SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Keshajiua na picha imeisha
Idd anakutana na vipingmizi viwili hapo, moja Soraya anazijua tabia zake tayari, mbili Talib anamjua vizuri Idd na tayari ameanza kupata wasiwasi, watakuwa maadui ambao kila mmoja anataka mali hizo hizo
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA: Hali hiyo ilikuwa hivyo hata kwa mama yake, huku Idd na baba yake pamoja na wale wazee wawili ambao walihisi kuwa Mahamud huwa anamshawishigi mwanae kukataa kuchumbiwa wakatabasamu kwa imani kuwa Soraya anamtaja Idd, “mbona simuoni?” aliuliza Soraya kwa sauti ya kunong’ona pia, huku anajitahidi kutazama vizuri upande alioelekezwa na yule mwanamke, “hujamuona tu?, hebu tazama vizuri kati ya wale wazee watatu kulia kwao si kuna yule kijana” alielekeza mwanamke yule na hapo macho ya Soraya yakatua kwa Idd, ambae macho yao yalipokutana na macho ya Soraya akaachia tabasamu pana………. ENDELEA…….
Tabasamu ambalo lilimchukiza Soraya, “huyu mshenzi nae yupo hapa” alijisemea Soraya huku anakwepesha macho yake na kutazama tena eneo lile lile aliloelekezwa, akawaona wale wazee watatu akiwepo baba mzazi wa Idd wana mtazama Idd ambae alisimanzika ghafla, “mbona simuoni bwana” alisema Soraya akitazama chini, na hapo yule mwanamke na watu wengine wakaingiwa na mashaka, “kwanza amefika saa ngapi?” aliuliza Soraya kwa sauti ya kunong’ona, “mjomba bado huja tuonyesha muhusika au bado huja muona?” aliuliza mjomba wake Soraya, na hapo tunaweza kugundua kuwa kila mmoja alitamani kuuliza swali kama lile kwa Soraya, baada ya kuona anashindwa kumuona mtu anae onekana wazi wazi kabisa, “bado sijamuona” jibu la Soraya ambalo lilitoka kwa sauti nyembamba na nyororo iliyojaa nidhamu na aibu ya hali ya juu, ya kujieleza kwa sauti, tena mbele ya watu wengi kama wale.
Hapo watu walicheka kidogo kwa kuona kuwa utani wa mwenyekiti umekuwa wa kweli, lakini kuna baadhi ya watu wachache walishajua kinachoendelea, “bi’Soraya umeshindwa kumuona mpendwa wako?” aliuliza Mwenyekiti huku watu wakiangua kicheko, wakihisi ni jambo la utani, Soraya akatazama tena lakini hakumuona mtu aliemtarajia, “lakini amefika saangapi wakati mimi nilitangulia?” Soraya alimuuliza yule mwanamke kwa sauti ya kunong’ona na kumfanya atoe macho kwa mshangao wa kutokumuelewa Soraya, “haya jamani mimi naona tusimchoshe Bi’Soraya ambae ametoka kwenye masaibu, hebu kijana simama akuone ili shughuri iendelee” alisema mwenyekiti, ambae baadae alijishtukia na kumtazama mjomba, “au tutakuwa tumekiuka?” aliuliza mwenyekiti, “ni kweli lakini kwa leo wacha tufanye hivyo ili kuokoa muda, na pengine ameshindwa kumuona kwasababu tupo wengi na wote tumevaa sare (alimaanisha Kanzu)” alisema Mjomba na hapo mwenyekiti akatazama upande aliokaa Idd ambae tayari alishaanza kupatwa na wasiwasi, “simama kijana, inaonekana leo umebadilika sana” alisema mwenyekiti na hapo watu wote wakamtazama Idd, ambae alisimama kwa kusuasua akiombea Soraya awe amesha uelewa uongo alioupanga na baba yake kumdanganya mzee Mahamud pamoja na wazee wa baraza.
Naam Soraya akiwa na hamu ya kumuona mtarajiwa wake akatazama kule waliko kuwa wanatazama watu wote waliokuwepo mule ndani, huku uso wake ukiwa katika nusu tabasamu na hofu ya shauku ikiwa imemjaa kifuani, lakini taratibu uso wake ulianza kubadilika na tabasamu kuyenyuka usoni mwake, kisha akatazama chini na kushika mikono yake akianza kuchezea vidole vyake.
Pale sebuleni palikuwa kimya kabisa, kila mtu akisubiri tamko la bi’Siraya binti Mahamud, zika pita dakika mbili, Idd akiwa amesimama bila Soraya kuongea lolote, “mjomba tuna subiri utuhakikishie kama huyu ndie mkwe mwenyewe” alisema mjomba ikiwa ni wazo ambalo wengi walikuwa nalo, pengine Soraya alikuwa anasubiri aambiwe athibitishe, lakini kitu ambacho wengi hawakukitegemea mschana Soraya alikuwa bado ameinamisha kichwa chini akatikisa kichwa kushoto na kulia kwa maana ya kukataa.
Hapo kila mmoja alishtuka na kutoa macho kwa mshangao, ikaanza minong'ono ya chini kwa chini, mingi ikiwa ni kushangaa kwanini mschana yule amefanya jambo kama lile, “biSoraya naona umetazama chini, hebu mtazame bwana Idd bin Mahadhi” safari hii aliongea mwenyekiti, ukweli Soraya aliinua uso na kumtazama tena Idd, aliekuwa bado amesimama, kisha akatikisa kichwa kushoto na kulia, akimaanisha vile vile kuwa anakataa, na hapo akazidi wachanganya watu, huku Idd alie onekana kufadhaika akikosa nguvu ya kuendelea kusimama na kukaa chini, tulia wewe mwenye kiti atarekebisha mambo” mzee Mahadhi alimweleza Idd kwa sauti ya kunong’ona, huku watuwote pia wakinong’onezana.
Hapo mwenyekiti pia akamtazama aliekuwa amekaa pembeni yake, “mbona sielewi elewi” alisema mwenyekiti kwa sauti ya kunong’ona, lakini mbona kama vile mwanzo alionekana kama mwenye furaha ya kutolewa posa” alisema yule mwingine kwa sauti ile ile ya kunong’ona, “hebu subiri kwanza” alisema mwenyekiti huku anainua uso wake kumtazama Soraya ambae alikuwa anajiandaa kuondoka pale sebuleni, “Soraya kumradhi kidogo” alisema mwenyekiti wa baraza, na hapo Soraya akasimama na kumtazama mwenyekiti japo hakuweza kumtazama usoni hata kwa sekunde mbili na kutazama chini, lakini mwenyekiti aliweza kuona machozi usoni mwa Soraya, “binti Mahamud, hujatoa jibu lolote tukalisikia, tunaomba utupe jibu nasi tuelewe” alisema mwenye kiti, huku watu wakiacha minong’ono na kusikiliza jibu la Soraya ambalo sasa alitakiwa kulitamka kwa sauti, (tutarudi).******
Naam Kijana Talib aliona kuwa daladala itamchelewesha, hivyo akaona ni bora achukue pikipiki ya kukodi, kipindi hicho Songea waliita yebo yebo, ambayo ilimpeleka mpaka mwembe chai nyumbani kwa Zido, ambapo nje ya nyumba hii, alikuta gari aina ya calina TI, na pikipiki mbili, akajua kuwa lazima watakuwa ndani, hivyo akaingia ndani na kuwakuta wamejaa pale uwani wakiugulia maumivu yao na kujaribu kumpa huduma ya kwanza yule alieteguliwa mkono, kwanza Talib alipowaona tu akahisi wenzake walikutana na ajari moja kubwa sana kama sio waliingia kwenye kambi ya wanajeshi kwa bahati mbaya, “oya imekuwaje tena mbona hivyo?” aliuliza Talib kwa mshangao, na hapo Vitus akaanza kumsimulia jinsi ilivyo kuwa, “yaani huwezi amini yule fala uliempora demu anajua kupigana mpaka nimeshangaa” alisema Vitus mwisho wa simulizi yake na kumshtua sana Talib, “au umemfananisha, yule fala anaweza kuwapiga namna hii?” aliuliza Talib akionyesha mshangao wa hali ya juu akukumbuka kuwauliza kuhusu kupokea simu, “ndio hivyo Talib, yule dogo utazania Jack chen, yaani anapiga makibadachi kama mchina” aliongeza Zido, na wakati Talib ana shangaa Vitus akauliza, “vipi yule demu amesemaje huko kwenu?” hapo ni kama Vitus alimkumbusha jambo Talib.
Hapo Talib aliwasimulia wakina Zido kilichotokea, na kinachoendelea kule kwao, “yaani yule fala Idd ndie anamuoa Soraya?” aliuliza Vitus kwa mshangao, “ndiyo hivyo, yaani hata mimi nimeshangaa sana, kweli ndege mjanja unasa kwenye tundu bovu” alisema Talib kwa sauti ya unyonge sana, akionyesha hajaridhika na kitendo cha Idd kumuoa Soraya.
Naam baada ya kujadili kwa muda mrefu, watu hawa wakakubaliana kuandaa mpango mwingine ili wahakikishe wanafanikiwa kile ambacho wamedhamiria, na baada ya hapo Talib akaomba nauli kwa wenzake ili arudi nyumbani, lakini ukweli ni kwamba hakukuwa na mwenye hata shilingi mia, kwasababu toka asubuhi hawakufanya biashara yao ya bangi na kumfanya Talib aondoke kwa miguu kurudi mjini ni mwendo wa kilomita kama nane hivi.******
Ukweli Higgno akiwa nje anaendelea kupika na kukausha samaki wake, huku anawaza na kuwazua matukio yaliyotokea mchana ule, hakujua kama ile simu aliyo iokota kule shambani kwa binti mwarabu ilishaita mara kadhaa kule ndani, na aliekuwa anapiga ni kijana Talib ambae mpaka sasa hakujua kama kijana huyu ambae alimpora Hilda toka kwake na kumdhihaki mara kadhaa, ndie binamu wa mschana mrembo, alie msaidia mara mbili (ambazo yeye anazifahamu).*****
Tukirudi nyumbani kwa Mahamud watu walikuwa wanasubiri sauti ya Soraya iseme kitu, jambo ambalo baba na mama Soraya au Laylah, dereva wake hawakuwa na shaka nalo, “sio yeye” ilikuwa ni sauti ya Soraya ambayo iliwasisimua na kuwashangaza watu wote waliokuwepo mule ndani, lakini ikawa tofauti kwa mwenyekiti ambae alicheka kidogo, “sasa nimekuelewa Bi’Soraya” alisema mwenyekiti, na watu wakashangaa kidogo ana maana gani, “kwa hiyo Soraya na Idd bado hawajaongea kwa jambo hili, lakini hatujachelewa, kwa kifupi huyo ni Idd bin Mahadhi na sisi wajumbe toka baraza la wazee tumekuja hapa kumsindikiza au kuiwakilisha familia yake kuja kuleta barua ya posa, akihitaji mutimize ibada ya ndoa kwa kuoana na kuishi kama mke na mume kama tuliovyoagizwa na mola wetu, na kwa umuhimu wa hilo unaweza kuona jinsi baba yako alivyoiandaa siku hii ya leo, kwa umuhimu wake basi tunaomba ukubali uchumba huu, na sisi tuweze kukabidhi barua ya posa” alisema mwenyekiti na hapo watu wakatulia kusikia Soraya atasema nini, “naomba muniwie radhi wazazi wangu na wageni wote mulio kuja hapa, ukweli ni kwamba ningejua kama kuna jambo hili hakika ningezuia pasifanyike maandalizi yoyote” alisema Soraya, kwa sauti ambayo ilikuwa ya upole ambayo ilikuwa ina ambatana na kilio cha kwi kwi, “kwanini Soraya tuweke wazi” alisema mwenyekiti kwa sauti ya upole, “tayari nina mchumba” alisema Soraya kwa sauti ile ile ambayo iliambatana na kilio cha kwikwi……… ITAENDELEA
 
Idd anakutana na vipingmizi viwili hapo, moja Soraya anazijua tabia zake tayari, mbili Talib anamjua vizuri Idd na tayari ameanza kupata wasiwasi, watakuwa maadui ambao kila mmoja anataka mali hizo hizo
Hamna
 
Back
Top Bottom