SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO: Baada ya kuongea sana na baba yake Higgno aliaga na kuelekea nyumbani kwake, akiwa amechukuwa baadhi ya vitu ambavyo aliona kuwa vingemfaa kupendesha kibanda chake endapo Soraya angekuja tena kule shambani, baadhi ya vitu alivyochukuwa ni shuka mbili safi, vyombo vya kupikia na kulia chakula, japo vichache lakini vyenye mtazamo wa kisasa mfano sahani zilikuwa za udongo, kisha akaondoka zake kushika njia ya kuelekea Mahilo, safari hii akipita njia ya mkato, Lakini wakati anaondoka na hajafika mbali mara akasikia ngurumo ya gari ikisikika kwa mbali toka kule alikotoka, mlio wa gari ambao aliufananisha na ule wa gari la Soraya, Higgno akasimama na kugeuka akitazama alikotoka….ENDELEA…….
Lakini hakuliona gari lolote likitokea zaidi ya kusikia ngurumo hiyo ya gari ambalo alianza kuamini kuwa linaweza kuwa ni gari la Soraya, yaani yule mschana chotara wa kiarabu, na sababu ya kuamini hivyo ni kuwa alimueleza kuwa kuna mzee anafahamiana nae huku Luhila.
Lakini ghafla ngurumo hiyo ya gari ikakatika, hapo Higgno akaendelea na safari yake huku mifuko ya Rambo ikiwa kwenye mikono yake kushoto na kulia, akitokomea kusini mwa mji wa songea akilikabili pori dogo la pembezoni mwa misitu ya matogoro, akiifuata njia ndogo na hafifu iendayo Linjumbwi, ambayo angeifuata kwa mwendo wa mita kama mia nane ndipo angeachana na njia hiyo na kufuata kinjia kingine kiendacho Mahilo, ambapo angetembea kwa mwendo wa mita elfu nne na mia mbili ndio angekuwa ameshafika shambani kwao.
Ukweli ni kwamba, lile gari lilikuwa ni lile Land Rover discovery la Soraya ambalo muda huo lilikuwa limesimama nje ya nyumba ya mzee Frank, na wakashuka Laylah na Soraya aliejiziba uso wake kwa niqab na kupokelewa na mzee Frank na mke wake, ikiwa ni muda mfupi sana toka Higgno ameondoka.
Soraya aliliona duka jinsi lilivyoteketea, “mh! kweli ililime chomwa” alisema Soraya baada ya kusalimiana na mama Higgno ambae hakuwa anajuwa kuwa ni mama wa mwanaume ambae anampenda kupita kiasi, “unadhani mwanangu yaani kuna kijana mmoja amelichoma makusudi kabisa na alipatia kutufanyia hivi” alisema mama Higgno kwa msisitizo.
Hapo kikapita kimya kifupi, huku Soraya akilitazama kwa umakini sana duka lile ambalo lilikuwa lime teketea kweli, kama ujuavyo maduka ya sehemu kama hizi huwa wanauza na mafuta ya taa ndani yake, “samahani baba kwani hili duka lilikuwa lina thamani ya shilingi ngapi?” aliuliza Soraya, wakati wanaelekea ndani, “mh! kwa kweli mpaka nichukuwe daftri nililo nunulia bidhaa za mwezi huu” alisema mzee Frank na Soraya akakubali kwa kichwa kuwa anachosema mzee Frank ni kweli.
Naam baada ya kuingia ndani waliongea mawili matatu, kuhusu ajali ile ya moto, huku Soraya akilaani vikali mtu aliefanya vile, “yaani mtu kama huyu, ni vyema kama mkimtolea taarifa polisi, ili akionekana akamatwe mara moja” kuna wakati Soraya alisema hivyo, huku Laylah akiongezea kwa kusema, kuwa “tena ni vyema ungeenda kituo cha karibu ukatoe taarifa kabisa, kama ulimuona huyo kijan basi siku nyingine unaweza kupajuwa anapoishi na kuwaeleza polisi wa mkamate” ushauri huo mzee Frank aliukubali na kuahidi kuwa ataenda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi mabatini, yaani pale FFU.
Maongezi yalichukuwa kama lisaa limoja mpaka saa sita na nusu, muda ambao Soraya aliaga kwaajili ya kuondoka, “nadhani ni vyema ungefungua duka jingine, maana ukikaa sana, unaweza kupoteza wateja” alisema Soraya, huku anatoa kiasi cha fedha Tsh laki mbili na kumpatia mzee Frank, “hii ungeanzisha ujenzi wa duka jingine hapo pembeni hilo lililoungua ungeliacha hivyo hivyo mpaka polisi waje kukagua” alisema Soraya huku mzee Frank na mke wake wakitoa macho kwa mshangao, kumbuka kuwa fedha hiyo ilikuwa ni nyingi sana, ingeweza kuwalipa mishahara walimu hata wanne au watano, “asante sana mwanangu mungu akubariki sana” alisema mama Higgno, ambae kama sio Soraya kuwa kumdaka basi angesha piga goti la kumshukuru, “usijari mama, nyie ni kama ndugu zangu na tutashirikiana kwa mengi sana, maana hata mchumba wangu wazazi wake wanaishi huku” alisema Soraya, akionyesha uso wa tabasamu na msisimko kwa jinsi wazazi wale walivyo na tabia ya kushukuru, ambao walishangaa tena hasa mama Higgno baada ya kusikia mschana yule tajiri anachumbiwa na kijana wa kule mtaani.
Soraya hakuishia hapo, alimsisitiza mzee Frank, kumaliza ujenzi haraka na kufanya makadirio ya duka lake ili amsaidie fedha za kununulia bidhaa, na hata Soraya na Laylah walipo ondoka kwa lengo la kuwa Soraya akamalize kazi zake na kujiandaa kwenda kwa mchumba wake, huku nyuma waliacha vicheko vya furaha “kijana gani huyo mwenye bahati hivi jamani?” aliuliza mzee Frank na mke wake akadakia, tena sio bahati ya kumpata mschana mwenye fedha ni kumpata mschana mwenye utajiri wa utu na roho nzuri” alisema mama Higgno, na hapo wakaanza kuchambua na kutafuta ni kijana gani mwenye bahati pale Luhila, wakitajiana jina moja baada ya jingine pasipo kulitaja jina la kijana mmoja tu nae ni kijana wao Higgno, kitendo kilicho wafanya wakose majibu, ******
Kati ya watu ambao, walikuwa wanaona muda unachelewa kwa siku hiyo ni mzee Mahadhi na kijana wake Idd, japo ilishatimia saa saba kasoro na wao walisha fika kwenye msikiti wa mkoa kwaajili ya swala ya adhuhuri, lakini bado waliona saa saba inachelewa kufika ili kikao cha kumsimanga mzee Mahamud kianze, huku wao wakijifanya hawajuwi chochote kuhusu chanzo cha habari hizo, wakipanga kushinikiza waombwe msamaha kwa kusingiziwa kitendo cha kumuwekea Soraya madawa na kama ikitokea hivyo basi hawata kubali msamaha mpaka Idd aozeshwe Soraya, kila walipo fikiria hivyo Idd na baba yake walijiona tayari matajiri, wanamiliki mali zote za bwana Mahamud ambazo hawa kuzijuwa chanzo chake.
Naam nusu saa baadae tayari walikuwa wamesha jumuika na wenzao kuswali swala ya adhuhuri na sasa walikuwa ndani ya ukumbi mkubwa wa baraza la wazee, huku ndani kukiwa na wajumbe kumi na nane pamoja na mwenyekiti na kijana Idd wakifanya idadi kuwa ishirini, “assalaam Alaykum wajumbe” alisalimia mwenyekiti ambae ni mzee wa makamo, “waalaykum salaam” waliitikia kwa pamoja wale wajumbe pamoja na Idd, kumbuka baba yake Idd ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wazee, “ndugu zangu tumekusanyika hapa kama nilivyo wadokeza ni kwa ajenda moja tu! ni kuhusu hizi jumbe zinazo samba kwenye simu zetu zikisema vibaya kuhsu mwenzetu yaani Mahamud, ni mwenzetu kwa maana ya muislam mwenzetu” alisema mwenyekiti na kuomba mmoja wa wajumbe asome ile messeji kwenye simu yake, na hata iliposomwa watu wote wakathibitisha kuwa sms zao zilikuwa zimeandikwa hivyo, yaani “imebainika kuwa tajiri mkubwa Mahamud Abdulkarim, ana lazimika kulala na binti yake kingono ikiwa ni imani ya kishirikina ambayo ina husishwa na biashara yake ya usafirishaji, Mahamud na mke wake wana fanya hivyo wakitimiza mashariti ya mganga wao aliewaambia kuwa mschana huyu asitembee na mwanaume mwingine yoyote zaidi ya baba yake akifanya hivyo utajiri wake unatoweka, tajiri huyu anafanya kila mbinu kuzuia mwanae asiolewe na kijana Idd Mahadhi ili kutimiza sharti la mganga, watumie wenzako wafahamu” mwisho wa ujumbe huo, idadi kubwa ya watu ilionekana kukunja sura kwa hasira na chuki, wakionyesha wazi wamekasirishwa na taarifa ile, kati yao wakiwepo Mahadhi na mwanae Idd waliojifanya kuumia sana na swala lile huku wachache wakionekana kusikitishwa akiwepo mwenye kiti, “ndugu zangu hii ni kashfa mbaya sana inamkuta mwenzetu, na sio yeye pekee na dini yetu kwa ujumla kwasababu yeye na familia yake ni waislam, na waislam wote ni ndugu, sasa tuna fanyaje kumnusuru ndugu yetu” aliongea mwenyekiti kwa sauti iliyojaa masikitiko makubwa, “samahani mwenye kiti, tunawezaje kumnusuru mtu ambae amejitakia mwenyewe” alisema mmoja wa wajumbe ni yule ambae siku ile ya jumapili alikuwa kwenye gari moja na Mahadhi, na mwingine akadakia “wewe mwenyewe uliona kwa macho yako jinsi alivyo tufedhehesha juzi” alisema mwingine kwa sauti ya hasira, “ni vyema kama tukimtenga hapa msikitini mpuuzi mkubwa” alidakia mjumbe watatu, “taratibu jamani, hebu tuwena khaba kidogo ili tuweze kujadili kwa kina swala hili” alisema mwenyewekiti na watu wote wakatulia, kisha mwenyekiti akaendelea, “naona kuna watu wanaamini kuwa ni kweli yale yaliyoandikwa kwenye messeji, ila tunapaswa kujiuliza baadhi ya maswali kabla ya kuhukumu” alisema mwenyekiti kwa sauti iliyojaa busara, hapo hapo Mahadhi kwa mara ya kwanza akaibuka, “sidhani kama kuna maswali ya kujiuliza, kwasababu wewe mwenyewe umeona kwa macho yako jinsi anavyokwepa binti yake asiolewe, maana siku ile alileta vijisababu vya uongo uongo” alisema Mahadhi kwa sauti iliyojaa jazba, huku mwingine akidakia, “ni kweli mwenyekiti, hebu fikiria inawezekanaje mschana anaenda kutolewa barua anaachiwa aende shambani, halafu ghafla unaambiwa ametekwa, huoni kama kuna mchezo uliochezwa na Mahamud mke wake na binti yao” alisema mjumbe huyu, akijiamini yeye na kuwa aminisha wenzake kuwa Mahamud anafanya mapenzi na binti yake, “na kwa kweli na msifu sana bwana Mahadhi na kijana wake, walikuwa wavumilivu sana siku ile, maana hata mimi nilichukizwa sana na jinsi walivyo fedheheshwa” alisema mmoja wa wajumbe huku mmoja akiongezea, “hakufedheheshwa peke yake, hata sisi tuliowapeleka tume fedheheshwa” ukweli idadi kubwa ili onyesha kuamini kuwa Mahamud alikuwa anatembea na mwanae, huku mke wake akiunga mkono kitendo hicho, “lakini jamani, mwenyekiti amesema kuwa tuna mswali ya kujiuliza, hebu tusubiri kwanza atuambie hayo maswali ambayo tuna paswa kujiuliza” alisema mmoja wa wajumbe, ambae alionekana kuhuzunishwa na kashfa iliyokuwa ina mkumba Mahamud, hapo wote wakatulia na kumsikiliza mwenyekiti, “kwanza ndugu zangu tunapaswa kujiuliza, ni nani ambae anasambaza ujumbe ule na ni kwa faida ya nani?” aliuliza mwenyekiti, huku akitazama uso wa kila mmoja kati yao, na alipofika kwa Idd na baba yake akawaona wakikwepesha macho yake, “mwenyekiti wewe mwenyewe una fahamu kuwa namba ni ngeni na simu imezimwa” alijibu mmoja wa wajumbe, “kwahiyo mtumaji wa ujumbe ule hakuwa na nia njema na bwana Mahamud ndio maana amejificha ?” aliuliza mwenyekiti, na hapo hakukuwa na jibu, hapo mwenyekiti akasema, “tukikaa kimya maana yake ni kwamba wote tumeona utata wa mtuma ujumbe, sasa niulize swali la pili” alisema mwenyekiti huku Mahadhi akiwaza moyoni mwake, “dah! mzee huyu ni nuksi kwelikweli maswali gani haya anauliza”, aliwaza Mahadhi, huku akiombea kuwa mwenyekiti asiulize swali jingine gumu, “swali la pili ni kwamba, lazima tujiulize,kwanini Mahamud afanye kitendo hicho na binti yake” aliongea mwenyekiti kwa sauti iliyojaa busara.
Swali hilo liligawika kwa pande mbili kimtazamo, wakati wengine wakiliona ni swali la kipuuzi, huku wengine wakiliona ni swali muhimu, “kwani ile messeji imesemaje, si anatimiza mashariti ya mganga” alisema mmoja wa wajumbe kwa sauti iliyojaa uhakika, “nadhani mjumbe hujui kwanini nasema hivi, kwasababu kwa yoyote anaemjua Mahamud, lazima atafahamu kuwa utajiri wa Mahamud umetoakana na tajiri Abdurkarim wa huko Oman, hakika ni tajiri mkubwa sana na katika ndugu zake Abdulkarim Mahamud ndie masikini, maana kaka zake na dada zake ni matajiri wakubwa sana huko kwao, sasa huo ushirikina unatokea wapi, wakati chanzo cha mali zake kina fahamika wazi wazi?” aliuliza mwenyekiti, na swali lile lilimshangaza na kumshtua Mahadhi ambae hakutegemea utambulisho ule wa utajiri wa Mahamud……… ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom