Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,870
- Thread starter
- #41
Sehemu ya 09
“Nani kasema?”
“Aliyekuwa akikaa na dada Monika ndiye anayeeneza habari hizi”
“Yeye kajuaje?”
“Mama ina maana ninapozungumza na wewe unakuwa wapi? Nilikueleza kuwa kabla ya kufa dada Monika alimpa siri kubwa ya maisha yetu na sababu ya kifo chake. Pia alimueleza kuwa alikuwa na siri nzito ambayo asingemwambia zaidi yangu mimi.”
ILIPOISHIA;
“Mmh, sasa huyo kijana kinamuhusu nini kututangaza vibaya?”
“Kinacho muuma ni kumuulia mtoto wake asiye na hatia.”
“Hivi baba yako akijua kuwa ndiye anayetutangaza vibaya kwa watu kutakuwa na usalama kweli?”
“Atamfanya nini?”
“Masalu wee acha baba yako hana dogo anaweza hata kumkata kichwa”
“Akimuua atapata faida gani si ndiyo atakuwa anaongeza chuki kwa watu.”
“Masalu mwanangu kwa umri wako hata nikueleza kitu hutanielewa, nakuomba kila ulilosikia liache lilivyo bado mtoto mdogo litakuchanganya”
“Sawa nimekuelewa, ila naomba ukweli wa jambo moja.”
“Jambo gani gani?”
”Kuhusu ukweli wa dada Monika”
“Ukweli upi?”
”Ni kweli amekufa?”
“Ndiyo”
“Amezikwa wapi?”
“Mmh! Si Makaburini”
“Makaburini gani?”
SASA ENDELEA.....
“Kwa kweli siwezi kujua makaburi gani sikwenda kuzika”
“Mama kuna makaburi tofauti na
tuliyoyazoea?”
“Hakuna”
“Na misiba yote huanzia kanisani kisha kupelekwa kuzikwa?”
“Ndiyo”
“Sasa msiba wa dada Monika mliupeleka kanisa gani?”
“Masalu hata ukijua itakusaidia nini, aliyekufa amekufa huwezi kumfufua.”
“Hata kama siwezi kumfufua da Monika ndiye kipenzi changu, kaburi lake kwangu ni kielelezo cha kumuona kipenzi changu”
“Masalu nakuomba suala hilo uachane nalo”
“Yote nitaachana nayo si la dada Monika”
“Masalu akitaka kujua mengi utakosana na baba yako”
“Kwa hiyo ukweli dada Monika maiti yake haikuzikwa?”
“Masalu nakuomba mwanangu chonde chonde achana na hayo ili maisha yako yawe salama”
“Kwa hiyo nikitaka kujua baba ataniua?”
“Hawezi kukuua ila utakuwa matatizoni”
“Mmh! Sawa mama,” nilikubali kwa shingo upande kutokana na kuonekana kumuweka mama katika wakati mgumu.
Sikutaka kumsumbua sana mama yangu kutokana na maelezo ya dada Monika, kila nilipomtazama nilimuonea huruma. Nilimuahidi mama toka moyoni mwangu sitaulizia lolote kuhusiana na dada Monika wala kitu chochote kuhusiana na familia yetu.
Kauli yangu ilimfurahisha mama na kuonekana hawezi kuamini nilichokisema.
“Kweli Masalu”
“Kweli mama, nakupenda sana mama yangu”
“Asante Masalu, nakuomba kila unachokijua huenda hata mimi mama yako sivijui kwa vile baba yako alimpenda sana Monika hata siri zingine sizijui ambazo alikueleza wewe na pengine kabla ya kufa angekueleza,” maskini mama yangu alisema huku akitokwa na machozi kitu kilichozidi kuniumiza nami machozi yalianza kunitoka kwa mbali.
“Nimekuelewa mama yangu, nimekuelewa sina budi kukusikiliza.”
“Asante Masalu, siku zote niliamini wewe na Monika ndio watoto wangu wanaonijali, endelea kunijali mwanangu wewe ndiye tegemeo langu soma unikomboe”
“Nitafanya hivyo mama yangu, nakuahidi kuwa kimbilio lako”
“Asante mwanangu”
Baada ya mazungumzo marefu tulirudi nyumbani, lakini bado yaliniacha na maswali lukuki moyoni mwangu, nilijikuta nakubaliana na shemeji, bwana ya Monika kuwa mwili wa dada umefichwa ndani pamoja na mtoto wa dada Mihayo.
SIKU TATU BAABAYE
Siku tatu baadaye nilipata taarifa za kusikitisha za kifo cha utata cha shemeji aliyekuwa bwana wa Monika. Taarifa zilizonitisha na kuamini mazungumzo yangu na mama juu ya taarifa zinazoisambwazwa na shemeji zilimfikia baba na kuamua kufanya umaruhuni wake.
Ndugu walisema aliporudi nyumbani alianza kusema anasumbuliwa na kichwa huku akisema kama akifa atakuwa ni baba. Na usiku alipiga kelele akimtaja jina la baba kitu kilichozidi kuaminisha kwamba anahusika moja kwa moja ili kumukomoa baada ya kusikia akitutangazia sifa mbaya familia yetu.
Kifo kile kiliongeza sifa mbaya kufikia hatua familia ya aliyekuwa mpenzi wa marehemu dada Monika kuja kutushambulia kwa maneno ya kutuita wachawi.
Siku hiyo nilikuwepo, mama wa marehemu alikuja nyumbani na kuanza kutoa shutuma nzito kusema kwa sauti ya juu huku watu wakisikiliza”
“Mmeniulia mwanangu kwa imani zenu za kichawi ili muwe matajiri, kumuua mtoto wa Mihayo hamkuridhika mmemuua Monika na kumficha ndani kama chama bado tu mmeona haitoshi mmemuua mwanangu.
Nawaambia damu ya mwanangu haiendi bure.”
Taarifa zile zilipelekwa kwa baba ambaye aliita polisi na kumchukua yule mama na kumpeleka kituoni. Kwa kweli kilichoendelea sikujua zaidi ya kumsikia baba akitamba atamuonesha.
Pamoja na yule mama kupelekwa polisi familia yetu ilitawaliwa na sifa mbaya ambazo wengi walizisikia na kuzisambaza kwa watu kuwa maisha yetu yametawaliwa na utajiri wa kishirikina ulikuwa ukipitia kidonda cha marehemu dada.
Nilijikuta nikiishi maisha ya kukosa amani hata tembea yangu ilikuwa ya mashaka kwa kuhofia maneno ya watu. Siku zilikatika walisema mchana, usiku wakalala. Walizungumza sana mwisho wakanyamaza na kusahaulika na maisha yakaendelea.
Katika maisha yetu hakuna kilichobadilika, nilimaliza kidato cha nne kwa kupata matokeo mabaya. Niliamini kufanya vibaya kulitokana na migongano ya mawazo iliyotokana na kuchanganywa na mambo yote yaliyotokea yakihusu familia yetu, na taarifa nilizopewa na dada Monika kifo chake na matukio mengi ya kishirikina yaliyoilenga familia yetu.
Wazo la kurudia mtihani wa kidato cha nne, lilipingwa na baba na kusema atanipatia shughuli nyingine. Roho iliniuma kwani ndoto zangu zilikuwa kusoma kwa bidii ili siku moja nimkomboe mama kwenye mateso ya kuwekwa kifungoni na baba.
Miezi sita baada ya matokeo mbaya ya kidato cha nne, baba alionesha mapenzi makubwa tofauti na zamani hata kuzunguka naye kila kona kwenye shughuli zake. Siku nyingine alinipa pesa za matumizi ambazo alinieleza ninunue kitu chochote nikitakacho.
Kwa akili za kitoto nilianza kubadilika na kuyaona yote niliyoelezwa juu ya ukatili wa baba ni uongo. Baba alikuwa mtu mzuri kwa kuninunulia nguo za thamani, nilionekana kweli mtoto wa mtu mwenye pesa tofauti na mwanzo nilivyokuwa nasoma shule.
Baba siku zote alinisikifia kuwa mimi ndiye mtoto anipendaye kuliko wote, kauli zile za baba zilinifanya nisahau hata wazo la kumuuliza juu ya dada Monika.
Siku moja tulikuwa tumekaa kwenye moja ya hoteli ya baba huku akiniruhusu kula nikitakacho, baada ya chakula baba alinichukua na kuingia naye kwenye ofisi yake iliyokuwa ndani ya hoteli ile ambayo sikuwahi kuingia siku za nyuma.
Baada ya kuingia ofisini baba aliendelea kunimwagia sifa.
“Masalu unajua nakupenda sana kuliko watoto wangu wote”
“Najua baba”
“Hebu niambie unataka nini nikufanyie ili ujue napenda sana”
“Cha kwanza kunipa nafasi ya kurudia masomo niliyoanguka katika mtihani wangu ili nifanye vizuri bado nina hamu ya kuendelea kusoma”
“Tofauti na hilo?”
“Siwezi kusema kwa sasa mpaka nitakapofanya mtihani wangu wa marudio.”
“Masalu, kusoma si muhimu sana kwako, kama pesa zipo nitakufungulia mradi wako ili uendeleze maisha yako”
“Lakini...”
“Masalu hakuna haja ya kubishana, naomba ujiandae kuna duka moja nimelifungua na kuanza kazi wewe ndiye msimamizi mkubwa “
Nilijikuta nakosa cha kuzungumza na kukubaliana na baba japo nafsi yangu ilitaka kusoma ili nimkomboe mama yangu.
Nilijua kukubali mradi ule japo utakuwa chini yangu bado utakuwa wa nguvu za kishirikina kwa ,kuhofia huenda siku za mbele baada ya kuoa na kupata mtoto akatolewa kafara.
Baba alinitolea hati za kumiliki duka lile lenye jina langu na kunionesha sehemu ya kusaini, Nilisaini na kuniahidi kunifanyia mambo makubwa kuliko ndugu zangu wote. Baada ya kutoka pale aliniingiza kwenye gari lake na kunipeleka mjini barabara ya Pamba kwenye duka langu.
Nililikuta duka lipo wazi na watu wakiendelea na mauzo ya vitu, lilikuwa duka kubwa la kuuza vitu vya jumla na rejareja. Tulipofika dada mmoja ambaye alikuwa akinifahamu aliniuliza:
“Leo Masalu ndiyo umeamua kuja?”
“Alikuwa anamalizia masomo,” baba alijibu.
“Karibu bosi”
“Asante,”
Nilijibu huku nikiingia dukani na kwenda kukaa kwenye kiti changu kilichoandaliwa kwa ajili ya kukalia niwapo kazini. Baada ya kukagua duka lililokuwa likilingana na maduka ya ndugu zangu. Baba aliondoka na kuniacha nisimamie duka langu.
Alinipitia jioni na kunirudisha nyumbani, nilipofika nyumbani nilimueleza mama kuwa nimepewa duka na baba. Ajabu mama badala ya kufurahi alitokwa na machozi