Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 2,117
- 5,240
- Thread starter
- #321
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA SABA: Naam hapo wote wakamuona mama soraya akija mbiombio ana simu ya mume wake mkononi, huku uso wake ukionyesha wazi kuwa alikuwa katika mashaka makubwa sana, “huuuwi baba Soraya najuta kupokea simu yako mume wangu, majambazi wame mkamata Soraya” alisema mama Soraya huku sauti yake ikiambatana na kilio, mzee Mahamud akainuka haraka na kumsogelea mke wake aliekuwa anakuja pale sebuleni na kuichukua yake toka kwa mke wake, “wanataka kuongea na wewe” alisema mama Soraya kwa saui ile ile ya kilio huku mikono akiipeleka kichwani, “kelele za nini sasa, mna mwaga mchele kwenye kuku wengi” alijisemea Talib kimoyo moyo huku usoni akijifanya kuwa katika mshangao…… ENDELEA
Mahamud akiwa wenye hofu na wasi wasi akaiweka simu sikioni na kuongea mara moja, “hallow mnashida gani na binti yangu” kisha akaonekana kutulia kimya akisikiliza kinacho ongelewa na mpigaji wa simu hiyo, na baada ya sekunde kama thelathini hivi akasikika tena mzee Mahamud akiongea kwa mara ya pili, “fedha nitawapatia lakini nawaomba msimdhuru mwanangu, pili naomba nusu saa nikusanye hiyo fedha” alisema Mahamud na kusikiliza jibu la ombi lake, inaonekana alisha kubaliwa maana alikata simu na kumtazama Talib, kisha akamuonyeshea ishara ya kumuita.
Talib akiwa anajuwa kuwa sasa anaenda kupewa fedha ya maana akainuka haraka na kumfuata mjomba wake huku akijitahidi kuficha furaha yake isionekane wazi usoni mwake, huku mama Soraya akiendelea kumporomosha kilio na tayari wanawake wengine ambao walikuwa wameshafika katika kundi la wegeni na wafanyakazi wake walishafika na kumchukua mama huyu kumpeleka kwenye chumba cha wageni kumtuliza, japo ilikuwa kazi bure kwasababu aliendelea kutiririsha kilio.
Wageni walio kuwa sebuleni ambao walishahisi kinachoendelea hivyo wakainuka wawili watatu wakajiunga na Talib kuongozana pamoja na mzee Mahamud wakaingia ndani ya ofisi ya pale nyumbani ya mzee Mahamud, “nini kimetokea bwana Mahamud” aliuliza mmoja kati ya wale ndugu na jamaa walio jiunga pamoja na Talib na mjomba wake, yaani bwana Mahamud alieonekana kubeba sura ya fadhaha na yenye wasiwasi kwa ghafla sana, “mwanangu ametekwa na majambazi wanahitaji million kumi ndani ya nusu saa, wameagiza nisimuambie mtu yoyote wala kuoa taarifa kituo chochote cha polisi, nikifanya hivyo watamuuwa mwanangu” alisema Mahamud kwa sauti iliyoonyesha wazi kuchanganyikiwa na tukio la kutekwa mwanae, huku anaelekea ukutani na kwenye picha yake kubwa na kuitoa ile picha, na hapo wote wakaona kipande cha mbao kilicho pachikwa mfano wa kizibo cha dirisha la kabati hata Talib ambae alishawahi kuingia mule ofisini mata kadhaa akaonekana kushangazwa na muonekano wa ile taswira, “wewe unaonaje Mahamud ni vyema kufuata maagizo hayo au utumie muda huo kuwa taarifu polisi ili….” alisema mmoja kati ya wale watatu walio ingia mule ofisini, lakini Talib akadakia haraka, “mh! anko usijaribu kuwazunguka wanaweza kummaliza kabisa” alisema Talib kwa sauti ya kukurupuka, kiasi cha wote kumtazama kasoro mzee Mahamud mwenyewe, ambae alikuwa anafungua kile kimfuniko cha mbao pale ukutani na kukuta kimlango cha chuma chenye funguo ya namba, “sikieni jamani, hata kama una mpango wa kupeleka hiyo fedha ni muhimu kushirikisha jeshi la polisi, inawezekana watekaji wanaamua kumuua Soraya mara baada ya kupata fedha zao ikiwa ni kufuta ushahidi wakihofia atakuwa amesha wagundua” alisema yule mzee alieshauri mwanzo, “ni kweli hilo ni wazo zuri, maana wamesema kuwa nimkabidhi Talib hizo fedha, hivyo basi Talib akiondoka kuwapekelekea na polisi nao waanze kumfuata Talib” alisema Mahamud, huku akimtazama yule mzee alietoa ushauri, wakati huo Talib alikuwa ana chezea simu yake kwa haraka sana kisha akaiweka mfukoni.
Naam wazo lile lilikuwa zuri sana kwa Mahamud ambae alifungua lile kabati na kutoa maburungutu ya fedha, zikiwa ni noti elfu kumi kumi, kila fungu likiwa na jumla ya million moja, na kuweka mezani akisaidiwa na Talib na wale wazee, alipomaliza akatoa simu yake na kuanza kutafuta namba ya mkuu wa polisi ambae angemsaidia katika swala lile la kumuokoa mwanae, huku Talib akionekana kuingiwa na uso wa mashaka, “nadhani huyu anaweza kuni saidia” alisema Mahamud, ambae alikuwa ameipata namba ya simu ya RTO, (Region Treffick Officer/kamanda wa usalama wa barabarani mkoa) ndie mtu aliemzoea kupita kiasi kutokana na kazi zake za kibiashara za usafirishaji, hapo Talib akajua kuwa mpango wake wa kwanza wa kupata fedha ambazo alikuwa anaziona mezani unaweza kushidwa, na pengine kufanikisha mpango wa pili, ambao ni wakumuuwa Soraya, “lakini anko…” kabla Talib hajamaliza neno lake mara simu ya Mahamud mkononi mwake ikaita, na alipoitazama ikaonyesha kuwa ni namba ile ile ya watekaji, “haooo wanapiga tena” alisema Mahamud kwa sauti iliyojawa na mashaka, huku anaipokea ile simu na kuiweka sikioni, “lakini nilisema mnipe muda wa kukusanya fedha sasa mbona…” alisema Mahamud kwa sauti iliyojaa wasi wasi, “sikia we mzee, najua una mpango wa kuwaambia polisi, sasa ukifanya hivyo usilete fedha ila subiri taarifa ya polisi ya kuokotwa kwa mwili wa Soraya” iliskika sauti nzito ya kiume ambayo iliambatana na kilio cha mbali cha Soraya akilalamika “niacheni jamani niacheni” hapo mzee Mahamud aliingiwa na hofu kubwa zaidi, “tafadhari usimdhuru mwanangu, sijaenda polisi wala kutoa taarifa polisi, nampa Talib fedha anazileta sasa hiv…” aliongea Mahamud na kabla hajamaliza kuongea mara akasikia kishindo cha kama vile simu ikidondoka chini na hapo ikakatika, hizi ni million nane wacha nipige simu msamala stendi walete million mbili ili Talib aende haraka, wamesema watamuuwa mwanangu” alisema Mahamud huku ana bofya simu yake kupiga kwenye ofisi yake ya msamala stendi.******
Wakati huo huo mzee Mahadhi na mwanae Idd, walikuwa wameshakutana na wazee wabaraza, wanaingia kwenye gari yao kuanza safari ya kuelekea kwa bwana Mahamud, “kijana umechukuwa maamuzi mazuri sana kumchumbia Soraya binti Mahamud, ni mschana mzuri anajiheshimu na wala hajawahi kusika hata mara moja amefanya yale ya kipuuzi yakuchukiza” alisema mmoja wa wazee waliopanda gari la bwana Mahadhi na Idd alikuwepo ndani yake akicheka cheka kicheko cha ushindi, “tena ni heshima kubwa sana kwa Idd kumchumbia binti wa Mahamud, nimepata kesi nyingi sana za vijana walioshindwa kupata nafasi hiyo” alisema mwingine, manaa mule ndani ya gari walikuwa wanne, yaani Mahadhi wazee wengine wawili na kijana Idd, ambae kama sio karafuu alizotafuna, basi mule ndani ya gari dogo wote wangekuwa wameshalewa kwa harufu ya pombe, “ni kweli bwana ilisadikika kuwa mzee Mahamud ndie anae mshawishi mwanae awakatae vijana wa Kiswahili ikiwa ni sehemu ya ubaguzi wa rangi” alisema mzee yule wa kwanza, “lakini mbele ya mwenyekiti sidhani kama ataleta ujanja wake” alisema Mahadhi, ambae ndie alikuwa dereva wa gari hili ambalo lilikuwa ni la pili toka nyuma, katika magari matano waliyokuwa nayo katika msafara ule, mbona yeye mke wake ni mngoni, kwanini yeye amzuie mwanae” alisema Idd, ambae uongeaji wake na sauti yake kama wale wazee wange kuwa makini basi wange gundua kuwa Idd alikuwa amelewa, baada yake walicheka kwa kumuunga mkono, “wala usiwe na wasi wasi kijana, kwa mwenyekiti amekwama, namfahamu yule mzee kwa maneno yake ya busara na mitego” alisema mzee mwingine huku safari inaendelea pasipo kujua kuwa huko kwa mzee Mahamud mambo yalisha haribika.******
Tayari Laylah alishapata nafuu na maumivu kuisha kabisa, hivyo akaruhusiwa kuondoka pale hospital, nae akaona itakuwa vyema akielekea nyumbani kwa boss wake akawajulishe hali yake, kisha aende nyumbani akapumzike, Laylah akiwa njiani aliendelea kutafakari hili na lile juu ya sabuni aliyokula na kumvuruga tumbo, hakika licha ya kuwaza kwa muda mrefu lakini alikosa jibu.
Lakini Laylah alipofika nyumbani kwa mzee Mahamud au ikulu ya mwarabu kama wanavyo paita na kukuta kuna mambo mengi yanaendelea pale nyumbani, kwanza maandalizi kama ya sherehe ndogo, hivyo akamtafuta Subira mfanyakazi wa Soraya, yaani yaya, na kumuuliza, “ndugu yangu kuna makubwa yametokea leo, mwenzio leo yule kijana Idd anakuja kuleta barua ya posa, wakati huo huo Soraya mwenyewe ametekwa na majambazi” alisema Subira kwa sauti iliyojaa masikitiko, ujue Subira ndie yaya wa Soraya toka Soraya akiwa mtoto mdogo sana, “mh! mbona makubwa Soraya kutolewa barua na Idd, Soraya kutekwa na majambazi” alishangaa Laylah na hapo kwa haraka akaanza kuchezesha akili, “mh! nimetoka nyumbani nikiwa mzima kabisa, nikashikwa na tumbo la ghafla na kushindwa kumpeleka Soraya shambani, Soraya kutekwa nyara, mbona kama kuna mchezo umechezeka,” aliwaza Laylah, “kwani Soraya mwenyewe ana fahamu kama leo anatolewa barua?” aliuliza Laylah, “ajue wapi wenzio wanataka wamshtukize ili ashindwe kukataa” alisema Subira na kumfadhaisha Laylah, “ina maana boss ameshindwa kuelewa kuwa Idd ni kijana mbaya kwa Soraya” alisema Laylah, “lakini mimi nina mashaka na Soraya, unadhani amesha gundua na kujisingizia ametekwa?” aliuliza Subira kwa sauti ya chini, “eti eeh! hebu ngoja kwanza nijaribu kumpigia” alisema Laylah huku anatoa simu yake na wote waka sogea pembeni zaidi huku Laylah anabofya simu yake na kuipiga namba ya Soraya.******
Sio kwamba tumewasahau babu mabudi na mama Hilda, hapana wakati kule mambo yanaendela hebu twendeni shambani kwa Soraya ambako mambo yalikuwa hivi.
Mara baada ya wale wakulima wake kukimbia na kutokomea upande wa mtoni, baada ya kuwafanyia ujanja na kuwatoroka wale watu alio wahisi ni majambazi, ambao walijiondoa lile vumbi na kumsogelea yeye Soraya ambae alikuwa amekamatwa na mmoja wao, “oya jamani eeh, huyu mtoto mimi simuachi hivi hivi, lazima nitoe gundu la kumla mtoto wa kiarabu” alisema mmoja wao na Soraya kusikia hivyo hata mwili ulimsisimka, maana alianza kuvuta picha ya maumivu atakayo yapata huku akisikilizia jibu atakalopewa na wenzake, “weweeee unaongea sasa hivi wakati mwenzio Zido alishapanga toka nyumbani, yaani akimaliza tu na mimi naingia” alisema mwingine huku Soraya akishindwa kuwatambua kwa sura vijana hawa
ambao bado walikuwa wamejiziba sura yao, “msinifanye hivyo nitawapa hela muniachie” alisema Soraya kwa sauti ya kinyonge iliyoambatana na kilio, hawa jamaa vipi si waje basi tumalize kazi” alisema mmoja wao na wakati huo huo wakasikia ngurumo ya gari, wakageuka kutazama upande ule na wakaliona Toyota carina likiibuka toka upande wa daraja la mahilo, “haooo! wanakuja” alisema mmoja wao huku wanaendelea kulitazama lile gari dogo ambalo lilisimama upande ule wa barabara, na wakashuka jamaa wawili ambao pia walivaa sox kama za wenzao, ambao waliwasogelea mpaka pale walipo, na walipowafikia Zido ambae bado aliziba uso alimsogelea kabisa Soraya aliekuwa bado ameshikwa na yule jamaa, “safi sana, sasa tuwasiliane na baba yake” alisema Zido huku akimtazama Soraya kwa macho ya tamaa na uchu, kisha akatoa simu yake na kupiga kwa mzee Mahamud na ndipo simu ilipo pokelewa na mama Soraya, hata hivyo alipewa Mahamud mwenyewe na kisha Zido akatoa maelekezo, kuwa wakitaka amuachie Soraya apewe million kumi na fedha hizo apewe Talib asiongozanae na mtu yoyote, na wala taarifa isifike polisi, “kwasababu kufanya hivyo ni kumpoteza Soraya” alisema Zido kwa msisitizo huku Soraya mwenye akisikia kwa masikio yake.
Kama tulivyosoma kwenye kipande kilichopita nyumbani kwa Mahamud, ni kwamba wakati wakiwa wanasubiri mpangilio wa fedha, huku wanapanga kumuingilia kimwili Soraya, Zido akipanga kuwa wakwanza kisha Vitus halafu wale wengine wanne kila mmoja akitaka kufanya hivyo, hakika Soraya alikuwa katika mashaka makubwa sana, wasi wasi na machungu makubwa, Soraya alililia kwa sauti akiomba wasi mfanyie kile walichohitaji kukifanya kwenye mwili wake, lakini hawa jamaa hawakuonyesha dalili ya kumuelewa Soraya.
Lakini wakati wanataka kumpeleka kwenye kibanda kidogo kilichopo pale shambani kwa lengo la kumuingilia kimwili mschana huyu mrembo wa kupindukia, mschana ambae alikuwa ndoto ya kila kijana mwenye fedha mjini Songea, mara ukaingia ujumbe kwenye simu Zido, ambao aliufungua na kuanza kuusoma kwa sauti “oya sikia, “jamaa anasema mwarabu anataka kututumia polisi hivyo tumpigie simu kumtisha” alisema Zido na kuanza kupiga simu kwa mzee Mahamud.
Hapo ndipo Soraya alipoanza kugundua kuwa mpango wa kumteka umeanzia kwa mtu wa karibu wa familia yao, ambao moja kwa moja alihisi kuwa ni wafanyakazi wa pale nyumbani kwao, na wakati Zido anaongea na simu yeye wakaanza kumkokota kumpelaka kwenye kibanda huku anapiga kelele za kuomba msaada, lakini wakati huo huo akasikia kishindo cha “guh!” kilichotokea pale alipokuwepo Zido, wote wakageuka kutazama wakamuona Zido akiwa ameanguka chini huku simu yake ikiwa pembeni imeanguka, karibu yake amesimama kijana mmoja alievalia kaptura ya jinsi bila ya shati “kijana mpole” alinong’ona Soraya, ambae uso wake ulianza kuachama kwa tabasamu la matumaini na furaha, tabasamu ambalo lilipochanua usoni mwake lilianzia tumboni kifuani mpaka usoni kwake…… ITAENDELEA