SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA TATU: alisema bwana Mahamud, huku kila mmoja anasiliza kwa umakini, “ila kwa kweli nisiwafiche ndugu zangu, sina uwezo wa kuileza familia yangu hasa Soraya mwenyewe juu ya jambo la ndoa kati yake na Idd na akanielewa, kama kweli mtaweza kumshawishi Soraya kwa namna yoyote mimi sina maneno” alisema Mahamud na wakakubaliana kuwa siku ya jumapili saa saba mchana baada ya swala, kuna wazee wataenda nyumbani kwa bwana Mahamud ili kufikisha ujumbe wa uchumba, wakipanga kuwa iwe ni jambo la kushtukiza… ENDELEA
Basi mzee Mahamud alikabidhiwa mkoba wa mwanae Soraya, kisha wakaogozana kutoka nje, wakiongea kwa furaha na amani kiasi cha kuwashangaza wakina Soraya waliokuwa wana mngojea mzee Mahamud, hakika usingejua kama kuna tatizo lilikuwepo kati yao, kilichowafanya Soraya na mama yake wajuwe kuwa walikuwa katika maongezi ya tukio la jana ni ule mkoba wa Soraya uliobebwa na mzee Mahamud, ambae alimkabidhi yeye mwenyewe, “angalia kama vitu vyako kama vipo vyote” alisema mzee Mahamud.******
Wakati huo nyumbani kwa mzee Komba, mama Hilda alimuwahi Hilda kabla hajaenda kusaka mtu wa kumnunulia pombe pasipo kujari gharama ya malipo yake itakuwa nini na kwa kiasi gani, maana hutokea wakati mwingine akanywa pombe nyingi, hata kununuliwa mishikaki na kupewa elfu mbili au moja ya kuondoka nayo, lakini kwenye malipo angetoa kitumbua na mlaji angetumia hata dakika mbili angekuwa amesha maliza na kuondoka zake, huku wakati mwingine hutokea mtu akampatia bia mbili au kopo nne za ulanzi wa mia tano tano, lakini malipo yake yaka chukuwa nusu saa nzima, akigawa kila kona ya mwili wake, ambayo ingesuguliwa kweli kweli, “mwanangu njoo nikuambie kitu, huko unakoenda utaenda baadae” alisema mama Hilda na kuanza kumueleza Hilda juu ya uamuzi wake yeye na baba yake wa kwenda kutengeneza mambo kwa mganga ili kuwa komoa wakina Higgno, na kumsaidia yeye kufanikiwa katika maisha haswa katika swala la kutulia na mwanaume wake ambae ni Talib.
Mwanzo Hilda alitaka kukataa mpango huo, kwasababu alikuwa anajuwa fika kuwa mambo yanayo mkuta sababu sio familia ya bwana Frank, ila ni yeye mwenyewe na ujinga wake, lakini aliposikia swala la kutulia na Talib hapo akakubali mara moja, kwasababu aliona akifanikiwa kumtuliza Talib basi maisha yake yatakuwa mazuri, “hapo mama umeongea, sasa tunaenda kwa mganga gani” aliuliza Hilda kwa shauku, “tutaenda kule mshambani Ngwendema, kuna kile kibabu Mabudi, kile kinaweza sana” alisema mama Hilda na hapo wakakubaliana kuwa wajiandae ili waondoke zao, yaani Hilda mama yake na mtoto wa Hilda.********
Naam huku mjini maeneo ya msikiti wa mkoa, Familia iliingia ndani ya gari na safari ikaanza kuelekea nyumbani, huku Soraya aliekuwa anaendesha gari lile pamoja na mama yake wakisubiri kwa hamu kusikia kilichozungumzwa huko ndani huku Talib akiwa kama wengine, hakujuwa kilichokuwa kinaendelea, alitulia akionekana kijana safi anatoka msikitini kufanya ibada, “hawa wana mipango gani?” alijiuliza Talib, ambae kwa haraka ungejuwa kuwa amekuja pale msikitini kwaajili ya swala, lakini ukweli safari hii ilikuwa mahususi kwaajili ya kuchunguza ratiba ya Soraya, ambae mara nyingi ijumaa huwa anaenda shaambani kwake, “vipi huko wamesemaje?” aliuliza mke wa Mahamud ambae alikuwa amekaa seat ya mbele katikati pembeni ya mume wake aliekaa upande wa kushoto, hapo Talib na wengine wakatega sikio kunasa umbea, “wamefafanua ilivyokuwa, kumbe kuna mtu ambae alifanya hivyo kwa lengo la kuwaibia maana waliwekewa wote wawili” alisema mzee Mahamud, huku safari inaendelea, “nani aliesema hivyo Idd au baba yake?” aliuliza Soraya kwa sauti ya hamaki, “alielezea baba yake, lakini alielezwa na Idd mwenyewe, kwasababu na yeye ameokotwa asubuhi akiwa amelala kwenye gari hajitambui” alisema Mahamud, ambae licha ya mashaka aliyokuwa nayo juu ya Idd, lakini alijifanya kuwa ameamini maneno ya Mahadhi na kijana wake, ili kusikia maoni ya mwanae Soraya, “hapana baba, na uhakika yeye tu, ile chupa yake ilikuwa inanuka pombe kabisa, ina maana mpaka analewa hakujuwa kama ni pombe?” aliuliza Soraya, huku Talib akijitahidi kutafsiri mazugumzo yale ili apate maana kamili ya maongezi yale yanayo muhusisha Idd, na akichanganya na mashaka yake juu ya ukimya na kuto kuonekana kwa Soraya jana usiku, “wameeleza mbele ya baraza la wazee, hivyo kuna mambo wameshauri na wamesisitiza tuelewe” alisema mzee Mahamud, “lakini baba Soraya, hata kama tuna potezea lakini ukaribu wa Soraya na Idd mwisho ilikuwa jana” aliongea mama Soraya akimaanisha anacho sema, kisha kikapita kimya kirefu huku gari likiendelea na safari, sauti ya redio ikiendelea kuwapa mwaidha ya ijumaa ile.*******
Baada ya kumaliza maongezi na baba yake na kupata chakula cha mchana kwa pamoja na wazazi wake, Higgno aliaga kuanza kuondoka kurudi nyumbani kwake kule shambani akipanga kwenda kumalizia kukagua mitego ya kanga na samaki na mingine ambayo hakuwa ameikagua asubuhi.
Higgno alitembea kwa haraka huku anakumbuka tukio la jana jioni kule bomba mbili alipomsaidia yule mschana aliekuwa amelewa sana, mschana ambae licha ya kuvaa mavazi nadhifu ya kiislam na kuonekana kuwa ametokea kwenye familia ya kitajiri lakini alionekana kuwa hakuwa anajitambua kwa ulevi, “dah! eti twende nyumbani, halafu wazazi wako wange ni bananisha na kusema mimi ndie niliekunywesha pombe” aliwaza Higgno huku akiendelea kutembea kwa speed, “ila mimi inabidi niache tabia ya kupiga piga watu, naweza kuuwa siku moja halafu kesi iwe kwangu… alafuuuu mbona yule aliemuita mama ni mweusi sio mweupe kama yeye” aliwaza Higgno ambae hakumaliza hata kijiji, mara akashtuka akikutana na wakina Hilda mama yake na mtoto wa Talib, yaani ile ghafla hawa hapa uso kwa uso, “shikamoo mama” alisalimia Higgno, huku akimtazama mama Hilda ambae alikuwa anatazama chini kama mwanae Hilda kwa macho ya aibu, “marahaba” aliitikia kifupi, huku akikwepesha macho yake yasikutane na macho ya Higgno sio tu mama Hilda hata Hilda mwenywe alikuwa hivyo hivyo.
Higgno hakuweza kuhoji lolote, kwssababu licha ya kukumbuka kilichotokea baina yao, pia hakuona sababu ya kufanya hivyo, akapiga hatua kuwaacha, lakini alikuwa amemsahau mmoja wao ambae kwa namna moja au nyingine hausiki, na wala hajui chochote, “baba umeniletea pipi?” aliuliza mtoto wa Hilda aliezaa na Talib, huku akionekana mwenye furaha baada ya kumuona Higgno baba yake wa hiyari, hapo mama Hilda na Hilda wakainua nyuso zao kumtazama Higgno, kuona ana muonekano upi wa sura yake, yaani kama ni hasira, na atamjibu nini yule mtoto, wakitegemea jibu baya na kali toka kwa Higgno, lakini baada yake wakashangaa kuona tabasamu usoni kwa Higgno, “sijabeba pipi, lakini utaenda kununua dukani” alisema Higgno huku anaingiza mkono mfuni kwake na kuibuka na noti kadhaa za elfu mbili mbili, akaichomoa moja na kumkabidhi yule mtoto ambae licha ya kukaa pamoja na Higgno na mama yake na kushuhudia mengi lakini hakuwa anayatambua maana yake, na yeye kuendelea kumchukulia Higgno kama baba yake.
Naam sio Hilda wala mama yake, hakuna aliekumbuka kumkumbusha mtoto yule mdogo kusema asante kwa Higgno, zaidi ya kutoa mcho yao kwa mshangao wa kuto kuamini, wakimtazama Higgno akiondoka zake na kutokomea mwishoni mwakijiji, wao wakija taratibu huku Hilda akiwaza na kuuchanganua moyo wa Higgno, ambae siku zote amemuonyesha moyo wa kibinadamu kama ilivyo kuwa leo, ame toa fedha ambayo yeye hutafuta kwa jasho na kuvumilia atakachofanyiwa na walevi kwa Elfu mbili hiyo, lakini leo imetoka bure kabisa, “hivi mama baada ya Talib kwanini tusimwambie mganga amfanye Higgno awe mwanaume wangu” aliuliza Hilda baada ya kufikiria kwa dakika kadhaa, “hata mimi naona hilo kama linafaa, maana huyu kijana ana moyo mzuri sana” alisema mama Hilda ambae alitulia kidogo, akiwaza jambo kabla hajacheka, tena mwenzio hapa nilikuwa na waza tutatoa wapi hela ya lamri, bahati nzuri tumeipata kiulaini kabisa, tutafute sehemu tuchenji” alisema mama huyu akionyesha kufurahia ile hela ya Higgno, “mama bwana ina maana Higgno ametoa hela ya kwenda kumtengenezea mwenyewe” alisema Hilda na wote wakacheka, “kwani hujui ng’ombe huwa anapikwa na mafuta yake” alifafanua mama Hilda.*******
Baada ya kufika nyumbani na kupata chakula cha mchana Soraya na Laylah wakaingia kwenye Land Rover discover na kuanza kuzunguka mtaani pengine wange kutana na Kijana mpole, mtaa wa kwanza kabisa ulikuwa ni bomba mbili, ambako walizunguka kila kona, wakidhania kuwa pengine kijana yule anaishi kule bomba mbili kwa sasa, lakini mpaka adhana ya magharibi ina adhiniwa hawa kuwa wamemuona kijana huyu, hivyo hawa kuwa na budi kurudi nyumbani, ambapo waliswali kwa pamoja, kisha Soraya akamsindikiza Laylah kwa gari na kurudi mwenyewe, kwasasa ni kama walikuwa marafiki tu.
Wakati huo huo Talib nae alishaenda kukutana na rafiki zake wakina Vitus na Zido, alienda kuwapa taarifa ya kughairishwa kwa safari ya Soraya kwenda shambani, hivyo wakaambizana kusubiri hiyo jumapili.********
Ukweli maisha yalikuwa magumu sana kwa yule mwanamke muhudumu wa pale Kuchile bar, ambae alilala na Idd usiku kucha, alishinda kutwa nzima akishindwa kuhudumia vizuri kutokana na kuto kueleweka vizuri kwa wateja, kutokana na meno yake kukanyagwa na Idd, na alipoona mambo yamezidi akaomba ruksa kwa manager wake akakimbia mtaani na kununua super glue, ambayo alijitahidi kuyanunganisha yale meno mpaka alipoweza na kurudi tena kazini na kuendelea na kazi zake, huku akikumbuka jinsi alivyo fanyiwa na Idd ambae alimfanyia mambo ambayo hakuwahi kufanyiwa na mlevi yoyote kwa miaka ya karibuni, “kunyonywa kitumbua” hakika mwanamke huyu alijikuta anatabasamu kila alipo kumbuka tukio hilo, hakufikiri kero ambayo mwenzie aliipata mara baada ya kugundua hali yake ya vidonda sehemu zake za siri, yeye alichowaza kuwa ikitokea akakutana nae basi itakuwa burudani kwake, kuanzia pommbe na kufaidi dudu.********
Hilda na mama yake wakiwa na mtoto mdogo wa Hilda alie
zaa na Talib, mida hii walikuwa mashambani, huko Ngwendema kilomita sita toka Luhila seko, ndani ya kibanda kimoja cha udongo ambacho kuta zake zilikuwa zime egama upande, kosa kushikizwa na miti kama kiegemeo basi mpaka sasa ingekuwa imeanguka, nyumba hiyo ambayo ilikuwa imezungukwa na vichwaka virefu vya nyasi na miti iliyo achiana nafasi, kilitundikwa tunguli zenye vijikamba vyekundu na vyeusi huku mipaka (paka/nyau) ya kila rangi ikiranda randa mida yote kuzunguka nyumba ile ambayo ukiachia Mganga mabudi Hilda mama yake na mtoto mdogo wa Talib, hakukuwa na mtu mwingine upweke ulizizima.
Hali ilionyesha kuwa tayari matibabu yalishaanza na yalikuwa yanaelekea kwenye hitimisho, “kwahiyo unataka bwana Frank na mke wake wawe masikini na wachukiwe na kila mtu pale mtaani, halafu binti yako aolewe na mtoto wa bwana Frank” aliuliza babu Mabudi mwenye umri wa miaka sabini, ambae alikuwa amekaa kwenye jiwe ambalo ndilo hutumia kama kiti chake, huku akiwa amejifunga kijinguo fulani ambacho kiukweli lengo lake ni kuziba sehemu muhimu za siri, japo hakikuweza kufanya hivyo na kusababisha wakina mama Hilda na Hilda, mwenyewe waliokaa chini kwenye kipande cha ngozi, wajionee wazi wazi sehemu nyeti za mzee huyu, “ndiyo baba yangu, yaani amekuwa kero kubwa katika maisha yangu na familia yangu” alijibu mama Hilda, “lakini mama mbona inaonyesha huyu bwana hana matizo yoyote na wewe, kiasi cha nyie kuhitaji binti yenu kwenda kuishi na kijana wake?” aliuliza babu Mabudi, “hata kama babu, lakini wamekuwa wakijidai sana na kutunyanyasa na umsikini wetu” alisisitiza mama Hilda.
Hapo mzee Mabudi alitulia kidogo, kama kuna kitu anatafakari, kabla hajainua uso wake na kumtazama Hilda, kisha akamtazama mama yake halafu akamtazama tena Hilda, “haya mama nitawasaidia, kwanza nimchanje huyu binti ili akionekana mbele ya kijana mwenyewe ampende hapo hapo na asimuachie hata kidogo, na hilo la kuwa susha hao wengine nitakupa dawa, utaenda kuweka karibu na kwao, ili wanapokanyaga tu iwe ndio umasikini wao” alisema Mabudi na hapo akamtaka mama Hilda aondoke nje na yule mtoto mdogo ili yeye aweze kubakia na Hilda mule ndani aweze kumchanja.
Mama Hilda alimchukuwa mjukuu wake na kutoka nae nje ya kibanda, akimuacha Hilda amekaa kwenye kipande cha ngozi mbele ya babu Mabudi “haya simama mjukuu wangu” alisema babu Mabudi huku na yeye anasimama na kusogea kwenye mkoba mmoja uliotundikwa kwenye mti uliokuwepo kati kati ya kibanda kile, “vua nguo zote mjukuu wangu wala usiogope” alisema babu Mabudi, ambae hakugeuka nyuma zaidi kuanza kupekuwa mkoba wake na kuibuka na kisu kidogo na kijifuko fulani kidogo kilichofungwa pia, kisha akageuka na kumtazama Hilda ambae alikuwa amevua gauni lake na kubakia na chupi na sidiria, mjukuu wangu wala usiogope vua tu tukamilishe dawa” alisema babu Mabudi, huku anasogea pale alipokuwepo Hilda ambae alikuwa anajiuliza avue au asivue…. ITAENDELEA
ila Hilda kapigwa aseee
 
Back
Top Bottom