SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TATU: lakini hakujuwa kuwa kusimamisha dudu ni dalili ya kuwa na uwezo wa kufanya mapenzi, “mh! baba atakubali kweli?” aliuliza Laylah, huku ana ingiza gia namba moja na kuondoa gari taratibu, “tutaanza kumueleza tukifika tu!” alisema Soraya, huku anamtazama mzee moja aliekuwa anakuja mbele yao na baiskeri huku macho yake yakilitazama gari lao, “hooo! Laylah simamisha gari huyo mzee ndiyo atakuwa mshenga” alipiga kelele Soraya, huku akimtazama yule mzee ambae alionekana wazi kuhitaji kuongea na Soraya, maana alikuwa ana shuka toka kwenye baiskeri na kuvuka barabara akilifuata gari ambalo lilikuwa limesha simama kwa mara ya pili…… ENDELEA….
Huku anatabasamu, “Soraya unataka kumueleza nini sasa?” aliuliza Laylah, kwa sauti ya kunong’ona, “nataka nimuambie kuhusu kumsaidia Higgno kuwa mshenga wake, si unamjuwa jinsi alivyo mstaarabu” alijibu Soraya kwa sauti ya chini, huku wakimtazama mzee Frank aliekuwa anazidi kulisogelea gari lao, “lakini unge subiri kwanza umjaribu kama anasimami….” alisema Laylah, ambae hakupata nafasi ya kumalizia ushauri wake, maana mzee Frank alisha wafikia na Soraya akashusha kioo, “sahamani wanangu habari za masiku” alisalimia mzee Frank aliesogea na kusimama kati kati ya kioo cha abiria wa nyuma dereva, “nzuri tu baba shikamoo” alisalimia Soraya huku salamu ya shikamoo ikigongana na ile ya Laylah, “marahaba jamani, niliwaona mume nipita kasi sana pale makutano nilitamani kuwa simamisha lakini nilishindwa” alisema mzee Frank ambae alionyesha hali fulani ya uchangamfu, Soraya akamtazama Laylah, “hooo! samahani sikukuona mzee wangu, nilikuwa nawahi huku” alisema Laylah na Soraya akadakia, “lakini hata hivyo nilipanga nije nyumbani kwako, maana kuna jambo nahitaji unisaidie” alisema Soraya, kwa sauti ya upole, “hoo hakuna shida mwanangu, utanikuta maana nitaenda mara moja huku juu kumuona kijana wangu nimpe taarifa ya kuungua kwa duka letu pale nyumbani halafu nitarudi nyumbani” alisema mzee Frank akimalizia kwa sauti ya unyonge.
Hapo Soraya na Laylah wakashtuka, na kuacha midomo wazi, maana duka lile walikuwa wanalifahamu vyema kabisa, “mh! unamaanisha ni lile duka la pale nyumbani?” aliuliza Soraya kwa mshangao na mzee Frank akaitikia kwa unyonge, kwa kutikisa kichwa juu na chini, “hooo! pole jamani, chanzo cha moto kilikuwa nini?” aliuliza Soraya kwa sauti yenye huruma ya hali ya juu, “chanzo hakija fahamika, ila nahisi kuna mtu amechoma moto kwa makusudi” alisema mzee Frank kwa sauti ya upole yenye majonzi, “hooo! jamani pole sana, kwanini sasa alifanya hivyo kwani muligombana?” aliuliza Soraya, ambae alionekana wazi kuhuzunishwa na jambo lile, “ni mambo ya vijana, huyo kijana simjuwi kwa jina alikuja asubuhi na kudai kuwa anamtafuta kijana wangu, kwamba amemkorofisha kwa kumuharibia mipango yake na akaahidi kumfanyia jambo baya, ndio usiku yakatokea hayo” alisimulia mzee Frank, “sawa basi wacha kwanza niende ofisini halafu nitakuja kuona huko nyumbani” alisema Soraya, “labda unaweza kunidokeza shida yako japo kidogo” alisema mzee Frank kwa sauti ya udadisi.
Hapo Soraya alicheka kidogo, huku Laylah akitamani kumzuia Soraya asiongee shida yake mapema kwa mzee huyu kabla hajahakikisha kama kweli Higgno ni kijana sahihi kwake, “ni nahitaji unisaidie kuwa mshenga wa kuleta barua ya uchumba nyumbani kwetu, nina mchumba wangu wa kule kule mtaani kwenu anataka kunichumbia” ilikuwa ni sauti nyororo iliyojaa aibu ya mschana Soraya, “haina tatizo tutakuja kuongea zaidi, kwasasa wahi kazini wacha na mimi nimuwahi huyu kijana kabla sijapishana nae” alisema mzee Frank nao wakaagana na Layalah akaondoa gari kueleka upande wa mjini, huku mzee Frank akipanda baiskeri yake kuelekea upande wa Mahilo, “Soraya si tume kubaliana, umchunguze kwanza yule mtu?” aliuliza Laylah, alieonyesha wazi kuto kupendezewa na haraka za Soraya, “kwani tatizo lipo wapi, kama kweli hawezi kulala na mwanamke si basi, lakini akiweza si huyu mzee ndie atakuwa mshenga?” aliuliza Soraya kwa sauti iliyojaa ulizo na mshangao, “sawa, lakini umefanya haraka sana kumuambia asije akatoa habari kwa watu na zikaanza kuzagaa na kumfikia baba yako kabla barua haija tolewa” alisema Laylah na hapo kikapita kimya kirefu huku safari ikiendelea, Soraya alionekana wazi kuchukizwa na masimango ya Laylah, Soraya alitumia muda huu wa kuwa kimya kuwaza na kukumbuka matukio yaliyo tukia katika faragha yake na Higgno huku wakati mwingine akiwaza juu ya janga lililomtokea mzee huyu alie fikiri kumfanya mshenga wa Higgno.*******
Talib aliamka mida ya saa mbili na robo na kujiandaa kisha akatoka zake na kwenda mwembe chai kwa kina Vitus, ambako aliwakuta wenzake wanaendelea kujiuguza huku wakijipooza kwa sigara yenye harufu mbaya iliyosokotwa kienyeji, “ooya washkaji, sasa mna weza kupona kwa habari nitakazowapa” alisema Talib, huku analiza vidole vyake kwa kuomba apewe ile sigara, “una habari gani mshakaji usije ukatusakizia tena kwa yule mshenzi” alisema Zido huku anampatia bangi, ambayo ilipofika tu mkononi kwa Talib ilipelekwa mdomoni na kuvutwa pafu moja kubwa kwa mkupuo mmoja, kisha kuubana moshi ndani ya mdomo wake kwa sekunde kadhaa kisha kuanza kuutoa taratibu akitumia pua na mdomo, ungesema anauonea ubahili, “nimesha muonyesha mimi ni nani, tena ashukuru amehama pale kwao, leo munge sikia amesha kufa” alisema Talib kwa sauti iliyotoka kwa shida, kwasababu hakutaka moshi wa bangi utoke kwa wingi, “haaa! umefanya msala gani tena?” aliuliza Vitus, huku wote wakishangaa na kushikwa na shauku ya kutaka kujuwa kilicho fanyika, “baba yake si anakile kijiduka sijui tuite genge, nimekitia moto” alisema Talib, huku anapeleka tena ile bangi mdomoni na kuivuta tena kama mwanzo, “weee! limeungua au walizima moto?” aliuliza mmoja kati ya wale vijana wanne waliokuwa wanaonekana kutapakaliwa na uvimbe mbali mbali sehemu za nyuso zao, huku mmoja kati yao akiwa ameupakata mkono uliokuwa umevimba, “wauzime?, hawajatoa hata kibiriti nimetia moto lote, na hapo nilitaka nimchome yeye mwenyewe kwenye kile kibanda chake” alisema Talib kwa sauti ile ile ya kuzuia moshi wa bangi usitoke hovyo, “hapo umefanya jambo la msingi sana, sema nini Talib, tuliacha simu yetu kule kwenye shamba la dada yako, hapa hatuna hata mawasiliano” alisema Zido, pasipo kujutia kitendo cha kuacha simu, “achana nayo cha msingi hamkuonekana sura, simu kitu gani si tutanunua nyingine, maana fedha ya mule ndani ni ndefu kinoma” hapo ungejuwa kuwa hivi vitu alivyo kuwa anavivuta ni vibaya kwake, maana akuonyesha kabisa kama anatilia umuhimu swala la simu, ambayo walikuwa wanaitumia kuwasiliana na wakati wa tukio la kumteka Soraya, “na kukubali mzee wa mipango, ila safari hii tujitahidi tufanikiwe” alisema Vitus.*******
Naam mida hii kijana Higgno, alikuwa amesimama mbele ya kitanda chake anakitazama kwa umakini huku ana jitabasamia mara kwa mara ungesema kuwa ndiyo anakiona kwa mara ya kwanza, “mh! hivi ni kweli kabisa yule mschana anasema mimi ni mpenzi wake, kwasababu nimemsaidia au amenipenda kweli kweli?” alijiuliza Higgno, kwa sauti ya chini iliyojaa furaha na mahsngao, akitamani usiku uanze upya, “yaani mschana mzuri mweupeee, mpaka nikimgusa najihisi nitampakaza rangi nyeusi” aliendela kujiwazia Higgno ambae alikuwa na safari ya kwenda kwa wazazi wake kupeleka mboga na kuwaeleza jinsi alivyo anguka kwenye nafasi za kazi.
Dakika chache baada Higgno alianza kujiandaa huku akiendelea kuwaza kuhusu mschana Soraya, ambae mpaka sasa hakuwa anajuwa kuwa ni mtoto wa tajiri Mahamud, “dah! sijui atakuja tena lini yule mtoto?” alijiuliza Higgno, ambae aliendelea kuwaza huku anajiandaa kwa kuvaa na kukusanya baadhi ya nyama na samaki, kisha akachukuwa kwale yaani ngereng’ende (kanga wa porini) wawili, kisha akaingia barabarani kuelekea Upande wa Chemchem, akiacha kupita njia ya mkato akichelea kulowa na umande wa asubuhi uliotanda kwenye vijinjia, viendavyo kondeni, kuvukia Luhila mashambani yaani upande wa njia panda ya Linjumbwi.
Lakini Higgno alifanikiwa kutembea mita kama mia mbili tu huku akiwaza na kujitabasamulia mwenyewe, na baada ya hapo alishtuka akiiona baiskeri iliyoshika kasi ikijichomoza ghafla kwenye kona kipofu yenye mteremko ikija mbele yake na kusimama kwa ghafla, baada ya mwendesha baskeri yule kumuona yeye, “wewe unawazimu, mbona una tabasamu peke yako?” aliuliza mzee Frank akimtazama Higgno kwa mshangao, “kwani ni zambi kutabasamu?” aliuliza Higgno akimtazama baba yake, huku wote wakiwa wamesimama, “ok! labda wewe mwenyewe ndie unajuwa kilicho kutabasamulisha, vipi safari ya wapi?” aliuliza mzee Frank, “baba bwana, yaani hata hunipi nafasi ya kukusalimia” alisema Higgno huku anaanza kufunga lile furushi dogo la nyama na samaki kwenye kitako cha baskeri ya baba yake, “shikamoo baba” alisalimia Higgno na akimaliza kufunga lile furushi na kubakia na wale kwale mkononi, “marhaba vipi kuna usalama huko shambani?” aliuliza mzee Frank, akionyesha kidole kule shambani kiasi cha Higgno kushtuka na kuanza kuufikiria ujio wa baba yake kule shambani, “au baba amegundua kuwa nimelaza mwanamke huku shambani?” alijiuliza Higgno huku akisoma akili ya baba yake, akaona kama ana kitu fulani kilicho mfanya aje asubuhi hii, “huko salama tu, mimi nilikuwa na kuja kukuambia kuwa jana nilikosa nafasi ya kazi, lakin…..” hapo Higgno alikumbuka kuwa hakuweza kumuuliza Laylah kwanini alimkosesha nafasi za kazi, “hooo! pole sana” alisema mzee Frank, huku anageuza baskeri na wakaanza kutembea kurudi alikotokea mzee Frank, “ndiyo hivyo baba, lakini naamini nikikutana na yule mzee nitafanikiwa kupata kazi” alisema Higgno akijitahidi kumuondoa baba yake unyonge, baada ya kumuona amenyongea, hakujuwa kama mzee wake pia alikuwa na yake kichwani mwake, “kweli Higgno week hii Imekuwa mbaya kwetu, inabidi tuwe wavumilivu katika kipindi hiki” alisema mzee Frank, kwa sauti tulivu yenye kuficha majonzi makubwa, “lakini baba sio tatizo sana, nitafanikiwa tu kupata kazi, au unawaza kuhusu lile tukio la bomba mbili?” aliuliza Higgno kwa sauti ya kuchangamka ili kuondoa unyonge wa baba yake, “hilo moja wapo, na hili la kukosa kazi pia, ila pia kuungua kwa duka letu pale nyumbani” alisema mzee Frank kwa sauti ya masikitiko makubwa sana, “duka limeunguwa, lime unguwaje unguwaje?” aliuliza Higgno na hapo baba yake akaanza kumsimulia jinsi ilivyo kuwa, yaani kuanzia ujio wa yule kijana mkorofi, ambae alidai amekorofishana nae na kumuharibia mipango yake na kuaahidi kuwa atamfanyia jambo, na jinsi walivyo uona moto wa ghafla ukiwaka dukani.
Mwisho wa simulizi, Higgno alikuwa amesha pata maswali mengi bila majibu, ni kijana gani ambae amemvurugia mipango yake na kuamua kuahidi kumfanyia jambo baya, “mh! hakujitaja jina kuwa ni nani?” aliuliza Higgno kwa sauti yake ya upole, lakini ikionyesha wazi kuwa imejawa na hasira kali, “kwani wewe humkumbuki kijana uliemkorofisha?” aliuliza baba Higgno wakiwa wanatembea, huku akimkazia macho mwanae ambae aliwaza kidogo, kisha aka guna, “mh! sidhani, au kuna watu niliwazuwia wasimbake mschana mmoja hivi” alisema Higgno akishindwa kumueleza vizuri mschana mwenyewe wala tukio lenyewe, “nadhani utakuwa unamfahamu, ipo siku tukikutana nae nitakuonyesha” alisema Higgno wakiendelea na safari.******
Soraya alifika nyumbani kwao na kumkuta mama yake akiwa sebuleni anaongea jambo na mjomba wake, akawasalimia kwa uchangamfu japo aliwakuta wakiwa katika mkao wa kujadili jambo kwa kina na umakini mkubwa, lakini alipo wasalimia nao wakachangamka kidogo, “naona usiku wa leo umeufurahia sana” alisema mama Soraya, wakati Soraya akipita kueleleka upande wa vyumbani, “sana mama, tena leo nitaenda tena, yaani kuzuri, nimekuta na samaki wazuri na wale kanga wa porini” alisema Soraya kwa uchangamfu ule ule, akipotelea koridoni, hapo mama Soraya akamtazama kaka yake, “mh! atakuwa hajasikia hizi habari, kwa kweli zinahuzunisha sana, sijui ni nani alietunga huu ujinga?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya chini, “sasa sikiliza ni bora hizi habari uwahi ukamueleze mumeo maana akianza kuzipata yeye mwenyewe anaweza kupata mstuko mkubwa sana, na huyu Soraya ni vyema ukimnyang’anya simu kijanja ili asije akatumiwa ujumbe huu, pia uongee na dereva wake asije akamuonyesha Soraya ujumbe kama huo endapo atatumiwa, japo ujumbe huu unatumwa kwa watu wakubwa” alishauri mjomba na mama Soraya akaunga mkono.
Naam mama Soraya akainuka haraka na kwenda nje ambako alikutana na Laylah na kumueleza marufuku ya kumpa simu Soraya wala kumuonyesha ujumbe waajabu unao sambazwa ili kujaribu kumchafua baba yake, ujumbe ambao wanahisi umeandikwa na familia ya mahadhi ili kumchafua baba yake Soraya na Soraya mwenyewe, kisha mama Soraya akaingia ndani, na kumuomba kaka yake kuwa aandike ujumbe unaopinga swala lile na kueleza kisa cha Idd kukataliwa na Soraya ya kwamba alitaka kumlewesha kwa lengo la kumbaka, pili Soraya tayari ana mchumba wake.
Baada ya hapo mama Soraya akaingia chumbani kwake kwenda kujiandaa, huku akipishana na Soraya alietoka chumbani kwake akiwa ameshaoga na kujiandaa vizuri kwa safari ya ofisini, akaaga kwa mjomba akimuagiza muagie mama yake, ambae aliambiwa kuwa na yeye anajiandaa kwenda huko huko ofisini, ila amesema muachie simu yako anahitaji kupiga sehemu atakuletea huko huko ofisini” alisema majomba ambae aliona umuhimu wa Soraya kutokuwa na simu kwa kipindi kile, “na kwani ya kwake haina dolla, (vocha/salio) mwambie asinimalizie” alisema Soraya huku anatoa simu yake kwenye mkoba na kuiweka juu ya meza, halafu akaondoka kueleka nje ambako alimkuta Laylah akiwa katika hali fulani ya taharuki, “kuna nini Laylah, mbona kama ume badilika ghafla?” aliuliza Soraya wakati Laylah akiondoa gari kueleka mjini, “wala hakuna kitu, kwani naonekanaje?” alisema Laylah, huku anaendesha gari kwa umakini sana, “nilikuona tu kama umepooza.*******
Ni kweli sms zilikuwa zime sambaa kwa watu wakubwa wenye heshima zao pale mkoani, hasa viongozi wa dini na wafanya biashara ambao walitumiana wao kwa wao, na nyingine zikisambaa mpaka kwa wafanya kazi wa mzee yule lakini ni wale wa ngaz za juu, kila mmoja akishindwa kujuwa chanzo cha habari hiyo, maana hata sms za kwanza zilitumwa kwa namba ngeni ambayo baada ya kutawanya sms hizo ilitolewa kwenye simu kabisa, hata mzee wa baraza alipojaribu kuipiga ile simu ambayo ilimtumia sms ili kujuwa huyo mtu ni nani, lakini haikupatikana kabisa, ndipo mzee huyu alipoanza kuwasiliana na wenzake yaani wajumbe wa baraza hilo la wazee wa baraza la dini, akiwataka wakutane ili kujadiri swala hili la bwana Mahamud kutembea na binti yake mwenyewe kwaajili ya imani za kishirikina ikisemekana anashirikiana na mke wake kutenda jambo hilo.
Mwisho wa siku wakakubaliana kuwa wakutane saa saba mchana baada ya swala ya adhuhuri ili waweze kujadili juu ya swala lile la bwana Mahamud, ambalo lilionekana ni kuleta kashfa katika dini yao.******
Higgno na baba yake walifika nyumbani na kushuhudia kwa macho yake gofu la duka lililo chomeka vibaya sana, huku baadhi ya watu wakilishangaa kwa haraka haraka, ungesema kuwa ni gofu ambalo hutumika kutupia taka taka na sasa zilichomwa moto, “mh! baba ni kweli kuna mtu amechoma au kuna shoti ya umeme ilitokea ikasabisha moto” aliuliza Higgno kwa mshangao, huku akiwa amesimama karibu na baba yake, “sidhani kama ni umeme, maana lazima ungesimama nyumba nzima” alisema mzee Frank, na wakajadili kwa muda mfupi halafu Higgno na baba yake wakaingia ndani kupeleka mizigo ambayo walitokanayo shambani, wakipokelewa na mama Higgno, “mwanangu, umeona watu wabaya walivyo tufanyia” alilalamika mama HYiggno kwa sauti iliyojaa machungu, “mama hupaswi kuwaza sana, japo inauma lakini tushukuru kuwa hawakuchoma nyumba kubwa” alisema Higgno na baada ya hapo akamsalimia mama yake, “marahaba, mwanangu haya nieleze kuhusu huko ulikoenda jana” alisema mama Higgno ambae alikuwa anaingia jikoni na kurudi na chupa ya chai, “nitakueleza baadae wacha kwanza tunywe sisi chai” alisema mzee Frank, huku anaelekea kwenye meza kubwa ya chakula, “najuwa tu mambo yameenda vizuri, maana nikiitazama sura ya Higgno naona kabisa imejawa na tabasamu la furaha” alisema mama Higgno huku anarudi jikoni, akimuacha mzee Frank anamtazama mwanae kwa jicho la uchunguzi na mashaka, na kabla hajauliza kitu mke wake alirudi sebuleni akiwa na sinia la viazi vitamu, “asante mwanangu nimeona mboga” alisema mama Higgno aliekuwa anaweka lile sinia mezani, mzee Frank na Higgno wakakaa kimya wakitazamana kwa macho ya chini chini na alipoondoka tu! mama Higgno mzee Frank, akamuuliza Higgno, “unajuwa hata mimi ninashangaa, licha ya kuunguliwa duka kukosa kazi lakini wewe unaonekana unachangamka tu! kwani una furaha gani wewe?” aliuliza mzee Frank, kwa sauti ya chini huku akimtazama Higgno aliekuwa anaandaa vikombe kwaajili ya kuwekea chai, “baba bwana unataka kunifanya nikuambie kabla ya muda” alisema Higgno huku anacheka cheka, “mh! umepata kazi sehemu nyingine, au?” aliuliza mze Frank, “baba bwana we subiri nitakuambia” alisema Higgno aliekuwa anaanza kumimina chai, “au umepata mwanamke” aliuliza mzee Frank na hapo Higgno, akacheka kidogo, “ni mzuri sana, lakini bado muda wa kukujulisha” alisema Higgno, ambae akili yake ilikuwa imesha kumbuka kwenda kuandaa na kuweka mazingira mazuri kule shambani hata ikitokea Soraya akaja tena basi akute mazingira mazuri.*********
Mzee Mahamud akiwa ndani ya ofisi yake ana endelea kuchambua majina ya watu ambao wangeingia katika hatua ya pili ya majaribio ya maombi ya kazi, akishirkiana na baadhi ya wasaidizi wake wa pale kwenye kampuni yake, ambao ni kama walikuwa wanamtazama boss wao Mahamud kwa macho ya pembeni yaliyojaa mshangao, kana kwamba ni mgeni machoni pao.
Sio kwamba mzee Mahamud hakuliona swala lile, ila alitulia kimya akijaribu kutafuta ni jambo gani ambalo liliwafanya wafanyakazi wake wamtazame kwa njia kama ile.
Wakati wanaendelea na kazi mara mlango ukafunguliwa na akaingia Soraya, “assalam aleykum” alisalimia Soraya, kwa sauti iliyo changamka, “waalaykum salaam” waliitikia wote waliopo mule ndani pamoja na mzee Mhamud, ambae alimtazama mwanae aliekuwa bado amesimama, “baba misikai naenda kumuona mzee mmoja hivi ameunguliwa na duka lake usiku wa kuamkia leo” alisema Soraya kwa sauti iliyo changamka, “ni mzee yupi huyo, na ilikuwaje akaunguliwa na duka lake” aliuliza mzee Mahamud kwa sauti ya mshangao na Soraya akamsimulia kukutana kwake na yule mzee kulikosababishwa na ajali ya baiskeri, na kupelekea kufahamiana nae, “leo wakati tuna toka kwa kina Laylah, ndio nimekutana nae asubuhi na kunisimulia juu ya hilo” alisimulia Soraya, “ok! naona hata usiku wako wa jana haukuwa mbaya, maana umechangamka kwa fauraha, vipi mazingira ya huko kwa kina Laylah ni mazuri?” aliuliza Mahamud, huku akicheka kidogo, “sanaaa, yaani sikujuwa kama kule mitaani ni kuzuri vile, tena baba na leo naomba na leo niende kulala kule kule” alisema Soraya kwa sauti ya kuomba, Mzee Mahamud akaangua kicheko kidogo, “unaenda kwa mkwe, maana tayari ulishamuona ile jumapili” alitania mzee Mahamud na hapo Soraya akatazama chini kwa aibu, akishindwa kutoa jibu, “ok! mutaondoka baada ya inshaa kama jana, lakini uwe makini mwanangu” alisema mzee Mahamud na Soraya akaachia tabasamu pana la furaha, “shukrani baba” alisema Soraya na kuaga kwa baba yake kisha akaondoka zake kutoka nje ya ofisi, akimuacha baba yake na wale wafanya kazi wakimsindikiza kwa macho mpaka alitoweka, Mahamud akacheka kidogo , “vijana bwana huyu mtoto hakuwahi kulala nje ya eneo la familia kama sio hapa basi dar au oman, sasa leo amelala kwa Laylah ndio kanogewa kabisa” alisema Mahamud, ambae hakujua kuwa wale wafanyakazi wake walikuwa wana waza ya kwao na kujipa majibu vichwani mwao.
Ukweli wafanyakazi hawa ni kati ya wae waliopata ujumbe kwenye simu zao, ambao ulikuwa unasema Mhamud anatembea na binti yake, ikiwa ni chanzo cha utajiri wake, sasa mmoja wao akaamua kuchomekea jambo ili wamuone boss atasemaje, “boss kuna umri ambao binti huwezi kuendelea kumzuia kufanya baadhi ya mambo” alisema mmoja kati ya wale watu aliokuwa nao, hapo ni kama Mahamud alishtuka jambo na kuinua sura yake kumtazama huyo mfanya kazi wake, “Jamal, unataka kusema inawezekana Soraya anatumia nafasi hii kukutana na mwanaume sio?” aliuliza Mahamud lakini katika hali ya mshango wa furaha na wale wafanyakazi wakaonekana kumshangaa Mahamud, “inawezekana boss, japo hatuwezi kuthibitisha” alisema Jamali na mwingine akadakia, “lakini Soraya kwa sasa ni mkubwa, na pengine huo ndio mwanzo wa yeye kuolewa” hapo Mahamud akacheka kicheko fulani cha furaha, “ok! sasa nimepata picha kamili Soraya alisema kweli juzi” alisema Mahamud na kuanza kuwasimulia wale wafanyakazi wake jinsi ilivyokuwa siku ile ya jumapili, bwana Mahadhi alipokuja kuleta barua ya posa, “hooo! kwahiyo boss huyo Idd ni yule mtoto wa mahadhi alietorokaga wakati ule kwenda south?” aliuliza Jamal kwa mshangao na masikitiko, “ndiyo huyo huyo kumbe unamfahamu?” aliuliza Mahamud, kwa mshangao na tahadhari, “dah! boss namfahamu vizuri sana, sidhani kama kuna mmoja wetu hamjuwi yule mshenzi” alisema Jamal, na mwingine akadakia, “dah! boss sijui kwanini uliwakaribisha wale washenzi, hapo walikuwa wanahitaji fedha zako tu na siylo mke” alisema kwa sauti ya huzuni na masikitiko, huku mtu wa tatu akadakia, “sasa ndio najuwa maana ya ile messeji, hapo wanataka boss amuozeshe Soraya kwa nguvu ili idd atimize malengo yake” kwa kifupi wale wafanyakazi watatu tayari walikuwa wamesha gundua mchezo mzima lakini bado bwana Mahamud ni kama alikuwa anashangaa, “mnasema messeji?’ ni messeji gani hiyo?” aliuliza Mahamud kwa mshangao na Jamal akatoa simu yake na kuifungua sms moja kisha na kumpatia boss wake.
Naam Mahamud akaifungua ile sms na kuanza kuisoma kwa tahadhari, “imebaini kuwa tajiri mkubwa Mahamud Abdulkarim ana lazimika kulala na binti yake kingono ikiwa ni imani ya kishirikina ambayo ina husishwa na biashara yake ya usafirishaji, Mahamud na mke wake wana fanya hivyo wakitimiza mashariti ya mganga wao aliewaambia kuwa mschana huyu asitembee na mwanaume mwingine yoyote zaidi ya baba yake akifanya hivyo utajiri wake unatoweka, tajiri huyu anafanya kila mbinu kuzuia mwanae asiolewe na kijana Idd Mahadhi ili kutimiza sharti la mganga, watumie wenzako wafahamu”, alimaliza kusoma Mahamud na wakati huo huo mlango wa ofisi ukafunguliwa na wote waka tazama mlangoni……….. ITAENDELEA
Nomaaaaa
 
Mkuu Leo umejuwa Kucheza kama Pele umeleta muda muafaka sio kwa unyongee huu na juwa wale team idd wanaleta majungu jinsi unavotuwaishia mapema😜😂😂
 
Mkuu Shusha vitu mida si ndo hii mpka team idd wakose amani😂😂😂Leo ndo siku yenyew yakuichakata kitumbua cha soraya
 
Nilikuambia upumzike leo, ona sasa unatulezea ka episode kamoja tu:
Kuna watu watakunywa sumu na kifariki ujue:
Kwa presha ya kukosa episode mbili:
 
Back
Top Bottom