SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA NNE
MTUNZI MBOGO EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU : Wakati Higgno awaza hilo mara aliona gari lile ambalo lishamsogelea na kubakiza umbali wa mita kama arobaini toka alipo yeye Higgno, mara Higgno akaliona lile gari likisimama ghafla na akaonekana mwarabu mwenyewe akishuka akitokea upande wa dereva na kuzunguka upande wa pili wa gari yaani upande wa kushoto na kuchungulia tairi la mbele, hapo akaonekana ana jishika kichwa kwa huzuni huku ana tazama alikotoka halafu akalitazama tena tairi. Kabla haja jua tatizo inaweza kuwa nini mara Higgy Wizzy akashangaa kuona vijana wawili wanatokea pembezoni mwa barabara upande wa kulia, yaani kwenye msitu wa mlima chandamali na kumfuata yule tajiri mwarabu, yaani Mahamud ENDELEA……

Hapo yule mzee alipowaona akataka kukimbilia kwenye gari maana ni wazi alishagundua kuwa vijana wale hawakuwa na nia nje kwake, hata Higgno pia aliliona hilo kutokana na vitu walivyo shika mikononi vijana wale wawili, ni panga la kuuwa lile la kukatia miti au nyama buchani, mwingine akibeba kipande cha mti mfano wa rungu lakini haikuwa bahati yake, maana vijana wale wawili ambao Higgno hakuwa amewafahamu ila kimuonekano aliweza kuona ni wa umri wake walimfikia na kumkamata mzee yule kabla hajaingia kwenye gari, halafu wakaanza kuongea jambo fulani na yule mzee akonekana kuwa mbishi, hapo ndipo Higgno ghafla alipomuona kijana mmoja akivurumisha ngumi kwenda shavuni kwa mzee Mahamud, ambae kabla hajakaa sawa akafyetuliwa miguu yote miwili na kujibwaga chini kama mzigo akitimuwa vumbi, huku kanzu yake nyeupe ikibadirika rangi na kuwa nyekundu, hapo Higgno akamuona mmoja kati ya wale vijana yani yule alieshika panga akilisogeza shingoni kwa mzee Mahamud aliekuwa bado ametulia pale chini akiugulia maumivu, huku kijana mwingine akienda upande wa dereva na kufungua mlango, wakati huo tayari Higgno alikuwa ameshasogea karibu na gari.*******
Naam wakati huo kule Luhila sec, mzee Komba ambae alikuwa amepewa shilingi mia tano na kununua ulanzi mwingi sana, ambao miaka hiyo ulikuwa unauzwa lita shilingi hamsini, na kuuleta pale nyumbani kwake, kisha akawaalika baadhi ya marafiki zake kama sita hivi, kisha akaungana nao pamoja na mke wake na kuanza kunywa ulanzi kabla hajaanza kuwaeleza alichowaitia, “ndugu zangu kuna jambo nimewaitia hapa, ninaomba munisaidie” ndivyo alivyoanza kuongea mzee Komba huku wenzake wakimsikiliza, “kuna jambo ambalo wengi hawalifahamu, ni kwamba kijana wa mzee Frank wa dukani ndie aliezaa na binti yangu Hilda, ila Hilda kwa kuona kuwa Talib ndie mwenye fedha nyingi akamsingizia ule ujauzito” alisema mzee Komba na kuwafanya wote waliokuwepo pale wakinywa ulanzi, washangae na kutazamana kwa mshangao, huku mke wake pia akishangaa maneno ya mume wake, akijiuliza mume wake ana maana gani kwa kusema vile, “na kuthibitisha hilo, kijana Talib alisema kuwa yeye alitembea nae mara moja na alitumia kinga na akamtaja Higgno kuwa ndie alie kuwa anatembea nae” alizidi kuongea mzee Komba, “ayaa, kwanini mulificha swala hili toka mwanzo?” aliuliza mmoja wawale jamaa waliokuwepo, “hatukukaa kimya bwana Njogopa, tulienda kwa bwana Frank nae akakataa kabisa kutupa ushirikiano, si unajua jinsi anavyojisikia yule bwana” alisema mzee Komba, huku ulanzi ukiendelea kunyweka, “sasa bwana Komba unahitaji msaada gani kwetu?” aliuliza mwingine, “usiwe na haraka ngonyani, utanielewa tu!” alisema mzee Komba na kuendelea kueleza, “sasa nimeona kuna katabia kanaendelea kwa yule kijana, sasa ameanza tena kumvizia mwanangu, hivi ninavyo kueleza wapo kwenye mahusiano, sasa sihitaji tena binti yangu azalie nyumbani, na kwa kuwa hawa watu walikataa mara ya kwanza basi safari hii nataka niwashike ugoni na wafunge ndoa ya mkeka” hapo walevi wote walipiga makofi kwa mpango mzuri uliowekwa na mzee Komba, “mpaka hapo jeuri yao imeisha, lazima watakoma” alisema mzee Ngonyani, na mwingine alie fahamika kama mzee Nyoni, akadakia, “tena kwa unyambilisi tunaenda kama tulivyo na mjumbe, barozi, mwenyekiti lazima wawepo” alisisitiza Nyoni.****
Mida ya swala ya alaasiri ilishawadia, lakini familia ya mzee Mahamud, haikumuona baba yao, japo haikuwa ajabu sana kwao maana ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa mzee huyu kukosa swala hii ambayo huswaliwa saa tisa au saa kumi kasoro za jioni, maana wakati mwingine uchelewa na kuswalia pale pale anapokuwepo, ila ni mara chache sana, mara zote huwai nyumbani na kuswali pamoja na familia yake.
Mama Soraya, binti yake Soraya, mtoto wa kaka yake, yaani Talib na wafanya kazi wake, waliswali kwa pamoja wakifuata utaratibu wa swala ya pamoja kama familia, ambapo wanaume hukaa mbele na wanawake hukaa nyuma, mpaka wanamaliza bado hawakumuona mzee Mahamud, wakaendela kumsubiri pasipo wasi wasi wowote, tofauti na Talib ambae alijifungia chumbani kwake akiwa mwenye mcheche wa kujua kilichotokea, kama ni mafanikio aliamini kuwa angepata mafanikio makubwa maana fedha ambayo mjomba alikuwa anaikusanya kwa siku ilikuwa ni zaidi ya million 5, kama wange gawana yeye asinge kosa million 1, ambazo alitaka akafungue mradi wa kuagiza samaki na dagaa toka ziwa nyasa, biashara ambayo aliamini kuwa ingemtoa kwenye umasikini.
Naam lisaa limoja baadae ndipo walipoliona gari la mzee Mahamud, likiingia pale nyumbani na kusimama, kisha akashuka mzee huyu aliebeba briefcases lake ambalo hukusanyia fedha, ambae muonekano wake ulimshangaza kila mtu pale nyumbani kwake, “mume wangu, umepatwa na nini jamani?” aliuliza mama Soraya kwa mshangao mkubwa huku akimtazama mume wake ambae ukiachilia kuchafuka kwa kanzu yake nyeupe, pia alikuwa amebandikwa plasta kwenye sehemu za baadhi ya mwili wake, kama vile usoni na kwenye kiwiko cha mkono wake, huku shavu lake la upande wa kulia likionekana kuvimba, “mh! mke wangu we acha tu mke wangu, naamini wema tunao utenda kwa watu, ndio ulionisaidia leo nimepona, vinginevyo, nilikuwa naibiwa kila kitu, na pengine ninge uwawa kabisa” alisema Mahamud kwa sauti ya kushukuru iliyochangamka, japo alionyesha wazi kuwa ametoka kwenye matatizo makubwa, “kivipi mume wangu, ulivamiwa na majambazi?” aliuliza tena mke wake, “siburi kwanza nioge kisha muite Soraya niwasimulie kwa pamoja kilichotokea” alisema mzee Mahamud, kisha akaekelea chumbani kwake, hawakujua kuwa Talib alikuwa karibu na dirisha la sebuleni akiwasikiliza, na hapo hakuwa amepata jibu sahihi kama wakina Zido walifanikiwa kuchukua fedha kwa mjomba wake au walishindwa.******
Higgno hakutaka tena kupitia jeshini, aliamua awahi nyumbani kujiuliza kile kilichotokea kule Msamala, kitu ambacho kilikuwa ni kipimo kwake kwa mzaoezi aliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka minne, saa kumi na mbili kasoro aliingia nyumbani kwao, akamsalimia baba yake aliekuwa dukani, kisha akaelekea chumbani kwake kwenye mabanda ya uwani, ambako kwa sasa alikuwa amejiwekea kitanda kizuri redio casset moja ndogo (ile ya kutumia mkanda) pia alikuwa na meza moja ndogo na sturi nne nzuri kabati dogo languo lenye kioo, vitu ambavyo alivinunua kwa fedha yake mwenyewe akizo zipata kule gereji.
Kule chumbani Higgno alijilaza kitandani na kuanza kufikiria kilichomtokea kule msamala, akisahau kabisa kuwa alikuwa ana ahadi ya kukutana na Hilda usiku ule zaidi aliwaza mengi juu ya tukio hilo ambalo mimi na wewe hatujui ilikuwaje, tukio ambalo lili mkumbusha miaka iliyopita pale alipomsaidia mschana chotara wa kiarabu, ambae hakupata tena bahati ya kumuona, japo na yeye alijua kuwa hata angemuona tena isingemsaidia kwasababu mschana yule mtoto wa kitajiri asingeweza kusimama na kuongea na yeye masikini, ambae alishindwa kuonekana hata kwa mschana masikini mwenzie Hilda.******
Saa mbili na nusu, baada ya kumaliza swala ya insha nakuingia mezani kwaajili ya chakula akiwa na familia yake yani mke wake binti yake Soraya na mpwa wake Talib, ndipo tajiri Mahamud akaanza kusimulia kilicho mtokea, “jamani leo ingekuwa ndio mwisho wangu” hivyo ndivyo alialivyoanza kusimulia baba Soraya, huku wote wakiwa na hamu ya kumsikiliza, Talib akiwa na hamu kubwa ya kisilikiza kuliko wengine, maana alikuwa na hamu ya kujua kama wenzake walifanikiwa au laa, “baba Soraya, unajua unanipa kihoro, si ueleze kilichotokea au umefumaniwa huko?” aliuliza mama Soraya na kuwa fanya Mahamud na mwanae Soraya kucheka, huku kwa macho ya wizi, Soraya alikuwa anamtazama Talib, akijiuliza kuwa kijana huyu alikuwa na ajenda gani ya siri, kwanini asingizie anaumwa huku anatoka kwa siri na hata sasa alionekana kuwa mwenye kiwasi wasi fulani, tena muda wote alikuwa anatazama mezani, hakuweza kumtazama mtu mwingine usoni japo kwa sekunde hata tatu, "wakati na toka stendi kuu ya msamala nikapita ile barabara ya nyuma, ambayo huwa napitaga kila siku, sasa kufika karibu na njia panda ya chandamali nikahisi kuna tairi limepata pata pancha, ile kushuka na kutazama nikaona tairi la upande wa kushoto lina pancha, kuna mbao nilikuwa nimeikanyaga ilikuwa inamisumari, lakini wakati nafikiria nifanyaje, ili nibadili tairi, ghafla nikaona vijana wawili wanatokea porini wananifuata mbio mbio, nikaona kuwa ule ulikuwa ni mtego, hivyo nikaona bora nikimbilie kwenye gari niondoke hivyo hivyo na pancha yangu, unadhani hata kwenye gari nilifika sasa, wale vijana wenye panga na rungu, wakanifikia na kuanza kunidai nitoe briffcase la fedha, nikawaambia kuwa sina briffcase, hapo nilipokea kipondo na kujikuta nipo chini, mmoja akaniwekea panga na mwingine akaenda kwenye gari kutafuta briffcase, bahati nzuri nikiwaga peke yangu, huwa naiweka kwenye buti, sasa alipoikosa akamueleza mwenzie “oya huku hakuna kitu” alisema yule mwenye rungu, huku anatoka kwenye gari, “ngoja nimkate mkono ili aseme” alisema yule mwingine huku anainua panga ili anikate mkono, hapo nikafumba macho “msinikate msinikate hela zipo kwenye….” unadhani hata nilimalizia kuongea, nikasikia sauti “muacheni huyo mzee aondoke zake” ilikuwa sauti tulivu ya upole, nikafumbua macho kumtazama huyu aliewaambia wale vijana, huku najisemea kimoyo moyo angalau angeongea kwa ukali ingesaidia kuwatishia wale vijana wezi, nilipomuona kijana mwenyewe, hakika nilikata tamaa ya kupona, japo alikuwa anakamwili mwili hivi, lakini hakuwa na chochote ambacho kinge saidia, “we mpuuzi inshu haikuhusu hebu tambaa” alisema yule mwenye panga, huku akimuonyeshea panga lake, lakini yule kijana hakuonyesha kuogopa, “nasema acheni inshu za ajabu muacheni huyo mzee” alisema yule kijana kwa sauti ile ile ya upole, wakati huo napiga mahesabu ya kuwahi bastora kwenye gari” simulizi ya mzee Mahamud ilimvutia sana Soraya, ambae aliifananisha ile ya mwaka 98, ambayo ilimtokea kule chuo cha ualimu.
“Basi kuona kuwa yule kijana mpole anawaharibia mpango wao yule mwenye panga akamfuata yule kijana mpole na kulifurumisha panga usawa wa kichwa, hapo ndipo nilipoona pambano la bila kiingilio, yule kijana kumbeni mahiri kwenye mapigano kama zile filamu anazo angaliaga Soraya, alikwepa lile panga na kumpiga zinga la ngumi, yule mwenye rungu nae akasogea akamtadika wakaenda wote wawili akawapiga kweli kweli mpaka wakakimbia, tena walikimbilia kwenye gari moja hivi nilishindwa kulisoma namba, lilikuwa mbali kidogo nalo likaondoka, yule kijana nilimpa laki moja akakataa, bahati nzuri aliniambia kuwa anasomea ufundi, nikamuambia akimaliza kusomea ufundi aje nimpe kazi, ila nimemueleza pia akiwa anatatizo lolote aje nitamsaidia, lakini kiukweli kabisa ingekuwa ni kipindi kile cha mtume, ningemuozesha Soraya” alimaliza kusimulia Mahamud, na kumfanya mkewe acheke huku Soraya akitazama chini na tabasamu la aibu, huku na yeye akivuta taswira ya kijana mpole aliemsaidia siku ile kule chuoni.
Simulizi hii ambayo iliwavutia wanafamilia wote, kasoro Talib peke yake, ambae kiukweli, alishindwa hata kumaliza chakula kwenye sahani yake, akatoka na kuelekea kwenye kibanda chake, ile hali Soraya aliiona, hata hivyo hakutaka kuonyesha kuwa ametia shaka juu ya Talib, Soraya alimaliza kula na kutoka nje ya nyumba na kuzunguka upande wanyuma ule wenye nyumba anayokaa Talib kwa mwendo wa tahadhari.
Lakini kila soraya alipokuwa anazidi kusogelea nyumba ya Talib ndipo alipokuwa anasikia harufu ya udi ikitokea chumbani kwa Talib, Soraya akazidi kusogea taratibu usawa wa dirisha la sebuleni la nyumba hiyo, na alipolifikia hakuona kitu chochote, akahamia dirisha la chumbani, yaani chumba anacholala Talib, na pasipo kujari kama atakumkuta akiwa katika hali gani, yani amevaa nguo au uchi, yeye akachungulia dirishani, kwanza alimuona akiwa amekaa kitandani ameinamisha kichwa huku mikono shavuni, akionyesha mwenye mawazo mengi sana, lakini mmoja kati ya mikono yake alikuwa ameshika kitu kinacho toa moshi, mwanzo alidhania kuwa ni udi, lakini sekunde chache baadae Soraya akamuona binamu yake Talib akipeleke kile kitu alichokishika mdomoni na kuvuta kama inavyo vutwa sigara, na baada ya kuitazama viuri sigara ile, Soraya akagundua kuwa haikuwa ile sigara ya kawaida, na kwamba hii imesokotwa kienyeji, “bado anavuta bangi” aliwaza Soraya kwa mshangao*****
Naam upande wapili, Higgno akiwa chumbani kwake, bado alikuwa anakumbuka tukio la kule msamala, “mh! walae wakina Vitus mbona walimvamia mjomba wake Talib, ina maana hawa mjui, au wamemzunguka rafiki yao” alijiuliza Higgno kwasababu aliwaona wale vijana wawili wakikimbilia kwenye lile gari, ambalo aliwaona wakina Vitus na kuondoka zao.
Sasa basi wakati anaendelea kuwaza hayo mara akasikia mlango wa chumba chake ukigongwa, sambamba na sauti chini kabisa ya kike iliyoita, “Higgy ni mimi” hapo ndipo akakumbuka kuwa Hilda aliesema angekuja, “dah! ndio usiku hivi?” aliuliza Higgno huku anajiinua kitandani na kuufuata mlango, akaufungua na kumkaribisha ndani rafiki yake huyu wa zamani, ambae alikuwa amejitanda kanga nyingi sana kiasi kwamba hata angekutana na mtu njiani asingemtambua, “mbona usiku sana Hilda, kwanini usije kesho?” aliuliza Higgno, lakini badala yake akamuona Hilda anacheka cheka, “mh! Higgno,bwana sasa hivi sisi ni wakubwa, kwani kuna mtu anatuzuia kuonana usiku” alisema Hilda huku anageuka na kufunga mlango, “lakini Hilda hii ni mida ya kulala” alisema Higgno, ambae alionekaa kushtuka kidogo kwa ujio wa Hilda usiku huu ambao ulikuwa ni wa saa tatu za usiku, “mimi wala sigombezwi au wewe unagombezwa kutembelewa usiku?” aliuliza Hilda, huku anatoa kanga moja baada ya nyingine na kubakia na kanga moja aliyojifunga kifuani, kisha akapanda kitandani, “lakini Hilda ujue mama na baba wanaingiaga humu chumbani muda wowote, sasa wakikukuta humu watanifikiria vibaya” alisema Higgno aliesimama kati kati ya chumba, huku anamtazama hilda aliejilaza kitandani kwake, “lakini Higgno unakumbuka tuliwahi kusema kuwa hata wakitufiria vibaya ndio na sisi tunapenda hivyo?” aliuliza Hilda akikumbusha maneno waliyo ambizana miaka mingi iliyopita wakiwa kidato cha kwanza, “sawa Hilda lakini ni miaka mingi imepita” alisema Higgno, ambae alishahisi nia ya Hilda kutaka waanzishe mahusino ya kimapenzi, “lakini Higgno si unakumbuka uliniambia utaendelea kunipenda, nikiachana na Talib ni kufuate wewe?” aliuliza Hilda kwa sauti ya kujifanya analalamika.
Naam kabla Higgno hajajibu mara akasikia sauti za watu wakisogelea ule mlango wa kibanda chake, zikiwa ni saut za wanaume watu wazima, “ukweli nakuambia bwana Frank, safari hii siwezi kukubali, tukimkuta binti yangu humu namuacha hapa hapa” ilikuwa ni sauti ya mzee Komba, huku sauti nyingine ikidakia, “yaani ndio atakuwa mke wake, si atakuwa anampenda yeye mwenyewe, kwanini atake kumzalisha tena mtoto wa watu bila ndoa” hiyo ilikuwa ni sauti ya mzee Nyoni, hapo Higgno akamtazama Hilda aliekuwepo pale kitandani, akimtazama kwa macho ya tabasamu… ITAENDELEA.
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA TANO
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Naam kabla Higgno hajajibu , mara akasikia sauti za watu wakisogelea ule mlango wa kibanda chake, zikiwa ni saut za wanaume watu wazima, “ukweli nakuambia bwana Frank, safari hii siwezi kukubali, tukimkuta binti yangu humu namuacha hapa hapa” ilikuwa ni sauti ya mzee Komba, huku sauti nyingine ikidakia, “yaani ndio atakuwa mke wake, si atakuwa anampenda yeye mwenyewe, kwanini atake kumzalisha tena mtoto wa watu bila ndoa” hiyo ilikuwa ni sauti ya mzee Nyoni, hapo Higgno akamtazama Hilda aliekuwepo pale kitandani, akimtazama kwa macho ya tabasamu….. ENDELEA
Tabasamu ambalo Higgno aliliona kama limejaa tafsiri ya usaliti mkubwa, na kabla hata hajasema lolote, Higgno akasikia sauti ya baba yake toka nje, “mwenyekiti, samahani kwanza kabla ya yote kuna jambo nahitaji kupata ufafanuzi, umekijuaje chumba cha Higgno?’ aliuza baba Higgno kwa sauti ya mashaka, “bwana Frank, mimi nimeitwa kuwakilisha upande wa serikali, kuhusu wamekijuaje chumba hilo mimi silijui, labda tumuulize mzee Komba” alisema huyo mwenyekiti, hapo kikapita kimya kifupi kabla mzee Nyoni hajapayuka, “sidhani kama swala la amejuaje lina umuhimu, cha msingi ni kujua kama Hilda yupo humu ndani au laa” ndivyo alivyo jibu mzee Nyoni, ambae alionekana kuwa alikuwa amelewa pombe aina ya ulanzi, “ni kweli, kwani hajui kama watu walichunguza mpaka kulijua hili” alisema Njogopa, na hapo mwenyeiti akasikika akibisha hodi, “Higgno fungua mlango, mimi ni mwenyekiti” hapo Higgno akamtazama tena Hilda pale kitandani na kumuona ndio kwanza analegeza kanga yake pale kifuani, hakika ungemuona usinge weza kukataa kuwa walikuwa wametoka kufanya jambo fulani.
Basi kiunyonge sana, Higgno akaenda kufungua mlango kundi la wazee likazama ndani, “si unaona mwenyekiti, nilikuambia, ukweli sikubali binti yangu aendelee kuzalia nyumbani” alisema mzee Komba kwa sauti ya juu iliyojaa lawama na malalamiko, huku wenzake wakisaidia kutoa maneno ya lawama,
Higgno alimtazama baba yake, ambae alimtazama kwa macho ya mshangao, “Higgno umeanza lini hii tabia?” aliuliza mzee Frank, ambae alishangazwa na swala la kukutwa Hilda mule ndani, “hayo hayatuhusu bwana, sisi tunacho taka, Higgno akabidhiwe mke, sisi tuondoke zetu” alisema mzee Ngonyani na Njogopa akadakia “sio mke pekee akabidhie na mtoto pia”.
Mzee Frank akashusha pumzi nzito, kisha akamtazama mwenye kiti, “sina ujanja mwenyekiti, ifanyike kama wanavyo taka wao” alisema Frank, kauli iliyomuumiza sana Higgno, ambae alishindwa kuelewa kwanini Hilda alifanya vile, maana hata alipokabidhiwa mke na mwenyekiti wakiandikishiana kwenye karatasi na watu kuondoka zao, huku baba yake Higgno akimueleza mwanae kuwa wataongea kesho, yeye apumzike na mke wake, ukweli Higgno hakutaka hata kupanda kitandani, alibakia amekaa kwenyestuli yake huku akijiinamia chini na kuwaza kwanini Hilda amemfanyia hivi, “Higgy kwanini sasa unakuwa hivyo kwani wewe si ulisema unanipenda jamani?” aliuliza Hilda kwa sauti ya kubembeleza, sauti ambayo Higgno alihisi kama vile inatoka kwa jinni, “au ulikuwa unanidanganya ulivyoniambia nikiachana na Talib nije kwako?” aliuliza Hilda huku akijiinua toka kitandani na kumsogelea Higgno pale kwenye stuli, huku akiiachia kanga ikimtoka kifuani na kuachia baadhi ya maungo yake yakionekana wazi wazi, ikiwa pamoja na maziwa yake ambayo kiukweli si vyema kufananisha na vazi la miguuni(ndara) lakini ndio Uhalisia, “Hilda zaidi ya hapo unakumbuka uliyonifanyia?” aliuliza Higgno kwa Hasira, ambazo alikuwa anajitahidi kuzidhibiti, “lakini Higgy ule ulikuwa utoto” alisema Hilda akijifanya kubembeleza, “ulikuwa na utoto gani, mtoto anayafanya uliyo yafanya, mtoto anabeba mimba, mtoto anavuta mabangi na kunywa pombe, mtoto anakuja kujifanya kunitembelea kumbe anakuja kuniletea matatizo?” aliuliza Higgno maswali mfululizo, ambayo jibu lilikuwa moja tu, “jamani basi nisamehe, subiri nipone na wewe nitakupa” alisema Hilda kwa sauti ile ile ya kubembeleza, “kwani nani amekuambia mi nataka, yani nimekusaidia leo hii asubuhi, usiku wake una nifanyia hivi, nimekukosea nini Hilda?” aliuliza kwa machungu Higgno, ambae sauti yake ilikuwa inakaribia kuangua kilio kwa uchungu aliokuwa nao, “kama hutaki sawa, lakini mimi ndio mkeo na nisikuone na mwanamke mwingine, ukigoma naenda kwa mwenye kiti” alisema Hilda, na hapo Higgno akapandwa na hasira kali sana, japo aliona kuwa maneno yale yana ukweli ndani yake, “na kwa taarifa yako kuanzia kesho nataka nguo mpya, mbona wewe unavaa vizuri” alisema Hilda na sasa Higgno aliona akimuachia ni sawa na kulea kidonda, hivyo akimzibua ngumi kadhaa atakuwa amemtia adabu, lakini kabla hajachukua maamuzi hayo, mara wote wawili wakasikia mlango wa chumba kile unagongwa, Hilda alishtuka sana akihisi moja kwa moja kuwa mtu anaegonga mlango alikuwa amewasikia kila kitu, maana alihisi kuwa mtu huyu alikuwa mlangoni anasikiliza wanachoongea, Higgno akainuka na kuufuata mlango, akaufungua kidogo na kuchungulia nje, hakumuona mtu, akatoka nje kabisa akamuona baba yake anamuita kwa ishara kuwa amfuate.******
Kumbe basi, baada ya kutawanyika muda ule, mzee Frank ambae alikuwa anawaza sana juu ya tukio lile ambalo alikuwa anahisi kuwa ni tukio la kutengeneza, hakuamini kuwa mwanae Higgno alikuwa ameanzisha mahusiano na mschana Hilda binti ambae, habari zake hazikuwa nzuri hata kidogo, hivyo akaamua kurudi kimya kimya kwenda kusikiliza maongezi ya mwanae Higgno na mschana Hilda, hivyo basi mzee Frank, alirudi taratibu na kusimama nje ya chumba cha mwanae Higgno, na ndipo alipoyasikia maongezi ya mwanae Higgno na mkwewe mpya kabisa, na kugundua kuwa mwanae hakuwa katika mahusiano na mschana huyu ambae amejitaja kuwa ni mgonjwa.******
Higno alifunga mlango na kumfuata baba yake, ambae alitembea mbali na pale kwenye mlango wa chumba cha Higno, “Higgno kwanini ulirudisha ukaribu na huyu binti?” aliuliza mzee Frank kwa sauti ya chini iliyoonyesha masikitiko makubwa sana kwa mwanae mara baada ya kusimama ubavuni kabisa mwanyumba kubwa, “baba sijui nisemeje, ila kwa kifupi mzee Komba na mtoto wake wameamua kuniharibia maisha yangu” alisema Higgno kwa sauti ya upole iliyojaa masikitiko, “wameamuwa kukuharibia kivipi, wakati wewe mwenyewe ndio umejisogeza kwa yule binti ambae amekuwa wa hovyo kabisa, wanawake wote hawa mpaka unaamua kumsogelea mschana huyu?” aliuliza baba Higno, japo ilikuwa ni ya chini lakini ilionyesha wazi mzee huyu amechukia, “baba kwanza naomba unisamehe kwa kukuletea aibu kama hii, ila ukweli ni kwamba, Hilda na baba yake waeamua kunikomoa” alisema Higgno na kuanza kusimulia ilivyo kuwa.
“Hapo wametupata, lakini nikuambie kitu mwanangu” alisema mzee Frank, mara baada ya Higgno kumaliza kusimulia jinsi ilivyokuwa mpaka Hilda akaja pale nyumbani kwao, “ili litaisha, na muda sio mrefu huyu mschana atakuwa mbali na wewe, ila cha msingi usije ukashiriki tendo na mschana huyu, kwasababu nilimsikia aliposema kuwa hawezi kufanya lolote mpaka apone, hivyo niwazi kuwa anaumwa gonjwa la zinaa, mimi nitaenda kukutana na mwenyekiti nimueleze ukweli juu ya hili, hata likitokea jambo lingine siku za mbele asishangae” alifafanua baba Higgno.
Naam huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya ya Higgno, akiishi na Hilda na mtoto wa Hilda aliezaa na Talib, huku Higgno akiwahudumia kwa chakula na mavazi, na kumfanya Hilda azidi kunawili na kupendeza, kitu ambacho wengi walikuwa hawakijui ni kwamba wawili hawa walikuwa wanaishi kwa ugomvi mkubwa, Higgno akikubari kuwaachia Hilda na mwanae walale kitandani huku yeye akilala chini, siku zote Hilda mchana kutwa angeshinda nyumbani kwa wazazi wake, angetumia fedha aliyoachiwa na Higgno kununua mboga nzuri na kupika kule kwa mama yake na kula pamoja nao, wakati mwingine angewapatia fedha kwaajili ya ulanzi au angekunywa nao na kurudi nyumbani kwa Higgno saa mbili au tatu za usiku.
Mzee Komba na mke wake walifurahi sana kuona mtoto wao akianza kupendeza na kuonekana ni mmoja kati ya wanawake wenye kupendeza pale mtaani, sasa hata ile tabia yake ya kutoa kitumbia kwa aajili ya kupata shilingi mia mbili aliiacha kabisa, Kwasababu hakuwa na sababu ya kufanya hivyo, maana kila kitu alikuwa anakipata kwa Higgno, japo vijana wengi wa pale mtaani walimlaumu na kumdharau Higgno kwa kukubali kurudiana na Hilda, mschana ambae alishapitia kwenye maovu mengi.
wazazi wa Higgno hawakuwahi kuongea neno lolote kwa wazazi wa Hilda, na hawakuwa na maelewano mazuri kutokana na jambo walilolifanya kwa kijana wao, japo walijitahidi kuongea vyema na Hilda na kumchukulia kama vile mkwe wao.*****
Mwaka 2004, ni mwaka toka siku ile ambayo bwana Mahamud alivamiwe na wezi na kusaidiwa na kijana Mpole ambae kwa bahati mbaya hakuwahi kulijua jina lake, japo alikubali lile ombi la kuwa akimaliza chuo angeomba kujiunga kwenye kampuni yake ya usafirishaji kama fundi wa magari.
Ni mwaka mmoja toka Talib na wenzake, washindwe kupora fedha kwa mzee Mahamud, na talib kuendelea kujifanya mtu mwema ndani ya nyumba ya Mahamud, yaani mjomba wake, ambae aliyakubali mabadiriko ya kijana huyu na kumueleza mke wake kuwa, wanahitaji kumpatia mtaji wa biashara kijana Talib, ili aanze kuandaa maisha yake, nao wakakubaliana kumpatia fedha kiasi cha shilingi za kitanzania, million mbili, nae akaanza biashara ya kununua na kuuza samaki na dagaa toka ziwa nyasa, ambazo aliuliza kwa bei ya jumla mjini songea, ni biashara mbayo ilianza vizuri sana kwa upande wa kijana Talib, huku akitumia lile gari dogo aina ya Hyundai, kijana Talib alizidi kuonekana maridadi, Waschana walianza kumpapatikia na yeye hakuwaacha salama, alipita nao kama wote, starehe za pombe na bangi hakuweza kuacha, aliendelea na kuzidisha mara dufu, japo alijitahidi kuficha ukweli huo mbele ya mjomba wake shangazi na wanafamilia wengine kama Soraya na wafanyakazi, japo kwa mlinzi hakuwahi kumficha na ndie aliekuwa mshirika wake mkubwa, maana kuna wakati alilazimika kuingiza waschana kwa kupitia pale langoni.
Tabia hiyo ilifanya biashara ya kijana huyu ianze kushuka taratibu, kwa maana ya kupoteza mtaji mwingi kwenye starehe na anasa, akajikuta ana anza kuingia kwenye madeni, hali ilikuwa ngumu, alihitaji fedha nyingi ya kufanyia starehe zake, kutokana na matumizi mabaya ya fedha na tamaa akajikuta anaitamani nafasi aliyokuwa nayo soraya, kiasi cha kumchukia na kumuona kuwa ndie kauzibe, anae sababisha yeye asipate nafasi nzuri kwa mjomba wake.
Ni mwaka pia toka Soraya alipogunduwa kuwa binamu yake bado anavuta bangi, tofauti na watu wanavyo muona, japo yeye aliamua kukaa kimya, Soraya pia licha ya kuzidi kukuwa na kupendeza, akisumbuliwa na wanaume kila kukicha, lakini bado hakuwa na mwanaume wala mchumba, alisema bado hakumuona mwanaume wa kuendana nae, pangine alidanganyika na filamu za kihindi, “ni miezi miwili toka Soraya amalize chuo na baba yake kumpatia kazi ya kusimamaia baadhi ya miradi, ambayo aliiandaa kwa aajili ya binti yake huyu, ambae hakuwa tayari kuona anaajiriwa na mtu au kampuni yoyote, mmoja kati ya mirad ambayo Soraya alipewa kuisimamia ilikuwa ni miradi ya mashamba huko mahiro, kando kando ya milima ya matogoro ambako mwenye Soraya alikuwa anapenda kutembelea huko kila mwishoni mwa week, hasa siku ya ijumaa anapokuwa ametoka msikitini, mara nyingi aliongozana na dereva wake yaani Laylah.
Ni mwaka pia toka Higgno akabidhiwe Hilda kama mke wake na kuanza kuishi maisha yaliyojaa maudhi na ukosefu wa amani, maana Hilda alizidi kuwa mwenye tabia mbaya kila kukicha, ukiachia tabia ya kulewa na kuchelewa kurudi huku akimuacha mtoto wake nyumbani kwa kina Higno, pia alianza tena kutoa kitumbua chake bila kukiheshimu, na safari hii hakukitoa kwa aajili ya kutafuta fedha kama ilivyokuwa zamani, ila kwaajili ya hulka aliyokuwa nayo na mara nyingi alifanya hivyo akiwa amelewa ulanzi, na wakati mwingine hutokea akamkosea adabu Higgno nae kushindwa kumuadhibu, maana kauli iliyotawala ni kwamba, “we nipige kama kweli mwanaume, kama sijaenda kwa mwenyekiti” hapo Higgno angekuwa mpole.

Zilikuwa zime pita siku chache toka zitangazwe nafasi za kazi kwenye kampuni ya tajiri Mahamud, nae akaandika barua ya kuomba kazi, ambapo alipewa majibu ya kuja pale kwenye ofisi za kampuni hiyo week tatu zijazo mbele, ikiwa ni jumatatu ya kwanza ya mwezi wa tisa, katika kufanya usaili, yaani interview, Higgno alitamani kupata kazi hiyo na alipanga kuwa endapo ataipata kazi hiyo basi ange mueleza boss wake yaani mzee Mahamud, ampange kwenye gari linalo safiri mbali, ili asiwe anashinda pale nyumbani kwao kuepukana na maudhi ya Hilda, mwanamke ambae ni kama alizaliwa kumnyima raha.*****
Naam siku tatu mbele, ikiwa ni siku ya juma nne, Hilda alienda mjini kukuangalia nguo zake na za mtoto, kwa fedha aliyoachiwa na Higgno ambae hakuwa na namna ya kumkwepa na kumnyima matumizi, na Hila akiwa ameshaingia mjii ana elekea majengo mitumbani, mara akashangaa kuona gari likisimama pembeni yake, “Hilda mambo vipi?” kwanza Hilda hakujua kama anasalimiwa yeye, pengine kulikuwa na Hilda mwingine, lakini alipotazama lile gari akaliona ni lile gari ambalo lilikuwa linamfuata Talib shuleni miaka ile, “na alipotazama vizuri akamuona Talib akimtazama kwa uso wa tabasamu” kwanza Hilda hakujua kuwa na yeye atabasamu au atulie, maana anakumbuka kuwa mara ya mwisho kijana huyu alimkataa mbele ya wazazi wake, “poa mambo Talib” aliitikia na kusalimia Hilda, “mbona mbali mbali ingia kwenye gari twenzetu” alisema Talib ambae kwenye gari alikuwa peke yake, …. ITAENDELEA.
 
Arosto umetuacha na Arosto 🎶
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA KUMI NA SITA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO : “Hilda mambo vipi?” kwanza Hilda hakujuwa kama anasalimiwa yeye, pengine kulikuwa na Hilda mwingine, lakini alipotazama lile gari akaliona ni lile gari ambalo, lilikuwa lina mfuata Talib shuleni miaka ile, “na alipotazama vizuri akamuona Talib akimtazama kwa uso wa tabasamu” kwanza Hilda hakujuwa kuwa na yeye atabasamu au atulie, maana anakumbuka kuwa mara ya mwisho kijana huyu, alimkataa mbele ya wazi wake, “poa mambo Talib” aliitikia na kusalimia Hilda, “mbona mbali mbali ingia kwenye gari, twenzetu” alisema Talib ambae kwenye gari alikuwa peke yake,
ENDELEA SASA...

Hapo Hilda kama hakuamini alicho ambiwa, maana alikurupuka haraka na kuingia kwenye gari, kama vile aliogopa Talib anaweza kugairi, “niambie Hilda, vipi umeshaolewa? mana naona unazidi kupendeza” aliuliza Talib, huku anaondoa gari kuifuata barabara ya Mbinga, “kuolewa mchezo, nipo tu nazuga na yule bwege” alisema Hilda kwa sauti ya kubeza, “bwege tena, bwege yupi huyo?” aliuliza Talib, huku mara moja moja akimtazama Hilda baadhi ya sehemu za mwili wake kama kuutathmini, “si yule Higno muliempiga siku ile” alijibu Hilda kwa dharau ungesema anamtambulisha mtu wa hovyo hovyo, “ok!!!! yule dogo, kumbe mlirudiana, hivi anaishugani siku hizi?” aliuliza Talib huku anaongeza mwendo kuifuata barabara hiyo na kupita mtaa wa majengo mitumbani, akipita kati kati ya mtaa wa misufini na mfaranyaki, “unadhani ni kuishi nae basi, si tunaishi kama kaka na dada” alijibu Hilda, “weweee usinidanganye yaani ukae tu na mtu anakutizama” alisema Talib, “unadhani Talib, sijui ana matatizo, unajuwa hajawahi kunigonga hata siku moja” alisema Hilda kwa kujiamini, “sasa kama jogoo hawiki unaendaje kuishi nae?” aliuliza Talib huku akiendesha gari kuingia kwenye daraja la mwembe chai, “mimi si namchuna tu kwaajili ya mtoto, lakini vitu vingine hakuna” alijibu Hilda ambae hakujuwa mpaka dakika hiyo walikuwa wanaenda wapi, zaidi alimuona Talib anakata kona kuingia upande wakulia na kuingia mtaa wa mwembe chai, “kweli bwana umenikumbusha, hivi mtoto anaendelea je, si atakuwa mkubwa sana siku hizi?” aliuliza Talib kwa sauti iliyojaa furaha, akiwa amekumbuka kuwa ana mtoto, “mkubwa tena umefanana nae huyoo, we si ulimkataa” alijibu Hilda, wakati huo Talib anasimamisha gari nje ya nyumba ya Zido, pembeni ya Toyota Crester lililo wekwa juu ya mawe, likionyesha kuwa ni bovu kwa muda mrefu, “dah! sio kwamba nilimkataa, unajuwa shangazi lazima angeniletea msala, ila natamani sana kumuona dogo, poa tutaongea baadae si tupo pamoja au una haraka ya kumuwahi mumeo?” aliuliza Talib, wakiwa bado ndani ya gari, “wewe tu! mi nipo free” alisema Hilda kwa kujiamini, “hapo sawa tuta tafuta sehemu tukae tule bata huku tunapanga mipango na jinsi ya kumlea dogo” alisema Talib, maneno ambayo yalipokelewa kwa furaha na Hilda.
Wawili hao walishuka toka kwenye gari na kuingia ndani ya nyumba ile wakipitia uwani, ndani waka wakuta wakina Vitus na Zido wakiwa na watu wengine kadhaa waliokuwa wana vuta bangi, “hoooo! naona leo umekuja na shemeji langu lenyewe” alisema Vitus, akishangaa kuona Talib yupo na Hilda.
Kitu ambacho kilitokea mahali pale ni kwamba, licha ya kuvuta bangi yeye na Hilda pia Talib aliwaita Vitus na Zido pembeni na kuwapa mpango mpya wakuweka maisha vyema, “mpaka sasa Soraya ndie kiwingu, ambae anazuia mimi nisipewe michongo ya maana, hivyo akipotea yule mimi ndio nakuwa stering” alisema Talib, akionyesha kuwa hakuwa anatania, “sasa unatakaje, hebu funguka tuweke mambo sawa” alisema Zido akionyesha kuutamani sana huo mpango mpya, “hapo ni kumuua Soraya ili mimi nisimamie michongo yote ya ofisi za mjomba” alijibu Talib, “huo mchongo sio poa, bora tumteke, kwanza tuna mkomba kila kitu, kisha tunapiga simu kwa mzee Mahamud na kumuambia atupe million mia moja ili tumuachie Soraya” alisema Zido, akitaka kiasi hicho kikubwa sana kwa kipindi hicho cha mwaka 2004, “eti eeh!, ila inabidi tuwe makini, maana sina hela hata kidogo, mtaji unazidi kukata tu! tukizubaa maisha yatakuwa magumu hapa mjini” alisisitiza Talib kisha wakaanza kusuka mpango wao utakavyo kuwa, wakiwa wamemuacha Hilda anavuta bangi, kitu ambacho Hilda hakuwa mvutaji sana, sema mara zote hufanya hivyo asionekane mshamba mbele ya Talib, japo kwa sasa alianza kuona ni kilevi kizuri kwake, “tena anko amesafiri kwenye kupokea vyuma kibao, anaonekana anamkwanja mrefu sana kwa sasa” alisema Talib, basi inabidi tumsubiri arudi ili mchongo usiwe na mzunguko mrefu” ******
Siku hiyo pia ndio siku ambayo mwana dada Soraya alipowekwa kikao na mama yake, akimtaka aache kukataa wanaume, maana miaka ishirini na nne aliyonayo ni umri wa kuolewa na kupata watoto, “vijana wote hawa wanao kutaka hujaona hata mmoja ambae anaweza kuwa mumeo, umri unaenda huo mwanangu, mwishowe uzeeke na kukosa wa kukupenda” alisema mama Soraya, wakati anaongea na mwanae mara baada ya swala ya adhuhuri, ambayo walisali wao na wafanya kazi, baba hakuwepo maana alikuwa amesafiri kwenda kupokea magari mapya mabasi aina ya marcopollo yaliyokuwa yaingie siku inayofuata, “lakini mama nahitaji kuchunguza kwanza, wanaume wengi nasikiaga ni waongo” alisema Soraya, ambae alionekana kukosa amani baada ya kuambiwa swala la kuolewa, “lakini si unafahamu kuwa kuolewa ni hesima na jambo la kheri kwa mwanamke wa kiislam?” aliuliza mama Soraya, “ndiyo mama sijakataa kuolewa, lakini nikimpata nitawajulisha” alisema Soraya kwa sauti ile ile ya kukosa amani, maana miaka zaidi ya mitano amekuwa akimfikiria kijana aliewahi kumuokoa asibakwe kipindi akiwa anasoma, “usimuige binamu yako, yeye yupo yupo tu!” alisema mama Soraya, na hapo ni kama mama Soraya akakumbuka jambo, “hivi Talib sijamuona kwenye swala, atakuwa wapi?” aliuliza mama huyu, ambae kwa muonekano ni mke wa tajiri kweli kwa vito vya thamani alivyovaa mwilini mwake, “sijui atakuwa wapi, labda ungempigia simu” alisema Soraya, akimaanisha Talib apigiwe simu ya mkononi, maana kipindi hicho tayari zilisha kuwepo songea, maarufu kwa jina la mobitell, “nimalize vocha zangu kwa lipi haswa, kwani yeye ni mtoto mdogo?” aliuliza mama Soraya ambae hakuhitaji jibu lolote zaidi ya kuinuka na kuelekea chumbani kwake, huku akimuacha Soraya anajiandaa kuanza mizunguko ya kukusanya mapato ya siku ile, hufanya hivyo kama baba yake hayupo.*****
Naam kijana Higgno akiwa amesha maliza mafunzo yake ya ufundi wa magari, alikuwa anaendelea kumsaidia baba yake shughuri za shamba huko Mahiro, ambako alienda asubuhi, na kurudi jioni, alishinda akifanya kazi na alipochoka alikaa kwenye kibanda kidogo cha udongo pembezoni mwa shamba na kujipikia ugali na mboga yoyote aliyoibeba au kuitafuta kule shambani, mara nyingi hutega mitego na kunasa wanyama wadogo wa porini, aliamua kufanya hivyo kipindi hiki alichokuwa anasubiri kwa hamu tarehe ya kufanyiwa usaili na kupata kazi hiyo ya ufundi kwa tajiri Mahamud, ambae licha ya kumsaidia kutoka kwenye mikono ya wezi na wanyang’anyi na kuwa na uhakika wa kupata ajira hiyo, lakini pia Higgno kwa upande fulani alikuwa amejawa na hofu kubwa sana, kuhusu mambo yaliyowahi kutokea baina yake na kijana Talib, ambae licha ya yote aliyofanyiwa na kijana huyu, lakini bado sasa anaishi na kumlea mwanae, ambae toka ameanza kuishi nao kipindi cha mwaka mzima hakuona dalili ya Talib kumuhudumia mwanae, japo mara kadhaa amemuona akitanua na wanawake huko mjini,
Hofu kubwa ya Higgno ni kuwa pengine angenyimwa
ajira na kijana huyo, labda ange toa sababu yoyote ya uongo ambayo ingemfanya mzee Mahamud asimpe ajira, japo hakuona kama Talib anaweza kuwa na sababu yoyote ya kuweza kumfanyia hivyo, “ila wavuta bangi bwana, hawanaga sababu za kuharibu” aliwaza Higgno, hata wakati alipofika Nyumbani aliendelea kuwaza.
Naam baada ya kuwasalimia baba na mama yake ambae alimkuta ana cheza na mtoto wa Hilda, hakuongea jambo jingine zaidi ya salamu na kuelekea chumbani kwake, ambako hakumkuta mtu, na alitegemea hilo kwasababu ni kawaida ya Hilda kurudi usiku sana akiwa amelewa, hivyo akaingia bafuni na kujimwagia maji kuondoa jasho tu! kwasababu alishaoga kule kule shambani kwenye mto mdogo unaotililisha maji mto Ruvuma, anapenda sana kuogeleaga kwenye mto huo, na hufanya hivyo kila siku.
Naam masaa ya lisonga hatimae saa tatu usiku, mida ya kulala, Higgno aliingia kitandani na mtoto wa Hilda, pasipo kumuona Hilda mwenyewe, hatimae akapitiwa na usingizi na kuamka asubuhi pasipo kumuona Hilda, kabla hajaenda shambani aliwajulisha wazazi wake juu ya kutokumuona Hilda usiku ule, “nenda kamtazame kwa wazazi wake” alishauri mzee Frank, na Higgno akafanya hivyo, “kwahiyo unatuuliza sisi au sisi tukuulize wewe mwenye mke?” hilo ndilo lilikuwa jibu la mzee Komba, “na ole wako kama ume mpoteza mtoto wangu, maana siku zote tunajua kama unamchukia” alisema mama Hilda, wakati Higgno anaondoka zake kurudi nyumbani ambako alimueleza baba yake yaliyojili nyumbani kwa kina Hilda, “hapo mwanangu twende haraka kwa mwenyekiti tukatoe taarifa na kisha twende kituo cha polisi” alisema mzee Frank, ambae alimuachia mke wake duka na kuondoka na Higgno kuelekea kwa mwenyekiti wa mtaa, ambako walitoa taarifa ya upotevu wa Hilda.
Mwenye kiti ambae anafahamu tabia za ulevi na ugawaji holela wa kitumbua chake ya Mschana Hilda, ambae alifungishwa ndoa ya mkeka na kijana huyu mpole na mstaarabu, akawashauri waende kituo cha polisi kutoa taarifa, nao wakafanya hivyo, na walipo kamilisha taarifa yao, wakaendelea na kazi zao za kila siku.
Naam jioni iliingia, hakuonekana Hilda wala taarifa ya Hilda, hatimae siku ya tatu ikawa hivyo hivyo, taarifa zilizidi kuzagaa mtaani kwa kutoweka kwa Hilda, huku mzee Komba na mke wake wakizidi kutangaza na kuapia kuwa endapo binti yao asipoonekana au akipatwa na mabaya, basi watawashataki wakina mzee Frank na familia yao.
wakina Higgno wakaendelea kumtazamia Hilda, hata giza lilipoingia na kwenda kulala bila kumuona mschana huyu, mpaka siku ya nne mida ya saa tano za usiku, wasi wasi ukiwa umetanda moyoni kwa Higgno na wazazi wake, wakihofia kupata kesi endapo kuna jambo baya litakuwa limempata Hilda, Higgno akiwa chumbani kwake na mtoto wa hilda, kwenye mabanda ya uwani na wazazi wake wakiwa chumbani kwao ndani ya nyumba kubwa, mara wakasikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yao, hapo hofu zikazidi kuwashika, wakidhania kuwa ni gari la polisi limekuja kuleta taarifa ya Hilda kama sio kuwasomba, wakiwa naendelea kujiuliza ndipo wakaanza kusikia milio mikali mfululizo ya honi za gari ikilindima nje ya nyumba yao...... ITAENDELEA
HAYA SASA HILDA KARUDI KWA BABA MTOTO WAKE, SORAYA MPANGO WA KUTEKWA UNAANDALIWA NA HIGG WZY KWAO GARI YAPIGA HONI USIKU NA HAJUI WAPI MKEWE HILDA KAENDA WALE WAZEE WA KUTABIRI SIWAONI AU BADO MUDA WENUUUUUU.
 
🔥🔥🏃🏃🏃🔥
 
Back
Top Bottom