SEHEMU YA 18
Baada ya kupanda juu ya kichunguu kifua wazi, alipanda na yeye na kuanza kunichanja kila kona ya mwili huku akinipaka ile dawa aliyochanganya na mafuta mazito. Alipomaliza tulitelemka na kurudi hadi ndani ya kilinge, ndipo aliponisemesha.
“”Habari za toka jana?”
“Nzuri mzee wangu, shikamoo.”
“Marahaba, kuna habari gani mpya?”
“Jana walinipigia simu usiku na kuniomba ninusuru maisha ya baba.”
“Uliwajibu nini?”
“Niliwaambia siwezi kujiteketeza mwenyewe.”
“Wao walisemaje?”
“Walinitishia kama baba akifa nitamla nyama.”
“Akawajibu nini?”
“Niliwaeleza kama walivyokula nyama ya dada Monika.”
“Wakasemaje?”
“Walishtuka na kunieleza kuwa habari nimezijulia wapi?”
“Mhu, ukawajibu nini?”
“Niliwambia nitawapeleka polisi na kuwafungulia mashtaka ya uuaji na kukaa na maiti za watu ndani?’
“Ehe! Wakasemaje?”
“Walishtuka na kuniomba ninusuru maisha ya baba.”
“Ukawajibu nini?”
“Niliwaeleza sipo tayari.”
”Wakasemaje?”
“Waliendelea kunibembeleza niende kwa vile uliniahidi nikitoka hapa nitakuwa kamili, nimewaeleza nitakwenda leo.”
“Wakasemaje?”
“Tumekubaliana, nikitoka hapa niende.”
“Sikuliza, una bahati kama usingekuja hapa na kujipendekeza jana ukaenda ungekwisha pale pale.”
“He!” Nilishtuka kusikia vile.
“Unashtuka, kama nilivyokueleza familia yako haina mapenzi na wewe kwa ajili ya mali.”
“Mmh! Sasa nikienda leo itakuwaje?”
“Leo usiende, nenda kesho kutwa ila kuna kitu kitatokea si cha kawaida kuwa tayari kukabiliana nacho.”
“Kitu gani hicho?”
“Wee nenda, ila majibu utayapata kujua kinga niliyokukinga inafanya kazi kiasi gani?”
“Niambie ili nijue ikiwezekana nisiende.”
“Lazima uendelea ili kuwaumbua wabaya wako.”
“Mmh! Sawa.”
“Baada ya kesho kwenda rudi tumalizie tiba, kwa vile hawatakubali kuona umwashinda.”
“Sawa nimekuelewa.”
“Nilitaka kusahau kitu kimoja, leo usioge wala kukutana na mwanamke kimwili ikiwezekana leo kila mmoja alale chumba chake au kitanda chake.”
“Sawa nimekuelewa.”
“Ndoto utakayoiota ndilo jibu la safari yako.”
“Nasahukuru kwa msaada wako.”
Baada ya mazungumzo, tulirudi hoteli tuliyokuwa tumepanga kwa ajili ya mapumziko, siku ile sikukaa kutokana na kuwa na alama nyeusi cha kuchanjwa na mganga.
Kwa vile hatukuruhusiwa kulala pamoja, tulichukua chumba cha vitanda viwili na kila mtu alilala kitanda chake. Usiku niliota ndoto nafukuzwa na kichaa mmoja ambaye katika kunifukuza aligongwa na gari, hapo hapo nilishtuka usingizini na kujiuliza kichaa yule ni nani na ndoto ile inaashiria kitu gani.
Siku ya pili nilimueleza mpenzi wangu ambaye alinishauri heri nisiende nyumbani ili kuepusha nilichokiota.
“Masalu kama mganga alikuambia utakachokiota ndicho kitakacho tokea, kwa nini uende.”
“Hilo wazo hata mimi nilikuwa nalo lakini mganga alisema lazima niende, ili nirudi na kupata dawa ya mwisho.”
“Kwa nini asikupe hiyo dawa?”
“Alisema lazima niende ili kuonesha uwezo wa kile alichokifanya jana.”
“Mmh! Mtihani mzito kweli.”
“Lakini kwetu hatuna kichaa.”
“Basi inawezekana utakutana naye njiani.”
“Kama ni hivyo bora nikodi gari mpaka mlangoni.”
“Bora ufanye hivyo.”
“Sawa, basi tuongozana wewe uende kwenu najua wamekutafuta sana.”
“Hata wakinitafuta mimi mtu mzima, kuna mdogo anajua kila kitu sidhani kama watasumbuka sana. Mbona tuliisha safiri zaidi ya wiki hakuna kilichoharibika?”
“Si uliaga?”
“Basi taarifa zangu watazipata kwa mdogo wangu na leo nikifika watapata jibu.”
“Mmh! Haya.”
Niliongozana na mpenzi wangu hadi kwao nilimtelesha na mimi kuendelea na safari yangu. Nilikwenda na gari hadi mlangoni na kutelemka, wote waliokuwepo walishtuka. Baba aliyekuwa amelazwa sebuleni aliponiona alipiga kelele.
“Mtoeni ataniua.”
“Baba siwezi kukuua, utajiua mwenyewe,” nilimjibu baba.
“Jamani mtoeni ataniua...”
“Masalu hebu toka nje,” dada alinifokea.
Niligeuka kutoka nje, kaka yangu alikuja kwa nyuma na kunishika kisogoni, mara alianza kupiga kelele kama mtu aliyepagawa na kupitia jembe na kutaka kunipiga nalo, alinikosa kosa mara mbili nilipoona hatanii nilitimua mbio, alinikimbiza mpaka barabarani huku akidhamilia kuniumiza.
Ilinibidi nivuke barabara bila kuangalia baada ya kuona nakufa najiona, baada ya kuvuka nilisikia kishindo nyuma yangu na kelele za watu. Nilipogeuja nilimuona kaka yangu akiwa chini akivuja damu kichwani.
Japo ajali ile ilifanya moyo uume na kupatwa na huruma, lakini sikutaka kurudi kuangalia, wakati huo watu walikuwa wakijaa kwenye tukio la ajali na kumzunguka kaka. Nilikodi teksi iliyokuwa ikipita kuwahi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilimpigia simu mpenzi wangu.
“Vipi Masalu mbona kama kuna tatizo?”
“Ndiyo.”
“Tatizo gani?”
“Si lakulizungumzia kwenye simu.”
“Upo wapi?”
“Nyumbani.”
“Nakuja sasa hivi.”
Baada ya kukata simu nilibaki nimejilaza kwenye kochi nilijiuliza vita nzito niliyoelezwa na mganga ndani ya familia yangu nini hatama yake.
Nilijiuliza kaka yangu bila kugongwa na gari alitaka kunifanya nini. Au alikusudia kuniua?
Njozi ile baada ya kuuona ukweli nilijuliza nini kitafuata.
Niliamini kama vita ya nguvu ya giza itashindikana basi watatumia nguvu za kawaida ili kunitokomeza duniani. Nilijiuliza kama itakuwa hivyo nitawezaje kuwaepuka? Nilipanga kuukimbia mji wa Mwanza ili kuokoa maisha yangu kwa kuliuza duka langu.
Wazo lile nilitaka nishauriane na mwenzangu kabla ya kutoa uamuzi, nilipanga akija nitamgusia suala lile ambalo kwa upande wangu lilichukua sura mpya ya kutishia maisha yangu. Wakati nikiwa kwenye dimbwi la mawazo mpenzi wangu aliingia kwa hali aliyonikutana nayo ya kujilaza mikono kichwani ilimshtua sana.
“Vipi?”
“Masalu?”
“Mambo mazito.”
“Kivipi?”
Nilimueleza niliyokutana nayo nyumbani, alibakia mdomo wazi asiamini nilichomueleza.
“Sasa bila kugongwa na gari ingekuwaje?”
“Hata sijui.”
“Sasa kwa nini mganga hakukuambia?”
“Aniambie nini wakati aliniambia nitakayo yaota ndotoni ndiyo nitakutana nayo.”
“Sawa, lakini alitakiwa akupe taadhari.”
“Mganga hawezi kukuambia kitu kijacho kabla ya kutokea ili usije sema uongo.”
“Pole sana mpenzi wangu sasa tutafanya nini.”
Mara simu yangu iliita nilipoangalia nilikuta ni dada, niliitazama bila kupokea kitu kilichomfanya mpenzi wangu kuuliza.
“Mbona hupokei na nani?”
“Ya dada”
“Anataka nini si alikufukuza?”
“Hata mimi nashangaa.”
“Usipokee.”
Kweli sikuipokea iliita mpaka ikakatika, baada ya kukatika haukupita muda iliita tena vilevile sikuipokea iliita mpaka ikakatika. Nilitaka kuizima lakini mpenzi wangu alikataa kwa kuniambia:
“Simu za ndugu zako usipokee, lakini zingine ziache ziingie.”
“Kutokana na vita hii nzito nilikuwa nimepanga kuuza duka langu niondoke Mwanza, ulikuwa na wazo gani?”
“Mmh! Ni haraka sana kwa nini tusirudi kwa mganga tumsikilize atasema nini?”
“Mganga kazi yake ni kunizundika ili nisidhurike na nguvu za wachawi, lakini si kuwazuia kunidhuru kwa siraha za kawaida.”
“Sawa, lakini kabla ya kufanya hayo tukamsuikilize mganga, si alikuambia urudi.”
“Mmh! Kweli, kuna umuhimu wa kwenda muda huu.”
“Hakuna tatizo ni muda mzuri.”
Nilikubaliana na mwenzangu kurudi kwa mganga, tuliongozana hadi kwa mganga, tulimkuta akihudumia wagonjwa. Ilitupasa kusuburi kwa zaidi ya saa nne. Ilipofika zamu yangu niliingia kwa mganga, aliponiona alitabasamu na kusema.
“Umeona?”
“Ndiyo.”
“Sasa ule ndiyo ubaya uliokuwa umekuzunguka, bila kupitia hapa alipokushika ungeanguka chini na kupooza kuanzia muda ule ungewekwa kwenye chumba chenye mwanga hafifu hayo ndiyo yangekuwa maisha yako mpaka unakufa.”
“Mmh! Na kaka yangu aliyegongwa na gari hakufa?”
“Hakufa”
“Atapona?”
“Atapona, lakini itachukua muda mrefu sana kupona, alipogongwa hakuumia. Wala ile haikuwa gari la ukweli kama ulivyodhania ni kinga yako mwilini hakuna wa kukuchezea. Atakayetaka kukuchezea atapatwa na mazito kuliko yaliyompata kaka yako.
“Kila tatizo litakalo kutokea utaliota usingizini kabla ya kukutoke.”
“Kwa hilo nashukuru, lakini wakitumia siraha?”
“Zindiko nililokuwekea hawawezi kukudhuru kwa kitu chochote.”
“Nilikuwa na wazo la kuuza duka ili nitoroke.”
“Wala usiende popote, hakuna wa kukugusa, watakuogopa kama ukoma, ila inabidi duka lako lifanyiwe zindiko bila hivyo mali zako zote zitamomonyoka na kukufanya maskini wa kutupa.”
“Na ndugu zangu?”
“Nao wana wakati mgumu si muda watakuwa na maisha magumu labda waangaike tena la sivyo kwa kutegemea ndagu ya kidonda wataadhirika.”
“Kwa hiyo unataka kuniambia kaka hakupata ajali?”
“Hakupata ajali ila amepata kichaa baada ya kutaka kukudhuru na kumrudia mwenyewe.”
“Lile gari na watu waliokuja walitokea wapi?”
Kile ni kiini macho tu lakini ile ndiyo kinga inayokulinda baada ya kumzuia ulipata nafasi ya kukimbia na kurudi kwako.”
“Na hali ya baba?”
“Mmh! Hali ya baba yako ndiyo hivyo umeshikiriwa na uhai wako, kubali uteseke baba yako apone.”
“Sipo tayari wacha afe, siwezi kuwaonea huruma tena ni watu wabaya wasiyo nitakia mema.”
“Basi leo nitamalizia kazi yangu, ukitoka hapa fanya mambo yako bila hofu atakaye kugusa atapotea.”
Mganga baada ya kusema vile alichukua dawa nyeusi iliyokuwa kwenye chupa na kuichanganya na asali kisha alisema niachame mdomo na kunichanja kisha alinipaka dawa kwa kutumia simbi.
Chale zingine alinichanja katikati ya utosi kifuani na mgongoni na sehemu zote za maungio ya mwili kisha alinipa ruhusa ya kurudi nyumbani na kunipa masharti yale yale ya kutolala na mwanamke kwa siku ile