SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE: Naam Mahamud akaifungua ile sms na kuanza kuisoma kwa tahadhari, “imebaini kuwa tajiri mkubwa Mahamud Abdulkarim ana lazimika kulala na binti yake kingono ikiwa ni imani ya kishirikina ambayo ina huusishwa na biashara yake ya usafirishaji, Mahamud na mke wake wana fanya hivyo wakitimiza mashariti ya mganga wao aliewaambia kuwa mschana huyu asitembee na mwanaume mwingine yoyote zaidi ya baba yake akifanya hivyo utajiri wake unatoweka, tajiri huyu anafanya kila mbinu kuzuia mwanae asiolewe na kijana Idd Mahadhi ili kutimiza sharti la mganga, watumie wenzako wafahamu”, alimaliza kusoma Mahamud na wakati huo huo mlango wa ofisi ukafunguliwa na wote waka tazama mlangoni……ENDELEA……….
Wakamuona mke wa Mahamud yaani mama Soraya akiingia mule ndani ya ofisi akiwa katika hali ya tabasamu, lakini lililoonekana wazi kuwa la mashaka mashaka, “nimepishana na wakina Soraya pale madizini, ina mana hajakaa kabisa ofisini” aliuliza mama Soraya akiendelea na lile tabasamu lake la bandia, huku moyoni mwake akiwa ana chunguza na kupima hali ya mume wake kama atakuwa amesha pata ile sms au bado, lakini akashindwa kumuelewa, maana alikuwa anaonyesha wazi kuwa mwenye uchangamfu wa kawaida tu! “mwanao ameenda kumtazama mzee mmoja hivi huko luhuila, amechomewa duka lake” alisema mzee Mahamud, kwa uchangamfu huku anamkabidhi Jamal simu yake, “mh! mzee yupi huyo na anamfahamu vipi?” aliuliza mama Soraya huku anaenda moja kwa moja nyuma ya kiti cha mume wake, ambae alimsimulia kama alivyosimuliwa na Soraya mwenyewe, “halafu ameomba tena kwenda kulala kwa Laylah, inaonekana ameyapenda sana mazingira ya huko” alisema mzee Mahamud, “mh! ameomba na leo akalale kwa Laylah?” aliuliza mama Soraya kwa mshangao wa mshtuko, “yes! lakini sio mbaya, Soraya anajuwa anachokifanya, hawezi kuwa anafanya upuuzi isitoshe ni mkubwa sasa” alisema mzee Mahamud akipuuza wasi wasi wa mke wake, “lakin hata kama ni mkubwa bado ni binti yetu, tunapaswa kujuwa kinachoendelea huko mitaani” alisema mama Soraya hata wakina Jamal walimuunga mkono kwa kukubaliana nae, “ni kweli boss anachosema mama, lakini yule ni mschana mkubwa anaweza kujitunza” alisema Jamal, na mama Soraya akasema, “hivi vitu havina kujitunza, hasa pale mtu anapozama kwenye mapenzi anakuwa kama kichaa, bora niwahi kabla hajapata ujauzito kabla ya ndoa, maana leo nimemuona amechanganka huyo, kama ametiwa ndimu” alisema mama Soraya, huku anawatazama wale waliokuwa ndani ya ofisi, kuanzia mume wake na wale wasaidizi wa mume wake kuwasoma kama walikuwa wanaunga mkono juu ya lile, “lakini leo tumuache aende kwa mwenzie, “kesho uongee nae, ili kama anamwenzie basi wafanye mpango wa kuleta barua” alisema Mahamud, “halafu nimekumbuka, hivi nakumbuka kuwa Soraya alisema kuwa anamchumba na ni yule kijana aliemsaidiaga inaweza kuwa ni kweli” alisema mama Soraya na hapo wale wasaidizi watatu wakathibitisha juu ya mkasa aliowasimulia mzee Mahamud, uliotokea siku ya jumapili yaani juzi, siku ambayo wakina Mahadhi walileta barua ya posa iliyokatiliwa na Soraya mwenyewe, “itakuwa bahati sana, maana nitapata nafasi ya kutimiza ahadi yangu ya kumpatia nyumba na gari” alisema Mahamud, huku akitabasamu akionyesha mwenye furaha, “lakini unajuwa umemtisha Soraya baada ya kumtilia mashaka kijana wake pale uliposema endapo takutana nae lazima umuulize maswali na akishindwa kujibu hauwezi kumkubalia amuoe mwanao” aliuliza mama Soraya, hapo Mahamud alitulia kidogo kabla hajajibu, “lazima nimuhoji huyo kijana, na sitanii endapo akishindwa kujibu maswali yangu hakika sita mkubalia kumuoa mwanangu” alisema mzee Mahamud akionyesha kuwa anamaanisha anachokisema, “kwani boss nikitu gani kinakupa mashaka juu ya kijana huyo?” aliuliza mmoja kati ya wakina Jamal, wakitegemea kuona mzee huyu akiwaza kwa huzuni kama vile hakupenda mwanae aolewe.
Hapo Mahamud akatabasamu kidogo, “ukweli kijana huyu amefanya mambo makubwa sana kwa binti yangu, kiasi kwamba nahisi hata mimi mwenyewe na upendo wangu mkubwa nilio nao kwa binti yangu pasipo kuwa na silaha yoyote kama yeye alivyokuwa, nisingeweza kumsaidia binti yangu hata mara moja, sasa yeye amemsaidia mara tatu, tena mara mbili zote katika hatari kubwa sana ya kugharimu maisha, nataka kumuuliza kwanini amekuwa anamsaidia Soraya?” alisema mzee Mahamud sasa akiwa ametuliza akili na hisia zake, hata sauti yake ilikuwa ni tulivu, “sasa boss, kwani kuna tatizo kwa kijana huyu kumsaidia Soraya?” aliuliza Jamal, kwa sauti ya mshangao, “ndio kuna shaka juu ya hilo Jamal, unadhani kuna msaada unakosa sababu?, tena mara tatu, kufa na kupona bila kukubali kitu chochote cha asante zaidi ya asante ya mdomo” alisema Mahamud na hapo wakina Jamal wakashangaa kidogo, “lakini boss si ungemfata moja kwa moja na kumuuliza huyo kijana” alishauri Jamali, “ingewezekana kama tunge kuwa tuna mfahamu” alisema mama Soraya, “kwahiyo licha ya kumsaidia Soraya mara tatu, lakini hamumjuwi, inawezekana vipi?” aliuliza Jamal, na hapo mze Mahamud, akasimulia visa vitatu ambavyo vilimkuta Soraya na kuokolewa na kijana huyo na mazingira tata ya kuachana kwao, “tena siku ile nilimuomba tuongozane nyumbani japo nikampatie chochote kama asante, lakini wapi alikataa kata kata” alisema mama Soraya, na hapo hata wakina Jamali wakashangaa pia, “kwa hiyo boss hakuna kikwazo zaidi ya swali utakalo muuliza huyo kijana?” aliuliza mmoja wa wale wasaidizi wa mzee Mahamud, “zaidi ya hilo sitojari kijana anatokea wapi hali ya maisha yake ipoje nitampa mke kwa mahali atakayoitaja Soraya mwenyewe” alithibitisha Mahamud, “kweli boss hiyo itasaidia, kuondoa haya maneno ya….” moja alijikuta ameropoka lakini akasita mara moja kw akuhisi kuwa pengine mama Soraya hakuwa anajuwa lolote juu ya zile messeji zinazo sambaa zikieleza kuwa yeye mama Soraya na mume wake wanashiriki kitendo cha baba na mtoto kufanya ngono kwaajili ya utajiri walionao, “ni kweli Ayubu, itasaida sana kuondoa hii kashfa, sijui ni nani anafanya hivi?” alisema Mahamud, na hapo mama Soraya akashikwa na mshangao, “ina maana umeshatumiwa messeji?” aliuliza mama Soraya kwa mhsngao, “unadhani shemeji sisi wote tumetumiwa, lakini huyu atakuwa ni huyo kijana ambae watu hawamjui kama alikuwa mwizi wa huko msumbiji kabla ya kuanza kuuza madawa ya kulevya, hatujuwi amerudije huku nchini, japo kuna habari zisizo rasmi kuwa amerudi bila kitu chochote, kwa maana amekimbia huko msumbiji” alifafanua Ayubu, na hapo Mahamud na mke wake waka tazamana kwa mshangao, “kumbe huyu kijana ni mbaya hivi?” aliuliza mama Soraya, kwa mshangao mkubwa, “tena na uhakika lengo lao likitimia na akimuoa binti yenu basi mutajuta kitakachotokea kwenye maisha yenu na binti yenu” alisema Ayubu, “ndio maana hata alipata uwezo wa kumuwekea Soraya dawa kwenye juice” alisema Mahamud, “boss bwana kuna bar wanauza juice ya asili, hapo Idd alikuwa anataka kufosi king” alisema Jamal na wote wakacheka, “ok! tuone mwisho wa mchezo wao utakuwaje” alisema mzee Mahamud na baada ya hapo mama Soraya akaaga na kurudi nyumbani, akimuacha mume wake na wale wakina Jamal wanaendelea na kazi zao huku wanaendelea kuzungumzia lile jambo.******
Mida ya saa nne na nusu za asubuhi, Mschana mmoja mtu mzima alionekana akikatiza Mitaa ya bombambili kwenye mtaa wa nyumba za NHC, wenyewe wanapenda kupaita Nation House, akielekea upande wa stendi ya bombambili, maarufu kama Sanga one, huyu alievalia suruali nyeusi ya jinsi, pasipo kujali kama ilimpendeza kwa wembamba na umbo lake la kizee lilivyo, huku juu akivalia kijitisheti ambacho kiliacha tumbo lake wazi kiasi fulani kinachoweza kumuonyesha mpenzi mtazamaji, michirizi ya ajabu iliyojaa juu ya kitovu cha mwanamke huyu mtu mzima, “njaa inaniuma kweli kweli, ngoja nikanunue japo hindi nitafune” aliwaza mwanamke yule mtu mzima, ambae alikuwa anamaliza safu ya nyumba ya NHC na kukamata barabara inayopandishia stendi, “leo kazini inabidi niwe mjanja niondoke japo na hata elfu tano, maana hii ya kulala na njaa sio nzuri” aliwaza mwanamke yule ambae sasa alikuwa anazidi kuisoelea stendi, ambayo ilikuwa na watu wachache tofauti na inavyokuwa jioni, huku amekazia macho jiko moja la mchoma mahindi.
Mwanamke yule alifika pale akionekana kuwa ni mwenyeji wa pale, alichagua hindi moja na kuweka shilingi mia tano mezani, kisha huku akionekana mwenye njaa kali akauweka ule muhindi mdomoni na kuuma kwa nguvu, lakini ghafla ikasikika kah! mlio ambao ulimfikia mchoma mahindi kama vile mwanamke yule alitafuna kipande cha plastic, mchoma mahindi alimtazama mwanamke huyu kwa tahadhari, akamuona ameganda kidogo na muhindi wake mkononi, kisha akamuona anapeleka mkono wake mmoja usawa wa mdomo na kukinga kitu fulani alichokitema, muuza mahindi akatoa macho kwa mshangao.
Ukweli ni kwamba ilibakia kidogo tu atimue mbio, ni baada ya kuona yule mwanamke akiwa ametema vipande viwili vya meno na fizi yake, maana amezoea kuona watu waking’oka meno na sio pamoja na fizi, lakini kilicho mshangaza na kuona ni tofauti ni kwamba hakuona damu wala dalili za damu, na alipotazama vizuri akagundua kuwa meno yale yalikuwa ni meno ya bandia, “pole sana dada yangu kumbe unatatizo la meno?” alisema muuza mahindi lakini pasipo kujibu lolote mwanamke yule akaweka muhindi wake kwenye mkoba wake chakavu kisha akayakweka na yale meno yake halafu akaondoka zake kueleka kwa fundi wake anae muungia ungia yale meno toka siku alipovunjiwa na mtu ambae hakuwa anamfahamu hata kwa jina, siku aliyolala nae pale Kuchile pub, “huyu mshenzi siku nikikutana nae lazima anilipe meno yangu, kunifanya anifanye meno avunje halafu asiniachie hata shilingi?” aliwaza mwanamke huyu, ambae kwasasa naweza kukutajia jina lake kuwa ni Sina, kikiwa ni kifupi cha Sinamengi, ni yule muhudumu wa Kuchile bar alieshirikiana na Idd kumnywesha dawa Soraya ili abakwe na Idd na mwisho wa siku wakajikuta wanapeana wenyewe.*******
Mida ya saa tano kasoro ndio mida ambayo Hilda alifika Lijumbwi, kwa babu Mabudi ambae alimkuta ndio kwanza anatoka porini kutafuta dawa, “umewahi sana mjukuu, mizimu iliniambia kuwa utaingia hapa wakati wa jua la utosi (mchana wa saa sita mpaka saa saba)” alisema Mabudi ambae kimoyo moyo alikuwa anashangaa ujio ule wa ghafla na kuanza kupanga majibu ya maswali ya lawama, ambayo aliyatarajia, maana alihisi kuwa Hilda amekuja kulalamika baada ya kuona mambo hayaendi kama yalivyo tarajia, “kwani babu ulijuwa kuwa leo nitakuja” aliuliza Hilda kwa mshangao huku anakaa kwenye kipande cha ngozi, na babu akiwa anakaa kwenye kile kipande chake cha mti mule ndani anacho kitumia kama kiti au kigoda, “ndio kwasababu jana usiku mizimu ilianza kuona mafanikio yakija kwa kasi” alisema Mabudi ambae aliupenda ujio wa Hilda, kwasababu alitamani sana kitumbua cha binti huyu, ambae mara ya mwisho alimpapasa tu!, “babu unatisha, ni kweli bwana jana, kuna mambo mawili yalitokea” alisema Hilda kwa mshangao, huku moyoni mwake akianza kuamini kuwa matukio ya jana ni matokeo ya kazi ya Mabudi, kuanzia kukutana na Talib na kuchoma duka la mzee Frank, “yaani Talib amejileta mwenyewe” alisema Hilda lakini akamuona Mabud ameshangaa, akionyesha kuwa hakumjua Talib ndiyo nani, “ni kijana mmoja mtoto wa yule tajiri mwarabu Mahamud, halafu duka la mzee Frank limeunguwa moto lote” alisema Hilda kwa sauti ya uchangamfu, huku akitazama kwenye kijinguo cha mzee Mabudi, ambacho siku zote huwa hakina uwezo wa kuhifadhi zana za kilimo za mzee huyu, hasa anapokuwa amekaa, “nilishaona toka jana usiku, sasa leo inabidi uwe mvumilivu kidogo usiwe na haraka ya kuondoka, inabidi nikufanyie dawa ambazo akikuona tena atakuganda muondoke wote” alisema Mabudi ambae alimpa maagizo Hiilda azunguke nyuma ya nyumba kwenda kuchimba mihogo na kuhakikisha anaichemsha, “wacha mimi niingie porini nikakutafutie dawa” alisema babu huku ana chukua kopo kubwa la maji na kutoka nje wakiongozana na Hilda aliechukuwa kijembe fulani kidogo upenuni na ungo kisha wakaachana Hilda akiingia shambani na Mabudi akizama porini, Hilda hakujuwa kuwa anachoenda kutengenezewa kule ambacho kilimponza mama yake siku mbili zilizopita.*****
Baada ya kuongea sana na baba yake Higgno aliaga na kuelekea nyumbani kwake, akiwa amechukuwa baadhi ya vitu ambavyo aliona kuwa vingemfaa kupendesha kibanda chake endapo Soraya angekuja tena kule shambani, baadhi ya vitu alivyochukuwa ni shuka mbili safi, vyombo vya kupikia na kulia chakula japo vichache lakini vyenye mtazamo wa kisasa, mfano sahani zilikuwa za udongo kisha akaondoka zake kushika njia ya kuelekea Mahilo safari hii akipita njia ya mkato.
Lakini wakati anaondoka na hajafika mbali mara akasikia ngurumo ya gari ikisikika kwa mbali toka kule alikotoka, na mlio wa gari ambao aliufananisha na ule wa gari la Soraya, Higgno akasimama na kugeuka akitazama alikotoka, ….nawasisitiza wale wanaohitaji kujitolea chochote kitu basi namba hiyo 0717924403, inasaidia kupata fedha ya kununulia bando na matengenezo madogo madogo ya computer…………. ITAENDELEA
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE: Naam Mahamud akaifungua ile sms na kuanza kuisoma kwa tahadhari, “imebaini kuwa tajiri mkubwa Mahamud Abdulkarim ana lazimika kulala na binti yake kingono ikiwa ni imani ya kishirikina ambayo ina huusishwa na biashara yake ya usafirishaji, Mahamud na mke wake wana fanya hivyo wakitimiza mashariti ya mganga wao aliewaambia kuwa mschana huyu asitembee na mwanaume mwingine yoyote zaidi ya baba yake akifanya hivyo utajiri wake unatoweka, tajiri huyu anafanya kila mbinu kuzuia mwanae asiolewe na kijana Idd Mahadhi ili kutimiza sharti la mganga, watumie wenzako wafahamu”, alimaliza kusoma Mahamud na wakati huo huo mlango wa ofisi ukafunguliwa na wote waka tazama mlangoni……ENDELEA……….
Wakamuona mke wa Mahamud yaani mama Soraya akiingia mule ndani ya ofisi.
Naam wachumba wamepishana, nasubili mkeka wa iddy unavyotiki
 
Aisee Idd anakwama Parefu janja zake zimeshajulikana, na taarifa zake zimeshajulikana
 
Back
Top Bottom