TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NNE: alichokishuhudia kilimshangaza na kumzizimisha mwili mzima, maana alimuona mke wake ana tembea taratibu kama zombie akihesabu hatua moja moja, miguu ametanua, mmoja kushoto mmoja kulia, ungejuwa wazi hakutaka ikutane kana kwamba uvunguni kwake kulikutana na dhahama kubwa, “mama Hilda mama Hilda” aliita mke wa Njogopa, aliekuwa amekaa karibu na mume wake pale kwenye mabenchi waliyo kalia wakina mzee Komba ambae ni kama alikuwa ameshikwa na butwaa, huku akimtazama mke wake ambae alishtuka sana alivyoitwa na mke wa Njogopa …….. ENDELEA….
Mke wa Njogopa aliinuka na kumfuata mke wa Komba ambae bado alikuwa amesimama anatazamana na mume wake, “vipi shoga mbona unatembea hivyo kuna usalama kweli?” aliuliza mke wa Njogopa, huku akimtazama mama Hilda aliesimama miguu pande, zaidi ya miguu pande ile ya kiaskari kwenye gwaride, “mwenzangu yamenikuta, sijui kuna mdudu gani ametambalia, yaani ninawashwa haijawahi kutokea” alidanganya mama Hilda, huku macho yako kwa mume wake, “jamani amekutambalia kwa bibi?” aliuliza mke wa Njogopa kwa sauti iliyojawa na huzuni, akivuta picha ya maumivu ya muwasho anaoupata mama Hilda, yaani mke wa mzee Komba, “yaani penyewe pale pale pamfuleni (mtoni au kisimani, sehemu wachotayo maji)” alijibu mama Hilda huku ana muonyesha ishara mume wake ya kumuita, nae akainuka na kuwasogelea, “jamani pole, basi wacha nikuache uende na shameji akakuangalie” alisema mke wa Njogopa na kuondoka zake, akiwaacha Komba na mke wake wakielekea nyumbani kwao.
“Mke wangu, mbona unatembea hivyo umepatwa na nini?” aliuliza mzee Komba, huku akimkokota mke wake ambae tembea yake ilikuwa ni kwa shida kubwa, “ndugu yangu, wakati wakurudi nilibanwa na mkojo njani, nikaingia kichakani kukojoa sijui amenitambaa mdudu gani, yani hapa mpaka chupi nimevua, haivaliki nina washwa kama upupu, nime jikuta mpaka kum.. yote nyekunduuu” alisema mama Hilda, huku anaingiza mkono wake kwenye sidilia yake na kutoa nguo yake ya ndani akamkabidhi mume wake mkononi nae akaishika na kuitazama halafu akaendelea uibeba, huku wakiendelea na safari, na walipo kuwa wanakatiza kwenye kichaka kimoja pembeni ya barabara mita chache kabla hawajafika nyumbani, mara wakaanza kusikia sauti ya kike ikitokea kichakani, “sio huko bwana” ilikuwa ni sauti ya kulalamika ya kike toka kichakani, “mara moja tu nakojoa haraka, mbona siku ile tulifanya na haukuumia” ilisikika sauti ya kiume ikibembeleza kilevi, “lakini wanasema sio kuzuri kuzoea nitashindwa kuzaa” ilisikika sauti ya kike, ambayo mzee Komba na mke wake walishaijua kuwa ni sauti ya binti yao, “lakini si mpaka ufanye sana halafu siku ile uliniambia tamu au ulinidanganya?” iliuliza ile sauti ya kiume, nadhani kutokana na ulevi hawakujua kama walikuwa wanasikika nje ya kichaka, “hata kama tamu lakini sio vizuri” alisema Hilda, huku wazazi wake wanasikia kila kitu na kushindwa kupita haraka eneo lile kutokana na mwendo mdogo wa mama Hilda, “sasa ndio unanyima” iliuliza sauti ya kiume, “na wewe kwa kung’ang’ania, haya basi ingiza lakini ukichafuka shauri yako” ukweli mzee Komba hakutamani kuendelea kusikiliza zaidi upuuzi wa mwanae ambae alikuwa analipia kwa gharama kubwa sana ulanzi aliounywa jioni ile.
Hawakuelewa kilichoendelea kwasababu hawakusikia sauti nyingine yoyote toka kichakani mpaka walipo toweka eneo lile la kichaka, ikionyesha kuwa binti yao aliweza kuhiimili kile alichokuwa anafanyiwa, “unajua mama Hilda sasa ibidi tuwe tunanywea nyumbani” alisema mzee komba huku wakiingia eneo la nyumbani kwao, “baba Hilda bwana yaani mimi naugulia maumivu wewe una uzungumzia ulanzi” alilalamika mama Hilda, “hapana mama Hilda, we si unaona anachokifanya mwanao, sasa unataka niwe namuona akishikwa shikwa na vijana” alisema mzee Komba na hapo mke wake hakujibu lolote mpaka walipoingia ndani, “chukua ungo njoo nao chumbani”, alisema mama Hilda, huku yeye akiongoza chumbani, na mzee Komba akaigia jikoni ambako alichukua ungo na kuelekea chumbani ambako alimkuta mke wake amelala kitandani akitazama juu, yaani chali amevua nguo zote huku miguu ameitanua kwa nguvu na kuikunja kama anaehitaji kujifungua, japo giza lilikuwa limetanda lakini mzee Komba aliweza kukisia kuwa kitumbua kilikuwa kime achama vibaya sana, “nipepee baba Hilda” alisema mama Hilda na mzee Komba akaanza kupepea kwenye kitumbua cha mke wake, kama vile anapuliza moto wa kuni au mkaa, akiupeleka ungo juu na chini.
Kazi hiyo ilidumu kwa muda wa lisaa lizima mpaka mama Hilda alipopitiwa na usingizi, lakini kazi haikuishia hapo, maana kila mama Hilda alipojiziuka na kubana miguu maumivu yalimlipukia na kumuamsha mume wake akiomba kupepewa kwenye kitumbua chake, na mzee Komba alifanya hivyo pasipo kujua alicho fanyiwa mke wake, na kama angekuwa na taa mule ndani, angeweza kuona vitu vyeupe mfano wa tui zito la nazi likichuungulia kwenye mlango wa kitumbua cha mke wake.
Shughuli iliendelea maraa kwa mara karibia usiku kucha, hata kulipokucha mzee Komba alikuwa na usingizi kama wote, huku mke wake akiamka na unafuu fulani japo alikuwa anatembea kwa kuchechemea.******
Ni kweli ilikuwa siku ya juma tatu, siku ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na Familia ya bwana Frank, maana ndiyo siku ambayo kijana wao alikuwa anaenda kujaribu bahati yake ya kuomba nafasi ya kazi, na walikuwa na asilimia kubwa ya kijana wao huyo kupata moja ya nafasi za kazi kati ya zilizotolewa, maana alisha ahidiwa na tajiri Mahamud mwenye kamumpuni hiyo ya usafirishaji.
Saa moja kasoro tayari Higgno alikuwa ameshafika nje ya ofisi za Mahamud Trans, eneo la NMC ikiwa ni shirika la kiserikali la kuhifadhi nafaka akiwa mmoja kati ya watu wachache, ambao tayari walikuwa wameshafika eneo lile kwa muda ule, ambao ulikuwa ni mapema sana, maana muda wa kuanza mchakato ulikuwa ni saa mbili kamili za asubuhi, Higgno akajichanganya na wenzake na kuanza maongezi ya hapa na pale, hasa wakizungumzia mabasi mapya mengi waliyokuwa wanayaona mbele yao, ambayo ubavuni yalikuwa yameandikwa SORAYA EXPRESS, “huyu jamaa anamkwanja mrefu, unajua haya mabus ni mpya kabisa yapo kama ishirini hivi” alisema mmoja wao, “hivi kwanini haya mabus amebadili jina hajaandika Mahamud?” aliuliza kijana mwingine huku Higgno akiwa msikilizaji tu!, “hii ni kampuni mpya ya mwanae, anampenda kinyama” alisema yule wa kwanza, “ebwana hee! unamfahamu huyo Soraya mwenyewe, ni demu mkali kinyama, nilimuonaga kitambo wakati anasoma Songea Girls, alisema mwingine akimsifia mtoto wa tajiri mwarabu Mahamud, “namfahamu yule demu ni mkali kinoma, sijui nani atakuwa ana kula ule mzigo” aliongea mwingine wakimfuambua macho kijana Higgno, ambae mwanzo hakujua kama Mahamud alikuwa na mtoto wa kike, yeye alikuwa anamjuwa Talib pekee.****
Soraya aliamka miida ya saa moja na robo na kuanza kujiandaa kwaajili ya kwenda ofisini kuwa hoji na kuwatahini watu waliokuwa wanahitaji kuwaajili, ukweli Soraya muda wote alikuwa anajiandaa mawazo yake yalikuwa ni namna gani atampata kijana mpole, ukweli alitaka kuonana nae haraka sana kwasababu aliona wazi wazazi wake wanaanza kumshuku kijana mpole bila sababu yoyote, “lazima nikutana nae haraka, hata kama watakutana nae tayari mimi nitakuwa nimesha kutana nae” aliwaza Soraya ambae hata mimi sikujua ana maana gani.
Wakati anaendelea kuvaa mara akaingia Subira, ambae humu chumbani ni kama kwake, kwasababu alimlea Soraya katika chumba hiki toka akiwa mdogo, “Soraya unahitaji masaada wowote?” aliuliza Subira, akimaanisha kama Soraya alikuwa anahitaji msaada katika mavazi, “hapana nimesha maliza, alisemema Soraya aliekuwa anajifunga ile niqab yake, yaani kitambaa cha kuzuia uso wake, “sawa ila naona kama baba yupo tayari na Laylah ameshafika” alisema Subira, ambae hakutoka mule chumbani mpaka Soraya alipomaliza kujiandaa, na wakatoka kwa pamoja mpaka Sebuleni, ambapo alimkuta baba yake akipata kifungua kinywa, “assalam alaykum” alisalimia Soraya kwa sauti iliyo pooza, “waalaykum salam, umeamkaje Sor…” kabla hajamalizia tayari Soraya alikuwa amesha ondoka kueleka ofisini, mzee Mahamud akamtazama kwa mshangao, “mh! ana nini huyu, au ni kwasababu jana nilionyesha kumtilia mashaka huyo kijana wake mpole” aliwaza Mahamud, “lakini lazima nimtilie mashaka, kwanini awe yeye tu! usikute ni mmoja kati ya wanao panga haya matukio, bora yule alienisaidia mimi aliomba apate kazi akimaliza chuo……” hapo Mahamud akasita kidogo, kuna kitu alikumbuka, alimkumbuka kijana aliemsaidia lakini hakumkumbuka jina, japo kwa Sura alikuwa na uhakika wa kumtambua, “sijui kama barua yake ilipita kati ya zile tulizo zichagua?” alijiuliza Mahamud huku anatazama upande wa kolido ilipo ofisi, akamuona Soraya anakuja toka ofisini amebabe begi lenye barua za maombi ya kazi, alipo mtazama usoni alimuona wazi kuwa binti yake amekosa amani, “Soraya upo vizuri kweli mwanangu?” aliuliza Mahamud wakati huo mke wake nae anatokea upande wa vyumbani, “unadhani kuna jingine ni lile lile la jana tu!, anamfikiria huyo kijana wake mpole” alisema mama Soraya ambae alikuwa amevalia mavazi ya kushinda nayo pale pale nyumbani” hapo Soraya hakutaka hata kujibu wala kugeuka, akaanza kuongoza kutoka nje, “eti! Soraya” alisema mzee Mahamud, unaweza kusema alikuwa anataka kupima kama binti yake alikosa amani juu ya jambo la jana, bahati nzuri Soraya hakuwa na kiburi na haikuwahi kutokea kuwanunia wazazi wake, alisimama na kugeuka kumtazama baba yake, wakati huo mama yake alikuwa anakaa mezani pamoja na mume wake, “unakumbuka niliwahi kusema kuhusu kijana alienisaidia wakati ule nilipo vamiwa na wale vibaka” alisema mzee Mahamud na Soraya akakumbuka vyema juu ya kijana huyu, “namkumbuka baba” aliitikia Soraya kwa sauti ya upole isiyo changamka kama alivyo siku zote, “hoo! ni yule ulieahidi kumpatia kazi, aliomba nafasi kweli?” aliuliza mama Soraya, “ndio nilitaka kumueleza Soraya kuwa tuweke nafasi moja ya dharula, ili kama ikitokea hatukuipitisha barua yake basi tutampatia nafasi hiyo, maana nakumbuka hatukuchukua barua za mafundi wasio na uzoefu” alisema Mahamud, “ndiyo baba bila shaka” alisema Soraya na wakati huo alitokea Laylah na kusalimia, kisha akapokea begi Soraya na wakaanza kutoka nje.
Mahamud hakuwaacha waondoke, maana bado aliona ishara ya mwanae Soraya kuwa katika hali tofauti, Laylah anadaa gari langu tutatumia hilo kwenda ofisini” alisema Mahamud, hakuwa na lolote zaidi ya kuhitaji kuwa karibu na binti yake pengine angemshawishi kurudi katika hali yake ya uchangamfu, “ndiyo boss” aliitikia Laylah, kisha wakaendelea kutembea kutoka nje, “leo ni kasheshe, bint Mahamud amekataa kunywa chai” alisema Mahamud akimueleza mke wake, “lakini baba Soraya, unajua bado sijaelewa, nikwamba hutaki Soraya aolewe na huyo kijana au kuna jingine?” aliuliza mke wa Mahamud, “mama Soraya, siwezi kusahau kile huyo kijana alichomsaidia Soraya, na nina uheshimu msaada huo, lakini lazima nimuulize swali langu, ambalo akishindwa kulijibu au kama jibu sitoridhika nalo basi hata Soraya akilia machozi ya damu, sitomkubalia” alisema Mahamud, akimalizia kunywa chai na kutoka nje kuungana na wakina Soraya kuelekea ofisini.
Wakati huo Talib, ambae ni mmoja kati ya watu walioamka mapema siku ile alikuwa ana wachungulia dirishani kutokea chumbani kwake, akisubiri waondoke ili na yeye aondoke zake kuelekea Luhila kwakina Higgno, ambako alikuwa ana pafahamu vyema kabisa, lengo lake lilikuwa ni kwenda kumfundisha adabu bwana mdogo huyu kwa kumkosesha fedha nyingi sana alizoishia kuziona kwa macho, “au kwanini nisi fanye mchongo wa kuingiza majambazi humu ndani ili wakavunje lile kabati la fedha ofisini kwa mjomba” aliwaza Talib akiwa bado dirishani awatazama wakina Soraya, ambao walikuwa wanaingia kwenye gari pamoja na mjomba wake, kisha gari linaondoka Laylah akiliendesha taratibu kutoka getini.
Nalilipotokomea nje tu! hapo hapo Talibu akachukua kisu fulani kirefu na kukiweka kiunoni mwake, akikibana na mkanda wa suruali yake akifunika na tishet lake ndefu, kisha akatoka na kuingia nyumba kubwa, akaenda sebuleni kwa shangazi yake ambae alikuwa anamalizia kunywa chai, “shikamoo shangazi” alisalimia Talib, ambae hutumia salamu hii kwa shangazi yake tu!, “marahaba, vipi kuna shida” aliuliza mama Soraya huku anamtazama Talib aliekuwa amesimama anamkodolea macho, “shangazi nilikuwa nahitaji kwenda kutazama biashara inaendaje, sasa niazime elfu tano nitakurudishia nikirudi” alisema Talib na hapo shangazi akaguna kidogo, “mh! mara ngapi nimesha kuazima fedha halafu hukurudisha, we sema naomba elfu tano” alisema shangazi huku anainuka na kuelekea chumbani kwake akimuacha Talib ana waza namna ya kuzipata fedha ofisini kwa mjomba wake, “lazima nipange mpango huo, na jua hiki kibabu tuna kifungia kwenye gunia halafu tuna zama ndani wanakomba mkwanja” aliwaza Talib na wakati huo shangazi yake akaja na elfu tano akamkabidhi na yeye akaondoka zake.*******
Naam! Higgno akiwa pamoja na wale wenzake ambao sasa walianza kuwa kama marafiki pale nje ya eneo la ofisi ya Mahamud Trans, maongezi yaliendelea huku kila muda ulivyosonga ndivyo watu walivyozidi kuongezeka, na mpaka saa mbili kasoro tayari watu zaidi ya mia tatu walikuwa wameshajaa eneo lile, hakika licha ya kuwa alishapewa ahadi ya kupewa kazi mwaka mmoja uliopita lakini kwa uwingi wa watu hawa ulianza kumtia mashaka kijana Higgno.
Naam wakiwa wamezama kwenye maongezi mara wakaliona Nisaan Patrol likiingia, “huyoooo! alisema mmoja wao huku wanatazama gari lile ambalo lilikuwa limepandishwa vioo vya giza, yaani Tinted, ambalo lilikuwa linapita karibu yao, na ghafla likapunguza mwendo na hawakujua kwanini, lakini alikusimama likaelekea moja kwa moja ndani ya geti la uzio mdogo wa ofisi na kuingia ndani kisha geti likafungwa.
Hapo zikapita dakika kumi ndipo mlango mdogo ulio ambatanishwa kwenye lile geti la chuma ulifunguliwa na akatokea mschana mmoja ambae kwa mbali Higgno hakuweza kumfahamu mschana yule alikuwa ameshika karatasi, mkononi mwake akiongozana na mlinzi wa kampuni ya ulinzi, “sogeeni msikilize” alipiga kelele yule mlinzi, na hapo watu kama mia tatu hivi wakamiminika karibu na lile geti, “haya sikilizeni majina yenu, ukiitwa unaingia ndani sitaki vurugu” alisema yule mlinzi, kisha akachukua lile karatasi toka kwa Laylah na kuanza kuita majina, ni majina ya watu ambao barua zao zilishateuliwa, na hapo ndipo Higgno alipoweza kumtambua yule mschana kuwa ni yule mwanamke ambae ni dereva wa yule mschana ambae alimsaidia mara mbili, (ndivyo alivyo mtambua yeye Higgno)
Higgno akiwa makini kabisa anasikiliza jina lake, alisikiliza kwa muda mrefu huku watu wakiitwa na kuingia ndani mpaka alipoona kurasa zote mbili za karatasi la majina lilielekea mwisho na yeye kuanza kukata tamaa, “haya jamani, nitaita majina matatu ya mwisho, kama hautosikia jina lako tutaomba uondoke eneo hili” alisema yule mlinzi nakuanza kusoma tena yale majina, muda wote Laylah alikuwa makini kuangalia waliokuwa wanaingia ndani, na mara kwa mara alilikuwa anamtazama Higgno ambae bado alikuwa anashangaa kuona yule mschana dereva wa yule mschana wa kiarabu yupo hapa kwa Mahamud.
Aliita jina la kwanza na mwenye jina akaitika na kuingia ndani, jina lililofua lilikuwa ni Higgno Frank, “nipooo” aliitikia Higgno kwa sauti ya juu kabisa, huku akijipenyeza kwenye kundi la watu kusogelea geti akiwa na bahasha yake ya vyeti vya chuo cha ufundi, lakini ile anataka kuingia tu! akazuiliwa mlangoni na yule mwanamke dereva, “wewe ndie nani vile?” aliuliza yule dereva huku anapokonya ile bahasha kwa Higgno na kuifungua, “Higgno Frank” alijibu, Higgno kwa sauti ya upole, huku anamtazama yule mwanadada ambae nae uzuri wake sio wa pole pole, aliekuwa anachomoa vyeti vyake na kuanza kuvitazama.
Laylah, alitazama vyeti vile huku mwingine wa mwisho alieitwa aliingia ndani na akimpita Higgno alieanza kushangaa kwanini yeye anakaguliwa vyeti pale mlangoni, “Higgno unaishi wapi kwa sasa?” aliuliza Laylah, huku anarudisha vyeti kwenye bahasha, “naishi mahilo shambani kwetu” alisema Higgno, ambae kudanganya kwake ni mara chache sana, wakati huo watu wengine walikuwa wanaondoka eneo lile, ni baada ya kushindwa kusikia majina yao, “unaweza kunipa namba zako za simu?” aliuliza Laylah, huku akimtazama Higgno, “hapana dada yangu sina namba yoyote ya simu, hata ya baba yangu sijaishika kichwani” alisema Higgno, “kwani baba yako unaishi nae huko shambani?” aliuliza Laylah, “hapana kule naishi mwenyewe” alijibu Higgno kwa sauti ya upole, hapo Laylah, akashusha pumzi ndefu huku anatazama chini, kisha akatulia kwa sekunde kadhaa na kuinua uso wake kumtazama Higgno, “sikia kaka yangu, jina lako liliitwa kwa bahati mbaya, lakini ki ukweli hauna sifa za kuwa mwajiriwa wa kampuni hii, hivyo unaweza kwenda” alisema Laylah, huku anampatia Higgno bahasha yake, kisha akaingia pamoja na mlinzi na kufunga geti huku Higgno akikosa nafasi ya kukumbusha kuwa alikuwa ana ahadi na mwarabu Mahamud…… ITAENDELEA