SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Leyla **** kwel atakuja kujuta anajifanya afisa mwajiri kumzuia boss mtarajiwa shenz kabisa 😀😀
Hana shida huyo, yupo kazini na ukizingatia tokea mwanzo barua ya jamaa ilipita kwa bahati mbaya.

Harafu tuachane na hayo, "jamani natafuta make wa kuoa, sharti awe hajui kusoma"🤣😂🔥😂🔥😂
 
Kwanini alitaka namba za simu wakat anaona hana sifa, Boss wake akijua atamfukizisha kazi
 
Hana shida huyo, yupo kazini na ukizingatia tokea mwanzo barua ya jamaa ilipita kwa bahati mbaya.

Harafu tuachane na hayo, "jamani natafuta make wa kuoa, sharti awe hajui kusoma"🤣😂🔥😂🔥😂
Hilda anakufaa kabisa
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TANO: “kwani baba yako unaishi nae huko shambani?” aliuliza Laylah, “hapana kule naishi mwenyewe” alijibu Higgno kwa sauti ya upole, hapo Laylah, akashusha pumzi ndefu huku anatazama chini, kisha akatulia kwa sekunde kadhaa na kuinua uso wake kumtazama Higgno, “sikia kaka yangu, jina lako lilitwa kwa bahati mbaya, lakini kiukweli hauna sifa za kuwa mwajiriwa wa kampuni hii, hivyo unaweza kwenda” alisema Laylah, huku anampatia Higgno bahasha yake, kisha akaingia pamoja na mlinzi na kufunga, huku Higgno akikosa nafasi ya kukumbusha kuwa alikuwa ana ahadi na mwarabu Mahamud ……. ENDELEA….
“huyu mwanamke anadhani na mimi nilikuwa mwanafunzi wa songea boys au?” alijiuliza Higgno kwa mshangao, akishindwa kuelewa alichofanyiwa na huyu mwanamke Dereva wa mschana mwarabu, halafu anafanya nini kwa huyu mzee, ina maana aliachaga kazi kwa yule maschana?” alijiuliza tena Higgno ambae aliendelea kusimama pale nje ya gate kwa dakika kadhaa, huku akiwaza afanye nini, maana hakuamini kama kweli ndoto zake za kupata kazi, zimeishia hewani, alitamani kugonga gate ili aombe kuonana na mzee Mahamud mwenyewe pengine ange mkumbuka au hata kwa kumkumbusha ilimradi apate kazi na kutimiza malengo yake ikiwa ni kupata kazi nzuri ambayo itampatia maisha mazuri, ambayo yange msaidia kupata mwanamke mzuri wa kumfanya mke wake, “sidhani kama mzee Mahamud anaweza kuninyima kazi, ikiwa nitakutana nae uso kwa uso” aliwaza Higgno, huku anaanza kuondoka taratibu eneo lile, nitamtafuta yeye mwenyewe, nitamtafuta kwa muda wangu, nadhani huyu mwanamke ameniwazia vibaya ndio maana amenikosesha kazi” hivyo ndivyo Higgno alivyo waza na kupanga huku analekea kituo cha dala dala na kupanda dala dala kuelekea nyumbani kwao.******
Wakati huo mzee Frank alikuwa dukani kwake anasubiri muda ufike na kijana wake aje kutoka kwenye maomba ya kazi akiwa na habari njema za kuwa amepata kazi, lakini wakati anasubiria wateja wake ambao mida hii sio sana kuonekana dukani, huku anamuombea mwanae mafanikio, mara akamuona kijana mmoja amesimama mbele ya dirisha la duka lake, “karibu kijana” alisema mzee Frank huku anasimama toka kwenye kiti, “naomba sigara” alisema yule kijana bila hata salamu kama ilivyo kwa wateja wengine wanapo fika pale dukani huwa wanasalimia kisha kueleza wanacho hitaji, mzee Frank akatoa sigara aliyo hitaji yule kijana mgeni machoni mwake na kumpatia pamoja na kiberiti, kijana yule akapokea na kuwasha sigara kisha akavuta funda moja kwa mkupuo na kutoa moshi kwa mwingi, “Higgno yupo” aliuliza yule kijana ambae hakika mzee Frank hakuwa anamfahamu, Higgno ametoka hata hivyo siku hizi hakai hapa, anaishi mashambani huko Mahilo….” alisema mzee Frank, na kabla hajamaliza kuongea yule kijana akamdaka juu kwa juu, “weeee! usijaribu kumficha huyo fala, nitakuharibia sasa hivi” alisema yule kijana kwa sauti ambayo ilionyesha ukorofi wa wazi kabisa na kumfanya mzee Frank ashangae, “kijana unamaana gani kusema hivyo mbona sikuelewi?” aliuliza mzee Frank kwa sauti ya mshangao, “utanielewa ukisha muona mwanao amededi, si unajifanya hunielewi” alisema yule kijana, ambae mzee Frank hakuwa anamjua kabisa, “kijana kuwa mstaarabu kidogo, umekuja hapa unahitaji sigara, na kabla hujalipa unaleta fujo za kitoto au ndio….” alisema mzee Frank na kama ilivyo kuwa mwanzo, kijana yule akamkatiza, “sigara ndio nini we mzee, acha mambo ya kijinga, unajuwa huyo choko wako amenipotezea fedha ngapi, tena amevuruga mipango yangu kibao” alisema yule kijana kwa sauti iliyo ashiria ukosefu wa amani, “unasema Higgno amekupotezea fedha nyingi kivipi?” aliuliza Frank, kwa sauti ya mshangao, “we mwambie huyo fala ajiandae nitakuja baadae kumfanyia kitu mpaka ajute kuingilia mambo yasiyo muhusu, yeye si anajifanya anajuwa kupiga, sasa amejiponza mwenyewe” alisema yule kijana, kisha akaanza kuondoka bila kulipia ile sigara.*******
Higgno pasipo kujuwa kuwa alikuwa ametembelewa na mgeni nyumbani kwao alielekea moja kwa moja mpaka matogoro kanisani, ambako ndio mwisho wa daladala na kuanza kutembea kwa miguu kuelekea mahilo, yaani kule shambani kwao, ni mwendo wa kilomita sita hivi toka aliposhukia daladala, akitumia lisaa lizima kwa mguu, njia nzima akiwaza kilicho mtokea, ilikuwa ni vigumu sana kuamini kilicho tokea.
Ukweli Higgno alikuwa na asilimia nyingi sana za kupata kazi, lakini kilichotokea ni kitendo cha ajabu sana kwake, yaani ndoto zake zimezimwa ndani ya sekunde chache tu, “yule mwanamke sijui nimemkosea nini mpaka anifanyie vile, sasa nikimuambia boss wake si anaweza kumfokea” aliwaza Higgno ambae toka mida ile mawazo yalikuwa ni hayo tu hata alipofika nyumbani kwake kule shambani, na akubadili nguo kisha akaingia porini kuanza kukagua mitego yake, ambayo alikuwa ana siku mbili hajaikagua, bahati ilikuwa kwake, Higgno alikuta mitego imenasa mawindo mengi sana kuanzia ile ya Ngolombwe (mnyama waporini mwenye kimo cha chini kidogo ya mbuzi, au swala), kanga, hata sungura na samaki kule mtoni, hivyo akabeba wanyama wake aliowakuta wakiwa na uafadhali, maana wengine alikuta wameshaanza kuharibika kutoka na kukaa muda mrefu kwenye mtego.
Higgno alipofika nyumbani akaanza kuandaa nyama ya Ngolombwe kwa kumchuna na kukata nyama ambazo aliona zinafaa kubanikwa na nyepesi kuziandaa, huku akifukia utumbo, miguu na kichwa, lakini huwezi amini licha ya kuwa busy na kukausha nyama ya Ngolombwe na sungura kadhaa walipo patikana na samaki pia ambao walikuwa ni wengi sana, lakini bado mawazo juu ya kukosa kazi yalimsumbua muda wote alijiuliza maswali yasiyo na majibu kutwa nzima, hata mida ya saa moja akiwa anaendelea na kazi yake, aliendelea kuwaza juu ya mschana yule aliemkosesha nafasi za kazi.
Naam saa mbili na nusu giza likiwa limedhaifishwa na mwangaza wa mbala mwezi angavu, mara akaona mwangaza wa taa za gari zikija barabara ile ya vumbi ya kutokea mjini, na lilipofika usawa wa shamba lao akaona kama gari lile lina sua sua kama vile dereva wa gari lile hakuwa na uhakika na kule anakoenda, mara akaliona gari lile linakata kona kuingia shambani kwake, hapo Higgno akajua kuwa ni wale jamaa wa jana wamekuja kumvamia hivyo akajiandaa kwa lolote.
Msomaji kabla hatujaendelea na kilichomtokea Higgno usiku huu, hebu tuone kwanini Layalah, alimkosesha kazi Higgno.*********
Turudi saa mbili kasoro za asubuhi, Mahamud na binti yake Soraya ambae muda wote akiwa anawaza juu ya kijana mpole, wakiwa ndani ya Nissan patrol lilikuwa linaendeshwa na mschana Laylah waliingia eneo la ofisi za tajiri huyu Mahamud, waliweza kuona watu wengi sana waliokuja pale kwaajili ya maombi ya kazi, “watu wengi hawana ajira” alisema Mahamud aliekuwa amekaa seat ya mbele pembeni ya dereva wake, huku Soraya akiwa amekaa seat ya nyuma peke yake akiwaza juu ya kijana mpole, kijana wa kwanza kumpenda na kuwa tayari kwa lolote, “Soraya inabidi usimamie kampuni kwa umakini ili tueweze kuitanua kampuni yetu na kutoa ajira nyingi zaidi” alisema Mahamud huku anageuka kumtazama mwanae, ambae licha ya kujivika niqab usoni mwake lakini alionekana wazi kuwa amenyongea, “ndiyo baba” aliitikia Soraya kwa kifupi, Mahamud akajuwa bado binti yake hakuwa sawa, hivyo akapeleka macho mbele.
Lakini wakati anapeleka macho mbele ndipo alipo muona kijana ambae kamwe sura yake asingeisahau hata kwa bahati mbaya, “punguza mwendo Laylah” alisema Mahamud huku akitazama kule walikosimama watu wengi waliokuwa wanasubiri ajira, na Laylah akapunguza mwendo, huku wote wakitazama kule alikokuwa anatazama mzee Mahamud.
Naam hapo ndipo moyo wa Soraya ulipolipuka kwa mshangao na mshtuko mkubwa, ni baada ya kumuona kijana mpole akiwa katika kundi la watu wanao subiri kuajiriwa, “unamuona yule kijana alievaa suruali ya kitambaa na shati la kuchomekea” alisema mzee Mahamud kwa sauti ambayo ilionyesha kuwa na shahuku isiyo na kifani, “huyu hata kama jina lake halitasomwa lazima apewe ajira, huyu ndie alienisaidia siku ile nilipo vamiwa na wale majambazi kule Msamala” alisema Mahamud na hapo Laylah akamtazama Soraya, ambae pia alikuwa anamtazama Laylah, kwa macho ya mshangao lakini wa furaha, “hoo! baba huyu ndie yule ambae ulisema anafaa kunioa” aliuliza Soraya kwa sauti ya uchangamfu, ikiwa ni mara ya kwanza toka kumekucha hata mzee Mahamud alifurahi kwa uchangamfu wa Soraya, kwanza alicheka kidogo, “ni kweli nilisema lakini simaanisha kama nitakulazimisha” alisema Mahamud, huku Laylah anakanyaga mafuta kuingiza gari ndani ya geti.
Yap! waliposimama na kushuka toka kwenye gari, mzee mahamud akaingia ofisini na Soraya abaki anamkabidhi Layla majina ya watu waliochagulia kufanyiwa majaribio ya ajira, “Laylah, nadhani umemkumbuka yule kijana mpole” alisema Soraya kwa sauti ya chini iliyojaa kihoro, “tena nimeshangaa kusikia kuwa ndie aliemsaidia boss siku zile” alisema Laylah kwa sauti ya chini pia, lakini bado ikiwa na mshangao, “sasa hakikisha haingii humu ndani, muambie akupatie namba yake ya simu pia hakikisha kama kweli anaishi kule shambani Mahilo” alisema Soraya huku anampatia karatasi zenye majina ya watahiniwa………. ITAENDELEA
 
🔥🔥🔥🔥🔥🔥
 
Back
Top Bottom