Simulizi: Tafadhali baba usitufanye misukule

Sehemu ya 13

“Masalu kwa nini hutaki kumsikiliza baba”
“Nimsikilize kwa lipi?”
“Juu ya wewe kuwa na mwanamke.”
“Mna uhakika gani?”
“Sisi hatuna uhakika ila kasema mwenyewe.”
“Ninyi mna wapenzi?” Niliwauliza.
“Tunao.”

“Sasa mimi nazuiwa na nini?”
“Si unajua hali yako haitaki uwe na mwanamke?”

“Kwa hiyo kidonda niwe nacho mimi maisha mazuri muwenayo ninyi, sikilizeni kila mtu ataubeba mzigio wake mwenyewe.”

“Masalu utakuja kuijutia kauli yako.”
“Sijuitii mbona dada Monika hakuijutia na mkiniua na ninyi mnafirisika kazi kwenu.”
Maneno yangu yaliwazima mdomo waliondoka na kuniacha wakiwa hawana hamu na mimi.

Tokea siku ile nikawa adui yao mkubwa, niliwashangaa kunikasirikia mimi kuwa na mwanamke wakati wao walikuwa na kila kitu. Kama mateso ya kidonda nimeyakubali bado hawaridhiki walitaka nikose na raha za dunia.

Ukali wa baba ulipogonga mwamba na kumtumia mama kunibembeleza, nani msimamo wangu ulikuwa pale pale wa kukataa kulala na mwanamke.
“Masalu jihurumie usije kufa kama dada yako Monika.”

“Mama mkiniua nani atakayebeba kidonda, dada Monika alinieleza kuwa wote mliotaka kuwapa kidonga mizimu iliwakataa.”
“Ni kweli, lakini unatakiwa uionee huruma familia yako.”
“Mama ninyi hamnionei huruma, mimi nitawaonea vipi?”

“Kumbuka kama utaendelea kufanya kama usipokufa wewe basi utampoteza baba yako.”
“Mama kila mwanadamu hufa kwa ahadi yake na wala si kwa ajili yangu.”
“Kwa hiyo una mwanamke?”
“Nilikuwa naye lakini sasa hivi kabakia rafiki.”

“Mbona baba yako kaelezwa kuwa unautia mwili wako uchafu ndicho chanzo wa kidonda chako kukauka na kufanya mambo yote yaanze kusimama?”
“Lakini mama kama kidonda nimekubali kwa nini mniwekee vikwazo kwenye maisha yangu?”

“Si vikwanzo bali masharti ya mizimu.”
“Kama ni masharti ya kunyanyasana mimi siyawezi, kama mali zenu chukueni na mimi niacheni na maisha yangu.”

“Masalu unajiamini nini mwanangu?”
“Sina cha kujiamini bali ukweli ndiyo huo.”
“Basi baba nakuomba nipo chini ya miguu yako kama una mwanamke achana naye.”
“Nikueleze mara ngapi kuwa sina.”

“Najua tumekufanyia kitu kibaya lakini mabadiliko ya kidonda chako ni hayo hayo.”
Niliachana na mama ambaye niliona na yeye ananizingua, sikutaka kukosa vyote, mavazi nilibadilika kuvaa siku zote nilivaa suruali za kitambaa ili kuogopa kukitonesha kidonda, sikuruhusiwa tena kuvaa viatu zaidi ya sandoz. Kila mmoja alinihoji uwezo wangu wa kifedha na mavazi yangu.

Nilikuwa na duka kubwa kuliko ndugu zangu, lakini wao ndio walionekana wana maisha mazuri. Nami sikutaka kushindana nao, kwa vile kidonda nilijua hakitoki mwilini mwangu nami niliamua kutumia kilicho ndani ya uwezo mwangu.

Nilianzisha tabia ya kumuhonga pesa mpenzi wangu ili naye afaidi kama ndugu zangu kutokana na kuonekana wao ndiyo wenye thamani. Siku moja niliamka asubuhi nyumbani kwangu kama kawaida na kushangazwa kukuta baba yangu na ndugu zangu wakiwa nje ya nyumba yangu.

Eti shida yao kubwa kunifumania na mwanamke, niliwashangaa watu wazima kama wale kuacha kazi zao ya msingi kutaka kunifumania mimi. Ajabu ya Mungu siku ile mpenzi wangu hakulala nyumbani, sikutaka kupigizana nao kelele. Niliwaruhusu wamtafute, walifanya upekuzi bila kuona lolote.

“Jamani kama bado hamharidhika semeni niwafungulie wapi mkatafute?”
“Wee chonga lakini lazima utakumbuka siku moja kuwa sisi tulitangulia kuzaliwa.”
“Hilo ni dua la kuku ambalo halitanipa asilani.”

Wote waliondoka na kuniacha nikijiuliza kama wangemkuta na mwanamke wangenifanya nini maana walionekana kabisa walikuja kishari.

Baada ya kuondoaka niliapa kufanya ninachokiweza sikuwa tayari kugeuzwa kitega uchumi cha watu. Niliendelea kufanya mapenzi na mpenzi wangu kama kawaida japo hata biashara kwenye duka langu zilidoda hazikwenda kama mwanzo.

Yote hayo sikuyafikiria zaidi ya kusubiri litakalo tokea japo mama alijitahidi kunibembeleza niachane na yote yanayoonekana yanaharibu biashara za familia yetu ikiwemo na yangu. Baada ya kuona maneno yamezidi nilianza kuwa mlevi kila muda nilikuwa nimelewa kitu kilichozidi kuichanganya familia yangu.

Siku moja nikiwa faragha na mpenzi wangu nilishangaa kuziona sehemu zangu za siri zimeingia ndani nilishtuka sana. Hali ile ilinifanya nikose raha kwa kuamini zile zilikuwa njama za familia yangu kutaka kuona sifanyi mapenzi na mwanamke.
 
Sehemu ya 14

Siku moja nikiwa faragha na mpenzi wangu nilishangaa kuziona sehemu zangu za siri zimeingia ndani nilishtuka sana. Hali ile ilinifanya nikose raha kwa kuamini zile zilikuwa njama za familia yangu kutaka kuona sifanyi mapenzi na mwanamke.

Katika kumbukumbu nilikumbuka siku moja kabla ya kutokea na tukio lile nilipokuwa na mpenzi wangu kuna kitu alinipaka kilichofanya nihisi kama kuwashwa baada ya kumaliza kufanya mapenzi. Na siku ya pili nilitokewa na tatizo lile, ilibidi nimbane kutaka kujua alinipaka kitu gani.

“Masalu juzi nilikutana na dada yako mkubwa aliniomba nikupake dawa hii, nilikataa lakini alinitishia kuniua. Unajua familia yako umeniandama sana kumbuka kuna wakati nikawa nakukimbia nawe ukaamua kutafuta mwanamke mwingine.

“Kitendo kile kiliniuma sana na kuamua kurudiana na wewe, ndipo juzi nilipokutana na dada yako aliyenipa dawa hii nikupake kabla ya kufanya mapenzi itasaidia kupunguza madhara yanayotokana na matatizo ambayo yangekupata.

“Nilikubali kuipokea kwa vile sikudhania kama dada yako angekufanyia kitu kibaya, kumbe nia yake ilikuwa hii ya kukufanya hivi.”
“Lakini kwa nini amenitenda hivi?” Nilijikuta nikilia kwa uchungu kwa kutendo cha dada yangu.

“Mpenzi sikuwa na nia mbaya kama ningekuwa na nia mbaya leo ningekuwepo hapa?”

“Ona jinsi ulivyonimaliza, hujui ugomvi wangu na familia yangu umekuwa kama mgeni unakubali kunimaliza, ona sasa,” nilisema kwa uchungu huku nikimuonesha sehemu zangu za siri zilizokuwa zimerudi ndani.
“Nisamehe Masalu sikujua yatatokea yaliyotokea.”

“Wameniweza,” nililalamika kwa uchungu.
Nilijikuta nikiapa kupambana nao, nilipanga sitakwenda tena dukani na nilikuwa nipo tayari kufa kwa njia yoyote ili tu niwaachie maisha yao.

“Masalu kwa nini usiende hospitali kuangalia afya yako kuliko kujikatia tamaa,” mpenzi wangu alinishauri.

“Hospitali haitasaidia kitu wameisha niweza kwa msaada wako, ona tena sina thamani ya wanaume, kimebakia kichwa kama kobe. Haya ni maisha gani ya kukoseshana raha.”
“Kama mambo ya kienyeji twende kuna babu mmoja namfahamu anaweza kazi hii.”
“Unanifikiri atanisaidia nini?”

“We, twende yote tutayajua huko huko.”
Nilikubaliana na mpenzi wangu niende kwa mtaalamu aliyekuwa akikaa Pasiansi kuvuka kota za benki. Sikutaka kupoteza muda tuliondoka muda ule ule kwenda kwa mtaalamu kuangalia tatizo langu kama linatatulika.

Kabla ya kwenda kwa mganga nilitulia ili nitafakali kama nitapata ufumbuzi wa tatizo langu bila kwenda huko. Baada ya sehemu zangu za siri kukosa nguvu nilipata mabadiliko mwilini kwa kidonda kuanza kutoaji maji upya huku biashara nazo zikifunguka.

Nilimtolea uvivu dada yangu kwa kumfuata kwenye duka lake na kumshutumu mbele ya wafanyakazi wake kwa kitendo chake cha kishrikina cha kumpa dawa ya kuniua sehemu za siri.

Dada alikimbia dukani huku watu wakiinishangaa, ugomvi wangu haukuishia pale nilimfuata kwake usiku akiwa na mume wake na kuendelea kumshtumu. Lakini dada alinisihi suala lile tukalizungumze kwa wazazi.
“Masalu utanilaumu bure mpango huo ni wa watu wengi si wangu peke yangu.”

“Kwa hiyo baada ya kunipa kidonda hamkuridhika mmeniua nguvu za kiume?”
“Lakini Masalu si ulielezwa madhara ya wewe kutembea na mwanamke?”
“Kuna madhara gani? Mbona ninyi mna wanaume na watoto au mnataka niwe shoga?”

“Hapana usifanye hivyo.”
“Nakuhakikishieni baada ya kuniua nguvu za kiume sasa natafuta mwanaume wa kufanya naye mapenzi,” nilisema kwa hasira.

“Masalu maneno gani hayo?’
“Tena kawaambie na wanga wenzako.”
“Masalu ukifanya hivyo utatudhalilisha.”
“Heri niwadhalilishe kuliko kunidhalilisha kuna faida gani ya mimi kuitwa mwanaume si bora niolewe?”

“Najua tumekukosea lakini unatakiwa ujue madhara yanayoweza kukupata, tumefanya vile kuokoa maisha yako.”
“Maisha yangu hamuwezi kuyaokoa ninyi si Mungu.”

“Hapana kutokana na kafara iliyofanywa ya utajiri, ukifanya kosa kama la Monika lazima wewe au baba mmoja wenu atakufa.”
“Wacha nife mimi kwani nina faida gani?”

“Hapana Masalu una faida kubwa kosa lako litagharimu mambo mengi katika familia yetu. Hatukuwa na jinsi imetubidi tufanye hivyo bila hivyo hali ilikuwa mbaya sana, muda wote huo baba alikuwa mgonjwa mahututi alikwisha anza kupooza sehemu moja.

Amini usiamini kuacha kwako kufanya mapenzi sasa hivi baba ndiyo ameanza kupata nafuu hata chooni anakwenda peke yake. Masalu hebu kuwa na huruma na baba hana nia mbaya sema ni kiburi cha Monika wala kidonda hiki kisingekuja kwako.”
“Ina maana Monika yeye alikuwa hana haja ya maisha mazuri kuwa na mtoto?”

“Maisha mazuri angeyapata tu, kidonda hivi kina muda wake ukikaa nacho kwa miaka ishirini hupotea na wewe kufanya mambo yako bila kipingamizi mtoto utapata tu mdogo wangu wala usijigeuze mwanamke.”

“Dada yaani nikae miaka ishirini bila kuwa na mwanamke nina mkataba na Mungu wa kuishi miaka yote hiyo?”

“Masalu usipofanya mapenzi utapungukiwa na nini?”
“Si swali la kuniuliza, kama inaona sipungukiwi na kitu mbona umemuhonga mwanaume gari?”

“Masalu sasa hayo maneno gani?”
”Huo ndiyo ukweli wenyewe, kila mwanadamu ameumbwa kufurahia mapenzi pia kupata watoto.”

“Najua ni kweli , lakini kumbuka lililotokea lilihatalisha maisha ya baba hatukuwa na jinsi.”
“Basi kama hamna jinsi niacheni niishi maisha niyatakayo.”

“Hapana mdogo wangu, hebu punguza munkari tukae kikao cha familia
Ili tutafute ufumbuzi wa tatizo lako.”
“Hakuna ufumbuzi wowote zaidi ya kuniongezea machungu, nakueleza ukweli sikupendi wewe na wote walionizunguka.”
“Masalu utatulaumu bure, kila kitu baba ndiye anayefahamu.”

“Sasa kama anafahamu kwa nini mnanitesa mimi si mgemuacha akafia mbali.”
“Masalu kuwa na huruma.”
“Niwe vipi na huruma wakati ninyi hamna huruma na mimi, mmemuua dada Monika bila kosa.”

“Masalu Monika kajiua mwenyewe, amekiuka masharti aliyopewa.”
“Muongo mkubwa, nina kila kitu mlichomfanyia, hivi dada kwa Mungu utamwambia nini ikiwa ulimtoa mtoto wako kafara ili upate mali?”
“Nani kakwambia?” Dada alishtuka kusikia vile.

“Nina siri ambazo hata wewe huzijui juu ya familia yetu inayoendekeza ushirikina.”
“Masalu una siri gani?”

“Ya wewe kumtoa mtoto wako ili upate utajili na kuwekwa ndani ya chumba.”
“Masaluu! Habari hizo umezitoa wapi?”
“Unaweza kuamini kuwa ni siri, kuna siri gani ikiwa dada Monika ndiye aliyekuwa akiipaka mafuta maiti ya mwanao.

“Wewee!” Dada alizidi kushangaa.
“Kibaya zaidi mmemuua dada Monika mmeshindwa kumzika na kumuweka ndani kama mwanao. Na wewe siku hizi ndiye unayempaka mafuta, hivi kwa mtindo huo kwa Mungu mtasema nini?”
“Masalu nani kakueleza yote hayo au mama?”

“Utamsingizia bure mama kama wewe, ninayo mengi ambayo wewe huyajui.”
”Masalu mambo gani?”
“Siwezi kukueleza muulize baba si ndiye anayefanya yote haya, hata hiki kidonda nilielezwa mapema kitanipata.”

“Na nani?”
“Na dada Monika, hata kifo cha alinieleza kitakavyompata.”
“Alijuaje?”
“Siku alipoondoka baba alimwambia lazima atakufa.”

“Monika muongo.”
“Kweli kabisa na hata alipotaka kufa alinieleza sema siku ya kufa nilikuwa shule kuna siri nzito alitaka kunipa lakini bahati mbaya sikuwepo. Hata mwanaume aliyekuwa akikaa naye hakumpa siri hiyo dada yangu amekufa na siri nzito hata sijui ni siri gani?”
“Wewe unamuamini?”

“Nisimuamini vipi hata bwana yake mmemuua.”
“Nani kakwambia tumemuua?”
“Najua kila kitu, mimi si mtoto ndiyo maana nimekueleza najua unayoyajua na usiyoyajua.”

Kila nililokuwa nikimueleza dada aliona kama maluweluwe, niliamua kuondoka huku nikiwa na akili kichwani mwangu.
Wazo la kwenda kwa mganga sikulitupa mbali japo lilikuwa mtihani kwangu. Lakini niliamini maisha yangu yananitegemea mimi mwenyewe si mtu mwingine.

Siku ya pili nilimpigia simu mpenzi wangu ili anifuate na anipeleke kwa mtaalamu huyo. Alinifuata na kunipelekwa kwa mtaalamu mmoja aliyekuwa maeneo ya Pasiansi nyuma ya kota za benki.
Tulipofika eneo la mganga tulikuwa kuna wagonjwa wengi kiasi, ile ilinipa moyo kuwa huduma za mganga ni nzuri.

Ilibidi tukae chini ya mti kusubiri wagonjwa wahudumiwe. Baada ya saa tatu ndipo tulipoitwa sisi muda ulikuwa ni saa kumi jioni. Tuliingia ndani na kuketi kwenye mkeka.
 
Sehemu ya 15

Wazo la kwenda kwa mganga sikulitupa mbali japo lilikuwa mtihani kwangu. Lakini niliamini maisha yangu yananitegemea mimi mwenyewe si mtu mwingine.

Siku ya pili nilimpigia simu mpenzi wangu ili anifuate na anipeleke kwa mtaalamu huyo. Alinifuata na kunipelekwa kwa mtaalamu mmoja aliyekuwa maeneo ya Pasiansi nyuma ya kota za benki.

Tulipofika eneo la mganga tulikuwa kuna wagonjwa wengi kiasi, ile ilinipa moyo kuwa huduma za mganga ni nzuri.

Ilibidi tukae chini ya mti kusubiri wagonjwa wahudumiwe. Baada ya saa tatu ndipo tulipoitwa sisi muda ulikuwa ni saa kumi jioni. Tuliingia ndani na kuketi kwenye mkeka.

“Huyu ni nani?” Mganga aliniuliza.
“Mchumba wangu,” nilimjibu.
“Mbona inaonesha kwenu hawamfahamu?”
“Ni kweli kwetu hawamfahamu.”
“Sasa kama kwenu hafahamiki mizimu hawezi kuzungumza mbele yake.”

“Kwa hiyo?”
“Akatusubiri nje.”
“Sweet kanisubiri nje,” nilimueleza mpenzi wangu ambaye alionesha hakupenda kutoka nje.

Mpenzi wangu alitoka nje na kuniacha na mganga ndani ya kilinge, baada ya kutoka nje, mganga naye alitoka nje na kurudi na kipande cha tawi la mti wa mnyaa na kuushikilia mkononi.

Alipoingia alikaa kwenye mkeka kisha alinipa kipande cha mnyaa ambacho nilishika kwa muda kisha aliniambia nikiachie. Baada ya kukiachia alisogeza karibu na sikio kama anasikiliza simu kisha alianza kuzungumza kama mtu anayezungumza peke yake:

“Masalu mimi jamani mbona kila siku matatizo sifai chini sifai juu, kiuno kinaniuma mgongo unaniuma miguu inanima kifua kinaniuma shingo inaniuma kichwa kinaniuma macho hayaoni vizuri choo sipate vizuri, jamani ni kwa sababu gani?

Masalu mimi nina tatizo gani jamani, mbona kila siku matatizo yanaongezeka ni kweli mganga atanisaidia mbona mimi ni maiti inayotembea ninayosubiri kufa. Ni kweli mganga atanisaidia? Mbona sina thamani ya dunia kifo changu kashikilia baba kama cha dada Monika.

“Maisha haya mpaka lini kidonda mimi na sasa wamechukua nguvu zangu za kiume. Nini kimebakia kama si uhai wangu, kweli mganga atanisaidia?”

Baada ya kusema yale aliondoka kipande cha mti wa mnyaa sikioni na kuutupia kwenye kapu la dawa lililokuwa pembeni yake.
“Umesikia?”

“Ndiyo.”
“Yaliyozungumzwa yana ukweli?”
“Ndiyo.”
“Unajijua kuwa wewe ni maiti?”
“Maiti?” Kauli ya mganga ilinishtua sana.
“Hujijui?”

“Sijijui.”
“Mpaka sasa hivi upo sawa ma nduguzo?”
“Kivipi?”
“Viungo vyako vipo sawa?”
“Vipo sawa.”
“Kipi kilichokuleta hapa?”

“Mambo mengi.”
“Moja wapo?”
“Ni mengi ila kubwa ni hii hali iliyojitokeza hivi karibuni ya kufa nguvu za kiume.”
“Hujui sababu zake?”

“Najua.”
“Sasa nini kimekuleta huku?”
“Mwenzangu alinieleza unaweza kunisaidia.”
“Nikusaidie nini?”

”Kuitoa hali hii?”
“Kidonda umeridhika nacho?”
“Nasikia nikikitoa panaweza kutokea matatizo katika familia nyetu.”

“Kama unajua hivyo kwa nini unataka dawa ya nguvu za kiume?”
“Kama utajiri ni wao lakini mapenzi ni haki yangu ya msingi.”

“Sikiliza kijana usijitoe akili, nini alichokueleza dada yako mkubwa juu ya kupona nguvu zako za kiume nini kitampata baba yako?”

“Kwa hiyo nibaki na hali hii milele?”
“Ni uamuzi wako, kupona upoteze watu au uendelee kuwa maiti inayotembea ili kuiokoa familia yako. Na hiyo mosi familia yako sasa hivi itakutuliza ndani kwa kupooza miguu utakuwa wa kula na kulala wao wanaponda maisha.”

“Eti?”
“Ukweli ndiyo huo mpango huo utatekelezwa mara moja baada ya kuonekana umekuwa mkaidi.”

“Sikubali.”
‘Kama hukubali utafanya nini?”
”Nitatibiwa kila kitu nihakikishe napona na litakalo watokea watajijua wenyewe.”
“Usiseme kwa hasira upo tayari kuisambalatisha familia yako?”
“Nipo tayari.”

“Kwa kukupa mfano mdogo dawa utakayokunywa utarudisha nguvu zako za kiume, lakini ukirudi nyumbani utamkuta baba yako yupo hoi kitandani.”
“Kitakachofuata?”

“Siku ukifanya mapenzi ndiyo siku ya kifo chake.”
“Mmh!” Niliguna.
“Ukweli ndiyo huo, chagua kusuka ama kunyoa?”

Nilibakia kimya kwa muda nikiwaza nitakachokifanya na matatizo ambayo yangeikuta familia yangu. Nilikuwa nipo radhi kuendelea na kidonda changu na kukosa nguvu za kiume. Lakini maelezo ya mganga kuwa wanataka kunigeuza msukule kwa ajili ya kuendeleza mali kilinichanganya sana.

Kufikia pale nilijikuta nikichanganyikiwa na kushindwa niegemee upande gani, lakini niliamini maisha yangu ni muhimu kuliko kitu chochote chini ya jua. Vile vile sikuwa tayari kumuhurumia mtu aliyepanga kuniangamiza kwa ajili ya tamaa zake za mali.

Uamuzi nilioamua ni kujitengeneza mimi na lolote litakalo tokea kila mmoja ataubeba msalaba wake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom