SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Awamu ijayo unijumuishe NAMI , Mkali wa hizi kazi😂😂😂
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA TANO
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA NNE: “mzee mwenzangu maneno gani hayo tuna watia laana watoto hebu temea mate chini” alisema mzee Frank, ambae bado alionekana kuchukulia kama utani juu ya maongezi yale, “we fanya mzaha bwana Frank, lakini chonde chonde, mueleze mwanao aache kuvuta bangi” alisema tena mzee Komba kwa sauti ile ile ya jazba, “taratibu basi mzee mwenzangu, hebu tulia unieleze Higgy amefanya nini” Higgno akiwa ndani aliweza kumsikia baba yake akiongea kwa upole, “sikia bwana Frank, unajua kwa sasa huyu mwanao ameanza tabia fulani za ajabu” alisema mzee Komba na kutulia kidogo…..ENDELEA……
Kama alivyotulia mzee Frank kwa kumsikiliza mzee Komba ambae hapo mwanzo hawakuwa wana mazoea ya karibu kama sasa, ni kutokana na ukaribu wa wa watoto wao, yani Higgno na Hilda, “jana amemvamia Hilda na marafiki zake kwa lengo la kuwafanyia fujo, matokeo yake wame mtandika yeye” alisema mzee Komba na hapo Frank akataka kucheka kidogo, lakini akaishia njiani, “mzee komba, kwani Hilda na Higgy wana ugomvi, mpaka atake kumpiga?” aliuliza bwana Frank kwa mshangao, “unadhani bange ina sababu” alisema mzee Komba, hapo bwana Frank akatabasamu kidogo, ni jinsi mzee Komba anavyo ng’ang’ania swala la bangi, “kwahiyo mzee Komba unaamini Higgno anavuta bangi na yeye ndie alie wavamia wakina Hilda” aliuliza Frank kwa sauti ya upole, hata Higgno aliekuwa anawasikiliza kule chumbani akamsifu baba yake kwa busara alizo nazo, “kwahiyo mimi na kudanganya?” aliuliza mzee Komba akiona kuwa mzee mwenzie analeta kitu kama dharau, “ok! unaweza kuwa sawa, vipi kuhusu hao marafiki wa Hilda walio mpiga Higgno una wafahamu?” aliuliza mzee Frank, “kwahiyo mimi nashinda shuleni sikuhizi?” aliuliza kwa hasira mzee Komba, “unaona ee?, hapo una weza kuona kuwa mimi na wewe hatuwezi kujua kinachoendelea baina ya wawili hawa mfano mimi naweza kukuambia kuwa Higgno hawezi kuvuta bangi, wala hawezi kuwa na tabia za ugomvi pia naweza kusema kuwa hata wewe hujawahi kuona au kusikia hata siku moja Higgy akimfanyia fujo Hilda” alisema mzee Frank kwa sauti tulivu, “kwahiyo unataka kusema hilda ndie aliemvamia Higgno?” aliuliza mzee Komba kwa sauti ya dharau, “hapana sio Hilda, nadhani ni hao marafiki zake, ambao mimi na wewe hatujui kama ni wakiume au wakike” alisema mzee Frank kwa sauti ile ile ya upole iliyo jaa busara, lakini bado Higgno akaendelea kumsikia baba yake Hilda aking’ang’ania kuwa Higgno alikuwa mkorofi, “bwaheee! iwe marafiki wa kiume au wakike, lakini ifike pahala Higgno ajue kuwa kuna urafiki wa kitoto na urafiki wa ujana” alisema mzee Komba na kuanza kuondoka, akimuacha mzee Frank ana msindikiza kwa macho lakini hakufika mbali, mzee Frank akamsemesha tena, “lakini mzee mwenzangu tusisahau kuwa TEMBELE LA UWANI ndilo linalosaidia wakati wa njaa” alisema mzee Frank, ambae hakusubiri jibu lolote toka kwa mzee Komba, aka ondoka zake na kuelekea dukani kwake.******
Naam mida ya saa sita mchana, barabara ya RMA, maeneo ya kanga ulaya, (kipindi hicho), lilionekana Land Rover Discover likitokea upande wa songea girls secondary, na kukata kulia kuifuata barabara ya delax hotel na kuongeza mwendo kidogo, kama mita mia mbili mbele lika punguza na kukata kona kushoto kueleka kanisa la jimbo kuu la songea na bila kuongeza tena mwendo gari hili ambalo lenye vioo vyeusi vya tinted, lililo shushwa kioo kimoja tu cha mbele upande wa dereva mmoja wakike, alievalia nguo nadhifu za kike, yaani gauni refu na la maua maua ya kijani na njano, lenyewe likiwa jekundu, lilienda mita mia na kukata kona kulia, kufuata barabara ya soko kuu, na kabla halijafika, barabara inayo tenga nisha soko kuu na mtaa huu likakata tena kushoto na kusimama mbele ya gate moja kubwa la kuingilia kwenye nyumba moja kubwa sana ya kifahari, ambayo watu wengi hawakuwa wanajua kama ile nyumba ni ya mtu binafsi kwa ukubwa na uzuri wake.
Dereva yule wakike alipiga honi mara mbili mfululizo, yani “piii piii” na gate likafunguliwa na mlinzi mmoja alievalia sare za wanamgambo wa serikali, gari likaingia likipita kwenye barabara nzuri iliyo tengenezwa kwa sakafu nzito iliyo pakana na bustani nzuri ya maua na nyasi fupi, na kwenda kusimama mbele ya nyumba moja kubwa kando ya nyingine mbili ndogo zilizopo mule ndani ya uzio mkubwa wa ukuta watofari za saruji.
Hapo Dereva akashuka haraka na kuwahi kufungua mlango wa nyuma wa abiria, lakini kabla hajaufikia tayari ulisha funguliwa na hapo akashuka mschana mmoja alievalia gauni fulani refu lenye rangi ya kijivu na pindo yeupe kwa mbele, ilikuwa ni baiubui na viatu rangi ya dhahabu vya mikanda vyenye visigino virefu, sio utani kwa mwaka huu wa tisini na saba viatu hivi mara nyingi ungeviona kwenye video, au magazeti ya wazungu, maschana huyu alie valia kilemba cheupe kichwani mwake, mwenye muonekano wa wazi kabisa kuwa ni mtoto wa kichotara wa kiarabu, alishuka toka kwenye gari akiwa amekumbatia madaftari matatu aina ya counter book, (kipindi hicho unge muona nayo mtoto wa tajiri pekee, tena mwenye kupenda kusoma) na karamu mbili za wino, yule Dereva wakike alijaribu kupokea daftari toka kwa mschana chotara, mwenye urefu wa wastani, kifua cha wastani, kiuno chembamba na makalio makubwa ya wastani yaliyobebwa na mapaja manene kiasi, “hapana dada acha tu!” alisema yule mschana ambae alijaaliwa kuwa na uso wa duara wa yai, mashavu manene kiasi, ambayo yalikuwa na kijiuwanja fulani ambacho kila mtu mwenye nacho lazima awe na dimples anapo tabasamu au kucheka, macho yake ya duara aliyo kuwa anapenda kuyapaka wanja yalichangia sana uzuri wake, hata pua yake ambayo ukiiangalia ungejuwa wazi huyu nichotara kwa kuchongoka kwake kama walivyo wazungu wahindi au waarabu wenyewe, midomo japo ilikuwa ni midogo, lakini ilikuwa na lips pana ambazo ungeombea awe anakula ndizi au ice cleam ya vijifuko, “sawa dada, nitakuwa ndani ya gari kama utakuwa na safari yoyote” alisema yule dereva wakike kwa heshima na utii, hapo mschana huyu mrembo na mzuri akasimama na kumtazama dereva wake, kwa sura ya tabasamu, “dada Laylah, mimi sina safari nyingine we nenda kapumzike nyumbani, uje jumatatu saa mbili unipeleke tution” alisema mschana yule kwa sauti iliyojaa upendo.
Hapo Laylah, ambae hakuwa chotara ila ni mschana wa asili ya kiafrika, aliinamisha kichwa na kusema, “asante dada” kisha akingia kwenye gari na kwenda kuliegesha kwenye sehemu ambayo kulikuwa na magari mengine manne likiwepo Hyundai na Nissan patrol na Toyota Land Cruser, huku yule binti mwenye uzuri wa ajabu akiingia ndani ya ile nyumba kubwa na ile anavuka kizingiti cha mlango akapokelewa na mwanamke moja mtu mzima, “salaam aleikum” alisalimia yule mwanamke ambae tunaweza kusema, angeweza hata kuwa mama wa mschana huyu mrembo, “aleikum salam yaya Subira” aliitikia kwa sauti ya furaha yule mschana huku anavua viatu vyake na kuingia ndani ya nyumba ile akikanyaga zuria la sufi lenye rangi ya samawati, “karibu dada, pole na masomo” alisema huyu mama mtu mzima huku ana mpokea daftari na kuogozana nae kuelekea sebuleni, “asante yaya Subira” alisema yule mschana, na wakati huo huo akasikia sauti ya mwanamke mtu mzima ikitokea sebuleni, “mpaka najuta kukuchukuwa uje uishi hapa nyumbani” ndivyo alivyo sikika mama huyo toka sebuleni na huyu mschana mrembo pia alitokea sebureni na kumuona mama mmoja, japo alikuwa na miaka kama arobaini hivi lakini uzuri wake ulionekana wazi wazi, ila huyu alikuwa mswahili kabisa, sio chotara, aliekuwa amevalia baibui jeusi, “yaani nilidhania kuwa utasoma kwa bidii kwa kuwa unajua maisha ya baba na mama yako kule nyasa lakini ndiyo kwanza unajiingiza kwenye uvutaji wa bangi, wizi wa vitu na kwenda kuuza ili upate bangi, kweli we mtoto, hakika ukimaliza mtihani wako unaelekea nyasa, sito weza kukuacha uishi hapa” alisema yule mama akimueleza Talib aliekuwa amesimama mbele yake ameshika mikono yake kwa mbele na kichwa ametazama chini kama vile anasikiliza kwa umakini kabisa maneno ya shangazi yake, “mama Soraya, nadhani kumrudisha Talib Nyasa ni kuzidi kumtengenezea maisha magumu, tunaweza kuongea nae akabadilika, maana anaweza kunisaidia kusimamia biashara zetu kuliko kutumia watu baki” ilisikika sauti ya kiume yenye lafudhi ya kiarabu, ilikuwa ni ya mzee Mahamud aliekuwa anatokea kwenye korido la vyumbani, alikuwa ni mwarabu kabisa mwenye mwili wa wastani alievalia kanzu nyeupe na baraghashia mkononi, “salaam aleikum baba, salaam aleikum mama” alisalimia yule mschana mdogo na kwa sauti ya unyenyekevu, “aleikum salaam” waliitikia wote wawili, yani mzee Mahamud na yule mama wa Kiswahili, “kuna lolote unahitaji mwangu” aliuliza yule mama aliekuwa anamsema Talib, yani shangazi yake Talib, akimuuliza yule mschana mrembo mdogo mwenye umri kama wa Hilda Komba, “hakuna mama, mi naenda kupumzika tu!” alijibu yule binti kwa sauti iliyojaa staha, kisha akaelekea upande wa kolido la vyumbani, yani kule anakotokea mzee Mhamud, “ana lolote huyu, basi anaenda kujifungia chumbani kwake atazame picha (filamu) za kihindi” alisema mzee Mahamud huku ana cheka, wakati anapishana na binti huyu, “ujaniletea mkanda mpya” alisema yule binti kwa sauti ya kudeka huku anaelekea chumbani kwake, akiongozana na yaya Subira.
Huyu anaitwa Soraya Mahamud, mschana mwenye miaka kumi na sita, mtoto pekee wa tajiri Mahamud, alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya secondary ya waschana, ya songea, akuwa anajulikana kama alivyo kuwa anajulikana Talib, sababu akuwa mtembezi sana, shuleni alipelekwa na gari na dereva wake mpya Laylah, baada ya dereva wake wakwanza wa kiume, kuonyesha dalili za kumtamani binti huyu mdogo, hivyo Soraya mwenyewe akaomba kwa baba yake abadirishiwe dereva, na akirudi nyumbani ujifungia chumbani kwake akitazama filamu, upend asana filamu za kihindi.
Tabia ya kujifungia ndani na kukwepa arafiki, ilimsaidia Soraya, kuto kuwa na fikra za kuwa na urafiki na mwanaume, labda wange kuwa ni kutoka shule ya songea wavulana, ambao nikama washirika wao wakaribu, kwenye matamasha mbali mbali ya masomo na michezo, ata burudani, sukuzote mmoja ange mwalika mwenzie, na kujumuika pamoja, ukweli Soraya ambae licha ya kuvunja ungo, miaka miwili iliyopita, lakini akuwa na wazo wala hisia ya kuwa na mpenzi akimini kuwa hakuna mwanaume ambae angeweza kumpenda na kumjali kama wafanyavyo vijana wa kihindi anao washuhudia kwenye filamu zao, wote aliwafananisha na binamu yake Talib, ambae ukiachilia kesi za fujo zinazo kuja kutoka shuleni kwao ikiwepo ya uvutaji wa bangi, pia alikuwa na tabia ya udokozi wa vitu vya ndani, ambavyo huviuza ilikujipatia fedha za matumizi yake yasio na msingi ya wanawake na bangi.******
Likizo ilianza vizuri kwa upande wa Hilda, maana alipata muda mwingi sana wakukutana na mpenzi wake Talib na marafiki zao Vitus na Joan, hasa mida ya jioni, akiaga anaenda kujisomea na rafiki zake na kwenda kukutana na wezake, maeneo ya uwanja wa zima moto, ambako upata starehe zao za vilevi vya bangi, na pengine wangepitia makutano kupata ulanzi mpaka saa mbili za usiku, hapo Hilda angebeba mishkaki kumi na kuelekea nyumbani akiwa na shilingi mia mbili ya ulanzi wa wazazi wake na kijitabu chochote cha simulizi za mapenzi, lakini hapo anakuwa tayari amesha ingia kwenye kichaka chochote cha karibu kupewa dudu na mpenzi wake Talib, maana toka ameanza mahusiano na kijana huyu hakuwahi kupewa dudu kitandani au sehemu yoyote tulivu kama chumbani, zaidi ya kwenye vyoo vya shule mashamba ya mahindi na sehemu nyingine kama hizo, Hilda akiwa ana jituma kutoa kitumbua kwa juhudi zake zote na kufanya yale anayoambiwa na Talib, hasa baada ya kuambiwa kuwa kijana huyu akimaliza shule, atakuwa msimamizi wa biashara zote za mzee Mahmud.
Nyumbani Hilda angeingia saa tatu kasoro au saa tatu na dakika zake na angepokelewa vizuri na wazazi wake ambao walikuwa wanajitapa mtaani kwa kuwa na binti mwenye bahati ya kuwa na urafiki na watoto wa matajiri.
Ilikuwa tofauti kwa Higgno, yeye aliona dunia inazidi kuwa ndogo, maana vijana wenzake walisha sikia habari ya kupigwa na mpenzi mpya wa Hilda, Higgno akiwa hatamani kuonekana mtaani, pia hakutamani shule ifunguliwe, maana alihofia mambo mawili, moja ikiwa ni kukabiliana na aibu ya kutandikwa na wakina Talib, pili endapo wakina Talib watahitaji kumtandika tena, Higgno aliona siku za likizo zinakimbia sana na siku ya kufungua shule inakuja kwa kasi, kwa kifupi eneo la shule aliliona chungu, na hata mtaani alipaona pachungu.
Higgno alianza tabia ya kutoka mida ya jioni na kwenda eneo la viwanja vya michezo vya jeshi la ulinzi, lililopo pembezoni mwa mlima wa chandamali, ambapo kulikuwa na michezo mbali mbali ya mpira wa miguu na mpira wa kikapu, hapo ange tazama mpaka saa kumi na mbili, na kurudi kwao Luhuhila, akipita pembezoni mwachuo cha ualimu cha matogoro.******
Naam! zikiwa zime bakia week mbili kufungua shule, Higgno akiwa anaelekea kwenye viwanja vya jeshini akakutana na mwanafunzi mwenzake wa Luhuwiko sekondary, japo hakuwa ana mazowea ya karibu na mwanafunzi huyo wa kiume ambae alikuwa kaka mkuu pale shuleni lakini alimsalimia kwa heshima pasipo kujali kama yeye hakuwa anamfahamu au laa, “hoo dogo, kumbe unaishi huku” alisema Yohane Kihiwili, ambae alikuwa amevalia kimichezo, yaani track ya chini na tishet juu, “hapana sikai huku, nakaa Luhila seko, vipi kwani unanifahamu?” aliuliza Higgno kwa sauti ya mshangao, “nakufahamu, wewe si ndie uliepigwa na Talib kwaajili ya kale kademu kavuta bangi?” aliuliza Yohane na swali hilo lilimshangaza na kumtia simanzi Higgno, hakutegemea kama ile habari ingesambaa kiasi kile, “dogo unataka nikusaidie mbinu za kuepukana na uonevu kama huo” aliuliza Yohane, wakati wanatembea kulekea jeshini, “braza Yohana ukifanya hivyo utanisaidia sana” alisema Higgno, na hapo Yohane mwanafunzi wa kidato cha nne, ambae alikuwa anaenda pale jeshini kuungana na baadhi ya askari ambao walikuwa wanajifunza sanaa ya mapigano kwenye bwalo la maaskari.
Na hayo yakawa ndiyo maisha mapya ya Higgno, sasa kila jioni alikuwa anaenda jeshini kufanya mazoezi ya ngumi, ikiwa ni Gou ju liu, (kwa kikorea) kama wajapan wanavyoita KARATE, au wachina wanavyoita KUNG FU, kwa maana ya kujilinda na kuuwa kwa kutumia mikono na miguu, Higgno alifanya hivyo hata wakati shule ilipofunguliwa, alipotoka shule alipitia moja kwa moja jeshini akiwa na Yohane ambae alikuwa ni mmoja wa wakufunzi wa sanaa hiyo ya mapigano yani Sen Sei (kwa kijipan), ambae alijitahidi kutumia uwezo wake wote kuhakikisha kijana Higgno ana wiva katika mafunzo hayo ya mapigano.******
Week tatu baada ya kufungua shule, wanafunzi wote wakike walipelekwa kwenye zahanati ya jeshi la ulinzi kwaajili ya kupima ujauzito, ikiwa ni utaratibu uliowekwa na shule hiyo mara wanafunzi wanapotoka likizo, na siku tatu mbele ndipo majibu ya vipimo hivyo, yalivyoletwa na kusomwa mbele ya wanafunzi wote pale shuleni…………….tuwemo katika sehemu inayofwata kujuwa nini kilitokea, mambo yanazidi kunoga taratiiiibuu bwana higg wizi anajifunza karatee shuleni wamepima mimba, comment yako like yako ndio itanipa hamasa ya kulete muendelezo hapa hapa jamii forums
 
Kaz nzuri mkuu
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SITA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA TANO: Higgno alifanya hivyo hata wakati shule ilipofunguliwa, alipotoka shule alipitia moja kwa moja jeshini akiwa na Yohane ambae alikuwa ni mmoja wa wakufunzi wa sanaa hiyo ya mapigano, yaani Sen Sei (kwa kijipan), ambae alijitahidi kutumia uwezo wake wote kuhakikisha kijana Higgno ana wiva katika mavunzo hayo ya mapigano.******Week tatu baada ya kufungua shule, wanafunzi wote wakike walipelekwa kwenye zahanati ya jeshi la ulinzi kwaajili ya kupima ujauzito, ikiwa ni utaratibu uliowekwa na shule hiyo, mara wanafunzi wanapotoka likizo na siku tatu mbele ndipo majibu ya vipimo hivyo yalivyoletwa na kusomwa mbele ya wanafunzi wote pale shuleni………ENDELEA…….
Na kati ya wanafunzi wakike mia moja na arobain na sita, wa shule hii ya Luhuwiko ni mschana mmoja tu aliekutwa na ujauzito wenye miezi miwili, “kutokana na sheria za shule hii Hilda Komba sio mwanafunzi wetu tena, amefukuzwa shule, na iwe fundisho kwa wanafunzi wengine” alisikika mwalimu mkuu,l aliesimama mbele ya mkusanyiko wa wanafunzi wote wa Luhuwiko sekondari, “na hili liwe fundisho kwa wanafunzi wengine ambao wanashiriki ngono” alisema yule head master alieonekana wazi kuwa ni mwanajeshi kwa sauti ya ukali.
Taarifa hii ilimuumiza sana Higgno, ambae alikuwa anaamini kuwa ipo siku Hilda angerudi kwake, tena aliamini kuwa sikucahe zijazo, ni mara baada ya Talib kumaliza shule, “lakini sasa kama amesha pata mimba si ndio mwanzo wa kuishi pamoja” mawazo hayo yalimjia Higgno, mara kwa mara akiwa njiani anaelekea jeshini kwenye mazoezi.*****
Hilda baada ya kusomewa hukumu yake ya kufukuzwa shule, aliingiwa na simanzi kubwa sana, moja kuwa na ujauzito, ambao aliamini unaweza kuwa chanzo cha kuachana na Talib, pili kufukuzwa shule, ingekuwa aibu kubwa kwake na wazazi wake, tatu alihofia kuchekwa na Higgno, lakini mara baada ya kukutana na Talib ambae alimuonya asimtaje pale shuleni kuwa yeye ndio muhusika na kumuaidi kuwa akimaliza shule na kukabidhiwa biashara na mjomba wake atamchukuwa na kuishi nae, hapo Hilda alianza kupata furaha na faraja, ongeza bangi na ulanzi, akasahau kabisa kuwa kuna jambo limemkuta shuleni, hata alipofika nyumbani, Hilda aliwanunulia ulanzi wazazi wake ambao walisha zoea swala hili kila siku.

Na wakati wanaendelea kunywa ulanzi, ambao siku za hivi karibuni walisha anza tabia ya kunywa pamoja na binti yao, ndipo Hilda alipoanza kuwasimulia kilicho mtokea.******
Naam saa tatu na nusu, ndio muda ambao mzee Frank akiwa na mwanae Higgno, walikuwa wanafunga duka ili waingie ndani, mara wakamuona mzee Komba anaingia pale nyumbani kwao, nao wakashangaa kumuona mzee huyu nyumbani kwao, “mh! ananini huyu bwana halafu amelewa vibaya sana” aliuliza mzee Frank kwa sauti ya chini, huku yeye na mwanae Higgno wakimtazama kwa tahadhari wakati huo Higgy Wizzy aliekuwa anajua tukio lililo mtokea Hilda, akiwa ana jiuliza mzee Komba amekuja kufanya nini, isije kuwa Hilda amemsingizia yeye ndie aliempa mimba, ……….. endelea

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA SABA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA SITA: Naam saa tatu na nusu, ndio muda ambao mzee Frank akiwa na mwanae Higgno, walikuwa wanafunga duka ili waingie ndani, mara wakamuona mzee Komba anaingia pale nyumbani kwao, nao wakashangaa kumuona mzee huyu nyumbani kwao, “mh! ana nini huyu bwana halafu amelewa vibaya sana” aliuliza mzee Frank kwa sauti ya chini, huku yeye na mwanae Higgno wakimtazama kwa tahadhari, wakati huo Higgy Wizzy alie kuwa anajuwla tukio lililo mtokea Hilda, akiwa ana jiuliza mzee Komba amekuja kufanya nini, isije kuwa Hilda amemsingizia yeye ndie aliempa mimba, endelea…….
“mbona mnafunga mapema duka au mme ridhika na visent mulivyo vipata?” aliuliza mzee Komba kwa sauti ya kilevi iliyo jaa jeuri na dharau, hapo Higgno na baba yake wakatulia kimya wakimtazama mzee Komba, “we dogo hebu nipatie sport mbili, alisema mzee Komba, huku akimpatia Higgno shilingi thelathini, kwa mgao wa sarafu ya shilingi ishirini moja na shilingi tano tano mbili, Higgno alimtazama baba yake, ambae alimuonyesha ishara kuwa aende akamchukulie, nadhani mzee Frank alichelea kusemewa vibaya na mzee Komba, maana toka siku ile alipomjia asubuhi kumshtakia Higgno urafiki wao ulipotea hapo hapo, Higgno akapokea ile fedha na kuelekea kwenye mlango wa duka na kuufungua, “unajua bwana Frank, sisi masikini huwa tuna ridhika z na vitu vidogo sana, mfano wewe saizi unafunga duka wakati watu kama wakina Mahamud ndio kwanza kama kuna kucha” alisema mzee Komba kwa sauti ambayo kama ungekuwepo na kuisikia ungejua ni mtu mwenye fedha na uwezo mkubwa wa kiuchumi, “ni kweli kabisa, bwana Komba, lakini sasa unawezaje kukesha wakati wateja wenyewe wamesha lala” alisema mzee Frank kwa sauti tulivu.
Mzee Frank akamsikia bwana Komba anaguna huku anatikisa kichwa kwa maskikitiko, “hizo ni dharau bwana Frank, inamaana mimi sio mteja?” aliuliza mzee Komba kwa sauti ya kilevi iliyoonyesha kusikitishwa, huku bado anatikisa kichwa kwa masikitiko na kufanya kama vile mtu anaita paka aje kukuchukua chakula, “sina maana hiyo Komba, na maanisha watu wengi wanakuwa wamelala” alirekebisha kauri yake mzee Frank, wakati huo Higgno alikuwa anatoka dukani akiwa na sigara mbili aina ya sport mkononi mwake, akampatia mzee Komba, “unaona dharau nyingine hii, kibiriti kikowapi?” aliuliza mzee Komba, hapo bila kuuliza Higgno akarudi dukani haraka, “unajua bwana Frank unamuharibu huyu mtoto, na atakuja kukupa shida sana hapo baadae” alisema mzee Komba kwa sauti ya kilevi, “kivipi bwana Komba?” aliuliza Frank, kwa sauti tulivu huku akimtazama kwa umakini mzee Komba, watu wanasema ukiona mlevi kaja kwako kwa shari, ujue alidhamilia, “huwezi kujua, lakini nadhani unakumbuka kipindi cha karibia na mavuno, huyu kijana wako alitaka kupigana na wakina Hilda, ukajifanya hujui sababu ni nini” alisema bwana Komba, na hapo mzee Frank akajua kuwa huyu bwana Komba bado alikuwa na kisa chake kile kile, “inamaana bado una yale yale?” aliuliza Frank kwa sauti ya tulivu, iliyoonyesha kuhuzunishwa kwake, “sikiliza Frank nikueleze kijana wako alivyo mbinafsi, huyu, aliona mwenzie amepata mwanaume mwenye fedha, mtoto wa tajiri ndio alitaka kuwatengenisha, sijui yeye angepata faida gani?” aliongea mzee Komba na kumshangaza mzee Frank, mwanaume! binti wa kidato cha kwanza!
Wakati huo tayari Higgno alikuwa ameshasimama karibu na mzee Komba akamkabidhi kibiriti, “niskie vizuri bwana Frank” alisema mzee Komba alieibana sigara yake mdomoni na kuiwasha, “nakusikiliza unieleze ubinafsi wa kijana wangu” alisema mzee Frank ambae alikuwa anajitahidi kuzuia jazba zake, bwana Komba akiwa asie na uharaka wote, alipiga pufu moja la sigara yake na kutoa moshi mrefu, ambao ulisambaa na kuwa fikia wakina Higgno na baba yake, ambao hawakuwa na budi ya kuvumilia, “huyu dogo ni mbinafsi sana, hakutaka mwenzie apate mwanaume tajiri, sasa kiko wapi, hapa tunasubiri ndoa muda wowote kuanzia mwezi wa kumi na mbili” alisema mzee Komba kwa majisifu na kumfanya mzee Frank ashangae kwa kuachama mdomo, “samahani bwana Komba najua mambo ya familia yako hayanihusu, lakini unamaanisha kuwa Hilda anaacha shule anaolewa…” kabla hajamaliza swali lake bwana Frank, mzee Komba akamdaka juu kwa juu, “kumbe sasa, hivi mwanamke hata akiwa waziri au rais wa nchi bila mume si anaonekana ni muhuni tu!, tena anaolewa na mtoto wa tajiri Mahamud” alisema kwa sauti ya kujisifu na majivuno ya hali ya juu.
Mzee Frank akamtazama Higgno, ambae kauli ya mzee Komba ni kama ili mtonesha kidonda, hivyo alitazama chini kwa huzuni ambayo mzee Frank aliiona wazi wazi, “nitafungua duka kubwa sana hapa kijijini, na sitokuwa na majivuno kama nyie” mzee Komba aliyasema hayo huku anaondoka zake na kuanza kuimba kilevi kwa sauti ya juu kabisa, “vandu vava mwenga (watu hawa jamani) “ alirudia mara kadhaa na alipofikia kipengere cha mbele yake akaimba, “vatu makoko, vandu makoko (watu ni mbwa)” aliimba huku ana kanya miguu chini kwa nguvu.
Frank na mwanae Higgno walimsindikiza kwa macho mpaka alipotoweka na kubakia wakisikia sauti yake kwa mbali ikizidi kutokomea kuelekea upande wa nyumbani kwake, ndipo bwana Frank alipohitaji ufafanuzi wa jambo hili, na Higgno akamueleza vyema kabisa kuwa Hilda amefukuzwa shule kwaajili ya ujauzito, aliopewa na Talib, ambae inasemekana kuwa ni mtoto wa tajiri mkubwa sana pale mjini songea, mwarabu Mahamud, “hata hivyo hainiingii akilini kama Mahamud ambae anasomesha mtoto wake wakike akubali kijana wake amuachishe binti wa watu shule” alisema mzee Frank wakiwa wanaingiza ndani ya nyumba yao, maana hata kibiriti walikisahau mzee Komba akaondoka nacho.*****
Naam siku iliyo fuata zikaanza kusambaa taarifa za Hilda kuacha shule kwaajili ya ujauzito, taarifa zilizo sambazwa na wazazi wake mwenyewe, sio kwa ubaya, ila kwa majisifu ya kuwa binti yao anaolewa na mtoto wa tajiri, mwarabu Mahamud, taarifa hizo ambazo ziliambatana na shutuma nzito kwa familia ya bwana Frank, shutuma ya kuwa familia hii haipendi binti yao aolewe na mtoto wa tajiri, ndio maana hata Higgno aliwahi kujaribu kuwavamia na kuwapiga, bahati nzuri aliambulia kipigo.
Wapo waliounga mkono jambo hilo, lakini wapo waliotia shaka juu ya hili, wakiamini kuwa kwa muonekano wa Talib hakuwa muoaji, swala hilo lilianza kuthibitishwa na Hilda ambae hakuwahi kuwaelekeza wazazi wake mambo yalivyokuwa yakienda, ikiwa ni pamoja kupungua kwa mapenzi yao na Talib, ambae sasa alikuwa anamkwepa mara kwa mara kila Hilda alipojaribu kumtafuta, na hata kuonekana kwake kulikuwa ni kwa nadra sana.
Siri iliwekwa wazi mwezi wa pili mwaka 1998, mwezi mmoja toka Higgno aingie kidato cha pili, miezi mitatu toka Talib amalize shule, ukimya ukiwa umetawala, hata zile mia mbili mia mbili za ulanzi na mishkaki hazikuonekana tena, tumbo la Hilda lilisha kuwa pevu, kiasi cha kuwa muda wowote mwezi huu wa pili alikuwa anatarajia kujifungua.
Baada ya kuona hakukuwa na dalili ya kuja kwa ujumbe wowote juu ya swala la kuolewa kwa Hilda ndipo mzee Komba alipoamua kujibeba yeye na mke wake na mwanae kwenda kwa mzee Mhamud kujieleza na kutafuta muafaka juu ya ujauzito na ndoa ya mwanae Hilda.****
Ilikuwa juma mosi, mida ya saa tano asubuhi, binti Soraya binti wa pekee wa tajiri mkubwa mjini songea bwana Mhamud, akiwa amesimama nje ya gate kubwa la shule sekondar ya waschana ya songea, huku amevalia nguo nadhifu za kiraia, gauni refu jekundu, kilemba hijab nyeusi viatu virefu vya mchuchumio, mkononi alikuwa na madaftari manne kama kawaida yake, mara likaonekana gari aina ya Land Rover discover likija na kusimama karibu yake, akaingia kwenye seat ya nyuma ya gari hilo na gari likaondoka kueleka upande wa mjini, likipitia RMA, “Laylah baba umemuacha nyumbani?” aliuliza Soraya, kwa sauti yake laini ambayo ukiisikia mara moja ungependa uisikie kila mara, “wote pamoja na mama wapo nyumbani, na nina imani ya kuwa bado wapo nyumbani kwasababu wakati natoka niliona kuna wageni wanaongea na mlinzi pale getini”, alijibu dereva wake ambae alikuwa makini sana kwenye kazi yake ya udereva, “wageni wa mama au baba?” aliuliza Soraya ambae alikuwa amebadilika kidogo tofauti na mwaka jana alivyokuwa anaonekana kuwa binti mdogo, sasa alionekana kuwa mschana angalau hata kifua chake kilichomoza maziwa mazuri yenye ukubwa wastani, hips zilizidi kutanuka na makalio yake kuongezeka ukubwa, urefu pia uliongezeka na kumfanya azidi kuwa mzuri wa sura na umbo pia.
Safari iliendelea kimya kimya kama dakika mbili hivi, ndipo Laylah akavunja ukimya, “Sora, vipi uliutazama ule mkanda jana” aliuliza Laylah huku akijichekesha kidogo, “kweli bwana umenikumbusha, niliutazama ni mzuri, mimi huwa natazamaga tu mikanda ya kihindi kumbe na ile ya wazungu ni mizuri” alisema Soraya akionyesha furaha, inaonyesha sasa alisha zoeana sana na dereva wake Layla “nimekubebea mwingine, lakini ni wa wamarekani weusi” alisema Layla, aliekuwa anaendelea kuendesha gari kwa umakini mkubwa sana, “afadhari niitazame leo usiku” alisema Soraya na sasa gari lilikuwa linaingia nyumbani kwao na kusimama nje ya gate na kupiga honi.
Gate lika funguliwa na hapo hapo wakawaona watu watatu, wakilisogelea gari lao, huku mwanaume mzee akiwa mbele anakimbilia gari na nyuma yake wanawake wawili wakimfuata, mama akiwa mtu mzima akiwa amemshika mkono mschana mjamzito, ambae mimba yake ilionyesha muda wowote anaweza kujifungua kwa ukubwa wake, “samahani mama naomba ninashida na wewe” alisikika yule mzee akiongea kwa sauti ya kuomboleza, huku akilikimbilia gari nusu aaguke kwa mbio alizotimua, lililokuwa linaanza kuingia ndani, lakini Layla hakusimamisha gari akaingiza gari ndani na lango likafungwa, “hebu simamisha gari” alisema Soraya, na Layla akasimamisha gari, “hivi umemsikia huyo mzee alikuwa anasema anashida na wewe vipi una mfahamu?” aliuliza Soraya kwa ile sauti yake nyororo ya kiarab, “siwafahamu, ila hao ndio niliokuambia kuwa ni wageni wa baba, nimewaona wanaongea na mlinzi” alisema Laylah, hapo Soraya akashuka toka kwenye gari, “we mlinzi, hao wazee hapo nje wanahitaji nini?” aliuliza Soraya, huku anatembea kumsogelea mlinzi, ambae kiukweli siku zote amezoea kumuona kwa mbali akiwa kwenye bustani ya mauwa anajisomea au amepumzika, vinginevyo hakuweza kumuona kwa ukaribu licha ya kukaa hapa getini kwa mezi saba sasa, siku zote alikuwa akipita getini huku amepandisha vioo vya gari, “boss haaa! wamesema wanataka kumuona baba au mama” alijibu kwa sauti ya uoga uoga yule mlinzi
Hapo Soraya akatazama kwenye maegesho ya magari na kuona magari yote yapo, ikionyesha kuwa watu wote wapo, ukiachilia Hyundai ambalo sasa lilikuwa halitumiwi na mtu, ni baada ya Talib kuzuiliwa kutumia gari hilo ambalo baada ya kumaliza shule na kupata daraja ziro kwenye matokea ya mtihani huo wa taifa, Nissan ambalo hutumiwa na baba yake lilikuwepo, Pajero la mama yake lilikuwepo, hata Suzuki maruti la kuendea sokoni pia lilikuwepo, sasa kwanini huja waruhusu, ina maana baba amekataa?” aliuliza Soraya huku amemkazia macho mlinzi, ambae alitazama kwanza upande wa kushoto wa jumba lile la kifahari, ambako kulikuwa na vijumba vinne vidogo vidogo, vijumba ambavyo kimoja wapo alikuwa anaishi Talib kwa sasa, ni mara baada ya kuzuiliwa kuingia nyumba kubwa kutokana na tabia yake ya udokozi iliyosababishwa na ulevi na uvutaji wa bangi.
Mlinzi hakumuona mtu yoyote, “Talib amenizuia nisiwafungulie” alijibu mlinzi….
Naam nini kitajili? Endelea Kufuatilia hapa hapa jamii forums.
 
Saf sana, naona hii kazi si muda itafika kwenye vitu vyangu, 👍👍👍👍👍👍😅😅😅
 
Nzurii iyoo
 
Jifahidi unapohadithia story ya mazingira flani, basi tabia za maeneo hayo ziendane na mazingira husika:
Na inatakiwa uyafahamu hayo maeneo ili hata wasomaji wanaoishi hayo mazingira wauone uhalisia wa story:
 
Back
Top Bottom