SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA TISINI
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TISA : Naam ni kweli swala hili liliwashtua vibaya sana, Mahamud na mke wake, na kuanza kujutia kile walicho kifanya kwa haraka haraka bila kuchunguza na kabla hawaja juwa wafanye nini wakasikia ngurumo ya gari nje ya nyumba yao, hapo wakatazamana kwa macho ya mshangao na wasi wasi, maan wao walishajuwa kuwa wakina Soraya wanakuja na wazazi wazi wa Higgno na Higgno mwenyewe.… ENDELEA………..
“Tunafanyaje?” aliuliza Mahamud kwa sauti ya kunong’ona, huku anamtazama mke wake, “tulia kwanza tusiwaonyeshe kama tuna watilia shaka, si unakumbuka hata nyuma tuliwashuku hivi hivi, lakini tukaja kukuta vingine” alisema mama Soraya kwa sauti ya chini, huku Talib akiwasikiliza kwa umakini japo hakuwa anawaelewa kwanini wanaongea vile, “tatizo shangazi we endelea kuwalea lea, yaani unaongea kwa sauti ya chini kwaajili ya Soraya” aliongea kwa sauti ya juu Talib, ambae hakujuwa kijacho, “hebu funga mdomo wako we mjinga…” alisema mama Soraya kwa sauti ya chini yenye kukalipia, na kabla hajamaliza wakashtuka kusikia nyanyo za watu zikikaribia mlango wa kuingilia sebuleni na wote wakatazama upande ule wa mlango, huku Talib mapigo ya moyo yakianza kumuenda kasi, maana alianza kuhisi kuwa vishindo vile sio vya watu wawili yaani Soraya na Laylah.
Ni kweli macho ya Talib yaliweza kuthibitisha hilo mara baada ya mlango kufunguliwa, aliefungua alikuwa ni Soraya akifuatiwa na Laylah, ambao walivua viatu vyao vya mikanda kwa kutumia miguu yao, nadhani unaweza kuvuta picha kamili, huku nyuma yao wakionekana wageni wengine watatu ambao walikuwa wanavua viatu vyao vya kutumbukiza, nao ni wanaume wawili na mwanamke mmoja, “msala” alinong’ona Talib, huku anainuka toka kwenye kiti pale kwenye meza kubwa ya chakula, akisahau hata kunawa na kuanza kutoka kuelekea upande wa mlango wa nyuma, “we! Talib unaenda wapi baada ya kusubiri kuwasalimia wageni” aliuliza mama Soraya, kwa sauti iliyojaa mshangao, lakini Talib aliekuwa kama amekimbizwa au teja aliemuona polisi hakugeuka wala kusimama, ndio kwanza akaongeza speed ya kuufuata mlango ule, ambao aligunduwa kuwa umeshafungwa mara baada ya kuufikia, ni kwamba mlango ulifungwa na kutolewa funguo toka lilipotokea lile utukio la jana usiku.
Hivyo Talib akageuka na kutazama alikotoka, akawaona wageni wale watatu ambao aliwafahamu mara moja kuwa ni Higgno na wazazi wake, hapo Talib akaona kuwa akizubaa anaumbuka kweupe kabisa, akatazama kushoto na kulia kama kuna mlango anaweza kuingilia ili asikutane na mzee Frank, ambae aliamini kuwa lazima atamkumbuka kuwa alienda kumsumbua pale dukani kabla ya kwenda kuchoma moto duka lake usiku, lakini hakuona mlango ambao anaweza kuingia kujificha, maana kila mlango alio uona ulikuwa ni wachumba cha mtu tena ambacho hatakiwi kuingia hata kwa bahati mbaya, na vilivyo bakia ni vya wageni, ambavyo lazima vilikuwa vime fungwa na funguo, hivyo akaona kama mbwai na iwe mbwai.
Talib aligeuka na kutazama sebuleni alikotoka, ambako aliwaona wageni wao wakiwa wanaingia sebuleni na kuanza kusalimia na shangazi yake na mjomba wake, ambao bado walionekana kuwa katika mshangao juu ya yeye Talib kwa kile alicho kionyesha, Talib akaona atumie nafasi hiyo kupita pale sebuleni na kutokea mlango mkubwa kuelekea nje, hivyo akapiga hatua za haraka kueleka sebuleni kwa lengo la kupita haraka sebuleni huku akisikia wageni wale wakisalimiana kwa sauti za furaha na kusimuliana mambo ya huko kijijini, “kwa kweli leo nimejiona kama mke wa mfalme jinsi watu walivyojaa barabarani kutushangaa” alisimulia mama Soraya, kwa sauti iliyochangamka kweli kweli.
Naam Talib alipokaribia pale sebuleni akakutana na wakina Soraya na Laylah, ambao walikuwa wanaelekea chumbani kwa Soraya, “we kaka Talib vipi mbona kama unahangaika?” aliuliza Soraya kwa sauti iliyoonyesha mshangao wa kudhihaki, ila ukweli hakuwa anashangaa, maana alikuwa anajuwa ni kwanini Talib alikuwa katika hali ile, swali hili japo alikujibiwa na Talib ambae aliendelea kutembea kuelekea sebuleni liliwashtua wakina mzee Mahamud na kuwafanya wote waliokuwepo pale sebuleni kutazama kule alikotokea Talib.
Naam hapo macho ya mzee Frank yalikutana na na macho ya Talib, na kumfanya Talib akwepeshe macho kwa mashaka makubwa aliyo kuwa nayo, huku mzee Frank akitoa macho ya mshangao na wakati huo Soraya na Laylah walikuwa wamesimama wanatazama mwisho wa Talib, “we! Talib hebu simama hapa, kwani una nini wewe unashindwa kuwasalimia wageni” alisema mama Soraya kwa sauti kali zaidi, yaani alimkalipia mtoto huyu wa kaka yake pasipo kujari wageni, lakini bado Talib hakutaka kusimama, “kwani huyu ni kijana wako pia?” aliuliza mzee Frank kwa mshangao, na hapo Talib akaona kuwa mzee Frank anataka kuharibu kabisa, hivyo akazidi kutembea kuondoka eneo lile, ambalo sasa alikuwa kati kati anakatiza, hisia zikiwa tofauti kwa Mahamud na mke wake, ambao walihisi kuwa Talib na mzee Frank ni kweli wanafahamiana na ni kweli mzee huyu ni tapeli kama anavyosema Talib, “kwani unamfahamu huyu?” aliuliza mzee Mahamud kwa mshangao wa tahadhari, “ndiyo ni yeye kabisa, ndie kijana aliekuja kunitishia na mwisho kuchoma duka langu” alisema mzee Frank na hapo ghafla mama Soraya akasimama, “weee! Talib hebu simama, na uje ukae hapa, ukitoka humu ndani na uondoke moja kwa moja nisikuone tena” ilikuwa ni sauti kali iliyojaa hasira kali sana, “tatizo shangazi unamsikiliza huyu tapeli” alisema Talib huku anapunguza mwendo na kusimama, watu wote wakaachama midomo kwa mshangao, hasa wakina Higgno na wazazi wake, “we Talib, huoni hata aibu, huyu baba amekutapeli nini, wewe si ulisema Higgno alikuvurugia mipango yako ndio maana umechoma duka lake moto” alisema Soraya, ambae aliunganisha simulizi na matukio ya kijana alie enda kumtishia mzee Frank dukani kwake, “we! Soraya lazima umtetee huyu mzee si wamesha kuroga” alisema Talib kwa sauti ya kali yenye upinzani, “hebu tulieni kwanza jamani mbona munatuchanganya, mara tapeli, mara kuchoma duka la watu, samahani mzee wangu hebu tuelezee ulikuwa unamfahamu vipi huyu Talib” alisema mzee Mahamud na hapo mzee Frank akaanza kueleza jinsi ilivyo kuwa siku ile ambayo duka lake lilichomwa moto, huku soraya akisogea sebuleni kusikiliza mkasa huo.*******
Naam Mzee Mahadhi akiwa hajuwi kilichotokea usiku, aliamka na kujiandaa kuelekea dukani kwake na alipotoka nje kutazama gari hakuliona, hivyo hakutaka kuhoji na kuondoka zake kuelekea kazini kwake, kitu ambacho hakukijuwa ni kwamba kijana wake Idd alikuwa anamsubiri atoke ili na yeye awasiliane na Talib ili wakawaone wale vijana wengine kama walifanikiwa kuondoka na fedha ili wakagawane na wao wakimbilie msumbiji.
Mahadhi alifika dukani kwake na kufungua kama ilivyo kawaida, huku akiwa na hamu kubwa ya kikao cha mchana wa saa saba, ambacho kingemsimanga Mahamud kwa kukubali kijana ambae sio muisilam kumchumbia binti yake, ukweli muda kila ulipozidi kwenda ndipo alipoanza kusikia habari za kuwa kuna tukio lilitokea jana usiku nyumbani kwa Mahamud, na kwamba jaribio limeshindwa la kumvamia na kumuibia, pia alizidi kupata habari ambayo ilianza kumchoma moyo wake kama ile ya kuwa mkwe wa mzee Mahamud ndie aliefanikisha kuwazuia wale majambazi, ambao mmoja kati yao alifanikiwa kumbia huku wengine sita wakitiwa mbaroni pamoja na vyombo vya usafiri walivyo vitumia ikiwa ni gari moja na pikipiki mbili.
Huwezi amini kama Mahadhi hakuhisi chochote kuhusu mwanae na gari lake kuhusika kwenye tukio lile, mpaka aliposhtuka kuona gari la polisi likija na kusimama dukani kwake, kisha polisi kumtangazia kuwa kuanzia muda huo yupo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, “kwalepi tena jamani, mbona fitina zishaanza jamaaa” alilalamika mzee Mahadhi, huku mawazo yake yakimpeleka kwenye kitendo cha kuandika ujumbe mfupi wa simu na kuutawanya kwa lengo la kumchafua Mahamud, “mzee unatuhumiwa kuhusika na tukio la uvamizi wa nyumba ya bwana Mahamud na kujaribu kuiba, baada ya gari lako kukutwa eneo la tukio na jitihada zinafanywa kumnasa Idd Mahadhi, ambae inasemekeana alikuwa ndie dereva wa gari hilo” alifanuliwa bwana Mahadhi kama ilivyo sheria na hapo ndipo akili ilipomkaa sawa, kwanza alikumbuka kuwa kijana wake ni muharifu kweli kweli, maana hata huko msumbiji alikuwa anaishi kwa kufanya uharifu, pia akakumbuka kuwa sio tu kuliona gari lake hata Idd hakuwa amemuona toka alipo achana nae jana asubuhi wakati anaenda dukani, na mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa ni jioni ya jana alipo mueleza kuhusu kuchumbiwa kwa Soraya.
Mahadhi alipewa nafasi ya kufunga duka lake na kupandishwa kwenye gari la polisi, safari ya ikaanza kueleka nyumbani kwake kumfuata Idd, huku njia nzima Mahadhi akiijutia nafsi yake kwa kumuendekeza Idd kijana wake, ambae nae alikuwa ndio kwanza bado amejikunyata kitandani huku anaugulia maumivu ya ng’olewa jino, kwa ngumi, nae bila kusita akamtaja Talib, kuwa ndie msusi wa mipango yote ya kumwibia mjomba wake, hivyo polisi mala baada ya kuwaacha wakina Mahadhi kituoni, wakaanza safari ya kueleka nyumbani kwa Mahamud, wakiwaacha Idd na baba yake wanachukuliwa maelezo, ambayo yalimsaidia Mahadhi kuachiwa muda mfupi baadae, baada ya kujieleza kuwa yeye akuwa anajuwa lolote kuhusu mpango huo, na kwamba gari alikuwa nalo kijana wake na akujuwa kama anaenda kulitumia kwenye uharifu.********
Naam baada ya mzee Frank kueleza jinsi alivyo kutana na Talib, huku mzee Mahamud akikumbuka kuwa siku hiyo tajwa, alimuona Talib akirudi nyumbani usiku kwa mwendo wa kuvizia, lakini Talib alipinga vibaya sana, “anko huyu mzee nimuongo sana tena tapeli, anajuwa kupanga uongo wake mpaka munaweza kumuamini” alisema Talib huku anaanza kuondoka, “usiondoke Talib, ukiondoka tu usije ukarudi kwenye nyumba hii” alifoka mama Soraya na wakati huo Soraya ametulia kimya kabisa anawasikiliza, “hebu niambie siku ile usiku ulikuwa unatokea wapi?” aliuliza Mahamud kwa sauti ya upole, mara nyingi hakupenda kumfokea Talib, “anko mimi nilikuwa na mishe zangu tu! wala sikwenda huko, nyie hamuwajuwi hawa ni waongo sana” alisema Talibu macho yakiwa makavu kabisa, usinge dhania kuwa alikuwa anahusika kwa asilimia mia moja na uharifu uliotokea kwenye duka hilo la mzee Frank, “hakika Talib unanishangaza sana, ni kitu gani kina kufanya uchome duka la watu” aliuliza Mahamud kwa mshangao na masikitiko makubwa, hapo Talib hakuweza kujibu lolote, akabakia ameinamisha kichwa chini, “ona sasa, leo hii unao wafanyia hivyo ndio wanakuja kuwa ndugu zako, umepata faida gani? au Higgno alikuvurugia mipango gani?” aliuliza tena Mahamud na hapo japo Talib alijuwa jibu sahihi la swala hilo, lakini alitoa jibu lake, “anko tatizo hamtaki kunisikiliza, hawa kuna watu watakuwa waligombana nao tu katika utapeli wao ndio wakawalipizia kisasi, na kwa kuwa mimi nilipita mchana wanaamua kuni singizia” alijitetea Talib bila hata chembe ya aibu, “hivyo ndiyo utakavyoenda kueleza polisi?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya ukali, na kuona hivyo mzee Frank akaona isiwe shida, “lakini mzee Mahamud, nadhani tufanye kama yamepita, maana tumesha kuwa familia moja, siwezi tena kwenda kutoa taarifa polisi kuwa nime muona kama nilivyo agizwa, ila naomba tu kijana ajirekebishe” alisema mzee Frank kwa sauti ya upole, unaona wenzako walivyo na moyo wa kusamehe, sasa wewe ni kitu gani ambacho Higgno alikukosea mpaka ukachome duka la baba yake?” aliuliza mama Soraya kwa sauti ya kusimanga iliyojaa masikitiko, “shangazi nilisha sema toka mwanzo huyu mzee ni bingwa wa kugeuza maneno, huyu ni tapeli, na alichotaka ni Higgno amuoe Soraya, anasema mimi nilisema amenivurugia mipango yangu anaweza kunivurugia mipango gani huyu masikin….” alisema Tarib kwa sauti iliyojaa ujeuri na ukizingatia alikuwa na hasira na Higgno, ambae ni mara ya pili alikuwa anamvurugia mipango yake, hapo kwa mara ya kwanza Soraya akafungua mdomo, “unajifanya hujui ni mipango gani alikuvurugia, sema unajifanya huijui niitaje” aliuliza Soraya huku anatoa simu kwenye mkoba wake, nilie ambayo iliokotwa kwenye tukio la uvamizi kule shambani, kisha akaipiga namba ya Talib mwarabu, ambayo ilikuwa juu kabisa, huku kila mmoja akidhania kuwa Soraya alikuwa anapiga simu kwa mtu ambae anaweza kutoa ushahidi, na hapo simu ya Talib ikaanza kuita kutokea mfukoni mwake, unajuwa nini kilifuata?
Ni katika hali ambayo Talib hakutegemea kabisa, kuwa simu ile aliyopiga Soraya ndio ilikuwa inaita mfuko mwake, na yeye akidhania kuwa ni Idd au mtu mwingine anampigia akatoa simu yake na kuitazama haraka haraka akaona jina Zido, akukumbuka kuwa simu ile ilisha potea kule shamba, unajuwa nini wewe sema kama unajuwa” alisema Talib, huku anaikata simu ile na kuiweka tena mfukoni, kwasababu asingeweza kuongea na Zido huku akiwaza kuwa wenzake wamesha achiwa au Zido hakukamatwa kama wenzake, “sema mbona kimya sasa” aliongea Talib huku watu wote wakimtazama, maana walishaona kuwa amepigiwa simu na Soraya na kuikata.
Na kama haitoshi Soraya akapiga tena, na ile simu ya Talib ikaanza kuita tena toka mfukoni mwake, Talib akaitoa tena na kuitazama akaona jina lile lile Zido, na hapo ndipo akili ilipomkaa na kukumbuka kuwa simu ile ilishapotea muda mrefu, tena ilipotea kwenye tukio la utekaji wa Soraya, akili ikamtuma kumtazama Soraya na alipomtazama akamuona ameishikilia simu mkononi, huku simu ile ikiendelea kuita, Talib akawatazama shangazi na mjomba wake, akawaona wanamtazama kwa macho ya sitofahamu, akawatazama wakina Higgno na wazazi wake pamoja na Laylah, nao walikuwa wanamtazama yeye ambae alikuwa ameishikilia simu ambayo ilikuwa inaendelea kulia, “ndio nini, sasa hiyo simu inanihusu nini?” alisema Talib kwa sauti ya kufoka, “unajifanya huijui? sema sasa unajifanya huijui? kwa taarifa yako hii ndio simu ambayo ulikuwa unatumia kupanga mipango ya kuniteka na kuniuwa, na ndio mpango ambao unasema Higgno alikuvurugia, kataa sasa kama nakusingizia” alisema Soraya kwa sauti ya juu na ya ukali pia, akiwaacha wazazi wake midomo wazi huku wakimtazama Talib kwa mshangao mkubwa, “we Soraya unaongea nini?” aliuliza mama Soraya kwa sauti iliyojaa mshangao na butwaa, “mama jana sikutaka kuongea mbele ya polisi, kwasababu ungesema namuonea” alisema Soraya huku ana weka sehemu ya messeji kwenye ile simu, “hii ndio simu ambayo wale watekaji walikuwa wanawasiliana na baba siku ile, tazameni hizi messeji halafu angalieni namba iliyo zituma hizo messeji” alisema Soraya huku anamkabidhi mama yake simu ile.
na hapo Talib akaanza kukumbuka jinsi alivyokuwa anatuma sms kwa zido kusisitiza kumuuwa Soraya mara tu watakapo kamilisha mpango wao, pia alipo wajulisha kuhusu mpango wa mjomba wake kuwajulisha polisi, Talib akawatazama shangazi yake na mjomba wake, ambao wote kwa pamoja waliinamia simu na kuanza kusoma sms zile zilizotumwa na mtu alieseviwa kwa jina la Talib mwarabu, “jamani jamani, hebu njooni muone huyu mtu, kweli unaweza kufanya hivi kwa ndugu yako” alilalamika mama Soraya, huku wakiwaita wakina mzee Frank nao wasogee, nao wakavutika pamoja Higgno na wakina Soraya, “huyu ni muuwaji mkubwa, na hiyo ya mwisho aliwaambia kuhusu funguo si munaona” alisema Soraya kwa sauti iliyojawa na msisitizo, “kaka atanisamehe kwahili, huyu namfunga akaozee jela maisha yake yote” alisema mama Soraya huku wanainuwa nyuso zao kumtazama Talib pale alipokuwa amesimama, hakika mtu sio panzia ya kwamba unalifunua unavyotaka..... ITAENDELEA
Talib!!!!
 
Wajumbe ni muda wa kulala hakikisha umetoa like ukimaliza kusoma sio unakurupuka tu.

jannelle karibu kijijini
mbuzi wa mshenga Muite mzee Njogopa alete dumu la ulanzi tumkaribishe mgeni

mankizzo finyango Mani Fabian msije lala njaa wakati kuna matembele hapo uani chumeni ila hakikisheni mmeyachambua vizuri mengine yana wadudu
Kwani uki like kisha ukasoma kuna shida?😃😃
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA TISINI NA MOJA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA TISINI “jamani jamani, hebu njooni muone huyu mtu, kweli unaweza kufanya hivi kwa ndugu yako” alilalamika mama Soraya, huku wakiwaita wakina mzee Frank nao wasogee, nao wakavutika pamoja Higgno na wakina Soraya, “huyu ni muuwaji mkubwa, na hiyo ya mwisho aliwaambia kuhusu funguo si munaona” alisema Soraya kwa sauti iliyojawa na msisitizo, “kaka atanisamehe kwahili, huyu namfunga akaozee jela maisha yake yote” alisema mama Soraya huku wanainuwa nyuso zao kumtazama Talib pale alipokuwa amesimama, hakika mtu sio panzia ya kwamba unalifunua unavyotaka………ENDELEA………
Maana wote walishangaa kuona pale alipokuwa amesimama Talib muda wote hakuwepo kabisa, ile wana tazama mlangoni ndio kwanza wakamuona Talib akimalizikia mlangoni, na kwa kasi ya ajabu akaokota viatu ambavyo sidhani kama vilikuwa vya kwake, alichojali yeye ni viatu vya kiume kisha akatokomea upande wa getini, mlinzi mgeni ambae aliwekwa pale baada ya Ndolite kuwa hospital akishindwa kumzuia kijana huyu wa mwenye nyumba akimuacha toke nje, sekunde chache wakifuatia wakina mzee Mahamud nao wakija mbio, mlinzi mzuie huyo asikimbie” alipiga kelele Mahamud, ambae alionyesha hasira za wazi kabisa juu ya Talib, “ameshaondoka mzee, alisema mlinzi huku anatoka nje na kumtazama Talib ambae alimuona akiwa anamalizikia upande wa kulia, ambako jana alikimbilia Idd, yaani kule ambako wakina Soraya jana usiku walikuwa wameegesha gari “yuleeee, alipiga kelele mlinzi, huku akimtazama Talib ambae alikuwa anapandisha upande wa kushoto kuelekea upande wa mtini pub na kutokomea zake, hata wakina Mahamud walipofika pale hawakuweza kumuona tena, zaid wali weza kuliona gari la polisi likiingia pale nyumbani kwao, likitokea upande wa soko kuu yaani upande wa kushoto wa jumba lile la kifahari la bwana Mahamud na kusimama nje ya geti, akashuka polisi kiongozi mwenye nyota moja, ambae ni Joanes Kiwili na kuwa salimia wote, kisha akeleza shida yake, samahani bwana Mahamud kuna kijana unaishi nae hapa nyumbani kwako anaitwa Talib?” aliuliza Kiwili swali ambalo lilimshangaza hata Higgno, kwasababu Talib na Kiwili walikuwa darasa moja kipindi wanahitimu elimu yao ya kidato cha nne, “ndiyo tena ametoka sasa hivi hapa munge tokea huku mungekutana nae hapo” alisema mama Soraya kwa sauti iliyojaa jazba na chuki juu ya huyu mtoto wa kaka yake, “ok! wacha tumfukuzie, kama tutamkamata tuta wajulisha, ila kwa kifupi ni kwamba yeye ni mmoja wa wanaohusika walioshiriki kupanga mipango ya kuvamia hapa nyumbani kwako jana usiku, akishirikiana na wenzie saba, mmoja ni kijana Idd Mahadhi ambae tume mkamata muda mfupi uliopita, alifafanua Kiwili wakati anataka kuingia kwenye gari ili waelekee upande ule alioelekea Talib, “bwana Polisi, naomba ufanye juu chini umkamate huyo mshenzi na mumpige haswa, maana yeye ndie aliepanga mpango wa kumteka mwanangu Soraya week iliyopita, tena alikuwa anasisitiza wamuuwe kabisa, na mukimkamata munijulishe nije nimuone kwanza sura yake, maana nahisi sikuwahi kumtazama usoni huyu muuwaji” alisema mama Soraya, kwa sauti ambayo wakina Higgno na wazazi wake na wakina Soraya, waliitafsiri kama hasira ya hali ya juu, “usiwe na wasi wasi mama yangu lazima tutamnasa” alisema Kiwili, huku anaingia kwenye gari na dereva akaondoa kuelekea upande ule, “jamani sijawahi kuona mtu kama huyu, kweli bangi ni mbaya, yaani anapanga kabisa kumuuwa dada yake, tume mvumilia kwa mengi, tume msaidia mengi leo anataka kunilipa machungu yasio na kifani, hapana lazima aende jela, hata kama atashinda kesi nitatumia gharama yoyote ile aende jela” alisemam mama Soraya wakati wanarudi ndani****
Hilda alikaa kwa muda wa dakika kumi nzima pale chini, huku anasikia watu wakijadili kuhusu tukio la mzee Frank na mke wake kufundishwa gari na wale waschana, huku habari za chini chini zikianza kuenea kuwa mmoja wa wale waschana ni mchumba wa Higgno, tena alitajwa yule mwarabu, pia moja kati ya yale magari ni la bwana Frank, wapo waliong’amua kuwa gari lile jingine alilopanda Higgno na yule mscha wa kiarabu ni la binti wa Mahamud, ambae ilidaiwa ndie mchumba wa Higgno, habari hizi ziliuchanganya moyo wa Hilda na kuivuruga akili yake, ukweli aliumia sana ungesema Higgno aliwahi kuwa mpenzi wake, na kwamba Soraya ndie aliemnyang’anya “ndio maana aliamua kumuacha Tembele kwasababu alikuwa amepata mtoto wa kiarabu” hayo yalikuwa ni maneno ya baadhi ya watu ambao hawakuwa wanajuwa ukweli wa mambo kuhusu Higgno na Hilda, “wewe hujui kitu, Tembele hakuwahi kuwa demu wa Higgno, kuna yule jamaa anaekaa kwa Mahamud aliingilia kati na kumpa mimba” alisema mwingine na hapo mwingine akauliza kwa mshangao, “ni yule jamaa mvuta bangi” swali ambalo lilizidi kumuumiza Hilda ambae mpaka muda huo alianza kuona kijiji kichungu, “ndiyo bwana nime kumbuka, tena mzee Komba na mke wake walimchezea mchezo wa ndoa ya mkeka Higgno na wakafanikiwa, sema aliekuja Kuharibu ni tembele mwenyewe, alikuja na yule mvuta bangi wake nyumbani kwa mzee Frank tena usiku, hapo mzee Frank akamtimua Tembele” alisema mmoja huku na mwingine akadakia, “halafu mama yake jana amefumaniwa, dah! yaani ametembezwa uchi uchi, yaani kumbe Tembele amerithi kwa mama yake wote Malaya” kauli hii ndio kama ilimgutusha Hilda na kuigundua tabia yake kuwa ni adui ya jamii, “lakini si huwa munaponea kwa Tembele? halafu nasikia anatoa mpaka mgongo” alisema mmoja na wote wakacheka, na hapo Hilda akainua uso wake kuwatazama wale vijana, ambao ni kama hawa kuwa wamemuona, akawaona watatu kati yao walishawahi kumuingizia dudu, nao walishamfanyia kitendo hicho kinyume na maumbile ya kawaida ya kupeana dudu, “kweli bwana yaani kama mbele tu” alisema mmoja na wote wakacheka tena.
Kwa kifupi maongezi yale yalimuumiza sana Hilda ambae aliamua kugeuka na kurudi nyumbani kwao, huku njia nzima akiwaza ataiweka wapi sura yake na ataanzaje kuingia pale na kukaa na shangazi yake, ambae lazima angemsimanga kutwa nzima kwa kitendo cha kumtelekeza baba yake, “sijui mama atakuwa bado yupo kwenye ofisi ya mwenyekiti?” alijiuliza Hilda ambae baada ya kuwaza sana akapata wazo la kwenda kukaa kwa babu mabudi kwa siku kadhaa ili kijijini papoe kidogo.
Hilda alipofika nyumbani hakuweza kumkuta shangazi yake wala mwanae, akajuwa tayari shangazi yake ameenda Zahanati kumtazama mgonjwa, hivyo akafungua mlango ambao alikuwa anaufahamu vizuri na kuchukua alichokiona kinamfaa kama vile nguo za kubadilisha zikiwepo kanga na gauni mbili, pia na shuka yake chakavu, kisha akaondoka zake kuelekea upande wa kusini wa kijiji kwa lengo la kuikamata njia ya kuelekea linjumbwi pasipo kujuwa mama yake yupo wapi.*******
Baada ya kutoka kituo cha polisi Mahadhi alienda moja kwa moja kwa mwenyekiti wa baraza la wazee na kuweleza kuhusu tukio la uvamizi jana usiku nyumbani kwa Mahamud, akaeleza kila kitu kilivyo mtokea na gari likikutwa eneo la tukio ambalo kijana wake idd amehusika moja kwa moja na sasa anashikiriwa na jeshi la polisi pamoja na wenzake, huku yeye akihojiwa na kuachiwa kwa makubarliano ya kwamba ataitwa pale atakapohitajika, “naomba unisaidie kwenda kwa Mahamud ukaongee nae yaishe, ukiachilia kuwa yeye ndie mtendewa lakini pia ni mtu mkubwa sana, ambae anaweza kuwashawishi na haya mambo yakaisha, ukichukulia mmoja kati ya watu waliopanga mpango huo ni mpwa wake Talib” alisema Mahadhi akiwa anamaliza simulizi yake, “lakini bwana Mahadhi, ifikie wakati waache walipie kwa maovu yao, kwanini waliamua kupanga tukio baya kama hili na hauoni kama itadhihirika kuwa wewe na mwanao mulipanga mambo mengi sana mabaya kuhusu familia ya Mahamud, muache ajifunze kutokana na makosa yake”alisema Mwenyekiti, akionyesha wazi kuwa hakupendezwa na kile kilichofanywa na Idd na wenzake, “lakini mzee wangu, swala hili litanichafua mimi pia litatuchafuwa sote tuliowahi kukaa na kuongea na Mahamud” alisema Mahadhi, akijaribu kumshawishi mwenyekiti, ambae alionekana kuelewa alichoambiwa, “ok! baadae saa saba tuna kikao na Mahamud, tutaongea nae ajaribu kuongea na polisi, wafunike swala hili tuje kuliongea nyumbani” alisema Mwenyekiti na wakakubaliana wakutane saa saba kule msikitini.*********
Naam kitu ambacho Hilda alikuwa hakijui ni kwamba jana usiku mama yake alitoka ofisini kwa mwenyekiti wa kijiji na kwenda nyumbani kwao ambako aliambulia kipigo na kuamua kukimbia pale nyumbani akienda kulala kwenye majengo ya shule ya msingi Luhila juu, na kuondoka pale mapema sana akielekea Linjumbwi, ambako aliamini kuwa ndio sehemu salama kwake kwa kipindi hiki kigumu kinacho mkabili, na huko Linjumbwi sio sehemu nyingine zaidi ya kwa babu Mabudi, akiwa tayari kukabiliana na chochote kitakacho mkuta kule Linjumbwi, maana alijuwa fika kuwa kwa siku atakazo kaa kule kwa Mabudi kitacho mtokea ni zaidi ya hatari kama ile siku moja tu alishindwa kutembea sasa kama akikaa siku zaidi ya moja itakuwaje, “sina la kufanya nitavumilia tu!” alisema mama Hilda ambae alitumia masaa matatu kufika nyumbani kwa Mabudi, ambako alipokelewa kwa furaha na matabasamu ya uchu na kwakuonyesha kwamba mabudu alikuwa anaisubiri bahati hii kwa hamu, ukweli hakumpa nafasi ya kupumzika mama huyu, mara moja akamchemshia viazi kisha akaingia porini kuandaa dawa yake ile ile tamu tamu, ambayo mama Hilda hupenda kuiita Juice.******
Upande wa pili nyumbani kwa Mahamud, licha ya wanafamilia walio ungana kujadili kwa kina juu ya tukio la kina Talib, pia walipanga kuhusu swala la ujenzi wa nyumba na maduka makubwa ya bwana Frank uanze mara moja, pia walijadili swala la dini kwa Soraya na Higgno, huku Soraya akiwa wa kwanza kusema kuwa yupo tayari kwa maamuzi ya Higgno, na Higgno akaomba kwa wazazi wake na kwa wazazi wa Soraya kuwa apewe muda na mwalimu ili aweze kumfundisha kuhusu dini ya kiislam, na hapo ndipo Mahamud akapiga simu kwa mwenyekiti na kumueleza kuwa asingeweza kwenda kwenye kikao walicho panga kutokana na mambo yaliyomtokea jana usiku, huku akiwaeleza kuwa kuhusu dini kijana Higgno alishaamua kubadili dini na kuwa muislam.*****
Talib baada ya kukimbia nyumbani kwa mjomba wake hakufika mbali kabla hajakamatwa na polisi na kupelekwa kituoni akifungiwa na wenzake wakina Idd, akikabiliwa na kesi ya kupanga njama za kuvamia kwa mjomba wake, pia kwa kosa la kupanga na kumteka Soraya.*****
Hilda alifika nyumbani kwa Mabudi akipokelewa na miguno ya mahaba na alipochungulia ndani ya kibanda akakutana na mziki mzito ambao mama yake alikuwa anapewa na kibabu kile chenye meno kama muhindi uliokosa mbolea, lakini hakuwa na ujanja na yeye alisubiri mpaka walipo maliza na kuingia ndani, ambapo alipokelewa kama alivyo pokelewa mama yake na kukubali maisha ya kuwa mke mwenzake na mama yake, huku wakigundua mbinu mpya ya kuweza kumkabili mzee Mabudi ambayo ni kufanya mapenzi kwa pamoja, iliwalazimu kwasababu hawakuwa na sehemu ya kwenda, miezi miwili mbele walijigunduwa kuwa walikuwa wana ujauzito.******
Miezi mitatu mbele Talibu na wenzake walihukumiwa kwenda jela miaka sita kila mmoja, huku mzee Komba akitoka zahanati akiwa amepooza mkono mmoja na mguu mmoja, matibabu yake yalisimamiwa na kugharamiwa na mzee Frank, ambae kwa sasa alikuwa ni mmoja wa watu wenye fedha upande wa songea mashariki, aliendelea kuwa mkarimu na msikivu kwa kila mtu, alimsaidia mwenyeshida na alijitolea kwa wenye uhitaji, pia alikuwa anamsaidia kwa hali na mali mzee Komba ambae alimtafutia mschana wa kazi na kuhakikisha kuwa anampatia kila kitu kama mahitaji yake ya kila siku pamoja na kumlipa mschana wa kazi, pia alimchukuwa mjukuu wa mzee Komba na kukaa nae nyumbani kwake, japo taarifa hizi zilikuwa ni maumivu makubwa sana kwa mama Hilda na binti yake Hilda, ambae aliwafanya vijana wa walaumu sana kuondoka kwake pale kijijini, maana ni kama mwenye nyumba alilishia ng’ombe Tembele lote la uwani, ambalo lilikuwa lina wasaidia sana vijana.
Mwezi mmoja mbele yaani mwezi wanne toka mwezi wa tukio, Higgno na Soraya walifunga ndoa kwenye msikiti wa mkoa na sasa wanaendelea kusimamia kampuni mpya ya mabasi yaendayo mikoani, ambayo Mahamud alimfungulia mwanae Soraya, aliwajengea jumba moja kubwa sana kule Mahilo kwenye eneo la kina Higgno, na sasa Soraya alikuwa mjamzito na wao ndio walikuwa wanasaidia malezi ya mtoto wa Hilda aliezaa na Talib, ambae alikuwa amechukuliwa na mzee Frank kwaajili ya kulelewa.
Hakika maisha yalikuwa mazuri kwa Higgno na Soraya ambao walipendana sana na waliishi kwa raha mustarehe, hapo ndio mwisho wa hadithi hii ya TEMBELE LA UWANI pengine kuna mambo nimeyapunguza kutokana na kazi nyingi ambazo zinasubiri na kuondoa ladha ya muwa ambayo hupatikana kwenye fundo, asanteni sana kwa kuwa pamoja na mimi kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa simulizi hii, najua mapungufu hayakosekani kwa maoni ushauri na mapendekezo basi unaweza kunifahamisha hapa au kwa
WhatsApp number 0743 632 247
Na yeyote anaetaka kutoa sapoti yake kwa mwandishi kwa chochote alichojaaliwa basi number ni 0743 632 247 mchango wako utampa motisha ya kuandika simulizi mzuri zaid na kugharamia vifaa, Ahsante sana wote ambao tulikuwa pamoja mwanzo hadi mwisho, kuisha kwa simulizi hii ndio kuanza kwa simulizi nyingie hapa hapa Jamii Forums, Kigongo kinakwenda kwa jina la KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
MUWE NA USIKU MWEMA
 
Back
Top Bottom