Simulizi: Tafadhali baba usitufanye misukule

Simulizi: Tafadhali baba usitufanye misukule

Sehemu ya 11

Nilijilazimisha kuikubali hali ile kwa vile sikuwa na jinsi, hata ningefanya nini isingebadilika. Siku zilikatika huku nikipata maswali mengi kutokana na kubadilika kuonekana mtu mwenye mawazo mengi. Watu wangu wengi wa karibu walitaka kujua sababu ya mimi kuwa katika hali ile.

Niliwaeleza nipo sawa, lakini hawakukubali na kunikubalia kwa shingo upande, siku zilikatika huku nikiendelea kuficha siri zangu. Tatizo lililonisumbua lilikuwa kwa mpenzi wangu ambaye siku za nyuma nilikuwa nikifanya naye mapenzi kufikia hatua ya kumuahidi kumuoa.

Mwanzo nilijitahi kumkwepa ili asijue sababu ya mimi kufanya vile, lakini kila siku zilipozua uongo alinikubali mwisho wa siku uongo uliisha.

“Masalu mbona siku hizi sikuelewi?”
’Kivipi?”
’Kila siku umekuwa mtu wa visingizio.”
“Lakini si nimekueleza sababu.”
“Sababu gani hizo?”

“Kwa hiyo unatakaje?”
“Nina hamu na wewe mpenzi wangu.”
“Si nimekueleza subiri mpaka tutakapooana.”
“Masalu usinitanie, si nini wewe uliyenilazimisha tufanye mapenzi kabla ya ndoa?”

“Ni kweli, lakini nimegundua tulifanya kosa.”
“Masalu niambie moja unanipenda hunipendi?”
“Nakupenda.”
“Basi nataka leo tulale pamoja.”

Kwa kweli kwangu ulikuwa mtihani mgumu wa kumkwepa mpenzi wangu nisifanye naye mapenzi. Jioni nilipotoka kazini alinipitia na gari lake na kwenda La Kailo hoteli, nilishindwa kumkatalia. Kumbe alikuwa amekwisha chukua chumba kabisa tulipofika tuliingia moja kwa moja ndani.
“Vipi mbona huku?” Nilimuuliza.
“Swali gani hilo masalu?”

Nilishindwa tena kumueleza kitu chochote, nilibakia kupelekwa kama mkokoteni usio na breki. Tulipoingia ndani mpenzi wangu alionekana na shauku kwa kunivamia kutaka mapenzi. Nilijiuliza nitawezaje kumkatalia tusifanye mapenzi ikiwa tayari ameisha lipia chumba.

Nilijiuliza kama nikifanya mapenzi itakaje, nilijikuta nikisemea mwenyewe “Liwalo na liwe” niliamua kufanya mapenzi siku ile. Kilichomshtua mpenzi wangu kutambaa nilichokuwa nimejifunga mguuni.
“Masalu nini hiki?”
“Niliumia,” nilidanganya.
“Sasa mbona umejifunga kitambaa badala ya dawa?”

“Natumia dawa za asili.”
“Ulifanya nini?”
“Niliumwa na nyoka wa maajabu.”
“Una maana gani?”
“Nilikuwa nimelala ndani nikaota nauwa na nyoka?”

“Ehe.”
“Nilipoamka si ndiyo nikakuta natokwa damu.”
“Mungu wangu, baada ya hapo ikawaje?”
“Nilikimbizwa hospitali, lakini kila dawa niliyowekewa ilizidi kulifanya donda kuzidi kuchimba.”
“Jamani ni nyoka gani huyo akuume kitandani?”

“Hata najua.”
“Mmekwenda kwa wataalamu wa jadi?”
“Nilikwenda ndiyo natumia tiba yao kidogo sasa sijambo.”
“Walikuambia nini kuhusiana na tatizo lako?”
“Alinieleza atanitibu tu hataki kuyachimba zaidi.”

“Mmh! Masalu pole sana mpenzi wangu, mbona hukuniambia mapema?”
“Sikupenda kukuumiza moyo mpenzi wangu nilijua tatizo ni dogo kumbe kubwa.”
“Mmh! Pole sana,” mpenzi wangu aliniambia kwa sauti ya huruma.

“Asante.”
Pamoja na mazungumzo yale mpenzi wangu alilazimisha lazima tufanye mapenzi kwa vile alikuwa na hamu na mimi sana. Nilijikuta sina jinsi zaidi ya kukubali kufanya mapenzi na mpenzi wangu kukiuka masharti ya baba. Siku hiyo sikurudi nyumbani nilala hotelini na mpenzi wangu mpaka asubuhi.

Siku ya pili nilirudi nyumbani majira ya saa tatu mara moja kwenda kubadili nguo kisha niende dukani kwangu. Mama aliponiona alishtuka na kuniuliza:

“Masalu ulikuwa wapi?”
“Nilikwenda kwenye sherehe ya rafiki yangu.”

“Kwa nini hukurudi?”
“Iliisha muda mbaya.”
“Mmh! Sawa baba yako leo hajalala ninavyozungumza wewe, ameondoka asubuhi kwenda kukutafuta.”

“Sasa ananitafuta mimi mtoto?”
“Hayo hayajui baba yako si unajua wewe ndiye mtoto wake wa mwisho.”
“Naelewa, lakini mimi sasa hivi ni mtu mzima.”
“Ina maana jana ulilala na mwanamke?”
“Mama kusema mtu mzima namaanisha kulala na mwanamke?”

“Sina baada hivyo, kulala nje siyo tija, wasiwasi wangu pengine ulimaanisha hivyo.”
“Lakini kumbukeni unaninyima haki yangu ya msingi.”
“Ni kweli, lakini ndivyo ilivyokuwa unatakiwa kuvumilia.

“Hayavumiliki.”
“Tutafanyaje?”
“Ipo siku nami nitapata ufumbuzi wa tatizo langu kama dada Monika.”
“Unataka kufanya kama dada yako? Usifanye hivyo bado tunakuhitaji.”
“Hamna shida na mimi wenye thamini kwenu ni hao wanaoishi maisha mazuri yasiyo na masharti.”

“Hapana Masalu utanifanya mama yako nife kwa mawazo hujui kiasi gani nilivyokuwa nawapenda wewe na Monika, ndiye watoto pekee mnaonijali. Baada ya kifo cha Monika umebakia wewe na wewe ukifa nami sitachelewa kufa sitakuwa na mtetezi wangu wa karibu.”
“Mama nakupenda sana, lakini baba hatutendei haki.”

“Najua tuvumilie, hata wewe si unajua maisha yangu yalivyo?”
”Nayajua mama.”
“Sasa kwa nini unakuwa hivyo, hebu tuvumilie.”

”Sawa mama.”
Nilimkubalia mama lakini moyoni nikiwa na siri nzito ya kitendo nilichokifanya na mpenzi wangu usiku kucha.
 
Masalu kesha haribu!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sehemu ya 12

“Mama nakupenda sana, lakini baba hatutendei haki.”
“Najua tuvumilie, hata wewe si unajua maisha yangu yalivyo?”
”Nayajua mama.”
“Sasa kwa nini unakuwa hivyo, hebu tuvumilie.”

”Sawa mama.”
Nilimkubalia mama lakini moyoni nikiwa na siri nzito ya kitendo nilichokifanya na mpenzi wangu usiku kucha.
Baada ya kujiandaa nilikwenda zangu dukani kwangu, nilipofika nilikuwa tayari wameisha fungua. Wahudumu wangu aliponiona walinieleza:

“Bosi mzee alikuja kukutafuta.”
“Amesemaje?”
“Kwa kweli haelewiki, sijui hukulala nyumbani.”

“Kama sikulala nyumbani mimi mtoto?”
“Tutajuaje, tumemkuta kabla ya kufungua duka, alipotuona tu alituuliza upo wapi, sisi tukamjibu tangia jana tulipoachana hatujui upo wapi?”

“Mzee yule anazeeka vibaya, sasa kasemaje?”
Tumemuona akitembea kona moja hadi nyingine kisha alitoweka bila kujua.”
“Achaneni naye.”

Nilisema huku nikikaa kwenye kiti changu, ajabu wafanyakazi walinishangaa jinsi nilivyoonesha sijali lolote. Haikuchukua muda baba aliingia huku akitweta.

“Masalu.”
“Naam baba, shikamoo”
“Marahaba, hebu njoo nje mara moja.”
Nilitoka nje kuzungumza na baba, baada ya kusogea pembeni baba aliniuliza.

“Masalu jana ulilala wapi?”
“Kwenye sherehe.”
“Sherehe ya nani?”
“Ya rafiki yangu.”
“Masalu kuna sherehe gani katikati ya wiki?”
“Birthday.”

“Hukulala na mwanamke wewe?”
“Mbona unaniuliza hivyo?”
“Masalu umelala na mwanamke,” baba alinilazimisha.

“Baba nimekueleza nilikuwa kwenye pati unanilazimisha nimelala na mwanamke,” nilijitia kujitetea.
“Masalu tusije laumiana ukirudia tena shauri yako.”

“Hivi baba kwa nini unanilazimisha kitu nisichokifanya, ulinikataza nisitembee na mwanamke si kufanya mambo mengine kama hili la jana nakushangaa unanitafuta kama mwizi.”

“Mmh sawa.”
“Baba mbona unataka kuninyima uhuru, niliyajua haya toka mwanzo ukabisha, ona sasa unanifuata kila kona,” nilijifanya kulalamika.
“Siyo hivyo, sipendi uingine kwenye matatizo.”

“Baba mi mtu mzima sasa vile vile najijali”
“Kama ni hivyo itakuwa vizuri, nisamehe kama nimekukwaza.”
“Nimekusamehe ila naomba uhuru sipendi nifuatwefuatwe”

Kauli yangu ilimfanya baba azidi kuomba msamaha, tulikubaliana asinifuatilie mambo yangu kwa vile nitajilinda mwenyewe.
Tokea siku ile hata nilipolala nje baba hakunifuatilia aliniacha niishi nitakavyo, mpenzi wangu alinishawishi nihame nyumbani ili tuweze kuwa naye siku zote.

Nilifikisha wazo kwa baba ambaye mwanzo alipinga lakini baada ya kumlazimisha alinikubalia kwa shingo upande. Nilipanga chumba maeneo ya Isamiro ambako nilipanga nyumba nzima. Niliendelea na tabia zangu za kufanya mapenzi na mchumba wangu ambaye alihamia kwangu kwa siri.

Siku moja baba alinifuata dukani na kuniita pembeni, baada ya kusogea pembeni aliniuliza.
“Masalu kwa nini hujiurumii.”
“Vipi?”

“Hebu nione kidonda chako?”
Nilimuonesha, kidonda changu, baada ya kukiangalia alisema:
“Si unaona!”
Nilishangaa sikujua alisema vile kumaanisha nini? Nilijikuta nikijiuliza kipi kilichomuonesha kitu kilichomshangaza.

“Kuona nini baba?”
“Ina maana huoni kidonda chako kinaonesha hujionei huruma maisha yako.”
“Bado sijakuelewa”
“Kidonda chako kinatoa maji?”
“Hapana.”
“Unajua kwa nini?”
“Hata sijui”

“Masalu unatembea na mwanamke wewe.”
“Baba mbona unang’ang’ania neno hilo?”
“Nakuomba uache, shauri zako.”
“Niache vipi wakati sifanyi”
“Masalu mimi baba yako nimewahi kuona jua kabla yako najua kila kitu, na sababu kubwa ya kuhama nyumbani ni kufanya uchafu wako. Huoni hata biashara sasa hivi zinadolola.”

“Baba tafuteni tatizo lingine siyo mimi”
“Mmh, haya mama yako asiye kunililia”
Baba aliondoka akiwa amechanganyikiwa, nami sikuwa tayari kuachana na mpenzi wangu, katika maisha niliamini raha ya mwanaume ni mwanamke na si wingi wa pesa. Siku hiyo hiyo ndugu zangu wote walikuja na kuniweka chini juu ya mimi kuwa na mwanamke.

“Masalu kwa nini hutaki kumsikiliza baba”
“Nimsikilize kwa lipi?”
“Juu ya wewe kuwa na mwanamke.”
“Mna uhakika gani?”
“Sisi hatuna uhakika ila kasema mwenyewe.”
“Ninyi mna wapenzi?” Niliwauliza.
“Tunao.”

“Sasa mimi nazuiwa na nini?”
“Si unajua hali yako haitaki uwe na mwanamke?”
“Kwa hiyo kidonda niwe nacho mimi maisha mazuri muwenayo ninyi, sikilizeni kila mtu ataubeba mzigio wake mwenyewe.”

“Masalu utakuja kuijutia kauli yako.”
“Sijuitii mbona dada Monika hakuijutia na mkiniua na ninyi mnafirisika kazi kwenu.”
Maneno yangu yaliwazima mdomo waliondoka na kuniacha wakiwa hawana hamu na mimi. Tokea siku ile nikawa adui yao mkubwa
 
Huo ndo uanaume Masalu. Ongeza jeuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom