SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI: Baada ya kughala ghala kwa dakika kadhaa huku anapiga kelele za mayowe, mama Hilda akatulia ghafla, na kusimama, akawatazama watu waliokuwepo mwanzo wamejaa eneo wakinywa pombe, sasa aliwaona wachache wanaume wawili na wanawake watatu, ambao pia walikuwa wanamalizia ulanzi uliobakia, wengine walishaondoka, hata mzee Njogopa na Nyoni na Ngonyani pia walisha ondoka, “nime lsema hawaniwezi, wanadhania sijajuwa walicho kifanya, dawa ya mchawi ni kumfanyia uchawi, lazima watakuwa wameenda kwa mganga ili kumuharibia mwanangu” alisema mama Hilda yaani mke wa mzee Komba kwa sauti ya hasira, iliyo maanisha kuwa anaamini alicho kisema……. ENDELEA NAYO

Sidhani kama kuna mtu alimsikiliza zaidi ya mwanae Hilda aliekuwa bado analia chini chini, “kweli mama, yaani yule mwana mama anaonekana ni mchawi kabisa, hata jana tulipoenda kule kwao, alikuwa ananitazama kwa jicho baya sana” alisema Hilda, kwa sauti iliyo ambatana na kiashilio cha kunyamaza kilio, hakuna mwingine aliewaunga mkono katika maongezi yao, zaidi ya kuendelea kunywa pombe ya mkopo ambayo kiukweli mpaka sasa mzee Komba uko chumbani kwake, alikuwa amekaa kwenye kingo ya kitanda chake ameinamisha kichwa, mikono shavuni, anajiuliza ata lipaje madumu kumi ya ulanzi, hakika hata ile aliyokunywa toka asubuhi alihisi inayeyula na kumletea kizungu zungu.
Mzee Komba, zaidi ya kuwaza deni la pombe, pia aliwaza mambo mengi sana, aliwaza jinsi alivyo waletea kashfa wakina Frank na mwenyekiti, aliwaza jinsi alivyojitangazia ufalme, na kueneza kashfa kwa familia ya mzee Frank, “yule kijana mshenzi sana, yaani amenitia aibu kiasi hiki” aliwaza kwa machungu mzee Komba. ******

Yap, maisha yakaendelea week ilikatika Higgno akiwa kule porini kwenye makazi mapya, makazi ambayo mzee Frank aliyaona kuwa yalikuwa yana faida kwake na kwa maendeleo ya familia nzima, maana Higgno alijituma na kufanya ubunifu mkubwa kule shambani, akiongeza kilimo cha mboga mboga na kupanda miti mingine ya matunda, huku kila jioni kijana huyu akifanya zoezi ya karate kwa juhudi kubwa.
kingine bwana Frank, aliona jinsi bwana Komba ambae amekuwa adui yake, jinsi alivyoishi kwa kujificha ficha kukwepa aibu, huku akitoa kipande cha shamba lake kulipia ulanzi alioukopa kwaajili ya kusherehekea mwanae kupatana na kijana mtoto wa tajiri, taarifa zilizoanza kusambaa ni kwamba mschana Hilda, yaani binti wa mzee Komba, sasa amepewa jina la TEMBELE LA UWANI kwa maana alikuwa chumba cha nadharia, kwav maana ya kwamba, mwanaume yoyote ambae angehitaji kujifundisha jambo lolote kwenye ngono, angeenda kujifunzia kwa Hilda, ambae hakuchagua mwanaume wala umri wa mwanaume ambae anaenda kumpa kitumbua, ilimradi angenunuliwa pombe au kupewa kete ya bangi, kilevi ambacho hata wazazi wake walikuwa wanajuwa kuwa binti yao alikuwa anakitumia, na kuzidi kuleta minong’ono kwa wananchi na wakazi wa Luhuila, ambao mwanzo walimuona Higgno ni mjinga na ndie anaefanya fitina ya kumkosanisha Hilda na Talib, na sasa walijuwa tabia halisi za binti huyu, ambae kwa jina la utani aliitwa TEMBELE LA UWANI,
Tembele la uwani ndiyo mboga ambayo hutumika kwa haraka na kuokoa wakati wa njaa na dhiki, bila kujari maji yanayotumika kumwagia na kustawisha mboga hiyo, ambayo mara nyingi, hukatizwa na kijifereji cha bafuni, mboga ambayo muda wowote unaweza kuichuma na kuitumia kwa uharaka pasipo usumbufu wakuitafuta au kuifuata mbali, japo haipewi heshima inayostaili.
Sifa hizo mpya za hilda, zilishamfikia hata Higgno aliekuwa shambani, ameshaanza kuzoea maisha ya huko shambani, japo siku moja ya juma tano week ya pili, baba yake alimtembelea Higgno kule shambani, “mwanangu kuna jambo nahitaji tuliongee” aliongea baba Higgy wakiwa wamekaa nje ya kibanda cha Higgno pale shambani, hapo kengele ya tahadhari ikagonga kichwani mwake, maana baba yake alionekana anajambo muhimu kweli kweli, “Higgno umekuwa kijana mkubwa sana, sawa sihitaji uoe kwasababu bado hujapata kazi ya kukusaidia, pengine una ndoto ya aina ya maisha unayohitaji kuishi, lakini inakuwaje sija kuona hata siku moja ukiwa hata na rafiki wakike ambae mnacheza cheza kidogo zaidi ya huyu mshenzi ambae sasa hivi wanamwita nani sijui, nae ulikataa kuwa haujawahi kushiriki nae tendo” aliongea bwana Frank, akishindwa kueleza moja kwa moja, na kumfanya higgno acheke kidogo, “baba unahaja ya kujiuliza sana, mimi nipo vizuri tu, lakini ukweli nimejikuta nikiwa busy na mzoezi, na mambo yangu, isitoshe baba toka Hilda aliponigeuka mara ya kwanza tukiwa form one, ukweli sijawahi kufikiria kama kuna mwanamke ambae atakuwa mkweli” alisema Higgno kwa sauti ya kujiamini, “kama swala ni hilo Higgno, basi niachie nikutafutie mschana ambae atakuwa rafiki yako na pengine baadae muoane, maana hivyo ndivyo walivyofanya wazee wetu hapo zamani” alishauri baba Higgno, yaani bwana Frank wakati wanamaongezi yao, “mh! sasa baba kama nisipo mpenda itakuwaje?” aliuliza Higgno, “kama hautompenda sawa tunatafuta mwingine, naimani atakuwa mzuri au kama kuna unaempenda sema tukaongee na wazazi wake, na pengine yeye mwenyewe” alisema mzee Frank, ambae licha ya kuongea vizuri na mwanae siku zote, lakini hakuwahi kuongea nae juu ya swala hili la mausiano.
Mwisho wa maongezi walikubaliana kuwa Higgno atafutiwe mwanamke ili awe rafiki yake kwa maana ya uchumba, na mwisho wa siku aje kuwa mke wake.*****
Siku ya moja, mida ya saa nne za asubuhi, mzee Mahmud, alikuwa ndani ya ofisi ya pale nyumbani kwake, yeye na mwanae Soraya, wakijiribu kupitia majina ya watu walioomba nafasi za kazi, ambazo, walizitangaza, kutokana na kuongeza magari mapya, ambayo ni mabasi makubwa ambayo walipanga kuyapa safari za mikoa ya mbali, kama vile dar es salaam , Dodoma, arusha na sehemu nyingine nchini, “naona atuta hangaika sana kupata madereva na mafundi wenye uzoefu, mfano huyu, aliwahi kufanya kazi kwa…” alisema baba Soraya, akitaja jina la kampuni mmoja ya zamani ya usafirishaji, “ni kweli hata mafundi naona wengi wametokea kwenye ule mradi wa barabara wa mtwara kolido” alisema Soraya, “ila kuna kama huyu hapa, yeye amemaliza chuo cha ufundi pale jimboni, wale jamaa wanafundisha vizuri sana, halafu wana nidhamu sana wanafunzi wa pale” alisema baba Soraya, huku wakizitenga barua kwa makundi, “hao wanafunzi usiwape kipaumbele sana wengine huwa wanategeaga kwenye masomo yao, bora hawa wenye uzoefu kwanza” alisema Soraya, huku akiichukuwa ile barua toka kwa baba yake na kuiweka pembeni, huku macho yake yakipita juu ya ile barua na kuona jina la Higgno Frank, “ila ni kweli, unajua wapo wanaochukuwa hata vyeti vya wenzao kwaajili ya kuombea kazi, hao tutawafanyia interview ya vitendo, endapo hawa hawatatoshea” alisisitiza baba Soraya yaani tajiri mwarabu, Mahmud.
Naam wakati wanaendelea kuchambua barua na majina, ni kama kuna kitu Mahmud alikumbuka, “hivi Talib yupo wapi?” aliuliza bwana Mahamud, “mh! sijuwi labda chumbani kwake, alijibu Soraya, hapo kikapita kimya kifupi, huku wanaendelea kusoma maelezo ya waombaji wa kazi, kabla Mahamud hajaongea tena, “nafirikiria kumpatia nafasi ya usimamizi wa mabasi ya zamani, yale ambayo tutayaondoa kwenye safari za mbali, tuyapeleke safari za karibu kama mbinga, njombe masasi, newala na tunduru” alisema bwana Mahamud, “ni vizuri ukimpa nafasi hiyo, lakini ulishawahi kumchunguza kama anafaa kusimamia hayo magari?” aliuliza Soraya, akiwa anafahamu baadhi ya maovu ya binamu yake, hapo baba yake alitulia kidogo, kama anawaza jambo, kabla hajamtazam mwanae, “kwanini unauliza hivyo Soraya, inamaana bado unamashaka na binamu yako?” aliuliza baba yake, yaani mzee Mahamud kwa sauti ya mashaka, “kwani baba wewe unaweza kumjaji mtu kwa kumtazama tu! mi naona kabla hujampa hiyo kazi, jaribu kwanza kumchunguza” alisema Soraya, na wakati huo mlango wa chumba cha ofisi iliyopo hapo nyumbani kwao ukagongwa na alieenda kufungua mlango alikuwa ni Soraya, “asalam aleykum” alisalimia Soraya kwa sauti iliyojaa heshima na adabu, na kumfanya baba yake atazame mlangoni, kuona mtu aliesalimiwa, akawaona watu wawili na sio mmoja wakiingia mule ofisini, “aleykum salaam” alikuwa ni mzee wa makamo mwenye asili ya kiafrika halisi, maana hakuchanganya rangi hata kidogo, alieongozana na kijana mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na saba, mpaka ishirini na tisa, wote wawili wakiwa wamevalia kanzu yeupe na baragashia zao vichwani mwao, “asalam aleykum” alisalimia tena Soraya kwa yule kijana ambae walikutanisha macho yao, na yule kijana akaitikia huku anaachia tabasamu pana, “aleykum salam”, Soraya akashindwa kumtazama kijana huyu usoni, na kujikuta akitazama chini, huku kikimponyoka kitabasamu cha aibu.
Naam wale wageni walipita ndani, “karibu bwana Mahadhi bin Salum, toka nirudi dar salaam atujaonana” alisema bwana Mahamud, akionyesha kuwa, alikuwa anamfahamu vyema huyu mzee mwenzie, ambae hata kwa umri ni kama walikuwa wanalingana na bwana Mahamud, “asante bwana Mahamud, tulipishana kidogo, nilisafiri kwenda mtwara kupokea mizigo toka South afrika, huyu kijana wangu alituma kwenye meli” alisema yule mzee Mahadhi Salum, huku akimuonyeshea yule kijana aliekuja nae, ambao sasa walikuwa wanakaa kwenye viti vya mule ndani ya ofisi ya nyumbani, Soraya akimtazama kijana huyu mtanashati akijaribu kumtathimini kama angefaa kuwa mume wake, hakujiuliza kama atakuwa ameshaoa au laa, “kwani huyu ni nani?” aliuliza Mahamud, huku akimtazama yule kijana, ambae kwa muonekano alikuwa ni kijana mtanashati, mwenye harufu ya maisha mazuri, ung’aavu wa ngozi yake na muonekano wa sura yake, viliashiria kuwa, alikuwa ni kijana mwenye mafanikio, kama sio kutoka kwenye familia yenye mafanikio, “huyu ni Idd, yule kijana wangu wa pili” alisema mzee Mahadhi, kwa sauti ya kujipata na kujigamba, “hooo Idd, aliadimika sana miaka ya hivi karibu” alisema mzee Mahamud, akionyesha anamkumbuka kijana huyu, ambae binti yake, licha ya kumuona kuwa ni kijana mwenye sifa za wazi, ambazo yeye anazihitaji, lakini pia alihitaji kujuwa sifa za kijana huyu za ndani, “alikuwa south afrika, amerudi siku tatu zilizopita, hivyo akaniambia twende kwa mzee Mahamud, nikamsalimie” alisema mzee Mahadhi Salum, kwa sauti ya kujinasib, huku Idd mwenyewe mara kwa mara akitabasamu, na kujichekelesha, huku akimtazama Soraya kwa macho ya kuibia, hata yalipo kutana macho yao, walitabasamiana na Soraya kutazama chini kwa aibu.
Sio kwamba wawili hawa hawafahamiani, wana fahamiana toka miaka mingi nyuma, walikuwa wanakutana mara kwa mara msikitini hasa siku za ijumaa kipindi kile wanasoma, walikuwa wana salimiana vizuri na kuoemeshana mawili matatu, hata akitokea Soraya akawa amevaa ile nikab ya kujiziba mdomo na pua, basi yeye mwenyewe ange muita na kumsalimia Idd, lakini walikosana mara baada ya Idd, kujaribu bahati yake kwa kuomba penzi la Soraya ambae hakumjadili hata mara moja, alimkatalia bila kumzungusha, na huo ndio ulikuwa mwisho wa ukaribu wao, japo wazazi wao walikuwa wanafahamiana vizuri, na marafiki, hawakuweza kuona wala kuwa karibu mpaka leo wakina Idd na baba yake walivyo kuja ofisini kwa akina Soraya, ikiwa imepita miaka zaidi ya mitano.
Mzee Mahadhi, licha ya kuwa mmoja kati ya wazee wa baraza la dini hapa mkoani Ruvuma, lakini pia, mzee huyu mwenye asili ya visiwani Zanzibar unguja mjini magharibi, kitongoji cha Mombasa, alikuwa anajihusisha na biashara ya nguo, kama vile kanzu mabaibui, baraghashia, magauni mazuri ya heshima, na nguo nyinginezo, za kawaida kwa wanaume na wanawake, “ok! karibu bwana Idd, naona umekuwa kijana sasa, vipi umeshaoa huko south afrika?” aliuliza mzee Mahamud kwa namna ya utani, Idd na baba yake wakatazamana na kucheka, huku Soraya, akimkata jicho baba yake akiamini kitachofuata ni kuzungumzia mambo ya kuoa na kuolewa tu! “aowe wapi, amesema anakuja kuolea nyumbani” aliwahi kujibu Mahadhi mwenyewe, ni jambo la kheri kuoa nyumbani, japo haijakatazwa kuolea mbali” alisema Mahamud.
Naam yalipita maongezi mawili matatu, kabla ya mzee Mahadhi salum hajaomba faragha kidogo na mzee Mahamud, “haina shida twende sebuleni, basi, tuwaache hawa huku ofisini” alisema Mahamud, nao wakatoka mule ofisini na kuwaacha Soraya na Idd mule ofisini, “niambie Soraya, unanikumbuka lakini?” aliuliza Idd mara tu baada ya wazazi wao kutoka mule ofisini, huku akimtazama Soraya usoni, na kama ujuavyo msomaji, Soraya licha ya kuwa mrembo pia ni mzuri wa sura na mwili, maana kila alivyozidi kukuwa ndivyo alivyo zidi kuwa na umbo matata, “nakukumbuka sana” alijibu Soraya huku ana jitahidi kukwepesha macho yake yasitazamane na macho ya Idd, “unanikumbuka kwa lipi Soraya?” aliuliza tena Idd kwa sauti nzito na tulivu, tofauti na mwanzo, “nikukumbuke kwa lipi kaka Idd?” aliuliza Soraya, huku ana jaribu kumtazama Idd usoni, akamuona anajilamba midomo huku amelegeza macho, “kwa lile ulilo nifanyia, najua ulikuwa ni utoto tu, lakini sasa umeshakuwa mkubwa” alisema Idd, kwa sauti ile ile nzito ya makusudi huku anaendelea kujiramba midomo yake, na macho yake kulegeza akiwa ameyaelekeza kwa Soraya ambae aliyakwepesha ya kwake, “we unakumbuka mambo ya zamani, kwani wewe ulikuwa mkubwa?” aliuliza Soraya huku akiwa anaanza kupekuwa pekuwa barua zilizopo mezani, “yah! kwani unaona nilikuwa mdogo?” aliuliza Idd, kwa sauti ile nzito iliyojaa majivuno, “hongera yako” alisema Soraya, huku akizidi kutawaliwa na aibu, maana alishindwa kukabiliana na mtu ambae anaonyesha wazi matamanio juu yake, “hongera ya nini Soraya, mbona vitu vya kwawaida tu!” alisema Idd kwa sauti ya kurahisisha, “wewe ndio unaona kawaida, lakini mwenzio… mh!” alisema Soraya huku anaichukuwa barua ya Higgno na sijuwi kwa kuchangachikiwa na maongezi akajikuta anaiweka kwenye kundi la barua za kundi la kwanza zilizopewa kipaumbele.
Naam wakati huo huo huku sebuleni kulikuwa na maongezi ambayo Soraya kama ange yasikia hakika, sijuwi kama angekubaliana nayo, “ndiyo hivyo bwana Mahamud, kijana wangu akasema hapana hawezi kuoa mwanamke yoyote sehemu yoyote, wakati kuna mschana mwenye kujiheshimu, alielelewa akaleleka na mschana mwenyewe ni mwanao Soraya, na ukiangalia watoto umri ndio unaenda hivyo” alisema bwana Mahadhi, kwa sauti ya chini iliyojaa msisitizo, muda huu mama Soraya alikuwa ameenda mjini, kuangalia vitu vya jikoni na wafanyakazi wake wawili, “hilo jambo kwa kweli hata mimi lina niumiza kichwa bwana Mahadhi, natamani sana binti yangu aolewe na mimi nipate mjukuu, lakini tatizo huyu Soraya, amekuwa mchaguzi sana wa wanaume, mapaka sasa anasema bado hajamuona mwanaume ambae atafaa kuwa mume wake, wote ni kama wana tamaa” alisema Mahamud kwa suti ya chini pia, “unajua kwanini Mahamud, ni kwasababu hajapata nafasi ya kuchunguza mwanaume wa kumfaa, naimani tukiwaweka karibu, basi watazoeana na kuchunguzana, ujuwe ndoa za sasa hivi, uanza na urafiki” alisema Mahadhi, kwa sauti ile ile ya chini, “sasa tutawawekaje karibu?” aliuliza Mahamud, kwa sauti ile ya chini, ungesema kuna mtu hawataki asikie, “hilo ni jambo rahisi, hebu niachie mimi nikupe mbinu, lazima tujitahidi kuwa tuna waweka karibu mara kwa mara na njia rahisi ni kuwa tuna watuma kwa pamoja mara kwa mara, mpaka watajikuta wanaingia kwenye urafiki ambao utasababisha ndoa” alisema Mahadhi, na wakaanza kupanga jaribio la kwanza, kabla ya kuagana na kuondoka zao********

Upande wa pili, kijana Talib, hakuwa tena na mtaji wa biashara, sio mtaji tu, hakuwa hata na fedha yoyote, kiasi cha kushindwa kuweka mafuta kwenye gari alilokuwa anatumia, yaani Hyundai, na kumlazimu kutembea kwa miguu kwenye baadhi ya matembezi yake, au kutumia daladala, kwenye matembezi ya mbali kama vile mwembe chai kwa bwana Zido na Vitus, ambako alilazimika kwenda kwaajili ya kufuata bangi na kupanga mipango ya kumteka Soraya ili wajipatie fedha nyingi, japo yeye alikuwa anawashauri wenzake kuwa, itafaa endapo watamuuwa kabisa, na yeye Talib kujinyakulia nafasi ya binti huyu wa pekee katika familia ile na kuwa msimamizi wa biashara ya mzee Mahamud.
“tunaweza kufanya hivyo, lakini wacha kwanza tuchukuwe mkwanja wa haraka, kisha tumuuwe, maana itasaidia pia kutunza siri, anaweza kututambua halafu ikawa shida” alisema Zido, siku tatu kabla ya tukio, “na nikifanikiwa kukamata nafasi hiyo, kwanza kila mmoja atatupiwa gari moja la maana, halaf nawakabidhi vitengo kwenye kampuni” moja ya ahadi ambayo Talib aliitoa kwa wenzake.*****

Naam zilipita siku tatu, juma moss moja, Soraya akiwa chumbani kwake akijaribu kutazama filamu moja ya kihindi, ambayo kiukweli ni kama hakuwa anaifuatilia, maana ukweli ni kwamba, maongezi ya siku ile usiku akiwa na baba yake na mama yake wanakula, ni kama yali mtonesha mschana huyu, ambae kila alipokumbuka maneno ya baba yake kuwa, endapo angempata kijana yule aliemsaidia kumuokoa mikononi mwa wanyang’anyi, ambae yeye alimfananisha kitabia na yule kijana mpole, alitamani sana ile bahati ingemkuta kijana mpole aliemsaidia sibakwe, “sijuwi kwanini niliondoa gari haraka siku ile, pengine angekuwa rafiki yangu” aliwaza Soraya, ambae hata yeye hakujuwa ni kwanini anawaza sana juu ya kijana ambae ametokea kumpenda na kuamini kuwa anafaa kuwa mume wake, “sijuwi nawaza nini mimi mtu sijamuona miaka na miaka, halafu hata hanijuwi na mimi simjuwi” alijisemea Soraya ambae aliona kama anawaza jambo ambalo lisinge wezekana, hivyo akaamua kulipotezeana kuwaza kuhusu miche ya matunda, ambayo ilibidi kesho kutwa akaichukuwe kule Seed farm ya Lumecha, ili ijumaa waipeleke kule shambani ikapandwe, lakini licha ya kujitahidi kupotezea bado akajikuta anavuta taswira ya sura ya kijana mpole, ambae kila alipomkumbuka aliona kama amekosa kitu muhimu sana, utazani alishawahi kuwa mpenzi wake na wakapotezana ghafla, kumbe ni watu ambao hawakuwahi kuongea hata kufahamiana majina, “sijuwi nikimuona atakuwa na mke tayari?” alijiuliza Soraya ambae ni kama alikuwa anaamini kuwa ipo siku atamuona yule kijana mpole.
Wakati Soraya anaendelea kupambana na mawazo juu ya kijana mpole, mara akasikia mlango wa chumba chake unagongwa, “ingia” alisema Soraya huku akijiweka vizuri na mlango ukafunguliwa akaingia mama yake, “mwanangu, na wewe kwa kutazama filamu, hebu jiandae anakuja rafiki yako Idd, baba yako anataka awatume sehemu” alisema mama Soraya, kwa sauti ya furaha na ucheshi, huku anatabasamu, “Idd?” aliuliza Soraya ka mshangao, “unashangaa nini mwanangu, nenda katembee saa kumi na mbili uwahi nyumbani” alisema mama Soraya, kwa sauti ya kubebembeleza na kumfanya Soraya akubaliane na mama yake.... Haya sasa soraya anawekwa karibu na idd ambae sio chaguo lake, ila lengo la wazazi wawe karibu wazoeane kisha ndoa, nini kitajiriiiii? Atakutana na kijana mpoleeee au ndio anaenda kuolewa na idd? Vip kuhusu talibu na mipango yake? Vip mama hilda na safari yake ya kwenda kwa mganga? Basi usiache Kufuatilia mkasa huu hapa hapa jamii forums.
 
Mbna kafupi mnoo 🤣😂🤣😂😂🔥🔥🔥🔥
 
Idd atapigwa Kibiti mtoto moyo uko kwa Higgy
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA: Wakati Soraya anaendelea kupambana na mawazo juu ya kijana mpole, mara akasikia mlango wa chumba chake una gongwa, “ingia” alisema Soraya huku akijiweka vizuri, na mlango ukafunguliwa akaingia mama yake, “mwanangu, na wewe kwa kutazama filamu, hebu jiandae anakuja rafiki yako Idd, baba yako anataka awatume sehemu” alisema mama Soraya kwa sauti ya furaha na ucheshi, huku anatabasamu, “Idd?” aliuliza Soraya kwa mshangao, “unashangaa nini mwanangu, nenda katembee saa kumi na mbili uwahi nyumbani” alisema mama Soraya kwa sauti ya kubembeleza na kumfanya Soraya akubaliane na mama yake…….. ENDELEA

Japo ilkuwa kiroho bwana shingo upande, maana Soraya alishamtilia mashaka kijana Idd toka kipindi kile alipo jaribu kumtongoza wakiwa wanasoma, na hata utazamaji wake wa kulambalamba midomo na kulegeza macho nao ulimfanya amtilie mashaka kijana huyu.*******

Upande wa pili nako, mara bada ya mzee Frank kukubaliana na mwanae Higgno kuwa anatakiwa kutafutiwa mschana ambae ata jenga nae urafiki kisha kuingia kwenye mahusiano, alienda kwa mke wake na kumueleza jambo hilo, ambae hakupinga, ila walikubaliana kuwa swala hilo wamueleze dada wa bwana Frank anae kaa bomba mbili, wakiamini atawasaidia kumpata mschana mzuri na mwema, anaefaa kuwa mke wa Higgno, hivyo bwana Frank akampigia simu dada yake huyu, akimueleza anatarajia kwenda kwake mchana wa siku hiyo, kuwa ana jambo muhimu la kujadiliana nae.*******

Idd Mahadhi Salum, akiwa amekaa sebuleni kwa mzeee Mahamud peke yake anamsubiri Soraya, alianza kukumbuka maisha yake ya miaka sita iliyopita, ambayo mara baada ya kumaliza shule, aliondoka nyumbani kwao kwa kutoroka akiwa na vijana wenzake wanne walielekea afrika ya kusini, ikiwa ni kwenda kutafuta maisha kama walivyo shauriana na wale wenzake, wote wakiwa ni watoto toka kwenye familia bora lakini waliokosa nidhamu.
Walifanikiwa kutoroka wakipitia msumbiji ambapo hawakufanikiwa kufika south afrika kama walivyo panga na kuishia msumbiji katika mji wa nampula baada ya kushiwa fedha, hivyo wakaanza kuishi pale Nampula wakiwa wameshindwa kurudi nyumbani wala kuendelea na safari, wakilazimika kuanza kubangaiza nakuishi maisha duni, wakati mwingine wakilazimika kuiba au kutapeli ili kujipatia mkate wao wa kila siku.
Idd na wenzake waliishi kwa mtindo huo wa udokozi na utapeli kwa mika mitatu, kila walicho kipata walikitumia kwa starehe ya pombe na wanawake, wakimini kesho wataiba tena na kuendelea kustarehe, huku mara kwa mara wakinusulika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali, tabia ambayo iliwasababishia watanzania wenzao kuto kuaminika kabisa ndani ya mji ule wa Nampula, maana ilifikia kipindi mtanzania hata ukifika polisi umeibiwa wewe kesi inakugeukia na kuonekana kuwa wewe ndie mwizi, yote ni kwasababu ya utapeli wa akina Idd na wenzake watatu.
Kama walivysema wahenga kuwa za mwizi ni arobaini, sijui hiyo arobaini ilikuwa ni siku week au miezi, lakini arobaini ikifika lazima utalipia ulivyo viiba, siku moja wakina Idd wakiwa katika harakati zao za wizi wakashtukiwa na kuandamwa vibaya sana na wanachi wenye hasira kali kama wanavyoitwa, kila mmoja alijaribu kujiokoa kwa namna yake, lakini kila walikokimbilia tayari walisha zungukwa, nao wakajitahidi kujipapatua lakini hali ikazidi kuwa mbaya, wakaanza kukamatwa mmoja baada ya mwingine, na kila aliekamatwa alizingirwa na kundi la wananchi kisha kushushiwa kipigo na kupoteza maisha.
Mpaka dakika za mwisho Idd alipoona kuwa amebakia peke yake na kundi la watu linamfuata akaamua ajisalimishe kwenye kituo cha polisi, na bahati nzuri wananchi walitii sheria kwa kuwaheshimu polisi.
Idd akiwa pale polisi ambapo aliishi maisha ya shida ya kukosa chakula na manyanyaso makubwa, mara akakutana na mtanzania mwingine mule ndani, waliongea mengi sana, wakitambulishana sehemu wanazo toka kule tanzania na kazi walizo kuwa wanazifanya huku ugenini, “achana na inshu za kizembe dogo ngoja boss wangu aje kunitoa nitamueleza kuhusu wewe, nadhani utapata dili za maana” alisema yule jamaa ambae hakukaa sana alikuja kutolewa na huyu boss wake ambae pia ni mtanzania.
Siku iliyofuata Idd akiwa ana waza atatokaje mule ndani ambamo hakuonja chakula kwa siku mbili nzima, huku akipania kuwa akitoka arudi tanzania hata kwa mguu, lakini bahati ikawa upande wake pia, maana nae alitolewa japo hakuwa na uhakika kama aliemtoa ni huyo boss wa yule jamaa au laa, lakini akiwa nje ya kituo cha polisi akamuona yule jamaa aliekuwa nae mahabusu akimfuata na kumuongoza kwenye gari moja la kifahari, na alipoingia ndani akakutana na jamaa mmoja mtu mzima hivi, mwenye muonekano wa kiboss kweli kweli.
Idd alifikishwa kwenye jumba moja kubwa la kifahari na kupewa huduma zote ambazo hata kwao hakuwahi kuzipata, japo baba yake alikuwa na kiuwezo kidogo, na baada ya kupumzishwa kwa siku mbili akila na kunywa vizuri, akaelezwa majukumu yake mapya, ambayo yalikuwa ni kutembeza dawa za kulevya akiongozana na yule mwenzie alitoka nae mahabusu,
Kazi ya kutawanya madawa ya kulevya kwenye kumbi mbali mbali za starehe, ilikuwa rahisi sana kwa kijana Idd, ambae aliifanya kwa juhudi akiamini kuwa hiyo ndiyo njia ya yeye kutimiza ndoto zake za kuelekea afrika ya kusini, ndoto ambayo aliitimiza mwaka mmoja baadae, baada ya kuanza kutumwa kwenda huko afrika ya kusini kubeba dawa haramu za kulevya na kuzipeleka msumbiji.
Maisha ya pombe na wanawake kwa kijana huyu yaliendelea na kushamili mara dufu zaidi ya ilivyo kuwa kipindi kile akiwa mwizi na tapeli, maisha ambayo yalimsahaulisha kama kuna kurudi tena Songea tanzania, zaidi ya kupiga simu kwa baba na mama yake akiwaeleza kuwa yupo afrika ya kusini anaendelea vizuri na anafanya biashara halali kabisa, na wazazi wao kuamini hivyo.
“Ndege wa porini hafugwi” huo ni msemo mwingine wa wahenga, kwa maana ipo siku atarudi kwao porini, na ndivyo ilivyo kuwa kwa Idd Mahadhi, ambae alilazimika kutoroka msumbiji na kukimbilia afrika ya kusini ambako hakukaa sana akarudi tanzania, ni baada ya kutokea ugomvi mkubwa kati ya kundi lao na kundi la jamaa moja, ambae pia alikuwa anajihusisha na uuzaji wa dawa hizo za kulevya, vilitokea vifo vingi sana, na kati ya walio uwawa ni boss wake Idd, na hapo Idd akabahatika kutoroka na kiasi fulani cha fedha, ambacho alitumia kununua nguo chache kwaajili ya biashara ya baba yake.
Sasa basi alipofika tanzania, aliwakuta vijana wenzake wengi wao wakiwa ni wenye mafanikio kuliko yeye ambae amekaa nchi za mbali akiponda starehe na kurudi tanzania akiwa mng’aavu wa ngozi na uzuri wa sura, hivyo ikamlazimu awaze jambo la kufanya, wakati huo huo akasikia habari ya kuwa mzee Mahamud, ameingiza magari mengi sana mjini songea, hapo akapata wazo moja zuri ambalo litamfanya aishi maisha mazuri, nalo ni kumshawishi baba yake kumsogeza karibu na Soraya, ili afunge nae ndoa na kuwa mmoja wa watu wanaostahili kutumia mali za mzee Mahamud, akichukulia kigezo cha kuwa baba yake ni mtu maarufu na kiongozi wa dini, lazima bwana Mahamud angekubaliana nae tu!
Ni kweli mtego wake ulienda kama alivyo panga, maana mpaka sasa alishafika nyumbani kwa kina Soraya, na alikuwa amekaa sebuleni anamsubiri mschana huyu atoke chumbani kwake waende kutembea, kwa lengo la wawili hawa wajenge urafiki ambao utawapelekea ndoa.
Akiwa katika kumbu kumbu nzito, kijana Idd mara pua zake zika sikia harufu kali ya marashi, sambamba na sauti ya visigino vya viatu vilivyo kuwa vinalizwa kutokea upande wakorido la vyumbani, nae akageuka kutazama, akajikuta akikodoa macho kwa mshangao akimtazama mschana mrembo mwenye kuvalia gauni refu zuri jeusi lenye hariri za dhahabu kwenye pindo zake, huku akijidundika vipuli vya dhahabu sehemu mbali mbali za mwili wake, “assalam alaykum” ilikuwa ni sauti nyororo ya kuvutia ya mschana Soraya, ambae leo hii alizidi kupendeza na kuwa mzuri usoni kwa Idd, “waalaykum salam” aliitikia Idd, ambae hakuona sababu ya kuendelea kukaa pale ndani kwa kina Soraya, “tunaweza kuondoka sasa?” aliuliza Idd huku akimkodolea macho Soraya, “uagi kwa mama?” aliuliza Soraya kwa maana ya kumkumbusha kijana huyu alieshikwa na bumbuwazi la matamanio, “ni kweli nilitaka kusahau” alisema Idd mfano wa mtu aliezinduka toka usingizini.
Soraya alimuita mama yake nae akaja, na Idd akaaga, kisha wakatoka nje na kuingia kwenye gari aina ya Toyota Cherser, gari pekee la mzee Mahadhi, “kaka Idd kwani tunaenda wapi, maana mimi saa kumi na mbili nataka niwe nyumbani, kwaajili swala” alisema Soraya huku anajifunga niqab yake usoni kuzuwia pua na mdomo wake visionekane, ni kawaida yake kufanya hivyo anapokuwa anaenda sehemu ambayo itamlazimu kushuka toka kwenye gari, “mbona muda mwingi sana, tutaenda bomba mbili nilikotumwa halafu tuna rudi zetu” alijibu Idd ambae kichwani mwake alishapanga kukaa sehemu na kuongea mengi na mschana huyu katika kumjengea uaminifu kwake.******

Mchana wa siku hiyo pia Frank aliondoka nyumbani kwake Luhila, akaelekea bomba mbili akitumia usafiri wake wa baiskeri, ambao amekuwa akiutumia kwa miaka yote, lengo lake likiwa ni kwenda kumuona mdogo wake wakike, alitumia lisaa limoja kufika bomba mbili, yaani nyumbani kwa mdogo wake wakike ambae amezoea kumuita dada, wakakaa chini na bwana Frank akamueleza shida yake, “kaka wala usiwe na wasi wasi kaka, kuna mschana mzuri tu! mtoto wa rafiki yangu, anafaa kabisa” alisema shangazi yake Higgno, “tena ungenieleza mapema, ungemkuta ili umuone kabisa” alisema shangazi, “sio mimi nimuone Higgno ndie anaetakiwa kumuona” alisema baba Higgno yaani mzee Frank, akionekana kujawa na furaha kubwa kwa kufanikiwa kwa haraka swala lake, ambalo aliamini sio tu kuleta heshima kwa kijana wake, pia linge mfanya hata mschana Hilda na familia yake wasipate nafasi ya kuwa karibu na Higgno, “wala usiwe na wasi wasi, nikisha ongea na mama yake nitakujulisha kinachoendelea” alisema shangazi, na hapo wakaanza kuongea mengi, hasa yanayohusu matukio na vituko, vilivyo tokea siku za hivi karibu nyumbani kwao.******
Idd na Soraya walienda moja kwa moja mpaka bomba mbili, huku njiani wakiongea hili na lile, ilimradi wasikae kimya, lakini mara kwa mara macho yao yalikutana kutokana na Idd kuwa anamtazama sana binti huyu, tena kwa macho ya matamanio ya wazi kabisa, wakati mwingine aliweza kumuona Idd akitazama pembeni kuwashangaa wanawake waliokuwa wanawapita, hasa wale wenye makalio makubwa, na walipofika bomba mbili walisimamisha gari nje ya nyumba moja kubwa sana ya kifahari, “nisubiri kidogo, nakuja sasa hivi” alisema Idd kisha akashuka toka kwenye gari na kuingia ndani ya ile nyumba akimuacha Soraya ana mtafakari, “mh! kaka Idd anaonekana ananitamani” aliwaza Soraya, “lakini baba na mama wanaonekana kama wana shadadia mimi kuwa na Idd” aliwaza tena Soraya ambae hakuona umuhimu wa yeye kuja huku, “halafu anaonekana anapenda sana wanawake wenye makalio makubwa” aliwaza Soraya na wakati huo huo, ikamjia kumbu kumbu ya kijana mpole, “sijui na yeye huko aliko atakuwa kama Idd?” alijiuliza Soraya, ambae siku zote kiu yake ilikuwa ni kukutana na kijana yule mpole hata kama atakuwa ameshaoa, kiu yake itaisha pale atakapomuona.
Wakati Soraya anaendelea kuwaza hayo mara akamuona Idd anatoka peke yake na kuingia kwenye gari, “amesema tuje kesho kutwa” alisema Idd huku anakaa kwenye seat ya dereva na kuondoa gari, “kwani ulitumwa nini?” aliuliza Soraya, huku gari likitembea taratibu kueleka barabara kuu, “nilipewa hela nilete, sasa sijui za nini” alisema Idd, ambae alikuwa anajuwa fika kuwa ulikuwa ni uongo mtupu, “ok! sasa ndio tuna rudi nyumbani?” aliuliza Soraya, “ndiyo lakini nilikuwa nawaza tutafute sehemu tule kachori na samaki wa kubanika” alisema Idd akijaribu kumtajia vitu ambavyo mschana huyu angevipenda, “hapo sawa twende zetu” alisema Soraya kwa furaha,
Na ikawa hivyo, walienda sehemu moja inafahamika kama kwa mkojani, ambako palikuwa panauzwa vitu vingi vidogo vidogo vya kula, kuanzia urojo, pweza chips kachori, vileja, na vingine vingi vinavyo patikana Zanzibar, hakika Soraya alionekana kupendezewa na mazingira yale na vyakula vya pale ukizingatia kuwa hakuwa mlaji wa chakula cha nje ya nyumbani kwao.******

Mida ya saa kumi na mbili kasoro, ndio mida ambayo bwnaa Frank aliaga kwa dada yake na kuondoka zake, akimuacha dada yake anapiga simu kwa huyo rafiki yake, “hallow best nina habari njema wangu, sijui utanipa nini?” alisema shangazi mara baada ya simu ile kupokelewa upande wapili, “chochote kinachoendana na habari hiyo njema” alisikika mwana mama upande wapili, “mama jiandae kwa kupokea posa, nakuletea mkwe wa kumuoa Joan” alisema shangazi kwa sauti iliyojaa shauku, kwanza ulisikika mguno toka upande wa pili, “mh! Joan yupi, huyu huyu wa kwangu?” aliuliza huyo mama kwa sauti ya kuto kuamini....... ITAENDELEA..

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA ISHIRINI MBILI: Mida ya saa kumi na mbili kasoro, ndio mida ambayo bwana Frank aliaga kwa dada yake na kuondoka zake, akimuacha dada yake anapiga simu kwa huyo rafiki yake, “hallow best nina habari njema wangu, sijuwi utanipa nini?” alisema shangazi mara baada ya simu ile kupokelewa upande wapili, “chochote kinacho endana na habari hiyo njema” alisikika mwana mama upande wapili, “mama jiandae kwa kupokea posa, nakuletea mkwe wa kumuoa Joan” alisema shangazi kwa sauti iliyojaa shauku, kwanza ulisikika mguno toka upande wa pili, “mh! Joan yupi, huyu huyu wa kwangu?” aliuliza huyo mama kwa sauti ya kutokuamini... ENDELEA NAYO SASA

“Kumbe je ni Joan wako huyo huyo, mwingine copy” alisema Shangazi na kuzidi kumshangaza mama Joan, ambae sijui kwanini alishanga kiasi kile.********
Japo swala hilo lilimpa moyo bwana Frank na kuona kuwa mwanae ataondokana na tatizo la kuingia kwenye aibu za mara kwa mara juu ya Hilda, lakini kiukweli bado kuna jambo lilimchangakidogo, “kwahiyo huyu mtoto ameshindwa kabisa kutafuta mwanamke yeye mwenyewe mpaka mimi niingilie kati?” alijiuliza bwana Frank akiwa maeneo ya mabanda mawili anateremka taratibu, akifuata barabara ndogo pembeni mwa barabara kuu ya kwenda Iringa, “sasa ndio tuna mpata huyu mwanamke halafu analeta kisingizio, kwa kweli sitomuelewa” aliendelea kuwaza bwana Frank, ambae mita chache alikuwa anaendelea kutembea kuelekea darajani.*****

Wakati huo huo, kule kwa mkojani, Idd alizidi kuiteka akili ya Soraya, kwa kumpeleka sehemu ambayo kiukweli ilimpendeza sana, waliendelea kununua vijidubwana na kuvila pale pale bila kuona aibu wala kujiuliza, wala Soraya hakuangalia hadhi yake, alifunua kidogo kitambaa chake cha niqab na kudumbukiza kachori, kisha kurudisha kitambaa, hakujali macho ya watu waliokuwa wanamshangaa, japo hawakufanikiwa kuiona sura yake, lakini walionekana kumshangaa sana,”vipi ume papenda hapa?” aliuliza Idd, wakiwa wamesimama nje ya gari lao, “mhhh! nimepapenda kwa kweli ni pazuri, pana nikumbusha forodhani kule Zanzibar, “yah! ni pazuri sana hapa, hasa ukija na mpenzi wako, tutakuja tena kesho kutwa tutapoenda kuchukuwa huo mzigo” alichokoza Idd pasipo kujuwa madhara au faida ya uchokozi huo, hapo ni kama alikuwa anamkumbusha jambo Soraya, “hivi kaka Idd, kwanini hujaoa mpaka sasa?” aliuliza Soraya na kumfanya Idd atabasamu, kwanza alianza kwa kubetua midomo, “haa unajua nini Soraya, wanawake wengi wanafuata mshimko, halafu sio type yangu, si unajua eeh!, lazima uwe na mwanamke ambae ukipitanae sehemu kila mtu anasema kweli yule ni mwanamke” maneno ya Idd yaliyojaa nyodo na kuambatana na sauti ya kubeza yalimfanya Soraya atabasamu, “kwahiyo umeshampata Wifi mwenye sifa unazo zitaka?” aliuliza Soraya, akijaribu kumtazama Idd usoni, akamuona anamkazia macho nae akakwepesha yake, “bado, sijampata, mi nataka nimpate mwanamke wa maana ambae nitamtunza kama mboni ya jicho langu” alisema Idd na kumfanya tena Soraya acheke chini chini, “basi huyo wifi yangu siku ukimpata atakuwa kiboko” alisema Soraya huku anaendelea kula kachori katika uso wa tabasamu, “unaweza hata ukawa wewe, si bado hujaolewa?” aliuliza Idd, akitaka kuufanya kuwa huo ndio uwe mwanzo wa kutupa ndoano zake, kwanza alishangaa kuona Soraya akitabasamu, “umechelewa mwenzio kuna mvulana nimesha pendana nae toka wakati ule wa shule” ilikuwa ni kauli ya kipuuzi na kizemmbe toka kwa Soraya, nasema ya kipuuzi kwasababu ni mambo ya kufikirika ambayo Soraya alijikuta ameropoka tu, lakini kauli hii ilimshtua sana Idd, ambae alijihisi kama yupo ndotoni, ghafla kikatawala kimya cha ajabu,
Kimya ambacho kiliambatana na unyonge wa wazi kabisa usoni kwa Idd na kumfanya Soraya ajuwe wazi kuwa jibu lake lilibadili hali ya Idd, “kaka Idd, naona kama umepachoka hapa, kama vipi turudi nyumbani” alishauri Soraya, “poa” alijibu Idd kwa kifupi, huku anaingia kwenye gari, na Soraya nae akaingia kwenye gari kisha safari ikaanza kimya kimya, huku Idd akiwaza kuwa “ni boya gani huyo anaekamua huyu demu, mi nilijuaga bado hajaguswa” aliwaza Idd, huku akiingia barabara kuu, hakujuwa kama mwenzie pia alikuwa anawaza ya kwake, “kumbe kujishauwa kote kule ulikuwa na yako”alijiwazia Soraya, huku safari inaendelea kwa speed, “lazima nimjuwe huyo boya, nitamuulizia Laylah, lazima atakuwa anamjuwa huyo fala, nitakachomfanya yeye mwenyewe atakijuwa” aliwaza Idd huku anaendesha gari kwa speed kama vile amechanganyikiwa, akikatiza eneo la daraja la bomba mbili, kitendo ambacho kilichangia Idd asimuone mzee mmoja mwendesha baiskeri aliekuwa anaingia barabara kuu, akitokea kwenye barabara ya pembeni, “Idd angaliaaa” alipiga kelele Soraya na Idd akazinduka toka kwenye wenge na kujaribu kumkwepa yule mzee mpanda baiskeri, lakini alishachelewa, maana katika kumkwepa alijikuta amemgonga kwa ubavu wa gari na kumsukuma pembeni, kiasi cha kumfanya mzee huyu na baiskeri yake kuangukia mtaroni, kisha Idd akakanyaga mafuta na kuongeza mwendo, haya sasa iddi ndio huyo kapewa majibu kapanic anataka amuulize layla ni nani huyo mchumba wa sorayaaaaa, higg wiz nae mchumba kapatikana anaitwa joan ni yule yule rafika wa hilda au kuna mwingneeeeee? Baba yake higg wiz kapata ajali, je higgno akijua atafanyajeeeee? hatari mwanawane ITAENDELEA...
 
Back
Top Bottom