TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THEMANINI NA SABA
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SITA : “lakini mkae mukijuwa kuwa kama wanataka kufanya lolote hawatokuja mapema kama munavyofikiria, kama vipi ngoja mimi niende nikajaribu kuwatazama, kama watakuwa wamesha ondoka basi na sisi tuondoke, ila kama wapo basi lazima tusubiri hapa hapa, hata kama mpaka asubuhi itabidi mulale ndani ya gari” alisema Higgno huku anafungua mlango na kushuka toka kwenye gari, lakini kabla hata hajafunga mlango, Laylah akasema, “kweli jamani waleeee wanakuja” hapo Higgno na Soraya wakatazama mbele na wote kwa pamoja wakaweza kuwaona vijana wanne waliovalia makoti meusi wakisogea kwa tahadhari kubwa kwenye geti la nyumba ya kina Soraya …………ENDELEA……….
Na walipo lifikia mmoja wao akasogea kwenye mlango mdogo ulioshikizwa kwenye geti lile, huku wengine wakijibanza kwenye ukuta wa uzio wa nyuma ile wakimuacha mwenzao anagonga hodi mara mbili kwenye geti lile, huku wakina Higgno kwa umakini mkubwa wakitazama tukio lile, ambalo lilikuwa linafanywa na watu ambao walikuwa wanauhakika ni wale marafiki wa Talib, ambao walikuwa nae muda fupi uliopita, “ina maana wana mpango mmoja na mlinzi wenu?” aliuliza Higgno huku wakiendelea kutazama kule langoni, “inawezekana maana huyu babu anamuogopa Talib utadhani yeye ndie mwenye nyumba” alisema Soraya, wakiwa wanatazama kule getini ambako mmoja kati ya wale jamaa wanne akigonga tena geti, mara mbili zaidi.
Naam wakina Higgno wakiwa wametulia pale waliposimamisha gari waliweza kuona geti dogo lina funguliwa kisha akatoka mzee Ndolitebhuku vijana wengine wakiwa bado wamejibanza kiwambazani, na ile babu Ndolite anachomoza tu wale jamaa wakamtaka na kumpiga kwa nguvu kisogoni, hapo hapo wakina Higgno wakamuona mzee yule akilegea na wao kumuacha akijibwaga chini kama mzigo, kitendo kilicho washtua wakina Laylah na Soraya, “Higgno mpigie simu yule rafiki yako polisi haraka wamesha muuwa babu” alisema Soraya kwa sauti iliyojaa wasi wasi, “wala usiwe na wasi wasi, atakuwa amezimia tu!” alisema Higgno, huku anatoa simu na kupiga ile namba aliyopewa na Kiwili, akaiweka sikioni na macho ameyaelekeza kule kwa kina Soraya kama walivyofanya Soraya na Laylah, ambao sasa waliweza kuliona gari la Idd likitokea upande wa Sokoni na kuja pale kwa akina Soraya, likasimama karibu na wale vijana nne, ambao walimuinua babu Ndolite na kumueka kwenye buti la gari lililokuja na wakina Vitus, Idd na Zido, “hallow Brother Kiwili, tayari wale jamaa wamesha kuja, na wanamchukuwa mlinzi” alisema Higgno ikionyesha kuwa tayari simu ilikuwa imepokelewa, huku akiendela kutazama lile gari ambalo lilizungukwa na wakina Vitus, ambao waliweza kumuingiza kwenye buti la gari hilo, “ok! hakikisha hawafiki mbali hao, sisi tunakuja” ndivyo Kiwili alivyo shauri na hapo Higgno akakata simu huku wakiwatazama wakina Vitus, ambao waligawana kama walivyo kuwa mwanzo, wale vijana wanne waliingia ndani ya lile geti la nyumba ya kina Soraya, huku wakina Vutis wakiingia kwenye gari na kuondoka zao kueleka upande wa sokoni, “Soraya mpigie simu baba na mimi nakuja sasa hivi” alisema Higgno, huku ana weka simu mfukoni na kuanza kukimbilia upande ule wa Sokoni, “Higgno kuwa makini wasije kukuumiza” alisema Soraya huku anachukuwa simu yake toka kwenye mkoba wake.******
Mzee Mahamud na mke wake, ndio kwanza walikuwa wanaanza kusinzia, ikiwa ni dakika chache mara baada ya kumaliza kupeana dudu, “yaani mume wangu kila siku unazidi kuwa kama kijana” alisema mama Soraya aliekuwa amelala pembeni ya mume wake, huku akihisi macho yake yanakuwa mazito kwa usingizi, Mahamud akacheka kivivu wakati huo huo simu yake ikaanza kuita, akaichukuwa kwenye meza ndogo ya pembeni ya kitanda na kutazama jina la mpigaji, akidhania kuwa atakuwa ni mwenyekiti ambae ametoka kuongea nae muda mfupi uliopita, lakini akashangaa kuona kuwa ni binti yake, “Soraya sijui ana nini usiku huu” alisema Mahamud, huku anatazama muda na kuona ni saa sita za usiku.
Mahamud alipokea simu na kuiweka sikioni, “Hallow Sor…” kabla Mahamud hajamaliza kuongea, tayari Soraya alishadakia kwa sauti ya chini tena kama ya kunong’ona, “baba kuna wezi wanaingia ndani”ndivyo alivyo sema Soraya, na kumfanya mzee Mahamud ashtuke na kuinuka toka kitandani, “we upo wapi na umejuwaje?” aliuliza mee Mahamud kwa sauti ya chini na ya mstuko, huku anapapasa kwenye kabati la nguo zake na kuchukuwa bukta huku mke wake, yaani mama Soraya akichungulia dirisha akiwa mwenye wasi wasi na uoga mwingi sana, akiweza kuona watu wanapita kwa tahadhari kubwa wakielekea upande wa nyuma ya nyumba yao, “nipo hapa kwenye kona na wakina Higgno na Laylah tunawaona wamengia ndani wapo wanne, Higgno anawakimbilia wengine wamemchukuwa babu mlinzi” alisema Soraya, na wakati huo mama Soraya alikuwa anashuka toka kwenye kitanda na kumfata mume wake, akimpa ishara ya kuto kupiga kelele, hapo Mahamud akamtazama mke wake ambae akamuonyesha ishara ya kuwa kuna watu wanapita nje, hapo Mahamud akiwa na bukta mkononi alikimbilia dirishani na kuchungulia kwa tahadhari, hapo akamuona mtu wa mwisho akimalizikia kuelekea upande wa nyuma ya nyumba, lakini hakuwa na silaha yoyote, “nimewaona ngoja niwawahi kabla hawaja ingia ndani” alisema Mahamud akiongea na simu, kisha akaikata na kuirushia kitandani, halafu akavaa bukta yake haraka huku mke wake akivaa gauni la kulalia, wasi wasi umemjaa kweli kweli.
Mahamud baada ya kuvaa bukta yake akalifuata kabati lake ambalo lilikuwa na silaha mbili moja ikiwa ni bastora na nyingine ni Shot gun, Mahamud akachangua Shot Gun, ni ile ambayo aliwahi kuibeba siku aliposikia vijana wa Songea boyz wanafanya fujo chuo cha ualimu, ambako Soraya alienda kwenye kikundi cha dini, kisha akamtazama mke wake na kumpa ishara ya kuwa mtulivu mule chumbani, kisha yeye akaufuata mlango kwa tahadhari kubwa, lakini kabla haja ufungua akasikia kocho kocho za mlango wa nyuma ukifunguliwa, hapo Mahamud akakumbuka kuwa funguo ya mlango huo ilitolewa taarifa ya kupotea jana yake, akafungua taratibu mlango wa chumba chake na kuacha wazi kidogo, yaani usawa wa kuweza kuchungulia na kwa bahati iliyopo ni kwamba mara zote huwa taa ya kwenye kirido haizimwi, hivyo ingekuwa rahisi kwake kuona wanaopita koridoni.*******
Idd akiwa na wakina Vitus na Zido aliondoa gari pale kwenye geti la nyumba ya bwana Mahamud na kuelekea upande wa Sokoni, ikiwa ni mita kama mia mbili tu mpaka sokoni, ambapo walisimamisha gari na kumshusha yule mzee ambae bado alikuwa amepoteza fahamu, wakamfunga kamba za mikono na miguu pia waka mziba mdomo kwa vitambaa vichafu vya kufutia gari, mwisho wakamlaza barabarani kwa lengo kuwa magari yanayotoka mikoani, yamkanyage, ambayo mengi yao kwa usiku ule ni magari makubwa ya mizigo, kisha wao wakaanza kurudi tena kule walikotoka, yaani kwa mzee Mahamud wakiamini kuwa muda mfupi ujao wenzao watatoka wakiwa wamebeba fadha za kutosha wawakabidhi na kuondoka zao.
Naam kitu ambacho Idd Vitus na Zido hawakukijuwa ni kwamba ile wanaondoka tu, Higgno akatokea kwenye moja ya chochoro za majengo yaliyopo hapa mjini na kusogea moja kwa moja mpaka pale alipokuwepo mzee Ndolite, ambae bado alikuwa hajarejewa na fahamu, kitu cha kwanza Higgno alimtoa Ndolite barabarani na kumsogeza pembeni, kisha akaanza kumfungua kamba huku anapiga tena simu kwa Kiwili, na kumueleza tukio lile, “sikia Higgno, achana na huyo mzee sisi tunakuja, kama umemuweka pembeni ya barabara wewe hakikisha hawatoki hao watu, hakikisha unaisoma namba ya gari” alisema Kimwili huku akianza kumpa maelekezo, Higgno kitu cha kufanya.******
vijana wanne wakiwa na uhakika wakuwa hakuna mtu anewafwatilia, walifanikiwa kuingia kwenye geti la Mahamud nakuufikia mlango wa kuingilia ndani mwake, kisha wakafungua taratibu na kwa tahadhari kubwa ya kuepuka kuwashtua waliolala, na walipofanikiwa wakagawana makundi mawili, wawili wakaingia ndani wawili wakabakia nje wakitazama usalama.
Naam huku wakifuata maelekezo wale wawili walioingia ndani walitembea kwa tahadhari kubwa sana kuelekea kwenye chumba ambacho walielekezwa kuwa ndiyo ofisi ya bwana Mahamud, na walifanikiwa kukipata chumba hicho ambacho kwa namna ya pekee kabisa na yakushangaza, Mahamud huwa hakifungi kwa funguo, nao wakaingia ndani na kutazama kwenye ukuta wa upande wa kushoto wa kile chumba, akaona kuna picha fulani ukutani, akaitoa na kuona mlango mdogo wa kabati, wenye kitasa cha duara chenye namba namba fulani, “mbili kushoto moja kulia sita kulia nne kushoto” alinong’ona mmoja, akimueleza mwezie ambae alifanya kama alivyo ambiwa, na kweli ule mlango ukafunguka hapo wakakutana uso kwa uso na maburungutu ya fedha, “lete mfuko haraka, alisema yule mfunguaji kufuri na mwenzie akatoa mfuko mkubwa wa rambo na wakaanza kuweka zile fedha, “oya tujisevia nyingine..” alisema yule mmoja na kabla hajamaliza akasikia “tulieni hapo hapo” wote wakageuka kwa ghafla, na kwa mshtuko mkubwa, hapo wakamuona mwarabu akiwa amemesimama mlangoni huku amewaelekezea mtutu wa bunduki yake aina ya shot gun.
Kumbe basi, mzee Mahamud, aliwaona wale jamaa wawili walivyokuwa wanapita pale koridoni, na walipopita wawili akaona kimya, akajuwa wameshaisha, hivyo akatoka na kuanza kuwa fuata kwa nyuma kwa mwendo wa tahadhari kubwa, akitaka kujuwa kwanza wanaenda wapi na kufanya nini.
Nae akawaona wanaongoza ofisini kwake na walipofika kule ofisini kwake akawaona wanafunua picha ukutani pale kwenye kabati lake la siri, bila kuhangaika hata kidogo, ikionyesha wazi kuwa wanajuwa kila kitu kuhusu sehemu ile, na alithibitisha kuwa wale jamaa walikuwa wanaifahamu vyema ofisi yake na walishapewa habari na taarifa zote kuhusu ile sehemu yake ya siri ya kuifadhia fedha, na hata walipoitoa ile picha wali elekezana namna ya kuifungua ile sehemu, ambayo hata binti yake Soraya hakuwa anaifahamu, “mbili kushoto moja kulia sita kulia nne kushoto” hakika ilimshangaza mzee Mahamud, ambae uzalendo ulimshinda baada ya kuwaona wanaanza kukusanya fedha na kuziweka kwenye mfuko wao, ndipo alipojitokeza na kuwaweka chini ya ulinzi.********
Naam Idd Zido na Vitus, baada ya kumuacha babu Ndolite kule barabarani, wakarudi pale nje na kusimamisha gari karibu kabisa na geti la bwana Mahamud, na kuanza kusikilizia kama wenzao watafanikiwa ili waondoke na mkwanja, “tukitoka hapa kituo cha kwanza ni mwembe chai” alisema Zido, huku wote wakiwa ndani ya gari macho kwenye geti la mzee Mahamud.
Na wakati wakiwa wanaendelea kusikiliza na kupanga jinsi watavyo ondoka pale, mara wakashtuka kuona kuna mtu amesimama kwenye mlango wa upande wa dereva, wote wakainua nyuso zao kumtazama, “Higgno,” alisema Vitus, kwa mshtuko, kama ambavyo alishtuka Zido maana na yeye alikuwa anaufahamu mziki wa Higgno kama ulivyo watokea kule shambani, “ndiyo fala gani huyo, Higg..?” aliuliza Idd, kwa sauti ya kilevi, huku Zido akimdaka juu kwa juu, “washagari tuondoke..” alipiga kelele Zido, lakini walishachelewa maana tayari Higgno alishafungua mlango na kuchomoa funguo kwa haraka, “pumbavu hebu lete funguo mshenzi wewe” alisema Idd, huku anatoka kwenye gari na kumfuata Higgno kwa mwendo wake wakilevi, hapo alipokelewa na ngumi moja nzito ya usoni, ambayo ilimrudisha kwenye gari na kwenda kujibamiza kwenye mlango wa gari lake, ambapo haukuweza kuvumilia ukaachia kioo cha kwenye mlango huo, “bwaaah!” kioo kikamwagika chini, huku wenzake wakishuhudia, “we mshenzi una vunja…” aliongea Idd na kushindwa kuendela baada ya kuhisi kuna kitu kigumu mdomoni mwake, akapeleka mkono ili kutema hicho kitu kigumu, hakuamini macho yake pale alipoona kipande kikubwa cha jino na damu nyingi zikijaa mkononi mwake, na wakati huo huo Vitus alifungua mlango wa gari ili akimbie kama ambavyo alifanya Zido, maana waliona kuwa hawakuwa na jinsi, lakini bahati haikuwa ya kwao, maana ile Vitus anafungua mlango tu! akashtuka kuona mlango ukikanyagwa kwa nguvu na kumbamiza kichwani kwa nguvu kiasi cha kujihisi mwili unakosa nguvu na kuanza kuona kizungu zungu, wakati huo akamuona mwenzie Zido akifanikiwa kutoka ndani ya gari na kuanza kutimua mbio kukimbilia upande wa soko kuu, lakini ile Higgno anataka kuanza kumkimbiza akaliona gari la polisi likitokea upande huo na kisimama ghafla, ni baada ya kumuona Zido kisha polisi wakaruka toka kwenye gari na kuanza kumfukuza zido ambae bada ya kuona polisi, alichepuka na kuingia kwenye chochoro za mitaa ya eneo hilo ambalo naweza kuliita ni kati kati ya mji.
Higgno alizubaa kuwatazama polisi wakizama kwenye chochoro aliyokimbilia Zido na hapo ndipo Higgno alipo kosea, maana ile anashtuka kumtazama Idd akamuona ndio anakimbia kueleka upande ule ambao gari la Soraya lipo, mita kama mia hivi, ile anataka kumkimbiza, akakumbuka kuwa kuna vijana wanne wameshaingia ndani, hivyo akajuwa kuwa mzee huyu hatokuwa na uwezo wa kuthibiti wale vijana wanne, kwahiyo ni lazima akamsaidie, hapo Higgno akaghairi kueleka kule na akaingia ndani, huku akimuacha Vitus amezimia kwenye mlango wa gari.******
Naam vijana wale wawili walionekana kushtuka vibaya sana, hawakuamini kama wamefumaniwa na mzee mwenyewe Mahamud, hapo wakajuwa kuwa kama wakizubaa wanaozea jela, hivyo ni vyema kama watafanya juhudi za kujinasua, kilichofanyika ni kama kujifanya wamesha kubali kukamatwa ili kumzuga Mahamud, wakatulia na kumsoma mzee Mhamud alegee, “muna fuata nini humu ndani, nani aliewatuma” aliuliza Mahamud kwa sauti ya mkwara na vitisho, lakini kabla wale jamaa hawajajibu mmoja wao akachomoka mbio kumfuata Mahamud, ambae bila kusita alikamua trigger na na kuruhusu risasi kutoka ambayo ilienda moja kwa moja kwenye mguu wa yule jamaa na kupasua eneo lote la goti la kijana yule, huku mlio mkubwa wa mlipuko wa risasi ukisikika na kutawanyika eneo kubwa, hapo Mahamud akaiweka sawa bunduki yake ili aikoki, lakini alikuwa ameshachelewa, maana kuona vile yule mwingine pia akaamua kujitetea kivyake kwa kukimbilia pale pale mlangoni, lakini Mahamud alikuwa mwepesi zaidi yake, maana aliishika ile bunduki kama gongo na kumpiga nayo yule jamaa kichwani, hakika ilituwa sawa sawa eneo la sikio na kumtupa ukutani, ambako alijibamiza na kuanguka chini kama furushi akiwa ameshapoteza fahamu, na ile Mahamud anajiweka sawa anashtuka akisukumwa toka nyuma na kuangukia ndani ya ofisi yake, bila kutarajia bunduki yake ilishamtoka mkononi, kugeuka nyuma tayari aliweza kuwaona vijana wengine wawili wakiingia mule ofisini kwake na mmoja akamsogelea na kumtwisha ngumi ya usoni, hapo Mahamud akajuwa akizubaa amekwisha, akaitazama bunduki yake iliyo chini, mita chache toka alipokuwepo, lakini ile anataka kuifuata akashtuka teke likituwa mbavuni mwake na kumtupa mbali na bunduki yake, na yule aliempiga akaifuata ile bunduki ambayo yeye alikuwa anaitegemea kwa wakati ule, wakati huo yule aliemtwanga risasi ya mguu bado alikuwa anagalagala chini, huku anatoa kilio kikubwa, na huyu mwingine kati ya wawili walioingia akaufuata ule mfuko wa fedha na kuendelea kuweka zilizobakia kwenye kabati, ambazo zilikuwa ni nyingi zaidi kuliko zilizopo kwenye mfuko.
Naam Mahamud jakuwa na ujanja akabakia ametulia akimtazama yule anaeifuata bunduki, ambae alipoifikia akainama kwaajili ya kuiokota………….. ITAENDELEA
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA THEMANINI NA NANE
MTUNZI
Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA SABA : na yule aliempiga akaifuata ile bunduki ambayo yeye alikuwa anaitegemea kwa wakati ule, wakati huo yule aliemtwanga risasi ya mguu bado alikuwa anagalagala chini, huku anatoa kilio kikubwa, na huyu mwingine kati ya wawili walioingia akaufuata ule mfuko wa fedha na kuendelea kuweka zilizobakia kwenye kabati, ambazo zilikuwa ni nyingi zaidi kuliko zilizopo kwenye mfuko.
Naam Mahamud jakuwa na ujanja akabakia ametulia akimtazama yule anaeifuata bunduki, ambae alipoifikia akainama kwaajili ya kuiokota………….. ENDELEA……….
Mahamud akiwa Hajuwi afanye nini, alimtazama yule jamaa ambae alikuwa anainama kuichukuwa bunduki huku kelele za vilio vya hofu zikisikika nje na ndani nyumba yake zikiwa ni za wakina mama, akiwepo mke wake na wafanyakazi wao wa ndani, ambao waligutushwa na mlio wa bunduki, ndipo Mahamud alipomkumbuka Talib, ambae aliamini kuwa alishaamka, akitamani aje kuwa mkombozi wake, kwssababu alijuwa kuwa Higgno yupo nje ana wafuatilia waliomchukuwa mlinzi wao kama alivyo ambiwa na Soraya.
Naam kabla yule kijana haja ikamata ile bunduki toka pale chini mara ghafla kama kimbunga Mahamud alimuona mtu mwingine akiingia na kumzibua yule kijana muokota bunduki teke la usoni, ambalo lilimtupa chini, hata alipojaribu kuinuka haraka alimuona kijana yule muokota bunduki akishindwa na kubakia akipepesuka kama mlevi, huku akiongezewa teke jingine la usoni, ambalo lilimtupa tena chini, safari hii akijibamiza kwa nguvu kiasi cha kichwa chake kutoa milio wa boga lililogonga sakafuni, Mahamud akamtazama kijana aliemsaidia kwa msahangao “vipi mzee upo salama” aliuliza kijana yule, na baada ya kujibu Mahamud, akajikuta ananong’ona kwa sauti iliyojaa mshangao na shukrani, “Higgno asante sana kijana wangu” alisema Mahamud huku anainuka toka chini, wakati huo huo yule akichota fedha akijaribu kubeba mfuko wa fedha na kuchomoka, maana alishaona kuwa hapa kuwa na usalama mahali pale, na huyu nae aliejibwaga chini pia akijaribu kuinuka na kukimbia, hapo Higgno akawahi kumdaka huyu mwenye kujibwaga akimtuliza kwa teke jingine la mzunguko, ambalo lilimrudisha ndani na kujigonga kwenye kona ya meza ya mule ofisini, akipiga kichwa chake kwenye paji la uso na kuanguka chini, akishindwa kuinuka na kubakia anahema kama kambale alietolewa kwenye maji.
wakati huo tayari yule mwingine mwenye mfuko wa fedha alisha ufikia mlango, hapo Mahamud akaiwahi shot gun na kuikoki huku anakimbilia koridoni, ile anafika koridoni tayari mwizi alikuwa anakaribia mlango, hapo Mahamud akanyoosha bunduki yake na kuminya kifyetulio, hapo ukasikika mlio mwingine wa mlipuko wa risasi. huku yule kijana akitupwa juu na kwenda kujibamiza kwenye mlango aliokuwa anaukimbilia, akifuatiwa na kilio kukubwa cha maumivu huku fuko la fedha likimtoka mkononi na kuanguka chini. tayari alisha kula risasi ya kwenye kalio la kushoto ambayo ilichana nyama za kalio hilo na kutapakaa, ungesema ni panya aliekanyagwa na gari, wakati huo zikasikika tena sauti za wanawake zikipiga yowe la uoga.
Naam dakika tano baadae tayari mzee Mahamud na Higgno walisha wadhibiti wale jamaa wote wanne, na hata polisi walipofika wakiwa wamesha mtia mbaloni Zido na mwenzie Vitus waliemkuta ndani ya gari amezimia, walikuta tayari wale jamaa wanne wameshafungwa kamba, huku wawili kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya kwa Risasi, na ndio wakati ambao Soraya na Laylah waliingia pale ndani, polisi walikuwa wamebaini uwepo wa gari moja na pikipiki mbili za waharifu, huku Higgno akiwakabidhi fungo ya gari lile ambao alimnyang’anya Idd kwenye gari, na hata Mahamud alipoliona akalitambua kuwa ni gari la bwana Mahadhi, “mahadhi ndie aliewatuma hawa watu kuja hapa kunivamia?” alijiuliza Mahamud kwa mshangao, “gari na pikipiki zitapelekwa kituoni kama ushahidi” alisema Kiwili, ambae ndie mkubwa wa kikundi kile cha polisi, hivi muligunduaje kama kuna tukio kama hili linaweza kutokea?” aliuliza Kiwili, huku akimtazama Higgno, Mahamud akisema kuwa hata yeye alitaka kuuliza swali lile lile, “mi mwenyewe nilipewe taarifa na Soraya” alisema Higgno akimtazama Soraya ambae alikuwa hajavaa niqab kwa maana hiyo uso wa mschana huyu na ndio wakati ambao Kiwili aliweza kuiona sura ya Soraya, na kukiri kuwa rafiki yake amepata mke kweli kweli, mi niliona tu watu wanazunguka zunguka toka mchana” alisema Soraya, akiwa anaficha kile anachokifahamu sijajua kwanini alifanya hivyo maana hata Higgno pia alishangaa.
Hakika Mahamud alimsifu na kumshukuru sana Higgno, “kuna wakati nafikiria uwe body guard wangu, lakini inakuwa vigumu kwasababu ni mkwe wangu na utakosa muda wa kukaa na mkeo” alisema Mahamud, katika kumshukuru Higgno, nadhani wa kumshukuru ni Soraya ambae alifanikiwa kung’amua juu ya dalili za kutendeka kwa tukio hili” alisema Higgno, kwa ile sauti yake tulivu.
Muda wote huo Talib alikuwa amejifungia chumbani kwake, hajui kinachoendelea, mchanga nyiko wa bangi ongeza pombe ulimfanya alale kama amewekewa ile dawa ya usingizi wa operation nusu kaputi, mpaka gari la polisi linaondoka kuwapeleka watuhumiwa kituoni na wengine Hospital, pamoja na mzee Ndolite, ambae sasa ndio alikuwa anarejewa na fahamu, Mahamud alieenda na gari lake Hospital, kuchunguzwa afya yake, kama angekuwa ameumia sehemu yoyote, “mke wangu hivi Talib, atakuwa salama kweli?” aliuliza Mahamud, wakati wakiwa njiani wanaelekea Hospita, gari la kina Soraya likiwa nyuma yao wanawasindikiza Hospital, “mh! unadhani kwa ulevi ule amesikia lolote?” aliuliza mama Soraya aliekuwa anaendesha gari.
Saa saba na nusu ndio muda ambao Mahamud alitoka Hospital, akiwa ameshapata huduma aliyo hitaji, japo hakuwa ameathirika sana na tukio lile zaidi ya ngumi na teke la mbavu, ambavyo haviku mletea mvunjiko wowote, akiachana na wakina Soraya ambao walielekea mashariki mwa songea, wakianza Makambi ambako walimuacha Laylah, kisha wao kueleka mtogoro, na kisha mahilo*******
Mida hii ya saa saba ndio mida ambayo Talib alikurupuka toka usingizini, pale juu ya kochi na kutazama saa ya kwenye simu yake, akaona muda unaeleka saa nane za usiku, “sijui wamesha fanikiwa hawajamaa?” alijiuliza Talib, ambae sio kuwa na usingizi wakuzidi, bali alihisi kichwa kizito na mawenge mengi ya usingizi, akiwa bado amejilaza kwenye kochi akataka kupiga simu kwa Vitus, lakini kutokana na kuzidiwa na usingizi, akaachana nayo na kuiweka simu mezani, kisha akajiegesha tena.
Sekunde chache mbele akasikia ngurumo ya gari likisimama nje ya geti, kisha akasikia geti likifunguliwa, kisha gari likaingia ndani na geti kufungwa tena, “mh! nani huyo usiku huu, ina maana anko alitoka?” alijiuliza Talib huku akijaribu kujiinua ili akachungulie, lakini akashindwa kutokana na uchovu wa pombe, akaamua kuachana na mpango wa kuinuka, na kujilaza vizuri, lakini muda huo huo akasikia vishindo vinataembea kuja kwenye ile nyumba yake na kuishia kwenye mlango wake, ikifuatiwa na mlango kugongwa hodi…………. ITAENDELEA