Mahamud pasipo kujuwa kuwa alikuwa anaweka kiapo, au nadhiri, “mimi nitawanunulia gari zuri jipya, wawe wanatembelea katika mizunguko yao, alisema mama Soraya, na kumchukiza zaidi Talib, “gari ni ni haki yao, kama ilivyo swala la nyumba, nita wajengea au kuwa nunulia nyumba nzuri, japo nitawatengea chumba chao humu ndani siku moja moja wawe wana pumzika hapa” ni kama zilikuwa simulizi za kuliwaza kwa Soraya, maana hakuamini kama anaweza kukutana na kijana yule, japo katika maongezi yao, mioyoni mwa wazazi wake kulikuwa na imani kuwa Soraya na kijana mpole wanafahamiana, ukweli Story hizi hazikumpendeza Talib, ambae alikuwa amejiinamia na kuendelea kula kimya kimya.*******

Giza lilishatanda kwa kiasi kikubwa, nyumbani kwa mzee Komba watu walikuwa wamejaa, maana kila aliepita njia alikuwa anakaribishwa, kuja kunywa pombe, tofauti na asubuhi, sasa walikuwepo wakina mama pia na mpaka sasa tayari mzee Komba aliagiza madumu mengine sita, na kufanya idadi kuwa kumi, toka asubuhi, ungesema kilabu cha pombe zile kimehamia nyumbani kwa mzee Komba, kwa uwingi wa pombe iliyonyweka na uwingi wa watu, nyimbo za kilugha zilitawala huku wengine wakicheza, nyimbo zilizovuma mahali hapo, ni kama vile ibesa mau, vandu makoko, tiuka lepa, uswengile na nyingine nyingi.
Lakini wakati burudani zinaendelea huku wakiamini zitaongezeka pombe za kizungu, mara wakamsikia mzee nyoni akipiga kelele za shangwe, “kamweli wetu huyoooooo” wote wakageuka kutazama kule iliko barabara ya kujia pale nyumbani na kumuona Hilda akiwa anakuja mbio mbio na mikono kichwani, hapo ukapita ukimya wa ghafla na sauti ya kilio ikapata nafasi ya kupenya na kuingia masikioni mwa walevi hawa, “waaa! waaaa! mayoooo! nakufa leo mimi!” ni kama Hilda aliongeza sauti baada ya kufika kwao.
Watu wote waliinuka na kumzunguka Hilda kutaka kujuwa kulikoni, “jamani kuna nini tena mbona Hilda analia?” yalikuwa ni maswali ya mshangao, yaliyoulizwa kwa sauti za chini za minong’ono, “mwanangu niambie, nini kimetokea, au Higgno amekupiga, niambie mwanangu tumpeleke polisi sasa hivi” hilo lilikuwa swali la mama Hilda yaani mke wa mzee Komba, “kwanza mwenzio yupo wapi, si ulisema mutakuja wote?” aliuliza mzee Komba, lakini jibu lilitoka moja, “mama Higgno amenipiga” alijibu Hilda, “eti amekupiga, asinitanie huyu mwanamke, kwanini anakupiga kwani lazima kuishi na mwanae, anaenuka umasikini, hebu twende huko huko” alisema mama Hilda huku anamshika mkono mwanae na kutaka kuondoka nae, “hebu subiri bi komba atueleze imekuwaje mpaka akapigwa” zilikuwa ni busara za mzee Kambanga, ambae alikuwa na masaa mawili toka amefika mahali pale, hivyo hata ulevi wake ulikuwa wastani, “eti Hilda imekuwaje kuwaje, yaani kwanini mama Higy amekupiga?” aliuliza bwana Nyoni kwa sauti ya kilevi, huku mzee Komba na watu wengine wakisubiri jibu, na nyuso zao wamezikunja kwa hasira, “mimi nilikuwa nimetoka mjini, ndio nikaenda kwa mume wangu, ndio nashangaa yeye ananiambia niondoke, ndio mimi nika mwambia kwanini niondoke kwa mume wangu, ndio yeye akachukuwa kuni na kuanza kunipiga nayo…” hapo hapo mzee Ngonyani akamkatisha, akionyesha kutokuelewa mada ile kama ilivyo kwa wenzake, “hapo hapo binti Komba, maana kama sijakuelewa hivi, ina maana mumeo ni yupi?” aliuliza mzee Ngonyani, kwa sauti yake ya kilevi, “kwani humjuwi mume wa Hilda, pombe mbaya sana, si yule kijana wa mzee Frank” alisema mzee Kambanga kwa uhakika wa asilimia mia moja, mpaka hapo mzee Komba alikuwa anahisi kizungu zungu, na pombe zikihama kichwani mwake, huku mke wake akiomba isiwe kweli anachohisi kime tokea, “wewe ndio hujuwi sasa, huyu binti mchumba wake ni yule mtoto wa mwarabu tajiri wa mjini, Mahamud” alisema mzee Ngonyani nae kwa uhakika wa asilimia mia moja, “mh! hapo mnanichanganya, maana mimi najuwa ni mwaka sasa Hilda anaishi na Higgno, sasa kuhusu huyo mchumba mtoto wa Tajiri ni ngeni kwangu” alisema Kambanga, na hapo ikaanza minong’ono ya chini nini ambayo ni kama ilikuwa inaleta ufafanuzi, “mh! ni kweli inachanganya, maana inasemekana jana huyu bnti alienda nyumbani kwa Frank na huyo mchmba wake” alisema mmoja kati ya wanakijiji waliokuwepo pale, na mwingine akidakia, “na leo Frank alikuja hapa na mwenyekiti kuvunja ndoa rasmi” alisema mwingine, “kwanini na wewe uende huko kwa Higgno wakati vitu vyako walisha vileta toka asubuhi, kwani mchumba wako yupo wapi?” aliuliza mama Hilda huku taratibu mzee Komba akigeuka na kulekea kwenye mlango wa nyumba yake na kuanza kupapasa kuingia ndani, maana hakukuwa na taa wala kibatari, “amenifukuza tena” alisema Hilda kwa sauti ya chini iliyojaa unyonge, hapo mama Hilda akapiga ukulele wa maana huku akijishika kichwani, “mayooo neneeeneee tumeumbuka sie jamani, huuuwwwwwi” alisema hayo huku anajilaza chini na kuanza kugala gala, kama mtu aliepewa taarifa ya kifo cha mtu muhimu kwake, “kumbe yule kijana yule na goti nilimpigia jana, mimi yoyoooooo, nitalipaje pombe ya watu mwenga” alipiga kelele mama Hilda, huku wenzake wakimshangaa na minong’ono ya chini chini ikiendelea, “jamani hapakaliki hapa, twende tukamalizie kilabuni” wale wenye mioyo dhaifu, walianza kutawanyika, na wenye mioyo migumu waliamua kwanza kumalizia pombe iliyobakia ndipo waondoke zao.
Baada ya kugala gala kwa dakika kadhaa huku anapiga kelele za mayowe, mama Hilda akatulia ghafla, na kusimama, akawatazama watu waliokuwepo mwanzo wamejaa eneo wakinywa pombe, sasa aliwaona wachache wanaume wawili na wanawake watatu, ambao pia walikuwa wanamalizia ulanzi uliobakia, wengine walisha ondoka, hata mzee Njogopa na Nyoni na Ngonyani pia walishaondoka, “nime sema hawaniwezi, wanadhania sijajuwa walicho kifanya, dawa ya mchawi ni kumfanyia uchawi, lazima watakuwa wameenda kwa mganga ili kumuharibia mwanangu” alisema mama Hilda yaani mke wa mzee Komba kwa sauti ya hasira, iliyo maanisha kuwa anaamini alicho kisema……. ITAENDELEA
 
Wameisha ingiza uchawi sasa familia ya komba oatamu
 
Back
Top Bottom