SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Jifahidi unapohadithia story ya mazingira flani, basi tabia za maeneo hayo ziendane na mazingira husika:
Na inatakiwa uyafahamu hayo maeneo ili hata wasomaji wanaoishi hayo mazingira wauone uhalisia wa story:
Vp kuna sehemu haijaendana na mazingira husika?
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA NANE
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SABA: Nissan ambalo hutumiwa na baba yake lilikuwepo, Pajero la mama yake lilikuwepo, hata Suzuki maruti la kuendea sokoni pia lilikuwepo, sasa kwanini huja waruhusu, ina maana baba amekataa?” aliuliza Soraya huku amemkazia macho mlinzi, ambae alitazama kwanza upande wa kushoto wa jumba lile la kifahari ambako kulikuwa na vijumba vinne vidogo vidogo, vijumba ambavyo kimoja wapo alikuwa anaishi Talib kwa sasa, ni mara baada ya kuzuiliwa kuingia nyumba kubwa kutokana na tabia yake ya udokozi iliyosababishwa na ulevi na uvutaji wa bangi, Mlinzi hakumuona mtu yoyote, “Talib amenizuia nisiwafungulie” alijibu mlinzi endelea…………
Na kumfanya Soraya ashangae, “ina maana huyo Talib ndie mwenye nyumba?” aliuliza Soraya kwa ukali, mlinzi akapiga kimya huku anatetemeka kwa uoga, nakuuliza wewe unaamrishwa na Talib?” aliuliza tena Soraya, “hapana Boss” alijibu mlinzi kwa sauti ya uoga, “mimi sio boss wako, mimi ni mtoto wa boss wako, hebu wafungulie haraka hao wageni, kama kuna mtu atakuzuia tena zaidi ya baba na mama mwambie aje kwangu aseme sababu ya kuwazuia” alisema Soraya ambae alionyesha kuchukizwa sana na tabia ile ya mlinzi.
Soraya alitoka na kulifuata gari lilipo, akaingia ndani ya gari na Laylah akaongoza gari mpaka karibu na mlango wa lile jumba kubwa la kifahari la tajiri mwarabu Mahamud, “iko wapi hiyo kanda?” aliuliza Soraya kwa sauti ambayo ilionyesha bado ilikuwa katika hali ya hasira na machukizo, “hii hapa” alisema Layla huku ana fungua mkebe kwenye dash board na kutoa video tape, akamkabidhi Soraya ambae alitazama kidogo picha ya kwenye kasha la ile tape, akigeuza mbele na nyuma, “asante, kesho ukija njoo na nyingine, si unajua kesho jumapili, saa nne unanipeleka TTC (tanzania teching college) kwenye join mass” alisema Soraya huku anafungua mlango na kushuka, huku amekumbatia daftari na ule mkanda wake wa video, “sawa” alisema Laylah, ambae alitakiwa kulipaki gari na kuondoka zake, maana kazi yake ilishaisha kwa siku ile, ikibakia kesho jumapili kama ilivyo utaratibu angekuja saa nne kumpeleka Soraya kwenye masomo ya dini, ambapo kila dini au dhehebu hukutana kwenye shule waliyo pangiwa, waislam walikuwa wanakutana TTC kule matogoro mita chache toka Luhuila Sekondari, ambako kulikuwa na shule ya songea wavulana, ambako pia walikuwa wanakutana wakristu wa dhehebu la roma.
Soraya alipiga hatua kadhaa kueleka mlangoni, kabla hajaufikia akaona mlango unafunguliwa akatokea Subira, mama mtu mzima ambae kazi yake ni kuhakikisha Soraya anafanyiwa shughuli zake zote, kama kufuliwa nguo, kusafishiwa chumba na mambo kama hayo, ambae sasa alimsogelea Soraya kwa lengo la kumpokea daftari, “hapana wewe wapokee wale wageni” alisema Soraya huku anageuka na kutazama kule getini, akawaona wale wageni wameshaingia na sasa wanakuja kule walikokuwepo wao.
Naam mzee Komba akiwa na familia yake, alimuona binti mzuri wa kustaajabisha akiwa amesimama anawatazama kwa kuwa hakumuona mara ya kwanza, akajua pengine ana taka kuwazuia wasiingie mule ndani, maana safari yao imekuwa na vikwazo toka wanakuja, ambapo walikosa hata shilingi mia tatu za nauli ya wote watatu, ni baada ya kwenda kuazima kwa watu wawili watatu na kuambiwa kuwa hawakuwa nazo fedha hizo, mtu pekee ambae sio kuwaazima tu! pengine ange wapatia kama majirani zake, alikuwa ni bwana Frank ambae kiukweli mzee Komba asigeweza kwenda kuazima kutokana na mambo ya siku zilizopita, hivyo basi pasipo kujali ujauzito wa Hilda wala umri walionao, ili walazimu kutembea kwa mguu umbali wa kilomita kumi.
Kimbembe ni baada ya kufika langoni kwa bwana Mahamud, ambapo walimkuta mlinzi alietaka wajitambulishe wao ni wakina nani na wanataka nini, maana alidhania kuwa ni omba omba ambao siku yao huwa ni ijumaa, “mimi ni mzee Komba, na huyu ni mke wangu” alianza kutambulisha mzee Komba akionyesha mama Hilda, alie simama na hilda, “huyu ni binti yetu, ndie mkwe wa bwana Mahamud, tumekuja kumuona sio kwa ugomvi ila kwa mema tu! tunataka kujua tunafanyaje kuhusu huu ujauzito, na kama watoto wataamua kuishi pamoja sisi hatuna kipinga mizi” alisema bwana Komba pasipo kujua kuwa anaemueleza hakuwa na msaada kwake, ilifaa aseme tu kuwa anaomba kumuona bwana Mahamud, “mh! mkwe wa boss kivipi?” aliuliza kwa mshangao mlinzi, huku anamtazama Hilda, ambae tumbo lake lilionekana wazi kabisa kwa ukubwa wake, “mchumba wa mtoto wa bwana Mahamud, hata huu ujauzito ni wa mtoto wa Mahamud” alisema Komba kwa ufafanuzi, “unamaanisha Talib?” aliuliza mlinzi kwa mshangao na tahadhari, “ndie huyo huyo” hapo zilitoka sauti za wote watatu, “mh! hebu subirini kidogo” alisema mlinzi akafunga kijigeti kidogo ambacho ndicho alikifungua ili kuwasikiliza wakina mzee Komba na kuelekea kwenye kijumba kidogo ambacho Talib alikuwa anaishi, akamueleza juu ya ule ugeni ndipo alipotoa amri ya kuwa wasiruhusiwe kuingia ndani.
Mzee Komba alipewa jibu hilo akajaribu kubembeleza, akijua kuwa akionana na bwana Mahamud ndio utakuwa mwanzo wa mafanikio yake yeye na familia yake , lakini alijikuta anatumia muda mwingi bila mafanikio, ndipo walipoamua kukaa pembeni ya ukuta wa uzio wa nyumba hii karibu kabisa na gate, akishindwa kurudi nyumbani kwa mambo mawili, moja ikiwa ni uchovu wa kutembea kwa miguu, aibu, na njaa, pili ikiwa ni aibu ambayo angeipata yeye na familia yake, ambao waliishi kwa kujitapa kuwa wanaenda kuwa matajiri, hata alipo muona Laylah akiingia na gari akajua sasa anapata muafaka wa jambo lake.
Nasasa ameruhusiwa kuingia anamuona tena binti huyu akimtazama kwa macho ya kiamri amri na ukali, isitoshe sasa akamuona tena yule binti anaingia ndani, lakini kuna mmama mmoja amesimama anawasubiri, hapo ndipo mzee Komba alipohisi kuwa anatimuliwa.
Lakini ilikuwa tofauti, maana yule mama aliwakaribisha ndani na kuwaongoza sebuleni, ambako waliwakuta mzee mwarabu mwenyewe na mke wake, ambao ni kama walishapewa taarifa ya ujio wao, maana walipokelewa kwa ukarimu, japo walionyesha alama za viulizo machoni mwao, “karibu sana jamani poleni kwa usumbufu, unajua Talib ni mkorofi na mkosa adabu sana huyu mtoto” alisema mke wa Mahamud, ambae sio mwarabu, kauli hii iliwafanya mzee Komba na mke wake kutazamana kwa mshangao kutokana na mambo mawili waliyo yasikia.
Moja ni kusikia kuwa Talib ni mkorofi aliekosa adabu, pili kujua kuwa Talib ndie aliewazuia wasiingie, na ukizingatia kuwa Talib ndie mkwe wao mtarajiwa.
Naam baada ya kusalimiana hapo wazee hawa wenye nyumba ambao hawakuonyesha ubaguzi wowote juu ya hali ya wakina mzee Komba, ambao hata muonekano wao ulionyesha wazi kuwa ni watu duni wasio na maisha bora kwa mavazi na usafi wa miili yao hasa miguu iliyo chafuka kwa fumbi la kutembea kwa miguu, waliwaomba waeleze dhumuni la ujio wao, “mzee sisi tumefika hapa kujua muafaka wa binti yetu, maana tumewasubiri mulete ujumbe kama ilivo taratibu za mila na desturi kama mlivyo ahidi kufanya hivyo mwezi wa kumi na mbili, lakini tumeona kimya” alisema mzee Komba, na kuwafanya mama na baba Soraya watazamane kwa mshangao wa sinto fahamu, “baba samahani kama vile sijakuelewa vizuri, kwani kuna ahadi tuliwahi kuitoa kuhusu kumsaidia binti yako?” aliuliza mama Soraya, ambae mara zote ndie mwenye uwezo wakuzungumza hasa wanapokuja wageni ambao sio wa kibiashara, kwasababu mume wake yaani bwana Mahamud, huwa sio muongeaji sana, swali hili liliwafanya mke wa mzee komba amtazame mume wake, ambae alikuwa anajiandaa kujibu, “labda hamja tufahamu, maana hatuja jitambulisha toka tumefika” alisema mzee Komba, huku baba na mama Soraya wakimsikiliza kwa umakini na macho yao wameyaelekeza usoni kwa mzee Komba, “kwa kifupi sisi ni wazazi wa huyu binti yetu Hilda, huyu ndie mschana aliepewa ujauzito na mtoto wenu” alisema mzee Komba ambae kwa uongeaji wake ni kama alikuwa na uhakika kuwa wazee hawa, yaani Mahamud na mke wake walikuwa wanafahamu kila kitu juu ya ujauzito wa Hilda, “mh! mtoto wetu?” alishtuka mama Soraya, huku anamtazama mume wake, ambae pia alikuwa anamtazama kwa mshangao, muda wote Hilda ambae kwa mbali alianza kusikia maumivu ya tumbo chini ya kitovu, alitulia na kutazama chini, “mzee una mzungumzia mtoto yupi au ume kosea nyumba, maana mimi nina mtoto mmoja tu tena wa kike, nadhani mulimuona hapo nje, ndie aliewaruhusu kuingia baada ya mtoto wa kaka yangu kuwazuia kuingia” alisema mama Soraya huku akimtazama Hilda na kisha kumtazama baba yake, “ni huyo uliemtaja mwanzo kuwa ni mkorofi” alisema mama Hilda, “mungu wangu, umepewa mimba na Talib?” aliuliza kwa mshtuko mama Soraya huku anamtazama Hilda ambae hakujibu lolote akibakia kutazama chini na kuhesabu vidole vyake vya mkono, maana hakuweza kujumlisha na vidole vyake vya mguu kutokana na kuzuiwa na tumbo lake mwenyewe, “jamani we binti unawezaje kukubali upuuzi huo, atakupeleka wapi huyu mshenzi?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya huzuni kubwa, “mama Soraya, hebu tulia kidogo, bado hatuja maliza swala hili” alisema mzee Mahamud kwa sauti tulivu.
Lakini mama Soraya akainuka kwa fujo toka kwenye kochi na kuelekea upande wa jikoni, “Khadija, hebu muite Talib haraka huko kibandani kwake” alisema mama Soraya kwa sauti ya ukali “ndiyo mama” ilisikika sauti toka upande wa jikoni, huyo mmoja kati ya wafanya kazi wa hapo nyumbani kwa mzee Mahamud, ambae alitoka nje haraka kwenda kumuita Talib
Dakika tatu baadae Khadija akarudi akiwa ameongozana na Talib, yeye akapitiliza na kumuacha Talib pale sebuleni, ambae ilionyesha kuwa hakuwa amejua alichoitiwa, nadhani hakujua kama wakina Hilda waliruhusiwa kuingia ndani baada ya kuwa akimueleza mlinzi awazuie, maana Talib alionyesha kushtushwa sana mara baada ya kuwaona wakina Hilda, “haya baba mke uliemuahidi kuwa utapeleka barua ndiyo huyu hapa amekuja” alisema mama Soraya kwa sauti ambayo aliilazimisha iwe tulivu, “mke mke yupi?” aliuliza Talib, na hapo kila mmoja mule ndani akamtazama Talib kwa mshangao, safari hii hata Hilda pia aliinua uso wake kumtazama Talib, kijana ambae alimtumia alivyotaka, akiamini kuwa mwisho wa siku ataolewa nae.
Mungu hamfichi mnafiki, macho ya Hilda yakakutana na macho ya Talib, ambae aliyakwepesha mara moja akishindwa kutazama macho ya mschana huyu, ambayo yalianza kutoka machozi, “Talib, inamaana hawa wazee wamemchukuwa binti yao kuja kukusingizia?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya ukali, “shangazi hii mimba sio ya kwangu” alisema Talib naye akipandisha sauti, “Hilda ni huyu au sio huyu?” aliuliza mzee Komba ambae mpaka hapo alikuwa ameshaanza kuchanganyikiwabkwa kuona mambo yanaenda ndivyo sivyo, “ndiyo huyu huyu” alijibu Hilda huku sauti yake ikiambatana na kilio cha kwikwi, “Talib, hebu tueleze, huyu mschana unamfahamu na tuleze kama ulishawahi kushirikiana nae tendo la ndoa” safari hii alisema bwana Mahamud mwenyewe, mjomba huyu mimi nilitembea nae mara moja tu! muda mrefu sana uliopita, toka mwezi wa nne, tena tulitumia kondom” alisema Talib pasipo kuweka tafsida mbele ya shangazi yake, hapo wote wakamtazama Hilda, hata baba na mama yake, lakini kabla mzee Komba hajaongea neno, mama Soraya akamuuliza Talib, “kwahiyo huyu binti anakusingizia sio?” ililikuwa swali lililo toka, kwa sauti ya ukali, “shangazi, ukinikalipia mimi utakuwa unanionea, ungemjua huyu mschana wala usinge nikalipia, kwanza ana wanaume wengi sana, mmoja wapo ni Higgy wizzy, anakaa nae huko huko kwao, pia anakunywa pombe, sasa huko anakokunywa pombe si anaweza kukutana na wanaume wengine” hapo mzee Komba na mke wake wakatazama chini kwa aibu, wakati mzee Mahamud na mke wake wakitazama kwa mshangao .……… endelea Kufuatilia mkasa huu hapa hapa jamii forums
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA TISA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA NANE: mama Soraya akamuuliza Talib, “kwahiyo huyu binti anakusingizia sio?” lilikuwa swali lililotoka kwa sauti ya ukali, “shangazi, ukinikaripia mimi utakuwa unanionea, ungemjua huyu mschana wala usinge nikaripia, kwanza ana wanaume wengi sana, mmoja wapo ni Higgy wizzy, anakaa nae huko huko kwao, pia anakunywa pombe, sasa huko anakokunywa pombe si anaweza kukutana na wanaume wengine” hapo mzee Komba na mke wake wakatazama chini kwa aibu, wakati mzee Mahamud na mke wake wakitazama kwa mshangao .……… endelea……..
Mpwa wao Talib, ambae hata uvaaji wake hapa mbele za wakwe zake ulionekana kuwa wa hovyo, akifanana nao wakwe zake ungesema wametoka sehemu moja, “Talib muogope mungu we mtoto, unasema kweli?” alisema shangazi kwa sauti ya masikitiko huku akimtazama Talib, ambae macho yake yalikuwa yanaonekana wazi kuwa ametoka kuvuta bangi, “kweli shangazi, hiyo mimba sio ya kwangu, ingekuwa ya kwangu si ningefukuzwa shule” alisema Talib pasipo kuuma uma maneno, hapo kikapita kimya kifupi kabla bwana Mahamud, haja mnong’oneza jambo mke wake, wakati huo mzee Komba na mke wake wanawaza juu ya aibu ambayo itawakuta huko mtaani kwao, baada ya kubainika kuwa Talib ameikataa mimba ya binti yao, maana hata kama walimkuta kijana mwenyewe tofauti na walivyo mfikiria kuwa ni mtoto wa tajiri, mwenye muonekano wa kitajiri, lakini bora angekubali tu! ili kufuta aibu yao, “haya we ondoka zako” alisema mama Soraya akimueleza Talib, ambae aliondoka kwa haraka kama kuku aliefunguliwa bandani kwa bahati mbaya.
Baada ya hapo mama Soraya akatoa noti ya elfu kumi na kumkabidhi Hilda, kisha wakaagana na kuwataka wajaribu kuongea na binti yao kuona kama kuna kijana mwingine ambae anaweza kuwa muhusika wa ujauzito huo.
Ukweli Hilda hakuamini macho na masikio yake, kile alicho kisema Talib ukweli, hawakuwahi kufika kwenye kituo cha dala dala za matogoro, Hilda akaanza kusikia uchungu wa uzazi, ikabidi wampitishie hospital ya mkoa, ambako alipokelewa na kujifungua samala kabisa mtoto wa kike, na hata siku ya pili walipo maliza taratibu za chanjo na kupewa ruhusa ya kwenda nyumbani, hawakuwahi kumjulisha mtu yoyote juu ya kujifungua kwa Hilda, wengi walijua baada ya mzazi kufika nyumbani na kusikika kwa sauti ya kichanga.******
Siku mbili mbele Higgy wizzy akiwa anaingia nyumbani kwao, akitokea shuleni akamuona mama yake akiongea na mama Hilda, yaani mke wa mzee Komba, ni kama kulikuwa na mjadala mzito sana kati yao, mama Hilda akionekana kulazimisha jambo fulani, ambae ile alipomuona tu Higgno, akamdaka juu kwa juu, “eti baba! wewe si ulikuwa una mahusiano na Hilda, hebu niambie hakuwahi kukuambia kama ana mimba yako?” aliuliza mama Hilda kwa sauti ya kulalamika na kuomboleza na kuwafanya mama Higgno na Higgino watazamane kwa mshangao, “heee! mwanangu, sio kwa ubaya, tunataka tujue kama wewe ndie baba wa mtoto, tunajua mnavyo pendana na mwenzio, najua huwezi kumkataa mwenzio, sema basi baba unafahamu kama Hilda alibeba ujauzito wako” alisisitiza mama Hilda kwa sauti ile ile ya kulalamika na kuomboleza.
Ukweli Higgno hakujua ajibu nini, maana jibu lazima lingeongozana na tusi au neno lisilofaa kuliongea mbele ya wakina mama wale, “mama Hilda, mbona nilishakuambia kuwa mwanangu hakuwa na mahusiano ya mapenzi na mwanao, isitoshe alipigwa nusu awe kilema kwa aajili ya binti yako pamoja na mume wako kuja kututukana kwa madai kuwa Higgno ana muonea wivu mwanao kisa anaolewa na mtoto wa tajiri” alisema mama Higgno kwa sauti ya upole yenye msisitizo, hapo kikapita kimya kifupi, huku mama Hilda akionekana anafikiria jambo, kisha akainua uso wake na kumtazama Higgno, “Higgy mwanangu sasa urafiki wenu uliishia wapi mpaka ukamuacha mwenzio anaingia kwenye mambo ya kipuuzi kama haya ya kutembea na jitu ambalo halina maana?” aliuliza mama Hilda kwa sauti ya masikitiko, sidhani kama kuna mtu kati yetu angeweza kutoa jibu la busara, hapo hata Higgno alikosa jibu na kubakia kimya, “Higgno ulimuachaje Hilda anaingia kwa lile jitu sijui vuta bangi, hata kama hamkuwa wapenzi, lakini kwanini ulimwacha mwenzio anaharibikiwa?” ukweli maswali yote yalikuwa magumu kwa Higgno, hata mama yake ilibidi amsaidie kujibu, “mama Hilda, usiongee kama labda mtoto amepatwa na tatizo ambalo hatuwezi kuishi nae tena, cha msingi ni kuangalia unaleaje mjukuu” alisema mama Higgno kwa sauti ya upole, ni kama mama Hilda alielewa, akaaga na kuondoka zake akionyesha kukosa amani moyoni mwake.
Hapo ndipo Higgno alipogundua kilicho mtokea Hilda ya kuwa amekataliwa na Talib, ukweli ilimshika huruma kubwa sana, alimlaani Talib kimoyo moyo kwa kumuharibia mschana aliempenda, Higgno aliumia sana ila hakuwa na la kufanya juu ya hilo, na alizidi kuumia zaidi hasa taarifa hizi zilivyozidi kutapakaa mtaani kwao hata shuleni pia, Higgno aliumia pia alipomuona mschana Joan, ambae ni chanzo cha Hilda kuingia kwenye mkumbo huo, akiendelea na masomo na kuambatana na wanaume wengine kama ilivyokuwa kwa wakina Talib kipindi kile hawaja maliza shule, lakini hakuwa na la kufanya zaidi ya kuangalia mambo yake.
Naam siku zilisonga maisha yakaendelea, Higgno akiendelea kufanya mazoezi ya karate kule Jeshini, japo mwalimu wake na rafiki yake Yohane alitoweka ghafla, mwezi mmoja tu baada ya kumaliza shule, japo kijana huyu yani Higgno, hakua mzuri darasani, lakini kiukweli aliipenda sana shule na alipangilia ratiba yake, ambapo asubuhi ya jumatatu mpaka ijumaa alienda shule na kupitia jeshini kwenye mazoezi, wakati wa jioni anaporudi toka shuleni, ambapo zilizidi kuwa mzuri kwenye sanaa hiyo ya mapigano, na kama ujuavyo wanajeshi mafunzo yao hutumia nguvu na uhakika wa vitendo, wakisistiza zaidi kumshambulia na kumuangamiza adui kabla haja kuangamiza wewe, japo ilikuwa ni kinyume na Karate inayo sisitizwa uraiani na kwenye vyuo vilivyopo chini ya vyama vya mchezo huo.
Licha ya kuhudhuria mazoezi kwa siku tano, lakini mara nyingi kijana huyu siku ya jumamosi angemsaidia baba yake kazi za nyumbani kwa kutwa nzima na jumapili angeenda kanisani matogoro, ambapo usali misa ya pili, ambayo utoka saa nne au saa tano, hapo angetembea taratibu akipita pembezoni mwa chuo cha ualimu na mpaka atakapo ipata njia panda ya kuelekea Luhila seko.*****
Naam wakati upande wa Talib mambo ya kizidi kuwa mabaya, akikimbiwa na marafiki zake kama wakina Vitus, ambao waliona Talib hakuwa na lolote kama ilivyokuwa zamani, na kumfanya kijana huyu azidi kuchakaa na kufanana na mtu ambae amekuja kuomba msaada kwenye nyumba ile ya mwarabu Mahamud.
Huku Soraya ambae alikuwa anazidi kukuwa na kupendeza zaidi akizidi kuishi kama malkia ndani ya nyumba ya wazazi wake, ambao walizidi kumpenda binti yao kwa jinsi alivyo fanya vizuri darasani, na kuwa mwenye tabia nzuri nyumbani na shuleni, sio kwamba mschana huyu hakukutana na vishawishi, ukweli ni kwamba alikutana na vishawishi vingi sana, vishawishi ambavyo kama ingekuwa ni kwa mschana jamii ya Hilda, angekuwa amesha sahau hata ladha ya dudu kwa siku ya kwanza ilikuwaje, Ukiachilia walimu wake wa shule ya waschana ya songea, ambao walijaribu kumshawishi kufanya nae ngono na kushindwa na kubakia wakimuheshimu na kumuogopa kwakujiona hawa kuwa na hadhi ya kuwa na mschana kama yule, pia watoto wa matajiri wenzake na baba yake na vijana wa rika lake, ambao pengine ni wanafunzi pia na vijana wakubwa kabisa, ambao wengi wao tayari walikuwa wamesha fungua biashara na ofisi zao kubwa tu!, ambao kila walipo pata nafasi ya kuwa karibu na mschana huyu walijaribu kutupia ndoana zao kwa Soraya, mschana ambae kwa kipindi hicho vijana wasinge acha kumtaja kama wanazungumza kuhusu waschana wazuri au warembo wa pale mkoani, lakini waliambulia patupu kwa maana hakuna hata mmoja aliefanikiwa hata kupata bahati ya kushika japo mkono wa mschana huyu, ikiwa ama ni salamu au katika jambo lolote, wote waliishia kumtazama kwa macho na kuvuta taswira, huku wakijisemea “dah! nikimpata huyu demu”
Sehemu ambayo Soraya alikuwa anakutana na kero za wanaume wenye uchu ni kwenye Joint mass, ambayo yeye kituo chake kilikuwa TTC, kule matogoro, ilifikia wakati wanafunzi wa kiume na baadhi ya wanafunzi wakike, ambao hawakuwa wanafunzi wa songea girls, hawakuweza kumsikiliza mwalimu kwa kumshangaa mschana huyu, ambae hata mara moja moja anapokuwa katika matembezi yake ya kawaida huwa anavaa niqab, (ninja) kuepuka usumbufu na kusabisha ajari kwa watu waliokuwa wakimshangaa kila anakopita.
Mwaka huo wa 1998 mwezi wa tano juma mosi moja, ikiwa siku moja kabla ya juma hili la join mass, ya week ya mwisho ya mwezi huu wa tano, kipindi ambacho wanafunzi walikuwa wanajiandaa kwenda likizo ya mwezi wa sita, huku wanafunzi wa kidato cha sita na wale wa grade A, wa mwaka wa pili wa chuo cha ualimu, walikuwa wamemaliza mitihani yao ya taifa, siku ambayo mchana wake kulikuwa na maafari ya kumaliza kwa wanafunzi wa chuo cha ualimu, ikifuatia na burudani ya music kwenye ukumbi wa sanaa na utamaduni wa chuo hicho nyakati za usiku, watu mbali mbali wakizamia kwenye burudani hii, wengi wao wakiwa ni raia toka maeneo ya karibu na wafunzi toka sekondari ya wavulana, ambao wengi wao huwa na wapenzi katika chuo hicho, ambacho kipo kilomita nne toka shuleni kwao.
Inasemekana siku hiyo ilipita salama kabisa, burudani iliisha kwenye saa sita za usiku na wanafuzi wakatawanyika, wale wa pale chuoni walienda kulala kwenye mabweni yao na wale wa zamiaji walirudi makwao, wengi wao wakiwa na imani kuwa siku hiyo ilipita salama, lakini ukweli ni kwamba haikuwa hivyo, (sina habari kamili ya tukio hili, nitasimulia kinachohusiana na simulizi hii).
kumbe usiku ule, kuna wanafunzi wawili wa shule ile ya songea wavulana, waliingia ugomvi na wanafunzi wenzao wanne wa chuo cha ualimu, chanzo kikiwa ni wivu wa mapenzi, ugomvi ulisababisha kifo kwa mwanafunzi wa shule ya songea wavulana, mwili wa mwanafunzi huyo uliokotwa siku ya pili pembezoni kwa viwanja vya michezo vya chuo cha ualimu, asubuhi na mapema polisi walifika na kufanya uchunguzi wa mwanzo, kisha wakaondoka na mwili wa marehemu pasipo kujua kuwa wakati huo huo, wanafunzi wa songea wavulana wanajipanga kuja kulipiza kisasi kwa kifo cha mwanafunzi mwenzao.
Kwa haraka mtu wa nje ya Chuo cha Ualimu na songea boyz secondary, asingejua kilicho tokea, maana shuguli nyingine ziliendelea kama kawaida, wanafunzi wa sehemu zote wakiruhusiwa kwenda kutembea kama ilivyo kawaida kwa siku za jumapili, yani kwenda kusali na kununua mahitaji yao, ikiwa na kukutana kwenye jumuiya za kidini, (joint mass) hata kijana Higgno ambae alieda kanisani matogoro hakuona wala kugundua chochote, mida hii ya saa mbili kwenda saa tatu, maana alikutana na baadhi ya wanafunzi wa songea wavulana, na wale wa chuo cha walimu, ambao alikuwa nao ndani ya kanisa mpaka mida ya saa nne na nusu walipoambiwa na padere kuwa “Nendeni na amani, akatoka nao pasipo kujua kuwa mida hiyo tayari mambo yalikuwa yamesha vurugika huko mtaani.
Maana wanafunzi wa songea wavulana waliovalia nguo za kiraia, walikuwa wamejificha vichakani kwenye njia zote za kuingilia pale chuoni na kuwashambulia wanafunzi wa chuo hicho waliokuwa wanarudi toka matembezi au kanisani, mbaya zaidi wanafunzi hao, walifikia hatua ya wakuwabaka wanafunzi wa kike waliowaona wanafaa kubakika kwa kuwasogeza kwenye mashamba ya mahindi na vichaka vya jirani kisha kumaliza haja zao.
Kwa upande wa mschana Soraya kama kawaida, mida hii ya saa tano kasoro alikuwa anakaribia kuingia pale chuoni akiwa yeye na dereva wake pekee, kitu ambacho hakikuwa kawaida kwake, maana mara nyingi huwa anawapa lifti wanafunzi wenzake anaowakuta njiani, lakini leo toka anaanza safari mpaka anamaliza safari yake hakumuona mwanafunzi mwenzake wa songea waschana aliekuwa njiani anaenda iwe songea boyz au TTC, “mbona kama leo hakuna wanafunzi?” aliuliza Soraya, ambae alianza kutilia mashaka hali ile ya ukimya wa barabarani, ambapo zaidi ya kuwaona vijana wawili waliovalia suruali za shule ya songea wavulana na tishet ya kiraia waliowapita mita chache nyuma yao, pia aliweza kumuona kijana mmoja mdogo, ambae japo alikuwa na mwili mkubwa kidogo, lakini alionyesha wazi kuwa mdogo, mwenye umri kama wa kwake, aliekuwa anakuja mbele yao usawa wa kituo cha daladala cha hapo chuoni, “ila leo tumechelewa, si unajua kuwa tunafika hapa saa nne kamili, pengine wamesha ingia” alijibu Laylah huku anapunguza mwendo na kuingiza gari kwenye kituo kidogo cha dala dala, ambacho siku zote humshusha Soraya na wenzake, “lakini leo pamepoa” alisema Soraya huku anatazama mbele, kumtazama yule kijana ambae alionekana yupo busy na kitabu chake mkononi, akionyesha wazi alikuwa anatoka kanisani, ambae sasa likuwa kama mita kumi tu mbele yao.
Soraya akatazama nyuma, kule alikotoka akawaona wale vijana wawili wakiwa wana kuja kwa kusua sua, “mimi nakusubiri hapa, kama hawatakuwepo basi tuondoke” alisema Laylah, na hapo Soraya akasubiri kwanza yule kijana aliekuwa anakuja mbele yao apite, akimsindikiza kwa macho kijana huyu, ambae ukiachilia umbo zuri la kiume liliokaa kimazoezi katika muonekano wa hali ya wastani urefu wa wastani weusi wa wastani, pia alikuwa na sura nzuri ya upole, ambae alilipita gari taratibu na kusalimia, “habari” alisalimia kijana yule ambae hakusubiri salamu yake kuitikiwa akaendelea na safari yake, ukweli Layla aliesalimiwa hakuitikia salamu ile, sijui kwanini, ila wote walimsindikiza kwa macho mpaka alipolipita gari lao aina ya Land rover discover, “kwanini hujaitikia” aliuliza Soraya huku ana jiweka sawa na kuchukua kijitabu chake kidogo cha dini, “sijui kwanini nimejikuta tu nashindwa kukuitikia” alijibu Laylah mbae kwa sasa alikuwa ana makadirio ya miaka ishirin na nane, wote wakacheka huku Soraya anafungua mlango wa gari na kushuka, kisha akatazama kushoto na kulia, akiwaona wale vijana wawili waliovalia suruali za shule na mashati ya kiraia wakipishana na yule kijana mpole alieshika kitabu cha dini, ambae alienda na kugeuka kutazama alikotoka, yani upande wake, hata macho yao yakakutana, Soraaya akamuona yule kijana akitoa macho kwa mshangao, kama wale vijana wawili pia ambao walikuwa wanakuja upande wake kwa mwendo ule ule wa kusua sua, Soraya hakuwajali watu hawa, maana alishazoea kutazamwa kwa macho ya matamanio, yeye akafunga mlango wa gari na kutembea kuelekea upande wapili wa barabara, kwa maana ya kuvuka barabara.
Ukweli Higgno ambae alikuwa amegeuka na kumtazama mschana alie kuwa ameshuka toka kwenye gari, alichanganyikiwa kwa uzuri wake, hakika hakuwahi kuona uzuri wa mschana huyu kwa mschana mwingine yoyote, lakini kiukweli ingekuwa kazi bure kwake, endapo angeendelea kumtamani mschana yule, ambae hata angefanyaje aliamini asingeweza kumshawishi kuwa nae, kama alimshindwa Hilda masikini mwenzie itakuwaje kwa mschana kama huyu ambae anaonekana wazi kuwa ni mtoto wa tajiri, tena chotara wa kiarabu, “oya subiri kwanza avuke barabara” Higgno alimsikia mmoja kati ya vijana wawili aliokuwa anapishana nao, “lakini huyu demu na mfahamu sio mwanachuo, huyu anasoma songea Girls” alisema mwingine, hapo ndipo Higgno, alipoanza kuhisi hatari iliyopo mbele ya yule mschana, akageuka kumtazama tena, sasa akiwa amesha pishana na wale vijana wawili ambao kimuonekano niwazi walikuwa ni wanafunzi wa songea boyz, Higgno akamuona yule mschana anavuka barabarana kuifuata njia nyembamba ya kuingilia chuo cha ualimu kupitia mazizini, na alitoweka kwenye nyasi ndefu, akawaona wale jamaa wawili wanaongeza mwendo kuekelekea kule kule alikoelekea yule mschana.
Ghafla ilimjia roho ya huruma sana kwa mschana yule asie na hatia, maana alijuwa fika kuwa kinachoenda kumtokea sio kitu kizuri hata kidogo”******
Taarifa za vitendo vya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya kuvamia wanafunzi wa chuo cha ualimu na kufanya vitendo vya ubakaji zilisambaa kwa kasi sana, sehemu ambazo ziliwahi kufika ni pamoja na shule ya sekondari ya waschana, ndio maana Soraya hakuwahi kuwaona wanafunzi wenzake njiani, maana tayari walisha zuiliwa wasiende kwenye joint mass songea boys na TTC, polisi wakajipanga na kuanza safari ya kuelekea TTC.
Mwanafunzi mmoja wa shule sekondari ya waschana anae fahamika kwa jina la Kuruthum, alikumbuka juu ya mwanafunzi mwenzao Soraya, ambae huwa wanaenda nae joint Mass, hivyo akaenda kwa mwalimu wakike msimizi wa waschana, (matron) na kumueleza kuwa ufanyike utaratibu wa kujulisha nyumbani kwa kina Soraya, kuwa mschana huyu asiende TTC.
Nikweli ukafanyika utaratibu, ikatafutwa namba ya simu kwenye kitabu cha orodha ya namba hizo za kampuni ya simu ya taifa, wakaipata namba ya simu ya nyumbani kwa mwarabu Mahamud, ambae alipoelezwa akashtuka sana, maana tayari binti yake alishaondoka kuelekea huko TTC, ukweli katika vitu vinne ambavyo usije ukacheza navyo mbele ya mzee huyu, ikiwa ni roho yake, mke wake, mali zake, binti yake alikuwa ni wa kwanza, kuna siku aliwahi kuulizwa ni kitu gani kinachoweza kumfanya apandwe na hasira wazi wazi, maana mzee huyu upole ilikuwa ndiyo sifa yake kuu, na yeye akajibu, “kwanza kabisa, mtu ambae atacheza na Soraya” hilo ndilo lilikuwa jibu la bwana Mahamud,
Na leo alithibitisha hilo kwa kuchukua silaha yake aina ya kurgger pamoja na mkebe mmoja wenye risasi zake kumi, akatoka bila kuongea na mtu akaingia kwenye gari na kuondoka pale kwake kwa mwendo wa ajabu.***********
Kumbe basi wakati huo tayari Soraya alifanikiwa kuvuka barabara akiliacha gari lina msubiri, ambalo tayari Laylah alikuwa ameshalizima kabisa, lakini mschana huyu mwenye uzuri kiwango cha dhahabu, alipotembea mita kama ishirini ndani ya njia nyembamba, iliyofunikwa na nyasi ndefu kushoto na kulia, ghafla akawaona vijana wawili wakiibuka mbele yake, ilikuwa ghafla kwasababu vijana hawa waliovalia kama wale aliowaona barabarani, yaani suruali za shule na mashati ya kiraia walitokea kwenye kichaka na kuanza kumfuata huku wamemkazia macho, hapo Soraya akajua dawa ni kurudi alikotoka, ile anageuka akashangaa kuona wale vijana wawili aliowaona barabarani, nao walikuwa mita chache nyuma yake, “mungu wangu nini kina nitokea, ni ndoto au kweli” alijiuliza Soraya, ambae alianza kuhisi miguu yake inakosa nguvu, akitabiri kinachokuja kumtokea ni wazi sio kitu kizuri kwake……...……… Itaendelea……
Comment yako like itanijulish kuw simulizi hii ina wafuatiliaji, nitapata hamasa ya kuileta kwa wakati.
 
"mschana huyu, ambae hata mara moja moja anapokuwa katika matembezi yake ya kawaida huwa anavaa niqab, (ninja) kuepuka usumbufu na kusabisha ajari kwa watu waliokuwa wakimshangaa kila anakopita"😂😂😂😂😂😂😂😂😂😅👍👍👍👍👍👍👍👍👍kazi nzuri sana mkuu
Naona vitu vyangu tayari vimefikiwa😂😂😅😂😂😅
 
Mambo ya Deus Frank Nyati yapo Kwa Higi Frank
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA TISA : ghafla akawaona vijana wawili wakiibuka mbele yake, ilikuwa ghafla kwasababu vijana hawa waliovalia kama wale aliowaona barabarani, yaani suruali za shule na mashati ya kiraia, walitokea kwenye kichaka na kuanza kumfuata huku wamemkazia macho, hapo Soraya akajua dawa ni kurudi alikotoka, ile anageuka akashangaa kuona wale vijana wawili aliowaona barabarani, nao walikuwa mita chache nyuma yake, “mungu wangu nini kina nitokea, ni ndoto au kweli” alijiuliza Soraya, ambae alianza kuhisi miguu yake inakosa nguvu, akitabiri kinachokuja kumtokea, ni wazi sio kitu kizuri kwake……...……… endelea……..
Lakini hakusubiri wale watu wamkute akiwa amesimama pele pale, akaona bora arudi alikotoka, pengine angepata msaada toka kwa Laylah, hivyo akaanza kurudi alikotoka huku mikono yake ameikumbatia kifuani ameshikilia kile kitabu chake cha dini, na wakati huo huo akasikia gari lake likiwashwa na ile alipowakaribia wale wavulana wawili ambao ni wazi kabisa kuwa ni wanafunzi wa songea Boys, waliokuwa wanatokea barabara kuu, akaamua awapishe kwa kupita kwenye nyasi kabisa, huku uso wake ukiwa umetawaliwa na uoga wa hali ya juu, lakini ni kama alikuwa amewarahisishia kazi wale vijana, hapo hapo mmoja wao akamsukuma kwa nguvu na Soraya akijikwaa kwenye nyasi na vile viatu vyake virefu, akajibwaga chinii puu, hapo Soraya akaachia kilio cha mwaka, lakini akakutana na kofi zito la usoni, “kimya wewe ukipiga kelele tutakuuwa hapa hapa” alisema mmoja huku wale wengine nao wakija na kuungana nao, hebu tulieni jamani, huyu demu mimi nilikuwa namtamani kinyama, nyie pigeni alafu mimi nitamalizia” alisema mmoja kati ya wale wanafunzi wawili walioongezeka, “jamani msinifanye hivyo nitawapa hela” alisema Soraya kwa sauti ya uoga na yakuomboleza, lakini hakuna hata mmoja alieonyesha kumsikiliza, ndio kwanza walianza kumshika viziri wawili wakimshika miguu mmoja akiamshika mikono, pale pale chini, halafu mmoja wao akashika gauni tayari kulipandisha juu, hapo Soraya akajua leo anatolewa uschana wake katika njia mbaya kuliko alivyotegemea tena kwa namna ya aibu kwa mtoto wa tajiri kama yeye,
Hapo Soraya akiwa ameshakata tamaa, alibakia ana toa mchozi wa kimya kimya na kufumba macho japo siweze kushuhudia kile kinachotaka kufanywa kwenye kitumbua chake, lakini kabla hata yule jamaa haja mfunua gauni lake, mara akasikia, “mwacheni huyo mwanamke” hapo Soraya akafumbua macho na kuwaona wale jamaa ambao walionyesha kushtuka na kumuachia Soraya, huku wakisimama na kumtazama aliewaambia wamuachie, hapo Soraya pia akainuka na kumtazama mtu huyo mwenye sauti ya upole, akamuona ni yule kijana aliewasalimia pale kwenye gari, ambae sio yeye tu alieona kuwa msaada unaweza kuwa mdogo sana kwa kumtegemea kijana huyu, kwasababu asilimia kubwa ya wale vijana wanne walimzidi kwa umri na maumbo yao makubwa, wakionyesha kuwa ni wanafuzi wa kati ya Kidato cha tatu mpaka cha sita, na huyu kama anasoma basi ni kidato cha kwanza au cha pili, maana hata kwa mtazamo walikuwa wanaendana kwa umri, hata wale vijana wanne walimdharau, “kum.. tutakukamua na wewe mwenyewe, hebu ondoka haraka” alisema mmoja wao kwa sauti ya kibabe, yenye mkwara mzito, hapo Soraya ambae alisha kata tama na utetezi uliokuja akaona kuwa mtetezi wake aliebakia ni mbio pekee, lakini viatu alivyovaa ndivyo vilivyo kuwa kikwazo kwake,
Lakini akatumia ujanja wa kuvua viatu kwa kutumia mguu, lakini hakumaliza hata kutoa kiatu kimoja, akadakwa mkono na mmoja wa wale vijana, Soraya hakuwa na ujanja, akabakia ana mtazama yule kijana mpole mwenye kujiamini, ambae ndiyo mtu pekee anaeweza kumsaidia, japo alishakata tamaa juu ya kijana huyu mdogo, “mugu wangu tenda miujiza” alijisemea Soraya, huku akijiona kuwa bado yupo kwenye hatari ya kubakwa na wanaume wanne, Soraya akamtazama yule kijana mpole kwa macho ya huruma, akamuona ametulia anawatazama wale vijana wa songea boys kwa zamu, “kama mnajua wazazi wenu waliwatuma kuja kusoma nasema muacheni huyo mschana haraka” alisema tena yule kijana mdogo, kwa sauti ile ile ya upole yenye kujiamini kiasi cha kuwafanya wale vijana wanne watazamane kwa mshangao, huku Soraya akianza kumuona yule kijana kuwa ni wakipekee kwa jinsi anavyojiamini, lakini wale vijana walimtazama kwa sekunde chache, waliachia kicheko cha nguvu kilichojaa dharau, “anasemaje huyu fala, anatujua sisi wakina nani?” aliuliza mmoja huku anawatazama wenzake.
Hapo Soraya, alijikuta anaomba japo kijana huyu, angekuwa na mwili mkubwa kidogo ange msaidia kuepukana na kibako hiki, na wakati huo huo ikasikika sauti ya Laylah, “we! Sorayaaaaaa” ilionyesha wazi kuwa tayari Laylah alijua kinacho taka kutokea kwa boss wake, maana hata gari tayari alishaliwasha, lakini soraya hakuweza kuitikia, maana alikumbuka kofi alilotandikwa usoni wakati ule, sasa Soraya akamuona kijana mmoja kati yao akimsogelea yule kijana mpole kwa hasira huku anasema,“mbona mnamkawiza huyu, mseng…” na kabla hajamalizia kauli yake, Soraya alimuona yule kijana mpole ghafla na kwa haraka akikifyetuwa kichwa chake kwanguvu kukivurumisha kwa mwanafunzi yule aliemsogelea, ambapo kilitua kati kati ya pua na macho, hakika hakikumuacha salama yule mwanafunzi, ambae alitoa mguno wa maumivu huku anajishika usoni kwa mikono yote miwili, muda huo huo tayari damu zilishatapakaa eneo lote la matundu ya pua mpaka kwenye mdomo na kidevu, hapo kijana mpole ni kama alichokoza nyuki, maana vijana wawili wengine walimvamia kijana huyu huku mmoja akibakia amemshikilia yeye Soraya, na yule mwingine akijishangaa damu zilizotapakaa usoni mwake, sasa Soraya akajua kuwa kijana mpole anapokea kipogo kizito.
Hapo Soraya akashuhudia kijana mpole akimkwepa mwanafunzi wa kwanza aliekuwa amerusha konde kwenda usoni, kijana mpole hakuangaika na huyu aliemkwepa, kwanza alirusha ngumi ya maana iliyotuwa usawa wa chembe ya moyo wa kijana wa pili na kumfanya ainame huku akijishika kwa maumivu makali huku akimuona yule mwingie na yeye akimvamia tena kijana mpole kwa kumrushia teke, hapo Soraya akamuona yule kijana anafanya kama vile anavyoona kwenye video, yani alikwepa kidogo na kuvulumisha ngumi nzito kwenye shavu la yule mwanafunzi wa pili, ambae alitema damu na kitu kama punje ya muhindi iliyochafuliwa na damu.
Mpaka hapo Soraya akapata matumaini ya kutoka salama mikononi mwa watu hawa waliokosa huruma, japo hawakuonekana kukubali matokeo,ni baada ya kuamua kumvamia tena wote watatu kwa pamoja, huku mwenzao akiwa bado amemshika Soraya, lakini kilichotokea ndicho ambacho kilimfanya Soraya amtazame vizuri kijana huyu usoni, maana aliwakwepa kwa ustadi na kuwashambulia kama mtu aliepata mafunzo ya kimapigano, na mashambulizi yake yalikuwa mazito.
Soraya ambae aliendelea kumsikia Laylah akiita kwa sauti ya juu, akamuona yule mmoja aliekuwa amemshika mkono akimuachia yeye mwenyewe, na kujaribu kwenda kuongeza nguvu ya kuwa saidia wenzake, hapo ndipo Soraya alipovua viatu na kuanza kukimbia kuelekea barabarani akiacha mapigano yanaendaelea, huku yule kijana akiwatandika wale wanafunzi kwa ngumi nzito za kikatili.
Pasipo kujua kilichotokea nyuma, Soraya aliingia kwenye gari na Laylah akaondoa gari kwa speed kurudi mjini, ambapo mita kama mia nne mbele, wakawaona polisi wengi wakiwa na magari mawili yaliyo simama na gari la baba yake soraya, yaani Nissan patrol, na hapo Soraya akamuambia Layla asimamishe gari.
Waliposimamisha gari tu! ndipo walipomuona mzee Mahamud akishuka toka kwenye gari lake na kuwafuata kwenye gari lao, “vipi mwanangu upo salama” aliuliza mzee Mahamud kwa sauti iliyojaa pupa na wasi wasi, ndipo Soraya alipo anza kumsimulia jinsi ilivyo kuwa.******
Wakati huo tayari Higgy wizzy alishawatandika vibaya sana wale wanafunzi wanne, akiwa amesha mvunja mmoja mkono mwingine mguu na yule aliempasua pua na mwingine alimtoa jino, sasa walikuwa hoi na Higgno akaanza kusikia saauti ya wanafunzi wengine wanakuja upande huo hivyo akaondoka zake, akijua kuwa wakiongezeka zaidi kuna hatari ya yeye kushindwa kuwamudu kimapigano.
Higgno alipofika barabarani hakutaka tena kufuata barabara, hivyo alivuka barabara na kuingia kwenye mashamba ya mahindi akapotelea huko kuelekea bondeni, yaani mtoni ili avukie kwao Luhuila, na hakufika mbali akasikia miungurumo ya magari yakiongozana kuja kule alikotoka na kusimama pale kwenye usawa wa kituo cha dala dala.******
Ilikuwa hivi, mara baada ya kumsimulia baba yake, jinsi alivyovamiwa na vijana wale wahuni, na kuokolewa na kijana yule asiemfahamu, ambae alimuacha bado anaendelea kupambana na wale vijana wahuni, ndipo mzee Mahamuda alipo waeleza polisi kuwa waelekee huko wakamsaidie kijana huyo muokozi wa binti yake, hata Soraya ambae alitamani kumuambia asante kijana yule mpole akaingia kwenye gari lake na Laylah akaendesha kuwafuata polisi na baba Soraya, ambapo dakika mbili zilitosha wao kufika eneo husika na kusimamisha magari yao.
Polisi wakashuka Haraka na kelekea kwenye ile njia ambayo Soraya alisema alikuwa amepita na kukutana na wale wanafunzi wahuni, hapo polisi kumi waliofuata ile barabara waliwaona vijana kama kumi na saba wakianza kukimbia maporini, huku wakiwaacha wenzao wanne wakiwa wanashindwa kukimbia vizuri kutokana na kujeruhiwa vibaya na kijana mpole, hata walipo kamatwa Soraya aliwatambua kama ni wale vijana waliotaka kumbaka.
Licha ya yote, lakini Soraya alisikitika kuto kumuona yule kijana mpole, na katika hali ambayo hata yeye mwenyewe hakuielewa alijikuta ana tamani kukutana na kijana yule, ambae sio jina tu! hata sehemu anayoweza kumpata hakuijua, hivyo akabaki akishindwa kuondoa kumbu kumbu ya kijana yule kwa muda mrefu sana, “Layalah, hivi wewe una mwanaume wako?” kuna siku Soraya akiwa kidato cha tatu, anatoka shule na Dereva wake, alimuuliza swali hilo, ambae alianza kwa kucheka kidogo, “ndio ninae lakini sijafunga nae ndoa” alijibu Laylah huku anacheka cheka, “na huwa unazini nae” aliuliza tena Soraya na kumfanya Laylah acheke kicheko cha aibu, “ndiyo huwa tunafanya mara moja moja” alijibu Laylah, akiendelea kuachia kucheko chake, “kwani ukiwa na mwanaume lazima mfanye?” aliuliza Soraya, hapo Laylah akashusha pumzi nzito, “mh! inategemea na mtu mwenyewe, kwani… kuna mwanaume unafikilia kumkubali?” aliuliza Laylah, kwa sauti ya mashaka, maana hakujua kama lile swali lita kuwa zuri kwa Soraya, itaendelea……..

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI : “na huwa unazini nae” aliuliza tena Soraya na kumfanya Laylah acheke kicheko cha aibu, “ndiyo huwa tuna fanya mara moja moja” alijibu Laylah, akiendelea kuachia kucheko chake, “kwani ukiwa na mwanaume lazima mfanye?” aliuliza Soraya, hapo Laylah akashusha pumzi nzito, “mh! inategemea na mtu mwenyewe, kwani… kuna mwanaume unafikiria kumkubali?” aliuliza Laylah, kwa sauti ya mashaka, maana hakujua kama lile swali lita kuwa zuri kwa Soraya, endelea……..
Ambae alitulia kwa sekunde kadhaa kama vile anatafuta jibu la kumpa dereva wake, yaani Laylah “mh! mi sijui” hilo ndilo lililokuwa jibu la Soraya, ambae mpaka anafika kidato cha tatu na miaka yake kumi na saba, hakuwa ameruhusu mwanaume aguse kitumbua chake, japo alishangaa kuona anatamani kumuona kijana mpole na kuwa nae karibu, “mh! akitaka tufanye nitamwambiaje” aliwaza Soraya.
Naam mschana huyu ambae ilisemekana kwa kipindi hicho alikuwa ndie mschana mrembo, zaidi aliepata kutokea mkoani Ruvuma kabla ya wakian Eveline (mwalimu nae anataka) au Malaika (bibi harusi mtarajiwa), aliendelea kusoma kwa juhudi huku taratibu siku zilivyo enda ndivyo alianza kusahau juu ya kijana mpole, aliemsaidia asibakwe, japo alianza kupata hisia za kuwa na mwanaume, lakini alijizuia kufanya hivyo kwasababu aliona kuwa, aina ya mwaume aliemuhitaji, pia alisaidiwa na maadili ya dini na heshima ya wazazi wake.
Soraya aliendelea kusoma kwa juhudi, huku burudani yake kubwa ikiwa ni filamu za kihindi za kizungu na zile za vichekesho za Kiswahili za wakina marehemu king Majuto, mzee small na wengine, (walazwe mahali pema pepon).*******
Higgno ambae licha ya kumsaidia mschana yule chotara kwa lengo la kumuokoa asifanyiwe udhalilishaji na wale wanafunzi watukutu, lakini kiukweli alishangazwa sana na uzuri wa mschana yule, huku akiombea japo amuote kwenye ndoto japo hata usku mmoja tu na roho yake itulie, lakini huwezi amini, hakuweza kuota hata ndoto inayofanana.
Ukweli Higgno hakuwahi kuwaza kuwa anaweza hata kupata nafasi ya kumsogelea mschana yule chotara ambae ukiachilia uzuri wake, pia hata hali ya kimaisha aliyonayo mschana yule, ambae hakumfahamu anatokea wapi na anasoma wapi, yeye Higgno alijiona kuwa asingefaa hata kuwa house boy wake, Higgno alitamani angezaliwa akiwa tajiri, maana hata Hilda asingemkimbia na kwenda kwa Talib, ambae sio kwamba ni mtoto wa tajiri ila ni ndugu wa tajiri, lakini kadiri siku zilivyo songa ndivyo Higgno alivyozidi kumsahau mschana yule chotara, ambae aliamini kuwa hatokaa akutana nae tena katika maisha yake, zaidi aliendelea kujituma katika mazoezi na masomo na kumsaidia baba yake kazi mbali mbali, akiamini kuwa juhudi zake ndizo zitakazo muokoa katika maisha yake na kuondokana na kudharauliwa.*******
Upande wa pili Hilda aliendelea kulea mwanae kwa shida, huku anajutia kitendo cha kujiingiza kwenye mapenzi na Talib, akimuacha Higgno, ambae alionyesha kumpenda na kumjali toka wakiwa wadogo, hawajui hata maana ya kupeana dudu, “Joan mshenzi sana, kweli nimeamini kuna watu wamezaliwa kuwaharibia wenzao maisha” alijisemea Hilda, ambae hakuweza kuvumulia kukutana na Higgno uso kwa uso, na kila alipomuona kwa mbali alimkwepa kwa kumkimbia, ni kutokana na aibu aliyokuwa nayo.
Mwanzo Hilda alikuwa mtu wa kujificha ficha kwa aibu, lakini siku zilivyozidi kwenda akaanza kuzoea na kujionea kawaida tu, hivyo akaanza kujiachi mitaani na kufanya kazi za nyumbani na shambani kama kawaida, huku akiendelea kulea mwanae, lakini yote kwa yote bado hakuweza hakuwai kukutana na Higgno uso kwa uso, ukiachilia kumkwepa mara chache anapomuona, pia ni kutokana na Higgno kutokushinda nyumbani, maana muda mwingi aliutumia shuleni na mazoezini.******
Naam Higgno alifanikiwa kumaliza kidato cha nne mwaka 2000, bahati haikuwa kwake, aliambulia division four ya point 28, ambayo inge muwezesha kujiunga na chuo cha ualimu, lakini katika za kitoto Higgno hakupenda kuwa mwalimu, hivyo akajiunga na chuo cha ufundi, akijiweka kwenye ufundi wa magari kwenye chuo kidogo cha ufundi kinacho milikiwa na kanisa catoriki, akiamini kuwa elimu hiyo inaweza kumsaidia kupata kazi itakayo muingizia kipato, lakini hakuwahi kuacha mazoezi ya karate, ni kama ulishakuwa ulevi wake.
Wakati huo huo mschana mrembo mwenye urembo wake akipata division one na kuendelea na kidato cha tano hapo hapo songea Girls, ni kutokana na wazazi wake kuomba asome shule hiyo ambayo ingemuweka karibu yao, hawakutaka wakae mbali na binti yao.
Kwa upande wa kijana Talib, maisha yalizidi kuwa magumu kwake, maana sasa hata vile vitu vidogo vidogo vya kuiba ili akauze apate fedha ya bangi alikosa, sasa alikuwa anaenda kujikalisha kwenye vijiwe vya wauzaji na wavutaji wa bangi, ili wenzake wanapo nunua na yeye adowee (agongee), maana hata rafiki yake Vitus hakujua yupo wapi toka walipomaliza shule na Talib kusitishiwa huduma za fedha na usafiri, Vitus nae akatoweka, sio Vitus peke yake hata marafiki wengine wakike na wakiume waliokuwa wanamfuata Talib kwaajili ya hela zake nao walitoweka, japo baadhi yao alikuwa anakutana nao, lakini hawakuwa na mpango nae, walimpita kama mtu ambae hawakuwa wanamjua.
Lakini siku moja Talib akiwa amewahi kweli kweli kwenye viwanja vya RMA, sehemu ambayo wavuta bangi wengi hutumia kama sehemu ya kununulia na kuvutia sigara hiyo, ambayo mpaka sasa nchini kwetu haijapata kibali cha kutumika, akiwapeke yake huku kiu ya kilevi hicho ambacho toka alipopewa jana kwa ule utaratibu wa mwenge hauvuki kijiji, akuwa amevuta tena mpaka leo, alijaribu kutafuta pisi pale chini, pengine angeweza kuviunganisha na kupata angalau kidogo ya kuvuta muda ule (wenyewe wanaita chaukucha), lakini hakupata hata mbegu ya mmea huo wenye majina mengi duniani.
Naam Talib akiwa amekosa bangi na kiu kali sana, wenyewe wanaita alosto, aliwaza mengi sana pale pembezoni mwa uwanja huu mkubwa wa michezo, ukweli alijiona kuwa anaonewa sana na kunyanyaswa na mjomba wake, ukweli hakuangalia matendo yake mabaya yaliyo sababisha hayo yote, ikiwa ni ulevi na utumiaji wa bangi, wizi na matukio mengine ya kuchukiza, Talib aliumia sana jinsi binamu yake Soraya alivyokuwa analelewa na kuhudumiwa kama malkia fulani, hakuna kitu alihitaji hakupewa, japo hakuwa na mambo mengi ya ziada zaidi ya mahitajio ya shule, nguo mpya na matoleao ya viatu na mapambo ya kisasa, hakuzuiliwa kutumia gari muda wowote alioutaka, japo hakuwa mtu wa safari za ovyo, likizo zake alikuwa anasafiri kwenye dar es salaam au dubai ambako ndiko nyumbani asili ya mzee Mahamud.
Naam wakati Talib anaendelea kuwaza na kunung’unika ndipo alipo shangaa kumuona Vitus akiingia sehemu ile, ukweli Talib alipatwa na mashangao mkubwa sana kumuona Vitus, sio kwasababu alikuwa hajamuona muda mrefu, la hasha, ni kwasababu Vitus aliingia pale akiwa na vijana wengine watatu wakitumia usafiri wa Toyota crester lenye music mkubwa sana, huku wao pia wakiwa wamevalia mavazi nadhifu ya kupendeza kuanzia matisheti suruali zao za jinsi rangi ya blue ya kuiva na mipauko, na raba kali sana miguuni mwao, wengine kati yao walivalia pete na cheni za dhahabu.
“Duh! Talib! ni wewe? mbona upo hivyo?” aliuliza vitus kwa mshangao huku anamtazama Talib kwa jinsi alivyochafuka na mavazi dhaifu, “ebwahee! Vitus una michongo gani siku hizi, mbona unawaka na pamba nyepesi” aliuliza Talib kwa mshangao, huku anamtazama Vitus ambae kiukweli ungedhania yeye ndie anatokea kwenye lile jengo la kifahari la mwarabu tajiri bwana Mahamud, “maisha tu mwanangu, vipi wewe mbona umechoka hivyo?” aliuliza Vitus swali ambalo Talib hakuweza kulijibu, Vitus akamtazama jamaa mmoja kati ya wale aliokuja nao, ambae alionekana kuwa ndie mmiliki wa lile gari, maana hata umri aliwazidi wakina Vitus, “Zido una mfahamu huyu jamaa?” aliuliza Vitus, na yule jamaa anaeitwa Zido ni kama hakumjari sana, lakini akajibu, “nisimjue huyu dogo fala wa pale kwa mwarabu” alijibu zido huku anazunguka gari kwenda kwenye buti na kulifungua, kisha mwingine akatoa mfuko mkubwa kama ule wa kuwekea unga wa sembe au mahindi wa kilo kumi, “sio fea bro, unamuitaje fala” alilalamika Vitus, huku wengine wakicheka, huku talib akishangaa na kutulia kinyonge, maana hakuwa na la kufanya, “kwani uongo huyu ni fala, anakaa kwa tajiri kama yule anashindwa kupiga hela mpaka anaishi kiboya kama hivi?” alisema Zido, huku ana ingiza mkono mfukoni mwake na kutoa lizzler huku wengine wakitulia na kushindwa kuchangia neno, “unadhani Vitus, huyu dogo fala sana, we unakuwaje hivi wakati yule mzee anamawe kibao anasaidia mpaka masikini wa mtaani, halafu we unakuja kuvuta cha ukucha hapa kijiwe” alisema Zido ambae sasa aliingiza mkono kwenye kile kiroba na kuibuka na kiasi fulani cha bangi, “hebu nyonga hii ushtue kidogo nikupe mchongo wa kufaidika, sio unaishi kindezi ndezi” alisema Zido, huku anampatia Talib ile bangi na lizzler (kiaratasi maalumu kwaajili ya kuviligia tumbaku ya asili, local sigaret, hapo sasa hata Talib mwenyewe akatabasamu huku anapokea ile bangi na karatasi ya kusokotea, mara moja akaanza kusokota bangi, huku tabasamu la fisi likitawala mdomoni mwake, ungesema anaandaa paja la kuku wa kienyeji.
Naam sijui Zido aliongea nini na Talib, lakini ghafla Talib alionyesha mabadiliko makubwa sana katika maisha yake, alianza kuwa msafi wa mwili na mavazi, alitumia muda mwingi kushinda nyumbani, pengine angetoka kidogo mchana na kurudi nyumbani, ambapo angesaidia kufanya kazi ndogo ndogo za pale nyumbani, kilichomfurahisha mjomba wake ni kitendo cha kushiriki swala zote tano pamoja na yeye, kwenye chumba ambacho kiliandiliwa kwaajili hiyo, mfano alfajiri na mapema angeamka na kuchukuwa udhu, kisha angeenda kugonga nyumba kubwa na kushiriki swala ya alfajil pamoja na mzee Mahamud shangazi yake na Soraya mwenyewe, pamoja na wafanya kazi wa mule ndani, mchana pia ingekuwa hivyo hivyo kwenye swala ya adhuhuri, hapo ange toka kidogo hakuna aliejua anakoenda, ila saa tisa na nusu angekuwa nyumbani anachukuwa udhu kwaajili ya swala ya alaasiri, ingekuwa hivyo swala ya magharibi na swala ya inshaa na kurudi chumbani kwake, ambako angejifungia kimya kabisa, huku muda wote ungesukia harufu nzuri ya manukat ya ubani au udi.
Ukweli Mahamud na mke wake walijikuta wanaanza kumuamini Talib na kumchulia kama kijana alieamua kubadilika, hivyo na wao wakaamua kuanza kumchukulia kama mwanafamilia wa kawaida, ambapo sasa ukiachilia kumruhusu kuingia nyumba kubwa kama zamani, pia alitumwa sehemu mbali mbali akitumia lile gari dogo aina ya Hyundai, yeye mwenyewe akiwa ni dereva, kamwe hakuacha kuswali na kuhudhuruia ibada ya ijumaa nakuzidi kuwa karibu na bwana Mahamud, ambae sasa alimueka karibu sana mtoto huyu wa shemeji yake, na kumshirikisha katika baadhi ya majukumu yake ya siri ikiwa ni pamoja na kwenda nae kwenye ukusanyaji wa fedha toka kwenye miradi mbali mbali,.
Kitu ambacho bwana Mahamud hakuwa anakijua ni kwamba, Talib alikuwa anakutana kwa siri na wakina Zido na Vitus, “vipi mipango inaendaje?” hilo lilikuwa swali la kila siku la Zido... Itaendelea……
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA MOJA : pia alitumwa sehemu mbali mbali akitumia lile gari dogo aina ya Hyundai yeye mwenyewe akiwa ni dereva, kamwe hakuacha kuswali na kuhudhuruia ibada ya ijumaa nakuzidi kuwa karibu na bwana Mahamud, ambae sasa alimuweka karibu sana mtoto huyu wa shemeji yake na kumshirikisha katika baadhi ya majukumu yake ya siri, ikiwa ni pamoja na kwenda nae kwenye ukusanyaji wa fedha toka kwenye miradi mbali mbali, Kitu ambacho bwana Mahamud hakuwa anakijua, ni kwamba, Talib alikuwa anakutana kwa siri kwa na wakina Zido na Vitus, “vipi mipango inaendaje?” hilo lilikuwa swali la kila siku la Zido... endelea……
Mara tu anapokutana na Talib, “mipango inaenda freshi, sasa anko ananiamini kinyama, mfano jana nilienda nae kwenye makusanyo na alijaza brief case mbili za mkwanja” alijibu Talib siku moja, “hapo sasa inabidi tuanze kupanga mchoni, tukizipata hizo mambo yatakuwa fresh kabisa” alisema Vitus akimtazama Talib ambae alikuwa anafakamia moshi wa bangi, ungesema hajaivuta kwa mwaka mzima, “lakini ana cha moto, anakuwa nacho kwenye gari” alitoa angalizo Talib, ambae ukimuona alikuwa ametakata na kuwa mng’aavu, sio yule wa mwaka mmoja uliopita, “hiyo haina shida tutaifanyia mchongo” alisema Zido.
Talib alitumia muda mfupi sana kuwepo pale kijiweni kwa kina Zido wakiongea mipango ambayo ilionyesha wazi kuwa walikuwa na mpango wa kumuibia mzee Mahamud, ambapo walianza kwa kumfanya Talib ajifanye amebadilika kitabia, ili aaminike kwa Mahamud, na baada ya hapo aanze kumchunguza mzee huyu mpaka ajue ratiba na michongo yake yote, ili iwe rahisi kumvamia na kumpora fedha nyingi atakazo kuwa nazo, na mwisho wa mipango yao Talib angevuta bangi nyingine pia angepewa nyingine ya kwenda kuvutia chumbani kwake, ambako uwasha ubani kwaajili ya manukato na kuondoa harufu ya bangi na sigara, wakati mwingine hata pombe alizokunywa kwa siri.*******
Siku zilienda, muonekano wa Hilda ulizidi kubadilika, na kuonekana sio mschana mdogo tena, alizeeka kwa kasi sana, mwili ulichoka na kukonda ilifikia kipindi alikosa hata fedha ya kumnunulia mwanae nguo nzuri na kumlazimu kuanza tabia ya kujirahisisha kwa wanaume ili wampe chochote ambacho kingemsaidia kuingia mtumbani kununua nguo za mwanae.
Tabia hiyo kiukweli ilimletea unafuu mdogo sana, katika maisha yake, japo fedha ndogo kama shilingi mia tano mpaka elfu mbili angeipata kwa kazi nzito ya kugeuka kidogo, inama binua makalio, binya tumbo lala hivi, kalia kwa juu na mwisho angeambulia shilingi hiyo mia tano na ikizidi sana mia nane au elfu moja, wakati mwingine angetangulizwa kwa offer ya ulanzi wa shilingi hamsini au mia moja na kumaliziwa na kupewa dudu, Hilda alizikumbuka fedha ndogo ndogo alizokuwa anapewa na Higgno bila mashariti yoyoye, ilifikia kipindi akawa anajiwazia kuwa kama ilikuwa lazima azae mapema ni bora angezaa na Higgno, maana yeye na mtoto wangepata matunzo, Hilda aliumia roho hasa alipomuona Hoggno akiwa anazidi kunawili na kupendeza, maana sasa licha ya kuwa alikuwa anasoma ufundi lakini alikuwa anapata kazi ndogo ndogo za watu walioleta magari yao pale gereji ya jimbo kuu la wacatoliki mkoa wa Ruvuma, kilicho msaidia Hilda ni kwamba hakuwahi kumuona Higgno akiwa na mwanamke kama mpenzi wake, ukweli alishukuru sana na hakupenda itokee siku amuone akiwa na mwanamke, Hilda alienda mbali zaidi akiombea Higgno asiwe na uwezo wa kuinua dudu yake, ili asije kupata mwanamke maishani mwake, kwasababu alihofia ataumia roho yake, huku yeye mwenyewe Hilda akiendelea kuvizia na kujirahisisha kwa wanaume ambao wengi wao walikuwa ni walevi wa pombe za kienyeji na waume za watu.
Tabia hii ya Hilda haikuchukuwa hata miezi miwili, akiwa tayari ameshatembea na wanaume zaidi ya kumi, Hilda alianza kuhisi maumivu makali na miwasho sehemu zake za siri, ikifuatiwa na maumivu chini ya kitovu, yaani karibu na kinena, na alipoanza kutoa maji ya njano mazito yenye harufu mbaya akaamua ajisalimishe Hospital, hebu ona alivyo Hilda.
Ukweli alienda dispensali ya pale mtaani na kukosa matibabu ya tatizo lake, akashauriwa aende hospital ya Jimbo kuu, angeweza kukutana na mdoctor wazuri wa tatizo lake la njia za uzazi, ni kweli hakuwa na fedha ya kuendea mjini, wala fedha ya kulipia matibabu, lakini hakupaswa kwenda kwenye kilabu cha ulanzi na kujirahisisha kwa mwanaume ili apate fedha hiyo, ambapo bahati ilikuwa upande wake na alijitokeza mmoja ambae alimnywesha pombe aina ya ulanzi, (bamboo juice) na mida ya saa nne za usiku walipokuwa wanarudi majumbani mwao, wakachepuka kidogo na kuingia kwenye shamba moja la jirani na barabara kisha wakapeana dudu.
Hilda akiwa kati hali ile ile iliyomfanya aende hospital, akakubali kutoa kitumbua kwa mlevi yule, ambae alishajua kuwa mwisho wa siku anatakiwa kutoa kiasi cha fedha ambacho katika makubaliano yao ilikuwa ni mia tano, ambayo ingemsaidia Hilda kwenda na kurudi mjini na kukata kadi ya matibabu, mlevi hakujua kama kule anakoingiza dudu yake kulikuwa kumeungua vibaya sana, na yale maji maji aliyokuwa anayasikia yakitelezsha dudu yake sio ute ute aliouzoea kwenyye kitumbua cha mke wake, ila ni usahaa ambao uliambatana na maumivu makali kwa Hilda, ambae licha ya kuwa alikuwa amekunywa pombe kiasi fulani lakini aliweza kuhisi maumivu hayo, ambayo hakuwa na budi kuyavumilia ili afanikiwe kuondoka na mia tano, ambayo inge msaidia kutatua shida yake hapo kesho.
Naam siku ya pili ilikuwa siku ya ijumaa, Hilda akalazimika kwenda hospital ya Jimbo kuu la katoliki mkoa wa Ruvuma, na baada ya kuchukuliwa maelezo na vipimo akagundulika ana muunganiko wa magonjwa ya zinaa, (sexual deseas combination), katika sehemu zake za kike, ambayo yalikuwa yamesha muathiri kwa kiasi kikubwa sana, doctor akamuandikia sindano tano, na dawa za kuzuia mamivu, na Hilda alipoenda kwenye dirisha la malipo akatajiwa gharama kuwa ni shilingi elfu nne na mia tatu, kwa kipindi hicho ungeifananisha na elfu alobaini au zaidi kwa fedha ya sasa, ambapo kiukweli gharama hiyo Hilda asingeiweza kabisa kuilipa.
Basi kwa unyonge Hilda akatoka nje ya Hospital, na kusimama akitazama upande wa barabara, akiwaza ataenda kupata wapi hela ya kununua dawa na sindano ili apone lile tatizo lake, ambalo doctor alimueleza kuwa anatakiwa kupata matibabu ya haraka sana, vinginevyo angeendelea kuathirika mpaka sehemu za ndani kabisa na pengine kutolea kabisa kizazi, na ukweli kabisa yeye alikuwa amebakiwa na shilingi mia tatu hamsini,
Wakati Hilda anaendelea kuwaza, huku amesimama pale nje ya hospital mara akamuona Higgno, akiwa na wenzake wawili wanapita pale mbele ya Hospital wamevalia nguo za ufundi wakionyesha wanaenda kupata chai, maana walikuwa wanalekea kwenye kimgahawa fulani kidogo pembeni ya Hospital ile ambayo ipo maeneo yale yale ya jimboni, “Higgnooo” Hilda alijikuta akiita kwa sauti ya juu, kiasi cha kuwashtua hata wagonjwa na watu wengine waliokuwepo pale hospital wanasubiri kupata huduma.
Naam Higgno na wenzake wakageuka kumtazama muitaji, na hapo ndipo macho ya Higgy Wizzy, yaliyojawa na mshangao ya kakutana na macho ya Hilda yaliyokata tamaa. itaendelea……

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA TATU
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI : Wakati Hilda anaendelea kuwaza, huku amesimama pale nje ya hospital mara akamuona Higgno, akiwa na wenzake wawili wanapita pale mbele ya Hospital wamevalia nguo za ufundi, wakionyesha wanaenda kupata chai, maana walikuwa wanalekea kwenye kimgahawa fulani kidogo pembeni ya Hospital ile ambayo ipo maeneo yale yale ya jimboni, “Higgnooo” Hilda alijikuta akiita kwa sauti ya juu, kiasi cha kuwashtua hata wagonjwa na watu wengine waliokuwepo pale hospital wanasubiri kupata huduma. Naam Higgno na wenzake wakageuka kumtazama muitaji, na hapo ndipo macho ya Higgy Wizzy, yaliyojawa na mshangao, yakakutana na macho ya Hilda yaliyokata tamaa. endelea……
Higgno Frank akasimama na kumtazama Hilda, huku wenzake wakiendelea kutembea kuelekea kule mgahawani, Hilda ambae hata kutembea kwake kulikuwa kwa shida kutokana na mumivu makali kwenye kinena, alivuta hatua kumfuata Higgno aliekuwa amesimama barabarani akimtazama kwa macho ya mshangao yaliyojaa huruma kwa jinsi alivyotembea kwa shida kuja pale alipokuwa yeye, huku uso wake akiulazimisha kuuwekea tabasamu, huku moyoni akijiuliza jinsi gani Higgno ataweza kumsemesha kutokana na yale aliyowahi kumfanyia wakati ule, maana hawakuwahi kuongea tena toka kipindi kile, “mambo Higgy” alisalimia Hilda, mara baada ya kumfikia Higgno, huku anatazama chini kukwepesha macho yake yasikutane na macho ya Higgno, “safi tu, vipi umemleta mtoto hospital?” aliuliza Higgno, ambae hakuonyesha dalili yeyote ya kwamba alishawahi kutendewa uovu na mschana huyu, “hapana mtoto nimemuacha na bibi yake nyumbani nimekuja mwenyewe naumwa” alijibu Hilda ambae bado hakuweza kumtazama Higgno usoni kutokana na aibu, “pole sana, unaumwa nini mpaka umekuja huku mbali si ungetibiwa kwa masister pale matogoro?” aliuliza Higgno huku akijaribu kumtazama vizuri mschana huyu ambae alikuwa ajamuona kwa karibu karibia miaka minne iliopita, maana toka wakiwa kidato cha kwanza, ukweli alikuwa amebadilika sana, yaani amechoka kiasi cha kwamba ingefaa awe dada wa tatu kuzaliwa mpaka kuja kwake kwa uzee aliokuwa nao Hilda, “tumbo na vipele, mwenzio maji ya kule mtoni hayanipendi” alijibu Hilda, sasa akianza kuchangamka na kujaribu kumtazama Higgno usoni, “pole sana, kwahiyo umeshatibiwa” aliuliza Higgno ambae kwa kiasi fulani alijiona kama amerejeshewa thamani yake ambayo ilipoteaga miaka mingi iliyopita, “nimeonana na doctor, ameniandikia sindano na dawa sasa hela jaitoshi, inatakiwa shilingi elfu nne na mia tatu na mimi nina mia tatu hamsini tu!” alisema Hilda, ambae alikuwa anaombea utokee muujiza na Higgno atoe hiyo fedha, “hoo kumbe hizo dawa zina bei kubwa” alisema Higgno huku anaingiza mkono mfukoni na kutoa kibunda cha noti za shilingi elfu moja moja na elfu mbili mbili, akachambua kidogo na kutoa noti tano za elfu moja moja, huku Hilda akitoa macho ya kutazama fedha zilizojaa mkononi kwa Higgno, “utanunua hizo dawa” alisema Higgno huku anamkabidhi Hilda ile elfu tano, ambae aliipokea akiwa haamini macho yake, hata Higgno alipoondoka hakuwa na habari, hakukumbuka hata kusema asante.
Hilda alinunua dawa nakuondoka pale hospital akiwa amechoma sindano ya kwanza, huku wakimueleza kuwa atafute dispensali ya karibu awe anachomea sindano, maana asingeweza kuja kuchoma sindano kila siku huku mjini, njia nzima aliwaza kile alichokiona kwa Higgno, ukweli alitamani kuwa karibu na Higgno, na ni lazima awe karibu na Higgno, kijana mwenye moyo na upendo wa kipekee, mvulana pekee aliyeonyesha mapenzi ya dhati kwake toka wakiwa wadogo mpaka leo hii anapo mkabidhi fedha nyingi kama hii kwaajili ya matibabu yake, alishindwa kumfananisha na mwanaume mwingine, akizingatia jana amelazimika kutoa kitumbua wakati anaumwa kwa malipo ya shilingi mia tano, wakati Higgno amemkabidhi mara kumi ya ile bure kabisa.
Hilda aliona njia pekee ya kuwa karibu na Higgno ni kumfuata pale Mgahawani na kuweka ahadi ya kukutana, hivyo Hilda alipitia pale mgahawani na kweli alimkuta ndio anamaliza kunywa chai tayari kurudi kazini, “sasa Higgno mimi .. mimi na ..naenda” aliaga Hilda kwa sauti ya kusita sita, akionyesha kuna jambo anahitaji kuongea, “sawa panda daladala, sisi ndio tunajiandaa kurudi gereji” alisema Higgno, huku anainuka na kuanza kumsindikiza Hilda, maana hakutaka wale wenzake wajue lolote kuhusu yeye na Hilda, ukizingatia Hilda alikuwa katika muonekano wa hovyo hovyo sana, hakupendeza machoni pa watu, “lakini Higgy, nilitaka kuuliza kama leo utarudi mapema nyumbani” alisema Hilda kwa sauti ya kujaribu, maana hakuwa na uhakika kama Higgno atalikubali swala hilo, nitachelewa kidogo, maana nitapitia mazoezini, labda kwenye saa moja moja nitakuwa nyumbani” alijibu Higgno, ambae hakuhisi chochote kibaya mbele yake, “basi ukirudi tu nitakuja” alisema Hilda huku anaachia tabasamu la furaha, ukinikosa dukani nitakuwa ndani kwangu, siku hizi nakaa kwenye yake mabanda ya uwani” alifafanua Higgno pasipo kujua madhara yake, japo Hilda hakuwa na nia mbaya alipoomba kwenda kwa Higgno.********
Naam mida ya saa nane za mchana, nyumbani kwa tajiri mwarabu Mahamud, yeye na familia yake, wakiwa wamesha swali adhuhuri, mzee Mahamud alijiandaa kwaajili ya kuanza kuzungukia ofisi zake kwaajili ya kukusanya mapato ya siku ile na ya jana jioni, “Talib yupo wapi, naona muda wa kuanza mipango umewadia” alisema mzee Mhamud, “mh! atakuwa chumbani kwake, maana alisema anajisikia kichwa kinamuuma” alijibu Soraya, ambae sasa alikuwa amesha maliza kidato cha sita, anajiandaa kwenda chuo kikuu baada ya kufaulu vizuri, “hoo! kumbe mbona hakuniambia mapema!? nilijua nina kampani kumbe leo nitakuwa peke yangu” alisema mzee Mahamud na kutoka zake nje, na dakika chache baadae likasika gari likiondoka.
Soraya akaingia chumbani kwake kwaajili ya kuangalia filamu kama kawaida yake toka akiwa mschana mdogo, lakini wakati anaingia chumbani kwake alitazama dirishani na kumuona Talib anatoka haraka na kuelekea upande wa mbele wa nyumba kubwa kwa mwendo wa kuvizia, “huyu baradhuli si alisema anaumwa kichwa sasa anaenda wapi?” alijiuliza Soraya huku anatoka haraka chumbani kwake kwa lengo la kwenda kumshushua binamu yake huyu, ambae kwa macho alionekana amebadilika kitabia,
Lakini hakuwahi kumkuta maana ile anatokea mlango mkubwa akaliona Hyundai ndio linatoka getini, “ana maana gani kukataa kuongozana na baba?” alijiuliza Soraya huku anarudi chumbani kwake.*******
Ni kweli mashaka ya Soraya yalikuwa ya kweli, maana Talib aliendesha gari kwa speed akiifuata barabara ya mbinga, na alipofika njia panda ya mwembe chai akakata kona kulia akiingia mtaa wa mwembe chai na kuifuta barabara iendayo matarawe na baada ya kutembea kwa mwendo wa mita mia mbili na nusu, aka kata kona kushoto akiingia na kuvuka nyumba mbili na kusimama kwenye nyumba ya tatu pembeni ya Toyota crester, akashuka na kuingia ndani upande wa uwani, “umechelewa Talib” alisema Zido mara baada ya Talib kuingia na kumkuta Zido akiwa na wakina Vitus na wale vijana wengine wawili aliokuwa nao siku ile kule RMA huku wana vuta bangi, “si unajua hii ni mida ya mkeka” alisema Talib huku anakwatua vidole vyake, ikiwa ishara ya kuomba apewe ile bangi na yule kijana akafanya hivyo, “ok! lete mchongo” aliuliza Zido, na hapo Talib akapiga pafu moja la bangi na kuuzuia moshi kwa sekunde kadhaa, kisha akaruhusu utoke, nao ukatoka kiasi kidogo sana tofauti na alivyo uvuta, “anko amesha toka home, nyie mukamvizie stendi ya msamala kwenye hii barabara ya juu” alisema Talib kwa sauti fulani ya puani kama anazuia moshi uliobakia usitoke mdomoni kwake, “mida gani” hapo ni kwenye saa tisa tisa hivi, maana lazima awahi alaasiri” alisema Talib kisha akavuta tena bangi na kuipiga mkupuo mmoja mreefu kabla hajarudisha bangi ya watu, “sasa nipe inshu niwahi home maana nimewaambia naumwa” alisema Talib ambae alipewa kete mbili za bangi zilizo kuwa zimesha sokotwa, kisha akaondoka zake kuwahi nyumbani akiwa amesha muuza mjomba wake kwa kete mbili za bangi.*****
Nyumbani kwa mzee Komba mambo yalikuwa moto moto, ni baada ya Hilda kufika nyumbani akiwa na mafungu mawili ya dagaa na baadhi ya viungo vya kuungia mboga hiyo ambavyo vilinunuliwa kwa fedha iliyobakia kwenye ile fedha aliyo pewa na Higgno, “mwenzetu vipi umepata buzi gani leo” aliuliza mama Hilda wakati wanaendelea kupika na mume wake akiwa amekaa kwenye mkeka anacheza na mjukuu wake huku anawasikiliza mwanae na mke wake, “Higgno huyo amenipa elfu tano” jibu la Hilda liliwashtua mama Hilda na mume wake yaani mzee komba, “unasema Higgno huyu huyu wa Frenk wa dukani?” aliuliza mama Hilda kwa mshangao, “ilikuwaje mpaka akakupa hela zote hizo?” aliuliza mzee Komba kwa mshangao, na Hilda akawasimulia ilivyo kuwa huku baadhi ya mambo akificha kama sababu za ugonjwa wake, japo kwa ufahamu wa wazazi wake walitambua tatizo nini, “unajua mama Hilda yule kijana ndie aliekuwa anampenda Hilda toka moyoni, sijui kwanini tulizuzuka na lile vuta bangi ambao halina cha utajiri wowote, halafu kumbe linakaa kwa shangazi yake” alisimanga mzee Komba, “kwahiyo umemwambia utaenda baadae, lakini si unaumwa wewe” alisema mama Hilda, yaani mke wa mzee Komba akiamini kuwa mwanae anaenda kutoa asante ya kitumbua kwa Higgno, “siendi kufanya chochote mama, kwani mtu mwenyewe hajaniambia kama ananitaka” alisema Hilda huku yeye na mama yake wanaendelea kupika na mzee Komba anacheza na mjukuu, “lakini mwanangu kusema ukweli Higgno unampenda sana” alisema mama Hilda, “lakini yeye mwenyewe ndie alienipa hela” alisema Hilda ambae aibu ilisha potea maishani mwake.
Maongezi yakaendela kwa muda fulani, huku mzee Komba akiwa kimya kama vile anawaza jambo fulani kabla hajasema “mama Hilda nadhani hii ndiyo nafasi pekee ya Hilda akaolewe na Higgno” alisema mzee Komba kama vile ameamka toka usingizini, “baba hilda bwana ndio kwanza watoto wanaanza kusemeshana, ndio unafikiria ndoa” alisema mama Hilda, huku Hilda akiombea kama ni ndoto ya baba yake basi naiwe kweli, tukisubiri mpaka wapange wenyewe tutachelewa” alisema mzee Komba akionyesha amepatia kweli kweli wazo lake la kuwa Hilda na Higgno wafunge ndoa, “lakini unadhani mzee Frank na mama Higgy watakubali kwa yale tuliyo wafanyia kipindi kile?” aliuliza mama Hilda kwa sauti ya kukata tamaa, “ndio maana nakueleza kuwa tukisema tusubiri wapatane wenyewe tutachelewa” alisema mzee Komba na kuahidi kuwa atawapa mpango kamili, chamsingi ni kwamba wampe shilingi mia tano tu!.
Mbele ya kuolewa na Higgno Hilda akatoa shilingi mia tano na kubakia na shilingi mia mbili tu, ikiwa ni hela ile ile ambayo alipewa na Higgno.******
Soraya akiwa chumbani kwake anatazama movie, huku anawaza kwanini binamu yake Talib alikataa kumsindikiza baba yake kwa kisingizio cha kuwa anaumwa na muda huo huo akatoka, mara akasikia sauti ya vishindo vya mtu upande wa nyumba za nje, nikule anakokaa Talib, Soraya akachungulia dirishani na kumuona Talib akitembea vizuri tu tofauti na mwanzo alipokuwa anatoka, alitembea kwa kuvizia na wasi wasi mwingi,
Soraya alimtazama binamu yake Talib na kumuona akiingia ndani mwake na kurudisha mlango, na sekunde chache baadae ikaanza kusikika harufu ya ubani ikitokea kwenye ile nyumba ya Talib, “mh sio bure huyu ana kitu anakifanya” aliwaza Soraya ambae akiwa chumbani kwake huwa anaondoa nguo zake zote na kubakia na gauni jepesi tena bila hata nguo ya ndani, labda angevaa pindi anapoenda kushiriki swala.******
Saa tisa na robo ndio muda ambao Higgno alikuwa amesha toka gereji anaeleka mazoezini kule jeshini, akipanda dala dala za msamala ili akashukie msamala sheri, kisha kupita njia ya mkato ya pembezoni mwa mlima chandamali na kuibukia kwenye ukumbi wa mazoezi, maana hiyo ndiyo ilikuwa njia yake ya kila siku.
Sasa Higgno alikuwa amesha shuka kwenye daladala anatembea taratibu kuifuata barabara ya vumbi iendayo stendi kuu ya msamala ikipitia nyuma ya kituo cha mafuta, na yeye angeachana nayo mita kama mia tano mbele na kufuata barabara ya kuelekea jeshini, wakati anaipita sheri akakutana na gari moja dogo aina ya Toyota Crester likiwa limeegeshwa pembeni ya barabara ile ya vumbi, milango ya gari ilikuwa imefungwa ila vioo vilishushwa nusu, ambavyo viliruhusu moshi wenye harufu ya bangi kutoka na kusambaa eneo lile la barabara ambalo Higgno alikuwa anakatiza.
Higgno akavutiwa na kugeuza shingo kutazama ndani ya gari lile pengine angeona watu waliopo mule ndani, ni kweli alifanikiwa kuwaona watu wawili ambao walikuwa busy na mambo yao ya uvutaji bangi, “huyu jamaa bado anavuta bangi tu!?” alijiuliza Higgno mara baada ya kumtambua mmoja wao, ambae alikuwa ni Vitus, ambae ni wazi kabisa hakumuona maana alikuwa busy na bangi lake,
Licha ya kukumbuka kile walichomfanyia miaka zaidi ya mitano iliyopita lakini Higgno akaachana nao na kuendelea na safari, maana KARATE inasema pigana kwasababu za msingi ikiwa ni kujiokoa na kifo au kuokoa, “sijui wanasubiri nini hawa washenzi” aliwaza Higgno huku anaendelea na safari yake.
Yap! Higgno alitembea taratibu kwenye barabara ile ya vumbi yenye vichaka pande zote, huku upande wa kulia ukiwa umeungana na msitu wa mlima wa chandamali, huku anakumbuka ambavyo wakina Vitus na Talib wakiwa na wakina Hilda na Joan pamoja na wenzao wawili jinsi walivyo msababishia ajari ya baiskeri na kumpiga vibaya sana pasipo kosa lolote, kumbukumbu hizi ambazo zilimjia mara tu baada ya kumuona Vitus, ilimkumbusha machungu aliyoyasahau ya kuibiwa rafiki yake na Talib, na kama haitoshi mzee Komba yaani baba yake Hilda, alikuja na kuwasimanga yeye na baba yake, akiwashutumu kuwa wanajifanya matajiri wakati kuna matajiri wakubwa na hawajisikii kama wao,
Sasa basi wakati Higgno anatembea huku anawaza hili na lile, akiwa anakaribia njia panda ya kwenda jeshini na ile ya kwenda stend kuu, mara akaliona gari moja aina ya Nissan Patrol likija mbele yake taratibu umbali kama wa mita mia moja hivi kutokea njia ya stendi kuu, huwa analifahamu gari lile kuwa ni la tajiri mwarabu Mahamud, ambae ilisemekana kuwa ni mjomba wake Talib, tajiri ambae binafsi Higgno hakuwahi kumuona mtoto wake hata mmoja, tajiri ambae Higgno na vijana wengi wenye ndoto kama zake ni kufanyia kazi kwenye magari yake ya kusafirisha mizigo au abiria yaendayo mikoa mingine na jijini dar es salaam,
Wakati Higgno awaza hilo mara aliona gari lile ambalo lisha msogelea na kubakiza umbali wa mita kama arobaini toka alipo yeye Higgno, mara Higgno akaliona lile gari likisimama ghafla na akaonekana mwarabu mwenyewe akishuka akitokea upande wa dereva na kuzunguka upande wa pili wa gari yaani upande wa kushoto na kuchungulia tairi la mbele, hapo akaonekana anajishika kichwa kwa huzuni huku ana tazama alikotoka halafu akalitazama tena tairi.
Kabla hajajua tatizo inaweza kuwa nini, mara Higgy Wizzy akashangaa kuona vijana wawili. wanatokea pembezoni mwa barabara upande wa kulia, yani kwenye msitu wa mlima chandamali, na kumfuata yule tajiri mwarabu, yaani Mahamud………. ITAENDELEA
 
Imeekaa pw sana,
 
Jion viwil vya moto
Sawa sawa mkuu, utakuwa umeupiga mwingi kama Mpanzu.😂😂😂😂

Harafu ikikupendeza niwekee picha ya Vitus, ulivomuelezea ni kama vile ninamjua kabisa.😅😂😅😂😅😂😅😂👍😅
 
Back
Top Bottom