Simulizi: Taifa La Moyo Was Shetani

Simulizi: Taifa La Moyo Was Shetani

bioto

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
1,261
Reaction score
2,099
TAIFA LA MOYO WA SHETANI.
NA..............HEMED MAYUGU.
NO................(01).
WHATSAPP.......0755577488.
SHARE NYINGI NDIYO FURSA YA KUIFURAHIA KILA
SIKU.
NAOMBA KU-SHARE KWA WINGI.
Ilikuwa tarehe mbili ya mwezi wa tano mwaka 2007
Sehemu nyingine zote za inchi ya Tanzania na mikoa
yake pamoja na wilaya zake karibu zote zilikuwa na
hali ya kawaida sana. Lakini siku hio kwa upande
wa Ukerewe ilikuwa ni tofauti kabisa, Siku ambayo
asubuhi ilionekana ina mawingu mazito ya mvua,
radi zikimulika kila mara huku zikiambatana na
miungurumo. Lakini hali hio ilibadilika ghafla na
kuwashangaza watu wanaoishi katika kisiwa hicho.
Hakuna ambaye aliamini kama mawingu yale ya
mvua yameshindwa kusababisha kunyesha kwa
mvua. Basi miyoni mwao walibaki na neno moja tu.
Huu ni muujiza wa mungu, neno hilo ndilo lilikuwa
tiba kwao. Kwa jinsi hali ilivyokuwa ya ajabu kila
mtu aliogopa kabisa kabisa, wengine wakisema
kabisa kuwa lazima watu tungepoteane kama mvua
ile ingenyesha. Anga ilikuwa imetanda wingu zito
jeusi ndi.....wingu hilo kwa hakika ilikuwa zito sana,
yaani hata watu walikuwa wakitoka wawili inje
ilikuwa si rahisi kuonana bila mwanga. Ndani watu
waliwasha vibatari vyao, chemli zao ili kupata
kuonana, wenye simu walikuwa washazima simu
zao wakiiofia hali hio kuwaletea madhara makubwa.
Kiujumla ni hali ambayo ilitisha sana. Lakini hali
ilipobadilika ghafla kila mmoja ilimpasa amshukuru
mungu kwa hofu walio kuwa nayo.
Ingawaje watu wengine walikuwa na hofu miyoni
mwao pindi hali ile ikiwepo lakini kwa wanaume
watano. Junanne, Said, faustini, Manyege na Mgusi
wao walifurahi sana kutokea kwa hali hio. Miyoni
mwao walijisemea kabisa kuwa tayari tumefanikisha
kile ambacho tunaenda kukifanya, hali ile ilikuwa ni
kiashilia kwao cha mafanikio ya jambo lao. Baada
ya hali ile kubadilika wanaume wale, ambao
walikuwa na familia zao walipigiana simu wakutane
kwa mganga wao wakafanya maswala yao. Kweli
hawakuchelewa wakawa wamefika kwa mganga
wao. Walipofika kwa mganga yule alicheka sana
baada ya kuwaona, kicheko cha mganga yule
mwanzo walikipokea hata wao nao wakacheka kwa
kuzania kuwa anacheka kwasababu tukio ambalo
aliwambia kuwa ni kiashilia tosha kwao limefanyika.
Lakini wao walikata ghafla kucheka baada ya
kumuona mganga yule aliyejulikana kwa jina la
TURUMANYWA kuendelea kucheka na kucheka huku
akichanganya na kukoroma. Kitendo hicho kila
mmoja alikishangaa, wote kwa pamoja wakajishauli
wakimbie wamuache mganga yule peke yake
wakizani labda anaenda kufa. Kwani hata mapovu
yalianza kumtoka mganga yule.
Wanaume wale wote kwa pamoja wakiwa katika
matayarisho ya kukimbia, mara walisikia sauti
ikitoka pasiko julikana huku ikiwasemesha. Sauti ile
ya ajabu kabisa hawakuwahi kuisikia hata mara
moja katika maisha yao. Ilikuwa ni sauti ya pekee
na ya kuchanganya. sauti ile ilikuwa imegawanyika
katika sauti karibu za kila rika. Ilikuwa ikibadilika
baada ya sekunde kadhaa na nyingine inaingia.
Nikisema kila rika namaanisha. Ilikuwa inabadilika
mara ya mtoto, mara ya kijana mara ya mzee mara
ya bibi mara ya mwanamke mara ya Baba mtu
mzima. Sauti ili iliyokuwa inatoka kusiko julikana
ilianza kwa kuyaita majina yao, Halafu ikaendelea na
kusema.
"Jumanne, Mgusi, said, faustini na manyege. Ha ha
ha ha! Msiniogope kabisa msiniogope. Nimekuja
kuwapa sharti la mwisho ili kuweza kuzichukua
dhahabu na Utajiri wenu katika pango la moyo
wangu. Sharti langu ni hili, naombeni kwa pamoja
mkamtafute bint mwenye umri wa miaka kumi na
mitano; bint ambaye ni bikra kabisa, bint huyo
mtamchukua mvuke naye maji mpaka kwenye
kisiwa changu, kisiwa ambacho ndimo kuna pango
la dhaabu na Utajiri mwingine mkifika pale kila
mmoja kwa nafasi yake, ahakikishe anamwingililia
bint yule kisha mtamuua kwa kumkata kichwa,
damu yake mmwage kwenye mfuniko wa shimo la
Utajiri na mwili wake mtauwacha pangoni hapo.
Mkishafanya hivyo basi shimo lile litafunguka na
kila mmoja hatajizolea Utajiri wa madini anayo
yataka" sauti ile ya ajabu ilimaliza kwa kusema
maneno "kwaheri nawatakia mafanikio mema"
Baada ya sauti ile kukatika pale pale na mganga
Turumanywa ambaye kipindi sauti ile ikisikika toka
kusikojulikana yeye alikuwa kimya kama kafumbwa.
Mganga yule Aliwauliza wanaume wale.
"Je mmeelewa mlicho ambiwa?"
"Ndiyo tumeelewa. Lakini mbona sharti gumu sana
mganga wetu. Huwezi kubadilisha?"Mgusi aliongea.
"Hapana, vijana hata ikiwa vipi ni ngumu kisiwa
chenye pango la mali huwa akifunguki bila sharti
hilo. Hio tu ndio huwa kafara ya pale na mkisha
maliza basi mtapata Utajiri wa kutosha mnaweza
kujikuta mnakuwa matajiri kuliko wote duniani, ninyi
shida zitawaisha kabisa" mganga alisema.
Baada ya kuambiwa maneno yale, wanaume wale
wote kwa pamoja waliaga kuondoka kutoka kwa
mganga yule nguli kurudi majumbani kwao. Njiani
walikuwa wakiulizana ni wapi watampata bint
ambaye umri wake ni miaka kumi na mitano halafu
bikra ili wamtowe kafara katika kisiwa cha shimo la
dhaabu. Kisiwa ambacho kilikuwa ni kidogo kama
kiwanja kimoja cha mpila wa mguu, kisiwa
ambacho nacho kimo ndani ya ziwa Victoria,
kimepakana kabisa na kisiwa hicho cha Ukerewe.
Wakiwa katika majadiliano yao, Jumanne alisema.
"Jamani mimi nina mtoto wa Dada yangu pale
nyumbani kwangu, umri wake ni miaka hio hio bila
shaka lazima atakuwa bikra" baada ya kusema hivyo
wenzake wote wakamgeukia na kumwangalia. Kisha
Manyege akauliza.
"Jumanne we unataka tukamtoe mtoto wa dada
yako?"
"Unazani manyege tutafanya nini, huu ni Utajiri
mwenyewe unajua hali ya sasa" baada ya kusema
hivyo wote walimtamaza kwa muda kama
wanatafakari jambo. Kwakuwa wote kwa pamoja lao
lilikuwa moja, walikubaliana jumanne akamchukue
mtoto wa dada yake, wakamtoe kafara. Alikuwa ni
bint mzuri ambaye alikuwa kwa jumanne kwa ajili ya
shule na haikuwa kama alijileta, jumanne
mwenyewe ndiye alimuomba kwa dada yake kuwa
aende asomee kwake kwakuwa mazingira ya
nyumbani kwa Dada yake ambaye alikuwa anakaa
maeneo ya kazilakanda Ukerewe ndani ndani kabisa
huko, kielimu yalikuwa si mazuri kwasababu
yalikuwa kijijini sana. Jumane alikuwa akiishi
mrutunguru alimchukua bint yule mdogo bado akiwa
yuko darasa la tano na kumwamishia mrutunguru
kuendelea na masomo yake. Bint yule kwa jina
alitwa Fatuma. Fatuma kweli kama mjomba wake
alivyokuwa anasema alikuwa na umri wa miaka
kumi na nitano pia alikuwa ni Bikra kabisa. Kwa
kipindi hicho fatuma alikuwa anasoma kidato cha
pili.
Baada ya makubaliano yao kukamiliaka watu wale
walimwachia jukumu jumanne aje awakabizishe
mtoto wa dada yake wakamtoe kafara katika kisiwa
cha pango la dhahabu ama wenyewe walikiita
kisiwa cha Shetani. Kisiwa ambacho usiku taa
zilikuwa zikiwaka lakini mchana kulikuwa hakuna
dalili kama huwa kuna mtu wala watu wanaoishi
katika kisiwa hicho kidogo. Kweli kilikuwa ni kisiwa
cha kusitajaabisha kweli kweli, na hakuna ambaye
alikuwa anaijua historia ya kisiwa hicho cha
maajabu ndani ya kisiwa cha Ukerewe. Kwa
asiyeijua Ukerewe mpenzi msomajia nayo pia ni
kisiwa ambacho kimo ndani ya ziwa Victoria,
Ukerewe nayo imegawanyika kivisiwa siwa.
Kikiwemo kisiwa cha Ukara, Goziba na kisiwa cha
Isizu Irugwa pamoja na Ukerewe yenyewe hivyo
vyote ndivyo vinaunda wilaya moja ya Ukerewe.
Mbali na visiwa hivyo ndani ya ziwa hilo hilo la
victoria huwa kuna tuvisiwa twingi, twingine tukiwa
kama mlima ya mawe imejaa mapango. Tuvisiwa
hivyo huwa havikaliwi na watu, kwasababu hata
eneo la kujenga nyuma havina bali ni mawe mawe
tu na mapango ya kutisha. Katika visiwa hivyo
humo ndimo kuna kisiwa hicho cha Shetani.
Ambacho kilikuwa na maajabu ya peke yake.
Baada ya kuachiwa jukumu la kuhakikisha
wanamchuku fatuma. Wakamtoe kafara katika
kisiwa hicho cha pango la dhaabu na Utajiri
uliokuwa umejaa madini ya kila aina, Jumanne
alianza kufanya process za kumshawishi Fatuma
kwa kumdanganya kuwa siku moja atamtoa auti
kwenda mwanza kwa ajili ya kulitembelea na
kuliona jiji hilo. Kama ujuavyo kawaida ya mtoto
akiahidiwa jambo zuri yeye huwa analivalia njuga
kweli kweli. Kwa bahati mbaya zaidi ilikuwa
nikipindi cha likizo. Fatuma alikuwa akimng'ang'aniz
a mjomba wake ampeleke Mwanza akapaone.
Muda huo tayari jumanne alikuwa kaisha wataalifu
wenzake kuwa tayari mambo yashakuwa mazuri
kwa ajili ya kumchukua Fatuma kumpeleka
kumfanyia upuuzi wa kumbaka kwanza kisha
kumchinja kama mbuzi ili tu wapate Mali kutoka
katika kisiwa cha Shetani.
******
Hatimaye siku walizo kuwa wamepanga kumpeleka
fatuma katika kisiwa hicho zilitimia. Jumanne aliaga
nyumbani kwa mkewe kistaarabu kuwa anampeleka
Fatuma Mwanza akapaone angarau kwa siku saba
za wiki, huko mwanza angeishi kwa Mjomba wake
na Jumanne mwenyewe. Bila kujua hata kuelewa
mkewe aliyekuwa anajulikana kwa jina la Restuta
alikubaliana na alichokisema mumewe. Walitoka
nyumbani asubuhi kwa kudai wanaiwahi meli ya
Asubuhi kwenda mwanza. Fatuma akiwa hajui na
mjomba wake walisonga kwenda Nansio, ambako
ndiko kuna kivuko cha meli kutoka Ukerewe kwenda
mwanza. Walipofika Nansio mjomba alimdanganya
mjomba wake kuwa meli imeisha waacha, kwahio
alitafuta gest ili walale kesho asubuhi waamkie
kwenye meli iwapeleke mwanza. Fatuma bila
kukataa kwasababu ajui chochote kilicho nyuma ya
pazia naye alikubali. Kumbe ndio usiku huo huo
walikuwa wamepanga na Rafiki zake kwenda
kumfanyia unyama wa kutisha bint yule. Ilikuwa
mida kama ya saa nne usiku, pale kwenye guest
ilikuja tax mjomba akamwambia bint yake kuwa
waende wakatembee tembee katika mitaa ya
Nansio. Kwa udogo wake akijua kabisa mjomba
wake anamjali fatuma aliongozana na mjomba wake
kutoka ndani ya nyumba ya kulala wageni. Safari
yao haikuwa mbali walielekea upande wa pili wa
mitaa hio ya nansio mitaa ambayo kulikuwa na
mitumbwi mingi ya wavuvi na kukiwa amna mtu
kabisa ziwani kwa muda huo, tayari rafiki zake na
jumanne yaani Mgusi, manyege, faustini na Said
Walikuwa washauandaa mtumbwi wao. Kwa ajili ya
kwenda katika kisiwa hicho. Walipofika pale ziwani
dereva Tax ambaye pia walikuwa wamemuahidi
malipo makubwa aliondoka na kuwaacha ingawaje
dereva yule alikuwa ajui ni nini kinaenda kufanyika
lakini malipo aliyopewa ya pesa yalikuwa ni
makubwa. Mazingira yale fatuma alishindwa
kuyaelewa ikambidi amuulize mjomba.
"Mjomba na huku usiku na giza hili tumekuja
kufanya nini?"
"Huku, kuna upepo mzuri we usikii?"Mjomba
alisema.
"Upepo mzuri sawa mjomba lakini mimi naisi baridi
sana. Ningeomba turudi nikalale"
Bado wakiwa katika mazungumzo yale mwanga wa
tochi ulionekana ukiwamulika, fatuma aliogopa sana
kuona vile, lakini mjomba wake akamwambia
asiogope. Kumbe tayari walikuwa ni marafiki zake
washaingia kwa lengo lao walilokuwa
wamerikusudia.
"Fatuma mama hawa ni rafiki zangu, sasa wanaboti
hapa twende wao watatufikisha mwanza" mjomba
alimdanganya bint wa dada yake. Lakini fatuma
alianza kutilia mashaka safari hio.
"Hapana mjomba tuache tusubili meli kesho saiv
usiku ni vibaya"
"Hapana, mimi natakiwa nifike kule napema kuna
maswala furani nayafuatilia"
Mjomba alisema, kisha akamvuta fatuma kuelekea
kwenye boti iliyokuwa imeandaliwa.
"Lakini mjomba vitu tumeacha gest?"
Fatuma aliuliza kwa wasiwasi kabisa bint wa watu.
"Usijali tutavikuta tukirudi pale ni kwa rafiki yangu
sana.
Baada ya kusema hivyo mjomba alimpakiza Fatuma
kwenye boti kwa kushirikiana na wenzake, fatuma
akiwa kabisa na wasiwasi, Mapigo ya moyo
yakimuenda mbio alikaa tu kwenye boti, moyoni
akijivunia mjomba wake. Kumbe mjomba kaisha
kuwa shetani si mjomba anaye mjua. Boti ilianza
safari kuelekea kisiwa cha pango la madini au
kisiwa cha Shetani.
 
NO. (02).
ILIPOISHIA.
Baada ya kusema hivyo mjomba alimpakiza Fatuma
kwenye boti kwa kushirikiana na wenzake, fatuma
akiwa kabisa na wasiwasi, Mapigo ya moyo
yakimuenda mbio alikaa tu kwenye boti, moyoni
akijivunia mjomba wake. Kumbe mjomba kaisha
kuwa shetani si mjomba anaye mjua. Boti ilianza
safari kuelekea kisiwa cha pango la madini au
kisiwa cha Shetani.
SONGA NAYO.
Watu wale baada ya kuiacha inchi kavu na kuingia
ndani ya maji Miyoni mwao walianza kuingiwa na
furaha ya kuupata utajiri wa mali nyingi, utajili
ambao hakika utakuwa wa haina yake. Mawazo yao
yalikuwa ya matamanio ya mali pekee.
Kwa pamoja wakiwa ndani yamtumbwi huo
walikikaribia kisiwa hicho. Kisiwa hicho cha ajabu
ndani yake kulikuwa kuna moto unawaka kuonesha
kuwa kuna mtu, Ndicho kisiwa hicho ambacho
walikwenda kuchukua utajili, kisiwa cha kumtolea
kafara Fatuma. Kwa mwendo wao wa kasi kabisa
ndani ya maji waligowa kwenye kisiwa hicho.
Kitendo cha kufika pale, mapigo ya moyo ya Fatuma
yalimwenda kasi akajua hapa tayari siku zake za
kufa zimefika.
"Mjomba na hapa tumekuja kufanya nini?"
Fatuma aliuliza baada ya kufika katika kisiwa hicho.
Kisiwa hicho ambacho yeye alikuwa anajua historia
yake kwa kusimuliwa na watu wakubwa kuwa ni
kisiwa kibaya, Hakuna mtu ambaye aliweza kufika
pale, kwasababu nikisiwa cha Shetani na kisiwa cha
majini, lakini siku hio alifika yeye hapo lazima
aliogopa. Swali la fatuma mjomba akulijibu,
alinyamaza kimya, hapo wasiwasi ukamuongezeka
zaidi fatuma. walianza kushuka kutoka kwenye boti
huku wamemshikilia fatuma. Wakawasha tochi
kuona njia kwasababu ya giza.
"Mjomba hapa tumekuja kufanya nini?"
Fatuma aliuliza tena, kipindi hiki ndio alikuwa
akianza kupiga kelele akijua kabisa anaenda kufa
kwasababu ya Historia ya kisiwa hicho, Mpaka hapo
Fatuma alikuwa ajajua mjomba wake kaja kumtoa
kafara, alikuwa akiogopa kufika katika kisiwa hicho
cha hatari. mjomba hakujali wala hakutaka kabisa
kusikia walimvuta fatuma kumsogeza katikati ya
kisiwa hicho, sehemu ambayo moto ulikuwa
unawaka, fatuma alikuwa anapiga kelele kumuita
mjomba kila walipokuwa wanapiga hatua kusogea
mbele, alikuwa akipiga kelele huku akisema.
"Mjomba huku tunaenda kufa turudi kwa mama,
mjomba nirudishe kwa mama nisife"
kelele zake zilikuwa kama anajisumbua tu, mjomba
akulijali. walizidi kusogea kuelekea sehemu iliyo
kuwa inawaka moto. Wakiwa karibu kabisa kufika
eneo hilo fatuma bado akipiga kelele za kuomba
msamaha moto ulizimika, wote kwa pamoja
walibaki na maswali wakijiuliza, bado wakiwa
wanajiuliza lilitokea joka kubwa, kubwa mithili ya
Anakonda, joka lile lilikuwa la ajabu sana, lilikuwa
likibadilika rangi mbalimbali huku likimelemeta.
Hapo kila mmoja alijikuta anaiyachia tochi yake
aliyokuwa ameshikiria na kukimbilia gizani, kabla
hata hawajapiga hatua kumi ilisikika sauti ikiwaita
majina yao.
"Manyege, faustin, mgusi, said na Jumanne mbona
mnakimbia, wakati mmekuja kwa ajili ya
kukamilisha swala lenu, au amtaki?"
Wote kwa pamoja walisimama kuisikia sauti hio
inatoka wapi, waligeuka nyuma hawakuona kitu
kwasababu ya giza nene lililokuwa limetawala hata
wao walikuwa hawaonani, tana kwa bahati mbaya
walikuwa wamevaa masharti mekundu na meusi,
sijui kwasababu gani, chini walikuwa wamevalia
kawaida majinsi kwa baadhi na wengine za
vitambaa vyeusi pia. Hata kama mwanga ule
ukuwepo lakini sauti ile ilikuwa ikiendelea
kuwasemesha.
"Msikimbie nimekuja kuwapokea"
Baada ya kusikia neno hilo hapo kila mmoja
mapigo ya moyo yalishuka, palepale mwanga
angavu kama taa ya umeme ukatokea. Kitendo cha
mwanga kuwaka walijikuta hawana fatuma, wote
wakabaki kuangaliana, mala sauti ilisikika tena
akiwasemesha, aliyekuwa akizungumza akuwa mtu
kumbe ni lile joka likisema.
"Msiwe na wasiwasi mtampata tu hapa hawezi
kwenda popote"
Kila mmoja alistaajabu sana, kuona joka lile
likiongea.
"Basi mtafuteni mimi nawasubili niwapeleke katika
shimo au kiota cha utajili"
Sauti ya joka ikiwa kama kiongozi wao walianza
kutafuta. Kipindi hicho fatuma yeye alikuwa
amenyamaza huku kajificha nyuma ya jiwa, hata
kulia kulikosekama hio ikiwa ni baada ya kuona
joka hilo halafu sasa aliona pia ndio nafasi ya
kuweza kumkimbia mjomba wake na timu yake,
hata maneno ya joka alikuwa akiayasikia, hapo
wasiwasi alikuwa unaongezeka kwa Fatuma.
Alitafuta namna ya kutoka sehemu hio ili atoroke
ndani ya kisiwa hicho, swali alilokuwa nalo
nikitoroka nitatoka kwa usafiri gani? Alikuwa
akijiuliza sana Fatuma wa watu, kulikuwa amna
usafiri kwasababu ajui chochote hata namna ya
kuwasha mashine la kwenye boti endapo akifika
ilipo. Moyoni aliingiwa na wazo moja kuu, alitamani
ajiue pale pale ili asife kwa mateso, alimini asipo
jiua basi kufa kwake kutakuwa kwa kuchinjwa
kwasababu tayari alisha gundua mjomba wake
anaweza kuwa anaenda kumtowa kafara, alikuwa
ajakosea mtu wa watu, ndio ulikuwa ukweli, aliwaza
namana gani ya kujiua, njia rahisi alikuwa hana,
angekuwa na kisu angejichoma, angekuwa na sumu
angekunywa, hayo ndio yalikuwa mawazo yake,
angekuwa na wazo la kujiponda kwenye jiwe kwa
kujirusha angefanya lakini akuwa na wazo lingine
taofauti na Sumu au kisu. Baada ya kuwaza sana,
Fatuma alikosa namna, kwa ujasiri kabisa mtoto wa
Dada yake Jumanne alijinyanyua alipokuwa
amechuchumaa nyuma ya jiwe huku machozi
yakimtoka, akajitokeza mbele kabisa ya watu wale
ambao kila mmoja alikuwa akigeuka upande wake
kwa ajili ya kumtafuta yeye.
"Mjomba mjomba, eeee mjomba"
Fatuma aliiita jina la mjomba wake, mithiri ya
wimbo.
Pale pale wote walimwangalia.
"Nishajua mimi ni kafara eee mjomba, nitakufa kwa
mateso makari eee mjomba,
Basi niko tayari oooo mjomba"
Fatuma aliimba, machozi matupu yakitiririka mithiri
ya matone ya mvua mashavuni mwake.
Mjomba alishindwa kumsogelea Bint yake.
"Mjomba fanya kazi yako uliyoniletea huku, si mimi
nitakufa kwa mateso pekee, naamini kabisa ipo siku
damu ya chozi langu itajilipa, naamini kabisa,
naamini ipo siku damu ya chozi langu itajilipa.
Umfiche mama yangu, usimfiche mama yangu, yote
kwako lakini lazima chozi langu la damu lilipwe"
Hayo yalikuwa maneno ya fatuma, kwa ujasiri
kabisa bint yule alitamka. Mjomba alishindwa
kuvumilia akatokwa machozi, wenzake
wakamkamata fatuma kisha wakamfunga kamba
mikonini, zoezi hilo lilifanywa na Mgusi, said na
Faustin. Manyege yeye akamshika jumanne na
kumjaza imani.
"Hoyo Broo jumanne hapa tumekuja kutafuta, hayo
huwa yapo, na hizo ni changamoto katika kazi,
hujawahi kusikia kuwa wewe huwezi, basi ndio
mfano wake, wewe jikaze ingawaje inauma, tukisha
fanikiwa mambo yatakuwa safi, mbona tutasahau
tu"
Ushauri wa manyege jumanne kidogo ulimwingia,
matamanio ya utajili na pesa za kutosha maishani
mwake vikamtawala.
Joka bado lilikuwa likiwasubili wao.
"Mmemaliza, naweza kuwapeleka?"
Joka lilisema.
Kila mmoja katika wanaume wale alitikisa kichwa
kuashilia wanaweza kuongozwa kuelekea mahala
shimo la utajili lilipo. Fatuma akiwa kashikiliwa
alikuwa anaongoza njia, machozi na kilio cha kwikwi
vikiwa avimuishii mtoto wa watu, alijifikilia sana
mengi moyoni mwake, lakini lakufa na kumwacha
mama yake kipenzi pekee na yeye ndiye alikuwa
anaonwa na kutegemewa kuliko wadogo zake
wawili, kwani yeye ndiye alikuwa mkubwa kwenye
tumbo la mama yake, hicho kiliimuuma sana, lakini
kulikuwa amna namna kwasababu alikuwa yuko
mbali na dunia ya watu ambao wangeweza
kumsaidia.
"Mama, mimi naenda kufa kifo cha mateso mama,
waangalie wadogo zangu mama, naamini mjomba
anaenda kunitoa kafara kwa ajili ya mali mama,
usije ukakubaliana na uongo atakao kwambia kuusu
habari zangu mama, naamini kabisa ukikubali
lazima utampa mdogo wangu mwingine akulelee.
Mi nakufa.....mi nakufa mama, Nakuacha katika
mateso na maumivu makubwa ya kunikosa
mwanao. Kwaheli mama kwaheli, kwaheli ya
kuonana tutaonana akhera kwa mwenyezi mungu na
hukumu zetu"
Yote hayo yalikuwa ni mawazo ya fatuma akijisemea
kimoyomoyo. Wakiwa wanaongozwa na joka bado,
hatimaye walifika pale walipokuwa wanapataka,
mwangaza bado ulikuwa nao ukiwafuata na
kuwamlikia.
"Tayari mnaweza kuiyanza kazi yenu, huu ndio
mfuniko wa mali na hili ndilo pango la kafara"
Joka lilisema. Wote wakilisikiliza joka lile la ajabu
na bila kuliogopa kabisa, yote kisa kupata utajili wa
mali na mabilioni ya mapesa, walizichana chana
nguo za fatuma. Bint wa watu alishindwa kupiga
kelele, kwasababu kelele ambazo alikuwa kaisha
zipiga zilikuwa azimletei hata utetezi wala msaada,
alijiona yuko katika jeshi kubwa la Shetani, jeshi
ambalo halina huruma, jeshi ambalo huruma yake
siku zote ni ya kuangamiza wala si ya kuokoa.
Alibaki kusimama, akisubili kuona nini kinaenda
kufanyika. Mpaka hapo machozi yalikuwa ndio
pekee yamesalia kama ishara ya maumivu moyoni
mwake, akiwa anamwangalia mjomba wake,
ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akivua suruali
yake, aanze kuufanya unyama, unyama wa kutisha
kabisa, unyama ambao kwakeli kwa mwenye roho
ya kweli si ya uchizi ni ngumu kabisa kuufanya.
Mjomba alimaliza kuzivua nguo zake za chini zote,
maumbile yake ya chini yote yakabaki kama alivyo
zaliwa. Fatuma alishindwa kumwangalia mjomba
wake akageuka nyuma. Kisha akasema mjomba
kwanini usinichinje tu kuliko kunibaka mimi mtoto
mdogo hivi, kwanini mjomba usinichinje tu kuliko
kunibaka mtoto mdogo. Kweli umeamua uniue kwa
nateso makari mala mbili"
Maneno ya fatuma mjomba akuyasikia, akiwa
amegeuka bint wa watu haelewi nini kinaendelea
alishitukia tu mikono ya mjomba wake akimshika
shingoni na kumuinamisha. Mjomba alianza kazi
mbaya kazi ya kishetani kabisa. Kwa maumivu
makari ambayo fatuma alikuwa akiyapata, huku
mikono yake ikiwa bado imefungwa kwa kamba,
alijikuta akipiga ukunga mzito na kuomba
msamaha, kwa mjomba, labda kuna kosa kubwa
alilomfanyia Basi amsamehe amwachie, lkini
mjomba akuelewa tena ndio alimuingilia mpaka
sehemu zote mbili, tupu ya mbele na nyuma. Kwa
mala moja mjomba yeye akiwa mfunguzi alimaliza
zikafuata zamu za wengine. Kwa maumivu yale yale
tena kila mmoja akiwa na mzigo wake tofauti
alifanya kama alivyotakiwa kufanya mpaka inafika
mtu wa mwisho fatuma nguvu zilikuwa zishamuishia
amebaki wa kupelekwa na kugeuzwa kila walivyo
taka wao, sauti nayo ilikuwa ishakata haitoki, zaidi
ni damu ndizo zilikuwa zikimvuja kotoka katika
maumbile yake ya Siri.
Hatimaye zoezi la kumbaka fatuma liliisha likabaki
zoezi la kumchinja na damu kuzimwaga kwenye
mfuniko wa Shimo au kiota cha utajiri wa madini ya
kila haina.
Kama shujaa aliyejitolea kafara yeye ndiye
aliyetakiwa kumchinja fatuma kama mbuzi, kwa
amri na muongozo wa joka lile mjomba alichukua
kisu kwenye begi dogo ya mgongoni waliyokuwa
wameongoza nayo. Kisu kikari kabisa kilichokuwa
kimeeandaliwa kwa ajili ya kazi hio, mjomba
alisogea kuifanya kazi yake ya mwisho ili
kukamilisha kisha kuupata utajili.
 
SEHEMU (03)
ILIPOISHIA.
Kama shujaa aliyejitolea kafara yeye ndiye
aliyetakiwa kumchinja fatuma kama mbuzi. kwa
amri na muongozo wa joka lile mjomba alichukua
kisu kwenye begi dogo ya mgongoni waliyokuwa
wameongoza nayo. Kisu kikari kabisa kilichokuwa
kimeeandaliwa kwa ajili ya kazi hio, mjomba
alisogea kuifanya kazi yake ya mwisho ili
kukamilisha kisha kuupata utajili.
SONGA NAYO.
Mjomba bila kuogopa kwa ujasiri na kisu chake
mkononi akamkamata kabisa kabisa fatuma,
ambaye alikuwa yuko chini, akiwa hoi, nguvu hana
kabisa. Mjomba alikiweka kisu shingoni mwa
fatuma, kisha akaanza kuikata shingo yake. Zoezi
alikumaliza hata dakika mbili akawa amemaliza
kisha akakiinua kichwa damu ikamiminwa kwenye
mfuniko wa shimo lenye mali.
Walipomaliza kumimina damu hio, haikuchukua hata
dakika mbili mfuniko wa shimo lile ulifunguka,
ulikuwa ni mfuniko mkubwa kweli, upana wake
ulikuwa kama wa take la lita elfu mbilia. Baada ya
mlango huo kufunguka kwa amri ya joka, Alianza
mjomba kuingia, huyu aliambiwa achukue mali kiasi
anachotaka akiingia kwenye shimo hilo, sababu
ikiwa kwamba yeye kajitolea kafara. Mjomba alirudi
kwenye begi yao, akachukua mfuko wake wa sembe
wa kilo Ishirini na tano kisha akazama ndani ya
shimo.
Ndani kulikuwa giza lakini alipoingia tu mwanga
ukawaka. Mjomba alistaajabu sana, huku juu
alikuwa anaona kama ni shimo lakini huko alikuta ni
bonge la jumba, jumba ambalo limegawanyika
kulingana na utofauti wa madini yalivyo pangana.
Akiwa anaendelea kukagua alitokea mtu, mtu huyo
alikuwa ni bint tu, maajabu ya mtu huyo alikuwa
anageuka sura mara ya Fatuma mala ya mtu
mwingine mjomba aliogopa sana, akataka arudi juu
bila kitu, mtu yule akamshika na kumwambia
"Usiogope wewe si umeijia mali ndio maana
umenitoa kafara, basi njoo chagua madini gani
unataka"
Bint yule alisema huku akiwa anamtajia aina ya
madini yaliyokuwemo ndani ya jumba hilo na
thamani yake. Yalikuwemo madini ya aina
mbalimbali hata mengine duniani huku hayapo lakini
thamani yake ni kubwa kuliko hata dhahabu.
"Sasa madini haya yenyewe yanatumika kufanya
nini?"
Jumanne aliuliza.
"Haya yanatumika kutengeza vitu vya ajabu ukiwa
ndani ya maoteli unaweza kukuta kitu kimening'inia
hewani tu, uoni kiliposhikiria basi haya ndio huwa
yanafanya hivyo, vingine vinatembea hewani"
Mtu yule alisema. Baada ya kuambiwa hivyo
Jumanne alianza kukusanya madini ya akila aina,
Dhahabu na Almasi akivipa kipaumbele kikubwa
akiamini kuwa ndio madini yanayopendwa sana
huku duniani, alibeba mpaka mfuko wake wa kilo
Ishirini na tano ukajaa madini matupu, ndani yake
mule Almasi na dhahabu vikiwa kama robo tatu.
Baada ya kujaza mnamefuko wake mjomba alitoka
ndani ya jumba hilo na kurudi inje ya shimo.
Iliyofuata ilikuwa zamu ya menyege mgusi, faustini
na Said wote kwa pamoja joka liliwaamuru waingie,
nao waliingia nao pia walistaajabu sana kukuta ni
jumba limesheeni kila aina ya madini. Walikutana
na mtu wa aina ile ile wakataka kukimbia nao pia
akawazuia na kuwaambia wachukue madini. Hawa
hawakuoneshwa aina tofauti za madini, hawa
waliambiwa wachukue tu madini basi. Walijichagulia
madini waliyokuwa wanaona ni mazuri kwao. Lakini
kama ilivyo kuwa kwa Jumanne nao walipendelea
kuchukua almasi na Dhahabu kwasababu ni madini
ambayo wameyazoea kwasababu huwa wanayasikia
na rangi yake wanaijua . Wote kwa pamoja
walipofikisha nusu wakaambiwa kuwa muda
umewatosha, wanapaswa watoke ndani ya shimo
hilo kwa ajili ya kujifunga. Wote watatu walitoka
ndani ya shimo hilo kwa haraka, lakini moyoni
walikuwa na maumivu, wakijiuliza imekuwa vipi
Jumanne ajaze kuliko wao inamaana kuna kitu
nyuma yake. Walifanikiwa kutoka inje ya Shimo la
Utajiri na mali nyingi, wakiwa inje Mgusi, faustin,
manyege, na Said walikuwa wakitupa macho yao
kwenye mifuko yao kisha kwenye mfuko wa
Jumanne wivu likuwa ukiwangia taratibu.
"Sasa nazani kila mmoja kapata Utajiri wa kutisha.
Nasema Utajiri wa kutisha kwasababu madini
mlionayo ni mengi kupita maelezo, madini hayo
kuna kokoto na vipande vikubwa, ukichukua kokoto
kwenye kiganja nipesa ambayo ni nyingi hata
kuishika utaogopa, hata vipande viwili kama kipande
cha mche wa sabuni cha mia mbili, pesa yake nayo
unaweza kuogopa kutoka inje ya bank"
Joka lilisema. Maneno ya joka lile kila mmoja
alikuwa akiyasikiliza kwa umakini huku akistaajabu
sana, hapo kila mmoja akajikuta anaamini ni utajiri
mpaka kufa kwake na kizazi na kizazi chake
kitabaki kuwa tajiri.
"Jumanne kachukua mengi kwasababu yeye
kajitolea kafara, ninyi wengine icho ndicho kipimo.
Hata hivyo hayo ni mengi mno tena sana"
Joka lile lilizidi kuwapa somo mashetani wale,
kipindi hicho wakiwa wanaongea tayari mfuniko wa
shimo la Utajiri ulikuwa ushajifunika, mwili wa
Fatuma na kichwa chake pembeni ukiwa umelala
pembeni yao ambako kulikuwa na pango moja
likiwa linatisha hatari.
"Utajiri mtakuwa nao tena ambao duniani haupo
zaid yenu, lakini pia Utajiri huo unamashariti"
"Mashariti!!?"
Wote wakiwa na mshituko waliuliza baada ya
kusikia Utajiri una masharti.
"Ndiyo, mashariti yenyewe ni haya Kila mwisho wa
mwezi, mnatakiwa mlete maziwa(matiti) ya
mwanamke kila mmoja wenu mawili katika kisiwa
hiki, mbili kila mtu inapaswa awe analala na
wanawake wawili walio olewa kila wiki.
Shariti la mwisho inampasa kila mmoja alale na
dada yake ndani ya mwezi wowote mala tatu na
ampe mimba, mtoto atakaye zaliwa baada ya miezi
tisa ni zawadi ya kisiwa hiki. Kumbuka hamtozaa
hata mtoto mmoja isipokuwa huyo wa Dada zenu.
Kwa maana hiyo hampaswi kuoa. Mwanzo
tunawapa miezi mitatu ya kwanza tu, kuwa kama
ofa lakini ndani ya miezi hiyo mnapaswa kuyaleta
matiti hayo hapa kisiwani. Miezi mingine mtafanya
kila mwisho wa mwezi. Kwa hapo mnaweza
kuondoka"
Joka lile lilisema kisha likatoweka, halikuwa na
maneno mengine zaidi ya hayo. Watu wale na
madini yao kila mmoja alishituka akashindwa
kuamini kile alicho ambiwa, hata walianza kuzilaumu
nafsi zao juu ya matamanio ya kutaka mali na
utajili.
Bado wakiwa wanajiuliza kila mmoja kivyake
ilisikika sauti ikiwasemesha.
"Usipotekeleza hata kimoja, basi kifo chako ni cha
mateso na aibu kubwa. Jitahidini mtoke hapa
mapema kabla ya saa kumi"
Sauti iliyokuwa ya kike ilisikika masikioni mwao,
hapo kila mmoja aliisi kuchanganyikiwa hakuna
ambaye alitamani kumtazama mwenzake usoni.
Jumanne aliutazama tena mwili wa Fatuma na
kichwa chake kikiwa pembeni, akatokwa na
machozi, akayakumbuka maneno ya mwisho ya
fatuma.
""""Mjomba fanya kazi yako uliyoniletea huku, si
mimi nitakufa kwa mateso pekee, naamini kabisa
ipo siku damu ya chozi langu itajilipa, naamini
kabisa naamini ipo siku damu ya chozi langu
itajilipa.
Umfiche mama yangu, usimfiche mama yangu, yote
kwako lakini lazima chozi langu la damu lilipwe"""
Maneno hayo makari kabisa Jumanne yalimuwasha
kwa muda. Tayari aliona kuwa ameisha jichimbia
shimo la laana katika maisha yake.
"Potelea mbali, itakavyo kuwa na iwe"
Jumanne alijisemea baada ya kuwaza sana.
Mida hio tayari ilikuwa mida ya saa nane na dakika
ishirini usiku, walijishauri ndani ya dakika kumi tu,
kila mmoja akabeba mfuko wake wa madini kisha
wakaondoka sehemu hio kurudi ilikokuwa boti yao.
Walifika na kuingia kwenye boti yao hawakuwa hata
na nafasi ya kupoteza kuendelea kuwepo kwenye
kisiwa hicho, waliwasha mashine yao na kutoka
hapo. Safarini Jumanne alikuwa na mawazo chungu
nzima, kuitoa roho ya mtu, tena mtoto wa Dada
yake wa kuzaliwa naye tumbo la mama mmoja na
Baba mmoja. Inauma usipime lakini matamanio ya
utajili na pesa amejikuta amefanya hayo. Boti yao
ilipokuwa inaendelea kusonga kurudi Ukerewe
yenyewe, Jumanne aliendelea kujilaumu sana.
Maneno ya Dada yake kipindi anamkabizi mtoto
wake, na ahadi ambazo yeye mwenyewe alizitoa
kwa Dada yake juu ya Fatuma vilikuwa pia
vinamwandama, hata neno potelea mbali kwa muda
huo halikuja tena, mwili mzima alichoka, mapigo ya
moyo yalikuwa yakimwenda kasi sana.
"Jumanne jumanne?"
"Eh!"
Jumanne alishituka kutoka kwenye wimbi zito la
mawazo baada ya kuitwa na mwenzake, muda huo
tayari walikuwa washafika.
"Shuka tushafika"
"Ooho! Kumbe"
Walishuka kwenye boti na kuianza safari ya kurudi
sehemu ambayo walikuwa wameweka makazi yao
kwa muda ili kujiegesha wasubili asubuhi mapema
wainze safari ya kurudi mrutunguru. Japo kuwa
wengine walikuwa na wivu juu ya mali alizopewa
jumanne, lakini walipoa na kusahau baada ya kuona
wana mashariti makubwa yenye kuumiza.
"Jamani hili ni jukumu zito sana, naogopa hata
nianzie wapi, kukata matiti ya watu, aaah mimi
siwezi kabisa. Kumkamata mtu na kumkata matiti,
jamani hapana nyie fanyeni tu"
Bado wakiwa njiani kabisa Said alianza kuonesha
udhaifu.
"Said rafiki yangu fanya yote lakini vile viumbe si
vya kawaida, vinatisha tujitahidi tu kufanya hivyo
tuishi kwa aman"
Faustin alisema.
"Kwa masharti haya mazito utafikiri tulichokitoa
hatujafanya kitu, vitu vyenyewe madini tu bora
yangekuwa mapesa hapa ningefanya kitu haraka,
lakini hapa bado kuuza mala tena ukamatwe
umeyatowa wapi, washikaji bora nife kwa hayo
mateso makari lakini si kwa kuishi nikiua watu
kisha nikate matiti yao, haiwezekani mimi nilijua
nimemaliza kumbe ndio naanza. Tazama hivi
kirahisi tu nilale na Dada yangu, nifanye naye
mapenzi mala tatu, tena hapate mimba azae mtoto
nimpeleke kwa mashetani yale. Kwa hali hii najutia
hata maamuzi yangu ya kumshawishi Jumanne
kumtoa Fatuma kafara, kabisa mungu anisamehe
uroho wa pesa mungu anisamehe sana"
Said alisema huku amesimama na wenzake
wamesimama wote wakiwa wanamwangalia. Mpaka
hapo jumanne alikuwa akitokwa na machozi,
maneno ya Mwenzao yalimuweka katika wakati
mgumu sana.
"Said tayari amna jinsi haiwezekani uruke mkojo
ukanyage mavi, maji ukishayavulia nguo shariti
uyaoge, amna jinsi ndugu yangu, hata ukilaumu zaid
ni kutukumbusha machungu. Unazani tumeyafanya
tunajua yangetukuta, kama umeamua jikatae kivyako
lakini usije ukatuweka sisi katika ubaya, Nazani hata
wewe umesikia ukienda kinyume au kukataa basi
utakufa na kifo chako kitakuwa ni kifo cha mateso"
Manyege alisema. Hapo pote bado walikuwa njiani
wakizungumza halafu wamesimama, muda ulikuwa
ushaenda tayari ilikuwa kama mida ya saa tisa na
nusu usiku.
Bado wakiwa wanajiuliza palepale kilizuka kiumbe
cha ajabu, kilichukuwa kinatisha hatari. Kiumbe
hicho kutoka miguuni mpaka shingoni alikuwa ni
Binadamu lakini kichwa chake kilikuwa ni kiumbe
cha kutisha ambacho hata akielezeki, mikono yake
ilikuwa na kucha utazani chuma. Wote walitoka
mbio kukimbia lakini walikuwa hawatoki pale pale
walikuwa wameganda.
"Msikimbie wala hata msikimbie wengine hamna
makosa mimi shida yangu ni mmoja tu, mmoja tu
ndiye shida yangu, kwasababu yeye anataka kuwa
mfano wa kile tulicho waahidi kuwa mtakufa kwa
mateso makari"
Kiumbe kile kilimaliza kuongea wote kwa pamoja
wakakaa kimya, wasiwasi ukiwa umewatawala.
"Najua ni mimi niko tayari unazani naogopa niko
tayari hata kufa kwa mateso hayo lakini nipokelewe
na mwenyezi mungu nikiwa nimesamehewa dhambi
yangu ya kuuwa kisa mali"
Said alisema kwa kujiamini kabisa, alijiona shujaa
kwa muda huo, sijui hata ujasiri wa kukijibu kiumbe
kile aliupata wapi wakati mwanzo naye alikuwa
katika kukimbia.
Itaendelea.
 
SEHEMU YA ( 04)
ILIPOISHIA.
"Najua ni mimi niko tayari unazani naogopa niko
tayari hata kufa kwa mateso hayo lakini nipokelewe
na mwenyezi mungu nikiwa nimesamehewa dhambi
yangu ya kuuwa kisa mali"
Said alisema kwa kujiamini kabisa, alijiona shujaa
kwa muda huo, sijui hata ujasiri wa kukijibu kiumbe
kile aliupata wapi wakati mwanzo naye alikuwa
katika kukimbia.
SONGA NAYO.
Kwa kasi ya ajabu kiumbe kile kilimfuata Said
alipokuwa amesimama. Kiumbe kila kilimkamata
said shingo na kulitoboa koo, kikakaamia kwenye
mikono kikaivunja kama kuni, haikupita sekunde na
mguu moja nao ukavunjwa akabaki na mguu mmoja
mzima, maumivu yalikuwa ni makubwa na makari
sana kwa said, lakini hata alipokuwa anapiga kelele
sauti yake ilikuwa haitoki, alikuwa asikiki kabisa
hata masikioni mwa Wenzake. Baada ya Zoezi hilo
kile kiumbe kiliamia kwenye macho ya Said
kilimbinya macho yake, yote yakatobolewa, hapo
said akabaki kilema kabisa asiye ona. Kilichobaki
moyoni mwa Said kilikuwa ni kilio cha bila sauti.
Baada ya kumaliza zoezi hilo kile kiumbe
kiliwageukia wenzake na Seid, ambao kipindi hicho
walikuwa wanatamani kufa kabisa, kilichofanywa na
kiumbe kile cha kutisha kiliwashangaza
hawakuamini kabisa. Baada ya kuwageukia kilicheka
sana, mala kikajigeuza na kuwa mwanamke mzuri
mwenye kupendeza, kisha mwanamke yule
akasema.
"Huu ni mfano kwanu mlio salia, naamini
hamtotuangusha, sasa mnaweza kubeba mizigo
yenu na kuondoka, chukueni na ya huyu mtaongezea
kwenu mlio na Madini machache"
Mwanamke yule alisema kisha akabeba mfuko wa
Said akaanza kuwagawanyisha. Manyege, Faustini
na Mgusi. Baada ya kugawanyishwa vizuri
Mwanamke yule alisema.
"Msiwe na wasiwasi wowote kuusu kutapeliwa au
kudhurumia na hata kunyang'anywa hakuna
atakayeweza kuwafanyia hivyo, hata mkiiyacha
mizigo hio hakuna atakaye ichukua. Zaidi mtaikuta
palepale. Lakini kuweni makini kwenye kuzitoa
kafara zenu msije kugundulika itakuwa hatari kwenu"
Mwanamke yule alisema kisha aliwaaga na
kuondoka, Wote wakiwa hawaamini kilichotokea
walimwangalia Said jinsi alivyokuwa anaangaika
pale chini. Walitamani kumsogelea lakini
walishindwa wakaogopa wakazani wanaweza
kurudiwa na kufanyiwa kama yeye.
Waliamua kuondoka na kurudi walipokuwa
wameweka makazi yao kwa muda.
Walifanikiwa kufika kwenye guest ambayo walikuwa
wameandaa kupumzika ili kesho waendelee na
Safari yao ya kurudi mrutunguru.
"Jamani Mimi nimepata wazo zuri!"
Manyege alisema wakiwa wamekaa chumbani
kwenye Guest wakijadili maswala yao.
"Wazo gani hilo?"
Faustini aliuliza.
"Tusirudi nyumbani asahivi, tufanye mpango tuuze
Mali zetu huku huku, au tupande Meli twende
mwanza huko lazima tukusanye mamilion na
mamilioni ya Mapesa"
"Kweli ulichozungumza uko sahihi kabisa manyege
Rafiki yangu"
Faustini alisema huku, Mgusi naye akifuatiya kwa
kuisaport kauli ya mwenzake.
Kipindi hicho chote Jumanne alikuwa amenyamaza,
kichwani alikuwa amejaza mrundikano wa mawazo.
" Jumanne vipi Kaka mbona huko hivyo?"
Mgusi aliuliza baada ya kumuona Jumanne hayuko
katika Furaha.
Richa ya kuulizwa Jumanne akulijibu swali la
mwenzake, alibaki kimya kama hajasikia kabisa.
"Jumanne hebu jaribu kuyaondoa mawazo katika
kichwa chako, tayari tumeisha yafanya na hayo yote
kwasababu kuuwepuka umasikini, hakuna haja ya
kujilaumu angali tayari tushamaliza kila kitu, Majuto
huwa ni mjukuu mwenye kuumiza na kusababisha
kujilaumu mwisho unafikia pabaya"
Mgusi alisema, wenzake wawili nao wakamuunga
mkono kwa alicho kisema.
"Mnacho ongea ni kweli kabisa, hata Mimi
mwenyewe siipendi hali hii initokee lakini nashindwa
kujizuia. Kila nikifikiria kulala na Dada yangu kitanda
kimoja tena Nina Dada mmoja tu, na Huyo ndiye
niliyechukua mtoto wake kafara hii ambayo
imetupatia hizi Mali. Nitaanza vipi hata
kumwangalia"
"Nikweli Jumanne, lakini mimi Nina wazo?" Faustini
alisema
"Wazo gani?"
Wote waliuliza.
"Kwa jumanne kweli kabisa si mchezo. Mi naomba
tukamilishe maswala haya yote tukamuombee
abadilishiwe kafara yake hii ya kulala na Dada yake"
"Kweli inaweza kuwa Rahisi kwa kiumbe hiki chenye
Sumu kari kama Cobra?"
Jumanne aliuliza.
"Hamna lazima tujaribu tusiogope kuuliza, kwani
inaweza kuwa rahisi kikubwa tujaribu"
Faustini alisema.
Hapo wote kwa pamoja wakakubaliana kuwa
watamsaidia Jumanne kuomba kafara yake
ibadilishwe. Kitendo cha kulala na dada yake
kilimuuma sana. Ni kweli si vyepesi kulala na Dada
yako ingawaje wengine wote walikubaliana nayo,
lakini ya Jumanne ilikuwa kali kwani alikuwa na
Dada mmoja tena ndiye alikuwa mama yake na
Fatuma. Kilicho mshinda huyo Dada yake alikuwa
ndiye mkubwa halafu sasa alikuwa kaisha zaa
watoto watatu. Hicho kilimpa Shaka Jumanne
kulifanya jambo hilo na Dada yake.
Kwakuwa walikubaliana vizuri mida hio ya Saa kumi
za alfajiri kuwa; wasafiri waende mwanza kwa ajili
ya kuyauza madini yao. Toka hapo hawakuwa tena
na wasiwasi kwasababu Jini lililo mcharanga Said
lilikuwa lishawaambia kuwa wasiwe na wasiwasi
katika kuuza Madini yao, hakuna hatakaye
wasumbua wala kuwadhulumu. Saa tatu waliamka
tayari kwa maandalizi ya Safari ya kwenda mwanza,
safari ambayo huwa inawatoa Ukelewe mida ya Saa
nane za mchana. Walikaa wakasubili meli ya
Nyeunge itoke mwanza ili wajipakie waje Mwanza.
Kama ujuavyo Jua huwa alichelewi kuyafikisha
masaa yake. Saa nane liyokuwa inangojewa kwa
hamu ilifika, wote wakapanda meli safari ikaanza ya
kuingia ndani ya jiji la mwanza huku mifuko yao ya
vigunia ikiwa imejaa Madini mbali mbali hasa
Dhahabu na Almasi. Hawakushitukiwa hata na mtu
yeyote kuwa wamaebaba nini kwenye vigunia vyoa,
walikuwa wamavifunga kwa Usitadi sana.
Kama kawaida masaa ya meli yalivyo machache
kutoka Ukelewe mpaka Mwanza. Saa kumi na mbili
walifika Kasitam ya Mwanza, kisha wakabeba
vigunia vyao kutoka kwenye meli na kuondoka.
Safari yao kutoka Kirumba kilipo kivuko cha Meli za
Nyeunge iliishia ndani ya Mwanza Hotel. Walipofika
mapokezi ya Hoteli hio walitaka kukaguliwa kabla
hata hawajaulizwa shida yao. Kwa pamoja wanaume
walikataa kukaguliwa, wakaomba waonane na
Meneja wa Hotel hio waongee naye. Askari
aliyekuwa anafanya upekuzi alishindwa kuwaelewa
watu wale, wote kwa pamoja akazani labda ni
vichaa kwani hata mifuko yao ya Madini hawakutaka
iguswe kabisa.
"Nitawapigia police simu?"
Mlinzi alisema.
"We acha hizo police kitu gani bhana we tuitie
meneja ndiye tuongee naye"
Faustini ambaye alikuwa anaonekana mzungumzaji
sana alisema na wazo lake likaungwa mkono na
wenzake wote.
"Ninyi wakaka mbona mko hivyo?"
Mdada aliyekuwa mapokezi alisema.
"Dada sisi hatuna tatizo kabisa kikubwa meneja tu"
Faustini alisema tena.
"Oyo washikaji ye, sikilizeni kwanza.
Dada unasikia, Tunaweka pembeni kabisa mifuko
yetu, halafu mtu asiiguse, halafu mtukague?"
Mgusi alisema.
"Kweli hilo ni sahihi"
Wenzake wote walimuunga mkono.
"Hivi ninyi mmetoka wapi?"
Mdada yule aliuliza.
"Sisi! tumetoka Ukerewe"
"Kumbe ndio maana, niwabishi kama nini, watu wa
huko huwa wabishi bila kujua, na mamifuko yao
hayo sijui yana nini....Basi sikieni tumeishajua kuwa
mmekosea aliyewambia hii ni hoteli ya wageni
kawadanganya hii sio guest. Kimtazamo tu ninyi
hamna adhi hata kidogo ya kukanyaga humu, sijui
imekuwaje tu mkafika...Fyuuuu!"
Bint yule isema huku akiwasonya.
Bahati nzuri kipindi hicho hapo mapokezi
walikuwepo wao tu, watu waliokuwa wanapita
walikuwa hawajali kabisa maswala yao.
"Wewe Dada, unaonekana unadharau sana, wewe
ndiye nitaanza kulala na wewe, nakwapia
nitakuingilia kila tundu la mwili wako mshenzi
wewe, bila kujali masikio wala pua kote
nitakufanya"
Faustin alisema.
"Unasema nini wewe mpumbavu?.......... Franck
tafadhali naomba uite police naona wapumbavu
hawa wamevuka mipaka sasa!"
"Jaribu uone kama kazi hii unaitaka, nitakufanya hii
kazi huiache na usipate kazi pengine popote
mpumbavu wewe"
Mgusi alisema.
Ni muda huo huo meneja wa Hotel alifika.
"Hapa kuna marumbano gani?"
Meneja aliuliza"
"Boss ni hawa wapuuzi, mi nahisi ni wachawi
maana hawataki kufuata taratibu za hapa"
Kabla hata hajasema chochote kwa watu wale
Meneja wa Hotel aliwaangalia kwa umakini, toka
chini mpaka juu huku bado vigunia vyao vikiwa
vimening'inia mabeganj mwao. Watu wale
hawakuwa hata na dalili za kuchoka kabisa,
nawakati mifuko yao ilikuwa na zaidi ya kilo
Therathini.
Baada ya kuhakikisha kuwa amewatazama kwa
muda akajilidhisha Meneja alisema.
"Ninyi vijana mmekosea njia au? Naombeni mtoke
kabla sijaita polisi"
"Mkubwa samahani, sisi hatuna tatizo kabisa na
maamuzi yako, lakini tunashida na meneja wa hoteli
hii tunashida ya muhimu sana kwake"
Magusi alisema.
Kipindi hicho chote Jumanne alikuwa akionesha
ishara ya kutikisa kichwa tu, pale alipokuwa
anakubaliana na wenzake.
"Meneja ndiye mimi, mnashida gani? au mmetumwa
kuniua?"
Meneja alisema.
"Kumbe ndiyo wewe, afadhali bhana, maana hawa
watu wako hawana Adabu kabisa, bora unipe mimi
niwafanye wake zangu wote"
Faustini alisema.
Maneno ya Faustini yalimshitua kila mmoja pale,
hasa yule mlinzi wa kiume huyo aliona kama ndiye
kadhalilishwa kupita maelezo.
 
Sehemu..................(05)
ILIPOISHIA.
"Meneja ndiye mimi, mnashida gani? au mmetumwa
kuniua?"
Meneja alisema.
"Kumbe ndiyo wewe, afadhali bhana, maana hawa
watu wako hawana Adabu kabisa, bora unipe mimi
niwafanye wake zangu wote"
Faustini alisema.
Maneno ya Faustini yalimshitua kila mmoja pale,
hasa yule mlinzi wa kiume huyo aliona kama ndiye
kadhalilishwa kupita maelezo.
SONGA NAYO.
"Hayo ni maneno yametamkwa na kinywa cha mtu
miongoni mwenu au tangazo limepita huko inje?"
"Hapana Mkuu, kwanza tunaomba tu utusamehe
huyu Rafiki yetu yupo kama kachizi kwasababu kuna
kitu ambacho tunahitaji msaada sana kutoka kwako,
ni ishu kubwa sana. Kwahio maneno yote hayo,
anahisi furaha mpaka anajiona kuchanyanyikiwa"
Jumanne alisema.
Hiyo ndiyo ilikiwa kauli ya kwanza kabisa kutoka
kwa Jumanne.
"Hata kama. Hivi kuna jambo ambalo ni zuri kuliko
Utu wa mwanadamu mwenzio?
Hayo ni maneno mazito kabisa ya kudhalilisha....
Okey tuyaache hayo ni jambo gani hilo ambalo
Munahitaji msaada?"
Mkurugenzi yule aliuliza.
Sogea kidogo hapa pembeni, Majura alimsogeza
mkurugenzi yule pembeni, na wenzake wakamfuata.
"Mkuu sisi hapa ni wenyeji lakini Kunabonge la
Biashara tuanahitaji msaada wako, tutakupa kiasi
furani ya tulicho nacho endapo utatusaidia"
Mgusi alisema. Pale wenzake wote wakaitikia.
"Kweli Mkurugenzi"
"Ni kitu gani hicho?"
Mkurugenzi yule aliuliza.
Swali lake halikujibiwa kwa Maneno alishangaa kila
mtu katika wale wanne akitoa kipande kimoja cha
Dhahabu kutoka kwenye mfuko wake wa Suruali, na
kumwambia apokee.
Mkurugenzi yule alitoa macho utafikiri mjusi
kabanwa na mlango, akuamini kabisa kama
alichokuwa anapewa ni vipande vya Dhahabu vyenye
ukubwa kama kipande cha Sabuni ya Shilingi mia
mbili kutoka kwa kila mmoja katika wale wanne.
Kabla hata hajavipokea vipande vile mkurugenzi
yule aligeuza shingo yake huku na kule kuangalia
kama kuna Usalama, alipogundua kuwa mambo
swali alisema.
"Okey rudisheni kwanza mfukoni, Twende huku
ndani tuongee vizuri hapa mambo hayatakwenda
vizuri"
Bila kuchelewa nao walivirudisha vipande vile vya
dhahabu, walivyokuwa wamevitenga kwa ajili ya
kumlainisha mkuregenzi huyo kisha wakamfuata
kule alipokuwa anaenda ndani ya Hotel ile.
Mapokezi pale Yule mlinzi na Bint wa mapokezi
wote walibaki wamezubaa hawakuamini kabisa
kama watu wale ambao wamefika hapo kwa
maneno ya Shombo ya kudhalilisha wamekubaliwa
na kusikilizwa na mkuregenzi wao kirahisi tu,
"Hapo amna hawa lazima watakuwa na mchongo wa
hatari"
Yule mlinzi alisema.
Kabla hata wenzake hajafika mbali Faustin alirudi
mbio pale kwa yule bint aliyekuwa mapokezi na
kumwambia.
"Mtoto mzuri usiuzunike kwa nilichokisema, lazima
utafurahi tu muda mfupi, we jiandae tu, lazima
nikufanye mambo mi nakwambia ukweli"
Baada ya kusema maneno hayo, Faustin ambaye
tayari akili zake zilikuwa zimeisha Anza kubadilika
kabisa zikawa katika Ushetani uliokamilika,aziogopi
hata kuongea matusi kwa watu, alirudi kwa
kuwakimbilia Wenzake kule walipokuwa wanaenda
huku begi yake ya kigunia ikiwa nyuma. Kweli pesa
mwana haramu, watu wale hawakuchoka kabisa,
yaani hata dalili za kuchoka hawakuzionesha
ingawaje walikuwa wanaumia lakini kuiachia mizigo
yao hapana.
Walipanda kwenye Ghorofa ya juu ya Hoteli hio
ndiko walienda kuongelea, mkuregenzi yule
aliwaingiza kwenye chumba cha siri kabisa
ambacho hakikuwa na kitu chochote, chumba hicho
kilikuwa Empty kabisa wala Kiti hakikuwemo.
"Eeee! Sasa hapa tunaweza kuongea vizuri vijana"
"Mambo ndio kama tulivyo kuonesha, unaona hizi
mifuko yote imejazana mizigo si Dhahabu tu hata
madini mengine nayo yamo, kuna madini ambayo
hata huyajui, kwahio fanya mpango tupate wateja
ninyi ndio mnawajua watu wanayo yataka madini
bhna"
Faustin alisema.
"Sawa, lakini Kwa upande wangu vipi sasa, hata
mimi lazima nipate fungu langu kama dalali"
Mkurugenzi alisema.
"Hilo tu, basi fanya hivi, Chukua hizi kama
kutukaribisha kwenye hoteli yako, pia kuishi humu
mpaka tutakapo pata wateja" Majura alisema huku
kila mmoja akiwa ameshikilia kipande cha Dhahabu
yake, na kumkabizi. Mkurugenzi yule alipokuwa
anaviona vipande vile vilivyokuwa vimenona alijikuta
anaisi anapaa, maisha yote Duniani kayamaliza.
Alikuwa anaogopa hata kuvipokea.
"Hivi Dhahabu nzito kama hii umeitolea wapi, yaani
toka kuzaliwa sijawahi kuiona kabisa"
"Ha ha ha ha! Basi leo umeiona"
Watu wale wote walicheka kisha wakasem hivyo.
Kwa jinsi vipande vile vilivyokuwa vikubwa
Mkurugenzi wa hoteli ile alidata kabisa. Alivipokea
kisha, akapiga simu mapokezi na kuwambia
wapange vyumba vinne vya wageni wale kwa wiki
kabisa.
Mambo ndio yalikuwa hivyo, wakakabiziwa vyumba
vyao vya kuishi na kulala pale Mwanza hotel. Baada
ya kupewa vyumba la kwanza kabisa kichwani mwa
Faustin alikuwa ni Bint wa mapokezi, alimfuata pale
pale. Mwanzo Bint yule aliweka ngumu kukubali.
"Unazani kilicho kufanya Uwepo hapa ni nini?"
Faustin alimuuliza yule Bint ambaye bado jina
alikuwa hajaliju, kipindi hicho mlinzi alikuwa
mlangoni inje asijue nini kinaendelea ndani.
"Hayo hayakuusu, Naomba unipishe, Usije kunialibia
kazi, nipo kazini na sistahili kuongea na mtu kwa
maswala ya kipuuzi kama haya"
Bint yule alisema.
"We usijali, mbona jepesi tu, hapa tutamleta
mwingine, maisha yetu yataamia Ulaya"
Faustin aliendelea kusema.
"Wewe hivi ni kichaa. Nitapiga kelele hapa"
Bint yule alisema.
Faustin akuchoka wala kuteteleka kwa maneno
mazito ya vitisho kutoka kwa biny yule.
"We sema sana, lakini ungejua kilichomsababisha
Boss wako kuwa mpole ni nini, basi mpaka hapa
usinge kuwa unabisha chochote. Tena ngoja
nikuthibitishie wewe ndiye naanzia kwa Maagizo
yangu"
"Maagizo yako?"
Yule Bint aliuliza baada ya maneno ya Faustin
kumtisha.
"Tazama, ili ni pambo moja, sasa fikilia nimeyajaza
kwenye mfuko wangu, utaki kutajilika. Kama
unashida ya pesa za kutosha nitafute kwa muda
wako"
Fausitin alisema kisha akakiweka kipande kidogo
kabisa kiasi kama kokoto kwenye dirisha la pale
mapokezi. Na kuondoka kurudi vyumbani.
Hata kabla hajapiga hatua zaidi ya sita. Yule bint
aliita kaka samahani, naomba urudi"
Faustin naye akulinga akageuka na kumrudia.
"Mimi ninaitwa LOVENESS. Chukua basi hii namba
yangu, Tutawasiliana"
"Ha ha ha ha ha! Yako sichukui mmmh! Chukua
yangu hii hapa utanitafuta mwenyewe kwa muda
wako?"
Faustin alisema huku akimwandikia bint yule Namba
za simu na jina lake.
Baada ya kumwandikia jina na namba za simu, Bint
yule alitabasamu na kusema.
"Kumbe wewe ndiye Faustin, jina lako Zuuri basi
nitakuja Chumbani kwako mida ya saa Nane hivi
Usiku kwasababu Shift yangu itaisha mida hio"
Bint yule alisema huku akilemba sauti.
"Kwani Chumba changu unakijua?"
"Mimi si ndiye nawapangia"
"Mh! Chumba changu ni namba ngapi?"
"Vyumba vyenu vimepanga. We ni wa pili Chumba
namba 205"
"Kweli kabisa Basi Usijali mi sina haraka sana na
wewe, ila Ukijifanya mjanja watoto wazuuri Humu
Town wamejaa tena wanashida na pesa. Naweza
kuwatafuta tena kwa kuita tu nachukua mzigo"
Faustin alisema.
"Jaman Usifanye hivyo, mimi nipo kwa ajili yako,
yaani utanifaidi utakavyo"
"Hapo umenena. Basi poa Mi nakuacha"
Faustin alisema na kugauka kurudi.
"Sawa, lakini usijisikie Vibaya, yani naweza kuja
hata kabla ya Muda huo"
"Ni wewe tu, utakavyo amua"
Fastin alisema.
Kwa muda huo sehemu ya mapokezi waliifanya
kuwa kama sehemu ya kutongozana wala si
Sehemu ya kazi.
Baada ya Faustin kuondoka, Bint yule alibaki na
washwa washwa. Mida hio ilikiwa tayari Ishatimu
saa moja inaelekea na Nusu. Kwa Bint yule
aliyejitambulisha kwa jina la Loveness alitamani
muda wake uishe ili aende Chumbani Kwa Faustin
kwa ajili ya kumtimilizia Haja zake, Loveness
alianza kuteseka na kuwaza. Mawazo ya wivu nayo
yakaanza kumuingia huku akiitazama Dhahabu
aliyopewa alijikuta anajisemea.
"Jaman Faustin usije ukamchukua mwingine"
Loveness Bint ambaye alikuwa mzuuri alijikuta
anazama katika mtego wa Shetani kwa Matamanio
ya mali na utajili.
*****
Usiku wa manane kila mmoja akiwa amelala
Chumbani kwake, Faustin akuwa peke yake
kitandani mwake alikuwa na Bint mwingine kabisa
tofauti na Loveness.
Kilichokuwa kinaendelea ndani ya Chumba hicho
ulikuwa ni Uchafu na udhinifu ambao unapigwa vita
katika vitabu vya mungu. Fausitin alikuwa
anayafanya hayo akiwa amesahau kabsa kuwa
nyumbani kamwacha mkewe. Yote hayo aliamini
sasa anaanza kulitekeleza Agizo la kishetani na
maandalizi ya kupata Kafara za kumpelekea Shetani.
Faustin akiwa anaendeleza uchafu wake, Loveness
bila hata kupiga simu kwa Faustin ili kumwandaa
alifika moja kwa moja kwenye mlango wa chumba
cha Faustin, na kugonga.
"Nani anagonga?"
Faustin aliuliza.
"Loveness"
Faustin alipolisikia jina la Loveness akushindwa
kuufungua mlango, aliufungua malango kisha
akamruhusu Loveness kuingia ndani ya Chumba
chake. Loveness alitaka kurudi mbio baada ya
kukutana na uso wa mwanamke mwingine kabisa
ambaye yeye akumtarajia.
Tena mwanamke yule alikuwa kama alivyo zaliwa,
halafu alichokua anakifanya ni kuchezea maungo
yake ya Siri. Muda huo hata faustini alikuwa hivyo
hivyo kama alivyo zaliwa.
"Unataka kurudi!..kama utaki pesa unaweza kurudi
tu, niache mi niponde raha zangu, na ukiondoka
usije ukaisogeza miguu yako karibu na mimi tena"
Faustin alisema kwa kujiamini kabisa baada ya
 
SEHEMU (06),
WHATSapp. 0755577488.
ILIPOISHIA.
Tena mwanamke yule alikuwa kama alivyo zaliwa,
halafu alichokua anakifanya ni kuchezea maungo
yake ya Siri. Muda huo hata faustini alikuwa hivyo
hivyo kama alivyo zaliwa.
"Unataka kurudi!..kama utaki pesa unaweza kurudi
tu, niache mi niponde raha zangu, na ukiondoka
usije ukaisogeza miguu yako karibu na mimi tena"
Faustin alisema kwa kujiamini kabisa baada ya
kumuona Loveness anataka kurudi nyuma.
SONGA NAYO.
Maneno ya Faustin yalimuingia Loveness akajiuliza
kwa muda lakini Matamanio ya kupata Mali na
utajili na yakaishinda Nafsi sahihi. Akajikuta naye
anaingia Ndani ya Chumba cha Faustin.
"Haaaa! Toto hilo, hizi pesa bhna"
Faustin alisema kwa mzaa. Kwa upole Loveness
alikaa kitandani upande wa chini huku mwanamke
mwenzake naye akiwa upande wa juu.
"Dada karibu"
Yule Mwanamke alisema.
Yule Mwanamke Mwingine alisema huku akimshika
Loveness kwenye bega lake la kulia.
Loveness hakusema kitu alibaki kimya tu.
"Baby achana naye, huyu kwanza bado nitaongea
naye"
Faustin alisema kumwambia mwanamke yule.
"Loveness huyu ni Malaya tu nimemkuta Town humu
si unajua nilikuwa na hamu muda mrefu kwahio
sikuwa na haja ya kukungoja wewe. Yeye anaitwa
Sauda!"
"Sasa ndiyo unifanyie hivyo Faustin?"
Laveness alisema kwa uchungu.
"Kwani Shida yako ni kuwa billionaire au nikuwa
mpenzi wangu wa ndoa Mimi haya ndiyo maisha
yangu, yaani Mimi kuoa haimo katika maisha yangu,
yaani labda wewe utakuwa pumzikio langu nikiwa
nakuja hapa mjini kwa ajili ya Mishe zangu kama
hutaki unaweza kusepa. Sauda nipe mambo naona
huyu analeta nyodo mbele ya miela"
Faustin alisema.
"Kweli Baby sogea nikupe Radha nzuuri mpaka
usaze"
Sauda alisema. Maneno ya Sauda yalikuwa sumu
sana kwa Loveness alijikuta anamwangalia kwa
jicho la hasira sema tu alikuwa hana namna ya
kufanya
Muda huo Faustin alimsogelea Sauda na kuanza
kuufanya upuuzi mbele ya Loveness. Kabisa
Loveness aliendelea kumwangalia Faustin na Sauda
wakiendelea kuufanya uchafu huku Sauda kahaba
aliyekuwa amekubuu ndani ya Jiji la Mwanza akiutoa
miguno ya mahaba ambayo ilikuwa inaingia moja
kwa moja katika masikio ya Loveness. Hali hio
ilimuumiza sana Loveness lakini kutoka alishindwa
kwasababu tu kaisha ambiwa akitoka tu, asiisogeze
miguu yake kwa Faustin. Pesa ni kitu cha ajabu
sana, tumuombe mungu atulinde juu ya ushetani wa
pesa atupe vya alali.
Faustin aliendelea kuuchezea mwili wa Sauda kwa
muda wa dakika kama therathini akawa amemaliza.
Sauda naona uko vizuri daah! Mtoto unajua hatari!"
Faustin alisema.
"Kweli Babe?"
"Mmmh sana tu, yaani wewe ni kifaa nitakupa Mali
ya kutosha tu"
Faustin alisema.
"Daah! Nitafurahi sana"
"Usijali mpenzi wangu"
Faustin alisema.
Muda huo Loveness aliendelea kunyamaza kimya
huku kainamisha kichwa chake, alikuwa na hasira
sana, moyoni alikuwa anajilaumu kwanini kairuhusu
Nafsi yake kutamani. Lakini kutoka alishindwa.
Bado moyoni alipata mgogoro moyo wake ulikuwa
umegawanyika katika vipengele vitatu. Nafsi moja
ilikuwa ikiongoza atoke katika chumba hicho na
ashikilie msimamo wake, Nafsi nyingine
ikimwambia aache asubili kupata Mali, Nafsi
Nyingine ilimwambia
"Kwani kufanya Mapenzi nae hata mala moja
akakupa madini hutashindwa we Fanya anavyotaka
ukipata chako, umekamilisha maswala yako, tayari
nawe utakuwa katika watu wenye mafanikio
makubwa"
Nafsi hii ndio ilikuwa inaongoza kuliko zote.
ingawaje na nyenzake ya kusema aache apate Mali
zilikuwa zinafanana lakini hio ya tatu ndio ilikuwa
kubwa sana. Nafsi ya kwanza alimpa wasiwasi
lakini ilikuwa haina nguvu kabisa katika chumba cha
Shetani.
"Loveness Toto zuuri hilo. Sasa ni zamu yako, nipe
basi mh!"
Faustin alisema huku akimshika Loveness kichwa
kumuinua.
"Babe kama ujatosheka si uje tu kwangu uwachane
naye huyo mbabaishaji!"
Sauda alisema.
"Usijali Sauda wewe umenitosha nataka kitu kipya
na ladha mpya kutoka kwa Loveness. Kama hataki
hatupishe niendelee kula ladha nzuuri kutoka kwako
Mtoto mzuuri"
Faustin alisema. Maneno yake yalimfurahisha sana
Kaaba Sauda.
"Lavenesa simama basi unipe ladha yako, nina
hamu na kitu chako"
Faustin alizidi kusema maneno machafu kabisa,
maneno ambayo yalikuwa ya kudhalilisha, lakini
basi tu, ni kwasababu alikuwa anajiamini kwa
alichonacho.
Muda huo huo Loveness naye alisimama mwenyewe
akazivua Nguo zake, hakuogopa tena kuufanya
uchafu aliokuwa anautaka Faustin. Nafsi ya Pili na
ya Tatu viliishinda nafsi ya kwanza, matamanio ya
pesa yakamtawala Bint wa watu.
"Sasa mambo ndio haya, lazima Nile Raha Duniani.
Mtoto unakiuno hatari"
Faustin alizidi kuyasema maneno ya kumpamba
Loveness ili apate kile alichokuwa anakihitaji.
Mambo yalikuwa mambo ndani ya chumba cha
Fausti, chumba kiligeuka ukawa ukumbi wa kufanyia
uzinzi kwa wanawake wote wawili, usiku wote
mpaka kunafika mida ya saa kumi ndio Faustini
alipata kulala na wanawake wake wote wawili.
******
Kumbe hayo hayakuwa kwa Faustin tu hata,
Manyege na Mgusi nao walikuwa na Makahaba
vyumbani mwao.
Lakini kwao ilikuwa tofauti kidogo kwani wao
walikuwa na Kahaba mmoja mmoja.
Kwa upande wa Jumanne yeye hakuweza kulala na
kahaba, kwa siku hio yeye alikataa. Bado mawazo
ya Fatuma yalimuingia kichwani mwake. Aliumia
sana, lakini namna ya kumrudisha haikuwepo tena,
kilichokuwa kimebaki kwake ni kutekeleza wajibu
wa mkataba aliosaini, mkataba wa shetani, mkataba
ambao lazima aufanye la sivyo kifo chake kitakuwa
cha mateso na aibu kubwa.
Mambo kwake yalikuwa magumu sana.
"Daah! Haya maamuzi magumu niliyatowa wapi
Mimi?"
Jumanne alijisemea. Alikuwa ni mtu wa kujilaumu
na kujijibu mwenyewe, majawabu yalikuwa anayatoa
mwenyewe nafisini mwake.
Kujilaumu na kujijibu nafsi zake zilifanya kazi hio.
"Ngoja tu huwa yanasaurika hata hivyo Mimi siyo wa
kwanza, huwa nasikia kwenye redio na huwa
nayasoma magazeti na hadithi za watu, huwa
wanatoa kafara kisha wanafanikiwa na kuishi kwa
Furaha. Hata Mimi nitaweza tu"
Jumanne aliendelea kutafakari. Mpaka asubuhi
kunakucha Jumanne usingizi kwake ulikuwa mtihani
hakufanikiwa kabisa kuupata alishinda macho usiku
mzima.
******
Asubuhi kuliko kucha, mida ya saa nne wote
walijikusanya na vigunia vyao vya madini kwenye
ghorofa ya juu ya Hoteli, huko walikuwa na kikao na
Mkurugenzi wa Hoteli hio alikuwa kaisha waletea
watu wa kufanya nao biashara. Muda huo tayari
walikuwa washawapa makahaba wao madini kiasi
kwa ajili ya starehe ya usiku mmoja walio lala nao,
akiwemo Loveness.
Wakiwa bado wamekaa huko huko juu mala kilikuja
kikundi cha watu saba kwa ajili ya kuongea nao ili
kufanya biashara ya madini yao.
Watu wale nao walifika na kukaa. Kwa watu waishio
ndani ya Jiji la Mwanza wanaijua Mwanza hotel
vizuri kwa juu kabisa kuna ukumbi mzuri kwa ajili ya
mikutano. Huko ndiko walikuwa wamekaa.
" jamani ndugu zangu hawa ndiyo wafanya biashara
wa madini. Wamekuja kuangalia na kukubaliana na
nyinyi ili mpate kuuza mzigo wenu kisha mkabiziwe
chenu nao waende zao"
Meneja au Mkurugenzi wa Hoteli alisema kuwambia
akina Jumanne na wenzake.
"Jamani ndugu wafanya biashara hawa ndio watu
ambao usiku nimewambia kuusu madini"
Mkurugenzi huyo alisema tena kuwambia wafanya
biashara wale wa madini.
Baada ya Mkurugenzi yule kusema hivyo wote kwa
pamoja walisimama na kuanza kusalimiana kwa
kushikana mikono. Kila mmoja alikuwa mwenye
Furaha sana.
"Jamani sisi tunashukuru sana na sisi kama
alivyosema Mkurugenzi hapa ni wafanya biashara
wa madini na tumekuja kuona na kupata uhakika juu
ya Jambo hili kwahio bila kupoteza muda
tungeomba mtuoneshe Madini yenu ili tupate
kuelewana"
Mtu mmoja aliyekuwa amevalia vizuri, suti ya nguvu
alisimama na kuwambia akina jumanne na wenzake.
"Mkuu hakuna shida sisi mzigo wetu huko vizuri
kabisa na wa uhakika. Labda cha kufanya ngoja
tuweke hapa mifuko yetu mtakuwa mnapita mmoja
mmoja na mnayakagua kisha mtatoa majibu yenu"
Mgusi alisimama na kusema hivyo. Kisha wote
wanne wakasimama na kuvifungua vigunia vyao
vilivyokuwa vimejaa madini ya kila aina na yenye
thamani kubwa kama dhahabu na mengine kuliko
dhahabu.
Baada ya kumaliza kuvifungua vifurushi hivyo
walivipanga vyote juu ya Meza kubwa iliyokuwepo
mbele yao. Baada ya zoezi lao, wafanya biashara
wale mmoja mmoja alisimama na kupita huku
akiingiza mikono kwenye mifuko ile na kuangalia
kama kweli ni madini sahihi.
Wote saba walimaliza kuikagua mifuko ya madini
walirudi kukaa kila mmoja alikuwa akitikisa tu
kichwa hawakuamini walichokutana nacho. Wote
walichanganyikiwa kabisa.
"Samahani eti, haya madini ya namna hio na mengi
tofauti tofauti mneyatolea wapi?"
Mtu mmoja kati ya wale alisimama na kusema.
"Nazani hilo halina jibu kikubwa tufanye biashara"
Mgusi alisema tena.
"OK, kwakeli mzigo Mkurugenzi ni wenyewe na
ambao ni wa ukweli kabisa"
Mtu yule yule alisema.
"Ni kweli hata Mimi mwenyewe nilipouona
nilichanganyikiwa"
Mkurugenzi alisema.
"Okey! jamani kama tulivyosema kuwa sisi ni
wafanya biashara wa madini. Lakini sio wenyewe
sisi ni wawakilishaji tu wenyewe wapo. Kila mmoja
hapa amekuja kumuwakilisha Bossi wake, kwahio
tuwaahidi kuwa kesho kutwa mabosi wetu watakuja
kuuchukua mzigo"
Mwanaume mmoja alisimama na kusema.
"Sawa lakini mbona hatujaongea bei?"
Faustin alisema.
"Kuusu swala la Bei msijali yaani hapo nyie subulini
utajili wa majumba na magari ya kufahari na
mabilioni ya pesa kwasababu tumeisha jua kila kitu"
Mwanaume yule alisema tena.
Baada ya kusema vile watu wale wote walisimama
na kuondoka na kuwaacha akina jumanne
wakiifunga tena mifuko yao ili kuiweka salama.
Bado wakiwa huko huko mkurugenzi wa Hoteli
alirudi tena, kwani alikuwa ametoka kuwasindikiza
wageni wale wa madini.
"Sasa nisikilizeni kwanza. Hawa jamaa kama
walivyosema niwawakilishi tu, kweli mizigo yenu
wameikubali sana, hapo walipo wamechanganyikiwa
kabisa. ni mzigo mkubwa mno huu, yaani ni
mabilioni ya mapesa. Kwahio mabosi wao watakuja
kuuchukua kesho kutwa. Mabosi wao sio weusi ni
wazungu tu"
Mkurugenzi alisema.
"Ni wazungu tu?!"
Faustin aliuliza kwa mshangao.
"Ndiyo yaani msiwe na shaka tena wamesema
wanaweza kuwajengea majumba makubwa na
magari ya kifahari halafu na pesa za kutosha"
Mkurugenzi yule aliwambia tena. Hapo wote
walijisikia Furaha sana, hata Jumanne naye
alichangamka vya kutosha kwa muda huo alijikuta
anayasahau tena aliyokuwa anayawaza.
"Sasa si mmeona Mimi niliwambia hapa amna
kurudi home twende zetu Mwanza tutauza mzigo
halafu kurudi kule tutakuwa tushakuwa matajili"
Faustin alisema.
"Ni kweli Faustin nimekukubali sana. Manyege
alisema.
Kisha nao wakabeba mifuko yao wakarudi nayo
vyumbani kwao kuiifadhi, hawakutaka kuiacha
kabisa mifuko yao. Kama walivyokuwa
wamehaidiwa na Lile jini lililo mcharanga Said
hakukuwa hata na usumbufu wa kusumbiliwa ambao
ulijitokeza kwao toka wafike.
 
SEHEMU YA (07).
WhatsApp. 0755577488.
ILIPOISHIA.
"Sasa si mmeona Mimi niliwambia hapa amna
kurudi home twende zetu Mwanza tutauza mzigo
halafu kurudi kule tutakuwa tushakuwa matajaili"
Faustin alisema.
"Ni kweli Faustin nimekukubali sana. Manyege
alisema.
Kisha nao wakabeba mifuko yao wakarudi nayo
vyumbani kwao kuiifadhi, hawakutaka kuiacha
kabisa mifuko yao. Kama walivyokuwa
wameahidiwa na Lile jini lililo mcharanga Said
hakukuwa hata na usumbufu wa kusumbiliwa ambao
ulijitokeza kwao toka wafike.
SONGA NAYO.
Baada ya kumaliza waliletewa break fast Vyumbani
mwao. Katika chumba cha Jumanne aliingia Bint
mzuuri. Jumanne alipomuona tu, akachanganyikiwa.
"Mrembo samahani wewe unaitwa nani?"
Jumanne aliuliza.
"Mimi naitwa Suzan"
Bint yule alijibu.
"Kumbe! Jina lako zuuri kama wewe ulivyo"
"Mimi mzuuri kwani?"
Suzan aliuliza.
"Ndiyo we ni mzuuri hatari"
"Kaka asante, Na wewe unaitwa nani?"
"Mimi ninitwa Jumanne"
Jumanne alisema.
"Ooh! Nashukuru kukufahamu kaka yangu"
"Usijali!"
Jumanne alisema. Muda huo natamanio yalikuwa
yashamwingia Jumanne kwa Bint yule
aliyejitambulisha kwa jina la Suzan. hakutaka
kumwacha akamwambia pale pale kuwa anashida
na penzi lake, Bint yule hakubisha kwasababu naye
tayari alikuwa kaisha jua habari zao kuwa
wanamadini mengi hatari.
Baada ya Bint yule kukubaliana na Jumanne ambaye
usiku hakufanya Chochote kwasababu ya mawazo
alimbidi aanze kuonesha utundu wake kwa Suzan,
Suzan naye alijiregeza kwa jumanne akajilainisha
kweli kweli. Jumanne akazidisha naye mbwembwe
zake akajisahau kabisa kabisa. Kumbe Bint yule
alikuwa na lake, alikuwa na sumu ambayo
ingemlewesha jumanne, sumu ambayo tayari
alikuwa kaisha iweka kwenye chai. Sumu hio
mahususi ilikuwa kwa ajili ya kumfanya jumanne
alewe kabisa na asinzie usingizi mzito kisha yeye
amuibie mzigo wake.
"Babe pasha kwanza tumbo ndio tuendelee basi!"
Suzan alisema kwa madeko.
"Hapana mi kwakeli Niko vuzuuri kabisa, labda
penzi lako tu ndiyo liwe chai yangu"
Jumanne alisema.
Kwa kuona kuwa watazungushana yule Bint alikubali
kwanza kumpa Jumanne penzi ili afanikishe
dhamila yake. Aliamini kabisa kuwa Jumanne
akisha Fanya naye Mapenzi tu, lazima Mwisho
anywe chai halafu ambacho kingefuata lazima
angesinzia kisha yeye akamwibia mfuko wake wa
madini. Basi naye alifanya kutekeleza, Jumanne
shetani aliyeamua kumtoa Mtoto wa Dada yake
kafara kisa Mali alijikuta anazama kwenye penzi la
Suzan. Baada ya kumaliza kweli alichukua chai na
kunywa, Suzan alikataa kuigusa chai ile ingawaje
Jumanne alikuwa amemuomba wanywe naye lakini
yeye alidai tayari. Kwa kuifukamia chai huku na
vutafunio vya nguvu vikiwa juu ya meza. jumanne
alijikuta anaisi usingizi mzito hata Kabla hajamaliza
kunywa chai, Macho yalianza kulewa lewa,
akazidiwa kabisa yeye mwenyewe alijitupa kitandani,
tayari usingizi ukawa umempitia.
Baada ya kuona mambo yako Vizuri Suzani aliamua
kukinyanyua kigunia cha Madini ya Jumanne
ambacho ndicho kilikuwa na Madini mengi na
yamchanganyiko wa madini mengi ya ufahari. Suzan
alijikunja kwa uwezo wake wote akashindwa kuutoa
mfuko Chini ulipokuwa, kila alipojaribu akashindwa.
Baada ya kushindwa alibeba vyombo vyake na
kurudi Jikoni alipofika akaichukua simu yake
mfukoni akampigia mtu. Mtu aliyekuwa akiongea
naye alikuwa ni Mkurugenzi wa hoteli hio, kumbe
naye tamaa ilimuingia akatamani kuiba mfuko wa
madini wa Jumanne.
Suzan akumwambia mengi zaidi, alimwambia kuwa
mfuko alimshinda kuuwinua lakini tayari mtu
mwenyewe kaisha lala fo fo fo. Mkurugenzi
alipoambiwa vile, alitoka alipokuwa kwa ajili ya
kwenda katika chumba cha Jumanne, Suzan naye
alitoka jikoni na kwenda huko huko, wote wawili
walikutana kisha wakaambatana kuzipanda ngazi
kwenye kwenye Ghorofa waliokuwa wanalala akina
Jumanne. Wakiwa wote wawili waliingia ndani ya
Chumba cha Jumanne. Mkurugenzi alipoingia kweli
alimkuta Jumanne amelala fofofo kabisa, kwahio
kulikuwa na kazi moja tu ya kuiba mfuko.
Mkurugenzi yule naye akiwa amejiandaa kabisa
naye akijua lazima abebe lakini alishindwa.
Akajaribu mala nyingi nako akashindwa.
Akamuomba Suzan wasaidizane lakini pia
wakashindwa. Mkurugenzi yule akagundua kuwa
wachukue baadhi ya madini na kwenda nayo. Bila
kuogopa aliufungua mfuko kisha aliingiza mikono
yake kwenye mfuko wa madini kwa lengo la
kuyachota.
"Unafanya nini sasa?"
Sauti ya jumanne ilisikika masikioni mwao. Wote
kwa pamoja walishituka lakini walipoangalia Bado
Jumanne alikuwa amelala Fo fo fo, ajui kabisa kile
kilichokuwa kinaendelea. Walipoona hivyo wakazani
labda alikuwa anaota ndoto, hilo hawakujali
wakaendelea na Zoezi lao. Lakini mkurugenzi yule
kila alipokuwa anaingiza mkono kwenye mfuko Sauti
ya Jumanne ilisikika tena ikisema vile vile.
Hapo wasiwasi ukaanza kuwaingia wakashindwa
kuamini.
"Yuko macho lakini?"
Mkurugenzi aliuliza.
"Mbona Boss amelala kabisa yaani hata aoni wala
kupepesa macho!"
Suzan alisema.
"Ebu sogea umguse kwenye macho?"
Mkurugenzi alisema.
Hata bila uoga Suzan alisogea na kufanya kama
alivyoa agizwa, lakini aliambulia jibu lile lile kuwa
Jumanne hayuko macho na amelala usingizi wa
kubeba unatumbukiza kwenye dimbwi la maji halafu
unamtoa bado akiwa amesinzia.
"Sasa ni nini?"
"Hata Mimi nashindwa kuelewa!"
"Okey ebu Suzan Jaribu wewe Mwenyewe kuingiza
mikono yako kwenye mfuko huu labda kwako
inaweza isitokee"
Mkurugenzi alisema.
Suzan naye akafanya kama alivyo ambiwa akaingiza
mkono kwenye kigunia cha Madini.
"Jaman kwahio amuelewi?"
Sauti ilisikika tena.
Hapo kila mmoja akataka kutoka mbio. Lakini
walishindwa kuufungua mlango. Mlango ulikuwa
mgumu ghafra.
"Msikimbie bhna wala msiogope. Lakini naombeni
muufunge mfuko wangu kama mlivyo ukuta halafu
ndio we mkurugenzi utoke. Lakini Suzan abaki
humu ndani mpaka nitakapo amka usingizini"
Sauti ya Jumanne ilisikika tena msikioni Mwao.
Zoezi lilikuwa gumu ghafra. Mkurugenzi na Suzan
hawakuamini kabisa kama Jumanne anaongea
kwani walipokuwa wanamwangalia alikuwa atikisiki
wala mdomo kucheza ila Sauti tu
Mkurugenzi aliinama kwa kuogopa akaanza
kuufunga mfuko. Baada ya kumaliza Sauti tena
ilisikika ikimsemesha.
"Nimekueshimu kwasababu umetusaidia kuwatafuta
Wateja lakini rizika na ulichopewa, mbona hata
chenyewe ni kikubwa tu, kama ukiona akikutoshi
tukimaliza Biashara zetu unitafute nitakupa namna
ya kuyapata madini haya. Kwahio unaweza kwenda,
Suzan baki na Mimi kwanza bado nashida na wewe"
Sauti ya Jumanne ilisema.
"Naomba unisamehe sirudii kabisa"
Mkurugenzi ilimbidi aombe msamaha mwenyewe.
"Unaweza kuondoka tu tayari Mimi nishakusamehe
lakini nishakwambia na njia Rahisi ya kuvitafuta"
"Sawa"
Mkurugenzi aliitikia na kutoka.
"Ndani ya Chumba. Suzan alibaki, alikuwa anaogopa
sana.
" Njoo usogee hapa kitandani Suzan"
Sauti ilisema.
Huku akitetemeka kabisa Suzan alikisogelea
kitanda.
"Usiogope Suzan, wewe mbona hauna kosa kabisa
kwanza nakupenda, una moyo mzuuri wala hata
usijali. Mimi nakupenda ndio maana Nimeomba
ubaki"
Sauti ya Jumanne ile ile aliendelea kusikika
Masikioni mwa Suzan. Kilichokuwa kinashangaza
zaidi Sauti tu ndio ilikuwa inasikika lakini Jumanne
alikuwa amelala Fo fo fo. Yaani hata mdomo
ulikuwa uchezi kuashilia kama kweli Jumanne
alikuwa anaongea.
"Naomba tu unisamehe sirudii!"
Suzan alisema. Huku akipiga magoti.
"Suzan! Suzan! Usiombe msamaha nimeisha
kwambia kuwa hauna kosa kabisa. Wewe Subili
Mimi niamke tu hapa. Nakupenda"
Sauti ilisema tena.
Suzan alishindwa aseme nini tena ilimbidi ajipe
ujasiri wa kiuoga ili asubili kile ambacho kingefuata.
"Nisikilize Mimi ni Moyo wa Mwili huu, sasa bado
sijatosheka na penzi lako yaani kila nikikuona
napagawa kabisa. Naomba basi unipe tu penzi lako"
Sauti ilisema.
"Mh!"
Suzan aliguna. Alishindwa kuamini kile alichokisikia.
"Umenielewa Suzan?"
Sauti ilisema tena.
"Ndiyo!"
"Haya vua Nguo zako unipandilie hapa kitandani"
Sauti ilisema.
Suzan aliogopa Sana, moyoni akaanza kujilaumu
kwanini kathubutu kutamani kwenda kuzichukua
dhahabu za watu, kwanini kapenda kuingia kwenye
Chumba hicho.
Alizivua Nguo zake kwa uoga hivyo hivyo kwa
uwoga wake huku akitetemeka.
"Usiogope Suzan nakupenda"
Sauti ilisema tena ili kumjaza Suzan Iman.
Sauti kweli ilikuwa ya Jumanne lakini Mwili wa
Jumanne ulikuwa kitandani haujitambui kabisa,
usingizi mzito ulio sababishwa na Dawa ambayo
Suzan mwenyewe alimuwekea kwenye Chai ulikuwa
umemteka.
Kitandani Mwili ulikuwa kama Marehemu.
"Suzan, Fanya haraka Mimi Nina hamu tazama
muda unaenda"
Sauti ilisema tena.
Hapo Suzan akili zake zilimpeleka mbali sana,
akawaza Hadith ya mwandishi mmoja Tanzania
iliyokuwa inasema. Kuwa Nililala na Maiti 20
Mochwali ili niwe tajili. Kitendo cha kuuona mwili
wa Jumanne kitandani haujielewi aliufananisha na
Maiti ya Mochwali.
Kulikuwa Amna namna. kwakuwa alikuwa
akiyapenda maisha yake alijikuta anaupandilia mwili
wa Jumanne pale kitandani na kuufanya kama
inavyotakiwa kufanywa. Mwili ulikuwa haujitambui
uko tepetepe kama umelowa kabisa, Hauna hamasa
kabisa. Alijing'ang'aniza kujinyonga juu ya Mwili wa
Jumanne ili mradi tu ajione kama anafanya kitu.
"Suzan komaa unilidhishe Mimi bado kabisa
ujanifaidisha kabisa"
Sauti ilisema tena.
Suzan naye akazidi kujinyonga juu ya Mwili lakini
Kitendo chake yeye mwenyewe alikuwa akionei
manufaa yoyote kabisa. Zaidi alikuwa anachoka
mwenyewe tu.
Ailizidi kufanya hivyo ndani ya Dakika Ishirini Suzan
nguvu zilimuishia kabisa, akachoka mwili mzima
Ghafra akaanza kuhemea juu juu. Ndani ya kichwa
chake Fikira zikampeleka mbali kabisa kama yupo
ndani ya shimo kubwa la kutisha lililokuwa
limetanda Giza Nene halafu Sauti za ajabu ndizo
zilikuwa zinasikika masikioni mwake. Akapiga
kelele kuomba msaada huku anakimbia lakini kila
alipokuwa anakimbilia alikuwa apaelewi kabisa.
Alipokuwa anatoka alijiona kama ndiko anarudi,
zilikuwa ni Sauti za kutisha kweli kweli. Sauti hizo
zingine zilikuwa zinadai Roho yao.
"Tupe Roho yetu, tupe Roho yetu"
Sauti za ajabu hizo ziliendelea kumtesa Suzan.
Mwisho akajikuta ameanguka juu ya Mwili wa
Jumanne na kupoteza fahamu. Muda huo huo
Jumanne naye aliamka.
Alishangaa sana kuukuta mwili wa Suzan juu yake,
hata yeye mwenyewe alianza kuogopa, akautoa
mwili wa Suzan juu ya mwili wake naye akasimama
huku akiogopa sana.
"Usiogope Jumanne huyu kaisha kufa. Lakini wewe
hujamuua sisi ndiyo tumamuua kwasababu yeye ni
kafara yetu kutoka kwako"
Sauti ile ile tena ilisikika masikioni mwa Jumanne.
 
SEHEMU (08).
WhatsApp. 0755577488.
ILIPOISHIA.
Muda huo huo Jumanne naye aliamka.
Alishangaa sana kuukuta mwili wa Suzan juu yake,
hata yeye mwenyewe alianza kuogopa, akautoa
mwili wa Suzan juu ya mwili wake naye akasimama
huku akiogopa sana.
"Usiogope Jumanne huyu kaisha kufa. Lakini wewe
hujamuuwa sisi ndiyo tumamuuwa kwasababu yeye
ni kafara yetu kutoka kwako"
Sauti ile ile tena ilisikika masikioni mwa Jumanne
SONGA NAYO.
Jumanne alishituka sana, kuisikia Sauti hio ambayo
ilikuwa inafanana ya kwake.
"Kwani wewe ni nani?"
Jumanne aliuliza.
"Jumanne usijali bhana sisi ndio tuliowapa Mali
hizo. Huyu alikuwa anataka kukuibia kwahio Mimi
kama mlinzi wa Mali hizi mpaka pale mtakapo
zikabizi mikoni kwa wafanya biashara ambao
watakuja kesho kutwa"
Sauti ilisema tena.
"Sasa mbona uonekani?"
"Huwezi kuniona Mimi na usifikiri kuwa mko peke
yenu. hapana huwa tupo sisi tukiwangalia ninyi"
Sauti hio hio ilisema.
"Kwahio wewe ni jini?"
Jumanne aliuliza.
"Ndiyo"
"Kwanini unatumia Sauti yangu?"
"Ni kwasababu Niko na wewe"
Jini alisema.
"Sawa, Sasa na hii Maiti itakuwaje si nitakamatwa
kuwa nimeua?"
"Hapana Wala hata haitojulikana leo itajulikana ninyi
mkisha toka humu"
"Kwahio nitakaa nayo humu hivi hivi na wakati mtu
kaisha kufa?"
Jumanne aliuliza.
"Itakubidi tu ukae nayo humu kwasababu hakuna
namna, lakini usiwe na Shaka hakuna atakaye ingia
humu zaidi ya wewe wengine hawatoingia kabisa na
hawatagundua"
Sauti ilisema. Jumanne alishindwa kuongea tena
alijiona kama anaongezewa msala Mwingine juu ya
msala. Kuishi na Maiti ndani ya chumba tena
Hotelini ambako si nyumbani kwake.
"Jumanne hio itakuwa ni Adhabu yako, kwasababu
unataka kuondolewa mtihani mmoja wa kulala na
Dada yako, kwahio lazima uishi na Maiti hii halafu
utabadilishiwa Sharti la kulala na Dada yako"
Sauti ilisema tena.
"Kwahio nikiweza kabisa kuishi na Maiti
nitabadilishiwa Sharti langu la kulala na Dada
yangu?"
"Ndiyo lakini Sharti la kuleta natiti mawili ya
wanawake kila baada ya miezi mitatu lazima
ulitekeleze"
"Sawa kama ni hivyo nitaishi nayo kwa muda huu"
Jumanne alisema.
"Sawa kwahio unaweza kuendelea na mambo yako"
Sauti ile ilisema.
Toka hapo haikusikika sauti tena. chumbani alibaki
Jumanne na Maiti ya Suzan. Bint mzuuri ambaye
kafa kifo cha kishetani kabisa kisa mali, kisa kupata
utajili kwa kushawishika na Meneja wa Hoteli.
Jumanne aliogopa sana kuiangalia Maiti ya Suzan
ambayo ilikuwa kitandani kwake, alifikilia mengi
sana kichwani mwake.
"Daah! Kama ni kuteseka basi ndiko huku, kuishi
tena na Maiti ndani ya chumba kwa siku mbili,
inamaana nitalala nayo kitandani. Mungu wangu,
sijui itakuwaje?"
Jumanne alijisemea.
Muda huo tayari Masaa yalikuwa yashaenda sana,
tayari ilikuwa ishatimu mida ya saa sita na dakika
47 yaani Saa saba kasoro dakika kumi na tatu.
"Ngo! ngo! ngo!"
Mlango uligongwa kwa nguvu.
Jumanne ndani alishituka sana, akajikuta anaanza
kutapatapa. Akachukua shuka haraka na kuifunika
shuka Maiti ya Suzan. Kisha akarudi mlangoni
ambako bado mgongaji alikuwa akiendelea
kugonga.
"Nani?"
Jumanne aliuliza.
"Jumanne mbona leo hutoki wewe, mpaka
tumeanza kuwa na wasiwasi tukafikili labda
ushajiuwa"
Sauti ya inje ilisikika. Haikuwa ya Mwingine Bali
ilikuwa ni sauti ya Rafiki yake Mgusi.
"Nakuja bhana ngoja nioge kwanza"
Jumanne alisema.
"Sawa Fanya haraka Mimi nakusubili hapa hapa
mlangoni"
Mgusi alisema.
Jumanne alioga haraka, alitumia dakika sita akawa
amemaliza, alijimwagia maji tu,Kisha akatoka bafuni
akazivaa Nguo zake na kutoka inje ya chumba
chake hakusahau kuufunga mlango wa Chumba
chake kisha akamfuata Rafiki yake kule alipokuwa
anaelekea.
"Walikwenda tena juu ya Hoteli hio, huko ndiko
wenzake walikuwa wamekaa wakipanga mipango ya
jinsi watakavyo tumia pesa zao endapo wakiuza
madini.
"Jumanne Mtoto alikulewesha nini?"
Faustin alisema baada ya kumuona Jumanne akifika
maeneo hayo"
"Jamani Mimi mwenzenu siko vizuri kabisa"
Jumanne alisema.
"Khaaah! Jumanne auko vizuri wakati sisi kipindi
tunatoka vyumbani kwetu Mimi nilipita kwenye
chumba chako kutaka kukwambia tutoke
nikashindwa, kwasababu nimesikia kama
purukushani na sauti za mtoto. Na sikuishia hapo
nimechungulia kwenye tundu la kuingizia funguo
mlangoni nimekuona na mtoto bhna. Lakini poa
kwasababu Jana ukufanikiwa amna noma"
Faustin alisema tena.
"Ni kweli Mtoto nilikuwa naye lakini mambo
yamenigeuka tena. Yaani nazidi kuishi kwa wasiwasi
sana siamini kinachoendelea maisha mwangu nini?"
"A aahaa! Nini kwani tena Jumanne?"
Mgusi alikuwa wa kwanza kuuliza.
"Twambie bhna tujue namna ya kusaidia"
Manyege alisema.
"Yule muudumu aliye niletea Chai alipoingia tu Mimi
nikapenda, sikuwa tena na haja ya kunywa chai zaidi
Mimi nilitaka tu penzi lake"
"Ni kweli nilikuona. Twambie nini sasa ambacho
kimekukuta?"
Faustin aliingilia mazungumzo ya Jumanne.
"Ebu Faustin tulia kwanza tumsikilize Mwenzetu"
Mgusi alisema.
"Basi hata yeye hakukataa. Hapo nikajikuta
nimezama kwenye penzi la Mtoto. Nilipomaliza
nikanywa Chai, lakini sikujua ni nini kilinikuta
nikalala kitandani. Uwezi amini nimeamka usingizini
nikakuta mwili wa yule Bint umenilalia na uko
mtupu kabisa. Sijui alikuwa anafanya nini juu ya
mwili wangu?"
"Jumanne unauliza alikuwa anafanya nini, alikuwa
anakupa Mapenzi!"
Faustin alisema tena.
"Sio hivyo tu, Faustin ni kwamba yule Bint alikuwa
amekufa"
"Oommmh! What?!!"
"Unasema umemkuta amekufa?!!"
"Kawaje?!!"
Wote watatu waliuliza kwa mshituko kweli kweli.
"Ndiyo hivyo! Hata Mimi siamini kabisa!"
Jumanne alisema.
"Sasa tutafanyaje? tayari hio ni kesi na tumeanza
kupata mikosi sasa"
Manyege alisema.
"Ni kweli kabisa"
"Ndiyo, mikosi hio"
Mgusi na Faustin walisema.
"Lakini mala nilisikia sauti ambayo inalandana
kabisa na ya kwangu ikinisemesha. Sauti hio Mimi
ilinishangaza sana, nikauliza wewe ni nani mbona
sikuoni? Yenyewe ikanijibu kuwa. Nisiogope yeye
nimlinzi wetu. Kumbe hapa tulipo hatupo peke yetu
Bali kuna mlinzi analinda Mali zetu, mpaka tutakapo
ziuza. Kumbe yule Bint kufa ni kwasababu alikuwa
anataka kunibia"
"Unasema je, kwahio kutaka kuiba ndiyo kafa?"
Manyege aliuliza.
"Ndiyo hivyo ndugu zangu"
Jumanne alisema. Tena alikuwa wanazungumza kwa
mashaka kweli.
"Sasa hio Maiti tutafanyaje kuitoa ndani ya hotel ya
watu kabla hajagundua kwasababu wakijua kama
muhudumu wao kauawa. Mmmh! sijue itakuwaje?"
Mgusi alisema.
"Yule Jini! mlinzi wa Mali zetu kanambia
hawatoweza kujua mpaka sisi tuondoke ndani ya
Hoteli hii"
"Duuh! Aisee Mimi nilikuwa nishaanza kutafakari
jinsi ya kutoroka!"
Faustin alisema.
"Sasa kuusu Hio Maiti itakuwaje hawo majini
wataondoka nayo?"
Mgusi alisema.
"Hapo napo kuna mtihani, lakini kanambia niishi
nayo mpaka pale nitakapo toka humu. Na hio ni
kwasababu ya kuwa Mimi nitabadilishiwa ile kafara
ya kulala na Dada yangu. Mama yake Fatuma"
Jumanne alisema.
"Safi tu kama mambo ndio hayo hakuna haja ya
kuwa na wasiwasi maana kila kitu kiko safi"
Faustin alisema.
"Faustin ebu tusichukulie juu juu kama hivyo, hapa
tupo ndani ya hotel na aliyekufa ni mfanya kazi wa
Hotel hii"
Manyege alisema.
"Ni kweli lakini naomba tuwaamini hawa majini
kwasababu wao ndiyo tunawafanyia wao kuwapa
kafara. Sasa cha kufanya tutulie hata wao hawawezi
kutufanya kuishi kwa wasiwasi. Hilo ni jambo
ambalo wamelifaya wao wala sio sisi kwahio
tusiwaze hio kesi kwetu haipo"
Mgusi alisema.
Kidogo maneno ya mgusi yaliwafanya wawe kidogo
wenye Furaha.
"Ni kweli kabisa kwasababu hata sauti hio ilisema
kuwa siyo Mimi niliyefanya Bali ni wao"
Jumanne alisema.
"Umeona kwahio msiwaze"
Mgusi alisema.
Waliendelea kuongea mambo mengine mpaka
inafika muda wa saa nane ndio waliona kuwa ni
wakati muafaka wa kwenda kupata chakula.
Walishuka kula. Baada ya kumaliza kula walirudi
vumba mwao kuiga tena, hapo wakikuwa
wanampango wa kutoka ndani ya hotel ile.
Baada ya kumakiza usafi wa mwili walihakikisha
milango ya vyumba vyao vimefungwa kikamilifu
kisha wakatoka na kwenda kutembea tembea ndani
ya mitaa ya Jiji hilo la mwanza. Walitembea huku
wakiwatazama Mabint walembo wa kujirusha nao.
Kwao sitarehe ndiyo ilikuwa kipaumbele.
Walitembea ndani ya Jiji hilo mpaka mida ya saa
kumi na mbili ndiyo wakarudi hotelini.
Walikaa eneo la ukumbi wa starehe wa Hoteli hio
huku wakinywa vinywaji. Muda wa saa mbili za
usiku kipindi wanakula, Taarifa ya habari alianza
kusomwa. Muhitasari wa habari hio uliwasitusha
sana, kwani msomaji alisema kuwa.
"" Maiti yakutwa mapangoni wilayani Ukelewe"
Maiti ya mtu iliyoneshwa haikutambulika, hapo
ndipo kila mmoja alitamani taarifa hio isomwe kwa
urefu ili apate kuona inamuusu nani.
Baada ya muhitasari matangazo ya wadhamini
kupita taarifa ikaanza kusomwa kwa urefu.
Taarifa ya Pili ilikuwa ni hio ya Maiti kukutwa
mapangoni wialayani Ukelewe.
Msomajia wa Habari aliisoma kwa ufasaha kisha
akamwachia Ripoter ailipoti kwa kina. Kumbe
haikuwa Maiti ya Mwingine Bali ya Said Rafiki yao
kipenzi ambaye alikufa kifo kibaya kwa
kucharangwa na Jini baada ya kwenda kinyume na
ilivyotakiwa.
Kila mmoja katika kikundi kile alisikitika sana,
waliogopa hata wao walipo uona mwili wa Said
kupitia television, hapo kila mmoja akajiapia
kupambana kwa nguvu zote kwa ajili ya kukamilisha
maswala ya kuzitoa kafara zao.
Usiku huo ulipita kwa mawazo sana kwa watu wale
ambao tayari walikuwa washabaki wanne tu.
Kwa wengine ilikuwa ni maumivu ya kuuona mwili
wa Said basi, lakini kwa Jumanne yeye ilimrudisha
tena Nyuma, akajikuta anawaza mala mbili, kulala
na Maiti ndani ya chumba, halafu tena Maiti ya Said
ilikuwa kama inamuhijia usoni mwake. Kitandani
Jumanne akashindwa kulala akakaa. Mwili wa
Suzan ulikuwa upo juu ya kitanda chake. Jumanne
alikuwa anawaza sana, alitamani usiku uche afadhali
angekaa kidogo kwa unafuu kwa kuongea na
marafiki zake. Usiku nao ulikuwa mrefu kwa
Jumanne akaanza kuomba na Dua kwa mungu.
Hapo shetani alimkumbuka mungua akasahau
dhambi kabisa. Jumanne aliomba mungu amlinde
badala ya kutubia dhambi zake alizozifanya. Mida ya
saa tisa za usiku ndio muda ambao Jumanne
kidogo usingizi ulianza kumvaa na kulala.
"Ngo ngo ngo ngo!"
Mlango wa Jumanne ulikuwa unagongwa na
wenzake kumwamsha. Tayari kulikuwa kumeisha
kucha.
Jumanne aliamka, kwanza alienda bafuni kuoga
kisha akatoka akavaa nguo zake kisha akatoka inje
ya chumba chake. mlangoni alikutana na
muhudumu Mwingine anakuja kumletea Chakula.
 
Sehemu..........(09).
ILIPOISHIA.
Hapo shetani alimkumbuka mungua akasahau
dhambi kabisa. Jumanne aliomba mungu amlinde
badala ya kutubia dhambi zake alizozifanya. Mida ya
saa tisa za usiku ndio muda ambao Jumanne
kidogo usingizi ulianza kumvaa na kulala.
"Ngo ngo ngo ngo!"
Mlango wa Jumanne ulikuwa unagongwa na
wenzake kumwamsha. Tayari kulikuwa kumeisha
kucha.
Jumanne aliamka, kwanza alienda bafuni kuoga
kisha akatoka akavaa nguo zake kisha akatoka inje
ya chumba chake. mlangoni alikutana na
muhudumu Mwingine anakuja kumletea Chakula cha
asubuhi.
SONGA NAYO.
Jumanne alishituka sana, mapigo ya moyo
yakamwenda mbio. Akajua hapo ndipo anaenda
kuumbuka.
"Wewe ndiye uliye gonga mlango?"
Jumanne alimuuliza muhudumu.
"Hapana, sijagonga lakini nimemkuta kaka wa
Chumba hiki akiwa amesimama hapa. Na kaniambia
nikusubilie utoke nikukabizi chakula ndani nisiingie"
Muhudumu alisema.
Hapo Jumanne akajua kumbe Alikuwa Mgusi ndiye
aliyekuwa anagonga mlango. Kwani hata hivyo
alimsikia yeye lakini alishangaa kukuta muhudumu
wa hotel ndiye yuko mlangoni kwake.
Jumanne alikichukua chakula akaingia ndani ya
Chumba chake kisha akaufunga tena mlango,
muhudumu yule hakupata kuchungulia ndani ya
Chumba cha Jumanne.
Jumanne alirudi chumbani kwake akakila chakula
chake. Hata muda muhudumu aliporudi Jamanne
alianza kwa kuuliza ni nani kisha akatoka na
vyombo inje na kumkabizi. Hivyo tu ndio ilikuwa
njia ya kuficha asigundulike kuwa ndani ya Chumba
chake kuna Maiti imelala kitandani.
Mchana wa siku hio hawakukaa chumbani, waliamua
kuwa wanakaa katika ukumbi wa chakula na
vinywaji katika Hotel hio. Usiku navyo ilikuwa hivyo
hivyo. Kesho asubuhi mapema kabisa saa moja na
nusu, wote walikuwa washaamka wameoga na
wamekaa kwenye chumba cha Mgusi wote. Hapo
walikuwa wakingoja matajili wa madini waje wapate
kuuza mzigo wao wa madini. Hapo tayari walikuwa
washatoa taarifa katika uongozi wa Hoteli kuwa hata
Chai wawapelekee katika chumba hicho.
******
Mida ya saa tano na dakika kama 12 ndio muda
ambao wafanya biashara wa madini walifika.
Ukumbi wa mikutano uliokuwa juu kabisa ya Hoteli
ile ulikuwa ushaandaliwa kwa ajili ya wageni
walikuwa wa kizungu. Kwa siku hio ndani ya Hoteli
hio hawakuruhusiwa kuingia wageni wengine zaidi
ya waliokuwemo tu. Hoteli mzima ilikuwa
imewekwa Chini ya ugeni ulio ingia. Ulikuwa ni
ugeni wa nguvu, sehemu ya parking ya magari
magari ya kifahari ndio yalipanga pale. Yalikuwa ni
magari zaidi ya kumi. Walioshuka mule walikuwa ni
wazungu kama Tisa wengine wote walikuwa ni
wenzetu. Kipindi wageni wale waliingia ndani ya
Hotel Jumanne na wenzake walikuwa ndani
wakichungulia Dirishani.
"Daah! Noma. Mmh! Namimi nikipata Gari kama
hio nitaishi kama Dunia ni yangu peke yangu"
Faustin alisema huku akisota gari Aina ya Range
Rover Spot lililokuwa miongoni mwa magari ya
Billionaires waliokuwa wamekuja kufanya nao
biashara.
"Duuh! Kweli ni Gari hivi kweli si ni bei kabisa
kuinunua gari hio?"
Manyege alisema.
Bado wakiwa wamezubaa huku ndani ya Chumba
cha mgusi wote wanne mlango uligongwa.
Mgusi akaenda kuufungua.
Alikutana na Mwanaume aliyekuwa amevalia vizuri
kabisa. Toka wafike hapo walikuwa hawajawahi
kukutana naye.
"Naombeni mnifuate.
"Msichukue Chochote na kama mnafunga milango
yenu fungeni"
Mwanaume yule alisema.
"Samahani Unaweza kutwambia wewe ni nani?"
Mimi ninaitwa Sajeti massalu pia ni mmoja wa
wakuruganzi katika Hoteli hii. Nimekuja kulisimamia
zoezi lenu"
Mwanaume yule alisema.
"Kwahio wewe ni polisi?"
"Ndiyo Mimi ni afisa wa police. Nimekuja badala ya
mkurugenzi aliyewapokea yeye kwa leo hayupo ni
Mgonjwa"
"Sawa, sasa tunaenda wapi?"
Jumanne aliuliza. Muda huu alipata ujasiri wa
kuuliza kwasababu alikuwa kaisha pata hamasa na
hamu ya kupata mapesa.
"Naombeni mnifuate na mjitahidi kufanya haraka"
Afisa police yule alisema.
Wote kwa pamoja walipelekwa chumba kizuuri
kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili yao. Huko
waliwakuta Mabint wanne. Mule ndani ya chumba
kulikuwa na Nguo, Suti na viatu vyote vya nguvu
vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yao.
"Jamani nazani asubuhi mmeoga na kwakuwa
tumeisha chelewa mtavaa hivyo hivyo hizo Nguo
harafu mifuko yenu kuna watu watakuja kuwabebea
na kuwapandishia juu ya hoteli, ninyi tayari
mshakuwa matajili"
Mkurugenzi huyo mpya kabisa alisema.
Zoeli lililokuwa linafuata ni akina Jumanne kuvaa
zile Nguo na suti safi kabisa za kupendeza suti za
bei mbaya, viatu vyenyewe vilikuwa vinang'aa kama
nini. Kila mmoja alikuwa anajiona kwenye kiatu
chake kama kioo ingawaje vilikuwa vyeusi.
Walipambwa vizuri na wale akina Dada safi kabisa.
Kweli walipendeza muda huo wakajiweka katika
Group la watu wenye miela yao, watu wenye
mapesa.
"Hapa mmh! Anambii mtu, nilivyo ng'aa hivi.
Siamini eti!"
Manyege alisema baada ya kukamilika.
"Ndugu yangu, ni kweli asikwambie mtu haya ndio
maisha baba, haya ndiyo maisha naonekana kama
wale jamaa walioingia na magari yao"
Faustin alisema.
Mgusi na Jumanne wao walikuwa wanaangalia
wenzao huku wakicheka na kufurahi tu.
"Sasa si tayari?"
Mkurugenzi aliuliza.
"Ndiyo mh. Tunaweza kuendelea na vitu vingine"
Majura alisema.
"Sasa twendeni mkafungue milango yenu kuna watu
wakubeba mizigo yenu ili ipandishwe juu kwa
matajili"
"Sawa lakini mifuko yetu yote imo ndani ya Chumba
kimoja kwahio twende wakasaidie ikabebwe"
Mgusi alisema kisha wakaongoza wote wanne na
mkurugenzi kutoka kwenye Chumba walivyokuwa
wanafanyiwa make up. Walisogea kwenye vyumba
vyao kwa ajili ya kwenda kuyachukua madini yao.
Walipofika hapo waliwakuta wanaume wanne nao
pia wamevaa vizuri tu, halafu wamesimama katika
kila Chumba wakingoja milango ifunguliwe waingie
wayachukie madini kisha wapandishe juu kwenye
kikao cha Biashara.
"Mizigo yote imo kwenye chumba hiki"
Mgusi alisema huku akiufungua mlango wa Chumba
chake.
Wale wanaume wengine waliingia na kubeba mizigo
kisha wakaongozana wote kupanda juu kwa ajili ya
Biashara.
Wakerewe wale walikuwa hawana kabisa wasiwasi
kwasababu walikuwa washaambiwa na Mashetani
yao kuwa hawatadhurumiwa hata kuibiwa chochote,
hicho kiliwaondoa wasiwasi sana.
Baada ya dakika kadhaa za kuzipandisha ngazi za
kwenda juu ya ukumbi uliokuwa juu kabisa ya Hoteli
hiyo, hatimaye walifika. Juu huko palikuwa
pamepambwa hatari ulinzi ukiwa umetawala kila
sehemu hiyo. Ingawaje zoezi lile lilikuwa la siri
lakini pia ulinzi kwa Chini nao ulikuwepo.
Waliokuwa wanaijua ishu hio ni baadhi ya watu
wachache.
Sehemu ya kukaa wao pamoja na pakuweka madini
yao ilikuwepo. Kulikuwa na vyombo vikubwa kabisa
vilivyokuwa vimewekwa kwa ajili ya kuyamwaga
mule ili iwe vyepesi kuonekana kwenye macho ya
matajili wale kutoka Inchi zilizo endelea. Kila mfuko
ulimiminwa kwenye chombo chake kilichokuwa
kimefungiwa mzani kabisa.
Kipindi madini Yale yanamiminwa matajili wale
walikuwa wanatikisa vichwa kuashilia kweli
wameangukia sehemu ambayo wanaweza kuzitoa
pesa zao zoote.
Katika madini waliyokuwa nayo, mfuko wa Jumanne
ulikuwa na uzani kama kilo 48 mifuko za wengine
zilikuwa na 37 na point kadhaa. Huwezi amini
walizidiana kwa point tu kitu ambacho kilikuwa
akileti utata.
Ingawaje wafanya biashara wale wa madini
walikuwa wachache lakini walikuwa ni Raia wa ichi
za marekani na mataifa ya ulaya kama uingeleza,
ujerumani pamoja na Urusi.
Hio ni kwa mujibu ya utambulisho wao. Wengi
walikuwa aelewi Lugha ya kiswahili lakini walikuwa
wamevaa vifaa maalumu masikioni mwao kwa ajili
ya kutafasili maneno ya Lugha ya kiswahili
kuyapeleka katika Lugha zao.
Baada ya kumaliza kujitambulisha zoezi lilofuata
lilikuwa la makubaliyano ya bei.
Kwa jinsi Walivyokuwa wanayatazama madini yale
mbele yao, kila mmoja alikuwa alikuwa anatamka
bei yake.
"Ningependa ya kiasi kama dola. 50000$"
Mmoja katika wale matajili alisema. Dola 50000 ni
zaidi ya milioni miamoja za kitanzania.
"Mimi ningependa nipewe ya kiasi cha Dola 70000"
Ambazo ni Zaidi ya Sh milioni miamoja sabini.
Matajili wale walizidi kugandana kwa Bei ya pesa
kila mmoja alitaka achukue mzigo wa kutosha.
Mpaka ilifikia Mwisho kwa makubaliano ya
kugawana mizigo ilimradi kila mmoja apate.
Kwa ujumla wa kifedha ambazo Timu ile ilipata kila
mmoja kama hivi.
Jumanne aliambiwa atapewa kiasi cha Dola.
500000$ ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni moja za
kitanzania.
Wengine walipata kiasi cha dola 360,000$ ambazo
ni zaidi ya milioni mia saba za kitanzania.
Zilikuwa ni pesa nyingi kweli kweli. Faustin
hakuamini Kabisa kiasi kile cha pesa kiasi ambacho
kwakweli ni kikubwa hasa. Dola 360000$ ni kiasi
kikubwa kwa maisha ya mtanzania.
Pesa zao watazipata vipi. "Mna bank account?"
Waliulizwa.
Yaani kwa wale wote walidai wanazo.
Pale zoezi lilifuata lilikuwa ni kuwaingizia pesa zao
kwenye Account zao za Bank ya CRDB, kwa njia
mtandao. Account zao zilijaa pesa. Pesa ambazo
walikuwa katika maisha yao hawakuwa kuziwaza.
Jumanne kiushika Bilioni na mamilioni kadhaa
katika pesa yake. Alisahau kabisa kama kaitoa
kafara ya mtoto wa Dada yake.
Siku hio kwao iliisha kwa Furaha sana. Wale
matajili walikabiziwa madini yao wakaondoka zao
hawakulala hata ndani ya Hoteli hio. Muda wa saa
kumi Jumanne na wenzake wote walikutana huko
huko juu ya Hoteli wakajadili mipango ya pesa yao
ndefu ambayo wemeivuna, pesa ya shetani pesa
ambayo ni laana.
Siku hio kwao ilikuwa ya Furaha sana.
Baada ya kuivuna mipesa yao siku iliyofuata
waliondoka ndani ya mwanza hoteli, na kurudi
Ukerewe. Kama Jumanne alivyokuwa ameahidiwa na
sauti ya Jini kweli taarifa za kifo cha Suzan
akuzisikia wala kuulizwa ingawaje Maiti waliicha
ndani ya Hoteli. Wafanya kazi wa Hoteli ile waliitoa
tena kwa madai ya kwamba alikufa kwa sumu
ambayo alikunywa yeye baada ya kwenda Katika
chumba hicho kufanya usafi. Hakuna aliyepingana
na Maelezo hayo ingawaje yalikuwa ni uongo
mkubwa.
******
Baada ya miezi miwili tangu wavune mipesa
walikuwa tayari washajenga majumba makubwa
ndani ya Ukelewe, tena waliamishia makazi yao
Nansio. Majumba yao yote yalikuwa yamewagarimu
dola 46000$ zaidi ya Shilingi milioni miamoja.
Zilikuwa ni mijengo ya maana. Hawakuishia kwenye
majumba tu, walikuwa na magari ya bei mbaya,
Jumanne alikuwa na Gari mbili ambazo zote
alizinunua kwa milioni 80 moja kwa milioni amsini
na nyingine kwa milioni 30. Wengine nao walifanya
hivyo hivyo katika Gari la milioni amsini na mengine
walikuwa wamenunua nagari ya Milioni 25. Magari
yao ya milioni amsini yalifanana yalikuwa ni aina
ya..........
watu wale wachafu hawakuishia kwenye magari na
majumba, walishilikiana na kuijenga Hoteli kubwa
ya Ghorofa mbili ndani ya Nansio Ukelewe. Hoteli
hio iliwagarimu kiasi cha pesa kama milioni 500 za
kitanzania, kiasi ambacho walijichanga milioni mia
mia kwa wengine watatu, Jumanne yeye alijitolea
kiasi cha Shilingi milioni mia mbili.
Hawakuishia hapo, waliamua kuzijenga Guest house
mbili mbili kila mmoja. Guest hizo ziliwagarimu
milioni amsini amsini. Guest hizo zilisambaa ndani
ya ukerewe, Jumla zilikuwa nane na zilijengwa;
mrutunguru, kazilakanda, muhande, maande,
bugunza Bugorola, kurwego na moja Nansio pale
pale.
Cha ajabu zaidi, Nyumba zao na Guest zote zilikuwa
na chumba maalumu ambacho kilikuwa na Shimo
leefu kabisa. Urefu wa mashimo yalikuwa na urefu
zaidi ya mita 50 kwenda Chini.
Kila mmoja alijenga nyumba kubwa nyumbani kwa
wazazi wao. Baada ya kumaliza walinunua Piki piki
za Boda boda Zaidi ya mia mbili, kuzinunua
walijichanga kila mmoja milioni mia moja. Pikipiki
hizo walizisambaza kwa vijana katika maeneo
waliyokuwa wamezijenga Guest zao, huo ulikuwa
mradi wao wa Pili mbali na Hoteli ambayo
ilisimamishwa Nansio.
 
SEHEMU...........(10)
ILIPOISHIA.
cha ajabu zaidi, kila Guest ilikuwa na chumba
maalumu ambacho kilikuwa na Shimo leefu kabisa.
Kila mmoja alijenga nyumba kubwa nyumbani kwao
kwa wazazi wao. Baada ya kumaliza walinunua Piki
piki za Boda boda. Kama mia mbili piki ambazo
wao walijichanga kila mmoja milioni mia moja,
wakazisambaza katika vijana ndani ya Ukelewe huo
ulikuwa mradi wao wa Pili mbali na Hoteli ambayo
ilisimamishwa Nansio.
SONGA NAYO.
"baada ya kuahkikisha kuwa wamekamilisha
maswala yao, Jumanne alimtembelea Dada yake,
huko alifika kumdanganya Dada yake kuwa
alimpeleka Fatuma Afrika kusini kusomea huko.
Taarifa hizo Dada mtu alizipokea kwa Furaha sana.
Hakuamini hata mumewe naye alizipokea na
kumsifu shemeji yake kwa maamuzi mazuuri
aliyoyafanya. Mungu wangu hawakujua tu lakini
wangejua kuwa Mali ambazo Jumanne anamiliki ni
kwasababu ya Bint yao hata wasingefurahi.
" Sasa Dada yangu na Shemeji nataka niwape mtaji
mjifungulie mradi wenu, nataka niwape milioni
ishirini si itawatosha?"
Jumanne aliuliza.
"Ni kweli kaka inatosha"
Dada alisema.
"Na nampango wa kuwajengea nyumba hapa katika
mji wenu huu"
Jumanne alisema.
Bado tu waliona ni jambo la Furaha kwao kabisa.
Jumanne alikaa nyumbani kwa Dada yake kama
siku mbili tu, muda huo alihakikisha kila kitu kuusu
ujenzi wa Nyumba ya Dada yake na Mumewe
pamoja na watoto wake wawili uwe umeanza
aliacha wanaanza kufyatua tofali na Ramani kabisa
ya Nyumba ishachorwa ilikuwa ni nyumba kubwa
ambayo itamgarimu Jumanne kiasi kama cha
milioni 30.
Baada ya kutoka kwa Dada yake alirudi Nyumbani
Nansio.
Wakiwa Nansio wote wanaume wale wanne
walikutana ndani ya Jengo zuuri na la kisasa kabisa
la Hoteli yao. Hotel ile ilikuwa imekamilika lakini
bado ilikuwa ijazinduliwa kwa ajili ya kuanza
kutumika. Mpaka hapo kila kitu kilikuwa kimo ndani
ya Hoteli yao na jina lake waliipa Jina la NANSIO
HOTEL.
"jaman tumeitana hapa kwasababu siku ambazo
zinatakiwa kuyapeleka maziwa ya wanawake
umekaribia bado wiki tu"
Jumanne alisema huyu ndiye alikuwa kachaguliwa
kama kiongozi wa kikundi hicho.
"Nazani hili halina shaka. Malaya wamejaa ndani ya
Ukerewe humu"
Manyege alisema.
"Si humu tu hata Mwanza kule yapo mengi tunasafiri
tu halafu tunaenda kuuchukua. Mimi ninalo Malaya
moja lipo mwanza hapo, niliahidi kulianzia lenyewe,
liko pale mwanza Hoteli lile lidada la Mapokezi pale
Mwanza Hoteli"
Faustin alisema. Alikuwa anamzungumzia Loveness.
Tayari Loveness naye aliingizwa kwenye Orodha ya
kufa.
"Mi pia lipo Namba zake za simu ninazo kwahio ni
kuagiza tu yanakuja yenyewe kisha kazi inaisha"
Mgusi naye alisema.
Mi sina sasa itakuwaje?"
Jumanne aliuliza.
"Usijali Jumanne Mimi lipo limalaya langu huko
huko mwanza lenyewe lina Rafiki yake naye ni
moto. Hayo tutayaomba yaje yoote.
Manyege alisema.
Hapo wote walikubaliana. Kwahiyo hali ya kuwaza
kuusu wanawake wa kwanza kabisa kukatwa
maziwa yao kwa ajili ya kafara iliisha.
"Nimepata wazo!"
Mgusi alisema.
"Wazo gani hilo mgusi?"
Jumanne aliuliza.
"Wazo langu ni kwamba kuusu wanawake wa
kuwatowa kafara tutakuwa tunachukua Namba za
Malaya ambao tutakuwa tunalala nao. Hata hao
wake za watu, Lakini wakutoa kafara wote tutakuwa
tunawatoa mbali, kama Ukara, kule Sizu. Hata
Bunda huko tunasafiri kwa ajili ya kuyatafuta.
Tukilitoa la mbali huko ni vigumu kujulikana"
Mgusi alisema.
"Wazo zuri Sana"
Jumanne alisema.
"Jamani nazani hilo halina Shaka hata humu humu
Ukerewe mbona Malaya wako wengi tu, tumejenga
Guest zetu nyingi na tumeweka mashimo marefu
kabisa kwa ajili ya kutupiamo miili ya tutakao kuwa
tunawaua. Kwahio sizani kama kuna kuogopa.
Ukifika Muda wa kutoa kafara tunasafiri mpaka
kwenye Hizo Guest huko lazima tupate manamke
mengi tu. Pesa tunazo za kutosha"
Faustini alisema.
"Ni kweli jamani sizani kama hapo kuna ubishi
ndani yake. Guest zitakuwa zinatuingizia pesa, tena
uzuri kila ya Guest tutaweka Baa ya kueleweka na
mziki mzito"
Jumanne alisema.
Hapo kila mmoja akakubaliana naye.
"Sasa mwenyekiti vipi kuusu wewe ile ishu ya Dada
yako ushabadilishiwa?"
Manyege aliuliza.
"Bado na labda tukipereka kafara yetu tutaulizia"
Jumanne alisema.
Akawakumbusha wenzake kuusu kuwafukuza wake
zao. Mpaka Muda huo kila mmoja bado alikuwa
anakaa na Mke wake bado walikuwa
hawajawafukuza.
"Daah! Tunashukuru sana kwa kutukumbusha tena
Mimi leo hii nafika namfukuza halafu nalichukua
limke la mtu moja usiku wa Leo nalianzia"
Faustin alisema.
Baada ya Faustin kusema hivyo wote kwa pamoja
walisem lazima wakifika ni kuwapa wake Zao taraka
kilichokuwa vichani mwao ni kulala na wake za
watu, pamoja na kulala na Dada zao kwa ajili
kuwapa mimba ya mtoto wa shetani.
Waliamaliza kikao, Lakini kabla hawajaondoka,
alitokea Mwanamke mzuuri mbele yao. Kila mmoja
alishituka kumuona mwanamke yule.
"Bado hamja nizoea tu?"
Mwanamke yule aliuliza.
"Tumeisha kuzoea lakini jinsi ulivyotokea ndio
maana tumeshituka"
Jumanne alisema.
"Vizuri sana. Leo ilikuwa ni mala ya Mwisho sisi
kuwa na ninyi hakutokuwepo tena ulinzi juu yenu
kutoka kwetu, kikubwa mnatakiwa kuwa makini
katika mambo yenu yote.
Hicho ni cha kwanza, Cha Pili Jumanne badala ya
kulala na Dada yako, tunataka tu umuuwe mumewe.
Utamuuwa kwa kumchinja na Damu yake uichukue
uje nayo, halafu Uandae chumba maalumu ambacho
kitakuwa ni maalumu kwa ajili yetu na wewe,
chumba hicho ikipambe kwa vitambaa vyekundu.
Kisha damu hiyo utaiweka kwenye chombo maalum
cha wazi halafu utaiweka ndani ya icho chumba.
Itakuwa ni zawadi kwetu.
Cha mwisho tunaomba msisahau agizo lolote
ambalo tuliwapa. Nazani nimeeleweka.
Baada ya kusema maneno hayo Mwanamke yule wa
kijini alipotea, alikuwa ni yule yule aliye mcharanga
Said baada ya kugoma kuusu kuwachinja wanawake
na kuwatoa maziwa yao kisha kuyapeleka kwa hayo
mashetani.
Wote walibaki vinywa wazi kwa muda wa sekunde
kadhaa.
" hiyo nzuri kumuuwa yule fara tu"
Faustin alisema.
"Kweli hiyo ni nyepesi ndugu yangu, maana ile ya
Dada yako ilikuwa ni hatari tupu"
Marafiki zake walisema.
Lakini Jumanne kidogo alibaki kimya bila kusema.
"Vipi Jumanne mbona unakuwa na Shaka katika
swala Jepesi kiasi hicho"
"Hapana yule Shemeji alinisaidia sana katika maisha
yangu mpaka kufika hapa labda hata ningekuwa
nishakufa. Alinisaidia siku moja tuko kijiweni Mimi
na yeye na jamaa zangu. Ghafla ulizuka Ogomvi
kidogo nichomwe kisu, cha Tumbo huwezi amini
aliudaka mkono wa mchomaji kisha akampiga teke
na kuanguka huko. Hiyo ni ndogo aliwahi kujitolea
pesa yake mfukoni kwa ajili yangu Mimi niliugua
karibu kufa. Hakukuwa na msaada kabisa wazazi
wangu walikuwa hawana la kufanya, alichukua pesa
yake ya mafao ya Baba yake yote ilikuwa kama
milioni mbili akajitolea kwenda kunitibisha
muhimbili. Namthamini sana, yaani ni Zaid ya
Shemeji. Alikuwa Mshauri mzuri sana kwangu. Sasa
inaniuma nitaanzaje kumuua. Tena kwa kumchinja
akiwa mzima si kwamba amekufa. Nawaza sana.
"Mmmmmmmh! Lakini Nazani amna namna Raha ni
zetu, sisi ni jamaa zako lazima tukusaidie, pesa
tunazo humu kuna watu wanashida na mipesa.
Tutachukua majambazi wataenda kumteka halafu
tutaenda kumchinja polini huko"
Faustini alisema. Ushauri wa Faustin mala nyingi
ulikuwa wa kipuuzi tu, alikuwa yeye afikrii mbali
sana. Wazo lake yeye lilikuwa ni pesa tu.
"Ni kweli Faustin lakini si Rahisi kiasi hicho!"
Mgusi alisema.
"Mgusi unazani kuna nini tena. Tena ningekuwa
Mimi Leo hii ningemaliza"
"Ni kweli Jumanne hata Mimi ngoja niliunge wazo
la Faustin. Linafaa kabisa.
Manyege alisema.
"Sawa tutafanya hivyo"
Mgusi naye ilimbidi akubaliane nalo. Japo kuwa ni
ngumu kulifanya zoezi hilo lakini kulikuwa amna
namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuwatuma watu
wakamvamie shemeji yake jumanne, ndani kisha
waondoke naye harafu wakamchinje.
"Maamuzi yako kwako Mwenyekiti wetu lakini
nakuomba uondoe mawazo ya uwoga. Kama
tuliweza kumfanyia unyama wa ajabu kabisa Fatuma
Leo ushindwe Baba yake.
Cha kukushauri tusilifanye sasa hivi tukio hilo Bali
tutalifanya tukisha toka kuyapeleka maziwa ya
wanawake"
Mgusi alisema.
Mgusi yeye alikuwa ni mshauri makini sana kwa
wenzake, yeye alikuwa si mtu wa kukurupuka
alikuwa kidogo anafikiria sana mpaka kuyatoa
maamuzi.
Moja kwa moja hoja alizozitoa Mgusi zilikubaliwa
na wenzake wote.
******
Baada ya kutoka kwenye kikao chao wote kwa
pamoja waliondoka kurudi majumbani kwao. Baada
ya kufika hakuna ambaye alizungumza kwa wake
zao zaidi ya kuzitoa taraka tu.
Ingawaje wake zao walijililia sana wakiomba
kusamehewa lakini wanaume wale hawakutaka
kusikia maneno ya wanawake zao. Taraka tu ndiyo
ilikuwa mbele ya maneno yao.
Waliwafukuza wake zao wote na kubaki mabachelor.
Usiku huo huo waliwapigia simu Malaya wao
ambao walikuwa wamepanga kwa ajili ya
kuwachinja na kuwakata maziwa yao.
waliwaomba wafike kesho yake Nansio hata kwa
meli ambayo inafika Nansio Jioni. Waliwatumia
Nauri kabisa ya kuwatowa huko. Loveness alikuwa
ni miongoni mwao, kipindi hicho Bint wa watu tayari
alikuwa kaisha acha Kufanya Kazi Mwanza Hoteli na
alikuwa kaisha fungua Duka lake la nguo pale
Mwanza mjini. Lilikuwa ni duka kubwa ambalo
lilikuwa limebeba bidhaa za gharama kiasi cha
milioni tano. Pesa hizo alizipata baada ya kuuza
madini ambayo alipewa na Faustin baada ya
kukubali kufanya naye uchafu wa mapenzi.
Wanawake wote ambao waliwaita ni wale wale
ambao walifanya nao mapenzi wakiwa ndani ya
Mwanza Hoteli, na wanawake wale wote tayari
walikuwa wameisha iacha kazi ya ukahaba na
wamebadilika kabisa walikuwa wakifanya biashara
zao ambazo ziliwaingizia pesa.
Kama walivyokuwa wameombwa Jioni ya siku
iliyofuata mida ya saa kumi na mbili wanawake
wale ambao kimaumbo walionekana wanavutia,
nyuso zao angavu kabisa walifika pale Nansio
Castam. Meli ya Nyeunge ikiwa ndio usafiri wao.
Jumanne, Mgusi, Manyege pamoja Faustin.
Wanaume wanne ambao walikuwa tayari washakuwa
maarufu sana ndani ya Ukerewe kwa pesa zao za
muda mfupi ambazo walikuwa wamezivuna kwa
kumtoa kafara mtoto wa Dada yake Jumanne,
walikuwa wameyapaki magari yao pembezoni mwa
Barabara ya kutokea ndani ya kivuko cha meli
wakiwangoja Malaya wao kama walivyokuwa
wanawaita wao.
Wanawake wale kwa pamoja nao walitoka inje ya
Geti la kivuko. Wanaume wale walishuka mmoja
mmoja kumpokea mwanamke wake. Jumanne na
manyege wao ndio walikuwa wa mwisho kwasababu
Jumanne alikuwa amjui mtu wake ambaye alitakiwa
amchukue, lakini wapowafikia tu, yule wa manyege
alimkumbatia na aliyebaki Jumanne alijua moja kwa
moja ndiye wakwake. Hata yule mwanamke
hakusita kwasababu tayari alikuwa kaisha ambiwa
mpango ulivyokuwa.
Baada ya kuwapokea kwanza wote walienda
kuiweka kambi nyumbani kwa Jumanne kiongozi
wao, ilikuwa ni sherehe kweli kweli na uchafu wa
kutosha. Walikuwa wakinywa vinywaji vikari kweli
kweli. Wanawake wengine wote walikuwa wakinywa
pombe zile bila hata kuogopa walikuwa wazoefu
sana lakini Loveness kwake ulikuwa ni mtihani.
Alikuwa hawezi kabisa kunywa pombe. Hata
alipokuwa anang'ang'anizwa kufanya hivyo yeye
alikataa kabisa.
Mida ya saa nne za usiku wanawake wengine wote
wakiwa wamelewa isipokuwa Loveness tu,
Wanaume wale waliondoka na wanawake wao
kutoka Nyumbani kwa Jumaine na kuelekea kwenye
Nyumba zao. Wanaume wale walikuwa hawajalewa
kabisa kabisa. Nyumba zao kwa uzuri zilikuwa
karibu sana na zimezungukana, Ilikuwa kama
mwendo wa dakika tano unafika katika nyumba ya
Mwingine.
 
Sehemu.......................(11),
ILIPOISHIA.
Mida ya saa nne za usiku wanawake wengine wote
wakiwa wamelewa isipokuwa Loveness tu,
Wanaume wale waliondoka na wanawake wao
kutoka Nyumbani kwa Jumaine na kuelekea kwenye
Nyumba zao. Wanaume wale walikuwa hawajalewa
kabisa kabisa. Nyumba zao kwa uzuri zilikuwa
karibu sana na zimezungukana, Ilikuwa kama
mwendo wa dakika tano unafika katika nyumba ya
Mwingine.
SONGA NAYO.
Baada ya kufika majumbani mwao wanaume wale
na Roho mbaya zao, Roho za kishetani walianza
kufanya mapenzi na wanawake wale.
Kwa Jumanne Manyege na Mgusi baada ya
kumaliza kufanya mapenzi na wanawake wao ambao
walikuwa wamelewa kabisa hata namna ya kujitetea
hawana walichukua Visu maalum kabisa vilivyokuwa
vimeandaliwa kwa kazi ya kuchinja na kukata kisha
wakawachinja. Visu hivyo vilikuwa chini ya Uvungu
wa kitanda. Jinsi walivyowashawishi mpaka
kuwachinja. Waliwanyanyua wanawake wale kuwatoa
kitandani na kuwaweka kwenye kiti kilichokuwa
mule mule ndani ya Chumba, kisha
wakawadanganya kwa kuwafunga vitambaa machoni
mwao ili wawape zawadi. Moja kwa moja
wanawake wale bila kujali wakizani labda ni zawadi
ya Pete ya uchumba nao walikubali wakafungwa
vitambaa machoni mwao. Kilichofanyika hapo
walishitukia tu visu vinapita mashingoni mwao.
Hakuna sauti yoyote iliyosikika kutoka kwa
wanawake wale. Vifo vyao wote watatu vilifanana,
hakuna ambaye alikufa kinyume namwingine
kwasababu njia za wauaji zilifanana.
Baada ya kuwakata shingo zao. Wanaume wale
walianza Zoezi la kuyakata maziwa wanawake wale.
Walipomaliza kuyakata maziwa yao. Walisogeza tu
Vitanda vyao ambavyo vilikuwa vimelificha shimo
ambalo lilikuwa ndani ya vyumba vyao. Shimo hilo
lilikuwa na mfuniko ambao ulikuwa umedizainiwa
kama Tiles za mule ndani ya majumba yao. Wote
waliyafunua mashimo yao kilichofanyika walizitupa
miili ya wanawake wale kwenye mashimo hayo
yaliyokuwa marefu hatari. Urefu wa mashimo kwa
kipimo chake yalikuwa kama mita amsini kwenda
Chini. Baada ya hapo walianza kazi ya kuufanya
usafi ndani ya majumba yao.
Kazi ilikuwa kwa Faustin baada ya kufanya mapenzi
na Loveness Faustin aliogopa kukifanya kitendo kile
kwa Loveness, kwanza kabisa alinogewa na mahaba
mazito ambayo alioneshwa na Loveness, kitu
kilichompeleka mpaka kuamini kuwa toka afanye
mapenzi hakuwahi kukutana na mwanamke kama
yeye. Penzi hilo lilikuwa tofauti kabisa na la mwanza
Hoteli walipokutana kwa mala ya kwanza miezi
miwili nyuma, walifanya lakini Loveness
alijing'ang'aniza kwahio hakufanya katika usawa.
Kingine kilicho mshangaza Faustin kwa Loveness
alikuwa ni mwanamke ambaye anajitambua na
kuvutia kweli kweli.
Kila alipokuwa anataka kulifanya zoezi la kumchinja
Loveness alishindwa. Faustin alifikia kabisa hatua ya
kumuweka Loveness kwenye kiti na akamfunga
kitambaa machoni kabisa lakini kukichukua kisu
kwa ajili ya kuua, Roho ilimuuma akashindwa.
"Potelea mbali wanawake wapuuzi hawajaisha, ngoja
nitawatafuta tu"
Faustin alisema kisha akamfungua Loveness
kitambaa usoni.
Loveness aliyafumbua macho yake akiwa
amejiandaa kabisa, akitegemea kuna Surprise
kutoka kwa mpenz wake. Lakini cha kushangaza
alimkuta Faustin amekaa Chini huku akimwangalia
usoni.
"Nini mpenzi wangu, mbona umezubaa hivyo.
Nimekuuzi?"
Loveness aliuliza kwa upole kabisa wala
hakukumbuka tena habari za Surprise.
Swali lake Faustin hakulijibu, alibaki kimya
akimwangalia tu.
"Faustin kama nimekuuzi naomba unambie!"
Loveness aliuliza tena.
"We mwanamke huwa unasali sana?"
Faustin aliuliza.
Loveness alinyamaza kimya kwa muda akilitafakari
swali aliloulizwa. Halishindwa kuyaamini masikio
yake.
"Faustin mbona umeuliza hivyo?"
"Nataka tu kujua, kwasababu naisi kukupenda kweli
kweli maana sikuwahi kabisa kupenda kama ninavyo
kupenda kwahio naamini wewe ni mwanamke
mwema"
Faustin alisema.
"Ni kweli huwa nasali kwasababu maisha haya bila
mungu matatizo yatakuandama mpaka basi"
Loveness alisema.
"Kwanini unasema hivyo Loveness?"
Faustin alimuuliza Loveness.
"Mimi ninaishi na Mama yangu na Mdogo wangu
wa kike, Baba yangu kaisha fariki. Licha ya hivyo
Baba yetu sisi alitutelekeza na akapotea. Tukabaki
Mimi, mdogo wangu na mama yangu, kipindi hicho
Mimi nilikuwa nasoma kidato cha tatu na mdogo
wangu alikuwa darasa la saba. Tuliishi kwa shida
sana baada ya Baba kututelekeza. Mimi na mama
na mdogo wangu tulianzisha timu yetu tukawa
tunaomba tenda za kulima mashamba ya watu hasa
majaruba ya mpunga kipindi cha mvua. Tulikuwa
tunalipwa pesa kiduchu tu. Halafu kipindi hicho pia
tulikuwa na Biashara ya matunda. Nimeuza sana
matunda hapo mwanza mjini nilikuwa natembeza.
Ni juzi tu hapa mwaka elfu mbili na nne.
Humo ndimo nilikuwa napata pesa ya karo na
mdogo wangu. Nilipomaliza form four niliendelea
kufanya kazi zangu za kuuza matunda huku
nikisubilia majibu yangu. Matokeo yalipotoka
nilijikuta Nina Four ya 26. nilikuwa nishajipanga
hapo nilienda kusomea maswala ya Hotel
management. Pale Hotelini ndio ulikuwa mwaka
wangu wa kwanza na nilikuwa na miezi mitatu tu
toka niajiliwe pale.
Kwa process hiyo ya maisha tulikuwa tukiishi kwa
kumtegemea mungu, sisi na kanisa, kanisa na sisi.
Mama yangu apendi kabisa tusiende kanisani. Hata
siku ile nakutana na wewe pale Hotelini ni Basi tu
ya kutamani lakini baadaye nilijilaumu sana kwanini
niliufanya upuuzi huo. Nilishindwa kuvumilia kukaa
nalo kwasababu lilikuwa linanikeleketa sana,
nikaamua nimwambia mama. Baada ya kumweleza
alinikemea sana, lakini huwezi kuamini bado
nilikuwa Nakuwaza tu wewe, si kwa mapesa na
utajili wako, hapana ila nakupenda tu, ingawaje
najua kabisa wewe ni mwanaume unaye penda
wanawake kwa ajili ya starehe zako. Kabla sijaja
huku nimeomba sana, kama kuna janga lolote
liniepuke, kama kuna ubaya wowote mungu anilinde
pia nimemuomba mama yangu akaniombea na
mdogo wangu wote wakaniombea japo sikuwambia
kuwa nakuja kwako, ila nimewambia kuwa kuna
maswala yangu tu nayafuatilia. Nampenda sana
Mama yangu, sitaki kumwacha akiumwa Mimi
nikiwa huku, nimekuja tu kwasababu ya mapenzi
yangu kwako. Jinsi ninavyo kupenda na naimani
wewe utakuwa Mume wangu. Hata kwa Ubaya wako
wa kishetani unao kutawala, kunywa pombe.
Unalewa ovyo ovyo kuwa na wanawake wengi.
Lakini napenda tu, hapo naamini kuna ukombozi wa
mungu juu yako, Sikuwahi kupenda kama
nikupendevyo wewe, Huo ndio ukweli wangu moyoni
mwako. Naomba uyabadilishe maisha yako, Uanze
kumtumikia mungu. Kingine labda nikushukuru kwa
kiasi chako cha madini uliyonipa. Nimepata pesa
nyingi tu, kama milioni kumi na saba. Nimefungua
Duka la nguo na nimejenga nyumba ya vyumba
vinne. Ambayo sasa ipo kwenye hatua za mwisho
kumalizika ili tuamie kwetu"
Loveness alisema.
Maneno ya Loveness yalimuingia Faustin kweli
kweli. Yalimuumiza na kumkeleketa vya kutosha.
"Nashukuru kwa maneno yako mazuri lakini naomba
tulale ili kesho uwahi kuamka mapema, ili uiwahi
meli ya asubuhi kurudi nyumbani kwa ajili ya
mama"
Faustin alisema. Aliamua awe mpole kwa muda
huo. Baada ya kusema hivyo Loveness alirudi
kitandani. Kitanda kikubwa cha sita kwa sita,
Godoro lenyewe kubwa kweli kweli.
Laoveness alilala lakini kwa Faustin mambo
yalikuwa magumu alikuwa anawaza kwanini
umeshindwa kumuua Loveness, kitendo ambacho
kwake mwenyewe alikiona chepesi tu.
"Daah! Unabahati yako Loveness endelea kumuomba
mungu wako maana kakuokoa sana. Lakini Mimi
Kwangu usitegemee kabisa kunambia Habari za
mungu. Maana nitakuwa masikini na Shida yangu ni
pesa tu...........sijui nitawambia nini Jamaa zangu,
na kama wao wamefanikiwa inamaana kesho lazima
tuupeleke maziwa katika kisiwa kila. Basi tu. Ngoja
nione kesho kuche"
Faustin alikuwa anawaza peke yake akiwa kitandani.
Muda huo huo ujumbe uliingia kwenye simu yake.
Alipoichukua simu kuangalia alikutana na ujumbe
kutoka kwa jamaa zake wakimwambiwa wao
wameisha kamilisha. Faustin akujibu ujumbe huo
uliokuwa umetoka kwa Jumanne, Alichokifanya
aliizima simu yake ili asije ukizwa kuwa naye
kafanikisha.
Faustin aliwaza sana. Usingizi ulikuja kumvaa mida
ya saa kumi kabisa.
Mida ya saa moja Loveness aliamka akamwamsha
na Faustin, kisha akaingia Bafuni kuoga kwa
maandalizi ya safari kurudi nyumbani. Baada ya
kumaliza alivaa nguo zake vizuri akachukua mkoba
wake. Faustin akaingia kwenye mfuko wake
mwenyewe akatoa kiasi cha pesa kama laki tatu
akamkabizi mwanamke. Baada ya hapo
akamchukua Loveness kwenye gari lake mwenyewe
na kumuwahisha kastam.
Walipofika kastam Loveness alimuuliza Faustin
kuusu wenzake aliokuwa nao usiku?
"We nenda hawo bado wanastarehe zao.
"Sawa mpenzi wangu. Lakini naomba uzingatia
nilichokuambia na Mimi pia nitakuwa nakuombea ili
mungu akufanyie wepesi ubadilike"
"Sawa jitahidi"
Faustin alimjibu Loveness. Jawabu lake kidogo
Loveness alikumridhisha.
"Najua hiyo ni roho ya Shetani ndiyo bado
Inakunyemelea. Lakini ukiwa na shida na Mimi
naomba unipigie simu nitakuja. Nakupenda sana"
Laveness alisema kisha akamchumu Faustin kwenye
mashavu, akashuka kutoka ndani ya gari na kwenda
kukata Tiketi, alipomaliza akakimbilia kwenye meli
muda tayari ulikuwa usharuhusu abilia kuanza
kuingia kwenye meli. Alipanda meli ya MV
BUTIHAMA.
Faustin alibaki akiwa mwenye mawazo, aliwaza
wapi atampata mwanamke wa kumchinja ili amkate
maziwa yake kwa ajili ya kwenda kuyatoa kafara.
Aliamua aende kwa Jumanne kiongozi wao aongee
naye. Faustin alifika nyumbani kwa Jumanne
akamkuta Jumanne anamwagilizia nyasi za ukoka
na Maua yaliyokuwa yamepamba nyumbani kwake.
Geti lilifunguliwa na Jumanne mwenyewe nyumba
zao hazikuwa na mlinzi kwani hawakutaka kujulikana
wanafanya nini.
"Ooh! Faustin za kuamka?"
Jumanne alimuuliza faustin.
"Salama tu sijui wewe?"
"Aaa mimi safi tu, tena ninafuraha isiyo na kifani.
Wewe mwenyewe massage si umeiona?"
"Ndiyo nimeiona. Ongereni sana!"
Faustin alisema. Alionekana mnyonge.
"Haya nambie mambo yako?"
Jumanne aliuliza.
"Mambo yangu ni poa lakini sio poa sana"
"Kwanini unasema sio poa sana?"
"Mambo yangu yamekwama. Yule mwanamke
nimeshindwa kabisa kumchinja. Yani kila nilipokuwa
najaribu nilishindwa. Roho iliniuma sana, nikajikuta
namuonea huruma bila kutaka"
"Umeshindwa! Sasa unategemea nini na sisi
wenyewe ndio tulipanga Leo usingi tuyapeleke.
Wengine wote tumefanikisha! Mimi nilijua wewe na
Ubabe wako ndiye ungekuwa wa kwanza kunijulisha
kuwa tayari, lakini nashangaa mpaka sasa bado
nilikuwa sijaupokea ujumbe wako! kumbe mambo
yenyewe ndiyo hayo!"
Jumanne alisema. Hakuamini alicho ambiwa na
Faustin, kwa jinsi walivyokuwa wanamjua
hakutegemea kitu kama hicho kutoka kwa Faustin.
Faustin alinyamaza bila kusema kitu alikuwa
ameinamisha tu kichwa.
"Umh na huyo mwanamke yupo umemuacha
Nyumbani?"
"Hapana kaisha ondoka, ndiye nimetoka
kumsindikiza sasa hivi!"
"What! Unafanya nini Faustin, yaani hapa tulipo
tumebakiza siku nne tu miezi mitatu ikatike bado
unafanya mistake kama hio! Sasa unataka tupereke
mzigo umeoza au unataka upereke peke yako?"
Jumanne alisema kwa sauti kubwa.
"Mwenyekiti nazani unachokizungumza siyo sahihi
kabisa. Upaswi kabisa kunilaumu badala yake
ungenishauri namna ya kufanya au nitafute
mwanamke Mwingine fasta halafu nikamilishe zoezi
lakini sio kunilaumu. Sio kwamba Mimi kwa
Loveness nimeshindwa kirahisi hivyo, naamini hata
wewe ungeshindwa. Yule si kawaida, yaani nilikuwa
nimefikia hatua nzuri ya kumfunga kitambaa ili
kumkata shingo lakini nimeshindwa kukishika kisu!
Nimeshindwa kabisa, mikono umekuwa mizito"
"Kwahio Faustin unataka kunambia mwanamke yule
ni Tofauti na wengine?"
"Siyo hivyo Jumanne! Ila inaonekana anasali sana,
yupo na mungu! Mungu wake anamsimamia labda
ndiyo maana. Lakini isingekuwa hivyo Mimi na
Roho yangu hii juu ya jambo hili nisingeshindwa
kabisa. Hapa naomba niingie zangu mtaani. Au
niingie zangu buguza kwenye ile Guest huko najua
sikosi janamke, halafu nitakamilishia huko huku
nitakuja na mzigo tu!"
Faustin alisema.
"Wewe Faustin habari za uko achana nazo sasa hivi
mapema. Guest zenyewe bado hazijawa full kabisa.
Cha kufanya wewe ingia humu Nansio yamo
manamke mengi ya kufikia, chukua uje ufanye
mambo ili usiku twende kuupereka mzigo"
 
SEHEMU YA (12).
ILIPOISHIA.
"Siyo hivyo Jumanne! Ila inaonekana anasali sana,
yupo na mungu! Mungu wake anamsimamia labda
ndiyo maana. Lakini isingekuwa hivyo Mimi na
Roho yangu hii juu ya jambo hili nisingeshindwa
kabisa. Hapa naomba niingie zangu mtaani, Au
niingie zangu buguza kwenye ile Guest huko najua
sikosi janamke, halafu nitakamilishia huko huku
nitakuja na mzigo tu!"
Faustin alisema.
"Wewe Faustin habari za uko achana nazo sasa hivi
mapema. Guest zenyewe bado hazijawa full kabisa.
Cha kufanya wewe ingia humu Nansio yamo
manamke mengi ya kufikia, chukua uje ufanye
mambo ili usiku twende kuupereka mzigo"
SONGA NAYO.
"Hapo sasa umenena. ngoja niingia mtaani"
Faustin alisema, kisha akaingia kwenye gari lake la
kifahari na kuianza safari ya kumtafuta Bint
Mwingine wa kukata maziwa. Kwao ilikuwa Rahisi
tu, haikuwa kazi kabisa kumpata mwanamke wa
kulala naye kwasababu wanawake wenyewe
walikuwa wakijigonga. Akiwa anaendesha taratibu
gari lake alimuona Bint mzuuri akitembea kwa
mguu, Ilikuwa ni mbali kidogo na Nansio mjini.
Baada ya kumuona Bint yule Faustin alisimamisha
Gari lake mbele ya Bint yule, kisha akatoa mkono
akionesha Ishara ya kumsimamisha.
"Mambo mrembo!"
Faustin alisema.
"Poa!"
Yule Bint alisema kwa sauti ya kuregeza. Mungu
wangu angejua kama anaongea na Shetani basi
asingethubutu hata kusimama.
"Unaelekea wapi Mrembo?"
Faustin aliuliza.
"Nafika tu hapo kwa Rafiki yangu"
"Si mbali sana!"
"Hapana ni Karibu tu"
"Mh! Sawa......lakini Mimi kidogo nahitaji twende
sehemu kidogo tukae tuzungumze huku tukishushia
moja barid moja moto"
Faustin alisema. Mwanaume mwenye pesa kwa
kujiamini kabisa aliongea.
"Mh! Lakini Mimi Nina Mtu wangu na namuheshimu
sana"
"Aaaa! Mtu wako kitu gani bhna, kwahio wewe
unajua upo peke yako? Kwanza huyo achana naye
we ingia kwenye ndinga tukaponde Raha, yaani
mtoto nzuri kiasi hiki bhna. Kwanini nisikuonge hata
Gari"
Faustin alizidi kumjaza sumu ya kumlainisha bint wa
watu.
"Sawa Lakini tusichelewe!"
Bint yule alisema.
"Usijali mrembo we panda kwenye gari twende zetu
kule upepo unakovuma"
Faustin alisema. Muda huo aliweka na nyimbo ya
Professor Jay ya Zari la Mentari.
"Unaitwa nani?"
Faustin alimuuliza Bint yule jina baada ya kukaa
kwenye gari.
"Naitwa Edina"
"Ooh! Edina jina zuuri kama ulivyo!"
Faustin alisema. Huku akiendelea kuliendesha gari
lake.
"Ushawahi kuolewa?"
Faustin aliuliza.
"Hapana! Lakini niliwahi kuzaa, Mtoto wangu alifariki
akiwa na miezi mitatu"
Edina alisema.
"Pole sana Edina. Kwahio unafanya shughuri gani?"
"Huwa tunafanya Biashara ya kulangua samaki"
"Mh kumbe! basi twende zetu mi nitakupatia mtaji
wa kutosha!"
Faustin alisema.
"Kweli?!"
Edina aliuliza kwa mshangao baada ya kuambiwa
atapewa mtaji wa kutosha.
"We usiwaze twende nikuoneshe watu wenye pesa
zetu tunavyo ishi bhana. Watu shida hatuna kabisa
wewe unawaza waza"
Faustin alisema.
Waliendelea kuongea upuuzi ndani ya Gari huku
Faustin akiendelea kuliendesha Gari lake.
Dakika kama kumi tu tayari walifika kwenye mjengo
mkubwa wa Faustin.
"Hapa ndiyo kwangu, ndipo napanga nikuweke
mwanamke mzuuri kama wewe?"
Faustin alisema. Edina wa watu alijikuta anafurahi
mpaka kupitiliza. Hakuamini kabisa kama ni kweli.
Waliingia ndani ya mjengo wa Faustin. Ndani
sebuleni tu kulikuwa na sehemu imetengwa na
kulikuwa na kabati la vinywaji vya kila aina.
"Huwa unakunywa pombe?"
Faustin alimuuliza Edina.
"Huwa nakunywa lakini siyo sana. Huwa nakunywa
bia mbili tu za Kilimanjaro"
"Basi Mimi nitakufundisha unywe zaidi ya hapo"
Faustin alisema.
Kisha akachukua Chupa ya kinywaji kikari kabisa
tofauti na Kilimanjaro aliyoiseme Edina.
Kinywaji kile kilikuwa ni kikari hatari, huwezi kunywa
grasi moja ukaacha kulewa.
Alimmiminia Edina kiasi cha Nusu grasi tu kisha
akamkabizi. Kitendo cha kuiweka kinywani mwake
Edina aliisi kama ni tamu tamu, lakini alipokuwa
anazidi kuinywa ukari Ndiyo uliongezeka.
"Umeisikiaje hiyo?"
Faustin aliuliza.
"Mwanzo ni tamu lakini mwisho inakuwa kari"
"Usijali ukiizoea itakuwa tamu mwanzo mwisho"
Faustin alisema, kisha akamuongezea Edina tena
kwenye girasi na kumwambia anywe tena.
Edina aliipokea grasi na kuiweka kinywani tena na
kuimeza pombe ile, nayo akaimaliza.
Haikupita hata dakika kumi Edina akaanza kulewa
kabisa.
Faustin alikuwa akimuita Edina. Edina akawa
anaitika kilevi levi. Muda huo Bint wawatu alikuwa
mbali kabisa kimawazo.
"Faustin alimbeba na kumpeleka kwenye chumba
maalumu cha kuchinjia ili kuyatoa maziwa.
Kwa kweli haikuwa kazi kukikata kichwa cha Edina
kisha akamkata maziwa yake.
Edina alikufa bila kutarajia, kupenda penda hovyo na
Kuparamia hovyo kisa mtu anapesa, anatembelea
Gari la kifahari, Basi hicho ndicho kilimkuta. Faustin
alifurahi sana baada ya kulimaliza zoezi lake la
kuyakata maziwa ya Binti yule.
Alipomaliza muda huo alimpigia Jumanne simu na
kumjulisha kuwa mambo yako vizuri.
Vyumba vyao vya kuchinjia walikuwa wanavifanyia
usafi wa hali ya juu sana ili kuhakikisha hakuna hata
tone la Damu linabakia.
******
Jioni walikuwa tayari washajipanga kama kawaida
yao. Mida ya saa nne walianza safari yao ya kwenda
katika kisiwa cha shetani. Walifika katika kisiwa kile
mida ya saa tano za usiku. Mazingira ya pale
yalikuwa kama yale yale ya mwanzo, Moto ulikuwa
unawaka kama kawaida. Joka lilifika na kuwapokea
kama mwanzo, likawaongoza mpaka sehemu kuliko
kuwa na pango la kafara.
Ndilo pango lile lile ambalo waliuwacha mwili wa
Fatuma, lakini siku hiyo hawakukuta kitu katika
pango lile. Waliambiwa wayaweke matiti Yale pale
pale kwenye pango la kafara.
"Ongereni sana, lakini msibadilike, mtafanywa kama
mwenzio alivyofanywa"
Joka lilisema.
"Sawa! Msijali sisi tutakuwa watiifu"
Faustin alisema.
"Wewe Faustin tunaomba usimkaribie tena yule
Mwanamke. Endapo ukithubutu tu Uhai wako
hutokuwepo tena, Lazima Ufe! Kwanza Namba yako
ya simu Ubadilishe ili kukata kabisa nawasiliano
naye"
Joka lilisema kumuonya Faustin juu ya Loveness,
alikusema sababu ya kwanini lilimuonya Bali onyo
lilifika.
"Kwa hayo machache kila kitu mnajua lakini
kumbukeni kuwa kila mwezi mnapaswa kuyaleta
maziwa ya mwanamke katika kisiwa hiki ofa yenu
imeisha Isha. Lakini niwakumbusheni kuwa chumba
maalum cha damu hakitakuwa kwa Jumanne tu Bali
hata kwenu, na ndani ya Chumba hicho mnatakiwa
mfanye kama alivyolezewa Jumanne. Lakini Damu
lazima muwe mnaziweka mala moja kila mwezi,
lazima mjaze damu kwenye vyombo ambayo
mtakuwa mnaiweka. Na chumba hicho ndicho
kitakuwa chumba kwa ajili ya mawasiliano yetu na
ninyi endapo mtahitaji msaada wa jambo lolote
kutoka kwetu. Kwa Maelezo hayo machache nazani
nimeeleweka bila shaka"
Joka lilisema. Wote kwa pamoja kuashilia kuwa
walielewa walitikisa vichwa. Walikuwa ni watu
wanne tu, waliokuwa wamesalia. Baada ya Maelezo
kukamilika walirudi kwenye Boti yao tayari kwa
safari ya kurudi kutoka kwenye kisiwa ikaanza ili
kujakuendelea na maisha ya utumwa wa shetani.
Vichwani mwao walikuwa wamesalia na kazi ya
kufanya mapenzi na Dada zao ili wawape mimba
wazae watoto wa kafara kwa ajili ya kisiwa hicho,
kazi ya kulala na wanawake za watu, na kazi ya
kuwakata wanawake maziwa pamoja na kazi kubwa
ya kumuuwa Shemeji yake na Jumanne, mume wa
Dada yake ambaye ndiye Baba yake Marehemu
Fatuma.
Waanaume wale walikuwa hawana kabisa wasiwasi
juu ya maswala yao, walijiona wamezoea hasa
Faustin wakati yeye alishindwa kwa Loveness.
Usiku kabisa mida ya saa saba ndiyo mida ambayo
walikuwa wanafika majumbani mwao.
Katika masharti mazito ambayo walikuwa
wamebakiza kuyatekeleza, Sharti la kulala na Dada
zao kwa wale wengine watatu liliwachanganya sana.
Walilala usiku huo wanawaza ni jinsi gani wataanza
kuwashawishi Dada zao ili wapate kufanya nao
mapenzi, halafu wabebe mimba kisha wazae
watoto.
Siku iliyofuata mida ya saa tano walikutana
Nyumbani kwa Jumanne ili wapange Jinsi
watakavyoishi ili isiwe vyepesi kwa watu
kuwagundua, hio ni kwasababu walikuwa hawana
wake wote. Walikuwa wamebaki mabachelor.
"Mimi Nina wazo?"
Manyege alisema.
"Wazo gani manyege?"
Jumanne ambaye alikuwa mwenyekiti aliuliza.
"Wazo langu hasa ni kwetu sisi watatu. Mimi,
Mgusi, na Faustin. kwakuwa sisi tuna Dada zetu
tena hawajaolewa, kwanini tusiwalete tukae nao,
kufanya hivyo naamini itakuwa rahisi kwetu
kuwashawishi ili wakubali tufanye nao mapenzi.
"Kweli kabisa umezungumza wazo malidadi kabisa.
Yaani wazo lako ni bomba kabisa!"
Faustin alisema kumpongeza mwenzake.
"Sasa vipi kuusu Jumanne?"
"Kuusu Jumanne tutatafuta limwanamke tu kama
geresha liwe nyumbani kwake kama mfanyakazi"
Manyege alisema tena.
"Ni kweli na itakuwa vizuri kwasababu muda
Mwingine utakuwa unapumzikiapo hapo hapo"
Faustin alisema.
"Mimi bado Nina shaka, hawo Dada zetu tukiwaleta
tukakaa nao, lazima wawe wapenzi wetu kwa muda
lakini Je na wanawake wengine hatutoweza kufika
nao hapa?"
Mgusi aliuliza.
"Mgusi unasema nini ndugu yangu. Guest zipo
kibao, bado tunamagari, pesa tunayo nyingi, na sasa
tutaanza kuzikusanya pesa zetu kupitia wasimamizi
wetu kutoka kwa madareva boda boda. Halafu kuna
Hoteli ambayo nazani mwezi ujao tutaizindua nayo
itatupa pesa. Guest ndani ya mwezi huu lazima
zikamilike kwa kuweka viti, vinywaji na mziki,
Kwahio mambo ya Malaya wengine tutakamilishia
huko huko"
Manyege alisema.
"Ni kweli hata Mimi nilitegemea jawabu hili, ni kweli
tumejenga Guest nane na tayari maboma kwa ajili
ya kumbi za disco na baa yameisha Isha"
Jumanne alisema. Tayari mambo yalianza kuwa
mazuri katika mipango yao. Kwahio kwa upande wa
kuwachukua wanawake wa kuwanjinja maziwa
itakuwa si kazi ngumu kwao watakuwa wanatoka
wanaenda kwenye majumba yao hayo ya starehe,
wakifika huko ni kuchinja na kuyachukua maziwa
(matiti)
"Lakini endapo tukitumia hizo Guest itakuwaje
maana tutakuwa tunachinja kwahio damu lazima
ziruke mbali na hilo usafi kwenye hizo Guest
tutauwendeshaje sisi?"
Jumanne aliwauliza wenzake. Kidogo kwa hilo
walianza kulitafakari kwa upya kwasababu wao
walikuwa wanachinja. Ingawaje kila guest ilikuwa na
Chumba maalum kilichokuwa na shimo reefu kabisa
kwa ajili ya kutupia miili ya wanawake watakao
kuwa wanawachinja, lakini kazi alibaki ni kuchinja
na kusafisha Damu.
"Kwa hapo nafikiri tunaweza kubadili namna
nyingine ya kuua tofauti na kuchinja. Nasema
tubadili kwasababu kuchinja sisi wenyewe ndio
tulijiwekea hatukupewa utaratibu huo. Mtu pekee
tuliyeambiwa kumchinja ni Shemeji yake na
Jumanne"
Mgusi alisema. Wazo lake lilionekana Bora sana
kwa Rafiki zake, walilipenda sana, wote kwa pamoja
wakakubaliana kuwa watafute sumu ambayo
itakuwa inatumika kuua harafu wao watakuwa
wanakata maziwa tu, hiyo itakuwa rahisi hata Damu
zikitoka watakuwa wameulekezea mwili kwenye
shimo la kuutupia.
ITAENDELEA.
usiikose hadithi hii nzuri ya kupendeza
 
SEHEMU YA (13).
ILIPOISHIA.
Mtu pekee tuliyeambiwa kumchinja ni Shemeji yake
Jumanne"
Mgusi alisema. Wazo lake lilionekana Bora sana
kwa Rafiki zake, walilipenda sana, wote kwa pamoja
wakakubaliana kuwa watafute sumu ambayo
itakuwa inatumika kuua harafu wao watakuwa
wanakata maziwa tu, hiyo itakuwa rahisi hata Damu
zikitoka watakuwa wameulekezea mwili kwenye
shimo la kuutupia.
SONGA NAYO.
Kuusu swala la kuchinja walikubaliana hivyo.
"Sasa kuusu kumchinja Shemeji yake Jumanne?"
Faustin aliuliza.
"Labda tumuulize Shemeji yake. Mwenyekiti wetu
unapanga lini kumchinja Shemeji yako?"
Manyege naye aliongezea swali juu ya swali.
"Naombeni kwanza tuvumilie mpaka nyumba
ambayo nawajengea ikamilike, nasema hivyo
kwasababu yeye ndiye anaisimamia. Na mpaka
hapa nimeambiwa matofari yashakamilika na kama
leo ni Alhamisi basi Jumatatu, wanaanza
kupandisha tofari kwakuwa tayari Msingi
ushamalizika, na nazani itachukua siku mbili kufikia
kwenye leta. Mafundi wapo kama kumi kwahio kazi
inaenda haraka. Baada ya hapo watafunga leta na
wataacha muda kama siku tano kwa ajili ya
kumwagilizia. Kwahio ndani ya mwezi nitahakiksha
nyumba inaisha kila kitu, mpaka langi, baada ya
hapo tutachinja"
Jumanne alisema.
Wote kwa pamoja walikubaliana"
"Naomba kesho nisafiri naelekea mwanza kidogo
bhana kupiga raha. pesa tunazo za kutosha Nansio
pamenichosha"
Manyege aliwambia wenzake. Baada ya kusema
hivyo wenzake nao walimuunga mkono na
wakakubaliana kuondoka wote wakaponde raha
ndani ya Jiji la Mwanza.
Siku zilizidi kwenda hatimaye wiki ikasalia mwezi
kuisha, mipango ya jumanne kuusu kumuua Shemeji
yake ilikuwa ishakuwa tayari, na mpaka muda huo
Nyumba ilikuwa ishakamilika kwa kila kitu, kama
alivyokuwa amepanga.
Kwakuwa wiki hiyo ndiyo ilikuwa ni ya kutoa kafara
wanaume wale walikaa tena kikao cha makubaliano
ya kufanya. Katika makubaliano yao walikubaliana
usiku huo wa siku hiyo hiyo ndiyo wawatume watu
wakamvamie Shemeji yake Jumanne ili wakaifanye
kazi ya kumchinja kisha waichukue Damu.
Makubaliano mengine yalikuwa ni kuwatafuta
wanawake wengine, na wanawake hawo
watawachinjia kwenye majumba yao ili wapate
damu za kuweka kwenye vyumba walivyoambiwa
wavitenge. Mpaka hapo bado walikuwa
hawajawaleta Dada zao kwa wengine watatu; Mgusi,
Faustin na manyege.
Masaa nayo huwa hayachelewi, hatimaye usiku
ulianza kuingia na majambazi kwa ajili ya kuvamia
yalikuwa yashaandaliwa. Waliondoka nayo kutoka
Nansio mida ya saa moja za usiku kuelekea huko
kazilakanda. Usiku wa manane ndiyo waliyatuma
majambazi kwenda kuivamia nyumba ya Shemeji
yake Jumanne. Kwa bahati nzuri au mbaya walikuwa
hawajaamia kwenye nyumba mpya ambayo
walijengewa na Jumanne.
Majambazi walifika wakaubomoa mlango na kuingia
ndani, Dada na shemeji yake Jumanne pamoja na
watoto walijaribu kujitetea lakini hawakuonewa
huruma. Dada yake na Jumanne alichomwa sindano
za masaa pamoja na watoto. Sindano hizo
ziliwafanya kusinzia, kisha majambazi yale
yakamfunga mikono na miguu, halafu mdomoni
walimjazia mavitambaa kisha wakamziba kwa
plasta, machoni wakamfunga kitambaa cheusi.
Baada ya zoezi lao wakamchukua na kutoka naye
kumpeleka kwa waliokuwa wamewatuma.
Wakiwa wenye Furaha walifikishiwa mtu wao usiku
huo wakaondoka naye wakasogea kwenye mapori
ya huko huko. Walipofika eneo ambalo waliona ni
sahihi kwao walimfungua kitambaa cha usoni. Toka
wanampokea Baba fatuma, Jumanne na wenzake
walikuwa awaongei, lakini walipomfikisha porini
walimfungua kitambaa alichokuwa kafungwa usoni,
Jumanne akiwa tayari na kisu mkononi halafu
Faustin akiwa na Chombo kwa ajili ya kujaza damu,
Baba yake Fatuma alitamani aseme chochote lakini
alikuwa hawezi kuzungumza neno lolote kwasababu
mdomo ulikuwa umefungwa. Kilichokuwa katika
kichwa chake alikuwa anaongea kwa fikira tu basi.
"Jumanne ulaaniwe na mwenyezi mungu maisha
yako yote, uishi kwa mateso milele, nakwapia hata
ile nyumba uliyoijenga Mke wangu hatoweza kuishi
mule na hatoweza, itabaki pale milele na
ningeomba ibomoke tu. Nitakufa kwa maumivu ila
naamini Chozi langu na hasira zangu zitalipwa na
watu wenye kuijua haki. Niuwe Jumanne"
Baba Fatuma alimaliza kwa kusema hivyo
kimoyomoyo. Kama vile mungu naye alikuwa
amewasitopisha watu wale àu mashetani wale
kuifanya kazi ya kumchinja mpaka amalize kuitoa
laana yake. Yaani alipomaliza kuisema kauli ya
"nichinje jumanne" kisu kilipita kwenye shingo lake
pale pale. Muda wa kuishi Baba Fatuma uliishia
pale pale.
Walipomaliza zoezi lao waliondoka usiku huo,
hawakutaka kusubili kuche kwasababu waliamini
ikigundulika itakuwa matatizo kwao. Hawakutaka
hata kwenda kwenye Guest yao iliyokuwa huku huko
kazilakanda, ingawaje Mpaka hapo kila kitu kuusu
Guest zao kilikuwa kimeisha kamilika lakini
hawakuthubutu kwenda kwasababu ya hofu. Guest
zao ndizo zilizokuwa bora ndani ya Ukelewe nzima,
waliziwekea Solar kubwa kabisa kwa ajili ya umeme,
na walikuwa wameweka mziki mzito pamoja na
kumbi za starehe kwa ajili ya kunywa na
kuserebuka, terevisheni kubwa za inchi 32, ndizo
zilikuwa kwenye kumbi zao na ilikuwa si moja
zilikuwa ni zaidi ya moja kwa kila Guest, Ukelewe
mzima wao ndiyo walianza kuisambaza DStv.
Kwahio mipira watu walikuwa wanaenda kutazama
kwenye mabaa yao kwa watu waliokuwa wanaishi
maeneo ya karibu na Guest zao. Hapo pote
walikuwa wanavuna pesa tu.
Siku iliyokuwa inafuata mida ya Jioni ya saa kumi
Jumanne aliondoka Nansio kurudi tena kazilakanda
kwa Dad yake kumliwaza. Tena alifanya hivyo
kwasababu taarifa za kuvamiwa na kuuliwa kwa
Shemeji yake zilimfikia. Alikwenda huko akiwa
kama ajui chochote. Kwenye msiba wa shemeji
yake jumanna hakukaa sana, alikaa pale siku mbili
tu kisha akaondoka kwa ajili ya kumtafuta
mwanamke wa kukata maziwa ya kuyapereka katika
kisiwa cha shetani.
Mambo yao yalikuwa kama hawali. Na kwa bahati
nzuri hata wale wengine walikuwa hawajawelata
Dada zao katika majumba yao kwa ajili ya
kuwafanya wake zao, walipanga baada ya kutoka
katika kisiwa hicho ndiyo wawalete Dada zao.
Kweli baada ya kuimaliza kazi ya kuwauwa
wanawake wengine na kuchukua damu zao
wakaziweka kwenye vyombo walivyokuwa
wameambiwa kuiweka damu katika vyumba
maalumu walivyokuwa wameambiwa wavitenge.
Baadaye waliyachukua maziwa ya wanawake
waliowachinja na kuyapereka katika kisiwa cha
Shetani. Walipofika kisiwani walipongezwa sana,
tena wakaongezewa na madini mengine kiasi cha
Nusu ya mifuko ya Shilingi mia.
Wanaume wale walifurahi sana, kwahilo waliona
mambo si mabaya. Yaani hata kuua sasa wao
walifikiri ni kama kazi zingine za kawaida.
Walifika tena wakaenda kuyauza madini yao kama
hawali wakati huu walipata kiasi kama milioni mia
moja kwa kila mmoja.
Baada ya kutoka kuyauza madini yao, waliizindua
kwanza Hoteli yao ya Nansio kwa ajili ya kuanza
kutumika ili nayo pia iwaingizie pesa, baada ya
kulimaliza zoezi hilo walijifikiria tena mradi
Mwingine ndipo walipopata wazo la kutengeneza
mitumbwi mitatu mitatu kwa ajili ya utegaji wa
dagaa.
Zoezi lao lilitekelezwa mala moja, wakanunua mbao
na mitumbwi ikaanza kutengenezwa ndani ya wiki
hiyo hiyo.
Bado mitumbwi ikiwa inaendelea kutengenezwa;
Manyege, Faustin na Mgusi, walikwenda kwao na
kuwachukua Dada zao, kwa ajili ya kuishi nao,
jumanne yeye aliendelea kuishi hivyo hivyo hakutaka
tena kumuweka mwanamke Mwingine, yeye aliona
kuishi hivyo bila mwananke haitakuwa na shida
yeyote.
Mpaka kufikia hapo kila kitu ambacho waliambiwa
ndani ya mwezi walikuwa washakimaliza. Hata
walichokuwa wamepanga wao nacho pia kilikuwa
kishamalizika.
Kila kitu ambacho walikuwa wameambiwa
kukitekeleza walikitekeleza kwa haraka
******
Baada ya kumaliza matanga ya msiba wa mumewe
Mama Fatuma alipanga kuhamia kwenye nyumba
ambayo Alijengewa na kaka yake, na uzuri nyumba
ile ilikuwa imejengewa pale pale nyumbani kwake,
kwahio ilikuwa ni kazi ya kuhamishia vyombo ndani
ya Nyumba hiyo tu. Usiku wa kuamkia siku ya
kuamia ndani ya nyumba mpya, mama yule aliota
ndoto ya kutisha; ndoto ile alikuwa akimuona
Mwanaye analalamika na kumpa onyo kari asije
akaikaribia Nyumba ile. Muonekano wa ndoto
ulikuwa ukimuonesha mama yule akiwa anataka
kuingia ndani ya Jumba lile, lakini alikuwa
anashindwa kwasababu Giza lilikuwa ni kubwa sana
na lilitisha, tena ulikuwa ni wakati wa mchana, kila
alipokuwa analazimisha alishindwa. Lakini ghafra
akiwa bado katika harakati hizo, Bint yake alimtokea
akiwa mule mule ndani ya nyumba ile, cha ajabu
alikuwa kashikilia kichwa chake mikononi mwake
halafu kikiwa kwenye tumbo (alikuwa kakibebea
tumboni) licha ya kuwa kichwa kilikuwa mikononi
lakini ndicho kilikuwa kinaongea.
"Mama usithubutu kusogea humu, ili ni shimo la
moto mama, shimo la giza, shimo ambalo shetani
anaishi mama, usije kusogea kabisa mama.
Usisogea na ukifanya hivyo utakuwa kama Mimi,
Mjomba siyo mtu nzuri kabisa mama"
Hiyo ndiyo ilikuwa sauti ya Fatuma akimuonya
mama yake. Baada ya kusikia tu hivyo mama yule
alishituka kutoka usingizini. Alikaa kitandani kwake
akiwaza sana, alijifikilia mengi sana, alikuwa
anajiuliza maswali mengi ambayo haya kumpa hata
majibu sahihi yenye uhakika. Alikuwa anapata hisia
ambazo zilikuwa ni za kweli kabisa lakini alishindwa
kuziamini. Kwani alikuwa anawaza kabisa
"kwamaana hiyo Bint yangu alichinjwa! Bint yangu
alitolewa kafara! Kwahio Mali za Jumanne ni kafara
ya damu ya Mwanangu!"
Mama yule aliwaza sana akiwa kitandani kwake
amekaa katika usiku wa Giza. Baada ya kuwaza
sana alirudi tena kujilaza kitandani, tayari muda
ulikuwa ushaenda kama mida ya saa tisa za usiku,
lakini hata alipojirudisha kitandani usingizi ukuja
tena mpaka kunakucha. Asubuhi na mapema
aliamka na kwenda ndani ya jumba lile la kifahari
kuangalia kama ni kweli alichokiona, lakini alipofika
alikuta hakuna dalili zozote za kile alichokiota
ndotoni. Toka muda huo alikuwa akifikiri sana, toka
asubuhi mpaka mchana hakuchukua maamuzi
yoyote ya kuhama, na wala hakufanya chochote
zaidi ya kuwapikia wanawe chakula, yote hayo
kwasababu ya mawazo.
Baada ya kumaliza kula chakula ambacho hakukila
vizuri alichukua mkeka na kuutandika inje kwenye
kenopi ya jumba na kujilaza. Baada ya kujilaza
haikuchukua hata dakika kumi, usingizi ulimpitia
tena. Ndani ya usingizi wake ndoto nyingine
ilimuhijia mama yule, ndoto hiyo ilikuwa ni ya Bint
yake yule yule, tena sasa ilikuwa ikimuonesha
Fatuma akiwa na kichwa chake vile vile mkononi
kakishikilia harafu anamzunguka, kichwa kilikuwa
kinaona kama kawaida, midomo ikicheza na ndicho
kilikuwa kinaongea.
"Mama! Mamaaa! Amka haraka utoke hapa,
ukiendelea kuwepo utakufa"
Baada ya kuyasikia maneno hayo mama yule
aliamka kutoka usingizini, aliyekutana naye ni
Fatuma yule yule akiwa amesimama mbele yake,
Damu nyingi zikimtoka kwenye shingo yake na
kichwa chake ambacho alikuwa amekishikilia.
"Mama naomba ikiwezekana hii Nyumba umwambie
Mjomba aje aimishe hapa maana inakupa mateso
mama, Naomba umpigie simu umwambie, sitaki
nikutese kwa namna yoyoye, na hivi nafanya
kwasababu nakuonea huruma, Mjomba siyo mtu
mzuri yule. Baada ya kunimaliza Mimi, akaja baba
yangu, mwisho ataamia kwako mama. Naomba
utoke hapa haraka"
Fatuma alisema kisha akatoweka. Pale pale mama
yule alishituka tena usingizini alipokuwa amelala.
Ndoto ile iliendana na ukweli kabisa kama vile
alikuwa na Bint yake wanaongea, lakini mazingira na
muonekano wa Bint yake vilimtisha sana. Eneo
lilikuwa pale pale wala hakuwa pengine, lakini damu
alizokuwa anaona zinamtoka Fatuma akuzikuta.
Mama Fatuma alianza kuteseka sana, mateso
kutoka kwa Mwanaye yalianza kumwandama.
Kwa utaratibu kabisa alianza sasa kuisi kitu cha
ukweli kutokana na ndoto hizo mbili za kutisha.
Alitoka pale na kurudi ndani ya Nyumba yake ya
zamani, nyumba iliyokuwa imejengwa kwa matofari
ya tope, juu ikiwa na bati zilizozeeka ndani ikiwa na
vyumba viwili. Alirudi mpaka Chumbani kwake
akakaa kitandani. Kichwani mawazo yalikuwa mengi
sana. akiwa Chumbani kwake Bint yake aliyekuwa
anamfuata Fatuma alimfuata ili kumuuliza kitu.
"Mama mbona leo uko hivyo, au unaumwa maana
toka asubuhi natoka kwenda shule nimekuacha
hauna raha kabisa.
"Hapana Sauda mwanangu, Niko vizuri lakini nawaza
tu mawazo ya maisha. Nianzie wapi ili ninyi mpate
kusoma kwa furaha"
Mama alisema kumwambia Bint yake aliyekuwa
anaitwa Sauda. Kipindi hicho Sauda alikuwa
akijiandaa na kuimaliza elimu ya shule ya Msingi.
"Usijali mama yangu, nakuhakikishia Mimi na
mdogo wangu sadick tutasoma na tutafauru na
Mjomba atatupeleka afrika kusini tukasome huko na
Dada Fatuma"
Sauda aliongea, kwa maneno yake alizani
yanamfariji mama yake lakini kumbe hapana, Mama
yeye alikuwa akiwaza vitu vingine kabisa tofauti na
alichomweleza Mwanaye.
"Nashukuru sana mwanangu kwa kulitambua hilo,
nawapenda sana"
Mama alisema ili kumfanya mwanaye asiendelee
kumtilia shaka.
"Asante mama. Kwahio mama huwezi kuwaza
tena?"
Sauda alimuuliza mama yake.
"Ndiyo mwanangu wewe nenda ukaoshe vyombo
halafu ujisomee"
Mama alisema huku akionesha Tabasamu kwa
mwanaye.
"Vyombo nishamaliza kuviosha mama, labda ngoja
niende nikajisomee"
Sauda alisema.
"Sawa mwanangu, nenda ukajisomee"
 
SEHEMU YA (14).
ILIPOISHIA.
Mama alisema ili kumfanya mwanaye asiendelee
kumtilia shaka.
"Asante mama. Kwahio mama huwezi kuwaza
tena?"
Sauda alimuuliza mama yake.
"Ndiyo mwanangu wewe nenda ukaoshe vyombo
halafu ujisomee"
Mama alisema huku akionesha Tabasamu kwa
mwanaye.
"Vyombo nishamaliza kuviosha mama, labda ngoja
niende nikajisomee"
Sauda alisema.
"Sawa mwanangu, nenda ukajisomee"
SONGA NAYO.
Sauda alimwacha Mama yake na kwenda
kujisomea.
Mama Fatuma alitawaliwa na mawazo siku mzima.
Hakuweza kufanya chochote mchana kutwa, usiku
hata chakula hakukila kabisa kwasababu ya
mawazo.
Usiku wa siku hiyo alishindwa kuupata kabisa
usingizi. Toka hapo alianza kuishi kwa kuiogopa
nyumba ile. Hakutaka kabisa kulisogelea jengo lile.
Mama Fatuma aliishi kwa kisasi na wasiwasi juu ya
ndugu yake. Alitamani amuite amuulize ukweli wa
vifo vya mwanaye na mumewe kama alihusika lakini
alishindwa na alitamani pia azipeleke taarifa hizo
kwa Baba yao napo pia aliona muda wake bado
alitaka apate uhakika zaidi na zaidi juu ya Jambo
hilo.
******
Wanaume wale watatu waliendelea kuishi kwa
matambo juu ya utajili wao. Nansio na Ukerewe
mzima walijulikana kwa kutoa misaada juu ya
matatizo yanayo wakumba watu, watu waliokuwa
wanahitaji msaada walipewa hata bila masharti.
Pesa walikuwa nazo sana, kwani ndani ya mwezi
huo walipata kuizindua Hotel yao, nayo ilianza
kuwaingizia pesa, pia mitumbwi takribani nane
waliyoitengeneza kwa ajili ya kutegea dagaa tayari
iliyanza kufanya kazi.
Ndani ya Mwezi huo huo walipata kuwaleta Dada
zao kwa ajili ya kuwafanya wake zao ili wazae nao
watoto kwa ajili ya kafara ya kisiwa cha Shetani.
Baada ya kuwafikisha Dada zao waliwaacha wazoee
kwanza.
Wengine wakiwa tayari washawafikisha Dada zao,
Jumanne alisafiri mpaka nyumbani kwa Dada yake
ili kumuomba aamie kwenye nyumba aliyomjengea,
lakini Dada aligoma kabisa kuingia ndani ya nyumba
ile, akumwambia kwanini hataki kuhamia ila
alimwambia kaka yake kuwa anasubili mpaka miezi
miwili iishe kwa ajili ya kumuenzi mumewe. Majibu
ya Dada yalimrizisha Jumanne. Yote ni kwasababu
akujua kilichokuwa moyoni mwa Dada yake aliamua
kumwacha na kurudi kuendelea na mambo yake.
Siku zilizidi kwenda, muda wa kuusogelea mwezi
mwingine nao ulizidi kwenda. Wanaume wale
waliendelea kuishi kwa kuwalala wake za watu,
kama kutekeleza agizo la shetani.
Muda huwa uchelewi, hatimaye siku za mwisho za
mwezi zilifika na zilikuwa zikiwangoja kupereka
matiti ya wanawake kwenye kisiwa cha Shetani.
Katika kufanya upuuzi wao wa kulala na wanawake
wengi, kwa kutumia Guest zao zilizokuwa
zimetapakaa ndani ya Ukerewe kwa kuwalala wake
za watu na wanawake wengine wanaojiuza,
walifanikiwa tena kuwachinja wanawake wengine na
kuyachukua maziwa yao kwa ajili ya kukamilisha
agano la kisiwa cha Shetani, kazi yao ya kuchinja
kama kawaida ilifanya usiku harafu siku ambao
ilikuwa inafuata usiku wake tena, ndio walikuwa
wanapereka kisiwani. Safari hii sasa ilikuwa ya mala
ya tatu wakawa wanapereka maziwa(Matiti) kwenye
kisiwa cha Shetani. Kipindi hiki walipongezwa tu
hawakupewa chochote. Baada ya wiki tangu watoke
huko kwenye hicho kisiwa cha Shetani, Taarifa za
kupotea kwa wanawake kutoka sehemu tofauti
zilianza kuzagaa ndani ya ukelewe, watu walikuwa
wanatembea kila sehemu wanaliongelea tukio la
kupotea kwa wanawake kwa mala nyingine tena,
ikumbukwe hii ni ya mala ya Tatu mpenzi msomaji
wa kisa hiki wanaume wale wanaenda kuzitoa
kafara katika kisiwa cha Shetani. Na mala zote hizi
taarifa za kupotea kwa watu zilikuwa zinatangazwa
kwenye vyombo vya Habari, cha kushangaza ni
kwamba watu wote waliokuwa wanapotea hata miili
yao ilikuwa haionekani kabisa.
"Hii mala ya Tatu watu kupotea ghafra ndani ya
wilaya yetu, mwanzo alianza mmoja tu, huyo
akapotea Mazima, mwezi uliofuata walipotea
wanawake wanne kwa wakati mmoja, cha ajabu
ndani ya Mwezi huo huo ndiyo alichinjwa mtu kwa
kukatwa kichwa huko kazilakanda. Bado hata
matukio ya nyuma yakiwa hajafutika kwenye
kumbukumbuku za watu, taarifa zingine zimetufikia
tena kuwa wanawake wengine wanne wamepotea,
wawili wakiwa wake za watu.
Sasa wamepotea wanaenda wapi kwa wakati
mmoja watu wanne, hili sasa lazima tulifanyie
uchunguzi wa kina sana na wa hali ya Juu"
"Mimi nazani kuna watu wanawachukua na kwenda
kuwauza hata inje ya inchi"
"Sawa lakini sizani naamini humu kutakuwemo na
ushirikiana hii Ukerewe si unaijua"
"Mpaka kichwa kimeaza kuniuma siamini kabisa,
maana Leo kwa mwenzangu kesho kwako, huwenda
mwanamke wako naye akachukuliwa, maana
wanaopotea wote ni wanawake tu"
"Ni kweli hata Mimi nimeanza kuogopa!
Unakumbuka miezi miwili nyuma tulipokea tena
taarifa za kupotea kwa wanawake wengine watatu
kutoka mwanza. Na ilisemekana kuwa wanawake
wale walisafiri kuja huku kwetu. Ila sasa
haikuthibitika huku walifikia wapi, na ndiyo mwezi
ambao huku alipotea mwanamke mmoja tu, kwahio
ukijumlisha yule mmoja na wa mwanza watatu!"
"Idadi inarudi pale pale ya watu wanne wote
wanawake kupotea kila mwisho wa mwezi"
"Wanawake wanne, kila mwisho wa mwezi!
Nimeanza kuwashitukia wale matajiri wanne"
Hayo yalikuwa ni mazungumzo baina ya maofisa
wawili wa ngazi ya juu kabisa ndani ya wilaya ya
Ukerewe. Maofisa hawo sasa walianza kutilia
mashaka juu ya kupotelea kwa watu ndani ya wilaya
hiyo, kilicho washangaza zaidi ni aina wa watu, wote
walikuwa ni wanawake tu, halafu walikuwa
wanapotea kwa wakati mmoja, ndani ya siku za
mwisho wa kila mwezi, halafu idadi ile ile kila
walipokuwa wanapotea.
Taarifa za kupotea kwa watu ndani ya wilaya ya
Ukerewe, azikuishia kutapakaa ndani ya wilaya hiyo
tu, zilivuka inje ya wilaya hiyo. Watu walianza kuishi
kwa taadhali sana huku wakiyahofia maisha yao.
Taarifa za kupotea kwa wanawake ndani ya Wilaya
ya Ukerewe ziliwafanya watu kujiuliza maswali
mengi yasiyo na majibu, Wanaume wanne
waliokuwa yanayafanya hayo nao wasi wasi ulianza
kuwaingia juu ya taarifa ambazo zilikuwa
zinatapakaa mitaani. Wanaume wale waliamua
kuitisha kikao wazungumze ili kujua muafaka wao.
"Naona kama vile mambo yamenza kuharibika,
itafikia kipindi tutagundulika!"
Faustin alisema huku wenzake wakimsikiliza kwenye
kikao.
"Ni kweli hata Mimi mwenyewe taarifa ambazo
zinatapakaa zinanitisha sana, maana kila mtu huko
mtaani anazungumzia swala la wanawake kupotea,
kila kilipo kijiwe cha watu taarifa hizo ndizo
zinazunguzwa tu, halafu ukipita kila mmoja
anakutupia Jicho"
Manyege naye alisema.
"Ndiyo maana tumeitana hapa tujadiliane ili tujue
namna ya kufanya labda tunaweza kuwaondoa watu
hofu na wasiwasi juu yetu" Jumanne alisema.
"Mwenyekiti, naomba tuongee na wale majini wa
kisiwa kile kwanza labda wanaweza kutusaidia
tukaliepuka jambo hili"
Mgusi alisema ushauri wake ulikubaliwa, kisha wote
wakasimama na kuongozana na Jumanne kuelekea
kwenye chumba alichokuwa amekitenga yeye kwa
ajili ya kuwasiliana na mashetani au majini wa
kisiwa cha shetani.
Baada ya kuingia kwenye chumba hicho walitamka
maneno yao ya kishetani waliyokuwa wameambiwa
kuyatumia wakitaka kuwasiliana na mashetani Yale,
wakiwa wanaendelea kuita ghafra chumba kile chote
kilitawala Giza zito kabisa lililokuwa linatisha. Timu
ile ya watu wanne ilianza kuwa na wasiwasi lakini
walivumilia.
"Ninyi Binadamu mna shida gani?"
Katika Giza hilo hilo
Sauti nzito ya kutisha kweli kweli ilisikika
ikiwasemesha.
Kuisikia sauti hiyo waliamini kuwa ni majini ya
kisiwa cha Utajiri au kisiwa cha Shetani.
"Ni kweli tunashida, maisha yetu yameanza kuwa ya
wasiwasi, watu wengi katika Ardhi hii wameanza
kutuhofia kwasababu ya taarifa za kupotea kwa watu
wengi ndani ya miezi mitatu.
Jumanne alisema.
"Najua mnataka msaada wetu, kuusu hili msiwe na
wasiwasi. Litakwisha lakini mnatakiwa mfanye
jambo moja kwa kila mmoja wenu ili kuwaepuka
watu hawa. Mnatakiwa mchinje watu mchana harafu
mkate maziwa yao, myalete katika kisiwa changu
mchana huo huo, mkifanikisha zoezi hilo zito
mtakuwa mmewafunga watu kuwatilia mashaka
yoyote"
Sauti ile ilisema, hapo haikusikika tena, wala
hakuna kilicho endelea, hata Giza la ndani nalo
lilififia likabaki giza lilikuwemo ndani ya chumba.
"Kama vile tunaongezewa tatizo juu ta ttatizo"
"Sielewi kabisa nitaishi vipi katika Dunia hii"
"Hakiamungu ningejua nisingethubutu"
"Daah! Kwakweli ni Bora hata na Rafiki yangu
kipenzi Said, kaisha sahau na naamini mungu
alimsamehe"
Kila mmoja aliwaza kivyake, hawakutegemea kabisa
kabisa kama wangeambiwa kufanya zoezi zito kama
hilo katika maombi yao.
"Mmelipokea je swala hili jamani?"
Jumanne aliwauliza wenzake baada ya kutoka
kwenye chumba cha siri, chumba ambacho kila
mmoja kilikuwa ndani ya nyumba yake. Kilikuwa ni
chumba cha pekee ambacho hakuna mtu Mwingine
tofauti na wenyewe aliyekuwa anaingia ndani ya
chumba hicho, Kilikuwa ni chumba ambacho
akifunguliwi mala kwa mala mpaka siku ya kuweka
damu, kilikuwa na giza muda wote. ndani vitambaa
vyekundu vilikuwa vimetanda kwenye kuta za
chumba hicho, vitambaa hivyo vilikuwa vimezunguka
mpaka vimeziba na madirisha.
"Mimi kwa upande wangu naomba tutekeleze tu,
hakuna namna zaidi ya kufanya, wametuahidi wao.
kwahio inaweza ikaleta mabadiliko na watu
wakatusahau kabisa"
Mgusi alizungumza.
"Ni sawa lakini ni kazi nzito, mchana kweupe huyo
mtu tutamchinjaje kwanza?"
Faustin alisema, aliisi kuchanganyikiwa.
"Utafikiri ndiyo tunaanza kuitoa kafara ya kwanza ili
tupate Mali, ni mateso sana! sana tu, na tunaonewa
kabisa Mimi ninasem kabisa tunaonewa"
Manyege naye alisema.
"Nani atatusaidia kufanya hayo yote, ni sisi
wenyewe hakuna mwingine ambaye anaweza,
tuliyataka wenyewe, cha kujitetea labda tuwaombe
watupe muda tushirikiane tuwe tunaanza na mmoja
mmoja kwanza halafu baada ya wiki tunafanya tena
kwa ajili ya Mwingine. Nasema hivyo kwasababu
itakuwa rahisi kushirikiana kwakuwa hili zoezi letu ni
vigumu kumshirikisha mtu Mwingine kabisa tofauti
na sisi. Na mpaka tuliko fikia naamini ni hatari zaidi
kwa kumwambia mtu"
Jumanne alizungumza, kidogo yeye aliupata Ujasiri
wa kuzungumza kiukakamavu.
"Mwenyekitu wetu, najua kabisa unatupenda lakini
mengine tujaribu hata kuwa tunakataa tutazoeleka,
badala ya kufurahia mavuno yetu sasa tunapata
shida"
Faustin alisema.
"Faustin Rafiki yangu, tufanye maji ukisha yavulia
nguo Sharti uyaoge. mwenyekiti kazungumza jambo
la Msingi, tuanze na mmoja mmoja"
Manyege alisema, Hiyo ndiyo ilikuwa hesabu yake
ya haraka yoyote.
"Manyege umezungumza vizuri lakini ngoja Mimi
niongee kwa kusema hivi, Duniani humu kuna
majambazi wependa pesa, kuna watu washapinda
akiri, hawo watu wanawaza kupata pesa kwa njia
yoyote. tusiogopea kuwatafuta watafanya kazi
kwajili yetu, kila mmoja atakuwa na kundi lake la
watu, tutawatoa mbali kisha tutawatawanya kwenye
magasti yetu huku Ukerewe, wataishi ndani ya wiki
mbili. Tutahakikisha ndani ya hizo wiki tuwe
tushakamilisha zoezi letu"
Mgusi alisema.
"Kwanini umesema hivyo mgusi?"
Jumanne alimuuliza.
"Najua tukifanya mala moja tutawahi kukamilisha,
harafu tukishapereka mambo yatakaa vizuri kwahio
tujitoe tu"
Mgusi alifafanua tena kwa ufupi. Maelezo ya mgusi
waliyakubari na wakakubaliana kuyafanyia kazi
kabisa. Baada ya makubaliano hayo walirudi
nyumbani kwao.
Kazi nyingine ilikuwa ni namna ya kuanza
kuwashawishi Dada zao, kila mmoja alipokuwa
anataka kujaribu kuzungumza aliogopa namna ya
kumuanza ndugu yake. Baada ya siku mbili toka
watoke kwenye kikao chao Mgusi, Faustin na
manyege walikutana wakashauliana wawanyweshe
Dada zao pombe walewe ili iwe kazi Rahisi hata
kwa kuwabaka.
Walikubaliana hivyo, na kweli walipofika majumbani
mwao siku hio walifanya kama walivyokubaliana.
Kweli kila mmoja alifanikisha kulala na Dada yake.
Asubuhi kulipokucha Dada zao walishangaa kujikuta
wamelala kitanda kimoja na kaka zao, tena kila kitu
kilikuwa wazi kabisa kuwa walifanya mapenzi.
Pande zote tatu, kulicharuka sana tu, kila mmoja
Dada yake alimuhijia juu.
Majawabu yao wote karibu yalifanana.
"Kaka ndio nini hiki umefanya?"
Swali hilo lilikuwa la kwanza kwa mabinti wote.
Lakini mambo yalikuwa ni magumu sana mpaka
kuwekana sawa. Mfano ni kwa Mgusi alivyokuwa
anajitetea kwa Dada yake baada ya ya kuulizwa
kwanini.
"Naomba unisamehe mdogo wangu nimefanya hivyo
kwasababu naogopa kufa, ningekufa kama
nisingefanya hivyo"
"Unamaanisha nini kusema hivyo?"
Dada alimuuliza kaka yake.
"Ngoja nikwambie ukweli, yani unavyoniona hapa,
usingekuwa wewe ningekuwa nishakufa, hata
asubuhi kusingekucha"
"Bado kabisa sijakuelewa unamaanisha nini?"
Dada limuuliza tena kaka mtu.
"Ninaishi kwa mkataba wa Shetani, Jini ambalo
ndilo lenye Mali hizi"
Mgusi alisema,
"Kwamaana hiyo wewe unashirikiana na Shetani
ndiyo maana umeamua kunifanyia upuuzi huu, kaka
kweli!"
Dada alisema, alijisikia maumivu makubwa sana.
"Sio kwamba nashirikiana naye, Jini huyo alikuwa ni
mpenzi wangu Lakini nilikuwa sijui kama ni Jini kwa
muda ambao niliishi naye, dawa ya pekee ya
kumuepuka ilikuwa ni kufanya mapenzi na wewe.
Naomba unisamehe. Naamini yule Jini angeniua
kabisa"
"Wewe umajuaje kama dawa ya pekee ni kufanya
mapenzi na Dada yako?"
Dada alimuuliza tena kaka yake.
"Huyo Jini mwenyewe ndiye aliyenambia. Tafadhali
mdogo wangu, naomba usiumie kwasababu
umeniokoa na hii ni siri tutaificha hakuna ambaye
anajua ukweli wa jambo hili zaidi ya Mimi na wewe
tu basi"
Mgusi aliendelea kujieleza kwa Dada.
"Lakini kaka Hujafanya vizuri kabisa na ningejua
Mimi nisingekuja kwako"
Dada alisema, ilifikia mpaka mdogo wake anatokwa
machozi, alijisikia uchungu sana kufanya mapenzi na
Kaka yake wa kuzaliwa naye baba mmoja mama
mmoja.
"Mecki mdogo wangu, kwahio wewe unataka nife
kwa mateso makari ya Jini, naomba unizoee kama
mpenzi wako tu, naomba tafadhali itakuwa ni siri
yetu"
Mgusi alizungumza kwa kina sana ili kumuweka
sawa Dada yake ambaye alijulikana kwa jina la
Mecki.
Ilikuwa ni ngumu kwa wote watatu, baada kujitetea
sana kila mmoja kwa maelezo yake bila mafanikio,
mwisho kila mmoja alitishia kujichoma kisu mbele
ya Dada yake. Kitendo cha kujitishia ndicho kilikuwa
kama dawa ya kuwekana sawa na Dada zao. Siku
hiyo wote walishinda ndani na Dada zao
wakiwekana sawa, kila mmoja alikuwa akimuahidi
Dada yake vitu vikubwa kabisa katika maisha yake.
 
SEHEMU YA (15),
ILIPOISHIA.
Ilikuwa ni ngumu kwa wote watatu, baada kujitetea
sana kila mmoja kwa maelezo yake bila nafanikio,
mwisho kila mmoja alitishia kujichoma kisu mbele
ya Dada yake. Kitendo cha kujitishia ndicho kilikuwa
kama dawa ya kuwekana sawa na Dada zao. Siku
hiyo wote walishinda ndani na Dada zao
wakiwekana sawa, kila mmoja alikuwa akimuahidi
Dada yake vitu vikubwa kabisa katika maisha yake.
SONGA NAYO,
Hapo ndipo mwanzo wa mahusiano ya kimapenzi
na Dada zao ulianzia.
Baada ya kulimaliza la Dada zao kwa wengine
watatu, wanaume wale walikutana tena
wakawatafuta wanaume wa kazi, wanaume wapenda
pesa, wanaume wenye utayari wa kufanya lolote
ilimradi walipwe pesa. ndani ya wiki moja
walitakiwa waikamilishe kazi iliyokuwa imeambiwa
kuifanya, kazi ya kishetani, kazi ya kuua kwa
kuchinja.
Baada ya kuwapata wanaume wa kutosha,
walijigawa katika vikundi vinne kila mmoja akiwa na
wanaume wa kazi watatu. Waliokuwa na Faustin
wao walisafiri mpaka kisiwa cha Ukara katika kata
ya katende, wengine walienda kwenye kisiwa kidogo
cha Sizu, na wengine walikwenda Buguza na
wengine walikwenda mkasaunga. Hizo ni sehemu
ambazo zipo Jirani kabisa. Baada ya kuhakikisha
kila mmoja kafika sehemu yake salama, kilichofuata
ilikuwa ni mipango ya kuingia mashambani kwa ajili
ya kutekeleza jukumu lao la kuchinja kisha
kuchukua matiti ya wanawake.
Ilikuwa ni kazi ya dhambi sana kwao lakini
walilazima kuifanya kwasababu ya matamanio ya
kishetani.
Siku ya Pili walipofika katika maeneo ambayo
walijigawa ndiyo siku ambayo walikuwa
wameipanga wafanye mauji ili waondoke mapema,
wayawaishe matiti ya wanawake kwenye kisiwa cha
shetani.
Walifanya kama walivyokuwa wamepanga, mida ya
saa kumi za Jioni walikuwa kwenye boti kuyapereka
maziwa(matiti) ya akina mama kwenye kisiwa cha
Shetani, wanaume wale walikuwa hawatambui
kabisa Kama walikuwa wanawachinja wanawake
wengine ambao walikuwa ni wake za wenzao,
hawakulijua hilo Bali walitaka kutekeleza agano lao
na shetani.
Siku iliyofuata taarifa za mauaji zilianza kutangazwa
kwenye vyombo vya habari kwenye vipindi vya
asubuhi, watu walizipokea taarifa hizo kwa
masikitiko makubwa sana, ndani ya wiki mbili tu
matukio mawili na mazito yametokea.
Kilichowaumiza zaidi matukio yote yaliwahusu
wanawake, lakini hili la kuuliwa kwa wanawake
kisha kukatwa kiungo muhimu katika maumbile yao
kiliwachanganya sana watu wa wilaya hiyo, tukio
hilo lilisababisha wanawake waanze kuogopa hata
kutoka inje ya miji zao. Lilikuwa ni tukio kubwa la
kushangaza na kusikitisha kweli kweli, tukio hili
lilisambaa ndani ya Ukerewe nzima, ndilo tukio
ambalo lilizungumzwa sana katika kila kona ya
wilaya hiyo na viunga vyake, mpaka leo hii
halisauriki kabisa katika kumbukumbu zao.
Richa ya matukio Yale kuwaumiza watu wengi,
warika zote na jinsia zote, wanaume wanne
waliokuwa wanahusika na matukio hayo yote wao
waliendelea kufurahia na kunywa pombe ndani ya
Jumba la Jumanne.
******
Siku tatu baada ya taarifa za mauaji kusambaa
sehemu mbali mbali za inchi, Mida ya saa kumi,
Faustin alikuwa kwenye gari lake akiwa anatoka
nyumbani kwake kuelekea katika mishe zake za
kawaida, Ghafra alimuona Loveness akisogea
kumfuata.
Kwakuwa alikuwa inje ya Geti Faustin alisimamisha
gari mbele ya Loveness.
"Ooh! Faustin mpenzi wangu?"
Loveness alisema baada ya kumuona Faustin.
Faustin akujibu chochote, zaidi alifika akamvuta
Loveness mkono na kumuingiza kwenye gari kisha
na kuondoka naye, walitoka kidogo inje ya Nansio
mjini sehemu ambayo ilikuwa haina watu wengi
ndiko ambako Faustin alilisimamisha gari, wote
wakashuka kwa ajili ya kuzungumza na Loveness.
"Wewe Mwanamke kwanini umerudi tena huku?"
"Samahani Faustin mbona umekuwa na hasira kiasi
hicho"
Loveness alisema. Mpaka hapo alikuwa kaisha
muuliza swali hilo tangu akiwa kwenye gari lakini
Faustin alikuwa ajibu.
"Hata usingeuliza Loveness, jawabu la swali lako
unalo wewe"
Faustin alisema kwa kufoka, hakutaka kumuona
Loveness kabisa kwenye macho yake, alifanya hivyo
kwakuwa alikuwa kaisha onywa na Joka la kisiwani
kuwa hapasi kumsogelea Loveness.
"Nimekuja kwasababu nakuonea huruma, maisha
yako yako hatarini"
Loveness alizungumza hivyo kisha akageuka
nakuondoka eneo walipokuwa wamesimama.
Alichokizungumza Loveness kilibaki kinamkeleketa
Faustin hapo aliamua kumuita Loveness asimame
kwanza wapate kuongea taratibu.
"Loveness naomba unisamehe tafadhali. Lakini
naomba tu unambie kwanini umesema maisha
yangu yapo hatarini"
Faustin alizungumza, alibadilika na kuwa mpore
ndani ya sekunde thelathini.
"Ndiyo Faustin uko kwenye hatari kubwa sana, we ni
mwanaume wa pekee ambaye nampenda kuliko
yeyote katika Uhai wangu huu, lakini nasikitishwa na
matukio yako Faustin, wewe ni shetani kabisa
ambaye unapaswa utubu dhambi zako mungu
atakusamehe"
Loveness alisema.
"Unamaanisha nini Loveness?"
Faustin aliuliza tena.
"Faustin usitake kunambia kuwa unachokifanya
ukijui, kwanza wewe ni mwanaume malaya,
mwanaume ambaye unafanya mambo ya kutisha,
haitoshi unawalala wanawake wa watu harafu bado
unaua!"
Laveness alizungumza.
Maneno ya Loveness yalimshitua sana Faustin,
hakutegemea kuyasikia maneno mazito kiasi hicho
kutoka kwa Loveness. Maneno ya Loveness
yalikuwa ni ukweli mtupu, ukweli ambao
haukujificha kabisa. Faustin alinyamaza kwa muda
huku akimwangalia Loveness ambaye machozi
yalikuwa yanamtoka kwa masikitiko makubwa Sana,
Loveness alikua akimuhurumia sana Faustin.
"Okey Loveness, naomba tuingie ndani ya Gari
tuongee vizuri"
Faustin alisema, Bila kubisha kwasababu alikuwa
anampenda Faustin, Loveness aliingia kwenye gari
tena ili waongee taratibu na Faustin
"Loveness naomba unambie Habari zangu
umezipata wapi?"
"Faustin mpenzi wangu nakuonea huruma sana,
hapa nilipo nisha fikiria sana juu ya maswala yako,
nimevumilia lakini kila kukicha mambo yanazidi
kurundikana. Naamini hata Mimi ningekuwa
nishakufa bila shaka!"
Loveness alizungumza, bado aliendelea kumuweka
Faustin kwenye wakati mgumu, bado hakuwa wazi
kabisa kivipi aliyajua matukio ambayo Faustin
alikuwa anayafanya.
"Loveness tafadhali mama! naomba uniweke wazi
nijue namna ya kufanya kabla sijaibika. Naomba
unambie taarifa zangu hizi umezijuaje na kama watu
washazijua wengi pia unambie!"
Kwakweli Faustin alistahili kuhurumiwa kwa Jinsi
alivyokuwa anazungumza.
"Ni watu wengi tu Faustin, na naamini hata wale
wanawake ambao tulikuwa nao siku ile
mkawanywesha mipombe mingi walikufa na wewe
na Wenzako ndio mliohusika. Sasa unataka kujua
nini tena kutoka kwangu wakati Mimi nikama
shuhuda wa hayo yote. Kwanini ufanye mambo hayo
ya kishetan? kwanini uwe mtumwa wa shetani?
kwanini usimrudie mungu wako ili usamehewe?.
Mpaka inafikia hatua mtu unakuwa na profile mbaya
hivyo unategemea msaada tena! labda nikwambie tu
kifo chako ni aibu na mateso makubwa?"
Laveness aliendelea kumkandamiza Faustin kwa
maneno makari ya vitisho vizito kabisa.
Faustin aliisi kufa ndani ya gari huku amekaa na
Loveness, upepo wa kujidai ulimuishia, ni siku kama
nne tu toka wawachinje watu mchana waziwazi
mapolini wakiamini kuwa watajikinga na kuhofiwa
na watu juu ya matukio yao ya dhambi lakini sasa
zinakuja taarifa zingine ambazo zinaumiza zaidi,
kwa maana hiyo ni kwamba walichokifanya
hakikuwa na faida kabisa kwao zaidi ya kumfaidisha
shetani wao.
"Loveness naomba msaada wako kama mambo
yashakuwa hivyo, ni kweli nimeua kabisa na hata
wewe nilitaka nikuue kama kafara ya kukupereka
kwenye kisiwa cha Shetani, kule ndiko tulitoa
madini yote ambayo baadhi nilikupatia, na mengine
ndiyo ambayo tumeuza sisi wenyewe na kupata
pesa ambazo tumejengea majumba, Guest na
Hoteli. Kwenye kisiwa kile huwa tunawaperekea
mashetani wa pale maziwa ya wanawake kila
mwisho wa mwezi, tukisha chinja huwa tunawakata
matiti ndiyo tunapereka huko, wanawake wote
ambao unasikia wanapotea ndani ya wilaya hii ya
Ukerewe ni sisi ndiyo tunawapoteza kwa kuwaua,
miili yao huwa tunaitupa kwenye mashimo marefu
yaliyomo kwenye kila Jengo linalotuhusu, ndio
maana wakipotea hawaonekani hata miili yao"
Faustin alizifunua siri zao zote kwa Loveness.
"Na kwenye hicho kisiwa unachokiita cha shetani
mlifikaje?"
Loveness aliuliza tena.
Baada ya kuulizwa hivyo Faustin alizidi
kuyaporomosha yote mwanzo mpaka mwisho, jinsi
walivyofika pale kisiwani, walijuaje habari za
kisiwani pale, mpaka walipomchinja Fatuma na
kumbaka kisha wakapewa madini ambayo
waliyatumia kupata Utajiri wa pesa.
"Bint wa miaka kumi na mitano halafu bikra, huyo si
alikuwa mtoto mungu wangu! Si laana hiyo Faustin.
Aa! sijui mliupata wapi ujasiri wa kufanya hivyo?"
Loveness alisema baada ya kusimuliwa kisa cha
akina Faustin walivyofanya mpaka kufika kwenye
kisiwa cha shetani. Ilimuuma sana Loveness, hasa
fatuma alimuuma zaidi kuliko vingine vyote.
"Ndiyo maana naomba unisaidie Loveness, naomba
unisaidie ili nikiepuke tu hiki kikombe"
"Ngoja nikwambie kitu, nyumbani kwako naomba
usirudi kama unataka msaada wangu"
Loveness alisema.
"Okey Niko tayari tuondoke wote hata sasa sitaki
nikae tena katika maeneo haya"
Faustin alikubalina moja kwa moja na ombi la
Loveness kuwa asirudi nyumbani kwake.
Baada ya faustin kukubali Loveness alimuomba
faustin waende kulala Guest, Kweli walienda guest
nyingine kabisa ndani ya Nansio, Faustin hakutaka
waende kwenye Guest yao ya kisheitwani. Hata
kuliendesha gari lake, Faustini alikuwa analiendesha
kwa taadhali kubwa sana, alikuwa anahofu akijua
kuwa anaweza kukamatwa muda wowote, mpaka
kufikia hapo Loveness alikuwa kaisha mshawishi
kuizima simu yake kabisa, kwa bahati nzuri kadi
yake ya Bank alikuwa nayo kwahio alipita Bank
akadro kiasi cha pesa cha kutosha kwa ajili ya
safari ya kwenda mwanza.
Usiku mida ya saa mbili wakiwa chumbani Loveness
alimshauri Faustin waanze kusari kwanza kabla
hawajalala.
Faustin akukataa ingawa hata kanisani alikuwa si
mtu wa kuudhulia lakini siku hio alikubali kupiga
magoti na kuanza kusali pamoja na Loveness ndani
ya Chumba walichokuwa, wakiwa katikati ya
maombi Ghafra ulivuma upepo mkari sana ndani ya
chumba chao, upepo huo uliwashitua sana, Faustin
akaanza kuogopa akatamani akimbie, kwani alianza
kuwaza kuwa ni wakati wake wa kufa kwa mateso
kama alivyokufa Rafiki yao kipenzi Said.
"Loveness aliendelea kuomba na kuomba ili
kulikabili tatizo hilo. Akiwa bado anaendelea
kuomba ilisikika sauti ya ajabu ikiwasemesha,
maneno yaliyokuwa yanatamkwa yalikuwa ni ya
vitisho. Faustin alizidi kuogopa lakini Loveness yeye
ndiyo alizidi kabisa kuomba ili mungu awaepushie
ushetani uliokuwa unawafuata. Huwezi amini kwa
maombi ya Loveness, hali hiyo ilichukua kama
dakika kumi ikaisha kabisa, hali iliyokuwepo hawali
ikarejea.
"Faustin unaogopa nini?"
Loveness aliuliza.
"Naogopa kufa kwa mateso, hivi hivi ndivyo
alivyouliwa Rafiki yangu Said"
"Usiogope mtumainie mungu wako, mambo yote
yatakuwa vizuri tu, nimekuja huku kwa kwasababu
ya mapenzi yangu kwako, siku zote niliamini wewe
ndiye chaguo langu, wewe ndiye niliyeumbiwa kwa
ajili yangu. Yote haya nimeyajua kwasababu kila
nilipokuwa naomba usiku na mchana, siku yoyote
hasa Jumapili ilikuwa lazima nikuombee. hata pale
nilipokuwa naitafuta namba yako ikawa ipatikani
sikufa moyo Bali nilitekeleza jukumu langu
lakukuombea kwa mungu. Kwakuwa kwako nilipajua
na nilijua ipo siku mungu ananiongoza na utatoka
katika utumwa wa shetani, sikuwa na shaka kabisa
kuusu uwepo wako labda ningekuta umekufa, lakini
ningejua mapema tu kuwa ushakufa"
Loveness alisema.
"Sasa ulijuaje kama Mimi namtumikia Shetani?"
Faustin alimuuliza Loveness tena swali lile lile
alilokuwa analiuliza tangu wakiwa kwenye gari inje.
"Tukifika nyumbani kwangu nitakwambia naomba
uwe na subira"
Loveness alisema.
"Lakini kuna siri ambayo nilikuwa sijakwambia
Loveness, Uwezi amini nimethubutu kufanya
mapenzi na Dada yangu kisa kutekeleza agano la
kisiwa cha shetani"
Faustin alisema huku machozi yakimtoka kabisa.
 
SEHEMU (16).
WhatsApp..........0755547788.
ILIPOISHIA.
Faustin alimuuliza Loveness tena swali lile lile
alilokuwa analiuliza tangu wakiwa kwenye gari.
"Tukifika nyumbani kwangu nitakwambia naomba
uwe na subira"
Loveness alisema.
"Lakini kuna siri ambayo nilikuwa sijakwambia
Loveness, Uwezi amini nimethubutu kufanya
mapenzi na Dada yangu kisa kutekeleza agano la
kisiwa cha shetani"
Faustin alisema huku machozi yakimtoka kabisa.
SONGA NAYO,
Alianza kuyajutia maamuzi yake baada ya kugundua
kuwa alikokuwa kulikuwa hapafai kabisa, mbali na
hilo walikuwa wanakosa namna ya kukimbia ili
kuacha kulitekeleza agano walilokuwa
wameandikishana na Mashetani wa kisiwa cha
Shetani.
"Usijali Faustin, kuwa kwako wazi inamaanisha kuwa
umeisha elewa kuwa ulichokuwa unakifanya
akistahili"
"Sawa Loveness najua kabisa unanipenda na ndiyo
maana umethubutu kurudi huku kwa ajili yangu,
lakini inauma sana, kulala na Dada yangu, tena kwa
ujasiri kabisa, nikijimini kisa kumfanyia ibirisi"
Faustin alizidi kuzungumza kwa maumivu makubwa
sana.
"Sawa Faustin naomba utoe tena mawazo hayo,
mungu kaisha kusamehe, kikubwa jifunge kwake,
kuanzia sasa mshikilie mungu, wewe na mungu,
mungu na wewe"
Loveness alizungumza, alijitahidi sana Bint wa watu
kumuweka sawa Faustin, alifanya hivyo sababu ya
mapenzi tu, mapenzi tu ndio yalimfanya kila mala
kumuombea Faustin, na maombi hayo aliyafanya
kila alipokuwa anaomba. Loveness alifanya hivyo
kwa moyo mmoja uliokuwa umeibeba imani thabinti
kwa mungu wake.
"Nimekuelewa Loveness mpenzi wangu, lakini kuusu
Dada yangu itakuwaje, nahitaji naye aokoke,
akombolewe kutoka katika hiyo mikono ya shetani"
"Usijali Faustin, Mimi niko pamoja na wewe,
naomba twende kwanza nyumbani ujipange vizuri,
tukifika kule tutaungana tutafanya maombi ambayo
yatamsimamia na hatoguswa na mikono ya shetani"
Loveness alisema.
"Sawa"
Faustin alijikuta anakubari. Walilala ili kuupumzisha
usiku, asubuhi na mapema waliamka wakajindaa
kwa ajili ya safari ya kuwapereka mwanza. Baada ya
kuyamaliza maandalizi, waliondoka kuiwahi meli ya
asubuhi ya kuwapereka Mwanza.
Mpaka kufikia mida ya saa saba walikuwa tayari
washafika mwanza, na uzuri hata gari la Faustin
waliondoka nalo hawakuliacha, hilo ndilo walitumia
kama usafiri Kwenda nyumbani kwa Loveness.
Nyumbani kwa Laveness ilikuwa kirumba ndiko
alikuwa akiishi yeye na Mama yake pamoja na
mdogo wake.
Mapokezi ya Faustin yalikuwa ya pekee sana katika
familia ile, hata mama yake Loveness alijisikia
Faraja sana kumuona Faustin mwanaume ambaye
wao walikuwa wakisimuliwa na Bint yao kuwa ndiye
mchumba wake.
"Pole sana Baba!"
Mama Loveness alisema. Baada ya Faustin kufika
pale na kuanza kuzungumza naye. Kauli hiyo
ilimwacha Faustin katika maulizo, hakutegemea
kabisa kama mama Loveness naye alikuwa anaujua
ukweli.
"Nishapoa mama"
Faustin aliitikia kiunyonge sana huku akiona aibu.
"Usione aibu mwanangu, hivyo huwa vipo katika
maisha ya Mwanadamu. Matamanio yakija huwa
yanakuja kushinda au kushindwa. Matamanio
yakikushinda lazima yatakufanya ufanye mambo
ambayo lazima ulimwengu ukushangae na kuumia,
lakini matamanio yakishindwa huwa ayaachi athari
mbaya Bali yanakuachia athari nzuri yakuridhika na
ulivyo barikiwa na mungu(vya halali)"
Mama Loveness alimwambia Faustin.
Walizungumza mengi sana, mazungumzo ambayo
yalimfanya Faustin kuwa na imani ya kweli kwa
mungu wake. Ni kweli alikuwa kaisha fanya mauaji
lakini kwa msaada wa Loveness alijikuta
anajichomoa kwenye jeshi la kumtumikia shetani.
Nguvu ya mungu ilikuwa msaada sana kwake.
Mchana waliongea usiku ulipofika kabla hawajalala
familia mzima waliungana wakaanzisha maombi
kwa imani yao ya kirokore.
Baada ya kufanya maombi ambayo yaliwachukua
lisaa lizima Faustin na Loveness usiku wakiwa
Chumbani kwao Kama wachumba ambao
walitegemea kuifunga ndoa yao muda si mrefu
walianza kuzungumza kwanza, mazungumzo yao
yalikuwa ni Yale ambayo Faustin alitaka kuyajua.
Loveness alijuaje kuwa Faustin ni mtumwa wa
Shetani.
"Taarifa za kupotea kwa wale wanawake ambao
mimi mwenyewe nilikuwa nao, mkawanywesha
pombe ninaona, ndizo zilikuwa za kwanza kabisa
kugundua kuwa ninyi ni wachafu, halafu maswali
yako uliyoniuliza nayo pia yalisababisha nifikiri sana.
Ila sasa kilichoniamsha zaidi ni taarifa za kupotea
kwa watu tena wote wa kike kila Mwezi ndani ya
Ukerewe, wengine wakiwa wake za watu, halafu
idadi ikiwa ni ilele watu wanne, moja kwa moja
nilijua wahusika ni ninyi, tena hapo niliamini hata
Mimi ni mungu tu alinilinda ndiyo maana ulishindwa
kuniua. Kuusu uzinzi na kuwalala wake za watu ni
Tabia yako tu, hata hawo wanawake mliokuwa
mnawaua lazima mlianza kufanya nao mapenzi.
Hicho ndicho kilinipa mwanga lakini naamini ni kwa
uwezo wa mungu. Niilijitahidi sana kukuombea ili
ujitoe kwenye hilo Jeshi la shetani. Inauma Faustin
kuendelea kuua watu tena wanawake. Mlianza na
wanne, mala nane mala kumi na mbili mala ishirini
na bado mnaishi unazani mngewatowa wengine
wapi? kama mnaowaua kila mwezi lazima
wangeisha. Baada ya kuwamaliza wengine, baadaye
mngeamia kwa Ndugu zenu, nao pia mngeua mala
mama zenu nao pia mngeua"
Laveness alisema. Maneno yake yalimuingia sana
Faustin machozi yalimtoka akajikuta anapiga magoti
chini na kuanza kumlilia mungu amsamehe kwa
uwovu wake mkubwa, dhambi kubwa ambayo
malipo yake kwa Mungu ni kutupwa Motoni bila
hata kuulizwa.
******
Usiku huu tena kwa Mama Fatuma mambo yalikuwa
ni magumu kweli kweli, Mama yule alikuwa amelala
usingizi akiwa hana lile wala hili mala mlango wake
ulianza kugongwa kwa fujo halafu kama vile
kulikuwa na Sauti ya mtu ikilia kuomba msaada.
Ndani ya usiku wa Giza mama yule alishindwa
kulala akashuka kitandani moja kwa moja bila hata
kuiwasha taa yake ya Chemri wala tochi yake kwa
ajili ya mwanga, Mama Fatuma bila kuogopa
akaongoza mpaka mlangoni, akalishika komeo la
mlango akaufungua mlango kisha akatoka inje.
Ndani ya Giza hilo hilo, inje alimkuta mwanamke
mtu mzima, mama yule alikuwa akimuonesha
Mama Fatuma Ishara kuwa amfuate alikokuwa
anaelekea usiku huo. Giza lilikuwa ni Nene kweli
kweli, kilichokuwa kinaonekana ni baadhi ya mauwa
ya njano yaliyokuwa kwenye kitenge chake
alichokuwa amejifunga kwa ajili ya kulala
kwasababu ya joto la kipindi hicho. Mama yule
mjane aliendelea kusonga mbele na yule nwanamke
alizidi kumuongoza kuelekea asikokujua usiku huo
wa Giza Nene. Aliendelea kutembea mpaka ikafikia
sehemu ambako ilikuwa ni nyumba kubwa mama
Fatuma akaongozwa kuingia ndani ya Jumba hilo,
naye bila kuogopa aliingia ndani ya Jumba hilo.
Jumba lile lilikuwa linatisha sana, ndani giza lilikuwa
nene zaidi ya giza la inje, lakini mtu aliyekuwa
anamuongoza alikuwa anamuona vizuri tu,
kwasababu yeye alikuwa amevaa nguo nyeupe ya
kulalia.
Waliingia mpaka Chumbani. Baada ya kufika
chumbani Mwanamke aliyekuwa anamuongoza
alikisogeza kitanda kutoka pahara pake, kumbe pale
kulikuwa na shimo, kwa maana hiyo kitanda
kilikuwa kimelificha shimo hilo.
"Chungulia ndani ya Shimo hili"
Hiyo ndiyo ilikuwa sauti ya kwanza ya mwanamama
aliyekuwa inamuongoza.
Naye kama vile alikuwa ajielewi, alichungulia ndani
ya Shimo hilo alikutana na Miili ya watu kama
wanne ikiwa inanuka hatari, Mama Fatuma aliinuka
haraka, aliogopa hata kuendelea kuchungulia ndani
ya shimo ilo.
"Hicho ndicho anachokifanya Mjomba Jumanne kwa
wanawake Mama, kumbuka kuwa akiwamaliza
wengine atahamia kwako mama"
Muda huo huo Mama Fatuma iliisikia sauti ya
mwanaye ikimsemesha, alipogeuka kweli alimkuta
Bint yake amesimama akimwangalia.
Vile vile alivyokuwa anamtokea katika ndoto akiwa
amekibeba kichwa chake tumboni.
"Tuondoke"
Sauti ya mwanamke aliyekuwa anamuongoza
kwenda katika jumba hilo ilisikika tena
ikimsemesha.
Mama fatuma lishituka sana, muda huo Bint yake
hakuwepo tena.
walitoka ndani ya Jumba lile kurudi walikotoka,
lakini wakiwa bado hawajatoka ndani ya uwanja wa
Jengo lile mala Jumanne alitokea mbele yake akiwa
mwenye hasira mkononi akiwa kashikilia kisu kikari
sana.
Bila kujali Jumanne alikiinua kisu chake kwa ajili ya
kumchoma nacho, Mama Fatuma alipiga kelele
akajikuta anashituka usingizini.
napo alikuwa akiota lakini cha ajabu alikuwa
hayumo ndani Bali inje ya nyumba tena amelala
chini.
Alishituka sana Mama Fatuma, alitamani apige
kelele za kuomba msaada lakini alishindwa, ulikuwa
ni usiku bado, alijizoa taratibu na kuusogelea
mlango kuufungua aingie ndani. Alipougusa mlango
kweli alikuta mlango haujafungwa na komeo la
ndani, aliingia ndani haraka na kuufunga mlango
moja kwa moja mpaka kitandani. Alipofika
kitandani alitumia mikono yake kuitafuta tochi yake
aliyokuwa anapenda kulala nayo kitandani, aliipata
akaiwasha kisha akakachukua kiberiti akaiwasha
chemri yake.
Baada ya kufanya hayo alianza kuwaza na kuwazua.
"Ni ndoto ya aina gani hii, au ni kweli"
Mama yule alijisemea mwenyewe.
Ile ndoto kwakweli alishindwa kuielewa, kama
ilikuwa ni ndoto kweli kwanini alijikuta inje, na kama
haikuwa ndoto mbona Jumanne hakumuua wakati
alikuwa na kisu mkononi na alikinyanyua kabisa kwa
ajili ya kumchoma. Vitu hivyo viwili bado vilimpa
utata mama wa watu.
"Ni kweli mlango niliiufungua mimi nikatoka, na
nakumbuka usiku niliufunga Mimi mwenyewe"
Mama Fatuma alijisemea tana. Alizidi
kuchanganyikiwa kwa ndoto yake. Je ilikuwa ni
ndoto kweli? huo ndio ulikuwa mgogoro kifuani
mwake.
Katika kuitafakari ndoto hiyo au tukio hilo
aliikumbuka na ndoto ambayo ali-iota alipolala
kwenye kenopi ya nyumba ya Kaka yake, aliota
ndoto ya mwanaye akimwambia kuwa "Mama sitaki
nikutese kwasababu ya Mjomba, Mjomba ni mbaya,
alianzia kwangu kisha kwa Baba sasa atahamia
kwako" Mama Fatuma aliyakumbuka maneno ya
Mwanaye aliyomwambia ndotoni, kisha
akayaunganisha na aliyokutana nayo kwenye hiyo
ndoto ya siku hiyo akajikuta anapata picha kuwa
Jumanne ni Shetani na ndiye anayewaua watu ndani
ya Ukerewe, akiwemo mwanaye na mumewe,
Mwanaye hakuwa Afrika kusini kama alivyokuwa
ameambiwa na Jumanne.
Usiku huo huo mwanamke yule aliapa kuamkia
Nansio kesho asubuhi.
Kulipokucha Kweli Mama Fatuma aliwaita wanaye
wawili Sadick na Sauda na kuwapa Maelekezo ya
nyumbani kwani yeye alikuwa amejiandaa kwa safari
ya kwenda Nansio kwa mjomba wao. kwa bahati
nzuri siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumamosi, siku
ambayo haikuwa ya Shule, Kwahiyo Sauda na
Sadick walikuwepo tu Nyumbani. Mama alifanya
maandalizi ya safari ya kutoka huko kazilakanda
mida ya saa mbili za Asubuhi kwa Piki piki ambayo
ilimchukua lisaa tu akawa amefika Nansio.
Nyumbani kwa Kaka yake alikuwa hapajui lakini
alikuwa anaujua mtaa ambao Kaka yake aliokuwa
anaishi. Alipofika kwenye mtaa huo aliulizia
nyumbani kwa Jumanne ni wapi, kutokana na
Umaarufu wao ndani ya Nansio na isitoshe nyumba
zao zilikuwa eneo moja tu, watu walimuelekeza kwa
Jumanne.
Nyumba ya Jumanne haikuwa na mlinzi wa Getini,
waliogopa kuwaweka hata walinzi kwa Hofu ya siri
zao kugundulika. Kwa bahati nzuri hata mlango
mdogo wa kwenye Geti ulikuwa wazi. Ndani ya uzio
wa ukuta uliokuwa umelizunguka Jumba la
Jumanne, Mama Fatuma alikuta kuna Magari kama
manne yamepaki. Yeye hakujua hilo lakini ndani
kulikuwa na kikao kinaendelea cha watu watatu.
Kikao hicho kilihusu kutoweka kwa Mwenzao
ambaye ni Faustin. Wakiwa hawana hili wala lile
mlango Uligongwa.
"Nani huyo ebu chungulia kwanza"
Jumanne alimuomba Mgusi achungulie mlangoni
kupitia kwenye tundu la lenzi lilikuwa kwenye
mlango.
"Ni Dada yako"
"Dada!"
Jumanne alishituka baada ya kuambiwa kuwa ni
Dada yake, Asubuhi kama saa nne na dakika kumi
na nane Jumanne aliiangalia saa yake ya ukutani.
Hakuamini kabisa kama ni Dada yake ndiye kaja
kwake. Jumanne mwenyewe alisimama kisha
akausogelea mlango na kuufungua.
Hali yaliyomkuta nayo Dada yake, ilimshitua sana
Jumanne, Mama Fatuma alikuwa kaukunja uso wake
kwa hasira.
"Dada karibu ndani"
Jumanne alisema kwa upole
TAENDELEA.
Usipitwe na hadithi hii kipindi kijacho.
 
SEHEMU (17).
ILIPOISHIA.
Jumanne alishituka baada ya kuambiwa kuwa ni
Dada yake, Asubuhi kama saa nne na dakika kumi
na nane Jumanne aliiangalia saa yake ya ukutani.
Hakuamini kabisa kama ni Dada yake ndiye kaja
kwake. Jumanne mwenyewe alisimama kisha
akausogelea mlango na kuufungua.
Hali yaliyomkuta nayo Dada yake, ilimshitua sana
Jumanne, Mama Fatuma alikuwa kaukunja uso wake
kwa hasira.
"Dada karibu ndani"
Jumanne alisema kwa upole.
SONGA NAYO.
"Jumanne sijaja hapa kwa ajili ya hili Jumba lako
au haya magari yako, na sijaja kwa ajili ya msaada
wowote kutoka kwako"
Mama Fatuma alisema, machozi ya maumivu
yalianza kumdondoka.
"Dada kwani kuna nini?"
Jumanne alimuuliza Dada yake.
"Jumanne kama ni uchungu niliusikia mimi, Mimi na
mume wangu hatukuhitaji msaada kutoka kwako
Bali wewe ndiye ulijipendekeza, ninachokihitaji
kwako ni kimoja tu, namuhitaji mwanangu,
namuhitaji Fatuma wangu akiwa mzima na akiwa
anatembea, namtaka mwanangu kabla sijakuitia
watu hapa"
Mama Fatuma alizungumza tena. Maneno yake
yalionesha tosha kuwa alikuwa tayari kwa lolote
lakini shida yake kubwa ni mtoto wake, mtoto wake
mkubwa aliyekuwa anampenda kwa dhati"
"Dada mbona unazungumza vitu ambavyo sivielewi.
Fatuma mbona yupo na anaishi yuko Afrika kusini
anasoma"
Jumanne alizidi kumdanganya Dada yake.
"Wewe Shetani ukunisaidia kuzaa, uchungu niliumwa
Mimi, mwanangu Mimi hakunishinda Jumanne,
namuomba hapa we shetani namuomba mwanangu"
Mama Fatuma alizidi kuongea kwa sauti kubwa
huku akilia.
"Dada tafadhali naomba uingie ndani kwanza
tuwekane sawa"
Jumanne alisema.
Mpaka hapo Mama fatuma alikuwa kaisha kaa chini
akilia kwa maumivu. Ndani ya Jumba la Jumanne
hakutaka kuingia, Uchungu wa mwana ulikuwa kama
unajirudia tumboni mwake.
"Jumanne hakika nakuapia nakupa dakika mbili
unambie mwanangu yupo wapi kama si hivyo, tone
la damu litajilipa hapa labda uniue na Mimi. Kabisa
Niue Mimi la sivyo namuhitaji mwanangu"
Mama Fatuma alizidi kugomba. Hata Mgusi na
manyege waliokuwa ndani nao walitoka, kelele za
Mama Fatuma walizisikia. Hawa hawakuwa na cha
kujadilia walijua kabisa kuwa Mama Fatuma
atawaletea makubwa, walimsogelea wakamkatama
kwa nguvu ya kiume, wakamziba mdomo asiongee
lolote au kupigs makelele kisha wakamuingiza
ndani.
Jumanne naye aliingia ndani.
Baada ya kufika ndani walimfunga tena miguu na
mikono. Uchungu wote wa mama Fatuma, uliishia
kwenye kamba.
"Jumanne kila kitu kipo wazi, unazani hata huyo
Fatuma utamtolea wapi?"
Manyege alisema. Jumanne alibaki kimya, hakuwa
na Jibu la kumjibu Rafiki yake.
"Mwambie tu kuwa Fatuma hayupo tena katika
Aridhi hii, kaisha kufa"
Mgusi alisema.
Kwakuwa Mama Fatuma alikuwa palepale lakini
kafungwa mikono na miguu halafu mdomoni akiwa
amejaziwa mavitambaa na wameziba kwa plasta
lakini alikuwa akisikia kila lililokuwa linazungumzwa.
"Jumanne hakuna njia nyingine Zaidi ya kumuua
huyu mama. Hiyo ndiyo njia ya pekee kama bado
unataka sisi tuishi"
Manyege alisema tena.
Alichokisema Manyege ndio ilikuwa njia pekee ya
kufanya kwa ajili kuziepuka miondamo ya Mama
Fatuma.
"Naombeni asife kwanza Dada yangu, tumuweke
humu humu ndani mpaka watu wasahau"
Jumanne alisema. Yani mpaka kufikia hapo Mama
Fatuma alikuwa kaisha poteza kumbukumbu
kwasababu ya alichokisikia kutoka kwa watumwa
wa Shetani, uthibitisho alikuwa kaisha upata kabisa
kuwa Mwanaye kaisha uliwa.
Walimbeba wakampereka kwenye kilichokuwa na
shimo na kumwacha humo. baada ya kumaliza
walienda kuongea na mashetani yao kwenye
Chumba cha Siri ambacho kilikuwa kimetengwa kwa
ajili ya kazi hiyo. Kwenye Chumba hicho waliende
kuuliza kuusu Faustin.
"Faustin kawa msaliti, tulimkataza lakini yeye
kaendelea kuwa karibu na yule mwanamke,
kilichobaki tunahitaji ninyi mkamuuwe kwa njia
yeyote mtakayoiona ninyi, na msipofanya hivyo
lazima mtalipa malipo makubwa kuliko ya hawali.
Malipo yake yatakuwa kwamba, lazima kumtoa
mzazi wenu mmoja kati ya Baba au mama hasa
hasa mama"
Sauti ile ile ambayo huwa inasikika kila
wanapokuwa wanaongea na mashetani ya Kisiwa
cha Shetani ilisema baada ya kuomba kuzungumza
nayo.
Hawakuishia kuuliza habari za Faustin tu, waliuliza
tena kuusu Mama yake na Fatuma wamfanye nini,
Jawabu lilikuwa ni moja ambalo lilifanana kabisa na
kama ambavyo Mgusi na manyege walivyo mshauri
Jumanne kumfanya Dada yake. Kwa maana hiyo
Mama Fatuma naye alistahili kufa.
"Baada ya kumaliza kuongea na mashetani ya kisiwa
cha Shetani, hakuna ambaye alitaka tena kuongea na
mwenzake. Manyege na Mgusi walitoka nyumbani
kwa Jumanne na kurudi kwenye Majumba yao
kujipumzisha, walikuwa na mawazo sana tena sana
tu.
" Dah! naogopa hata kuishi katika Dunia hii, mambo
yanazidi kuniwia magumu kabisa, nimeisha Fanya
mauaji ya watu zaidi ya watano, Bado natakiwa niue"
Manyege alijiwazia mwenyewe baada ya kufika
kitandani, hata Dada yake ambaye tayari alikuwa
kaisha mfanya mkewe kwa ajili ya mimba ya mtoto
wa kupereka katika kisiwa cha Shetani, alimuona
kaka yake hayuko katika usawa. Ndipo alipomfuata
Chumbani kumuuliza.
"Mgusi, umekuwaje mbona una mawazo sana?"
"Ebu niache kwanza, Fanya mambo yako!"
Mgusi alimjibu Dada yake Jibu moja la nguvu.
Dada yake aliumia sana kujibiwa vile.
"Mgusi nashukuru sana kwa jawabu lako"
Dada yake Mgusi(Meck) alisema kisha akatoka
chumbani mule kwa hasira na kumwacha kaka yake
aliendelea kuwaza.
Mawazo yalikuwa mengi sana kwa wanaume wale
watatu, kila mmoja alikuwa anajilaumu sana. Kila
walipokuwa wanajiuliza Faustin kawezaje kukimbia
na kujikinga kutoka kwenye mikono mibaya ya
Shetani, hawakupata majibu kabisa kwani wao
hawakuwa na wazo la kurudi kwa mungu, waliogopa
kuraruliwa kama alivyofanywa Said Rafiki yao
kipenzi ambaye alijiengua mwanzo kabisa baada ya
kuona masharti yote waliyopewa hayamfai.
******
Baada ya kumwacha kaka yake Chumbani Meck
alipitiliza mpaka Jikoni, alichokifanya kule alichukua
kisu tu kisha akajichoma tumboni, wala hata
hakufikiria uchungu wa kujichoma kisu. Meck alijiua
kwasababu alikuwa kaisha kuwa kama Shetani,
kitendo cha kufanya mapenzi na Kaka yake ndicho
kilimfanya ajichome, alikuwa anaishi kwa basi tu, na
ndio maana alipojibiwa vibaya na Kaka yake
hakuona tena umuhimu wa kuishi.
Baada ya kujichoma kisu, alipiga makelele ya
maumivu, lakini kelele zake hazikusikika Chumbani
alikokuwa kaka yake.
Akiwa kitandani, Mgusi aliisi kawa amemuuzi Dada
yake. Alitoka chumbani haraka haraka, akaanza
kumtafuta Dada, alianzia sitting room hakakuta
empty, akaenda Jikoni hata kabla hajaufikia mlango
Damu zilimshitua, kwani tayari zilikuwa zishatapakaa
eneo lote la Jikoni na zilikuwa zinaanza kutoka inje
ya chumba cha Jiko.
Mgusi alishituka sana akaufungua mlango haraka
sana.
Alichokikuta kilikuwa hakina vipimo vya ziada, zaidi
ya kusema kuwa Meck alikuwa kaisha fariki. Mgusi
hakuamini kabisa, aliona kama vile misara inazidi
kumwandama.
Alipiga kelele sana Mgusi, kelele zake zilikuwa si
Chochote mbele ya Maiti ya Dada yake, kilichokuwa
kimesalia ni kwenda kuuzika mwili wa Dada yake.
******
Naye pia akiwa na mawaza Jumanne aliingia
kwenye chumba ambacho walikuwa wamemuweka
Dada yake ambaye alikuwa kaisha poteza fahamu.
Jumanne alifika akapiga magoti mbele ya Dada
yake, kisha akaanza kumfungua kamba za mguuni.
Jumanne alikuwa amepoa sana.
"Dada naomba unisamehe kwa yote ambayo
nishakufanyia, ni kweli kabisa Fatuma niliua
mwenyewe na Mali hizi zote ni kwasababu ya Tone
la Damu ya Fatuma Mwanao. Nilimuua hata
mumewo, Mimi mwenyewe ndiye nilimchinja kwa
kutumia mkono wangu.
"Kwahio sina Ujanja Zaidi ya kutekeleza kila Jambo
kwasababu naogopa kufa, nahitaji nitimilize agizo
nililopewa. Watoto wako Mimi nitawalea hata
usijali" Jumanne alisema kisha akainama Chini ya
uvungu wa kitanda kilichokuwa chumbani humo,
akakichukua kisu kwa ajili ya kumchinja Dada yake,
kilikuwa ni kile kile Chumba cha Kuchinjia.
"Jumanne acha unachokifanya kiache ni kibaya,
acha kabisa usikifanye utakufa kwa mateso Zaidi
kama ukifanya hivyo"
Ilikuwa ni Sauti ya Mtu ikimsemesha Jumanne.
Sauti hiyo ilimshitua sana kwani alikuwa
anaitambua.
"Jumanne acha kabisa kulifanya jambo hilo acha
utakufa acha kabisa"
Sauti ilisikika tena kwa mala ya Pili masikioni mwa
Jumanne.
"Faustin,........Faustiniiii!"
Jumanne aliliita jina la Faustin kwani sauti iliyokuwa
inasikika ilikuwa ni ya Faustin.
Jumanne aliangaika sana kugeuka uku na kule
kumtafuta Faustin lakini alikuwa amuoni.
Sauti ya Faustin ilizidi kumsumbua Jumanne, alizidi
kusikika na kusikia Masikioni mwa Jumanne. Sauti
hiyo ilipozidi kumtesa Jumanne alitoka chumbani
mule kama vile aelewi chochote mpaka Chumbani
kwake kitandani, akiwa kitandani Jumanne Bado
alipata Shida sauti ilizidi kumtesa na kumtesa
Masikioni mwake ikaendelea kusikika, Chumbani
akashindwa kukaa, akatoka huku akiyumba yumba
kama mlevi aliyebugia pombe aina ya Gongo. Alizidi
kutoka Mpaka inje kabisa ya Geti ya Nyumba yake,
hali ikamuwia ngumu, akaanza kulia mwenyewe
kama mtoto huku akiwa anazidi kutembea kusogea
kwenye makazi ya watu wengi. Watu nao
walipomuona akilia huku akitembea walianza
kumfuata ili kumuuliza analilia nini. Watu walipo
mfikia walimuliza lakini Jumanne hakuzungumza
Chochote zaidi ya kulia. Alizidi kusogea mpaka
setani ambako watu walikuwa ni wengi zaidi akakaa
chini akazidi kulia, watu nao walizidi kujazana
kusikiliza kilichokuwa kinamliza mtu mzima
mwenye mipesa yake.
Taarifa zake zilimfikia rafiki yake Manyege; kidogo
muonekano wa Manyege ulikuwa Tofauti na
wengine, yeye alikuwa na unafuu, alikuwa hawazi
sana kama wengine. Manyege alipozipata taarifa
hizo naye alitoka kwake na kuzipereka kwa Mgusi.
Alipofika kwa Mgusi Manyege alichoka na kuchoka,
kwani limkuta Mgusi vile vile alivyo kaa na mwili
wa Dada yake. Muda huo damu zilikuwa zishaanza
kugandana kwenye nguo za mgusi.
"Mgusi ndugu, wewe mwenyewe ndiye umeua?"
Manyege alimuuliza mwenzake, lakini swali lake
halikujibiwa, Mgusi alibaki kimya kimya kama vile
asikii kabisa alichokuwa anasemeshwa na
Mwenzake.
"Mgusi mambo yashaanza kuaribika, amka mtaani
huko kumeharibika Jumanne analia tu aeleweki
analilia nini anaweza hata kututaja, maana
inavyosemekana ni kwamba jamaa kachanganikiwa
kabisa, ajielewi na ajielewi"
Manyege alisema huku akimtikisa Mgusi. Richa ya
kutikiswa bado Mgusi hakuzungumza Chochote
aliendelea kukaa kimya, hali hiyo ilizidi
kumshangaza sana Manyege. Akazania labda Mgusi
nae kaisha fariki lakini kope za macho zilikuwa
zinacheza cheza, pia alikuwa akihema kabisa. Baada
ya kuona kuwa ajibiwi halafu mwenzake yuko pale
ni mzima, Manyege aliamua auchukua mwili wa
Meck auweke pembeni na kumnyanyua mwenzake.
Alijitahidi sana kumsimamisha lakini Mgusi alikuwa
hana hata uwezo wa kusimama.
"Mh! Hii sasa hatari kama ni kwisha ndiyo huku"
Manyege alijisemea, Muda huo huo alisikia
makelele ya Watu huku wakisema piga huyo piga,
piga kabisa hawo wauawe, dhambi zake zilipwe
kwa tone la Damu yake"
Kelele hizi zilimshitua sana Manyege ndani ya
Jumba la Mgusi. Manyege alichungulia Dirishani
kuona nani anapigiwa kelele. Alichokiona
kilimshutua sana, akaanza kutapatapa ndani ya
nyumba ya Mgusi, kwani aliona Jumanne ndiye
anashushiwa kipigo na Wanaichi wenye hasira kali
huku wakiongozana naye kurudi nyumbani kwake.
Nguvu na ujasiri wa kuendelea kumsaidia Mgusi
zilimuhishia kabisa manyege, ndipo alipotoka mbio
kurudi nyumbani kwake haraka. Alipofika hakuwa na
muda wa kupoteza alifika akamvuta mkamshika
mkono Dada au mpenzi wake, wakatoka inje mpaka
kwenye Gari na kuanza safari ya kuikimbia Nansio.
******
Wananchi wenye Hasira Kali tayari walikuwa
washamfikisha Jumanne Nyumbani kwake,
hakukuwepo cha mwenyekiti wa kijiji wala cha
Askari polisi aliyejitokeza kumtetea Jumanne, na
wangejitokeza mbele ya watu wenye hasira zile
wangeunganishwa.
"Tunajua pale hukutaja vyote naomba urudie na
utwambie ambavyo ulituficha?"
Ilikuwa ni sauti ya mwanaume mmoja bausa
ikimuuliza Jumanne, kidume yule alikuwa amejazia
kweli kweli.
"Nilimuua mtoto wa Dada yangu ili kupata pesa"
"Kingine"
Wanawake ambao Walikuwa wanapotea ndani ya
Nansio humu nao tuliua sisi"
Jumanne alisema, hio ilikuwa mala ya Pili
kuyatamka maneno hayo, mala ya kwanza
alijiropokea mwenyewe baada ya kufika kwenye
mkusanyiko wa watu
"Ulikuwa unashirikiana na nani?"
Aliulizwa tena.
"Nilikuwa nashirikiana na Wenzangu wawili Manyege
na Mgusi "
Jumanne alisema. Alimsahau Faustin kabisa
kumsema kwenye kundi lile la watu wenye Hasira.
"Na Faustin?"
Uliulizwa tena kuusu Faustin.
"Huyo alikuwa ajui Chochote kuusu mauaji ya watu,
alikuwa anashirikiana nasi kwa vingine tu lakini
alikuwa auwi kabisa"
Jumanne alisema.
 
SEHEMU (18)
ILIPOISHIA.
"Nilikuwa nashirikiana na Wenzangu wawili Manyege
na Mgusi "
Jumanne alisema. Alimsahau Faustin kabisa
kumsema kwenye kundi lile la watu wenye Hasira.
"Na Faustin?"
Uliulizwa tena kuusu Faustin.
"Huyo alikuwa ajui Chochote kuusu mauaji ya watu,
alikuwa anashirikiana nasi kwa vingine tu lakini
alikuwa auwi kabisa"
Jumanne alisema.
SONGA NAYO.
Faustin anamungu wake Hakutajwa kabisa kama
naye alikuwa muhusika katika mauwaji.
"Jamani ameficha kitu?"
Kidume kilichokuwa mbele kama kiongozi
kiliwauliza, mkononi kilikuwa kimeshikilia panga.
"Bado kaficha hajatwambia ni wapi walikuwa
wanawapereka baada ya kuwaua"
Wananchi walisema.
"Umesikia Kumbe bado hujasema wapi huwa
mnawapereka"
Kidume kile kiliinama na kumuuliza Jumanne.
"Tulikuwa tunawakata matiti na kuyaperekea
mashetani wa Kisiwa cha Shetani. Huko ndiko
tuliyachukua madini, na ndiko tulimchinjia Mtoto wa
Dada yangu. Yeye yumo humo ndani, naye nilitaka
kumuua, Mimi mwenyewe ndiye nilimuua na Mume
wake"
Jumanne alisema na alizidi kuufungukia ukweli.
"Aaaaaa!"
Watu hawakuamini kabisa kabisa alichokizungumza
Jumanne.
"Sasa baada ya kufanya hivyo miili yao mlikuwa
mnaipereka wapi?"
"Humo ndani ya majumba yetu na Guest pamoja na
Hoteli yetu kuna mashimo marefu ambayo huwa
tunaitumbukiza miili tukiisha maliza kukata maziwa"
Jumanne alisema tena kipindi hiki hakuacha hata
kimoja, aliusema ukweli wote, ukweli ambao kila
mtu alistaajabu sana, wengine wakawa wanajiuliza
kaupata wapi Ujasiri wa kuweza kumchinja mtoto
wa dada yake, Mume wa Dada yake halafu pia
alitaka kumchinja Dada yake.
Baada ya ukweli wote Jumanne alinyanyuliwa na
Bausa lile mpaka ndani akawaoneshe shimo hilo
lilivyo. Waliingia mpaka kwenye Chumba
kilichokuwa na Shimo, bado Mama Fatuma alikuwa
ndani ya chumba hicho ajitambui kabisa hata
kamba alizokuwa amefungwa mikononi zikiwa bado
zimemfunga. Kitendo kile kiwasikitisha sana watu
waliofanikiwa kufika chumbani, walimfungilia Mama
Fatuma kamba alizokuwa amefungwa kisha
wakamtoa inje kwenye upepe na kuanza kumpepea
kama angeweza kurudi katika hali ya kawaida.
Ndani Chumbani walikisogeza kitanda pembeni,
walipokisogeza walikuta kuna visu viwili vikubwa na
vilikuwa ni visu kweli kweli.
"Mh! Kweli ninyi mlikuwa ni wauwaji"
Mwanaume mmoja alisema.
Haya na hilo Shimo liko wapi?"
Jumanne aliulizwa, Kwa Jinsi mfuniko wa shimo lile
ulivyokuwa umedizainiwa kama sura ya vigae
vilivyokuwa ndani ya Chumba hicho, ilikuwa si rahisi
kwa mtu kuiligundua kwa kukurupuka, umakini
uliitajika sana ili kuligundua shimo hilo.
Alipoulizwa alionesha na mwenyewe akalifungua.
Alipolifungua shimo hilo, kidogo watu wakimbie
ndani ya Chumba hicho ilifumuka harufu nzito kweli
kweli kutoka katika miili ya Marehemu.
Watu waliziba pua zao ilimradi tu wapate
kuchungulia ndani ya Shimo hilo ili wapate
kushuudia urefu wa shimo hilo na miili mingapi
ilikuwemo. Ndani ya shimo hilo kulikuwa Giza,
ilikuwa si rahisi kuona mwisho wa shimo hilo bila
mwanga. Watu walifuata tochi zao kwenye miji zao
kwa ajili ya kumlikia ili wapate kushuudia ndani ya
shimo. tochi moja nayo ilikuwa haitoshi walitumia
tochi zaidi ya tatu, walichokutana nacho mule kweli
walisikitika sana, miili ya watu ndiyo ilikuwa
ikionekana ikiwa inatembelewa na Funza tu,
kwakweli watu waliumia sana, hapo Hapo baadhi
wakajigawa wengine wakaenda nyumbani kwa
Manyege na kwa Mgusi,
Haikupita hata Robo saa Mgusi naye akaletwa pale
pale kwa Jumanne, akaungaunganiswa. Mgusi naye
tayari alikuwa na kesi mbili za kujibu kwasababu
alikutwa na mwili wa Dada yake, ukiwa na kisu
tumboni kwa maana hiyo watu walijua moja kwa
moja kuwa yeye ndiye aliyeua. Halafu kwa Mgusi
watu hawakusumbuka kabisa kumkamata kwani
mpaka anakamatwa yeye bado alikuwa yupo kama
zezeta. Watu walijikusanya wengi sana nyumbani
kwa Jumanne. Japo kuwa viwanja vyao vilikuwa
vikubwa havikutosha watu kuingia ndani ya uzio wa
ukuta uliokuwa umelizunguka jengo la Jumanne,
hivyo watu walipanda juu kwenye ukuta wakakaa ili
wapate kuwashuudia watumwa wa shetani. Kama
kawaida hata waandishi wa habari nao walikuwa ni
miongoni mwa watu waliokuwepo kwenye tukio hilo
wakichukua taarifa zao. Police hakurusiwa kusogea
pale, watu walikuwa tayari wapigwe mabomu ya
machozi lakini watu wao wawafaidi wenyewe.
Manyege hakupatika kwake kwa muda huo lakini
watu walijua kabisa kakimbia. Kukimbia kwake
hakukuwa na tiketi ya watu kumwacha. Kila mmoja
alisema.
"Ndani ya Ukelewe hii utaenda wapi Shetani
manyege, utakamatwa kabla hujafika popote" muda
huo waliwapigia simu watu wa sehemu tofauti
katika vijiji vilivyokuwa Jirani na Nansio ili waanze
kumsaka, hasa hasa waliopewa taarfa walikuwa ni
dareva Bodaboda. Kwani hata taarifa za kukamatwa
zilichelewa, mule mule ndani ya Nansio alikamatwa
hata kabla hajaivuka.
Baada ya kukanatwa naye alishushiwa kipigo cha
maana kisha akaletwa kwa wenzake. Bahati mbaya
zaidi muda huo huo Dada yake Jumanne (mama
Fatuma) aliamka kutoka katika kupoteza fahamu.
Alipo amka alishangaa kukuta mkusanyiko mkubwa
wa watu wengi nyumbni kwa kaka yake.
Hakiamungu mwanamke yule alikuwa Kama vile
ameshituka kutoka usingizini baada ya kuota ndoto
kama vile mwanaye anachinjwa, alipiga kelele za
kumuomba mwanaye huku akilitaja jina la kaka yake
amrudishe mwanaye. Mama Fatuma alijikuta
anapiga makelele mengi huku akisogea alipokuwa
kaka yake, alikuwa akitembea huku akiyumba
yumba, kwasababu ya alichokuwa amekisikia kutoka
kwa watu wale kuwa mwanaye kaisha fariki kilimpa
hasira sana, alipomuona tena kaka yake, Mama
Fatuma kwa hasira alizokuwa nazo alijikuta
anaanguka chini mzima mzima kama mzigo wa
kumi ndiyo uliotupwa chini na kupoteza tena
fahamu kwa mala nyingine. Pale pale watu
wakambeba na kuanza kumpepea tena, lakini
haikusaidia hali yake ilionekana kuwa mbaya zaidi
ndipo walipochukua maamuzi ya kumkimbiza
hospitali pale Nansio kwa ajili ya matibabu.
Nyumbani kwa Fausitin Dada yake naye alikuwa
kaisha jiua kwa sababu halijihofu kuwa hata yeye
anaweza kuunganishwa kwenye kesi ya Mauwaji.
Watu walipokwenda ili kijithitibitishia walikuta Dada
mtu kaisha fariki, lakini walipofanya upekuzi napo
pia walilikuta Shimo ndani ya Nyumba yake, harafu
miili ya watu ikiwa mule mule. Mbali na hilo hata
Chumba cha kuwasiliana na shetani nacho
walikinasa.
"Hapa hakuna cha Faustin naye lazima akamatwe
aunganishwe."
Wanaume wa kazi waliokuwa wanaifanya kazi ya
upekuzi walisema.
Lakini kilichokuwa kinaleta utata ni wapi Faustin
yupo, muda huo huo walijaribu kufuatilia
wakagundua kuwa Faustin yupo Mwanza.
"Mwanza! Kumbe mwanza hapo tu ngoja
tutamuibukia"
Bausa aliyekuwa kama ndiye kiongozi wa watu wote
pale alisema. Baada ya kusema hivyo aliamuru
Jumanne na wenzake wafungwe kamba ndefu kisha
wawafunge kwenye pikipiki halafu wawavurute
kutoka nyumbani pale mpaka eneo la wazi kabisa
kwa ajili ya zoezi lingine lililokuwa linawafaa.
Walivutwa Mpaka kwenye eneo zuri lilokuwa pana
kisha wakafungwa kamba wote kwa pamoja, halafu
kilicho fuata kila mtu aliamuriwa achukue Jiwe
Dogo Dogo ambalo siyo zito lenye uzani kama
Nusu kilo kisha asogee na kuwaponda mpaka
watakapo kufa. Lilikuwa ni zoezi Gumu sana lakini
kwa watu wenye hasira lilikuwa ni Zoezi jepesi tu,
watu waliyakusanya mawe tena mengine yalikuwa
na zaidi ya kilo mbili na kusogea kuwaponda,
walipondwa na kundi kubwa la watu waliokuwa zaidi
ya Elfu moja na mia tano.
Kwa kiasi hicho kikubwa cha watu kilichotokea pale
ni Maiti tu ndizo zilisalia. Lakini bado watu
hawakurizika walikusanya kuni na matairi ya kwenye
magari yao yakachomolewa kisha wakawakunjia
kwenye hayo hayo matairi, wakawamwagia mafuta
wakawaunguza. Watu waliamini kuwa bila
kuwaunguza watu kama wale wanaweza kurudi tena
katika Dunia na kuyafanya waliyokuwa wanayafanya.
"Bado Faustin ajiandae lazima naye akipate
kilichowakuta wenzake"
Bausa aliyekuwa anawaongoza wenzake alisema.
Baada ya kumaliza kuuwasha moto, watu waliamia
tena kwenye majengo ya watu wale nayo
yakawashwa moto, palikuwa hapatoshi ndani ya
Nansio. Walibomoa kila kitu kilichowahusu watu
wale, Hoteli, majumba yao, Magari yao, maguest
yao, hata ambayo yalikuwa yamesambaa sehemu
zingine nao yaliunguzwa, mitumbwi na makokoro
yao ya kuvulia dagaa navyo viliunguzwa ndani ya
Nusu saa.
Kufikia mida ya saa nane kilichokuwa kimesalia
kwenye vichwa vya watu ni hadithi tu kuusu vifo vya
Jumanne na timu yake.
Kwa bahati mbaya kilichotokea usiku wa siku hiyo
ni kwamba Mama Fatuma alifariki. Kesho yake watu
walizipokea taarifa za kifo cha mama huyo kwa
masikitiko makubwa sana, hawakuamini kama kweli
mama yule alifariki, iliwauma na ikawauma sana,
tena kilichowauma watu sana ni kwamba kifo chake
kilisababishwa na ushetani wa kaka yake.
"Mungu ailaze roho yake mahara pema peponi"
"Amiin, kaacha watoto wawili wa kike na wakiume"
"Mimi kaniuma sana Mama Fatuma, kwakweli
alikuwa mwanamke mwenye moyo wa aina yake"
Hayo yalikuwa ni baadhi tu ya mazungumzo ya watu
waliozipokea taarifa za msiba wa Mama Fatuma.
Yalikuwa ni maumivu makubwa hasa kwa watoto
wake Sadick na Sauda walipozipata taarifa za kifo
Cha mama yao.
Watoto wale walikuwa wanalia tu muda wote, hasa
Sauda yeye alizimia mala mbili katika siku hiyo,
Mama yao aliwaaga kuwa anaenda kwa kaka yao na
aliwaahidi kuwa angerudi siku hiyo hiyo lakini
kumbe alikuwa anaenda kufa. Watoto wale iliwauma
iliwauma.
Mbali na watoto wake hata Baba na Mama yake
ambao umri ulikuwa ushawaacha na walijaaliwa
kuwa na watoto hawo wawili Mama Fatuma na
Jumanne au Shetani.
Wengi sana waliudhulia katika mazishi ya Mama
Fatuma, Mama aliyewaumiza watu karibu wote
kwasababu kifo chake kilisabishwa na kudai haki
yake.
Kutokana na hasira ambazo watu walikuwa nazo
waliamua moja kwa moja wakapanda mitumbwi yao
wakaingia majini, moja kwa moja kuelekea mwanza
kumtafuta Faustin hawakuwa na mzaa kabisa,
kwasababu ushetani wao ndiyo ulio sababisha
kuawa kwa watu ambao hawakuwa na hatia.
Walikuwa ni kikundi cha watu zaidi ya amsini
waliokwenda mwanza kumtafutaFaustin. Watu wale
walifika mwanza salama. Taarifa za watu hao
Faustin alizipata vizuri sana hata kabla hawajafika
Mwanza, hapo faustin aliomba aende akawapokee
wakerewe wenazake.
"Faustin mpenzi wangu utauliwa"
Loveness alimwambia faustin kipindi faustin
anamwambia kuwa anaenda kuipokea timu
iliyokuwa imekuja kumsaka.
"Usijali loveness kipenzi changu, kama nikifa basi
mungu atakuwa ametaka kwasababu mimi nilikuwa
mfanya dhambi, kwahio dhambi zangu ngoja
zikalipwe kwa damu yangu, lakini kama mungu
hajapenda nitarudi na nitaishi na wewe"
Hilo ndilo jawabu ambalo Faustin alimwambia
Loveness kisha akaenda kuwapokea. Yeye ndiye
alikiwa wa kwanza kufika kirumba mwaloni.
Kweli fauatin alikuwa amejiandaa kuwapokea vizuri
tu. Watu kutoka Ukerewe walipo fika kirumba
mwaloni, Faustin aliwaona akawasogelea, ilimuuma
hata yeye lakini alilazimika ili kuilipa dhambi yake,
kwakuwa muda huyo alikuwa kaisha kuwa mrokore
safi tena ndani ya muda mfupi wa siku mbili.
Faustin akisogea kuwapokea watu wale, Loveness
naye alikuwepo pale ila mbali kidogo akimuombea
mchumba wake kwa mungu aweze kuepukika na
kifo kwani aliamini kabisa kuwa kaisha kuwa
mtumikiaji wa mungu. Richa ya kuwa Faustin
aliwasogelea watu wale na kuwasalimia tena kwa
kiruga cha kwao lakini watu wale walishindwa
kumtambua kabisa kama ni yeye badala yake wao
walimfanya msaada kwao wa kumtafuta Faustin.
Faustin mwenyewe alijishangaa kabisa, mpaka
akawauliza mnaye mtafuta mnamjua. Wao
wakasema ndiyo, hapo Faustin alipata ujasiri wa
kuwambia kuwa hakuwahi kumuona. Hiyo ndiyo
ikawa ponapona ya Faustin, imani yake ilimponya,
watu walimtafuta sana Faustin bila mafanikio,
Mwisho wakarudi zao Ukerewe wakiamini kabisa
kuwa Faustin huwenda alijiua.
Baada ya matukio hayo Faustin na Loveness
walimua nao kusafiri mpaka Ukerewe kwao na
Jumanne kwa ajili ya kuwapa pole. Kwa machungu
waliyokuwa nayo Faustin na Loveness walijitolea
kuwasaidia watoto wa Marehemu kwa hatua yeyote
ile ambayo wangeifikia. Maisha ya Faustin
yalibadilika yakawa kwa mungu kitu ambacho
kilisababisha hata ndugu zake kutomtambua kabisa,
alichokuwa anakifanya yeye aliwasaidia ndugu zake
na wazazi wake kwa moyo wake wote huku akiamini
siku moja mungu atawafunulia ukweli. IAMINI
IMANI YAKO ITAKUPONYA KWA MUNGU.
ALLAH YU PAMOJA NASI KWA NJIA NJEMA.
Mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom